Professional Documents
Culture Documents
Katiba Fci
Katiba Fci
1. Katiba hii itajulikana kama katiba ya Shirika lisilo la kiserikali la Foundation For
Community Involvement (FCI)
2. Katiba hii itaanza kutumika mara tu Shirika litakaposajiliwa
IBARA 2:Tafsiri
IBARA 3:Utangulizi
Kwakuwa: Tunatambua kuwa jamii yoyote yenye maendeleo endelevu hutokana na ushiriki wa
wananchi katika kupanga na kutekeleza shughuli za maendeleo.
Kwakuwa ;ushiriki huu ujenga uendelevu wa miradi na usawa katika matumizi ya rasilimali za
nchi kwa kuzingatia makundi ya watu wenye mahitaji maalumu wakiwemo
vijana ,wanawake,wazee,na watu wenye ulemavu na watoto
Hivyo ; kwa kuzingatia uwezo na nia tuliyonayo kwa kauli moja tumeamua kuanzisha shirika
hili kwa nia ya kuhamasisha ushiriki wa jamii katika shughuli za maendeleo kwa kuzingatia haki
na usawa wa kijinsia kwa watu wote wenye mahitaji maalumu.
Kuwa na jamii imara yenye Afya bora na maendeleo endelevu ya kijamii na kiuchumi.
IBARA 11: Kauli ya Dhamira
1. Kujenga uwezo jamii ya watu wenye mahitaji maalumu juu ya stadi za maisha na
ujasiliamali.
2. Kuhamasisha jamii juu ya ushiriki sawa wa shughuli na miradi ya maendeleo.
3. Kutetea haki za binadamu kupitia uraghabishi na uchechemuzi wa Sera na Mikakati
mbalimbali.
4. Kuamsha mwamko wa wananchi katika kutambua na kulinda haki za watu walio katika
makundi maalumu.