Ebook Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako

You might also like

Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 176

KIPAJI

Joel Arthur Nanauka


Jinsi Ya Kusimamia Na
Kukuza Biashara Yako
(How To Manage and Grow Your Business)

Joel Arthur Nanauka


©2022 Joel Arthur Nanauka

Haki zote zimehifadhiwa. Huruhusiwi kunakili,


kudurufu au kutumia sehemu ya kitabu hiki bila idhini
ya mwandishi. Kufanya hivyo itakuwa ni ukiukwaji wa
haki za mwandishi, na ukiukwaji wa taratibu hii
unaweza kupelekea mashitaka toka kwa waandaaji wa
kazi hii.

Joel Arthur Nanauka


Dar-Es-Salaam, Tanzania. East Africa
Simu: +255 756 094 875 / 0745 252 670
Barua pepe: jnanauka@gmail.com
Tovuti: www.joelnanauka.com

Kimesanifiwa na Andrew Rwela


Simu: 0743 200 738
Barua pepe: rwelaandrew@gmail.com

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | i


YALIYOMO

Vitu Muhimu Vya Kufahamu Kabla Biashara Yako Haijakua 01


Jinsi Ya Kupata Fedha Za Kukuza Biashara Yako 19
Aina Ya Biashara Inayofanikiwa 34
Makosa 4 Ya Yanayoua Biashara Nyingi Na Namna Ya 52
Kuyaepuka

Jinsi Ya Kutengeneza Mfumo Utakaokuza Biashara Yako 67


Haraka

Mambo Yanayodumaza Biashara 89


Unachotakiwa Kufanya Baada Ya Kufeli Kwenye Biashara 102
Sababu Zinazopelekea Wasomi Wengi Kufeli Kwenye 123
Biashara Wanazoanzisha

Watu Wa Karibu Wanavyoweza Kuua Biashara Yako Na 134


Jinsi Ya Kuwakabili

Aina 5 Za Rekodi Muhimu Zitakazokusaidia Kukuza 148


Biashara Yako

Hitimisho 157
Kuhusu Mwandishi 159

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | ii


Utangulizi

Kuna watu wengi sana ambao wamefanikiwa


kuanzisha biashara na baada ya muda mfupi
biashara zimekufa au zimedumaa, hazikui tena.

Kuna watu ambao wameishia kwenye madeni


makubwa kwa sababu walichukua mikopo ili
kuanzisha au kukuza biashara zao.

Wapo wengine ambao wameishia kugombana na


ndugu ambao waliwahusisha kwenye biashara hizo
kwa sababu ndugu au rafiki zao walikuwa sehemu
ya kuwafelisha.

Nimeshakutana na watu ambao bado wameajiriwa


na inawapa changamoto kubwa sana kusimamia
biashara walizoanzisha, pamoja na kujitahidi
kuweke mtaji mkubwa ila haijasaidia kabisa kukuza
biashara zao.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | iii


Kitabu hiki ni maalumu kwa mtu ambaye anatamani
kupata mbinu sahihi zitakazomsaidia kuwa na
usimamizi wenye ufanisi katika biashara yake na
kujua mambo anayotakiwa kuyafanya ili kukuza
biashara aliyoanzisha.

Kanuni na mbinu utakazojifunza kwenye kitabu hiki,


zimetumiwa na watu wengi waliofanikiwa kukuza
mitaji yao na kupanua biashara zao.

Nasubiri kusikia ushuhuda wa mafanikio yako ya


kibiashara baada ya kuanza kutumia maarifa
utakayojifunza kutoka kwenye kitabu hiki.

See You At The Top

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | iv


Sura Ya Kwanza

Vitu Muhimu Vya Kufahamu


Kabla Biashara Yako Haijakua

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 01


AINA YA BIASHARA AMBAYO
NI NGUMU KUIKUZA

Sio kila biashara iliyomfanikisha mwingine itakufaa


na wewe pia. Ni muhimu sana kujua ni biashara gani
ambayo haikufai. Yapo mambo manne unayoweza
kuyaangalia kama dalili au ishara ya biashara
isiyokufaa.

Jambo la Kwanza: Umesukumwa na mtu lakini


wewe hauna hamasa ndani yako.

Kuna zile bishara mtu mwingine anakushinikiza


sana kuifanya labda kwa sababu yeye kaimudu
vyema basi anataka na wewe uingie.

Lakini pia kuna watu wenye tabia ya kushinikiza


mawazo yao tu ndiyo yasikilizwe. Watakusukuma
na kukushawishi kwa nguvu zote ufanye kile
wanachokitaka. Kuwa makini nao.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 02


Labda ni mzazi na ndiye anayekupa mtaji au ni
mwenza wake basi anaamua kufanya ilihali ndani
yake hana hamasa kabisa. Hii sio kiashiria kizuri
kabisa. Usifanye biashara ambayo unasukumwa
kufanya na wengine ikiwa haujavutiwa kutoka ndani
yako.

Ni watu wachache sana waliosukumwa kwenye


biashara ambazo hawana hamasa ndani yao na
wakafanikiwa. Wengi wao waliishia kufeli na kujutia.
Ukisukumwa hautakuwa na hamasa ya
kufanya mambo mwenyewe.

Kukosa kwako hamasa kutakuyumbisha sana


wakati wa changamoto.

Jambo la Pili: Unavutiwa na faida yake tu bila hata


kujua changamoto zake.

Mara nyingi unapowauliza watu kuhusu biashara ya


kufanya watakuambia faida utakayoipata tu
bila kukuambia hatari zake.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 03


Mtu atakuambia ukienda ukichukua lori la vitunguu
ukasafirisha ukaja kuuza unapata faida zaidi ya
nusu ya mtaji. Lakini hawakuambii kwamba lori
linaweza kuharibika, hawakuambii bei sokoni
zinabadilika badilika, panaweza kuwa na mzigo
mkubwa sokoni bei ikashuka.

Wala hawakuambii bidhaa inaweza kuoza kabla ya


kufika sokoni. Unapoingia unajikuta umepata
mambo tofauti na ulichokisikia. Unapoambiwa faida
tu bila hata kujulishwa changamoto zake hiyo sio
dalili nzuri ya biashara inayokufaa.

Hakuna biashara ambayo haina changamoto.


Unapoona unavutiwa na faida tu lakini hujui
changamoto zake, sikushauri kuifanya mpaka
ufanye utafiti yakinifu.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 04


Jambo la Tatu: Ina faida kubwa lakini wewe hujui
faida hiyo inapatikanaje.

Unakutana na watu wanakuambia yaani hapa


ukiweka milioni moja tu, utakuwa unapata laki mbili
kila siku.

Huambiwi hiyo laki mbili inapatikanaje. Hiyo sio


biashara inayokufaa kabisa kwani hautaweza
kuikuza. Ni lazima ujue mchakato mzima wa
utengenezaji wa faida wa biashara unayotaka
kuifanya.

Au unamkuta mtu anasema weka laki tano halafu


baada ya muda itazaliana. Pesa sio kama mbegu za
machungwa. Hata mbegu ya machungwa haizai
usipoipanda. Uko mchakato ambao unatokea
lazima uonekane.

Usipokuwa unajua mchakato wa upatikanaji wa


faida kwenye biashara hiyo basi chukua hicho kama
kiashiria cha biashara isiyokufaa. Hakikisha

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 05


unajua faida inatengenezwaje. Ielewe biashara
kwanza kabla hujavutiwa na faida yake.

Jambo la Nne: Unataka kufanya kwa sababu watu


wengi wanaifanya.

Hatufanyi biashara eti kwa sababu kila mtu


anafanya. Kumbuka kinachokufanikisha kwenye
biashara sio kile unachokifanya, bali ni vile wewe
ulivyo katika biashara unayofanya. Kwenye kila
biashara ambayo kuna mtu amefaulu, kuna aliyefeli
na hataki kabisa kuisikia.

Tafakari: Je, kwenye biashara ambayo unataka


kuifanya sasa hivi, kuna jambo lolote katika haya
manne?

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 06


JE, KATIKA MAKUNDI HAYA 4 YA BIASHARA,
YA KWAKO IKO WAPI?

Ili uweze kuisimamia na kuikuza biashara yako kwa


mafanikio, ni muhimu kujua ni kundi lipi ambalo
biashara yako ipo. Kwenye biashara kuna makundi
manne ya biashara, ukishaijua biashara yako iko
kundi lipi, itakupa mbinu nzuri za kutumia ili
kuisimamia na kuikuza.

Kwa mujibu wa wataalamu wa Taasisi ya Ushauri ya


Boston Consulting Group (BCG), biashara huwa
zinagawanywa kwenye makundi makubwa manne
kulingana na kasi ya ukuaji wake (growth) na
ukubwa wateja waliopo sokoni (share).

Hii husaidia mwenye biashara kufanya maamuzi ya


kujua ni biashara/bidhaa gani anatakiwa kuendelea
nayo, ni ipi ambayo anatakiwa kuachana nayo na ipi
ambayo anatakiwa kuwekeza zaidi.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 07


Kundi la kwanza: Biashara nyota (star business)

Hii ni biashara ambayo inakua kwa kasi kubwa na


unaweza kupata wateja wengi kama utaamua
kuweka nguvu zako zote hapo.

Kwenye kundi hili la biashara unapaswa uwe


unafanya uwekezaji mkubwa na wa mara kwa mara
kwa ajili ya matangazo na ubunifu zaidi, yaani kila
pesa ambayo unaipata unajitahidi kuirudisha tena
kwenye mzunguko wa biashara hiyo.

Kwa hiyo, kama huna misuli ya kuendelea


kuwekeza pesa hili sio kundi sahihi kwako. Hii ni
aina ya biashara ambayo faida yake hautaiona kwa
muda mfupi bali ni baada ya muda mrefu kupita, ila
ikianza kukupa faida huwa ni endelevu na kwa
muda mrefu.

Mara nyingi bidhaa ambazo zilikuwa za kwanza


kuingia sokoni au ambazo hakuna mbadala wake
huwa zinaangukia kwenye kundi hili.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 08


Kundi la pili: Biashara ng’ombe wa maziwa (Cash
cow business)

Hii ni biashara ambayo inakua taratibu lakini ina


wateja wengi sana. Ni biashara ambayo ukuaji wake
si wa kasi sana lakini ina uhakika wa wateja wa kila
siku.

Kibiashara hili ndilo kundi unaloshauriwa uwekeze,


kwa sababu ni biashara ambazo zinahudumia watu
wengi sana hata kama hazikui kwa haraka. Kwa
mfano uhitaji wa biashara ya chakula ni mkubwa
sana lakini ukuaji wake sio mkubwa sana.

Unaweza usitengeneze milioni mia kwa pamoja


lakini una uhakika wa kutengeneza elfu hamsini kila
siku. Biashara ya aina hii ni ile ambayo haina ukuaji
wa kasi ila una uhakika wa kuuza na huwa
inashughulika na mahitaji ya kila siku ya watu.
Mfano wa biashara kwenye kundi hili ni pamoja na
chakula, maji, nguo n.k.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 09


Unaweza kutumia faida unayoingiza kwenye kundi
hili kuwekeza katika maeneo mengine ya
biashara unayoyataka.

Kundi la tatu: Biashara kiulizo (Question mark


business)

Hii ni aina ya biashara ambayo inakua kwa haraka


sana lakini bado haijakamata kiwango kikubwa cha
soko/wateja.

Inaweza kuwa ni bidhaa mpya ambayo wateja bado


hawajaizoea, au inauzwa kwa bei kubwa kuliko
washindani wake, au watu kubadilisha kutoka
kwenye bidhaa walizozizoea kuja kwenye bidhaa
hiyo inawalazimu kutumia gharama kubwa.

Kundi la nne: Biashara mbwa (dog business)

Hili ni kundi la biashara ambazo zinakuwa taratibu


na soko unaloweza kulipata ni dogo pia. Hizi ni
biashara ambazo zipo njia panda, zinaweza
zikaanguka muda wowote.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 10


Ni biashara ambayo mara nyingi inachukua pesa
nyingi kuliko kuingiza pesa. Nyingi wa biashara hizi
huwa kwenye wakati ambao soko lake halikui na
uwekezaji wake unaohitajika huwa ni mdogo.

Kwa sababu hiyo, mara nyingi biashara hizi huwa


zimeshikilia mitaji mikubwa na hivyo kama watu
wengine huamua kuziuza ili kuingiza pesa kwenye
biashara zilizo kwenye makundi mengine.

Watu wengi huishia kuziuza au kuzifunga, na


endapo watachelewa kuchukua hatua basi huwa
zinakufa na wanapata hasara.

Tafakari: Je, wewe biashara/bidhaa ambazo


unauza kwa sasa, umeshajua inaangukia kundi
gani? (Kama una biashara/bidhaa zaidi ya moja,
kila moja iwekwe kwenye kundi husika).

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 11


NJIA 3 ZA KUJUA BIASHARA INAYOKUFAA

Wiki chache zilizopitita kuna mtu alinitumia ujumbe


mfupi ukisema nina milioni moja hapa, unanishauri
nifanye biashara gani?

Watu wengi sana inapofika suala la biashara ya


kufanya wanaangalia kwanza kiwango cha pesa
kisha wanaangalia aina ya biashara ya kufanya.
Lakini natamani ujue kwamba yapo mambo ya
msingi ya kuzingatia kabla hujaanzisha biashara.

Kama umenifuatilia kwenye baadhi ya video zangu


youtube utagundua kwamba mara nyingi nasisitiza
mtu afanye biashara ambayo anaipenda au
biashara ambayo inajihusisha na vitu
anavyovipenda.

Hapa nataka nikuongezee mambo mengine matatu


ya kukusaidia kujua biashara inayokufaa.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 12


i. Fanya biashara ambayo umejenga ujuzi nayo.

Ukishakuwa mfanyabiashara mkubwa unaweza


usilihitaji sana hili kwa sababu tayari utakuwa
umetengeneza mfumo unaokusaidia kuendesha
biashara.

Kwa hiyo hata kama huna ujuzi nayo utakachofanya


ni kuajiri wataalam wa biashara hiyo na mambo
yakaenda sawia kabisa. Lakini ikiwa ndio unaingia
kwenye biashara hiki ni kitu cha muhimu sana
kukizingatia.

Unapoanza, lazima utafute maarifa na ujuzi sahihi


wa biashara unayotaka kuifanya. Kuna viwango
viwili vya maarifa unayohitaji kujijenga nayo ikiwa
ndio unaanza chini kabisa.

Cha kwanza ni maarifa ya jumla kuhusu biashara


(General Business Knowledge). Huu ni ufahamu wa
jumla kuhusiana na mambo ya biashara na fedha.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 13


Cha pili ni maarifa maalumu juu ya biashara
unayoitaka (Specific Business Knowledge). Huu ni
ufahamu thabiti kuhusiana na biashara unayotaka
kuifanya. Inawezekana unajua kuhusu biashara kwa
ujumla lakini hujui kuhusiana na biashara ya kuuza
karanga.

Unaweza ukawa na maarifa juu ya biashara kwa


ujumla lakini huna maarifa thabiti kuhusu biashara
ya nguo. Kwa hiyo ili uweze kuifanya biashara
unayoitaka hakikisha unatafuta maarifa maalum
kuhusiana na biashara hiyo.

Maarifa ya jumla yanakupa kujua biashara kwa


upana wake lakini maarifa maalum yanakupa kujua
tu biashara uliyoamua kujifunza ili uianzishe. Watu
wengi huingia kwenye biashara kwa maarifa ya
jumla na matokeo yake huwa wanafeli kwa sababu
kuna vitu vingi vilivyojificha ambavyo wanakuwa
hawavijui kuhusiana na biashara husika.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 14


ii. Tafuta biashara ambayo unaweza ukaianza
sasa hivi.

Moja ya changamoto ya watu wengi ni kwamba


wanapanga mipango ya biashara ambazo hawana
uwezo nazo kwa sasa. Inaweza kuwa kwa sababu
ya kimtaji au hawana uwezo wa kulifikia soko
wanalolikusudia. Kwa sababu hiyo wengi
wanashindwa kuifikia mipango hiyo.

Unapopanga kufanya biashara anza kufanya


biashara ambayo una uwezo nayo kwa sasa.
Usipoanza hivyo maana nyepesi ni kwamba
hautakuja kuanza. Kuna watu wengi sana nakutana
nao na wananiambia wanataka kuwa
wafanyabiashara wakubwa sana.

Swali ninalowauliza ni katika hali waliyonayo sasa ni


kipi wanaweza kukifanya ili kije kiwafikishe kwenye
ndoto kubwa wanazozitamani. Wengi ukiwauliza
hivyo watakujibu sina mtaji. Hapa tatizo sio mtaji,
tatizo ni kutokuwa tayari kuanza na biashara
inayofanana na rasilimali ulizonazo.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 15


Kubali kuanza na kitu ulicho nacho huku ukiendelea
kufikiri pakubwa. Hakikisha unachagua biashara
ambayo unaweza ukaanza leo kutokana na
rasilimali ulizo nazo.

Anza na kile kidogo ulicho nacho mahali ulipo.


Jiulize, nina nini mkononi leo?, na nina uwezo gani
kwa sasa?. Angalia biashara ambayo iko ndani ya
uwezo wako, usisubiri kufanya vitu ambavyo viko
juu ya uwezo wako.

Kumbuka ni bora ndege mmoja uliyenaye mkononi


kuliko wale elfu moja walioko mwituni.

iii. Jiulize, una uwezo wa kuwafikia wateja katika


biashara unayotaka kuifanya?

Mimi ninapouza vitabu swali langu la kwanza ni,


mteja wangu ni nani na ninawezaje kumfikia. Kwa
hiyo kabla hujaanzisha biashara yako jiulize, katika
watu walionizunguka ni nani wanaweza kuwa
wateja wako.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 16


Ukiweza kujijibu swali hili basi hii ni ishara njema
kwako. Tambua kwamba hakuna maana ya kufanya
biashara ikiwa huwezi kuuza au kufikia walengwa.

Uzuri wa biashara upo katika uwezo wako wa


kufanya mauzo (Kama unataka kuuza zaidi, tafuta
kitabu changu kinachoitwa Mbinu za Kuuza Zaidi).
Lengo la biashara ni kupata faida, na faida ni
matokeo ya wewe kuuza bidhaa.

Jitahidi kuchagua biashara ambayo unawajua


wateja wake na una uhakika wa kuuza. Vinginevyo
biashara hiyo haikufai kabisa.

Tafakari: Katika mambo haya yaliyojadiliwa, ni


kipi/vipi ambavyo unajivunia kuwa unavyo?

Ni vipi ambavyo unakosa na ungetamani


kuvipata?

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 17


Sura Ya Pili

Jinsi Ya Kupata Fedha Za


Kukuza Biashara Yako

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 19


Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 20
Uaminifu wako unawahakikishia usalama wa pesa
yao lakini pale wanapoona ukakasi wanashindwa
kukusaidia hata kama wangetamani wakusaidie.

Wakati nachapisha kitabu changu cha Timiza


Malengo Yako mtaji wangu mkubwa niliupata kwa
marafiki zangu kwa sababu nilikuwa naaminika
kwao, walinipatia bila riba na niliwalipa baada ya
kuuza kopi kadhaa.

Hata wewe ukijenga uaminifu basi ndugu na


marafiki watakuwa msaada kwako. Changamoto ya
pili ni uwezo wako wa kulielezea wazo lako la
biashara kwao. Wengi wanashindwa kulielezea
wazo lao la biashara kwa ufasaha na ubayana.

Kwa hiyo inamuwia ugumu mwingine kukusaidia.


Kumbuka ni kazi mtu kukusaidia kwenye kitu
ambacho hajakielewa vizuri. Hakikisha unajua
kulieleza wazo au biashara yako kwa uyakinifu
wake.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 21


Usijieleze kama mtu ambaye hana uhakika wa kile
anachotaka kukifanya, au kama mtu asiyejua
anachokitaka. Kuwa na uhakika na wazo lako au
biashara yako na jieleze kwa namna ya kushawishi
mtu akuelewe ili aone uthamani wa wazo lako na
hapo ndipo atakapokuwa radhi kukufadhili.

Onyesha hamasa na nia ya dhati ya kutaka kufanya


biashara unayotaka kufanya. Hamasa na ujasiri
wako unawahakikishia wengine kuliamini wazo lako
na kuamua kukusaidia.

ii. Kuuza mali zako binafsi.

Unaweza ukaamua kupata mtaji wa biashara


unayoitaka kwa kuuza baadhi ya vitu unavyomiliki.
Unaweza ukaamua kuuza baadhi ya samani zako,
simu, tv, kompyuta n.k.

Kumbuka unapoamua kuuza vitu haimaanishi


kwamba hauvihitaji, la hasha, ni vile tu kupata mtaji
wa biashara ni muhimu kuliko vitu hivyo kwa wakati
huo.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 22


Jaribu kujikagua ujue nini unaweza kuuza ili upate
mtaji unaouhitaji. Kuna watu ambao wanakaa na
mitaji yao. Unakuta akiamua kuuza simu yake tu
anapata pesa ya kutosha mtaji anaouhitaji.

Kwa hiyo jiangalie kama unaweza kutumia njia hii


kupata mtaji au kuongezea kwenye kiwango
kinachopungua.

iii. Kuweka akiba binafsi.

Hii ni rahisi zaidi kama tayari una chanzo kingine


cha kipato. Kwa mfano kuna watu wengi
wameajiriwa na wanataka kuanzisha biashara.
Unachotakiwa kukifanya ni kuanza kujiwekea akiba
mpaka ifikie kiwango kile walichokuwa wanakihitaji
ili kuanzisha biashara.

Kwenye kila kipato unachopata unaweza ukaamua


kutenga asilimia fulani kama akiba ili ile akiba ndio
uje kuitumia kama mtaji. Wakati mwingine unaweza
kuamua kuweka akiba ili kujijengea nidhamu binafsi
kifedha.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 23


Ukishindwa kuwa na nidhamu ya fedha huwezi
kuwa na mafanikio mazuri kwenye biashara.
Kuweka akiba ni moja ya madarasa muhimu ya
nidhamu ya fedha.

Kama unasumbuliwa sana na nidhamu hii, tafuta


kitabu changu cha Money Formula (Elimu Ya Fedha
Isiyofundishwa Shuleni), kimewasaidia wengi sana
kujenga nidhamu ya fedha.

Lakini pia, akiba kidogo unayojiwekea inathibitisha


ni kwa kiasi gani umejidhatiti kwenye kutimiliza
wazo lako la biashara. Hata ukienda kwa mtu
ukamweleza kwamba umefanikiwa kupata kiasi
kadhaa na unaomba msaada kwenye kilichobaki
atakuelewa kirahisi. Atakuona kama umedhamiria
kikwelikweli.

Ni rahi kwa mwenye kidogo kusaidiwa kuliko asiye


na kitu japo kidogo. Kanuni inasema mwenye nacho
ndiye huongezewa. Mtu anaanza kujiuliza kama
wewe mwenye wazo umeshindwa kutafuta hata
kitu kidogo najuaje kama una dhamira ya dhati.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 24


Kwa hiyo kwa kuweka akiba utajihakikishia kianzio
cha mtaji wako.

iv. Vikundi vya kuweka na kukopa

Njia hii inakurahisishia kupata fedha nyingi kwa


gharama nafuu. Vikoba vingi na SACOSS riba zao ni
nafuu sana. Unachotakiwa kufanya ni kuangalia
wapi unaweza kujiunga kisha ukaweka malengo
yako.

Kwa mfano unasema mimi nataka kuchukua mkopo


wa milioni kumi baada ya miezi sita. Halafu
unaenda kuangalia masharti yao yakoje halafu
unaangalia natakiwa ninunue hisa za shilingi ngapi
ili nikidhi vigezo vya kukopesheka.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 25


v. Ubia, mwekezaji au mwanahisa.

Ubia ni ushirika wa kibiashara, yaani mimi nina kitu


na wewe una kitu halafu tunaviunganisha kupata
kimoja tunachokikusudia. Mfano, una mtaji mdogo
kwa hiyo unaamua kumtafuta mshirika wa
kibiashara ili naye achangie mahali panapopwaya.

Kwa kufanya hivyo unamaanisha biashara hiyo


itamilikiwa na nyie wote kufuatana na namna
mlivyokubaliana.

Ubia mwingine waweza kuwa wewe una ujuzi


mwingine ana fedha kwa hiyo mnaungana kuufanya
ujuzi wako uwe biashara. Kwa mfano wewe ni
mtaalamu wa kutengeneza samani lakini huna
fedha za kufungulia ofisi na kununulia malighafi,
unachofanya ni kuingia ubia na mwenye fedha na
biashara ikasimama vyema.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 26


Waweza pia kuamua kuuza hisa au kumtafuta
mwekezaji ili awekeze fedha zake kwenye wazo
lako la biashara. Unapotumia njia hii, ni vizuri
makubaliano yenu yawe kwa maandishi na
ikiwezekana mumshirikishe mwanasheria.

vi. Kutumia taasisi za fedha.

Unaweza ukatumia Benki au taasisi ndogo za


ukopeshaji (Micro-finance). Changamoto ya taasisi
za kifedha ni kwamba riba yake ni kubwa kidogo na
masharti yake ni magumu ndio maana nimeiweka
mwishoni kabisa ili isiwe kipaumbele cha kwanza.

Watu wengi huwa wanakimbilia njia hii lakini


mwishoni wanaishia kwenye majuto. Hii ni kwa
sababu wanatumia lugha ya ushawishi kukutaka
ukope na wengi wanakopa bila hata kujua undani
wa mambo.

Itumie njia hii ikiwa tu umeelewa vizuri masharti na


riba yake.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 27


Usiende kukopa kwenye taasisi za fedha kama
huna uelewa wa kutosha kuhusu huduma zao.

Kama wewe kwa sasa uko kwenye matatizo ya


madeni nakushauri ungana na wengine waliosoma
kitabu changu cha Namna Ya Kuondokana Na
Madeni ambacho kimewasadia sana.

Tafakari: Je, kwa hali yako ya sasa unafikiri njia


gani unaweza kutumia kupata pesa?
Kumbuka, unaweza kutumia njia zaidi ya moja
kupata pesa unayoitaka.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 28


HATUA 5 ZA KUMSHAWISHI MTU AKUPE PESA
ZA WAZO LAKO LA BIASHARA

Kuwa na wazo la biashara ni jambo moja lakini


kupata fedha za kulifanya wazo hilo liwe halisi ni
kitu kingine. Inahitaji ujuzi ili kuwafanya watu
wengine waingie ubia au wawekeze kwenye wazo
lako la biashara.

Kuna watu ambao wamefanikiwa kwenye biashara


sio kwa sababu walikuwa na pesa au mitaji
mikubwa ila kwa sababu waliweza kuliuza wazo lao
vizuri na likawapatia mtaji.

Zifuatazo ni hatua tano zitakazolifanya wazo lako la


biashara liuzike na hivyo watu wengine waje
kufanya ubia na wewe au kuwekeza au kukupa
mkopo au labda hata kukusaidia kifedha.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 29


i. Prepare and practice (fanya maandalizi na
mazoezi ya kutosha.)

Unapowasilisha wazo la biashara kwa mtu, kuna


mambo kadhaa ambayo anayazingatia na
kuyaangalia. Kwa hiyo jaribu kuangalia namna gani
bora ya kuliwasilisha wazo lako itakayowavutia
wengine.

Fikiria kama umepewa dakika mbili tu za


kuwasilisha wazo lako la biashara kwa tajiri
mkubwa ambaye yupo tayari kukusaidia ikiwa
ataridhika na maelezo yako. Tengeneza picha hiyo
kichwani mwako halafu ujiulize utamwambia nini ili
aridhie wazo lako.

Ukiona huwezi kumuelezea mtu wazo lako kwa njia


rahisi, yaani kwa maneno machache lakini
yanayoeleweka sana ujue bado wazo hilo haliwezi
kupata msaada kutoka kwa wengine.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 30


Unapokuwa unajiaandaa hakikisha pia unaweza
ukasema kwa nini unataka ufanye kile unachosema
unataka kukifanya.

Unapokuwa kwenye maandalizi zingatia pia


kwamba watu watakukosoa. Wengi wanapokuwa
wamepata wazo la biashara huwa wanadhani kila
mtu atawaelewa kwa sababu tu linaeleweka.

Wengi watakukosoa na hata kukukatisha tamaa.


Kila mtu atasema yake. Kwa hiyo hakikisha
unajiandaa kukabiliana na changamoto hizo.

ii. Show emotional connection (Onyesha kwamba


wazo hilo ni la kwako)

Liwasilishe wazo lako la biashara kama wewe ndiye


mmiliki halali na linahusiana moja kwa moja na
wewe. Kuna mtu akiliwasilisha wazo lake la
biashara, unaona kabisa kwamba anafanya ili tu
apate fedha na sio zaidi ya hapo.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 31


Usizungumze tu eti kwa sababu ni wazo zuri, ni
wazo la kuingiza pesa, n.k. mara nyingi watu
watakusaidia kwenye kitu ambacho kwanza
kinaugusa moyo wako. Kama halijagusa moyo wako
hakuna namna linaweza kugusa mioyo yao.

iii. Sell your ability (uza uwezo wako).

Ninapokuwa na pesa za kuwekeza lazima niwekeze


kwa mtu mwenye uwezo. Unapomwambia mtu
uzuri wa wazo lako la biashara mwonyeshe pia
uwezo wako wa kulitekeleza wazo hilo.

Mwonyeshe uzoefu ulionao katika biashara, jinsi


ulivyowahi kufanya biashara kama hiyo au
inayofanana na hiyo huko nyuma.

iv. Make it visual (ljengee picha wazo lako)

Hakikisha unapoliwasilisha wazo lako la biashara


unalijengea picha. Unaweza ukachora vielelezo au
namna yoyote inayoijenga picha ya wazo lako
kwenye fikra za watu wanaokusikiliza.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 32


Hii itawafanya watu wahusianishe wazo lako na
picha inayowawasilishia kwa urahisi. Ni rahisi sana
watu kuelewa wazo ambalo lipo kwenye picha au
michoro kuliko maandishi.

v. How will it grow (onyesha jinsi wazo lako


litakavyoweza kukua)

Mtu hawezi kuambatana na wazo lako la biashara


ikiwa wazo hilo halikui au ni la muda mfupi.

Hakikisha unaweza ukaonyesha jinsi wazo lako


litakavyoweza kukua kutoka hapo lilipo mpaka kule
ambako haujakufia bado.

Tafakari: Je, ni kitu gani ambacho umekuwa


haukitumii unapokuwa unawashawishi watu
kukubaliana na wazo lako?

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 33


Sura Ya Tatu

Aina Ya Biashara Inayofanikiwa

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 34


MBINU 5 UNAZOWEZA KUTUMIA KUANZISHA
BIASHARA YENYE MAFANIKIO

Kuna mbinu nyingi sana unazoweza kuzitumia


kuanzisha biashara yenye mafanikio, lakini mimi
katika ufundishaji wangu nimegundua zipo mbinu 5
ambazo kila nilipozifundisha zimeleta matokeo
makubwa sana.

Mbinu hizi kuna baadhi ambazo nimezitumia mimi


binafsi kwa sehemu, lakini zipo ambazo
niliwafundisha wengine na wakazitumia
zikawaletea matokeo mazuri.

Mbinu ya Kwanza: Taaluma yako (Profession)

Mbinu hii inahusisha wewe kujiuliza una taaluma


gani, ili uweze kuanzisha biashara yako kutokana
na taaluma uliyonayo. Kwa mfano, kama taaluma
yako ni ualimu basi unaweza ukaanzisha biashara
kama vile kItuo cha “tuition” au shule.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 35


Kama wewe taaluma yako ni utabibu basi unaweza
kuanzisha kituo cha afya, kliniki, duka la madawa
au hata hospitali.

Katika taaluma kuna namna kuu mbili (02)


unazoweza kuzitumia.

Namna ya kwanza: Fanya mwenyewe (do it


yourself)

Kwenye kundi hili unaamua kufanya mwenyewe.


Mfano, kama wewe ni muhasibu unaweza
ukaanzisha ofisi ya uhasibu au ukaguzi wa
mahesabu.

Taaluma yako ni mtaji wako mzuri unaoweza


ukaugeuza kuwa biashara kubwa. Angalia taaluma
uliyosomea ujue watu wanaweza kukulipa nini
kulingana na ujuzi ulioupata kwenye taaluma hiyo.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 36


Namna ya pili: Jenga timu ya kufanya pamoja (build
team to do together)

Hapa mnaweza kuungana watu kadhaa mkajenga


timu ya kufanya kazi pamoja. Mnaweza mkaungana
walimu watatu au watano wa masomo tofauti
mkaanzisha kituo cha QT (qualifying test) na kutoa
huduma bora na iliyokamilika.

Usiidharau taaluma yako ni mtaji mkubwa kabisa


wa kukutajirisha. Cha msingi ni ujifunze kuifanya
taaluma hiyo kuwa ujuzi unaoweza ukautendea kazi
ili ukuzalie matunda. Usisubirie ajira tuu wakati
unaweza kujiajiri mwenyewe.

Hakuna taaluma ambayo huwezi kuifanya biashara.


Kila taaluma ina biashara ndani yake, ni kazi yako
tu kuifichua biashara hiyo na kuianzisha.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 37


Mbinu ya Pili: Uzoefu (experience)

Mbinu ya pili ni kutumia kila uzoefu ulioupata au


kuupitia, ni fursa ya wewe kuanzisha biashara
fulani. Kuna watu wengi leo duniani wanaoingiza
pesa nyingi kwa sababu ya uzoefu walioupata
mahali na wakautumia kama fursa ya kibiashara.

Kuna aina tatu za uzoefu unazoweza kuzitumia.

Aina ya 1: Painful experience (uzoefu uliokupa


maumivu)

Unaweza kuwa umewahi kupitia mambo kwenye


maisha yako yaliyokuumiza sana. Mara nyingine
hata hupendi kabisa hata kukumbuka. Lakini nina
habari njema kwako, uzoefu huo unaweza kuwa
mtaji mzuri wa kukufanya uwe milionea.

Mungu hawezi kukuacha ukapitia maumivu kama


hakuna kusudi katika maumivu hayo. Kwenye kila
maumivu kuna kusudi ndani yake. Na kusudi hilo ni
kwa ajili ya kukunufaisha wewe.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 38


Changamoto ya watu wengi ni kwamba
wanashindwa kugeuza maumivu yao kuwa fursa ya
kuwanufaisha. Wanaishia kuona maumivu bila
kuona utamu ulioko ndani yake.

Nilikutana na dada mmoja ambaye anafanya


biashara ya kupika chakula kwenye matukio
mbalimbali (catering services), na biashara yake
ilikuwa inafanya vizuri sana. Nilipomuuliza siri yake
alinisimulia kisa kilichonisikitisha sana.

Anasema kwamba yeye alilelewa na ndugu, na


alipokuwa huko alilazimika kuwa mtu wa kufanya
kazi zote peke yake kutokana na mazingira
aliyoyakuta. Kitu kimojawapo ambacho kilikuwa
kinamuumiza ni kwamba alikuwa na umri mdogo
lakini alilazimika kupika chakula cha watu wengi kila
siku.

Ile hali ilimfanya ajue kupika aina mbalimbali za


vyakula tena kwa ustadi. Ni kweli ni uzoefu
uliomfanya aumie sana lakini ulimpatia ujuzi

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 39


mkubwa uliomsaidia kuanzisha biashara ya kupika
vyakula kwa mafanikio.

Usiruhusu maumivu yakutafsiri badala yake utumie


uzoefu wa maumivu hayo kukuletea faida. Tafuta
kwa undani kujua faida iliyofichika kwenye
maumivu uliyowahi kupitia. Inawezekana uzoefu
huo japo ulikuwa na maumivu, ukakufanya uwe
tajiri mkubwa sana.

Aina ya 2: Joyful experience (uzoefu wenye


furaha ndani yake)

Huu ni uzoefu wenye furaha ambao kila


unapoukumbuka unakufanya ufurahie. Pengine
labda uliishi kwenye familia yenye duka ukajifunza
kuliendesha na kujikuta unatamani kufanya kitu
kama hicho pia kwenye maisha yako binafsi.

Jamii za kihindi na kiarabu, zimefanikiwa sana


kwenye eneo hili. Niliwahi bahatika kusoma nao
shule ya msingi, ilikuwa wakati sisi tukitoka shule
tunaenda kucheza, wao walikuwa wanaenda

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 40


moja kwa moja kwenye maduka ya baba zao bila
hata ya kubadilisha sare za shule. Huko atajifunza
namna ya kuwahudumia wateja, atajifunza bei za
vitu, atajifunza miiko yote ya biashara n.k.

Hii inawafanya watoto wao kuwa na uzoefu


mkubwa sana kwenye biashara hata wanapokuwa
wakubwa na kuanzisha biashara zao wanakuwa na
mafanikio makubwa kwa sababu ya uzoefu ndani
ya familia.

Jiulize, Je ulijifunza nini ambacho kilikuwa kizuri


kutoka kwa wazazi wako? kutoka kwa marafiki au
ndugu waliokuzunguka? Uzoefu huu unaweza
ukawa ni fursa ya kibiashara.

Usizidharau nyakati za namna hiyo. Kuna mtu


inawezekana alikuwa anamsaidia mamaye kuandaa
juisi au hata kupika chakula mgahawani. Mtu huyu
atashangaza sana ikiwa anahangaika kupata wazo
la biashara ili hali amewahi kuwa na uzoefu wa
namna hiyo.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 41


Aina ya 3: Planned Experience (uzoefu uliopangilia
kuupata)

Huu unahusisha ajira unayoifanya au mahali


ulipojitolea kufanya kazi ili upate uzoefu wa kazi
(Volunteer). Usifanye kazi mahali eti tu kwa sababu
unataka mshahara, kumbuka pia kupata uzoefu
utakaoweza kukusaidia kwenye maisha yako
binafsi.

Yawezekana kuwa hujaajiriwa, tafuta kwenda


mahali ambapo utajitolea kufanya kazi ili uupate
uzoefu unaoutaka kwa ajili ya mipango yako ya
mbele. Ni kweli wanaweza wasikulipe kabisa lakini
watakuachia uzoefu mkubwa utakaokufanya uweze
kujiajiri au kuanzisha biashara yako mwenyewe.

Mbinu Ya Tatu: Mtandao (network)

Mtandao wako ndio utajiri wako. Mara nyingi sana


fursa unazozitafuta zipo kwa watu walio kwenye
mtandao wako. Jiulize je, mtandao wako una fursa
gani?

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 42


Thamani yako imebebwa na watu waliokuzunguka.
Unapochagua biashara unapaswa pia kuzingatia
aina ya watu waliokuzunguka. Hapa kuna maswali
unaweza ukajiuliza yatakayoweza kukutengenezea
wazo la biashara.

a. Watu wengi waliokuzunguka wapo kwenye


sekta gani? Mfano kuna watu ambao
wamezungukwa na watu wanaofanya kazi
mahotelini. Hapo lazima ujiulize naweza kupata
fursa gani kwa kuzungukwa na watu kama hao.
Unaweza kuamua kuanza kusambaza mayai au
kuku mahotelini.

b. Watu wengi waliokuzunguka wana umri gani?


Kila kundi la umri lina mahitaji yake. Kujua ni watu
wa umri gani wamekuzunguka kutakupa kujua
mahitaji yao hivyo kukurahisishia kuzalisha wazo la
biashara.

c. Watu waliokuzunguka wanatumia pesa zao


kununua nini zaidi? Jaribu kuangalia watu
waliokuzunguka ofisini au kanisani kwako, au

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 43


msikitini kwako, au kwenye magrupu yako ya
mitandaoni. Ukijua wanachonunua zaidi utajua
uanzishe biashara gani itakayofaa.

Inawezekana sasa hivi, hauna hao watu lakini


unaweza ukaweka mkakati wa namna ya
kutengeneza watu wanaokufaa kwenye mtandao
wako. Ili kufanikisha kutengeneza mtandao wako
wa kibiashara huna budi kuzingatia yafuatayo

Watambue - ujue ni aina gani ya watu


unaowahitaji katika biashara yako

Waoorodheshe - kwa majina yao

Watafute – wafuate ukaongee nao.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 44


Mbinu Ya Nne: Kipaji (Talent)

Kipaji ni uwezo wa kipekee uliopewa na Mungu


kufanya jambo Fulani wa urahisi na ufanisi kuliko
wengine. Wengi wanapowaza kipaji wanafikiri tu
vile vinavyoonekana kwa urahisi kama vile kuimba,
kucheza mpira au kuchora.

Lakini kwa kweli kuna vipaji vingi sana ambavyo


mara nyingine hata wenye vipaji wanashindwa
kukubali kwamba ni kipaji.

Kwa mfano , kuna watu ni manguli wa kupangilia


mambo ya kuwaleta watu pamoja, hata kwenye
magroup ya WhatsApp au kwenye familia huwa
tunao watu wa namna hii. Ukiwapa nafasi
wanafanya kwa ustadi wa hali ya juu sana.

Hiki pia ni kipaji. Kuna watu ambao wana uwezo wa


kufanya mauzo ya ufanisi mkubwa sana. Kitu
muhimu unachopaswa kujua ni kwamba kipaji
ambacho hakijanolewa hakiwezi kikakuletea pesa.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 45


Kwa hiyo unapaswa kukigeuza kipaji chako kiwe
ujuzi ili kiweze kukuletea faida. Kumbuka kwamba
watu hawalipii kipaji chako, wanalipia ujuzi
uliozaliwa kutoka kwenye kipaji hicho.

Kipaji ni kitu ambacho hata mtu mwingine anaweza


kuwa nacho, lakini sio kila mtu anaweza kukipa
kipaji chake uthamani. Thamani unayokipa kipaji
chako ndiyo inayoamua faida utakayoipata
kutokana na kipaji hicho. Hakikisha unakinoa na
kukibadilisha ili kikuzalie matunda.

NB: KIPAJI kinakupa NAFASI lakini UJUZI (skills)


unakupa PESA

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 46


Mara zote kitu kilichochakatwa ni ghali kuliko kile
kilicho ghafi. Hata kipaji chako kinahitaji
kuchakatwa ili kiweze kuwa ghali. Hatua zifuatazo
zitakusaidia ili kukifanya kipaji chako kigeuke kuwa
biashara.

Hatua ya 1: Gundua kipaji chako.

Hapa ndipo changamoto ya wengi, kuna watu


wanadiriki hata kusema mimi sina kipaji lakini
ukweli ni kwama hakuna mtu asiye na kipaji. Kuna
video nyingi sana nimeelezea kwenye YouTube
namna ya kugundua kipaji chako,zitafute ujifunze.

Hatua ya 2: Kinoe kipaji chako.

Ukishagundua kipaji chako usikimbilie kukionyesha


kwa wengine unapaswa ukiingize kwenye
mchakato ili kichakatwe vizuri. Ni hatari
kukionyesha kipaji chako kabla hujakinoa.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 47


Wakati wa kukinoa kipaji ndio kipindi kigumu zaidi
kwa sababu watu wanakuwa hawakuoni wala
kukuthamini.

Hiki ni kipindi cha maumivu, lakini kiwango chako


cha kukinoa kipaji ndicho kinachoamua thamani ya
kipaji chako.

Hatua ya 3: Kioneshe kipaji chako

Kuna wakati utalazimika kukionyesha kipaji chako


bila hata ya kulipwa. Kwenye hatua hii kitu muhimu
sio kulipwa, bali ni watu kikiona kipaji chako. Watu
wakikiona utatengeneza uhitaji wa kipaji chako.

Watu wataanza kukutafuta kwa sababu wanakihitaji


kipaji chako hapo ndipo utaweza kuifanya kuwa
biashara.

Hatua ya 4: geuza kipaji chako kikulipe

Ukishakionyesha kipaji chako utasababisha uhitaji


na hapa ndipo watu wataanza kukulipa.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 48


Unapoanza watu watakulipa kidogo sana lakini
mara zote hakikisha unazalisha matokeo
yanayozidi gharama waliyokulipa. Daima fanya
Zaidi ya watakachokulipa

Hatua ya 5: Panua kipaji chako

Baada ya kufanya yote hapo juu hapa unapaswa


ukifanye kipaji chako kuwa biashara kubwa.
Unaweza ukakifanya kifike nchi nzima.

Lakini pia unaweza ukakifanya kiwe kimataifa zaidi.


Kama una mpango wa kutumia kipaji chako kama
biashara, nakushauri tafuta kitabu changu
kinachoitwa KIPAJI (Jinsi Ya Kukigeuza Kipaji
Chako Kuwa Biashara), kitakusaidia sana.

Mbinu Ya Tano: Unachokipenda (your passion)

Kitu kingine unachoweza kukitumia katika


kuanzisha biashara inayoweza kufanikiwa ni
kuangalia vitu unavyovipenda.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 49


Kwa mfano, akaja mtu na kukuambia chagua kazi
yoyote unayotaka kuifanya na mimi nitakulipa
milioni 20 kwa mwezi utachagua kazi gani?

Kile utakachokichagua ndicho kitu unachokipenda


zaidi. Kwa maneno mengine, haujachagua kwa
sababu kinalipa zaidi ila umechagua kwa sababu
unakipenda, kwa kuwa chochote ambacho
ungechagua malipo yangefanana.

Chunguza vitu unavyovipenda, kwa sababu


kwenye kila anachokipenda kuna biashara
iliyofichika ndani yake. Mara nyingi sana ni vyema
ukafanya biashara kwenye vitu unavyovipenda.

Kwa mfano mtu anayependa sana watoto, anaweza


kufungua shule ya awali, au eneo la michezo ya
watoto, au duka la nguo la watoto, au kuuza lishe
za watoto au hata kufanya kipindi maalumu cha
Watoto kwenye televisheni, saluni ya watoto au
duka la vitabu la watoto.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 50


Kwa kufanya hivyo itamkutanisha na watoto huku
ikiwa inamuingizia faida kubwa kabisa. Mungu
amekuumbia kitu unachokipenda, ili ukifanye kitu
hicho kwa ubora, halafu kwa kufanya hivyo watu
waje wakulipe.

Lakini mwisho wa siku kimekufurahisha wewe zaidi


ya hao waliokulipa. Watu wanaweza kustaafu kazi
lakini hawawezi kustaafu yale wanayoyapenda.

Tafakari: Katika mbinu mbalimbali zilizojadiliwa


kwenye Sura hii, wewe unaona ni ipi ambayo
unaitumia/unataka kuanza kuitumia?

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 51


Sura Ya Nne

Makosa 4 Ya Yanayoua Biashara


Nyingi Na Namna Ya Kuyaepuka

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 52


MAKOSA MANNE YANAYOFANYWA NA
WAANZILISHI WENGI WA BIASHARA

Umeshawahi kuona biashara inaanza kwa kasi


sana, inachanua inapata umaarufu, inaonekana
inauza sana, lakini baada ya muda inakufa na
hauisikii tena?

Kuna watu wengi sana wanaanzisha biashara lakini


baada ya muda hazifiki mbali. Unakuta ameanzisha
biashara leo, baada ya mwezi au miezi miwili
imeshakufa.

Wakati mwingine tatizo hata sio mtaji, wala wateja,


au eneo biashara ilipo. Kuna makosa yaliyozoeleka
ambayo watu hata hawayapi uzito, lakini kiukweli
ndiyo yanayowagharimu, unatakiwa uyafahamu na
uyaepuke ili ufanikiwe kwenye biashara
unayofanya.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 53


Kosa la Kwanza: Kutopata muda wa kuisimamia.
(Bossy attitude)

Watu wengi wanaanzisha biashara lakini hawapati


muda wa kuisimamia. Sababu inaweza kuwa ni
kutokana na ukweli kuwa kuna kitu kingine
wanakifanya kwa hiyo wanakosa kabisa muda wa
kuisimamia.

Lakini wakati mwingine sio kwamba wametingwa


sana bali wana mtazamo wa kibosibosi. Hapa
nazungumzia ule mtazamo wa kwamba kwa
sababu mimi ndio nimeanzisha basi mimi ndiye
bosi, sitakiwi kufanya kazi badala yake mimi ni mtu
wa kupiga simu tu na kuulizia nini kinaendelea na
kutuma watu wengine.

Hali hii ndiyo inaua biashara nyingi. Unapoianzisha


biashara ni kama vile unapopata mtoto mchanga.
Hivi umeshawahi kujiuliza kwa nini mama
mfanyakazi akijifungua anapewa likizo ya
kujifungua?

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 54


Mara nyingi wanampa likizo sio tu kwa ajili ya yeye
kupata muda wa kurejesha afya yake, bali pia ni
kwa ajili yakumpa nafasi ya kumlea kichanga wake
na kumpa matunzo stahiki.

Sababu ni kwamba wanataka ahakikishe huyu


mtoto amekua ndipo aendelee na majukumu yake
ya kazi. Sasa na wewe unapoanzisha biashara ,
tengeneza muda wa kuisimamia na kuilea biashara
yako mpaka isimame. Kadiri uwezo wako wa
kusimamia unavyozidi kuwa mdogo ndivyo
unavyohatarisha biashara yako kufa.

Unapoanza biashara inakutegemea wewe, halafu


baade ndipo itegemee mfumo. Kwa hiyo usianze
kwa kuifanya biashara itegemee mfumo, anza kwa
kuifanya ikutegemee wewe kisha ndipo uanzishe
mfumo baada ya biashara kusimama.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 55


Kosa la Pili: Kutaka kupanuka kwa haraka kabla
biashara haijakita mizizi.

Kwenye kila biashara kuna kitu kinaitwa grafu ya


kujifunza (Learning Curve). Hii ni namna mtu
unavyojifunza kitu hatua kwa hatua kuanzia
unapoanza mpaka unapokifanikisha kitu hicho.
Haijalishi umesoma kiasi gani lakini biashara yoyote
ina kitu cha kujifunza.

Kwa hiyo unapoanza, unatakiwa kupata muda wa


kujifunza zaidi kuhusu undani wa biashara
unayoifanya. Ndipo sasa, baada ya kuwa na
uhakika kwamba umeuelewa undani wa biashara
hiyo uanze kupanuka kwa ukubwa zaidi.
Usiharakishe kabla hujajifunza hata kama una mtaji
mkubwa.

Kwenye kupanuka kuna kupanuka kwa wima


(Vertical Expansion) na kupanuka kwa ulalo
(Horizontal Expansion) . Kupanuka kwa wima ni
pale unapoipanua biashara kwa ukubwa na kina
zaidi.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 56


Ni kupanuka ambako biashara inajikita mizizi zaidi
na unajaribu kwenda juu zaidi kwa kupata maarifa
zaidi huku ukiendelea kujenga mtandao. Huu ni
upanukaji mzuri kwa biashara inayoanza.

Kupanuka wa ulalo ni pale ambapo biashara inakua


kwa kuanzisha matawi mapya sehemu zingine.
Wakati ule upanukaji wa kwanza unahusisha
kupanuka bila kuhama, hii inahusisha kupanua
mipaka yako kwa kusambaa kwenye maeneo
mengine pia. Huku ni kupanuka kuzuri kwa biashara
iliyosimama tayari.

Usitamani kupanuka kwa haraka sana kabla


hujaweka mizizi ya kujitosheleza utafeli mbeleni.
Jifunze kuwa mvumilivu na mwenye subira.
Biashara nyingi ambazo zilipanuka kwa wima kabla
ya kupanuka kwa ulalo, zilifeli.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 57


Kosa la Tatu: Kuangalia undugu na urafiki badala
ya uwezo

Unakuta mtu anapoanzisha biashara na kuajiri watu


wa kufanya nae kazi, badala ya kuangalia mtu
mwenye uwezo anaanza kutafuta ndugu na
marafiki bila hata kuzingatia uwezo wao. Hili ni
jambo hatari sana linaloua biashara nyingi.

Sababu ya kwanza, wengi wanafaya hivyo kwa


sababu wanaona urahisi kwa kuwa hawatahitaji
kuwalipa kabisa ndugu au watawalipa kidogo, kwa
hiyo wanaona wanaokoa gharama. Hapa pana
hatari kubwa kwa sababu vitu vya bure ni ghali.

Usipomlipa mtu anakosa hamasa ya kufanya kazi


kwa hiyo anakuwa hajali chochote. Atawajibu
vibaya wateja, atakuwa mvivu na kufanya tabia
zozote zilizo hatarishi kwa biashara. Pia
unashindwa kumuwajibisha mtu wa namna hii kwa
sababu haumlipi.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 58


Kitu hatari zaidi ni kuwa unamuweka kwenye
wakati mgumu kwa kumpa kishawishi cha udokozi,
kwani anakuingizia hela huku yeye hapati
chochote. Kwa hiyo anaamua kujilipa mwenyewe
kwa sababu anajua hata akiiba hutampeleka polisi
wala kumchukulia hatua zozote za kisheria.

Sababu ya pili ni kuwa, wanaajiri ndugu na marafiki


kwa sababu wameona hawana kazi ya kufanya.
Hupaswi kumuajiri mtu eti kwa sababu tu hana kazi
ya kufanya. Sio kila ndugu au rafiki ambaye hana
kazi ya kufanya anapaswa kufanya kazi kwenye
biashara yako.

Epuka sana kuajiri ndugu kwenye biashara. Epuka


sana kuleta urafiki kwenye biashara. Ajiri watu kwa
kuzingatia weledi wao na sio mahusiano uliyonayo
na wao. Na unapomuajiri mtu jitahidi sana kuwa na
mkataba naye. Hata kama biashara ni ndogo kiasi
gani, mkataba ni kitu cha muhimu sana.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 59


Usipofanya hivyo huyu mtu ataichukulia poa
biashara yako, hataipa umakini unaostahili.

Kosa la Nne: Kutumia pesa ya mauzo badala ya


pesa ya faida iliyopatikana.

Watu wengi sana wakishaanzisha biashara zao na


kuanza kufanya mauzo wanawehuka sana
wanapoona mauzo makubwa. Utasikia mtu
anakwambia biashara yangu inafanya vizuri sana,
naingiza milioni moja kwa siku.

Swali ni katika mauzo hayo ya milioni moja faida ni


shilingi ngapi?

Jifunze kutofautisha kati ya mauzo na faida maana


pasipo kujua unaweza kukuta unatumia fedha ya
mtaji ukidhani ni faida ili hali sio. Hakikisha unajua
kupiga mahesabu ya faida ili kutenga faida na mtaji.

Na unapopiga mahesabu ya gharama za uendeshaji


usisahau kujilipa mwenyewe, na gharama zingine
ndogo ndogo kama nauli na kupiga simu.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 60


Kuna watu wengi ambao wanauza sana lakini
hawapati faida, na baya zaidi ni kwamba hawajui
kwamba hawapati faida. Jitahidi sana kujua namna
ya kupiga mahesabu ya faida yako halisi. Ukilijua
hili utaulinda mtaji wako na hivyo kuifanya biashara
yako isimame.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 61


ZIFAHAMU TABIA NNE ZINAZOONGOZA KUUA
BIASHARA NYINGI

Haijalishi una wateja kiasi gani, au mtaji kiasi gani


au upo sehemu nzuri kiasi gani, au bidhaa zako ni
bora na za kipekee kiasi gani, biashara yako
inaweza kuwa hatiani na hata kufa kabisa.

Ziko tabia zinazoua biashara kwa uharaka sana.


Ukiziendekeza tabia hizi ni kikwazo kikubwa kwa
maendeleo ya biashara yako.

Tabia hizi zimeua biashara za watu wengine, hivyo


ni muhimu kuwa macho ili usije ukala mrama.

Tabia Ya Kwanza: Kufanya mambo kwa mazoea/


kuleta mazoea.

Watu wanapoanza biashara wanakuwa makini na


nidhamu ya hali ya juu. Kama inahitaji kuwahi
mapema watawahi sana, kama inahitaji usafi
watakuwa wasafi sana, lakini baada ya muda

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 62


wanaizoea biashara yao. Mbaya zaidi hawaishii tu
kuizoea, lakini wanaanza kuleta mazoea kwenye
biashara zao.

Wanaacha kuyafanya mambo yale yaliyokuwa


yanawapa ubora wa biashara yao kwa wateja
wanaanza kufanya mambo wanavyojisikia.
Matokeo yake ni kwamba wateja wanaacha kuja
kwa sababu ya kutoridhishwa na huduma.

Ukiizoea biashara, itakukimbia kwa sababu kwa


kawaida biashara haitaki uizoee. Ukiizoea inatafuta
mtu mwingine ambaye ataiheshimu.

Tabia Ya Pili: Kuendesha biashara kirafiki.

Ninaposema kirafiki namaanisha kushindwa


kuweka bayana mipaka kati ya biashara na
uswahiba. Madhara yake ni kujikuta unamkopesha
rafiki na haijulikani atarudisha lini.

Pia unashindwa kumhudumia vizuri kwa sababu ni

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 63


rafiki hivyo anashindwa kuipata ladha kamili ya
huduma zako, yaani unamchukulia poa na
haumuhudumii kulingana na thamani ya pesa yake.

Hii inamfanya ashindwe kuwaeleza vizuri wengine


ubora wa huduma zako. Mwekezaji yeyote hawezi
kuwa radhi kuwekeza kwenye biashara yako ikiwa
atajua unaendesha mambo kirafiki.

Ukileta urafiki usio na mipaka kwenye biashara


utaua biashara yako. Bora watu wakuchukie kwa
kuwa na mipaka bayana kuliko wakakucheka baada
ya biashara yako kufa.

Tabia ya Tatu: Kuacha kujitangaza.

Kuna kiwango watu wakifika wanaacha kujitangaza


kwa sababu biashara zao zimepata umaarufu na
wateja wa kutosha. Biashara inahitaji kuendelea
kujitangaza bila kukoma. Katika mfumo wa
matangazo kama hausikiki basi hakikisha
unaonekana.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 64


Kama huonekani basi usikike, vikikosekana vyote
viwili biashara yako itaanza kudhorota. Hii ndio
sababu, kampuni kubwa na zinazojulikana vizazi
hadi vizazi kama Coca-Cola huwa haziachi
kujitangaza miaka yote.

Tabia Ya Nne: Huduma mbaya kwa wateja.

Eneo lenye changamoto Zaidi hapa ni pale mteja


anapokuwa na malalamiko. Sio watu wengi wanajua
namna ya kusikiliza na kutatua malalamiko ya
wateja. Kumbuka kila mteja ambaye hajaridhika na
huduma zako atapeleka taarifa mbaya kwa
wengine kuhusu biashara yako.

Wakati huo huo kila mteja unayemrishisha


unamfanya kuwa mfuasi wa biashara yako.
Anafanyika balozi na wakili wa biashara yako kwa
wengine. Kama ungependa kujua aina za wateja na
namna bora ya kuwahudumia, tafuta kitabu change
kinachoitwa Saikolojia Ya Mteja, kitakusaidia sana.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 65


Tafakari: Je, katika biashara unayofanya sasa
hivi, ni makosa gani ambayo umegundua huwa
unayafanya?

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 66


Sura Ya Tano

Jinsi Ya Kutengeneza Mfumo


Utakaokuza Biashara Yako Haraka

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 67


MAMBO 9 MUHIMU YA KUZINGATIA KABLA
HAUJATENGENEZA MFUMO WA KUKUZA
BIASHARA YAKO.

Ili biashara iweze kustawi kunapaswa kuwa na


mikakati inayohusisha mambo kadhaa.

i. Wazo bora la biashara

Wazo lako la biashara ndio kitu ambacho kitakupa


nguvu ya ushindani sokoni, yaani linakupa uwezo
wa kumiliki soko kubwa kuliko wengine. Pia wazo
bora hukubalika na hukupa faida kubwa.

ii. Timu bora ya kuendesha biashara

Ili kuweza kubadili wazo bora kuwa biashara yenye


mafanikio kunahitaji watekelezaji bora. Lengo la
timu ni kuziba mapungufu yako kwa kuongeza
nguvu zao, ujuzi na ufanisi kwenye maeneo
ambayo wewe huwezi kuyamudu vyema. Timu bora
itakufanya utekeleze wazo lako barabara ni hivyo
kukupa usitawi.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 68


iii. Mpango mkakati wa biashara.

Mpango mkakati na andiko la biashara ni dira ya


kukuelekeza nini kifanyike kila siku na kifanyike
kwa namna gani ili kupelekea ustawi wa biashara
yako. Pia inakupa picha ya ulipotoka, ulipo na
unapoelekea ili kukutia hamasa unapotimiza
malengo na kukuonya unapoonekana kusuasua.

iv. Upatikanaji wa mtaji

Huu ni ujuzi ambao kila mfanya biashara anapaswa


kuwa nao ili umsaidie kila anapotaka kuanzisha
biashara.

v. Fahamu bidhaa yako na ubora wake.

Uza bidhaa unazozijua vizuri. Usiuze kitu ambacho


huna ufahamu nacho hii itakufanya ushindwe
kuwapa wateja wako taarifa sahihi na hivyo
kupoteza uaminifu kwao.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 69


vi. Ujuzi juu ya fedha

Kama mjasiriamali lazima ujue mambo mbalimbali


yanayohusiana na fedha. Elimu juu ya fedha ni kitu
muhimu sana kwenye biashara.

Tunaposema faida tunasema fedha kuongezeka


kwenye mfuko wako, lakini sio kila fedha
zinapoongezeka inamaanisha unapata faida.
Lazima ujue lugha ya kifedha na misamiati yake. Hili
ni la muhimu sana katika usitawi wa biashara yako.

vii. Fahamu namna ya kuuza.

Hii inahusisha matangazo, utafutaji wa masoko na


uuzaji wenyewe. Mfanyabiashara anapokosa mbinu
za kuuza, haijalishi ubora wa bidhaa alizonazo,
biashara yake itafeli. Jitahidi kupata ujuzi wa kuuza.
Kitabu changu cha Mbinu Za Kuuza Zaidi,
kitakusaidia kujenga uwezo huu.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 70


viii. Ujuzi wa utawala na uongozi

Kuwa na mtaji mkubwa wa biashara na kuwa na


wazo zuri ni kitu kimoja, ila kuwa na uwezo wa
kusimamia biashara yako ni kitu kingine. Ili kukuza
biashara lazima ujenge uwezo wa kuongoza
wengine na kuhusiana na watu.

ix. Jenga kuaminiwa (Build Trust)

Watu wakikuamini hawatapata shida kutumia


bidhaa yako. Unapoaaminiwa na watu katika
maeneo mbalimbali inakupa urahisi kufanya
biashara kwa sababu watu wataihaimishia imani
hiyo kwenye kile unachokiuza.

Tafakari: Ukiangalia kwa sasa kwenye biashara


unayoifanya, ni kitu gani ambacho unakikosa
ambacho unahitaji kukifanyia kazi kwa haraka?

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 71


AINA TANO ZA MIFUMO ITAKAYOKUZA
BIASHARA YAKO KWA HARAKA

Unapotaka kukuza biashara yako kuna mfumo na


maeneo maalumu unayopaswa kuyaangalia. Hata
kwenye mwili wa binadamu kuna maeneo nyeti na
viungo vya msingi vya kuvizingatia ambavyo
visipokaa vizuri mwili wa binadamu unaweza kuwa
kwenye hatari kubwa.

Katika biashara kuna maeneo ambayo kama


unataka kukuza biashara yako lazima
uyashughulikie kwa haraka sana na kwa umakini
mkubwa ili uweze kupata matokeo ya haraka sana.

Yafuatayo ni maeneo ya kuyapa kipaumbele


unapotengeneza mfumo wako wa biashara:

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 72


Mfumo wa kwanza: Tengeneza mfumo utendaji
(Create performance system.)

Huu ni mfumo unaoonyesha unapata matokeo ya


namna gani na ufuatiliaji wake. Lazima ujiulize kama
una mfumo unaoweza kukuonyesha biashara yako
inafanyaje kazi.

Hapa inategemea na biashara unayofanya, lakini


mfumo huu unapaswa kuwa unakupa ripoti za
biashara yako, yaweza kuwa ripoti ya siku, au wiki
au mwezi.

Ili uweze kutengeneza mfumo mzuri lazima uwe na


vigezo unavyoweza kuvitumia kama sehemu ya
kupata ripoti ya utendaji.

Yaweza kuwa idadi ya wateja unaowahudumia kwa


saa au mwezi, au idadi ya bidhaa ambazo wateja
wamezirudisha kwa sababu ya kutokidhi viwango
vya ubora wake, au hata idadi ya bidhaa
unazoziuza.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 73


Ni muhimu kujua ubora wa uendeshaji wa biashara
yako unapimwa na nini. Unapaswa ujue wewe
unaipimaje biashara yako kama inaendeshwa vizuri.
Ni muhimu sana kupima ufanisi wa uendeshaiji wa
biashara yako.

Hii inajumuisha kujua uwezo wa kiutendaji wa


wafanya kazi wako pia.

Mfumo wa pili: Uwekezaji kwa wafanyakazi


(Investment to staffs)

Unapaswa kuwekeza sana kwenye wafanyakazi


wako. Hii inahusisha maeneo mawili, la kwanza ni
mahusiano.

Unahusianaje na wafanyakazi wako, je ni


mahusiano rafiki yanayoleta afya kwa biashara
yako au ni mahusiano yaliyojaa hofu, chuki na
unafiki.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 74


Huna budi kutengeneza mahusiano yanayowafanya
wafanyakazi wako wajione familia na sehemu ya
muhimu kwa mafanikio ya biashara yako.
Mahusiano yanayowafanya waone fahari kufanya
kazi na wewe na wewe sehemu ya maono ya
biashara yako.

Mazingira yanayowahamasisha kuwa chachu ya


ukuaji wa biashara yako. Ajione kama ikifeli
biashara na yeye anafeli.

Eneo la pili la kuwekeza kwenye timu yako ni


maarifa.

Wekeza kwenye kuwafundisha, watafutie


semina za kuongeza maarifa yao.

Kuna wakati kampuni moja ya ndege inaitwa Delta


Airlines, ilichaguliwa kama kampuni bora ambayo
wafanyakazi duniani kote wanapenda kufanya kazi
kwenye hiyo kampuni. Walipoenda kufanya
mahojiano na Mkurugenzi wake walimuuliza
kwamba mbona siku zote tumesikia

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 75


kwamba biashara ina maeneo makubwa matatu
mabayo ni wateja, wamiliki na wafanyakazi, na siku
zote tumeambiwa kwamba mteja ni mfalme
tukiamini kwamba mteja ndiye mtu wa kwanza
anayepaswa kuzingatiwa kwenye biashara.

Pia kwamba mmiliki ndiye anapaswa kupata faida


kubwa. Je, imekuwaje wewe mpaka umekuwa
kampuni bora ambayo kila mtu anatamani kufanya
kazi nayo?

Alichowajibu ni kwamba yeye anaamini kwamba


mtu muhimu zaidi kwa kampuni ni mfanyakazi, kwa
sababu mfanyakazi akiwa na furaha atamuhudumia
mteja vizuri.

Mteja akihudumiwa vizuri atafurahia huduma zako


na kuendelea kuzitumia kila siku na hata kuthubutu
kuwaambia wengine habari za kampuni yako. Hii
itazalisha faida kubwa ambayo wamiliki wa
kampuni watafurahia.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 76


Kwa hiyo usije ukadharau kuwekeza kwa
wafanyakazi wako ikiwa unataka biashara yako
ikue.

Mfumo wa Tatu: Washindani (Competitors)

Hufanyi biashara katika kisiwa ambako uko peke


yako. Ni jambo la hekima kujifunza kutoka kwa
washindani wako. Haujifunzi kutoka kwao eti kwa
sababu unataka kushindana nao au labda kwa
sababu unataka kuiga kutoka kwao, la hasha,
unajifunza ili ujue vitu gani bora zaidi unavyopaswa
kufanya.

Kumbuka kwenye kila unachokifanya vizuri leo kipo


kitu kingine kizuri zaidi cha kufanya kesho. Hutajua
cha kufanya kesho kama hauko radhi
kujifunza.Tafuta kujua wanafanya nini, wanafanyaje
vitu vyao, mbinu zao, n.k. itakusaidia kutoachwa
nyuma sana. Utakuwa mtu unaeenda na
mabadiliko.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 77


Ni vyema ukawa na intelijensia ya kibiashara
(Business Intelligence). Huu ni uwezo wako wa
kutafuta taarifa mbali mbali zinazohusiana na
biashara unayoifanya. Huu ni ujuzi muhimu sana
kwanye kukua kwa biashara yako. Usijaribu
kupuuzia hata kidogo kama unataka ufike mbali
kibiashara.

Eneo mojawapo la kupata taarifa hizo ni kutoka


kwa washindani wako, lazima ujue wananunua wapi
bidhaa zao, wananunua wapi malighafi zao,
wanajitangaza kwa namna gani na vitu
vinavyofanana na hivyo.

Mfumo wa nne: Mfumo wa usambazaji (Distribution


system)

Tunaishi katika ulimwengu unaoenda kasi sana, na


hakuna mtu anayetaka kukipata kitu kwa
kuchelewa wakati kuna mfumo rafik zaidi. Kwa hali
hiyo, unapaswa ujue ni namna gani rahisi
iwezekanavyo inayoweza kutumiwa kufikisha
bidhaa zako kwa wateja wako.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 78


Jitahidi kumfanya mteja wako atumie juhudi ndogo
sana kuipata bidhaa yako. Lakini pili hakikisha
unamfanya atumie muda kidogo kuipata bidhaa
yako. Kwenye soko la sasa hivi yeyote
anayewafikia wateja wake kwa urahisi
anawashinda wapinzani wake kwa urahisi sana.

Mfumo wa Tano: Teknolojia (technology)

Unapaswa ujue namna unavyoweza kutumia


teknolojia kukuza biashara yako. Matumizi ya
teknolojia yanalenga kukuokolea muda na gharama.
Pia yanalenga kukuongezea ufanisi wa kiwango cha
juu zaidi.

Unaweza kutumia mifumo ya automasheni


(Automation) ambapo mitambo inajiendesha
yenyewe bila kutumia watu, au inatumia maroboti
kufanya kazi.

Mfano makampuni ya simu yanapokutumia jumbe


zao huwa wanatumia mfumo huu.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 79


Badala ya watu kuanza kutuma jumbe kwa
mamilioni ya wateja wao teknolojia hii inafanya
watu wapate jumbe kwa kutumia mfumo maalumu
uliosetiwa kutuma kwa muda maalumu.

Pia unaweza ukatengeneza mfumo ambao


unakutengenezea ripoti wenyewe bila wewe
kuanza kuhangaika na kupoteza muda, hii
itapunguza gharama za kumuajiri mtu akuandalie
ripoti za biashara yako, lakini pia inapunguza
makosa ya kibinadamu katika kuandaa ripoti hizo.

Siku hizi ziko aplikesheni nyingi kwenye simu na


kompyuta zinazoweza kufanya mambo kama haya.
Ni wewe tu kujua namna ya kuzitumia. Hakuna
biashara ambayo haiwezi kutumia teknolojia.

Ni jukumu lako kujua unapaswa kutumia teknolojia


gani kuboresha na kukuza biashara yako.

Tafakari: Katika Mifumo hii iliyoelezwa, ni upi


ambapo unahitaji kuanza kuutumia kwenye
biashara yako kwa sasa hivi?

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 80


Badala ya watu kuanza kutuma jumbe kwa
mamilioni ya wateja wao teknolojia hii inafanya
watu wapate jumbe kwa kutumia mfumo maalumu
uliosetiwa kutuma kwa muda maalumu.

Pia unaweza ukatengeneza mfumo ambao


unakutengenezea ripoti wenyewe bila wewe
kuanza kuhangaika na kupoteza muda, hii
itapunguza gharama za kumuajiri mtu akuandalie
ripoti za biashara yako, lakini pia inapunguza
makosa ya kibinadamu katika kuandaa ripoti hizo.

Siku hizi ziko aplikesheni nyingi kwenye simu na


kompyuta zinazoweza kufanya mambo kama haya.
Ni wewe tu kujua namna ya kuzitumia. Hakuna
biashara ambayo haiwezi kutumia teknolojia.

Ni jukumu lako kujua unapaswa kutumia teknolojia


gani kuboresha na kukuza biashara yako.

Tafakari: Katika Mifumo hii iliyoelezwa, ni upi


ambapo unahitaji kuanza kuutumia kwenye
biashara yako kwa sasa hivi?

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 81


NJIA NNE ZA KUKUZA SOKO LA
BIDHAA/HUDUMA YAKO

Bila kujali biashara yako ni ya aina gani, au ina mtaji


kiasi gani, au ipo kwenye sekta gani, una nafasi ya
kuikuza na kufanya ifikie viwango vya juu kabisa.

Kuna njia 4 ambazo unaweza ukazitumia kukuza


biashara yako. Kadiri unavyoweza kuzijua njia hizi
kwa haraka ndivyo unavyoweza kujihakikishia
kukua kwako kwa uharaka Zaidi. Ili upanue biashara
yako kuna vitu viwili vikubwa vinavyopaswa
kuhusika kwenye mkakati wako.

Cha kwanza ni bidhaa zako, na cha pili ni soko


unalouzia bidhaa hizo. Kutokana na haya mawili
ndio tunapata njia hizi nne ya kupanua biashara.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 82


i. Market penetration (Kujiimarisha Kwenye Soko
Ulilopo).

Kwenye hii mbinu unabaki katika soko lilelile, ukiuza


bidhaa zilezile. Hii inamaanisha kama ulikuwa
unauza nguo eneo la soko la Manzese, utaendelea
kuuza nguo hapohapo Manzese.

Unachokifanya ni kujaribu kunyang’anya wateja


kutoka kwa wafanyabiashara wengine wanaofanya
biashara kama yako waliopo kwenye eneo lako ili
waje kwako.

Namna rahisi ya kulifanikisha hili ni, kwanza lazima


uwekeze nguvu kubwa matangazo ili watu
waendelee kukufahamu. Cha pili ni kutoa ofa na
promosheni za mara kwa mara ili kuwashawishi
wateja wa mahali pengine wakujie wewe.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 83


ii. Product development (Unaingiza Bidhaa Mpya
Kwenye Soko Lilelile).

Katika njia hii unatumia mkakati wa kutengeneza


bidhaa mpya katika soko lilelile.

Unachokifanya ni kuongeza orodha ya bidhaa. Kwa


mfano kama ulikuwa unauza sabuni tu, kwa njia hii
unaamua kuongeza na mafuta pia.

Cha muhimu ili njia hii ikunufaishe, kwanza lazima


ufanye utafiti wa kutosha kujua watu wanahitaji nini
ili usije ukapeleka bidhaa mpya sokoni ilihali bidhaa
hiyo haihitajiki. Pia lazima ufanye utafiti wa bei ya
bidhaa unayotaka kuileta.

Kumbuka kama biashara yako haipanuki Zaidi


huwezi kuongeza kipato kupitia bishara hiyo pia.

Usilete bidhaa mpya sokoni kabla hujafanya utafiti


wa kutosha. Kwa hiyo hapa pia hubadilishi soko ila
tu unaongeza bidhaa.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 84


Kwa mfano kama unauza chakula gengeni unaamua
kuanza kuuza na juisi ya matunda hapohapo.

iii. Market development (Unahamisha bidhaa


uliyonayo kwenda kwenye soko jipya).

Kwanye njia hii unatumia bidhaa zilezile ulizonazo,


lakini unachokifanya ni kutafuta soko jipya. Kwa
mfano kama wewe una duka la mahitaji ya
nyumbani mtaa A, unachofanya ni kuanzisha duka
lingine la mahitaji ya nyumbani mtaa B.

Watu wengi wanakwamishwa sana na hofu ya


kuingia kutafuta soko jipya la bidhaa zao.
Wanaogopa kutafuta watu wapya, wanaogopa
kwenda kutafuta sehemu mpya ya masoko.

Umeshakutana na watu ambao tangu uwe mdogo


mpaka umekua duka lake liko pale pale, hawezi
hata kwenda kufungua lingine mtaa wa pili. Kuna
watu ambao wanazalisha bidhaa nzuri sana lakini
shida yao ni kwamba hakuna mtu anayemjua kwa
sababu hana ujasiri wa kutafuta masoko mapya.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 85


Yaani wanaomjua ni wale waiomzunguka tu. Sio
lazima usubirie wateja wakufuate, unaweza
ukaamua kuwafuata waliko.

Unaweza kuamua kwenda wilaya nyingine au mtaa


mwingine, au mkoa mwingine, panapobidi hata nchi
nyingine ili tu kupata aina mpya ya masoko.
Unapotumia njia hii fokasi kubwa ni kupanua
mtandao wa wateja.

Wakati mafanikio yako yamejificha kweye ujasiri


wako wa kutafuta soko jipya la bidhaa zako. Tafuta
soko jipya, tafuta wateja wapya.

iv. Diversification (Bidhaa mpya kwa soko Jipya)

Njia hii inahusisha upanuzi wa vyote soko na


bidhaa kwa pamoja. Kwa lugha nyingine ni kwamba
unaleta bidhaa mpya na unaanzaisha masoko
mapya. Kwa maana kama hapa ulikuwa unauza
mchele, unaamua kwenda mtaa mwingine na kuuza
unga.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 86


Kwa hiyo badala ya kuuza mchele uleule unaamua
kuwaletea unga. Kwenye kuweka utofauti katika
kitu unachokifanya unaweza ukafanya mambo ya
aina mbili, la kwanza ni kuamua kuuza kitu
kinachoendana au kushabihihana na unachouza
sasa.

Kwa mfano, kama kwemye mkoa wa Mwanza una


duka la unga, Mtwara una duka la mchele, lakini
Dodoma una duka la mbogamboga. Hivi vyote ni
vyakula lakini kwenye kila sehemu kuna aina yake
ya chakula.

Hapa pia unaweza ukaweka vitu ambavyo


vinategemeana, kitu ambacho kinaweza kikakipa
thamani kitu unachakifanya. Kwa mfano, unauza
vifaa vya shule, unaamua kuweka na mashine ya
kutolea kopi.

Au unafuga kuku unaamua kununua na mashine ya


kutotoleshea vifaranga hapohapo. Kama unauza
vipodozi unaamua kuuza na bidhaa za urembo.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 87


Pili, unaweza ukaamua kuuza vitu ambavyo
haviendani kabisa. Kama ulikuwa unauza vitabu
unaamua kuanza kuuza duka la vifaa vya ujenzi pia.
Kitakachokuongoza ni uhitaji wa soko lako kwa
wakati huo. Usifanye upanuzi huu bila kufanya
utafiti yakinifu.

Tafakari: Katika njia hizi nne za kupanua biashara


yako, ni ipi ambayo unaona inafaa kuitumia
kwenye biashara yako kwa sasa?

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 88


Sura Ya Sita

Mambo Yanayodumaza Biashara

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 89


VYANZO VITANO VINAVYOSABABISHA
BIASHARA ISIKUE

Kuianzisha biashara ni kitu kimoja na lakini kuifanya


biashara hiyo ikue ni kitu kingine kabisa.

Kuna watu wengi ambao wameanzisha biashara na


zimedumaa. Ukiangalia leo ni kama ilivyokuwa
mwaka jana au mwaka juzi. Lakini kuna vitu
unapaswa kuviangali ili ujue kama biashara yako
inakua au la ili ujue hatua gani unapaswa kuchukua
Hizi ni sababu kwa nini biashara haikui.

Chanzo Cha Kwanza: Kutokuwa na mpango na


malengo ya ukuaji wa biashara yako (No growth
goals and plans)

Hii inamaanisha ni kweli mtu ameanzisha biashara


lakini hakuna malengo yoyote wala mkakati thabiti
wa kuifanya biashara hii ikue. Ni vigumu kukikuza
kitu ambacho hujakipangilia wala kukiandaa.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 90


Hakikisha unapoanzisha biashara unakuwa na
mipango kabambe ya kuifanya ikue na unaitekeleza
ili uone malengo yako yakitimia.

Ili biashara yako ikue lazima uweke malengo ya


ukuaji wake. Lazima uwe unajiuliza kama leo
nahudumia wateja kumi kwa siku, baada ya miezi
sita unataka wafike wangapi? Na unafanyeje kufikia
idadi hiyo.

Chanzo Cha Pili: Kukosekana kwa mtandao wa


kibiashara. (lack of business network)

Kwenye biashara ni kitu muhimu sana kuwa na


mtandao wa biashara hiyo. Kuna aina mbili za
mitandao ya kibiashara unayoihitaji kwenye
biashara yako.

Wa kwanza ni mtandao na wafanyabiashara


wanaofanya biashara kama yako. Yaani kama
wewe ni muuza nguo unapaswa kuwa na mtandao
na watu wengine wanaouza nguo kama wewe.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 91


Je, unawafahamu wafanyabiashara wangapi
wanaofanya biashara kama yako? Hawa ni watu
wanaokupatia bidhaa na taarifa za muhimu.

Hii ni muhimu kwa sababu kuna siku utaishiwa


bidhaa na utawahitaji wao ili kupata ili tu uweze
kumuhudumia mteja wako ambaye hutaki
kumpoteza.

Lakini pia kuna taarifa mpya kuhusu biashara


unayoifanya utazikosa kwa sababu tu huna watu
karibu wanaofanya biashara kama yako. Kwa hiyo
unapokuwa na mtandao wa namna hii hutapitwa na
taarifa muhimu kuhusu biashara yako.

Wa pili ni mtandao na wateja wako. Ni muhimu


kujua wateja wako na namna unavyoweza
kudumisha mahusiano nao kila wakati. Hakikisha
haupotezi muunganiko ulionao kati yako na wateja
wako.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 92


Jitahidi kuwa na mahusiano yenye afya na watu
wanaokuletea mzigo iwe malighafi au bidhaa
zilizochakatwa tayari. Mfano mahusiano na
kiwanda au mtu anayekuuzia mzigo kwa jumla.

Pasipo hawa huwezi kuwa na biashara. Kwa kadri


unavyozidi kuwa na mtandao imara ndivyo na
biashara yako inavyozidi kukua. Lakini unapokosa
mtandao na makundi haya mawili huwezi kuwa na
biashara inayokua.

Chanzo Cha Tatu: Kutaka kufanya kila kitu wewe


mwenyewe. (Doing it all youself)

Kuna kitu kinaitwa ugonjwa wa waanzilishi


(Founders Syndrome) . Hii ni hali ambapo
mwanzilishi wa kampuni au biashara haamini katika
kuwaachia majukumu watu wengine.

Utakuta yeye peke yake ndio anajua kila kitu, hii


inamaanisha kufa kwake ndio mwisho wa biashara
hiyo.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 93


Ni lazima ujue kugawa majukumu kwa wengine kwa
uzuri kabisa. Hii itakupa wepesi na ufanisi wa
kufanya mambo mengine huku ukisaidiwa na
wengine. Kwa maelezo zaidi tafuta video zangu
Youtube nilizofundisha kuhusu kugawa majukumu
kwa wengine na namna sahihi ya kufanya hivyo.

Kitu cha pili kwenye hili ni wewe kutengeneza


mfumo ambao utakusaidia kuendesha biashara kwa
niaba yako. Hii itaifanya biashara iendelee hata
wewe unapokuwa haupo.

Hii itarahisisha sana ukuaji wa biashara yako.


Mfumo utakupunguzia mzigo mzito uliokuwa
unaubeba peke yako.

Watu wengi hawapendi kuwa na mifumo kwa


sababu inawajibisha. Wanaona kama kuwa chini
ya mfumo kunawakosesha uhuru. Lakini mfumo
unakujengea nidhamu ya biashara hivyo
kukufanya ukue na kusitawi zaidi.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 94


Chanzo Cha Nne: Kukosa mkakati wa kimasoko
(No strategic marketing)

Huwa tunaamini kwamba ukiwa na bidhaa bora basi


watu watanunua, lakini ukweli ni kwamba haitoshi
tuu kuwa na bidhaa bora. Kuna watu wana bidhaa
bora lakini wanauza kidogo na kuna watu bidhaa
zao hazina ubora lakini wanafanya mauzo
makubwa.

Watu wengi wana biashara lakini hawana mkakati


wa kimasoko. Watu wasipojua ulichonacho
hawawezi kukutafuta hata kama ulichonacho ni
bora na muhimu sana kwao. Kwa sababu hii huwezi
kuwa na biashara inayokua.

Andaa mkakati mzuri wa kimasoko, ujue unataka


kuuza nini na kwa nani. Wafanye watu waijue
bidhaa yako.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 95


Chanzo cha Tano: Kupanga bei kwa kuhofia bidhaa
kutouzika/kukudodea (fear based pricing)

Mfanya biashara akiwa anaendeshwa na hofu


katika kupanga bei zake ni vigumu biashara yake
kukua. Bei ya bidhaa inaathiri sana mtiririko wa
wateja kwenye biashara yako. Ukikosa mkatati
mzuri wa kupanga bei ujue utakosa wateja pia.

Kama ungependa kujua mbinu za kisaikolojia za


kupanga bei, unaweza kutafuta kitabu changu cha
Mbinu Za Kuuza Zaidi, nimeeleza mbinu namna ya
kufanya hivyo.

Tafakari, Ukiangalia kwa Upande wako, ni chanzo


gani ambacho kimechangia kudumaa kwa
biashara yako?

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 96


EPUKA SABABU HIZI TATU AMBAZO
HUSABABISHA BIASHARA NYINGI KUFELI
MAPEMA.

Moja ya takwimu zinazoshangaza sana kwenye


ulimwengu wa biashara na mafanikio ni kwamba
biashara nyingi sana zikianza ndani ya miaka miwili
zinafeli.

Wataalam wanasema takribani katika kila biashara


kumi zinazoanzishwa nane zinafeli ndani ya miaka
miwili. Swali kubwa ni kwa nini watu wakianzisha
biashara zinafeli. Inawezekana na wewe umewahi
kuanzisha biashara na ikafeli, au unaendesha
biashara sasa inayozidi kufeli.

Ni vyema sana ukajua sababu zinazoongoza kuleta


changamoto ili uweze kujinasua na mkwamo huu.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 97


Sababu Ya Kwanza: Kushindwa kutofautisha
matumizi binafsi na matumizi ya kibiashara.

Kwenye elimu ya biashara na uhasibu kuna kanuni


muhimu sana inayosema wewe na biashara ni vitu
viwili tofauti kabisa. Mara nyingi watu
wakishaanzisha biashara na ikaanza kufanya vizuri
wanashindwa kutofautisha kati ya matumizi yao
binafsi na yale ya kibiashara.

Wakina mama ni wahanga sana kwenye eneo hili.


Akishaanza tu kufanya biashara basi kila hitaji lake
litatatuliwa na pesa ya kwenye biashara bila kujali
ni faida au mtaji.

Mtu anaweza akawa na duka la mahitaji ya


nyumbani, lakini kila kitu kikiisha nyumbani
atachukua dukani bila kufidia gharama zake.
Mwisho wa siku duka linaanza kufa taratibu.

Kwa hiyo wewe kama umeanzisha biashara


haijalishi ni ndogo au kubwa kiasi gani ikumbuke

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 98


kanuni hii ya kutofautisha kati ya matumizi binafsi
na yale ya kibiashara.

Njia rahisi ya kutatua hili ni kuhakikisha una kitabu


cha kutunza hesabu za biashara yako na kuandika
kila kitu ili kuepusha muingiliano huo.

Sababu Ya Pili: Kupanua biashara kwa haraka bila


kujenga mizizi.

Kwenye biashara mara nyingi kuna ile hali ya


kutaka kujaribika kutaka kukua zaidi na zaidi kwa
muda mfupi.

Unapoanza biashara mara nyingi inakuwa


inachanua na mambo yanakua sawa sana. Hii
inahamasisha sana mtu kuwa na pupa ya kujitanua
bila hata kuwekeza kwenye kujenga msingi imara
wa biashara na ndipo uendelee kujipanua.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 99


Siku zote kumbuka hii kanuni, “kadiri
unavyokwenda chini sana ndivyo utakavyokwenda
juu Zaidi.” Kwa hiyo biashara yako inapaswa iwe
kubwa kwa kadiri ya msingi unaoutengenezea na
sio kwa kuangalia uharaka wa kapanuka kwake.

Usipanue biashara kwa ukubwa sana kama


hujaweka msingi ulioenda chini sana hasa hasa
misingi inayohusiana na kujenga mifumo imara ya
biashara yako.

Sababu Ya Tatu: Kuwekeza pesa nyingi kwenye


vitu ambavyo havihusiani moja kwa moja na
uzalishaji katika biashara.

Hapa nazungumzia matumizi ya kibiashara ambayo


hayaongezi uzalishaji. Kwa mfano mtu ana mtaji wa
milioni moja analipia ofisi laki sita halafu laki nne tu
ndio anaweka kwenye kununua bidhaa na mambo
mengine. Hapo upo njia panda ya kufeli.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 100


Au mtu amefanikiwa kidogo tu halafu anaenda
kununua gari la gharama kubwa ambalo anatumia
gharama kubwa kuliendesha pia.

Kila kitu unachotaka kuwekeza pesa nyingi kwacho


jiulize kama kina uhusiano wa moja kwa moja na
uzalishaji. Kama jibu ni hapana basi achana nacho
au ukiwekee bajeti ndogo zaidi ili kwenye uzalishaji
ndio kuwe na uwekezaji mkubwa Zaidi.

Tafakari: Kuna sababu yoyote kati ya hizi


imeshawahi kukufelisha au umemuona mtu akifeli
kwa sababu hiyo?

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 101


Sura Ya Saba

Unachotakiwa Kufanya Baada


Ya Kufeli Kwenye Biashara

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 102


UFANYE NINI UKIPOTEZA MTAJI?

Mimi binafsi nimewahi kupoteza mtaji kwenye


biashara zaidi ya kumi nilizowahi kufanya maishani
mwangu. Swali la msingi linakuja, ufanye nini
unapojikuta umepoteza mtaji?

Wengine baada ya kupoteza mtaji walijikuta


wameacha kabisa kufanya biashara. Wengine
wameingiwa na hofu kubwa sana kiasi cha
kupoteza kujiamini kwao. Wengine wamekata
tamaa hawaamini kama wanaweza kufanya
biashara tena.

Jambo la Kwanza: Tafuta chanzo kilichofanya


upoteze mtaji wako

Nilipopoteza mtaji kwenye biashara nilizokuwa


ninafanya ilinibidi nitafute chanzo cha tatizo hilo.
Niligundua kuna vyanzo mbalimbali. Yaweza kuwa
kutokuwa na maarifa maalum kuhusiana na
biashara unayofanya.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 103


Yaweza ikawa usimamizi mbovu wa biashara, hii
inahusisha haswa matumizi mabaya wa fedha
zinazopatikana kwenye biashara.

Wewe pia juilize tatizo lilikuwa nini haswa mpaka


ukapoteza mtaji wako. Ukipata majibu haya
umetatua Zaidi ya nusu ya tatizo lako.

Jambo la Pili: Jidhatiti kwenye kwenye kile chanzo.

Ukishajua labda umepoteza mtaji kwa sababu ya


usimamizi mbaya wa biashara jambo linalofuata ni
kutafuta ufumbuzi wake. Hapo nataraji uandae
mpango mkakati wa namna wa kuleta utatuzi wa
kudumu kwenye changamoto hiyo.

Jambo la Tatu: Jiimarishe kihisia.

Unahitaji uimara wa kihisia unapojikuta umepoteza


mtaji. Kupoteza kunamfanya mtu kuathirika kihisia.
Hii inamfanya apate wakati mgumu sana linapokuja
suala la kuanza tena.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 104


Kama hujawa imara vya kutosha ukirudi tena
kwenye biashara utaingia na hali ya hofu na woga.

Jambo la Nne: Anza tena

Unapoanza tena unaweza kuamua kuanza kwa


kidogo zaidi ya kile ulichowekeza awali ili upate
muda wa kurejea hali yako ya awali. Upate muda
wa kupona maumivu ya kupoteza. Usiogope
kuthubutu tena na tena.

Usikae muda mrefu sana bila kuanza tena. Usisusie


biashara yako, amka tena kama shujaa huku ukiwa
na funzo jipya zaidi ulilolipata kwenye kupoteza
kwako mtaji. Kufeli kwako ni ada unayolipia kwenye
shule yako ya biashara.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 105


JE, NINI KINAFANYA MTU AFELI KWENYE
BIASHARA ALIYOIANZISHA?

Kuna watu wengi walishawahi kuwa na ndoto.


Pengine hata na wewe umewahi kuwa na ndoto
lakini leo ni kama vile umeikatia tamaa.

Umeshawahi kujiuliza nini kinasaabisha ule


msukumo na hamasa uliyokuwa nayo kupotea. Nini
huwa kinawasababisha watu waishie njiani.

Ni muhimu sana kujua ili na wewe usiwe mmoja wa


wale watakaoishia njiani. Zifuatazo ni sababu za
kwanini watu wanapoteza hamasa, kukata tamaa
na kuishia njiani.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 106


Sababu ya Kwanza: Kutilia shaka uwezo wao.

Mara nyingi kinachokufanya usifanikiwe sio kwa


sababu huna uwezo wa kufanya hivyo ila ni kwa
sabababu ya kuwa na wasiwasi juu ya uwezo huo.
Kuna watu wana uwezo mdogo sana
ukiwalinganisha na wewe lakini wameweza kufanya
makubwa zaidi yako.

Tofauti yenu ni kwamba wao waliamini katika


uwezo wao huo mdogo wakati wewe unautilia
mashaka uwezo mkubwa ulionao. Haijalishi uwezo
wako ni mkubwa kiasi gani kama huamini katika
uwezo huo, hautaweza kufanikiwa.

Hali ya kutilia mashaka uwezo wako inasababishwa


sana na kusikiliza kile watu wanakuambia kuliko
kujisikiliza wewe ndani yako. Wapo watu wengi
ambao kazi yao ni kuwakatisha tamaa wengine. Kila
kitu kwao ni haiwezekani.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 107


Utasikia mtu kama wewe huwezi kabisa kufanya
kitu kama hiki, umri wako bado sana, hauna uzoefu
wa kutosha kufanya kitu hiki, historia yako
hairuhusu, wewe ni maskini hivi vitu wanafanya
matajiri n.k.

Unapoyaamini maneno yao unaanza kupoteza


uwezo wa kujiamini kwenye kila jambo maishani
mwako. Kujiamini kwako ni muhimu sana kuliko
kusubiri watu wengine wakuamini.

Kama utajiamini unaweza ukaendelea mbele na


biashara yako bila kujali wangapi wanaamini
kwenye uwezo wako.

Haijalishi watu wangapi wanakuamini ukijitilia


mashaka mwenyewe kukuamini kwao ni bure
kabisa.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 108


Sababu Ya Pili: Kufeli ulikowahi kukupitia nyakati
za nyuma.

Watu wa namna hii kila siku wanabaki tu kusimulia


jambo hilo walilowahi kufeli maishani mwao.
Utakuta mtu alilima mara moja akapata hasara basi
kila wakati atabaki tu kulalama, nilipoteza mtaji,
nilipoteza mtaji, nilipoteza mtaji.

Usiruhusu kushindwa mara moja ndio kuwe


utambulisho wako. Usiruhusu kufeli kukuamulie
utakuwa nani kwenye maisha. Hakuna mtu ambaye
hajawahi kufeli au kushindwa jambo kwenye
maisha.

Ni wale tu wanaokataa kuamriwa maisha na kufeli


huko, ndio wanaoibuka washindi. Mafanikio ni
matokeo ya kushindwa kwingi kulikokupa madarasa
mengi ya kukukamilisha ili uweze kuifikia ndoto na
malengo yako.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 109


Nia yako inapaswa kuzidi kushindwa kwako. Kuna
mtu anaitwa Michael Jordan, ni mtu maarufu sana
kwenye kwenye tasnia ya mpira wa kikapu nchini
Marekani na duniani kote. Amekuwa na mafanikio
makubwa sana katika wakati wake wa kuwa
mcheza mpira wa kikapu.

Kitu usichokijua kumuhusu ni kwamba siku


wanachagua timu ya kikapu ya shuleni kwake kiwa
bado kijana mdogo, aliachwa kwa sababu
alionekana hafai na hawezi.

Lakini baadae ameacha historia yenye ladha tamu


sana katika mchezo huu kwa sababu ya ubora na
uwezo wake. Hii ni kwa sababu hakuruhusu
kushindwa huko kuyatafsiri maisha yake.

Usiruhusu kitu ambacho kimekushinda leo kiamue


utakuwa nani kesho. Kila kushindwa ni fursa ya
kuanza upya katika ubora maridhawa. Usikubali
kukata tamaa eti kwa sababu biashara yako imefeli.
Inawezekana kuinuka tena.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 110


Sababu Ya Tatu: Hawaoni matokeo kwa haraka.

Unaweza kuanzisha biashara na usione faida kwa


haraka. Habari njema ya kukumbuka ni kwamba
kuna mambo ambayo yatachukua muda kutokea.
Sio kila mbegu ikipandwa itaota ndani ya muda
mfupi.

Kama biashara uliyoianzisha inachukua muda mrefu


sana basi usisahau kuwa mvumilivu. Uvumilivu
wako ni wa muhimu sana. Nikukumbushe tu
kwamba ukitaka kujenga ghorofa ndefu sana huna
budi kutumia muda murefu kuchimba chini sana ili
uwe na msingi ulio imara.

Kuna wakati hutapata matokeo, sio kwa sababu


hayapo lakini kwa sababu muda wake haujafika
bado. Usikate tamaa kwa sababu huoni matokeo ya
haraka. Ikiwa unajua unachofanya ni kitu sahihi kazi
yako ni moja tu, SONGA MBELE!!!

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 111


Sababu Ya Nne: Kosa la kujilinganisha na wengine.

Kuna mtu aliwahi kusema ukurasa wako wa kwanza


waweza kuwa ndio ukurasa wa kumi wa mtu
mwingine. Usikae ukaanza kuona mbona fulani
yupo kule wakati mimi bado nipo pale pale.

Kumbuka wewe ni mtu wa pekee, una safari ya


kipekee kulinganisha naya wengine. Usijilinganishe
na wengine. Unaweza kujifunza kwa wengine lakini
kamwe usithubutu kujilinganisha nao.
Unachotakiwa kufanya ni kuweka juhudi na bidii
katika biashara unayoifanya sasa.

Lakini waliotangulia mbele wasikukatishe tamaa


kuona kama haiwezekani. Usisahau kwamba kila
mtu aliyebobea sasa siku moja alikuwa
mwanafunzi. Biashara yoyote unayoiona
imesimama sasa kuna siku ilianza mahali fulani.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 112


Kwa hiyo usiogope kuanza eti kwa sababu kuna
wengine wameshafanya kile unachotaka ukifanye.
Usijifananishe nao, wala usiyaendeshe maisha yako
kwa kutaka kulazimisha kuwa kama mtu Fulani.

Sababu Ya Tano: Kuridhika Mapema.

Kuna watu wengi sana ambao wamelazimika


kukwama mahali walipo kibiashara kwa sababu tu
wanaona wanapata kifaida cha kuwatosha ili hali
mioyo yao inatamani pakubwa zaidi. Usikubali
kuishia hapo ulipo wakati kuna mahali pazuri zaidi
unapatamani.

Wala usikubali kukata tamaa eti kwa sababu kwa


sasa huoni kama unaweza ukasonga mbele zaidi ya
mahali ulipo. Hakuna kukubaliana na hali halisi. Hali
halisi ni wewe kupafikia mahali unapopatamani
ndani yako. Hali halisi ni wewe kupavuka hapa
palipokukwamisha. Hiyo ndiyo hali halisi.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 113


Wewe ni bora zaidi ya hapo na unao uwezo wa
kutoka mahali ulipokwama, unaweza kukivuka
kihunzi hicho. Kumbuka Penye nia pana njia.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 114


CHUKUA HATUA ZIFUATAZO ILI UINUKE TENA
BAADA YA KUFELI KWENYE BIASHARA YAKO

Mojawapo ya ugumu utakaokutana nao kwenye


maisha ni kuanzisha biashara na ikafeli. Kuna
wengine wameshindwa kuinuka tena na kuendelea
na biashara baada ya kufeli mara moja au mara
kadhaa. Hatua hizi zitakusaidia kujua ufanye nini
baada ya biashara yako kufeli.

Hatua Ya Kwanza: Julize swali la kwa nini nimefeli?

Usipojua sababu iliyokufanya ufeli ni vigumu sana


kuinuka tena maana inawezekana hata ukiamua
kuanza upya tena sababu ileile itakufelisha tena.
Lakini pia itakuwa vigumu kuja na mkakati rafiki wa
kukufanya ufanikiwe maana utafanya kwa
kubahatisha.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 115


Yapo maswali ya kujiuliza ili kujikagua na kujua
chanzo cha kufeli kwako. Jiulize, je wazo lako la
biashara lilikuwa sahihi? Yawezekana ulilikurupukia
tu kwa sababu kila mtu anafanya lakini kiukweli
kabisa halikuwa sahihi kwako.

Jiulize je, nilipoweka biashara yangu ni mahali


sahihi? Yaweza kuwa una wazo zuri kabisa la
biashara lakini mahali ulipoianzishia ndipo penye
changamoto. Ukijua mahali ndipo tatizo la kufeli
kwako basi itakulazimu uhame ili usiendelee kufeli.

Je, ulijitangaza vya kutosha? Ukiwa na huduma au


bidhaa nzuri lakini watu hawakujui haina maana
kabisa. Ni sawa na hakuna.

Je, gharama za uendeshaji wako zipoje?


Inawezekana gharama za uendeshaji wa biashara
yako ni kubwa zaidi kuliko mapato unayoingiza Kwa
hiyo kabla hujaendelea na hatua za mbele ni
muhimu sana kujijibu vizuri maswali haya ili upate
chanzo halisi cha kufeli kwa biashara yako ndipo
uendelee na mengine.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 116


Ni maswali muhimu kama unataka kuanza upya iwe
biashara nyingine au kuifufua ileile.

Hatua Ya Pili: Fufua tena hamasa yako (rekindle


your passion)

Lazima uzingatie kuifufua tena hamasa ya kufanya


biashara baada ya kufeli. Huwezi kuendelea ikiwa
umepoteza hamasa. Usijaribu kuanza upya ikiwa
ndani yako umepoteza hamasa ya kufanya
biashara. Pata muda wa kutosha wa kuiamsha
hamasa yako tena.

Sijaribu kuanzisha biashara kwa sababu ya kutaka


kufukia mashimo. Kuna watu ambao wakifeli
kwenye biashara anaamua kuanzisha tena au
kuanzisha biashara nyingine mpya ili tu
kuwaonyesha watu kwamba hajashindwa na
anaweza.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 117


Wanafanya hivyo si kwa sababu wanataka
kufanikisha biashara zao ila kwa sababu tu
wanataka kuficha aibu ya kufeli.

Usichukue hatua ya kuanzisha biashara eti kwa


sababu unataka kuficha aibu ya kufeli kwako.
Itafute ile hamasa yako uliyoipoteza kwa kufeli
kabla hujaanza kujijenga upya.

Unaijengaje hamasa yako upya ni kwa kutafuta


taarifa chanya na sio hasi, kusikiliza vitu vya
kukujenga na kuwaza mawazo chanya.

Hatua Ya Tatu: Huishwa kisaikolojia

Unapofeli kuna madhara makubwa yanatokea


katika akili yako na hisia zako. Unachokihitaji hapa
ni uponyaji wa kihisia. Kufeli kunaambatana na mtu
kuanza kuona kama hawezi, kujiona sio mtu wa
maana, kujihisi huna thamani tena.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 118


Pia unaanza kujisikia kama wewe sio mtu mwenye
hatma ya mafanikio. Hali hizi ni vipingamizi vikubwa
ya biashara yako. Kuna watu watatumia kufeli
kwako kukulaumu, watakuambia ulikuwa na pesa
nyingi na umezichezea, haya yote yanaweza
kukufanya ujisikie hatia kubwa moyoni mwako.

Sasa hapa unaanza tena kubeba mzigo wa hatia na


unapoteza kujiamini kwako. Unaweza ukajikuta
unajificha tu, hutaki watu wakuone. Kila mtu unahisi
anakuzodoa hata kama kiukweli kabisa hana
mpango na wewe. Yaweza kuwa labda hata hajui
kinachoendelea kwenye maisha yako.

Uponyaji wa kisaikolojia pia unahusisha


kushughulikia mtazamo wa kufeli ulioumbika ndani
yako kama matokeo ya kushindwa kwa biashara
yako. Kushindwa mara moja haikufanyi wewe kuwa
mshindwa daima.

Usiruhusu kushindwa kukutafsiri wewe kama


mshindwa.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 119


Ifanye akili yako ikatae mtazamo wa kushindwa.
Usiruhusu kukata tamaa itawale akili yako.
Unaweza kutafuta msaada wa kisaikolojia
unapoona mambo yamekuzidia sana ili mradi tu
upone.

Usipofanyia kazi hili unaweza kuharibikiwa sana


kimaisha. Kuna watu wameishia kujidhuru kwa
sababu ya kukosa msaada kwenye eneo hili,
wengine hadi wamejnyonga.

Usikipuuzie hiki kipindi. Watu wengi wanaoanzisha


biashara tena bila kufanyia kazi hali hii huishia
kufeli tena.

Hatua Ya Nne: Pata mawazo na ushauri wa mtu


mwingine.

Watafute watu wanaofanya biashara kama yako


upate mwongozo na ushauri wao juu ya kufeli
kwako. Yawezekana kuna mtu pia amewahi kufeli
kama wewe na akainuka tena hii itakupa wepesi wa
kuinuka tena maana una mfano ulio hai.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 120


Jaribu kuzungumza nao, wadadisi, pia kuwa mkweli
kwao ili wakujulishe wapi umekosea na uchukue
hatua gani.

Pia watafute walezi wako (Mentors). Sijajua kama


una mlezi kwenye maisha yako lakini kama huna
nakushauri umtafute haraka iwezekanavyo. Hawa
ni zaidi ya washauri na makocha wa maisha yako.
Ni kama wazazi au walezi wako kwenye eneo
unalowapa nafasi.

Kama unataka kufanya biashara basi mtafute


mentor ambaye ni mfanya biashara pia. Yeye
atakuwa kama baba yako kwenye biashara. Ni
watu wanaokuonyesha njia na kukuelekeza kitu cha
kufanya.

Kwenye nyakati za kufeli kwenye biashara ndio


nyakati muhimu sana kwa watu hawa kuwepo
kwenye maisha yako. Hivyo unapofeli mtafute
mentor ili upate mwongozo wa nini cha kufanya ili
uweze kuinuka tena.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 121


Hatua Ya Tano: Kuwa na mpango bayana na
ufanye maandalizi thabiti.

Baada ya hatua zote hapo juu unapaswa ukae chini


utengeneze mpango mzuri wa namna ya kuinuka
tena. Fanya maandalizi ya kuanza upya ukiwa na
nguvu mpya na kasi mpya. Kumbuka bila kujali
umefeli mara ngapi unaweza kuinuka tena. La
msingi ni kuzingatia hatua hizi.

Tafakari: Kama uliwahi kufeli kwenye biashara


uliyowahi kuifanya huko nyuma, ni hatua gani
ambazo unaona unapaswa kuzichukua kwa sasa?

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 122


Sura Ya Nane

Sababu Zinazopelekea Wasomi


Wengi Kufeli Kwenye Biashara
Wanazoanzisha

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 123


Moja kati ya uzoefu ambao nimekutana nao ni suala
la wasomi wengi kutofanya vizuri kwenye biashara.
Mbaya zaidi hata wale waliosomea mambo ya
biashara ndio kwanza hawana hata biashara ndogo
au wakijaribu kutumia usomi wao wa darasani
wanajikuta wamefeli kabisa.

Wengi wao wanaamini labda kwa sababu ni wasomi


wakianza biashara basi watafanikiwa lakini cha
kushangaza wengi wanaishia kufeli vibaya kwenye
ulimwengu wa biashara.

Katika kutafiti nimegundua kwamba zipo sababu


sita zinazopelekea wasomi wengi kufeli kwenye
biashara.

Sababu Ya Kwanza: Shuleni wasomi


wanafundishwa kuepuka kufeli.

Kwenye mifumo ya shule kufeli ni jambo la aibu


sana. Kufeli kunakufanya uonekane kama huna
akili. Lakini inapokuja kwenye biashara mambo
yako tofauti kabisa.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 124


Wakati kwa wasomi kufeli ni ishara ya kutokuwa na
akili huku kwenye biashara kufeli ndio darasa
lenyewe unalopaswa kupitia kabla haujafanikiwa.

Huwezi kufuzuu shule ya biashara kama hujawahi


kufeli kwa sababu madarasa ya biashara yapo
katika kufeli kwako. Waliofanikiwa kwenye biashara
walifeli kwanza ndipo wakafuzu lakini kwa wasomi
wanasoma kisha mitihani halafu vyeti.

Kwa mtazamo huu huwafanya washindwe kufanya


vizuri kwenye biashara maana shule imewaandaa
kushindwa kuhimili misukosuko ya kufeli, ilihali
kufeli ndio darasa lenyewe kwenye biashara.

Kufeli ni ada unayolipia kwenye shule ya biashara.


Wasomi wengi wanasubiria mpaka wawe na
uhakika sana kwamba wanachokifanya
hakitawapelekea kufeli. Hii inawafanya waishie
kusubiri hakikisho hilo mpaka wanazeeka.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 125


Kiukweli kwenye biashara huhitaji kila kitu kiwe
sawa kwa asilimia mia. Kwa ufupi wasomi wengi
wakiona kuna dalili za kufeli kwenye wanachotaka
kufanya basi wanaogopa kufanya kwa sababu
kwenye tafsiri yao, wakifeli wataonekana hawana
akili.

Wasomi kabla hawajachukua hatua ya kujikana


wanaanza kujiuliza itakuwaje nikifeli jambo
linalowanyima hamasa ya kufanya. Lakini kwa
upande mwingine wa wale wasiokuwa wasomi
wanajiuliza hivi itakuwaje likifanikiwa? jambo
linalowapa hamasa ya kuchukua hatua.

Sababu Ya Pili: Kutaka Raha Za Haraka (Instant


gratification)

Wasomi wengi wamefundishwa kujiridhisha. Watu


wengi sana wapo tayari kufanya vitu vinavyowapa
hakika ya sasa hata kama hajui sana kuhusu
baadae yake. Hii inawafanya baadae kuteseka.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 126


Hali hii inasababishwa na kukosa ufahamu wa
kifedha. Kuna tofauti kubwa sana kati ya kusoma
darasani kisha kufaulu na kuwa na ufahamu wa
elimu ya fedha. Ufahamu wako juu ya fedha ni wa
muhimu sana katika mafanikio ya kibiashara kitu
ambacho wasomi wengi wanakikosa.

Wasomi wengi kwa sababu ya kukosa ufahamu wa


kifedha wanawekeza kwenye vitu vinavyotumia
fedha badala ya kuwekeza kwenye vitu
vinayoingiza fedha. Kwa hiyo hata akianzisha
biashara fokasi yake kubwa ni kutaka watu
wamuone ameanzisha biashara kubwa.

Kwa hiyo ataweka mtaji mkubwa zaidi kwenye vitu


ambavyo haviingizi fedha badala ya kuwekeza
fedha nyingi Zaidi kwenye bidhaa anayotaka
kuiuza.

Yaani atataka kupata ofisi kwenye eneo la gharama


na ikiwezekana ghorofani, utakuta ananunua
samani za bei ghali, anairemba ofisi kwa gharama
kubwa sana, kununua gari la gharama kwa ajili yake

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 127


kama mkurugenzi n.k Hata maisha ya wasomi
wengi ukiyafuatilia wana matumizi makubwa kuliko
vipato vyao.

Wanatumia fedha nyingi kulinda hadhi zao kuliko


kwenye kuwekeza. Kwa kawaida matumizi yako
kwenye mambo ya msingi (Basic Needs)
yanapaswa kutozidi asilimia hamsini ya kipato
chako lakini wasomi wengi wanatumia zaidi ya
hapo.

Kwa hiyo hata akianzisha biashara tabia hii inaingia


moja kwa moja kwenye biashara yake. Atajikuta
anatumia zaidi ya faida anayoitengeneza.

Sababu Ya Tatu: Kiburi cha maarifa (Intellectual


Arrogance).

Watu wengi wakishasoma na kupata vyeti vyao


wanaanza kuamini kama wao ndio wanajua kila kitu.
Kiburi hiki kinawafanya wasiwe tayari kujifunza.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 128


Kuna vitu ambavyo wangejifunza wangepata
matokeo makubwa sana kwenye biashara lakini
usomi wao hauwaachi wakafanya hivyo.

Kuna tofauti kubwa kati ya kusoma na kuelimika.


Kusoma kutakupa vyeti lakini kuelimika ni matokeo
ya maarifa uliyoyapata. Unaweza ukasoma na
usielimike. Na unahitaji sana elimu kuhusiana na
kujitambua na maendeleo binafsi.

Ni kazi sana kwa msomi kujifunza kwa mtu


mwingine hasa yule ambaye amefanikiwa lakini
hana elimu ya darasani. Haijalishi amefanikiwa kiasi
gani wasomi watapata ugumu kumsikiliza.

Hili linachelewesha biashara za wasomi wengi


sana. Unakuta kuna mtu amefanikiwa sana kwenye
biashara fulani ingawa sio msomi, lakini msomi kwa
kiburi cha maarifa hataki kwenda kujifunza kwake,
anaamua kuanza tu, matokeo yake anafanya
makosa ambayo angeweza kuyaepuka.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 129


Sababu Ya Nne: Mashindano (Competition)

Mfumo wa elimu ya darasani unafundisha sana


mashindano. Kila mtu shule anapambana kuwa juu
ya wengine. Hii inasababisha ubinafsi na
kukimbizana kwingi. Mara zote darasani
wanakuambia lazima uwe wa kwanza.

Hii ni falsafa mbaya sana kwenye ulimwengu wa


biashara maaana inakufanya mara zote uangalie
nani anakuzidi badala ya kufokasi kwenye malengo
yako. Ushindani ni kitu kinachowatoa wengi
kwenye njia zao na kuwafanya washindwa
kufanikiwa.

Wakati darasani tunafundishwa zaidi (Competition-


Ushindani) ili kuwa juu yaw engine, kwenye
biashara unahitaji (Collaboration-Ushirikiano) ili
uweze kufanikiwa kwa haraka.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 130


Darasani ili ufaulu utakuta mtu anaficha materials
yake, hashirikiani na wenzake na mtihani anafanya
peke yake, kwenye biashara unahitaji kuhusiana na
wengine ili uweze kufanikiwa.

Mashindano yanakufanya ujifungie wakati biashara


inakutaka ufunguke. Huwezi kujenga mtandao wa
kibiashara kama umejifungia kwenye mfumo wako
mwenyewe.

Sababu Ya Tano: Wana njia mbadala nyingi (Too


Many Alternatives).

Mtu ambaye hajasoma sana hana njia mbadala


nyingi. Akikipata kitu cha kumtoa kimaisha
atakishikilia kwa nguvu zake zote , lakini wasomi
hawahitaji kujipa taabu hiyo. Wao wanajua
wakishindwa hili watakimbilia hili.

Unapokuwa na njia mbadala nyingi huwezi


kuwekeza nguvu zako zote kwenye kitu
unachokifanya.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 131


Na kwa sababu hiyo hata kama ulikuwa na uwezo
wa kufanikiwa utashindwa kwa sababu
changamoto ndogo tu itakufanya ukimbilie mbadala
mwingine uliouandaa .

Watu wengine wanafanikiwa kwa sababu


wameweka fokasi yote hapo. Ili ufanikiwe lazima
utumie falsafa ya kuchoma meli zako zote
niliyoilezea vizuri kwenye kitabu changu cha Timiza
Malengo Yako, falsafa hii imewasaidia watu wengi
sana kufanikiwa.

Sababu Ya Sita: Hawako tayari kuanza chini.

Shule imewaandaa kuwa watu wenye vyeo


maofisini. Kwa hiyo wanapomaliza shule wanajiona
kama mabosi na kuwa hawatakiwi kufanya kitu kwa
mikono yao. Kwa mantiki hii hawezi kukubali
kuanzia padogo panapompa majukumu ya
kiutendaji badala ya yale ya kiutawala.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 132


Anaweza akawa na mtaji, ana fursa nzuri lakini
anaogopa kuanzia chini kwa sababu anaona aibu.
Hili ni tatizo kubwa sana. Kumbuka ili ufanikiwe
wakati mwingine lazima ukubali kuanzia chini.
Kuanzia padogo kunakupa fursa kubwa ya
kujifunza kuliko kuyakuta mambo yote yapo sawa.
Kwenye biashara hatusubiri tuwe wakubwa ili
kuendesha mambo vizuri, lakini tuendesha mamba
vizuri ili ili tuwe
wakubwa.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 133


Sura Ya Tisa

Watu Wa Karibu Wanavyoweza


Kuua Biashara Yako
Na Jinsi Ya Kuwakabili.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 134


NJIA 5 ZINAZOTUMIKA NA WATU WA KARIBU
KUUA BIASHARA YAKO

Hivi unajua kwamba kuna biashara nyingi amabazo


zimeuawa na watu walio karibu na mwanzilishi wa
biashara ?.

Nimekutana na watu wengi sana ambao ukiwauliza


kwa nini biashara zao zimeshindwa kuendelea, au
kupanuka au zimedumaa watakupa sababu ambazo
zinahusisha nguvu ya ndugu, jamaa au marafiki.

Watu wa karibu kwa ujumla wanaongoza kwa kuua


biashara. Na kuna namna watafanya, yaani utafikiri
wamefundishwa kuifanya biashara yako ianguke. Ni
muhimu sana kujua namna hawa watu wakaribu
wanavyoweza kuua biashara yako ili ujue namna ya
kuwakabili.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 135


Njia Ya Kwanza: Wanataka punguzo la bei mpaka
chini kabisa.

Yaani mtu wako wa karibu ambaye ungetegemea


afurahie na kujitoa zaidi kukusaidia ndio anakuwa
wa kwanza kutaka punguzo kubwa. Kwa hiyo
badala ya kukufanya upate faida kubwa
wanakufanya upate faida ndogo sana kwa sababu
ya mapunguzo wanayoyaomba.

Utashangaa ndugu au rafiki yako wa karibu, yuko


tayari kununua kitu kwa bei ghali mahali pengine ila
kwako anataka umpunguzie hadi chini kabisa.

Njia Ya Pili: Hawatangazi biashara zako

Mara nyingi watu wa mbali ndio wanasifia biashara


yako, utaona ndio wanasaidia kutangaza biashara
yako. Ndugu wengi wa karibu hawana muda wa
kutangaza biashara yako.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 136


Unakuta mtu ni ndugu au rafiki yako wa karibu
lakini hata siku moja hajawahi kupost kwenye
mitandao ya kijamii au hata kuweka kwenye status
yake ya WhatsApp .

Wakati mwingine wanakuwa mstari wa mbele wa


kuikandia kabisa. Kwa kufanya hivyo wanachangia
kufa kwa biashara za watu wao wa karibu.

Kama una watu wako wa karibu wanafanya


biashara, basi jifunze kuwasaidia watu wako wa
karibu. zitangaze biashara zao. Watie moyo na
kuwatetea inapobidi.

Njia Ya Tatu: Hawakupi mrejesho wa mambo


mabaya

Watu wengi wa karibu badala ya kukuambia


unapokosea wanakunyamazia badala yake
wanakwenda kukusema vibaya kwa wengine.
Ndugu anaweza asiridhishwe na bidhaa zako
badala ya kurudi na kukuambia ukweli ili
ujirekebishe anabaki tu kunung’unika.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 137


Mwisho wa siku unashindwa kusaidika na matokeo
yake ni wateja kuacha kabisa kununua bidhaa zako.
Kwa kufanya hivi wamechangia kuiua biashara
yako.

Njia Ya Nne: Wanakatisha tamaa kwa maneno.

Umeshakutana na mtu unamwambia bwana


nimeanzisha biashara halafu anakujibu, “kwa kweli
biashara zimeingiliwa mwaka huu, na wewe una
biashara?” wanaweza kukuambia wazi wazi au
kukusengenya pembeni.

Watu wengi waliokatishwa tamaa kwenye biashara


wamefanyiwa hivyo na watu wa karibu. Maneno ya
ndugu na marafiki yanaumiza zaidi kuliko yale ya
watu wa mbali. Kwa sababu yanaingia ndani kabisa
na yanabeba uhalisia mwingi.

Hebu tuwe wazuri katika kuwatia moyo watu wetu


wa karibu, badala ya kuumiza tugange mioyo.
Tuwainue wanapokwama kwenye biashara zao.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 138


Tuwafariji na kuwasaidia. Tuwe mstari wa mbele
kuwashauri na kuwakemea inapobidi ili tu waweze
kusimama kwenye biashara zao.

Njia Ya Tano: Wanakopa na hawalipi.

Ukienda kwenye madaftari ya madeni ya


wafanyabiashara unakuta majina ya ndugu ni mengi
sana kuliko wale wasio ndugu. Inakuwa shida
kuwadai watu wa namna hii maana wanajua sio
rahisi kuchukuliwa hatua.

Kuwa makini nao. Lakini wewe pia usimfanyie hivyo


mtu wako wa karibu anapoamua kuanzisha
biashara yake. Usiwaruhusu ndugu waue biashara
yako jikwamue kwenye makucha yao.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 139


MADHARA 6 YA KUAJIRI NDUGU KWENYE
OFISI/KAZI YAKO

Moja kati ya kitu nakutana nacho sana ni pale mtu


anaponiambia nilianzisha biashara au ofisi na
kuwaweka ndugu zangu ili tufanye kazi kwa pamoja
kusudi tujikwamue kutoka kwenye umasikini kwa
pamoja.

Lakini badala yake ndugu hao ndio wamegeuka na


kuwa ndio chanzo cha mimi kufeli. Ni kweli kwamba
ziko kampuni, taasisi au mashirika ambayo yaliajiri
ndugu na yamesimama imara kwa kufanya hivyo
lakini kwa asilimia kubwa watu wengi wameumizwa
badala ya kusaidika.

Nataka tuone madhara 6 ya kuajiri ndugu na namna


unavyoweza kufanya ili kukabiliana nayo pale
unapotaka kuchukua hatua ya kuajiri mtu yeyote
ambaye ni ndugu kwenye biashara yako.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 140


Changamoto Ya Kwanza: Kukosa Vigezo
(Discounting qualification)

Hii ni pale ambapo unakubali kuajiri mtu mwenye


sifa isiyokidhi vigezo achukue nafasi fulani kwa
sababu tu ni ndugu na unataka kumsaidia.

Hii inaathiri sana kwenye uzalishaji au utendaji kwa


sababu mtu mwenye uwezo mdogo amepewa
kufanya majukumu yanayozidi ubobezi wake.

Ili kukabiliana na hili ni sharti uwe na yafuatayo.

i. Family employment policy (Sera Ya Ajira Kwa


Wanafamilia): Andaa utaratibu maalumu uliondikwa
unaoelezea msimamo wako na vigezo ambavyo
ndugu wanapaswa kuwa navyo ili waweze kuajiliwa
kwenye biashara yako.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 141


ii. Avoid creating posts for family (Usijilazimishe
Kutengeneza Nafasi Kwa Ajili Ya Ndugu):

Epuka kutengeneza nafasi za kazi ili tu uweze


kuwaajiri ndugu zako wasio na kazi. Toa kazi pale
tu penye uhitaji.

Hatutengenezi nafasi kwa sababu kuna mtu


unataka aje kukaa, tunatengeneza nafasi kwa
sababu ina mchango kwenye uzalishaji.

iii. Universal rules of work (Sheria Sawa Za Kazi):

Usiwe na upendeleo kwa ndugu zako mkiwa kazini.


Tengeneza vigezo na sheria zinazotoa muongozo
na kumdhibiti kila mtu pasipo kujali wadhfa wake.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 142


Changamoto Ya Pili: Personal professional
conflicts (Malumbano binafsi ya kifamilia kuletwa
kazini/ofisini)

Kuna mstari mwembamba sana wa kutenganisha


mambo ya kifamilia na yale ya kiofisi. Kukiwa na
ugomvi nyumbani basi unahamia ofisini.

Mfano mtu amenidhamishwa kazini na ndugu yake


kwa kupunguzwa mshahara au kupewa barua ya
onyo halafu anaenda kushitaki kwenye vikao vya
familia. Hii inaathiri kote yaweza kuwa mahusiano
ya kifamilia au utendaji kazi ofisini.

Hii ni changamoto ambayo hupaswi kuipuuza ikiwa


utafanya maamuzi ya kuajiri ndugu mahali pako pa
kazi.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 143


Changamoto Ya Tatu: Disciplining challenge
(Changmoto ya kunidhamisha)

Kuna ugumu sana kwenye kumnidhamisha mtu


ambaye ni ndugu yako. Fikiria ndugu yako wa damu
amefanya kosa linalosababisha afukuzwe kazi au
hata afunguliwe mashitaka kabisa na wewe ndiye
unapaswa kufanya maamuzi hayo.

Inaleta ugumu sana kwenye kumchukulia hatua


ndugu yako inapotokea amefanya makosa kazini.
Kinachotokea ni watu kuanza kukuona kama una
upendeleo kwa vile usivyoweza kumuwajiisha
ndugu yako.

Changamoto Ya Nne: Unrealistic expectations


(Mataraijio yasiyo na uhalisia)

Hapa kuna pande mbili za matarajio yasiyo na


uhalisia. Ya kwanza ni pale unapoamua kumuajiri
ndugu ukiamini kabisa kwamba kwa sababu yeye
anajua hii ni biashara yetu basi atajitolea kwa uzito
zaidi ya wengine na kuwa mstari wa mbele

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 144


kuwajibika ili kuleta faida kubwa zaidi. Unatarajia
atakuwa mwaminifu na hatakuwa mzembe wala
mvivu kazini.

Upande wa ndugu yeye anakuwa na matarajio


tofauti kabisa. Utasikia anasema hii ni biashara ya
ndugu yangu bwana.

Nitaenda mda wowote ule. Anajua anaweza


akatumia rasilimali vibaya maana anajua
hutamuwajibisha. Anafuja kwa sababu tu anajua ni
vya ndugu.

Haya ni matarijio mawili yanayokinzana kabisa, na


matokeo yake ni makwaruzano na magomvi hali
inayoathiri biashara. Watu wengi wamekatishwa
sana tamaa kwa sababu ya vitu kama hivi. Pale kile
ulichotarajia kikaja kuwa ndivyo isivyo inaleta
mkanganyiko na fadhaa.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 145


Changamoto Ya Tano: Ditching formalities
(Kupuuzia utaratibu.)

Mara nyingi unapoajiri ndugu inakuwa kazi sana


kufuata utaratibu. Moja kati ya vitu vigumu sana ni
kumpitisha kwenye “interview” kama unavyofanya
kwa wengine wasio ndugu. Matokeo yake mtu
anafanya kazi hana mkataba, wala hamna mahali
popote walipoandikishana, wala hakuna
makubaliano yoyote rasmi.

Mwishowe huleta malumbano makubwa kazini. Hii


inaweza kupelekea ugomvi ambao haukuwa wa
lazima.

Changamoto Ya Sita: Challenging relationship with


other collegues. (Changamoto ya mahusiano kati
ya ndugu aliyeajiriwa na wafanyakazi wengine)

Mara nyingi watu walioajiriwa na ndugu zao huwa


wanapenda kujionyesha kama wana mamlaka
makubwa kuliko wengine wote hata kama wana
cheo kidogo.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 146


Hii inapelekea kuwa na mahusiano yasiyo rafiki kati
yake na wafanyakazi wengine. Pia inaweza
kuharibu uhusiano wako wewe na wafanyakazi
wengine.

Maana kuna vitu ndugu atavifanya na wote


wataona kwa sababu ya mamalaka uliyompa ilihali
hujampa mamlaka yoyote Zaidi ya yale anayostahili.

Lengo la kuijifunza haya ni ili ukiweza basi usifanye


maamuzi ya kuwaajili ndugu, lakini hata ukiamua
hiyo uchukue tahadhari ya namna ya kukabiliana na
hayo ili biashara yako isije ikaharibiwa kwa uwepo
wa ndugu.

Kumbuka sio kila ndugu ni mbaya lakini huna budi


kuchukua tahadhari kabla ya hatari.

Tafakari: Je, ni hatua gani ambazo unaona


unapaswa kuzichukua kwenye biashara yako
kuhusiana na kuajiri ndugu wa karibu?

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 147


Sura Ya Kumi

Aina 5 Za Rekodi Muhimu


Zitakazokusaidia Kukuza
Biashara Yako

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 148


Unapokuwa unafanya biashara kuna aina fulani za
rekodi ambazo ni muhimu kuwa nazo. Kuna msemo
unaosema mali bila daftari hutumika bila habari.

Watu wengi wanapoanza biashara wanafanya


hovyo hovyo tu bila hata kutunza kumbukumbu za
biashara zao. Matokeo yake ni kwamba wanajikuta
wamemaliza mtaji bila hata kujua pesa zilitumikaje.

Unatakiwa uwe na rekodi nzuri ili uweze kukua na


sio usubiri ukue ndipo uweke rekodi zako vizuri.
Bila kujali unafanya biashara gani rekodi zitakupa
picha nzuri ya biashara yako na zitakuonyesha
maeneo unayoweza kukua kwa haraka.

Kwenye biashara yoyote rekodi hizi tano ni muhimu


kuwa nazo.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 149


Aina Ya Kwanza Ya Rekodi: Mauzo ya kila siku
(Sales records)

Katika hili kuna vitu viwili ambavyo unaviwekea


kumbukumbu. Cha kwanza ni kumbukumbu ya
bidhaa ulizouza kwa siku. Kwa mfano utarekodi
nimeuza mashati mawili au nimeuza suruari tano.

Ni vizuri kuviainisha kwa majina yake kwa sababu


inakusaidia kupata kitu kinaitwa business trend.
Kwa sababu utakapokuwa unarekodi mauzo ya
bidhaa kwa majina yake itakufanya ujue bidhaa zipi
zinatoka kwa uharaka.

Hii itakurahisishia kujua ni vitu gani vinauzika kwa


uharaka kuliko vingine. Pia itakupa kujua mlolongo
(trend) wa utokaji wa bidhaa zako. Utakuwa unajua
ni vitu gani huwa vinauzika lini. Mfano nini kinauza
zaidi mwezi wa kwanza).

Utajua ni wakati gani au siku gani bidhaa aina


Fulani zinauzika. Au tarehe zipi katika mwezi vitu
vinatoka sana.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 150


Usipoweka rekodi ya mauzo ya kila siku itakuwa
vigumu kwako kujua haya na kujipanga ili uweze
kuwamudu wateja wako.

Cha pili ni rekodi ya kiwango cha pesa ulichoingiza


kila siku.

Mfano leo nimeuza laki moja au elfu hamsini. Hili ni


jambo muhimu sana. Huhitaji kuwa na kompyuta
kufanya hili jambo.

Unaweza kuwa tu na daftari lako dogo. Hakikisha


unafanya kitu hiki hata kama wakati mwingine
unaona ni mzigo lakini huna budi kuzingatia.

Aina Ya Pili Ya Rekodi : Matumizi ya kila siku

Ni muhimu sana kuielezea pesa yoyote inayotoka


kwenye biashara kwa kuainisha imekwenda wapi.
Usichukue tu pesa ya kwenye biashara bila kuweka
kenye rekodi ya matumizi yako.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 151


Hili ni jambo la muhimu kulifanya kwa sababu
linakujulisha gharama zako nyingi za matumizi
zinaenda wapi. Hili litakusaidia ujue unapotaka
kupunguza gharama za uendeshaji kwenye
biashara yako upunguze wapi.

Usipoandika hautajua pesa yako inakwenda wapi.


Unapaswa kujua kila senti inayoingia kwenye
biashara yako inatokea wapi. Kwenye rekodi hii pia
utajua ni matumizi gani ni ya lazima, ni yapi ni ya
kila siku, ni yapi yanaepukika, ni yapi
yanapungukika, n.k.

Aina Ya Tatu Ya Rekodi: Bidhaa zako (Stock yako).

Hapa nazungumzia bidhaa zinazobaki baada ya


mauzo ya kila siku. Jitahidi kujua mara kwa mara ni
“stock” kiasi gani imebakia kwenye biashara yako.

Usipojua stock iliyobaki ni kiasi gani unaweza tumia


pesa kwenye mambo mengine wakati kumbe kuna
bidhaa muhimu imeisha na inahitajika sana.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 152


Hii itakusaidia kuweka vipaumbele katika manunuzi
ya mzigo mpya. Hebu jiulize je, unajua ni stock kiasi
gani uliyonayo kwenye biashara yako. Ukiona
huwezi kujibu kwa wepesi ujue hauko makini
kwenye kipengele hiki.

Aina Ya Nne Ya Rekodi: Madeni.

Madeni yapo katika makundi mawili. Moja ni yale


unayodaiwa na wengine. Lazima uwe na
kumbukumbu ya madeni unayodaiwa. Yaweza
kuwa kuna bidhaa ulichukua kwa mkopo au deni
lingine lolote.

Mbili ni madeni ambayo wewe unawadai wengine.


Rekodi ya madeni ni muhimu kwa sababu inakupa
kujua afya ya biashara yako. Unapojikuta una
madeni mengi unayodaiwa kuliko mtaji wa biashara
yako tafsiri nyepesi ni kwamba biashara hiyo iko
mbioni kuanguka.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 153


Unapogundua una madeni mengi unayowadai watu
wengine maana yake ni kwamba unapaswa kubadili
mfumo wako wa ukopeshaji. Yaweza kuwa kwa
kuweka ukomo wa mtu kulipa au kwa kuweka
ukomo wa kiwango cha mtu kukopa bidhaa.

Mfano sitakopesha mtu bidhaa zinazozidi elfu kumi.


Au sitamkopesha mtu asiye na uwezo wa kulipa
ndani ya wiki mbili. Kwa hiyo usipuuze kuweka
rekodi ya madeni.

Aina Ya Tano Ya Rekodi: Orodha ya wateja


(Customer database).

Ni muhimu sana kuwa na takwimu za wateja wako.


Unapaswa kujua walinunua nini kutoka kwako. Zile
bidhaa anazonunua mteja mara kwa mara ndiyo
machaguo ya upendeleo wake (Customer
Preference).

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 154


Ukiwa na rekodi hiyo utajua namna ya kumpa
kilicho bora Zaidi ili aendelee kuwa mteja wako. Pia
ni rahisi kumkumbusha kila unapoleta mzigo mpya.

Wateja waliowahi kununua kutoka kwako ni mtaji


mkubwa sana kwako kwa sababu vitu vingi
unavyoviuza vinanunuliwa zaidi ya mara moja.

Orodha ya wateja pia inakusaidia kujua


mlolongo(trend) wao. Mfano kuna mtu ananunua
bidhaa fulani kila mwanzo wa mwezi. Ukijua trend
ya wateja wako ni silaha kubwa kwa mauzo ya
biashara yako.

Takwimu ya wateja wako inakupa kuisoma tabia


yao ya manunuzi na msukumo wao linapokuja suala
la manunuzi. Ni mfano wa vile mitandao ya simu
inapokutumia ujumbe kukujulisha kwamba kifurushi
chako kinakaribia kuisha.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 155


Lengo lao sio kukufanya ujue tu lakini ni kukufanya
ukumbuke kufanya manunuzi ya kifurushi kingine
kwa sababu wameijua tabia yako kwa kuangalia
takwimu yako.

Tafakari: Je, katika biashara yako unayoifanya


sasa, ni rekodi gani ambazo hauzifanyi vizuri na
unahitaji kuzifanyia kazi ili uweke kukuza
biashara yako.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 156


Hitimisho

Sina shaka kuwa baada ya kumaliza kusoma kitabu


hiki, umejifunza mambo mengi ambayo unaweza
kuanza kuyafanyia kazi unaposimamia na kukuza
biashara yako.

Kumbuka kuwa, siku zote kuna changamoto kubwa


unapotaka kuanza kufanya kitu kipya au
kutengeneza mfumo mpya wa biashara, hata hivyo
ni jambo linalowezekana kuzishinda changamoto
hizo zote.

Kumbuka kuwa, mabadiliko yoyote yale ambayo


utaanza kuyachukua kuhusiana na biashara yako,
yanaweza kuchukua muda kabla haujaona matokeo
ambayo unayatamani, usikate tamaa.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 157


Ukitumia mbinu fulani na isipokupa matokeo
makubwa mara ya kwanza, usikate tamaa, jaribu
kwa mara nyingine na utaona matokeo yanazidi
kuongezeka.

Usisahau kumshirikisha mtu mwingine ambaye


unaona anahitaji maarifa yaliyomo kwenye kitabu
hiki ili naye pia aweze kupata mbinu bora za
kusimamia na kukuza biashara yake.

See You At The Top

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 158


Kuhusu Mwandishi

Joel Arthur Nanauka ni mwandishi wa vitabu na


mwalimu katika maeneo ya uongozi, biashara na
kujitambua.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 159


Ni mhitimu wa masomo ya biashara na uongozi kutoka
chuo kikuu cha Dar es Salaam na Stashahada ya juu ya
Diplomasia ya Uchumi kutoka kituo cha mahusiano ya
nje (Centre For Foreign Relations).

Mwaka 2020 alitajwa katika orodha ya vijana 100


wenye ushawishi zaidi katika bara la Afrika na pia
kijana mwenye ushawishi zaidi Tanzania katika eneo la
ufundishaji watu kujitambua (Personal Development).
Pia aliwahi kutajwa kama kiongozi bora kijana wa
Dunia mwaka 2012, nchini Taiwani, China.

Amekuwa mkufunzi wa wakurugenzi wa kampuni


binafsi na mashirika ya umma kupitia taasisi ya
wakurugenzi Tanzania (IoDT) katika eneo la
kuendesha mabadiliko katika taasisi (Change
Management )

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 160


Joel ni mwalimu (Certified Trainer) katika eneo la
biashara na ujasirimali anayetambuliwa na kutumika
kufundisha mitaala ya vyuo vikuu vya Regent na
Joseph Business School vyenye makao yako makuu
nchini Marekani.

Pia amekuwa mlezi wa wajasiriamali wa Afrika kupitia


shindano maalumu la Africa Entrepreneurship Award
linalofanyika kila mwaka chini ya Benki ya BMCE
iliyoko nchini Moroco.

Joel alikuwa ni mmoja wa timu maalumu ya


wataalamu walioteuliwa na serikali chini ya Baraza la
Uwezeshaji la Taifa (NEEC) katika kuandaa muhtasari
wa mtaala maalumu wa ujasiriamali wa Taifa.

Joel Arthur Nanauka amekuwa mkufunzi wa vyombo


vya habari tangu mwaka 2018 kupitia taasisi ya
Tanzania Media Foundation (TMF) katika eneo la
biashara na uongozi.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 161


Amewahi kufanya kazi na Umoja wa Mataifa (UN)
kupitia shirika la UNESCO na baada ya hapo alianzisha
taasisi ya Africa Success Academy ambayo kwa sasa
ndiye mkurugenzi wake.

Joel amemuoa Rachel na wamebarikiwa Watoto


watatu wa kike: Joyous, Joyceline na Jonel

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 162


VITABU VINGINE VILIVYOANDIKWA
NA JOEL ARTHUR NANAUKA.

HARDCOPY (Nakala ngumu)

1. Timiza Malengo Yako (Mbinu 60 walizotumia


watu maarufu kufanikiwa)

2. Ishi Ndoto Yako (Siku 30 za kuishi maisha


unayotamani)

3. Tabia 12 Zinazoleta Mafanikio.

4. Ishinde Tabia Ya Kughairisha Mambo.

5. Ongeza Kipato Chako (Maarifa juu ya fedha,


Biashara na uwekezaji)

6. Nguvu Ya Mwanamke.

7. Mbinu Za Kufanikisha Ndoto Katikati Ya


Changamoto.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 163


8. How To Pass Your Exams With Ease.

9. Uzalendo Na Ujenzi Wa Taifa.

10. Ufanisi Kazini.

11. Boresha Mahusiano Yako.

12. Money Formula.

13. Core Genius.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 164


eBooks / SOFTCOPY (Nakala laini).

1. Money Formula (Elimu ya fedha isiyofundishwa


shuleni)

2. Hatua Sita Za Kujiajri

3. Muongozo Wa Mafanikio

4. Core Genius (Jinsi ya kugundua uwezo wako wa


kipekee)

5. Jinsi Ya Kufanikiwa Katikati Ya Nyakati Ngumu.

6. Saikolojia Ya Mteja

7. Mbinu Za Kujenga Ujasiri Na Kujiamini.

8. Surviving The Crisis.

9. Namna Ya Kuondokana Na Madeni

10. Uzalendo Na Ujenzi Wa Nchi.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 165


11. Mbinu Za Kuongeza Kipato.

12. Strategy 2021, Siri Za Kupata Matokeo


Makubwa Ndani Ya Mwaka Mmoja.

13. Nifanye Biashara Gani?

14. Marafiki.

15. Ufanisi Kazini.

16. Kiongozi Wa Tofauti.

17. Sayansi Ya Tabia.

18. Mbinu 8 Za Maandalizi Ya Kufaulu Mitihani


Kwa Kiwango Cha Juu.

19. Siri 12 Wanazotumia Wanafunzi Bora Ndani Ya


Chumba Cha Mitihani.

20. Maono.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 166


21. Mafanikio Ya Kifedha Kwa Wanandoa.

22. Kuyaishi Maono Yako.

23. Nguvu Ya Mwanamke.

24. Ishinde Tabia Ya Kughairisha Mambo.

25. Ishi Ndoto Yako.

27. Mbinu Za Kuongeza Kipato Chako.

28. Uzalendo Na Ujenzi Wa Nchi.

29. Pigania Maono Yako.

30. Vita Ya Mkombozi Wa Familia.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 167


Kozi Za Joel Nanauka, Unaweza Kuzisoma Online.

1. Mbinu Za Kuuza Zaidi.

2. Jinsi Ya Kujenga Kipato Cha Uhakika Kwa


Kujiajiri.

3. Jinsi Ya Kuondokana Na Madeni.

4. Money Formula

Kupata kozi hizi wasiliana nasi

Whatsapp: 0762 312 117

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 168


TEMBELEA MITANDAO YA KIJAMII
YA JOEL NANAUKA.

YouTube: Joel Nanauka (Utapata VIDEO nyingi za


kukufundisha mambo mbalimbali)

Instagram: JoelNanauka_ (Utapata mafunzo kila


siku yatakayokusaidia kupiga hatua katika maisha)

Facebook: Joel Nanauka (Utapata mafunzo kila


siku na pia shuhuda mbalimbali za watu
walionufaika na mafunzo)

Twitter: jnanauka.

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 169


Unaweza kupata vitabu vingine vilivyoandikwa na
JOEL NANAUKA kutoka TIMIZA MALENGO
BOOKSHOP tunapatikana Njia Panda Chuo Kikuu
Ubungo, wasiliana nasi kwa namba zifuatazo.

Instagram:

1. @TimizaMalengo_Bookshop

Simu: 0745 252 670 | 0756 094 875

2. @DivineDestiny_Bookstore tunapatikana
Bamaga.

Simu: 0762 312 171

Jinsi Ya Kusimamia Na Kukuza Biashara Yako | Joel Arthur Nanauka | 170

You might also like