Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 4

Lot size, Pips, na Liverage.

Mambo vipi, natumaini somo la misamiati limekaa kidogo, japo linahitaji kujikumbushia ili
ikae kichwani vizuri, lakini usijali, kadri utakavyokua ukijihusisha na Forex, itazidi kukaa tu
kichwani. Sasa embu ngoja tuangazie upande wa namna gani kwa pesa yako ndogo
unaweza kufanya biashara kubwa na faida yako inakuaje.

Tulipokua tukizungumzia Pips, tuliona ni ule utofauti kati ya bei ya kipande kimoja cha
sarafu flani, ambayo wewe uliingilia sokoni mpaka mahali ambapo ipo kwa wakati flani,
ama iwe upande wa faida, au upande wa hasara. kwa mfano ulinunua kipande kimoja cha
Euro (yaani Euro moja) kwa Dollar 1.2154, kisha ikapanda mpaka kufikia bei ya 1.2155
inamaana ukizitoa izo bei utakuta zina utofauti wa 0.0001, ikimaanisha kwa kila Euro
moja uliyoinunua kwa bei ya mwanzo, ukija kuiuza kwa bei hii utakua na faida ya Dollar
0.0040 kwa kila Euro moja, ambayo sasa katika pips, kwavile hizo namba ni nne na sio 5,
hapo utakua na pips 1. Chukua mfano wa biashara ya mpunga, ukinunua magunia ya
mpunga kwa bei ya gunia 1 la mpunga kwa Shilingi 10000, ukasubiri bei ipande mpaka
10500 kisha ukayauza, inamaana utatengeneza faida ya shilingi 500 kwa kila gunia,
ndivyo ilivyo hata hapa.

Sasa embu angalia hiyo biashara ya hapo juu, yaani kwa hizo bei, ukiuza Euro 1 unapata
faida ya Dollar 0.004, ambayo ni ndoogo saana, yaani hata Dollar 1 haifiki!!! sasa
inatakiwa uuze vipande vingapi ili angalau uone faida ya kueleweka?! hapo ndipo ujuzi
wa Lot size unapokuja kutumika. Lot size ni idadi ya vipande vya fedha unavyoamua
kuvinunua ili uje uviuze kwa bei ya juu, au kuviuza ili uje uvinunue kwa bei ya chini zaidi
upate faida. Katika Forex, kuna makundi makuu matatu ya lot size, ambayo ni Standard
lot, Mini lot, na Micro lot. Ngoja tuyazungumzie hapa chini.

1. Standard Lot: Hii ndio idadi kubwa zaidi ya vipande katika forex, ambapo unakua
unauza au unanunua vipande 100,000 na hua inawakilishwa na 1. Kwahiyo, katika
trade yako upande wa lot size ukijaza 1 ujue unafanya biashara ya vipande laki moja,
ambapo tukichukua mfano wetu pale juu, kama kila kipande kitakupa faida ya
0.0001, ambayo ni pip 1, basi faida kamili itakua ni 0.0001 kuzidisha na vipande
100,000 ambayo itakua Dollar 10. Lakini pia ikiwa upande wa hasara, utakua na
hasara hiyohiyo ya Dollar 10. Kwa maana hiyo, kwa lot size ya 1, kila pip 1 itakupa
Dollar 10 ziwe faida ama hasara. Haufungwi kuweka lot ya 1 kama ukiamua kutumia
lot size hii, unaweza ukaweka Lot ya 2, ambayo ni vipande 200,000, lot ya 10
ambayo ni vipande 1,000,000 na kuendelea, lakini kwa mtu mwenye mtaji mdogo
haushauriwi kutumia aina hii ya lotsize, kwa sababu kwa siku bei inaweza ikaenda
hata zaidi ya pip 50, sasa chukulia mfano, una mtaji wa Dollar 100, ukaweka lot
size 1, kisha bei ikatembea kwa pip 10 tu kinyume na wewe, ina maana hasara yako
itakua hivi, kwa lot hii, kama pip 1 itakupa hasara ya Dollar 10, basi hizo pip 10
zitakupa hasara ya Dollar 100.!! inamaana mtaji wako wote tayari umeshaungua
hahahahahaha…!! lakini kuna mlafi mmoja anaetaka faida kwa haraka ataitumia,
shauri yake.!!
2. Mini Lot: Hii hua ni idadi ya kati ya vipande katika forex, na hua inakua na vipande
10,000 na kuandikwa kama 0.1, kwa maana hiyo, kwa trade yetu yenye pip 1, yaani
faida au hasara ya Dollar 0.0001 kwa kipande, tukizidisha kwa hivyo vipande vyetu
tunapata jumla ya Dollar 1 tu ya faida au hasara, hii pia unaweza kuiongeza kama
utaamua kuuza vipande vingi zaidi, ambapo unaweza kuiweka kama 0.2, 0.3,0.7 na
kuendelea. hii pia haushauriwi kuitumia, kwani haitochelewa kukukaushia mtaji,
kama ukiitumia, kwa mtaji wa Dollar 100, halafu bei iende pips 50 kinyume na wewe,
ambayo ni kasi ya kawaida kwa siku, utakua na hasara ya Dollar 50, yaani tayari nusu
ya mtaji wako imekatika.
3. Mini Lot: Hii ndio idadi ya chini zaidi ya vipande, ambayo inakua na vipande 1000 tu
na inaandikwa kama 0.01, ambapo kwa pip 1, yaani faida au hasara ya 0.0001 kwa
kipande, tukizidishia hapa tunapata jumla ya Dollar 0.1 tu ya faida au hasara.!! kuna
lilafi linaona kama hichi kifaida ni kidogo sana, litaelewa tu maana yake siku
likichoma account hahahaha.!! hapa kama bei itatembea pip 50 upande wa faida
utakua na faida ya Dollar 5, na ikiwa hasara itakua ya Dollar 5 pia, hauchomi account
kizembe japo hata faida pia itakua kidogo kidogo, ndo uvumilivu wenyewe. Ukihitaji
kuiweka mara mbili andika tu 0.02, mara tano 0.05, na kuendelea.

Sasa hebu jiulize kitu kimoja, kama bei ya Euro 1 ikiwa Dollar 1.2154, na tumeona idadi ya
chini zaidi ya vipande vya kuingia navyo sokoni ni lot ya 0.01 ambavyo ni vipande 1000,
sasa jumla ya Dollar zitakazotumika kununua hiyo idadi ya vipande ni 1.2154 mara 1000
ambayo ni Dollar 1215.4!!! sasa wewe kwa mta ji wako wa Dollar 100 utawezaje kufanya
biashara hii kama mtaji wako hauwezi kununua hata idadi ya chini zaidi ya vipande??!!
Hapa ndipo elimu ya Liverage inapoingia, twenzetu…

Liverage, tulisema ni kile kiasi cha pesa ambacho broker anakuongezea, ili uweze
kufanya biashara. Baada ya brockers kuona wateja wao wengi wana mitaji midogo
isiyoruhusu wao kufanya biashara kabisa, au kufanya biashara kidogo, wakaamua kuwa
wanawaongezea mitaji, ambayo wewe hutoiona kwenye account yako, ili waweze
kufanya biashara kubwa, wanunue na kuuza vipande vingi, maana mteja akifanya
biashara kubwa, hata faida ya broker nayo inakua kubwa. Pesa hii utaongezewa kulingana
na mtaji ulioweka, na hua inakua katika mfumo wa wastani, mfano 1:100, 1:200, 1:500,
1:1000, na vinginevyo. inamaanisha nini? kwa mfano kwa liverage ya 1:100, inamaanisha
kwa kila Dollar 1 unayoweka kama mtaji, basi broker anakuongezea dollar 100. Kwahiyo
ukifungua account ya Dollar 100 kama mtaji, broker atakuongezea dollar 100 mara 100,
ambapo utakua na dollar 10,000 japo wewe utakua unaiona ileile dollar 100 yako,
unaona sasa kwa dollar 10,000 unaweza ukafanya biashara nzuri.

Mimi ningekushauri uwe unachagua liverage ya 1:500 ili kwa mfano ukiweka dollar mia,
utakua na jumla ya dollar 100 mara 500 ambayo ni dollar 50,000! nyingi sana
kufanyia biashara!! Najua sasa unajiuliza, huyu broker ananipa hizi pesa zoote, je
nikizichoma si atapata hasara yeye?! hahahaha yeye sio mbulula kiasi hicho, pale
ambapo trade ulizoweka zitakua na hasara kiasi cha kufikia kile kiasi ulichoweka kama
mtaji, basi broker ataikata palepale ili pesa aliyokupa yeye isije ikaungua kwa upuuzi
wako.!! hahahahahaha na hapo ndipo tunasema umechoma account!!

Kwa kifupi…

Kwa lot ya…

1, pip 1 itakupa dollar 10


0.1, pip 1 itakupa dollar 1
0.01, pip 1 itakupa dollar 0.1

Liverage ndio kitu kinachoweza kufanya uchome account, tofauti na biashara zingine
ambapo hata ukiuza kwa bei ya hasara basi utapata walau pesa flani, lakini hapa kwa vile
umekopeshwa mtaji mkubwa unaweza kupata hasara kubwa sana, na inapofikia kiasi
ulichowekeza kwa brocker, basi anachukulia hiyo hasara yote ni yako, anachukua pesa
yake we unabaki mtupu.

Kwakweli, hili somo la leo, unaweza hata kulitumia kama vocha uongee na mpenzi
wako!! hahahahaha tukutane hapo mbele.

Jisajili XM Global

Wasiliana nami https://t.me/NFP24


Follow me on X

Jiunge na Channel yetu ya Telegram

You might also like