Nursery & Primary School: Standard Seven Test 2021 Elimu Ya Dini Ya Kiislamu / Muda: 1:30

You might also like

Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 4

KINYEREZI ISLAMIC SCHOOLS

NURSERY & PRIMARY SCHOOL


ARABIC & ENGLISH MEDIUM
STANDARD SEVEN TEST 2021
ELIMU YA DINI YA KIISLAMU / MUDA: 1:30
JINA : ………………………………………………………TAREHE:………………………
MAELEKEZO
1. Mtihani huu una sehemu A, B na C.
2. Jibu maswali yote katika kila sehemu
3. Andika majina yako matatu katika kila karatasi uliyopewa

SEHEMU A: (TAREKH, SUNNAH NA HADITH)


Katika swali la 1-10 chagua jbu sahihi zaidi na uandike herufi yake kwenye karatasi
ya majibu uliyopewa.
1. Kwa mujibu wa Qur aan lengo la kuumbwa mwanadamu ni
(A) Kufanya mambo mema
(B) Kusoma elimu ya akhera
(C) Kujiandaa na akhera
(D) Kula na kustarehe
(E) Kumuabudu Mwenyezi Mungu
2. Ni mitume gani wawili kati ya wafuatao waliumbwa bila baba?
(A) Mussa (a. s) na Muhammad (s. a. w)
(B) Adam (a. s) na Mussa (a. s)
(C) Nuhu (a. s) na Issa (a. s)
(D) Issa (a. s) na Adam (a. s)
(E) Issa (a. s) na Lut (a. s)
3. Moja ya miujiza nabii Mussa (a. s) ni fimbo yake ya kawaida kugeuka kuwa ;
(A) Chatu
(B) Kamba
(C) Mamba
(D) Simba
(E) Nyoka
4. Mwaka aliozaliwa Mtume Muhammad (s. a. w) umepewa jina la mwaka wa tembo
kwa sababu
(A) Makuraishi walianza kuabudu tembo
(B) Paltokea tembo wengi pale Makkah
(C) Tembo aliingia katika al-ka’abah
(D) Jeshi la tembo lliangamizwa na Allah (s. w)
(E) Palitokea vita vya tembo pale Makkah
5. Mtume Muhammad (s. a. w) alishushiwa Qur aan kwa mara ya kwanza akiwa
(A) Jabal Hiraa
(B) Al-ka’abah
(C) Jabal Thawr
(D) Darul Aqam
(E) Nyumbani kwake
6. Makafiri wa Makkah waliwatesa waislamu wanyonge kwa
(A) Kuwaroga
(B) Kuwaibia
(C) Kuwapiga

1
(D) Kuwaritadisha
(E) Kuwafitinisha
7. Vita vya Badr vilipiganwa baina ya waislamu na
(A) Manaswara
(B) Wanafiki
(C) Maquraishi
(D) Mayahudi
(E) Warumi
8. Makhalifa wawili waongofu wa Mtume (s. a. w) wa kwanza na wa tatu ni
(A) Abubakar (r. a) na Ali (r. a)
(B) Abubakar (r. a) na Uthman (r. a)
(C) Abubakar (r. a) na Ali (r. a)
(D) Omar (r. a) na Ali (r. a)
(E) Uthman (r. a) na Ali (r. a)
9. Safu ya kupinga ukoloni nchini ilikuwa na waislamu wengi kwa sababu ___________
Zaidi
(A) Walikuwa wanajua siasa
(B) Walipenda madaraka
(C) Walikuwa wasomi
(D) Walinyanyaswa
(E) Walikuwa wengi
10. Katika sharia ya kiislamu, Hadith maana yake ni;
(A) Maneno ya mtume Muhammad (s. a. w)
(B) Maneno ya maswahaba wa Mtume (s. a. w)
(C) Maneno ya wanazuoni
(D) Maneno yaliyomo katika vitabu mashuhuri
(E) Maneno ya kumsifu Mtume (s. a. w)

SEHEMU B: (QUR’AN)
Jibu maswali yote katika sehemu hii.
Katika swali la 11-20 chagua kifungu cha maneno kutoka ORODHA B kinachowiana na
kifungu cha ORODHA A, kisha uandike herufi yake katika karatasi ya majibu uliyopewa.
ORODHA A
11. Hukmu ya tanwiin
12. Mwenye kumiliki siku ya malipo
13. Mbingu zitapo pasuka
14. Kujikinga na shari
15. Kinywaji cha watu wa peponi
16. Suuratul Mulk
17. Ni kipi kilichowapelekeni motoni?
18. ‘Illiyyin’
19. Lakini nyinyi mnapenda Zaidi Maisha ya dunia
20. Mim sakna

ORODHA B

2
(A) Ikh-fau shafawiy
(B) Siku ya kiyama
(C) Iq-labu
(D) Tasniim
(E) Suuratul Fatiha
(F) Juzuu ya Qadisamia
(G) Sijjiin
(H) Suuratul Nnaas
(I) Juzuu ya Tabaaraka
(J) Suuratul A’laq
(K) Daftari la amali za watu wema
(L) Suuratul A’alaa
(M) ………Hatukuwa miongoni mwa waliokuwa wakisali
Orodha A 11 12 13 14 15 16 17 18 19 20
Orodha B

SEHEMU C: (AKHLAQ, TAWHIID NA FIQH)


Jibu maswali yote katika sehemu hii
Katika swali la 21-50 andika neno linalokosekana tu katika sentensi zifuatazo
21. Muumin wa kweli ni yule anayefuata ___________________ na Sunnah katika
Maisha yake
22. Vazi la mwanamke ni kufunika mwili mzima isipokuwa ________ na vitanga na
nyayo
23. Mara tunapomsikia mwenzetu kapiga chafya tunamuombea dua kwa kusema
______________________________
24. Nguzo ya kwanza ya uislamu ni ____________________________________
25. Swala zote tano za faradhi zina jumla ya rakaa ____________________________
26. Mtume Muhammad (s. a. w) amesisitiza usafi kwa kusem
“___________________________________ ni nadhifu basi jisafisheni”
27. Mtume Muhammad (s. a. w) ametukataza kula kwa kutumia mkono wa
________________
28. Swala huanza kwa takbira ya kuhirimia kwa kusema
_________________________________
29. Sehemu ya nguo iliyoingia najisi ya nguruwe htwaharishwa kwa kuosha mara
____________
30. Nyumba ya Allah (s. w) (Al-ka’abah) ndio ___________________ cha waislamu
wote duniani
31. Swala ya faradhi ambayo ni lazima iswaliwe kwa jamaa ndio iswihi ni
__________________
32. Swala ya sunnah inayoswaliwa katika mwezi wa ramadhani tu inaitwa
__________________
33. Mifugo inayotolewa Zakat ni Ngamia, Mbuzi, Ng’ombe na
______________________
34. Lengo la Zakat na Sadaqat ni kutakasa mali na __________________________ya
mtoaji
35. Muislamu hulazimika kutoa Zakat ya __________________iliyofikia nisaab

3
36. Qur aan inabainisha kuwa usiku wenye cheo (Laylatul Qadr) ni bora kuliko miezi
__________
37. Katika kalenda ya kiislamu mwezi wa Ramadhani huanza baada ya mwezi wa
____________
38. Funga ya Arafa ni siku ya tarehe __________________________ Dhul-Hijjah
39. Sunnah moja wapo katika mwezi wa Ramadhani ni kuzidisha kusoma
___________________
40. Nguzo ya tano ya uislamu ni kuhiji katika nyumba ya Allah (s. w) iliyopo mjini
_______________________________
41. Ibada ya kuzunguka Al- Ka’abah mara saba wanayofanya mahujaji inaitwa
______________
42. Sunnah ya kuchinja siku ya idil Hajj hutukumbusha historia ya Ibrahim (a. s) na
____________________ (a. s)
43. Idadi ya jumla ya nguzo za uislamu na nguzo za Imani ni
__________________________
44. Sura ya Qur aan inayomtakasa Allah (s. w) na kila sifa ya upungufu inaitwa
__________________________
45. Malaika wa Allah (s. w) aliyemteremshia Mtume Muhammad (s. a. w) Qur aan
anaitwa ________________________
46. Kitabu pekee cha Allah (s. w) ambacho lugha yake inazungumzwa hivi leo ni
_____________________________
47. Mtume Muhammad (s. a. w) alipendeka sana kwa watu wake na kupewa majina ya
_______________________________ na Aswaadiq
48. Maisha ya akhera huanza kwa kukata roho na mwisho ni mja mwema kuingia
____________
49. Kuamini kuwa shari zote zinatokana na Allah (s.w) ni nguzo ya _______________ ya
imani
50. Kujisalimisha kwa kumtii Mwenyezi Mungu ndio maana halisi ya dini ya
_________________

KINYEREZI ISLAMIC SCHOOLS . MOB: 0756 700 750 , 0735 750 700
“QUALITY EDUCATION SHAPED BY ISLAMIC VALUES”

You might also like