Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 2

TAARIFA YA IDARA YA VIJANA CHAMA CHA VIJANA WAKUBWA (Y.

A)

SEHEMU A: Malengo ya Chama.


1. Kusajili vijana wote walioko kwenye umri wa vijana wakubwa. (Y. A).
2. Kununua bendera ya chama
3. Kuhitimisha walau vijana 10 kwenye kozi ya Kiongozi mwandamizi na Kiongozi
Mkuu.
4. Kupeleka vijana kambini na kwenye kongress
SEHEMU B Taarifa ya utendaji kazi
Bwana asifiwe, ifuatayo ni taarifa ya utendaji kazi ya mwaka 2023 Chama cha
vijana wakubwa Y A
Idadi ya vijana Waliosajiliwa ni 10, Idadi ya vijana wote kanisani 22, Idadi ya
vijana ambao hawajasajiliwa ni 12. Idadi ya vijana waliobatizwa 10( walio sajiliwa)
idadi ya vijana Waliosajiliwa walio na ushirika kanisa mahalia 6. Idadi ya vijana
Waliosajiliwa wasio na ushirika kanisa mahalia 4.
Idadi ya vijana walioshiriki kozi ya uongozi Hakuna, Idadi ya vijana vijana walio
hitimu kozi mbalimbali, Kiongozi Mkuu kwa mwaka 2023 ni 0, Kiongozi
mwandamizi kwa mwaka 2023 ni 0. Idadi ya vijana walioko mafunzoni kwenye
kozi mbali mbali, Kiongozi Mkuu 0. Kiongozi mwadventista 1.
Idadi ya vijana walioshiriki kwenye mikutano mbalimbali ya vijana ngazi ya
kanisa, mtaa na field ni 0. Idadi ya matukio ya matendo ya huruma yaliyofanyika
kwa mwaka ni 1 thamani ya pesa iliyotumika 300,000.

SEHEMU C: Taarifa ya vifaa vya idara Chama cha Vijana wakubwa (Y.
A)
Muongozo 1 wa Kiongozi mwandamizi.
Muongozo 1 wa Kiongozi muadventista
Fomu moja ya usajili wa kujiunga na Chama na fomu 10 za Waliosajiliwa mwaka
uliopita.
Daftari moja la majina ya wanachama.
SEHEMU C: Malengo ambayo hayakufikiwa
1. Kusajili vijana wote
2. Kuhitimisha vijana
3. Kununua bendera ya chama
4.Kupeleka vijana kwenye mikutano na kongresi
SEHEMU D: Mapendekezo au maoni ya mkurugenzi aliyepita.
Vijana Tunapaswa kujitathimini kulingana na taarifa yetu ya utendaji kazi kwa
mwaka 2023, kwa maana hairidhishi. Pia vijana tu jitahidi kuhusika walau kwa
70%-95% katika shughuli za Chama na idara kwa ujumla.
Tunapaswa kuzingatia nafasi tuliyopewa na kanisa kukitumikia Chama hiki
chenye thamani kubwa, tukitambua kuwa tunajitolea kumtumikia kristo, katika
kazi ya utume. Mwisho vijana tunaombwa kuwa na sare za idara, kulipa Bima na
viingilio kwa ajili ya mikutano ya idara pamoja na kulipa ada ya uanachama kwa
ajili ya kuendesha Chama katika kanisa mahalia.

Mwisho wa taarifa ya idara ya vijana Chama cha vijana wakubwa (Y. A)


Imeandaliwa na mkurugenzi wa Chama Sabato Mtesigwa Mashenene.

You might also like