Maana Ya Misamiati Mbalimbali Katika FOREX

You might also like

Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 4

Maana ya misamiati mbalimbali katika FOREX

Baada ya kumalizana na utangulizi wa awali, sasa ni wakati wa kuzama ndani zaidi, na


kuangalia misamiati mbalimbali ambayo utaitumia katika hii biashara, kila eneo hua lina
lugha yake, kwahiyo hata huku pia kuna lugha yetu. Bila kupoteza muda tuitupie macho
misamiati hiyo;-

Pair: Tuliona katika biashara ya mpunga kuna vitu viwili vinavyohusika, yaani pesa na
mpunga, sasa katika forex, pia kuna bidhaa mbili mbili zinazohusika na zote zikiwa ni
sarafu lakini za nchi tofauti, na hizi ndizo tunaita pair, mfano USDCAD, EURZAR, GBPJPY,
na nyingine kibao utakutana nazo. katika pair hizi, unapoamua kuuza ya upande wa
kushoto inamaana unanunua ya upande wa kulia, vilevile unaponunua ya upande wa
kushoto inamaana unauza ya upande wa kulia, kama ilivyo unapouza mpunga inamaana
unanunua pesa, na unaponunua mpunga unakua unauza pesa!!! (hapa kwenye wali hapa
bila shaka patamkosha sana mdogo wangu).

Unaweza ukajiuliza hivi vifupi vya hizi pair virefu vyake ni nini? ipo hivi, herufi mbili za
mwanzo za sarafu flani hua zinasimamia jina la nchi ambamo hiyo sarafu inatumika, na
herufi ya mwisho inasimamia aina ya sarafu hiyo, mfano;-

TZS ni TanZanian Shilling (japo hii haipo katika chart za Forex)


USD ni United States Dollar
GBP ni Great Britain Pound
EUR ni Euro (pesa ya ukanda wa Ulaya)
CAD ni CAnadian Dollar
JPY ni JaPanese Yen
ZAR ni South African Rand (sarafu pekee kutoka Africa iliyo kwenye chart za fx)
NZD ni New Zealand Dollar
AUD ni AUstralian Dollar
Na nyingine nyingi.

Sarafu hizi hua zinafanya CROSS ili kutengeneza pair, na kwa maana hiyo kama pair
itatengeneza kwa cross ya sarafu zenye nguvu, basi pair hiyo kasi yake inakua kubwa na
kwahiyo ni nzuri kuzifanyia biashara. Sarafu zenye nguvu, ya kwanza ni USD kwa sababu
Dollar ya kimarekani kwanza ndio imewekwa kama hazina ya dunia, pili marekani ni taifa
lenye uchumi mkubwa, ina jeshi imara, na siasa yenye afya, kitu kinachofanya sarafu
yake isiyumbe ovyo, zingine zenye nguvu ni EUR, GBP, CAD, JPY, na CHF. kwa maana hiyo,
cross zenye kasi kubwa na nzuri kufanyia biashara ni kama EURUSD, GBPUSD, USDJPY,
CHFJPY, GBPJPY, EURCAD, na nyinginezo zitakazo tokana na sarafu hizo juu.

Pair ambazo zinakua hazina kasi kubwa, ni zile zinazotengenezwa na moja au zote mbili
zinatoka kwenye kundi la sarafu dhaifu kama NZD, AUD, NOK, kwahiyo pair kama
AUDNZD, NZDCAD, USDNOK, AUDUSD zinakua hazina kasi kubwa katika hali ya kawaida.

Hizo ndizo PAIR bwana, na ndizo bidhaa tunazoenda kucheza nazo sokoni
hahahahaha, tuendelee na misamiati yetu…

Base Currency: Hii ni sarafu ya mwanzo ya pair yako, mfano una USDJPY basi USD ndio
Base currency, kwa hiyo, unapo bofya kitufe cha kuuza pair, unayoiuza hua ni hii base
currency, na unapo bonyeza kitufe cha kununua pair, unakua unainunua hii hii base
currency. chochote utakachofanya, iwe kuuza au kununua unakua unaifanyia hiii.

Quote Currency: Hii ni sarafu ya pili ya pair yako, mfano una CADCHF basi CHF ndio
Quote currency, na kwa hivyo, ukibovya kitufe cha kuuza pair, basi unakua umeinunua hii
quote currency, vilevile ukibofya kitufe cha kununua pair, hii unakua unaiuza. Hivyo
chochote utakacho kifanya, kitatokea kinyume kwa hii, ni kwasababu kitendo halisi
kitakua kimeitokea Base currency hiyo ya juu, sjui tumeelewana??

Sarafu ikiwa Base katika pair flani, haimaanishi itakua base kwenye pair zote, kwingine
inaweza kua Quote, mfano katika USDJPY USD ni base, lakini katika EURUSD USD
imekua quote, kwahiyo inategemeana na pair yenyewe, hizi hauzipangi wewe,
zilishapangwa tayari, wewe ni kuchagua pair tu.

Bulls au Buyers: Hawa ni wanunuzi wa pair flani, ambapo kitendo wanachokifanya cha
ununuaji kinaitwa Buying au Going Long. Wanunuaji wakiwa wengi kwa kawaida lazima
bei ya hiyo bidhaa ipande juu, kwahiyo wewe unapotaka kuwa Bull au Buyer mwenye
faida unatakiwa ununue pair mwanzoni kabisa wakati bulls wanaingia kipindi bei bado
ipo chini, ili bei ikipanda juu we utaenda uiuze huko juu kwa bei ya faida!! (najua
unajiuliza utajuaje kama bei ndo ipo chini ili ununue ipande ukaiuze juu?? usijali,
maadamu tupo pamoja, nitakupa ufundi hahahaha..) kwahiyo ukiskia “the price is
bullish” ujue bei inavutia kununua hapo ilipo, kwasababu inaenda kupanda.

Bears au Sellers: Hawa ni wauzaji wa pair flani, kwahiyo ni kinyume cha Bulls, na kitendo
wanachokifanya cha uuzaji kinaitwa Selling au Going Short. Wauzaji wa bidhaa wakiwa
wengi, maana hiyo bidhaa ni nyingi sokoni, na hivyo lazima bei yake ishuke chini, kwa
maana hiyo ili uwe Bear au Seller mwenye faida, lazima uuze pair mwanzoni kabisa
kipindi bei ipo juu, ili bei ikishuka chini kabisa unakuja kuinunua kwa bei chee kabisa!!
yote haya tutajifunza, vuta subira. Kwahiyo ukiskia “the price is Bearish” ujue kwa bei
ilipo, inashawishi kuuza kwasababu inaenda kushuka.

Price: Hii ni bei ya base currency dhidi ya quote currency kwa wakati wowote ule, mfano
ukiambiwa sasahivi price ya EURUSD ni 1.13090 ujue Euro moja inauzwa kwa USD
1.13090 kwa wakati huo. Kwa kawaida chati za ma broker wengi hua zinatoa bei katika
viwango vinne vya desmali, yaan mfano EURUSD ni 1.1309, yaani baada ya icho kituo
zinafata namba nne, isipokua pair za Japanese Yen (JPY), ambazo zenyewe zinakua na
viwango viwili vya desmali, mfano USDJPY price yake ni 108.97. Lakini kuna baadhi ya ma
broker wanaweka bei za kawaida kwa viwango vitano vya desmali, na zile za JPY kwa
viwango vitatu, mfano EURUSD ni 1.12708 na USDJPY ni 107.324 pia sio kesi.

Bid price: Hii ni ile bei ya kuuzia pair flani ambayo anakupa broker, hua ni bei ya kushoto
unapoangalia pair yako

Ask price: Hii ni bei ya kununulia pair flani ambayo anakupa broker, hua inakua upande
wa kulia, na ni kubwa ukilinganisha na bid price.

Spread: Huu ni utofauti kati ya ask price na bid price za pair flani, yaani ukichukua ask
price ukatoa bid price, kinacho baki ndio spread, na ndio hua faida ya broker. mfano
ukikuta umewekewa USDJPY 112.698/112.700 basi Bid price ni 112.698 na Ask price ni
112.700, kisha spread inapatikana kwa kuzitoa bei hizo, ambayo ni 112.700-
112.698=0.002, tutaidadavua vizuri mbele.

PIP: Huu ni utofauti wa bei ile uliyoingilia sokoni na bei ile uliyotokea sokoni, na hua
inakua ni bei ya kipande kimoja cha fedha, na ndio itatumika kukokotoa faida yako.
Mfano ulifanya biashara ya EURUSD, ukainunua ikiwa katika Dollar 1.1309, inamaana
kipande kimoja cha Euro ulikinunua kwa bei hiyo, kisha ukasubiri bei ipande, na ilipofika
1.1329 ukaamua kuiuza, inamaana kipande kimoja cha Euro ulikiuza kwa Dollar hizo,
ambazo kwako ni faida kwani umeuza kwa bei ya juu kuliko uliyonunulia. sasa kupata
pips, chukua bei uliyouzia utoe bei uliyonunulia: 1.1329-1.1309=0.0020, ikimaanisha kwa
kila kipande cha Euro ulichouza ulipata faida ya Dollar 0.002, lakini hapa kwenye pips
sifuri za mbele hua hazihesabiki, kwahiyo tutakua na pips 20.

Hapo juu tumeona kupata pips kwa broker mwenye viwango vinne vya desmali, kwa
yule mwenye viwango vitano, ile namba ya mwisho hua tunaikadiria, mfano, EURUSD
kutoka 1.13090 hadi 1.13293, utofauti ni 1.13293 kutoa 1.13090 ambayo ni 0.00203, na
hii itakua pips 20.3, sawa na 20 tu kwa makadirio. Kwa pair za JPY, ukiwa na USDJPY
kutoka 132.35 hadi 132.60 hapo utakua na pips 25, na ukipewa USDJPY kutoka 132.352
hadi 132.609 utakua na pips 25.7 sawa na 26 kwa makadirio.

Lot size: Hii ni idadi ya vipande vya sarafu unavyoviingiza sokoni kwa wakati mmoja,
utagundua kwamba idadi hii ya vipande utakayvyoingiza sokoni ukizidisha na faida kwa
kila kipande tuliyoipata hapo juu kwenye pips, ndipo utapata faida yako kamili. hua kuna
mifumo mitatu ya uchaguzi wa lot size ya kutumia, kubwa kabisa ikiwa Standard lot,
inayokua na vipande 100000 vya sarafu flani, ya kati ikiwa Mini lot yenye vipande
10000, na ya chini kabisa ikiwa micro lot, yenye vipande 1000.

Kuna watu hesabu kwao ni mama mkwe, sasa wanapoona vijihesabu hapo juu
wanachanganyikiwa hahahahahaha!!! kwenye platform utakayokua unatumia karibu
kila mahesabu yamefanywa kwaajili yako, kwahiyo wewe iyakua ni kusoma tu, wala
usjali.

Jisajili XM Global

Wasiliana nami https://t.me/NFP24

Follow me on X

Jiunge na Channel yetu ya Telegram

You might also like