Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 26

HULKA ZA WATU

(TEMPERAMENTS)

Christopher Cyprian Kulimbi Mugini- KIONGOZI MKUU (MASTER GUIDE) Page 1


HULKA ZA WATU(TEMPERAMENTS)
Utangulizi
Hulka ni tabia ya asili ya mwanadamu isiyoonekana kwa macho
bali kwa matendo. Tabia hii inategemea mtu na mtu, na kwamba
kila mmoja ana sehemu/kundi lake. Yakobo 2:17 hutueleza kuwa
Imani iendane na matendo hii itatusaidia kujua hulka ya mtu
isiyojulikana.
Mungu pekee ndiye ajuaye kila kitu hatuwezi kumficha
chochote.Katika utendaji kazi wa kanisa Mungu alichunguza
hulka ya kila mtu na ndio maana wengine ni wachungaji,
wainjilisti, walimu, wafalme,mitume na manabii, Mfano Daudi.
Kama tusipojua nafasi ya hulka katika utendaji kazi wa
kanisa/biashara/kazi yoyote huduma hiyo inaweza kudidimia.
Kwa nini? (aliyepewa nafasi hana hulka ya uongozi/hamasisha).
Kanisa linaloongozwa na Roho Mtakatifu ni lazima lizingatie
huduma za kanisa kulingana

Christopher Cyprian Kulimbi Mugini- KIONGOZI MKUU (MASTER GUIDE) Page 2


na hulka ya kila mmoja.Roho Mtakatifu anaweka karamasawasawa na apendavyo yeye
kwa kufuata hulka ya kila mmoja ndani yake.Kama wewe ni mpole/mkimya si dhambi
bali ni nafasi ya kanisa kukutumia unapostahili ili kuujenga mwili wa Kristo.
Kama wewe ni mbunifu na mtu wa ratiba si dhambi bali ni kazi ya kanisa kukuweka
katika huduma ambayo utaleta mapinduzi ya kiroho kwa haraka sana na kubuni
mikakati ya Injili.

UMUHIMU WA KUJUA HULKA ZA WATU


Kujua hulka za watu hutusaidia:- a.Kuwajua watu vizuri
b.Kushughulika na watu kwa urahisi
c.Kuchukuliana na watu kwa uvumilivu

FAIDA ZA MTU KUELEWA HULKA ZA WATU


1.Kutengeneza pale palipo na udhaifu :

Christopher Cyprian Kulimbi Mugini- KIONGOZI MKUU (MASTER GUIDE) Page 3


Mfano:-

 Kuthibiti hasira na kiburi (Koleriki)

 Kuthibiti hali ya kutojiamini au kukosa ujasiri(Melankoli)

 Kuthibiti tabia ya kuongea kupita kiasi(Sanguine)

 Kuthibiti uvivu na kuwa mchapakazi(Flegmatiki)

MAKUNDI YA HULKA (Temperaments)

Mwanafalsafa aliyeitwa Hippocrates alikuwa wa kwanza kuwaweka watu katika


makundi manne(4).
Makundi hayo ya hulka yalijulikana kama ‘’Temperaments”. Neno Temperaments
linatoka katika lugha ya kilatini na lina maana ya kuchanganya kwa
vipimo.Hippocrates alizungumzia kuchanganya vitu vya majimaji, na majina manne
yalimjia mawazoni ambayo ni;

Christopher Cyprian Kulimbi Mugini- KIONGOZI MKUU (MASTER GUIDE) Page 4


1. Sanguine 2.Choleric
3.Melancholy
4.Phlegmatic
JINSI YA KUGUNDUA HULKA YAKO

Ili kugundua hulka yako jibu maswali yafuatayo kwa uaminifu.

i. Je huwa ninachukua hatua(react) ya kujibu mapigo muda ule ule ninapotendewa


jambo au huwa sifanyi haraka kuchukua hatua kujibu mapigo kwa jambo
nililotendewa?

ii. Je huwa mimi ni mwepesi wa kutenda mara moja au huwa nabaki mtulivu na
kusubiri?

iii. Je huwa natunza kwa muda mrefu hisia kwa jambo lililotendwa kwangu au natunza
kwa muda mfupi tu na kisha kutoweka?

iv. Je ninapokosewa naweza kusamehe?

v. Je huwa ninakuwa na kinyongo na kuchukia ninapotukanwa?

Christopher Cyprian Kulimbi Mugini- KIONGOZI MKUU (MASTER GUIDE) Page 5


Ikiwa majibu yatakuwa yafuatayo basi mtu huyo ana hulka ya Choleric au
Melancholy.

a) Kwa kawaida siwezi kusahahu matusi niliyotukanwa nayakumbuka kwa muda


mrefu na ninapoyakumbuka na kuyafikiria najisikia vibaya.

b) Naweza kuwa na kinyongo dhidi ya aliyenikosea kwa muda mrefu kwa siku
nyingi na kwa majuma mengi

c) Huwa nawakwepa wale walionikosea , sitaki kukutana nao

d) Huwa sitaki kuzungumza na wale walionikosea

Lakini majibu yakiwa yafuatayo basi mtu huyu ana hulka ya sanguine au
phlegmatic

a) Situnzi hisia mbaya

b) Siwezi kumkasirikia mtu kwa muda mrefu

Christopher Cyprian Kulimbi Mugini- KIONGOZI MKUU (MASTER GUIDE) Page 6


c) Huwa ninasahau upesi matusi niliyotukanwa

d) Wakati fulani naelekea kuwa na hasira lakini naidhibiti.

Baada ya kugundua kuwa yeye anaweza kuwa na hulka aina ya choleric au


melancholy, anapaswa kujibu maswali yafuatayo ili ajue hulka yake hasa ni ipi
kwamba ni choleric au melancholy.Maswali hayo ni:-

a) Je, huwa ninaonyesha kwa haraka hali ya kutaka kupambana dhidi ya mabaya
niliyotendewa?.

b) Je, huwa nadhihirisha chuki yangu kwa maneneo au kwa matendo?

c) Je, huwa ni mwepesi kutukana ninapotukanwa?

d) Je, huwa ninapotendewa mabaya nabakia mtulivu kwa nje lakini kwa ndani
nikiwa nahangaika na kuumia?

Christopher Cyprian Kulimbi Mugini- KIONGOZI MKUU (MASTER GUIDE) Page 7


e) Je, huwa naogopa kupoteza tumaini kiasi kwamba nakosa maneno yafaayo na
ujasiri kwa kujibu na hivyo kuamua kunyamaza kimya?

f) Je, inatokea mara kwa mara ya kwamba sijisikii vibaya muda ule ule
ninapotendewa ubaya lakini baada ya saa chache au kesho yake ndiyo naanza kuwa
na hisia kwa ubaya niliyotendewa?
Kama jibu ni ndiyo kwa swali la (a)-(c) basi mtu huyo ana hulka ya
Choleric
Na kama jibu la swali la (d)-(f) ni ndiyo basi mtu huyo ana hulka ya Melancholy
Jibu likiwa ni ndio kwa maswali yafuatayo basi mtu huyo ana hulka ya
Sanguine.
Maswali hayo ni:-b

a) Je, huwa natunza hasira ghafla dhidi ya mabaya niliyotendewa?

b) Je, ninakuwa mwepesi kukasirika nakutenda kwa haraka bila kufikiri?

Christopher Cyprian Kulimbi Mugini- KIONGOZI MKUU (MASTER GUIDE) Page 8


Kama jibu kwa maswali yafuatayo ni ndiyo basi mtu huyo ana hulka ya
Phlegmatic.

a) Je,sisumbuliwi na hisia zangu kwa urahisi?

b) Je, huwa na baki mtulivu, asiyejali ninapotendewa mabaya?

1: SANGUINE- Bwana mtazamia mema

SILIKA YAKE

 Anajipenda/nadhifu
 Anapenda sifa na kutambuliwa kuwa yupo
 Ni muongeaji sana/mtoa hadithi nyingi
 Mchangamfu na anapenda mizaha,/kuchekesha
 Hana msimamo wala aibu
 Kutokubali kushindwa na kutazamia mzuri(optism)
 Si mwepesi wa hasira
SANGUINE KAMA MZAZI

Christopher Cyprian Kulimbi Mugini- KIONGOZI MKUU (MASTER GUIDE) Page 9


Familia inakuwa na furaha muda wote: Mama/Baba anachekesha watoto ,
kuwapa hadithi za hapa na pale na kucheza nao
Anabadilisha tatizo kuwa kitu cha kawaida:Hubadili ukubwa wa tatizo kuwa
wa kawaida ili kuinusuru familia kukosa furaha
Anasahau majukumu ya watoto: Huingilia majukumu ya watoto na
kuwafanya wasahau ni nini majukumu yao.
Hana Mpangilio: Kazi zake ni za kushitukiza tu_hakuna ratiba
Hasikilizi mpaka mwisho: ni mwepesi kudakia na kusema nimekuelewa kumbe
hajui lolote.
Ana hasira za haraka: Hushindwa kujitawala na kufanya maamuzi bila
kufikiria.
SANGUINE KATIKA KAZI

Ni mtu wa kujitolea:Ni wepesi kujitolea kufanya kazi hata kama ni ngumu


haiwezi

Christopher Cyprian Kulimbi Mugini- KIONGOZI MKUU (MASTER GUIDE) Page 10


Ni muhamasishaji mkubwa : Hushawishi wengine kufanya kazi hata kama
hawaziwezi
Huanza kazi kwa mbwembwe: Akianza kufanya kazi utadhani itaisha kwa
muda mfupi kwa sababu ya madoido yake
Hakati tamaa mapema na hufanya uamuzi haraka sana
Kwenye kikao anapenda kujua agenda mapema
Anahitaji kusimamiwa: Muda mwingi anautumia kuongea na kutafuta wapi
kuna kundi la watu wamejikusanya.
Mwepesi kusahau majukumu yake:Kazi inaweza isiishe kwa muda
uliopangwa na yeye haoni tatizo.
Hafuati mpangilio: Anaangalia kazi inayombana ndio anahangaika nayo
kwanza. Ni rahisi kutengeneza madeni.
Si mtu wa nidhamu: Ni mtu wa ahadi njoo kesho kila siku kumbe hawezi
kufanya,

Christopher Cyprian Kulimbi Mugini- KIONGOZI MKUU (MASTER GUIDE) Page 11


na ukimkuta kwa bahati mbaya; nilipata dharura, tufanye kesho
SANGUINE KATIKA MARAFIKI

Anatengeneza marafiki kwa haraka sana:Hatakama ni mgeni sehemu yoyote


ni mwepesi kupata marafiki na kuongea nao
Anapenda watu:Anapenda kukaa mahali palipo na watu ili aongee nao
Anaonekana ni mtu wa
nidhamu:Hufanya jambo lolote analoambiwa pasipo kupima uzito, hata hivyo kazi
humshinda.
Habebi malalamiko:Nivigumu kulalamika mbele ya rafiki zake ila hulalamika
chini kwa chini.
Anachukia kuwa peke yake ; Kumkuta akiwa peke yake basi ameshindwa
kabisa.Anapokosekana watu/watoto
/marafiki humuulizia

Christopher Cyprian Kulimbi Mugini- KIONGOZI MKUU (MASTER GUIDE) Page 12


Anapenda kujibu maswali ya wengine:Swali akiulizwa rafiki yake kabla
hajajibu yeye tayari amekwisha msemea/mjibia
Ni mwepesi kuomba msamaha: Aligundua amekosa ni mwepesi kuomba
msamaha hata kwa kupiga magoti-janja yake ili awe salama lakini hajajutia kosa
Hapendi kusikiliza: Anachukia maongezi/maelezo marefu hivyo hukatisha kwa
kuingilia ili naye azungumze.
Anarudia hadithi: Huwa anaongea na kujisahau na kujikuta anarudia
aliyoyasema mwazo
HITIMISHO LA SANGUINE

Inapotokea ukafanya kazi/ ni rafiki wa mtu ambaye ni Sanguine unashauriwa ufanye


yafuatayo:
Muombe Mungu amsaidie kupunguza hasira

Christopher Cyprian Kulimbi Mugini- KIONGOZI MKUU (MASTER GUIDE) Page 13


Unatakiwa kila wakati uwe na furaha

Unatakiwa uwe mwepesi wa kujua kama amekasirika au anafuraha


Usiache kumsifia katika kila jambo

Uwe mwepesi kuomba msamaha unapogundua umefanya kosa


Unatakiwa usionekana kila wakati umenyong’onyea
Mshirikishe katika kusoma Biblia na maombi

2: CHOLERIC- Bwana chuki

SILIKA YAKE

 Mgomvi na mwepesi wa hasira


 Mchapakazi hodari na mwenye akili nyingi
 Hapendi kukaa bila kazi yeyote
 Si rahisi kukatishwa tamaa
 Amezaliwa ni kiongozi(anapenda ukubwa/vyeo)

Christopher Cyprian Kulimbi Mugini- KIONGOZI MKUU (MASTER GUIDE) Page 14


 Anajiamini katika kufanya maamuzi
Mfano: Julius Cesar, Hannibal (North Africa), Dikiteta Stalin, Hitler, Mussolini n.k
CHOLERIC KAMA MZAZI

Anatumia sauti ya uongozi: Hutumia uongozi wake hata akiwa nyumbani na


kuudhihirisha kila eneo katika familia yake
Ni mtu wa mipango: Huanzisha mipango na malengo yanayotakiwa kutimizwa
na familia
Anahamasisha familia kutenda: Hapendi kuona familia imekaa bila kazi, kama
mtoto amekaaa bila kazi anajitahidi amtafutie kazi awajibike
Kila wakati anatumia amri: Anaamrisha wakati wote na anatumia sauti ya
uongozi hata kwa mwenza wake, baba/mama.
Hana uvumilivu kwa utendaji mbovu: Hapendi kuona kazi inafanywa chini ya
kiwango wahusika huwakemea/kuwaonya

Christopher Cyprian Kulimbi Mugini- KIONGOZI MKUU (MASTER GUIDE) Page 15


Haachi watoto wapumzike: Watoto hawafurahii anapokuwa nyumbani maana
muda wote ni kazi tu na kusumbuana naye.
CHOLERIC KATIKA KAZI

Anatamani malengo yafikiwe: Ni mtu anayependa mipango yake itimie kama


ilivyopangwa
Ni mhamasishaji mzuri: Hapendi kuona watu wamekea bila kazi
Anatazama ukubwa wa kazï: kila kazi inaipa uthamani mkubwa na kujitahidi
kuifanya vizuri
Anatekeleza kwa haraka jambo: sio mtu wa kujivutavuta katika kazi na
anasisitiza uzalishaji
Kosa dogo ni tatizo: Unatakiwa kuwa makini unapofanya kazi na mtu huyu,
kosa kwake ni uzembe unaotakiwa adhabu

Christopher Cyprian Kulimbi Mugini- KIONGOZI MKUU (MASTER GUIDE) Page 16


Haelezi kazi kwa kina: Anapogawa kazi haielezi kwa kina ambavyo inatakiwa
kufanyika na kwa kiwango gani
Anaweza asiheshimu mawazo ya wengine: Hupuuzia mawazo ya wengi kwa
kuamini ya kuwa akishindwa yeye hakuna mwingine anayeweza
Anachukizwa na vitu vidogovidogo: Huwa na hasira nyingi na hana huruma
Anapenda kuwa kuwa boss na si rahisi kupongeza kwa kitu kizuri
CHOLERIC KATIKA MARAFIKI

Anahitaji marafiki kidogo: si mwepesi kutengeneza marafiki


Anafanya kazi kimakundi:Anapenda kushirikiana na watu katika makundi pale
tu anapoona kuna jambo analohitaji kutoka kwao

Christopher Cyprian Kulimbi Mugini- KIONGOZI MKUU (MASTER GUIDE) Page 17


Anaongoza na kutekeleza: Yeye ni kiongozi wa wote na huwaelekeza ni nini
kinatakiwa kufanyika.
Kila wakati yuko sahihi:Katika marafiki zake yeye anafikiri anachokifanya ni
bora na sahihi kuliko wengine wanachokifanya
Anafanya vizuri katika dharura.

Anajifanya kutumia watu; Mwanzoni ataonekana anashirikiana na wenzake


kumbe asilimia kubwa anatumia mawazo yake
Anaamua kwa ajili ya wenzake: Anaweza kuamua kwa niaba ya wenzake na
uamuzi huo ni lazima uheshimiwe.
Hawawezi kusema nimekosa: Ni mgumu wa kuomba msamaha
HITIMISHO LA CHOLERIC

Ikitokea ukawa unafanya kazi kwa karibu na choleric unatakiwa kufanya


yafuatayo:
Fanya kazi kwa ubora

Christopher Cyprian Kulimbi Mugini- KIONGOZI MKUU (MASTER GUIDE) Page 18


Usifanye bila kujua anataka ufanyeje yeye

Usijaribu kujionyesha kuwa unajua kuliko yeye


Kila hatua unayoifikia omba akueleze kabla
hujaanza hatua nyingine
Usiwe mtu wa kujiamini sana bali tegemea ushauri wake kwanza
Mweleze kuwa unajisikia vizuri kufanya kazi na yeye
Mfanye ajali shida za wenzake

Mshauri awe tayari kusamehe na


kuwavumilia wenzake

Christopher Cyprian Kulimbi Mugini- KIONGOZI MKUU (MASTER GUIDE) Page 19


MELANCHOLY- Bwana Mkamilifu
SILIKA ZAKE

 Anapenda nyimbo/muziki na Sanaa


 Ni mkimya , asiye na maneno mengi
 Huuliza maswali kila jambo/Kuhoji
 Hufanya vitu kwa mpango( ratiba, muda)
 Si rahisi kusahau mabaya aliyotendewa
 Ni mtu wa huzuni na mwenye mawazo
 Hapendi kutawaliwa/kuwa chini ya mtu
MELANCHOLY KAMA MZAZI
Anaweka viwango vya juu:Anaamini katika mafanikio ya kiwango
cha juu
Anataka kila kitu kifanyike kwa wakati:Mzazi huyu anapenda
familia yake ifanye mambo kulingana na wakati uliopangwa, hapendi
mtu kutoa udhuru
Anaweka nyumba katika mpangilio mzuri:Mwanafamilia akitoka
ni lazima atoe taarifa anakwenda wapi? Na akichelewa vivyo hivyo atoe
sababu za kuchelewa

Christopher Cyprian Kulimbi Mugini- KIONGOZI MKUU (MASTER GUIDE) Page 20


Anashawishi kukuza vipaji: anapenda watoto wake wawe wabunifu
kwa kuwafundisha na kuwapa nafasi ya kufikiri kwanza.
Anakatisha tamaa watoto: Hajui kumtia moyo mtoto , ukifanya
vibaya unaambiwa live.
Anaweka malengo yasiyofikiwa: Malengo ni makubwa kuliko
uwezo ulio nao familia
Hukasirishwa makubaliano
yanaposhindwa kutimizwa:
MELANCHOLY KATIKA KAZI
Ni mtu wa ratiba: ukichelewa
hutamkuta, anajali wakati
Anafanya kazi kwa umakini;kazi yake huvutia, hapendi kulipua
kazi
Anahitaji ufafanuzi wa kina; kuepusha maswali
Ni mchumi;hatumii pesa ovyo hovyo

Christopher Cyprian Kulimbi Mugini- KIONGOZI MKUU (MASTER GUIDE) Page 21


Anapenda kumaliza kazi alioianza
Si mtu wa watu-hupendakukaa peke yake
Huchagua kazi ngumu; lengo apate
changamoto
Ni mgumu kuridhika; hadi afanye utafiti wa kujiridhisha
Anafikiria sana kupitisha kazi:kupitisha kazi ifanyike bila
kuthibisha hawezi
MELANCHOLY KATIKA MARAFIKI
Anafanya marafiki kwa tahadhari;
hapendi marafiki-kukosa imani nao
Ni mwaminifu na wa kujitoa: hufanya jambo bila
kulalamika
Husikiliza malalamiko; hupokea na
kutatua malamiko
Hufikiria wenzake
Hutatua matatizo ya wengine
Huchukia wanaopinga jambo
alilolianzisha

Christopher Cyprian Kulimbi Mugini- KIONGOZI MKUU (MASTER GUIDE) Page 22


Hana marafiki wa karibu Haamini mtu
mwingine.
HITIMISHO LA MELACHOLY
Ikitokea unafanya kazi na mtu wa jamii ya melacholy
unatakiwa ufanye yafuatayo:
Usiwe mchelewaji na mwenye kutoa
udhuru
Uwe makini sana na kazi anazokupa
kufanya
Hakikisha unamaliza kazi ulizopewa kwa muda na si vinginevyo
Unatakiwa uwe makini na swali
analokuuliza
Usiwe na mizaha mbele zake

3. PHLEGMATIC- Bwana Mtulivu

SILIKA YAKE
Mwenda pole kwa kila jambo Ni mtulivu
mwenye subira
Anapenda amani na mwenye upendo Muoga na
mbinafsi(hatoi kitu kwa
upendo)
Mvivu(mpenda starehe) na mlalamishi Ni mvumilivu
hakasirishwi kirahisi
PHLEGMATIC KAMA MZAZI
Ni mzazi mzuri:Watoto wanampenda kwa kuwa
hawakemei/kuwasumbua
Anachukua muda kwa watoto: Hutumia muda mwingi kukaa na
watoto

Christopher Cyprian Kulimbi Mugini- KIONGOZI MKUU (MASTER GUIDE) Page 23


Hana haraka: hufanya mambo pole pole sana
Hakuna nidhamu: Baba/Mama hana msimamo hivyo maadili ya
watoto hupungua
Hakuna mipango yoyote nyumbani;
hakuna mpangilio katika kuongoza familia
PHLEGMATIC KATIKA MARAFIKI
Ni rahisi kuambatana na mtu Ni msikilizaji
mzuri

Ana huruma

PHLEGMATIC KATIKA KAZI


Hupenda kutazama wengine wakifanya kazi
lakini sio yeye kufanya kazi
Anapenda sana kupumzika Anapinga
mabadiliiko
Anapenda kuhukumu wengine
wanapokosea
Hasisimui; kuleta hamasa ya mabadiliko

Hapendi kujishughulisha

Christopher Cyprian Kulimbi Mugini- KIONGOZI MKUU (MASTER GUIDE) Page 24


HITIMISHO LA PHLEGMATIC
Ikiwa unafanya kazi na mtu wa jamii ya phlegmatic au ndiye mkuu wako
wa kazi, unatakiwa ufanye yafuatayo:
Akikupa kazi usitegemee maelezo ya ziada Uwe na ujasiri wa
kufanya kazi peke yako
Anaweza kukukosoa pasipo maelekezo ya nini ufanye sasa
Omba msaada kwa rafiki mwingine kuliko yeye
Usitegemee akuite , ni lazima ujitume
kumaliza kazi yako
Uwe mbunifu la sivyo hutaweza kusonga mbele

Onyesha ujasiri wa kufanya kazi na kutoa maamuzi

MWISHO

 Je unaridhika na kuishi na tabia hiyo uliyo nayo?

 Yupo mtu mmoja tu anaweza kubadili tabia yako; YESU


KRISTO MWANA WA MUNGU

 Siri ya mabadiliko ya hulka/tabia ni YESU PEKEE

 Chukua hatua umwendee YESU upate kubadilisha tabia yako


uwe kiumbe kipya:2 wakoritho 5: 17

Christopher Cyprian Kulimbi Mugini- KIONGOZI MKUU (MASTER GUIDE) Page 25


Christopher Cyprian Kulimbi Mugini- KIONGOZI MKUU (MASTER GUIDE) Page 26

You might also like