Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 1

TANZANIA ASSEMBLIES OF GOD KIMARA

MAOMBI YA KANISA 31/12/2023 - 7/1/2024


1. OMBA REHEMA: [Zaburi 130:3-4]
- Mshukuru Mungu kwa sababu ya wingi wa rehema, neema, uvumilivu, msamaha na uponyaji wake
kwetu kibinafsi, familia, kanisa pamoja na taifa letu kwa mwaka mzima.
- Omba roho ya hofu na kumcha Mungu kwa watu wote tunapouelekea mwaka mwingine.
- Ombea na Kataa roho ya uasi na machukizo ya namna zote.
2. MSHUKURU MUNGU KWA MAISHA YA ROHONI: [ Zaburi 23:3]
- Mshukuru Mungu kwa ajili ya uzima na afya ya rohoni
- Mshukuru Mungu kwa ajili ya kila kazi njema ya Roho mtakatifu ndani yetu katika kutufanya
imara maongozi ,kudumu na kuendelea ktk neema ya wokovu.
3. MSHUKURU MUNGU KWA AFYA NA UPONYAJI : [ wagalatia 2:20]
- Mshukuru Mungu kwa ajili ya uzima, afya njema na uponyaji wake juu ya miili yetu, familia,
jamaa pamoja na kanisa tulipokua wagonjwa.
4. MSHUKURU MUNGU KWA AJILI YA UPATIKANAJI WA MAHITAJI
MBALIMBALI:
[ Mathayo 6:26]
- Mshukuru Mungu kwa ajili ya baraka zake juu ya kazi ya mikono yetu.
- Mshukuru Mungu kwa ajili ya chakula mavazi malazi
- Mshukuru Mungu kwa Uwezo wa kujiendesha kimaisha sambamba na ufikiwaji wa gharama
mbalimbali za kimaisha na familia.
- Mshukuru Mungu kwa ajili ya uwezeshaji wake kwa wazazi katika majukumu yao juu ya familia
zao
5. MSHUKURU MUNGU KWA AJILI YA HUDUMA MBALIMBALI ZILIZO FANYIKA
KATIKA KANISA:
[1kor 12:11]
- Mshukuru Mungu kwa utendaji wa huduma zote zilizo tendeka kanisani, ibada , Uimbaji, na
Mkutano mbalimbali
- Mshukuru kwa ajili ya watenda kazi wote katika kanisa letu, kwa kujitoa kwao katika huduma
mbalimbali, wa Chungaji, Wazee wa kanisa, Mashemasi, pamoja na vikundi vyote vya uimbaji.
- Mshukuru Mungu kwa ulinzi na uponyaji wa Taifa letu.
Kutoka [33: 13-15]- Jiweke wakfu kibnafsi, familia, na kanisa kwa ajili ya mwaka unaokuja uwepo
wa Bwana uende pamoja nasi.

You might also like