Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 4

ROHO ZA JUPITA NA MIHURI YA UTAJIRI YA MFALME SOLEIMAN

Katika zama za kati, waganga na wachawi waliamini kila sayari ina umuhimu mkubwa kwa
maisha ya binadamu na kila sayari ina nguvu zinazoweza kutumika kusaidia kazi za kichawi.
Alama maalumu zilitumiwa kwa ajili ya sayari husika ili kuvuta na kubeba nguvu iliyopo
kwenye sayari .
Alama hizo zilipatikana kwa mara ya kwanza kutoka kwenye kitabu cha miujiza cha hapo kale
kilichopewa jina la mihuri ya mfalme soleiman au ufunguo wa mfalme Soleiman,
kilichoandikwa kutoka katika maandishi ya mfalme soleiman mwenyewe .
Kitabu hicho kilifichwa kama hazina ya siri kwa maelfu ya miaka mingi.na baadae kuja
kunakiliwa katika vitabu mbalimbali vya elimu za kichawi;
Makuhani, Marabi na Wajuzi wa siri za Ulimwengu wa Kale waliamini kwamba "Sayari" zina
uwezo mkubwa juu ya hisia, tabia, na sifa za kimwili za Mwanadamu pamoja na "Ulimwengu
wa roho."
Katika kipindi hicho wataalamu wengi Walijua juu ya "Sayari" saba na kwa ujuzi wao sayari
hizo zilikuwa ni Jua, Mwezi, Zebaki, Zuhura, Mirihi, Jupita na Zohali na waliamini kwamba kila
alama iliyochorwa na mfalme Soleiman inaweza tumiwa na mtaalamu kutengeneza hirizi yenye
kuvuta nguvu ya Sayari fulani na kuamuru roho inayotawala sayari hiyo kutii ombi la mwenye
hirizi au talasimu, hirizi inaweza kuwa katika muundo wa pete,bangili , kipande cha nguo, cheni
nakadharika
Maalim shafii the don anasema kitu cha muhimu katika uandaji wa hirizi za kinajimu ni kuwa
utengenezaji wake ni lazima uratibishwe kwa usahihi na unajimu wa jadi. Ikiwa hirizi
imeandaliwa katika wakati usiofaa au ikiwa imeandaliwa na mtu mwenye elimu ndogo ya
kinajimu basi hata utoe kafara gani , hirizi hiyo inakua ni kipande cha nguo tu au pambo lisilo
na nguvu za kichawi.
Kwa kawaida mtaalamu humuuliza mteja wake juu ya ombi alilonalo, linaweza kuwa mali,
upendo, afya, nakadharika, kisha mtaalamu ataachagua hirizi inayovuta nguvu ya sayari
inayotawaliwa na roho mwenye uwezo wa kutimiza ombi hilo .
Matumizi ya hirizi za kinajimu ni njia nzuri za kutimiza jambo lolote unalotamani litimie, iwe
umaarufu, ulinzi,afya ya mwili , mahusiano , utajiri, mamlaka nakadharika, katika miaka ya kale
watu walipeana hirizi hizi kama zawadi .
Hivyo siku ya leo , Maalim shafii the don ameona ni vyema akupe na wewe zawadi hii, upate
kufahamu elimu ya sayari ya jupita na nguvu yake katika kuvuta kutupa utajiri kwa kutumia
nguvu za mihuri mitatu ya mfalme Soleiman , siku ya leo tutaongelea Jupita na Jinsi mihuri ya
mfalme Soleiman inavyoweza kuvuta utajiri.
Awali ya yote napenda kuwakumbusha wale wanaotaka utajiri juu ya pete na mafuta ya mami
wata , kwa wale wanaotaka kusafisha njia zao za kipato na kujiondolea vifungo vya kimaisha
pamoja na kung’arisha nyota zao usipitwe na mafuta ya awla bulbul, kwa wale wenye kuhitaji
elimu za tiba asili na kufahamu mambo yanayofanyika katika ulimwengu wa siri usithubutu
kupitwa na vitabu vya Maalim shafii the don.
kuwasiliana na Maalim shafii the don usisite kumpigia simu katika nambari yake inayoanza na
+255 692 007 575. Karibu
Jupita ni sayari ya 5 mbali na Jua na sayari kubwa zaidi katika Mfumo wa Jua.
Katika chati ya asili inachukuliwa kuwa sayari ya bahati nzuri, matumaini, mafanikio, ukarimu.
Jupita huleta furaha maishani. Ni sayari ya ustawi wa kimaisha. Roho mwenye kutawala jupita
ana uwezo wa kutoa bahati, afya, furaha, mali, ujuzi, elimu ya juu, maono nakadharika.
Huko Babeli roho ya Jupita alikuwa Marduk , Mfalme wa Miungu.. Marduk anaaminika
kutengeneza ardhi na anga na ndiye aliyeweka nyota mbinguni na kuunda kalenda.
Kwa wagiriki roho wa sayari ya Jupiter ni mungu wa Kigiriki, aitwae Zeus, naye anasifa ya
nguvu za kimamlaka na huitwa bwana wa Anga, mungu wa mvua na mkusanyaji wa mawingu
mwenye kuwakilishwa kwa radi. Uwezo wake ulikuwa mkubwa kuliko wengine wote.
Katika unajimu wa Vedic, Jupiter inajulikana kama sayari ya utajiri, na kwenye chati ya
kuzaliwa kwa mtu basi huyo anayezaliwa wakati huo atakuwa mtu mwenye mafanikio ya
kifedha na ustawi wa kila Nyanja, na kama ikiwa dhaifu katika chati ya kuzaliwa ya mtu basi
inaweza kusababisha matatizo ya kifedha, vikwazo vikubwa katika utafutaji wa mtu na huyo mtu
anakuwa mtu wa kupata hasara,kupoteza na ana uwezekano mkubwa wa kufa masikini kama
hatojiongeza kukutana na wataalamu wa maswala ya kinajimu na kujua vizuri asili ya kuzaliwa
kwake .
India wanamfahamu Brahaspati kama guru na bwana wa Jupiter: wakiamini kuwa bwana
brahaspati ni reincarnation ya Vishnu . Brahaspati anafahamika kama mwalimu wa Miungu,
roho yenye ujuzi wa kinajimu, Sayansi na hisabati , wafuasi wake hufanya matambiko katika
siku ya alhamisi ili kupata utajiri
Hirizi iliyoandaliwa kwa ajili ya jupita huleta utajiri na bahati nzuri, huvuta heshima, nguvu ya
kimamlaka na kuthaminiwa na watu , humfanya mwenye kuivaa hirizi hiyo kuwa na uwezo wa
kukabiliana na changamoto zote za maisha . kwa Warumi roho au mungu mwenye kutawala
sayari hiyo ndio mfalme wa miungu yote,naye anaitwa jupita kama lilivyo jina la sayari
Hirizi za jupita hufanya kazi ya kumlinda mtu kutokana na hatari Zote za Kidunia, huleta bahati
katika Kamari, biashara na kesi , mtu mwenye kusumbuliwa na kesi akivaa pete au kutembea na
hirizi ya jupita basi kesi yake itakuwa nyepesi hata kama ilikuwa ngumu kiasi gani na mwishoni
ataibuka mshindi wa kesi hiyo, kutokana na nguvu ya sayari ya jupita, hirizi yake huongeza
Utulivu wa Akili, humfanya mtu aweze kuwaza kwa kina lakini kubwa zaidi ya yote ni kuvuta
bahati nzuri na kumfanya mtu awe na uhuru katika maswala ya kifedha kwasababu hukuza
uchumi wa mtu
Muhuri wa Kwanza wa Jupiter uliochorwa na mfalme soleiman
unaaminika kuleta utajiri, bahati na mafanikio katika biashara ya aina
yoyote Muhuri huo unaundwa na tabia za sayari ya jupita na unatumika
kuiamuru roho inayotawala sayari ya jupita,
katika sayari ya jupita kuna majina ya malaika wenye mamlaka juu ya
roho inayotawala sayari hiyo, majina ya malaika hao huandikwa kiebrania katika muhuri wa
mfalme wa mfalme soleiman , kuna malaika Parasiel , ambaye ni bwana mwenye elimu na ujuzi
wa kuzipata hazina zilizofichwa , malaika mwingine anaitwa Netonieli malaika anayefanya mtu
awe maarufu kwa kumpa nyota kali ya mvuto, malaika mwingine anaitwa Devekia ,malaika
huyu huleta Amani na Utulivu , na jina la malaika wa nne ni Tsedekia , malaika huyu huleta
utajiri na utukufu. Muhuri huo umeandaliwa kwa maombi ya Zaburi 111

Muhuri wa pili wa mfalme soleiman huleta Heshima, Utajiri, Bahati,


Mafanikio na Amani ya Akili. Kwa jina lingine huitwa Pentacle ya Pili ya
Jupiter, ikiandaliwa vizuri na mtaalamu inaweza kutumika kupata utajiri,
utukufu, heshima , hadhi na bahati zingine zinazohitajika.
Roho za muhuri huu huwa na tabia ya kuzalisha bahati nzuri na mafanikio,
heshima na kila aina ya mema. Katikati ya Hexagram kuna herufi za
majina ya mungu ,muhuri huu umeandaliwa kwa maombi yanayotoka
katika Zaburi 112:3 "Nyumbani mwake mna utajiri na mali, na haki yake hudumu . milele ".

Muhuri wa tatu hutumika kwa ajili ya ulinzi dhidi ya nguvu za giza , lakini kwakuwa mada yetu
ni utajiri basi elimu hiyo ni ya siku nyingine, muhuri wa nne wa Jupita,hutumikia kupata utajiri
na heshima, na kumfanya mvaaji wa hirizi au pete inayoandaliwa kwa muhuri huu kuwa na mali
nyingi.
Juu ya talasimu kuna Jina IH, Iah . Chini yake ni Majina ya
Malaika Adoniel na Bariel ,. Adonieli , jina lenye maana
"Bwana katika Mungu," na ni malaika mwenye kuleta
rehema na neema, malaika huyu hutoa sifa na shukrani kwa
Mungu daima katika ibada, na mvaaji atavuta baraka zitokazo
kwa malaika huyu..
malaika barieli ni malaika mwenye kutoa nguvu za unabii na
kumfanya mvaaji pete au hirizi kuwa mtu mwenye maono .
muhuri huu umeandaliwa kwa maombi ya Zaburi ya 112 , na
maombi ya Zaburi 113, na kuna wimbo maalumu unaohusishwa katika uandaaji wa mihuri hii ,
wimbo huo unausisha majina ya mwenyezi Mungu yanayojulikana na watu wachache sana na si
vyema kuyataja hovyo
Hirizi hii inapokuwa imevaliwa , mvaaji hatakiwi kuivaa akiwa anafanya mambo
yatakayounajisi mwili wake kwani akifanya hivyo laana kubwa inaweza mkumba, huenda akawa
kichaa au akapoteza maisha yake au mikosi ikamuandama hadi anaingia kaburini.
Na huu ndio mwisho wa darasa la leo. Usipitwe na darasa lijalo. Wakati wote ulikuwa na mimi
Radi Ibrahim Nuhu

You might also like