Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 163

MONEY PASSCODE

Siri Zitakazokusaidia Kupata


Mafanikio Ya Kifedha

Isaack Nsumba
Hakimiliki

Kitabu hiki kimeandikwa na Isaack Nsumba,


Haki zote zimehifadhiwa. Huruhusiwi kunakili au
kudurufu sehemu ya kitabu hiki bila idhini ya
mwandishi. Kufanya hivyo itakuwa ni ukiukwaji wa
haki za mwandishi na mchapaji. Ikigundulika hatua kali
zakisheria zitachukuliwa dhidi yako.

Isaack Nsumba
Dar Es Salaam, Tanzania, East Asfrica
Simu: +255 654 722 733
Website: www.isaacknsumba.com
Tovuti: nsumbaisaack@gmail.com
YALIYOMO
Utangulizi 2
Sura ya Kwanza: Viashiria 5
vitakavyokusaidia kujua hali yako ya
kifedha ni mbaya 2

Sura ya Pili: Mambo 3 Muhimu


unayoyahitaji kabla ya kupata fedha 2

Sura ya Tatu: Aina kuu 2 za Ujuzi


muhimu unaohitaji kuhusu fedha 2

Sura ya NNe: Makosa ya kifedha


unayotakiwa kuyaepuka 2

Sura ya Tano: Kanuni Muhimu


unazotakiwa kuzitumia, ili zikupe
mafanikio ya kifedha 2
Sura ya Sita: Mambo
yatakayokusaidia kuivutia fedha
katika maisha yako 2

1
Sura ya Saba: Mambo makubwa 3
yanayoweza kuathiri hali yako ya
kifedha 2

Sura ya Nane: Mambo


yatakayokusaidia kuzilinda na
kuzitunza fedha zako zisipotee 2

Hitimisho 2

Kuhusu Mwandishi 2

2
Utangulizi

Nadhani umewahi kujiuliza,


inawezekanaje mtu akawa wa mwisho
darasani na asiye na ufaulu mzuri
katika masomo afanikiwa sana
kifedha zaidi ya mtu aliyekuwa
anafanya vizuri darasani?

Au umewahi kujiuliza, inawezekanaje


mtu aliyesoma masuala ya fedha
chuoni akawa na matatizo mengi ya
kifedha na kuonekana
kutokuyafurahia maisha tofauti na
mtu ambaye hakuwahi kusoma
masomo hayo?

Lakini pia yawezekana ulikuwa


ukiamini kuwa ukisoma, ukapata kazi

3
nzuri na mshahara mzuri tayari
umefanikiwa kutatua matatizo ya
kifedha, cha ajabu ni kwamba baada
ya kuyafanya yote hayo hali iko
palepale.

Au uliamini kuwa siku


utakapoongezewa mshahara ndipo
utaanza kuwa na hali nzuri ya kifedha,
ila tangu mshahara umeongezeka hali
yako ya kifedha bado ni ileile, yaani ni
kama hakuna kilichobadilika.

Wakati mwingine unafanya kazi au


biashara, fedha unapata ila baada ya
muda hujui zimekwenda wapi?

Umekuwa mtu ambae, kila


unaposhika fedha unajikuta
umezitumia katika namna ambayo

4
baada ya muda unajutia kwa sababu
umezitumia katika mambo yasiyo na
msingi?

Au pengine, kila unapopata fedha


huwa kuna matatizo yanaibuka
ambayo yanahitaji fedha ili yatatuliwe,
baada ya fedha kuisha na matatizo
yanatoweka?

Kuna watu hawafanyi kazi kama


wengine ila wanaonekana
wamefanikiwa zaidi kifedha kuliko
wanaofanya kazi.

Kuna watu hawakuwa na ufaulu mzuri


sana katika masomo yao lakini
wamepiga hatua kubwa kifedha kuliko
wale waliokuwa na ufaulu mzuri
darasani.

5
Maswali hayo na mengine mengi
yanajibiwa ndani ya kitabu hiki
kitakachokwenda kukupa SIRI
ZITAKAZOKUSAIDIA KUPATA
MAFANIKIO YA KIFEDHA.

Mafanikio ya kifedha yanaanzia katika


ufahamu, ukifanikiwa kuwa na
ufahamu wa mambo gani yakupasayo
kufanya na ukayafanya ipasavyo
suala la kupata mafanikio ya kifedha
ni la kutegemea.

Ungana na wengine wengi ambao hali


zao za kifedha zinakwenda kugezwa
mara baada ya kuyaweka katika
matendo maarifa yaliyo ndani ya
kitabu hiki, nimekuombea kwa Mungu
kitabu hiki kiwe sehemu ya vitabu
vitakavyobadili maisha yako.

6
Sura Ya Kwanza
Viashiria 5 Vitakavyokusaidia Kujua
Kuwa Hali Yako ya Kifedha ni Mbaya

The School of Success Academia ni


taasisi inayohusika na kuwapatia
watu elimu kuhusu mafanikio, katika
ushauri wao walishauri kwamba, ili
mtu aweze kufanikiwa kifedha
atalazimika kuwa na utaratibu wa
kujifanyia tathimini na uchambuzi
binafsi kuhusu hali yake ya kifedha
(Personal Financial Analysis and
Evaluation).

Angalia mambo yafuatayo na kisha


ujitathimini, ikiwa utaona kiashiria
chochote kati ya hivi basi ni wazi
kwamba hali yako ya kifedha ni

7
mbaya, utalazimika kuweka juhudi za
makusudi ili kuirekebisha.
Kiashiria cha Kwanza; kuwa na
chanzo kimoja cha mapato
Kwa mujibu wa Robert kiyosaki,
binadamu wamegawanyika katika
makundi makubwa matatu hasa
katika fedha, Kundi la kwanza
wanaitwa maskini, kundi la pili
wanaitwa watu wa kipato cha kati na
kundi la tatu ni matajiri.

Mtu ambae yupo katika hatari kubwa


ni yule ambae anategemea chanzo
kimoja cha mapato ndicho kiweze
kumsaidia kutatua matatizo yake yote
yahusuyo fedha, hii ni sifa mojawapo
ya masikini au ni dalili ya mtu kuingia
katika umasikini.

8
Hii imewafanya wengi waaamini
kwamba kipato chao hakitoshi, ukweli
ni kwamba ili mtu afanikiwe kifedha
anatakiwa kugawa namna ambavyo
mahitaji yake yatatatuliwa na vyanzo
tofauti vya mapato.

Ikitokea majukumu yote


yakaelekezwa katika sehemu moja
hiyo sehemu lazima ielemewe na
kushindwa kubeba majukumu hayo,
tafsiri nyepesi ya maisha magumu ni
kwamba majukumu ni mengi kuliko
uwezo wa kuyabeba.

Yawekezaka leo maisha yako


yanategemea chanzo kimoja cha
mapato ulichonacho, hiko kinatakiwa
kuwa kama ngazi ya kuanzia (primary
source), unatakiwa kujiwekea

9
mikakati ili kutoka katika chanzo
chako cha mapato cha sasa upate na
chanzo kingine pia (secondary sorce).

Kiashiria cha Pili; Mapato kuishia


katika mahitaji
Ukiona kwamba, unafanya kazi na
unapata fedha kupitia kazi hiyo lakini
mapato yote unayopata yanaishia
katika kula, kuvaa, kulipa kodi na bili
ni kiashiria kuwa una hali mbaya sana
inayohitajki kushughulikiwa haraka.

Unahitaji kufanya kitu ili kubadilisha


hali yako ya sasa, kwa maneno
mengine ni kwamba unafanya kazi ili
kusukuma siku na sio ili kupiga hatua.
Unatakiwa kuwa na kipato
kitakachokuwezesha kula, kuvaa,
kutibiwa, kusafiri, kulipa gharama za
10
maisha, kuweka akiba pamoja na
kufanya uwekezaji.

Kwa mujibu wa Elizabeth Warren


katika kanuni yake ya 50/30/20 rule
ambayo mimi naiita Triangulation Of
Financial Decision .

Kanuni hiyo inasema, kila


mwanadamu anatakiwa kuitumia
fedha yake kwa kufanya maamuzi ya
aina kubwa tatu, yaani kutumia
(Spending) kuweka akiba (Saving)
pamoja na kuwekeza (Investing).

Kwahiyo ukiona fedha yako


unayopata inaishia katika aina moja
ya maamuzi yanayohusu kuitumia
Spending ujue una hali mbaya.

11
Ikiwa mshahara wako wote unaishia
kwenye kula, kuvaa, kulipa kodi
pamoja na matibabu bila kubakisha
kiasi cha kuweka akiba na kuwekeza
ni wazi kwamba unahitajika kufanya
kitu ili kushughulikia hali yako ya
kifedha.

Isaack Newton alikuja na kanuni yake


inayoitwa Law of Inertia (kanuni ya
kuchukua hatua) kanuni hii inasema
kwamba, An object at rest, tend to
stay at rest untill when outside power
is acted upon it .

Tafsiri yake ni kwamba, kitu kikiwa


katika hali fulani, kitaendelea kubaki
katika hali hiyo, mpaka pale ambapo
nguvu ya ziada itatumika ili kukitoa
katika hali hiyo.

12
Kama unataka kubadilisha hali yako
ya sasa unatakiwa kuichukia kiasi cha
kuchukua hatua za haraka sana ili
kukabiliana nayo, kama usipofanya
hivyo hali hiyo itaendelea kubaki.

Kumbuka, mambo hayabadiliki kwa


sababu tu unayachukia jinsi yalivyo,
ila yanabadilika kwa sababu
unayachukia kiasi cha kuchukua
hatua madhubuti ili kuyabadilisha.

Kiashiria cha Tatu; Matumizi


Kuongezeka sawasawa na ongezeko
la Kipato.
Kama hapo awali ulikuwa ukipata kiasi
fulani cha fedha na matumizi yako
yalikuwa yanalingana na mapato
yako, leo kiasi cha fedha unachopata

13
kimeongezeka lakini bado matumizi
yako yameongezeka pia, una hali
mbaya na inaashiria kuwa
hautafanikiwa kifedha kama
hautaibadilisha hali hiyo.

Ikitokea kila unapojitahidi kuongeza


kipato ndivyo na matumizi
yanavyozidi kuongezeka pia basi ujue
kuwa unaishi sawasawa na kanuni la
Parkison inayosema mara nyingi
matumzi huongezekla kadri ambavyo

Ili uweze kufanikiwa unatakiwa


kuhakikisha matumizi
hayataongezeka sawasawa na kasi ya
ongezeko la kipato chako.

14
Katika sura zinazofuatia utajifunza ni
namna gani unaweza kulifanikisha hilo
au kukabiliana na hali ya namna hiyo.

Kiashiria cha Nne; Matumizi kuwa


Makubwa kuliko Mapato
Utajua kama matumizi yako ni
makubwa kuliko mapato pale ambapo
utahitaji nyongeza ya mapato kutoka
sehemu nyingine ili uweze kufanya
mambo fulani.

Yaani, ikiwa unakopa ili kulipa kodi au


gharama za kuendesha maisha yako
ni kishiria kuwa matumizi yako ni
makubwa kuliko mapato yako.

Hautakiwi kuwa na matumizi


yanayolingana na kipato chako au
yanayozidi kipato chako, wakati wote

15
matumizi yako yanatakiwa kuwa
madogo chini ya mapato uliyonayo
(your expenses must be below your
income).

Kama matumizi yako ni makubwa


kuliko mapato yake tafsiri yake kuna
mambo mawili yanayoendelea katika
maisha yako.

Jambo la kwanza ni kweli kipato


chako ni kidogo kiasi cha kushindwa
kukidhi mahitaji muhimu ya maisha
yako na tafsiri ya pili ni kwamba,
umeshindwa kupanga bajeti na
kuweka vipaumbele kiasi cha
kutokujua ni maeneo gani muhimu
unayotakiwa kuzielekezea fedha
zako.

16
Kwa namna yoyote unatakiwa
kuongeza kipati chako au kupanga
bajeti ili kuielekezea fedha yako
katika maeneo fulani ili usije jikuta
unatumia fedha mpaka zinaisha ndipo
unakuja kugundua kuna kitu cha
muhimu ulitakiwa kufanya na
haujafanya, ikifika hapo unalazimika
kwenda kukopa jambo ambalo
litaathiri hali yako ya kifedha.

Kiashiria cha Tano; Maisha yako


kuendeshwa kwa Mikopo.
Kwenye maisha kuna wakati
utalazimika kukopa ili kutatua
changamoto fulani iliyokuja katika
wakati ambao hauna uwezo wa
kifedha wa kuitatua.

17
Ila ukiona katika maisha yako,
umefika hatua ambayo unategemea
mikopo kwa sehemu kubwa ndipo
uweze kuyaendesha basi uje una hali
mbaya kiasi kwamba kama
usipoishughulikia mapema inaweza
kuathiri yali yako ya kisaikolojia na
hata afya ya mwili pia.

Ukiona wewe kila unapopata


changamoto fulani ya kifedha wazo
linalokuja ni kukopa fedha mahali hiyo
ni hali mbaya, unatakiwa kuweka nia
thabiti ya kuhakikisha unaondokana
na madeni.

Kukopa hakutakiwi kuwa kama ndio


mikombozi wako namba moja kila
unapohitaji fedha, kukopa kuwe ni njia

18
ya mwisho kabisa baada ya njia zote
kushindikana.

Kumbuka, mikopo haitatui tatizo, ila


inalisogeza tatizo mbele ambapo kwa
sehemu mbeleni linaweza likawa ni
zito zaidi ya vile lilivyo leo.

Wewe fikiria, umepata changamoto


inayohitaji kutatuliwa kwa 400,000
ukaenda kukopa fedha ambayo
utailipa kwa riba.

Baada ya muda lile tatizo litakuwa


palepale ila litakuwa limeongezeka
uzito, yaani tatizo la 400,000
utalitatua kwa fedha zaidi ya 400,000
ambayo ni hela uliyokopa na riba
yake.

19
Ikiwa kuna point yoyote kati ya hizo
inakugusa basi ni wazi kuwa hali yako
ya kifedha sio nzuri na unatakiwa
kuweka mkakati utakaokuwezesha
kuchukua hatua za kuibadilisha.

20
Sura Ya Pili
Mambo 3 Muhimu Unayoyahitaji
Kabla Hujapata Fedha

Kwa mujibu wa waandishi mbalimbali


na wataalamu wa masuala ya
mafanikio akiwemo ndugu Morgan
Housel ambaye ni mwandishi wa
kitabu cha The Psychology Of
Money (saikolojia ya Fedha)
imethibitika kwamba fedha
inatanguliwa na mambo kadhaa kabla
ya yenyewe.

Hii ni kusema kwamba kuna mambo


muhimu sana ambayo mtu yeyote
anatakiwa kuwa nayo kabla hajapata
fedha, mambo haya yamewasaidia
watu wengi katika safari ya mafanikio

21
yao ya kifedha, sina shaka hata wewe
yatakusaidia sana.

Emanuel Olumide ambae ni mkufunzi


wa masuala mbalimbali lakini pia ni
mwandishi wa kitabu cha The School
of Money anasema Money has soul,
body and spirit, most of people strive
to have its body and forget spirit and
soul

Kwa tafsiri iliyo nyepesi ni kwamba


fedha ina mwili (upande
unaoonekana) na roho (upande
usioonekana) watu wengi wanaitafuta
fedha inayoonekana na kusahau
fedha isiyoonekana.

Mtu mmoja aliwahi kusema kama


matajiri wote leo hii wakichukua fedha

22
zao na kuwapa maskini wote, baada
ya muda wale matajiri watarudi katika
utajiri wao na maskini watarudi katika
umaskini wao.

Hii ni kwa sababu umiliki wa fedha


hauanzii nje, umiliki wa fedha na
mafanikio yake yanaanzia ndani na
ndio maana ni vigumu sana mtu
kuendelea kuwa na fedha alizonazo
nje kama ndani yake hana fedha
zisizoonekana.

Kuna mambo makubwa matatu


ambayo kila aliyefanikiwa kifedha
anayo, kwa sababu nawewe
umedhamiria kuyapata mafanikio ya
kifedha basi utalazimika kuwa na
hayo mambo, ili yakusaidie.

23
Jambo la kwanza:
Mtazamo, Fikra na Imani chanya
kuhusu Fedha.
(Positive Money-Mindset and
Perception)

Mwandishi nguli wa masuala ya


mtazamo, akili na ufahamu ili kupata
mafanikio ya kifedha bwana T. Harver
Eker aliandika kitabu kinaitwa The
Secrets Of millionaires Mind (Siri
zilizopo katika akili za mamilionea)
katika moja ya nukuu zake anasema
In your life, you cannot be more than
how you conceptualize yourself
(katika maisha hauwezi kuwa zaidi ya
vile ambavyo unajiona wewe
mwenyewe).

24
Kwa maneno mengine ni kwamba
mafanikio yako ya kifedha ni matokeo
ya mtazamo, fikra na Imani uliyonayo
juu yako wewe mwenyewe na juu ya
fedha.

Ni vigumu sana kufanikiwa kifedha


ikiwa Imani yako na mtazamo wako
juu ya fedha haukusapoti.

Mike Phillips ni mmoja kati ya


wataalamu wa masuala ya mafanikio
waliokuja na sheria muhimu ambazo
kila anaetaka kufanikiwa kifedha
lazima azitumie, katika moja ya sheria
yake anasema Fedha huwa
zinakwenda kwa watu ambao
wanaamini kuwa fedha ziko kwaajili
yao

25
Kwa mujibu wa kanuni hiyo ni
kwamba mtu yeyote anayetaka
kufanikiwa kifedha ni lazima kwanza
ashughulike na mtazamo wake
kuhusu fedha kutoka katika hali ya
kuamini kuwa haiwezekani mpaka
kuamini kuwa fedha zipo kwaajili yake
na kuna uwezekano wa yeye
kuzipata.

Kuna fikra za aina mbili linapokuja


suala la fedha, aina ya kwanza
inaitwa Scarcity Mentality hizi ni
fikra za uhaba na kutokutosheleza
kwa fedha.

Mtu yeyote mwenye fikra za aina hii


anaamini kwamba fedha hazipo,
fedha hazitoshi na kwa sababu hiyo
yeye hawezi kupata fedha zaidi ya

26
zile alizonazo leo, amejiwekea ukomo
wa kiwango cha pesa anachoweza
kumiliki kwa sababu anaamini fedha
hazitoshi.

Kwa upande mwingine mtu wa aina hii


anamini kwamba, umaskini wake ni
matokeo ya kitendo cha matajiri
kujikusanyia fedha, wengi wanaamini
wao ni maskini kwa sababu fedha
nyingi zipo mifukoni mwa matajiri.

Kama kuna mtu yeyote unamuona


amefanikiwa kifedha basi unatakiwa
kujua kuwa kuna siku aliyashinda
mawazo, mitazamo na Imani hasi
kuhusu fedha.

27
Kwahiyo nawewe leo ukibadili
mtazamo ulionao utafanikiwa sana
kifedha.

Aina ya pili ya fikra na mtazamo


kuhusiana na fedha inaitwa
Abundance Mentality hizi ni fikra za
utoshelevu, ni fikra ambazo kila
anaetaka kufanikiwa kifedha
anatakiwa kuwa nazo.

Mtu mwenye fikra za namna hii


anaamini kuwa kuna fedha nyingi
sana duniani nayeye anaweza
kuzipata ikiwa atajua kimpasacho
kufanya.

Lakini pia, mtu mwenye fikra za aina


hii anazo nguvu, anayo shauku na
juhudi katika utafutaji wake huku

28
akiamini kuwa kama kuna wengine
walifanikiwa, basi nayeye atafanikiwa,
na kwa sababu ya Imani yake hiyo
tayari ana uwezekano mkubwa sana
wa kufanikiwa.

Katika kuchambua aina za fikra, Imani


na mitazamo kuhusu fedha ambayo
watu wanazo kuna makundi makubwa
matatu ya watu tunawapata,
hakikisha wewe haupo katika kundi
lolote kati ya haya.

Kundi la Kwanza; wanaoamini kuna


watu maalumu wameumbwa
kufanikiwa kifedha.

Hili ni kundi la watu ambao


wamejenga mtazamo, fikra na Imani
ndani yao kuwa kuna watu maalumu

29
tofauti na wao ambao wameumbwa
kufanikiwa kifedha na mafanikio ya
kifedha yapo kwaajili ya hao tu na sio
wengineo.

Watu wa aina hii wameshajitoa kabisa


katika kundi la watu wanaoweza
kupata mafanikio ya kifedha, pamoja
na ukweli kwamba Imani na mitazamo
hiyo imekuwa sugu ndani yao bado
wanafanya kazi ili kutafuta fedha za
kuendeshea maisha japo juhudi zao ni
kubwa kuliko matokeo ya juhudi zao
bila kujua kuwa juhudi zao zinatakiwa
kuambatana na mtazamo sahihi. Na
kwa sababu mtazamo walionao sio
sahihi inakuwa vigumu kwao
kufanikiwa.

30
Kundi la Pili; Wanaoamini na
kuihusianisha fedha na uovu.

Hawa ni wale ambao huitazama fedha


kama chanzo cha uovu, watu wa aina
hii wanaamini kuwa kila aliyefanikiwa
kifedha kuna kitu alifanya ndicho
kilicholeta mafanikio yake ya kifedha
na sio kanuni za kawaida.

Watu wa aina hii ni wale ambao


wamesikia shuhuda nyingi za watu
waliojaribu kutafuta mafanikio kwa
kanuni za kawaida wakafeli, na
shuhuda za watu waliofanikiwa
kupitia njia haramu wakayapata
jambo ambalo liliwafanya wahitimishe
kuwa mafanikio yoyote ya kifedha ni
matokeo ya uovu fulani uliofanyika.

31
Ni ukweli usiopingika kwamba kuna
watu wengi ambao wamefanikiwa
kifedha kwa kutumia njia zisizo halali,
lakini ni ukweli usiopingika pia kuwa
kuna uwezekano wa mtu kufanikiwa
kifedha kwa kutumia kanuni za
kawaida kabisa kama ambazo
unajifunza katika kitabu hiki,
nimekuombea kwa Mungu wewe pia
ukawe mmoja kati ya watu
watakaofanikiwa sana.

Unachotakiwa kufahamu ni kwamba


fedha sio mzizi wa maovu yote
yanayotendeka, ila kwa sehemu
kubwa chanzo cha maovu mengi ni
ukosefu wa fedha (Money is not root
cause of all evils, but at most
absence and lack of money it is)

32
Watu wanaua wenzao, wengine
wanaiba, wanawake wanajiuza,
wanaume wanakuwa mashoga, watu
wanavunja sheria ili kuhakikisha
wanapata fedha, kwahiyo fedha ni
chanzo cha maovu mengi hasa pale
inapokosekana.
Kundi la Tatu: Wanaoamini katika
kusaidiwa, kurithi au kubahatika.
Katika kundi hili wanaingia wote
ambao wanaamini kwamba matajhiri
wengi na watu wote waliofanikiwa
kifedha wana bahati ya mafanikio,
wamerithi kutoka kwa ndugu au
wazazi wao au wamesaidiwa na watu
wengine.

Watu wa namna hii wanasumbuliwa


na tatizo la kisaikolojia linaitwa

33
Entitlement Mentality (hali ya
kuamini kuwa kuna watu
wanaotakiwa kuwajibika kwa niaba
yao) pamoja na Extrovert Disorder
hali ya kuamini kuwa nguvu ya
kuyabadilisha maisha yao hutoka nje
na sio ndani yao.

Watu wa aina hii mara nyingi ni rahisi


sana kuwakuta wanawalalamikia watu
wengine kama ndugu, jamaa, wazazi
au marafiki kwa kutokuwasaidia.

Hawaamini kabisa kama wao


wanaweza kutafuta mafanikio na
yakatokea bila kuwategemea watu
wengine, hakikisha unakuwa ni mtu
unaeamini kwenye uwezo binafsi,
Mungu alikuumba kama kiumbe

34
kinachoweza kujitegemea (Self-
Depending Creature).

Hii haiondoi ukweli kwamba


kusaidiwa kupo, ila kusaidiwa
hakutakiwi kuwe kipaumbele chako
cha kwanza bali kunatakiwa kuwe ni
sehemu ya nguvu ya nyongeza
unayojitaji katika juhudi ulizokwisha
kuzianzisha wewe binafsi.
Jambo la Pili:
Uimara wa Hisia zako
(Emotional Muscles/Strong
Emotions)

Utafiti uliofanywa na wataalamu


mbalimbali wa masuala ya mafanikio
ya kifedha umebainisha kuwa
binadamu anapatwa wakati mgumu
sana pale ambapo mazingira

35
yanamtaka ajioneshe kuwa ana fedha
kwa kufanya vitu ambavyo havihitaji.

Hii ni kwa sababu ya kitu kinaitwa


Social Proof ambacho kinawafanya
watu wengi kuithibitishia jamii kuwa
wanazo fedha, hawana ugumu wa
maisha, wanayafurahia na tayari
wameshafanikiwa.

Changamoto kubwa ni kwamba wengi


huwa wanafanya haya wakiwa bado
hawajapata mafanikio thabiti ya
kifedha na wala hawajaweka misingi
mizuri ya mafanikio yao, kinachotokea
ni kwamba baada ya muda
wanapoteza fedha zote walizokuwa
nazo na kurudi katika hali ya dhiki
tena.

36
Hata hivyo, utafiti uliofanywa na
Poffesor Stanley Danko aliyeandika
kitabu cha The Millionaire Next Door
umeonesha kuwa matajiri wengi
huishi maisha ya kawaida sana, kwa
sababu hawajibidiishi ili kuonekana
kama wana fedha, bali wanajibidiisha
ili kupata mafanikio zaidi ya kifedha.

Utafiti huo umebainisha kuwa


kinachowasaidia matajiri kuishi
maisha ya kawaida licha ya ukweli
kwamba wana fedha nyingi sana ni
uimara wa kihisia walionao na uwezo
mkubwa wa kuhimili hisia zao.

Hii ni kwa sababu kuna wakati


ambapo mazingira yanawataka
Kuvimba/kujimwambafai na kitu

37
pekee kinachowasaidia kutokufanya
hivyo ni Emotional Muscles

Kama hautakuwa na huu uwezo wa


kuhimili hisia zako, mara baada ya
kupata fedha utajikuta unaingia katika
mtego wa kutaka kufanya mambo ili
kuithibitishia jamii kuwa una fedha
hata kama mambo hayo hayapo
katika orodha ya vipaumbele vyako,
jambo hili limeathiri hali ya kifedha
kwa watu wengi sana.

Kwa sababu ya kukosa hisia imara na


uwezo wa kuhimili fedha ndipo mtu
huweza kuchukua mkopo anaotarajia
kufanya biashara, mara baada ya
kupata mkopo huo akaenda kununua
gari ili watu waone kuwa
amefanikiwa.

38
Kwahiyo, kabla haujapata fedha
mkononi unahitaji kuwa na hisia imara
zitakazokusaidia kuwa na nidhamu
pamoja na uwezo wa kusimamia
vipaumbele vyako hata kama
mazingira yanakutaka uende kinyume
navyo.
Jambo la Tatu:
Akili, Ufahamu na Maarifa sahihi
Kuhusu Fedha
(Financial Intelligence)

Mwandishi na mwalimu aliyebobea


katika masuala ya elimu ya mafanikio
ndugu Robert Kiyosaki katika tafiti
zake alithibitisha kuwa tofauti kubwa
iliyopo kati ya matajiri na maskini ni
katika ufahamu ambao kila kundi
linamiliki kuhusiana na fedha.

39
Kwa maneno mengine ni kwamba,
matajiri wote wana kitu
wanachokifahamu kuhusu fedha
ambacho kama maskini wakipata
nafasi na wao wakakifahamu basi
watahama kutoka katika kundi la
masikini na kuhamia katika kundi la
matajiri.

Kwa bahati mbaya sana ufahamu


kuhusu masuala ya kifedha hautolewi
shuleni wala vyuoni na ndio maana
kuna uwezekano mkubwa wa mtu
kusoma sana na akapata ufaulu mzuri
katika masomo yake ila katika maisha
ya kawaida akawa na matatizo mengi
ya kifedha ambayo ukiyafuatilia
utabaini kuwa chanzo chake ni

40
ukosefu wa maarifa sahihi kuhusu
fedha.

Watu wengi wanadhani kuwa


mafanikio ya kifedha ni kuwa na
fedha nyingi mfukoni, kuwa na fedha
ni sehemu ndogo sana ya mafanikio
ya kifedha; sehemu kubwa inakutaka
umiliki maarifa na ufahamu sahihi
kuhusu fedha.

Ufahamu huo ndio utakusaidia kujua


namna gani unaweza kutengeneza
fedha, kuisimamia, kuilinda na
kuitunza pamoja na kuizalisha.

Ukikosa ufahamu hata kama ukipewa


fedha nyingi leo baada ya muda
zitapotea kwa sababu umekosa

41
maarifa yanayoweza kukusaidia
kuzilinda zisipotee.

Utafiti uliochapishwa na gazeti la


Forbes unaonesha kuwa matajiri ndio
watu ambao wanaongoza kwa
kutafuta maarifa yanayohusu fedha.

Lakini pia ni watu ambao wako tayari


kuyagharamikia kwa kiasi kikubwa ili
waweze kuyapata, katika hali ya
kawaida tulitegemea wao
wasihangaike kwa sababu tayari
wanazo fedha, ila wanajibidiisha
kutafuta maarifa kwa sababu wanajua
ni nyenzo muhimu itakayowawezesha
kutunza mafanikio yao ya kifedha.

42
Sura ya Tatu

Aina kuu 2 za Ujuzi Muhimu


unaohitaji Kuhusu Fedha.
(Basic Money Relating Skills)

Katika kitabu chake kinachoitwa Why


A students works for C student and B
students works for the Governmnet
mwalimu nguli wa masuala ya
mafanikio ya kifedha Robert Kiyosaki
anaeleza sababu mojawapo
inayowafanya watu ambao hawakuwa
na uwezo mzuri katika masomo yao
au wale ambao hawajasoma sana
kumiliki fedha nyingi huku
wakiyafurahia maisha wakati wale
waliosoma sana na kufanya vizuri
katika masomo yao wakiishia kuwa na

43
vipato vigogo ambavyo wakati
mwingine havikidhi mahitaji
waliyonayo.

Yawezekana hata wewe umewahi


kujiuliza swali la namna hiyo kwamba
inawezekanaje mtu ambae hajasoma
akafanikiwa zaidi katika eneo la
kifedha na kumuacha mbali mtu
ambae amesoma sana.

Ukweli ni kwamba unaweza kuwa ni


mtu uliyefanikiwa sana kitaaluma na
uliyefeli sana kifedha (You can be
academically successfully and
financially failure).

Tena wakati mwingine mtu anaweza


akawa amesoma masomo ya
usimamizi wa fedha na biashara

44
(Banking and Finance Management)
lakini bado suala la fedha kwake
likawa ni fumbo, katika sura hii
utapata majibu ya maswali hayo na
yatakusaidia sana kufanya maamuzi
sahihi.

Linapokuja suala la fedha kuna aina


kuu mbili za ujuzi muhimu ambazo kila
mtu anaetaka kufika mbali kifedha
anatakiwa kuwa nazo.

Kutokuwa na aina hizi za ujuzi


kunaweza kuathiri hali yako ya
kifedha hata kama unapata kipato
kikubwa au umesomea masuala ya
fedha, lakini pia kuwa na aina hizi za
ujuzi kunaweza kukupa mafanikio ya
kifedha hata kama kisomo chako sio
kikubwa, kipato chako kinaonekana ni

45
kidogo na uwezo wako katika
masomo haukuwa mzuri.
Aina ya kwanza;
Ujuzi wa kuizalisha Fedha
(Money Making Skills)
Mtu mmoja aliwahi kusema kama
matajiri wote leo hii wakichukua fedha
zao na kuwapa maskini wote, baada
ya muda wale matajiri watarudi katika
utajiri wao na maskini watarudi katika
umaskini wao.

Kitakachowafanya matajiri warudi


katika utajiri wao ni kwa sababu
wanamiliki ujuzi wa namna gani ya
kuizalisha fedha, ujuzi huu
unaambatana na mtazamo sahihi
tuliojifunza katika sura ya kwanza.

46
Aina hii ya ujuzi ndio ilimfanya
billionea mmoja kwa ujasiri kusema
chukua vyote nilivyonavyo leo ila
niachie uhai baada ya muda nitakuwa
na kila nilichonacho sasa

Kwa maneno mengine anasema


kwamba nina ujuzi wa kuzalisha
fedha ambao unaweza kunisaidia
wakati wowote na mahali popote
kupata fedha bila kujali ni mgeni au
mwenyeji na bila kujali nimesoma au
sijasoma.

Mtu mwenye aina hii ya ujuzi


atafanikiwa sana kifedha kwa sababu
fedha inavutika kwa mtu anaejua
namna nzuri ya kuizalisha.

47
Ndio maana, kuna watu waliwahi
kuwa na fedha, wakafirisika na
kupoteza kila walichokuwa nacho na
baada ya muda wakarudi tena kuwa
na fedha, ni kwa sababu walipoteza
fedha na hawakupoteza ujuzi wa
kuizalisha fedha.

Mtu mwenye ujuzi wa kuzalisha fedha


atafanikiwa sana hata kama uwezo
wake darasani ulikuwa mdogo, hata
kama alitokea katika familia ya chini
au hata kama hajasoma masuala
yanayohusu fedha.

Hii ndio sababu haswa kwanini watu


ambao hawakusoma sana
wamefanikiwa zaidi kifedha kuliko
waliosoma sana, ni kwa sababu
waliosoma kuna ujuzi hawana ambao

48
wale waliokuwa na uwezo mdogo
darasani wanao.

Ndani ya ujuzi wa uzalishaji wa fedha


kuna aina ndogondogo (semi-skills)
za ujuzi ambazo unatakiwa kuwa
nazo.

Aina ya kwanza; ujuzi wa kuuza


(sales and marketing skills) kila mtu
anahitaji kuwa na ujuzi wa kujitangaza
pamoja na kuuza, kama una bidhaa,
kipaji, huduma au taaluma yoyote ile
basi unahitaji ujuzi wa kuuza ili kile
ulichonacho kiweze kupokelewa na
jamii yako.

Kutangaza ni kuwafanya watu wajue


kile ulichonacho na namna wanaweza

49
kukipata, kuuza ni kufanikiwa kutoa
fedha katika mifuko yao na kuileta
katika mifuko yako.

Watu wengi wanao uwezo wa


kutangaza ila hawana ujuzi wa kuuza,
yawezekana hata wewe una kipaji,
una huduma, una wazo na
umefanikiwa kuwafanya watu wajue
ila linapokuja suala la kuuza kile
ulichotangaza unapata changamoto,
zipo kozi nyingi zinazofundisha ujuzi
wa kuuza na zitakusaidia.

Aina ya pili ya ujuzi; ujuzi wa


kuhusiana na kushirikiana na watu
(Network Skills) moja kati ya mambo
ambayo shule haiyafundishi na
haiyatilii kipaumbele basi mojawapo

50
ya mambo hayo ni ujuzi wa kuhusiana
na watu.

Shule imejikita zaidi kutufanya tuwe


watu tunaojitegemea (Independent
People) bila kujua kwa upande fulani
imepandikiza ubinafsi ndani ya watu
na ndio maana hakuna kushirikiano
katika kazi za kitaaluma.

Maisha yanakutaka uwe na ujuzi


mzuri wa kuhusiana na kushirikiana
na watu, hii ni kwa sababu asilimia
kubwa ya yale unayoyahitaji yapo
katika mikono ya watu.

Kuna watu wana ufahamu juu ya kile


unachotamani kujua, kuna watu wana
uwezo wa kukukutanisha na mtu
ambae umekuwa ukitamani kukutana

51
nae lakini pia kuna watu wamefika
mahali ambapo umekuwa ukitamani
kufika, njia rahisi ya kunufaika na wao
ni kuwa na ujuzi wa namna gani ya
kuji-connect nao.

Kati ya zawadi yenye thamani kubwa


Mungu amekupa ni kuwaweka watu
katika dunia, hauwezi kufahamiana na
kila mtu ila unaweza kufahamiana na
watu wachache tu na ukanufaika
kupitia hao.

Aina ya tatu ni ujuzi wa kutatua


matatizo (Problem Solving Skills)
tafsiri mojawapo ya fedha kutoka kwa
wataalamu wa mafanikio inasema
Money is a transaction of value
(Fedha ni mbadilishano wa thamani)
Thamani ni jawabu unalompatia mtu

52
Fulani juu ya changamoto
inayomkabili.

Hii tafsiri yake ni kwamba mtu asiye


na fedha ni kwa sababu kuna thamani
hajatoa, ukubwa au udogo wa
thamani ndio unamua ukubwa au
udogo wa kiasi cha fedha
unachoweza kupata.

Kwa maneno mengine ni kwamba mtu


anaetatua matatizo makubwa ndiye
mwenye uwezo wa kuingiza fedha
nyingi zaidi.

Kwahiyo, badala ya kulalamika ajira


hakuna, maisha magumu, fedha
hazipo anza leo kutengeneza ujuzi
utakaokusaidia kutatua tatizo fulani
katika jamii na ujuzi huo ukufanye

53
uwe mbeba majibu (Solution Oriented
person) na fedha itakufuata.

Kama leo hauna fedha haina maana


kwamba mtaani hakuna fedha ila ina
maana kubwa tatu; mosi, yamkini
haujafanya chochote kinachoshawishi
watu kukulipa, au umefanya na
haujahitaji kulipwa; pili, yawezekana
hauna money making skills (ujuzi wa
kutengeneza fedha) hivyo
umeshindwa kuzalisha fedha kwa
sababu haujui uizalishaje; tatu,
yawezekana una hiyo money making
skills na haujaamua kuitumia ili
ikusaidie kupata fedha.

Kwahiyo, hauna fedha kwa sababu


hizo tatu, na sio kwa sababu

54
haujasoma, au hauna network au
watu wa kukusaidia.

Angalizo; Katika kutatua matatizo


epuka Sana dhana ya kutaka kutatua
kila tatizo, chagua aina ya matatizo
unayoweza kutatua na ujiimarishe
katika hayo, hakuna aliyepewa uwezo
wa kutatua matatizo yote.

55
Sura Ya Nne
Makosa ya Kifedha Unayotakiwa
Kuyaepuka
(Common Money Mistakes to Avoid)

The school Of Financial Success ni


taasisi inayojishughulisha na utoaji wa
elimu ihusuyo mafanikio ya kifedha
pamoja na kufanya tafiti mbalimbali
juu ya sababu zinazoathiri hali ya
kifedha kwa watu wengi.

Mwaka 2017 ilifanya utafiti wake


uliodumu kwa miaka mitatu na
kuchapishwa mnamo mwaka 2019 na
katika utafiti huo walichukua masikini
50 kati ya hao wakawagawa katika
makundi mawili, kundi la kwanza
walipewa mambo wanayotakiwa

56
kufanya na kundi la pili walipewa
mambo ambayo hawatakiwi kufanya
kuhusu fedha.

Baada ya muda, kundi la kwanza


waliopewa mambo wanayotakiwa
kufanya kuhusu fedha waliendelea
kuwa maskini huku wale ambao
walipewa maelekezo ya mambo
wasiyotakiwa kufanya kuhusu fedha
hali zao za kifedha zilibadilika.

Mwisho wa utafiti ilibainika kuwa kwa


asilimia 85% matajiri wamefanikiwa
kuwa matajiri kwa sababu kuna
makosa ya kifedha waliyaepuka
ambayo masikini wengi wanayafanya
mara kwa mara na ndio maana
wanaendelea kuwa maskini.

57
Sura hii imejikita zaidi katika
kukufanya uyajue makosa ya kifedha
ambayo hautakiwi kuyafanya kabisa
kuhusu fedha ikiwa unatamani kupata
mafanikio ya kifedha.

Kosa la kwanza;
Kudharau Kiasi Kidogo
(Ignoring Small Amount)

Mohammed Dewji ana kampuni


inaitwa Mohamed Enterprises
ambayo inauza matrekta na wakati
mwingine inauza sabuni za kuogea
zenye thamani ya shilingi 500, katika
hali ya kawaida ilikuwa ni rahisi kwa
billionea kama yule kutokuitilia
maanani hiyo shilingi 500 ya sabuni
ila ni kwa sababu anajua nafasi ya

58
kiasi kidogo katika kuleta kiasi
kikubwa.

Kuna watu ambao changamoto za


kifedha wanazokutana nazo leo ni
kwa sababu wanadharau kiasi kidogo,
kitendo cha kudharau kiasi kidogo
kina madhara makubwa ya aina mbili.

Kwanza, unaweza ukashindwa


kuongeza kipato chako hasa pale
ambapo inakulazimu kukiongeza
kidogokidogo.

Pili, unaweza kupoteza fedha nyingi


bila kujua kwa kuzitumia
kidogokidogo na usijue kama
zinapotea mpaka baada ya muda
fulani kupita ndipo unaweza kuona
gape la kile ulichopoteza.

59
Darren Hardy katika kitabu chake
kinachoitwa The Compounding
Effect anasema There is huge
reaping from small actions that can
be done repeatedly (kuna mavuno
makubwa kutoka katika vitendo
vidogovidogo vitakavyofanyika mara
kwa mara)

Hii ni kusema kwamba, kama


utapoteza fedha ndogondogo kila
siku kwa kuidharau baada ya muda
utakuwa umepoteza fedha nyingi
sana, lakini pia kama utawekeza kiasi
kidogo kila siku baada ya muda
utakuwa na uwekezaji wa maana.

Biblia inasema
mambo madogomadogo ataanguka
kidogokidogo Sira19:1

60
Kwahiyo, unaweza ukaamua kufika
mbali kwa kuanza kuweka akiba na
kuwekeza kidogokidogo au ukaamua
kutokufika popote kwa kuendelea
kuishi maisha ya kupoteza
kidogokidogo (naomba urudie tena
kuisoma hii sentensi).

Kumbuka, matokeo ya maamuzi yako


hautayaona leo, ila ni hakika kwamba
kuna siku utayaona kwa uwazi kabisa,
fanya maamuzi ambayo hautayajutia
kesho na keshokutwa ikifika.
Kosa la Pili;
Kutumia sawa na au zaidi ya
unachoingiza
(Spending equal or more than what
you earn)

61
Wataalamu wa masuala ya mafanikio
wamebainisha katika takwimu
mbalimbali kuwa maskini wengi ni
watu ambao matumizi yao
yanakwenda sambamba na kipato
chao, lakini pia wakati mwingine
wanatumia zaidi ya kile
wanachoingiza na ndipo inawalazimu
kuingia kwenye madeni.

Yaani, kila fedha inayopatikana


inaishia katika matumizi, wengi
wanaingia katika kundi la wale
wanaolalamika kuwa vipato vyao
haviwatoshi, ukweli ni kwamba sio
vipato vyao havitoshi ila hawana
ufahamu wa kutosha juu ya kugawa
kipato ili kitoshe kufanyia matumizi
muhimu, kuweka akiba pamoja na
kuwekeza.

62
Matajiri ni watu ambao matumizi yao
ni madogo kuliko kipato chao, yaani
kwa namna yoyote ile wanahakikisha
matumizi yao hayalingani wala kuzidi
kipato walichonacho.

Kama leo unataka kutoka katika kundi


la masikini na kuingia katika kundi la
watu watakaofanikiwa kifedha epuka
kufanya kosa la kutumia zaidi ya kile
unachoingiza kwa sababu kama
matumizi yako yatakuwa makubwa
zaidi ya pato lako ni rahisi sana
kuingia katika madeni yasiyo ya
lazima na ambayo yataathiri hali yako
ya kifedha.

63
Kosa la Tatu;
Kukopa ili kuanzisha biashara
(Taking loan, for business startup)

Harvard Business School kitengo cha


tafiti, katika tafiti zao zilizofanywa
miaka ya hivi karibuni zilibainisha
kuwa asilimia 85% ya biashara nyingi
zinakufa miaka miwili hadi mitano
baada ya kuanzishwa.

Katika kutafuta kujua sababu za kufa


kwa biashara nyingi ilibainika kuwa
zinaathiriwa na mikopo ambayo
ilitumika kuanzishia biashara,
kuvunjika kwa biashara kunaathiri hali
ya kifedha ya mtu kwa sababu
pamoja na kuvunjika huko bado
atalazimika kulipa deni.

64
Unashauriwa kuchukua mkopo
kuendeleza biashara pale ambapo
umeanzisha na umeona muelekeo wa
soko na sio kukopa fedha ili
kuanzisha biashara kwa sababu
itachukua muda biashara yako
kusimama na kuanza kukuletea faida
nzuri kiasi cha kulipa deni pamoja na
kukupatia kiasi cha kuendeleza
biashara yako.

Japo wapo watu waliokopa


wakafanikiwa ila takwimu zinaonesha
kundi la waliofeli ni wengi zaidi, ikiwa
utaamua kukopa fedha ili kuansisha
biashara basi unashauriwa kutafuta
mtaalamu wa masuala ya fedha na
biashara (Business and Finance
Expert) ili akusaidie katika usimamizi
wa biashara hiyo ili ikuletee matokeo

65
mazuri na usiingie katika kundi kubwa
la wanaofeli kwa kukosa msaada na
muongozo wa kitaalamu.
Kosa la Nne;
Kufanya uwekezaji bila kuwa na
taarifa za kutosha
(Investing with no enough data)
Katika tafiti zilizofanywa hivi karibuni
zimeripoti juu ya ongezeko la
makampuni na mashirika yanayolenga
kuwasaidia watu kuongeza kipato
chao kupitia wao kuwekeza katika
mashirika hayo kimeongezeka kwa
asilimia 67% kulinganishwa na miaka
ya nyuma.

Makampuni hayo yanajumuishwa na


yale yote ambayo yanaendeshwa
kupitia biashara za mtandaoni (online
66
marketing) hii ni fursa ya kuongeza
kipato lakini ni wakati wa kuwa makini
sana kwa sababu na matapeli
wanaitumia hiyo kama nafasi ya
kuwatapeli watu.

Watu wengi sana wamepoteza fedha


zao kupitia hizo Online Business kwa
sababu waliwekeza bila kuwa na
taarifa za kutosha, wewe epuka kuwa
miongoni mwa watakaotapeliwa au
kupoteza fedha zao kwa kuamua
kutafuta taarifa za kutosha ili
kujiridhisha kabla hujawekeza fedha
zako huko.

Tafuta watu unaowaaamini


waliofanikiwa katika hiyo Online
Business na uwaulize maswali
wakusaidie, hudhuria kozi mbalimbali

67
kupitia mtandaoni ikiwezekana
uwekeze ukiwa na ufahamu wa
kutosha (full details).

Unahitaji ufahamu wa aina mbili, aina


ya kwanza ni ule unaohusu jinsi
biashara inavyoendeshwa na aina ya
pili ni jinsi faida inavyopatikana. Haya
mawili yatakusaidia kujua kama unao
uwezo wa kushiriki au la.

Kama unataka kufanya biashara


tofauti na ya mtandaoni bado utahitaji
kuwa na ufahamu wa kutosha juu ya
uwekezaji utakaofanya, kiwango
chako cha ufahamu kinakupunguzia
hofu lakini pia kinakuongezea utulivu
wakati wa uwekezaji wako.

68
Hakikisha unaepuka kosa la kufanya
uwekezaji mahali ambapo hauna
ufahamu wa kutosha kuhusu mahali
hapo, haufanikiwi kwa sababu tu
umewekeza, ila unafanikiwa kwa
sababu una ufahamu wa kutosha juu
ya eneo ulilowekeza.
Kosa la Tano;
Kupuuzia elimu ya fedha
(Not giving priority to financial
education)
Katika kitabu chakekinachoitwa
Increase Your Fnancial IQ (Ongeza
Kiwango chako cha Ufahamu
kuhusiana na Fedha) ndugu Robert
Kiyosaki anasema Kati ya mambo
yanayoathiri hali ya kifedha ya mtu
yeyote moja ya mambo hayo ni
ufahamu wake Kuhusu Fedha

69
Na kutokuwa na ufahamu kuhusu
fedha ndicho kitu
kinachowatofautisha watu wanaofeli
na wanaofanikiwa kifedha, kwahiyo
kama unataka kuwa mmoja kati ya
wakataofanikiwa sana kifedha epuka
kosa la kupuuzia elimu ya fedha.

Watu wote wanatafuta fedha, cha


ajabu sio wengi ambao wanajibidiisha
katika kutafuta elimu ya fedha ili
iwasaidie katika maisha yao.

Na kwa bahati mbaya sana, elimu ya


fedha haifundishwi shuleni na ndio
maana hata watu waliosoma na
kufanikiwa sana katika taaluma zao
wakati mwingine na wao wana

70
changamoto za kifedha kama
wengine ambao hawajasoma sana.

Kwa sababu ya kukosa maarifa ya


kifedha, watu hufanikiwa kupata
fedha ila wanafeli kwenye namna ya
kuzitunza na kuzilinda ili zisipotee.

Kumbuka, kadri unavyozidi kuweka


juhudi katika kutafuta maarifa
yahusuyo fedha ndivyo
unavyopunguza uwezekano wa
kufanya makosa ya kifedha
yanayotokana na kitendo cha kukosa
ufahamu na maarifa.

71
Sura Ya Tano
Kanuni Muhimu Unazotakiwa
kuzitumia, Ili zikupe Mafanikio ya
Kifedha
(The Golden Rules, For Financial
Success)

Mafanikio ya kifedha sio suala la


bahati wala sio muujiza; mafanikio ya
kifedha ni matokeo ya kanuni
zilizotumika ipasavyo.

Ndio maana kuna watu wana elimu


kubwa, kuna watu wanajihusisha sana
na mambo ya Mungu ila bado wana
matatizo mengi ya kifedha kuliko mtu
wa kawaida.

72
Kimsingi, kuna kanuni nyingi sana
zinazotawala maisha hizi zinaitwa
Universal Laws of Success (kanuni
zinaotawala maisha kwa ujumla)
halafu kuna kanuni maalum
zinazotawala maeneo fulani (Specific
laws that govern certain areas).

Sura hii imejikita zaidi katika kuelezea


kanuni zinazotawala eneo la fedha
Money Governing Laws kanuni hizi
zimepimwa na watafiti mbalimbali na
kubainika kuwa ndizo zilizochangia
mafanikio ya kifedha kwa wengi na
zinakwenda kukufanikisha hata wewe
pia ukizitumia.

Hii ni kwa sababu haufanikiwi kifedha


kwa sababu yoyote ile, ila

73
unafanikiwa kifedha kwa sababu
unafuata kanuni.
Kanuni ya kwanza;
Money=value=Money

Kanuni hii inasema kwamba, fedha ni


sawasawa na thamani, lakini pia
thamani ni sawasawa na fedha.

Kuna tafsiri kubwa mbili kuhusu


fedha, ya kwanza inasema money is
transaction of value (Fedha ni
mbadilishano wa Thamani) nay a pili
inasema Money is a reward that a
person is given after solving a certain
problem (Fedha ni zawadi ambayo
mtu hupewa mara baada ya kutatua
tatizo fulani).

74
Jim Rohn aliwahi kusema kwamba
You are not paid because of TIME
you spent in doing something, but
because of the VALUE you bring
(haulipwi kwa sababu ya MUDA
unaotumia kufanya kitu, ila kwa
sababu ya THAMANI uliyonayo au
unayozalisha).

Kwa maana iliyo nyepesi ni kwamba,


kiasi cha malipo ambacho unaweza
kupewa kinaamuliwa na thamani
unayotoa ukipewa nafasi ya kufanya
kitu na sio ugumu wa kazi au muda
uliotumia.

Kwa maneno mengine ni sawa na


kusema kwamba, kama leo hauna
fedha sio kwamba mtaani fedha
hakuna ila ni kwa sababu

75
haujaonesha thamani uliyonayo ili
kuifanya fedha ivutike kuja upande
wako, katika sura inayofuata
utajifunza Mambo yatakayokusaidia
Kuivutia fedha katika maisha yako

Kumbuka, kama unataka


kutengeneza fedha hakikisha
unatafuta kwa bidii kuwa mtu
mwenye thamani, dunia haikupi fedha
kwa sababu inakuonea huruma au
kwa upendeleo, inakupa fedha
kulingana na thamani uliyonayo.

Mwandishi nguli na mwalimu


aliyebobea sana katika masuala ya
maisha na mafanikio Dr Myles
Munroe aliwahi kusema kwamba If
you want to become successful,

76
become a person of Value kama
unataka kufanikiwa, usipoteze nguvu
na muda wako kutafuta mafanikio,
tafuta kuwa mtu wa thamani na
mafanikio yatakufuata.

Ni thamani ndiyo inawafanya


wafanyakai wawili katika kampuni
moja kulipwa mishahara tofauti, ni
thamani ndio inayafanya makampuni
mawili yanayozalisha bidhaa
zinazofanana kutofautiana katika
mauzo yao.

Uzuri ni kwamba, kadri ambavyo


utajiongezea THAMANI ndivyo
unajiweka katika nafasi nzuri ya
kupata FEDHA

77
Kanuni ya Pili;
Par
Independence.

C, Northcote Parkson alikuja na


kanuni inayosema kuwa Expenses
Always Rise To Meet an Income
(Mara zote matumizi huongezeka ili
yakutane na kipato au matumizi
huongezeka kadri ambavyo kipato
kinaongezeka).

Kuna watu ambao kipato chao cha


sasa ni kikubwa kuliko kile
walichokuwa wanaingiza hapo
mwanzo, cha ajabu ni kwamba
pamoja na kuongezeka kwa kipato
chao bado wanakutana na ugumu
waliokuwa wakikutana nao kabla
kipato chao hakijaongezeka.

78
Yaani, ni kama kuongezeka kwa
kipato hakujaleta mabadiliko yoyote,
ni kweli kipato chao kimekuwa lakini
bado kinaonekana kama hakitoshi.

Kanuni hii inasema kuwa fedha


haijawahi kutosha, kwa sababu kadri
ambavyo inaongezeka ndivyo
ambavyo matumizi huongezeka pia,
matumizi huongezeka kwa
kubadilisha mfumo wa maisha au kwa
kuongeza maeneo ambayo fedha
inatumika.

Hii ndio sababu kwanini watu


wanabadilisha simu, wanabadilisha
nyumba walizokuwa wakiishi,
wanabadilisha aina ya uvaaji na
maeneo wanapokwenda kula,
wengine huacha kupika chakula na

79
kuanza kula chakula kilichopikwa
tayari ambacho ni gharama.

Kama unataka kufanikiwa unatakiwa


kuivunja hii kanuni na kuenenda
kinyume nayo kwa kufanya mambo
yafuatayo.
1. Kutokuongeza matumizi kabisa
Tumeangalia kuwa watu wengi
huongeza matumizi kadri ambavyo
kipato chao kinaongezeka, kufanya
hivyo kunaongeza ugumu na
kukaribisha matatizo ya kifedha
mengi zaidi.

Wewe unatakiwa kuhakikisha


hauongezi matumizi, hii itakusaidia
kuishi katika mfumo uleule wa maisha
na kile kipato kilichoongezeka

80
kukitumia kwaajili ya mambo ya
maendeleo.

Kulingana na utafiti uliofanywa na


Morgan Housel katika kitabu chake
cha The Psychology Of Money
(Saikolojia ya Pesa) imethibitika
kwamba Pesa isipowekewa mikakati
huwa ina tabia ya kujiendesha
kimatumizi.

Tafsiri yake ni kwamba kama


usipoweka mikakati wa kutokuongeza
matumizi basi utajikuta umelazimika
kuenenda sawasawa na matumizi
yaliyoongezwa na fedha.

Law of Compesation inasema kama


ukifeli kupanga basi umepanga kufeli
na kufeli kutachukua nafasi kwahiyo

81
kama usipoweka nia ya kutokuongeza
matumizi basi matumizi yatajiongeza
yenyewe bila kujua, ni lazima uweke
nia thabiti na dhamira kuwa matumizi
yako yatabaki vilevile licha ya
kuongezeka kwa kipato chako.
2. Kuongeza matumizi kwa kiwango
Kidogo.
Ikiwa utshindwa kabisa kuyaacha
matumizi yako yabaki kama
yalivyokuwa kabla kipato chako
hakijaongezeka basi unaweza
kuamua kuwa utaongeza matumizi
lakini kwa kiwango kidogo.

Lengo la kufanya hivyo ni kupata


kipato cha ziada utakachowekeza
pamoja na kuweka akiba bila kuathiri
maisha yako ya kila siku.

82
Utakapokuwa unaongeza matumizi
unatakiwa kuongeza kwa kuzingatia
maeneo muhimu, mfano kuongezeka
kwa gharama za uendeshaji wa
shughuli zako ili kuongeza uzalishaji
zaidi.

Kama leo kipato chako kimeongezeka


kwa asilimia 20% basi matumizi yako
yanatakiwa kuongezeka chini ya
asilimia 50% ya ongezeko la pato
lako.

Mfano: kipato chako cha mwanzo


kilikuwa ni 500,000 na kikaongezeka
kwa asilimia 20% (100,000) na
unatakiwa kuongeza kipato chako
kwa asilimia zilizo chini ya 50% ya
ongezeko la pato lako.

83
Tafsiri yake utatakiwa kuongeza
matumizi chini ya shilingi 50,000 au
yasizidi shilingi 50,000 ili kiasi
kinachobaki katika ongezeko la pato
kitumike kama sehemu ya akiba na
uwekezaji.
3. Ongeza kipato Zaidi.
Ikitokea, kipato chako kimeongezeka
na ongezeko la kipato chako likaja na
ongezeko la matumizi la lazima kiasi
kwamba ukakosa kiasi cha kuweka
akiba pamoja na kuwekeza basi
utalazimika kutafuta njia ya kuongeza
kipato.

Hii ni kwa sababu, kiashiria


kimojawapo cha dalili mbaya ya
kifedha ni pale ambapo unafanya kazi
na fedha yako yote unayopata
inaishia katika matumizi, kama una
84
hiyo changamoto nashauri utafute
namna ya kuongeza kipato kwa
kutengeneza mferejeji mpya
utakaokuingizia fedha (New Stream
Of Income).
Kanuni ya Tatu;
Triangulation of Financial Decision
(50/30/20 Rule)

Kanuni hii inasema hivi, katika kila


fedha utakayopata unatakiwa
kuifanyia maamuzi makubwa matatu
kuihusu. Kanuni hii imeelezewa kwa
namna tofautitofauti na wataalamu
mwalimbali.

Elizabeth Warren anasema 50%


inatakiwa kuwa ni kwaajili ya
matumizi ya lazima (needs) 30%
inatakiwa kuwa ni kwaajili ya

85
matumizi yasiyo ya lazima (wants) na
20% inatakiwa kuwa ni kwaajili ya
akiba na uwekezajji
(Saving&Investment).

George Clackson anasema 50%


inatakiwa kutumika katika akiba na
uwekezaji, 30% inatakiwa kutumika
katika mahitaji muhimu huku 20%
ikitumika katika matumizi yasiyo ya
lazima.

Hitimisho la pamoja: kiasi cha


kuwekeza, kiasi cha akiba na
matumizi hakiwezi kulingana kwa
sababu hata mapato hayalingani kwa
wote, kinatofautiana kutoka mtu
mmoja na mwingine kulingana na
kipaumbele cha kila mmoja.

86
Lengo ni kukuonesha jinsi
unavyotakiwa kukigawa kipato chako
na kuwa na maamuzi nacho (taking
Control of Over Your Income).

Mfano: Kama utaamua kuwekeza na


kuweka akiba kwa kutumia 20% ya
kipato chako huku 50% na 30%
ukiitumia katika mahitaji muhimu
pamoja na yale yasiyo muhimu
unaweza kuamua kupunguza kiasi
katika maeneo hayo mawili na
kuongeza katika eneo la akiba na
uwekezaji.

Ili uweze kufanikiwa katika hili


unatakiwa kufanya mambo makubwa
mawili.

87
Jambo la kwanza ni kujua jumla ya
kipato chako kwa siku, wiki au mwezi,
hii ni hatua mojawapo ya ufahamu
(Awareness Level) ambayo
itakusaidia sana kufanya maamuzi.

Hauwezi kujua asilimia 50% ya kipato


chako ni shilingi ngapi ikiwa haujui
jumla ya pato unalopata.

Jambo la pili ni kuamua namna


utakavyofanya maamuzi ya kipato
chako kila utakapopata.

Hii ni hatua ya pili ya utendaji


(Practice Level) ambayo inatanguliwa
na hatua ya kwanza ya kuwa na
ufahamu.

88
Mfano: katika hatua ya kwanza
umebaini kuwa jumla ya kipato chako
ni shilingi 1,000,000.

Kwahiyo 50% itakuwa ni 500,000,


30% itakuwa ni 300,000 na 20%
itakuwa ni 200,000.

Kwahiyo, itakuwa kama ambavyo


jedwali linaonesha:

1: (Kwa Mujibu wa Elizabeth Warren)


50% 30% 20%
Matumizi Matumizi Akiba na
ya lazima yasiyo ya uwekezaji
(Needs) lazima (Saving &
(Wants) Investment)
500,000 300,000 200,000

89
2: (Kwa mujibu wa George Clackson)
50% 30% 20%
Akiba na Matumizi Natumiz
uwekezaji ya lazima i yasiyo
(saving&Investme (Needs) ya
nt) lazima
(wants)
500,000 300,000 200,00
0

Kumbuka, Haufanikiwi kifedha Kwa


sababu unaingiza kiasi kikubwa, ila
unafanikiwa kwa sababu unabakisha
kiasi kikubwa kwaajili ya akiba na
uwekezaji mara baada ya kufanya
matumizi yako muhimu.

90
Namna ya kuitumia hii kanuni ili ikupe
matokeo.
Imebainika kwamba watu wote
wanaujua umuhimu wa kuweka akiba
na uwekezaji lakini bado sio wengi
waliofanikiwa kufanya hivyo.

Wengi huja kushtukia kuwa


wanatakiwa kuweka akiba na
kuwekeza wakati huo fedha zote
zimetumika na kuisha au zimebaki za
kusukumia siku wakati wanasubiri
kupata fedha nyingine.

Kwa mujibu wa saikolojia ya fedha


imebainishwa kuwa binadamu
hufanya matumizi kulingana na hela
aliyonayo katika akili yake.

91
Hii ni kusema kwamba, akili ya
mwanadamu huwa inapanga namna
ya kuitumia fedha kulingana na fedha
iliyopo mfukoni au katika akaunti, ndio
maana wengi wakianza kutumia fedha
huwa wanatumia hadi inaisha ndipo
huja kukumbuka kuwa walitakiwa
kutenga kiasi cha kuweka akiba
pamoja na kufanya uwekezaji.

Njia rahisi ya kuepukana na hii


changamoto inayowakumba wengi ni
kutumia mbinu ya Prior Expenditures
Exclusion (Mbinu ya kutenga kiasi
Fulani kabla ya kufanya MATUMIZI).

Mbinu hii inasema kwamba, katika kila


fedha unayoipata na iliyo ya kwako,
kabla haujaanza kuitumia amua kiasi

92
utakachotenga kwaajili ya akiba na
uwekezaji na ufanye hivyo kabla.

Faida mojawapo ya kufanya hivi ni


kuilazimisha akili yako ifanye
matumizi kulingana na kiasi
kitakachobaki mara baada ya kutoa
kiasi kwaajili ya akiba na uwekezaji.

Katika kutekeleza hili unaweza


kutumia njia mbili, njia ya kwanza ni
kufungua akaunti ambayo kila
utakapopata fedha utakwenda
kuiweka huko kama akiba na akaunti
hiyo hautakuwa na mamlaka ya kuitoa
hiyo fedha mpaka baada ya muda
Fulani kupita.

93
Njia ya pili ni kutumia makato ya juu
kwa juu, hapa unalazimika kuwaambia
benki kwamba mara baada ya
kupokea fedha katika akaunti yako
wao wakate kiasi fulani na kukiweka
katika akaunti yako ya akiba na
uwekezaji.

Njia zote ni nzuri, ila hii ya pili ni nzuri


zaidi na nimeitumia hata mimi na
imenisaidia sana,

Faida ya njia hii ni kwamba kwanza


inaokoa muda wa wewe kwenda
benki kufanya muamala, lakini pia
inakuhakikishia kufanikiwa katika
lengo lako kwa sababu inakuwa
katika mikono ya watu wengine
ambao wao ni kazi yao kukusaidia
wewe kutimiza lengo ulilojiwekea.

94
Kanuni ya Tatu;
Law of Compound Interests

Kama umewahi kukopa fedha ambayo


ulitakiwa kuirejesha kwa riba baada
ya muda fulani utakuwa unafahamu
kuwa kadri ambavyo ulizidi kukaa na
hiyo fedha ndivyo ilivyozidi
kuongezeka.

Hii inaitwa kanuni ya mlimbikizo


ambayo katika kitabu chake cha The
Power of Compound ndugu Darren
Hardy ameitafsiri kama There is huge
reaping from small actions that can
be done repeatedly over time

Yaani, kuna mavuno makubwa kutoka


katika vitendo vidogovidogo

95
vinavyotendeka kwa muda mrefu kwa
kujirudiaruida.

Kwa mujibu wa hii kanuni ni kwamba,


fedha kubwa ni muunganiko wa fedha
ndogondogo nyingi zilizokusanywa
kwa muda mrefu.

Hii ni sawasawa na kusema kwamba,


kila unaemuona ana uwekezaji
mkubwa, amefanikiwa kifedha alianza
kukusanya fedha kidogokidogo na
hapa ndipo ule msemo wa Kiswahili
unaosema haba na haba hujaza
kibaba unapothibitisha ukweli wake.

Yawekenaka unataka kuanza kuweka


akiba ila unaona kama hauna uwezo
wa kuweka kiasi kikubwa, anza na
kiasi unachoweza kuweka hivi sasa,
96
kama ni kuwekeza anza na
hichohicho kiasi kidogo ulichonacho.

Usisahau maneno ya Lao Tzu


yanayosema A journey of Thousand
miles begins with a songle step
(safari ya maili elfu moja inaanza na
hatua moja).

Hakikisha katika safari yako ya


kuelekea mafanikio ya kifedha uwe ni
mtu unaepiga hatua kila mara bila
kujali ni ndogo kiasi gani, baada ya
muda utajikuta umefika mahali
ambapo usingefika kama usingekuwa
na ujasiri wa kupiga hatua
ndogondogo.

97
Kanuni ya Nne;
Law of Conservative
Kanuni hii inasema kwamba, Wealth
creation is an outcomes of keeping
much money (mafanikio ya kifedha ni
matokeo ya kubakisha kiasi kikubwa
baada ya kupokea pato lako la siku,
wiki au mwezi).

Unachotakiwa kujua ni kwamba,


haufanikiwi kifedha kwa sababu
unapokea mshahara au kipato
kikubwa, ila unafanikiwa kwa sababu
unaweza kubakiza kiasi fulani katika
kile unachopata.

Dalili mojawapo ya mtu anaefanikiwa


kifedha ni uwezo wa kubakisha kiasi
fulani cha fedha na dalili ya mtu

98
anaekaribia kufeli ni ile hali ya
kutumia fedha yote anayopata bila
kubakisha kiasi chochote, wewe upo
katika kundi gani?

Msingi mkubwa wa mafanikio ya


kifedha haupo katika kupata mapato
makubwa ila upo katika kuweza
kubakiza kiasi fuulani cha fedha kabla
au baada ya matumizi ya siku, wiki,
mwezi au mwaka.

Yaani, kama unalipwa shilingi


5,000,000 na unaimaliza yote katika
matumizi yako umezidiwa mafanikio
na mtu anaelipwa shilingi 500,000 na
anabakisha kiasi fulani.

99
Kama unataka kufanikiwa kifedha
hakikisha kila wakati unakuwa ni mtu
ambae unalazimisha matumizi yako
yasilingane au kuzidi kipato chako,
yaani kipato chako kisiishie katika
matumizi.
Kanuni ya Tano;
Law of cause and effect
Kwa mujibu wa hii kanuni ni kwamba,
kuna kichocheo katika kila hali
ambayo mtu anapitia kifedha (there is
cause in every situation).

Yaani, hakuna namna masikini


anaweza kuwa tajiri kama hatofanya
mambo ambayo matajiri waliyafanya
walipokuwa masikini ndipo
yakawafanya wao wawe matajiri.
Lakini pia endapo matajiri wakifanya

100
mambo ambayo maskini hufanya
baada ya muda watarudi katika
umaskini wao.

Kwa lugha rahisi ni kwamba kanuni hii


inakanusha neno bahati mbaya kwa
kuonesha kwamba, kila hali katika
maisha imechochewa ndipo ikatokea.

Kama unataka kufanikiwa kifedha


utalazimika kujua mambo
yanayoweza kuchochea mafanikio ya
kifedha na uyafanye mambo hayo.

Katika kitabu chake kinachoitwa


Million Dollar Habit (tabia za watu
waliofanikiwa kifedha) Brian Tracy
ameonesha ni kwa namna gani kuna
utofauti mkubwa sana wa kitabia kati
ya matajiri na maskini.
101
Ni ukweli usiopingika kwamba,
masikini wana tabia ambazo
zinawafanya waendelee kuwa maskini
na matajiri wana tabia zinazowafanya
wawe matajiri.

Mojawapo ya tabia kubwa


inayowafelisha wengi ni tabia ya
kuwa na matumizi yanayolingana au
yanayozidi mapato.

Ili kujihakikisha kuwa unafanikiwa


kifedha ni muhimu sana kuhakikisha
kuwa matumizi yako hayalingani wala
kuzidi mapato yako, ukifanya hivyo
baada ya muda fulani utakuwa
umepiga hatua kubwa sana.
Kama utanaza kujenga tabia
zilizowasaidia wengine kufanikiwa
102
kifedha baada ya muda nawewe
utafanikiwa pia lakini pia kama
utaendelea kuzipuuza utaendelea
kubaki vile ulivyo leo bila kupiga
hatua yoyote ile.

Hakikisha kila unachofanya kuhusu


fedha kinachochea mafanikio yako
yatakayoonekana baada ya muda
fulani, usipofanya hivyo utakuwa
unachochea kufeli na kuanguka
kwako. Kumbuka kila matokeo
yamesukumwa na kichocheo fulani,
kama unataka kubadilisha matokeo
badilisha kichocheo.

103
Kanuni ya Sita;
Law of Accumulation
Mkurugenzi wa kampuni ya
Mohammed Enerprises Mo Dewji
alihojiwa kwa kuulizwa ni kitu gani
kinachangia mafanikio yako ya
kifedha katika majibu yake alisema
nahakikisha fedha zangu zinatoka
katika vyanzo vingi nilivyowekeza
Hii ni kusema kwamba, hategemei
chanzo kimoja cha mapato, ila
muunganiko wa vyanzo vingi vya
mapato ndivyo vinamuwezesha kuwa
na mafanikio makubwa ya kifedha.

Kumbuka, Kama utakuwa


unategemea chanzo kimoja cha
mapato uko katika hatari endapo
chanzo hicho kimoja kitapata

104
changamoto lakini pia kitaelemewa
kwa sababu ni vigumu sana kutatua
matatizo yako yote ya kifedha kwa
kutegemea chanzo kimoja.

Chanzo ulichonacho leo unatakiwa


kukitumia kama chanzo cha awali
(primary Source) kutengeneza
vyanzo vingine vya fedha.

Msanii wa muziki Diamond Platnumz


alianza kukitumia kipaji chake kama
chanzo cha awali cha mapato na
kutoka katika kipato alichokuwa
akipata ndipo akatengeneza vyanzo
vingine kama wasafi Tv, wasafi Radio,
wasafiBet pamoja na vingine.

105
Yawezekana umeajiriwa, mshahara
unaoupata kutoka katika ajira yako
unaweza kuuwekea mikakati
ukakusaidia kutengeneza mfereji
mwingine wa fedha.

Ikiwa una chanzo chochote


kinachokuingizia fedha leo, unaweza
kukitumia hicho kama chanzo cha
awali kutengeneza chanzo kingine,
inawezekana kabisa na ndio maana
kuna watu wamefanikiwa ili kukupa
wewe ushuhuda kwamba hata wewe
unaweza kufanikiwa pia. (Some has
succeded as proof that you can as
well).

106
Kanuni ya Saba;
Law of Trade-Offs

Katika kitabu chake cha The 15


invaluable laws of growth cha kwake
John C Maxwell anatafsiri kanuni hii
kwa kusema ili kupata mafanikio
makubwa ya kifedha, utalazimika
kuweka mikakati ya makusudi ili
kuhakikisha unajinyima baadhi ya
mambo ili uwekeze (you must be
willing to to diminishing or losing one
quality, quantity, property or set of
design in return of gaining in other
aspect).

Matajiri ni watu ambao kwa namna


yoyote wanajinyima kufanya mambo
fulani yanayoweza kuwapa raha leo ili
kuiwekeza fedha katika mambo

107
ambayo yatawapatia faida kubwa
mbeleni.

Watu wengi wanasumbuliwa na hali


ya kutaka kuonekana na wengine
kwamba wamefanikiwa Social Proof
bila kujua kwamba kwa kufanya hivyo
wanapoteza fedha nyingi sana
ambazo wangezitumia katika
kuwekeza zingewaletea faida.

Kama unataka kupiga hatua, jitahidi


kadri uwezavyo uwe ni mtu mwenye
uwezo wa kuhimili hisia zako, ili usije
jikuta unaendeshwa na hisia za
kutaka kuonekana kwa kutumia fedha
zako katika mambo ambayo
hayakusaidii kupiga hatua zaidi.

108
Will Rodgers aliwahi kusema kwamba

Tunatumia fedha ambazo hatuna,


kununulia vitu tusivyovihitaji ili
kuwafanya wengine watuone kuwa
tuna fedha, kama unataka kufanikiwa
hakikisha wewe haufanyi hili kosa
ambalo limewagharimu wengi.

Badala ya kununua simu ya gharama


ili watu wakusifie nunua simu ya
kawaida na kiasi kingine kitumie
katika akiba na uwekezaji, kumbuka
kuwa jukumu la kuyafanya maisha
yako yawe bora ni la kwako wewe
mwenyewe.

109
Kila wakati kabla hujatumia fedha
yako jiulize hiki ninachofanya
kinachangiaje kunifanya nipate fedha
zaidi? lakini jiulize hiki ninachotaka
kufanya, kama nisipofanya
kinawezaje kuleta madhara?

Ukigundua kuwa hakileti madhara


usikifanye, hapa ndipo utagundua
kuna nguo hukutakiwa kununua, kuna
vitu hukutakiwa kumiliki, hukulijua hilo
kwa sababu hukujiuliza hayo maswali.

Kumbuka, Usipokuwa makini


unaweza tumia fedha nyingi sana ili
kujionesha kuwa una fedha jambo
ambalo litayaathiri maisha yako kwa
sehemu kubwa sana na
kukusababishia majuto baadae.

110
Kanuni ya Nane;
Law of Attraction
Kanuni hii inaelezea uhusiano uliopo
kati ya mafanikio ya kifedha na Imani
au mtazamo ambao mtu anao kuhusu
fedha.

Kanuni inasema kwamba, fedha


hujipeleka na kujisalimisha kwa watu
wanaoamini kwamba fedha zipo
ikwaajili yao na wanaweza kuzipata
endapo watazitafuta

Kupitia kitabu cha The Secrets of


Millionares Mind, Money Mindset
pamoja na The Psychology Of Money
vinafundisha kwamba, kiwango cha
mafanikio ya kifedha ambacho mtu
anacho kwa nje ni matokeo ya Imani

111
aliyonayo juu ya uwezekano wa yeye
kumiliki kiasi fulani.

Kama unaamini uwezo wa kumiliki


milioni moja hauna, hata ikitokea
ukapata millioni moja itashuka mpaka
ifike katika kiwango unachoamini
ndicho halali yako na ndicho
unachopaswa kumiliki, yaani hauwezi
kupata mkononi mwako kile ambacho
akili yako haiamini kwamba
inawezekana.

Mawazo yako, mtazamo wako, Imani


na fikra zako ni kama sumaku, Hii ni
kwa sababu mtazamo ulionao ndani
ndio huyafanya maisha yako ya nje
yawe ya aina fulani, law of
correspondace inasema hali ya mtu
ya nje ni matokeo ya vile alivyo ndani.

112
Usiwe aina ya mtu unaeamini kwamba
fedha ni chanzo cha uovu, ukiamini
hivyo kupitia Imani yako unaifukuza
fedha na fursa zinazoweza kukusaidia
kupata fedha.

Anza leo kubadilisha mtazamo ulionao


na fikra zako kuhusu fedha, amini
kwamba fedha ni chanzo cha majibu
mengi ikiwepo na chanzo cha maovu
mengi ikikosekana.

Lakini pia jiaminishe kuwa wewe ni


mmoja miongoni mwa wengi wenye
haki ya kufanikiwa sana kifedha, hata
kama unadhani kuwa wanaofanikiwa
kifedha ni wachache, basi amini
katika hao wachache wewe ni
mmojawapo.

113
Sura Ya Sita
Mambo yatakayokusaidia kuivutia
Fedha katika maisha yako
(How to Attract and Make Money
Chase You)

Umewahi kukuta watu wanalalamika


kwamba maisha magumu na fedha
hakuna? Bila shaka umewahi
kukutana na hiyo hali ya watu
kulalamika au hata wewe mwenyewe.

Ukweli ni kwamba, bila kujali watu


watalalamika kiasi gani kwa kusema
kwamba fedha hakuna, kuna watu
wakati huohuo wanaendelea kujipatia
fedha.

114
Wakati wa janga la Corona kulikuwa
na malalamiko mengi sana juu ya
kushuka kwa uchumi, kudhoofika kwa
mzunguko wa fedha na maisha kuwa
magumu, wakati huohuo kuna watu
waliendelea kupata fedha.

Kuna mambo kadhaa ambayo


ukiyajua na kuyafanyia kazi
yatakusaidia kuivutia fedha katika
maisha yako hata kama wengine
watakuwa wakilalamika kuwa fedha
haipatikani.
Jambo la kwanza: Ujuzi

Tafiti kadhaa zimeonesha kuwa watu


wenye ujuzi wana nafasi kubwa ya
kuivutia fedha katika maisha yao na
wamekuwa wakitengeneza fedha

115
nyingi zaidi kutoka katika ujuzi
walionao.

Kwahiyo, ili na wewe uweze kuivutia


fedha katika maisha yako utalazimika
kuwa na ujuzi na kama hautajibidiisha
kutafuta ujuzi sio rahisi kuivutia fedha
katika maisha yako, kwa sababu
fedha inavutika zaidi kwa watu wenye
ujuzi.

Wakati unatafuta ujuzi kuna aina ya


ujuzi unaolipa zaidi (The most
profitable Skills) na aina hii ya ujuzi ni
ule tuliojifunza katika sura ya pili,
(kama umesahau rudi ukajikumbushe)

Inahitaji kujitoa, nidhamu na kufanya


kwa muendelezo ili ufike hatua ya
kuwa mbobevu katika ujuzi fulani ili

116
watu wengine wakutafute na wawe
tayari kukulipa.

Jiulize, ni aina gani ya ujuzi utaanza


kuujenga ambao utakusaidia kuvutia
fedha zaidi?

Na kama una ujuzi wowote


unaohitajika lakini bado haupati fedha
kupitia huo yawezekana kuna mambo
yafuatayo hujayaweka sawa.

Moja, hujaunoa vya kutosha kiasi cha


watu kuwa tayari kukulipa, hii ni kwa
sababu wanalipwa watu ambao ni
wabobevu wa mambo.

Utalazimika kuwa mbobevu zaidi ya


washindani wako, ili uonekane kirahisi
na uweze kulipwa vizuri.

117
Mbili, Hujautangaza ujuzi ulionao vya
kutosha katika maeneo ambapo
unahitajika, kama una ujuzi na hakuna
anaejua kama unao hakuna namna
unaweza kupata fedha, wafanye watu
wajue kama wewe una ujuzi
unaoweza kuwasaidia wao kutatua
kitu fulani.

Tatu, Umepungukiwa ujuzi wa


kimasoko na mauzo, yaani
umeshindwa kuugeuza ujuzi wako
kuwa fedha.

Kuwa na ujuzi ni jambo moja, ila


kuuuza ujuzi wako kiasi cha watu
kuwa tayari kukulipa ni jambo jingine,
ukigundua kuwa umepungukiwa
uwezo wa namna hiyo hakikisha
unaanza kuujenga mara moja.

118
Jambo la pili: Thamani
Tumeumbwa na Mungu mmoja ambae
mbele zake sisi zote tuna thamani
sawa ila duniani hapa hatulingani
thamani (isome hii sentensi mara mbili
kabla hujaendelea mbele).

Kuna wale ambao wamekubali


thamani yao ibaki vilevile ilivyo na
kuna wengine ambao wameamua
kuongeza thamani yao, sijajua wewe
upo kundi gani kati ya haya mawili.

Kama leo unalipwa 300,000 tafsiri


yake ni kwamba thamani yako ni hiyo
(hicho ndicho kiasi unachopaswa
kulipwa).

119
Kama unataka kulipwa zaidi ni lazima
ufanye jitihada za kujiongezea
thamani zaidi ya ile uko nayo leo.

Unachotakiwa kufahamu ni kwamba,


kila mtu anaweza kuamua thamani
anayotaka kuwa nayo na watu
wakamlipa kulingana na thamani
yake, kama leo usipoamua thamani
unayotaka kuwa nayo watu
watakuamulia na watakulipa
wanavyotaka wao.

Unachotakiwa kufahamu ni kwamba,


haulipwi kile unachotaka, unalipwa
kulingana na thamani yako, kama
unataka kulipwa na kupata fedha
zaidi hakikisha unajiongeza thamani
zaidi.

120
Kuna mambo mawili yanayoamua
thamani yako, jambo la kwanza ni
upekee ulionao, kuna watu ambao
umesoma nao kozi moja, mna
majukumu sawa na mnafanya kazi
moja ila mnalipwa tofauti kwa sababu
ya upekee ambao kila mmoja anao.

Jambo la pili ni kile unachoweza


kutoa (what you can deliver) kama
unataka kuongeza thamani
itakayokusaidia kulipia fedha zaidi
basi hakikisha katika kila eneo
utakalowekwa unaweza kufanya kitu
kizuri ili kushawishi fedha zaidi ije
upande wako.

Kumbuka, kuna watu wengi


wanaofanya kile unafanya na wapo
wengi waliosomea ulichosomea, ili

121
uweze kuwa wa tofauti ni lazima uwe
na matokeo ya tofauti.

Hii ndio sababu kuna wachezaji wa


mpira wanaocheza timu moja ila
wanalipwa kiasi tofauti,
kinachowatofautisha ni kile ambacho
kila mmoja anafanya akiingia uwanjani
na mchango alionao katika timu
husika.

Jiulize, ni thamani gani unayopeleka


katika eneo lako la kazi, katika
biashara au katika eneo lolote lile ili
ikusaidie kuvutia fedha zaidi.

122
Sura ya Saba
Mambo Makubwa 3 Yanayoweza
Kuathiri Hali Yako Ya Kifedha

Kimsingi, hali yako ya kifedha


inaamuliwa na mambo makubwa
matatu, mambo haya ndiyo yanaweza
kuamua uwe mtu utakaefanikiwa sana
kifedha au usifanikiwe.

Ukiweza kuyashughulikia maeneo


haya sawasawa na maelekezo
utakayopata katika sura hii sina shaka
utafanikiwa sana katika eneo la
fedha.
Jambo la kwanza;
Fikra (Money Mindset)
Wataalamu wa masuala ya mafanikio
wamefanya utafiti na katika tafiti zao

123
ikabainika kuwa hali ambayo
mwanadamu anayo kwa nje ni
matokeo ya hali aliyonayo kwa ndani,
na hata kama ataigiza kwa nje; baada
ya muda hali halisi ya ndani
itajidhihirisha tu.

Hii ni kusema kwamba, mtu yeyote


aliyefanikiwa kifedha lazima alianza
kwanza kushughulika na fikra
alizonazo kuhusu fedha.

Kuna aina mbili za fikra ambazo


unatakiwa utumie mojawapo kati ya
hizo, kama kweli umedhamiria kupata
mafanikio ya kifedha.

124
Aina ya kwanza ni fikra za uhaba
(Scrarcity Mindset)
Mtu yeyote mwenye fikra za namna
hii ni yule anaeamini kuwa fedha
hazitoshi, fedha hazipatikani kirahisi,
fedha zipo mikononi mwa watu
wachache tu.

Mtu mwenye fikra za namna hii


anaamini kuwa hakuna fedha za
kumtosha kila mtu, anaamini hawezi
kupata mafanikio ya kifedha
makubwa zaidi ya yale aliyonayo hivi
sasa, kama wewe una fikra za aina hii
nakushauri uhame haraka na uhamie
katika fikra za aina ya pili
utakazojifunza hivi karibuni.

125
Watu wenye fikra za namna hii
wanaamini kuwa wao wana fedha
chache kwa sababu kiasi kingi cha
fedha kipo katika mikono ya matajiri,
kwa maneno mengine wanaamini
kuwa umaskini wao umesababishwa
na matajiri wachache jambo ambalo
sio kweli.

Brian Tracy katika kitabu chake cha


21 secrets Success of Self Made
Millionaire anasema There is no
limit, except the limit you place on
yourself, by your own thinking
(Hakuna mipaka, isipokuwa ile
uliyojiiwekea wewe mwenyewe kwa
fikra zako).

126
Aina ya pili ni fikra za utoshelevu
(Abundance Mindset)
Mtu mwenye fikra za aina hii anazo
juhudi za utafutaji kwa kutumia
maarifa na mbinu sahihi huku
akiongozwa na Imani kuwa fedha
itapatikana kwa sababu ipo ya
kutosha.

Mtu mwenye fikra za namna hii ana


uwezo na nafasi kubwa sana ya
kujitengenezea fedha mahali ambapo
wengine hawajaona kama kuna fedha
imejificha.

Fikra ni kama tochi, ukiwa na fikra za


utoshelevu zitakusaidia kuona fursa
na kuzitumia, ukiwa na fikra za uhaba
ni vigumu sana kuziona fursa hata

127
kama utakuwa mahali ambapo kuna
fursa za kutosha.

Kama ilivyo rahisi kutafuta fedha za


kutosha na ukazipata ukiwa na fikra
za utoshelevu ndivyo ilivyo vigumu
kufanikiwa kifedha ukiwa na fikra za
uhaba.
Jambo la pili;
Maarifa ya Kifedha (Financial
Literacy)
Aina ya maarifa na ufahamu ulionao
kuhusu fedha ina uwezo mkubwa wa
kuamua uwe mtu utakaefanikiwa
kifedha au uwe mtu utakaekuwa na
hali mbaya kifedha (poor financial
status).

128
Hali yako ya kifedha haiamuliwi na
kiwango chako cha elimu, inaamuliwa
na kiasi na ubora wa maaarifa
uliyonayo kuhusu fedha.

Brian Tracy katika kitabu chake


kinachoitwa Million Dollar Habits
ambacho kinafundisha juu ya sifa na
tabia ambazo watu waliofanikiwa
sana kifedha wanazo.

Sifa mojawapo ya watu hao ni watu


wenye maarifa na wanaendelea
kujikusanyia maarifa zaidi.

Maarifa uliyonayo kuhusu fedha


yatakusaidia kufanya mambo
yafuatayo.

129
1. Kuivuta fedha ije kwako, Watu
wenye maarifa na ufahamu kuhusu
masuala ya fedha wanao uwezo
mkubwa sana wa kupata fedha
ambayo hawana, hii ni kwa sababu
maarifa waliyonayo yanasimama
kama sumaku.

Maarifa waliyonayo yanawasaidia


kujua nini wanaweza kufanya
ambacho kitawasaidia kutengeneza
fedha.
2. Kuitunza fedha unayopata, Kama
hautakuwa na ufahamu wa kutosha ni
rahisi sana kupoteza fedha mara
baada ya kuipata, kuna watu wengi
ambao kwa kukosa ufahamu na
maarifa wamepoteza fedha nyingi
sana.

130
Wewe usiwe mmojawapo kwa
kutokutafuta maarifa, fedha inahitaji
ulinzi ili isipotee na ulinzi wa fedha
unategemea sana kiwango cha
maarifa aliyonayo mtu.

3. Kukigawa vyema kipato chako,


Katika sura zilizopita tumejifunza
maamuzi matatu ambayo unatakiwa
kufanya katika kila fedha inayopita
mikononi mwako na iliyo ya kwako,
kitu pekee kitakachokusaidia kufanya
na kulitekeleza hilo ni maarifa na
ufahamu ulionao, hauwezi kujua
namna sahihi ya kuigawanya fedha
yako ikiwa hauna ufahamu na maarifa
ya kutosha.

131
4. Kufanya tathimini na kuchukua
hatua. Maarifa ya kifedha
yatakusaidia kuwa mtu mwenye
uwezo wa kujifanyia tathimini na
upembuzi juu ya hali yako ya kifedha
ili uweze kujua unapiga hatua au
umekwama.

Mtu yeyote asiyefanya tathimini hana


uwezo wa kufanya maamuzi sahihi
yampasayo ili kurekebisha hali yake
ya kifedha.

Hii ni kwa sababu atakuwa hajui


anaingiza kiasi gani, anatumia kiasi
gani na kiasi gani kinabaki na
anafanyia nini, hii ndio sababu kubwa
watu wakipata fedha zinaishia kulipa
madeni na kufanyia matumizi ya
kawaida.

132
Na kwa sababu mtu hana maarifa
haoni kama hizo ni dalili mbaya na
kwamba kuna hatua anatakiwa
kuchukua haraka iwezekanavyo.
Jambo la Tatu:
Hali ya kiroho (Spiritual Factor)
Hali ya kiroho uliyonayo ina nafasi
kubwa sana ya kuamua hali yako ya
kifedha, kwa maneno mengine ni
kwamba kuna uhusiano mkubwa sana
kati ya hali ya kifedha aliyonayo mtu
na hali yake ya kiroho.

Ndio maana, kuna familia ukienda


utakuta wanafamilia wana hali fulani
ya maisha inayoendana na kufanana
kwa wengi katika familia hiyo.

133
Kuna familia ukienda utakuta kila
wanapokaribia kupata mafanikio
huwa kuna kitu kinaibuka na
kusambalatanisha mafanikio yao.

Kuna wakati mtu anaweka juhudi


ambazo ukiziziangalia unaona kabisa
kuwa huyu anastahili kufanikiwa, ila
ghafla kuna kitu kinatokea na
kuharibu kila kitu.

Inakuwa ni kama kuna kamba


zinamshikilia ili kumzuia asipige
hatua, kamba hizi mara nyingi ni
mambo yasiyoonekana katika hali ya
kawaida ambayo huwa yanaitwa
Invisible lopes .

Kuna watu ambao wanasumbuliwa na


roho za urabifu (destructive spirits)
134
pamoja na roho za utapanyaji
(wasting spirits).

Roho za uharibifu zinafanya kazi ya


kuharibu na kuvuruga kila mpango na
mradi ili kuhakikisha hakuna
mafanikio yanapatikana.

Roho za utapanyaji zinafanya kazi ya


kupoteza fedha inayopatikana, ndio
maana kuna watu wakishika fedha
inakuwa kama kuna upepo unawapitia
kiasi kwamba wanaelekeza fedha zao
katika maeneo ambayo
hayawazalishii faida na mwisho wa
siku wanakuwa wamepoteza fedha
nyingi bila wao kujua.

Ndio maana, kuna watu wanapata


fedha nyingi, ila ukiangalia maisha
135
yao ni kama hakuna mabadiliko
yoyote yanayotokea, hii ni kwa
sababu fedha wanapata sawa, ila
zinaisha katika maeneo ambayo
hayachangii chochote katika kukuza,
kuboresha na kuimarisha hali zao za
kifedha.

Ili mtu aweze kushughulikia hali ya


namna hii ni muhimu sana
kujikusanyia nguvu za kiroho ili
zikutane na ufahamu pamoja na
juhudi alizonazo ndipo apate
mafanikio, vinginevyo hakuna
kitakachofanikiwa.

Mmoja wa watu wenye mafanikio


makubwa ya kifedha alipoulizwa

katika kuchangia mafanikio ya

136
kifedha alijibu kuwa mtu yeyote
hatakiwi kulipuuzia, wala kuipuuzia
nguvu ya kiroho, kwani ina nafasi
kubwa sana katika kumletea
mafanikio na kumsaidia kuyatunza
huku yeye akidumu katika mafanikio
hayo .

Hii itoshe kukufanya usilichukulie


kiwepesi suala la kiroho na kulipuuzia
kana kwamba halina uzito, kuna
umuhimu mkubwa sana wa
kuunganisha vyanzo vyako vya
mapato na Baraka pamoja na nguvu
za Mungu.

137
Sura Ya Nane
Mambo Yatakayokusaidia Kuzilinda
na Kuzitunza Fedha zako Zisipotee
(How to Secure and Protect Your
Money)
There is battle to fight for you to
reach at the top, after reaching, there
is another battle to fight for you to
stay at the top (unatakiwa
kupambana ili ufike kileleni, ukifika
unatakiwa kupambana ili uendelee
kubaki kileleni).

Watu wengi tunajitahidi sana


kupambana ili kuhakikisha tunapata
fedha, baada ya kuzipata ni
wachache sana ambao huwa
wanaendelea kupambana ili

138
kuhakikisha wanazilinda fedha
walizopata ili zisipotee.

Kwa jinsi mfumo wa maisha ulivyo,


utagundua kwamba kuna mambo
mengi sana yamedhamiria kuichukua
fedha iliyo mfukoni au katika akaunti
yako, usipoiwekea ulinzi itatoka
kwako na kupotelea kusikojulikana.

Kuna vitu vinaitwa Money Stolers


hivi vinalenga kuiba fedha kutoka kwa
mtu mmoja, kuna watu wengi
walipata fedha na baada ya muda
wakazipoteza au kuzitumia katika
namna ambayo wanajutia mpaka leo.

Kuna mambo kadhaa yanaweza


kukusaidia kuzilinda na kuzitunza
fedha zako zisipotee ili usiwe mmoja
139
kati ya watu ambao huwa
wanapoteza fedha mara baada ya
kuzipata na kuishia kujuta.
1. Nguvu ya Kiroho (Spiritual Power)
Kuna uhusiano mkubwa sana kati ya
hali ya mtu ya kifedha na hali yake ya
kiroho, kuna watu ambao kila
wanapopata fedha huwa wanapatwa
na matatizo na baada ya matatizo
kuisha na fedha inakuwa imeisha kwa
sababu waliitumia katika kutatua
matatizo yaliyokuwa yanawakabili.

Katika hali ya namna hii, hiki ni


kiashiria kuwa kuna hali ya kiroho ya
mtu inayomfanya akumbwe na
matatizo kila anaposhika fedha,
baada ya fedha yoote kutumika katika

140
matatizo hayo ndipo na matatizo
hutoweka.

Yaani, fedha isipokuwepo kunakuwa


hakuna matatizo, fedha ikipatikana na
matatizo yanaibuka, ni kama vile
matatizo huwa yanasubiri fedha ije
ndipo na yenyewe yaanze.

Au, kuna watu ambao kila


wanapoanzisha mradi, huwa unaana
kwenda vizuri lakini baada ya muda
unaharibika, hii ni ishara kwamba
kuna kitu hakiko sawa.

Tatizo la namna hii linaweza


kushughulikiwa endapo muhusika
atapatiwa msaada wa kiroho.

141
Nguvu ya kiroho inakusaidia
kukuwekea uzio wa ulinzi (Protective
Fence) ambao kazi yake ni
kupambana na kila hali inayoweza
kujipanga kukudhoofisha au
kukuangusha.

Nguvu ya kiroho pia inakusaidia


kukabiliana na roho za uharibifu
(Destructive Spirits) pamoja na roho
ya kutapanya (Spirits of Waste).

2. Hisia Imara (Strong Emotions)


Nilipokuwa Nasoma kitabu
kinachoitwa SAIKOLOJIA YA FEDHA
(The Psychology Of Money)
kilichoandikwa na Morgan Housel
nilijifunza jambo moja la ajabu sana
kuhusu fedha.

142
Nilijifunza kwamba, fedha huwa ina
sauti, na ukiishika inaanza
kukuongelesha na kukuelekeza
namna gani inataka uitumie na
usipokuwa na hisia imara utaitumia
vile yenyewe inataka na sio vile
ambavyo wewe unataka.

Kwa kutokuwa na uimara wa kihisia,


watu wengi walipata fedha na
wakaanza kuzitumia katika namna
ambayo hawakukusudia walipokuwa
wanazitafuta.

Hii imewahi mtokea mtu mmoja,


aliomba mkopo ili kuboresha na
kukuza biashara yake, na baada ya
kuupata mkopo huo akaenda kununua
gari ya kutembelea jambo ambalo
lilimgharimu sana kwa sababu gari

143
haikuwa ikimzalishia fedha na bado
alitakiwa kulipa mkopo wake na riba.

Kiashiria kimojawapo kwamba una


hisia zisizo imara ni kuwa na
mchecheto wa kununua vitu (Impulse
Purchasing) yaani unakuwa ni mtu
unaenunua kila kinachokuja mbele
yako hata kama haukihitaji, ila
unaunua kwa sababu una fedha.

Kwa kutokuwa na hisia imara wengi


wamejikuta wakinunua vitu bila
mpangilio (Prompt Buying) hiki ni
kiashiria kuwa wanaendesha na fedha
na sio wao wanaiendesha fedha.

Kumbuka, usipokuwa na hisia imara


kuna mazingira yatakutaka ujioneshe
kuwa una fedha, na kadri

144
utakavyokuwa ukifanya hivyo ndivyo
fedha zitakavyokuwa zinatoweka
kwako na mwisho unaweza kuwa ni
mtu unaejutia na kujilaumu sana.
3. Bajeti na Malengo (Budget and
Goals)
Kama usipokuwa na malengo katika
maisha utajikuta unatumia kila fedha
inayopita katika mikono yako. Njia
rahisi kabisa ya kuzilinda fedha zako
zisipotee ni kuwa na malengo.

Kama hauna malengo tayari umekosa


jambo mojawapo ambalo ni la msingi
sana linaloweza kukusaidia kulinda
fedha zako, hii ni kwa sababu faida
mojawapo ya kuwa na malengo
yanakujengea nidhamu ya matumizi
(Spending Discpline).

145
Lakini pia, malengo yanakuonesha
mahali ambapo unatakiwa
kuzielekezea fedha zako (Focusing
Direction) kwa kukuonesha namna
gani uzitumie.

Wafanyakazi wawili wanaolipwa


mshahara sawa mmoja huweza
kutumia sehemu ya mshara wake
kuwekeza akiwa na lengo la
kuongeza kipato huku mwingine
akitumia fedha yote anayopata kwa
sababu hana malengo.
4. Ufahamu (Financial Literacy)
Mtu aliye na maarifa ana faida kubwa
sana, hii ni kwa sababu maarifa
yanamsaidia kujua namna sahihi ya
kutumia fedha zake na kumuwezesha

146
kufanya kila maamuzi yahusuyo fedha
kwa kuongozwa na ufahamu sahihi.

Hata katika kuwekeza, mtu mwenye


maarifa atawekeza kwa sababu kuna
ufahamu unamuongoza, na hii
inaweza kumsaidia kuepukana na
suala la kupoteza fedha zake.

Ripoti kadhaa zinaonesha kwamba,


matajiri ndio watu ambao huongoza
kwa kusoma vitabu kila mwaka,
nilipofuatilia ili kujua sababu ya wao
kusoma vitabu nikagundua kwamba
lengo lao ni kuwa na maarifa
yatakayowasaidia kulinda na
kuyatunza mafanikio
waliokwishakupata.

147
Unaweza ukafanikiwa kupata fedha,
ila kama hauna maarifa unaweza
jikuta unapoteza fedha zote
ulizotengeneza.

Ili kujihakikishia ulinzi wa kutosha


kuhusu fedha zako, ni muhimu kuwa
mtu ambae hautalichukulia kiwepesi
suala la maarifa yahusuyo usimamizi
wa fedha wala kulipuuzia.

148
Hitimisho
Mtu mmoja aliwahi kusema kwamba
having knowledge without practice,
is like knowing where to go without
get started; you can
yaani, kuwa na maarifa bila
kuyatendea kazi, ni sawasawa na
kujua mahali pakwenda huku ukiwa
hujachukua hatua, huwezi kufika
kokote na utabaki palepale.

Maarifa yaliyomo ndani ya kitabu hiki


ni siri zilizowasaidia watu wengi
kufanikiwa kifedha, nimezitumia na
zimeniletea matokeo makubwa na
ndio maana nikazileta kwako baada
ya kuthibitisha na kujiridhisha kuwa
zinafanya kazi.

149
Kama unataka kuungana na watu
ambao baada ya muda hali zao za
kifedha zitabadilika basi usiache
kutendea kazi kila ambacho
umejifunza ndani ya kitabu hiki.

Na ili kujihakikishia unapata matokeo


makubwa zaidi nashauri ukisome
kitabu hiki mara kwa mara.

150
Orodha ya Vitabu Vya Isaack
Nsumba
1. Sanaa Ya Utongozaji 01 |
Kinafundisha Namna Ya Kuwa
Mwanaume Mwenye Mvuto na
Ushawishi Kwa Mwanamke.

2. Sanaa Ya Utongozaji 02 |
Kinafundisha Namna Ya Kuwa
Mwanaume Mwenye Mvuto na
Ushawishi Kwa Mwanamke.

3. Money Passcode | Kinafundisha


Siri Zitakazokusaidia Kupata
Mafanikio ya Kifedha.

4. Biashara Mtandaoni | Kinafundisha


Muongozo Utakaokusaidia
Kujitengenezea Kipato Kupitia
Mtandao.

151
5. Huyu Ndiye | Kinafundisha
Muongozo Utakaokusaidia
Kumtambua Mwenzi Sahihi.

6. Muache Aende | Kinafundisha


Mbinu Za Kutumia Ili Kumsahau Mtu
Anaekuumiza, Asiyekupenda Wala
Kukuthamini.

7. Lugha Tano Za Msamaha |


Kinafundisha Namna Ya Kuomba
Msamaha Unaoponya Majeraha ya
Mwenzi wako na Kukufanya
Usamehewe.

8. Usimuache Aende Zake |


Kinafundisha Namna Ya Kumtunza Na
Kumlinda Mwenzi Wako Pamoja Na
Kudumisha Uhusiano Wenu.

152
9. The Golden Woman | Kinafundisha
Tabia Zinazomvutia Mwanaume Kwa
Mwanamke Na Namna Ya Kuwa
Mwanamke Wa Tofauti.

10. Mwanamke Mashine |


Knafundisha Uwezo Wa Kipekee Ulio
Ndani Ya Mwanamke Na Namna Ya
Kuutumia Ili Kuleta Mafanikio.

11. Emotional Muscles | Kinafundisha


Namna Ya Kukabiliana Na Hisia Kama
Vile Wivu, Hasira, Huzuni Pamoja Na
Hofu.
12. Boresha Mahusiano Yako |
Kinafundisha Mambo Ya Kufanya Ili
Uwe Na Mahusiano Bora Na
Utayoyafurahia.

153
13. Sanaa Ya Mawasiliao Katika
Mahusiano | Kinafundisha Namna Ya
Kuwasiliana Kwa Ufanisi Pamoja Na
Kutatua Changamoto Za
Kimawasiliano.

14. Maisha Ni Kusudi | Kinafundisha


Namna Ya Kuligundua Na Kuliishi
Kusudi La Kuumbwa Na Kuwepo
Kwako Dunaini.

15. Sanaa Ya Kutoa Na Kupokea


Katika Mahusiano | Kinafundisha
Namna Ya Kutoa Katika njia
Inayogusa Moyo wa Mpokeaji, Na
Kupokea Katika Namna Inayogusa
Moyo wa Mtoaji.

154
16. Dhihirisha Uanaume Wako |
Kinafundisha Namna Ya Kuwa Vile
Impasavyo Mwanaume Kuwa.

17. Mwongozo Wa Usomaji Wa


Vitabu | Kinafundisha Namna
Unavyoweza Kuwa Msomaji Mzuri Wa
Vitabu Na Nwenye Mafanikio Katika
Usomaji.

18. Namna Ya Kuuteka Moyo Wa


Mwanaume | Jinsi Ya Kumpata
Mwanaume Umtakae Au Kumteka
Mwanaume Uliyenae.

19. Hatua Za Kufuata Ili Kurudiana Na


Ex Wako | Kinafundisha Hatua Kwa
Hatua na Namna Unavyoweza

155
Kumrudisha Ex Wako Pamoja na
Kufufua Penzi Lililokufa Au Kupooza.

20. Shule Ya Biashara | Siri


Zitakzokusaidia Kufanikiwa Katika
Biashara Yako, Namna ya Kuisimamia
na Kuikuza.

NB: Vitabu vyote vimeandikwa kwa


lugha ya Kiswahili na unaweza
kuvipata kupitia namba 0654722733
(TUMA UJUMBE WHATSAPP).

156
Tembelea Mitandao Ya Kijamii Ya
Isaack Nsumba Ili Kujifunza Zaidi
Youtube: Isaack Nsumba
(Utapata VIDEO Nyingi Za
Kukufundisha Mambo Mbalimbali)

Instagram: Isaack Nsumba


(Utapata Mafunzo Kila Siku
Yatakayokusaidia)

Facebook: Isaack Nsumba


(Utapata Mafunzo Kila Siku Na Pia
Shuhuda Mbalimbali)

Twitter: Isaack Nsumba


(Utapata Mafunzo Kila Siku
Yatakayokusaidia)

157
Tiktok: Isaack Nsumba
(Utapata Video Fupifupi Kila Siku
Zenye Uwezo Wa Kukuongezea
Ufahamu Zaidi).

158
Kuhusu Mwandishi

Isaack Nsumba, ni mwandishi wa


vitabu, Makala na Muandaaji wa
Maudui (Content Creator) lakini pia ni
mwalimu mbobevu (An Expert
Teacher) katika masuala yoote
yanayohusu Mahusiano, Uchumba,
Ndoa, Malezi, Uchumi pamoja na
Uongozi.

Kitaaluma Isaaack ni muhitimu wa


masomo ya Sanaa na Elimu (Bachelor
of Arts with Education) kutoka Chuo
kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAINT
AUGUSTINE UNIVERSITY OF
TANZANIA).

Mwaka 2022 alitajwa kama


mwandishi bora chipukizi (The Best
Young Author) na kutunukiwa tuzo ya
159
mwandishi bora chipukizi Tanzania
(The Best Young Author Award in
Tanzania).

Isaack ni Mkurugenzi (Chief Executive


Officer) na mwanzilishi wa taasisi ya
Wisdom For Winning inayohusika na
utoaji wa elimu ya kujitambua, Elimu
ya Mahusiano, Uchumba, Ndoa,
Malezi, Uchumi pamoja na Uongozi
ambayo ndiyo anayoiongoza kwa
sasa.

Kwahiyo, ukiwa unamuhitaji kwaajili


ya semina za vijana, wanawake au
wanaume, semina uongozi, semina za
uchumi, fedha na biashara pamoja na
makongamano yoote ya kanisani
unaweza kuwasiliana na namba
zilizopo katika kitabu hiki kwa kutuma
kupitia whatsapp.

160

You might also like