Forex Nini

You might also like

Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 2

FOREX NINI?

Utangulizi

Umewahi kusafiri kutoka nchi moja kwenda nyingine?! kama umewahi, basi bila shaka
pale mpakani ulikutana na vibanda vya kubadilishia fedha, unawapa pesa ulizotoka nazo
kwenye nchi moja wanakupa pesa za nchi unayoenda kuingia.

Hata kama haujawahi kutoka nje ya nchi usijali, huenda umewahi kukutana na vibanda
vinavyojulikana kama “Bureau De Change” maeneo ya benki, mitaa iliyo changamka au
viwanja vya ndege, sasa hiyo ndio inayoitwa FOREX!!!, Kuna mtu atakua anajiuliza
kwamba “kwaiyo inabidi niende mpakani nikatafute eneo nijenge kibanda changu na
nitafute mtaji mkubwa ndipo niweze kufanya hii biashara??!!” Hahahahaha sio hivyo
bana, utakua na uwezo wa kufanya hii biashara hata ukiwa kitandani, tena hata kwa mtaji
usiotosha hata kununua baiskeli hahahahaha, ngoja tuendelee…

FOREX ni nini
FOREX ni ufupisho wa “FOReign EXchange” ikimaanisha ubadilishaji wa fedha za kigeni,
kama wanaoufanya hao tuliowaona hapo juu, kwa hiyo hapa bidhaa zinazobadilishwa ni
fedha tupu! unakua unauza fedha uliyo nayo na kununua fedha nyingine unayoihitaji kwa
wakati huo. Kabla ya maendeleo ya mtandao wa intaneti ilikua ngumu sana kwa wafanya
biashara wadogo kama sisi kuingia katika soko hili, ilikua ikifanywa na mabenki na taasisi
nyingine kubwa za kifedha, kwani ingehitaji pesa nyingi saaana kuifanya, lakini tuishukuru
sana teknolojia na brokers wanaotuunganisha na soko na kutupatia leverage, kwani sasa
tunaweza kuingia sokoni muda wowote na kwa mtaji wowote.

Usijali kuhusu misamiati unayokutana nayo, muda si mrefu tutaizungumzia…

Utakua ukifanya forex kupitia intaneti, na hautakua na kazi ya kusubiri au kutafuta mteja
kwani soko lipo masaa 24 kwa siku na siku 5 kwa wiki, wikiendi tu ndio hakuna soko,
utakachokua unakifanya ni kuchambua muendelezo wa sarafu flani kwa muda uliopita,
labda soko la kubadili EURO na USD, ili kuona kama kuna fursa ya kuuza ama kununua.
inakua vipi unauza au kununua?! (kwenye mafunzo haya tutatumia sana mfano wa
biashara ya mpunga kwa sababu mdogo wangu alinichekesha sana siku aliponiambia
kwamba kwa jinsi anavyoupenda wali, siku wakitangaza kanisani kwamba wali ni
haramu yupo tayari kuliasi kanisa ili tu aendelee kula wali hahahahaha!!!)

Chukulia mfano unafanya biashara ya mpunga, kwa kawaida utasubiri wakati wa mavuno
ambapo thamaani ya mpunga dhidi ya pesa itakua imeshuka sana, na unajua kabisa
baada ya kipindi hiki bei ya mpunga lazima ipande, ndipo utanunua mpunga na kwa
maana hiyo utakua umeiuza pesa, kisha utautunza mpunga kwa muda flani ukisubiri bei
ipande, kisha ikipanda hadi panapokuridhisha utauuza mpunga na kuinunua tena pesa,
na lile ongezeko la bei ndilo litakua faida yako, na akaunti yako itakua imekua!!!

Vivyohivyo kwenye biashara ya forex, chukulia unafanya biashara baina ya EURO na


DOLLAR, itabidi usubiri mpaka pale ambapo bei ya Euro itakua chini zaidi dhidi ya Dollar
na ioneshe kila dalili kwamba baada ya hapo itapanda, kisha utazitumia Dollar kuinunua
Euro, kwaio utanunua Euro kwa kuuza Dollar, kisha utasubiri bei ya Euro itakapopanda
hadi panapokuridhisha, ndipo utaziuza tena Euro na kurudisha Dollar, kwahiyo lile
ongezeko la bei ndilo litakua faida yako.

Utamu unakuja hapa, kwenye forex tunasema “vice versa is true”, kwaiyo ukiona tena
thamani ya Dollar imepanda hadi mwisho dhidi ya Euro, na kuna kila dalili kwamba
thamani ya dollar inaenda kuporomoka, utaiuza palepale na kununua Euro, kisha
ikiporomoka tu utaenda kuinunua kwa bei ya chiiini zaidi kwa kuuza zile Euro, kwahiyo
inakua faida juu ya faida hahahahaha!!!!

Najua unajiuliza maswali mengi sana kama utajuaje kama bei ndio inaenda kupanda ili
ununue?! au bei ndo inaenda kushuka ili uuze?! na hayo yote unayafanyia wapi?! usijali,
tuliza papara niulize kwanza maswali kuhusu hii mada, kisha tukutane hapo mbele!

Bofya hapa

https://t.me/NFP24

Follow me on X

Jiunge na Channel yetu ya Telegram

You might also like