Katiba Ya Mbauda Market

You might also like

Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 14

KATIBA YA TIMU YA

MBAUDA FOOTBALL CLUB

YA MWAKA 2024
KATIBA YA MBAUDA MARKET
FOOTBALL CLUB
KATIBA YA TIMU YA MBAUDA MARKET F.C

YALIYOMO
IBARA KICHWA CHA HABARI
UTANGULIZI

SURA YA KWANZA
Mbauda market na wachezaji wake
Viongozi na umoja wa kujitegemea

Sehemu ya kwanza
Mbauda market na wachezaji wake

1. Kutangaza timu ya mbauda market f.c


Tangazo la timu uongozi na umoja
Utekelezaji wa shughuli za timu

Sehemu ya pili
MALENGO MUHIMU NA MISINGI YA MUELEKEO
WA TIMU NA SHUGHULI ZAKE .

2. Timu na wachezaji wake


Ujenzi na umoja wa kujitegemea
Haki ya kupata elimu nyinginezo
KATIBA YA TIMU YA MBAUDA MARKET F.C

SURA YA PILI
HAKI NA WAJIBU ,HAKI NA USAWA

4. . Uhuru wa maoni
. Uhuru wa kushiriki shughuli za timu
. Wajibu wa kutii sharia za nchi

Sehemu ya kwanza
KIONGOZI WA TIMU
5. kiongozi wa timu
. Timu na mamlaka yake
. Utekelezaji wa shughuli za timu
. Mamlaka ya kuteua kushika nafasi za madaraka ya
timu
. Sifa za mtu kuteuliwa kushika madaraka ya timu
. utaratibu wa uchaguzi wa viongozi wa timu
. Wakati na muda wa kushika madarak ya timu
Sehemu ya pili
MWENYEKITI WA TIMU
6. Mwenyekiti wa timu na kazi zake
. kiapo cha mwenyekiti kushika madaraka ya timu
Sehemu ya Tatu
KATIBU WA TIMU
7 Katibu wa timu mamlaka na kazi zake
. Uwajibikaji katika timu
KATIBA YA TIMU YA MBAUDA MARKET F.C

SURA YA TATU
MAKATIBU WA MATAWI NA MIKOA
8. Makatibu wa matawi na mikoa
. makatibu wa matawi na wanachama
. Wanachama na kadi za wanachama
Sehemu ya kwanza
TAMKO LA WANACHAMA KUHUSU TIMU
9. Tamko la wanachama kuhusu timu
. wanachama kutoa taarifa kuhusu timu
. Utaratibu wa uchaguzi kwa wanachama kushika madaraka
. Tume ya uchaguzi kwa wanachama

Sehemu ya pili
OFISI YA TIMU
10. Ofisi ya Timu
. secretary wa timu
. utaratibu wa shughuli za timu
. kuitisha mkutano mkuu wa timu
. kiongozi kuhutubia mkutano mkuu wa timu
. vikao vya viongozi wa timu
. kutangaza nafasi zilizo wazi katika timu
. kamati ya timu
.utaratibu wa kutunga sharia kuhusu mambo ya timu
. kuhifadhi na kutilia nguvu uhuru wa majadiliano na
shughuli za timu
KATIBA YA TIMU YA MBAUDA MARKET F.C

UTANGULIZI

11. MSINGI WA KATIBA

Kwakuwa sisi ni wananchi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ,


tumeamua rasmi na kwa dhati kujenga katika nchi yetu jamii
inayozinagia misingi ya uhuru, haki, undugu na amani.

Na kwakuwa misingi hiyo yaweza tu kutekelezwa katika jamii


yenye demokrasia ambayo serikali yake inasimamiwa na bunge
lenye wajumbe waliochaguliwa na linawakilisha wananchi na pia
lenye chombo huru kinachotekeleza wajibu wa kutoa haki bila
uwoga wala upendeleo wowote na hivyo kuhakikisha haki zote za
kibinaadam zinadumishwa na kulindwa na kila mtu unatekelezwa
kwa uaminifu.

Kwahivyo basi katiba hii imetungwa na timu maalumu ya mbauda market


f.c ya hapa Arusha Tanzania kwa niaba ya wananchi kwa dhumuni la
kujenga jamii kama hiyo . na pia kwajili ya kuhakikisha timu yetu
inaongozwa na kufuata misingi ya kidemokrasia na ujamaa.
KATIBA YA TIMU YA MBAUDA MARKET F.C

12. MALENGO MUHIMU YA TIMU

MBAUDA MARKET F.C ni timu moja ya kidemokrasia na kijamaa na sio


ya kisiasa
Mambo yote ya timu yatasimamiwa kwa muujibu wa katiba hii

Utekelezaji wa shughuli zote za timu katika mikoa yote zitatekelezwa


na kudhibitiwa na vyombo vyenye mamlaka za utendaji na kamati
yenye mamlaka ya kutunga sharia na kusimamia utekelezaji wa
shughuli za timu

Timu na wachezaji wa mbauda market f.c ni timu inayofuata misingi ya


kidemokrasia na haki ya kijamii na kwahiyo mwisho

(a) Wachezaji ndio misingi ya timu na watapata mamlaka yote


kutoka kwa wanachama wake kwa muujibu wa katiba hii.
(b) Lengo kuu la timu ni kushinda mashindano yote
yatakayoanzishwa hapa nchini , iwe bara au visiwani.
(c) Wanachama watashiriki katika shughuli za timu yao kwa
muujibu wa katiba hii
Lengo la katiba hii ni kuwezesha ujenzi wa timu yetu ya mbauda market
f.c kwenye umoja na kujitegemea
KATIBA YA TIMU YA MBAUDA MARKET F.C

13. HAKI YA KUPATA ELIMU

Wanachama wa timu wataweka utaratibu unaofaa kwaajili ya


kufanikisha utekelezaji wa haki ya mtu kujipatia elimu, na haki ya
kupata msaada kutoka kwa jamii wakati wa uzeeni au malazi au hali ya
ulemavu. Na katika hali nyingine mtu kuwa hajiwezi na bila kuathiri haki
hizo timu. utawekwa utaratibu wa kilamtu aishi kwa jasho lake.
a) Kila mwanachama anayo haki ya kujielimisha , na kila
mwanachama ata huru kutafuta elimu katika fani
anayoipenda hadi uopeo wowote
b) Timu itafanya jitihada kuhakiisha wanachama wanapata
fursa sawa na zakutosha kuwawezesha kupata elimu na
mafunzo katika ngazi zote za shule na vyuo vinginevyo
vya mafunzo.
KATIBA YA TIMU YA MBAUDA MARKET F.C

14. HAKI NA WAJIBU

Kila mwanachama --

(a) Ana uhuru wa kutoa maoni na kueleza fikra zake.


(b) Anayo haki ya kutafuta na kupokea habari au kutoa habari
kwenye vikao vya timu
(c) Ana uhuru wa kufanya mawasiliano kuhusu timu yake na haki
ya kutoingiliwa katika mawasiliano yake
(d) Anayohaki ya kupewa taariwa wakati wote wa matukio ya
timu ikiwa safarini au katika mambo mbalimbali ya kimichezo
au ya kijamii.

Uhuru wa kushiriki kazi za timu

Kila mwanachama anayo haki ya kushiriki kazi ya timu kwa masharti na


usawa wa kushiriki nafasi yoyote katika kazi za timu

Wajibu wa kutii sharia za nchi

Kila mwanachama ana wajibu wa kutii katiba hii na sharia za nchi zilizotungwa na
mamlaka husika
KATIBA YA TIMU YA MBAUDA MARKET F.C

15. KIONGOZI WA TIMU

Kutakua na kiongozi wa timu ya mbauda market f.c . atakua kiongozi wa timu na


ataongoza timu pamoja na wanachama wake kipindi chote ,

.atakua na mamlaka yote ya juu yanayohusu timu .

Atahusika na usimamizi wa kuhifadhi katiba hii na utekelezaji wa shughuli zote za


timu hii .

Kiongozi wa timu atakua na madaraka ya kuteua watu watakaoshika nafasi za


uongozi , watakaowajibika kuweka sera za michezo na timu kiujumla na ,
watendaji wakuu watakaowajibika kusimamia sera za michezo na taasisi hii
(mbauda market f.c) katika utumishi wa timu , na nafasi ambazo zimetajwa katika
katiba hii.

Sifa ya mtu kuteuliwa kushika nafasi


a) Awe anajua kusoma na kuandika
b) Ametimiza umri wa miaka 18
c) Awe mwanachama wa mbauda marketing kwa kipindi
cha mwaka mmoja
d) Amelipia kadi yake ya uwanachama kwa muda wa miezi
sita
e) Amehudhuria vikao vya wanachama mara 10
KATIBA YA TIMU YA MBAUDA MARKET F.C

16. UTARATIBU NA UCHAGUZI WA VIONGOZI WA TIMU


Kutakuwa na utaratibu wa kuchagua viongozi wa timu . uchaguzi huu
utasiamamiwa na wajumbe watakaochaguliwa na kiongozi mkuu wa
timu.

a) Kiongozi mkuu atamteua mwenyekiti kuwa jaji wa kuamua nani ameshinda

katika nafasi ilio ombwa na kugombewa.

b) ili tawi liweze kufanya uchaguzi, linatakiwa kufikisha wajumbe 45

c) Kila mkoa kutakua na tawi moja kubwa na tawi litatoa kionngozi wa tawi na

mwenyekiti wa tawi, katika mkoa kiongozi wa tawi mkoa na mwenyekiti wa

matawi mkoa watakua wajumbe wa mkutano mkuu wa kitaifa , na

mkutanoo mkuu uta fanyika popote pale watapochagua wajumbe wa

mkutano mkuu

WAKATI NA MUDA WA KUSHIKA MADARAKA YA TIMU

Kiongozi wa timu ni kiongozi wa juu Zaidi na muda wake wa kuondoka

madarakani katiba hii haikuweka wazi mpaka timu ipate mafanikio makubwa.

a) Mwenyekiti na viongozi wengine watashika madaraka kwa


muda wa miaka mitano , na utafanyika uchaguzi wa kupata
viongozi wengine wajumbe wa matawi na wenyeviti
wamatawi na mikoa , wajumbe wa mikutano mikuu mkoa na
kila tawi litatoa wajumbe watano wa mkutano mkuu wa
mkoa
KATIBA YA TIMU YA MBAUDA MARKET F.C

17. MWENYEKITI WA TIMU NA KAZI ZAKE

Bila kuathiri kifungu chochocte cha ibara ya kumi , mwenyekiti wa timu atafanya kazi zake na
kusimamia timu pamoja na shughuli zake zote za timu kwa kushirikiana na kiongozi wa timu

(a) Mwenyekiti atapokeaa usajili wa wanachama wapya, pamoja


na wachezaji kipindi cha dirisha la usajili . pia atahakikisha
wanachama wanalipia kadi pamoja na kujaza fomu maalumu
za kujiandikisha
(b) Kiongoz wa timu , mwenyekiti wa timu na katibu wa timu
pamoja na wajumbe waliochaguliwa kuingia katika kamati
kuu ya timu , watakaa na kujadili kuhusu mambo ya timu
pamoja na malengo yote yaliopendekezwa katika timu

KIAPO CHA MWENYEKITI KUSHIKA MADARAKA YA TIMU

a) Mwenyekiti atakula kiapo cha kuongoza timu mbele ya


kiongozi mkuu na ataapa kwamba hatohujumu timu ikiwa
katika mashindano wala kusaliti wakati wowote wa
mapambano ya kimaendeleo
b) Mwenyekiti ataapa kwa kushika katiba hii kwa
mkono wakulia na mkono wa kushoto atashika mpira
wa kuchezea kwa miguu mbele ya kamati kuu.
KATIBA YA TIMU YA MBAUDA MARKET F.C

18. KATIBU WA TIMU – MAMLAKA NA KAZI ZAKE

Katibu mkuu wa timu ndiye mtendaji mkuu wa timu na atasaidiana na


mwenyekiti wake katika kusimamia kazi na shughuli zote za timu, kuandika
barua zote za mwaliko na kuwakilisha timu katika vikao vya idara za michezo
a) Katibu atahakikisha anafuatilia kwa ukaribu Zaidi mipango
na malengo ya timu ili kujua timu imefika wapi na
inafanya nini
b) Katibu ni muhimu kujua timu imepata ushindi katika
mashindano

MAKATIBU WA MATAWI NA MIKOA

Kutakua na makatibu wa mikoa ,matawi na wanachama . makatibu hawa


watatoka ndani ya mikoa tu. Na wanachama wao watatoka katika matawi yao
, makatibu hawa bila kuathiri katiba hii wataruhusiwa kufanya vikao ndani ya
mikoa yao kwa kujadili maswala ya timu na malengo kiujumla
a) Makatbu hawa ndio misingi mkuu wa timu kwa kuhakikisha
wanachama wao wanalipa ada za kadi zao kwa wakati na ndio
wasimamizi wakuu wa maswaka ya fedha ndani ya mikoa yao

19 TAMKO LA WANACHAMA

a) Tamko rasmi la wanachama linatakiwa liwasilishwe kwa mwenyekiti kwa


muujibu wa masharti na ibara hii litatolewa kwa kutumia fomu maalum
itakayowekwa kwa muujibu wa sharia iliyotungwa na kamati maalum.

b) Mwenyekiti atawasilisha kwa kamati ya maadili nakala moja ya kila tamko


rasmi lililowasilishwa kwake kwa muujibu wa ibara hii.
KATIBA YA TIMU YA MBAUDA MARKET F.C

20. OFISI YA TIMU

a) Kutakua na ofisi ya timu ambayo itakua ndani ya mkoa wa Arusha ,


na ofisi ndogo mkoa wa Dar-es-salaam
b) Tutakua na secretary wa timu ambae atafanya kazi zote za kiofisi na
kuwakabidhi wahusika wakuu wa ofisi

21. MKUTANO MKUU WA WANACHAMA

a) Kuitisha mkutano mkuu wa wanachama jambo muhimu na


mwenyekiti atahutubia mkutano huo ataongelea mambo
mbalimbali ikiwemo rasilimali fedha pamoja na kutangaza nafasi
zilizowazi, kuwakumbusha wanachama kuhusu vikao vya timu.
b) Kuwakumbusha makatibu kutunga sharia kuhusu mambo ya fedha
, kuhifadhi na kutilia nguvu uhuru wa majadiliano na shughuli za
timu

HITIMISHO
Napenda kuwashukuru mashabiki wa timu ya Mbauda market f.c
kwa kushirikiana na wadau wote wa mpira wa miguu , Mungu
awabariki.

Arusha- Tanzania
15 JANUARY 2024

You might also like