Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 2

MKATABA WA UPANGISHAJI NYUMBA

Mkataba huu umefanyika tarehe………. Mwezi…………...mwaka……….… kati ya Ndugu


ASHA SAIDI ACHIMPATE WA SHANGANI, MTWARA ambaye ni mwenye nyumba
iliyopo Mangowela na Ndugu…………………………………………………………………..….. wa
Mtwara

MAKUBALIANO

1. Mkataba huu unahusu nyumba inayokodishwa kwa matumizi ya makazi tu kwa muda
wa miezi…………. Kuanzi tarehe ……….. Mwezi………..mwaka………….. Hadi
tarehe……….…mwezi……….... mwaka………... kwa malipo ya
Tshs………………………..….Kwa mwezi ambayo kwa miezi ………..… sawa na
Tshs………………………………….….
2. Pango linaweza kubadilika wakati wowote kutegemea maboresho ya jengo.
3. Mabadiliko yoyote ya pango yatolewe taarifa kwa mpangaji ndani ya miezi mitatu (3)
kabla ya pango kumalizika.
4. Pia mpangaji kama atahitaji kuendelea kukodi nyumba anatakiwa atoe taarifa kwa
mwenye nyumba miezi mitatu (3) kabla ya kumalizika mkataba.
5. Endapo mwenye nyumba atasitisha mkataba huo kabla kumalizika mwenye nyumba
itabidi kurudisha kodi ya nyumba ya miezi yote iliyobaki.

Pia endapo mpangaji atasitisha mkataba mpangaji hatarudishiwa kodi yake ya miezi
iliyobaki.

MASHARTI YA UPANGISHAJI

1. Mpangaji atatumia vyumba/nyumba katika hali ya usafi kwa muda wote wa mkataba
huu
2. Mpangaji atamruhusu mwenye nyumba kwa muda wowote ule unaofaa kuingia ndani
ya nyumba ili kufanya ukaguzi baada ya kupokea taarifa isiyofaa.
3. Mpangaji haruhusiwi kufanya mabadiliko ya nyumba, kujenga kwa kuongeza kitu
chochote bila ruhusa ya mwenye nyumba au wakala wake.
4. Mpangaji atalipa bili ya maji na umeme endapo vifaa kama bulb tube, tube light, switch
za kuwashia umeme zimeharibika mpangaji ndipo atalazimika kununua na kuvifunga
au kuvipachika.
5. Vifaa vya bomba kama vile bob cork water tap na vitasa na kadhalika vikiharibika ni
jukumu la mpangaji kununua vifaa hivyo na kuvifunga sehemu husika.
6. Mpangaji haruhusiwi kutupia takataka au vitu vigumu chooni au ndani ya chemba za
choo na endapo bomba za maji machafu zimeziba kwa kutupia vitu vigumu mpangaji
atalazimika kuzibua kwa gharama zake.

Mpangaji anapaswa kulipa pango kabla ya kuingia na kila baada ya kuisha kwa pango lake.

Mwenye nyumba na mpangaji kwa pamoja tumekubaliana na masharti yaliyomo kwenye


mkataba huu.

JINA LA MWENYE NYUMBA…………………………………………………………………………..

SAHIHI YA MWENYE NYUMBA…………………………..

NAMBA YA SIMU ……………………………………….. TAREHE…………………………………

JINA LA MPANGAJI……………………....…………………………………………………………….

SAHIHI YA MPANGAJI……………………………………..

NAMBA YA SIMU ……………………………………….. TAREHE…………………………………

You might also like