Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 30

Kupata nakala hii yote mpaka mwisho wasiliana na +255 684

408 755

NGUVU YA KUFIKIRI KWA


UKUBWA

GODIUS RWEYONGEZA

WWW.SONGAMBELE.CO.TZ

1|G o d iu s Rwe yo nge za


Kupata nakala hii yote mpaka mwisho wasiliana na +255 684
408 755

Yaliyomo
Sura ya kwanza: Kwa nini unahitaji kufikiri kwa ukubwa Error!
Bookmark not defined.
Sura ya pili: fikiri kiukubwa kiuchumi ..... Error! Bookmark not
defined.
Sura ya tatu: kufikiri kikubwa hakuhitaji visingizio.......... Error!
Bookmark not defined.
Fikra kubwa kimaisha ........... Error! Bookmark not defined.
Vitu viwili vitakavyokufanya uwe mtu mwenye fikra kubwa
mara zote ............................... Error! Bookmark not defined.
Usikubali kuishi maisha ya kawaida ....... Error! Bookmark not
defined.
Usiogope kukosea; .................. Error! Bookmark not defined.
Usisubiri ruhusa kufikiri kwa ukubwa: mambo 10 ambayo
hupaswi kusubiri ruhusa ili kuyafanya.... Error! Bookmark not
defined.

2|G o d iu s Rwe yo nge za


Kupata nakala hii yote mpaka mwisho wasiliana na +255 684
408 755

Sura ya kwanza: Kwa nini


unahitaji kufikiri kwa
ukubwa
Nimepata wazo la kuandika kitabu hiki
baada ya kusoma makala mtandaoni
inayosema kwamba Sam Altman ambaye
ni mkurugenzi wa OPEN AI ana mpango
wa kutafuta kiwango cha dola trilllioni tano
mpaka saba kutoka wawekezaji kwa ajili ya
kampuni yake ya OPEN AI.

Hiki kitu kilinitafakarisha, kumbe badala


ya kufikiria kwa namna ya ukawaida,
nilipaswa kuwa nafikiria kwa mabilioni na
matrilioni. Ukiwaambia watu kuwa
unataka kuwa bilionea, wanakushangaa. Ila
cha kushangaza, ni kwamba wakati wewe
unaona soo kufikiri kwa ukubwa, kuna

3|G o d iu s Rwe yo nge za


Kupata nakala hii yote mpaka mwisho wasiliana na +255 684
408 755

watu ambao wanafikiri kwa ukubwa zaidi.


Kama kuna watu wanafikiri kwa ukubwa
kama huu, wewe pia unapaswa kuwa
unafikiri kwa ukubwa zaidi ya hapo.
Uwezo na akili tuliyonayo ni kubwa. Sasa
uspofikiri kwa ukubwa ni sawa na kuwa na
shamba kubwa na zuri na lenye rutuba,
halafu bado unalia njaa. Unajua kwa nini?
Unalia njaa kwa sababu hulitumii shamba
lako!

Siwataki Watu Wanaofikiri Kwa Udogo.

Donald Trump ni mfanyabiasahara


maarufu marekani, anamiliki kampuni
inayowekeza kwenye majengo, ana
majengo makubwa zaidi pale NEW YORK
CITY, lakini pia amekuwa rais wa
Marekani mwaka 2016 mpaka 2020; na
hata ninapoandika hapa yupo anafanya

4|G o d iu s Rwe yo nge za


Kupata nakala hii yote mpaka mwisho wasiliana na +255 684
408 755

kampeni za kurudi ikulu mwaka 2024.


Moja ya usemi wake mkubwa ni kwamba
mimi siwapendi watu wenye ndoto ndogo.

Kwenye hili tulionekana kwenda sawa na


Donald Trump, mimi mwenyewe
siwapendi watu wenye ndoto ndogo. Mara
zote nawapenda watu wenye ndoto kubwa
na wale wote wanaofikiri kwa ukubwa.

Ndoto kubwa zinakupa hamasa ya kusonga


mbele.

Ndoto kubwa zinakufanya usongembele na


kufanya makubwa bila ya kurudi nyuma.

Ndoto kubwa zinawahamasisha na


wengine pia kufanya makubwa, hasa wale
wanaokufuatilia. Ndoto kubwa, ndio
zimeifanya dunia kuwa bora leo hii.

5|G o d iu s Rwe yo nge za


Kupata nakala hii yote mpaka mwisho wasiliana na +255 684
408 755

Kitabu hiki ni mwongozo utakaokusaidia


wewe kuanza kufikiri kwa ukubwa kila
mara. Kuchukua hatua sashihi, na kufikia
ndoto kubwa.

Nina uhakika kama umeweza kununua


nakala ya kitabu hiki, ni wazi kuwa wewe
ni mtu wa kufkiri kwa ukubwa pia. Anza
kufikiri kikubwa, na chukua hatua za
kikubwa.
Kuwa na ndoto kubwa kama vile utaishi milele, ishi leo hii
kama vile unaenda kufa kesho.

Umeshaona hili, kuna watu wana ndoto


kubwa mpaka unaweza kushangaa. Eti
Elon musk ana ndoto za kupeleka watu
kwenye sayari ya mirihi (mars). Sam
Altman ana ndoto za kujuenga kiwanda
chenye thamani ya dola trilioni 5 mpaka
saba! Kumbuka hizi ni dola za kimaekani!

6|G o d iu s Rwe yo nge za


Kupata nakala hii yote mpaka mwisho wasiliana na +255 684
408 755

Eti mwanzilishi wa Alibaba ana ndoto ya


kuifanya kampuni yake idumu kwa karne
tatu! Hizi ni baadhi ya ndoto na fikra kubwa
ambazo watu wanazo na wanazifanyia kazi
sasa hivi ninavyoongea na wewe. Hivi
wewe una ndoto kubwa yoyote ile kwenye
maisha yako. Ni ndoto gani hiyo uliyonayo
kwenye maisha yako.

Ukweli ni kuwa kwenye maisha yako


unapasawa kuwa na ndoto kubwa ambazo
unazo. Ziwe kubwa sana ambazo kuja
kufikia miaka kadhaa ijayo. Zinaweza
zisiwe ndoto ambazo zitafanikiwa au
kufikiwa leo hii. Zinaweza kuwa ndoto za
hata miaka hata 100 ijayo. Kiufupi ni
kwamba fikiri kiukubwa mara zote. Naam,
fikiri kiukubwa.

Unajua kwa nini unapaswa kufikiri


kiukubwa?

7|G o d iu s Rwe yo nge za


Kupata nakala hii yote mpaka mwisho wasiliana na +255 684
408 755

1. KWA SABABU uwezo tulionao ndani


yetu ni mkubwa kuliko unavyoweza
kufikiri. Sisi binadamu tuna uwezo
mkubwa kabisa ambao muda mwingi huwa
hatuutumii, watafiti mbalimbali
wamefanya tafiti mara kwa mara na kurudi
kwenye kitu kimoja tu, kuwa uwezo ambao
tunautumia sasa hivi ni mdogo
kulinganisha na uwezo ambao tunao ndani
yetu.Yaani, kwamba ni kama tunatumia
chini ya asilimia kumi ya uwezo wetu
ambao tunao sasa hivi.

Gunduzi kubwa ambazo tunaona kutoka


kwa watu kama Elon Musk, watu kama
Albert Einstein, yaani, hawa watu wote na
sifa zote walizonazo, ni kwamba
wameweza kutumia uwezo wao chini ya
asilimia kumi. Hii ndiyo kusema kwamba
sisi tunao uwezo mkubwa kuliko hata
tunayofikiri. Uwezo wako ulionao sasa hivi

8|G o d iu s Rwe yo nge za


Kupata nakala hii yote mpaka mwisho wasiliana na +255 684
408 755

ni mkubwa mno kuliko unavyofikiri,


kiufupi ni kwamba kama ukiweza
kuutumia uwezo huu kwa viwango
vikubwa, kama ambavyo unapaswa
kutuumia, utaweza kupata matokeo
makubwa kuliko unavyopata sasa hivi.

Lakini swali la harakaharaka hapa ni


kwamba, kama sisi binadamu tuna uwezo
mkubwa wote huo ni kwa nini watu
hawautumii. Kuna sababu kadhaa kwa nini
watu hawatumii uwezo wao. Sababu ya
kwanza ni kwa sababu watu wengi
hawajui kama wana huo uwezo. Yaani, ni
sawa mtu ana dhahabu ndani yake lakini
hajui kwamba anayo. Kwa hiyo huyu mtu
anazunguka huku na kule akitafuta
dhahabu, lakini kumbe anaicha ndani
kwake.

9|G o d iu s Rwe yo nge za


Kupata nakala hii yote mpaka mwisho wasiliana na +255 684
408 755

Au nadhani kwa mfano mzuri zaidi nikupe


mfano wa ngano. Ngano inaweza
kutengeneza mandazi, chapati, sambusa,
kachori, biskuti… orodha ya vitu ambavyo
vinaweza kutengenezwa na ngano ni vingi
kiasi kwamba huwezi kuvimaliza, lakini
kwa upande mwingine ni kwamba
ukinunua ngano ukaitumia kutengeneza
mandazi pekee haimaanishi kwamba hiyo
ngano haiwezi kutengeneza hivyo vitu
vingine. Inaweza kufanya hivyo vizuri sana
ila ni kwamba hujaitumia kufanya hivyo
vitu. Sasa chukulia uwezo wako mkubwa,
uwezo uliolala ndani yako kama ngano,
ukiutumia tu kutengeneza mandazi kila
siku, haimaanishi kwamba hauwezi
kutengeneza sambusa, au chapati na
vingine vingi. Ukipewa elimu ya kuutumia
vizuri uwezo wako, maana yake unaweza
kuutumia kwa viwango vikubwa zaidi.

10 | G o d i u s R w e y o n g e z a
Kupata nakala hii yote mpaka mwisho wasiliana na +255 684
408 755

Kitu cha pili kinachofanya watu wengi


wasitumie uwezo mkubwa walio nao ndani
yao ni kwa sababu tu ya uoga.

Unapoanza kutumia uwezo unaanza


kufikiri kiukubwa, unaanza kufikiri vitu
vikubwa ambavyo wengine hawaoni. Au
ambavyo wengine wanaona kwamba
haviwezekani. Sasa unapoanza kufikiri
kwa ukubwa kiasi hiki, maana yake
utakuwa unaaenda kinyume na jamii ya
watu wengi walivyozoea. Watu wengi
wamezoea kuchukua hatua na kufanya vitu
vya kawaida. Ukianza kuzifanyia kazi
ndoto na malengo yako makubwa kama
haya uliyonayo maana yake kuna watu
wataanza kujiona kama wanacheza vile.

Sasa hakuna mtu ambaye angependa


kujiona kama anacheza. Kila mtu
angependa kuona kwamba anafanya kazi
na anajituma.

11 | G o d i u s R w e y o n g e z a
Kupata nakala hii yote mpaka mwisho wasiliana na +255 684
408 755

Ebu pata umezaliwa na kukulia kwenye


jamii ambapo kila mmoja alikuwa anafikiri
kwamba maisha ni kuwa na nyumba, kuoa
au kuolewa na kufanya mambo mengine
katika namna ya kikawaida. Hakuna kitu
cha zaidi ya hapo. Mara ghafla baada ya
kuwa umesoma kitabu hiki unaanza
kufikiri kiukubwa, unaanza kuwa na ndoto
kubwa zaidi ya hizo.

Ndoto ambazo watu wengine hawana,


ndoto ambazo wengine wanaona kwamba
haziwekekani kufanyika na kuwa kwenye
uhalisia. Unadhani watu wengine
watalichukuliaje hili. Si wataona kwamba
umekengeuka, si wataona kwamba
umeanza kuvuka mipaka ambayo
walikuwa wamekuwekea hata kama
hawakukwambia kwamba kuna mipaka
hiyo?

12 | G o d i u s R w e y o n g e z a
Kupata nakala hii yote mpaka mwisho wasiliana na +255 684
408 755

Ujue jamii yetu, ni kama inakuwa


imetuchorea, mipaka kwenye maeneo
mbalimbali kwenye maisha. Na mipaka hii
ni kwamba huwezi kuvuka hapa; yaani,
hapa ndiyo mwisho. Ukiendelea mbele
imekula kwako. Sasa unapoonesha ujasiri
na kuonesha kwamba unaweza kwenda
mbele zaidi na kufanya zaidi, unaanza
kuonekana kama mpinzani na mtu ambaye
anakwenda kinyume na jamii kiujumla.

Lakini kama unataka kufanya makubwa ni


sharti uweze kufikiri kikubwa kama hivi na
zaidi ya hapo. Kufikiri kikubwa ni kuwa
ndoto ambayo ni kubwa na ambayo
inawashangaza wengine kiasi kwamba
ukiwaambia wengine wanaona kama
haiwezekani ila kwako wewe unaona
wazi kuwa inawezekana. Kufikiri kwa
namna hii kunahitaji uwe mtu ambaye
unajiamini pasipo na shaka. Uwe na imani

13 | G o d i u s R w e y o n g e z a
Kupata nakala hii yote mpaka mwisho wasiliana na +255 684
408 755

kali kwamba hicho kitu hata kama ni


kikubwa namna gani, lazima tu utakifikia,
na uchukue hatua, hata kama ni ndogo
kuelekea ndoto yako hiyo kubwa. Ukweli
ni kuwa miaka kumi kutoka sasa utakuwa
jinsi ulivyo leo hii, kama hutaanza kufikiri
kiukubwa na kuanza kuchukua hatua
kuelekea huko unapotaka kufika. Na
mbaya zaidi ni kwamba kutokana na
mabadiliko ambayo yanatoke kwenye hii
dunia sasa, inawezekana hata hapo
utakapokuwa patakuwa pa chini zaidi
kutokana na mabadiliko ambayo yanazidi
kutokea.

Tatu ni kwa sababu tumezungukwa na


watu wengi ambao hawatumii uwezo
wao. Ni wengi mno kiasi kwamba
inaonekana kawaida kutotumia uwezo
wako. Na wengi hawa ndio unawaiga,

14 | G o d i u s R w e y o n g e z a
Kupata nakala hii yote mpaka mwisho wasiliana na +255 684
408 755

hawahawa ndiyo wanaitwa wanyonge.


Kufikiri kikubwa maana yake unakataa
kuitwa mnyonge. Wanyonge siyo watu
wanaofiukiri kikubwa, na ukweli ni
kwamba vitu vinyonge haviishi. Kabisa,
mimi sitaki wewe uwe mnyonge. Kama
wewe ni mgugaji unajua, hili, ukichukua
kuku wako, kumi halafu kuku mmoja
akawa mnyonge. Huyu ataonekwa na kila
kuku. Ukiwapa kuku wako chakula, wata

Watu waliotunguzubnguka wana mchango


mkubwa sana kuhusu namna mabavyo
tunaweza kuwa. Ndiyo maana unaona
kwamba kwenye jamii wazazi wanataka
watoto wao wawe kama watu ambao
wazazi wameona. Mzazi anaoona kwamba
mtoto anapaswa kuwa mwanajeshi eti kisa
kaona mjomba alikuw amwanajeshi na
alikuwa na hela. Hivyo anamtaka mwanae

15 | G o d i u s R w e y o n g e z a
Kupata nakala hii yote mpaka mwisho wasiliana na +255 684
408 755

kuwa mwanajeshi. Hiki kitu siyo sawa, kila


mtu kuna kitu anachoweza kufanya. Ksa
sababu mjomba alikuw amwanejeshi,
haimaanishi kwamba nwa mwanaae awe
mwanajeshi. Inawezekana mwanae ni
mchoraji, hicho ndicho kitu anachopaswa
kufanya.

Kama unataka kufikia ndoto kubwa.


Zungukwa kwanza na watu wenye ndoto
kubwa na waoafikiri kikubwa. Kama
hufikirii kikubwa wewe siyo rafiki yangu.
Hiyo ndiyo inapaswa kuwa motto yako.
Kama kwenye jamii unayokaa hakuna watu
ambao wanafikiri kiukubwa, unapaswa
kutoka kwenye mazingira hayo na kwenda
kwenye mazingira ambayo utakutana na
watu ambao wanafikiri kiukubwa. Kama
hali yako kiuchumi sasa hivi hairuhusu,
anza kukutana na watu hawa ambao
wanafikiri kikubwa kupitia vitabu vyao.

16 | G o d i u s R w e y o n g e z a
Kupata nakala hii yote mpaka mwisho wasiliana na +255 684
408 755

Soma vitabu vyao, utajifunza mengi na


kama utayafanyia kazi ni wazi kuwa
utaweza kupata matokeo unayotaka.

Kuna jamaa mmoja alikuwa anafikiri


kiukubwa kweli. Alikuwa na uzito
ulipoitiliza, mnene na afya yake ilikuwa
inadorora, lakiini alipoanza kufikiri
kiukubwa, hatua kubwa aliyoichukua muda
huohuo, ilikuwa ni kwenda kuchukua nguo
za mtyu aliyekuwa anataka kumfikia.
Alienda dukani akanunua nguo hizi kabla
hata hajafikia ukubwa huo wa mwili.
Wakati ananunua hizo nguo, mwenye duka
alimshangaa sana na kumuuliza hizi nguo
unamnunulia nani? Jamaa akasema
kwamba ninaenda kuvaa hizi nguo. Japo
kimwili alikuwa bado anaonekana mnene,
ila kifkra alikuwa tayari ameshakuwa na

17 | G o d i u s R w e y o n g e z a
Kupata nakala hii yote mpaka mwisho wasiliana na +255 684
408 755

mwili wa kawaida. Hii ndiyo nguvu ya


kufikiri kiukubwa.

Kufikiri kiukubwa ni kuona kwamba


umefikia lengo kubwa wakati wengine
wakiwa wanaona kwamba huna hili wala
lile. Kufikiri kikubwa ni kwenda hatua ya
ziada, wakati wengine wanaona kwamba
hupaswi kwenda zaidi ya hapo.

2. Kufikiri kutakufanya uende nje ya


boksi.

Kufikiri kikubwa ni kwenda nje ya boksi.


Ni kufanya mabo ambayo wengine wanao
na kwamba haiwezekani kufanya. Kufikiri
kikubwa ni kufikiri yasiyowezekana sasa
hivi na kuyaona waziwazi kuwa
yanawezekana. Wakati Alexander
Abaraham Bell anafikiri juu ya namna ya
kuwasiliana na watu bila kuonana na bila

18 | G o d i u s R w e y o n g e z a
Kupata nakala hii yote mpaka mwisho wasiliana na +255 684
408 755

ya kuwa na waya wa kuunganisha watu hao


wawili, alikuwa amefikiri kiukubwa.

Alikuwa amefikiri nje ya boksi. Ni


wachache sana walioweza kuona kitu kama
hiki. Lakini yeye aliona kwamba ni kitu
ambacho kinawezekana na alikifanyia kazi
kikaja kwenye uhalisia. Wakati Galileo
Galilee anasema kwamba ni dunia
inayolizunguka jua na siyo jua ambalo
linaizunguka dunia, alionekana
amekengeuka ila kwake walikuwa
amefikiri kiukubwa na kinyume kabisa na
namna ambavyo watu wengi walikuwa
wanafikiri.

Kufikiri kiukubwa ni
kujichangamotisha, ili uondoke kwenye
ukawaida.

19 | G o d i u s R w e y o n g e z a
Kupata nakala hii yote mpaka mwisho wasiliana na +255 684
408 755

KUPATA NAKALA YA KITABU HIKI CHOTE MPAKA MWISHO


HAKIKISHA KWAMBA UNALIPIA SHILINGI ELFU KUMI TU
(10,000/-)

Kitabu Cha softcopy

NAKALA NGUMU NI 20,000/-

Lipia kwa namba ya simu 0684 408 755 jina litatokea Godius
Rweyongeza

3. KUFIKIRI KIUKUBWA
KUNAKUFNYA UWEKE NGUVU NA
JUHUDI ZAKO eneo moja. Kufikiri
kikubwa kutakufanya UKAE chini na
uanze kujiuliza hivi ni kwa namna gani
naweza kufikia lengo na ndoto yangu
kubwa niliyonayo. Ni nini kinatakiwa ili
niweze kufikia lengo hili na ndoto hizi. Ni
kitu gani ambacho ninatakiwa kuwa nacho
ili niweze kufikia lengo na ndoto hizi
kubwa.

20 | G o d i u s R w e y o n g e z a
Kupata nakala hii yote mpaka mwisho wasiliana na +255 684
408 755

Ukipata nafasi ya kujiuliza haya maswali


huwezi kubaki ulivyo. Usijiulize maswali
haya juujuu, badala yake fanya kitu. yaani,
jiulize maswali huku ukiwa na kalamu na
karatasi, kisha andika majibu ambayo
yanakuka kutokana na majibu ya maswali
haya. Kufkiri kikubwa kunakusaidia
usiweke juhudi na nguvu zako sehemu
ambayo siyo sahihi.

4. Kufikiri kikubwa kunakufanya uchukue


hatua za tofauti. Ni ukweli usiopingika
kuwa hatua ambazo anachukua mtu
ambaye anafikiri kwa ukawaida na mtu
ambaye anafikiri kwa ukubwa ni tofauti.

Kama unataka kufanya makubwa fikiri


kiukubwa, maana kufikiri tu kikubwa
kutakufanya uchukue hatua kubwa zaidi.
Hatua unazochukua ukiwa unafikiri kwa

21 | G o d i u s R w e y o n g e z a
Kupata nakala hii yote mpaka mwisho wasiliana na +255 684
408 755

udogo haziwezi kuwa sawa na hatua


unazochukua pale unapofikiri kiukubwa.
Ndiyo maana nakususitiza sana kuwa
unapaswa kufikiri kwa ukubwa. Mara zote
lenga kulifikia jua, kiasi kwamba hata
itatokea hujaliifikia jua, basi utaweza hata
kuangukia mwezini.

5. Kufikiri kiukubwa kunakufaya uweze


kukuana na watu wanaofikiri kiubwa zaidi
ya wewe. Ukweli ni kwamba ndege wa wa
aina moja huwa wanaruka pamoja. Kama
unafikiri kwa udogo huwezi kukutana na
watu wanaofikiri kwa ukubwa. Ni mpaka
uanze kufikiri kwa ukubwa pia ndiyo
utaweza kukutana watu ambao kwa upande
wao wanafikiri kikubwa. Vitu vya aina
moja mara zote ndiyo huwa vinakaa
pamoja. Kama hufikiri kikubwa anza sasa
kufikiri kikubwa.

22 | G o d i u s R w e y o n g e z a
Kupata nakala hii yote mpaka mwisho wasiliana na +255 684
408 755

Kama unataka kukutana na watu


wanaofikiri kwa ukubwa anza wewe
kufikir kwa namna ambavyo wao
wanafikiri. Hapa simaanishi kwamba uwe
na ndoto zilezile walizonazo wao, bali fikiri
kwa ukubwa kulingana na ngazi uliyopo,
kusudi lako na jambo ambalo wewe
mwenyewe ungependa kufanyia kazi.

Napenda kumalizia sura hii kwa kusema


kwamba unapaswa kulenga kulifikia jua,
kiasi kwamba ikitokea hujaweza kulifkia
jua basi walau utaangukia hata mwezini.
Naam, kuwa na ndoto kubwa kama vile
utaishi milele, ila ishi siku hii ya leo kama
vile unaenda kufa kesho. Kitu kikubwa
zaidi ni kwamba unapofikiri kiukubwa
usibaki tu kufikiri kiukubwa, bali chukua
hatua hata kama ni kidogo iili uweze
kufikia ndoto zko kubwa

23 | G o d i u s R w e y o n g e z a
Kupata nakala hii yote mpaka mwisho wasiliana na +255 684
408 755

6, Unapaswa kufikiri kwa ukubwa kwa


sababu umezaliwa ukifiri kwa ukubwa

Tangu utotoni ulikuwa ukifirikiria kwa


ukubwa. Kufikiri kwa ukubwa ni kitu
ambacho wewe mwenyewe unacho
kwenye maisha yako, ulipokuwa mtoto
ulipokuwa unauliza kwamba ukikua
unataka kuwa nani, ni wazi kuwa ulikuwa
ukiwaambia watu juu ya ndoto zako kubwa
ulizonazo. Ulikuwa ukiwaambia kuhusu
malengo makubwa ambayo unataka
kuyafanyia kazi. Inawezekana ilikuwa ni
doto yako ya kuwa rubani, au ndoto yako
ya kuwa daktari, au ndoto yako kubwa ya
kuwa mwalimu n.k.

Ulipokuwa unasema ndoto kama hizi


utotoni, hakuna mtu ambaye alikwambia
kwamba haiwezekani kuifanyia kazi na
kuifanikisha ndoto yako kubwa hiyo.
Hakuna mtu ambaye alikwambia kuwa

24 | G o d i u s R w e y o n g e z a
Kupata nakala hii yote mpaka mwisho wasiliana na +255 684
408 755

haijawahi kutokea., kila mmoja


alikwambia kwamba inawezekana. Na
pengine ulipongezwa.

Hii mara nyingi ilikuwa ni ndoto ambayo


ilikuwa ni kubwa kiasi kwamba watu
wengi walikuwa wanaona kwamba
haiwezekani kuifikia, lakini walikwambia
inawezekana. Walikupongeza na hata
kukupa moyo kwamba uifanyie kazi.
Lakini sasa ulivyozidi kukua ndivyo
ambavyo watu walianza kukwambia
kwamba haiwezekani. Hivyo, wewe
mwenyewe ukaanza kuona kama vile
haiwezekani kufanyia kazi ndoto zako
mpaka zikawezekana na hatimaye
ukazikatia tamaa. Ukweli ni kuwa ndoto
zako kubwa zinawezekana

Tofauti kubwa uliyonayo sasa hivi na


utotoni ni kwamba sasa hivi wewe
umeshakuwa mtu mzima. Inawezekana

25 | G o d i u s R w e y o n g e z a
Kupata nakala hii yote mpaka mwisho wasiliana na +255 684
408 755

utotoni kuna ndoto kubwa ambayo ulikuwa


unataka kufanyia kazi mpaka kuitimiza, ila
hukuweza kufanya hivyo kwa sababu tu
hukuwa na maamuzi ya mwisho. Ni kweli
ulikuwa unapenda kufanyia kazi kitu fulani
na kikaja kwenye uhalisia, ila ukweli ni
kwamba huo uamuzi wa mwisho hukuwa
nao. Watu wengine, lada wazazi wako,
walimu, wachungaji n.k. ndiyo walikuwa
na uwezo huo. Leo hii una huo uamuzi.

Kitu kikubwa aambacho kinaweza


kinakuzuia sasa hivi kuchukua hatua
kwenye kufanyia kazi malengo na ndoto
zako kubwa ambazo umejiwekea ni kwa
sababu

 yale maneno ambayo uliambiwa


kwamba haiwezekani.

26 | G o d i u s R w e y o n g e z a
Kupata nakala hii yote mpaka mwisho wasiliana na +255 684
408 755

 Au kwamba utaweza kufanyia kazi


hki kitu kama nani.
 Wasiwasi, hofu na uoga wako
(Kumbuka kuwa uoga wako ndiyo
umasikini wako)
 Kukosa nidhamu kwenye kufanyia
kazi ndoto yako kubwa

Nje na hapo, ni ukweli kuwa ndoto yako


kubwa inawezekana.

7. Unapaswa kuwa na ndoto kubwa kwa


sababu ni haki yako ya kuzaliwa kuwa na
ndoto kubwa.

Tofauti na haki nyingine zote, haki hii ya


kufikiri kwa ukubwa na kutenda kwa
ukubwa haipatikani mahakamani. Ni haki
ambayo unaipata kwa kuifanyia kazi Ni
mpaka uifanyie kazi, ndiyo utakuja kupata
matokeo ambayo unataka.

27 | G o d i u s R w e y o n g e z a
Kupata nakala hii yote mpaka mwisho wasiliana na +255 684
408 755

Kabla sijamalizia sura hii ningependa


kukusisitiza wewe kuanza kufikiri
kiukubwa. Ndoto ndogo siyo viwango
vyako wewe. Anza kufikiri kiukubwa,
anaza kuishi kiukubwa na chukua hatua
katika namna ya ukubwa.

Swali ambalo huwa napata kutoka kwa


watu wengi ni kwamba, je, nikishaanza
kufikiri kiukubwa, je, ninapaswa
kuwaambia watu juu ya ndoto yangu
kubwa ambayo natakafanyia kazi.?

Zamani nilikuwa nawaambia watu kuwa


wawaambie wengine juu ya ndoto zao
kubwa na malengo yao makubwa. Lakini
sasa hivi nimeona hilo linakuwa
linawafanya wengi wakate tamaa, maana
asilimia kubwa ya watu ambao wanakuwa
hawaoni ule ukubwa wa zile ndoto

28 | G o d i u s R w e y o n g e z a
Kupata nakala hii yote mpaka mwisho wasiliana na +255 684
408 755

anazokuwa nazo mtu. Wanachoweza


kufanya ni kukatisha watu tama.

Hivyo, basi, kitu kikubwa na cha muhimu


zaidi ni kuhakikisha, baada ya kuwa
umeanza kufikiri kwa ukubwa, unachukua
hatua na kufanyia kazi kile ambacho
unafikiri kwa ukubwa. Kamwe usikubali,
kuendelea kufikiri kwa namna ya
ukawaida.

29 | G o d i u s R w e y o n g e z a
Kupata nakala hii yote mpaka mwisho wasiliana na +255 684
408 755

KUPATA NAKALA YA KITABU HIKI CHOTE MPAKA MWISHO


HAKIKISHA KWAMBA UNALIPIA SHILINGI ELFU KUMI TU
(10,000/-)

Kitabu Cha softcopy

NAKALA NGUMU NI 20,000/-

Lipia kwa namba ya simu 0684 408 755 jina litatokea Godius
Rweyongeza

30 | G o d i u s R w e y o n g e z a

You might also like