Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 17

SWALA NA ADHKAR (SWALA NA DUA

Katika makala hii utajifunza baadhi ya dua za kila siku lakini pia utajifunza swala na
namna ya kuswali. Endelea kusoma kitabu hiki uapate kuijua swala, na mafunzo yake,
na zijue duamba mbalimbali ambazo inakupasa kuzijua.

1. Dhikri ya kuleta wakati wa kuamka kutoka usingizini Mtume (s.a.w) alipoamka


kutoka usingizini alikuwa akisema: Al-hamdulillahilladhy ahyaanaa ba'adamaa
amaatanaa wailayhi nnushuuru" “Sifa zote njema anastahiki Allah ambaye ametupa
uhai baada ya kutufisha na ni kwake tu ufufuo." Mtume (s.a.w) amesema: "atakaye
amka usiku kisha akasema: Laailahaillallaahu wah-dahu laa shariika lahu, lahulmulku
walahul-hamdu wahuwa a'laa kulli shay-in qadiiru, “Hapana Mola ila Allah, Mpweke
asiye na mshirika, ni wake ufalme na ni zake sifa njema, ni muweza juu ya kila kitu;
Kisha akasema "Rabbigh-fir-ly" “Ee, Mola nisamehe" Basi atasamehewa. Na kama
atasimama akaenda kutawadha kisha akaswali basi swala yake itakubaliwa."

2. Dhikri ya kuleta wakati wa kuvaa nguo Al-hamdulillaahi lladhy kasaany hadha


(thawba) warazaqaniihi min ghairi hawlin minny walaaquwwat" "Sifa zote njema ni
za Allah ambaye amenivisha nguo hii na kuniruzuku pasina uwezo wala nguvu kutoka
kwangu."

3. Dua ya Kuvua Nguo "Bismillah" "Kwa jina la Allah (nina vua)."

4. Dua ya Kuingilia Chooni Muislamu akiingia chooni atangulize mguu wa kushoto


na kusema: (Bismillah) “Allahumma inni a'uudhubika minal-khubuth wal-khabaaithi"
(Kwa jina na Allah). Ee, Allah najikinga kwako na maovu yote na wafanya maovu"

5. Dua ya Kutoka Chooni Muislamu akitoka chooni hutanguliza mguu wa kulia na


kusema: “Ghuf-raanaka" “Nakuomba msamaha (Ee Allah)

6. Dhikri wakati wa kutoka Nyumbani Bismillahi tawakkal-tu 'alallaahi walaahawla


walaaquwwata illaabillaahi Kwa jina la Allah, ninajitegemeza kwa Allah, na hapana
uwezo wala nguvu ila vyote vinatokana na Allah"

7. Dhikri wakati wa kurejea nyumbani Bismillahi walaj-naa, wabismillaah kharaj-naa


wa'alaa Rabanaa tawakkal-naa. “Kwa jina la Allah tunaingia na kwa jina la Allah
tunatoka, na kwa Mola wetu tunategemea."

8.Dua ya Kuingia Msikitini Tukiingia msikitini tunatanguliza mguu wa kulia na


kusema: “A'udhubillaahil-'adhiim wabiwajhi-hil-kariim. 'Wasul-Twaanihil-qadiimi
minash-shaytwaanir rajiim Bismillaah wasw-swallatu wassalaam a’laa rasuulillah ,
Allaahummaf-tahaly ab-waaba rah-matika". “Najikinga kwa Allah aliye mtukufu, na
kwa uso wake mtukufu, na kwa utawala wake wa kale, kutokana na sheitwani
aliyeepushwa na rehema za Allah,Kwa jina la Allah na Rehma na Amani ziwafikie
Mtume wa Allah Ee! Allah nifungulie milango ya rehema zako."

9.Dua ya kutoka Msikitini Tukitoka msikitini tunatanguliza mguu wa kushoto na


kusema: “Bismillahir wasw-swalaatu was-salaamu 'alaa rasuulillaahi, Allaahumma
inny as-aluka min fadh-lika, Allaahumma A'iswimniy, minash-shaytwaanir-rajiimi."
“Kwa jina la Allah na rehema na amani zimfikie Mtume wa Allah; Ee!
Allah,nakuomba katika fadhila zako, Ee! Allah nilinde kutokana na shetani
aliyeepushwa na rehema zako (aliye laaniwa)."

10. Dhikri za Kuleta Asubuhi na Jioni “Allahumma 'aafiniy fiy badaniy,Allahumma


'aafiniy fiy sam-'iy. Allahumma 'aafiniy fiy baswariy,Laailaha illaa anta. (Mara tatu)
Ee! Allah nipe afya ya mwili wangu,Ee! Allah nipe afya ya usikivu wangu (masikio
yangu),Ee! Allah nipe afya ya uoni wangu (macho yangu). Hapana Mola ila wewe
(mara tatu).

Allahumma inniy a'uudhubika minal-kufri, walfaq-ri, waa'uudhubika


min'adhaabil-qabri, Laailaha illa anta. (mara tatu) Ee! Allah hakika mimi najilinda
kwako kutokana na ukafiri; na ufakiri; na najilinda kwako kutokana na adhabu ya
kabri; Hapana Mola ila wewe." (Mara 3)

“Has-biyallahu laailaha illaahuwa 'alayhi tawakkal-tu wahuwa rabbul-'arshil-adhiimi.


(Mara saba asubuhi na jioni). Allah ananitosha, hapana Mola ila yeye. Kwake yeye
ninategemea, na yeye ni Mola wa arshi tukufu (mara saba asubuhi na jioni).

“A'uudhubikalimaatillaahi ttaammaati min-sharri maa khalaqa." (mara tatu jioni)


“Najikinga kwa maneno timilifu ya Allah kutokana na shari ya alivyoviumba" (mara
tatu jioni).

“Bismillahi lladhii laayadhurru ma'asmihi shay-un fiyl-ardhi walaa fissamaai


wahuwas-samii'ul-'aliimu. (mara tatu). “Kwa jina la Allah ambaye hakidhuru kwa jina
lake kitu chochote kile kilichoko ardhini wala mbinguni, naye ni Msikivu Mjuzi.

"Sub-haanallahi wabihamdihi, 'adadakhalqihi, waridhwaa nafsihi wazinata ‘arshihi


wamidaada kalimatihi, (Mara tatu) “metakasika Allah na sifa zote njema ni zake kwa
hisabu ya viumbe vyake, na radhi yake (mara tatu kila asubuhi)

“Allahumma inny as-aluka 'il-man-naafiaa, wariz-qan twayyiba, wa-'amalan


mutaqabbala". “Ee! Allah nakuomba unipe elimu yenye manufaa, na riziki iliyo nzuri
na amali (ibada) yenye kukubaliwa.

" Sub-hanallahi wabihamdihi." (mara mia) Ametakasika Allah na sifa zote njema ni
zake.
“Laailaha illallahu, wah-dahu laa sharikalahu, lahul-mul-ku walahul-hamdu wahuwa
'alaa kulli shay-in qadiiru" (mara mia) “Hapana Mola ila Allah, mpweke, asiye na
mshirika, ni wake ufalme na ni zake sifa njema zote, na yeye yuko juu ya kila kitu.

Mwenye kusoma Ayatul-Kurisiyy (2:255) pindi anapoamka atalindwa kutokana na


mashetani (majini) mpaka jioni, na atakayesoma jioni atalindwa nayo mpaka asubuhi.
Mwenyezi Mungu hakuna Mola ila Yeye, (na) ndiye Mwenye uhai wa maisha,
Msimamia kila jambo. Kusinzia hakumshiki wala kulala. Ni Vyake (peke yake vyote)
vilivyomo mbinguni na vilivyomo katika ardhi. Na nani huyo awezaye kuombea
mbele Yake (Allah) bila ya idhini yake? Anayajua yaliyo mbele yao (viumbe) na
(yajayo) nyuma yao; wala (hao viumbe) hawalijui lo lote katika yaliyo katika ilimu
Yake (Mwenyezi Mungu) ila kwa alipendalo (Mwenyewe). Enzi yake imeenea
mbingu; na ardhi; wala kuvilinda hivyo hakumshindi; na Yeye (peke yake) ndiye
aliye juu na ndiye aliye Mkuu. (2:255)
Mwenye kuzisoma mara tatu asubuhi na jioni sura zifuatazo zinamtosheleza na kila
kitu:
Suratul-Ikhlas (112:1-4) Sema, Yeye ni Allah aliye mmoja tu Allah ndiye
anayestahiki 475 kukusudiwa (na viumbe vyote). Hakuzaa wala hakuzaliwa. Hakuna
hata mmoja anayefanana naye." (112:1-4)
Suratul-Falaq (113:1-5) Sema: Ninajikinga kwa Mola wa ulimwengu wote.Na shari
ya Alivyoviumba. Na shari ya giza la usiku liingiapo.Na shari ya wale wanaopulizia
mafundoni.Na shari ya hasidi anapohusudu. (113:1-5) Suratun-Naas (114:1-6) Sema:
Ninajikinga kwa Bwana Mwenye kuwalea watu. Mfalme wa watu. Muabudiwa wa
watu. Na shari ya mwenye kutia wasiwasi mwenye kurejea nyuma. Atiaye wasi wasi
nyoyoni mwa watu. (Ambaye ni) katika majini na watu." (114:1-6)

Kumswalia Mtume Asubuhi na Jioni Mtume (s.a.w) amesema:Mwenye kuniombea


rehema asubuhi mara kumi na jioni mara kumi, nitamuombea shufaa (masamaha) siku
ya kiyama.
“Allahumma swali'alaa Muhammad wa'alaa aali Muhammad, kamaa swallayta 'alaa
Ibraahiima wa'alaa aali Ibraahiim, Innaka hamidun majiidu, allahumma baarik-'alaa
Muhammad wa-'alaa aali Muhammad, kamaa barak-ta 'alaa Ibraahiima wa-'alaa aalii
Ibraahiima, Innaka hamidunmajiidu." Ee Allah! Mrehemu Muhammad na jamaa zake
(wafuasi wake) Muhammad kama ulivyo mrehemu Ibrahiim na jamaa zake (wafuasi
wake) Ibrahiim, hakika wewe ni mwenye kusifika mtukufu. Ee Allah! Mbariki
Muhammad na jamaa zake Muhammad kama ulivyombariki Ibrahim na jamaa zake
Ibrahiim, Hakika wewe ni Mwenye kusifika Mtukufu. Mtume (s.a.w) amesema:
"Anayeniswalia mara moja, Allah (s.w) humswalia mara kumi." (Muslimu)
Pia Mtume (s.a.w) amesema: “Bahili ni yule ninapotajwa, haniswalii (haniombei
rehema na amani kwa Allah)." (Tirmidh) Kumswalia Mtume (s.a.w) kumeamrishwa
kwa waumini kama tunavyojifunza katika aya ifuatayo: “Hakika Mwenyezi Mungu na
Malaika wake wanamswalia Mtume (wanamtakia rehema na amani). Basi, enyi
mlioamini mswalieni (muombeeni Mtume) rehema na amani." (33:56)

11. Kuomba Msamaha na Kutubia Amesema Mtume (s.a.w): “Naapa kwa Mwenyezi
Mungu hakika mimi ninamtaka msamaha Mwenyezi Mungu na ninatubia kwake
katika kila siku zaidi ya mara sabini." (Al-Bukhari).
“Astagh-firu llaha waatuubu ilahi." (mara mia) “Namuomba msamaha Allah na
ninatubia kwake."

Pia Mtume (s.a.w) amesema: "Yeyote anayesoma maneno yafuatayo, Mwenyezi


Mungu atamsamehe hatakama anamakosa ya kukimbia vitani:
“Astagh-firu llaahal-'adhiimal-ladhii laaillaha illahuwalhayyul qayyuumu wa-atuubu
ilayhi." “Namuomba msamaha Allah, Mtukufu ambaye hapana Mola ila yeye, aliye
Hai, aliyesimama kwa dhati yake na ninatubia kwake."

Amesema Mtume (s.a.w): "Hakuna mja yeyote yule anayefanya dhambi kisha
akatawadha vizuri na akaswali rakaa mbili, kisha akamtaka Mwenyezi Mungu
msamaha ila atasamehewa". (Abu Daud na Tirmidh) 12. Dhikri ya kuleta baada ya
kupatwa na janga au balaa “Laailaha illa llahul-'adhwiimul-haliimu, laa ilaha illa llahu
r a b b u l - ' a r - s h i l ' a d hwi imi , L a a i l a h a i l l a l l a h u rabbussamaawaat
warabbul-ardhwi,warabbul-'ar-shilkariimi. “Hapana Mola ila Allah, aliye mtukufu
mpole, Hapana Mola ila Allah, Mola wa arshi tukufu, Hapana Mola ila Allah, Mola
wa mbingu na ardhi na Mola wa arshi tukufu. “Laailaha illaa-anta Sub-hanaanaka
inny kuntuminal Dhw- Dhwaalimiina." Hapana Mola ila Wewe, Utukufu ni wako,
hakika mimi ni miongoni mwa waliodhulumu nafsi zao. 13.Unapokutana na adui au
mtawala dhalimu “Hasbunallahu wani'imal-wakiilu" “Allah anatutosheleza Naye ni
mbora wa kutegemewa.

14.Dua ya Kulipa Deni "Allahummak-finiy bihalaalika'an haraamika wa-agh-niy


bifadhw-lika 'amman siwaaka." Ee Allah! Nitosheleze na halali yako na Uniepushe na
haramu yako, na Unitosheleze kwa fadhila zako nisiwahitaji wengine asiye wewe.

15.Dua anayoleta yule aliyefikwa na jambo gumu “Allahumma laasah-la illaa


maaja-'al-tahu sah-laa, wa anta taj-'alul-haz-na idhaashi-ita sah-laa. Ee Allah hakuna
jepesi ila ulilolifanya jepesi, nawe unalifanya gumu kuwa jepesi ukitaka.
16.Dua ya kuomba unapotokewa na jambo usiloliridhia au unaposhindwa kufanya
jambo Amesema Mtume (s.a.w) (katika Sahihi Bukhari): "Muumini mwenye nguvu
(qawiyyu) ni bora na anapendeza zaidi kwa Allah (s.w) kuliko muumini dhaifu, na
wote wanakheri. Fanya pupa kwa kile kitakacho kunufaisha na taka msaada wa Allah
wala usichoke, na kikikupata kitu chochote kibaya basi usiseme lau kama
ningelifanya kadha na kadhaa yasingenitokea haya, lakini sema: "Qaddarallahu
wamaa shaa-af-a'la. “Amepanga Allah na analolitaka anafanya." Hakika Allah
analaumu mwenye kukata tamaa, lakini usivunjike moyo, na ukishindwa na jambo
kabisa sema: "Has-biya llahu wani-i'mal-wakiilu" "Allah ananitosheleza, Naye ni
mbora wa kutegemewa."

17.Dua ya Kumuombea mgonjwa wakati wa kumtembelea “Laa ba-asa twahuurun


in-shaa-allahu." “Hakuna neno, (ugonjwa) ni kusafishwa na dhambi anapopenda
Allah." (Al-Bukhari) Anasema Mtume wa Allah: "Hapana yeyote Muislamu
anayemtembelea mgonjwa ambaye wakati wake wa kufa bado haujafika na
anamuombea mara saba. “As-alullaah l-a'dhiima rabal-a'r-shi l-a'dhiimi
an-yash-fiyaka. “Namuomba Allah Mtukufu, Mola wa arshi tukufu akuponyeshe."
Isipokuwa Allah humponyesha mgonjwa huyo." (At-Tirmidh na Abu Daud)

18.Dua anayoomba mgonjwa aliyekata tamaa na kupona “Allahumma gh-fir-liy


war-hamniy wa-alhiq-niy birrafiiq il-a-a'laa" 481 Ee! Allah, nisamehe na unirehemu
na unikutanishe na waja walio katika daraja za juu".

19.Dua ya kuomba mvua “Allahumma asqinaa ghaythan mughiithan mariian mariia'a,


naafia'an ghayradhwaarrin, a'ajilanghayra aajilin. Ee! Allah tunyesheleze mvua yenye
kuokoa, nyingi, yenye kustawisha, yenye manufaa isiyodhuru.

20.Dua ya kuleta wakati unapovuma upepo Allahumma inniy as-aluka khayrahaa


wa-au'udhubika minsharrihaa. Ee, Allah! Ninakuomba unipe kheri ya upepo huu na
uniepushe na shari yake.

21.Dua ya kuleta wakati mvua inanyesha “Allahumma Swayyiban naafia'n “Ee Allah
ijaalie iwe mvua yenye manufaa."

22.Dua ya kuleta baada ya mvua kunyesha Mutwir-haa bifadh-lillahi warah-matihi.


Tumepata mvua kwa msaada na rehema ya Allah."
23.Dua ya kusema unapoanza kula Unapoanza kula hunabudi kusema: “Bismillaahi"
“Kwa jina la Allah" Na ukisahau kusema hivyo wakati wa kuanza, ukikumbuka
wakati unaendelea kula sema: “Bismillahi fiy awwalihi wa-aakhirihi" “Kwa jina la
Allah katika mwanzo wake na mwisho wake" 24.Dua ya kushukuru baada ya kula
“Al-hamdulillahilladhii atw-a'maniy hadhaa warazaqaniyhi min ghayri hawlin minniy
walaa quwwatin" “Shukurani zote anastahiki Allah ambaye amenilisha chakula hiki
bila ya uwezo wala nguvu yoyote kutoka kwangu."

25. Dua ya mgeni kumuombea mwenyeji aliye mlisha chakula “Allahumma


baarik-lahum fiymaa razaq-tahum, wagh-fir lahum war-hamhum." 483 Ee Allah,
wape baraka kwa hicho ulicho wapa,wasamehe na warehemu."

26. Dua ya kuleta baada ya kupiga chafya Unapopiga chafya hunabudi kusema:
“Al-hamdulillaahi" “Sifa zote anastahiki Allah." Kisha ndugu zako Waislamu
watasema: “Yar-hamuka llahu." “Allah akurehemu." Kisha utajibu kwa kusema:
"Yah-diykumullahu wayusw-lihi baalakum." "Allah akuongozeni na kuwasahilishia
mambo yenu." Kama anaeambiwa ni mwanamke
“Utasema yar-hamuki llahu”

27. Dua ya kuwaombea maharusi (waliooana) “Baarakallahulaka,wabaaraka


a'layka,wajamaa'baynakumaa fiy khayrin" “Allah akubariki wewe na yeye
(mkeo/mumeo) na awaunganishe katika kheri."

28. Dua ya kuleta unapoanza kufanya tendo la ndoa “Bi smi l lahi A l lahumma
jannib-nashshay - twaana wajannibish-shytwaana maarazaq-tanaa". “Kwa jina la
Allah, Ee Allah muweke shetani mbali nasi na muweke shetani mbali na hicho
ulichoturuzuku."

29. Dua ya kuleta unapopandwa na hasira “Au'udhubillaahi minash-shaytwaani


rrajiimi" “Najikinga kwa Allah na shetani aliyelaaniwa."

30. Dua ya kuleta mwisho wa kikao (mkutano) "Sub-haanaka llahumma


wabihamdika, ash-hadu an-laa ilaha illa anta as-taghfiruka wa-atuubu ilayka."
"Utukufu ni wako, Ee Allah, nakutukuza. Ninashuhudia kuwa hapana Mola ila wewe.
Nakuomba msamaha na ninatubia kwako."

31. Dua unayomuombea yule aliyekufanyia jambo zuri “Jazaka llahu khayran"
“Allah akulipe kheri."

32. Dua ya kuomba kuepushwa na shirk “Allahumma inniy au'udhubika an-ush-rika


bika waanaaaa'lamu, wa-astagh-firuka limaa laa-aa'lamu." "Ewe Allah, najikinga
kwako nisikushirikishe huku nikijua na naomba unisamehe kwa lile (baya)
nitakalolifanya bila kujua."

33.Dua ya kupokelea sadaqa au zawadi "Baarakallahu fiykum." “Baraka za Allah


ziwe juu yenu." Na aliyetoa zawadi/swadaqa na akaombewa hivi atajibu "Wafiyhim
baarakallahu." "Pia Allah awabariki."

34.Dua ya kupanda mnyama/chombo cha usafiri “Bismillah wal-hamdulillahi,


sub-haanalladhiy sakhkharalanaa haadhaa wamaa kunnaalahu muq-riniyna wainna
ilaa rabbinaa la mun-qalibuuna.“Kwa jina la Allah na sifa zote ni za Allah. Utukufu ni
wa yule aliyetutiishia kipando hiki, tusingeweza kukitumia kwa uwezo wetu wenyewe,
na kwa Mola wetu ndio marejeo.

35.Dua ya Safari “Allahu akbaru, Allah akbaru, Allahu akbaru, sub-haana lladhiy
sakh-kharalanaa hadhaa wamakunnaa lahu muqriniyna, wainnaailaa rabbinna
lamunqalibuuna. Allahumma innaa nas-aluka fiy safarinaa hadhal-birri wa-ttaqwa,
waminal-a'mali maatar-dhwaa, Allahumma hawwin a'laynaa safaranaa hadha wat-wi
a'nnaa budahu, Allahuumma antasw-swaahibu fiy ssafari, wal-khaliyfatu fiyl-ahli.
“Allah ni mkubwa, Allah ni mkubwa, Allah ni mkubwa, ametakasika ambaye
ametudhalilishia sisi hiki (chombo au mnyama), na hatukuwa sisi kwako ni wenye
uwezo, na sisi kwa Mola wetu tutarejeshwa. Ee Allah, hakika sisi tunakuomba katika
safari yetu hii wema na ucha Mungu, na katika matendo unayoridhia, Ee, Allah ifanye
nyepesi safari yetu hii na ufupishe umbali wake. Ee Allah, wewe ndie mwenzangu
katika safari na mchungaji wa familia yangu.

36.Dua ya kupokea habari ya kufurahisha “Al-hamdulillahilladhiy bina-a'matihi


tatimmu sw-swaalihaatu." “Shukurani zote anastahiki Allah ambaye kwa neema yake
hizi nzuri imekamilika."

37.Dua ya kupokea habari za kuhuzunisha “Al-hamdulillahi a'laa kulli haali"


“Shukurani zote anastahiki Allah kwa hali zote."

38.Dua ya kuingia sokoni “Laa illaaha illa llaahu wah-dahu laashariikalahu,


lahul-mulku walahul-hamdu, yuh-yi' wayumiitu wahuwa hayyun laa yamuutu
wahuwa a'laa kullishay-in qadiiru." “Hakuna Mola ila Allah aliye mpweke, hana
mshirika, ni wake ufalme,na ni zake sifa njema, anahuisha na anafisha, naye ni hai
asiyekufa, kheri iko mikononi mwake, na yeye juu ya kila kitu ni muweza."

39.Ubora wa kusalimiana Mtume (s.a.w) amesema “Hamtoingia peponi mpaka


muamini na hamtaweza kuamini mpaka mpendane. Je, nikufahamisheni jambo
ambalo mkilifanya mtapendana? Jambo hili ni kutoleana salaamu." (Muslim)
Ukamilifu wa salaamu ya Kiislamu ni “Assalaamu a'laykumu Warahmatullahi
wabarakaatuhu." “Amani ya Allah, Rehema zake na Baraka zake ziwe juu yenu."
Anayesalimiwa analazimika kujibu kwa kusema: “Waa'laykumu ssalaamu
warahmatullahi wabarakaatuhu." “Nanyi pia amani ya Allah, Rehema zake na Baraka
zake ziwe juu yenu."

40.Ubora wa kumkumbuka na Kumtukuza Allah wakati wa mapumziko A'bdullaah


Ibn Qays (r.a) ameeleza kuwa Mtume (s.a.w) alimuuliza: "Ee 'Abdullah Ibn Qays, ni
kufahamishe hazina miongoni mwa hazina za Peponi? Kisha Mtume (s.a.w)
akamwambia sema: “Laa haula walaaquwwata illaabillahi." "Hapana uwezo wala
nguvu ila kutoka kwa Allah." (Bukhari na Muslimu)

Mtume (s.a.w) amesema, maneno anayopenda Allah kuliko yote ni manne


“Sub-hanallahi, Wal-hamdulillahi, Walaa ilaaha illallaahu, Wallaahu Akbaru."
“Utukufu ni wa Allah, shukurani zote anastahiki Allah, Hapana Mola ila yeye, Allah
ni Mkubwa." (Muslimu)
Abu Hurayrah (r.a) ameeleza kuwa: Mtume (s.a.w) amesema, "Kuna maneno mawili
(2) ambayo ni mepesi katika ulimi na mazito katika mizani na anayopenda Allah,
nayo ni: “Sub-haanallahi wabihamdihi, wasubuhaana llaahila'dhiim." “Utukufu ni wa
Allah na shukrani zote anastahiki yeye. Utukufu ni wa Allah aliye mkuu." (Bukhari na
Muslimu)

Jabir Ibn Abdullah (r.a) amesimulia kuwa Mtume (s.a.w) amesema: Hakika dua
kubwa ni kusema: “Al-hamdulillaahi" “Shukurani zote anastahiki Allah." Na hakika
namna bora ya kumkumbuka Allah (dhikri) ni kusema: “Laailahailla llaaha." “Hapana
Mola ila Allah." (Ahmad)

Mtume (s.a.w) amesema, amali njema ya kudumu ni kusema: “Sub-haanallahi,


wal-hamdulillaahi, walaailaha illallaahu walaahu akbaru walaahawla walaaquwwata
illaabillaahi." Utukufu ni wa Allah na shukurani zote anastahiki Allah, na Hapana
Mola ila Allah na Allah ni mkubwa. Hapana uwezo wala nguvu ila kutoka kwa
Allah."

41.Dhikri ya kuleta wakati wa kulala Alikuwa Mtume (s.a.w) akienda kulala usiku,
akiweka pamoja viganja vyake kisha akivipulizia na akivisomea suratul-Ikhlas,
suratul Falaq na Suratun-Naas, kisha akipangusa kwa hivyo viganja vyake kiasi
anachoweza katika mwili wake, akianza kichwani, usoni na mbele (akifanya hivyo
mara tatu.) (Bukhari na Muslimu)

Mtume (s.a.w) amesema: "Ukienda kulala soma Ayatulkursiyyu kwani Allah


ataendelea kukuhifadhi, wala hakukaribii shetani mpaka asubuhi." (Al-Bukhari)

Mwenyezi Mungu, hakuna Mola ila yeye, ndiye mwenye uhai wa milele, msimamia
kila jambo. Kusinzia hakumshiki wala kulala. Ni vyake (peke yake vyote)
vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini. Na nani huyo awezaye kuombea mbele
yake bila ya idhini yake? Anayajua yaliyo mbele yao (viumbe) na (yaliyo) nyuma yao;
wala (hao viumbe) hawalijui lolote katika ilimu yake ila kwa alipendalo. Enzi yake
imeenea mbinguni na ardhini, wala kuvilinda hivyo hakumshindi; Na yeye (pekee)
ndiye aliye juu na ndiye aliye mkuu." (2:255)

Alikuwa Mtume (s.a.w) akitaka kulala, anaweka mkono wake wa kulia chini ya shavu
lake, kisha anasema: "Allahumma qiniy a'dhaabaka yaumatab-a'thu i'baadaka." "Ee!
Allah nikinge mimi kwa adhabu yako siku utakapowafufua waja wako."

Pia Mtume (s.a.w) wakati wa kulala alikuwa akisema: “Allahumma Bismika amuutu
wa-ahyaa. “Kwa jina lako, Ee Allah ninakufa na nina kuwa hai." uzi na ndiye
Mwenye hikima (2:32)

DUA ZA SWALA

SWALA
Umuhimu wa Kusimamisha
Swala Kwa mujibu wa Hadith ya Ibn Umar (r.a) tuliyoirejea mwanzoni, kusimamisha
swala ni nguzo ya pili ya nguzo za Uislamu. Katika kuonyesha umuhimu wa
kusimamisha nguzo hii Mtume (s.a.w) amesema:  Swala ndio nguzo kubwa ya Dini
(Uislamu) mwenye kusimamisha swala amesimamisha dini (Uislamu) na mwenye
kuiacha swala amevunja Dini . (Uislamu)

Katika Hadithi nyingine, amesimulia Jabir (r.a) kuwa Mtume wa Allah amesema:
 Tofauti yetu sisi (Waislamu) na ukafiri ni kuacha swala h. (Muslim) Pia Mtume
(s.a.w) amesema:  Tofauti iliyopo kati yetu (Waislamu) na wengine (wasiokuwa
Waislamu) ni swala (Ahmad, Abu Daud, An-Nasai, Tirmidh) Kutokana na hadithi
hizi, tunajifunza kuwa mtu ambaye hasimamishi swala, hatakama anajiita Muislamu
si Muislamu bali ni kafiri kama makafiri wengine. Anakuwa kafiri kwa sababu
amekanusha amri ya Allah iliyowazi kama inavyobainika katika aya zifuatazo:
 Waambie waja wangu walioamini, wasimamishe swala. (14:31)  Basi simamisheni
swala, kwa hakika swala kwa waumini ni faradhi iliyowekewa nyakati makhsusi. h
(4:103)  Na waamrishe watu wako kuswali (kusimamisha swala) na uendelee
mwenyewe kwa hayo... h (20:132).

Tukumbuke kuwa hawi Muumini yule anayekuwa na hiari katika kutekeleza amri ya
Allah na Mtume wake kama tunavyokumbushwa katika aya ifuatayo:  Haiwi kwa
mwanamume aliyeamini wala kwa mwanamke aliyeamini, Mwenyezi Mungu na
Mtume wake wanapokata shauri, wawe na hiari katika shauri lao. Na mwenye
kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hakika amepotea upotofu ulio wazi h.
(33:36)

Lengo la Kusimamisha Swala


Bila shaka swala imepewa umuhimu mkubwa kiasi cha kufanywa nguzo kubwa ya
Uislamu kutokana na lengo lake. Lengo la swala limebainishwa katika Qur-an kama
ifuatavyo  ”Soma uliyoletewa wahyi katika kitabu (Qur-an) na usimamishe swala.
Bila shaka swala (ikiswaliwa vilivyo) humzuilia (mwenye kuswali na) mambo
machafu na maovu, na kwa yakini kumbuko la Mwenyezi Mungu (lililomo ndani ya
swala ni jambo) kubwa kabisa (la kumzuilia mtu na mabaya). Na Mwenyezi Mungu
anayajua mnayoyatenda.” (29:45).

Kutokana na aya hii tunajifunza kuwa lengo la kusimamisha swala ni kumtakasa mja
na mambo machafu na maovu. Kwa maana nyingine, tunajifunza kuwa swala
ikisimamishwa vilivyo, humfanya msimamishaji awe mtu mwema mwenye
kutakasika na mambo machafu na maovu na mwenye kuendea kila kipengele chake
cha maisha kwa kumtii Allah (s.w).

Labda tujiulize swali:  Ni nguvu gani au ni msukumo gani uliomo katika swala
unaomfanya mwenye kuswali atakasike na maovu na awe na tabia njema anayoridhia
Allah (s.w) Linaloleta mabadiliko haya makubwa katika tabia na utendaji wa
Muumini, ni lile kumbuko la Allah (s.w) lililomo ndani ya swala. Kwa hiyo lengo hili
la swala litapatikana tu pale mwenye kuswali atakapokuwa na mazingatio na
kumkumbuka Allah (s.w) katika kila hatua ya swala.

Maana ya Swala
Maana ya Swala
(a) Kilugha Katika lugha ya Kiarabu neno  Swalaat lina maana ya  ombi au  dua.
Katika Qur-an tunaamrishwa kumswalia Mtume, yaani kumuombea dua Mtume
(s.a.w) katika aya ifuatayo:  Hakika Mwenyezi Mungu na Malaika wake
wanamswalia Mtume (wanamtakia Rehema). Basi, enyi mlioamini mswalieni
(muombeeni au mtakieni Mtume) Rehema na muombeeni amani (33:56)

Vile vile katika Hadith, Mtume (s.a.w) anatuambia:  Yule atakayealikwa kwenye
karamu ya harusi aitikie wito huo, kama hataweza kuitika amswalie (amuombee dua)
aliyemkaribisha. (Muslimu).

(b) Kisheria Katika sheria ya Kiislamu,  swalaa ni maombi maalumu kwa Allah (s.w)
yanayofanywa kwa kufuata utaratibu maalumu uliowekwa na Allah (s.w) na
kufundishwa kwa matendo na Mtume wake. Katika maombi haya maalumu mwili
mzima huhusika katika maombi haya kwa kusimama, kurukuu, kuitidali, kusujudu,
kukaa na kuzingatia yale yote anayosema katika kuleta maombi haya.

Kusimamisha Swala.
Maana ya Kusimamisha Swala Kusimamisha swala ni tofauti na kuswali. Kuswali ni
kufanya vitendo vya swala kama vile kusimama, kurukuu, kuitidali, kusujudu, n.k.
Kusimamisha swala ni kuitekeleza swala kwa kuchunga na kutekeleza kwa ukamilifu
yafuatayo:

(i) Sharti zote za swala.


(ii) Nguzo zote za swala.
(iii) Kuwa na khushui (unyenyekevu) wakati wote wa kutekeleza sharti na nguzo za
swala.

Mtu akiswali bila ya kuzingatia na kutekeleza kwa ukamilifu mambo haya matatu,
ataonekana kuwa kaswali, lakini atakuwa hajasimamisha swala na atastahiki
kuadhibiwa vikali na Mola wake kama tunavyojifunza katika aya ifuatayo:  Basi
adhabu kali itawathibitikia wanaoswali, ambao wanapuuza swala zao (kwa
kutozisimamisha), ambao hufanya ria (107:4-6).

Kupuuza swala ni pamoja na kutotekeleza ipasavyo sharti za swala, nguzo za swala,


na kutokuwa na unyenyekevu wakati wa kutekeleza sharti na nguzo za swala. Hivyo,
swala inayokubalika mbele ya Allah (s.w) ni ile iliyosimamishwa kama
tunavyojifunza katika aya zifuatazo:  Hakika wamefuzu waumini ambao katika
swala zao ni wanyenyekevu . (23:1-2)  Na ambao swala zao wanazihifadhi . (23:9)
Kuhifadhi swala ni kutekeleza kwa ukamilifu sharti na nguzo zote za swala.

Sharti za Swala
Sharti za Swala Sharti za swala ni yale mambo ya lazima anayotakiwa Muislamu
ayachunge na kuyatekeleza kabla hajaanza kuswali. Mambo haya ni:
1. Twahara.
2. Sitara.
3. Kuchunga wakati.
4. Kuelekea Qibla.

Zifuatazo ni nguzo za Swala:


1. Nia - dhamira moyoni.
2. Takbira ya kuhirimia (au Takbira ya kufungulia Swala).
3. Kusoma suratul-Fatiha.
4. Kurukuu.
5. Kujituliza katika rukuu.
6. Kuitidali (kusimama kutoka katika rukuu).
7. Kujituliza katika itidali.
8. Kusujudu.
9. Kujituliza katika sijda.
10. Kukaa kati ya sijda mbili.
11. Kujituliza katika kikao cha kati ya sijda mbili.
12. Kusujudu mara ya pili.
13. Kujituliza katika sijda ya pili.
14. Kukaa Tahiyyatu.
15. Kusoma Tahiyyatu.
16. Kumswalia na kumtakia rehema Mtume (s.a.w) na Waislamu.
17. Kutoa Salaam.
18. Kuswali kwa kufuata utaratibu huu (1 - 17).

Nguzo hizi za swala tunaweza kuzigawanya kwenye makundi manne:


(a) Nia.
(b) Nguzo za matamshi (visomo)
(c) Nguzo za vitendo.
(d) Kufuata utaratibu. Katika nguzo 18,

nguzo za matamshi ni hizi tano zifuatazo:


(i) Takbira ya kuhirimia swala.
(ii) Kusoma suratul-Fatiha (Al-hamdu).
(iii) Kusoma Tahiyyatu.
(iv) Kumswalia Mtume.
(v) Kutoa Salaam.
Nguzo zote zilizobakia, ukiacha nia na kufuata utaratibu ni nguzo za vitendo.

Sunnah za Swala
Sunnah za Swala Vipengele vya sunnah katika swala ni vile ambavyo mwenye
kuswali akivitenda husaidia sana kukuza daraja ya swala yake na kuipa nguvu na
msukumo mkubwa wa kuiwezesha kufikia lengo lililokusudiwa kwa urahisi zaidi.

Ama mwenye kuswali akiacha kipengele chochote katika vipengele vya sunnah,
swala yake itakamilika iwapo atatekeleza vipengele vyote vya nguzo. Katika Hadith
tumeona kuwa Mtume (s.a.w) katika swala yake pana vipengele vya ziada ya nguzo
kama ifuatavyo:
1. Kuinua viganja vya mikono mkabala na mabega, usawa wa vigingi vya masikio
wakati wa kuhirimia swala, kwenda kwenye rukuu, baada ya rukuu na baada ya
kutoka kwenye Tahiyyatu ya kwanza.
2. Kusoma dua baada ya takbira ya kuhirimia.
3. Kuanza na a fudhubillaah (kumlaani Shetani) kabla ya kuanza kusoma
suratul-Fatiha.
4. Kuitikia  Aamin hbaada ya kumaliza Suratul Fatiha.
5. Kusoma aya za Qur-an baada ya Suratul-Fatiha katika rakaa mbili za mwanzo. 6.
Kuleta Tasbih, Tahmid na dua katika rukuu, itidali na sijda.
7. Kutoa takbira katika kubadilisha kitendo kimoja kuendea kingine isipokuwa tu
kutoka kwenye rukuu kwenda kwenye itidali ndipo tunaposema:  Sami fAllahu
liman hamidah - Rabbanaa lakal-hamdu .
8. Kukaa na kusoma Tahiyyatu kila baada ya rakaa mbili, kwa swala zenye rakaa
zaidi ya mbili.
9. Kusoma dua baada ya kumswalia Mtume na kabla ya kutoa Salaam.

Namna ya kuswali kama alivyoswali Mtume


(s.a.w)
Mtume (s.a.w) ametuagiza katika Hadith maarufu kuwa tuswali kama alivyokuwa
akiswali. Hivyo katika sehemu hii tutajitahidi kuonesha utekelezaji wa swala hatua
kwa hatua kwa kurejea Hadith Sahihi za Mtume (s.a.w):

1. Nia na Takbira ya kuhirimia


Nia ni kudhamiria moyoni kuwa unaswali, swala unayoikusudia kisha unaanza swala
kwa kusema: “Allaahu Akbar” Allah ni Mkubwa kwa kila hali”. Wakati wa kuhirimia
swala ni sunnah kuinua viganja vya mikono,mkabala na mabega. Kuhusu unyanyuaji
wa mikono mkabala na mabega imeripotiwa kuwa Mtume (s.a.w) alikuwa akifanya
hivyo katika sehemu nne tofauti:
1. Wakati wa kuhirimia swala (kuanza swala).

2. Wakati anaposema Allaahu Akbar kwa ajili ya rukui.

3. Wakati anaposimama kutoka kwenye rukuu.

4. Wakati anaposimama kutoka kwenye tahiyyatu ya kwanza ili kuendelea na rakaa


ya tatu.

Hii tunaipata katika Hadith aliyosimulia Abdullah bin ‘Umar kuwa: “Mtume (s.a.w)
aliposimama kwa ajili ya swala alinyanyua mikono yake mkabala na mabega yake na
kisha kuhirimia (kusema Allahu Akbar). Alipotaka kurukuu alinyanyua mikono kama
alivyofanya kwanza na aliposimama kwa ajili ya itidali alifanya hivyo hivyo na
alisema Allah anamsikia yule anayemsifu. (Bukhari, Muslim na Bayhaqi).
Nafa’a(r.a) ameeleza kwamba Ibn ‘Umar (Abdullah)(r.a) aliposimama kwa ajili ya
rakaa ya tatu alikuwa akinyanyua mikono; jambo ambalo alilihusisha na Mtume
(s.a.w). (Bukhari, Abu Dawud, Nasai).

Baada ya kuhirimia swala mwenye kuswali hushusha mikono yake na kuiweka


kifuani, mkono wa kulia ukiwa juu ya mkono wa kushoto kwa mujibu wa Hadith
zifuatazo: Hulab At-Tai(r.a) amesimulia: “Nilimuona Mtume (s.a.w) akiswali hali
ameweka mkono wake wa kulia juu ya mkono wa kushoto juu ya kifua chake.”
(Ahmad na At-Tirmidh)

Naye Wail bin Hijr (r.a) ameripoti: “Niliswali pamoja na Mtume (s.a.w) na aliweka
mkono wake wa kulia juu ya mkono wa kushoto juu ya kifua chake”. (Ahmad na
At-Tirmidh).
Imamu Abu Dawud na Nasai wamepokea kutoka kwa Ibn Khuzaimah kuwa Mtume
(s.a.w) alipokuwa akiswali alikuwa akiweka mkono wake wa kulia juu ya kiwiko
(wrist) cha mkono wa kushoto na sehemu ya mkono inayofuatia kiganja .

2. Kusoma Dua ya Kufungulia Swala


Kusoma dua ya kufungulia swala ni sunnah. Katika Hadithi ya Bukhari na Muslim
iliyosimuliwa na Abu Hurairah (r.a), baada ya kuhirimia swala Mtume (s.a.w)
alikuwa akileta dua ifuatayo: “wajahtu wajhi lilladhi fatwaras-samaawat wal-ardha
hanifam-muslima wamaa kaana minal-mushrikina. Inna swalatiy wanusukii,
wamah-haya, wamaamatiy, lillahi rabil-alamiina laa sharikalahu wabidhalika umirtu
wa-ana minal-mushrikiina.”“Nimeuelekeza uso wangu kwa yule aliyeziumba mbingu
na ardhi. Nimeacha dini za upotovu. Mimi si miongoni mwa washirikina. Hakika
swala yangu (na ibada zangu zote) na uzima wangu na kufa kwangu (yote) ni kwa
ajili ya Mwenyezi Mungu, bwana (Rabbi) wa walimwengu wote. Hana mshirika wake.
Na haya ndio niliyoamrishwa na mimi ni wa kwanza walio jisalimisha kikamilifu kwa
Mwenyezi Mungu. (6:79, 162-163)

3. Kupiga Audhu Billah Kabla ya kuanza kusoma Qur-an ni amri ya Allah (s.w)
kujikinga na sheitwani kama inavyodhihirika katika aya ifuatayo: 109 “Na ukitaka
kusoma Qur-an piga Audhu billah (jikinge) kwa Allah (akulinde) na Sheitwani
aliyefukuzwa (kwenye Rehema). (16:98) Hivyo tuanze kusoma Qur-an kwa kusema
“A’udhu-billahi minash-shaytwanir- Rajiim” Najikinga kwa Allah na sheitwan
aliyefukuzwa-kwenye Rehma yako

4. Kusoma Suratul-Fatiha Kusoma Suratul-Fatihah ni nguzo ya tatu ya swala na ndio


nguzo kubwa ya swala. Tunasoma suratul-Fatiha kama ifuatavyo:- Bismillahir
Rahmaanir Rahiim (1) Alhamdu liLLahi rabbil-’Aalamiin (2). Rrahmaanir Rahiim (3)
Maaliki yaumiddiin (4) Iyyaakana ‘abudu waiyyaaka nasta‘iin (5) Ih
dinasw-swiraatwal mustaqiim (6) Swiraatwa lladhiina an ‘amta ‘alaihim; ghairil
maghdhuubi ‘alaihim wala dhw-dhwaaliin (7) 110

Tafsri:
(1) Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema na mwenye kurehemu: (2)
Shukrani zote anastahiki Mwenyezi Mungu, Mola wa Walimwengu wote: (3) Mwingi
wa Rehema mwenye kurehemu (4) Mwenye kumiliki siku ya malipo: (5) Wewe tu
ndiye tunayekuabudu, na wewe tu ndiye tunaye kuomba msaada: (6) Tuongoze njia
iliyonyooka: (7) Njia ya wale uliowaneemesha; siyo (ya wale ) waliokasirikiwa, wala
ya wale waliopotea

5. Kusoma Qur-an baada ya Suratul-Fatiha Katika rakaa ya kwanza na ya pili ni


Sunnah baada ya kusoma Suratul-Fatiha kuleta Surah au aya nyingine za Qur-an:

6. Kurukuu Baada ya kusoma Suratul-Fatiha na Surah nyingine, au baadhi ya aya


katika sura nyingine unasema Allahu-akbar kisha unarukuu (kuinama). Rukuu ni
nguzo ya swala pamoja na kujituliza humo. Katika rukuu ni sunnah kumsabihi Allah
(s.w) kwa kusema kimya kimya mara tatu au zaidi “Subhana Rabbiyal’Adhiim”
“Utukufu ni wako Ee Bwana (Mlezi) wangu Uliye mkuu”

7.Kuitidal
Kuitidali ni kusimama wima kutoka kwenye rukuu, ni sunnah kusema wakati wa
kunyanyuka maneno haya:“sami’a llahu liman hamidahu” Mwenyezi Mungu
anamsikia kila mwenye kumhimidi. Na baada ya kusimama sawa ni sunnah kusema
“rabbanaa walakal-hamdu”ewe mola wetu sifa zote za ukamilifu ni zako. Pia ni
sunnah kusema maneno haya “rabbanaa walakal-hamdu mil-as-samaawati
wamil-al-ardhi wamil-amashi-ita minshai-in ba’adah”
Ewe Mola wetu sifa zote za ukamilifu ni za kwako, kutoka mbinguni, kutoka ardhini
na katika vitu vyote vilivyo baina yao (mbingu na ardhi) na kutoka katika vinginevyo
unavyo viridhia

8.Kusujudi
Ni nguzo pamoja na kujituliza katika sujudi. Mkusujudi ni kuvituliza chini viungo
saba kwa utaratibu wa swala. Vingo hivyo ni , paji a uso, viganya viwili vya mikono,
magoti mawili na matumbo ya nyayo za vidole vya miguuni.viungo vyote hivi
vinatakiwa vielekee kibla. Paji la uso ni pamoja na pua iguse chini.utasema kwenye
sijda “subhaana rabbiyal-a’alaa” utukufu ni wa kwako Mola uliye tukuka.

9.kukaa baina ya sijda mbili


Hiki ni kitako kinachopatikana baada ya kutoka kusujudi. Sifa ya kikao hiki ni kukalia
unyayo wa mguu wa kushoto na kuweka mikono miwili juu ya mapaja. Ni sunnah
kusema maneno haya: “rabbigh-firliy warhamnii wa’afinii warzuqniy”Ewe Mola
wangu nisamehe, na unirehemu, na unipe afya na uniruzuku

10.kikaa tahiyyatu
Katika kukaa Thiyyatu mtume alikuwa akikalia futi la mguu wa kushoto na
kusimamisha futi la mguu wa kulia na katika tahiyyatu ya mwisho alikaa chini na
kuulaza mguu wa kushoto katika uvungu wa mguu wa kulia na alisimamisha futi la
mguu wa kulia, katika vikao vyote hivyo viwili,

Mtume (s.a.w) alivilaza viganja vyake juu ya mapaja karibu na magoti kama
tunavyoelezwa katika hadith ifuatayo: Abdullah bin Jubair(r.a) ameeleza kuwa wakati
Mtume (s.a.w) alipokaa tahiyyatu, alikuwa akiweka kiganja chake cha mkono wa
kulia juu ya paja lake la kulia na kiganja cha mkono wa kushoto juu ya paja la mguu
wa kushoto na alikuwa akinyoosha kidole chake cha shahada (wakati wa k u s e m a ,
“ A s h - h a d u anllaaillaha illallah) na kukiegemeza juu ya kidole gumba na alikuwa
akiweka kiganja chake cha mkono wa kushoto juu ya goti lake (la mguu wa kushoto).
(Muslim).

11. Kusoma Tahiyyatu Kusoma tahiyyatu ni nguzo ya swala. “Tahiyyatu” ina maana
ya “Maamkizi”, ukiwa umekaa kikao cha tahiyyatu unaleta maamkizi kama ifuatavyo:
“Attahiyyaatu lillaah, wasw-swalawaatu, watwa-yyibaatu, assalaamu ‘alaika
ayyuhannabiyyu, warahmatullaahi wabarakaatuhu, assalaamu ‘alay-naa wa-’alaa
‘ibaadillaahi swswaalihiina. Ash-hadu an-llaailaaha illallaahu wa-ash-hadu anna
Muhammadan ‘abduhuu warasuuluhu”. “Maamkizi yote ni ya Allah, na swala zote
na yote mazuri, Amani iwe juu yako, ewe Mtume na Rehma na Baraka za Allah. Na
amani iwe juu yetu na juu ya waja wema wa Allah. Ninashuhudia kuwa hapana Mola
ila Allah. Na ninashuhudia kuwa Muhammad ni Mja na, ni Mtume wake”. (Muslim).

12. Kumswalia Mtume (s.a.w)


Kumswalia Mtume (s.a.w) ni nguzo ya swala inayofuatia baada ya kusoma Tahiyyatu.
Kumswalia Mtume si faradhi katika swala tu bali pia ni faradhi kumswalia kila
anapotajwa kwa jina lake. Msisitizo wa amri ya kumswalia Mtume unaonekana katika
aya ifuatayo:

“Hakika Mwenyezi Mungu anamteremshia Rehema Mtume; na Malaika wake


(wanamuombea dua). Basi; enyi Mlioamini msalieni (Mtume, muombeeni Rehema)
na amani”. (33:56)

Pia hadithi zifuatazo zinasisitiza umuhimu wa kumswalia Mtume (s.a.w) kila


atajwapo na kila mtu apatapo wasaa. Ali (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah
amesema: Bakhili ni yule anayesikia nikitajwa, lakini haniswalii. (hanitakii rehma).
(Tirmidh).

Abu Hurairah amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: “Anayenitakia Rehma


(anayeniswalia) mara moja, Allah humrehemu mara kumi”. (Muslim).

“Ibn Mas’ud amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: Atakayekuwa kipenzi


changu katika watu, katika siku ya Kiama atakuwa ni yule aliye mbele kuliko wote
katika kunitakia Rehma (kuniswalia). (Tirmidh).

Namna ya kumswalia Mtume (s.a.w) imeelezwa katika Hadithi nyingi lakini


iliyomashuhuri katika hizo ni ile iliyosimuliwa na Abdur- Rahman bin Ubaidillah(r.a)
na kupokelewa na Maimamu wote wa Hadithi kuwa Mtume (s,.a.w) ametufundisha
tumswalie (tumtakie Rehma) kama ifuatavyo;

“Allahumma swalli ‘alaa muhammad wa’alaa aliy Muhammad kamaa swallaita ‘alaa
ibraahima wa’alaa ali ibraahim innaka hamiidum-majid. Wabaaik ‘alaa muhammad
wa’alaa ali muhammad kamaa barakta ‘alaa ibraahima wa’alaa ali ibraahima innaka
hamiidum-majid”

Ewe Mola mrehemu Muhammad na wafuasi wake kama ulivyomrehemu Ibrahim na


wafuasi wake hakika wewe ni mtukufu na msifiwa wa haki. Ewe Mola mbariki
Muhammad na wafuasi wake kama ulivyombariki Ibraahim na wafuasi wake hakika
wewe ni wewe ni mtukufu na msifiwa wa haki.

13. Dua kabla ya salamu


Ni sunnah kuleta dua kabla ya salamu. Dua hizi ni nyingi ila miongoni mwanzo ni
Dua aliyotufundisha Mtume (s.a.w) kwa msisitizo mkubwa kama
tunavyofahamishwa katika Hadithi ya Muslim, iliyosimuliwa na Ibn Abbas, ni hii
ifuatayo: Allahumma Inni-audhubika min-’adhaabi-lqabri,Wa-auudhubika min fitnatil
masiihi-ddajjaal, Wa-auudhubika min fitnatil-mahyaa wal-mamaati, “Ee Allah
najikinga kwako kutokana na adhabu ya kabr, na najikinga kwako kutokana na fitina
za masiihi Ddajjaal na najikinga kwako kutokana na matatizo ya maisha na mauti.

Sijidat-Sah-wi (Sijda ya kusahau) Sijdat Sah-wi ni sijidah anayoileta mtu kabla ya


kutoa salaam ili kufidia kitendo cha sunnah alicho kisahau kwa mfano kusahau kukaa
tahiyaatu ya kwanza.Vile vile mtu akisahau au akikosea jambo lolote ambalo
halibatilishi swala kwa mfano akaswali rakaa tano badala ya rakaa nne kwa swala ya
Adhuhuri. Kabla hajamaliza swala alete sijidat Sahau. Hivi ndivyo tunavyojifunza
kutokana na Hadithi zifuatazo: Abdullah bin Mas’ud (r.a) amesimulia: Mtume wa
Allah alituswalisha Adhuhuri rakaa tano.Tukamuuliza kama pameamrishwa na
Mwenyezi Mungu kurefushwa swala akajibu, La! Tukamuambia: “Umetuswalisha
rakaa tano. Akasema (Mtume): Mimi ni binaadamu kama nyinyi, nakumbuka kama
mnavyokumbuka na nasahau kama mnavyosahau. Kisha akasujudu sijdah mbili
zikawa ni fidia kwa kusahau. (Bukhari na Muslim).

Muhimu:
Kumbuka kuwa sijda hii Mtume (s.a.w) aliileta baada ya kutoa salaamu na baada ya
kukumbushwa. Abdullah bin Buhaymah (r.a) amesimulia kuwa Mtume (s.a.w)
aliswalisha swala ya adhuhuri, akasimama baada ya rakaa mbili, alipomaliza swala
akasujudu mara mbili huku akisema: “Allah Akbar” katika kusujudu na katika
kuinuka, wakati amekaa kabla ya kutoa salaam, na watu wakasujudu pamoja naye. Hii
ilikuwa ni kufidia ile tahiyyatu ya mwanzo aliyoisahau”. (Muslim)

14. kutoa salamu.


Kutoa salamu ni nguzo katika nguzo za swala. Ukamilifu wa kutoa salamu ni kusema
“as-salaamu alykum warahmatullahi wabarakaatuh” salamu zipo mbili yakwanza
utatoa upande wa kulia na ya pili utatoa upande wakushoto. Sifa ya kugeuka kwa
kutoa salamu ni kuwa utageuka mpaka mashavu yawze kuonekana kwa mtu aliye
nyuma.

Lugha ya Swala Lugha ya swala,


kuanzia kwenye Takbira ya kuhirimia Swala mpaka kumalizia swala kwa Salaam, ni
Kiarabu. Hekima yake iko wazi. Kiarabu ndio lugha ya Qur-an tukufu na kwa hiyo
ndio lugha rasmi ya Kiislamu inayowaunganisha Waislamu wote ulimwenguni.
Waislamu ni umma mmoja tu na Waislamu wote ni ndugu moja wasio baguana kwa
lugha, rangi, taifa wala ubaguzi mwingine wa aina yoyote ile.Muislamu yeyote
anaweza kuwa Imamu mahali popote ilimradi tu awe anatekeleza masharti ya
Uimamu. Muislamu hana msikiti maalum. Misikiti yote ni yake na anaweza kuswali
kwenye msikiti wowote ulimwenguni bila ya kupata tatizo lolote la lugha. Kwa
sababu hii kila Muislamu inabidi ajifunze kiasi cha uwezo wake kutamka, kwa
Kiarabu yale yote tuyasemayo katika swala.

Mambo yanayobatilisha Swala


Mtu akiwa katika swala yuko katika hali maalum na haruhusiwi kufanya kitu kingine
nje ya swala hata vile vitendo vya kawaida alivyovizoea. Hivyo ukiwa ndani ya swala
ukifanya au kukitokea moja ya mambo yafuatayo, swala yako itakuwa imebatilika na
itabidi uanze upya.
(a) Kutoelekea Qibla kwa kifua pasi na dharura yoyote ya kisheria.
(b) Kupatikana na hadathi kubwa, ndogo au ya kati na kati.
(c) Kufikwa na najisi mwilini, nguoni au mahali pa kuswalia.
(d) Kuvukwa na nguo ukawa uchi. Wanaume wanaovaa shati fupi wajihadhari sana
hapa kwani,hasa wakati wa kurukuu na kusujudu, migongo yao (viuno vyao) chini ya
usawa wa kitovu (panda za makalio) huwa wazi na hivi huhesabiwa kuwa wako uchi.
(e) Kusema au kutamka makusudi lau herufi moja yenye kuleta maana nje ya maneno
ya swala.Mtume (s.a.w) amesema:  gHakika ya hii swala, haifai ndani yake maneno
ya watu kwani swala yenyewe ni Tasbih, Takbir na kusoma Qur-an. (Muslim)
(f) Kula au kunywa japo kwa kusahau.

(g) Kufanya jambo lisilowiana na swala mfululizo mara tatu. (h) Kuiacha nguzo
yoyote ya swala
(i) Ukizidisha nguzo yoyote ya swala makusudi.
(j) Kumtangulia Imam au kuchelewa kwa nguzo mbili za kimatendo kwa makusudi.
(k) Kutia nia ya kuikata swala au kujishauri moyoni kuwa uikate au usiikate swala.
(l) Kuwa na shaka kuwa umetimiza au hujatimiza sharti au nguzo yoyote ya swala.
(m) Kupotewa na akili au kulala ndani ya swala.
(n) Kutoa Salaam kwa makusudi kabla ya kwisha swala.
(o) Kuswalishwa na asiyekuwa Muislamu.
(p) Kukhalifu utaratibu wa nguzo za swala, yaani kutangulia kutekeleza nguzo ya
swala kabla ya kutekeleza nguzo inayostahiki kutangulia katika utaratibu wa swala.
(q) Kuleta dua ya kuomba kitu haramu au muhali.
(r) Kumshirikisha Allah (s.w) katika kuleta dua yaani kuleta dua ya kuomba kitu cha
halali lakini humuombi Allah (s.w) peke yake.

Dua na Dhikri Baada ya Swala


Ni vizuri mara Muislamu anapomaliza kuswali kama hana dharura yoyote asiondoke
bila ya kuleta Dhikri na dua kama alivyofundisha Mtume (s.a.w), kwani zina
umuhimu mno katika kumsaidia mja kufikia lengo la swala na lengo la kuumbwa
kwake kwa ujumla iwapo atayafahamu na kuyazingatia yale anayoyatamka. Kutokana
na Hadithi iliyosimuliwa na Samura bin Jandab(r.a) na kupokelewa na Bukhari(r.a),
baada ya swala Mtume (s.a.w) aliwageukia Waislamu aliokuwa akiwaswalisha. Kisha
aliomba maghfira (msamaha) mara tatu na kuongezea maneno yaliyoelezwa katika
Hadithi zifuatazo: Thawban (r.a) amesimulia kuwa Mtume (s.a.w) alipomaliza swala
aliomba maghfira (msamaha) mara tatu kwa kusema: Astagh-firullah (Mara tatu)
 Ninaomba msamaha kwa Allah h na kusema “Allahumma Antassalam
waminkas-salaam Tabaarakta YaaDhal jallaali Wal-ikraam.”  Ewe Allah, wewe ni
Amani, na kwako ndiko iliko Amani. Wewe ndiye Mbariki Ewe Mwenye Utukufu na
Heshima (Muslim)

Baada ya nyiradi hizi, ni vizuri pia kuomba dua yoyote kulingana na haja zako kwa
lugha yoyote. Jambo hili la kuomba dua baada ya swala, umuhimu wake unadhihirika
katika hadithi ifuatayo: Abu Umamah amesimulia kuwa: Iliulizwa:  Ee Mtume wa
Allah. ni dua gani ambayo hukubaliwa zaidi? h (Mtume) alijibu: (moja) ni ile ya
katikati ya nusu ya pili ya usiku na (pili) kila baada ya swala ya faradhi . (Tirmidh)

Hivyo ni jambo la msingi mno kuomba dua yoyote kila baada ya swala na dua zilizo
nzito zaidi ni zile zilizomo kwenye Qur-an na hadithi za Mtume (s.a.w). Kwa mfano
ni vizuri kila baada ya swala, au baada ya dhikri zilizotajwa tuombe dua ifuatayo:
Rabii ij’alnii muqiimas-swalaati wamindhurriyyatii Rabbana Wataqabbal du ’aaai.
Mola wangu! Nijaalie niwe msimamishaji swala, na kizazi changu! (Pia kiwe hivi).
Mola wetu! Na upokee maombi yangu mengine...  (14:40-41).

WASILIANA NASI KWA


TOVUTI: www.bongoclass.com
Email: admin@bongoclass.com
Simu: :+255675255927

You might also like