Kisw 7 Unet - MR No Time

You might also like

Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 4

@UNET EXAMS 0767190058 / 0754452285

SEHEMU A (Alama 35) PAPER 16


Sikiliza kwa makini hadithi utakayosomewa na msimamizi, kisha jibu swali la 1 - 5, kwa kuweka
kivuli katika herufi ya jibu lililo sahihi katika karatasi ya kujibia.
1. Kwa mujibu wa habari uliyosomewa, unadhani kina Juju walijuaje kuwa mahali mashua yao ilipogota
kuna karibia kukucha?
A: Walisikia sauti za watu B: Walisikia sauti za ndege C: Walisikia sauti za wanyama
D: Walisikia jogoo akiwika E: Walisikia jogoo akilia [ ]
2. Imeelezwa kuwa dhoruba ilitokea katika kisiwa gani?
A: Wete B: Pemba C: Nungwi D: Zanzibar E: Unguja [ ]
3. Kama umesikiliza kwa makini habari uliyosomewa, tuambie jina la mtu aliyekuwa wa kwanza kuhisi
mahali mashua yao ilipogota palikuwa panakaribia kukucha.
A: Janja B: Jojo C: Jaja D: Juju E: Jeje [ ]
4. Baada ya dhoruba kutokea, vyombo vingi walivyosafiria wavuvi vilienda mrama. Nini maana ya msemo
kwenda mrama?
A: Kupoteza nguvu B: Kwenda kasi C: Kupoteza mwelekeo
D: Kwenda taratibu E: Kwenda ovyoovyo [ ]
5. Kwa mujibu wa habari hiyo, unadhani Juju na wenzake walikuwa ni akina nani?
A: Walinzi wa bahari B: Wavuvi C: Wafanyakazi wa melini
D: Wafanyabiashara E: Wakulima [ ]
Katika swali la 6 - 35, weka kivuli katika herufi ya jibu lilio sahihi katika karatasi ya kujibia.
6. Mwalimu Masumbuko ana utaratibu wa kuandikiwa majina ya wasumbufu darasani. Bainisha kauli ya
utendaji ya sentensi hiyo.
A: Kutendewa B: Kutendwa C: Kutendeka D: Kutendana E: Kutendeana [ ]
7. Ningekuwa na hela ningelima shamba lote. Badili sentensi hiyo kuwa katika kauli ya kutendesha?
A: Nikiwa na hela nitalimisha shamba lote B: Ningekuwa na hela ningelimia shamba lote
C: Ningekuwa na hela ningelimisha shamba lote D: Ningekuwa na hela ningelimiana shamba lote
E: Ningekuwa na hela shamba lote lingelimika [ ]
8. Tulikwenda kumsalimia mwanafunzi mwenzetu aliyefiwa na wazazi wake na tukampa ………….Tumia
moja ya nahau zifuatazo kukamilisha sentensi hiyo.
A: mkono wa heri B: mkono wa Idi C: mkono wa buriani
D: mkono wa ihsani E: mkono wa pongezi [ ]
9. Wachezaji wa timu ya Mtibwa Sugar walikula kiapo ili wasitoe siri ya kambini. Ni nahau ipi inasadifu
msemo kula kiapo cha siri?
A: Kata tamaa B: Pata ahueni C: Tia hatiani D: Kaza kamba E: Kula yamini [ ]
10. Utatumia nahau gani kati ya zifuatazo kumuelezea mtu mwenye tabia ya kukasirika kila wakati?
A: Timua mbio B: Kunja ndita C: Chanja mbuga D: Kaa chonjo E: Piga ishara [ ]
11. “Mzee Kondo amekuwa na tabia ya kujisomea magazeti kila siku.” Tambua nafsi ya sentensi hiyo.
A: Kwanza umoja B: Pili umoja C: Tatu umoja D: Pili wingi E: Tatu wingi [ ]
12. Ipi kati ya sentensi zifuatazo ipo katika nafsi ya pili wingi?
A: Tumekunywa maziwa yote. B: Amekunywa maziwa yote. C: Wamekunywa maziwa yote
D: Mmekunywa maziwa yote. E: Umekunywa maziwa yote [ ]
13. Bainisha kauli taarifa ya sentensi hii;- “Nitaimba wimbo wangu kesho”
A: Alisema kuwa ataimba wimbo wake kesho B: Alisema kuwa angeimba wimbo wake kesho
C: “Alisema kuwa angeimba wimbo wake siku inayofuata” D: Alisema kesho ataimba wimbo wake
E: Alisema kuwa angeimba wimbo wake siku inayofuata
14. Walikuwa wameanzisha bustani yao. Kama ungeambiwa uibadili sentensi hiyo kuwa katika kauli
taarifa, lipi lingekuwa ni jibu lako?
A: “Tutaanzisha bustani yetu B: “Tumeanzisha bustani yetu” C: Tumeanzisha bustani yetu
D: “Tulianzisha bustani yetu” E: “Tunaanzisha bustani yetu” [ ]

@UNET EXAMS 0767190058 / 0754452285


15. Kama ujuavyo methali huwa na pande mbili zinazokamilishana. Katika muktadha huo, upi ni ukamilisho
wa methali ifuatayo? “Mkono uliotia jiwe majini……………………………….
A: ndio utakaotia jiwe kichwani B: ndio utakaokatwa C: ule ule utaepua
D: ule ule utaopoa E: ndio huo utakaolipasua [ ]
16. Unaye rafiki anayependa kufanya mambo bila kuyajua undani wake na mara zote mambo hayo huishia
kumdhuru mwenyewe. Utatumia methali gani kumuonya mtu huyo?
A: Usiibe kabla giza halijaingia B: Usichokula usikichachishe C: Usifunue kinywa kama hukijui ulacho
D: Usile na kipofu ukamshika mkono E: Usiache mbachao kwa msala upitao [ ]
17. Methali zifuatazo zinalandana kimaana isipokuwa moja tu. Tumia ujuzi wako kuitambua.
A: Panya wengi hawachimbi shimo B: Kidole kimoja hakiui chawa C: Jifya moja haliinjiki chungu
D: Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu E: Mkono mmoja haulei mwana [ ]
18. Chuguza methali zifuatazo kisha ubaini moja unayoweza kuitumia kumuonya mtu mnyimi asiyependa
kutoa akiogopa ataishiwa.
A: Mkono usioweza kuukata ubusu B: Mkono utoao ndio upatao C: Mpata radhi hupata hadhi
D: Mpanda hila huvuna ufukara E: Mpiga ngumi ukuta huumiza mkonowe [ ]
19. Tumia ujuzi wako wa lugha za kifasihi, kubaini kitendawili ambacho jibu lake ni kibatari.
A: Tatu tatu hadi Ulaya B: Napigwa faini kosa silijui C: Natumia nne, mbili, tatu
D: Jini mnywa damu, haangazi bila damu E: Mwavuli wa mwitu una nguzo moja [ ]
20. Kwa mfano umepita karibu na shamba la minazi na katika moja ya mnazi ukamuona mtu akichuma na
kudondosha nazi chini. Ni kitendawili kipi kitakujia kichwani kutokana na ulichokiona?
A: Amchukuapo hamrudishi B: Amekula ncha mbili C: Ajihami bila silaha
D: Ana mali lakini nguo havai E: Aliyefuatwa amekuja bali aliyefuata hajaja [ ]
21. Ni kundi lipi la maneno ambalo limebeba nomino za dhahania pekee?
A: Utukufu, Upole, Ungo, Ukarimu B: Uzuri, Shibe, Upendo, Hasira C: Upepo, Njaa, Kima, Kiu
D: Mapenzi, Uchungu, Chuma, Chuki E: Ubaya, Zuri, Ukingo, Unyenyekevu [ ]
22. Laiti ningejua kuwa yeye hapendi mayai nisingempikia. Neno yeye limetumika kama aina gani ya neno?
A: Kivumishi B: Nomino C: Kiwakilishi D: Kielezi E: Kiunganishi [ ]
23. Wanafunzi wa shule ya Mapambano wamekwenda ziara ya mafunzo. Maneno yenye ukolezo na mstari
yanasifa gani inayofanana?
A: Yote ni nomino B: Yote ni viunganishi C: Yote ni vihisishi
D: Yote ni vielezi E: Yote ni vihusishi [ ]
24. Kama ukidondosha silabi ya mwisho katika neno sakafuni, utapata aina gani ya neno?
A: E B: N C: T D: U E: V [ ]
25. Kalulu, mwanafunzi wa darasa la tano alisema “Nimekwenda nyumbani nimemkuta baba hayupo”
Unadhani Kalulu alikosea wapi?
A: Kusema alimkuta wakati hakumkuta B: Kusema alimkuta kumbe yupo
C: Kusema nilimkuta badala ya nilifika D: Kusema nilimkuta wakati hakwenda
E: Kusema hakumkuta wakati hayupo [ ]
26. Mwalimu angalifundisha vizuri………………….Kifungu kipi kinakamilisha kwa usahihi sentensi hiyo?
A: tungelifaulu B: tungafaulu C: tungefaulu D: tutafaulu E: tungalifaulu [ ]
27. Mama amenituma mkate uliotengenezwa kwa unga wa nafaka kwa ajili ya kunywea na chai asubuhi. Kwa
neno moja unadhani mama amenituma nini?
A: Andazi B: Mofa C: Bumunda D: Chapati E: Kababu [ ]
28. Daktari alitupa ufafanuzi wa ugonjwa uliokuwa unamsumbua babu. Kipi ni kisawe cha neno lenye mstari?
A: Matibabu B: Hotuba C: Fasili D: Chanzo E: Sababu [ ]
29. Garimoshi ……………tutaanza safari yetu. Ni muundo upi unafaa kukamilisha sentensi hiyo?
A: ikija B: akija C: vikija D: likija E: kikija [ ]
30. Chunguza maneno yafuatayo kisha ubaini neno lililotofauti na mengine.
A: Kicheko B: Ucheshi C: Kichekesho D: Cheka E: Mchekeshaji [ ]
@UNET EXAMS 0767190058 / 0754452285
31. Unaitambuaje Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa hapa nchini Tanzania kati ya taasisi zifuatazo?
A: BAKITA B: MKUKUTA C: MKURABITA D: TAKUKURU E: KIUTA [ ]
32. Shangazi Mage ni mfanyabiashara wa nafaka pale katika soko la Tandika. Unafikiri Shangazi Mage anauza
bidhaa gani?
A: Shuka, Vitenge na Khanga B: Viazi, Mihogo na Magimbi C: Mchele, Ulezi na Mahindi
D: Mabegi, Mikanda na Viatu E: Machungwa, Maembe na Maparachichi [ ]
33. Mwazani, mwanafunzi wa darasa la sita ameshindwa kuyapanga maneno yafuatayo kialfabeti. Ukiwa
kama mjuzi wa matumizi ya kamusi lipi litakuwa ni jibu lako utakalomsaidia Mwazani?
[buza, bubu, bunga, bunge, buti]
A: Bubu, Bunga, Bunge, Buza, Buti B: Bubu, Bunge, Buti, Buza, Bunga
C: Bunga, Bubu, Bunge, Buti, Buza D: Bubu, Bunga, Bunge, Buti, Buza [ ]
E: Bunga, Bunge, Bubu, Buti, Buza
34. Kwa mujibu wa elimu ya viambishi, unafikiri katika neno hili “amemjengea” vipi ni viambishi awali?
A: ame- B: amem- C: a- D: -jeng- E: -ea [ ]
35. Kabla ya uhuru wa nchi yetu, babu zetu walinyanyasika sana chini ya utawala wa kikoloni. Neno lenye
mstari lina silabi ngapi?
A: Saba B: Nane C: Tano D: Kumi na nne E: Sita [ ]

SEHEMU B: (Alama 5)
Umepewa insha yenye sentensi (5) zilizoandikwa bila kufuata mpangilio maalum, zipange sentensi hizo
ili zilete mtiririko mzuri wa mawazo kwa kuzipa herufi A, B, C, D na E. Siliba herufi ya jibu sahihi.
36. Bundala aliwaona wanyama wawili kwa mbali wakitembea kuelekea upande wao. [ ]
37. Bibi alinyanyua shingo ili awatazame vizuri, akasema, “Wale sio ng’ombe ni tembo. [ ]
38. Wakiwa wanakaribia kufika shambani, [ ]
39. Bundala aliuliza, “Umejuaje kuwa wale ni tembo?” Bibi akajibu nimeona masikio na mikonga [ ]
40. Alimshika bibi yake kwa woga, huku akisema, “Bibi! bibi! Unawaona wale ng’ombe?” [ ]

SEHEMU C: (Alama 10)


Soma kwa makini utenzi ufuatao kisha jibu swali la 41 - 45 kwa kuandika jibu katika fomu ya kujibia.
Kuwajuza natamani, Teknolojia hizi,
Na ukweli ujueni, Faidaze kwa vizazi,
Somo kuwapatieni, Ubunifu ugunduzi,
Faida yake mjue. Himahima twendelee.

Dunia kama Kijiji, Palipo mwanya wa rushwa,


Ni TEHAMA usihoji, TEHAMA huteremshwa,
Marekani Msumbiji, Kodi nyingi huzalishwa,
Ni mafupi masafae. Mapato yasipotee.

Utandawazi hakika, Utenzi mwisho mefika,


Dunia kuunganika, Chini kalamu naweka,
Kotekote kwafikika, Somo limekamilika,
Hili ulizingatie. Tijaye mzingatie.
Maswali.
41. Ukiusoma vizuri utenzi huo unagundua kuwa malenga alitaka kutoa ujumbe gani kwa hadhira?
…………………………………………………………………….
42. Utenzi huu una jumla ya beti ngapi? ………………………………..
43. Kila mshororo wa utenzi huu una jumla ya mizani mingapi? …………..…………………
44. Andika kina cha kiishio cha utenzi huu……………………
45. Kipi ni kirefu cha neno lililoandikwa kwa herufi kubwa katika beti za utenzi huu?
……………………………………………………………………………..………………………….……

@UNET EXAMS 0767190058 / 0754452285

You might also like