HAYA NDIYO QUR'an IMENIFUNZA-Qur'an Na Uthibitisho Wa Sayansi Ya Karne Ya Ishirini Na Moja

You might also like

Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 165

HAYA NDIYO QUR‟AN

IMENIFUNZA:
(Toleo la Pili)

Qur‟an na Uthibitisho wa Sayansi, Teknolojia na Gunduzi


za karne ya Ishirini na moja

Abuu Farheen Farid

IbnuRajab Allhassany

1
HAYA NDIYO QUR‟AN IMENIFUNZA:
(Toleo la Pili)
Qur‟an na Uthibitisho wa Sayansi, Teknolojia na Gunduzi
za karne ya Ishirini na moja

Barua pepe: faridhamad78@gmail.com


Simu: +255 748 202 226
Whatsapp: +255 777 002 226
Dar es Salam, Tanzania.

ISBN: 978-9912-40-528-8

Kimerejelewa na:
Shaykh Mohamed Abbas,
Mkurugenzi,
African Muslim Agency,
Tawi la Tanga.

Al-Akh Mohamed Abdallah Kifosha,


Tanga,
Tanzania.

Mpiga chapa:
Truth Printing Service
geofreymakula@gmail.com
Ubungo, Dar es Salam, Tanzania.

2
UFUNGUO WA KITABU

Allah (Subhanahu) anasema ndani ya Surat Al-Baqarah;


“Hichi ni Kitabu (Qur‟an) kisichokua na shaka ndani
yake; ni uwongofu kwa wachamungu. Ambao huyaamini
ya ghaibu na hushika Sala, na hutoa katika tuliyo wapa.”
(02:2-3)
Allah (Subhanahu) amesema aidha;
“Na ikiwa mna shaka kwa hayo tuliyo mteremshia mja
wetu basi leteni sura moja ya mfano wake, na muwaite
mashahidi wenu badala ya Allah, ikiwa mnasema kweli”
(02:23)
Allah (Subhanahu) amesema pia ndani ya Surat An-Nur;
“Allah ni Nuru ya Mbingu na Ardhi. Mfano wa Nuru yake
ni kama vile shubaka lenye kuwekwa ndani yake taa.
Taa ile imo katika tungi. Tungi lile ni kama nyota inayo
meremeta, inayo washwa kwa mafuta yanayo toka
katika mti ulio barikiwa, mzaituni. Si wamashariki wala
magharibi. Yanakaribia mafuta yake kung‟aa wenyewe
ingawa moto haujayagusa- Nuru juu ya Nuru. Allah
humwongoa kwenye Nuru yake amtakae. Na Allah
huwapigia watu mifano. Na Allah ni Mwenye kujua kila
kitu.” (24:35)

3
YALIYOMO:
UFUNGUO WA KITABU............................................................................................... 3
KUHUSU KITABU: .................................................................................................... 6
MAKOSA YA CHAPA NA UANDISHI: ...................................................................... 7
DIBAJI ....................................................................................................................... 8
SHUKRANI............................................................................................................... 10
UTANGULIZI ........................................................................................................... 12
HISTORIA YA KUSHUSHWA KWA QUR‘AN TUKUFU......................................... 16
JE! QUR‘AN IMEPITWA NA WAKATI AU IPO MBELE YA WAKATI .................. 20
UTHIBITISHO NDANI YA QUR‘AN ....................................................................... 21
Qur‘an na Sayansi, Teknolojia na Teknohama .............................................. 22
Qur‘an na Asili ya Ulimwengu (The Big Bang Theory) ............................. 24
Qur‘an na Sayansi ya Anga (Astrology)...................................................... 26
Qur‘an na Uhusiano wa Wakati (Time Relativity) ..................................... 29
Qur‘an na Sayansi ya safari za anga za mbali (Space Travelling) .......... 33
Qur‘an na Sayansi ya asili na maendeleo ya kukuwa kwa Mwanadamu
(Embryolojia) .................................................................................................. 43
Qur‘an na Kalenda (Moon and Solar Calenders) ....................................... 56
Qur‘an na Nguvu ya mvutano (Force of Gravity)...................................... 58
Qur‘an na Kemia ya Mmenyuko (Kutu/Rust) ............................................. 74
Qur‘an na Sayansi ya Milima ........................................................................ 78
Qur‘an na Gunduzi za vyanzo vya Moto ..................................................... 83
Qur‘an na Sayansi Anatomia ya Viumbe .................................................... 85
Qur‘an na Sayansi ya Bahari (Oceanography) .......................................... 91
Qur‘an na Sayansi ya Hyndrolojia (Mzunguko wa Maji) ........................ 101
Qur‘an na Sayansi ya Alama za Vidole ..................................................... 105
Qur‘an na sababu za makatazo ya muziki ............................................... 108
Qur‘an na Sayansi ya Wanyama (Zoolojia) .............................................. 119
Qur‘an na Matokeo ya Sayansi ya Kitabibu ............................................. 125
Qur‘an na Sayansi ya vita vya anga .......................................................... 145

4
Qur‘an na Sayansi ndani ya Tetemeko la Ardhi ...................................... 153
Qur‘an na Sayansi ya Mwisho wa Ulimwengu (The Big Crunch Theory)
....................................................................................................................... 158
HITIMISHO ........................................................................................................... 163
REJEA ZA KITABU: .............................................................................................. 165

5
KUHUSU KITABU:

„Haya ndiyo Qur‟an Imenifunza‟ ni chapisho ambalo


husheheni uchambuzi na ufafanuzi wa kina ndani ya Qur‘an.
Chapisho hili lilianza kwa toleo lake la kwanza ambalo lilibainisha
na kutoa baadhi ya nukta muhimu ambazo waandishi
wamejifunza na kufaidika na elimu yake kupitia Qur‘an tukufu.
Malengo makubwa ya kuandaa machapisho haya ni kuifikia jamii
kielimu kwa nukta ambazo waandishi wamezipitia na kukusanya
baadhi ya mafunzo muhimu ndani yake. Mafunzo ambayo
yamekusanywa kupitia katika vitabu mbali mbali vya wafasiri wa
Qur‘an.
Machapisho na maudhui ya „Haya ndiyo Qur‟an Imenifunza‟
katika hatua hii yamekuja na toleo la pili ambalo limefafanua na
kuchambua kwa kina namna ambavyo waandishi wamejifunza
matokeo kadhaa ya Kisayansi na maendeleo ya Kiteknolojia ya
karne ya ishirini na ishirini na moja yalivyobainishwa kwa kina
ndani ya Qur‘an tukufu. Toleo hili limebeba tafiti, uchambuzi
sambamba na maelezo ya kina juu ya namna ambavyo sayansi
na teknolojia inavyoendelea kuikiri Qur‘an kwa vitendo, matukio
na maandishi yenye kutunzwa na kunukuliwa katika nyanja
mbali mbali duniani.
Kupitia toleo hili, utajifunza namna ambavyo masuala kadhaa ya
kisayansi yalivyofafanuliwa ama kutolewa ishara zake ndani ya
Qur‘an. Qur‘an ambayo alishushiwa Mtume Muhammad (Rehma
na Amani ziwe juu yake) katika karne ya saba. Utajifunza na
kuelimika namna ambavyo matokeo kadhaa wa kadhaa ya
gunduzi za kisayansi katika karne ya ishirini na ishirini na moja
yanavyoendelea kuitumia Qur‘an kama chanzo kikuu cha elimu
ambayo huhitaji uchambuzi wa kitaaluma kuweza kufahamika.
Matokeo makubwa ya kisayansi juu ya kuumbwa kwa
ulimwengu, sayansi ya bahari, milima, uzazi wa mwanadamu, na
mengine mengi tuliyoyakusanya ndani ya Kitabu hichi ndiyo
ambayo Qur‘an Imetufunza.

6
MAKOSA YA CHAPA NA UANDISHI:

Alhamdulillah, sifa zote anastahiki Allah (Subhanahu) muumba


wa mbingu na ardhi. Ambaye ameturuzuku neema ya Uislamu
na Qur‘an kuwa ni Dira na Muongozo wa maisha yetu. Mbali na
neema hizo zote, yeye ndiye alietuumba wanadamu katika
umbile lililo bora na kisha akatujalia sifa ya upungufu katika kila
jambo tulitendalo. Kwa minajili hiyo, natanguliza samahani kwa
kila nukta ambayo itabainika kuwa na mapungufu katika hatua
zote, hakika ukamilifu ni wake Allah (Subhanahu) kila kazi ama
amali ya mwanadamu haikosi kuwa na mapungufu. Hivyo,
nawaomba ndugu zangu wasomaji kunipa udhru katika nukta
yoyote ambayo itabainika kuwa na makosa katika uandishi ama
uchapaji. Namuomba Allah (Subhanahu) awape elimu yenye
manufaa na awajaalie ufahamu na mazingatio katika kila nukta
ndani ya Kitabu hichi. Aamin.
Abuu Farheen Farid Bakar Hamad

7
DIBAJI

Bismillahir Rahmanir Rahim,


Sifa njema anazistahiki Allah mtukufu, bwana wa viumbe vyote,
mwingi wa Rehema na Uweza, Na sala na salamu zimuendee
mbora wa viumbe, na mjumbe wa Allah Muhammad (Rehema
na Amani ya Allah imshukie), aliyetumwa kwa viumbe wote.
Amma baadu:
Hatunabudi kurejesha shukrani za dhati kwa Allah mtukufu
ambaye ametuwafikisha kutekeleza yale aliyotuwajibishia. Kama
ambavyo pia tuna muomba Allah mtukufu atupe mwisho
mwema.
Namshukuru ndugu yangu Abuu Farheen Farid Bakari Hamad,
na wenzie alioshirikiana nao (Allah awahifadhi) kwa kuniteuwa
kuwa miongoni mwa wenye kuandika dibaji ya kitabu hiki
kinacho zungumzia Qur‟an na Uthibitisho wa Sayansi,
Teknolojia na Gunduzi za karne ya Ishirini na moja,
ambacho amekiita: "Haya ndiyo Qur‟an Imenifunza", kwa
uweza wa Allah mtukufu nimekipitia kitabu chote mwanzo hadi
mwisho na nikabaini kwamba ni kitabu muhimu sana chenye
faida kubwa sana hasa kwa jamii ya karne hizi tunazo ishi na
hata zijazo.
Kitabu hiki kitakua ni msaada kwa wale waliosoma Qur‘an na
wakawa hawakubahatika kusoma Sayansi, na pia kwa wale
waliosoma sayansi na wakawa hawakubahatika kusoma Qur‘an,
bali kwa wale walio jaaliwa kusoma vyote viwili, kitakuwa ndio
zaidi.
Maashaallah, kitabu kimesheheni vipengele vya nyanja zote
zinazoelekeza kujikita katika kumtambua Allah mtukufu,
muumba wa ulimwengu na vilimwengu na hatimaye kumuabudu
na kumpwekesha katika ibada.
Namuomba Allah mtukufu awabariki na kuwaandalia malipo
makubwa katika mizani ya mema yao wote walioshiriki katika

8
kufanya upembuzi huu wakakusanya majumui kutoka katika
rejea mama na za msingi.
Mapungufu ya kibinadamu hayakosekani, hivyo tuna waasa
wasomaji wa kitabu hiki wakiona madosari madogo madogo
wajue kwamba ni ya kibinadamu kwani mkamilifu ni Allah
mtukufu pekee.
Wabillahi Tawfiq.
Shaykh Mohammad Abbas

9
SHUKRANI

Tumekuwa tukiishi na ndoto za kukamilisha toleo hili la pili la


maudhui yetu pendwa ya „Haya Ndiyo Qur‟an Imenifunza‟
mara tu baada ya kukamilika kwa toleo la kwanza ambalo
tulilichapisha mapema mwaka 2022 katika mwezi mtukufu wa
Ramadhani.
Alhamdulillah, kwa idhini yake Allah (Subhanahu) na mamlaka
yake ya kuturuzuku afya, ari, na uhai imetuwezesha kukamilisha
chapisho hili adhimu. Sifa na stahiki zote za shukrani ni zake
Allah (Subhanahu) mdhamini na mmiliki wa kila jambo hapa
duniani na akhera.
Sala njema na Salamu tunazitanguliza kwa mtukufu wa darja,
Mtume Muhammad (Rehma na Amani ziwe juu yake) pamoja
kuwapelekea salama na Amani hizo kwa jamaa zake, wake zake,
maswahaba zake, na wote watakaomfuata katika wema mpaka
siku ya mwisho.

Kadhalika, natanguliza shukrani za dhati kwa wote walioshiriki


kwa namna moja ama nyengine katika hatua zote za uandaaji,
utayarishaji hadi ukamilishaji wa chapisho hili, kwa hakika
wamekuwa na nafasi kubwa katika kila nukta ya mafanikio yote
ya chapisho hili.
Aidha, nitakuwa mchoyo wa fadhila kama nisipo mshurukuru
kwa dhati kabisa Shaykh Mohammad Abbass ambae ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya African Muslim Agency Tawi
la Tanga kwa kujitoa kwake kukipitia na kukirejea kitabu hiki,
pamoja na uadhishi wake mzuri wa dibaji yenye kutoa dira
madhubuti kwa msomaji.
Ama kwa upande mwengine, napenda kuwashukuru wadau
wote ambao kwa namna ya pekee wamekuwa ni msaada
mkubwa katika hatua zote muhimu za chapisho hili. Wamekua
mstari wa mbele kuhakikisha kwamba chapisho hili linakamilika
na kuhakikisha lengo kuu la matayarisho na uchapishaji wa

10
kitabu hiki linafikiwa. Kwa muktadha huo namshukuru sana
Shaykh Mohamed Rajab (Ibnrajab), Al-Akh Mohamed Abdallah
Kifosha, Mudir Mussa Abdallah Amir, pamoja na wote ambao
wamekua ni viungo muhimu katika kila nyanja ya ukamilishaji
wa chapisho hili.
Kwa ujumla, namuomba Allah (Subhanahu) ampe kila mmoja
mema na rehma zake, aweke wema na mchango wao katika
chapisho hili katika mizani ya matendo yao mema. Namuomba
Allah (Subhanahu) awape kila hitajio la nafsi zao, awawaruzuku
afya, hekima, na taqwa ya kuendelea kuitumikia dini na jamii ya
Kiislamu kwa ujumla. Aamin.
Abuu Farheen Farid

11
UTANGULIZI

َ ُّ‫﴾ ٱ ْق َس ْأ َو َزب‬٢﴿‫ي َعلَق‬


‫ك‬ ْ ‫ًسبىَ ِه‬
َ ‫ٱإل‬
ِ ‫ق‬ َ ﴾١﴿‫ق‬
َ َ ‫خل‬ َ َ‫خل‬
َ ‫ك ٱلَّ ِري‬
َ ‫ن َز ِب‬ ْ ِ‫ٱ ْق َس ْأ ب‬
ِ ‫ٱس‬
﴾٣﴿‫ٱأل َ ْك َسم‬

‖Soma kwa jina la Mola wako aliyeumba. Amemuumba


mwanadamu kwa pande la damu. Soma na Mola wako ni
mkarimu sana.‖ (96:1-3)
Tangu kuumbwa kwa viumbe (Wanadamu) hapa duniani,
wasomi na watafiti nguli wa sayansi wamekuwa wakiendelea
kujaribu kuifahamu na kuijua asili, sababu na madhumuni
makuu ya kuumbwa kwao. Jitihada na tafiti hizo zikazalisha
dhana mbali mbali zikiwa kama matokeo ya gunduzi zao. Kupitia
dhana hizo watu wengi wakaegemea na kuzitakidi kuwa ndio
misingi mikuu ya imani zao.
Dini na vitabu mbali mbali vya kiimani vikaundwa na kutungwa
ikiwa ni matokeo ya gunduzi na tafiti zilizowashibisha wafuasi
kutoka katika majaribio kadhaa ya kuijua asili ya mwanadamu
hapa ulimwenguni. Kadhalika, katika utafutaji wa kujua asili ya
kuumbwa kwa mwanadamu na ulimwengu kwa ujumla,
iliwachukuwa miaka na mikaka, karne na dahari, huku
ukiwapitisha watafiti na wafuasi wao katika ustarabu, mila, na
imani mbali mbali. Mwishowe, zikazaliwa dini na imani za
kupangwa ambazo zilifunganishwa na vitabu vilivyo aminika na
wafuasi wao kuwa vinavyo asili ya ufunuo wa kimungu. Kwa
upande mwengine, wengine wakiamini na kutakidi imani zao
katika dini za kutungwa ambazo kwa kiasi kikubwa ziliegemea
moja kwa moja katika uzoefu tu wa kibinadamu.
Historia inatueleza kuwa, matokeo ya tafiti hizi yalizalisha
matabaka mengi miongoni mwa wanadamu, ambao
walitegemea zaidi mafundisho kutoka kwa watafiti na wafuatiliaji
wa masuala ya asili ya mwanadamu. Katika kuyathibitisha
matokeo ya utafutaji wa ukweli juu ya asili ya mwanadamu na
matokeo yake; Imam Ibn Jawzy (Rehma za Allah ziwe juu yake)
alieleza katika kitabu chake mashuhuri ‗Talbis Iblis‘ kuwa

12
matokeo ya tafiti hizo, yalizalisha makundi manne makubwa.
Makundi hayo akayafafanua na kuyabainisha namna ambavyo
zilijengwa imani zao, na kutakidi juu ya kuumbwa kwa viumbe
na ulimwengu kwa ujumla.
Imam Ibn Jawzy (Rehma za Allah ziwe juu yake) akaeleza kuwa
tafiti hizo zilizalisha kundi la Wasekula (Kundi la Watu wasio na
dini) ambao waliamini kuwa hakuna Mungu wala Muumba, na
vitu vyote vinavyoonekana katika ulimwengu, pamoja na
ulimwengu wenyewe vilikuwepo na vitaendelea kuwepo bila ya
uwepo wa Mungu wala Muumba, na hakuna nguvu yoyote
ambayo imeanzisha na inayoweza kusimamia kuendeleza
matukio ya viumbe na ulimwengu wao.
Kutokana na matokeo ya utafiti wao walikanusha uwepo wa
Mungu kwa sababu walishindwa kumfahamu kwa hisia zao na
wakashindwa kutumia akili zao. Kutokana na imani zao hizo, Ibn
Jawzy (Rehma za Allah ziwe juu yake) alieleza kuwa kwa mtu
mwenye akili timamu sio rahisi kwake kutilia mashaka uwepo wa
Muumba. Kwani katika hali ya kawaida, mtu akipita kwenye
kipande cha ardhi kisicho na majengo, kisha akarudi na kukuta
ukuta umejengwa hapo atagundua kuwa lazima kulikuwa na
mjenzi aliejenga ukuta huo.
Kundi la pili ni kundi la Wanaasili (Naturalist), ambao waliamini
kuwa kila kitu katika huu ulimwengu hakikuumbwa na yoyote,
bali ni matokeo ya uoto wa asili. Wakaamini kuwa ulimwengu na
walimwengu wote umezaliwa na vipengele vinne muhimu
ambavyo ni Dunia, Maji, Mito na Anga. Katika imani yao ni kuwa
vipengele hivyo vinne ndivyo haswa chanzo cha asili ya
ulimwengu na walimwengu kwa ujumla wake.
Ama kwa upande mwengine, Ibn Jawzy (Rehma za Allah ziwe
juu yake) akaeleza kuwa kundi la tatu katika matokeo ya tafiti
za asili, waliamini juu ya ushirika wa uwili (Dualist) waliamini
kuwa ulimwengu umeumbwa na unaendeshwa na nguvu za
miungu wawili ambao ni Muumba mwema na Muumba muovu.
Wakisema kuwa Muumba mwema ni muumba wa mwangaza na
muumba muovu ni Muumba wa giza. Imani yao ikaegemezwa
13
kuwa miungu hiyo miwili ndio miungu ya milele ambayo daima
walikuwa na watakuwa na nguvu juu ya kujua, kusikia, kuona
na mengi mengine ambayo yatahakikisha ustawi mzuri wa
ulimwengu na walimwengu. Dhana na imani hizi, ndizo ambazo
siku zote huwatoa viumbe katika kumtambua na kumjua
Muumba wa hakika na kuwazuia watu kujua ubainifu wa hakika
katika kumtambua Muumba wa kweli.
Kundi la nne ambalo lilizalishwa na jitihada za utafutaji wa
ukweli na hakika ya kuumbwa kwa ulimwengu na viumbe ni
kundi la Wanafalsafa, ambao kwa mujibu wa Ibn Jawazy
(Rehma za Allah ziwe juu yake) ni miongoni mwa waliokumbwa
na hadaa na vitimbi vya ibilisi (Laana za Allah ziwe juu yake).
Aliwahadaa na kuwafanya waamini juu ya maoni, mawazo, fikira
na mitazamo ambayo haitegemei mafundisho ya unabii, Uungu
wala imani yoyote isipokuwa kile wanachokitafakari na kukiwaza
viongozi wao. Wanafalsafa waliamini na kuabudu mawazo na
mitazamo ya viongozi wao, huku kila jambo katika ulimwengu
walilihukumu na kutoa miongozo kwa mujibu wa mitazamo hiyo.
Baadhi ya wanafalsafa, kupitia Imani yao yaliegemea zaidi na
kuamini mawazo na matokeo ya kundi la wanaasili (wasio amini
dini) ya kwamba ulimwengu hauna Muumba wala mwenye
kuusimamia. Kwamfano, miongoni mwa mawazo ya wanafalsafa
walidai kuwa dunia ni sayari iliyo katika utupu wa ulimwengu, na
kwamba kila sayari ina walimwengu wake kama ilivyo sayari ya
dunia. Wote katika wanafalsafa wanaamini kuwa dunia haina
mwisho kama ambavyo haikuwa na mwanzo.
Kutokana na ukweli kuwa dhana zote hizo hazina hakika. Kupitia
Qur‘an tukufu aliyoteremshiwa Mtume wa Allah (Sala na Salam
ziwe juu yake) ambayo ndio inayothibitisha kwa wazi na
ufafanuzi murua ambao unakinaisha juu ya asili ya kuumbwa
kwa Ulimwengu na walimwengu. Vile vile, Qur‘an ndio kitabu
pekee ambacho kadiri miaka na karne zinavyokwenda, ndivyo
mambo kadhaa yanaendelea kuthibitishwa ndani yake. Mbali na
masuala kadhaa kuhusu kuumbwa kwa ulimwengu na
walimwengu, Sayansi na miamala mbali mbali ya kijamii, kitaifa

14
na kimataifa imeendelea kuikiri Qur‘an kwa vitendo na
maandishi.
Kutokana na msingi huu sasa, kila mwenye akili timamu, humili
kuamini kuwa dhana pekee ambayo itahakikisha na kuaminika
kuwa ndio ya hakika ni sharti kuwa, dhana ama imani hiyo iwe
imekamilika na kuaminika kuwa imetoka moja kwa moja kwa
Muumba. Qur‘an ikiwa ndio chanzo kikuu cha Imani ya Kiislamu,
na ndio kitabu kinachofuatwa na kutegemewa na waumini wake.
Waislamu wanaamini kuwa Qur‘an ni muongozo kwa viumbe
wote. Hii ni kwa sababu ujumbe wa Qur‘an unaaminika kuwa ni
wa nyakati zote na unapaswa kuwa muhimu kwa kila zama.
Kutokana na asili ya kushushwa kwa Qur‘an, pamoja na yale
ambayo imejumuisha ndani yake, ni dhahiri kuwa Qur‘an
inatosha kutoa majibu ya uhakika juu ya kila jambo. Jambo hilo
liwe ni la kiimani, kiitikadi, kitabibu, kidiplomasia ama miamala
mengine muhimu ndani ya jamii ya Kitaifa na Kimataifa.
Kutokana na ukweli huo, huenda kama kila mmoja katika
kuutafuta ukweli wa uhakika wa kuumbwa kwa ulimwengu,
wangelijikita katika kutafuta ukweli huo kupitia Qur‘an, basi
kusingekuwa na mapote ya dhana ambazo hazina mashiko.

15
HISTORIA YA KUSHUSHWA KWA QUR‟AN TUKUFU

Qur‘an ilianza kumshukia Mtume Muhammad (Swala na amani


ziwe juu yake) mwaka 610 A.D. alipokuwa na umri wa miaka
arubaini. Mtume Muhammad (Swala na amani ziwe juu yake)
alianza kushushiwa Qur‘an akiwa pangoni katika mlima Hira
(Jabal Hira) katika usiku wa mwezi wa Ramadhani kama Qur‘an
yenyewe inavyotufahamisha:

‖Ni mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa hii Qur‘an‖


(2:185)

Allah (Subhanahu) anasema pia;

"Hakika Tumeiteremsha (Qur‘an) katika Laylatul-Qadr (usiku


wenye hishima kubwa). Na jambo gani litakujulisha (hata
ukajua) ni nini huo usiku wenye hishima kubwa? Huo usiku wa
hishima ni bora kuliko miezi elfu. Huteremka Malaika na roho
(Jibriil) katika usiku huo kwa idhini ya Mola wao kwa kila jambo.
Ni amani (usiku) huo mpaka mapambazuko ya alfajiri." (97:1-
5)

Tunajifunza kutokana na aya hizi kuwa mwezi wa Ramadhani


umetukuzwa kutokana na Qur‘an kuanza kushuka katika mwezi
huu. Pamoja na funga kufaradhishwa kwa umma za Mitume
wote wa Allah (Subhanahu); kwa upande wa umma wa Mtume
Muhammad (Rehma na Amani ziwe juu yake), funga
imefaradhishwa iwe katika mwezi wa Ramadhani ili iwe ni
pamoja na kusherehekea kushuka kwa Qur‘an na kilele cha
sherehe hii kinakuwa katika usiku wa hishima (Laylatul-Qadr)
ambamo Qur‘an ilianza kushuka.

Mtume (Swala na amani ziwe juu yake) alikuwa akizidisha


kusoma Qur‘an katika mwezi huu na alikuwa akikaa Itiqaf katika
kumi la mwisho la Ramadhani ili aweze kudiriki kilele cha
sherehe. Usiku wenye hishima (Laylatul-Qadr) ulifichwa kwa
Mtume (Swala na amani ziwe juu yake) lakini alifunuliwa na

16
Mola wake kuwa unapatikana katika kumi la mwisho la
Ramadhani. Ni sunnah kwa Waislamu kuzidisha kusoma Qur‘an
katika mwezi mzima wa Ramadhani na kukaa Itiqaf katika kumi
la mwisho, ili kushiriki kikamilifu katika sherehe ya kumbu
kumbu ya kuanza kushuka Qur‘an. Historia ya kuanza kushuka
Qur‘an kwa Mtume Muhammad (Swala na amani ziwe juu yake)
kupitia kwa Malaika Jibril (Alaihi Salam) inasimuliwa vyema
katika Hadith ya bibi 'Aisha (Radhi za Allah ziwe juu yake)

Bibi 'Aisha (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema: "Kilichoanza


katika Wahyi wa Mtume (Swala na amani ziwe juu yake) ni
ndoto za kweli. Alikuwa Mtume (Swala na amani ziwe juu yake)
haoti chochote isipokuwa kilitokea kama alivyoota. Kisha akaona
ni bora kujitenga. Akawa anakwenda Jabal Hira kujilinda na
maovu. Basi alikuwa anakwenda Jabal Hira akifanya ibada
masiku mengi na alichukua masurufu kwa ajili hiyo.

Masurufu haya kila yalipokwisha alirudi tena kwa Bibi Khadija,


aliemtayarishia masurufu kama yale (ya kwanza) mpaka
ikambainikia haki akiwa pangoni Hira. Basi akamjia Malaika
(Jibril) humo pangoni akamuamrisha kusoma, Mtume (Swala na
amani ziwe juu yake) alijibu: "Sijui kusoma". Alinibana kwa
nguvu mpaka nikahisi taabu. Kisha akaniachia na kuniamrisha
tena kusoma na nikajibu: Sijui kusoma: Kisha akanibana tena
kwa nguvu kwa mara ya pili mpaka nikahisi taabu. Kisha
akaniachia na kuniamrisha tena kusoma. Nilijibu tena, "sijui
kusoma". Akanikumbatia tena kwa nguvu kwa mara ya tatu
mpaka nikahisi mashaka, kisha akaniachia na akasema:

"Soma kwa jina la Mola wako aliyeumba. Amemuumba


mwanaadamu kwa pande la damu. Soma na Mola wako ni
Karimu sana. Ambaye amefundisha kwa msaada wa kalamu.
Amemfundisha mwanaadamu mambo aliyokuwa hayajui."
(96:1-5)
Mtume wa Allah alirejea na Wahy huu, huku akitetemeka kwa
khofu aliyokuwa nayo. Alikwenda kwa mkewe Khadijah na
akamhadithia yale yote yaliyomtokea kisha akasema; "Nakhofia

17
kuwa kitu kinaweza kunitokea ". Khadijah alijibu: "Hapana!
Naapa kwa jina la Allah, Allah (Subhanahu) hatakufedhehesha.
Unakaa vizuri na kuwafanyia wema ndugu na jamaa zako,
unawasaidia masikini na fukara, unawakirimu wageni na
unawasaidia waliokabiliwa na matatizo. "Kisha Bibi Khadijah
alimchukua Mtume (Swala na amani ziwe juu yake) mpaka kwa
bin-ami yake, Waraqa bin Naufal bin Asad bin Abdul Uzza,
ambaye alikuwa Mkristo. Waraqa wakati huo alikuwa mzee sana
na alikuwa hawezi kuona tena. Khadijah alimuambia Waraqa
"Sikiliza hadithi ya mpwa wako, Ewe Bin-ami yangu" Waraqa
aliuliza, "Ewe Mpwa wangu umeona nini?" Mtume wa Allah
alimuhadithia habari yote kama alivyoona. Waraqa akasema:
"Huyu ni yule mtunza siri (Malaika Jibril) ambaye Allah
(Subhanahu) alimtuma kwa Mussa. Natamani ningelikuwa kijana
na kuishi mpaka wakati huo watu wako watakapokukataa na
kukufukuza." Mtume wa Allah (Subhanahu) akauliza:
"Watanifukuza?" Waraqa akajibu kuwa watafanya hivyo na
akasema, "Yeyote aliyekuja na kitu kama hicho ulichokuja nacho
alifanyiwa uadui na watu wake, na ningejaaliwa kubakia hai
mpaka siku hiyo watu wako watakapokufukuza, ningelikusaidia
kwa hali na mali." Lakini baada ya muda mfupi Waraqa alifariki
na Wahyi mwingine ulikawia kuja kwa kipindi kirefu. (Sahihi
Bukhari)
Tunajifunza kutokana na Hadith hii kuwa kabla Mtume (Swala
na amani ziwe juu yake) hajaanza kushushiwa Qur‘an kupitia
kwa Malaika Jibril (Alaihi Salam) alikuwa akipata Wahy kwa njia
ya ndoto.
Qur‘an yote kwa ujumla imehifadhiwa katika ubao mtukufu wa
Allah (Subhanahu) ulio katika Arshi yake kama
tunavyofahamishwa katika Qur‘an:

"Bali hii ni Qur‘an tukufu iliyotolewa katika Lawhi Mmahfuudh


(huo ubao uliohifadhiwa)." (85:21-22)

Kisha kutoka Lawhi Mmahfuudh Qur‘an ilishushwa mpaka


wingu wa kwanza. Kisha kutoka humo ikashushwa kidogo
kidogo kwa Mtume (Swala na amani ziwe juu yake) kupitia kwa

18
Malaika Jibril (Alaihi Salam) kwa kipindi chote cha Utume cha
miaka ishirini na tatu.

"Kwa hakika hii (Qur‘an) ni kauli (aliyokuja nayo) Mjumbe


Mtukufu (Jibril), Mwenye nguvu na cheo cha hishima kwa Allah
(Subhanahu). (81:19-20)
Kama tunavyojifunza katika Hadith, aya za mwanzo kumshukia
Mtume (Swala na amani ziwe juu yake) ni aya tano za mwanzo
za suratul-‘Alaq. Aya zilizofuatia katika sura hii (96:6-19)
zilishuka siku za baadaye. Aya ya mwisho kumshukia Mtume
(Swala na amani ziwe juu yake) alipokuwa katika Hija ya kuaga
(Hijjatul Wadaai) ni aya ya tatu ya suratul Maida (5:3) ambayo
imeashiria mwisho wa wahy wa Qur‘an, Allah (Subhanahu)
amesema:

―Leo waliokufuru wamekata tamaa katika dini yenu, basi


msiwaogope, bali niogopeni mimi. Leo nimekukamilishieni dini
yenu, na kukutimizieni neema yangu, na
nimekupendeleeni Uislamu uwe dini yenu.‖ (05:03)
Pia tunajifunza kutokana na historia ya kushuka Qur‘an kuwa
sura ya kwanza kushuka nzima (ikiwa na aya zote) ni Suratul-
Fatiha (Al-hamdu) na imekuwa ndio sura ya kwanza katika
msahafu. Katika mtiririko wa kushuka suratul-Fatiha ni Wahy wa
tano. Sura ya mwisho kushuka ikiwa nzima ni Suratun-Nasr,
sura ya 114 katika utaratibu wa kushuka.

Kwa hakika Qur‘an ni maneno matukufu ya Allah (Subhanahu)


ambayo yalihifadhiwa katika ubao mtukufu (Lawhi
Mmahfuudh), kisha akateremshiwa kiumbe mtukufu Mtume
Muhammad (Swalla Allahu alaihi wa Salam) katika mwezi
mtukufu wa Ramadhan.

19
JE! QUR‟AN IMEPITWA NA WAKATI AU IPO MBELE YA
WAKATI

Miaka takribani elfu moja mia nne (1400) imepita tangu Wahy
(ujumbe) wa kwanza wa Qur‘an kuanza kumshukia Mtume wa
Allah (Rehma na Amani ziwe juu yake) kupitia kwa Malaika
Jibril. Karne kumi na nne (14) zimepita tokea karne ya saba
ambayo ndio karne ya Qur‘an, ilishushwa kutoka katika ubao
uliotukuka kumshukia Mtume wa Allah (Rehma na Amani ziwe
juu yake).
Inasemwa kuwa Qur‘an ilishushwa katika karne iliyoitwa ya giza
la elimu, karne ambayo haikuwa na wala haikutegemewa kuwa
na maendeleo makubwa ya kiugunduzi katika masuala kadhaa
wa kadhaa. Tofauti na karne ya ishirini na ishirini na moja
(miaka 1400 baada ya Qur‘an kushushwa) kipindi ambacho
maendeleo makubwa ya Sayansi, teknolojia na teknohama
yamedhihiri, huku yakileta matokeo chanya ya urahisishaji wa
masuala mbali mbali ambayo hapo awali hayakuwepo.
Maendeleo makubwa yakaonekana katika sekta tofauti kama
vile usafiri na usafirishaji (Maji, Anga, Ardhi), tiba, mawasiliano,
na mengine mengi yasiyokuwa hayo. Huku ikionekana kwa
dhahiri kuwa karne za ishirini na ishirini na moja ndio karne za
maendeleo, ndio karne za mwangaza wa kielimu na
kiutandawazi, kutokana na hatua za ugunduzi zilizofikiwa
kulinganisha na karne ya saba (ambayo Qur‘an ilishushwa).
Kutokana na dhana hizo ambazo zimeendelea kuoteshwa ndani
ya fikra za walio wengi, hoja ya msingi ni kwamba; ni kweli
karne ya Qur‘an (Karne ya saba) ndio karne ya kiza cha elimu?
Na Je! Kwakuwa Qur‘an imeshushwa katika kipindi hicho,
tuamini kuwa imepitwa na wakati? Ili kujibu hoja hizi za msingi,
tuangalie baadhi ya nukta ambazo zilitajwa ndani ya Qur‘an
miaka 1400 iliyopita na namna ambavyo iliigharibu Sayansi na
wanasayansi karne kumi na nne (14) kuweza kuyafahamu na
kujifunza ndani yake.

20
UTHIBITISHO NDANI YA QUR‟AN

Allah (Subhanahu) ameifanya Qur‘an kuwa ni kitabu ambacho


kimetofautishwa na vitabu vyote duniani. Qur‘an tukufu ikiwa ni
miongoni mwa miujiza mikubwa ya Mtume Muhammad (Rehma
na Amani ziwe juu yake) ambao siku zote umekua mbele ya
wakati, mbele ya zama zote na mbele ya elimu za watu wote
duniani. Tofauti na vitabu vyengine vyote, Qur‘an ndio kitabu
pekee ambacho kinaweza kusomwa na kurejewa mara nyingi
bila kupoteza ladha kwa msomaji, huku ikiweza kusomwa na
kusomwa kwa miaka yote ya uhai wa mwanadamu bila
kumchosha.
Allah (Subhanahu) ameifanya Qur‘an tukufu kuwa ni muujiza
wenye kujitosheleza, muujiza ambao wenyewe unaweza
kujieleza na kuwaeleza wasioamini juu ya ukweli wa ujumbe
wake. Qur‘an imekuwa ni muujiza ambao yenyewe hutoa
changamoto kwa watafiti na wasomi wakubwa wa sayansi
duniani, na kisha kutoa na kufafanua majibu yake bila kuhitaji
msaada wa uchambuzi.
Kwa wafuatiliaji wa Qur‘an, unaweza kugundua kuwa kitabu
hichi kitukufu kimekuwa kikifafanua masuala mengi ya kibingwa
katika fani zote za sayansi. Haikuacha ndani yake chochote
katika yale ambayo mwanadamu anayahitaji ili aweze kuishi na
kuendelea katika huu ulimwengu. Kama ilivyokuja katika Surat
Al-Isra‘ Allah (Subhanahu) anasema kuwaambia viumbe;
―Sema: Wangeli kusanyika watu na majini ili walete mfano wa
hii Qur‘an basi hawaleti mfano wake, hata wakisaidiana wao
kwa wao. Na hakika tumewaeleza watu katika hii Qur‘an kwa
kila mfano. Lakini watu wengi wanakataa isipokuwa kwa
kukanusha tu.‖ (17:88-89)
Kadhalika, Qur‘an imekuwa ni kitabu ambacho miujiza ya elimu
ilio ndani yake imekua ikishuhudiwa katika nyanja na nyakati
zote duniani. Tofauti na vitabu vyengine ambavyo kawaida
vimekuwa vikiathiriwa na mabadiliko ya zama na nyakati, Qur‘an
imeendelea kuwa mbele ya elimu na akili za wanadamu

21
kwakuwa haina mafungamano yoyote ya muda, zama wala jamii
fulani. Kutokana na ukweli huu juu ya Qur‘an, siku zote
imeendelea kukidhi haja na mahitaji ya viumbe katika njanja na
fani mbali mbali.
Wanasayansi na wasomi kadhaa wamekuwa wakijaribu kuipa
Qur‘an changamoto au kufanya tafiti za kutafuta na kubaini
makosa ndani yake, ila wamekuwa wakigonga mwamba
kwakuwa ahadi ya Allah (Subhanahu) juu ya ujumbe uliopo
ndani ya Qur‘an imeendelea kusimama bila kutingishwa kwa hali
yoyote ile. Wapo baadhi ya wanasayansi ambao walihoji juu ya
taarifa za kuumbwa kwa mbingu na ardhi huku wakisema kuwa
wakati muumba anaviumba vitu hivi yeye alikua wapi? Baada ya
miaka kadhaa kupita sayansi ikaja kuthibitisha kuwa kabla ya
kuumbwa kwa ardhi na mbingu, vipo baadhi ya vitu ambavyo
vilishaumbwa, kama vile maji. Walichoshindwa kufahamu ni
kuwa jambo hilo lilishafafanuliwa na Qur‘an katika karne ya
saba.

Qur‘an imeeleza kwa kina hatua zote za uumbaji wa mbingu na


ardhi na kipindi ambacho kilitumika kuumba maumbile hayo.
Mbali na elimu nyengine nyingi ambazo zimekuwa zikiendelea
kuthibitishwa na sayansi zama hadi zama. Matokeo yote haya
yamekuwa yakithibitisha ukweli wa elimu ya kina ndani ya
Qur‘an, kama ambavyo imethitibisha masuala kadhaa ya
kisayansi, teknolojia na teknohama.

Qur‟an na Sayansi, Teknolojia na Teknohama


Kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa ndani ya Qur‘an tukufu na
kuzingatia mambo kadhaa yaliyozungumziwa ndani yake,
nathubutu kusema na kuvunja ile dhana ya kwamba Karne ya
Qur‘an ni karne ya kiza cha elimu na badala yake tunasema
kuwa karne ya saba ndio karne ya mapinduzi ya kielemu na ndio
karne ya sayansi na teknolojia.

22
Hili limekuja baada ya kuona mambo mengi ambayo
yamefafanuliwa na Qur‘an katika kipindi hicho, ambayo
iliwachukuwa manguli na wabobezi wa sayansi, takribani miaka
elfu moja kuweza kuyafahamu na kuyatumia. Kutokana na hoja
hii, tunasema kuwa karne ya ishirini na ishirini na moja ni karne
za matumizi ya elimu ambayo ilitolewa na Qur‘an kupitia kwa
Mtume wa Allah (Rehma na Amani ziwe juu yake) karne ya
saba.
Wakati Qur‘an inaanza kushushwa kwa Mtume wa Allah, amri ya
kwanza aliyopewa ni kuamrishwa kusoma, kama ilivyokuja
katika Surat Alaq; baadhi ya wafasiri wa Qur‘an wanasema kuwa
amri ya kusoma imekuja kufungua enzi mpya, enzi ya sayansi
na teknolojia, enzi ya kusoma na kutumia uwezo mkubwa wa
kitafiti na kigunduzi wa kuijua dunia na mifumo yake, kumjua
mwanadamu na utaratibu wake, ili elimu hiyo impelekee kiumbe
katika kumjua Muumba wake na kumpwekesha kwa ibada na
stahiki zake zote.
Hivyo, Mtume wa Allah alitumwa kuufikisha ujumbe huu wa
kielimu, elimu ya juu yenye mkusanyiko wa maarifa ya fani
tofauti. Mtume ambae hakujua kusoma wala kuandika, bali
alifundisha na kufafanua mambo makubwa ambayo yamekuja
kuwashangaza wengi miongoni mwa wanasayansi mashughuri.
Mfano mzuri, ni Dokta Maurice; mwanasayansi na daktari
bingwa wa upasuaji wa binadamu, aliandika katika kitabu chake
„The Bible, the Qur‟an and Science (2004) kuwa; Qur‘an
ndio kitabu pekee katika ulimwengu huu kilichoeleza kwa kina
na ufasaha juu ya habari za kuumbwa kwa mbingu na ardhi,
pamoja na namna ambayo uumbaji ulivyofanyika. Wakati Qur‘an
inaelezea habari za kuumbwa kwa ulimwengu, kitabu chenyewe
hakikuwepo. Aidha, kupitia tafiti yake pia alisema kuwa
alishangazwa kupata taarifa ndani ya Qur‘an juu ya matukio ya
asili ambayo maana yake inaweza tu kueleweka kupitia ujuzi wa
kisasa wa kisayansi.
Allah (Subhanahu) anaelezea ndani ya Qur‘an kauli ambayo
ilimfanya Dokta Mourice kusema maneno hayo kuwa;

23
―Na yeye ndiye aliye ziumba mbingu na ardhi katika siku sita. Na
kiti chake cha Enzi kilikuwa juu ya maji.‖ (11:07)
Qur‘an inafafanua na kujibu hoja dhaifu za baadhi ya
wanasayansi ambao walihoji juu ya uumbaji wa mbingu na
ardhi. Kauli ya Allah (Subhanahu) inathibitisha kuwa kabla ya
kuumbwa kwa mbingu na ardhi, tayari alishayaumba maji
ambayo ndiyo yalibeba arshi (kiti cha enzi) yake. Ingawaje
ilionekana kuwa ni ajabu maji kuweza kubeba kitu chochote hali
ya kuwa yenyewe ni kimiminika, na yalihitaji kitu cha kuyabeba.
Sayansi inathibitisha kuwa maji yanaweza kuwa katika hali kuu
tatu; kimiminika, gesi, na pia maji yanaweza kuwa na hali ya
mgando. Kwa mujibu wa tafiti za uumbaji wa dunia,
wanasayansi wanathibitisha kuwa hapo awali maji yalikuwa
katika umbile moja kubwa la mgando ambalo lilikuja kuyeyuka
baada ya kuubwa kwa ardhi na mbingu.
Hivyo, kutokana ukweli unaothibitishwa kuwa Qur‘an imebeba
elimu kubwa ndani yake na pia karne ya Qur‘an ndio karne ya
mapinduzi ya kielemu. Zifuatazo ni nukta muhimu na matokeo
kadhaa ya tafiti za Sayansi, teknolojia na teknohama
yakionyesha namna ambavyo Qur‘an imekua ikifafanua masuala
mengi ambayo hawakuyahafahamu hapo kabla.

Qur‟an na Asili ya Ulimwengu (The Big Bang Theory)


Uumbaji wa ulimwengu unaelezewa na wanajimu (Wasomi wa
mambo ya Anga) kama jambo linalokubalika na wengi, maarufu
kwa jina la 'The Big Bang'. Inaungwa mkono kwa data za
uchunguzi na majaribio zilizokusanywa na wanaastronomia na
wanajimu kwa miongo kadhaa. Wanasema kuwa ulimwengu
ulikuwa umbile moja imara na kisha baada ya hapo ikaja ‗Big
Bang‘ (Mtawanyiko) ambao ulisababisha kuundwa kwa
Ulimwengu. Ambao ndani yake kukapatikana mgawanyiko wa
kuunda nyota, sayari, jua, mwezi, na kadhalika. Baadhi ya
wanasayansi wa mambo ya anga wanasema kuwa ulimwengu
ulianza katika umbile moja la mkusanyiko wa gesi. Kisha
kutokana na mabadiliko ya hewa mkusanyiko ule ukaanza kupoa
24
na kujikusanya na kuwa pande moja lililoganda. Kisha baada ya
hapo ndipo ikatokea huo mpasuko ambao ulikuja kutenganisha
pande hilo la gesi lililoganda.

Qur‘an iliizungumzia gesi hiyo karne ishirini na moja zilizopita,


huku Allah (Subhanahu) akitumia neno la mvuke au moshi
(dukhaan) kama ilivyokuja ndani ya Surat Fussilat;
―Kisha akazielekea mbingu, na zilikuwa moshi, akaziambia hizo
mbingu na ardhi: Njooni, kwa khiyari au kwa nguvu! Vyote viwili
vikasema: Tumekuja nasi ni watiifu.‖ (41:11)

Aya hii inathibitisha na kuziweka sawa gunduzi za wanasayansi


wanaosema na kukubali kuwa ulimwengu uliumbwa awali ukiwa
katika umbile la gesi au moshi. Iweje Qur‘an hii ya Karne ya
saba ifafanue kwa uwazi juu ya masuala haya yote, masuala
ambayo yamekuja kufahamika na wanadamu miaka mingi badae
na kwa kutumia vifaa vya teknolojia ya hali ya juu. Basi hakika
hii Qur‘an ni uongofu.

Kwa mujibu wa mtandao wa Science Photo Library kwenye


makala yake ya mwaka (2020) wanasema kuwa; Picha ya dhana
ya Nadharia ya Big Bang. Mlolongo wa matukio kutoka sekunde
chache za kwanza na uundaji wa mgando na mpasuko. Hizi
huungana na kuunda nyuroni na protoni ambazo kwa upande
wake zilipasuka na kuwa sayari, galaksi na hatimaye kuwa
ulimwengu unaopanuka kila wakati takriban miaka bilioni 15
baadaye.

25
Katika mtazamo huo ambao ulikuja takribani miaka elfu moja
baadae na wengi miongoni mwa wanasayansi wa anga
wanakubaliana moja kwa moja na dhana hiyo ya sayansi. Qur‘an
iliyoshushwa karne ya saba imefafanua na kuweka bayana
jambo hilo na hivyo sayansi ikaifata na kuikiri kwa tafiti na
majaribio mbali mbali. Allah (Subhanahu) anasema ndani ya
Qur‘an;
―Je! Hao walio kufuru hawakuona kwamba mbingu na ardhi
zilikuwa zimeambatana, kisha Sisi tukazibabadua? (21:30)

Wafasiri wa Qur‘an wanaifafanua kauli ya Allah (Subhanahu)


kuwa; “mbingu na ardhi zilikuwa zimeambatana, kisha
Sisi tukazibabadua” na kusema kuwa maana yake, Hapo
mwanzo vyote (ardhi na mbingu) vilikuwa pande moja,
lililoshikamana na kurundikana kimoja juu ya kitu chingine, kisha
Akavitenganisha, na akazifanya mbingu saba na ardhi kuwa
saba, akaweka anga kati ya ardhi na mbingu ya chini kabisa.
Kisha akateremsha mvua kutoka mawinguni na kuotesha mimea
kutoka ardhini.

Hivyo basi kwa mujibu wa ushahidi wa Qur‘an juu ya kuumbwa


kwa Mbingu na Ardhi pamoja na namna ambavyo Sayansi
ilivyokuja kuikiri Qur‘an. Qur‘an ambayo ilishushwa karne ya
saba, karne ambayo waliita kuwa ni karne ya giza la elimu na
sayansi. Wanasayansi hao hao baada ya miaka takribani elfu
moja kupita tafiti zao waliikiri Qur‘an kwa vitendo na maandishi
huku matokeo ya ugunduzi, tafiti na elimu bobevu yakiendelea
kukubali yale mambo yote ya kisayansi ambayo yalifafanuliwa
na Qur‘an.

Qur‟an na Sayansi ya Anga (Astrology)


Maendeleo ya Kisayansi na Teknolojia yameendelea kuikiri
Qur‘an, Kitabu ambacho kiliteremshwa katika jangwa karne
takribani ishirini zilizopita. Kwa muda mrefu wanafalsafa na
wanasayansi wa bara Ulaya waliamini kwamba dunia
imesimama katikati ya anga, ulimwengu na maumbile mingine
yote, pamoja na jua vinazunguka kuizunguka dunia. Baada ya
26
hapo mwana jografia wa ulimwengu alikuja na dhana yake
katika karne ya kumi na mbili, Bwana Nicholas Copernicus
aliweka mbele nadharia yake ya Heliocentric ya Mwendo wa
Sayari kuwa jua limetulia na sayari nyengine zote ndizo
zinazozunguka kulizunguka jua.

Mnamo mwaka 1609, mwanasayansi wa Kijerumani, Yohannus


Keppler alichapisha makala yake iliyoitwa ‗Astronomia Nova‟
aliandika na kuhitimisha kuwa; sio tu kuwa sayari zote ikiwamo
dunia hulizunguka jua, bali kila sayari inajizungusha katika
muhimili wake katika kasi inayotofautiana na sayari nyengine.
Kabla ya uvumbuzi huu, ilifikiriwa kuwa jua lilikuwa limesimama
na halizunguki kwenye muhimili wake kama ilivyo dunia na
sayari nyengine.

Tukiweka matokeo ya ugunduzi huo wa wanasayansi mbali


mbali ambao ulifanyika takribani miaka elfu moja na zaidi baada
ya Qur‘an kushushwa, kisha tukalinganisha na matokeo ya
kisayansi ya sasa ambayo baada ya mapitio na marejeo ya
gunduzi zao, walikubali na kukiri kuwa walikosea.

Badala yake wakakubaliana moja kwa moja na kile


kilichofafanuliwa na Qur‘an katika karne ya saba. Allah
(Subhanahu) anasema ndani ya Qur‘an kuhusu Sayari na
mizunguko yake (Solar System);
―Na Yeye ndiye aliye umba usiku na mchana na jua na mwezi,
vyote katika anga vinaogelea katika mihimili yake‖ (21:33)

Ibn Kathir (Rehma za Allah ziwe juu yake) amefafanua kauli ya


Allah (Subhanahu) “Vyote (jua na mwezi) katika anga
vinaogelea” amesema maana yake ni kwamba; Jua lenye nuru
yake na njia yake na mzunguko wake na wakati uliowekwa, na
mwezi ambao unang'aa kwa nuru tofauti na unasafiri kwa njia
tofauti na una wakati wake uliowekwa. Ibn Abbas (Rehma za
Allah ziwe juu yake) amesema kuwa maana ya kauli hiyo ya
Allah (Subhanhau) ni kwamba; Jua na Mwezi vinazunguka kama
gurudumu linalozunguka, kwenye duara.

27
Karne ya Qur‘an (karne ya saba) ndiyo ilikuwa karne ya ufunguzi
wa zama za kielimu na ndio karne pekee iliyofungua milango ya
tafiti na gunduzi mbali mbali za Kisayansi na Teknolojia. Kwani
baada ya Qur‘an kueleza kuwa sayari zote pamoja na jua na
mwezi kila kimoja huzunguka katika muhimili wake, ndipo juhudi
za ziada za kigunduzi kuchukuliwa na kisha matokeo yake
yakaja kueleza na kuithibitisha Qur‘an.

Mitaala mbali mbali ya kisomi katika mashule ikafanyiwa


marekebisho makubwa kwa lengo la kuingiza matokeo ya
ugunduzi mpya juu ya mizunguko ya sayari. Miongoni mwa
mabadiliko makubwa ambayo yamefanyika katika mitaala hiyo ni
pamoja na kubadilisha dhana ya kuwa, jua kama sayari
nyengine huzunguka katika muhimili wake kwa muda
uliopangiwa.

Wakaongeza kuwa kwa mujibu wa ugunduzi wao mpya


wanasema kuwa hulichukua jua takribani siku ishirini na tano
kukamilisha mzunguko mmoja katika muhimili wake. Kadhalika,
wanasema kuwa jua huzunguka katika anga ya dunia kwa
wastani wa kilomita mia mbili arubaini (240kms) kwa sekunde.
Na huchukua takribani miaka milioni mia mbili kuuzunguka
Ulimwengu mzima.

28
Allah (Subhanahu) amesema juu ya hilo;
―Haliwi jua kuufikia mwezi, wala usiku kuupita mchana. Na
vyote vinaogelea katika njia zao.‖ (36:40)
Kauli hii ya Allah (Subhanahu) inathibitisha juu ya mienendo ya
sayari hizo ambazo kila moja huzunguka katika nafasi na wakati
wake. Kutokana na mihimili yake, hazikufanywa kimoja kuenda
mbele ya mwenzake kama ambavyo mchana hauwezi kuingia
katikati ya usiku. Kila kimoja kina wakati wake, safari na njia
zake ambazo vimepangiwa.

﴾٥﴿‫ن‬
ْ َ‫ن يَ ْعل‬
ْ َ‫ًسبىَ َهب ل‬
َ ‫ٱإل‬
ِ ‫ن‬َ َّ‫َعل‬
‖Kamfundisha mwanadamu aliyokuwa hayajui‖ (96:05)

Qur‟an na Uhusiano wa Wakati (Time Relativity)


Kwa mujibu wa wanasayansi wa anga na wanajimu wa sayari,
wanasema kuwa ndani ya dunia yetu muda hupimwa kulingana
na namna ambavyo dunia huzunguka katika muhimili wake,
muda ambao huweka hesabu ya siku. Vile vile, tunaweza
kuhesabu idadi ya miaka kadiri dunia inavyolizunguka jua, au
kwa namna ambavyo mwezi huzunguka katika muhimili wake
kuizunguka dunia.

Pamoja na vipimo vyengine vya muda kama vile miezi, masaa,


dakika na sekunde vikiwa ni vigawanyo vya kawaida
vilivyoundwa na mwanadamu ili kugawanya siku na miaka
inayozingatiwa kwa kawaida katika vipimo. Walakini, vitengo hivi
vyote ni vya kipekee kwa sayari yetu ya dunia. Wanasayansi hao
walisema kuwa vipimo hivi ni vya kipekee katika kupima idadi ya
masaa, siku, miezi na miaka ndani ya dunia yetu kwa sababu
vipimo hivi haviwezi kuwa na maana sawa ukiwa ndani ya sayari
nyengine tofauti na dunia yetu.

Kwa mujibu wa mtafiti wa masuala ya anga Dokta Nabil


amesema katika kitabu chake „Uislamu; Ushahidi wa
Sayansi ya Kisasa‟ kuwa; siku moja (masaa 24) katika sayari
ya dunia, ni sawa na siku 118 katika sayari ya Venus.

29
Akaongeza pia, siku moja ndani ya sayari ya Jupiter ni sawa na
masaa tisa na dakika hamsini na tano (Masaa 9, Dakika 55).
Kwa mujibu wa dhana maarufu ya fizikia ya Einstein inasema
kuwa uwiyano wa muda hutegemea namna ambavyo kitu
kinavyotembea kwa kasi yake. Dhana hii imekuja kuthibitishwa
na gunduzi juu ya namna ambavyo sayari tofauti huzunguka
katika mihimili yake huku kila moja ikiwa na kasi yake.

Hivyo basi, kwa mujibu wa dhana hii, na kwa mujibu wa


matokeo ya kitafiti ya karne ya ishirini ambayo yamekuja
kugundua kuwa muda ndani ya ulimwengu huu hauwezi kuwa
sawa katika sayari zote, ni lazima utatofautiana kwa kuzingatia
ukubwa wa sayari na kasi ambayo huzunguka sayari hiyo
kulizunguka jua. Kwa mujibu wa mtandao wa „Universe
Today‟ wanasema kuwa siku moja ndani ya sayari ya Pluto ni
sawa na siku 6, masaa 9 na dakika 36 ya masaa ya dunia.

Kadhalika, wamefafanua kuwa mwaka mmoja ndani ya sayari ya


Pluto ni sawa na idadi ya miaka 248 katika miaka ya dunia.

Kitengo cha usimamizi na uratibu wa safari za anga (NASA)


kimetoa takwimu za mapishano ya siku katika sayari tofauti na
kuzifafanua kama ambavyo picha invyoonekana hapo chini;

30
Kadhalika, katika kuthibitisha juu ya dhana ya uhusiano wa
wakati, angalia namna ambavyo nyakati zinavyokuwa na
utofauti mkubwa baina ya nchi na nchi, kulingana na masafa ya
mabara. Tunaona vipimo vya siku (Mawio na machweo)
hutofautiana kwa kiasi fulani kutoka nchi moja ndani ya bara
moja na nchi nyengine iliyo katika bara jengine. Sote
tunakubaliana kuwa idadi ya masaa ya funga ya Ramadhani
hapa nchini sio sawa na idadi ya masaa ya baadhi ya nchi za
bara Ulaya. Zipo nchi ambazo wakati hapa nchini tukifunga kwa
takribani masaa kumi na mbili, wao hufunga masaa zaidi ya
kumi na tano ikiwa ni miongoni mwa visithibitisho kwa uwiyano
wa wakati (Time relativity).

Haya yote ni matokeo ya tafiti na gunduzi zilizofanywa na


wanasayansi kadhaa wa kadhaa katika karne za ishirini na
ishirini na moja. Kutokana na matokeo haya ulimwengu umekua
ukisimama kidedea kuwapongeza na kuwanyanyua kwa heshima
kutokana na kazi kubwa waliyoifanya kujua namna ambavyo
wakati hutofautiana ndani ya ulimwengu mmoja.

Tafiti na gunduzi hizi zinasemwa kuwa ni miongoni mwa


uwekezaji mkubwa ambao Nchi za Ulaya zimezifanya katika
matumizi ya wataalamu waliobobea katika anga, sambamba na
matumizi makubwa ya vifaa vya teknolojia ya hali juu ambavyo
hutumika kuwasaidia wanasayansi hao kufikia katika matokeo
ambayo tumeyaeleza.

31
Qur‘an inatueleza kuwa elimu na sayansi iliopo ndani ya
uhusiano wa wakati ndani ya ulimwengu huu, ulishatolewa
ufafanuzi wake miaka elfu moja iliyopita, huku baadhi ya
wanasayansi wakiumiza kichwa kujadili yawaje kitabu ambacho
kilishushwa jangwani, ndani ya karne ya giza la elimu,
kilichoshushwa kwa Kiumbe ambae hakuwa na elimu, kiweze
kufafanua masuala mazito yenye kuhitaji ujuzi na vifaa vya
kisayansi ya kisasa!
Qur‘an kupitia Surat Al-Hajj, Allah (Subhanahu) anasema;
―Na hakika siku moja kwa Mola wako Mlezi ni kama miaka elfu
mnavyo hisabu nyinyi.‖ (22:47)

Miongoni mwa kauli za Allah (Subhanahu) ambazo zinathibitisha


kuwa Qur‘an ilishaeleza juu ya Uhusiano wa Wakati, na kupitia
aya hii Allah (Subhanahu) anaeleza mahusiano ya wakati kati ya
namna ambavyo wanadamu wanavyo hisabu katika ulimwengu
wao na namna ambavyo unahusiana na wakati huo huo mbele
ya Allah.

Allah (Subhanahu) anasema pia ndani ya Surat As-Sajdah;


―Anapitisha mambo yote yalio baina ya mbingu na ardhi, kisha
yanapanda kwake kwa siku ambayo kipimo chake ni miaka elfu
kwa mnavyo hisabu nyinyi.‖ (32:05)
Allah (Subhanahu) anasema pia ndani ya Surat Al-Ma‘arij;
―Malaika na Roho hupanda kwendea kwake katika siku ambayo
kadiri yake ni miaka Hamsini elfu!‖ (70:04)

Hivyo basi, kutokana na ufafanuzi huu wa aya kadhaa za


Qur‘an, zote zikithibitisha kuwa Allah (Subhanahu) ameumba
kila sayari ni yenye kutofautiana katika mahusiano ya muda
wake na sayari nyengine. Mahusiano ambayo kwa yakini hapo
awali wakati sayansi na teknolojia inaanza kushika hatamu
yalionekana kana kwamba ni jambo la mchezo na lisilo
wezekana. Kwa nukta hizi pia tunaweza kueleza pale Allah
(Subhanahu) aliposema juu ya kuumba mbingu na ardhi kwa
siku sita alimaanisha siku sita zenye urefu tofauti na siku
ambayo tumeizoea katika ulimwengu wetu.

32
Lakini kadiri zama na nyakati zilivyokwenda huku maendeleo
makubwa ya kigunduzi kufikiwa, sayansi imekuja kuikiri Qur‘an
kwamba kwa hakika ―Muda unao mahusiano‖ ndani ya huu
ulimwengu. Mahusiano ambayo hutofautiana kulingana na
umbali wa sayari moja hadi nyengine, mahusiano ambayo
hutegemea na kasi ambayo sayari moja huzunguka katika
muhimili wake, aidha, mahusiano ambayo hutegemea na nani
haswa hupima kiwango hicho cha wakati.

Qur‟an na Sayansi ya safari za anga za mbali (Space


Travelling)
Historia za kisayansi zinatueleza kuwa kwa miaka kadhaa hapo
nyuma juhudi mbali mbali zilifanyika sambamba na tafiti na
uwekezaji mkubwa katika kuhakikisha wanaweza kumpeleka
mwanadamu katika masafa ya mbali ya anga. Safari za anga ya
mbali zimekuja zikijadiliwa na kuratibiwa kwa kasi sana na
taasisi ya anga ya marekeani NASA. Taasisi ambayo ilianza
harakati za kufanikisha safari hizo mnamo mwaka 1958.
Tafiti na maendeleo ya sayansi na teknolojia iliwapa mwangaza
mkubwa wa kuweza kufanikisha safari hizo, ingawaje haikuwa
rahisi kwakuwa safari za anga za mbali zilihitaji uchambuzi na
utafiti wa kina ili kuhakikisha mafinikio, bali kuhakikisha usalama
wa wataalamu ambao watasafiri kuelekea anga za mbali. Kwa
muda mrefu mataifa makubwa duniani yalifanya mipango
kemkem huku wakipeana changamoto baina yao kwamba ni
nani atafanikiwa kufanya safari hiyo mwanzo.
Utandawazi na uwekezaji wa hali ya juu ulipaswa kuwasaidia
kwa kiasi kikubwa kufikia malengo waliyo yaweka.

33
Walichoshindwa kutambua kuwa Allah (Subhanahu) kupitia
Qur‘an tukufu alishafafanua juu ya mwenye mamlaka ya juu ya
kuwawezesha kufanya safari hizo. Wanasayansi kupitia
majaribio tofauti ambayo hayakuwapa matunda ya mafanikio
walishindwa kutambua kuwa mbali na elimu, sayansi, na
maendeleo makubwa ya kiteknolojia hayawezi kuwawezesha,
bila ya kupata idhini ya mwenye mamlaka ya safari za anga za
mbali. Allah (Subhanahu) anasema ndani ya Surat Ar-Rahman;
―Enyi makundi ya majini na watu! Mkiweza kupenya kwenye
mbingu na ardhi, basi penyeni! Hamtapenya ila kwa kupewa
madaraka.” (55:33)
Wafasiri wa Qur‘an tukufu wameifafanua kauli ya Allah
(Subhanahu) wakisema kuwa; Allah (Subhanahu)
anawabainishia waja wake kuwa kama wataweza kupenya nje
ya mipaka ya mbingu ama kupenya chini ya mipaka ya ardhi
basi wapenye ili kuikimbia adhabu yake na ufalme wake. Aidha,
wakasema kuwa madaraka yaliyokusudiwa hapa ni ufalme wake
wa utendaji kwa kila alipendalo na kuwa kila jambo lipo kwenye
umiliki wake. Wapo baadhi ya wanachuoni waliofafanua neno
madaraka kuwa ni elimu na upeo wa kuweza kupenya kwa
idhini yake.
Hivyo basi, kutokana na ukweli huo wa Qur‘an, mnamo mwezi
Julai mwaka 1969 baada ya tafiti za kina kufanyika pamoja na
kupewa mamlaka ya elimu na Allah (Subhanahu), safari ya
kwanza ya mwanadamu kutua katika ardhi ya mwezi ilifanyika
huku Kamanda Neil Armstrong na rubani wa mwezini bwana

34
Edwin Aldrin wakiwa ndio binadamu wa kwanza kupewa
madaraka na Allah (Subhanahu) kupaa kufika anga za mbali.
Taarifa katika mtandao wa NASA zinaeleza kuwa upo mpango
mwengine ambao wameuweka kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka
2025 wanatafanikiwa kuwapeleka wanaanga wengine 25 katika
ardhi ya mwezi. Ila bila kusahau kuwa itafanikiwa endapo
watapewa mamlaka na Allah (Subhanahu).
Miaka kadhaa baadae, tumeshuhudia safari nyingi zikifanyika
ambazo baadhi zilifanikiwa na baadhi kupata changamoto, ikiwa
ni pamoja na kugharimu maisha ya wana anga kadhaa. Kupitia
safari ya kwanza ya wanadamu kutua katika uso wa ardhi ya
mwezi ambayo iliwachukuwa wana anga hao kusafiri umbali wa
masafa ya kilomita 376,400, yapo matukio makubwa ambayo
tunapaswa kuyafahamu. Matokeo ambayo wanasayansi hawa
wameyaona na kuyasimulia kwa ulimwengu mara tu baada ya
kurejea ndani ya sayari ya dunia.
Kutokana na taarifa za wanasayansi hawa juu ya yale waliyo
yashuhudia huko pamoja na mlolongo mzima wa safari yao ulio
uwacha ulimwengu mdomo wazi, huku wakiwa na masuali
lukuki, masuali ya kuwa kivipi Qur‘an iliyoshushwa karne ya
saba iliweza kueleza juu ya mambo kadhaa kuhusu mwezi katika
kipindi ambacho hakuna kiumbe aliyeweza kufika katika anga za
mbali.
Nidhamu ya mzunguko wa mwendo wa kinyume cha saa
(kuzunguka kutoka kulia kwenda kushoto) katika
kuufikia mwezi:
Kwa mujibu wa taarifa iliyorushwa mubashara ulimwenguni
kuhusu safari hiyo, inaeleza kuwa chombo ambacho walikitumia
kusafiri katika masafa hayo ya mbali ambacho kilipewa jina la
Apollo 11, mara tu baada ya kutoka na kupenya nje ya sayari ya
dunia kilianza kuzunguka katika obiti (mihimili ya mwezi) kutoka
kulia kwenda kushoto huku kikiendelea kukaribia ardhi ya
mwezi. Wanasayansi wanakiri kuwa sayari zote huzunguka
katika mihimili yake kwa mwendo wa kinyume cha saa yaani
huzunguka kutoka kulia kwenda kushoto.

35
Ilisemwa pia haikuwezekana kuufikia mwezi kwa kufanya
mzunguko mwengine wowote isipokuwa kwa kuzunguka kwa
mwendo wa saa, na jambo hili lilielezwa na wanasayansi kuwa
ni kutokana na maumbile ya sayari zote zimeeumbwa
kuzunguka katika muhimili wake kwa kufata nidhamu hiyo.

36
Nidhamu hii inatuthibitishia kuwa kila umbile ndani ya
ulimwengu limeumbwa na Allah (Subhanahu) kwa kufata
utaratibu maalumu kama ule ambao mahujaji hutufu nyumba
tukufu ya Kaaba kwa kuizunguka kutoka kulia kwenda kushoto.

Bwana Neil alipoulizwa juu ya suala hili, alifafanua kuwa katika


obiti za sayari zote ulimwenguni upo mvutano wa graviti ambao
huifanya sayari hizo kuzunguka katika mzunguko wa kutokea

37
kulia kwenda kushoto, hivyo iliwalazimu kuufuatisha mzunguko
huo ili kuepuka kikinzana nguvu ya mvutano huo ili usilete
madhara kwao na kwa chombo chao. Kwa tafakuri za kina, tukio
hili linathibitisha kuwa wanasayansi hawa hawakuweza kupenya
nje ya mbingu na kuufikia mwezi isipokuwa na mamlaka ya
Allah (Subhanahu) kwani hawakuweza kupata njia yoyote
mbadala ya kuufikia mwezi isipokuwa kwa kufata nidhamu
aliyoiweka Mwenye Mamlaka.
Ushuhuda wa Neil Armstrong kuhusu kupasuka kwa
mwezi:
Allah (Subhanahu) kupitia Surat Al-Qamar amesema katika
karne ya saba;
―Kiama (Saa) kimekaribia, na mwezi umepasuka!‖ (54:01)
Ibn Kathir (Radhi za Allah ziwe juu yake) amemnukuu Anas bin
Malik (Radhi za Allah ziwe juu yake) akisimulia kuwa Imam
Ahmad amepokea kutoka kwa Anas bin Malik akisema; ―Watu
wa Makka walimtaka Mtume wa Allah (Rehma na Amani ziwe
juu yake) awaonyeshe muujiza, ndipo wakashuhudia mwezi
ukipasuka vipande viwili katikati ya mji wa Makka.‖
Qur‘an tukufu inaeleza habari za mwezi kupasuka ikiwa ni ishara
ya kuonyesha kuwa kiyama kimekaribia huku wafasiri wa Qur‘an
wakifafanua aya hii kwa kutumia Hadithi kadhaa sahihi juu ya
tukio la muujiza wa kupasuka kwa mwezi, ikiwa ni miongoni
mwa miujiza mikubwa ya Mtume wa Allah (Rehma na Amani
ziwe juu yake). Wanasayansi wa karne ya ishirini hawakuacha
kupinga na kuona kuwa ni jambo lisilo na mashiko huku kwa
kebehi na dharau wakiwageukia waumini kwa masuali kadhaa
yasiyo na majibu.
Ni kweli, kutokana na maendeleo finyu ya sayansi na teknolojia,
halikuwa jambo jepesi kulithibitisha ingawaje bado suala hili
likaendelea kuwaumiza kichwa watafiti na wasomi wa masuala
ya anga. Kutokana na mamlaka ya elimu na vipawa
walivyopewa watafiti wa masuala ya anga wa karne ya ishirini,
mnamo mwaka 1969 safari ya Neil Armstrong ilikuja kutoa

38
uthibitisho wa kuikiri Qur‘an. Katika taarifa ya Bwana Neil
akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo wa kimataifa
mara tu baada ya kurudi kutoka katika misheni ya mwezi,
aliulizwa na mwandishi mmoja kuhusu faida za safari hiyo.
Bwana Armstrong alisema kuwa miongoni mwa faida kubwa
waliyoipata ni kuthibitisha kuwa ipo athari ya kuthibitisha kuwa
mwezi unawezekana kuwa ulipasuka vipande viwili.

Jibu hili sio tu kwamba lilishangaza ulimwengu, bali liliwacha na


kiu ya kutaka kujua zaidi kuhusu ugunduzi huo. Katika
kuthibitisha habari hiyo, bwana Neil alionyesha baadhi ya picha
ambazo alizichukuwa akiwa katika uso wa ardhi ya mwezi
pamoja na vipande vya mawe ambavyo inasemwa kuwa yalifika
kilogramu 25 ambayo aliyachukuwa kwa ajili ya uchunguzi na
utafiti wa ziada. Taarifa hiyo inaeleza kuwa baada ya utafiti wa

39
kina wa vipande hivyo, ilithibitika kuwa ni miongoni mwa
ushahidi wa athari za mpasuko wa ardhi ya mwezi.

Taarifa hizi, zimeendelea kuwa na mijadala mikubwa katika


mitandao huku wengi miongoni mwa watu wakiamini kuwa ni
taarifa zilizoongezwa ndani ya taarifa kuu ya Bwana Neil, watu
kadhaa wakiwamo wasomi wa masuala ya sayansi ya anga
wameonekana kuendelea kukataa uthibitisho huu huku hoja zao
za msingi wakisema kuwa ulimwengu haupaswi kuamini kila kitu
kinachoonyeshwa kupitia mitandao. Kwa upande mwengine
baadhi ya wanasayansi ambao wamekuwa wakitumia picha za
mnato ambazo zimekuwa zikichukuliwa na salaiti kadhaa
ambazo zinafuatilia masuala ya ulimwengu zimekuwa
zikiendelea kuthibitisha juu ya athari za kupasuka kwa mwezi.
Ingawaje wengi bado wamekuwa wakitoa dhana tofauti kama
vile, wakisema kuwa picha hizo zinaonyesha kuwa ni athari za
mtetemeko wa mawimbi ya mzunguko wa mwezi katika obiti
yake. Haya yote ni kusema kuwa wameendelea kukataa muujiza
wa Qur‘an na wanaendelea kuficha baadhi ya taarifa ambazo
zinaweza kuufanya ulimwengu kuikubali na kuisadiki Qur‘an
katika masuala yake ambayo imeyaeleza katika karne ya saba.
―Na wakiona Ishara hugeuka upande na husema: huu uchawi tu
unazidi kuendelea.‖ (54:02)

40
Ugunduzi wa Sayari (nyota) yenye sauti ya kugonga:
Katika kuendelea kutoa ufafanuzi kuhusu matokeo ya safari ya
kwanza ya wanadamu katika uso wa ardhi ya mwezi, inaelezwa
kuwa safari hiyo iliweza kugundua kuhusu uwepo wa nyota
kubwa ambayo huonekana duniani nyakati za usiku ambayo kwa
kutumia kifaa maalumu cha kunasa sauti, waliweza kugundua
kuwa inatoa sauti mfano wa sauti ya mtu anae gonga mlango
wa mbao kwa kutumia vidole vyake.

Wengi miongoni mwa wanasayansi wa masuala ya anga, haswa


wale wa mataifa shindani walionyesha wasiwasi juu ya usahihi
wa taarifa hizo, ingawaje kadiri muda na zama za maendeleo ya
sayansi na teknolojia zilivyokua zikiendelea kukua, ndivyo
taratibu walivyoonekana kuzikubali taarifa hizi. Kwa mujibu wa
mtandao mmoja wa wana anga wanasema kuwa, wanasayansi
wamegundua kuwa ipo nyota ambayo imeonekana na
kusikilikana kuwa na sauti mfano wa nyundo yenye kugongwa
kwa nguvu kubwa. Mtandao huo ukaeleza kuwa sababu kubwa
ya sauti hiyo hutokana na athari ya namna ambavyo nyota hiyo
huzunguka katika obiti yake kwa kasi, kiasi ambacho hutoa sauti
hiyo kwa nguvu na kasi ya hatari.
Watafiti wa masuala ya mawimbi ya sauti wanasema kuwa kwa
mwanadamu wa kawaida haiwezekani kusikia sauti za nyota
hiyo na nyengine kadhaa kutokana na kiwango cha mawimbi ya

41
sauti kuwa chini ya kiwango ambacho uwezo wa usikivu wa
mwanadamu kuweza kunasa kwa ufasaha. Wakaeleza kuwa
kutokana na matokeo ya safari ya kwanza ya nje ya dunia,
ilipekea wanasayansi kutafiti na kuchunguza kwa kina juu ya
madai ya bwana Neil Armstrong na wenzake. Madai ambayo
yalikuja kuwezesha kugunduliwa kifaa maalumu cha kupima na
kusikiliza sauti za sayari tofauti kwa kutumia mawimbi yake ya
mtetemeko wa sauti.

Kadhalika, kupitia kifaa hicho, ndicho kilichoweza kugundua


sauti za sayari na nyota kadhaa katika ulimwengu, kama vile
ilivyogunduliwa sauti ya Jua kuwa ni sauti ya mgurumo wenye
miripuko kadhaa wa kadhaa.
Kwa hakika, kila hatua na matokeo ya sayansi na teknolojia,
yamekuwa yakiwa na ufafanuzi wa kutosha ndani ya Qur‘an.
Kitabu ambacho kimeshushwa katika karne ya saba, karne
ambayo haikuwa na uwezo wa kuunda ama kuvumbua kifaa
chochote cha kunasa sauti ya sayari ndani ya ulimwengu. Cha
ajabu kabisa habari zote juu ya nyota hii pamoja na sauti yake,
yalishaelezewa na Mtume wa Allah (Rehama na Amani ziwe juu
yake) huku ikisemakana kuwa hakukuwa na uwezekano ya
kiumbe huyo akiwa katika zama hizo kusimulia na kueleza
kuhusu sauti na tabia za nyota hiyo.
Qur‘an tukufu imefafanua na kueleza juu ya sauti ya nyota hiyo.
Huku Allah (Subhanahu) akiapa kwa kutumia sifa, sauti na
maumbile ya nyota hiyo. Allah (Subhanahu) amesema ndani ya

42
Surat At-Tariq ambayo kwa lugha ya Kiingereza hitwa ‗The night
comer‘ au ‗The Knocker‘
―Naapa kwa mbingu na kinachokuja usiku. Na nini kitakacho
kujulisha ni nini hicho kinacho kuja usiku. Ni nyota yenye
mwanga mkali.‖ (86:01-03)
Kwa hakika Allah (Subhanahu) ni mbora kwenye kuumbwa na
kuyabainisha kwa waja wake ili iwe ni fundisho na muongozo
wa maisha yao.

Qur‟an na Sayansi ya asili na maendeleo ya kukuwa kwa


Mwanadamu (Embryolojia)
―Soma! Na Mola wako Mlezi ni mkarimu kushinda wote! Ambaye
amemfundisha kwa kalamu.‖ (96:3-4)

Dokta Zakir Naik katika kitabu chake cha ‗Qur‘an na Sayansi ya


Kisasa‘ ameeleza kuwa kikundi cha wanachuoni wa Kiislamu
huko nchini Yemen walipewa maelekezo na kiongozi Mkuu wa
Nchi hiyo, kukusanya baadhi ya Aya za Qur‘an ambazo
zimefafanua masuala ya kuumbwa kwa mwanadamu na
kuzifanyia uchunguzi kupitia sayansi ya kisasa.

Mara baada ya kuzikusanya aya hizo pamoja na baadhi ya


Hadith, walizitafsiri kwa lugha ya Kiingereza na kisha
wakampelekea mmoja kati ya wasomi mashughuri na nguli wa
sayansi ya embryolojia, Dokta Keith Moore. Baada ya kupewa
aya hizo, Dokta Moore alizisoma kwa makini na kisha alisema
kuwa taarifa zote ambazo zimeelezwa ndani ya aya alizopewa
kuhusiana na kuumbwa kwa mwanadamu, zinakubaliana moja
kwa moja na matokeo ya tafiti na gunduzi za sayansi ya kisasa.
Aliongeza, kuwa zipo baadhi ya taarifa ambazo zimeelezwa na
Qur‘an kuhusu masuala ya kuumbwa kwa mwanadamu ambazo
hakuweza kuzitolea ufafanuzi kwa kuwa bado sayansi
haijathibitisha ukweli wake, hivyo asingeweza kutoa ufafanuzi
wa jambo ambalo hakuwa na ujuzi nalo.

43
Miongoni mwa mambo ambayo alisema Qur‘an imefafanua
wakati ambao sayansi haijafika katika tafiti zake ni kauli ya Allah
(Subhanahu);
―Amemuumba mwanadamu kwa tone la damu‖ (96:02)
Kwa mujibu wa Dokta Naik, wakati aya hii inapelekwa kwa
mtafiti huyo hakuweza kuthibitisha kwa upande wa sayansi
kwamba mwanadamu katika kuumbwa kwake hupitia hatua ya
pande la damu. Baada ya kulipitia suala hilo, ilimlazimu kufanya
tafiti ya kina juu ya hatua za awali za uumbaji wa mwanadamu,
pamoja na kusoma kwa undani mfumo mzima wa embyolojia ya
mwanadamu huku akishirikiana na wataalamu wenzanke katika
fani hiyo.

Mara baada ya tafiti hiyo alisema kuwa; ―Laiti kwamba


ningeliulizwa maswali haya (Ufafanuzi wa Sayansi ndani ya
Qur‘an) miaka thelathini iliyopita nisingeweza kujibu hata nusu
ya maswali yote, kwa sababu ya uhaba wa taarifa za kisayansi
katika wakati huo.‖

Kauli na hitimisho la Dokta Moore linathibitisha kuwa siku zote


Qur‘an imekuwa mbele ya wakati, imekuwa mbele ya
maendeleo ya sayansi na teknolojia. Qur‘an imekuwa ikiendelea
kuwapa changamoto mbali mbali za kitafiti na kiugunduzi. Dokta
Joe Simpson kutoka chuo cha tiba cha Marekani alisema kuwa;
―Ndani ya Qur‘an upo ufafanuzi ambao baada ya karne nyingi
kupita zilikuja kugundulika kuwa zinazo mchango mkubwa
katika matokeo ya sayansi ya sasa.‖

Miongoni mwa mambo ambayo yamekuwa na mchango mkubwa


ama yamekuwa ni chachu ya maendeleo kadhaa ya kisayansi
katika fani ya embryolojia (Chanzo na maendeleo ya makuzi ya
mwanadamu) ni pamoja na ufafanuzi wa kina juu ya hatua
mbali mbali za makuzi ya kiumbe ndani ya tumbo la mama.
Maendeleo ambayo yamefafanua hatua zote za uumbwaji wa
mwanadamu, kuanzia akiwa tone la manii kutoka katika uti wa
mgongo wa baba yake hadi kuwa ni mbegu mkusanyiko (mbegu

44
za baba na mama) kufikia hatua ya kuwa pande la damu na
hadi kuwa kiumbe hai.

Maji ya Mchupo yatokayo baina ya Mifupa ya Mgongo na


Mbavu:
Mnamo mwaka 500 (miaka zaidi ya elfu moja iliyopita) Allah
(Subhanahu) alisema ndani ya Qur‘an kuwa;
―Hebu naajitazame mwanadamu ameumbwa kwa kitu gani?
Ameumbwa kwa maji yatokayo kwa kuchupa. Yatokayo baina ya
mifupa ya mgongo na mbavu.‖ (86:5-7)

Ibn Kathir (Rehma za Allah ziwe juu yake) amesema akifafanua


kauli ya Allah (Subhanahu) kuhusu maji yatokayo baina ya
―Mifupa ya mgongo na mbavu” amesema maana yake ni
maji ambayo yametoka katika mgongo wa mwanaume na
mbavu ya mwanamke na kisha kuchanganyika na kupatikana
mtoto kwa idhini ya Allah (Subhanahu).

Sayansi ya karne ya ishirini na ishirini na moja haikuweza


kuyapinga maneno haya, ingawaje iliwachukuwa miaka mingi
sana kuweza kuifahamu na kuweza kujua kwa hakika juu ya
maji yaliyozungumzwa na Qur‘an. Awali wanasayansi wa
masuala ya embryolojia waliamini kuwa mbegu za uzazi za
mwanaume huzalishwa na kuhifadhiwa kwenye kokwa mbili za
kiume (korodani). Kadhalika kupitia sayansi yao ya awali
hawakuweza kutofautisha kati ya mbegu za kiume na maji ya
uzazi.

Baadhi ya watafiti na madaktari wa sayansi ya uzazi


(Embryolojia) wanasema kuwa mbegu za uzazi huhifadhiwa
katika neva ambayo huitwa kwa kitaalamu epididymis (ngiri)
ambayo hukaa juu kidogo ya kokwa mbili za kiume (korodani).
Ndani ya mbegu za uzazi hupatikana asilimia mbili hadi tano
pekee ya maji ya uzazi ambayo hutumika katika utungaji wa
mimba. Baada ya mbegu hizo kuzalishwa husafirishwa kupitia
katika mirija ambayo huitwa ‗Vas Deferens duct‘huku
zikizunguka kibofu cha mkojo.
45
Mfumo wa Uzazi wa mwanaume

Baada ya kufika kwenye kibofu, mbegu nyengine asilimia tisini


huzalishwa kutoka katika tezi dume kisha kuhifadhiwa hapo
kusubiri maji ya uzazi ambayo huteremshwa kutoka katika
kiungo ambacho huitwa Abnorminal Aorta ambacho kipo
baina ya mifupa ya mgongo na mbavu ya mwanaume. Kisha
mchanganyiko huo ndio haswa sasa huzalisha maji ambayo
yapo tayari kwa ajili ya uzalishaji katika mfuko wa uzazi wa
mwanamke ambao umebeba yai ambalo limepevuka.

Kuthibitisha juu ya mchanganyiko huu ambao wanasayansi


wameuelezea. Qur‘an ilitoa nuru juu ya jambo hili ambalo kwa
uwazi ilifafanua juu ya namna maji mchangayiko ya uzazi na
mbegu za kiume zinavyoweza kuwa ni sababu ya uzazi na
kupatikana kwa kiumbe kwa idhini yake. Allah (Subhanahu)
amesema;
―Hakika Sisi tumemuumba mtu kutokana na mbegu ya uhai iliyo
changanyika. (76:02)

46
Qur‘an ilieleza kuwa maji ya uzazi yanatoka baina ya mifupa ya
mgongo na mbavu, ukiangalia katika picha hapo juu sehemu
ambayo imezungushiwa ndio sehemu ambao Qur‘an imeieleza.
Wanasayansi wa fani ya uzazi wa mwanaume wanaeleza kuwa
sehemu hiyo ipo mshipa mkuu wa neva (abnominal aorta)
ambao umeenda moja kwa moja katika ubongo wa
mwanadamu.

47
Wapo baadhi ya wanasayansi wanaosema kuwa uzalishaji wa
mbegu za uzazi huanzia katika ubongo kwa mfumo wa hisia
kisha kusafirishwa katika sehemu hiyo kwa ajili ya kuwekwa
tayari kwa ajili usafirishwaji wa mwisho kuelekea katika tezi
dume kabla ya kutolewa (ejaculation).
―Hebu naajitazame mwanadamu ameumbwa kwa kitu gani?
Ameumbwa kwa maji yatokayo kwa kuchupa. Yatokayo baina ya
mifupa ya mgongo na mbavu.‖ (86:5-7)

Utambuzi wa jinsia ya mtoto:


Miaka takribani elfu moja na zaidi ilipita hadi kufikia katika karne
ambayo wanasayansi wa uzazi na makuzi ya mwanadamu
kutambua kuwa jinsia ya mtoto au kitunga cha mimba kilichomo
ndani ya tumbo la mama hutegemea na aina ya maji ya uzazi
yaliyoingia ndani ya yai wakati wa upandikizaji. Kwa mujibu wa
matokeo ya tafiti zao za awali, wanasema kuwa jinsia ya mtoto
hutegemea aina ya yai la mama ambalo limepevuka na kukaa
tayari katika mji wa mimba.

Matokeo ya tafiti hizi za awali hazikuwaridhisha baadhi ya


wanasayansi na iliwabidi kurudi tena kufanya majaribirio kadhaa
wa kadhaa kwa msaada mkubwa wa vifaa vya thamani na
teknolojia ya juu. Baada ya tafiti za kina kwa vipindi na miongo
kadhaa ndipo walikuja na matokeo kuwa katika kila mbegu za
uzazi ambazo mwanaume hutoa ndani yake hujumuisha
Kromosoma za kiume na kike (X na Y).

Hivyo, kwa mujibu wa matokeo hayo, pale ambapo maji ya


uzazi yanaposheheni Kromosoma nyingi za Y ndivyo mtoto wa
Kiume hupatikana, na zinapokuwa kromosoma X ni nyingi,
mtoto wa kike hupatikana. Hivyo basi baada ya Kromosoma za
baba kutoka zikiwa ni aidha X au Y, huenda kukutana na
Kromosoma za mama ambazo ni X tupu kisha hutengeneza
mchanganyiko wa geno ambao huenda ukawa ni XX ama XY.

48
Ukiangalia mchoro hapo juu unaweza kuona namna ambavyo
mchanganyiko wa kromosoma unavyo fanyika huku
ukitengeneza na kuamua jinsia ya mtoto kwa kuchanganya
mbegu za baba (X au Y) na zile za mama (X). Maelezo na
ufafanuzi huo umekuja baada ya tafiti na kazi kubwa za
kimaabara kufanyika. Tafiti ambazo zilionekana kuwa ni ushindi
mkubwa uliopatikana ndani ya karne ya ishirini. Walishindwa
kutambua kuwa hivyo hivyo, ndivyo Qur‘an ilivyobainisha juu ya
uzazi na jinsia ya watoto; Allah (Subhanahu) anasema ndani ya
Surat Ash-Shura;
―Ufalme wa mbingu na ardhi ni wa Allah; anaumba apendavyo,
anamtunukia amtakaye watoto wa kike, na anamtunukia
amtakaye watoto wa kiume, au huwachanganya wanaume na
wanawake, na akamfanya amtakaye tasa. Hakika Yeye ni mjuzi
mwenye uweza.‖ (42:49-50)

Kutokana na ufafanuzi huu ambao umeandikwa kwa kina katika


vitabu tofauti vya fani ya asili ya mwanadamu, ni dhahiri kuwa
matokeo ya kisayansi yanaikiri Qur‘an. Hakuna miongoni mwa
wanasayansi wa sasa ambao watakaa na kukana kuwa jinsia ya
mtoto huamuliwa kwa idhini ya Allah (Subhanahu) kupitia
kromosoma za baba ambazo zimetoka katika maji yake ya uzazi.
Kama hivyo ndivyo, Qur‘an ilieleza sayansi hii na ilisubiri tu

49
wasomi na watafiti wa masuala haya kuja kuikiri na kuiweka
katika vitabu vyao. Allah (Subhanahu) anasema;
―Na kwamba Yeye ndiye aliye umba jozi (pea) mbili, dume na
jike. Kutokana na mbegu ya uzazi inapo miminwa.‖ (53:45-46)
Tunakubaliana kuwa mbegu za uzazi hutolewa na baba, na
kama Qur‘an ilivyoeleza kuwa ni maji mchupo, yenye
kumiminika kutoka katika mifupa baina ya mgongo na mbavu.
Kutokana na kauli hii ya Allah (Subhanahu) tunaweza
kuthibitisha kuwa mbegu ya uzazi inayomiminwa kutoka kwa
baba, na ndio maji ambayo wanasayansi wanakiri kuwa
yamebeba kromosoma za kike na kiume ambazo ndizo hizo
zilizotajwa na Qur‘an kuwa ni jozi mbili.

Ulinzi wa mtoto akiwa ndani ya tumbo la mama:


Allah (Subhanahu) anasema ndani ya Qur‘an kuwa;
―Anakuumbeni katika matumbo ya mama zenu, umbo baada ya
umbo, katika viza vitatu.‖ (39:06)

Ibn Kathir (Rehma za Allah ziwe juu yake) amefafanua kauli ya


Allah (Subhanahu) juu ya viza vitatu na kusema kuwa maana
yake; kwanza ni kiza cha tumbo la uzazi, pili ni kiza cha plasenta
ambayo ni kama blangeti, na tatu ni kiza cha tumbo la mama.
Profesa Keith Moore, nguli wa masuala ya uzazi na maendeleo
ya mwanadamu aliandika katika tafiti yake aliyoifanya kwa
kushirikiana na Chuo Kikuu cha cha Anatomia cha Mfalme Abdul
Aziz cha nchini Saudi Arabia (1982); alisema kuwa; Elimu ya
Kisayansi katika masuala ya uzazi na maendeleo ya
mwanadamu (Embryolojia) haikuwa na maendeleo makubwa
kwa takribani miaka 2000 iliyopita. Hadi kufikia karne ya kumi
na saba ambapo darubini (microscope) ya kwanza iligunduliwa,
na ndio iliyowezesha kutafiti na kufuatilia kwa undani hatua za
mwanzo za kukua kwa mwanadamu.

Kwa mujibu wa Profesa Moore, anaongeza kusema kuwa


kutokana na uwepo wa darubini uliwawezesha kufahamu kuwa
mwanadamu ndani ya tumbo la mama yake amezungukwa na

50
matabaka matatu ambayo ni ngome dhidi ya madhara mbali
mbali ya ndani. Akafafanua kuwa matabaka hayo ni pamoja na;
a) Ukuta wa tumbo la mama
b) Ukuta wa Uterasi
c) Utando wa amniochorionic unaojumuisha amnioni
iliyounganishwa na chorion

Mbali na majaribio na tafiti mbali mbali zilizofanywa ili kufahamu


hatua za awali za mwanadamu, Profesa Moore anasema kuwa
hatua na matabaka haya hayakuweza kugunduliwa wala
kuzungumzwa kwa hali yoyote ile, hadi ilipofika karne ya kumi
na saba (karne nane baada ya kushushwa Qur‘an). Ingawaje
jambo ambalo lilimshangaza zaidi Profesa huyo, ni kuona kuwa
Qur‘an ilishazungumzia kwa undani juu ya sayansi hiyo katika
kipindi ambacho hakukuwa na wala hakukutegemewa kuwa na
uwezekano wa kuona na kugundua kiumbe kilichomo ndani ya
tumbo la mama.

Kutokana na ufafanuzi wa Qur‘an, Profesa Moore alisema ndani


ya Kitabu chake cha „Maendeleo ya Mwanadamu‟ kuwa;
―Imekuwa wazi kwangu kuwa Maneno haya (Qur‘an)
yameshushwa kwa Muhammad kutoka kwa Mungu/Allah,
kwasababu elimu kubwa miongoni mwa elimu ambazo
zimejumuishwa ndani yake hazikuwa zinatambulika na Sayansi

51
hadi kufikia karne kadhaa baadae. Jambo hili linanipa ushahidi
kuwa Muhammada ni mjumbe wa Mungu/Allah.‖

Hatua za makuzi ya mtoto ndani ya tumbo la mama:


Allah (Subhanahu) amesema ndani ya Qur‘an akifafanua juu ya
hatua ambazo mwanadamu hupitia akiwa katika tumbo la mama
yake kuwa;
―Kwa yakini tumemuumba mtu kutokana na asili ya udongo.
Kisha tukamjaalia awe tone la mbegu la uzazi katika kalio
maadhubuti. Kisha tukaliumba tone kuwa damu iliyo ganda,
na tukaiumba damu kuwa pande la nyama, kisha tukaliumba
pande la nyama kuwa mifupa, na mifupa tukaivika nyama.
Kisha tukamfanya kiumbe mwengine mpya. Basi ametukuka
Allah Mbora wa waumbaji.‖ (23:12-14)

Yusuf Alhaj Ahmed, aliandika katika kitabu chake cha „Miujiza


isiyotetereka ya Qur‟an‟ akieleza habari ya Profesa Marshal
Johnson ambae alisomewa aya ya Qur‘an inayofafanua juu ya
hatua ambazo mwanadamu hupitia akiwa ndani ya tumbo la
mama yake kama zilivyokuja ndani ya Surat Az-Zumar na Surat
An-Nuhu, Allah (Subhanahu) aliposema;
―Amekuumbeni kutokana na nafsi moja. Kisha akamfanya
mwenziwe katika nafsi ile ile. Na akakuleteeni wanyama wa
mifugo jozi nane. Anakuumbeni katika matumbo ya mama zenu,
umbo baada ya umbo katika viza vitatu. (39:06)

52
Allah (Subhanahu) amesema pia;
―Mna nini hamueki heshima kwa Allah? Na hali Yeye
kakuumbeni daraja baada ya daraja.‖ (71:13-14)

Prosefa Marshal baada ya kusikia maneno hayo ya Allah


(Subhanahu) alisikika akisema kwa mshangao mkubwa kuwa
jambo hili haliwezekani, na kama ni kweli Qur‘an imeeleza
masuala haya kwa Muhammad, huenda moja kati ya mambo
matatu yanaweza kuwa yametokea. Profesa Marshal alieleza
kuwa jambo la kwanza; ―Kama ni kweli Qur‘an aliyoshushwa
kwa Muhammad imesema haya, basi bila shaka alikuwa na kifaa
aina ya darubini yenye uwezo mkubwa ambao iliweza
kumuwezesha kukagua na kuchambua kila hatua za maendeleo
ya mtoto akiwa tumboni mwa mama yake.‖

Dhana ya kwamba Mtume alimiliki kifaa hichi, haikuweza kuwa


na mashiko kwa kuwa sayansi haikuweza kuvumbua kifaa
chenye uwezo wa kuona maendeleo ya mtoto hadi ilipofika
miaka ya 1940, miaka takribani 1200 baada ya Qur‘an
kushushwa.

Pili; Profesa Marshal alisema kuwa kama hivyo sivyo, basi elimu
juu ya hatua hizo ambazo mwanadamu anapitia katika tumbo la
mama yake ilikuwa ni elimu ya kubahatisha ambayo ilikuja

53
kuendana na matokeo ya kisayansi. Hoja hii haikuwa na uzito
kwakuwa kadiri matokeo ya sayansi yalivyokuwa yanashamiri,
ndivyo iliendelea kuthibitishwa kuwa Qur‘an ilishatangulia
ugunduzi wao. Hivyo Mtume wa Allah (Sala na Amani ziwe juu
yake) asingeweza kubahatisha na kupatia kila kitu.

Tatu; kama sio hayo yote mawili, basi lazima Muhammad atakua
ni Mtume na Mjumbe wa Allah (Subhanahu) na amepewa elimu
na mwenye elimu zaidi ya mambo. Hii ndio hoja ya yenye nguvu
na inayoonyesha ukomavu wa elimu na ambayo inampasa kila
mtu aweze kuibeba na kuiamini.

Kwa upande mwengine, Profesa Keith Moore alisema kuwa


hatua za umbwaji na maendeleo ya mwanadamu
zilizofafanuliwa ndani ya Qur‘an zimeelezwa kwa ufasaha zaidi,
na niwepesi kuweza kuzitofautisha. Sababu kubwa ni kwamba
hatua zilizotajwa ndani ya Qur‘an zinafafanua kila hatua
kutokana na umbile la mtoto kuanzia anapokuwa mbegu ya
uzazi hadi kufikia hatua ya kuwa kiumbe hai. Tofauti na hatua
hizo hizo zinavyoelezea na wanasayansi kwa kutumia hisabu ya
wiki na nambari ikianza na hatua kwanza hadi ya nne.

Profesa Keith Moore, anakiri kuwa katika kitabu chake cha


„Developing Human‟ ametumia zaidi falsafa ya Qur‘an katika
kuzifafanua hatua za kukuwa kwa mwanadamu, na kwa mujibu
wa chapisho lake anazifafanua hatua hizo kama ifuatavyo;
Hatua ya kwanza, ni ile ambayo Qur‘an imeieleza kuwa ni tone
la maji ya uzazi, ambayo kwa mujibu wa Profesa Moore
anasema kuwa maji haya yanapofikia siku ya ishirini na nne
mbegu hiyo huonekana kama umbo la ruba (mchoro A) na kisha
umbile hilo hubadilika na kuwa umbile la pande la damu
lililotulia (mchoro B)

54
Profesa Moore akaendelea kueleza kuwa baada ya hatua hiyo,
mwanadamu hupitia katika hatua za kuwa ni pande la nyama
ambalo mwanzo wake huwa na pingili kama za mgongo ama
shanga (mchoro A), kisha katika siku ya ishirini na nane ndipo
mabadiliko ya pande hilo la nyama huanza, tayari kwa ajili ya
kuwekwa mifupa (mchoro B)

Katika siku ya hamsini na mbili na kuendelea, Profesa Moore


anasema kuwa hiyo ndio hatua ambayo baadhi ya tabia na sifa
za kibinadamu huanza kuonekana kwa mtoto aliyeko tumboni,
na hapo ndipo mifupa na ishara za viungo vyengine huonekana.

55
Profesa Moore akaendelea kueleza kuwa hatua inayofuata
baada hiyo ni ile hatua ya makuzi ya kasi na mabadiliko ya
haraka kwa mtoto. Hatua ambayo viungo vyote muhimu tayari
vimeshapandikizwa kuanzia macho, pua, mikono, miguu, na
vyengine. Na ndio hatua ambayo kiumbe anaweza kuzaliwa na
kuwa salama hata kama ikitokea kuzaliwa kabla ya muda wake
kufika. Akaongeza kuwa hatua hii ndio ile ambayo Qur‘an
iliposema kuwa “Kisha tukamfanya kuwa kiumbe
mwengine mpya”

Kwa hakika ametakasika Allah (Subhanahu) mbora wa kuumba.

Qur‟an na Kalenda (Moon and Solar Calenders)


Miongoni mwa mambo makubwa ambayo yanathibitisha kuwa
Qur‘an ipo mbele ya wakati na ilishafafanua kila kitu ambacho
kinahitaji ujuzi na utaalamu wa sayansi ili kuzifahamu, ni pamoja
na namna ambavyo Qur‘an ilivyozungumzia kwa kina kuhusu
elimu ya hisabu za kalenda. Miongoni mwa matokeo ya sayansi

56
ya karne ya ishirini na ishirini na moja, ni vipimo vya masiku,
miezi, na miaka ambayo hupimwa na kuhesabiwa kwa ustadi
kwa kutumia kalenda za kisasa.
Allah (Subhanahu) amesema ndani ya Surat Al-Kahf;
﴾٢٥﴿‫سعب‬
ْ ِ‫ي َوٱ ْش َدادو ْا ت‬ ْ ‫َولَبِثى ْا فًِ َك ْه ِف ِه‬
ِ ‫ن ثَالثَ ِهئَة‬
َ ‫سٌِي‬
―Na walikaa katika pango lao miaka mia tatu, na wakazidisha
tisa‖ (18:25)
Kauli hii ya Allah (Subhanahu) inawazungumzia waja wake
ambao walikimbia katika mji wao kwa kuogopa fitna na uadui na
kuamua kwenda kujificha katika pango ambalo kwa mujibu wa
Qur‘an tukufu walikaa ndani yake kwa muda wa miaka mia tatu
na wakaongeza miaka mengine tisa. Kauli hii ni miongoni mwa
maajabu makubwa ya Qur‘an ambayo ilishushwa karne ya saba.
Ndani ya kauli hii juu ya idadi ya miaka kuna elimu kubwa
ambayo imefunganishwa ndani yake, elimu ambayo kwa undani
unaelezea utofauti wa hisabu za kalenda ambazo huhesabiwa
kufuata mwenendo wa jua na zile ambazo hufuata mwenendo
wa mwezi (muandamo).
Ibn Kathir (Rehma za Allah ziwe juu yake) akifafanua maana ya
kauli ya Allah (Subhanahu) juu ya; “Miaka mia tatu, na
wakazidisha tisa” amesema katika tafsiri yake ya Qur‘an
kuwa; Urefu wa muda ulikuwa miaka mia tatu pamoja na tisa
katika miaka ya mwezi mwandamo, ambayo ni miaka mia tatu
katika miaka ya jua. Tofauti kati ya miaka mia moja ya
mwandamo na miaka mia ya jua ni miaka mitatu, ndio maana
baada ya kutaja mia tatu, Allah (Subhanahu) anasema
akaongeza tisa.

Qur‘an iliyoteremshwa karne ya saba kupitia aya hii, ilikuwa


inamfundisha Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) juu ya
hesabu za miaka katika kalenda za mwezi mwandamo na
kalenda za mwezi unaofuata mwenendo wa jua.

57
Wasomi na wanasayasi wa hisabati, hawakulijua jambo hili hadi
ilipofika karne ya ishirini na ishirini na moja, ndipo walipokuja
kujua kuwa kwa kufuata mwezi mwandamo mwaka unakuwa na
siku mia tatu hamsini na nne tu, na kwa kufuata mwezi
unaofuata mwenendo wa jua, mwaka huwa na siku mia tatu na
sitini na tano. Ambapo tofauti ya mwaka wa mwezi mwandamo
na mwaka wa jua ni siku kumi na mbili. Hivyo, miaka mia tatu
kwa mwaka wa jua ni sawa na miaka mia tatu na tisa kwa
mwaka wa mwezi mwandamo. Hii ni miongoni mwa dalili kuwa
Qur‘an ipo mbele ya muda na itaendelea kuwa mbele ya muda.

Qur‟an na Nguvu ya mvutano (Force of Gravity)


Qur‘an tukufu katika karne ya saba ilishatoa ishara juu ya
uwepo wa vitu ambavyo vinaonekana kwa macho ya kawaida ya
mwanadamu, na vile ambavyo havionekani. Tunaposema kuwa
Karne ya saba ndiyo karne ya sayansi na teknolojia
tunamaanisha kuwa ndio ilikuwa karne iliyo bainisha mambo
mengi makubwa ambayo yanahitaji elimu na ujuzi wa hali ya juu
kuyafahamu.
Allah (Subhanahu) kupitia Surat Al-Haaqqa amesema;
﴾٣٣﴿ َ‫صسوى‬
ِ ‫﴾ َو َهب ال َ ت ْب‬٣٣﴿ َ‫صسوى‬
ِ ‫وب ت ْب‬ ِ ‫َفال َ أ ْق‬
َ ِ‫سن ب‬
―Basi naapa kwa mnavyo viona, Na msivyo viona‖ (69:38-39)

58
Allah (Subhanahu) ametumia kiapo katika kueleza juu ya uwepo
wa vitu vingi ndani ya ulimwengu ambavyo vyengine amewapa
wanadamu uwezo wa kuviona kwa macho yao ya kawaida, na
vipo miongoni mwa vitu hivyo ambavyo havionekani kwa macho
ya kawaida. Mara zote Allah (Subhanahu) anapotaka kuelezea
mambo makubwa ambayo yanahitaji umakini wa viumbe,
hutumia viapo akiashiria uzito wa ujumbe huo.
Miongoni mwa vitu visivyoonekana, wanasayansi wa karne ya
ishirini na ishirini na moja wamekuja kugundua kuwa upo
mwangaza ambao hauonekani kwa macho ya mwanadamu
(Invisible light) wakasema kuwa; Urefu wa mawimbi ya
mwangaza hupimwa kwa nanomita. Nanomita moja ni sawa na
bilioni ya mita. Mwangaza unaoonekana una urefu wa mawimbi
kuanzia takribani nanomita 400 hadi nanomita 700. Mawimbi
mafupi kuliko nanomita 400 au zaidi ya nanomita 700,
hayaonekani kwa macho ya binadamu. Utafiti huu ni kwa mujibu
wa jarida la Discovering the Universe la mwaka 2002.
Kutokaana na ufafanuzi huo si shaka kuwa ugunduzi huu
umeikiri Qur‘an kupitia aya ya 38-39 ya Surat Al-Haaqqa
iliyoshushwa karne kumi na nne zilizopita.

Kupitia mwangaza huu usionekana, ndio ambao hutumika katika


mambo kadhaa wa kadhaa, kama vile kutumika katika kifaa cha
kuangalia mifupa (X-Rays Machine) ambacho huutumia
mwangaza kupenya kwenye mwili wa mwanadamu na
kumuezesha binadamu kuona mfupa uliopo ndani ya mwili
ambao bila huu mwangaza isingekuwa rahisi kuonekana.

59
Kadhalika, katika kuthibitisha kuwa Qur‘an ipo mbele ya wakati,
na kwamba wanasayansi ya karne ya ishirini na ishirini na moja
kuna mambo mengi ambayo hawakuyajua kabla, hali ya kuwa
Qur‘an ilishayashiria na kuyafafanua katika karne ya saba. Allah
(Subhanahu) kupitia Surah Luqman amesema;
ِ َ‫ً أَى ت‬
‫وي َد‬ َ ‫س‬ ِ ‫ود تَ َس ْوًَ َهب َوأَ ْلقًَ فًِ ٱألَ ْز‬
ِ ‫ض َز َوا‬ َ ‫وب َواتِ بِ َغ ْي ِس َع‬
َ ‫ٱلس‬
َّ َ َ ‫خل‬
‫ق‬ َ
﴾١١﴿‫ن‬ْ ‫بِك‬
―Ameziumba mbingu bila ya nguzo mnazo ziona; na ameweka
katika ardhi milima ili isikuyumbisheni.‖ (31:10)
Ibn Kathir (Radhi za Allah ziwe juu yake) katika tafsiri yake
amesema juu ya kauli ya Allah (Subhanahu); “Ameziumba
mbingu bila ya nguzo mnazo ziona” kuwa kauli hii ni
ushahidi wa Tawhid ambao Allah (Subhanahu) anaeleza nguvu
zake za hali ya juu katika kuumba mbingu na ardhi na vyote
ambavyo vimo katikati yake. Akiendelea kufafanua juu ya kauli
kuhusu nguzo zisizo onekana, Ibn Kathir (Radhi za Allah ziwe
juu yake) amewanukuu Al-Hasan na Qatadah (Radhi za Allah
ziwe juu yao wote) wamesema kuwa; Mbingu haina nguzo
zozote, zinazoonekana wala zisizo onekana.
As Saadi (Rehma za Allah ziwe juu yake) katika kutafsiri kauli ya
Allah (Subhanahu) kuwa; ―Ameziumba mbingu bila ya
nguzo mnazo ziona” amesema kuwa; Allah (Subhanahu)
anapambanua nguvu na ukuu wake kwa waja wake
kuwaonesha baadhi ya ishara zake na miongoni mwa maajabu
ya uumbaji wake na ukarimu wake.
Hiyo ni Qur‘an iliyoshushwa kwa Mtume wa Allah (Subhanahu)
miaka 1400 iliyopita, ambapo baada ya karne kadhaa kupita,
wanasayansi wa kisasa waliipitia na kuitumia aya hii katika
nidhamu za kitafiti. So hivyo tu, bali matokeo ya tafiti zao katika
karne ya kumi na nane yakaja pia kubaini kuwa baina ya
mbingu na ardhi ipo nguvu ya asili ambayo kazi yake kubwa ni
kuzuia maumbile yote ya mbingu na vile vilivyobebwa,
visianguke katika mgongo wa ardhi. Uthibitisho wa hili ulitolewa
na mwanasayansi mashughuri Issac Newton alipokuja na

60
dhana yake ya ―Nguvu za Mvutano‖ kitaalamu inaitwa
“Gravitational Force”
Kwa mujibu wa ugunduzi wa mwanasayansi Issac Newton
anahoji kuwa; umewahi kujiuliza jinsi sayari hulizunguka jua?
dunia inavyouvuta mwezi katika mzunguko wake, na mwezi
unaivutia dunia, kwa hivyo zote hazipaswi kugongana? kwanini
mwezi hauanguki? kwa nini inaendelea kuizunguka dunia? Hoja
hizi zote zinajibiwa na nguvu ya mvutano kati ya mbingu na
ardhi ambazo ndizo hufanya kila kitu kuenda katika utaratibu
ambao Allah (Subhanahu) ameuweka na kuvifanya viwe na
utulivu kwa amri na matakwa yake.

Kwa mujibu wa Issac Newton amesema kuwa; mvuto (gravity)


ni nguvu inayounganisha mihimili miwili, kisha mwanasayansi
huyo akatoa baadhi ya mifano ya nguvu hiyo ya mvutano na
kusema kuwa;
 Ipo nguvu inayofanya kazi kati ya Jua na Dunia zisikusane
na kugongana.
 Ipo nguvu inayowajibika na kuufanya mwezi kuzunguka
Dunia.
 Ipo nguvu ambayo huyafanya mawimbi ya bahari
kuongozwa na nguvu kutokana na mwezi.
 Ipo nguvu ambayo inashikilia gesi zote kwenye jua.
 Kuna nguvu inayotenda juu yetu hutufanya tutembee
ardhini na kutufanya tusielee angani. Jambo ambalo

61
halipo kwenye baadhi ya sayari nyengine. (Ndio maana
mara zote wana anga huonekana kuelea bila kugusa chini
wawapo nje ya dunia kwakuwa hakuna nguvu ya
mvutano yani zero gravity)

Umbile la Dunia, Mzunguko, na Kivuli


Katika kuzichambua kwa uchache baadhi ya nguvu za mvutano
ambazo amezizungumza mwanasayansi huyu juu ya nguvu
ambayo inasababisha mawimbi ya bahari kupwa na kujaa,
baadhi ya wanasayansi wa mambo ya bahari wanasema kuwa
mwenendo wa mwezi ndio haswa unao endesha tabia ya bahari
ya kupwa na kujaa, ikisaidiana kwa karibu na namna ambavyo
Allah (Subhanahu) alivyoiumba dunia kuwa na umbile la duara
tenge (Umbo la yai). Katika mazingira ya kawaida, kwa wale
wafuatiliaji wa tabia ya bahari wanaweza kuthibitisha kuwa
kadiri mwezi unavyo kuwa, ndivyo tabia ya mawimbi ya bahari
yanavyobadilika.

Ukienda mbali zaidi kwenye sayansi hii, utagundua na


kuthibitisha kuwa inapotokea kupatwa kwa mwezi, mawimbi ya
bahari husogea zaidi katika ardhi kuliko kipindi cha kawaida cha
kuchomoza na kuzama kwa mwezi. Ambayo hii inathibitisha ile
nguvu ya mvutano ambayo mwezi kuongoza mawimbi ya
bahari.

Aidha, kwa mujibu wa wanasayansi wa mambo ya bahari,


wanathibitisha kuwa umbile la dunia kuwa ni duara tenge (umbo
la yai) ndilo linalosababisha kupatika kwa hali ya kupwa na
kujaa kwa maji. Sababu kuu ikiwa ni umbile la dunia, na laiti
kuwa dunia ingeumbwa katika umbile la mviringo basi
kusingekuwa na uwezekano wa kupatikana ardhi kavu bila ya
maji ya bahari.

Allah (Subhanahu) amesema pia ndani ya Qur‘an tukufu karne


ya saba akithibitisha juu ya umbile la dunia kupitia kivuli kama
alivyosema ndani ya Surat Al- Furqaan;

62
―Je! Huoni jinsi Mola wako Mlezi anavyo kitandaza kivuli. Na
angeli taka angeli kifanya kikatulia tu. Kisha tumelifanya jua
kuwa ni kiongozi wake. (25:45)

Ibn Kathir (Rehma za Allah ziwe juu yake) katika kutafsiri kauli
ya Allah (Subhanahu) aliposema kuwa; “Je! Huoni jinsi Mola
wako Mlezi anavyo kitandaza kivuli.” Amewanukuu Ibn
Abbas, Ibn Umar, Mujahid na wengine wakisema kuwa; Kivuli
katika aya hii kinakusudiwa ni kipindi cha kuanzia mwanzo wa
machweo hadi jua linapochomoza.

Wanasayansi wa karne ya ishirini na ishirini na moja wamekuja


kuikiri Qur‘an kwa kuthibitiha kuwa kutokana na umbile la dunia,
pamoja na mzunguko wake ndio unaotengeneza pande mbili za
dunia ambazo, moja huwa na mwangaza wa jua na nyengine
kuwa na kiza ama kivuli. Kwa mujibu jarida la “The Science of
Sunlight and Shadows” liloandikwa na Sandy Robert
(2022); Sandy anasema; ―Inachukua saa 24 kwa Dunia
kukamilisha mzunguko mmoja kwenye muhimili wake.
Mzunguko huu huweka baadhi ya sehemu za dunia kwenye
mwangaza wa jua unapogeuka. Wakati sehemu moja ya dunia
inapolikabili jua, huwa na mchana. Na pindi sehemu hiyo ya
dunia inapogeukia mbali na Jua, huwa na usiku. Sehemu ya
dunia iliyo karibu na Jua wakati wowote inapata jua moja kwa
moja kwa karibu zaidi.‖

Akaongezea kusema kuwa; Wakati mwingine mwangaza huo


huzuiwa. Unaona hali ya kuzuiwa kwa sehemu ya dunia kila
wakati unapotazama kivuli chako au kusimama chini ya kivuli
cha mti. Kwa sababu dunia inazunguka, pembe ya mti huo
kuhusiana na jua hubadilika wakati wa mchana. Kwa hivyo saizi
na mwelekeo wa kivuli hubadilika pia.

63
(Picha kwa hisani ya mtandao wa Science Friday)

Hivyo ndivyo Allah (Subhanahu) alivyofanunua juu ya mzunguko


wa dunia ambao ndio huzalisha kivuli. Kivuli ambacho
wanasayansi wa karne ishirini na ishirini na moja wamekuja
kuikiri Qur‘an juu ya habari hiyo. Ingawaje wanasayansi
wamesema kuwa kuvuli hicho ni kile cha jua linapoanza
kuchomoza, baadhi ya wafasiri wa Qur‘an wameenda mbali zaidi
na kufafanua kivuli alichokitaja Allah (Subhanahu) kuwa pia
kilikusudiwa kile kivuli cha usiku unapo ingia.

Ufafanuzi huu wakauthibitisha kwa kauli nyengine ya Allah


(Subhanahu) aliposema;

―Sema: Mwaonaje, Allah angeli ufanya usiku umekukalieni moja


kwa moja mpaka siku ya kiyama. Mungu gani asiye kuwa Allah
atakae kuleteeni mwangaza? (28:71)

Hizi zote ni ithibati kuwa Allah (Subhanahu) ameiumba dunia


katika umbile lake na kulipangia mwenendo wake, na akaifanya
iwe na vizuizi ambavyo ndivyo vitaizuia isiwatingishe
walimwengu kutokana na mzunguko wake. Mzunguko ambao
ukazalisha kivuli chenye kuja na kuondoka. Jambo hilo pia
limekuja kuthibitishwa na wanasayansi takribani miaka 1400

64
baada ya Qur‘an kushushwa, kwa hakika angetaka basi
angekifanya kivuli hicho ni chenye kubaki moja kwa moja.

Tukiendelea kuifanyia uchambuzi aya ya Surat Luqman, Ibn


kathir (Rehma za Allah ziwe juu yake) amesema kuhusu kauli ya
Allah (Subhanahu) “Na ameweka katika ardhi milima ili
isikuyumbisheni.” Maana yake ni kwamba; Milima inayo
tengemaa na kuipa ardhi mizani, isije ikatikisika kwa maji yake.
Kwa kauli hii ya Allah (Subhanahu) ilithibitisha kuwa dunia
inazunguka na kutembea hivyo, ili viumbe tusiweze kuhisi wala
kutingishwa na mzunguko huo, Allah (Subhanahu) ameiweka
milima kutengeneza utulivu wa wa dunia. Hili linathibitishwa na
wanasayansi wa anga katika karne ya 18 walikuja kuthibitisha
hilo; nikinukuu Makala ya “CoolCosmos” wamesema kuwa;
Dunia Inazunguka kwa kasi ya takriban maili 1,000 (kilomita
1600) kwa saa na kulizunguka Jua kwa kasi ya maili 67,000
(kilomita 107,000) kwa saa.

Hatuhisi mwendo wowote kwa sababu kasi hizi ni za kudumu.


Kasi inayozunguka na ya mzunguko wa Dunia huwa na usawa,
kwa hivyo hatuhisi kuongeza kasi au kushuka kwa kasi.
Unaweza tu kuhisi mwendo ikiwa kasi yako itabadilika.

Kwa mfano, ikiwa uko kwenye gari ambalo linatembea kwa kasi
ya kufanana kwenye barabara iliyonyooka, huwezi kujisikia
mwendo mwingi. Walakini, gari linapoongeza kasi au
kupunguzwa kwa mwendo kwa kuzuia breki, unahisi mwendo na
mabadiliko hayo.

Allah (Subhanahu) kupitia Qur‘an ambayo aliishusha karne ya ya


saba, alishaeleza juu ya namna ambavyo dunia inazunguka na
namna ambavyo imeiwekea mihimili yake ili isiwatingishe wala
kuwaangusha viumbe wengine. Na haya ndio miongoni mwa
maajabu ya Qur‘an yanayothibitisha kuwa Qur‘an siku zote
imekuwa mbele ya wakati na mbele zaidi ya Sayansi na gunduzi
kadhaa wa kadhaa katika karne baada ya kushushwa kwa

65
Qur‘an. Miongoni mwa thibitisho hizo ni kama vile ugunduzi wa
nguvu mvutano (gravitational forces).

Umeshawahi kusikia ama kuona jua linawaka katikati ya usiku


wa manane? Wanasayansi wa Jografia ya dunia wanaeleza
kuwa; Jua la usiku wa manane (midnight sun) ni tukio la asili
linalotokea wakati wa kiangazi katika maeneo ya kusini mwa
mzingo wa Antarctic na kaskazini mwa mzingo wa Aktiki - ikiwa
ni pamoja na Norway ya Kaskazini.

Dunia inazunguka kwenye muhimili ulioinama unaohusiana na


jua, na wakati wa miezi ya kiangazi, Ncha ya Kaskazini inaelekea
kwenye dunia yetu. Ndio sababu, kwa wiki kadhaa, jua halitui
juu ya mzingo wa Aktiki. Svalbard ni mahali nchini Norway
ambapo jua la usiku wa manane hutokea kwa muda mrefu zaidi.
Hapa, jua halitui kati ya tarehe 20 Aprili na 22 Agosti (Miezi
Mitano).

(Picha ya moja kati ya siku ambazo jua halizami, picha


imechukuliwa katikati ya usiku wa manane)

Allah (Subhanahu) alishafafanua kupitia Qur‘an iliyoshushwa


karne ya saba. Amefafanua juu ya watu wa miji hii, ambao kwao
hawakuwekewa pazia la kuwakinga na jua. Allah (Subhanahu)
anasema ndani ya Surat Al-Kahf;

66
ْ ‫ج َعل لَّه‬
‫ن ِهي‬ ْ َّ‫طلع َعلًَ َق ْىم ل‬
ْ ًَ ‫ن‬ ْ َ ‫هب ت‬
َ ‫ج َد‬
َ ‫س َو‬
ِ ‫و‬
ْ ‫ٱلش‬
َّ ‫ع‬
َ ‫ط ِل‬ َ َ‫ح َّتً إِذَا َبل‬
ْ ‫غ َه‬ َ
﴾٣١﴿‫س ْتسا‬ ِ ‫دوًِ َهب‬
―Hata alipo fika matokeo ya jua aliliona linawachomozea watu
tusio wawekea pazia la kuwakinga nalo.‖ (18:90)
Baadhi ya wafasiri wa Qur‘an (wa karne za sasa) wameitafsiri
aya hii kuashiria maeneo hayo ambayo jua kwa takribani miezi
mitano halizami na kusema kuwa kutokuzama kwa jua ndio
pazia ambalo hawakuwekewa. Ingawaje, wafasiri wengine
wanasema kuwa pazia lilokusudiwa ni nyumba za makazi na
nguo za kujistiri. Hizi zote ni dalili kuwa Qur‘an imeitangulia
sayansi kwa kipindi kikubwa. Maana ni dhahiri kuwa bila ya
uwepo wa utandawazi, ingekuwa vigumu kujua kuwa ipo
sehemu ndani ya dunia hii ambayo wanapitia katika kipindi
ambacho hakuna usiku wenye kiza, kutokana na jua kutozama.
Ametakasika Allah (Subhanahu).

Nguvu ya Mvutano na Sayansi ya Ndege Ulaya


Uwepo wa nguvu hizi, ndizo ambazo zimesaidia kwa kiasi
kikubwa ugunduzi wa usafiri wa anga (Ndege Ulaya) ambazo
hutumia nguvu mvutano hizi kuiwezesha kupaa angani, kusafiri
na kutua ardhini. Elimu na ujuzi wa namna ya kuiunda ndege
Ulaya moja kwa moja umetoka kupitia Qur‘an ikiwa inamuelezea
ndege mnyama anavyopaa angani na kutua.
Allah (Subhanahu) anasema ndani ya Surat Al-Mulk;
―Kwani hawawaoni ndege walioko juu yao namna wanavyo
zikunjua mbawa zao, na kuzikunja? Hawawashikilii ila Mwingi wa
Rehema (Allah). Hakika Yeye ni Mwenye kuona kila kitu.‖
(67:19)

Ibn Kathir (Rehma za Allah ziwe juu yake) katika tafsiri yake,
amesema juu ya kauli ya Allah (Subhanahu) “Wanavyo
zikunjua mbawa zao na kuzikunja” maana yake ni
kwamba; wakati fulani hutandaza mbawa zao kwa upepo
(kuteleza) na nyakati nyengine huzikusanya na kutandaza
(kupeperusha) mbawa wakati wa kuruka. Aidha akasema
kuhusu kauli ya Allah kuwa; “Hawashikilii ila Mwingi wa
Rehema” kuwa maana yake ni kuwa; Allah (Subhanahu)
67
huwainua juu hewani kwa kuwatiishia upepo kwa REHEMA ZAKE
na upole WAKE.

Unaweza kuona maneno machache yaliyotumika ndani ya


Qur‘an ikimuelezea ndege anavyopaa angani kwa kutumia
mbawa zake na Rehma za Allah (Subhanahu) kuufanya upepo
uwapeperushe, ila kwa kutumia elimu hiyo wanasayansi wa
karne ya kumi wameitumia kuunda na kufanikisha kwa idhini ya
Allah (Subhanahu) kifaa ambacho kinafanana kiumbo na kitabia
na mnyama ndege. Kwa mujibu wa sayansi ya uhandisi wa
ndege ulaya, ili ndege iweze kupaa, kwanza; ni lazima pua yake
iwe imechongoka, kama Allah (Subhanahu) alivyo uumba
mdomo wa ndege mnyama.

Kadhalika, kwa mujibu wa Qur‘an (aya tuliyoieleza hapo juu) ili


kiumbe ndege aruke ni lazima atawanye mbawa zake kuruhusu
hewa iingie ndani ya mabawa na ile nguvu ya mvutano
imsukume kwa kasi. sayansi hiyo hiyo imetumika kuunda ndege
ulaya na kuifanya iwe na mabawa mawili ambayo ndani yake
kumewekwa vimbawa vyembamba ambavyo rubani huvitanua
wakati wa kupaa, na kuvikunja wakati wa kutua (Kitaalamu
huitwa Reverse Thrust) ambavyo kitaalamu vinaitwa (Wings
Flaps and Spoilers)

(Picha imepatikana kwenye mtandao wa google)

Hivyo hivyo, ili kiumbe ndege aweze kuelea na kusafiri kwa


muda mrefu juu ya anga, Allah (Subhanahu) amemuumba akiwa

68
na mifupa michache na isiyo na uzito mkubwa ili kumfanya
alingane na kasi ya upepo na hewa iliopo angani. Na kwa
upande wa ndege ulaya, waundaji wakafata nidhamu hii ya
Qur‘an na kuiunda ndege kwa kutumia mali ghafi nyepesi
ambazo huitwa mali ghafi za teknolojia ya juu, pamoja vifaa
vyengine ambavyo vimetayarishwa maalumu kuwa vyepesi.
Wahandisi wa ndege ulaya wanasema kuwa ndege ili iweze
kuruka na kuelea angani ni lazima iundwe kwa kutumia asilimia
hamsini ya mali ghafi hizo nyepesi, asilimia ishirini ya
aluminiamu, asilimia kumi na tano ya titanium, huku asilimia
kumi ya chuma na shaba (hutumika kuunda dhana za kutuwa)

(Picha imepatikana kwenye mtandao wa Google)

Allah (Subhanahu) alivyomuumba kiumbe ndege amemjaalia


kuweza kuvuta na kuhifadhi gesi ya oksijini kabla ya kuruka kwa
kiwango ambacho kitatosha kwa kipindi chote akiwa anaelea
kwenye anga. Cha kushangaza zaidi, ndege ulaya pia, wahandisi
wa ndege wameziunda kwa kupewa uwezo wa kukusanya gesi
hiyo kwa ajili ya matumizi wakati wote wa safari na ule wakati
wa dharura.

69
(Picha zimepatikana kwenye mtandao wa Google)

Naweza kuthibitisha kuwa ujenzi na uundaji wa ndege ulaya


(ndege za kubeba abiria na mizigo) zimeundwa kwa kutumia
elimu kubwa iliopo kwa kiumbe cha Allah (Subhanahu) ndege
mnyama. Wakati tukifanya uchambuzi huu tulibaini kuwa ndege
ulaya imebeba sifa zote za ndege mnyama wakati wa kupaa na
kutua. Namna ambavyo ndege ulaya ilivyoundwa ni kuwa;
katika hatua za kupaa angani hutumia matairi yake (Landing
gears) kuvuta kasi na mara tu baada ya kuacha ardhi, matairi
hayo hufungiwa ndani ya mahala maalumu ili kuiruhusu ipae
bila wasi wasi.

70
Kwa upande mwengine, ndege mnyama pia hutumia miguu
yake miwili kukimbia na kuvuta kasi ya kuruka. Mara baada ya
kuacha ardhi hukunja miguu yake ndani ya tumbo lake kwa
hekima na elimu ya Allah (Subhanahu)

71
Kadhalika, nidhamu hiyo hiyo imetumika katika kuunda namna
ambavyo ndege ulaya hutumia matairi (maringi/landing gears)
kutua na kuiwezesha kutembea katika barabara maalumu
(runway). Namna hiyo pia ndivyo ambavyo ndege mnyama
alivyoumbwa na Allah (Subhanahu) kwamba hutumia miguu
yake miwili kusaidia kutua katika adhri. Ndege mnyama huanza
kuifungua/kuifichua miguu yake kutoka katika manyoya ya
tumbo na mbavu zake mara tu anapokaribia kutua katika ardhi.
Jambo ambalo limefanywa kwa nidhamu sawa na hatua za
kiusalama za kutua kwa ndege ulaya. Kwa mujibu wa hatua za
usalama za kutua kwa ndege, inatakiwa inapokaribia wastani wa
baina ya futi 1000 hadi 500 rubani hupaswa kuanza kufungua
matairi kutoka katika sehemu maalumu na kuyaweka tayari kwa
ajili ya kumsaidia kutua kwenye ardhi.

72
Kutokana na haya yote, Je! Bado tunaweza kusema kuwa
Qur‘an imepitwa na wakati kwa kuwa ilishushwa katika karne ya
saba ambayo haikuwa na uwezo wa kugundua na kufafanua kila
nukta za ishara za kisayansi? Kujibu kauli hii, Allah (Subhanahu)
katika ujumbe wa kwanza wa kushushwa kwa Qur‘an alisema
kumwambia Mtume wake;

﴾٥﴿‫ن‬
ْ َ‫ن يَ ْعل‬
ْ َ‫ًسبىَ َهب ل‬
َ ‫ٱإل‬
ِ ‫ن‬َ َّ‫َعل‬
‖Kamfundisha mwanadamu aliyokuwa hayajui‖ (96:05)
Ibn Kathir (Rehma za Allah ziwe juu yake) amesema katika
Tafsiri kuwa; Kuna simulizi inayosema, "Yatunze maarifa (Elimu)
kwa kuyaandika." Vilevile, kuna msemo usemao: "Mwenye

73
kutenda kulingana na anachokijua, Allah (Subhanahu) atampa
elimu asiyoijua." Aidha, amesema pia; Allah (Subhanahu)
alimtukuza mwanadamu kwa kumpa elimu, na ni hadhi ambayo
Baba wa Wanaadamu, alitukuka kuliko Malaika.

Qur‟an na Kemia ya Mmenyuko (Kutu/Rust)


Kwa mujibu wa wanasayansi wa Kemia (Chemistry) wanasema
kuwa, Kutu ni mmenyuko wa oxidasheni. Chuma humenyuka
pamoja na maji na oksijeni na kuunda oksidi ya chuma yenye
kiwango cha tatu, ambayo tunaona kama kutu. Chuma
inapogusana na maji na oksijeni ndipo huzalisha matokeo ya
kutu. Baada ya majaribio kadhaa, wakagundua njia ambazo
zinaweza kuifanya chuma isimenyuke (kufanya kutu). Miongoni
mwa njia na mbinu za kisayansi ambazo hutumika kuzuia chuma
kufanya kutu ni kwa kutumia shaba ambayo itapakwa juu yake
na kuzuia gesi ya oksidi isiweze kuzalisha kutu juu ya chuma.

Majaribio kadhaa wa kadhaa yamefanyika kuthibitisha ukweli


huu, huku wanafunzi na wanasayansi mbali mbali wakitumia
majaribio hayo kuitafuta dawa ya hakika ya kutu katika chuma.
Kwa mujibu wa jarida la BBC la BITESIZE lilieleza na
kuthibitisha kuwa shaba kwa mujibu wa malighafi zilizo
tengenezewa haiwezi kufanya kutu.

Aidha, wakasema kuwa matumizi ya shaba katika kukilinda


chuma kuota kutu ndio miongoni mwa njia madhubuti za
kuhakikisha hakuna matokeo ya kutu katika chuma ambacho
kimechanganywa ama kufunikwa na madini ya shaba.

Kadhalika, kwa mujibu wa jarida la SPM CHEMISTRY


liloandika juu ya njia za kuzuia mmenyuko (kutu) liliandika
kuwa; Kupakwa kwa chuma na safu nyembamba ya shaba
ambayo haina umeme mkubwa kama vile bati, fedha au shaba
itazuia chuma kilicho chini yake kuguswa na maji na hewa, na
hivyo kuzuia chuma kushika kutu. Yakiwa haya yote ni matokeo

74
ya majaribio ya kisayansi ambayo yalikuwa takribani miaka 1400
baada ya Qur‘an kushushwa.

Qur‘an katika karne ya saba, ilieleza namna ambavyo matumizi


ya shaba yanavyoweza kukilinda chuma kutokana na kutu
wakati inamsimulia Mtume wa Allah (Subhanahu) habari ya mja
mwema Dhul-Qarnaini, alipokuwa akiujenga ukuta mkubwa wa
kihistoria ambao matokeo yake ni kuufanya ukuta huo hadi leo
karne ya ishirini na ishirini na moja kuwa ni miongoni mwa
maajabu makubwa na matokeo makubwa ya kisayansi ambayo
yalifanyika karne ya saba. Allah (Subhanahu) anasema ndani ya
Surat Al-Kahf;

―Hata alipo fika baina ya milima miwili, alikuta nyuma yake watu
ambao takribani hawakuwa wanafahamu lolote. Wakasema:
Ewe Dhul-Qarnaini! Hakika Juju-wa-maajuju wanafanya
uharibifu katika nchi. Basi je, tukulipe ujira ili utujengee baina
yetu na wao ngome?‖ (18:93-94)

Baada ya watu hao kutoa maombi yao kwa mja mwema huyo
aliwajibu kile alichojaaliwa na Allah (Subhanahu) kuwajibu
katika utiifu wake, kisha akawapa mbinu bora zaidi za kumlipa
kuliko ujira walio omba. Hapo ndipo ile sayansi ambayo tulianza
kuifafanua ilitumika na baadae wanasayansi wa karne kadhaa
mbele wakaja kuikiri Qur‘an juu ya sayansi hiyo ya Kemia.

Dhur-Qarnaini aliwajibu kuwa; kama Qur‘an inavyosema:


―Nileteeni vipande vya chuma. Hata alipo ijaza nafasi iliyo kati
ya milima miwili, akasema: Vutukuteni. (Washeni moto
mviunguze vyuma hivyo) Hata alipo kifanya (chuma) kama moto
akasema: nileteeni shaba iliyo yayuka niimwagie.‖ (18:96)
Wafasiri wa Qur‘an wanasema kuwa maana ya kauli ya Allah
(Subhanahu) “Vukuteni” ni kuviunguza vyuma ili viwe kama
matofali ambayo atayapanga baina milima miwili hiyo na kisha
akajaza sehemu ya juu kwa shaba. Kuhusu suala la kumwagia
shaba juu ya chuma ambayo ilifunika baina ya milima ile miwili,

75
Qur‘an, karne ya saba ilikuwa inafundisha matumizi ya shaba
katika kukilinda chuma kisipate kutu.

Allah (Subhanahu) alimpa elimu kiumbe huyu aujenge ukuta


huu uwe ni uzio baina ya watu wa nchi ile na Juju-wa-
maajuju ambao walikuwa wakifanya uharibifu mkubwa. Duru
za kisasa zinatueleza kuwa zipo dalili zinazothibitisha uwepo wa
ukuta mkubwa na nimiongoni mwa kivutio kikubwa cha kitalii
huko nchini China ambao unaitwa ‗The Great Wall of China‘.
Ingawaje hakuna ushahidi wa moja kwa moja kuthibitisha kuwa
ukuta huo uliotajwa ndani ya Qur‘an ndio huu The Great Wall of
China. Jambo la msingi ni kwamba Qur‘an inathibitisha kuwa
matumizi ya shaba huweza kukifanya chuma kisipate athari ya
kutu ambapo ni jambo ambalo liliwachukua wanasayansi miaka
kadhaa kuweza kujua kuhusu elimu hii.

Taarifa za kihistoria zinatueleza kuwa ukuta huu wa china


ulijengwa kuanzia karne ya tano hadi ya nane na lengo kuu
likiwa kuufanya ukuta huo uwe ngome dhidi ya maadui wa nchi
hiyo.

(Picha kwa hisani ya mtandao wa Google)

76
(Picha kwa hisani ya mtandao wa Google)

Katika kuthibitisha kuwa ukuta huo ulikuwa ni ngome ambayo


hadi sasa upo madhubuti na kwa mujibu wa Qur‘an kuwa ukuta
huo ndio ambao umewafungia viumbe hao. Lengo la kujengwa
ukuta huo kwa kutumia chuma na shaba ni kuulinda usiweze
kuharibika kutokana na kutu na kutokana na kuvunjwa na
maajuju, Allah (Subhanahu) alisema pia katika Qur‘an karne ya
saba baada ya kujengwa ukuta huo;
―Basi hawakuweza kuukwea, wala hawakuweza kuutoboa‖
(18:97)

Ibn Kathir (Rehma za Allah ziwe juu yake) amesema kauli ya


Allah (Subhanahu) kuwa; “Hawakuweza kuukwea, wala
hawakuweza kuutoboa” maana yake ni kwamba Allah
(Subhanahu) anatuambia kuwa Ya‘juj wa Ma‘juj hawakuweza
kuupanda wakavuka upande wa pindi (kutokana na urefu wake)
na wala hawakuweza kupenya katika sehemu ya chini kutokana
na umadhubuti wake ulioundwa kwa chuma na shaba. Na
akaongeza kuwa kauli hii inathibitisha ugumu wa kitendo hicho.

77
Qur‟an na Sayansi ya Milima
Qur‘an haikuacha jambo lolote ambalo linathibitisha ukuu wa
Allah (Subhanahu), Qur‘an imekuwa ni kitabu ambacho
kushushwa kwake kumeleta mapinduzi makubwa ya kielimu
hapa duniani, ambapo wasomi, watafiti na wagunduzi nguli
wamekuwa wakiisoma na kuitumia katika masuala kadhaa wa
kadhaa. Msomi na mtaalamu nguli wa sayansi ya bahari
(Marine Science) Professor Tom Garrison mwaka 2014 aliandika
kitabu chake “Oceanography” ikiwa ni matokeo ya utafiti
wake kuhusu tabia ya milima.

Mwanasayansi huyo aligundua kuwa katika ardhi ambayo


tunaikanyaga ni moja kati ya sehemu au matabaka saba ya
ardhi ambalo limeenda chini zaidi ya kilomita elfu mbili.
Akasema pia baada ya tabaka hili gumu lipo tabaka jengine la
ardhi ambalo lina asili ya kimiminika, kama ambavyo picha
inaonesha hapo chini;

Hvyo basi, kila mlima ambao umesimama juu ya mgongo wa


ardhi unayo mashina yake ambayo yanakisiwa kuwa ni asilimia
kumi na tano ya urefu wa mlima husika, ambayo mashina hayo
yapo katika lile tabaka la pili ambalo lina asili ya kimiminika.
Kutokana na matokeo ya tafiti hiyo, Professor Tom Garrison
alihitimisha kwa kusema kuwa; kutokana na asili ya ardhi na
uwepo wa milima yenye mashina katika tabaka la ardhi lenye

78
maji maji basi upo ewezekano kuwa milima yote huelea kama
zinavyoelea meli baharini.

Baada ya matokeo ya tafiti hii kutoka mwaka 2014, taasisi


kubwa ya kitafiti ya mambo ya asili (Discovery Science) mwaka
2017 ilifanya utafiti kuangalia matokeo ya utafiti wa Tom na
kugundua kuwa kadiri mlima unavyopungua barafu yake kwa
sababu yoyote ile basi urefu wa mlima huo utaongozekana
kutokana na kupungua kwa uzito wa mlima, na ikitokea barafu
kuongezeka (haidhuru hakuna ushahidi wa kisayansi juu ya
kuongezeka kwa barafu) basi na mlima utapungua urefu na
kudidimia chini kutokana na kuongezeka kwa uzito.

Maana ya hitimisho hili ni kuwa, milima yenye barafu huwa na


uzito mkubwa kulinganisha na milima isiyo na barafu. Hivyo
basi, inapotokea barafu kuyeyuka juu ya mlima, huufanya mlima
huo kupungua uzito wake.

79
80
Tafiti hii ikaja kupewa nguvu zaidi na ile kanuni ya Akimidi
maarufu ambayo inaelezea vyema namna kitu kinavyoweza
kuelea na kuzama ndani ya chombo chenye kimiminika huku
ujazo ukipima uzito wa kitu.

Wakati wanafanya tafiti hiyo, taasisi ya Discovery Science


kupitia mtafiti wao aliyeitwa Mc Manchini alingua kuwa Mlima
Denali uliopo Alaska unakuwa kiurefu kwa wastani wa 0.08
mpaka 0.11 sawa na milimita 2 hadi 3 kwa mwaka. Wakaeleza
kuwa sababu ya mlima huo kuongezeka urefu ni kutokana na
matokeo ya mabadiliko ya tabia nchi ambayo yanasababisha
kiwango cha joto kuongezeka na hivyo theluji (barafu) iliopo juu
ya mlipa huu kuyeyuka kwa kasi sana. Na kadiri barafu hiyo
inavyo yeyuka ndivyo mlima unavyopungua uzito kisha unaelea
kuenda juu. Haya ni baadhi ya makubwa ambayo yamefanyika
81
katika karne za ishirini na ishirini na moja, unaweza kujiuliza
kwanini tumeifafanua sayansi hii. Lengo letu ni kuthibitisha
kuwa haya yote yalishaelezwa na Allah (Subhanahu) kupitia
Qur‘an ndani ya karne ya saba.

Karne ambayo kutokana na uhaba wa sayansi katika kipindi


hicho hawakujua na hawakuweza kutumia mbinu za kisasa za
kisayansi kufanya uchambuzi wa kila kitu ambacho kimeelezwa
ndani ya Qur‘an. Allah (Subhanahu) anasema ndani ya Qur‘an;

―Na katika ishara zake ni vyombo vinavyo kwenda na kurejea


baharini kama vile vilima.‖ (42:32)
Kadhalika, amesema Allah (Subhanahu) katika Sura nyengine
kuwa;

―Na ni vyake Yeye hivi viendavyo baharini vilivyo undwa kama


vilima‖ (55:24)

Ibn Kathir (Rehma za Allah ziwe juu yake) anafafanua kuwa;


Allah (Subhanahu) anaonenyesha miongoni mwa dalili na ishara
za ukuu wake kwa kuvifananisha vyombo vya baharini vya
usafiri na usafirishaji vinavyo elea ni kama vile inavyo elea
milima. Qur‘an siku zote ipo mbele ya wakati kwani
iliwachukuwa wana sayansi miaka takribani 1400 kujuwa kuwa
milima inaelea. Kadhalika wapo miongoni mwa wanasayansi
ambao hawakuamini kuwa milima inayo mashina ambayo
imekita chini ya ardhi. Allah (Subhanahu) anasema ndani ya
Qur‘an;

―Kwani hatukuifanya ardhi kama tandiko? Na milima kama


vigingi?‖ (78:6-7)
Tunafahamu maana ya vigingi, kwa faida zaidi vigingi ni viguzo
au mti uliokitwa chini ya ardhi madhubuti kabisa kwa ajili ya
kufungia kamba ya mnyama ili asikimbie na namna hiyo ndivyo
ambavyo milima imeumbwa na kutengenezewa mizizi yake

82
imara chini ya ardhi kwa kazi maalumu ambayo tulishaifafanuwa
hapo awali.
﴾٥﴿‫ن‬
ْ َ‫ن يَ ْعل‬
ْ َ‫ًسبىَ َهب ل‬
َ ‫ٱإل‬
ِ ‫ن‬َ َّ‫َعل‬
‖Kamfundisha mwanadamu aliyokuwa hayajui‖ (96:05)

Qur‟an na Gunduzi za vyanzo vya Moto


Qur‘an inatuthibitishia kuwa mambo mengi ya kiugunduzi
yamekuwa yakiikiri kwa vitendo, huku wavumbuzi wakianza kwa
kuitilia shaka na mwisho baada ya majaribio ya muda mrefu
wakija na hitimisho la kuikubali na kuwapa ari ya kuisoma zaidi.
Allah (Subhanahu) alifafanua namna ambavyo njia mbali mbali
za mwanadamu anazoweza kutumia katika kupata nishati ya
moto na umeme katika Surat Yasin;
―Yeye ndie Allah ambae amekujaalieni kupata moto kutokana na
mti wa kijani nanyi mkawa kwa huo mnawasha.‖ (36:80)

Imam Al-Kurtuby (Rehma za Allah ziwe juu yake) amesema


kuwa kauli ya Allah kuwa; “Yeye ndiye amekujaalieni
kupata moto kutokana na mti wa kijani” amesema maana
yake ni moto ambao unapatikana kutokana na vile vijiti viwili;
kile ambacho kinalala chini na kile ambacho kinasimama na
kupekechwa kisha kutokana na msuguano ukatokea moto.

Imam Ibn Kathir (Rehma za Allah ziwe juu yake) katika tafsiri
yake alisema kuwa kauli ya Allah; “Yeye ndiye amekujaalieni
kupata moto kutokana na mti wa kijani” maana yake kuwa
ni Ikiwa mtu anataka kuwasha moto, lakini hana kitu cha
kuwashia, basi huchukua matawi mawili ya kijani kibichi kutoka
kwa miti na akasugua mti mmoja dhidi ya mwengine, na moto
hutolewa kutokana na miti hiyo.

Katika vitabu vya historia, vinaeleza kuwa miongoni mwa mbinu


ambazo zilitumika katika kipindi cha nyuma, kipindi kabla
sayansi ya nishati kuzalisha matokeo ya viberiti (vya miti), gesi,
umeme wa moto. Qur‘an ilishawafundisha viumbe namna ya

83
kupata nishati hiyo. Huku ikiwa ni miongoni mwa dalili za ukuu
wa Muumba wao.

Taarifu za kihistoria zinatueleza kuwa miongoni mwa njia


maarufu za kuwasha moto, ukiacha ile ya kusugua mawe mawili
ambayo sayansi yake imetoka kwenye miti, mbinu ya kutumia
miti ndio mbinu maarafu kutumika ambayo huitwa ―Ulindi na
Ulimbombo‖

Kwa mujibu wa duru za historia, zinasema kuwa katika karne ya


ishirini na ishirini na moja bado wapo miongoni mwa wanadamu
ambao wanaendelea kuienzi njia hii. Kwa mujibu wa jarida la
“Fahariyangu” la mwaka 2013 walisema kuwa‖ Ulindi na
Ulimbombo, ni njia ya asili ya kuwasha moto ambayo hadi sasa
inaendelea kutumika na jamii ya Wahdzabe.

84
Allah (Subhanahu) kutokana na hilo akasema;
―Je! Mnauona moto mnao washa? Ni nyinyi mlio uumba mti
wake au Sisi ndio Waumbaji? (56:71-72)
Hiyo ndiyo Qur‘an, hicho ndicho kitabu kitukufu kilicho shushwa
karne ya saba kikiendelea kuwa ni mfano na ufunuo wa elimu
kwa ulimwengu. Je! Bado tunazo hoja za kusema na
kuthibitishwa kuwa Qur‘an imepitwa na wakati?

Qur‟an na Sayansi Anatomia ya Viumbe


Allah (Subhanahu) anasema ndani ya Surat Fussilat kuwa;
―Tutawaonyesha Ishara zetu katika upeo wa mbali na katika
nafsi zao wenyewe mpaka iwabainikie kwamba haya ni kweli.‖
(41:53)

85
Wafasiri wa Qur‘an wameiangalia kauli hii ya Allah (Subhanahu)
na kuifafanua kwa kina sana. Wakasema kuwa kila nukta katika
kauli hii ina umuhimu mkubwa wa kila kiumbe kiutafakari mara
nyingi juu ya maisha yake kwa ujumla.

Ibn Kathir (Rehma za Allah ziwe juu yake) amesema kuwa kauli
ya Allah kwamba; “katika upeo wa mbali na katika nafsi
zao wenyewe” maana yake ni Allah (Subhanahu)
anamzungumzia mwanadamu na muundo wake wa mwili. Kama
inavyofafanuliwa katika sayansi ya anatomia, ambayo
huonyesha hekima ya Muumba na mielekeo tofauti na asili iliyo
kinyume ambayo watu wanayo, nzuri na mbaya. Na hukumu za
kimungu ambazo mwanadamu ametiishwa nazo, hana uwezo
wa kuzibadili na ambazo hana uwezo nazo.

Tunaona hapa Qur‘an inazungumzia jambo kubwa sana la


sayansi ya anatomia ya mwanadamu. Kwa mujibu wa
wanasayansi wa fani hiyo wanasema kuwa anatomia maana
yake ni fani katika sayansi ya kibiolojia inayohusika na utambuzi
na maelezo ya miundo ya mwili ya viumbe hai. Kwa mujibu wa
sayansi ya anatomia ya mwanadamu, wanasayansi wanasema
kuwa ndani ya mwili wa mwanadamu zipo seli nyingi ambazo
zimekuwa na kazi tofauti.

Miongoni mwa seli hizo, ipo seli iitwayo „melanocytes‟ ambayo


kazi yake kubwa ni kuzalisha seli nyengine muhimu iitwayo
„Melanin‘ ambayo ni seli (dutu) muhimu ndani ya mwili wa
mwanadamu, seli hiyo hutumika kuizifanya nywele kuwa na
rangi ya asili na yakuvutia (Nyeusi), macho na ngozi. Kadiri
mwili unavyozalisha melanini zaidi, ndivyo macho yako, nywele
na ngozi zinavyo kuwa na rangi ya asili ya weusi. Hivyo hivyo,
kadiri mwili wa mwanadamu unavyopungua kuzalisha melanin
ndivyo ngozi, nywele na macho yanavyo badilika rangi kutoka
kuwa na rangi nyeusi kwenda kahawiya au nyeupe.

Ingawaje kwa mujibu wa wanasayansi wa anatomia ya viumbe


hai wanasema kuwa; zipo sababu nyingi ambazo husababisha

86
mwili wa kiumbe hai (haswa mwanadamu) kupungua uwezo wa
kuzalisha melanini. Wakasema kuwa miongoni mwa sababu hizo
ni umri kuwa mrefu, hivyo seli hizo hupungua uwezo wa
kuzalishwa na kufanya viungo hivyo; macho, nywele na ngozi
kupoteza ile rangi yake ya asili.
Kwa mfano kadiri melanini inavyopungua kuzalishwa ndani ya
mwii wa mwanadamu ndivyo nywele zake zinavyofanya weupe
(mvi).
Kwa mujibu wa Makala ya mwana anatomia Bing Zhang na
wenzake ya mwaka 2020, wakiwa wanafanya tafiti ya sababu
nyengine ambazo husababisha uhaba wa uzalishwaji wa melanin
ndani ya mwili wa mwanadamu wamesema kuwa; ―Tunapenda
kukiri kuwa, kutokana na tafiti yetu tumegundua kwamba
msongo mkubwa wa mawazo na hofu ya juu inaweza kupelekea
kupungua kwa kiasi kikubwa sana cha uzalishaji wa melanin
ndani ya mwili wa mwanadamu na hivyo kusababisha nywele
kuwa nyeupe.‖
Aidha, kwa mujibu wa jarida la NIH News in Health lililo
andika juu ya sababu za nywele kuwa nyeupe (kutoa mvi)
amesema Dr. Ya-Chieh Hsu wa Chuo Kikuu cha Harvard
kuwa; ―Tafiti inaonesha kuwa msongo wa mawazo na hofu
husababisha kupungua kwa uzalishwaji wa seli za melanin na
mwisho wake kupelekea nywele kuwa na mvi.‖
Hivyo hivyo, Dr. Chieh akaongezea kuwa; hakutegemea kuwa
msongo wa mawazo na hofu unaweza kuwa na athari mbaya
zaidi kwa mwanadamu, kama hii ya kubadilisha muonekano wa
nywele zake ambao utakuwa ni wakudumu. Katika jarida hilo pia
wakaambatanisha picha hii kufafanua zaidi;

87
Kauli ya Allah (SUbhanahu) aliposema kuwa; “Tutawaonyesha
Ishara zetu katika upeo wa mbali na katika nafsi zao
wenyewe” hizi ndizo miongoni mwa ishara zake katika nafsi
zetu wenyewe na ndizo ambazo zinatupaswa kuifahamu Qur‘an
na zinatupaswa kuikiri kwa kauli na vitendo.

Sayansi hii ya anatomia juu ya melanin ambayo tumeifafanua


hapo juu, iliwachukuwa wanasayansi karne na dahari kuitambua
na kujuwa kuwa msongo wa mawazo na hofu iliyo kuu inaweza
kumfanya mtu afanye mvi.

Mbali na kuwa Allah (Subhanahu) amesema kuwa anazionesha


ishara zake kupitia vitu mbali mbali, Sayansi ya anatomia ya
karne ya ishirini na ishirini na moja imekuja kuikiri kauli ya Allah
(Subhanahu) aliposema ndani ya Surat Al-Muzammil;
―Basi nyinyi mkikufuru, mtawezaje kujikinga na Siku ambayo
itawafanya watoto wadogo waote mvi?” (73:17)

Ibn Kathir (Rehma za Allah ziwe juu yake) amesema katika


tafsiri yake akifafanua kauli ya Allah (Subhanahu) kuwa; “Siku
ambayo itawafanya watoto wadogo waote mvi” amesema
kuwa Hii itatokea kwa sababu ya ukali wa vitisho vyake,
matetemeko yake ya ardhi na mkanganyiko wake wa kutisha.

88
Ufafanuzi huu wa kauli ya Allah (Subhanahu) unathibitisha
matokeo ya tafiti mbali mbali za wanasayansi wa karne ya
ishirini na ishirini na moja kuwa inapotokea mshtuko, hofu, ama
hangaiko la moyo, basi hata mtoto mchanga anaweza kuota
mvi. Haidhuru, jambo hili hawakuweza kulikubali wanasayansi
hao kabla ya tafiti na majaribio yao kadhaa ya kimazingira na
yale ya kimaabara.

Tukirejea kauli ya Dr. Maurice katika kitabu chake cha ‗The


Bible, The Qur‘an and Science‘ aliyosema kuwa Qur‘an ndio
kitabu pekee ambacho aliweza kukuta na kusoma mambo
kadhaa ya kiasili ambayo hakuweza kuyapatia maana na
ufumbuzi wake isipokuwa kwa kutumia Sayansi na Teknolojia ya
sasa. Ni sawa pia wale wanasayansi ambao kwa zaidi ya karne
kumi na nne baada ya kushushwa kwa Qur‘an hawakuweza
kukubali na kuamini kuwa mtoto mdogo anaweza kuota mvi.
Wanasayansi kupitia tafiti na majribio mbali mbali wamekuja
kuikiri kauli hii ya Allah (Subhanahu) na kuthibitisha kuwa
Qur‘an imekuwa ikiwapa changamoto mbali mbali za kitafiti,
kwani, ukiisoma Qur‘an kupitia aya ambazo Allah (Subhanahu)
ameelezea uzito na vitisho ambavyo vitatokea katika siku ya
Kiyama basi ni dhahiri kuwa hakuna nafsi ambayo haitopata
hofu kubwa na msongo wa mawazo ambao utatikisa na
kupepeta nyoyo za kila kiumbe.

Hadith sahihi za Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) katika


vitabu mashughuri vya Hadithi (Bukhary na Muslimu)
vinathibitsha kuwa Mtume wa Allah alisema na kukiri kuwa uzito
na vitisho vya siku ya kiyama ambavyo vimetajwa ndani baadhi
ya Surah vimemtoa mvi.

Kama ilivyokuja katika Hadith kuwa; Amepokea Imam Tirmidhi


(Radhi za Allah ziwe juu yake) kutoka kwa Ikrima; kutoka kwa
Ibn Abbas (Radhi za Allah ziwe juu yao wote) amesema;
Amesema Abubakri (Radhi za Allah ziwe juu yake) kumwambia
Mtume; ―Ewe Mtume wa Allah, umekuwa na mvi.‖ Akasema
Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake); ―Wamenipa mvi Surat

89
Hud, Surat Al-Waqi‘ah na Surat Al-Mursalat, na Surat Nabai na
Surat Quwirrat.‖

Baadhi ya wanazuoni wa Hadithi wanasema kuwa hizi ni


miongoni mwa sura ambazo zimebeba ujumbe mzito sana
kuhusu ya masuala mbali mbali ikiwamo matokeo makubwa
vitisho na vitimbi vya siku ya kiyama. Hadithi pia inatuthibitihia
kuwa kile ambacho kimetajwa na Qur‘an juu ya watoto wadogo
kutoa mvi kinawezekana kama ambavyo wanasayansi wamekuja
kuikiri na kuithibitisha sayansi iliyopo nyuma ya jambo hilo.
Kwa uchache tuangalie namna ambavyo Allah (Subhanahu)
alivyofafanua matukio hayo ya kutisha kupitia sura mbali mbali
ndani ya Qur‘an, ili nasi tuweze kufanya ulinganishi wa
kimazingira juu ya kile kilichosemwa na Qur‘an na kile ambacho
wanasayansi wamekigundua na kuikiri sayansi ya Qur‘an
iliyoshushwa katika karne ya saba;
Surat Al- Waqi‟ah (56);
―Itakapo tikiswa ardhi kwa mtikisiko. Na milima itapo
sagwasagwa. Iwe kama mavumbi yanayo peperuka.‖ (56:4-6)

Surat At-Takwir (81);


―Jua litakapo kunjwa. Na nyota zikazimwa. Na milima
ikandolewa. Na ngamia wenye mimba pevu watakapo achwa
wasishughulikiwe. Na wanyama wa mwituni wakakusanywa. Na
bahari zikawaka moto.‖ (81:1-6)

Hakika kwa uzito na hofu ya kiasi hicho ni lazima hata mtoto wa


siku moja, mwili wake lazima usite kuzalisha melanini na ile
rangi nzuri ya nywele alizo umbwa nazo zibadilike rangi na kuwa
nyeupe mithiti ya mzee wa miaka mingi. Hii ndio Qur‘an ambayo
ilikuja kufungua enzi mpya ya sayansi na teknolojia.

―Basi nyinyi mkikufuru, mtawezaje kujikinga na Siku ambayo


itawafanya watoto wadogo waote mvi?” (73:17)

90
Qur‟an na Sayansi ya Bahari (Oceanography)
Bahari na Mwangaza wake:
Allah (Subhanahu) amemsimulia Mtume wake kupitia Qur‘an juu
ya uovu wa makafiri, huku akimpigia mifano kadhaa wa kadhaa
ya kufananisha ukafiri wao huo. Aidha, wakati ujumbe huo
ukiwasilishwa kwa njia hiyo ya mifano, Allah (Subhanahu) ndani
ya ujumbe huo akafunganisha ishara na alama muhimu sana za
kisayansi ambazo hadi kufikia karne ya ishirini ndio undani wa
masuala hayo yamekuja kujulikana. Allah (Subhanahu)
amesema ndani ya Surat An-Nur;

―Na walio kufuru vitendo vyao ni kama sarabi (mazigazi)


uwandani. Mwenye kiu kuyadhania ni maji. Hata akiyaendea
hupati chochote. (24:39)

Ibn Kathir (Rehma za Allah ziwe juu yake) ameifafanua kauli hii
ya Allah (Subhanahu) na kusema kuwa; ―Makafiri
wanaowalingania wengine ukafiri wao, wakidhani kuwa wana
vitendo na imani nzuri, na hali sivyo hivyo. Mfano wao ni kama
sarabi inayoonekana katika tambarare ya jangwa, ikitazamwa
kwa mbali kana kwamba ni bahari ya kina kirefu, au sarabi
inayoonekana kwenye eneo kubwa la ardhi lililo tambarare
ambalo ndani yake huonekana kama mfano wa maji.‖ Katika
ufafanuzi wa kauli ya Allah (Subhanahu), kuna nukta ya msingi
sana ambayo tunakusudia kuifafanua kwa uchache.

Allah (Subhanahu) ndani ya aya hii ameelezea juu ya sarabi au


kwa lugha nyengine mazigazi yanayoonekana mara nyingi
kwenye jangwa, lami au bahari.

Wanasayansi wa fani la fizikia (Physics) wanaifafanua sarabi


kwa mujibu wa kanuni na mbinu zao ambazo zimezalishwa na
majaribio mbali mbali ya kitaalamu. Wanasema kuwa sabari ni
mwonekano wa udanganyifu wa kitu cha mbali au vitu
vinavyosababishwa na kupinda kwa miale ya mwangaza katika
tabaka za hewa lenye msongamano mzito.

91
Kupitia kanuni za kifizikia wakafafanua zaidi na kusema kuwa
katika hali fulani, kama vile sehemu ya lami au hewa ya
jangwani inayochomwa na jua kali, hewa hiyo hupoa kwa kasi
kwa mwinuko na hivyo huongeza msongamano na nguvu ya
kuakisi. Mwangaza wa jua unaoakisiwa kuelekea chini kutoka
sehemu ya juu ya kitu—kwa mfano, sehemu ya juu ya ngamia
jangwani—itaelekezwa kupitia hewa baridi kwa njia ya kawaida.

Wakati mwingine, ukiwa juu ya maji, safu ya hewa baridi na


nzito huweka safu ya joto. Na kutoa kitu mfano wa kile kinacho
onekana, ambacho miale ya mwangaza itafikia jicho ambalo
hapo awali lilielekezwa kukitazama kitu hicho. Kwa hivyo, kitu
kisichoonekana, kama mashua chini ya upeo wa macho.

Hakika hii ndio Qur‘an, ambayo inaendelea kuwashangaza na


kuwafunza wengi mambo makubwa ambayo ili kuyafahamu na
kuyaelezea kwa ufasaha, huhitaji elimu na nidhamu za sayansi
ya kisasa.

92
Dr. Philips msomi na mbobezi wa masuala ya mazingira ya
bahari alishangaa na kustaajabu kuona Qur‘an iliyoshushwa
karne ya saba imezungumzia kwa kina juu ya sayansi ya bahari.
Sayansi ambayo iliwaharimu watafiti na wasomi wa sayansi
takribani miaka elfu moja kuifahamu. Baada ya matumizi
makubwa ya vifaa vya hali ya juu huku mamilioni ya fedha
yakitumika katika kuijua na kuitafiti bahari na sayansi yake,
ndipo wakaifahamu kwa uchache.

Kwa upande mwengine wakishangazwa na namna ambavyo


Mtume Muhammad (Rehma na Amani ziwe juu yake)
aliwafundisha maswahaba zake kwa uwazi kupitia Qur‘an
tukufu. Wanasayansi wa mambo ya bahari wanakiri kuwa kwa
muda mrefu hawakuwa wakijua kuwa katika maumbile ya
bahari, yapo mawimbi ya juu na yapo mawimbi yaliyo ndani ya
bahari (mkondo). Kwa mujibu kwa mtandao wa National
Geographic waliandika kuwa takribani miaka mia moja iliyopita
hadi kufikia mwaka 2010 wanasayansi wa bahari wamefanikiwa
kuzamia chini ya bahari na kufikia kima cha mwisho ikiwa ni futi
thelathini na tano elfu (35000 futi) tu. Kama ambavyo picha
inaonesha hapo chini.

93
Kwa mujibu wa mtandao huo pia wanasema kuwa; ―Matumizi na
utambuzi wa bahari umeongezeka katika karne ya ishirini na
ishirini na moja, na teknolojia ya kisasa ya kompyuta imesidia
kuwawezesha wanasayansi kupima mali inayopatikana ndani ya
bahari kwa kiwango cha kimataifa.‖ Takwimu zinatuonyesha
kuwa asilimia sabini (70%) ya dunia ni bahari, na wanasema
kuwa bahari ndio sehemu ambayo imehifadhi viumbe hai vingi
zaidi ya ardhi.

94
Bahari ni maji, na maji ni uhai. Allah (Subhanahu) amesema
ndani ya Qur‘an;
―Na tukajaalia kutokana na maji kila kilicho hai.‖ (21:30)

Wanasayansi wakati wanaisoma aya hii iliyoshushwa karne ya


saba, hawakuweza kuikubali kwa kuwa katika kipindi hicho
hawakuwa na maendeleo yoyote ya sayansi na teknolojia
ambayo ingeweza kuwasaidia kulifahamu jambo hili. Baada ya
miaka na karne kadhaa kupita huku tafiti mbali mbali zikifanyika,
walikuja kuikiri Qur‘an kwa kauli zao na maandishi yenye
kudumu. Kwa mujibu Tom Garrison (2016) alisema kuwa;
Maisha, angalau kama tunavyoyajua, hayangeweza kufikirika
wala kuwezekana bila uwepo wa maji. Maji yanaweza kuhifadhi
joto, kutunza halijoto ya wastani, kuyeyusha kemikali nyingi, na
kusimamisha virutubisho, taka n.k.

Kadhalika, Allah (Subhanahu) kupitia Qur‘an ambayo ilishushwa


karne ya saba, kwa Mtume wake ambae hakujua kusoma wa
kuandika kabla ya hapo, amefafanua kwa kina juu ya matabaka
ya bahari pamoja na tabia, asili na uhusiano wa bahari na
mwangaza. Ikafafanua mambo ambayo wanasayansi wa karne
ya ishirini na ishirini na moja yaliwashangaza na wengi miongoni
mwao waliamua kufuata dini ya Uislamu.
Allah (Subhanahu) anasema ndani ya Surat An-Nur;
―Au ni kama giza katika bahari kuu, iliyofunikwa na mawimbi juu
ya mawimbi, na juu yake yapo mawingu. Giza juu ya giza.
Akiutoa mtu mkono wake anakaribia asiuone. (24:40)

Kwa mujibu wa wafasiri wa Qur‘an wamefafanua kauli hizi za


Allah (Subhanahu) na kusema kuwa huu ni mfano wa giza
ambalo limo ndani ya mioyo ya makarifi. Kutokana na uzito wa
upotevu wao ukafananishwa na giza ambalo lipo bahari kuu.
Aidha, kupitia aya hii, Allah (Subhanahu) ametumia mfano wa
makafiri kuelezea kima cha upotevu wao huku akitoa ishara
kubwa za kisayansi ambazo watafiti na wasomi nguli wa Sayansi
ya Bahari wameyaeleza na kuyagundua.

95
Kwa mujibu wa Tom Garrison katika kitabu chake cha Sayansi
ya Bahari amesema kuwa; Katika sehemu kubwa ya bahari,
eneo la uso (au safu iliyochanganyika) yenye joto kiasi, maji
yenye msongamano wa chini hufunika safu inayoitwa
pycnocline. Msongamano unaongezeka haraka na kina katika
pycnocline. Chini ya pycnocline kuna kina kirefu eneo la maji
baridi, mazito - karibu 80% ya jumla ya kiasi cha bahari.

Kwa lugha nyepesi, bwana Garrison anasema kuwa bahari


imegawika katika matabaka makubwa matatu ambayo
yanatofautishwa na kina cha maji pamoja na msongamano wa
maji. Amesema kuwa ipo sehemu ya juu ambayo ni wastani wa
asilimia mbili ya habari yote. Kisha kuna sehemu ya pili ambayo
inakadiriwa kuchukua wastani wa asilimia kumi na nane ya
bahari yote ambayo inaitwa pycnocline kisha sehemu ya chini
kabisa ambayo inaitwa tabaka la chini ambalo linakadiriwa
kukusanya asilimia thamanini ya bahari yote.

Hivyo basi, Allah (Subhanahu) aliposema kuwa; “Au ni kama


giza katika bahari kuu, iliyofunikwa na mawimbi juu ya
mawimbi, na juu yake yapo mawingu. Giza juu ya giza.”
Dhahiri kuwa alikuwa akiifahamisha dunia juu ya elimu ya bahari
na matabaka yake. Alikuwa anawapa mwangaza wanasayansi
wa bahari kuisoma vizuri bahari na kuijua. Kwani kwa mujibu wa
wanasayansi hao wanakiri kuwa kadiri unavyozama kwenda

96
chini kwenye tabaka lengine ndivyo ambavyo nuru ya
mwangaza inavyopotea.

Kadhalika, katika kuthibitisha kauli ya Allah (Subhanahu) ndani


ya sayansi ya karne ya ishirini na ishirini na moja wanasema
kuwa mwangaza wa jua haupenyi kirahisi katika bahari.
Ingawaje kwa wastani wa tabaka la kwanza ambalo lina wastani
wa kina cha futi 2000 ndio tabaka pekee ambalo huruhusu
mwangaza wa jua kuingia kwa asilimia chache sana.

Kwa upande mwengine, tabaka la pili na la tatu ni matabaka


ambayo hujitengenezea mwangaza yenyewe kutoka kwenye
viumbe hai na mimea ambayo inapatikana humo. Sayansi ya
bahari imekuja kuikiri Qur‘an juu ya kauli ya Allah (Subhanahu)
aliposema kuwa bahari ni giza juu ya giza.

Baadhi ya watafiti wa masuala ya bahari wameyagawa


matabaka ya bahari kwa mujibu wa namna ambavyo mwangaza
wa jua unavyoweza kupenya ndani yake. Wakasema kuwa
tabaka la kwanza linaitwa tabaka la mwangaza wa jua (sunlight
zone) ambalo limeitwa kwa usahihi kwa nafasi yake katika
usawa wa uso wa bahari, eneo hili la mwanga wa jua, pia
huitwa eneo la uso au eneo la epipelagic, huenea kuelekea chini
mita 2000 au takribani asilimia mbili ya kina cha wastani cha
bahari. Wakati wa mchana, humulikwa kabisa na jua, kwa hiyo
huitwa eneo la mwanga wa jua. Pia inachukuliwa kuwa safu
yenye joto zaidi.

Tabaka la pili ni tabaka la mwangaza hafifu au mesopelagic


zone huanzia mita 2000 na kuenea chini hadi mita 10,000 hivyo
kufanya takriban asilimia 18% ya kina cha jumla cha bahari.
Kwa ujumla ni eneo hafifu sana, lakini hupokea mwanga wa jua
wakati wa mchana ambao unatosha kwa usanisinuru (kijani
kibichi) kutokea. Bahari ya kina kirefu - safu ya tatu na ya
mwisho - inaenea kutoka hatua ya mita 10,000 hadi sakafu ya
bahari, bila kujali ni kina gani. Kwa uchache, hufanya 80% ya
kina cha bahari. Ni eneo lenye baridi kali ambalo halipati

97
mwangaza wa asili kabisa. Viumbe wanaoishi katika ukanda huu
ni bioluminescent; yaani wanazalisha na kutoa nuru yao
wenyewe.

Hivi ndivyo sayansi ilivyoikiri Qur‘an ambayo ilishushwa karne ya


saba. Matabaka haya ndiyo yale ambayo Allah (Subhanahu)
amesema kuwa;
“Au ni kama giza katika bahari kuu, iliyofunikwa na
mawimbi juu ya mawimbi, na juu yake yapo mawingu.”
(24:40) na zaidi ya hapo katika lile tabaka la tatu ambalo
hakuna mwangaza wa jua ambao unaingia bali viumbe walioko
huko hujitengezea wenyewe mwangaza ili waishi, imekuja
kuithibitisha kauli ya Allah (Subhanahu) kuwa kutokana na giza
lililopo ndani yake;
―Akiutoa mtu mkono wake anakaribia asiuone.” (24:40)

Kutokana na tabia na sifa zilizopo katika tabaka la chini la


bahari, ni dhahiri pia kuwa endapo mtu akiutoa mkono wake
hawezi kuona. Ukiingatia maelezo ya Qur‘an ambayo
yameelezea giza la bahari katika karne ya saba, na kwa
kufananisha na matokeo ya kisayansi ya bahari ambayo
yamekukuja kubainisha kuwa bahari imekuwa na sifa hizo.
Haitoshi kuwa ni mawaidha kwetu kutafakari juu ya ukuu wa
Allah (Subhanahu) katika umbaaji, na uendeshaji wa mambo
yote wanayo yajua na wasiyo yajua viumbe. Hakika hii ni Qur‘an
ya ajabu.

Makutano ya Bahari Mbili


Takribani miaka elfu moja mia nne imepita tangu Allah
(Subhanahu) ameishusha Qur‘an tukufu, ambayo imekuja
kuzungumzia kwa kina juu ya makutano ya bahari mbili ambazo
hazichanganyiki. Qur‘an ilieleza kwa kina juu ya suala hili, kiasi
ambacho iliwaacha na changamoto kubwa wengi miongoni mwa
wasomi na watafiti wa masuala ya bahari. Allah (Subhanahu)
amesema ndani ya Qur‘an;
―Anaziendesha bahari mbili zikutane; Baina yao kipo kizuizi
zisiingiliane.‖ (55:19-20)
98
Wanazuoni wa tafsiri ya Qur‘an wameifafanua aya hii kama
ambavyo yenyewe inajieleza na hakuna tofauti yoyote ya
kimaana. Kwa upande mwengine, wanasayansi wa masuala ya
bahari wamesema kuwa mpaka uliopo kati ya bahari ya Pasifiki
na Atlatiki ni kama msatari tenganishi wa dunia mbili. Na
inaonekana kama vile bahari hizo mbili hukutana na
kutenganishwa na ukuta usioonekana ambao unazizuia bahari
hizo sizichanganyike.

Tunaweza kujiuliza kwa nini hazichanganyiki? Wanasayansi wa


mambo ya habari na watafiti wanasema kuwa bahari hizi mbili
zinamsongamano (kasi ya mzunguko wa maji) tofauti na namna
tofauti za kikemia baina yao. Wakaongeza kuwa mpaka ambao
umezitofautisha bahari hizi mbili kitaalamu unaitwa (Ocean
Cline) ambao ni mpaka unaozitofautisha bahari kutokana na
ukomo na mteremko wa bahari hizo.
Haya yamezungumzwa na mgunduzi maarufu aliyeitwa Jacques
Cousteau ambae ameongeza kwa kusema kuwa maji bahari
yenye utofauti wa kiwango cha chumvi huonekana kana

99
kwamba yametenganishwa na mpaka usioonekana huku kila
moja ikiwa na aina yake ya viumbe hai na matumbawe. Baadhi
ya wanasayansi wa bahari wanasema kuwa ukuta huo usio
onekana baina ya bahari mbili hutokea pale tu bahari hizo
zinavyotofautiana katika wingi wa chumvi mara tano au zaidi.
Ufafanuzi huu wa Mr. Jacques umekuja kuikiri Qur‘an pale Allah
(Subhanahu) aliposema;
―Nae ndie alie zipeleka bahari mbili, hii tamu mno, na hii ya
chumvi chungu. Na akaweka baina yao kinga na kizuizi
kizuiacho.‖ (25:53)

Wanasayansi wa Fizikia wanasema kuwa kila bahari huwa na


chembe ndogo ndogo za atomia ambazo huungana na kusaidia
katika mzunguko wa bahari hizo. Hivyo basi kwa mujibu wa
dhana hiyo wanasema kuwa miongoni mwa sababu nyengine
ambayo zinazifanya bahari hizi zisichanganyike ni kuwa kila
moja ina aina yake ya chembe za atomia ambazo zikiungana
huzunguka katika mizunguko tofauti, yani chembe za bahari
moja huzunguka kuelekea kulia na chembe za bahari nyengine
huzunguka kuelekea kushoto. hivyo huyafanya maji ya habari
moja isiweze kuchanganyika na bahari nyengine kwa kuwa maji
yake yanazunguka katika muelekeo unaotofautiana.

﴾٥﴿‫ن‬
ْ َ‫ن َي ْعل‬
ْ َ‫ًسبىَ َهب ل‬
َ ‫ٱإل‬
ِ ‫ن‬َ َّ‫َعل‬
‖Kamfundisha mwanadamu aliyokuwa hayajui‖ (96:05)

100
Qur‟an na Sayansi ya Hyndrolojia (Mzunguko wa Maji)
Allah (Subhanahu) amesema ndani ya Qur‘an kuwa;
―Na tukajaalia kutokana na maji kila kitu kuwa hai.‖ (21:30)
Nidhamu na Imani juu ya umuhimu wa maji haiwezi kupingika
katika dunia. Viumbe, mimea pamoja na ardhi huhitaji maji
katika ustawi na maendeleo ya makuzi. Maji yamekuwa ni
kiungo muhimu cha uhai wa viumbe wote duniani, kuanzia
wanadamu, mimea, wanyama na hata baadhi ya shughuli mbali
mbali za kiuchumi na kimaendeleo.
Huenda kutokana na umuhimu wake (maji) ndio sababu kubwa
ambayo iliwafanya watafiti na wasomi kutaka kufahamu zaidi
juu ya asili na mzunguko wa maji. Kutokana na jitihada za
kuyafahamu maji kiundani, wasomi na watafiti wakaja na
nidhamu maalumu ya kielimu ambayo itajikita moja kwa moja
katika kuyafahamu maji kuanzia asili, hadi namna ambavyo
yanavyoleta manufaa kwa viumbe kwa ujumla.
Wasomi hao wakaja na fani ya ‗Hyndrolojia‘ ambayo inasemwa
kuwa ni utafiti wa usambazaji na harakati za maji juu na chini ya
uso wa dunia, pamoja na athari za shughuli za binadamu juu ya
upatikanaji wa maji hayo. Kupitia tafiti hizi za hyndrolojia
mnamo mwaka 1580 mtafiti mmoja aliyeitwa Bernard Palissy
alikuwa mtu wa kwanza kueleza dhana ya siku hizi ya
‗mzunguko wa maji‘. Yeye alielezea jinsi maji yanavyovukiza
(Evaporate) kutoka baharini, kupoa na kutengeneza mawingu.
Mawingu yakapandishwa kisha kugandana na kuanguka kama
mvua.

Maji hayo (kutokana na mvua) hukusanyika kama maziwa na


vijito na kurudi baharini katika mzunguko unaoendelea. Katika
karne ya 7 B.C., Thales wa Mileto aliamini kwamba upepo
ambao hubeba mvuke wa maji ya bahari ndio ambao
huyachukua maji hayo na kuyapandisha juu mawinguni na kisha
kurudi kama mvua.

101
Kabla ya hapo hakuna miongoni mwa wanasayansi ambae alijua
kwa uwazi juu ya vyanzo mbali mbali vya maji yatokayo chini ya
ardhi. Wote waliamini kuwa maji yapatikanayo ndani ya bahari
ndio yanayopenya na kutawanyika nchi kavu (barani), cha
kushangaza zaidi hata wale wasomi na manguli wa sayansi
ambao walipewa vyeo na utukufu wa kuwa ni watu wenye
uwezo mkubwa wa kufikiria, pia waliamini katika dhana hizi.

Ilipofika karne ya kumi na tisa dhana ya Aristotles iligunduliwa,


ambayo ilikuja kueleza kuwa maji yaliyogandishwa juu ya
mapango ya milima yenye baridi ndio hutengeneza maziwa ya
chini ya ardhi na kisha kuzalisha chemchem. Hivyo kutokana na
dhana hii, ndipo sasa wanasayansi wakafahamu kuwa maji
ambayo hutoka chini ya ardhi huzalishwa na kukusanywa kwa
njia ya maporomoko ya maji kutoka milimani.

Kuzingatia na hatua za kielimu ambazo wanasayansi wamepiga


katika kuyafahamu maji na mzunguko wake, huenda ikawa ni
ajabu kubwa kwa wanadamu wengine, lakini kwa kuzingatia
elimu ya Qur‘an hili sio jambo jipya kabisa kwani Allah
(Subhanahu) amesema ndani ya Qur‘an kuhusu jambo hili;
―Je! Huoni kwamba Allah ameteremsha maji kutoka mbinguni.
Kisha akayapitisha kwenye chemchem katika ardhi, kisha kwa
maji hayo akatoa mimea yenye rangi mbali mbali?‖ (39:21)

Kwa mujibu wa Ibn Kathir (Rehma za Allah ziwe juu yake)


amesema maana ya kauli hii ya Allah (Subhanahu) ni kwamba;
Allah (Subhanahu) huteremsha maji kutoka mbinguni, na
yakatua katika ardhi, kisha hutiririsha apendavyo, na hutiririsha
chemchem kubwa na ndogo kadiri inavyohitajika. Sa‘id bin
Jabayr (Rehma za Allah ziwe juu yake) amesema pia maana ya
kauli hii ya Allah (Subhanahu) ni kuwa; Maji yanayoanguka
kutoka angani asili yake iko kwenye theluji, ikimaanisha kuwa
theluji inarundikana milimani, kisha hushuka chini ya milima na
chemchem inatiririka kutoka chini yake.

102
Qur‘an kupitia aya hii ilifundisha fani ya hyndrojia ya maji,
ilifungua mwangaza wa kuonyesha namna vyanzo mbali mbali
vya maji vinavyopatikana. Ikiwa ni fani ya elimu ambayo
imekuwa ikisomwa na kufanyiwa tafiti kwa zaidi ya miaka elfu
moja. Allah (Subhanahu) anaeleza pia ndani ya Qur‘an kuwa;
‖Na hukuteremshieni maji kutoka mbinguni, na kwa hayo
huifufua ardhi baada ya kufa kwake. Hakika katika hayo zipo
ishara kwa watu wanao zingatia.‖ (30:24)

Wafasiri wa Qur‘an wanasema kuwa maana ya kauli ya Allah


(Subhanahu) kuwa “kwa hayo (maji) huifufua ardhi baada
ya kufa kwake” maana yake ni kuipa tena uhai na rutba ardhi
ambayo ilikuwa kame isiyomea chochote. Hivyo kutokana na
mzunguko wa maji yanayoteremka kutoka mbinguni na kuingia
ndani ya ardhi huifufua na kuifanya iwe mpya tena kwa kuwa
amejaalia kutokana na maji kila kitu kuwa hai. Aya hii pia
inaendelea kuthibitisha kuwa Qur‘an ilishafundisha juu ya
nidhamu ya mzunguko wa maji na athari zake kwa viumbe,
mimea na ardhi kwa ujumla.

Aidha, katika kuelezea na kufafanua juu ya mzunguko wa maji


ambao kupatikana kutoka chini ya ardhi kupitia chemchem,
Allah (Subhanahu) amesema ndani ya Qur‘an;
―Na tumeteremsha kutoka mbinguni maji kwa kiasi na
tukayatuliza (kuyapenyeza) katika ardhi. Na hakika Sisi
tunaweza kuyaondoa.‖ (23:18)

Kama ambavyo wanasayansi ya Hyndrojia wanavyosema kuwa


miongoni mwa chanzo kikuu cha maji ni chemchem ambazo
huzalisha maji kutoka chini ya ardhi ambayo huhifadhiwa
kutokana na maji ambayo mvua au maji ambayo yamehifadhiwa
kutoka milimani. Ibn Kathir (Rehma za Allah ziwe juu yake)
amesema kufafanua kauli ya Allah (Subhanahu) “Na
tukayatuliza (kuyapenyeza) katika ardhi” amesema maana
yake ni kuwa; maji yanapoanguka kutoka mawinguni, Allah
(Subhanahu) huyajaalia kuyatuliza katika ardhi, kisha akaifanya

103
ardhi kuyahifadhi ndani yake ili mbegu, mimea na chemchem
ziweze kupatikana.

Dhana ya mzunguko wa maji ambayo inadaiwa kugunduliwa na


Aristotles kuwa maji yanayopatikana kutokana na chemchem ni
yale ambayo aidha yamedondoka kama mvua kutoka katika
mawingu ama ni yale ambayo yaliganda kwenye milima mirefu
yenye baridi kisha yalipoyayuka ndio yakaanguka chini ya mlima
na kisha kuzama ndani ya ardhi. Hakika elimu na ufafanuzi huu
unathibitishwa na Qur‘an kama ambavyo tumeeleza hapo awali
na kwamba matokeo ya gunduzi juu ya mzunguko wa maji
(Hyndrolojia) ulishafanyiwa uchambuzi wake na Mtume (Rehma
na Amani ziwe juu yake) karne ishirini zilizopita.

Katika kutilia uzito juu ya sayansi ya mzunguko wa maji, Qur‘an


kupitia Surat Al-Mulk inafafanua na kuthibitisha kuwa ardhi inao
uwezo wa kuhifadhi maji na yasionekane wala kuwa na manufaa
yoyote kwa viumbe kwa idhini yake Allah (Subhanahu).
Uthibitisho ambao uliwachukua wanasayansi wa fani ya
hyndrolojia miaka zaidi ya elfu moja kufahamu. Allah
(Subhanahu) anasema;
‖Sema: Mwaonaje, yakiwa maji yenu yamedidimia chini, nani
atakueleteeni maji yanayo miminika?‖ (67:30)

Mbali na kuthibitisha kuwa vyanzo vya maji ya chemchem


hutokana kupitia materemsho ya maji kama ambavyo inaelezwa,
bali aya hii Allah (Subhanahu) anadhihirisha ukuu wake katika
kufanya kile atakacho na ni mtihani kwa wale wasio amini juu
kuwa kila elimu juu ya jambo lolote lile liwe la kisayansi ama la
kimazingira basi asili yake ni Qur‘an.

104
Qur‟an na Sayansi ya Alama za Vidole
―Na (taja) aliposema Ibrahim: ―Rabb (Mola) wangu nionyeshe
vipi Unahuisha wafu?‖ (Allah) Akasema: ―Je kwani huamini?‖
Akasema: ―La! (Naamini) lakini moyo wangu utumainike.‖
(Allah) Akasema: ―Basi chukua ndege wanne wazoeshe kwako,
(kisha uwachinje), kisha weka juu ya kila jabali katika hao
(ndege) sehemu yao; kisha waite watakujia mbio (ukiwaona
wanavyoumbika); na jua kwamba hakika Allah ni ‗Aziyzun-
Hakiym (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika - Mwenye hikmah
wa yote)‖. (02:260)

Wakati tunafungua kipengele hiki, tumeona tuanze na aya hii ya


Surat Baqarah kwa kuwa ina ujumbe mzito katika yale ambayo
tunakusudia kuyafafanua. Allah (Subhanahu) kupitia aya hii
anamsimulia Mtume wake (Rehma na Amani ziwe juu yake)
habari ya Nabii Ibrahim (Rehma na Amani ziwe juu yake)
alipoomba kuonyeshwa namna Allah (Subhanahu)
atakavyofufua wafu siku ya kiyama. Hakika hiki ni kisa maarufu
sana ndani ya Qur‘an na kimesimuliwa na kufanyiwa uchambuzi
na Maulamaa wengi wa tafsiri ya Qur‘an.

Allah (Subhanahu) Akamtakabalia Ibrahim ombi lake na Akampa


matumaini kwa kumtaka achukue ndege wanne. Maulamaa wa
Tasfiri wamekhtilafiana kuhusu aina ya ndege waliotajwa kwani
haikuelezwa ni ndege aina gani. Allah (Subhanahu) Akamtaka
Ibrahim awazoeshe kwake kwanza wamzoee, kisha awakate
vipande vipande. Ibrahim akawazoesha, kisha akawachinja na
kuwatoa manyoa na kuwakata vipande vipande, kisha
akavichanganya vipande hivyo pamoja. Kisha akagawa vipande
na kuviweka katika vilima vinne au saba. Ibn 'Abbaas
amesema, "Ibrahim aliweka vichwa vya ndege hao katika
mikono yake".

Kisha akafanya kama Allah alivyomuamrisha kuwaita hao ndege


kwake. Akashuhudia kwa macho yake manyoya, damu na
viungo vya hao ndege vikiruka kujiunga na kiungo cha mwili
wake kila mmoja mpaka kila ndege akarudi kuwa hai na wakawa

105
wanakuja mbele ya Ibrahim wakitembea haraka kuelekea
kwake, lengo ni ili Ibrahim ashuhudie kwa dhahiri kuhuishwa
kwa ndege hao na apate matumaini ya uweza wa Allah
(Subhanahu).

Unaweza kujiuliza Sayansi ya alama za vidole ina mahusiano


gani na kisa cha ndege wa nabii Ibrahim! Mnamo mwaka 1880
mwanasayansi nguli Sir Francis Galton aligundua kuwa alama za
vidole zinaweza kuwa na mchango mkubwa sana katika
utambuzi na ubainifu wa wahalifu. Katika ugunduzi wake alibaini
kuwa alama za vidole ni alama za kipekee za mtu ambazo
huweza kumbainisha na kumtofautisha mtu mmoja na
mwengine.

Kadhalika, katika ugunduzi wake alibaini kuwa alama za mtu


mmoja haziwezi kufanana na mwengine hata kama wakiwa
watoto pacha. Aidha, alisema kuwa hakuna kufanana kwa alama
za vidole za mtu mmoja kuanzia kipindi cha miezi mitatu kabla
ya kuzaliwa hadi kufa kwake. Hivyo kwa mujibu wa ugunduzi
huu, vyombo mbali mbali vya dola nchini Uingereza vilianza
kutumia mbinu ya kukagua alama za vidole katika matukio mbali
mbali ya kihalifu ili kubaini na kumtambua muhalifu.

Kila binadamu ndani ya huu ulimwengu anazo alama zake za


vidole ambazo hazifanani na mwengine. Kwa kutumia kifaa
maalumu, husomwa alama hizo na kuweza kutambua ni nani
haswa mwenye alama hizo. Kutokana na maendeleo makubwa
ya sayansi katika karne ya ishirini na ishirini na moja, na
kutokana na kuaminika kwa uhalisia na usalama wa alama za
vidole, vifaa kadhaa vya kielektroniki vimewezeshwa kuwa na
teknolojia ya alama za vidole katika matumizi.
106
Kwa sasa tunashuhudia simu janja zikifungwa na kufunguliwa
kwa kutumia alama za vidole ambavyo haiwezi kuruhusu
kufunguka bila ya alama za vidole vya muhusika. Kadhalika,
tunashuhudia vifaa mbali mbali vya mahudhurio katika taasisi na
mashirika mbali mbali vikitumika kutambua muda, jina na siku
ya mfanyakazi kufika kazini kwa kutumia alama za vidole.

Allah (Subhanahu) wakati anamuonyesha Nabii Ibrahim namna


ambavyo ndege aliowachinja na kuwatofautisha vipande vyake
wanajikusanya kwa kila mmoja kufata kiungo chake haikuwa ni
jambo la kuburudisha tu. Bali alikusudia kutuonyesha namna

107
ambavyo kila kiumbe katika huu ulimwengu anao utofauti
kutokana na kiumbe mwengine.

Mfano huo, unathibitisha kuwa Allah (Subhanahu) kupitia alama


hizo za kipekee kwa kila kiumbe ndivyo ambavyo atawafufua
walimwengu wote na kila mmoja kukusanywa na viungo vyake
popote pale vilipo bila ya kuchanganyika (kiungo cha mmoja
kupewa mwengine). Wakati wanasayansi hawa wanagundua juu
ya utofauti wa alama za vidole kwa wanadamu katika miaka ya
thamanini, Qur‘an ilishafafanua juu ya matumizi ya alama hizo
za vidole miaka elfu moja mia nne iliyopita.
Allah (Subhanahu) anasema ndani ya Qur‘an;
―Anadhani mtu kuwa Sisi hatutaikusanya mifupa yake? Si hivyo!
Sisi tunaweza hata kuziweka sawa sawa ncha za vidole vyake!
(75:3-4)

Allah (Subhanahu) anawafafanulia wale wasio amini juu ya


ufufuo, huku wakiuliza kuwa atawezaje mtu kutambulika na
kukusanywa na viungo vyake. Allah (Subhanahu) anawajibu kwa
kuwaambia kuwa kama ambavyo aliweza kuweka alama za
vidole kuwa za pekee kwa kila mtu ndivyo ambavyo ataweza
kuwakusanya hata wakiwa vipande vilivyopoteana masafa ya
mbali mno.

Qur‟an na sababu za makatazo ya muziki

Uislamu kupitia mafunzo ya Qur‘an tukufu pamoja na Sunna za


Mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) zimefundisha juu ya
uharamu wa muziki. Ukakataza kuimba, kusikiliza na hata
kushiriki kwa namna moja ama nyengine. Makatazo ya muziki
yakawa ni miongoni mwa makatazo mengi aliyokuja nayo
Mtume Muhammad (Sala na Salamu zimuendee juu yake) huku
ikisisitizwa kuwa masuala na mafunzo yote ambayo ametufunza
tuyachukue na kuyashika kwa meno ya magego, huku
tukitakiwa kuyawacha makatazo na makaripitio yote
yaliyokatazwa katika mafunzo yake.

108
Uislamu unatufunza na kututhibitishia kuwa kila jambo ambalo
limekatazwa kupitia mafunzo yake basi huwa na madhara
makubwa kwa viumbe. Hivyo kupitia misingi hiyo tunahimizwa
kujiweka nayo mbali ili tuweze kuwa na mafanikio ya kidunia
pamoja na mafanikio makubwa mbele ya Allah (Subhanahu).
Kutokana na ukweli kuwa Qur‘an ilishushwa na makatazo ya
muziki katika karne ya saba, walio wengi miongoni mwa
wanadamu hawakujua athari zake. Wengi waliamini na
kuchukua nidhamu ya kuacha kila ambacho kimekatazwa na
Qur‘an huku ikiaminika kuwa na athari japo kuwa kwa wakati
huo upeo wa kutambua athari zake haukuwa wazi sana.

Kwa mujibu wa wanasayansi wa masuala ya akili na saikolojia


ya mwanadamu wanasema kwamba; muziki kama ambavyo
unaaminika kuwa unaweza kuponya (afya ya akili), kuburudisha
na kufundisha, pia muziki unaweza kuleta madhara makubwa
kwa wasilikizaji. Unaweza kujiuliza maana halisi ya falsafa hii!
Kwa mujibu wa Tom Hunt mwanasayansi mbobezi wa falsafa za
akili alisema akiiambia televisheni ya Al-Jazeera kuwa; kila kitu
katika huu ulimwengu kina asili ya mtetemeko (Vibration) katika
masafa maalumu ambayo ndio hutengeneza mahusiano ya
usafirishaji wa mawasiliano ya mwanadamu.

Kwa mujibu wa Tom anaongeza kuwa namna mtu anavyo


ongea, mtetemeko wa sauti yake kutoka katika boksi la sauti
katika koo yake, huzalisha mtetemeko (vibration) na
kusafirishwa kupitia ulimi na mdomo kisha ndipo mtu
anaesikiliza hupokea mawimbi ya mtetemeko wa sauti kupitia
masikio yake ambayo huyasafirisha mawimbi hayo kuyapeleka
kwenye ubongo ambao huyatafsiri na kisha akili humfanya
atende ama kuitika kwa mujibu wa kilichosemwa.

109
Tom, akaendelea kufafanua kuwa hisia za mwanadamu,
mawazo na matokeo ya hisia, yote yapo katika mfumo wa
mtetemeko wa sauti ndani ya ubongo. Ndio maana mtu
anapokuwa macho (hakulala) akili yake hutenda kwa mujibu wa
hisia, mawazo ama maelekezo. Bali hali hiyo huwa tofauti
endapo mtu huyo anapokuwa amelala, kwakuwa hakuna
maingiliano ya sauti, hivyo akili ya mtu huyo haiwezi tena
kudhibiti mawazo, hisia na matendo kwa kipindi chote cha kulala
kwake.

Hivyo basi, kwa ufafanuzi huu mfupi tunaweza kusema kuwa


usikivi wa mwanadamu unao mchango mkubwa katika kuamua
mawazo, hisia na maamuzi ya matendo ya mtu. Kwa mujibu wa
Makala ya Al-Jazeera (2020) walisema kuwa ala zote za muziki
kabla ya karne ya ishirini zilipangwa na kuwekwa katika masafa
ya sauti (frequency) ya umbali wa 432 Hertz. Masafa ambayo
watumizi wa muziki na wataalamu wa ala wanasema kuwa
huufanya muziki unaozalishwa na ala hizo kuwa na sauti za asili
na wenye upekee wa mrindimo.

Kupitia masafa hayo ya 432 Hz yaliaminika kuwa ndio masafa


ambayo huzifanya ala za muziki kuburudisha na kutoa matokeo
mazuri kwa wasikilizaji. Hivyo kila aina ya muziki katika kipindi
hicho kilitumia masafa (frequency) hiyo. Miaka sabini ya
matumizi ya masafa hayo (432 Hz) Mkutano Mkuu wa Kimataifa

110
wa Muziki na Ala Duniani ulitoa mapendekezo ya kubadilisha
masafa ya 432 Hz na kuwa 440 Hz.

Baada ya mabadiliko hayo, wasomi mbali mbali wa masuala ya


muziki walieleza kile ambacho wamekitafiti kupitia mabadiliko ya
masafa hayo. Alan Cross, mtayarishaji nguli wa muziki na
mtangazaji wa kituo cha redio nchini Marekani alisema kuwa
wakati akihojiwa na Al-Jazeera; Asili ya muziki na masafa ya ala
za muziki yalipangwa na kugunduliwa na dhana maarufu ya
Pythagorean. Dhana ambayo ilikuja kuweka misingi ya masafa
ya ala za muziki na kupanga namna ambayo muziki usikike.

Kwa mujibu wa dhana hiyo, masafa ya 432 Hz ndiyo yaliufanya


muziki usikike kuwa na ladha na mrindimo wa asili zaidi kwa
msikilizaji ili uweze kufikia lengo maalumu linalokusudiwa na
msikiliza husika. Masafa ya 432 Hz ndio yalioufanya mziki kuwa
ni burudani, kitulizo na ponya kwa wasilizaji. Kupitia masafa
hayo (432 Hz) yaliwezeshwa kupenya kwenye masikio ya
msikilizaji na kuleta athari ya wastani ya lengo lililokusudiwa.
Kwa mujibu wa Bwana Cross, mabadiliko ya masafa kutoka 432
Hz hadi 440 Hz hayakuwa ya bahati mbaya, yalipangwa na
kupangiwa dhamira maalumu kwani kuna utofauti mkubwa wa
ladha ya mirindimo ya muziki unaotumia masafa ya 440 Hz na
ile ambayo hutumia masafa ya asili ya 432 Hz.

111
Kutokana na ufafanuzi huo, Bwana Cross aliulizwa na mwandishi
kuwa; anahisi kwamba mabadiliko ya masafa hayo ya muziki
duniani yanayo mpango maalumu tofauti na wa kitaaluma ya
muziki? Alijibu kuwa; Ukweli ni kwamba kila mtu (wataalamu wa
muziki) anayo dhana yake katika jambo hilo!

Wapo wanaoamini kuwa mabadiliko haya yalitokana na


kufanyika kwa ushawishi mkubwa wa Chama na Nazis (Chama
cha Hitler) ambapo masafa haya kama yalivyo, yalipangwa
maalumu kuwa ni yenye ukali na ushawishi mkubwa katika
masikio ya watu. Yakafaywa kama ni nyenzo ya kueneza dhana
potofu (propaganda) kupitia ala za muziki na tungo zenye
kupambwa kwa muziki kwa ajili ya kuwateka watu kiakili na
kuwaongoza kwa makundi katika vita kuu za dunia mnao miaka
ya 1945.

112
Kadhalika, wapo miongoni mwa watafiti wa masuala ya muziki
na ala wanaosema kuwa mabadiliko ya masafa ya muziki kutoka
masafa ya 432 Hz kwenda 440 Hz yametokana na kusababishwa
na familia tajiri na yenye ushawishi mkubwa katika dunia ya
Rockefeller. Ambapo inasemwa kuwa walitaka kuutumia muziki
kuhakikisha maslahi yao katika akili za wafuasi wao. Baada ya
ufafanuzi huu, Bwana Cross aliulizwa pia juu ya maoni yake
katika kuutumia muziki kuwashawishi na kuwatawala watu
kihisia na kiakili. Alijibu kwa kusema kuwa miziki unaweza
kutumika kubadilisha matendo na tabia ya mtu. Na kwa
uthibitisho juu ya dhana hiyo, alisema kuwa unaweza kuenda
katika vituo maalumu vya tiba ya akili vinavyotumia miziki
maalumu kuwasaidia wagongwa kupata utulivu akili na nafsi
kutokana na wasiwasi.

Aidha, Bwana Cross akasema kuwa unaweza kuenda katika


kumbi za muziki na starehe (Night Clubs) kisha subiri mtu aweke
wimbo mzuri ambao unaburudisha ama kuwapa watu
uchangamfu, utaona kila mtu ana chizika kihisia na kupandwa
na kichaa cha furaha. Aliongeza kuwa sababu hiyo ndio maana
kila nchi inao wimbo wa Taifa – ambao umeandaliwa kuleta
hisia za uzalendo.

113
Ndio maana kila kikosi cha wapiganaji kinao wimbo wa kishujaa
na kujaza morali ya mapigano ama maandamamo. Kwa
kuongeza akasema pia, tunaona hata vikundi vya mazoezi
namna ambavyo hutunga nyimbo kadhaa za kuongeza morali
wakati wa mazoezi kwa kuamsha hisia za ari na kupandisha
kiwango cha nguvu ya mwili na akili. Si hivyo tu zipo nyimbo
ambazo hutumika katika maandamano ambazo zimeundwa
kujenga ujasiri na kuondoa hofu na uoga hata kama kutakuwa
na vizuizi vya nguvu na dola.

Tukirudi katika mtazamo wa mabadiliko ya masafa ya muziki


kutoka 432 Hz hadi kufikia 440 Hz unaweza kuona sababu ya
watu wengi kuamini kuwa zipo sababu za siri za mabadiliko
hayo. Sababu ambazo huenda zikawa zimetokana na jamii za
siri ambazo walikuwa na dhumuni la kuubadili muziki na
kuufanya uwe na chanzo cha mambo tofauti katika ulimwengu.

114
Mwandaaji mashughuri wa muziki duniani Bwana Guiseppe Vardi
alikuwa ni muungaji mkono mkuu wa masafa ya 432 Hz na ndio
maana masafa hayo pia huitwa ‗Vardi‘s La‘. Inaaminika kuwa
ndio falsafa ya asili yenye mrindimo wa uhakika wa kihisabati
ambao huenda sambamba na mtetemeko wa ulimwengu.
Uwiyano huo, kwa mujibu wa wanasayansi wa Ulimwengu
wanaamini kuwa ndio masafa sawa na masafa ya sumaku
umeme ya dunia.

Dhamira kuu ya kufanya tafiti juu ya ufafanuzi huu, ni


kubainisha juu ya mitazamo tofauti ya wasomi wa masuala ya
muziki duniani. Kadhalika, ni kubainisha mahusiano yaliopo kati
ya muziki na athari zake kwa wasikilizaji ili tutakapo elezea juu
ya namna ambavyo Qur‘an imeharamisha muziki katika karne ya
saba iwe ni wepesi kufahamu sababu na msingi wake mkuu.
Ufafanuzi ambao umetolewa na kunukuliwa na wataalamu mbali
mbali juu ya athari na malengo makuu ya kuandaliwa kila aina
ya muziki, haukufanyika katika karne za mbali. Bali tafiti hizi
zilifanyika mnamo karne ya ishirini na ishirini na moja huku
matokeo yake yakibainisha kwa uwazi athari za muziki kwa
msikilizaji. Si hivyo tu, bali matokeo ya tafiti hizo yamefafanua
hadi namna ambavyo dhana mbali mbali za namna muziki
hutumiwa katika kupandikiza mambo kadhaa wa kadhaa yenye
msukumo hasi kwa jamii haswa ya vijana. Jamii ambayo ndio uti
wa mgongo wa maendeleo na tenda kazi ya kizazi kipya.

Mbali na kuwa wasomi na wanasayansi wa masuala ya muziki


kushindwa kutambua mapema athari za muziki na namna
ambayo muziki huweza kuathiri matendo na tabia za
mwanadamu, Uislamu kupitia nyenzo zake kuu za mafunzo na
misingi ya maisha ambayo ni Qur‘an na Sunna za Mtume
Muhammad (Rehma na Amani ziwe juu yake) ulishafundisha
misingi ya kukataza na kuuharamisha muziki katika jamii yake.
Uharamu wa muziki ndani ya Qur‘an na Sunna unaendelea
kuthibitisha kuwa mafunzo ya yapatikanayo ndani yake
hayakuwa tu ni maneno ya kiumbe yoyote kama ambavyo

115
wengi waliamini na kuaminishana hapo awali, bali yanathibitisha
kuwa ni maneno matukufu kutoka kwa mtukufu.

Haidhuru, Qur‘an haikuileza na kufafanua kwa uwazi juu ya


uharamu muziki, badala yake ilitumia maneno ya kinaya ambayo
wafasiri wa Qur‘an wamekubaliana kuwa maneno hayo
yamekusudia kuutaja na kuuharamisha muziki. Allah
(Subhanahu) anasema kupitia Qur‘an tukufu akiuharamisha
muziki kuwa;
‖Na wachochee uwawezao katika wao kwa sauti yako, na
wakusanyie jeshi lako la wapandao farasi na waendao kwa
miguu. (17:64)

Ibn Kathir (Rehma za Allah ziwe juu yake) amesema katika


tafsiri yake kuwa maana ya kauli ya Allah (Subhanahu) ya
kusema “Kwa sauti yako” inamaanisha kuwa ni burudani za
kukonga nyoyo na kuimba. Huku akisema kuwa anaekusudiwa
kuambiwa hapa ni Ibilisi (Laana za Allah ziwe juu yake) kuwa
aendelee kuwapoteza wale atakao waweza kwa kupitia sauti
yake ambayo ni muziki. Kupitia aya hii, Allah (Subhanahu)
ametumia neno sauti ya Ibilisi au Shetani akiulezea muziki. Bali
pia kauli hii ya Allah (Subhanahu) inafafanua namna ambavyo
muziki unavyoweza kuwachochea watu kubadilika kitabia na
kuingia katika yale ambayo yamekatazwa.

As Sa‘adi (Rehma za Allah ziwe juu yake) akafafanua pia kauli


ya Allah (Subhanahu) “Kwa sauti yako” na kusema kuwa
maana yake ni muito au uhamisishaji wowote ambao mtu
huufanya kuwaita watu katika yale ambayo yanamkasirisha
Allah (Subhanahu) na kumpeleka mtu katika yake
yaliyoharamishwa ambayo ni katika njia ya Shetani.
Allah (Subhanahu) amesema pia katika Surat Luqmaan;
―Na miongoni mwa watu wapo wanao nunua maneno ya
upuuzi, ili wawapoteze watu na njia ya Allah pasipo kujua, na
wanaichukulia ni masihara.‖ (31:06)
“Maneno ya upuuzi” ndio kauli ambayo Allah (Subhanahu)
ameitumia akiimanisha muziki. Kwa mujibu wa Ibn Kathir

116
(Rehma za Allah ziwe juu yake) amesema “wanao nunua
maneno ya upuuzi” ni wale ambao wanajiweka mbali na kuipa
mgongo Qur‘an, na wasio faidika na maneno ya Allah
(Subhanahu) badala yake, hugeukia kusikiliza zumari na nyimbo
ambazo zimeambatana na ala za muziki.

Ibn Kathir (Rehma za Allah ziwe juu yake) amemnukuu Imam


Qatadah (Rehma za Allah ziwe juu yake) akisema kuwa maana
ya “wanao nunua maneno ya upuuzi” maana yake ni kuwa;
hawatumii fedha zao katika njia ya Allah (Subhanahu), bali
huzitumia katika kununua upuuzi wa muziki ambao wanaupenda
zaidi, na kadiri wanavyopotea katika kupenda kusikiliza maneno
ya Allah (Subhanahu) ndivyo ambavyo anavyozama zaidi katika
kuupenda muziki zaidi na zaidi.

As Sa‘ad (Rehma za Allah ziwe juu yake) amefafanua katika


tafsiri yake kuwa kauli ya Allah (Subhanahu) juu ya “Maneno
ya upuuzi” amesema yanajumuisha mambo mengi ikiwamo
kauli za uongo, hadithi zisizo na maana, kusengenya, kuimba
na ala za muziki, umbea, na mengi mengine ambayo hayana
faida kwa mfanyaji katika dini yake wala dunia yake. Yamkini,
ufafanuzi wa makatazo ya muziki kupitia Qur‘an umekuja
kueleza na kubainisha juu ya athari zake huku ukiutaja kwa
majina na kauli tofauti.

Kwa hakika kwa mja yoyote mwenye busara na upeo kiasi wa


elimu na ufahamu akisoma ufafanuzi na makatazo ya muziki
kupitia Qur‘an tukufu yaliyotolewa karne ya saba, kisha akarejea
hadith sahihi za Mtume wa Allah juu ya miziki na baada ya hapo
akasoma na kuzingatia ufafanuzi wa wasomi wa mambo ya
muziki juu ya athari zake, ni dhahiri anaweza kuona na
kutanabahi matokeo mabaya yanayoweza kusababishwa na
muziki hapa duniani na mbele ya Allah (Subhanahu).

Ibn Jawzy (Rehma za Allah ziwe juu yake) aliandika katika


kitabu chake ‗Talbis Iblis‘ kuwa; muziki na kuimba hupelekea
katika mambo wawili, kwanza humtoa mtu katika kumkumbuka

117
Allah (Subhanahu), na pili hupelekea katika matamanio ya
mambo maovu haswa katika uzinifu. Aliongeza pia; Iblisi alikata
tamaa baada ya kuona waumini wameacha na kujiepusha na
kusikiliza na kuimba nyimbo zenye ala za muziki. Alipoona hivyo,
aliwaletea nyimbo badala yake ambazo hazitumii ala za muziki.
Jambo ambalo liliwasogeza taratibu kutoka katika kusikiliza
nyimbo zisizo na ala za muziki, hadi kuwarejesha tena katika
kuimba na kupiga miziki na ala mbali mbali.

Je! Kama athari za muziki zimeelezwa na kufafanuliwa vyema na


Qur‘an, sambamba na maelezo ya kina yaliyofanywa na
wanazuoni wakubwa wa tafsiri huku maelezo yao
wakithibitishwa waziwazi na sayansi katika karne ya ishirini na
ishirini na moja. Tunahitaji waadhi gani tena kutuelemisha na
kutukataza juu ya muziki na athari zake?

Kwa msingi huo; bado tunaweza kusema tunahitaji miziki ndani


ya Uislamu au maisha yetu kwa ujumla, baada ya kuchambua
athari zake? Je! Wale ndugu zetu ambao wamekuwa wakibuni
njia mbali mbali za kuuingiza muziki ndani ya dini kwa kisingizio
cha Qaswida hawaoni kwamba wanaendelea kuipoteza jamii
haswa ya vijana ambayo matendo hayo huwakimbiza kutoka
katika kuchukua mazingatio ya mafunzo ya Qur‘an badala yake
kuelekea miziki (Inayoitwa Qaswida) Tumche Allah (Subhanahu)
na tuogope na kuchunga mipaka yake.

Kadiri zama zinavyosogea ndivyo zile athari ambazo zilitazamiwa


kuzalishwa na muziki zinadhihiri. Kwani hatuoni namna ambavyo
muziki unavyotumika kuhamasisha mambo lukuki ya kipuuzi.
Muziki umekuwa ni chombo na silaha madhubuti ya kuharibu
fikra za kiitikadi sahihi, mila, desturi n ahata murua wa
kibinadamu. Muziki umekua ukihimiza na kushajihisha ushoga,
ulevi, usagaji na mambo kadhaa wa kadhaa ambayo yapo nje
kabisa ya misingi ya Uislamu, bali hata nidhamu ya kawaida ya
maumbile.
―Haumwi (na nyoka) Muumini katika tundu moja mara
mbili.”
118
Qur‟an na Sayansi ya Wanyama (Zoolojia)
Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia katika karne ya ishirini na
ishirini na moja yamemuezesha mwanadamu kusoma na kutafiti
masuala mbali mbali. Miongoni mwa matokeo makubwa ya tafiti
hizo ni kupatikana elimu juu ya biolojia ya wanyama, sayansi
ambayo imewawezesha kutambua na kusoma kwa kina ufalme
wa wanyama kuanzia tabia zao, aina zao, maumbile, uzawa wao
na hata asili ya kukuwa kwao.

Sayansi ya Wanyama kitaalamu huitwa “Zoology” ni miongoni


mwa fani na matawi ya biolojia ambayo husomwa na
kufundishwa kwa kina katika nidhamu ya kuwatambua
wanyama katika nyanja zao. Taarifa za kitafiti zinatueleza kuwa
nidhamu na sayansi ya zoolojia iligunduliwa kwa mara ya
kwanza katika karne ya kumi na sita, ambapo mtafiti Aristotle
aligundua na kuwagawa wanyama katika makundi mawili
makubwa. Kundi la wanyama wenye damu nyekundu na wale
ambao hawana, kama vile wadudu na viumbe hai wengine
wadogo wadogo.

Mgawanyo huo wa Aristotle, ulidumu hadi ilipoisha karne ya


kumi na sita, ndipo wanasayansi wengine wakaja na matokeo ya
tafiti ambazo zimekuja kuipambanua kwa kina fani hii ya
wanyama, na kuifanya kuwa pana na kuwa na vigawanyo vingi
vya wanyama kwa mujibu wa matabaka tofauti. Maendeleo
hayo ndio yalikuja kuikuza fani hii na kuifanya iwe ni nidhamu
yenye kusomwa kitaaluma na wataalamu wabobevu kupatikana.

119
Wanasayansi wanakisia kuwa zipo aina takribani milioni 8.7 za
viumbe hai katika dunia. Aidha, inakisiwa pia, kuwa kati ya
milioni moja hadi mbili za viumbe wote hai duniani ni wanyama
na wadudu wengine.

Ili mtu awe ni nguli na mbobevu katika fani na nidhamu hii


humpasa kupitia katika mafunzo rasmi ambayo yameandaliwa
huku yakianza katika ngazi ya awali ya shahada hadi kufika
katika ngazi ya uzamivu (PhD). Kutokana na ukweli kuwa elimu
na ugunduzi juu ya masuala ya sayansi ya wanyama ilikuja
miaka kadhaa baada ya kushushwa kwa Qur‘an (karne ya saba)
inaweza kuwa ajabu kuwa Qur‘an hiyo ilishafanya uchambuzi na
kubainisha juu ya elimu ya sayansi ya wanyama.

Qur‘an imefafanua na kubainisha namna ambayo katika fani ya


kuumbwa kwa ulimwengu ni pamoja na kuumbwa kwa aina
tofauti za wanyama, wenye sifa na tabia tofauti, wenye vinasaba
na tabia za kibiolojia tofauti pamoja na maumbile yao. Sayansi

120
ya wanyama ilifafanuliwa katika karne ya saba miaka takribani
elfu moja kabla ya matokeo ya tafiti ya Aristotle ambaye
inaaminika kuwa ndiye „Baba wa Sayansi ya Wanyama‟.
Qur‘an katika kufafanua taaluma hii, kwanza ilianza kueleza
kuwa wanyama nao ni viumbe na ni mkusanyiko wenye
mchanganyiko wa aina mbali mbali za viumbe wenye aina,
tabia, na maumbile tofauti, Surat Al-An‘am;
―Na hapana mnyama katika hii ardhi, wala ndege anayeruka
kwa mbawa zake mbili, ila ni umma kama nyinyi. Hatukupuuza
kitabuni kitu chochote. Kisha kwa Mola wao Mlezi
watakusanywa.‖ (06:38)

Kwa mujibu wa ufafanuzi wa kisayansi juu ya fani ya Zoolojia,


tulieleza kuwa miongoni mwa nidhamu za taaluma hiyo ni
kujifunza na kujua mjumuiko wa wanyama na tabia zao, pamoja
na mambo kadhaa yanayowahusu. Qur‘an kupitia Aya hii
ilifungua mlango wa elimu juu ya kutambua juu ya umma ama
mkusanyiko wa wanyama wenye maisha ambayo yanafanana na
umma ama mkusanyiko wa viumbe wengine hai kama vile
mwanadamu.

Ibn Kathir (Rehma za Allah ziwe juu yake) amesema kuwa


maana ya kauli ya Allah (Subhanahu) “ila ni Umma kama
nyinyi” maana yake ameeleza kama alivyomnukuu Mujahid
(Rehama za Allah ziwe juu yake) akisema ameumba aina tofauti
ya viumbe hai. Amemnukuu Qatadah (Rehma za Allah ziwe juu
yake) pia akisema kuwa maana ya kauli hiyo ni kuwa Ndege ni
Umma, Majini ni Umma, Wanadamu ni Umma, kama vile walivyo
Umma wanyama wengine.

Aidha, katika kuendelea kufafanua juu ya sayansi ya wanyama,


Allah (Subhanahu) amesema ndani ya Qur‘an kuwa;
―Na hakuna mnyama yoyote katika ardhi ila riziki yake iko kwa
Allah. Naye anajua makao yake na mapitio yake.‖ (11:06)
Baadhi ya wanazuoni wafasiri wa Qur‘an wanasema kuwa aya
hii inatafsiri ile kauli ya Allah (Subhanahu) kuwa
“Hatukupuuza kitabuni kitu chochote” wakasema kuwa

121
inathibitisha juu ya elimu juu ya sayansi ya wanyama (Zoology)
kuanzia chakula cha kila aina ya wanyama, uzazi na makuzi yao.
Na hii ilitosha kuwa ni ishara na ufafanuzi wa kuwawezesha
wanasansi wa karne za sasa kupata mwanzo mzuri wa kigunduzi
katika kujua tabia za wanyama.

Kadhalika, Allah (Subhanahu) amesema pia ndani ya Qur‘an


kumfahamisha Mtume wake (Rehma na Amani ziwe juu yake)
akifafanua aina mbali mbali za wanyama kuwa;
―Na Allah ameumba kila kinyama (kiumbe hai) kutokana na
maji. Wengine katika wao huenda kwa matumbo yao, na
wengine huenda kwa miguu miwili, na wengine huenda kwa
miguu mine.‖ (24:45)

Kwa mujibu wa wafasiri wa Qur‘an wanasema kuwa kauli hii ya


Allah (Subhanahu) inabainisha aina na tabia tofauti za wanyama
kwa kubainisha namna ambavyo hutembea katika mgongo wa
ardhi kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyengine.
Wanaotembea kwa kutumia tumbo ni wale ambao
hawakuumbwa kuwa na miguu kama vile nyoka. Na wale
wanaotembea kwa miguu miwili kama vile ndege na wale
ambao hutembea kwa miguu mine ni ule mjumuiko wa
wanyama wakubwa. Tunawezaje kusema kuwa tafiti za
Aristotle ndizo pekee zilizoweza kugundua sayansi ya wanyama!
Hali ya kuwa Qur‘an ilishafafanua hadi aina za wanyama na
mienendo yao ambayo haikuwa rahisi kwa kipindi ambacho
Qur‘an ilishushwa kubainika.

Qur‘an tukufu haikuishia tu katika kufafanua tabia na mienendo


ya wanyama tofauti bali pia iliufahamisha ulimwengu hata
baadhi ya faida na matumizi ya baadhi ya wanyama. Allah
(Subhanahu) amesema ndani ya Surat An-Nahl kuwa;
―Na wanyama hoa amekuumbieni. Katika hao mna vifaa vya
kutia joto, na manufaa mengineyo, na baadhi yao mnawala. Na
wanakupeni furaha pale mnapo warudisha jioni na mnapo
wapeleka malishoni. Na hubeba mizigo yenu kupeleka kwenye
miji msiyo weza kuifikia ila kwa mashaka ya nafsi.‖ (16:5-8)
122
Sayansi juu ya Wanyama na matumizi yake imeelezwa vyema
kupitia Aya hizi, Ibn Kathir (Rehma za Allah ziwe juu yake)
amesema maana ya kauli ya Allah (Subhanahu) “Katika hao
mna vifaa vya kutia joto” amesema ni fadhila za Allah
(Subhanahu) alizoziweka kupatikana kutokana manyoya na
nywele za wanyama hoa ambazo hutumika kutengeneza nguo
nzito kwa ajili ya kuzuia baridi na mazulia ya mapambo.

123
Kadhalika, akafafanua kuwa kwa kauli ya Allah (Subhanahu)
kuwa; “Na manufaa mengineyo, na baadhi yao mnawala”
amesema maana yake ni kinywaji cha maziwa kinachopatikana
kupitia wanyama hao, na nyama inayopatikana kutokana na
baadhi ya wanyama hao walioruhusiwa kuliwa. Kupitia Aya hizi
pia Allah (Subhanahu) anaendelea kutoa mafunzo juu ya sayansi
ya wanyama katika kubainisha matumizi yao katika kumsaidia
mwanadamu kubeba mizigo mizito ambayo bila ya msaada huo
ingelikuwa tabu kufanikiwa.

Ibn Kathir (Rehma za Allah ziwe juu yake) amesema kuwa


maana ya kauli “Na hubeba mizigo yenu kuwapeleka
katika miji msioweza kufika ila kwa tabu ya nafsi”
amesema kwamba ni msaada na Rehema za Allah (Subhanahu)
kuwaumba wanyama ambao watakuwa na uwezo wa
kuwabebea mizigo kuwasafirisha katika masafa ya mbali
(alielezea kuenda Hijja na Umra) ambayo bila ya msaada huo
ingelikuwa vigumu kufika.

Hizi zote zilikuwa ni ishara za elimu kuhusu wanyama kitabia,


manufaa, na pamoja na mambo mengi ambayo yaliwachukua
wanasayansi wa karne za sasa miaka mingi kuweza kung‘amua.
Allah (Subhanahu) amesema pia;
―Na farasi, na nyumbu, na punda ili muwapande, na kuwa ni
pambo. Na ataumba msivyo vijua.‖ (16:8)

124
Unaweza kuona hapa namna ambavyo Qur‘an inaendelea kutoa
ufafanuzi juu ya aina nyengine za wanyama ambao matumizi
yao yametofautishwa na lile kundi la kwanza. Kundi hili likawa
na madhumuni ya kutumika kama msaada wa usafiri kuwabeba
watu na mali zao. Mbali na wanyama hawa wakubwa, Qur‘an
imefafanua pia tawi jengine la zoolojia kwa kuelezea aina tofauti
za wadudu na ndege. Kama ambavyo Qur‘an imemtaja na
kumuelezea kwa kina mdudu Nyuki (16:68), Buibui (29:41),
Mdudu Chungu, mbu (2:26), Nzi (22:73) na hata samaki wa
baharini (5:96, 18:61, 37:142). Na huu ndio Umma wa
wanyama na wadudu na hivyo ndivyo ambavyo Qur‘an
imeifafanua elimu juu ya wanyama na mazingira yao ili iwe ni
ubainifu kwa viumbe na Rehema kwa wenye kutafakari.

Qur‟an na Matokeo ya Sayansi ya Kitabibu

Sayansi na maendeleo yake ya Kiteknolojia yameleta mapinduzi


makubwa katika nyanja mbali mbali. Miongoni mwa matokeo na
maboresho yaliyozaliwa na maendeleo ya kisayansi ni pamoja
na gunduzi kadhaa za kitabibu ambazo matokeo yake yameleta
mwangaza kwa ulimwengu, huku ikiokoa na kunusuru afya na
siha za maelfu ya viumbe. Karne takribani ishirini na moja
zilizopita, Mtume wa Allah (Rehma na Amani ziwe juu yake)
alifundisha kwa wafuasi wake juu ya makatazo kadhaa wa
kadhaa yaliyotokana na Qur‘an ambayo kwa kipindi kirefu wengi
miongoni mwa watu hawakujua sababu na msingi mkuu wa
makatazo hayo. Jambo ambalo lilipelekea wale ambao
hawakuwa na Imani thabiti kuwa ngumu kwao kukubali na
kujiweka mbali na yale yote yaliyo katazwa.

Sayansi na teknolojia ikashika hatamu huku baadhi ya


wanasayansi nguli wakaamua kuketi na kutafiti kwa kina sababu
na misingi mikuu ya makatazo ya baadhi ya mambo ambayo
yaliwekwa na Qur‘an miaka elfu moja mia nne iliyopita. Kwa
kutumia taaluma, vifaa na nyenyo kadhaa za kisasa wali,
waliibuka na matokeo ya kushangaza ambayo yanaikiri na
kuakisi sababu kuu za makatazo yaliyowekwa na Qur‘an tukufu.
125
Matokeo ya Sayansi na makatazo ya kula Mzoga na
kunywa damu:
Allah (Subhanahu) kupitia Qur‘an tukufu iliyoshuhswa kwa
Mtume wa Allah (Sala na Salamu ziwe juu yake) karne ya saba
ilikuja na kukataza moja kwa moja kunywa damu, damu hiyo
iwe ni ya binadamu au hata ya mnyama. Allah (Subhanahu)
anasema ndani ya Surat Al-Baqara;
―Yeye (Allah) amekuharamishieni mzoga tu na damu.‖
(02:173)

Wafasiri wa Qur‘an wanasema kuwa makatazo ya nyama ya


mzoga na damu yamekuja kwasababu vitu vyote hivi sio safi na
havina manufaa yoyote kwa wanadamu. Kwa mujibu ya
mafundisho ya Uislamu mnyama yoyote anaechingwa kwa
kufuata masharti ya sharia za Qur‘an ni lazima achinjwe kwa
kukatwa mshipa wake mkubwa wa shingo ili kuruhusu kiwango
kikubwa cha damu kiweze kutoka na kuifanya nyama yake iwe
salama kutokana na madhara yote ambayo hupatikana ndani ya
damu.

126
As-Saad (Rehma za Allah ziwe juu yake) amesema akifafanua
juu ya makatazo ya nyama za mzoga amesema kuwa kusudio la
makatazo haya ni kuwa nyama ya mzoga sio salama kwakua
mtu hajui sababu za kufa kwa mnyama huyo, na huenda sababu
ya kifo ni kutokana na maradhi ambayo huenda yakampata yule
mwenye kula nyama hiyo. Hivyo hivyo, akaeleza kuwa na damu
ya mnyama huwa na madhara makubwa kwa mnywaji.

Ufafanuzi huu unathibitishwa moja kwa moja na matokeo ya


tafiti mbali mbali za kitabibu ambazo zinaonyesha wazi wazi
madhara ambayo hupatikana ndani ya damu ya mnyama au
binadamu. Kwa mujibu wa Makala iliyochapishwa na mtandao
wa Healthline (2022) wamesema kuwa unywaji wa damu (ya
mnyama ama binadamu) huhatarisha usalama wa mnywaji kwa
kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kuweza kuambukizwa
maradhi ya asili yanayopatikana katika damu.

127
Aidha, wamesema kuwa unywaji wa damu huongeza kiwango
cha madini chuma ndani ya mwili na kufikia kiwango cha juu
ambacho hakihitajiki ndani ya mwili, na hupelekea kusababisha
magonjwa mengi sugu kama vile shindikizo la damu, magonjwa
ya ini, magonjwa ya viungo na uharibifu wa mfumo wa kinga ya
mwili. Matokeo haya yamekuja baada ya kugundulika viini
hatarishi ambavyo hubaki kuwa hai kwa kipindi kirefu ndani ya
damu.

Ingawaje wataalamu wa afya wanasisitiza kuwa unywaji wa


damu usichanganywe (kimaana) na njia ambazo hutumika
kuwaongezea damu wale ambao wamepungukiwa kwa sababu
njia ya kuongeza damu ni salama kwa kuwa damu hiyo

128
huingizwa moja kwa moja katika mishipa ya muhitaji, hivyo
haipiti katika mzunguko wa kawaida wa chakula. Na hata hivyo
inasisitizwa kuwa kabla mtu kuongezewa damu ni lazima
ifanyiwe vipimo vya usalama wa maradhi kadhaa wa kadhaa.
Damu chanzo muhimu sana cha vinasabata vyote vya
binadamu, makatazo yake kwa mujibu wa sayansi ya tiba
yamefafanua athari zake ikiwa ni pamoja na uwezekano wa
kupandikiza vinasabata ambavyo ni huenda vikakinzana na vile
vinasaba vya asili vya mtu. Tunashuhudia wimbi kubwa la
ongezeko la maradhi mengi duniani, huku watafiti wa masuala
ya afya na tiba wakiyaelekeza moja kwa moja kuwa chanzo
chake ni muingiliano wa damu. Matokeo haya ya kitafiti na
kisayansi yamekuja kuonyesha ulimwengu kuwa kila jambo
ambalo limekatazwa na Qur‘an basi zipo sababu za msingi juu
ya makatazo yake kwa viumbe.

Matokeo ya Sayansi na makatazo ya Nyama ya nguruwe:

Uislamu tangu kuja kwake katika ulimwengu, ulikuja na


makatazo mbali mbali ikiwa baadhi ya makatazo hayo ni yale
ambayo yalitolewa kwa hatua kadhaa, na yale ambayo yalikatwa
na kukatazwa moja kwa moja. Qur‘an ikiwa ndio nyenzo kuu ya
Imani ya Uislamu umekataza na imetoa miongozo mbali mbali
katika vyakula ikiwamo nafaka, mimea, na nyama. Ndani ya
miongozo hiyo ya vyakula, ilibainisha wazi wazi katazo la kula
nyama ya Nguruwe.

Katazo na uharamu wa nyama ya nguruwe ukaifanya Qur‘an


kuwa ni kitabu pekee ambacho kimeweka na kubainisha sharia
hiyo wazi wazi, jambo ambalo liliwafanya wengi miongoni mwa
watu (wasomi) kutaka kuufahamu undani wa katazo hilo.
Wasomi na watafiti wa masuala ya tiba na vyakula
hawakuwaridhika tu na katazo hilo, na yote ni kwa sababu
ilishawabainikiwa kuwa kila katazo ambalo lilitolewa na Qur‘an
basi limekuwa na mahusiano ya moja kwa moja na matokeo
makubwa ya kisayansi.

129
Kama ambavyo Sayansi imeendelea kuikiri Qur‘an katika
masuala mbali mbali, Mwanasayansi wa tiba ya wanadamu
Profesa Dana Hunnes wa Chuo Cha Nadharia na Vitendo vya
Afya ya Jamii cha Marekani alisema akihojiwa na jarida la ZME
Science (2023) alisema; ―Sitapenda kushauri ulaji wa mazao
ya wanyama, na kwa msisitizo kabisa ulaji wa nyama ya
nguruwe.‖ Akaongeza kuwa miongoni mwa sababu za kusema
maneno hayo ni kwamba nyama ya nguruwe imesheheni
kiwango kikubwa cha mafuta na lehemu.

Sayansi inathibitisha kuwa ipo tofauti kubwa kati ya mfumo wa


mmeng‘enyo wa chakula wa ngurume kulinganisha wa
wanyama wengine ambao wameruhusiwa kuliwa. Madaktari wa
mfumo wa chakula wa wanyama wanasema kuwa nguruwe
tofauti na wanyama wengine ambao wameumbwa kuwa na aina
mbili za matumbo. Matumbo ambayo hutumika kwa madhumuni
tofauti kulingana na ukubwa na umbile la mnyama huyo.
Wanyama kama ng‘ombe, mbuzi, kondoo, ngamia na wengine
wameumbwa huku wakiwa na tumbo maalumu ambalo
hutumika kuchuja na kupembua chakula alichokula kwa masaa
nane kabla ya chakula hicho kupelekwa kwenye mfumo wa
umeng‘enyaji. Mara tu baada ya chakula kuingia ndani ya
kinywa cha mnyama hupelekwa kwenye sehemu maalumu kwa
ajili ya kuchuja chakula chenye sumu na hatarishi na kile
ambacho kipo salama.

Chakula ambacho kipo salama kitasafirishwa kupelekwa kwenye


mmeng‘enyo na kile kichafu kutolewa kwa njia ya haja kabla ya
kungia katika mfumo wa damu. Mfumo huu unautofauti
mkubwa na namna ambavyo nguruwe ameumbwa, kwani
nguruwe hana sehemu maalumu ya kupembua chakula, badala
yake mara tu chakula kinapoingia kupitia kinywa chake hutumia
takribani masaa matatu hadi kuingizwa katika mfumo mzima wa
mwili wa nguruwe, hakuna upembuzi wa mchakato wa
kutenganisha kati ya chakula salama na kile kisicho salama
ndani ya mfumo wa mmeng‘enyo wa nguruwe.

130
Kwakuwa Allah (Subhanahu) ndio muumbaji wa kila kiumbe hai,
na ndie anaejua kipi ni manufaa na salama kwa waja wake, na
kipi si salama, aliweka muongozo kupitia Qur‘an juu ya ulaji wa
vyakula na wanyama kama ilivyokuja ndani ya Surat An-Nahl;
―Basi kuleni katika vile alivyo kupeni Allah, vilivyo halali na
vizuri.‖ (16:114)

Kutokana na ufafanuzi huu na muongozo wa Qur‘an juu ya


nyama ya nguruwe, basi utaona kuwa nguruwe hayupo katika
vyakula (nyama) halali na wala hayupo katika vile vilivyo vizuri.
Tafiti nyingi zimefanyika na matokeo mbali mbali yameelezwa
juu ya madhara ya nyama ya nguruwe katika sayansi ya tiba na
afya ya mwaadamu. Matokeo ya tafiti iliyofanyika mwaka 2011
na ZME Science inaeleza kuwa; majaribio ya takribani watu laki
moja ambao walikula nyama ya nguruwe wamekuwa na
uwezekano mkubwa wa kupata magonjwa sugu kama vile
kisukari kwa asilimia 35%, kuziba kwa mishipa ya damu
nakadhalika. Huku tafiti hizo zikieleza kuwa sababu kuu ni
kwamba lehemu na mafuta yaliyomo ndani ya nyama ya
nguruwe ni yakiwango kikubwa, ambacho kiwango cha kawaida
cha joto la mwili hakiwezi kuunguza.

Kutokana na madhara hayo na mengine mengi ambayo


hatujayaeleza, jarida moja limeandika kuwa katika karne ya
ishirini zipo nchi ambazo huzuia ulaji wa nyama ya nguruwe kwa
kiwango kikubwa katika majira ya baridi. Ikaelezwa kuwa
sababu kubwa ni kwamba kipindi hicho joto la mwili hushuka
kwa kiwango kikubwa na husababisha uwezo wa mwili kusaga
na kumeng‘enya chakula kuwa mdogo zaidi.

Allah (Subhanahu) amesema;


―Amekuharamishieni nyamafu (mzoga) tu, na damu, na nyama
ya nguruwe na mnyama aliye chinjwa kwa ajili isiokuwa ya
Allah. (16:115)
Allah (Subhanahu) amesema pia;
―Mmeharamishiwa nyamafu (mzoga), na damu, na nyama ya
nguruwe, na mnyama aliyechinjwa kwa ajili asiye kuwa Allah, na
131
alie kufa kwa kunyongeka koo, na aliye kufa kwa kupigwa, na
aliye kufa kwa kuanguka, na alie kufa kwa kupigwa pembe, aliye
liwa na mnyama, ila mkimdiriki kumchinja. Na pia ni haramu
kula nyama aliye chinjiwa masanamu. Na ni haramu kupiga
ramli. Leo walio kufuruwamekata tamaa na Dini yenu; basi
msiwaogope, bali niogopeni Mimi. Leo nimekamilisha Dini yenu,
na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni
UISLAMU uwe ndiyo Dini yenu. (05:03)

Na kwa hakika katika kuchunga yale yaliyoharamishwa


juu ya yale yaliyo halali, Allah (Subhanahu)
akaikamilisha dini na neema zake kwa viumbe.
Matokeo ya Sayansi juu ya faida za Tende:
Allah (Subhanahu) ameitaja tende ndani ya Qur‘an katika kisa
cha Mama Maryam (Amani ya Allah iwe juu yake). Wakati
Maryam (Amani ya Allah iwe juu yake) akiwa na mimba ya Nabii
wa Allah Issa, huku ikiimpa uzito mkubwa wa maumivu na dhiki
za mimba kama ilivyokuja ndani ya Surat Maryam;
―Kisha uchungu (wa mimba) ukampeleka kwenye shina la
mtende; akasema: Laiti ningeli kufa kabla ya haya, na nikawa
niliye sahaulika kabisa!‖ (19:23)

Kisha Allah (Subhanahu) akasema pia;


―Pakatangazwa kutoka chini yake: Usihuzunike! Hakika Mola
wako Mlezi amejaalia chini yako kijito kidogo cha maji! Na
litikise kwako hilo shina la mtende, utakuangushia tende nzuri
zilizo mbivu. Basi kula, na kunywa, na litue jicho lako. (19:24-
26)

Qur‘an imeitaja tende huku ikiifunganisha na uchungu wa


mimba. Bila shaka Qur‘an katika karne ya saba ilikua inatoa
bishara njema ya kitabibu juu ya matumizi ya tende. Wafasiri wa
Qur‘an wamezifafanua kauli hizi za Allah (Subhanahu) kwa kutoa
faida mbali mbali. Ibn Kathir (Rehma za Allah ziwe juu yake)
amesema katika tafsiri yake akinukuu kauli ya Amr bin Maymun
kuwa kauli ya Allah (Subhanahu) juu ya kumtaka Maryam ale
tende; amesema hakuna kitu muhimu na chenye faida nyingi
132
kwa mama ambae yupo katika hatua za kujifungua kuliko tende
kavu na zilizokomaa vizuri.

As-Saad (Rehma za Allah ziwe juu yake) amesema akifafanua


kauli ya Allah (Subhanahu) “Na litikise kwako hilo shina la
mtende, utakuangushia tende nzuri zilizo mbivu. Basi
kula, na kunywa, na litue jicho lako” amesema kuwa kauli
hii ilikuwa ni kumpa uhakika kuwa atakua salama kutokana na
maumivu ya kujifungua (kuzaa) kwa kuwa amempa chakula
kizuri na chenye afya na kinywaji salama.

Karne kadhaa baada ya maelezo juu ya faida za tende kutolewa


na Qur‘an. Imetambuliwa kisayansi kwa ushahidi wa tafiti
kadhaa, kuwa tende imesheheni faida nyingi kwa mwanadamu
haswa kwa mwanamke katika kipindi cha kujifungua.
Wanasayansi wamethibitisha kuwa tende zina wingi wa
nyuzinyuzi (fibers) ambazo husaidia kuondoa kabisa tatizo la
kufunga choo na ni madini muhimu ambayo hulainisha misuli
wakati wa kujifungua. Hivyo hivyo, tende imethibika kuwa na
virutubisho sukari vya asili ambavyo huupa nguvu mwili
kutokana na uchovu wa uzazi.

Kadhalika, wanasayansi wa tiba wamethibitisha kuwa tende


imejumuisha madini joto ya chumvi ya asili kama vile
magnesium kwa ajili ya afya ya seli za mwili, potasiamu kwa ajili
ya kuipa nguvu misuli na madini ya chuma kwa ajili ya kusaidia

133
kurejesha damu iliyopotea wakati wa kujifungua. Vilevile, tende
inawingi wa madini ambayo huchochea na kusaidia kutatua kuta
za njia za uzazi ambazo huzalishwa kutoka katika tenzi ya
pituitary, pamoja na faida nyingi nyengine ambazo
imefafanuliwa na wanasayansi.

Hatua za uzazi wa mtoto katika kipindi cha kujifungua


na namna tende inavyoweza kusaidia kufungua njia za
uzazi

134
135
Amri ya Ibada ya funga na faida zake kiafya:
Mbali na makatazo, Qur‘an imebainisha masuala na mambo
mbali mbali ambayo iliyafanya kuwa ni wajibu kwa kila kiumbe
kuyatekeleza, katika hayo zikawemo ibada, pamoja miamala
mengi mengine ambayo baada ya muda mrefu kupita ndipo
ulimwengu ulikuja kubaini umuhimu na faida zake kwa mtu
mmoja mmoja na jamii kwa ujumla. Kupitia maamrisho mengi,
zilibainika faida lukuki kwa viumbe na umma katika nyanja
tofauti, kama vile kiimani, kiafya na kijamii.

Allah (Subhanahu) kupitia Qur‘an iliyoshushwa kwa Mtume wake


ilikuja kuifaradhisha funga na kuifanya kuwa ni miongoni mwa
nguzo tano za Uislamu. Funga ni miongoni mwa ibada ambazo
zimewekewa wakati wake maalumu kwa wanadamu (waumini)
kuitekeleza kwa mujibu wa sharia na taratibu zilizowekwa.

Historia za ibada zinatuambia kuwa funga ni miongoni mwa


ibada kongwe kutekelezwa katika umma na zama tofauti. Lengo

136
na madhumuni makuu ya ibada ya funga ikiwa ni kumuwezesha
mfungaji kuufikia ucha Mungu kupitia kujizuia kula, kunywa na
vyote ambavyo huweza kumfuturisha mfungaji, kama ilivyokuja
ndani ya Surat Al-Baqara Allah aliposema;
―Enyi mlio amini, mumeandikiwa kufunga kama walivyo
andikiwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kuwa wacha Mungu.‖
(02:183)

Funga kwa upande mmoja imefanywa kuwa ni mazoezi ya Imani


ya muumini katika kuzuia nafsi yake, kuacha matamanio ya
haramu pamoja na kuwa na uvumilivu wa kuacha vile ambavyo
anaweza kuvimiliki, kuvitenda na kujiweka mbali na vile vitu
anavyovipenda (vyakula, vinywaji na matamanio). Qur‘an
ikaeleza malengo ya funga ikiwa ni kumfanya mfungaji aweze
kufikia darja ya taqwa; kwa kufuata na kutekeleza yote ambayo
imefunganisha nayo, huku akiacha bila ya kutozwa nguvu na
yeyote katika ambayo yanaweza kumuondoa katika utiifu wa
Allah (Subhanahu).

Ibn Kathir (Rehma za Allah ziwe juu yake) amesema katika


kufafanua maana ya amri hii ya funga kuwa; Kauli ya Allah
(Subhanahu) kuhusu kuifaradhisha funga kwa waumini, ni
pamoja na kujizuia kutokana na kula chakula, kunywa na
kukidhi matamanio ya kimwili kwa ajili ya Allah pekee. Hivyo,
funga husafisha nafsi ya mfungaji kutokana na matendo maovu
na tabia chafu.

Mbali na faida za kiimani ambazo zimewekwa kuwa ndio lengo


mama la funga, vile vile funga inasemwa kuwa ni tiba ya mwili
juu ya maradhi mbali mbali yanayoweza kumsumbua
mwanadamu. Baadhi ya wataalamu wa masuala ya afya na
anatomia ya mwanadamu wanasema kuwa; ni jambo ambalo
wangeweza kuwashauri watu wote, kufunga kwa siku hata tano
kila mwezi, ili aweze kuusaidia mwili kupambana na baadhi ya
maradhi na kuusafirisha kutokana na sumu za vyanzo mbali
mbali.

137
Kwa mujibu wa Dokta Eric Berg (DC) mtaalamu wa masuala ya
mfumo wa mmeng‘enyo wa chakula wa mwanadamu, ameeleza
katika Makala yake „My Opinion on Fasting Ramadhan and
Immune system‟ yani „Mtazamo wake juu ya kufunga
mwezi wa Ramadhan na kinga ya mwili‟ alisema; mtu
anapofunga hupelekea kupungua kwa uzalishaji wa cytokines
ambazo hutumika kusafirisha mionzi ya kemikali ndani ya kinga
mwili ya mwanadamu, kemikali ambazo kwa kiasi kikubwa ndizo
husababisha uundwaji wa vivimbe ndani ya mwili.

Dokta Eric akaongeza kuwa; mtu anapofunga kwa kipindi cha


siku kumi hadi thalathini, funga huchochea ongezeko la
uzalishwaji wa macrophages ambazo ni seli zenye uwezo wa
kupambana na kushambulia kwa kasi kubwa aina nyingi za
virusi pamoja na bakteria ndani ya mwili. Ambazo kila jambo au
kitu ambacho kitachochea uzalishaji wa macrophages ndivyo
ambavyo jambo hilo husaidia kwa kiasi kikubwa kinga mwili
kuweza kupambana na vimelea na virusi hatari vinavyoweza
kusababisha maradhi na magonjwa kadhaa ndani ya mwili wa
mwanadamu.

138
Dokta Eric aliongeza kueleza na kufafanua faida nyingi za funga
ikiwa ni pamoja na kuchochea kwa kiasi kikubwa mmeng‘enyo
wa chakula, kupunguza na kuzuia msongo wa mawazo,
kuusaidia mwili kuzalisha vitoa taka mwili (Anti-Oxidants). Elimu
na ujuzi juu ya faida hizi umekuja baada ya maendeleo ya
sayansi na teknolojia, maendeleo ambayo yaliwezesha kufikiwa
kwa kupitia tafiti mbali mbali za kutambua na kuainisha matokeo
ya funga kwa kiumbe hai.

Kutokana na matokeo ya tafiti hizi ambazo zimewezesha


kufahamu juu ya faida mbali mbali za funga, Sayansi inaendelea
kututhibitishia kuwa Qur‘an ipo mbele ya wakati, kwani amri ya
funga kwa waumini ilikuja katika karne ambayo haikuwa rahisi
kujua kwa undani faida na makusudio yake nje ya makusudio
makuu ya kiimani. Matokeo haya yameendelea kuushangaza
ulimwengu na walimwengu wasio amini juu ya Utume wa
Muhammad (Rehma na Amani ziwe juu yake), masuala haya
yakawafanya kujiuliza, iweje Qur‘an katika karne ya saba
iamrishe funga yenye faida hizi zote hali yakuwa wenyewe
hawakujua faida zake.

Kwa hakika ujumbe wa Qur‘an umehakikisha na kuthibitisha


kuwa hayakuwa maneno ya kiumbe yoyote, bali ni elimu ya juu
kutoka kwa Mjuzi wa mambo yote, anaejua kila jambo ambalo
ni manufaa kwa waja wake, basi akawaamrisha kulifanya.
Kutokana na faida za funga kwa wanadamu, Allah (Subhanahu)
kupitia Qur‘an akaifanya iwe ni wajibu kwa kila muumini
139
(isipokuwa walioruhusiwa kwa sharti maalumu) kufunga katika
kipindi maalumu cha mwezi wa Ramadhani, ili wafungaji wapate
faida za kiimani juu ya utekelezaji wa ibada hiyo, bali kupata
faida za kiafya ambazo sayansi ya karne ya ishirini na moja
zimekuja kuzibainisha.

Hivyo hivyo, kutokana na faida nyingi za kiafya zinazopatikana


kutokana na funga, madaktari bingwa wa masuala ya afya ya
mwanadamu wamekuwa wakipendekeza na kuijumuisha funga
katika matibabu yao ya magonjwa mbali mbali. Ukisoma katika
vitabu kadhaa vya afya na mtibabu vya karne ya ishirini na moja
utabaini ujumuishwaji wa njia mbadala ya kufunga
(Intermittent fasting) katika kupambana na magonjwa
mengi sugu.

Baadhi ya watafiti wa masuala ya afya na funga, wanasema


kuwa katika kipindi cha mwezi wa Ramadhani (kipindi cha siku
thalathini) mwili wa mwanadamu hupitia katika hatua tatu
muhimu, Wanasema kuwa katika hatua ya kwanza ambayo ni
kipindi cha siku chache za kwanza za kufunga, funga hupelekea
kiwango cha sukari na kiwango cha shindikizo la damu hushuka
na kuwa la kawaida, hali ambayo huuruhusu mwili kuanza
kujisafisha kutokana na sumu na taka mwili mbali mbali.

Katika hatua ya pili, mfumo wa mmeng‘enyo wa chakula wa


mwanadamu huanza kukubaliana na hali ya kukosa chakula na
vinywaji kwa muda mrefu, hivyo mfumo huo hutumia nishati
iliopo ndani yake kutibu vijeraha vya seli, pamoja na kujisafisha
katika utumbo mpana. Aidha, katika hatua hii, ndio ambayo
baadhi ya viungo vya ndani huanza kujitibu vyenyewe kwa
kutumia uzalishaji wa viinilishe vya ndani kwa njia ya kutoa taka
mwili.

Hatua ya tatu, ambayo mwili hua umepata nguvu ya ziada


kutokana na maboresho na ponya ya seli mbali mbali ambazo
husaidia mwili kupata uwezo na kuongezeka kwa umakini katika
kutekeleza mambo kadhaa. Kadhalika, katika hatua hii, mwili wa

140
mwanadamu hufanya kazi katika kiwango chake cha juu, kiasi
ambacho hata uchovu wa kufunga huondoka moja kwa moja.
Katika kuthibitisha juu ya ufafanuzi huu wa hatua hizi za
mabadiliko katika mwili wa mwandamu yanayoelezewa na
funga, Imekuja katika Sahihi Bukhari kuwa; ((―Alikuwa Nabiy
(Rehma na Amani ziwe juu yake) linapoingia kumi la mwisho la
Ramadhani; alikuwa akikaza shuka lake. (Yani akijibidiisha
katika kutenda mema) na kujiweka mbali za wake zake, na
akihuisha usiku kwa kufanya ibada na akiamsha ahli zake.‖))
Hadithi hii inaweza kutumika kututhibitishia namna ambavyo
mwili hupata nguvu, kuongezeka kwa umakini katika hatua ya
tatu ya kipindi cha funga.

Matokeo ya Sayansi na Sheria ya Unyonyeshaji wa


mtoto (Breastfeeding)
Kwa miongo kadhaa sasa, wasomi, watatifi na madaktari
wakishirikiana na taasisi mbali mbali za kiserikali na zisizo za
kiserikali kwa nyanja zote za kitaifa na zile za kimataifa
zimekuwa zikihimiza na kushajihisha kwa nguvu kubwa juu ya
umuhimu wa unyonyeshaji sahihi wa watoto. Tafiti mbali mbali
zimekuwa zikifanywa kuthibitisha na kubainisha umuhimu wa
kunyonyesha kwa watoto na mama, huku miradi na warsha
kabambe zikipangwa kuhakikisha watoto wanapata lishe sahihi
kwa kipindi maalumu kupitia maziwa ya mama.

141
Juhudi hizi zimekua zikilenga kuhakikisha kuwa mtoto anapata
nafasi adhimu ya kunyonya maziwa halisi ya mama kwa kipindi
ambacho wataalamu wa afya wamekipendekeza. Shirika la Afya
Duniani (WHO) wamekua wakitoa miongozo ya mara kwa mara
juu ya unyonyeshaji sahihi wa watoto huku ikilenga maslahi
mapana ya afya ya mtoto na mama kwa ujumla. Shirika hilo
limekua likitumia njia mbali mbali katika kushajihisha, ikiwamo
kuanzishwa kwa siku maalumu ya unyonyeshaji duniani. Lengo
likiwa ni kuueleza ulimwengu juu ya umuhimu wa
kumnyonyesha mtoto maziwa ya mama kwa kipindi cha miaka
miwili ya mwanzo.

Jitihada hizi zimekuwa zikipata ushindani mkubwa kutokana na


uwepo wa biashara ya maziwa mbadala kwa ajili ya watoto.
Jambo ambalo mara kwa mara limekua likipigiwa kelele na
mashirika mengi duniani kukataa na kutahadharisha juu ya
madhara ambayo huenda yakampata mtoto endapo atakosa
kiwango sahihi cha maziwa halisi ya mama kwa kipindi
kilichowekwa.

Kwa mujibu wa wataalamu na wabobezi wa masuala ya afya ya


mama na mtoto wanashauri na kusisitiza kuwa mtoto anapaswa
kunyonyeshwa (moja kwa moja kutoka katika titi la mama)
pekee bila kupewa chakula chengine chochote, maziwa ya unga
wala juisi za kutengeza kwa kipindi cha miezi sita ya kwanza.
Aidha, wakasisitiza kuwa mtoto anapaswa kuendelea
kunyonyeshwa kwa kipindi chote cha mwaka wa kwanza hata
kama atakuwa na chakula chengine mbadala. Wakaeleza kuwa
sababu kubwa ikiwa ni kwamba; maziwa ya mama yamesheheni
kiwango kikubwa mno cha virutubisho muhimu ambavyo
vinahitajika katika makuzi ya mtoto. Daktari bingwa wa masuala
ya watoto Rebecca Taylar (2022) alinukuliwa na jarida la Afya la
Marekani (WebMD) akisema kuwa maziwa ya mama yanavyo
vimelea muhimu vya kumsaidia mtoto kupambana na virusi na
bakteria hatari kwa afya yake. Kadhalika, ameongeza kusema
kuwa mtoto alienyonya kwa usahihi kwa angalau kipindi cha
miezi sita ya kwanza hupungukiwa kwa asilimia kubwa

142
uwezekano wa kupata pumu na ugonjwa wa mzio (allergies), na
pia hupunguza uwezekano wa mtoto kupata matatizo ya
masikio, mfumo wa upumuaji na kuharisha.

Hivyo hivyo, kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa na mtandao wa


WebMD zimeeleza kuwa watoto walionyonya kwa usahihi
wamekuwa wakihusishwa kuwa na matokeo ya uwezo mkubwa
wa akili na ufahamu katika ukuaji wao, pamoja na kukua
wakiwa na uzito unaolingana na mwili wake, na kuondokana na
tatizo la uzito uliopitiliza. Kubwa zaidi, jarida hilo linaeleza kuwa
watoto walionyonya kikamilifu kwa kiwango kikubwa wamekuwa
na uwezekano mkubwa wa kulindwa na tatizo la vifo vya hafla
vya watoto ambao huitwa SIDS (Sudden Infant Death
Syndrome).

Kwa upande mwengine, WHO (Shirika la Afya Duniani) linaeleza


kuwa unyonyeshaji ulio sahihi hupunguza kwa kiasi kikubwa
uwezekano wa mama kupata saratani ya matiti na saratani ya
mlango wa kizazi. Shirika hilo limeeleza kuwa ongezeko kubwa
la saratani za matiti na shingo ya kizazi duniani limesababishwa
kwa kiasi kikubwa na namna ambavyo wanawake wengi
kukepwa kunyonyesha kwa usahihi, na badala yake kutumia
maziwa mbadala kwa ajili ya watoto wao. Kwa mujibu wa
mtandao wa WebMD wanaeleza faida za kunyonyesha kwa
mama ikiwa ni pamoja na kumsaidia kupunguza uzito
uliosababishwa na mimba kwa haraka zaidi. Wakaongeza
kusema kuwa unyonyeshaji uliosahihi husaidia kurejesha umbile
la kawaida la mfuko wa uzazi kirahisi kuliko njia nyengine
zinazotambulika.

Faida za unyonyeshaji uliosahihi zimekuwa zikielezwa kwa kina


na kwa kutumia tafiti nyingi, huku matokeo chanya ya faida hizo
yakiendelea kuuamsha ulimwengu juu ya mpango sahihi wa
unyonyeshaji. Matokeo yote haya yamekuja kutokana na
maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia ulimwenguni,
kiasi ambacho imewawezesha wasomi kujikita katika kutambua
masuala kadhaa yenye manufaa kwa jamii husika.

143
Ulimwengu wa karne ya ishirini na moja umekuwa ukionekana
kuwa na mwanga mkubwa wa kielimu huku ikionekana bila
kuwa na wataalamu na watafiti hawa, faida nyingi zisingeweza
kuonekana.

Ulimwengu ulichoshindwa kutambua kuwa, elimu zote hizi,


ikiwamo hizi za unyonyashaji zilishaelezwa na kufafanuliwa
katika karne ambayo inaaminika na kuaminishwa kwa jamii
kuwa ilikuwa ni karne ya kiza cha elimu. Qur‘an tukufu
iliyoshushwa kwa Mtume Muhammad (Rehma na Amani ziwe
juu yake) ilishaweka sharia na muongozo juu ya unyonyeshaji
miaka 1400 iliopita. Ilishatoa mwangaza juu ya elimu hiyo
kwakuwa faiza zake zilishatambuliwa kabla ya karne ya ishirini
na moja. Ulimwengu wa karne ya ishirini na moja ulishindwa
kujua kuwa, wanachokiita ugunduzi katika masuala ya
unyonyeshaji, ulishafanyika karne ishirini zilizopita, na kutokana
na ugunduzi huo Qur‘an ikaweka sharti za unyonyeshwaji wa
watoto.

Qur‘an iliweka vipimo sahihi kwa kuhakikisha maslahi mapana


ya mama na mtoto, kwa kuzingatia faida zote ambazo zimekuja
kufafanuliwa na wanasayansi. Allah (Subhanahu) anasema
ndani ya Qur‘an Surat Al-Baqara;
―Na wazazi wanawake wawanyonyeshe watoto wao miaka miwili
kaamili kwa anae taka kutimiza kunyonyesha.‖ (2:233)
Allah (Subhanahu) amesema pia katika Surat Ahqaf;
―Na kuchukua mimba kwake hata kumwachisha ziwa ni miezi
thelathini.‖ (45:15)

Matokeo ya Sayansi katika karne ya ishirini na moja yanaikiri


Qur‘an moja kwa moja, ufafanuzi wa aya hapo juu unadhihirisha
kuwa Qur‘an imetoa muongozo wa kipindi sahihi cha
kunyonyesha mtoto huku mafundisho ya Mtume wa Allah
(Rehma na Amani ziwe juu yake) yakieleza faida zake. Zipo
Hadith nyingi sahihi ambazo zinafundisha juu ya umuhimu wa
maziwa ya mama kwa mtoto pamoja na umuhimu wa mama
kunyonyesha.

144
Baadhi ya wanachuoni wakaeleza kuwa sharti la baba wa mtoto
kumtunza mama mwenye kunyonyesha kwa chakula na mavazi
ni kwasababu ya umuhimu wa kitendo cha kunyonyesha kwa
mama kwa mtoto wake. Mbali na kuwa kunyonyesha
kunamfanya mtoto kuchukua vinasaba kadhaa kutoka kwa
mama huku ikiwa ni njia nzuri ya kutengeneza maingiliano ya
kihisia na kinasaba baina ya mama na mtoto.

Historia zinatueleza kuwa miaka kabla ya kuzaliwa kwa Mtume


Muhammad (Rehma na Amani ziwe juu yake) Waarabu
wakiwapeleka watoto wao mara baada ya kuzaliwa kunyonya
kwa mama mwengine katika vijiji, ili kupata lafuzi nzuri ya lugha
kama ambavyo alipelekwa Mtume wa Allah kwa Mama Halima
na Mama Thuwayba. Hii ndio Qur‘an, huu ndio uongofu kutoka
kwa Allah (Subhanhu)

Qur‟an na Sayansi ya vita vya anga


Kwa mujibu wa mtandao wa Combat Aircraft wa Marekani;
Ndege za Kivita na mashambulizi zinawakilisha baadhi ya
mashine zenye uwezo mkubwa zaidi katika nyanja ya nguvu za
kijeshi kwa sababu ya muundo wao, kasi na silaha. Mnamo
miaka ya 1900 ndio chimbuko la gunduzi la ndege za angani
zilianza kutumika katika vita ya kwanza ya dunia.

(Ndege ya kwanza ya kivita – Kwa Munjibu wa Google)


Ingawaje, katika hatua za awali, ndege zilizokua zikitumika
hazikua kwa ajili vita na mashambulizi badala yake zilikua kwa

145
ajili ya kutoa msaada wa haraka na kusambaza wanajeshi na
vifaa mbali mbali. Kutokana sababu kadhaa za kulinda anga
katika uwanja wa vita, mwaka 1914 ndege maalumu za kivita
zilivumbuliwa. Kwa mujibu wa mtandao huo, matumizi ya ndege
za kivita zilianza kuchepua zaidi katika vita ya pili ya dunia.
Ndipo ndege kadhaa za kivita ziliundwa kwa malengo tofauti,
kama vile kulinda anga, kuongeza mbinu na mikakati ya kivita,
hadi kuwa zana imara ya kukubebea mizinga na mitutu ya
maangamizi.

Gunduzi za ndege za kivita zimekuja kuwa na mapinduzi


makubwa katika uwanja wa vita huku zikibadilisha nidhamu ya
asili ya vita ambayo ilikuwa ni vita ya ardhini. Nidhamu ambayo
ilitumia zaidi vifaa vya ardhini kama vile magari na silaha
nyengine ambazo zilitumika katika nyakati hizo. Historia za
ugunduzi wa ndege za kivita zinatueleza kuwa zilipitia katika
hatua tofauti za maendeleo kutoka katika ndege za kawaida
ambazo zilihitaji muongozaji (rubani) katika miaka ya awali, hadi
kufikia ndege zisizo na muongozaji (rubani) katika karne ya
ishirini na ishirini na moja.

146
(Ndege za kivita zisizo na rubani – Drones)

Hizi zote ni katika neema za elimu ambazo Allah (Subhanahu)


amewaruzuku viumbe. Duru za kielimu zinatufahamisha kuwa
miongoni mwa njia imara sana na yenye ufanisi mkubwa katika
ulinzi ni kuhakikisha ulinzi wa anga unaimarika vyema. Nchi
kadhaa zimekua zikiwekeza kiasi kikubwa cha rasilimali katika
kuhakikisha inalinda mipaka yake katika nyanja zote, lakini
nguvu kubwa imewekwa katika ulinzi wa mipaka ya anga yake.
Mbinu na vifaa kadhaa vimekuwa vikitumika kulinda anga katika
masafa marefu na mafupi huku ndege za kivita zikichukua
sehemu kubwa katika kuhakikisha ulinzi huo. Ndege ambazo
zimewezeshwa kuwa na silaha maalumu kwa ajili ya kulinda na
kushambulia adui kwa ufanisi mkubwa. Matokeo haya ya
kigunduzi katika tasnia ya ulinzi wa anga inayo historia kubwa
ndani ya Qur‘an. Kadhalika, fani na elimu juu ya ulinzi wa anga
kutumia ndege za kivita inayo ufafanuzi wake katika kutumika
miaka 1400 iliyopita.

Mnamo miaka ya 571 A.D kulitokea bwana mmoja akiitwa


Abraha ambae alijenga hekalu lake na kuwataka watu wote
katika jamii ya waarabu waache kuzuru nyumba ya Allah
(Subhanahu) ‗Al-Kaaba‘ na badala yake wote waende kuzuru
hekalu lake katika Nchi ya Yemen. Alitokea bwana mmoja katika
147
jamii ya Waarabu wa Makka aliamua kuenda Yemen na
kulichafua hekalu la bwana Abraha kwa kinyesi na kisha kurudi
Makka.

Baada ya Abraha kufikiwa na taarifa kuwa mmoja katika watu


wa Makka amefanya tukio hilo, alikasirika na kuandaa jeshi
kubwa sana ambalo lilitumia ndovu (tembo) kwa ajili ya
kuishambulia Makka na kulivunja Al-Kaaba. Wanachuoni wa
Sera (historia) wanatueleza kuwa walipokaribia mji mtukufu wa
Makka, wale wanyama wao (tembo) waligoma kuingia ndani ya
mji wa Makka. Wapo miongoni mwa wanajeshi wa Abraha walio
amua kurudi nyuma na wapo ambao waliwalazimisha tembo
kuingia ndani ya mji wa Makka.

Wanajeshi ambao waliendelea na kuwalazimisha ndovu waingie


Makka, walianza kuona makundi makubwa ya ndege
yakiwasogelea, tahamaki wakidondokewa na vijiwe vyenye moto
ambavyo viliachiwa na ndege wale kutoka katika miguu yao na
midomo yao, juu ya vichwa vyao. Historia inatueleza kuwa kila
aliyedondokewa na kijiwe hicho alijeruhiwa kana kwamba
mabaki ya kitu kilicho tafunwa na kutemwa (mass destruction).

Historia ya Abraha na jeshi lake la tembo, limefafanuliwa ndani


ya Qur‘an kupitia Surat Al-Fil. Surah ambayo ilikuja kuubanishia
ulimwengu wa ulinzi wa kijeshi kuwa upo uwezekano wa

148
kutumia zana za ulinzi za anga kupigana na adui mwenye zana
nzito za ardhini. Abraha alimiki wanajeshi na akamiliki wanyama
wakubwa na wenye nguvu. Lakini Allah (Subhanahu) akatumia
mbinu ya anga kwa kuwatumia wanyama wadogo (ndege)
wakiwa na silaza nzito za maangamizi.
Allah (Subhanahu) anasema ndani ya Surat Al-Fil;
‖Kwani hukuona jinsi Mola wako Mlezi alivyowatenda wale
wenye tembo? Kwani hakujaalia vitimbi vyao kuharibika? Na
akawapelekea ndege makundi kwa makundi. Wakiwatumia
mawe ya udongo wa motoni, Akawafanya kama majani
yaliyoliwa na kutemwa? (105:1-5)

Sayansi inauaminisha ulimwengu kuwa ndege za kwanza za


kivita pamoja na mbinu za mashambulizi ya anga zilianza miaka
ya tisini katika vita ya pili ya dunia. Ingawaje Qur‘an
inathibitisha kuwa mbinu na zana hizo zilishatumika kabla, na
elimu juu ya matumizi yake zilishaelezwa katika karne ya saba.
Wafasiri wa Qur‘an wamefafanua kwa mitazamo mbali mbali juu
ya tukio hili, huku wakiwaelezea aina ya ndege na namna
ambavyo walivamia jeshi la tembo.

Ibn Kathir (Rehma za Allah ziwe juu yake) amesema katika


tafsiri yake akiwanukuu Ibn Abbas na Ad-Dahhak wakisema juu
ya kauli ya Allah (Subhanahu) “Makundi kwa makundi”
wamesema kuwa maana yake ni ndege waliojipanga, kundi
moja likifuatiwa na kundi jengine. Mujahid amenukuliwa
akisema kuwa maana ya kauli hiyo ya Allah (Subhanahu) ni
kuwa ndege hao walikuja katika makundi tofauti yenye
kupishana. Ibn Zayd akasema kuwa maana yake ni kuwa ndege
hao walikuwa wakija katika makundi tofauti, kundi moja
likitokea upande huu na kundi jengine likitokea upande
mwengine.

Tafsiri zote hizi zinathibitisha namna ambavyo hata ndege za


kivita ambavyo hutumia nidhamu ya kushambulia zikiwa katika
makundi maalumu na mpangilio maalumu.

149
(Ndege za kivita zikiwa zimefatana katika kikundi)

(Aina nyengine ya kikundi cha ndege za kivita)

Surat Al-Fil pia imeeleza namna ambavyo ndege hao


walivyoshambulia jeshi la ndovu. Kama ilivyokuja kuwa;
“Wakiwatumia mawe ya udongo wa motoni” Ibn Kathir
(Rehma za Allah ziwe juu yake) amesema katika tafsiri yake;
Allah (Subhanahu) alipotaka kuwashambulia watu wa ndovu
aliwatuma ndege juu yao wakiwa wanatokea baharini. Kila
ndege mmoja alibeba vijiwe katika miguu yao na kimoja katika
midomo yao. Unaweza kuona kuwa sayansi ya ulinzi wa anga
haukuweza kuacha kuikiri Qur‘an kwa namna ambavyo hutumia
nidhamu mbali mbali zilizomo ndani yake.

150
Qur‘an inathibitisha kuwa ndege walioshambulia jeshi la ndovu
walitokea baharini. Tunawezaje kupingana na hili wakati mara
nyingi tunashuhudia kwenye mitandao tukiona mipango kadhaa
ya kivita kutumia ndege zikianzia kwenye manuari ya kijeshi
baharini na kuelekea katika uwanja wa vita.

Kadhalika, Qur‘an imeeleza pia, ndege waliotumwa kushambulia


jeshi la ndofu walibeba vijiwe vya moto katika miguu yao miwili
na kwenye midomo yao. Kama ilivyokuja ndani ya Surat Al-Fil;
“Wakiwatumia mawe ya udongo wa motoni” vijiwe
ambavyo waliwalenga maadui, vimethibitishwa kuwa ni vijiwe
vya moto ambavyo vilitumika kama silaha za kuwaangamiza
maadui. Qur‘an imethibitisha pia kuwa kila ambae aliangukiwa
na kijiwe hicho kilimuangamiza na kumfanya kama majani
yaliyoliwa na kutemwa.

151
Tunafahamu namna ambavyo ndege za kivita zinavyotumika
kushambulia, zote husafiri kuelekea kwenye uwanja wa vita kwa
kasi sana huku zikiwa zimebeba silaha hatari katika tumbo la
ndege hizo. Hutumia kifaa maalumu kuachia na kurusha silaha
hizo katika eneo kusudiwa.

(Ndege za kivita zikiwa zimebeba makombora kwenye tumbo la


ndege)

152
(Ndege za kivita zikishambulia kwa kurusha makombora)

Kwa hakika hii Qur‘an ni kitabu cha mazingatio, ni neema kwa


wenye kutafakari. Allah (Subhanahu) amesema ndani ya Surat
Al-Baqara;
―Hiki ni KItabu kisichokuwa na shaka ndani yake; ni uongofu
kwa wachamungu‖ (02:02)
Tumuombe Allah (Subhanahu) aturudhuku mazingatio
yanayopatikana ndani ya Qur‘an ili tuufikie uchamungu wa
kweli.

Qur‟an na Sayansi ndani ya Tetemeko la Ardhi


Kwa mujibu wa wataalamu wa jeolojia (taaluma ya ardhi)
pamoja na machapisho mbali mbali ya kitafiti yanasema kuwa
ardhi pamoja na mgawanyiko wake wa mabara tofauti, asili
yake ni pande moja la ardhi. Ardhi ambayo kutokana na nguvu
za asili ambazo zilizalisha mvutano, na kisha kupelekea
mtetemeko ambao uliigawa ardhi katika matabaka makuu
ambayo kwa sasa ndiyo yanayoitwa mabara.

153
Hivyo, kwa mujibu wa wataalamu hao, chanzo kikuu cha
mgawanyiko wa mabara ni tetemeko kubwa la ardhi ambalo
lilitokana na nguvu za asili, ambapo matokeo ya tetemeko hilo
ikaigawa ardhi katika mapande kadhaa ambayo baadae mipaka
ya nchi mbali mbali iliundwa, ambazo kwakutumia mgawanyiko
huo zilitambulika na kutofautishwa na nchi nyengine.
Kwa mujibu wa mtandao wa California Academy of Science
kupitia jarida lake la Plate Tectonics: Shaping the
Continents (2019) wanasema kuwa kwa takribani miaka
bilioni moja, dunia imekua ikiendelea kubadilika kutokana na
mzunguko wa sahani ya dunia ambayo huzunguka na kuigawa
katika matabaka tofuti kwa mujibu wa nguvu ya asili. Mzunguko
huo wa sahani ya dunia ulianza kwa kuigawa ardhi ya dunia
katika bara moja kubwa ambalo lilizungukwa na bahari moja
kuu. Kwa mujibu wa jarida hilo wanasema kuwa baada ya miaka
150, bara hilo kubwa likaendelea kugawika na kuigawa bahari
katika mabara mengine tofauti ambayo yote yalitokana na
mtetemeko wa ardhi.

154
Wataalumu wa masuala ya jolojia wanasema kuwa chanzo kikuu
cha tetemeko la ardhi ni nguvu ya asili ambayo hutokana na
msuguano na msigano wa miamba chini ya ardhi, pale ambapo
muhimili wa ardhi unaposhindwa kuzuia mgandamizo huo, ndipo
hutokea mpasuko na msigano wa sahani ya ardhi na kuzalisha
mtetemeko.
Sayansi inathibitisha kuwa msuguano na msigano wa miamba
ya chini ya ardhi husababisha mtetemeko wa sehemu ya juu ya
ardhi pamoja na mpasuko na uharibifu mwengine kulingana na
kiasi cha mtetemeko huo. Jambo ambalo si katika ugunduzi wa
kushangaza katika jicho la Qur‘an, kwani Allah (Subhanahu)
anasema ndani ya Qur‘an;
―Na ameweka katika ardhi milima ili ardhi isikuyumbisheni.‖
(31:10)
Tunatambua kuwa milimia imefanywa kama ni vigingi yenye
mashina chini ya ardhi ambayo kazi yake kubwa ni kuifanya
ardhi kuwa tulivu na kuhimili misuguano ya miamba chini yake.
Ahadi ya Allah (Subhanahu) juu ya kuifanya milima kuwa ni
mihimili ya ardhi haiwezi kuwa sababu ya kuzuia matetemeko
ambayo yamekadiriwa kutokea na Muumba ambae ameifanya
milima hiyo kuwa mihimi yake.

Wakati karne ya ishirini na moja ikisemwa kuwa ndio karne ya


sayansi na teknolojia, wanasayansi wanakiri kuwa hadi sasa
hakuna kifaa wala teknolojia ambayo humuezesha mwanadamu
kutambua na kutabiri tetemeko la ardhi kuwa litatokea lini na
katika eneo gani. Jambo ambalo bado linaifanya Qur‘an
kuendelea kuwashangaza wanasayansi, kwani katika karne ya
saba, karne iliyoitwa ya kiza cha elimu ilishaeleza juu ya
tetemeko kubwa ambalo litatokea na kusababisha maafa na
madhara makubwa. Tetemeko ambalo litaifanya ardhi
kutingishika kutokana na kushindwa kuhimili msuguano na
msigano mkubwa wa miamba (Vigingi vya milima).

155
Allah (Subhanahu) anasema ndani ya Surat Az-Zalzala;
―Itakapo tetemeshwa ardhi kwa mtetemeko wake! Na
itakapotoa ardhi mizigo yake!‖ (99:1-2)
Ibn Kathir (Rehma za Allah ziwe juu yake) amefafanua juu ya
tetemeko lililotajwa ndani ya aya hiyo na kusema kuwa hilo ni
tetemeko la mwisho ambalo litaikumba dunia na viumbe kwa
ujumla. Aidha, ameendelea kueleza kuhusu kauli ya Allah
(Subhanahu) “Na itakapotoa ardhi mizigo yake” amesema
kuwa maana yake ni matokeo ya mtetemeko huo ambao
utawatoa maiti na kila kilichozikwa ndani ya tumbo la ardhi.
Qur‘an imelielezea tukio hilo pia katika Surat Al-Hajj na kulitaja
kama ni tukio la hatari na kuogofya kama ilivyokuja;
―Enyi watu! Mcheni Mola wenu Mlezi. Hakika tetemeko la saa
(Kiyama) ni jambo kuu.‖ (22:1)
Allah (Subhanahu) akasema juu ya matokeo ya tetemeko hilo
kuwa;
―Siku mtapo liona (tetemeko), kila mwenye kunyonyesha
atamsahau amnyonyeshae, na kila mwenye mimba ataharibu
mimba yake. Na utaona watu wamelewa, na kumbe
hawakulewa. Lakini adhabu ya Allah ni kali.‖ (22:2)
Imam Al-Fawzan (Allah amhifadhi) wakati akilolea ufafanuzi juu
ya aya zilizoelezea habari ya tetemeko alisema kuwa; Kauli ya
Allah (Subhanahu) juu ya tetemko hilo, inaelezea kile
kitakachotokea wakati wa tukio la Kiyama, ardhi itatetemeka,
itapasuka na kuangusha mapande mapande, na kutengeneza
nyufa zilizo wazi. Mtetemeko huo utaonekana kwa vishindo
vyake na ardhi kukosa utulivu uliozoeleka. Kadhalika, kuhusu
ardhi kutoa mizigo yake, Imam Al-Fawzan (Allah amhifadhi)
amesema kuwa; ardhi itatoa kila kilichomo ndani ya yake
ikiwamo miili ya wafu na mali (madini) yote yaliomo ndani yake.
Historia za matetemeko ya ardhi duniani inatueleza kuwa tukio
la kwanza la tetemeko ambalo lilishangaza dunia lilitokea
mnamo mwaka 1831 kwa mujibu mtandao wa „Science for

156
Changing World‟ ambao kwa kutumia tafiti kadhaa
zilizowezeshwa na vifaa vya kisasa, waliweza kutambua na
kusoma historia za matetemeko. Kadhalika matokeo kadhaa ya
misuguano ya ardhi yanaonekana katika mgongo wa ardhi. Hivi
karibuni tumeshuhudia mpasuko mkubwa katika bonde la ufa
ambalo unagawa baadhi ya nchi za Afrika mashariki kama vile
Kenya, Tanzania, Uganda na Burundi ukiendelea kutanuka huku
wanasayansi wakisema kuwa ni matokeo ya msuguano wa
ardhi.

157
Hizi zote ni sehemu na mifano wa matokeo ya matetemeko
ambayo yameelezwa ndani ya Qur‘an. Mbali na matukio kadhaa
wa kadhaa ya matetemeko ambayo tunayashuhudia katika
kipindi cha sasa, huku matetemeko hayo yakiacha athari kubwa
za mali na kugharimu uhai wa viumbe wengine. Kila nukta
katika maisha juu ya mgongo wa ardhi ni sehemu ya mazingatio
na funzo ambalo kiumbe hupaswa kujipa tahadhari juu ya
uwepo na ukuu wa Allah (Subhanahu). Matokeo yaliyofafanuliwa
ndani ya Qur‘an karne ya saba kisha sayansi kuja kuyakiri baada
ya karne ishirini kupita, pia ni sehemu ya mazingatio ambayo
kila mwanadamu anapaswa kuzingatia na kuchukua faida ndani
yake.
Qur‟an na Sayansi ya Mwisho wa Ulimwengu (The Big
Crunch Theory)
Sayansi, pamoja na wanasayansi wanakiri na kukubali kuwa
ulimwengu na vilimwengu vyote viliumbwa, kinyume na
mitazamo na dhana zao za awali kuwa ulimwengu ulitokea
kutokana na uoto wa asili usio na muumba wala mwenye
kuusimamia. Kwa mujibu wa tafiti na mijadala ya muda mrefu
ambayo ilionekana kukataa ukweli juu ya umbwaji wa
ulimwengu. Matokeo ya tafiti na mijadala hiyo ikazalisha dhana
maarufu Big Bang ambayo inakubalika na kundi kubwa la
wanasayansi wa karne ya ishirini na ishirini na moja, haswa wale
wabobezi wa masuala ya anga za mbali.
Dhana hiyo inayothibitisha (kwa mitazao ya kisayansi) kuwa
ulimwengu uliumbwa kutoka katika asili ya umbile moja la gesi
mgando, ambayo baada ya kutokea mripuko mkubwa (The Big
Bang) ukalitenganisha umbile hilo na kupatikana mgawanyiko
wa ardhi na mbingu, na baina ya hivyo zikawepo nyota, sayari
na maumbile mengine ambayo yamejenga ulimwengu (The
Galaxy). Dhana hii ikawa ni matokeo makubwa ya kuufahamu
ulimwengu na asili yake, ambayo yalipatikana karne kumi na
nne baada ya kushushwa kwa Qur‘an tukufu. Qur‘an ambayo
ndiyo iliyowafungua macho na maono ya kuweza kuifahamu asili
ya uhakika ya kuumbwa kwa ulimwengu.

158
Allah (Subhanahu) katika karne ya saba, alifafanua masuala
yote ya kuumbwa kwa ulimwengu, huku akieleza kwa kina juu
ya hicho ambacho kimeitwa mripuko mkubwa (The Big Bang)
wakati ambao wanasayansi hawakua na elimu yoyote kuhusu
habari hizo. Allah (Subhanahu) akasema ndani ya Qur‘an kuwa;
―Je! Hao walio kufuru hawakuona kwamba mbingu na ardhi
zilikuwa zimeambatana, kisha Sisi tukazibabadua? Na tukajaalia
kutokana na maji kila kitu kuwa hai? Basi je, hawaamini?
(21:30)
Allah (Subhanahu) amesema pia;
―Na Yeye ndiye aliye umba usiku na mchana na jua na mwezi,
vyote katika anga vinaogelea katika mihimili yake‖ (21:33)
Kutokana na uthibitisho wa Qur‘an juu ya kuumbwa kwa
ulimwengu katika maumbile ya ardhi na mbingu, ndiyo ambayo
yaliwafanya baadhi ya wanasayansi kukata shauri na kukiri kuwa
Qur‘an ndio kitabu pekee ambacho kimezungumzia kwa kina juu
ya asili ya kuumbwa kwa ulimwengu. Baada ya Qur‘an
kuwathibitishia hilo, sambamba na matokeo ya sayansi yao,
likazuka suali kubwa na lenye mjadala kuhusu mwisho wa
ulimwengu.

Wanasayansi wa masuala ya anga kwa muda mrefu wamekuwa


wakipinga juu ya habari zote zilizomo ndani ya Qur‘an zinazo
zungumzia mwisho wa ulimwengu (kiyama). Wapo baadhi
ambao waliamini kuwa baada ya mripuko mkubwa (The big
Bang) hakutakuwa na uwezekano wa tukio lolote jengine
ambalo litaweza kuuvunja ulimwengu. Wakati dhana hizo
zikiendelea kukuwa ndani ya vichwa vya wasomi na watafiti wa
kisayansi, Qur‘an katika karne ya saba ikawa imeshafafanua juu
ya tukio kubwa ambalo litaashiria na kusababisha kuvunjika
vunjika kwa ulimwengu.

Allah (Subhanahu) amesema ndani ya Surat Al-Qasas;


―Kila kitu (kilichopo ndani ya ulimwengu) kitaangamia,
isipokua Yeye.‖ (28:88)

159
Allah (Subhanahu) amesema pia ndani ya Surat Al-Rahman;
―Kila kilioko juu yake kitatoweka. Na atabaki Mwenyewe Mola
wako Mlezi Mwenye utukufu na ukarimu. (55:26-27)

Kauli zote hizi zinathibitisha pasi na shaka yoyote kuwa


ulimwengu na vitu vyote vilivyomo ndani yake vitaondoka na
kuharibiwa kabisa. Wafasiri wa Qur‘an wamefafanua kauli za
Allah (Subhanahu) kuhusu „Kutoweka na Kuangamia‟
wakasema kuwa maana yake ni kuwa, kila kitu kilichoumbwa na
Allah (Subhanahu) wakiwemo viumbe (wanadamu, majini, na
wanyama) watakufa na kupotea kabisa, na kisha maumbile yote
mengine ya ulimwengu yataharibiwa na matokeo kadhaa
ambayo yatatokea siku ya kiyama kama ilivyokuja ndani ya
Surat Az-Zumar;
―Na litapulizwa baragumu, wazimie waliomo mbinguni na
waliomo katika ardhi, isipo kuwa aliye mtaka Allah. Kisha
litapulizwa tena mara nyengine. Hapo watainuka wawe
wanangojea. (39:68)

Ibn Kathir (Rehma za Allah ziwe juu yake) amesema akiifafanua


aya hii kuwa; baragumu (sauti kali) litapulizwa na viumbe wote
walioko katika ardhi na wale walioko mbinguni watakufa na
atabakia yule ambae ametaka abaki (Malaika wa Mauti) ambae
nae atakufa na kubakia Allah (Subhanahu) pekee, Mwenye
kudumu milele ambae Mwenye mwanzo na asiye kuwa na
mwisho. Na hapo atasema kuulizwa ulimwengu; ((Ni nani
Mfalme wa siku ya leo? Kisha atajibu kuwa; ni Allah
(Subhanahu) pekee, Mwenye kutiisha kila kitu, na Naamrisha
kila kitu kiwe ndiyo mwisho.))

Kutokana na ufafanuzi huu, Qur‘an imethibitisha kuwa


ulimwengu utakuwa na mwisho, na mwisho wake utakuja
kutokana na mpasuko mkubwa wa sauti ya baragumu ambayo
tumeifafanua hapo juu. Maelezo haya alifundishwa na Mtume
wa Allah (Rehma na Amani ziwe juu yake) miaka takribani elfu
moja mia nne iliyopita, huku ikiwaacha wanasayansi na kibarua
kipevu cha kuweza kuyatafiti na kuyaweka katika dhana zao.

160
Wanasayansi hawakuacha kuendelea kufanya tafiti mbali mbali
za kuthibitisha mwisho wa ulimwengu (kutoka na mitazamo yao)
huku vifaa kadhaa vikiundwa kusaidia uchunguzi wa mwenendo
wa ulimwengu. Hata hivyo, duru za kihistoria za kisayansi
zinathibitisha kuwa upo uwezekano kwa ulimwengu ambao
uliumbwa na kuanzisha kwa mripuko mkubwa (The big Bang)
kuwa utamalizika kama ambavyo ulianza. Walichoshindwa kujua
ni kwa namna gani jambo hilo litatokea.

Mnamo mwaka 2003, mwanasayansi maarifu wa masuala ya


anga Dokta Jennifer Bigman alikuja na nadharia yake ambayo
aliita ‗The Big Crunch‘ na kuichapisha katika kitabu chake
akisema kuwa; tafiti zimethibitisha kuwa lipo tukio ambalo
litasababisha msagiko na kuvunjika vunjika kwa ulimwengu na
maumbile yote, na kuuwacha ukiwa na kijiumbile kidogo chenye
wastani wa punje ndogo isiyokamatika wala kuonekana kwa
macho.

Kwa mujibu wa Dokta Jennifer (2003) anaeleza kuwa ‗The big


Crunch‘ ni nadharia ambayo inathibitisha kuwa ulimwengu na
vyote vilivyomo vitaharibiwa na msagiko mkubwa ambao
umezalishwa na hatua na muendelezo wa utanukaji wa sayari ya
dunia. Mwaka 2008 mwanasayansi mwengine kutoka Chuo cha
Stanford alieleza akisisitiza juu ya tukio la msagiko wa
ulimwengu kupitia kitabu chake alichokiita „Introduction to
Cosmology‟, Dokta Gerry Hishaw alisema kuwa; kutokana na
asili ya ulimwengu kuumbwa kutokana na mripuko uliomkubwa,
tafiti zinaeleza na kuashiria kuwa upo uwezekano wa maumbile
yote yaliyozalishwa na mripuko huo kurudi katika asili yake ya
awali ya kuwa pande moja na kisha kusagika na kupotea kabisa.
Gerry (2008) akaeleza kuwa zile hatua zote ambazo zilipitia
katika kuumbwa ulimwengu kutoka katika umbile moja zitarudi
kwenye asili yake na kisha kusababisha nguvu ya mvutano na
mtanuko ambayo italipasua na kulisaga umbile hilo na kuwa ni
vumbi jembamba lenye kutawanyika.

161
Kwa wafuatiliaji wa Qur‘an, wanaweza kuthibitisha kuwa kila
kitu katika fafanuzi za wasomi hawa zilishabainishwa ndani ya
Qur‘an karne kadhaa hapo nyuma. Qur‘an imeelezea mpasuko
na msagiko huu kwa kina kupitia sura mbali mbali, huku
ikibainisha kwa namna tofauti ya matukio ambayo yanaendana
moja kwa moja na matokeo ya gunduzi za big crunch. Allah
(Subhanahu) amesema ndani ya Surat Al-Inshiqaq;
―Mbingu itakapo chanika. Na ikamsikiliza Mola wake Mlezi, na
ikapaswa kumsikiliza. Na ardhi itakapo tanuliwa.‖ (84:1-3)
Akasema pia Allah (Subhanahu) ndani ya Surat At-Takwir;
―Jua litakapo kunjwa kunywa. Na nyota zikazimwa. Na milima
ikaondolewa. (81:1-3)
Kadhalika, Allah (Subhanahu) amesema ndani ya Surat Al-
Infitar;
―Mbingu itakapo chanika. Na nyota zitapo tawanyika. Na habari
zitakapo pasuliwa.‖ (82:1-3)

Ingawaje, watafiti na wasomi hawa iliwachukua miaka na karne


kadhaa kuweza kuthibitisha katika mlengo wa kisayansi juu ya
uhakika wa kuisha kwa ulimwengu, Qur‘an ikawa ndio rejea za
uhakika kuhusu kubainisha juu ya tukio hilo. Ufafanuzi huu wa
Qur‘an ndio ambao siku zote umekuwa ukiwaleta wanasayansi
karibu zaidi na kuamini juu ya ukweli wa ujumbe wa Allah
(Subhanahu) kwa Mtume wake. Aidha, Qur‘an ikiwa ndio kigezo
cha kupima matokeo mengi ya kisayansi ambayo
wameyavumbua katika tafiti zao. Majibu na fafanuzi hizi za
Qur‘an kuhusu mwisho wa ulimwengu ndizo ambazo zilimuibua
Dokta Morrison kusema kuwa;
―Kutokana na namna ambavyo ulimwengu umeumbwa, na
namna ambavyo umepangiliwa kwa utaratibu wake juu ya kila
kitu. Kuanzia asili ya kuumbwa kwake, maendeleo yake na
harakati zote za maumbile ya ulimwengu, bila shaka yoyote,
yupo muumba ambae anausimamia kuanzia kuanzishwa kwake
hadi mwisho wa muda wake.‖
―Allah ndiye Muumba wa kila kitu, na Yeye ndiye Mlinzi juu ya
kila kitu.‖ (39:62)

162
HITIMISHO

Ushusho wa Qur‘an umekuja kuwa ni Rehma katika ulimwengu


kupitia kwa Mtume wa Allah (Sala na Amani ziwe juu yake).
Imefanywa kuwa ni nyenzo adhimu kwake katika kuufundisha
Umma juu ya misingi mbali mbali ya maisha katika nyanja zote,
Kiimani, Kielimu, kimazingira, na nyanja zote muhimu ambazo
zitamfanyia mwanadamu wepesi wa kuishi, kutenda, na
kutekeleza miamala mengi mengine. Qur‘an imefanywa kuwa ni
dira imara ambayo kila kiumbe ndani ya ulimwengu huihitaji ili
kustawisha Imani na maisha yake kwa ujumla.
Qur‘an imeshushwa kuja kuwa ni ufunguo wa zama mpya za
elimu. Haikuacha kufundisha na kutoa mwangaza wa kielimu juu
ya masuala yote ambayo yanahitajika na viumbe, kuanzia
kuumbwa kwao, kukua, chakula, biashara, pamoja na harakati
mbali mbali ambazo viumbe hupitia hadi kufikia katika hatua
yake ya mwisho ndani ya ulimwengu. Kutokana na ukweli
kwamba Qur‘an ndio kitabu pekee chenye kuzingatia na
kubainisha masuala yote yamhusuyo mwanadamu na mienendo
yake, haikuwa ajabu kuona kuwa kwa karne kadhaa zilizopita
hadi sasa Qur‘an imeendelea kuwa na wapinzani wakubwa.
Tunaendelea kushuhudia matukio kadhaa yanyoashiria au
kuonyesha upinzani juu ya ujumbe uliopo ndani ya Qur‘an, huku
baadhi yao wakiahidi kutumia maisha yao, fedha, na rasilimali
mbali mbali kwa lengo la kubainisha mapungufu yaliyopo ndani
yake. Haidhuru, juhudi hizo zimekuwa zikigonga mwamba
kwakuwa hiki ni kitabu kisicho na shaka ndani yake. Kutokana
na matokeo ya kushindwa kubaini au kuonyesha mapungufu
yoyote yaliyomo ndani ya Qur‘an, watafiti na wanasayansi
kadhaa wakaamua kuitumia katika kuyatafiti mambo mazito
ambayo yamebainisha ndani yake. Mbali na maendeleo
makubwa ya kitafiti yaliopo ndani ya karne ya ishirini na moja,
bado wanasayansi hao wanakiri kuwa Qur‘an ndio kitabu pekee
ambacho kimeeleza masuala mengi ambayo yanahitaji elimu na
ujuzi mkubwa wa kisayansi ili kuweza kuyaelewa.

163
Wasomi na watafiti mbali mbali wa masula ya vitabu vya kale
wanakiri kuwa Qur‘an ndio kitabu pekee ambacho kimekuwa
kikitoa changamoto zisizoweza kujibika kwa viumbe, kisha kutoa
majibu na kubainisha udhaifu mkubwa wa viumbe hao. Kama
hivyo ndivyo, tunapaswa kuisoma Qur‘an kwa mazingatio,
tujifunze na kukimbilia kupata faida zilizomo ndani yake. Hakika
hii ni nuru ambayo Umma wa Kiislamu umeachiwa na kiongozi
mtukufu, na Qur‘an ndio ukamilifu wa dini na mfumo mzima wa
maisha ya mwanadamu.
Qur‘an ndio kitabu kinachorejewa zaidi duniani katika masuala
mbali mbali yanapotatiza vichwa vya wasomi. Tunaona namna
ambavyo Qur‘an imetumika kuwezesha masuala kadhaa ya
kisayansi katika fani mbali mbali kama vile fani za kitabibu,
anga, na mengine lukuki ambayo tunapaswa kuyasoma na
kuyazingatia. Kitabu hiki, kimeeleza kwa kiasi namna ambavyo
Qur‘an imekua mbele ya wakati katika masuala mbali mbali, ili
iwe ni ujumbe kwa jamii na ulimwengu kwa ujumla. Kila
mwenye akili atafakari, kila mwenye macho aone na kila
mwenye kusikia, asikie na kuitangaza elimu na miongozo juu ya
Qur‘an.
Kitabu hiki kimegusa kwa kiwango kidogo sana juu ya
uthibitisho wa sayansi na teknolojia ndani ya Qur‘an, hakika hizi
ni miongoni mwa fursa ambazo kila mwenye nafasi anapaswa
kuziunga mkono kwa hali na mali ili jamii ifaidike na kuelimika
katika kuijua Qur‘an. Hii ni sehemu yetu katika kutekeleza
wajibu wetu wa kuifunza Qur‘an. Haya yote ni neema za Allah
(Subhanahu) kuturuzuku afya na uhai wa kukamilisha kitabu
hiki. Elimu ni bahari kila mmoja huogelea kwa kiwango chake
alichojaaliwa na Allah (Subhanahu) na „HAYA NDIO QUR‟AN
IMENIFUNZA‟

164
REJEA ZA KITABU:

Tafseer Ibn Katheer: Tafseer Al-Qur‘an


Tafseer Al-Kurtubi: Tafseer Al-Qur‘an
Tafseer A‘Saad: Tafseer Al-Qur‘an
The bible, The Qur‟an and Science: The Holy Scriptures
Examined in The light of Modern knowledge (2004) by Dr.
Mourice Bucaille.
The perfect guide to the science of the Qur‟an: by Imam
Al-Suyuti, translated by Munir Fareed (2000)
The Qur‟an and Modern Science: Compatible or
Incompatibe, by Dr. Zakir Naik (2007)
Oceanography: An Invitation to Marine Science, by Tom
Garrison (2016)
The Unchallangable Miracles of the Qur‟an: The facts that
can‘t be deniel by science, by Yusuf Al-Had Ahmad (2016)
Why Islam? Proofs of modern science, by Dr. Nabil A. Haroun
(2003).
The devil Deceptions (Talbis Iblis): Sufis and Music, by
Imam Ibn Jawz
Does music influence people? Documentary by Amrwaked
Delves, 2022 (Aljazeera English)
My Opinion on Fasting Ramadhan and Immune System,
Documentary by Dr. Eric Berg (DC), 2022 (Youtube)

165

You might also like