Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 5

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MAHAKAMA YA MWANZO WILAYA YA DODOMA

ILIYOPO DODOMA MJINI

KATIKA JENGO LA KITUO JUMUISHI CHA UTOAJI HAKI

DODOMA (IJC)

SHAURI LA MIRATHI NA. 30/2023

ZAITUNI d/o JUMA HUSEN……….……….…………..……MWOMBAJI

JUMA s/o HUSEN ALLI………….………..….……………..MAREHEMU

Tarehe ya kupokea shauri 3/3/2023

Tarehe ya mwisho kusikilizwa 21/3/2023

Tarehe ya Uamuzi 23/3/2023

Mbele ya C. Chambora – Hakimu Mkazi II

UAMUZI

Hili ni shauri la mirathi namba 30/2023 ambapo Zaituni Juma anaomba


kuteuliwa kuwa msimamizi wa mirathi ya marehemu Juma Husen
Alli.Baada ya kupokea shauri tangazo lilitoka na kubandikwa alipokuwa
anasihi marehemu na ofisi za serekali ya mtaa.

Lengo la tangazo lilikuwa ni kuruhusu kama kuna pingamizi la maombi


haya liletwe ili mwombaji asiteuliwe kuwa msimamizi wa mirathi ya
marehemu.

1
Mwombaji alileta maombi yake kwa kuambatanisha muhtasari wa kikao cha
familia kilichokaa tarehe 7/12/2022 na yeye kupendekezwa kuwa
msimamizi wa mirathi ya marehemu.Mwombaji pia aliambatanisha cheti
cha kifo cha marehemu chenye namba 2014763A kilichotolewa tarehe
27/02/2023 na wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA-Registration
Insolvency and Trusteeship Agency) inayohusika na usajili wa vizazi na vifo
na kuomba ateuliwe kuwa msimamizi wa mirathi.

Sm;1 Zaituni d/o Juma (41) baada ya kuthibitisha alisema marehemu


alikuwa anaitwa Juma Husen Alli Marehemu alikuwa ni mkulima na alifariki
Tarehe 25/6/1998 na kuacha watoto wawili ambao ni

1. Husen s/o Juma (47)


2. Zaituni d/o Juma (41)

Kuhusu mali, marehemu ameacha kiwanja kipo Nkuhugnu hana mali


nyingine kwanza marehemu hajajenga

Sm;2 Jackson s/o Maduma Muhenga baada ya kuapa alisema,


anamfahamu mwombaji walikuwa na kiwanja chao cha mirathi baada ya
baba yao kufariki wakawa wamekabidhiwa mirathi yeye na kaka
yake.Mpaka marehemu anafariki kiwanja kilikuwa hakijafanyiwa malipo ya
aina yoyote marehemu alikuwa anafanya kazi Dodoma General Refferal
Hospital.Marehemu alikuwa na nyumba baada ya barabara kupita akapewa
kiwanja Mahungu kata ya kizota na marehemu alifariki miaka ya tisini na
kenda.

2
Sm;3 Steven s/o David baada ya kuapa alisema anamfahamu mwombaji ni
mtoto wa marehemu wamekuwa wakiishi nae mtaa mmoja wa kizota
kuanzia miaka ya 1992 baba yake alikumwa anafanya kazi Dodoma
Regional Referral Hospital alistaafu mwaka 1995 kulingana na afya yake
alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kisukari na shinikizo la damu.Mwaka
1996 alihamia mtaa wa Nkuhungu alifariki tarehe 25/6/1998.

Marehemu ameacha watoto wawili Husen s/o Juma (toka mwaka 2000
haonekani yuko mafichoni) na Zaituni d/o Juma (41).Marehemu ameacha
kiwanja kimoja kipo maeneo ya Mahungu.Huo ulikuwa mwisho wa shauri
upande wa mwombaji.Mahakama ilikuwa na hoja moja tu:-

1. Je, mwombaji ateuliwe kuwa msimamizi wa mirathi?

Mahakama baada ya kupokea ushahidi wote na kuonesha kuwa hakuna


pingamizi na hata baada ya tangazo kutolewa hakukuwa na pingamizi,
mahakama inaona mwombaji anastahili kuteuliwa kuwa msimamizi wa
mirathi ya marehemu kama alivyoomba kwa sababu sheria inaruhusu.

Katika kesi ya Sekunde Mbwambo dhidi ya Rose Ramadhani


[2004]TLR 439 mahakama ya rufaa na kwa tafsiri ya mahakama isiyo rasmi
toka lugha ya kingereza ilisema:-

“Msimamizi wa mirathi anaweza kuwa ni mjane au mgane wa marehemu,


wazazi, mtoto au watoto wa marehemu au ndugu wa karibu ”

Mwombaji ni mtoto wa marehemu hivyo mahakama inaona anastahili


kuteuliwa kuwa msimamizi wa mirathi ya marehemu kama alivyoomba
kulingana na kesi ya muongozo/mfano (precedent) hapo juu.

3
Kwakuwa Zaituni Juma amekizi vigezo kwa mamlaka mahakama iliyopewa
na kifungu namba 2(a) Jedwali la V la Kanuni za Mirathi Katika Mahakama
za Mwanzo, Sheria ya Mahakama za Mahakimu Sura ya 11 Mapitio ya
Mwaka 2019, mwombaji ameteuliwa kuwa msimamizi wa mirathi ya
marehemu Juma Husen Alli

Imesainiwa

C.Chambora –RM II

23/3/2023

AMRI

1) Mwombaji ameteuliwa kuwa msimamizi wa mirathi ya marehemu


Juma Husen Alli kuanzia leo tarehe 23/3/2023
2) Msimamizi apewe hati ya usimamizi wa mirathi Fomu Namba 4 ya
fomu zilizokubalika kwa Mahakama za Mahakimu kwa Mahakama za
Mwanzo kama zilivyotangazwa kwenye gazeti la serekali namba 943
la tarehe 6/11/2020.
3) Msimamizi alete orodha ya mali kwa kujaza fomu namba 5 ya fomu
zilizokubalika kwa Mahakama za Mahakimu kwa Mahakama za
Mwanzo kama zilivyotangazwa Kwenye gazeti la serekali (hapo
juu).Orodha hiyo iwashilishwe ndani ya mwezi mmoja kuanzia
sasa.Msimamizi anaamriwa kuleta taarifa hizo mwisho tarehe
21/4/2023.
4) Taarifa za mgawanyo wa mirathi ziwasilishwe mahakamani ndani ya
muda wa miezi minne (siku 120), kuanzia tarehe ya leo uamuzi

4
ulivyosomwa, kwa kujaza fomu namba 6 ya fomu zilizokubalika katika
gazeti la serekali hapo juu.
5) Shauri hadi tarehe 21/7/2023 kwa ajili ya kufunga mirathi baada ya
kupokea hesabu za mirathi.

Imesainiwa

C.Chambora –RM II

23/3/2023

Uamuzi huu umesomwa leo tarehe 23/3/2023 na Charles Chambora -


hakimu mkazi, mwombaji akiwepo katika mahakama ya wazi.

Imesainiwa

C.Chambora –RM II

23/3/2023

Haki ya rufaa iko wazi ndani ya siku 30 kuanzia leo

Imesainiwa

C.Chambora –RM II

23/3/2023

You might also like