Legal Opinion On Carnal Knowledge of Animal

You might also like

Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 3

16 Aprili 2024

USHAURI WA KISHERIA KUHUSIANA NA KOSA LA UBAKAJI WA KUKU.


Mnamo tarehe 12/4/2024 Rodgers Charles Sunday mwenye umri wa miaka 41, mpiga debe,
mkazi wa usagara wilayani Misungwi Jijini Mwanza alikamatwa na jeshi la polisi kwa tuhuma
za kumuingilia kuku kwa lengo la kujiridhisha kimapenzi. Tukio hili linasadikika kufanyika
nyumbani kwa dada yake hapo usagara Mwanza, kuku huyo akiwa chini ya umiliki wa dada
yake.

HOJA
Je kuku ni mnyama? Kama kuku ni mnyama ni sheria gani zinamlinda?
Je kitendo kilichofanywa na bwana Rodgers Charles Sunday ni kosa kisheria?

SHERIA
Sheria ya Makosa ya Jinai, Sura ya 16, Marejeo ya 2022
Sheria ya Ustawi wa Wanyama, Sura ya 154, Marejeo ya 2008
Black’s Law Dictionary, Chapisho la 6

UCHAMBUZI WA HOJA.
Je Kuku ni mnyama? Kama kuku ni mnyama ni sheria gani zinamlinda?

Katika ukurasa wa 87 wa Black’s Law Dictionary mnyama amefafanuliwa kama kiumbe


chochote kilicho hai chenye uwezo wa kujongea kutoka sehemu moja kwenda sehemu
nyingine, ukiachana na binadamu. Pia kifungu cha 3 cha Sheria ya Ustawi wa Wanyama,
mnyama amefafanuliwa kama kiumbe hai kilicho au kisicho na uti wa mgongo ukiachana na
binadamu.

Hivyo, kwa fafanuzi hiyo kuku nae ni mnyama kwa kuwa ni kiumbe hai chenye uwezo wa
kujongea kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine na pia ni kiumbe hai chenye uti wa
mgongo.

Zipo sheria zinazolinda Wanyama nchini Tanzania ambazo ni Sheria ya Ustawi wa Wanyama
na Sheria ya makosa ya Jinai. Sheria hizi zinalinda usalama wa Wanyama hapa nchini kwa
kupinga vikali matendo ya kikatili dhidi ya Wanyama, kuibiwa kwa Wanyama na kuwaingilia
Wanyama kimwili.

Kifungu cha 59(1)(a) cha Sheria ya Ustawi wa Wanyama imekataza vitendo vya ukatili kwa
Wanyama kama kuwapiga, kuwabebesha mizigo mikubwa, kuwatembeza masafa marefu,
kuwachokoza, na kuwatisha. Pia kifungu cha 59(1)(g) cha sheria hio kinasema mtu yeyote
hapaswi kuruhusu mnyama kufanyiwa matendo yoyote ya kikatili.

Kifungu cha 59(2) cha Sheria ya ustawi wa wanyama kimetoa adhabu kwa mtu yeyote
atakaefanya ukatili au kuruhusu ukatili kufanywa kwa wanyama kutumikia kifungo
kisichozidi mwezi mmoja au kulipa faini ya Shillingi 100,000/=

Kifungu cha 325 cha sheria ya makosa ya jinai kinasema kuwa mtu yeyote ataeua,
kusababisha ulemavu au kujeruhi mnyama yoyote mwenye uwezo wa kuibiwa atakua
ametenda kosa la jinai.

Kifungu cha 154(1)(b) cha sheria ya makosa ya jinai kinakataza kuingilia kimwili kwa
wanyama na binadamu.

Hivyo basi, sheria zinazolinda Wanyama ni Sheria ya Ustawi wa Wanyama na Sheria ya


Makosa ya Jinai.

Je Kitendo kinachosadikika kufanywa na bwana Rodgers Charles Sunday ni kosa kisheria?

Kifungu cha 154(1)(b) cha Makosa ya sheria ya Jinai kinaeleza kuwa kumuingilia mnyama
kimwili ni kosa la jinai lenye kifungo cha maisha, au kifungo cha miaka isiyopungua 30.

Kwenye Kesi ya MATHIAS BARUA dhidi ya JAMHURI, mrufani Mathias Barua alifungwa
kifungo cha miaka 30 na mahakama ya wilaya ya Korogwe kwa kosa la kumuingilia ng'ombe
kimwili kinyume na kifungu cha 154(1)(b) cha Sheria ya Makosa ya Jinai. Mahakama ya
rufaa haikutengua kifungo hicho kwa kuwa mrufani alikiri kutenda kosa wakati wa kusikiliza
rufaa.
Hivyo, ni kosa kisheria kwa binadamu kumuingilia mnyama yoyote yule kimwili kwa lengo la
kujiridhisha kimapenzi.

USHAURI
Hivyo basi, ili bwana Rodgers Charles Sunday akutwe na hatia dhidi ya tuhuma za
kumuingilia kuku kimwili kwa lengo la kujiridhisha kimapenzi yabidi kuwepo uthibitisho ya
kuwa kuku ameingiliwa kimwili na bwana rodgers kutoka kwa afisa mifugo, uwepo wa
mashahidi walioshuhudia hilo tukio ili kutoa ushahidi juu ya tukio hilo na pia bwana yabidi
apewe fursa ya kujitetea dhidi ya tuhuma zinazomkabili.

You might also like