Professional Documents
Culture Documents
Mnyama Wa Ufunuo
Mnyama Wa Ufunuo
Kutokana na Ufunuo 17:3, mnyama huyu ana mwanamke aliyeketi juu yake,
na kwa sababu unabii unatafisiri mwanamke kama kanisa, na mnyama
kama taifa. Je kuna taifa au serikali ambayo imechanganywa pamoja na
kanisa kama kitu kimoja? Ndiyo! Vatican, ni serikali au taifa ambalo
limechanganywa pamoja na kanisa la Romani Katoliki kama kitu kimoja, na
kuongozwa na mtu mmoja ambaye ni Papa.
Ufunuo 17:9 “Hapo ndipo penye akili zenye hekima. Vile vichwa saba ni
milima saba anayokalia mwanamke huyo.”
“Ni ndani ya mji wa Roma, uitwao Mji wa vilima saba, hivyo eneo lote la
Serikali ya Vatican limewekewa mpaka kikamilifu.” –The Catholic
Encyclopedia, p 529.
ENCYCLOPÆDIA BRITANNICA
Kwa hiyo unabii huu wa Ufunuo 17:3, unaonyesha wazi kuwa mwanamke
aliyeketi juu ya mnyama, amekaa juu ya vilima saba vya mji wa Roma. Kwa
vyovyote, ni Vaticani na kanisa la Romani Katoliki ambavyo vimekaa juu ya
milima saba, na kutimiza unabii huu. Danieli 7:23 inasema mnyama wa
mwisho (Roma) anatofautiana na wanyama wengine watatu waliopita. Kwa
hakika hakuna taifa wala ufalme mwingine ambao una kanisa na serikali,
harafu kwa wakati huo huo umekaa juu ya milima saba. Ila ni kanisa la
Romani Katoliki pekee.
Ufunuo 17:15 “Kisha akaniambia, Yale maji uliyoyaona, hapo aketipo yule
kahaba, ni jamaa na makutano na mataifa na lugha.”
Na Juni, 2008 mataifa 174 katika mataifa 192 duniani, yana serikali zao
zikiwakilisha Vatican. Hivyo, kanisa la Romani Katoliki linatimiza unabii huu
kwa ukamilifu.
Danieli 7:25 “Naye atanena maneno kinyume chake aliye juu, naye
atawadhoofisha watakatifu wake Aliye juu; naye ataadhimu kubadili majira
na sheria; nao watatiwa mikononi mwake KWA WAKATI, NA NYAKATI
MBILI, NA NUSU WAKATI.”
Ezekieli 4:6 “…siku arobaini, siku moja kwa mwaka mmoja, nimekuagiza.”
Kwa hakika, hizo ni miaka 3 na 1/2 au wakati, nyakati mbili, na nusu wakati,
ambazo ni miezi 42 au siku 1260 za unabii ambazo mnyama angetawala
kisha angepata pigo la mauti au kuchukuliwa mateka. Je mnyama alipata
pigo la mauti mwaka huo 1798 B.K?
Ufunuo 13:3 “Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa
jeraha la mauti, na pigo lake lake la mauti likapona…”
Ufunuo 13:3 “Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa
jeraha la mauti, NA PIGO LAKE LA MAUTI LIKAPONA. Dunia yote
ikamstaajabia mnyama yule.”
Kama tulivyoona, upapa ulipata jeraha la mauti mwaka 1798 B.K. Vaticani
ilibaki kama kanisa tu bila nguvu za kisiasa, na unabii ulisema jeraha hili
lingepona. Je jeraha la mauti lilipona? Baada ya jeraha la mauti kutokea
miaka kadhaa badaye katika mwaka 1929 B.K. Italia ikautambua mji wa
Vaticani kama serikali ya kujitegemea, hii ilimfanya papa kuwa na nguvu
tena kama mtawala wa kisiasa na kidini. kama unabii ulivyosema kwamba
jeraha la mauti lingepona, na upapa ungerudishiwa tena uwezo wake wa
kanisa na serikali kwa pamoja. Hebu angalia magaziti yaliyotoa taarifa hiyo
jinsi waandishi wake walivyotumia lugha ya unabii bila ya wao wenyewe
kujua.
…naye hayuko tokea 1798 B.K. mpaka kusaini kwa mkataba uliofanyika
katika ikulu ya Lateran katika mwaka 1929 B.K. Vaticani ilikuwa kanisa tu
bila uwezo wa kiserikali.
…naye yu tayari kutoka 1929 B.K. mpaka leo kanisa la Romani Katoliki lina
nguvu za kisiasa na kidini, “kanisa & sesikali” au mwanamke juu ya
mnyama.
Unabii huu ni ushahidi ulio wazi sana ambao karibu kila mtu hawezi
kusumbuka kuelewa kwamba ni kanisa gani hapa duniani lililobadilisha
sheria za Mungu. Ni kanisa moja tu la Romani Katoliki ndilo lililobadilisha
sheria za Mungu kama Danieli 7:25 inavyodai kuwa. Kanisa la Katoliki
limebadilisha sheria ya pili inayozuia kuchonga sanamu ya kitu chochote
kile (angalia Kut 20:4). Katika katekism kanisa limeirarua amri ya 2 kisha
likaigawa amri ya 10 katika sehemu mbili ili kuonyesha amri 10 zote. Lakini
Je ni nani hapa duniani anayedai kuwa anauwezo wa kubadili amri za
Mungu?
“Papa anauwezo wa kubadili majira, kubadili sheria, na kuachana na
mambo yote, hata maagizo ya Kristo!” “Papa anayo mamlaka na mara
nyingi ameyatumia, kuachana na amri ya Kristo.” –Decretal, de Tranlatic
Episcop. Cap. (The Pope can modify divine law.) Ferraris’ Ecclesiastical
Dictionary.
“Bila shaka kanisa la katoliki hudai kuwa badiliko, (la Sabato Jumamosi
kwenda Jumapili) ilikuwa ni kitendo chake…na kitendo hicho ni ALAMA ya
mamlaka yake katika mambo ya kidini.” –H.F. Thomas, Chancellor of
Cardinal Gibbons
Yohana 10:33 “Wayahudi wakamjibu, kwa ajili ya kazi njema hatukupigi kwa
mawe; bali kwa kukufuru, na kwa sababu wewe uliye mwamadamu
wajifanya mwenyewe u Mungu.”
Ufunuo 13:17 “tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza,
ispokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, au hesabu ya jina lake.”
Ufunuo 13:18 “Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu
hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinaadamu. Na hesabu
yake ni mia sita, sitini na sita.”
Kwa hiyo “VICARIUS FILII DEI” ndilo jina linalotumiwa na mamlaka ya Upapa
na kumthibitisha Papa kama kichwa cha kanisa.
V 5
I 1
C 100
A 0
R 0
I 1
V 5
S 0
F 0
I 1
L 50
I 1
I 1
D 500
E 0
I 1
Jumla 666
Filii Mwana
Dei Mungu
Email Sabbathmtesigwa@gmail.com