Mambo Ya Ndoaa5

You might also like

Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 177

Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B.

Saimon

MAISHA YA NDOA
MAMBO YA KUZINGATIA ILI KUWA NA NDOA
YENYE FURAHA

EDWARD B. SAIMON

1
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

2
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

MAISHA YA NDOA
© Edward B. Saimon

P. O. B0x 1369 Kigoma

Simu: +255 753 018 397


Barua pepe: kiookigoma@gmail.com

Toleo la Kwanza 2020

Kimechapishwa na
Mpango Mkakati Technologies Co. LTD
P. O. BOX 5562 Dar es salaam, Tanzania
www.mpangomkakati.co.tz
info@mpangomkakati.co.tz
+255 715403214/ +255 767238675

Haki zote zimehifadhiwa.

Hairuhusiwi kuiga, kunakili au kudurufu kitabu hiki au kwa njia


nyingine yoyote bila idhini ya mwandishi isipokuwa kama rejea ya
utafiti na mafunzo.

3
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

YALIYOMO
SHUKRANI 7

DIBAJI 9

UTANGULIZI Error! Bookmark not defined.

SURA YA KWANZA 1

KUSUDI 1

Kuhusu kuumba 8

SURA YA PILI Error! Bookmark not defined.

MAMBO YA KUJUA KABLA YA KUOA AU KUOLEWA 12

SURA YA TATU Error! Bookmark not defined.

CHANZO/ASILI YA TABIA ZA WATU 30

SURA YA NNE 33

KUCHAGUA MARAFIKI 33

Mambo ya kuzingatia 34

MAANA YA NDOA KWA MUJIBU WA SHERIA ZA NCHI 43


Namna za kufunga ndoa kwa mujibu wa sheria za nchi 44

SURA YA SITA 54

MAANA NA MAKUSUDI YA NDOA YA KIKRISTO 54

Ndoa ya kikiristo ni nini? 54

Mambo muhimu juu ya ndoa ya Kikristo 55

KUSUDI LA MUNGU JUU YA NDOA 65

4
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

7.4Kwanini ni mhimu kuwa na ndoa 67

7.5 Sababu zisizo sahihi; 69

SURA YA NANE 75

MAMBO YANAYOMHUSU MWANAMUME 75

SURA YA TISA Error! Bookmark not defined.

MAMBO YANAYOMHUSU MWANAMKE 86

SURA YA KUMI Error! Bookmark not defined.

TOFAUTI ZA KIMAUMBILE KATI YA MWANAMUME NA


MWANAMKE 94

SURA YA KUMI NA MOJA 104

NAFASI YA MWANAMKE KATIKA NDOA KIBIBLIA 104

Matumizi ya kinywa chako 109

SURA YA KUMI NA MBILI 115

MAMBO YA KUFANYA ILI KUMSAMEHE MWENZI


WAKO 115

Mambo ya kuimarisha ndoa yako 117

SURA YA KUMI NA TATU 133

MAWASILIANO KAMA MSINGI MKUU KATIKA NDOA 133


Ndoa ni kujengana kila leo 136

Ongea kile unachomaanisha; 138

SURA YA KUMI NA NNE 151

NDOA YENYE FURAHA 151


5
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

KUHUSU MWANDISHI MWANDISHI 161

6
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

SHUKRANI
Kwanza kabisa ninapenda kutumia nafasi hii kumshukuru Mungu
wetu wa Mbinguni ambaye alinitambua kabla sijazaliwa kwa
mafunuo yake kwangu kupitia Roho Mtakatifu ambaye
ameniwezesha kupata maneno ya kuzungumza na wewe juu ya
maisha ya ndoa; na hasa mambo unayopaswa kuyafahamu ili kuwa
na ndoa yenye furaha. Ninaamini maneno yaliyomo katika kitabu
hiki yatatengeneza kitu kipya ndani yako. Heshima na utukufu apewe
yeye tu, maana bila yeye nisingeliweza kitu.

Pili nina mshukuru sana mke wangu mpenzi Bi Leah Lukios pamoja
na wanangu wapenzi Jenivela, Saimon na Saraphina kwa moyo
wao wa uvumilivu kwangu pamoja na kuwa nami bega kwa bega
wakati wote na hasa wakati nikiandaa kitabu hiki. Kuna wakati
nilikata tamaa na kuvunjika moyo lakini kila nilipowatazama nilitiwa
moyo na kupata nguvu za kuendelea zaidi. Kuna wakati mke wangu
alikesha pamoja nami mezani nilipokuwa ninaandika na mara zote
alisikika akisema “kazana mume wangu Mungu analo kusudi la
kuponya ndoa za watu kupitia wewe”. Maneno hayo yamekuwa
yakinisukuma kuendelea.“Kitu pekee ninachoweza
kukuhakikishia mke wangu ni kwamba ninakupenda sana na
mara zote ninakuombea, nami ninaamini kwamba wewe na
watoto wetu mnaniombea maana ninauona ulinzi wa Mungu juu
yangu”.
7
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

Ninawashukuru baba na mama Bwana na Bibi Bihaga Saimon


Masela kwanza; walipoona inafaa walikubaliana kupitia uchumba na
baada ya kuungana Mungu akawafanikisha nikazaliwa. Hili ni jambo
muhimu sana maana ninaamini wakati wao wakichumbiana na
kukubaliana mahali fulani wapo walioshindwa kukubaliana. Kwa
kipekee sana ninamshukuru mama yangu Bi Jenivela kwa kufanyika
baraka katika maisha yangu. Bado ninaamini kwamba Mungu
alikutumia vema kusimama kama, mwalimu, mwelekezaji na
mshauri wangu. Itoshe kuamini kwamba Mungu alikutumia wewe
kuwa mama yangu. Kuna wakati nawaza hivi kama huyu Jenivela
asingelikuwa mama yangu ningelikuwa hivi kweli?

Shukurani zangu pia zimwendee mchungaji wangu Zacharia


Andrea (Mchungaji kiongozi wa FPCT misheni ya Mwanga), yeye
ni baba yangu kiroho, huyu mara zote kwangu amekuwa na atabaki
kuwa mfano wa kuigwa (role model). “Baba ninakupenda na
kukuheshimu sana. Ulikubali kutumika nami nikiwa si kitu kwa
macho ya wanadamu, lakini katika macho ya rohoni Mungu
alikutumia ukaniona. Sina cha kukulipa zaidi ya kukuombea
kwa Mungu akupe maisha marefu na kukuinua katika utumishi
wake”. Wengine ambao siwezi kuacha kuwashukuru ni wazee wa
Kanisa pamoja na kanisa la FPCT Majengo kwa ujumla wenu.
Mmekuwa mkinitia moyo pale nilipolegea kama mwanadamu,
8
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

hamkusita kuniombea wakati wote. Mungu tunayemtumikia na


ample kila mmoja wenu kwa kadri ya haja ya moyo wake.

Orodha ya waliogusa maisha yangu ni ndefu sana kila mmoja kwa


jinsi ya tofauti, kwa msingi huo sio rahisi kumtaja kila mmoja hapa
na haimaanishi wale ambao wametajwa ni bora kuliko wale ambao
sikuwataja, hapana. Ukweli ni kwamba kila mara nilipokuwa
nikiandika eneo hili nilipata wakati mgumu sana. Lakini nataka kila
mmoja aelewe kuwa ninatambua, kuthamini na kuheshimu mchango
wake katika kuifanikisha kazi hii. Na kwa namna ile ile
ninayothamini mchango wako ninakusihi mpendwa wangu ukubali
kuzipokea shukrani zangu. Mungu akubariki sana.

DIBAJI
Kiini cha ustawi wa jamii ni ndoa. Tangu awali Mungu aliweka ndoa
kuwa taasisi ambayo inaamua ustawi na mustakabari wa ulimwengu.
Ni katika ndoa Mungu aliagiza kuzaa, kuongezeka, kuijaza nchi na
9
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

kuitiisha. Jukumu hilo halikukabidhiwa kwa kanisa, taasisi za kijamii


wala taasisi za kiserikali. Ni katika karne za hivi karibuni, baada ya
wanandoa kushindwa kutimiza wajibu wao, taasisi zingine zimeamua
kuingilia kati ili kurekebisha mambo. Hata hivyo lazima tujue,
pamoja na jitihada zinazofanywa na taasisi hizo, jukumu hilo ni la
wanandoa. Hivyo ndivyo Mungu anavyolitazama na huo ndio
ukweli.

Hatuwezi kuwa salama ikiwa tutapuuzia changamoto zinazoendelea


kujitokeza katika mahusiano ya ndoa. Japokuwa kila mmoja anaweza
kuwa na namna yake ya kuyatazama matatizo na changamoto hizo
lakini ni muhimu tukakubaliana kwa pamoja kuwa bado Mungu
anayo hekima na uwezo wa kututoa katika changamoto hizo na anao
watu wake aliowateua ambao kwa kuwatumia hao anaweza
kuzungumza na jamii ili kuleta uponyaji kamili. Jambo la muhimu ni
kutambua kuwa tumefika hapa tulipofika kwasababu ya kukosa
maarifa.

Biblia inasema “Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa


(HOSEA 4:6)”. Tupo kwenye kipindi ambacho njia pekee ya
kujikwamua kutoka katika changamoto hizi ni kupata maarifa sahihi.
Yamkini tulilelewa katika mazingira ambayo hatukuwa na maarifa
lakini nyakati na mazingira yalitulinda na tukawa salama. Maadili
yalikuwa mazuri, teknolojia ilikuwa chini na maisha kwa ujumla
yalikuwa tofauti sana na sasa. Kadiri tunavyozidi kwenda mbele
10
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

mambo yanabadilika na kwa kuwa hatuna uwezo wa kuzuia


mabadiliko ni muhimu tukajua namna ya kuenenda kulingana na
mabadiliko. Kutojua mambo hakutokufanya uepukwe na madhara ya
kutojua. Utaangamia tu hata kama hutopenda kuangamia. Kutamani
kutoangamia haitoshi kukulinda usiangamie. Ili kuwa salama njia ni
nyepesi sana; pata maarifa.

Tukijua kuwa kila mmoja, mwanamke na mwanaume, ana wajibu wa


kutimiza; ni muhimu kutambua kuwa kulaumiana juu ya nani
alipaswa kufanya nini kamwe haitotusaidia. Kila mmoja ana wajibu
wa kujifunza na kujua yampasayo kufanya. Hata kama si kwaajili ya
Mungu basi tujitahidi kutunza mahusiano yetu kwaajili ya watoto
ambao hawana hatia hata kidogo. Hata hivyo, ikiwa ni kwa ajili ya
Mungu au kwa ajili ya watoto, ufahamu sahihi kwa kila mmoja ndio
kiini cha mafanikio katika mahusiano.

Uzuri wa kitabu hiki ni kuwa kitakusaidia wewe msomaji kupata


uelewa mpana kuhusu ndoa katika mtazamo wa kibiblia, kisaikolojia
na kisheria. Hapa umeshika mwongozo ambao unaweza kutafsiri
hatima ya maisha yako na kubadili kabisa mtazamo wako juu ya
mwenzi wako. Nikutakie kila lenye heri katika kujifunza huku.
Asante

Deogratius Sukambi
Mwalimu, Mshauri na Mchambuzi wa Mahusiano na Ndoa

11
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

UTANGULIZI
Kitabu hiki kinahusu mambo ya ndoa ambayo unatakiwa
kuyafahamu ili kuwa na ndoa yenye furaha.Nimesukumwa
kuandika kitabu hiki kwa sababu mambo yanayohusu ndoa kwa
walio wengi yanaonekana kutofahamika kwa sehemu kubwa kama
ilivyotazamiwa. Hatari kubwa inayolikabili kanisa la sasa na jamii
ni pamoja na vijana kutokujua nini wanatakiwa kufanya
wanapofikia hatua za kutaka kuingia kwenye ndoa.

Mpango wa Mungu kuhusu ndoa unalenga watu wawili,yaani mume


na mke, waishi pamoja maisha yao yote kwa ajili ya utukufu wa
Mungu.Hii ina maana katika kusudi la Mungu hakuna mawazo ya
watu kuachana wala kutengana ndio maana anasema “anakuchukia
12
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

kutengana” Malaki 2:16. Mungu alifanya hivyo makusudi kwa kuwa


alikusudia kujiandalia familia au taasisi imara kwa ajili ya
kuendeleza uumbaji na utendaji wake.

Kutokana na mazingira na ukengeufu wa mioyo ya wanadamu


vijana wamekuwa wepesi kuwazia harusi na mwonekano wa nje
wa harusi badala ya kufikiria lengo la msingi ambalo ni maisha
baada ya kufunga ndoa. Zipo baraka nyingi katika maisha ya ndoa
na pia changamoto zaweza kutokeza kwenye maisha ya ndoa.
Kwahiyo katika kitabu hiki nitazungumzia juu ya mambo ambayo
vijana wote na watu wengine kama vile wazazi, jamaa na marafiki
wanapaswa kuyafahamu kabla ya kuanza mahusiano
yatakayowawezesha kuingia kwenye maisha ya ndoa. Pia nitatoa
ushauri juu ya namna bora ya kupunguza uwezekano wa kutokea
kwa changamoto na kukabiliana nazo kwa wakati.

Moja ya changamoto kubwa katika kizazi hiki inayohatarisha


ustawi wa ndoa ni vijana wanaotazamiwa kuoa au kuolewa kukosa
maarifa juu ya mambo muhimu ya kuzingatia kabla ya kuchumbia
au kuchumbiwa ambayo hujumuisha maisha binafsi ya kiroho,
namna anavyojitambua, anavyomfahamu Mungu, anavyohusiana
na vijana na watu wengine, sifa za mume au mke tarajiwa,sifa za
wazazi wa mume au mke tarajiwa, kuomba uongozi wa Mungu

13
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

katika kumpata mume au mke na mipango ya kiuchumi ya


kukamilisha taratibu za kufunga ndoa na kuanza maisha ya ndoa.

Ikiwa kila kijana anayetarajia kuoa au kuolewa atakuwa na maarifa


ya kutosha katika maeneo yaliyotajwa hapo juu na kuyazingatia
katika mchakato wote kuelekea kwenye maisha ya ndoa itasaidia
kupunguza changamoto katika maisha ya ndoa.Kutokana na
kukosekana kwa stadi na maarifa miongoni mwa vijana
wanaojiandaa kuingia kwenye ndoa, wamejikuta wakitumia muda
mwingi kujadili namna harusi yao itakavyozidi harusi
zilizotangulia, magauni gani mapya yatakavaliwa na mambo
yanayofanana na hayo ili kila mmoja ajue kweli harusi
imefanyika.Wanaondoa waliokuwa na mawazo kama hayo kabla ya
kuolewa walijikuta kwenye madeni yasiyolipika kutokana na kunia
makuu kupita uwezo wao na kwa kweli mambo hayo kwa sehemu
ni chanzo cha migogoro kwenye ndoa zao hata kupelekea
kukosekana kwa furaha na amani ndani ya ndoa.Kuna maarifa
mengine yanayopaswa kuzingatiwa na wanandoa baada ya kuoana
ili ndoa yao idumu kuwa ya amani na furaha.

Kwahiyo malengo makuu ya kuandika kitabu hiki ni kutaka


kufufua na kuchochea hali ya kutafuta maarifa miongoni mwa
vijana wanaotarajia kuoa au kuolewa na miongoni mwa wanandoa
ili hatimaye wawe na ndoa zenye amani na furaha.

14
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

Hivyo,ninategemea wale wanaotarajia kuingia kwenye ndoa na


wale walioko katika ndoa watakisoma kitabu hiki ili kiweze
kuwaongezea maarifa wao wenyewe au/na uzao wao.Ninawashauri
wanandoa kukaa pamoja ili wapate nafasi ya kunong’onezana
baadhi ya mambo mazuri au yenye mapungufu yanayowagusa ili
kama kuna waliyobaini kama mapungufu waweze kufanya
masahihisho na hatimaye kuwezesha uponyaji wa majeraha ya
ndani yaliyokuwepo kwa utukufu wa Mungu.

Mwisho ingawa sio kwa umuhimu,ninawasihi kupitia jina la Yesu


Kristo mnaposoma kitabu hiki mkiwa pamoja kama wanandoa na
mkagundua kuna mahali mlifanya vizuri kwa msaada wa Mungu
tumieni nafasi hiyo kujipongeza na kumshukuru Mungu pamoja
kama mke na mume hasa mkikumbuka mahali ambapo Mungu
alipowatoa pamoja na magumu ambayo Mungu aliwavusha.

15
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

SURA YA KWANZA

KUSUDI

Watu wengi wameshindwa kuelewa maana halisi ya maisha ya ndoa


jambo linalowapelekea kuishi maisha ya watu wengine au kutamani
kuishi kama akina fulani.Ukweli ni kwamba kila aliyeumbwa na
Mungu aliumbwa kwa
kusudi maalumu.Mungu wetu aliye mwaminifu kwa kujua hilo
amemweka mtu mwingine (mwanamke) ambaye anakuja kwenye
maisha yako kama msaidizi wa kusaidia kutimilizwa kwa kusudi la
Mungu katika maisha yenu. Mungu aliumba kila kitu kwa kusudi
maalum. Hakuna kilichoumbwa na Mungu ambacho hakina kusudi
la kuumbwa kwake Mithali16:4. Kadhalika, Mungu aliruhusu
kuwepo kwa maisha ya ndoa kwa makusudi maalumu, mwanaume

1
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

na mwanamke wanaoingia kwenye ndoa ni lazima wawe na kusudi


la kutimiza katika maisha yao na kwa ajili ya Mungu mwenyewe.

1.1 Kusudi ninini?

Ni wazo au lengo lililowekwa ndani ya akili yako ili liwe kama


dira ambayo utaweza kuitumia kuongoza maisha yako ili kutimiza
lile ambalo Mungu ameweka katika maisha yako.Kwa maneno
mengine unaweza kusema ni sawa na lengo, dhumuni au
shabaha.Ni ile hali ya kufanya jambo ambalo husababisha wajibu
ambao hutokeza tabia na mwenendo wa kilicho kusudiwa. Ili
kulibaini kusudi lako lazima uwe umejitambua.Kwa kuwa kila kitu
kimeumbwa kwa kusudi maana yake kujaribu kutenda au kwenda
kinyume na kusudi ni kutenda dhambi. Ni vizuri kulitafuta kusudi
la kuumbwa kwako ili kuishi katika hilo kila mara.

1.1.1 Kujitambua

Kujitambua ni neno la kiswahili linalotokana na neno tambua


ambalo maana yake ni kujielewa vilivyo bila kuacha shaka.Hivyo,
kujitambua ni kujielewa wewe ninani? Una mahitaji gani ya msingi?
Kwanini ulizaliwa na kuwa hapo ulipo? Wengine wanategemea nini
kutoka kwako? Nenda mbele zaidi kujua wengine wanakuonaje?
Nini ni mtazamo wao kwako hasa? Je mtazamo huo ni chanya (+) au

2
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

hasi (-). Jitambue katika maeneo yafuatayo:- kimwili, kiroho, kiakili,


kijamii na kiuchumi.

a) Kimwili

Kujitambua kimwili ni jumla ya mambo yote ya nje ya kimaumbile


ukianzia namna mtu anavyoonekana alivyo. Kwa mfano ni mrefu au
mfupi, mnene au mwembamba, mwanamke au mwanaume, umri
wako umeenda, mtu wa makamo, mzee, n.k.), rangi yako (mweusi,
maji ya kunde au mweupe), hali ya afya yako n.k. Kwa kawaida sifa
hizi za kimaumbile kwa sehemu kubwa zinategemea wazazi
waliokuzaa au mazingira ulimokulia. Katika eneo hili la kujitambua,
kwa vyovyote vile na kwa hali yoyote ile mtu alivyo anapaswa
kujiona na kujikubali kuwa yeye ni wa thamani, ni mzuri, ni
mrembo, anafaa, anaweza kutimiza kusudi lolote ikiwemo kuwa
mume au mke wa mtu.

Mwanzo 26:7 watu wa mahali hapo wakamwuliza habari za mkewe.


Akasema, ni ndugu yangu huyu maana aliogopa kusema, ni mke
wangu, watu wa nchi wasije wakamwua kwa ajili ya Rebeka; kwa
maana alikuwa mzuri wa uso na 1samweli 25:3 inasema na jina la
mtu huyo aliitwa Nabali; na jina la mkewe aliitwa Abigaili, na huyo
mwanamke alikuwa mwenye akili njema, mzuri wa uso; bali yule
mwanamume alikuwa hana adabu, tena mwovu katika matendo yake;
naye alikuwa wa mbari ya Kalebu. Mistari hii inatuomyesha kwamba
watu wanatazma sura pia kwa maana ya umbo la mtu ili kukidhi haja
3
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

ya kuingia kwenye ndoa. Kumbuka huyu unayetaka kuungana naye


ni mwenza wa maisha sio wa muda fulani hapana ni wa kufa na
kuzikana kwahiyo tazama kiwe kitu roho inapenda ili kujiepusha na
kujuta mbeleni.

b)Kiroho
Kujitambua kiroho inajumuisha mambo yanayohusiana na imani
kama vile kumwamini au kutokumwani Mungu, masuala ya toba na
kusamehewa dhambi, kuokoka, kuliamini neno la Mungu, kuwa
mtakatifu, kuongozwa na Roho Mtakatifu, kumwabudu na kumsifu
Mungu, kwenda kanisani kusali (kanisa gani), huduma yako kanisani
(mwimbaji, mwinjilisti, kukarimu wageni, mwombaji, mwalimu,
n.k.), ufahamu wako kuhusu nafasi ya Mungu katika maisha yako,
uongozi wa Mungu, kujilinda na dhambi n.k. Kabla ya kuingia
kwenye ndoa hakikisha unaujua upande uliosimama kiroho na hata
wale wanaokuzunguka wakikutazama wathibitishe hilo.Ukiamua
kuwa rohoni lazima kujijua kiroho umesimama kiasi gani,unaelewa
nini juu ya mpango wa Mungu. Unatakiwa kuzithamini ibada za
kanisa huku ukiiogopa dhambi.Amini juu ya uwepo wa Mungu ma
ana ukiamini utaona mafanikio makubwa.

c) Kiakili

Kujitambua kiakili ni hali ya mtu kuwa na uwezo wa kupambanua


mazingira yanayomzunguka na kufanya maamzi yaliyo sahihi
kutegemeana na jinsi alivyojifunza kutoka kwenye mazingira
alimokulia kuanzia alipokuwa tumboni mwa mama yake, wakati wa
uchanga/utoto na kuendelea hadi utu uzima.Kila mtu ana akili

4
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

isipokuwa aliyezaliwa na mtindio wa ubongo. Katika jambo hili kila


anayefikiria kuingia kwenye maisha ya ndoa au yule aliyeko kwenye
ndoa ana akili. Hata hivyo, ni vizuri kila mtu anayeingia kwenye
ndoa au aliyeko kwenye ndoa awe na uwezo wa kutambua ni mambo
gani anayafahamu na yale asiyoyafahmu ili aweze kujifunza kwani
elimu haina mwisho.

Kabla hujaamua kuingia au ukiwa kwenye ndoa unatakiwa kuielewa


vizuri akili yako kwamba inaweza na haiwezi kufanya mambo gani
kwa kuwa hapa ndipo utofauti na mipango ya Mungu kwa kila
mmoja wetu inapoonekana. Ukishindwa kuielewa akili yako
utawasumbua watu maana hata utakapoambiwa kwamba jambo hili
liko juu ya uwezo wako hautakubali utataka makubwa wakati akili
yako kwa muda huo inaweza madogo na kwa kuwa hujaijua
utailazimisha. Kwa hiyo kabla ya kuamua kuingia kwenye ndoa au
hata kama ulikwisha kuingia basi jipe muda kuitambua akili yako
kwamba inaweza nini na haiwezi nini.

Baada ya mwanadamu wa kwanza kuanguka dhambini moja ya tokeo


kubwa lililotokea na ambalo linatukabiri sote ni ile hali ya kupoteza
uelewa wetu wa asili na uwezo wetu katika kutambua mambo
likiwamo kusudi la Mungu kwetu. Lakini ukweli wenyewe hakuna
kitu cha maana maishani kama kule kujua kwanini ulizaliwa,
kwanini upo duniani mpaka sasa wakati wengine wanakufa kila siku
na ni nini lililo kusudi la Mungu kwako. Ni muhimu kulijua hili bila
kujali wewe ni mdogo au mkubwa kiasi gani. Usiseme umri wangu
umeenda itanisaidia nini kujua kusudi la Mungu kwangu na sababu
ya kuwepo kwangu. Wakati wako unaweza kuwa umepita lakini kwa
imani unaweza ukapokea uwezo wa kutimiza kusudi lako katika
muda uliobaki. Mungu aliyekuleta duniani ni mwaminifu na analo

5
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

kusudi kwa ajili yako. Cha msingi pigana kulijua kusudi


uliloumbiwa.

Ni muhimu kulijua kusudi la Mungu kwako; kila mara jitahidi kujua


kwa nini ulizaliwa. Ni muhimu kujua sababu ya kuzaliwa kwako na
yaishi maisha yako ili kuitimiza sababu hiyo. Mipango, mikakati na
mawazo mazuri sio mbadala wa kusudi la Mungu kwako. Kusudi
hilo ndilo linalotoa picha katika ulimwengu wa roho juu ya mke au
mume wa namna gani anayekufaa, lakini kwa kuwa hujalijua kusudi
la kuumbwa kwako ni rahisi kuoa au kuolewa na yeyote mwisho wa
siku inakuwa ngumu sana kutimiza kusudi la maisha yako. Kumbuka
katika maisha ya ndoa ni mwanamke ndiye aliyeumbwa kwa ajili ya
mwanamume, kwahiyo mwanamume unahitaji msaada wa Mungu ili
kumpata yule aliyeumbwa kwa ajili yako, yule anayekuja kusaidia
kutimizwa kwa kusudi lako.

Hakikisha lile zuri ulionalo au unaloliwaza lisiwe zuri machoni pako


tu bali liwe ni lile ambalo Mungu alikuleta duniani kwa ajili yake
Isaya 55:8-9. Maana Mungu anathibitisha kuwa mawazo yake si
sawa na mawazo yetu wala njia zetu si njia zake. Kwa maana kama
vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zake zi juu
sana kuliko njia zetu, na mawazo yake kuliko mawazo yetu.
Ukiliangalia andiko hilo kwa makini unaweza kuona bayana kwamba
kuna wakati tunawaza tofauti na Mungu, tunapanga tofauti na vile
ambavyo Mungu amepanga. Kuna wakati njia zetu za kufanya vitu ni
tofauti na njia ambazo Mungu angetumia kulifanya jambo hilo.

Kama tunataka kuona kusudi la Mungu maishani mwetu likitimia


lazima tuanze kuwaza na kupanga kama Mungu, na kutumia njia na
mikakati ya ki-Mungu kukamilisha mambo maishani mwetu.
Mawazo ya Mungu yapo juu sana ya mawazo yetu na njia zake zipo
6
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

juu kuliko zetu. Mipango yake iko juu kuliko yetu na kadhalika
mikakati yake kuliko yetu Yeremia 29:11. Maana nayajua mawazo
ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si
ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.

Siri kubwa iliyofichika hapa ni kwamba Mungu kabla hajamweka


Yeremia kuwa nabii kwa mataifa alikuwa na kusudi aliloliweka
ambalo aliliona halitaweza kufanikiwa pasipo kumuumba Yeremia.
Hivyo basi tambua kwamba kabla Mungu hajakuleta duniani alianza
kuliumba kusudi lako ili uweze kuishi kwalo. Kwa kawaida mtu
kabla ya kuonekana katika ulimwengu wa mwili huanza
kuthibitishwa na kuonekana katika ulimwengu wa roho. Yaani wewe
kuishi kwako sio kwa sababu ya kitu kingine ila unaishi kutokana na
kusudi ambalo Mungu ameliweka ndani yako.

d) Kijamii

Kujitambua kijamii inajumuisha uwezo wa mtu kuishi maisha fulani


yanayokubalika kulingana na jamii inayomzunguka.Ni mhimu kuishi
maisha yanayotambulika kwa mjibu wa jamii husika kwa kuwa
tunategemea mwezi wa maisha atatokana na jamii.Masuala
yanayomtambulisha mtu kijamii ni pamoja na lugha yake ya asili,
kabila lake, utaifa wake, elimu yake, mila na desturi, chakula kikuu,
mavazi, n.k. Ni vizuri kumfahamu vizuri kijana unayemtazamia
kwamba awe mwenza wako wa maisha kwa kuwa kushindwa
kumfahamu mtu huyo vizuri kunaweza kutokeza matatizo na
migogoro baadaye.

e) Kiuchumi

Yapo mambo yanayoweza kumtambulisha mtu kiuchumi. Mfano wa


mambo hayo ni kama kazi anayofanya ili kujipatia kipato. Kazi
7
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

inaweza kuwa ya kuajiriwa au kujiajiri kupitia biashara, ufugaji, kazi


za ufundi, shughuli za kilimo, n.k. Mara nyingi kazi anayofanya mtu
iwe ya kujiajiri au kuajiriwa inategemeana na ujuzi au maarifa
aliyopata kabla.Hivyo ni vizuri kijana kabla hajafanya maamuzi ya
kuingia kwenye ndoa awe amejitambua kuwa yeye anafanya kazi
gani au ana uwezo wa kufanya kazi gani. Kumbuka kwamba duniani
hapa utu na thamani ya mtu hupimwa kwa kazi. Usitake kuingia
kwenye ndoa bila kujua ni namna gani utapata kipato chako halali
kwa ajili ya kuitunza familia maana baada ya kuungana na kuwa
mwili mmoja ni matumaini yetu kwamba mtaanza kuwa na watu
wengine nyuma yenu ambao watahitaji matunzo yenu kama wazazi.
Ni vizuri kujua unayetaka kuingia naye kwenye maisha ya ndoa
anafanya kazi gani ili kujipatia kipato na kujikwamua kiuchumi.

1.2 Kusudi la Ndoa/Maisha ya Ndoa

Yapo makusudi ya maisha ya ndoa kwa wanandoa wenyewe, kwa


Mungu, kwa kanisa na kwa jamii inayowazunguka. Kwa muhtasari
makusudi ya ndoa ni pamoja na kumkamilisha mwanaume,
kuondoa upweke, kukidhi tamaa ya mwili, kuendeleza uumbaji wa
Mungu, kumwabudu na kumsifu Mungu, kuboresha hali ya kijamii
na kiuchumi ya wanandoa kwa kuwa ni afadhari kuwa wawili
kuliko mmoja maana mmoja akianguka mwenzake anaweza
kumwinua.

1.2 Kuhusu kuumba


Ni kufanya kitu kutoka kwenye tupu au isiyotokana na kitu kingine.
Mungu alimwumba mwanamume na mwanamke kwa mfano wake
mwenyewe. Roho ya mwanamume na mwanamke ni ya aina moja na
hiyo ndio iliyoumbwa. Hakuna roho ya mwanamke au ya
8
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

mwanamume, roho ni roho, ni pumzi ya Mungu ambayo humpa


mwanadamu uhai Mithali 20:27. Kwahiyo mwanamume na
mwanamke walianza kuwepo wote katika ulimwengu wa roho kabla
hawajawa katika mwili, hakuna aliyemtangulia mwenzake. Na hapa
ndipo penye utata kidogo kwa kuwa wanaume hujidhani kuwa ni
bora kuliko wanawake jambo ambalo si sahihi hata kidogo kwa kuwa
wote walikuwepo hapo mwanzo.

Ukitaka kuthibitisha kwamba wote walikuwepo soma Mwanzo 1:26-


28 Ndipo Mungu akasema, “natufanye mtu kwa mfano wetu, kwa
sura yetu, wakatawale juu ya samaki wa baharini na ndege wa
angani, juu ya mifugo, juu ya dunia yote, na juu ya viumbe wote
watambaao juu ya nchi.’’Kwa hiyo Mungu alimwumba mtu kwa
mfano wake mwenyewe, kwa mfano wa Mungu alimwumba,
mwanaume na mwanamke aliwaumba. Mungu akawabariki na
akawaambia, “Zaeni mkaongezeke, mkaijaze dunia na kuitiisha.
Mkatawale samaki wa baharini, ndege wa angani na kila kiumbe hai
kiendacho juu ya ardhi.’’

Ukianza kusoma mistari hiyo hapo juu utagundua kwamba sentensi


ya kwanza iko katika umoja lakini kadri unavyoendelea maneno
yanageuka na kuwa katika wingi, unaona Mungu anasema
wakatawale na sio akatawale maana ilitazamiwa kwamba kwa kuwa
Mungu alianza kusema na tufanye mtu na sio watu angeendelea
kusema akatawala na sio wakatale. Lakini kwanini neno wakatawale
limekuja? Je liko hapo kimakosa au ndivyo Mungu alivyokusudia?
Ukweli ni kwamba katika ulimwengu wa roho wote wawili
mwanamke na mwanamume waliumbwa na kupewa mamlaka sawa
na huo ndio ugomvi mkubwa kwa kuwa wote waliambiwa kwenda
kutawala kila kilicho duniani. Changamoto inayokuja kwa kiumbe

9
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

mwanadamu ni kushindwa kutofautisha wakati na namna ya


kutawala huko.

Mungu alimfinyanga mtu mmoja kutoka mavumbini lakini


mwanamke alifinyangwa kutoka ndani ya mwanaume kwa ajili ya
mwanaume ndio maana hakuna mahali unapoona mwanamke baada
ya kutoka katika ubavu akipuliziwa pumzi ya uhai, ni kwa kuwa
pumzi hiyo alikuwa nayo tayari toka ilipopulizwa na Mungu katika
mtu wa kwanza 1Wakorintho 11:8-9. Swali linabaki kwanini
mwanamke atoke ubavuni mwa manamume? Maana yake ni kwamba
mwanamke aliletwa duniani kwa ajili ya mwanamume ingawa jambo
hili halimfanyi mwanamume kuwa bora kuliko mwanamke
isipokuwa linampa wajibu wa kuhakikisha aliyeletwa kwa ajili yake
anapata huduma na matunzo stahiki.

Kama mwanamke na mwanamume waliumbwa wote ilikuwaje


Mungu amwambie mwanamke kwamba tamaa yake itakuwa kwa
mwanamume? Hili ni tamko la aina gani? Baada ya mwanadamu
kuliasi kusudi la Mungu mambo yalianza kuharibika na kuingilia
mfumo wa utendaji wa taasisi ya ndoa. Kulaumiana na kujiona bora
kuliko mwingine kukaanza, haya yanathibitiswa na jibu la Admu
kwa Mungu alipoulizwa je umekula matunda ya ule mti
niliokukataza kwamba usile matunda yake? Badala ya kujibu ndio au
hapana yeye alijibu “yule mwanamke uliyenipa” ikimaanisha yeye
Adamu ni bora sana asingeweza kukosea katika yale aliyoelekezwa,
isipokuwa huyo mwanamke ndiye tatizo. Lakini ni huyu huyu
Adamu ambaye mapenzi yalipokuwa motomoto alisema “huyu ni
nyama katika nyama zangu na mifupa katika mifupa yangu”

Tunajifunza nini kutokana na majibu ya Adamu kwa Mungu?


Adamu anajaribu kulihamishia tatizo kwa mwenzake ili huyo
10
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

mwenzake aonekane ndiye mkosaji lakini yeye siyo mkosaji hata


kidogo. Hii ndio hali halisi ya ubinadamu, binadamu siku zote
hujiona mwema kuliko mwenzake, hujisikia mkamilifu kuliko
wengine na huamini katika akili na upeo wake kuliko wa mwenzake.
Mambo ya kujiona bora, asiyekuwa na mapungufu, kumwona
mwingine kuwa mkosaji, asiyejua na mengine yanayofanana na hayo
unapoingia kwenye ndoa unatakiwa kuwa umeshayafisha zamani
(natural death), ukikosea ukangia nayo kwenye ndoa jua utapata tabu
sana. Kwasababu badala ya kushughulikia jambo kwenye ndoa
katika hali ya ubinadamu utalishughilikia kama malaika na
binadamu.Ukiona katika maisha ya ndoa wanandoa hawako tayari
kuchukuliana mizigo, kila mmoja anataka kujibebea mzigo wake
mwenyewe, anajiona ni bora na asiyekuwa na makosa kuliko
mwenzake ndoa hiyo iko karibu na kukata roho.

Katika maisha ya ndoa tunachukuliana mizigo, hatujipendezi


wenyewe, hatujioni bora zaidi ya wenzetu bali tunawatanguliza
wenzetu. Kama mke na Mume kila mmoja akiingia kwenye ndoa na
andiko la mkatawale basi ndoa itakuwa ndoano, maana kila mmoja
atataka kutawala jambo ambalo haliwezekani kwenye maisha ya
ndoa kwa kuwa wanaoingia kwenye ndoa ni binadamu. Hakuna
asiyekuwa na mapungufu kila mmoja ana mapungufu yake ambayo
mwenzake ndiye aliyeletwa kwa ajili ya kuyaziba. Kama kwenye
ndoa wewe na mwenza wako mnaweza kufikia hatua ya kuwaza na
kuamua kama alivyofanya Adamu jua ndoa yenu iko hoi bini taabani.
Hata hivyo hamjachelewa, neema ya Mungu imefika mlangoni
kwenu ikiwataka mkae chini na kufikiri njia bora na sahihi ya
kwenda kwa ajili ya utukufu wake, yeye ndiye mwanzilishi wa ndoa
na shabaha yake haikuwa kama hivyo mnavyofanya leo; anawasihini
mbadilike.

11
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

SURA YA PILI

MAMBO YA KUJUA KABLA YA KUOA


AU KUOLEWA
Nikiwa katika kusoma Biblia nilikutana na mstari katika
1Wakorinto 7:8-9 unasema “Lakini nawaambia wale, wasiooa
bado na wajane, Ni heri wakae kama mimi nilivyo, lakini ikiwa
hawawezi kujizuia, na waoe, maana ni afadhali kuoa kuliko
kuwaka tamaa”.

Unajua baadhi ya malezi, madhehebu, wazazi, mila na desturi


vinachangia kwa kiwango kikubwa utaratibu wa wapi pa kuanzia ili
kumpata mke au mume. Kila kundi lina mfumo na utaratibu wake
ambao lingependa kuona vijana wake wanaufuata pale wanapotaka
kuoa na kuolewa. Pamoja na kwamba kila kundi katika makundi
tajwa hapo juu lingependa kuona vijana wao wakifuata utaratibu ule
waliouweka lakini si kila kundi linatilia maanani kuwafundisha
vijana wake mambo hayo, si vijana wengi wenye uelewa wa kutosha
kuhusu maamuzi haya makubwa. Wengi wao wameingia kwenye
ndoa kwa msukumo wa mwili na wakati mwingine kwa kuiga
marafiki zao mwisho wa siku wamejikuta wakilaumu kwa nini
nilimuoa au niliolewa na huyu.

Nikiwa katika shughuli zangu za kila siku nimekuwa nikikutana na


wanandoa ambao kama Biblia ingeweka kipengele kinachoruhusu
kuachana, kuoa au kuolewa na mtu mwingine, nakuhakikishia kuna
ambao wako kwenye ndoa wangekuwa wameshafanya hivyo na
wengine wasingekubali kuolewa au kuoa tena. Kama hujanielewa,
jaribu kupita mtaani kwenu ongea na walokole na hata wasiokuwa
walokole waulize hivi “Ikitolewa amri kwamba ndoa zote
12
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

zivunjwe na watu warudi ujanani na kuanza mchakato wa kuoa


na kuolewa upya ni wangapi wanaweza kuoa au kuolewa na
wenzi walionao sasa”? Majibu watakayokupatia ndio
yatakayokuthibitishia hiki ninachokuambia, bila shaka umeanza
kuelewa ni kitu gani ninachokimaanisha.

Siyo hilo tu lakini pia nimewahi kuwasikia baadhi ya wanandoa


wanasema“Ninaendelea kuishi hapa kwa sababu ya watoto”,
yaani watoto ambao walipatikana kwenye ndoa wamepata thamani
inayomfanya kuendelea na ndoa hiyo kuliko yule aliyeungana naye
na kuahidi kuishi naye hadi kifo. Matamshi ya namna hii ni kiashiria
kwamba pamoja na kuwaona wakiishi pamoja lakini uhai wa
ndoa hiyo ulikwisha kuondoka yaani ndoa hiyo ilishavunjika
isipokuwa wanaendelea kuishi pamoja kwa sababu ya hofu kwa jamii
na watu wanaowazunguka ikiwa ni pamoja na kuogopa kutengwa na
makanisa yao. Bahati mbaya kiwango cha wenye kauli za namna hii
kinaongezeka siku hadi siku. Wanandoa wengi wana vilio, haijalishi
jinsi zao, kuna mateso ya kila namna kwenye baadhi ya ndoa na hii
ni kutokana na msingi uliojengwa kabla ya ndoa hizo kuanzishwa
maana maandiko yanasema kama msingi ukiharibika mwenye haki
atafanya nini.

2.1 Siyo kila ndoa ni ya ki-Mungu

Ni vizuri kufahamu kwamba sio kila ndoa inayofungwa inakuwa ni


mpango wa Mungu, haijalishi ndoa hiyo imefungwa kanisani au la.
Pamoja na kwamba unaweza kuwa kwenye ndoa ambayo kiasili
haukuwa mpango wa Mungu, ukiisha kuingia jua umeingia, ukijaribu
kutoka humo hesabu kwamba unatenda dhambi soma Malaki 2:15-
16 Je, BWANA hakuwafanya wao kuwa mmoja? Katika mwili na
katika roho wao ni wa Mungu. Kwa nini wawe mmoja? Kwasababu
13
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

Mungu alikuwa akitafuta mzao mwenye kumcha Mungu. Kwa hiyo


jihadharini wenyewe katika roho zenu, mtu asivunje uaminifu kwa
mke wa ujana wake.“Ninachukia kuachana,’’asema BWANA,
Mungu wa Israeli, “pia nachukia mtu anayejivika jeuri kama vazi,’’
asema BWANA Mwenye Nguvu. Kwa hiyo jihadharini wenyewe
katika roho zenu, wala msije mkavunja uaminifu. Wakati Mungu
anawahimiza watu wake kuoana katika mapenzi yake shetani naye
anapambana kuhakikisha watu wanaoana katika hila. Kwasababu
anajua kwamba ndoa ikisimama vilivyo mahitaji mengine
yatajisawazisha. Asikudanganye mtu hakuna namna unavyoweza
kusimama kuomba, kuimba au kuhubiri kama ndoa yako haina
amani. Kama unaona kuna watu mambo yao ya kimaisha au huduma
yanasonga mbele kwa kasi jua ndoa zao zina amani ya kutosha.

Kila mara shetani anajaribu kuwavuruga wanandoa na kuwafanya


waishi maisha tofauti na yale ambayo Mungu aliwakusudia. Ni kwa
sababu hii ndio maana Paulo aliwaambia Wakorinto kwamba, “wale
wasiooa bado, Ni heri wakae kama mimi nilivyo, lakini ikiwa
hawawezi kujizuia, na waoe, maana ni afadhali kuoa kuliko kuwaka
tamaa”. Paulo aliona shida na maudhi yaliyokuwa kwenye ndoa
kutokana na migogoro aliyokuwa akikutana nayo. Fahamu kwamba
ni furaha kubwa kwenye ufalme wa giza mtu anapooa au kuolewa
kinyume cha mapenzi ya Mungu. Hii ni kwa sababu Shetani anajua
akifanikiwa kukushawishi ukaoa kinyume na mapenzi ya Mungu,
ameharibu hatima (destiny) yako na kile ambacho Mungu
alikukusudia.

2.2 Kuoa na kuolewa katika mapenzi ya Mungu

Kuoa au kuolewa katika mapenzi ya Mungu ni changamoto


inayowakabili vijana wa kizazi cha leo. Ni vizuri ukafahamu
14
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

unapofanya maamuzi ya kuoa au kuolewa, Shetani anaweza


kutumia nafasi hiyo kupenyeza mawazo yake ndani yako juu ya
nani anafaa zaidi kuwa mwenzi wako wa maisha. Lengo lake ni
kuhakikisha anakuunganisha na mtu ambaye anajua atakumaliza
kiroho. Haimaanishi atawazuia msiende kanisani, bali ni kuhakikisha
kile ambacho ungefanya kwa kuwa na mtu sahihi hakifanikiwi.
Kwahiyo kama kijana ni jukumu lako kuwa makini kufuatilia juu ya
kile unachotii ili kujua ni wazo la nani, Mungu au shetani?

2.3 Ni wajibu mkubwa

Ndani ya ndoa kuna wajibu mkubwa unaokusubiri kama baba au


mama. Ni ukweli usiopingika kwamba unapoamua kuingia kwenye
ndoa ni kukubali kwamba muda na uhuru wako utabanwa na mwenzi
wako. Huwezi kupanga au kutenda kama ulivyo kuwa ukitenda hapo
awali ulipokuwa peke yako, kwasababu sasa si mmoja bali wawili.
Maandiko yanasema usile nyama ikiwa kula nyama ni kwazo kwa
mwenzako,hivyo kama liko jambo ambalo unaona ukilitenda
litamfanya mwenzako akwazike basi achana na jambo hilo.

Usiingie kwenye ndoa na fikra za upande mmoja wala harakati. Ndoa


ni wito wa mapungufu na uvumilivu ambao ni lazima uwe tayari
kuchukuliana na mwenzi wako katika mapungufu yake. Kuna vitu
hamtaweza kufanana kwa sababu ya mapungufu yaliyopo kwa kila
mmoja, kabla ya kuamua kuingia kwenye ndoa unapaswa kutafakari
juu ya majukumu yanayokuja kwako, hekima na busara katika
kuzikabili changamoto za ndoa, kama vile kuzaa au kutokuzaa,
kutokujiweza katika masuala ya unyumba, matumizi ya fedha, tabia
za mwenzi wako n.k. Haya ni mambo ya msingi kuyaweka akilini
kabla ya kuamua kwamba unaingia kwenye ndoa au la. Kama majibu
kwenye maeneo yote yatakuwa ndiyo basi ingia.

15
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

2.4 Uhusiano na wazazi wako

Mwanzo 2:24, “Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na


mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili
moja”. Zaburi 45:10-11 anasema, “Sikia binti utazame utege sikio
lako. Uwasahau watu wako na nyumba ya baba yako na mfalme
atautamani uzuri wako, maana ndiye bwana wako naye
umsujudie.” Ukiingia kwenye ndoa, mtu wa kwanza kushirikiana
naye ni mke au mume wako na sio baba wala mama yako. Maana
yake mke wako na mama yako katika mkitadha huu wote wanabaki
kuwa wanawake wawili walioolewa na wanaume wawili tofauti
yaani baba yako na wewe. Na kwa kuwa wewe mwanaume ndiwe
unayeambatana na huyu mwanamke unapata wajibu wa kumlinda
dhidi ya maadui ambapo maadui namba moja ni ndugu zako
mwenyewe. Hawa ndio ambao wanadhani wana haki ya kuamua
chochote juu yake na ndio maana wako radhi kukupa habari za
mapungufu yake bila kutaja kwa namna yoyote mazuri yake.

Baadhi ya wazazi wasingependa kuona ukiwa mbali nao, wanataka


waendeleze maamuzi na utawala juu yako bila kujali umeshakuwa
kwenye ndoa, haiwezekani. Unapoamua kuolewa, wa kwanza sio
baba wala mama, wa kwanza ni mume wako baada ya Yesu. Na
mwanaume unapoamua kuoa wa kwanza katika maisha yako baada
ya Yesu ni Mke wako. Kuoa au kuolewa na kuendelea kutegemea
maelekezo na maamuzi toka wa wale ulioachana nao ni shida kubwa
inayohitaji dawa. Ni hatari sana mtu ameoa au ameolewa lakini
baada ya Yesu anayefuata ni mtu mwingine tofauti na mke au mume
hapo hatutegemei ndoa yenye furaha na amani.

16
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

Ili kujenga ndoa imara iliyokusudiwa na Mungu anayetakiwa kuwa


wa kwanza baada ya Yesu moyoni mwako ni mke au mume wako.
Ikiwa hujafikia maamuzi ya namna hii moyoni mwako bado
hujafikia utayari wa kuoa au kuolewa na ukijidanganya vinginevyo
lazima utaleta shida mbele ya safari.

2.5 Inakuunganisha na familia nyingine.


Unafahamu watu wengi wakioa au kuolewa wanafikiria mahusiano
yao wenyewe tu; ni hatari sana. Kwasababu unapooa unaingia
kwenye undugu na familia nyingine tofauti. Ndio maana unapotaka
kuoa au kuolewa sio suala la kumtazama kijana au kumtazama
msichana; Ni mhimu utazame hali ya familia yake ili ujue unaingia
kwenye familia ya namna gani. Unaweza ukaingia kwenye familia
ambayo ni wavivu, wachoyo, wasiomcha Mungu n.k nakuhakikishia
jasho litakutoka. Usijidanganye hata siku moja kwamba mkishakuwa
pamoja utamshawishi kubadirika, mwenye uwezo huo ni Mungu
pekee, usijidanganye wala kudanganyika.

2.6 Imani yako inaweza kubadilika

Wasomaji wa biblia wanafahamu juu ya mfalme Sulemani. Biblia


imeweka wazi juu ya hekima aliyokuwa amejaliwa na Mungu
ambayo ilipelekea wasichana toka sehemu mbalimbali duniani kuja
kuiona, walipoikuta hawakutaka kuondoka. Kosa kubwa la mfalme
huyu ni kwamba wale wasichana walikuja na miungu yao na
aliwakaribisha wao na miungu yao na kuwapa mahali pa kujenga
vibanda vya miungu yao 1Wafalme 11:4,“Maana ikawa, Sulemani
alipokuwa mzee, wake zake wakamgeuza moyo wake, afuate miungu

17
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

mingine, wala moyo wake haukuwa mkamilifu kwa BWANA Mungu


wake, kama moyo wa Daudi baba yake.”

Nimeona vijana wengi ambao kabla ya kuoa au kuolewa wanakuwa


moto kwenye wokovu lakini wanapoingia kwenye ndoa wanapoa
mpaka wanakuwa kama barafu. Ukiwauliza ni nini kimewafanya
wapoe kiroho kwa kiwango hicho, hawana majibu sahihi. Kuna
wengine wanafikiri ni kuolewa tu na mtu yoyote kwasababu anasema
Bwana asifiwe, ibilisi pia huwa anaweka watu kwake huko ndani ya
watu waliookoka.

2.7 Unawajibika zaidi

Kama hujawa mtu wa kuwajibika basi usiingie kwenye ndoa. Kuoa


au kuolewa kunakufanya uwajibike zaidi kwa mwenzako 1Timotheo
5:8. Huyo ambaye ameokoka, lakini hatunzi watu wa nyumbani
mwake hasa, ameikana imani, ni mbaya kuliko mtu ambaye
hajaokoka. Inaonyesha kuwa unaweza ukaingia kwenye ndoa,
ukakosa mbingu kwasababu umeshindwa kuwatunza watu wa
nyumbani mwako na kwa ajili hiyo unahesabika kuwa umeikana
imani Tito 2:3-5,“Vivyo hivyo na wazee wa kike wawe na mwenendo
wa utakatifu, wasiwe wasingiziaji na wenye kutumia mvinyo bali
wafundishao mema ili wawatie wanawake vijana akili, wawapende
waume zao, watoto wao, wenye kiasi, kuwa safi, kufanya kazi
nyumbani mwao, kuwa wema na kuwatii waume zao ili neno la
Mungu lisitukanwe”.

Kijana wa kiume kama hajaoa anakuwa hana wajibu,wakati


mwingine mambo yakimzidia akakosa sabuni ya kufulia nguo hana
shida, anaibadilisha na kuitundika mahali ipigwe upepo kidogo ili
angalau jasho lipungue na baada ya siku mbili anaivaa tena. Lakini

18
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

pia kwa kijana unaweza usikute jiko la kupikia kwasababu haoni


sababu ya kuwa nalo maana anaweza kuishi kwa kutumia ziara za
kushitukiza kwa ajili ya kupata chakula. Lakini ukiamua kuoa
haijalishi unafunga au hufungi, unanjaa au huna ni lazima chakula
kiwemo nyumbani mwako. Yaani hata kama haupo au huna hamu ya
kula siku hiyo wale walioko nyumbani mwako kula ni lazima. Kuoa
maana yake ni kuitangazia dunia kwamba umeamua kuwajibika na
unaweza kutunza familia.

Kama unataka kuolewa lazima ukubali kuwajibika la sivyo usiolewe


maana huwezi kuendelea kuishi maisha ya usichana wakati wewe ni
mke wa mtu. Ulimwengu wa wanando ni tofauti na ulimwengu wa
ujana. Hii ina maana kwamba unapoamua kuolewa marafiki zako wa
ujanani wanabadirika kwasababu unakuwa umeingia kwenye
ulimwengu mwingine wenye kanuni na taratibu tofauti na zile
ulizokuwa ukizitumia hapo awali, hivyo unawahitaji marafiki
wanaoendana na ulimwengu huo.Kosa kubwa ambalo baadhi ya
wanandoa wanalifanya ni kuingia kwenye ndoa lakini wanaendelea
kubaki katika ulimwengu wa maisha ya kabla ya kuolewa. Ndugu
duniani hapa matabaka yapo, ukishaamua kuhama kutoka ulimwengu
wa ujana na kuingia ulimwengu wa wanandoa jua umetoka tabaka
moja kuingia jingine na kila tabaka lina kanuni zake za kuishi.

Ukiingia kwenye ndoa kuna mabadiliko ya kitabia, kimwenendo na


kimtazamo ambayo ni lazima kuendana nayo. Kama ulizoea kuosha
vyombo vichache kwa kuwa ni vya kwako peke yako, sasa baada ya
kuolewa umekuta mume wako ana marafiki na ndugu wengine
ambao mara kwa mara huja kumtembelea, maana yake ni kwamba
vyombo vya kuosha vitaongezeka, na kama ulikuwa hujui kupika
aina fulani ya chakula sasa baada ya kuolewa unakuta aina ile ndio
pendeleo la mume wako hivyo unalazimika kuanza kukipika.Ni
19
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

mhimu sana kama binti kufikiri unadhani huo ni muda mwafaka wa


kuwa kwenye ndoa, maana kama hutaweza na ukajilazimisha kuingia
ili tu na wewe uonekane umeolewa kama rafiki zako waliotangulia
lazima Kristo atatukanwa kwa ajili yako.

2.8 Unaweza kubadilisha utumishi na wito wako

Unamkumbuka mtu mmoja aitwaye Samson mnadhiri wa Mungu,


alipomwoa Delila, utumishi wake ulibadirika Waamuzi 16:21. Huyu
alikuwa ni mtumishi wa Mungu kabisa, lakini hakujua kwamba yule
mwanamke aliyempenda na kusisitiza aruhusiwe kuishi naye alikuwa
ni “wakala” wa adui; baada ya kuingia ndani alitumia nafasi yake
kama mke kumbembeleza ili amweleze siri ya nguvu zake. Samsoni
alijitahidi kuficha lakini kutokana na ujuzi wa Delila katika
kubembeleza Samsoni alishindwa kujizuia mwisho akaeleza ukweli
kuhusu chanzo na asili ya nguvu zake.

Tunajifunza nini kutokana na kisa hiki? Kwamba mnapounganishwa


kwenye ndoa inatakiwa muwaze kusaidiana, mtu asitumie udhaifu
wa mwenzake kumuangusha, kumzamisha, asitumie makosa hayo
kumpeleka jehanamu. Inatakiwa ujitahidi kumpata mwenzi ambaye
ukiwa na udhaifu atakusaidia, ukiwa kwenye dhambi akuombee,
ukiwa unaelekea jehanamu akusaidie kwenda mbinguni. Zipo ndoa
ambazo wanandoa wamefikia hatua ya kutoaminiana kila mmoja
anazo siri ambazo hataki mwenzake azijue, kila mmoja anajitahidi
kumficha mwenzake, maana yake kuna eneo ambalo kila mmoja
asingetaka liingiliwe, ndio maana linafungwa na kisha anatembea na
ufunguo mfukoni.

20
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

2.9 Kuleta marafiki au maadui

Hesabu 12:1-2 kisha Miriamu na Haruni wakamnenea Musa kwa


sababu ya mwanamke Mkushi aliyemwoa; wakasema, Je ni kweli
Bwana amenena na Musa tu? Hakunena na sisi pia? Maana yake ni
kwamba ndoa ya Musa ilileta ugomvi kati yake na ndugu zake jambo
lililopelekea msafara kusimama kwa muda wa siku saba.Kosa hili la
Miriamu lilifanya kusanyiko la Mungu kusimama, unaweza kuona
namna hali ilivyo. Kilichowasumbua ni Musa kuoa mwanamke
Mkushi; alioa mahali ambapo hawakutarajia. Naamini Musa katika
kujieleza atakuwa aliwathibitishia namna Mungu alivyosema naye
juu ya kumuoa mwanamke yule, wale watu wakasema, “haiwezekani
Mungu anasema na Musa peke yake”. Ndoa hii ilisababisha ugomvi
kati ya Musa na dada yake, Mungu akampa adhabu dada mtu, kaka
mtu akapata shida, Israeli nzima ikapata shida Hesabu 12: 2b-10.
Maana yake ni kwamba usipokuwa makini ndoa yako inaweza kuwa
chanzo cha shida na mgawanyika kwenye familia.

Suala ninalozungumzia hapa sio familia au ndugu kukuchagulia


unayetakiwa kumwoa hapana ila ni kukupa kibali na wafurahi.
Unaweza ukajidanganya kwamba hawaelewi, hawajaokoka, nina
uhuru wa kujiamlia kwa hiyo hawahitaji kuelezwa. Ndio maana
unahitaji kuomba, kwasababu suala la kutaka kuleta msichana ndani
sio la kwako peke yako, linawahusu wazazi na ndugu zako kwa
sababu unawaingiza kwenye familia nyingine. Naamaanisha
kuwashirikisha ili waweze kujua nini kinaendelea, ni muhimu
kufiriki na kuomba sana maana jambo lenyewe ni la kifamilia maana
ni jambo linaloziunganisha koo mbili au zaidi.

2.10 Uko tayari kuoa au kuolewa?


21
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

Unadhani umefikia mahali ambapo hali yako ya ndani na nje


inakuruhusu kuoa au kuolewa? Ninazungumzia utayari wa kuoa au
kuolewa, sizungumzii miaka bali ninazungumzia hali yako ya ndani
maana kuoa au kuolewa ni zaidi ya umri. Nimeona mtu ana miaka
arobaini, lakini hali yake ya ndani haiko tayari kukaa na mwanamke
au mwanaume, mawazo yake na kufikiri kwake havionyeshi utayari
wa kuwajibika maana hawajibiki hata kwa mambo yake mwenyewe
anawezaje kuwajibika kwa mambo ya mtu mwingine. Ni muhimu
kujua kuwa ndoa ina milima na mabonde, kuna kupanda na kushuka
na kwamba kwenye ndoa ni mahali ambapo uhuru wako binafsi
unafungwa kidogo kwa ajili ya faida na manufaa ya mwenzako. Je!
uko tayari kupanda na kushuka milima iliyo katika ndoa? Je
unadhani ni wakati mwafaka kukubali uhuru wako kuminywa
kidogo kwa manufaa ya mwenzako? Je uko tayari ukiambiwa na
watu wako wa karibu juu ya madhaifu ya mke/mume na kuvumilia?
Au ndio ukisikia utatoka mbio na kuanzisha valangati?

Usisahau huyo unayekwenda kuishi naye sio malaika ni mwanadamu


ambaye ni kiumbe wa ajabu sana na hata Mungu mwenyewe anapata
taabu kumsimamia. Mwanadamu kila mara anatamani kuwa huru,
anatamani kutumikiwa, kuamrisha, kutawala na si rahisi sana
kukubali kuwa chini ya maelekezo fulani ambayo mwenyewe
hayapendi. Utakumbuka baada ya Mungu kukamilisha uumbaji wa
mwanadamu alisema tazama kila kitu ni chema na cha kupendeza
akastarehe na kupumzika. Sakata la mwanadamu lilipoanza Mungu
akasema ninaghairi kumuumba mwanadamu na kwasababu hiyo
nitamfutilia mbali Mwanzo 6:5-7 inasema BWANA akaona jinsi
ambavyo uovu wa mwanadamu umekuwa mkubwa duniani na ya
kuwa kila mwelekeo wa mawazo ya moyo wake wakati wote
ulikuwa mbaya tu. BWANA akasikitika kwamba alimwumba
mwanadamu duniani, moyo wa Mungu ukajaa masikitiko. Kwahiyo
22
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

BWANA akasema, “Nitamfutilia mbali mwanadamu niyemwumba


kutoka kwenye uso wa dunia, wanadamu na wanyama, pamoja na
viumbe vitambaavyo na ndege wa angani. Kwa maana nasikitika
kwa kuwaumba.’’Ni muhimu kujiaminisha na kukubali kwamba
katika hali yoyote nitasimama na huyu mpaka mwisho.

Mwingine wazazi wake wanamtegemea kwa kila kitu, kwahiyo kabla


hujafikiria kuoa au kuolewa fikiria hilo. Maana baada ya kuoa au
kuolewa wa kwanza kwenye maamuzi na huduma ni mke au mume
wako. Haimaanishi ukioa au kuolewa usiwasaidie wazazi hapana
isipokuwa huwezi kuwasaidia moja kwa moja kama ulivyokuwa
unafanya zamani. Mfumo wa namna ya kufanya jambo hilo
unabadirika itakulazimu ujadiliane na mwenzako kwanza. Wakati
mwingine inawezekana umeoa au umeolewa na mtu ambaye hana
mzigo na wazazi wake, kila mtu anaishi kivyake kama simba porini,
suala la kusaidia wazazi halimo ndani yake lakini wewe umekuwa na
mzigo huo na umekuwa unawatunza hatua kwa hatua, fikiria
litakuumiza kiasi gani. Utafika wakati utakuwa unachukua vitu
kisirisiri unapeleka kwa wazazi, kufanya hivyo ni dhambi.

2.11 Uko tayari kuolewa na nani?


Wengine hawana muda wa kufikiria mambo kama haya, ukiwauliza
uko tayari kuolewa na nani, anasema na mtu aliyeokoka. Bwana
anawajua walio wake, hakuna mtu kwa jinsi ya nje atakayemjua
aliyeokoka kitabia. Wengi wanasema wameokoka ingawa matendo
na tabia zao ni sawa na ambao hawajaokoka, wengine wanasema
‘bwana asifiwe’ lakini siyo Bwana Yesu. Wengine wanasema nataka
kuolewa na mtumishi bila kuhesabu gharama za huo utumishi, ni
muhimu kuhesabu gharama kwanza, usijaribu kufananisha ndoa yako
na ya mtu mwingine, hujui ilikotoka, tamani ndoa yako na sio ya mtu
mwingine maana mapito yake huyajui. Unasema unataka mtumishi,
23
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

watumishi wako wengi, sema unataka mtumishi wa namna gani?


Unasema ninataka mhubiri, nabii ni mhubiri, mwinjilisti ni muhubiri,
mwalimu anahubiri lakini kitabia hawafanani.

Kama unataka mtumishi, ni muhimu useme unataka mtumishi wa


aina gani. Kwa mfano ukisema nataka mwinjilisti, lazima uwe
umejiridhisha kwamba una neema ya kukaa na mwinjilisti. Si unajua
mwinjilisti hakai nyumbani, anazungukazunguka huku na kule na
akikosa watu wa kuwachapa injili huko nje anakuja kuchapa injili
nyumbani hata kama mmeokoka. Na ujue hawezi kumaliza ibada
mpaka awepo mtu wa kutubu kama hajatubu ataendelea. Kama
hauko tayari kuchukuliana na mtu wa namna hiyo unadhani nini
kitatokea.

Kama unataka kuolewa na nabii jipange, kwasababu nabii huwa


hajui kuongea na watu, muda mwingi yuko kimya, manabii mara
nyingi wanafungwa midomo sio wasemaji. Wakati mwingine
unatamani mngeomba pamoja, lakini Mungu anataka awe peke yake,
soma biblia utaona maisha yao yalivyo; kila kitu kinachomzunguka,
kila anachovaa, anachokutana nacho, Mungu anaweza kukigeuza
kuwa ujumbe. Kwahiyo usishangae akakutazama na akaishia kupata
mahubiri toka kwako, halafu mkirudi nyumbani mnaanza
kugombana; kwani wewe hukujua kama ni nabii na anaweza kupata
ujumbe unaosema “Kama vile mke wako alivyovaa, ndivyo na kanisa
langu lilivyo asema, Bwana”

Mungu wetu ni fundi sana anampa kila mtu sawa na kusudi la


kuumbwa kwake; mfano kuna baadhi ya wanaume hawana ndevu
jambo linalowafanya wajisikie vibaya kwa kufikiri mwanaume ni
kuwa na ndevu. Lakini ukweli ni kwamba wanaume wengine
wametengenezwa bila ndevu ili kuwahudumia wanawake wasiotaka
24
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

wenye ndevu. Na hali kadharika hata wanawake wameumbwa kwa


namna tofauti ili kukidhi haja za wanaume. Chakushangaza unakuta
kijana anamwoa msichana mwenye rangi nyeusi akiwa anamwona
lakini baada ya kumfikisha ndani anataka awe na rangi nyeupe,
unajiuliza huyu wakati anamwoa hakumwona? Hiyo ni sawa na
kumwambia Mungu alikupatia usichokitaka, kwamba niliyekuwa
namtaka ni mweupe, haiwezekani! Mungu alipomuumba huyo
alimtazama na weusi wake aliona kila kitu ni chema kwake.

Mwili ni kama nyumba, kuna wengine hawawezi kupendeza mpaka


wapake rangi fulani kwenye miili yao. Nimeona kijana anampenda
msichana anayeweka rangi kwenye midomo na kucha zake, anachora
kwenye nyusi kidogo, lakini baada ya kumwoa anapiga marufuku
hilo. Wakati unamfuatilia hukuliona, leo umemfikisha ndani
unamwambia sitaki rangi, hapo ni kumwonea, maana ulimkuta
nazo.Kama ulikuwa humtaki akiwa amejinakshi na rangi hukutakiwa
kumfuatilia, maana wako wengine wakimwona anayejipaka rangi
mioyo inawachomoka.Nataka nikusaidie kupunguza ugomvi ndani
ya ndoa yako; maana vitu ambavyo Mungu amepanga mfanye
pamoja ni vikubwa kuliko mnavyofikiri, hamhitaji kutumia muda
mwingi kushindania vitu vidogovidogo ambavyo mlitakiwa
kuvijadili kabla ya kuoana. Mna mambo muhimu ya kufanya kiasi
kwamba kuanza kushindana na kubishana juu ya vitu hivyo ni
kutokuelewa utaratibu wa Mungu ulivyo juu ya kumpata mwenzi wa
maisha.

2.12 Muda gani ambao ungetaka kuoa au kuolewa


Biblia inasema katika Mhubiri 3:1 “Kwa kila jambo kuna majira
yake chini ya mbingu”; Mungu anapokuacha uzaliwe ujue
ameshatembea na wewe katika maisha yako, amesharatibu mambo
yako hatua kwa hatua; anajua kitu gani utafanya, maisha yako
25
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

yatakuwaje n.k. Akifika mwisho wa maisha yako anarudi mwanzo


kisha anatangaza mwisho tangu mwanzo; kwa hiyo kuanzia hapo
unapozaliwa jua maisha yako yamesharatibiwa. Ni vizuri uufahamu
huu mstari maana unakujengea msingi mzuri wa maisha Isaya 46:9-
10

Mungu anapokuletea mawazo ya kuoa au kuolewa, ni kwa ajili ya


kuimarisha maisha na makusudi yako hapa duniani. Anakuletea mtu
atakayekusaidia.Wengine wanatamani kuoa au kuolewa siyo kwa
sababu mpango wa Mungu umefika; ila ni kwasababu wanaona muda
wao wa kuoa au kuolewa umefika, wengine wanaona umri
umesogea. Mpango wa Mungu juu ya maisha yako haubadilishwi na
jinsi wewe, ndugu au rafiki zako mnavyohesabu miaka.

2.13 Uko tayari kuzaa, kutunza na kulea watoto wangapi


Niliwahi kuwauliza vijana ambao walikuwa wameoana muda si
mrefu, lengo la kuwauliza nilitaka kufahamu kama kweli walikuwa
wamejadili mstakabali wa maisha yao baada ya kuungana na kuwa
mke na mume, niliwauliza mna mpango wa kuzaa watoto wangapi
kama Mungu akiwajalia uzao? Walinijibu Mungu anajua.
Nikawauliza ninyi je! Wakajibu “hatujui maana kuzaa ni mpango wa
Mungu”.Tunajifunza nini kutokana na majibizano haya? Ukitazama
kwa makini utagundua kwamba wengi wanaingia kwenye ndoa bila
kupata wakati mzuri wa kujadili vitu hivi mhimu katika maisha ya
ndoa na hayo ndiyo makosa ya wengi walioko kwenye ndoa. Kabla
ya kuungana hawajipi muda wa kujadili juu ya idadi ya watoto na
jinsi zao. Wakishaingia vurugu zinaanza ona sasa unazaa zaa tu au
unanizalia watoto wa kike tu ndio nini sasa? Kwa taarifa yako
nakutangazia kwamba hakuna mtoto anayezaliwa kwa bahati mbaya,
lazima wanaozaa wajue kwamba sasa mtoto anatakiwa kuzaliwa.

26
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

Mimi na mke wangu kabla hatujaoana tulipata wakati tukajadili idadi


na jinsi ya watoto ambao tunapenda Mungu atujalie kuwapata
tutakapoingia kwenye ndoa, tulijadili pia muda (interval) ili
ituwezeshe kujipanga na kukusanya nguvu za kuwahudumia kwa
mahitaji ya msingi.Ashukuliwe Mungu ametupatia kile
tulichokihitaji kabla ya ndoa yetu. Mungu ana utaratibu wa uzazi
kwa kila ndoa anayoisimika. Nimeona watu wakishindana ndani ya
ndoa, mama anataka watoto wengi wamzunguke kama timu ya
mpira, baba hataki na ugomvi mkali unatokea.

Mwingine anamzalisha mke wake kila mwaka. Umewahi kufikiri


kila mwaka unazaa, mtu yuko kwenye ndoa miaka mitano, tayari ana
watoto wanne na bado anaendelea kuzaa. Nilikuwa mahali fulani
kwenye ibada nikamsikia mama mmoja akifurahia muujiza ambao
Mungu alikuwa amemtendea kwa kumponya, akasema, “Sasa
nitakuwa tayari kuzaa mtoto mwingine”, nikataka kujua wakati huo
alikuwa na watoto wangapi. Akasema, “wanne tuu” akiwa na maana
kwamba anatamani mtoto mwingine nikashangaa. Kadiri unavyozaa
watoto wengi ndivyo unavyokuwa na wajibu zaidi wa kulea. Watoto
hawafanani na huwezi kuwalea ki-ujumla jumla. Kila mtoto ameitwa
kivyake, ana mpango wake, ana njia yake na tabia yake na ana
namna yake ya kumtunza, hawafanani.

Kila mtoto anayezaliwa lazima umlee kwa uangalifu sio unajikuta


hujamfikisha mahali fulani katika kumlea tayari umezaa mwingine;
unafikiri mchezo. Hao watoto wawili hujawafikisha mahali tayari
umezaa mwingine, ni kitu kigumu hujawahi kuona. Maana yake
mtoto wa kwanza hatapata umuhimu na nafasi ya matunzo kama
inavyotakiwa kwasababu anakimbiliwa aliye mdogo; akija mwingine
anakimbiliwa aliye mdogo zaidi, hao waliotangulia wanajikuta wako
27
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

kivyaovyao.Watu wengi hushangaa kwanini watoto waliozaliwa kwa


kufuatana fuatana karibu wanagombana na kutoelewana. Sababu ni
huyu mkubwa kuona ameingiliwa na huyu mdogo, na huyu mdogo
kuona mkubwa ameshakuwa mkubwa, kwa hiyo mimi niliye mdogo
ndiye mwenye haki zaidi.

Msichana mmoja nilimuuliza, umemaliza darasa la ngapi, akasema


kidato cha sita, kwa nini huendelei na shule? Akasema, sithubutu
kumwambia baba anisomeshe zaidi maana ninawaangalia wadogo
zangu huku nyuma walivyo, ninaangalia na hali ya baba kifedha,
amenisaidia nimefika kidato cha sita sasa nikifikiria wadogo zangu
naona wacha na wao wasogee sogee angalau wafike sekondari kama
mimi. Huyu msichana amemaliza kidato cha sita anataka kuendelea
na masomo, lakini hawezi kuendelea kwasababu anaangalia hali ya
wazazi wake, anataka angalau na wadogo zake wasome, lakini sio
kwamba anafurahia kuishia kidato cha sita. Haya mambo
yanafikiriwa na kujadiliwa kabla ya ndoa, kuyaleta kwenye mjadala
ndani ya ndoa ni sawa na kupigana vita bila maandalizi.

Mwanamke aliumbwa kwa ajili ya mwanamume na siyo


mwanamume kwa ajili ya mwanamke. Hivyo mwanamume
anawajibika kujua ni mwanamke yupi katika wengi aliyeumbwa kwa
ajili yake. Maana katika hao wengi kuna walioumbwa kwa ajili ya
walimu, maaskari, madaktari, wafanyabiashara, wachungaji,
wahubiri, waimbaji, wacheza mpira, wanamitindo, wacheza mieleka,
waigizaji n.k. “Ni hatari sana kuoa mwanamke ambaye aliumbwa
kwa ajili ya askari, mcheza mieleka au mwanamitindo wakati wewe
ni mchungaji au mhubiri”

28
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

2.14 Maswali ya tafakuri

1. Kwa jinsi unavyoelewa unadhani Ndoa ni nini?


2. Je kuna wakati umewahi kufikiria kwanini kabla ya ndoa
kufungwa tunaulizwa, ”umekuja kufunga ndoa kwa hiari yako
mwenyewe bila kushurutishwa”?
3. Unakubali kuolewa/kumuoa huyu mwanamume/mwanamke na
kuishi naye maisha yako yote?
4. Je! utamtunza na kumpenda siku zote, katika shida na raha?
5. Na je! umewahi kufikiri nini kinaweza kutokea ikiwa mmoja wa
wafunga ndoa atajibu hapana?

29
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

SURA YA TATU

CHANZO/ASILI YA TABIA ZA WATU


Asili ni mwanzo wa mtu au kitu, tabia ya mtu aliyozaliwa nayo, kiini
cha jambo, kitu cha awali; kwahiyo mwonekano/kutenda au
kutotenda kwa mtu (mke au mume wako) ni matokeo ya:-
1. Malezi yake
2. Makuzi yake

Malezi; Ni matunzo anayopewa mtu kutoka kwa wazazi na ndugu


wa karibu kutoka kuzaliwa kwake mpaka anapokuwa mtu mzima.
Hapa ikumbukwe kwamba masikio ya watoto sio haya ya kawaida,
isipokuwa masikio ya watoto ni macho.Wataalam wa saikolojia
wanasema watoto hutendea kazi vile wanavyoviona kuliko vile
wanavyoambiwa. Kwahiyo kama maisha ya wazazi hayaeleweki
msitegemee watoto kutenda mema ati kwa kuwa mnawaelekeza au
kuwaambia. Kwahiyo ni vizuri katika kipindi hiki ambacho mna
watoto wadogo kuhakikisha matendo yenu kama wazazi yanaendana
na maneno na siyo ile ya fuata maneno yangu na siyo matendo. Kwa
uzoefu wangu ni ngumu sana mtu kucheza nje ya uwanja wa makuzi
na malezi, ni kwa neema ya Mungu tu mtu anaweza kujikwamua
katika uwanja huo.

Makuzi; yanajumuisha mazingira, matunzo, malezi, marafiki na


watu wa karibu. Matunzo ya mtoto yanasisitizwa sana katika kipindi
cha siku 1000 za kwanza yaani kutoka mimba kutungwa mpaka
mtoto anapoachishwa kunyonya. Hii ina maana kwamba katika
kipindi ambacho mama ni mjamzito apate matunzo na muda wa
kupumzika. Hali kadhalika mtoto anapozaliwa anyonye maziwa ya
mama pekee kwa kipindi cha miezi sita ya mwanzo; yaani katika
kipindi hicho mtoto asipewe kitu kingine isipokuwa maziwa ya
30
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

mama pekee kwani wataalam wanasisitiza kwamba maziwa ya mama


yana kila kitu kinachohitaji kwa makuzi ya mtoto.

Kupuuzwa kwa ushauri wa kitaalam juu ya namna ya kumhudumia


mama mjamzito pamoja na mtoto baada ya kuzaliwa kunapelekea
udumavu kwa watoto; na katika maisha yetu kuna watu waliokosa
matunzo wakiwa wadogo hali iliyopelekea ukuaji wao kuwa wa
mashaka na wengine kutokana na kukosa matunzo hayo walidumaa.

Udumavu ni nini hasa? Ni ile hali ya kimo cha mtoto kutoendana


na umri wake. Mtoto akikosa matunzo anayoyastahili katika kipindi
cha siku 1000 anadumaa, bahati mbaya sana udumavu huu
unarekebishika katika kipindi cha siku 1000 tu, tofauti na hapo hali
hiyo haitarekebishika kwa kipindi cha maisha yake yote. Hii ni
kusema kwamba hatima ya mtoto inajengwa katika kipindi cha siku
1000. Kama wazazi na walezi ni mhimu kutumia muda wetu mwingi
kujenga msingi huu mapema, tumwombe Mungu atupe uelewa wa
namna ya kufanya kwa ajili ya hatima ya watoto wetu katika kipindi
hiki.

Athari zinazotokana na udumavu hujidhihirisha ukubwani ambako


ndiko kuliko na majukumu makubwa likiwemo la ndoa. Mtoto
aliyedumaa hawezi kujifunza sawasawa na wenzake, uelewa wake
unakuwa chini ikilinganishwa na wanzake, yaani katika kila kitu
anakuwa wa mwisho au haelewi ingawa nia na hamu ya kuelewa
inakuwepo. Kwa maneno rahisi, uwezo wa ubongo wake kuelewa na
kutunza mambo hutengenezwa katika kipindi cha siku 1000 tofauti
na hapo mtu anaweza kuwa mkubwa lakini ubongo wake ukawa na
uwezo mdogo. Ni sawa na flash au memory card ambayo ukubwa
wake ni GB 2 hata kama ungefanyaje haiwezi kuongezeka na kuwa
na ukubwa wa GB 8.
31
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

Ukitaka kupima athari za udumavu kwa wanaokuzunguka ni rahisi,


jaribu kutazama maamuzi wanayoyafanya lakini pia watazame
baadhi ya watu wazima unaowafahamu na watazame wanapochangia
mada kwenye mikutano au vikao. Kuna wakati mtu anaelezea
kwenye mkusanyiko au kikao,lakini kila unapomsikiliza unashindwa
kuelewa anakoelekea,wakati mwingine kwenye kikao anatokea mtu
kuchangia mada lakini akianza anakuja na mada tofauti na iliyopo
mezani mpaka unashindwa kuelewa hivi huyu ndugu alikuwa hapa
au? Hata kwenye ngazi ya familia haijawahi kukutokea unaacha
maelekezo kwa watoto lakini unaporudi unakuta mtoto mmoja
katekeleza kitu tofauti na kile ulichoelekeza?

Kwa kuwa athari za udumavu hujitokeza ukubwani nakuambia


ikitokea katika kutafuta mke au mume ukaangukia mikononi mwa
yule ambaye matunzo yake katika kipindi cha siku 1000 yalikuwa ya
kusuasua na kupelekea kudumaa hataweza kuwa msaidizi au kichwa
kizuri kwenye ndoa yako. Mke au mume ambaye alidumaa anaishi
bila utaratibu, hajui nafasi yake na hawezi kusimama kwenye nafasi
hiyo. Anadhani anaweza kuwa kwenye kila nafasi, usishangae siku
moja unarudi ukakuta sahani zimehamishiwa chumbani, ukijaribu
kuuliza imekuwaje sahani ziko chumbani utaelezwa mlolongo wa
sababu mpaka utaamua kukaa chini. Na kama ni mwanamume
unashangaa anaondoka nyumbani bila kuacha hela ya matumizi
lakini anaporudi mchana anaulizia chakula wakati anajua fika
alipoondoka hakuacha fedha kwa ajili ya matumizi ya siku hiyo.

32
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

SURA YA NNE
KUCHAGUA MARAFIKI
Rafiki ni mtu unayemfahamu, unamwamini na unayempenda sana
katika maisha yako ambaye mara nyingi si mtu wa familia yako.
Wataalam wanasema; watu wawili hawezi kuwa marafiki isipokuwa
75% ya tabia na mwenendo wao vimefanana. Biblia inasema watu
wawili hawezi kutembea pamoja isipokuwa wamepatana Amos 3:3.

Kimsingi maisha ya watu hujengwa na au kubomolewa na marafiki.


Kuna watu wengi wamepotea njia, wameacha wokovu na hatimaye
kuharibikiwa kwasababu ya marafiki. Kwa hiyo kama mke au mume
wako ana marafiki wa aina fulani elewa kwamba kwa kiwango cha
75% anafanana nao na usisahau kwamba urafiki huchochea udhaifu
au uwezo ulio ndani ya mtu Mithali 27:17 na Mithali 13:20. Bahati
mbaya sana somo kuhusu marafiki halifundishwi sana makanisani
ndio maana hata walokole wamejikuta wakiwa na marafiki wasiofaa
na kupelekea vijana wanapofanya maandalizi kwa ajili ya kuoana
hawawezi kuyatazama malezi na makuzi ya wale wanaotarajiwa
kuwa wenzi wao wa ndoa.

Rafiki wa kweli hafuati umaarufu au pesa ulizonazo, anafuata tabia


uliyonayo. Marafiki wanaokutafuta kwasababu una kitu hao sio
marafiki ni wasaka tonge, wanakufuata kwa kuwa una kitu, siku
ukiishiwa hutawaona. Lakini marafiki unaokuwa nao wakati wa
shida na raha ndio marafiki ambao malengo, tabia, fikra na usemi
wenu vinafanana. Hao ndio marafiki zako wa kweli; siku ukiwa na
shida, huna hela au umefilisika watabaki kuwa rafiki zako; hao ndio
marafiki wa kweli.Kitu cha msingi unachotakiwa kuwa nacho akilini

33
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

ni kwamba kuna wakati rafiki zako wanaweza kugeuka kuwa


maadui.

4.1 Mambo ya kuzingatia


Kuna watu wana uchungu mioyoni, miili yao ina makovu na wengine
wamepata ulemavu wa maisha, ukiwasikiliza kwa makini utagundua
kuwa ni wale waliokuwa rafiki zao ndio waliowatendea
hayo.Marafiki ni wazuri kama ukimpata rafiki sahihi lakini ukimpata
asiyefaa maisha yako yanakuwa mashakani maana wakati wote
atakuwa akikushawishi kutenda mabaya. Kuna mtu anaweza kuwa
rafiki yako hata watu wakiwaangalia wanaona kama ni ndugu na si
watu wengine tu lakini hata wewe unaweza kuhisi hali hiyo ya
urafiki ambao ni kama undugu.

Hivi unajua kwamba maadui wengi wa leo kabla hawajawa maadui


walikuwa marafiki. Wahanga wakubwa wa marafiki kugeuka kuwa
maadui ni wanawake, kwasababu wanawake huwa radhi kufungua
mioyo yao kwa haraka zaidi kuliko wanaume.Na kwa kadiri
wanavyofungua mioyo yao haraka ndivyo wanavyopata maumivu
haraka. Ni muhimu kabla ya kufungua moyo na kuamua kuwa na
rafiki ujiulize, Je anaamini kile unachokiamini; anaelewa nini kuhusu
ndoa, anaelewa nini kuhusu mafanikio ya kiroho na kimwili;
mwenyewe anajionaje na anawaonaje wengine;anakuonaje, ni makini
kiasi gani linapokuja jambo linalokuhusu;unaweza kumuonya
akaelewa bila kukasirika n.k

Baada ya kujiridhisha, sikiliza moyo wako unakuambia nini, ukiona


unapata amani juu ya unayetaka awe rafiki yako basi endelea
atakuwa ni rafiki mzuri, lakini kama kuna mahali moyo unasita na
34
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

kupata shaka jipe muda wa kumchunguza wala usijidanganye


kwamba urafiki wenu utambadilisha au mtakuwa marafiki katika
yale mnayokubaliana tu lakini katika yale msiyokubaliana
mtagawana njia, ukiingia kwenye mtego huo nakuhakikishia utajua.

Katika kujenga msingi wa urafiki wenu jitahidi kuhakikisha


humwambii kila kitu kinachokuhusu maana anaweza kuzitumia
taarifa hizo kukudhuru. Changamoto ambayo baadaye hugeuka kuwa
mwimba kwa marafiki wengi ni kule kuaminiana kupita kiasi
ambapo hakuna mnachomfichana, siku mmoja akikengeuka siri zile
mlizoelezana zinageuka kuwa mwimba na uchungu kwako. Kitu cha
msingi na mhimu mheshimu na kumpenda kama rafiki, mpongeze
anapofanya vizuri, msaidie na mfundishe pale asipojua. Kama rafiki
hakikisha unampa pole na kumtia moyo anapopitia magumu, jiweke
kwenye nafasi kwamba shida yake ni yako na inapotokea
mmeshindwa kuelewena katika jambo fulani basi kaeni chini
mzunguze. Lakini kamwe usidhani yeye ni moyo wako wa kutunza
kila kitu, weka mipaka na kanuni za yapi anaambiwa na yapi
yatabaki kuwa yako na Mungu wako. Ukiamua kueleza kila kitu
kwake jiandae kuumia muda si mrefu na kwa kiwango kile
ulichoufungua moyo wako ndicho hicho kitakachotumika
kukuumiza.

Kama mtu anataka kubaini ulivyo ndani atawangalia rafiki zako;


kutokana na aina yao hata kama unasema, “Bwana asifiwe”, hata
kama unapiga pambio mpaka jasho linatoka haijalishi, kama marafiki
zako ni wabaya kuliko watu wa dunia bado wanaokutazama watahisi
mapungufu kwako na wataona unahitaji msaada. Kitu pekee
kitakachofanya watu wawe na mashaka juu yako ni maswali
yasiyojibika watakayokuwa nayo hivi ndugu huyu akiwa na wale
marafiki zake wanaongea nini? Kutokana na mazoea uliyonayo na
35
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

marafiki zako hata ukiambiwa jambo baya kuwahusu inakuwa


vigumu kuamini na kuliona kama linavyosemwa, ni muhimu kuwa
mwangalifu na marafiki ulionao Zaburi 1:1

4.2 SIFA ZA RAFIKI BORA

Ni ukweli usiopingika kwamba kila rafiki uliyenaye katika maisha


anao mchango katika kukujenga au kukubomoa. Jambo hili lazima
ulipe uzito unaostahili, usidhani rafiki ni rafiki tu na kudhani wewe
utambadilisha kama ana tabia zisizofaa hata yeye anayo nafasi ya
kukubadilisha; waswahili wanasema, “Ndege wa rangi moja huruka
pamoja”, kwahiyo kabla ya kuamua yupi anafaa kuwa rafiki yako
jiulize mnafanana rangi? Mnaweza kuruka pamoja? Usijidanganye
hata siku moja kwa kudhani ukiwa na rafiki mbaya utaendelea kuwa
na msimamo uleule; ukweli ni kwamba kile unachokisikia, kukiona
na kukipata nafasi ndani yako kinafanyika sehemu ya maisha yako.
Mfano kama umezoea kukaa na rafiki ambaye anaweza kutamka
lolote bila kujali mkusanyiko wa watu hata wewe kidogokidogo
utavutwa na tabia hiyo. Kwahiyo tabia za rafiki uliyenae zina nafasi
ya kujengeka katika maisha yako, kwa mantiki hiyo kama unataka
kuwa mtu wa maana lazima uwe na rafiki wa maana pia kwa sababu
vile alivyo ndivyo atakavyotoa mchango wake kwako.

Wataalam katika masuala ya maendeleo wanasisitiza kwamba


ukitaka kufanikiwa katika maisha jitahidi kuwa na rafiki ambaye
anawaza mema (positive thinker) ili ukikata tamaa akutie moyo.
Hata katika kujifunza tunajifunza kwa wale waliofanikiwa ili
ituongezee mwendo. Fikiria rafiki yako kila muda mnapokutana
analalamikia jambo fulani au anamlalamikia mtu fulani kwamba
alisababisha yeye kuwa katika hali hiyo, utafanya nini ili wewe
usijikute ukimchukia mtu huyo? Ukweli hutakuwa na chaguo zaidi
36
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

ya kuungana na rafiki yako kumchukia anayetajwa hata kama kisa


chenyewe hukijui kwa hiyo ukitaka kujijenga katika maisha yako
chagua kuwa na rafiki mwenye sifa zifuatazo:-

4.2.1 Anamjua Mungu

Tambua kile alichonacho rafiki yako ndicho atachokupa maana


hawezi kukupatia kitu ambacho hana, ni vizuri maisha yake yenyewe
yaonyeshe na kushuhudia kweli ana hofu ya Mungu. Siyo kuwa na
rafiki ambaye kila jambo kwake ni sawa tu, analishabikia kila
kinachokuwa mbele ya macho yake, hajali linampendeza Mungu au
la! Yeye huendelea nalo kwa kuwa lina manufaa kwake. Tambua
kwamba asili yetu ni Mungu na kwamba siku moja tutarejea kwake
kwa ajili ya kutoa hesabu ya matendo yetu tuliyoyatenda tukiwa
duniani. Kumbuka kwenye ulimwengu wa biashara kuna msemo
usemao, “biashara ni asubuhi jioni mahesabu”, na hata katika
ulimwengu wa mwili tunatakiwa kuishi tukijua kwamba tunafanya
biashara na jioni inakuja ambapo tutatakiwa kutoa hesabu kwa
aliyetupatia uhai huu.

Pamoja na kwamba mambo ya dunia yanaonekana kupendeza na


kuvutia kwa macho lakini yasikufanye usahau kwamba yanapita, ni
ya muda kitambo angalia sana yasikutenge na Mungu. Hivyo rafiki
mzuri kwako ni yule anayekukumbusha ulikotoka, ulipo na
unakokwenda na kwamba huko uendako ni watu wana namna gani
wanaotakiwa kwenda. “Watu wawili hawawezi kwenda pamoja
isipokuwa wamepatana”. Hakikisha mwendo mnaotembea na rafiki
yako ni mwendo ulio na nuru ya Mungu ili mambo yenu yafanikiwe.
Ni maombi yangu kwako ndugu msomaji wangu kwamba Mungu
akufanyie neema neno hili likuingie na lifanyike baraka kwako.

37
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

4.2.2 Anayejiheshimu

Ni vizuri rafiki yako ajue maana ya heshima na ajiheshimu na


kuwaheshimu wengine bila kujali jinsi walivyo. Hapa sizungumzii
kupiga goti, sauti ya upole, hapana ni zaidi ya hayo; heshima ni
namna unavyowaelewa watu na utu wao. Anachokifanya ndicho
hicho anachokimaanisha hana utofauti wa kauli ya mdomo na moyo
wake. Thamani ya watu haijengwi na kipato, mwonekano au maneno
mazuri ambayo yanazungumzwa isipokuwa utu. Ni mtu ambaye
anawajali watu kama anavyomjali Mungu, kwasababu kumpenda
Mungu pasipo kuwapenda watu ni kazi bure Luka 2:52.

Hakikisha rafiki yako asiwe miongoni mwa wale wanaojitahidi


kuonyesha wanampenda Mungu ingawa matendo na maneno
vinapishana. Unaweza kumkuta mtu kila kipindi cha ibada hakosi,
anashiriki vizuri tu lakini yeye na jirani zake hawasalimiani na hata
hawawezi kuazimana vitu. Rafiki kama huyu sio rafiki wa
kushirikiana naye. Hata kama binadamu wote siyo wema kwa maana
kwamba kila mmoja anayo mapungufu yake, hakikisha rafiki yako ni
yule anayetenda wema na kuondoka zake bila kusubiri shukurani.
Hata kama watatokea wale wasiompenda na kumshuhudia uongo
bado litainuka kundi jingine litakaloshuhudia wema wake.
Katika dunia ni jambo la kawaida kumchukia binadamu mwenzako
halafu ukasema nampenda Mungu, kwasababu kiasili binadamu
tumeumbwa na wivu fulani wa kutaka kila kitu kizuri kiwe chako,
ndio maana ukiona mtu anayekubali mwenzake anamzidi katika
jambo fulani anakuwa amevuka kiwango na kwa mwelekeo wa
kawaida anakuwa ameanza hatua ya ukomavu (Maturity). Katika hali
ya kawaida hatutegemei uwapende wazazi halafu uwachukie watoto
wao kwa kuwa watoto ni sehemu ya wazazi Mathayo 5:43-48

38
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

4.2.3 Kielelezo safi

Kuwa kielelezo ni ile hali ya kuwa mfano bora katika jambo fulani
kiasi kwamba watu wanatamani kuwa kama wewe, unaelekeza njia
na watu wakiifuata wanafika bila kupotea. Rafiki mzuri mwenendo
wake unatakiwa kuwa na mwelekeo mzuri, sio lazima awe kiongozi
au mtu maarufu ndani ya jamii lakini anatakiwa kuwa mtu ambaye
anajua kwamba anaishi ndani ya jamii ambayo inahitaji kujifunza
kutoka kwake. Kuwa kielelezo ni kitu muhimu sana kwa kuwa
atakuachia mambo mazuri ambayo utayatumia katika maisha yako.
Japokuwa wapo watu wenye maadili mema katika jamii lakini bado
unamhitaji Mungu ili akuwezeshe kudumu katika kuwa kielelezo
maana katika dunia ya sasa unaweza kujikuta uko katikati ya jamii
iliyomomonyoka kimaadili wakabadilisha mfumo wako wa maisha
kwa ujumla wake. Hivyo rafiki uliyenaye hakikisha wakati wote
anaongea mambo ambayo yanajenga na yenye manufaa kwa jamii
inayo mzunguka, sio mtu aliyejaa majungu na visasi ndani yake.

4.2.4 Muwazi na mkweli

Watu wanaokuwa marafiki ni wale walioshibana ambao wakiwa


pamoja mioyo yao inaridhika kwahiyo ni lazima uhakikishe kwamba
rafiki yako ni yule ambaye anapokuwa na wewe moyo wake
unakuwa na nguvu ya kusonga mbele; awe muwazi kwako (hali ya
kweli itoke ndani yake) aseme na kutenda kana kwamba anajiambia
au anajitendea mwenyewe. Hii ni moja ya nguzo ya urafiki wenu na
kama mnapokijipima bado hali hii haijitokezi jueni urafiki wenu una
dosari. Kama una rafiki ambaye siyo muwazi urafiki wenu una dosari
kuwa makini naye na anza kujipanga maana lolote laweza
kutokea.Uwazi ni ishara kwamba mmeanza kuaminiana katika

39
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

urafiki wenu pasipo unafiki. Kwa kuwa ni mtihani kutambua ukweli


kuhusu mambo anayokwambia; usiwe mwepesi wa kuamini mpaka
pale moyo utakapojiridhisha.

4.2.5 Anayekubali kuonywa

Unapochagua rafiki ni vema kila mmoja mkajua ninyi ni binadamu


sio malaika na hata urafiki wenu ni kati ya binadamu na binadamu na
sio kati ya binadamu na malaika au malaika na malaika. Sifa kubwa
inayotengeneza ubinadamu ni “udhaifu na au mapungufu” ambapo
urafiki huja kwa ajili ya kujaziliza/kukamilisha. Kwasababu hiyo
urafiki huwa na maana ikiwa kila mtu ana uhuru wa kumuonya au
kumwelekeza mwezake kwa upendo naye kuwa tayari kusikiliza
kile anachoambiwa.Pamoja na hayo usiwe mwepesi kuchukua
maamuzi magumu kulingana na kitu au hali uliyoiona kwa rafiki
yako; jaribu kutulia na kutafakari kisha kupitia upendo wako kwake
unaweza kuibua kitu bora zaidi ambacho kitaufanya urafiki wenu
kuwa wa maana sana. Haimaanishi mkiwa marafiki kila wakati
mtakubaliana katika kila jambo, kuna wakati mnatofautiana kila
mmoja akiamini katika mlengo wake lakini namna mnavyomaliza
tofauti hizo ndio udhihirisho wa ubora wa urafiki na kumaanisha
kwenu.

Adui mkubwa wa urafiki ni mmoja kati yenu kujiona mwenye haki


au anayejua kuliko mwingine jambo ambalo siyo sahihi hata kidogo.
Hii ni kwasababu kuwa marafiki ndiko kunakowafanya
mnakamilishane katika kuleta maendeleo yenu.Msikilizane na
muonane kuwa wote mnahitajiana na kutegemeana kwa ajili ya
kufanikisha yaliyo mbele yenu. Hii ndio sehemu muhimu sana kwa
kuwa inaonyesha ni kwa kiasi gani mnakubaliana ili kutimiza
malengo yenu maana hatua hii isipofanyika kwa uangalifu inaweza

40
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

kuleta madhara makubwa. Hii hatua inakuwa na ugumu kama rafiki


yako hatambui misingi ya urafiki wenu na kuipa nafasi kwa ajili ya
kufikia mahali mlipokusudia. Mnapokuwa mkisaidiana jua kwamba
hakuna mtu ambaye alikuwa vizuri kwa asili yake bali wote
mnatengenezwa kuwa wazuri mnapokubali.

4.2.6 Mpenda maendeleo

Rafiki mzuri ni yule anayethamini maendeleo yako na hahuzunishwi


na kufanikiwa kwako, yaani anavyoonekana ukiwa naye ndivyo
alivyo hata usipokuwa naye. Wataalam wamethibitisha kwamba
maneno ya kweli kutoka kwa rafiki yako ni yale anayoyazungumza
bila wewe kuwepo, hivyo jitahidi kujua ukiwa haupo rafiki yako
huzungumza nini kukuhusu ikihusianishwa na maendeleo yako.
Shida kubwa inayoukabiri urafiki wetu ni ama kuongea mambo
tofauti na yale ambayo huyasema tukiwepo au kushindwa kufuatilia
nini marafiki zetu huongea wakati sisi hatupo.
Kama binadamu, kuna wakati tunapitia nyakati na vipindi vigumu,
kuna kipindi tunajikatia au tunakatishwa tamaa; wakati ukiwa katika
kipindi hicho unamwona mtu ambaye unajua fika hali hiyo anaielewa
lakini bado anaonekana kama haelewi kinachokukabili wala
mazingira unayopitia; huyo sio rafiki mzuri. Rafiki mzuri atapenda
kuona furaha yake panakuwa na furaha yako ili wote mfurahi
pamoja.

Hakuna urafiki mzuri kama kumwona mwenzako analia nawe ukalia


pamoja naye ili siku nawe utakapolia mlie wote. Ni mtu ambaye
anakufikiria katika mipango yake na anakuhusisha pale inapobidi. Ni
mtu anayejali kesho yako iwe katika hali iliyo njema na usahihi ili
kuleta ustawi bora wa yale magumu. Hali hii pia iwe ndani yako na

41
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

wala usitegemee kuiona kwa mwingine wakati wewe ndani kuna


ubinafsi.

Kujali matatizo, hisia na changamoto anazopitia rafiki yako ni ishara


ya kutambua udhati wa urafiki wenu na nafasi yako kwake, kwa
sababu ni kwa kiwango kilekile anavyokutambua ndivyo
atavyokuhusisha nje ya hapo hawezi kukuhusisha. Huwezi kujivuna
kwamba huyu ni rafiki mzuri kama hujaona namna anavyohusika na
maisha yako kujua unafanya nini na unamatarajio gani. Urafiki sio
suala la kula na kunywa pamoja, au kushirikiana mavazi bali ni
pamoja na namna mnavyofikiria kesho nzuri kwa pamoja. Japo
unatakiwa kuwaza vizuri kwa wote lakini rafiki lazima usimamie
kuhakikisha kwamba mnatembea pamoja ili kifike kipindi mtu
mmoja akipata na mwingine akikosa iwe haina shida kwa kuwa
unajua akipata yeye umepata wewe kama hamjafika hapo basi huo
sio urafiki wa kweli.
4.2.7 Anayetambua udhaifu wako
Rafiki wa kweli hatumii udhaifu wako kukufanya uwe mnyonge bali
husimama katika nafasi ya kukutegemeza ili uweze kuimarika na
uonekane wa maana.Unapoutambua udhaifu wa rafiki yako
chukuliana naye kwakuwa hata wewe ni dhaifu katika upande
mwingine, inabidi furaha ya rafiki yako liwe burudiko kwako si
vinginevyo. Kama mtu anaangalia udhaifu wako tu ili autumie isivyo
sawasawa jua kwamba mtu huyo hana shirika la kweli nawe maana
unahitaji kuona namna anavyoonyesha upendo wake kwako pamoja
na udhaifu ulionao.

4.2.8 Anayependa ushirikiano

Rafiki inabidi atambue thamani ya uwepo wako katika maisha yake


hata kama ingewezekana kuyaendesha peke yake kwa kuwa
42
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

anatamani mfanikiwe kwa pamoja. Pindi anapokusudia kufanya


shughuli yoyote atambue uwepo wako ili kuongeza nguvu na
kufanya shughuli hiyo kwa ufanisi zaidi. Hamshirikiani kwasababu
mnatakiwa mshirikiane tu, bali ni hali yenu ya ndani ndiyo
inayokuwa na uhitaji huo, utendaji wenu unatawaliwa na furaha.
Hana ubinafsi ndani yake bali anafanya yote kwa moyo wa kupenda
na huku akitambua kuwa wewe ndio yeye kwa hiyo kama nafsi yake
ilivyo ndivyo anavyoona fahari juu yako.

SURA YA TANO
MAANA YA NDOA KWA MUJIBU WA
SHERIA ZA NCHI
Hii ni sheria inayotoa miongozo kuhusu haki na wajibu wa
wanandoa kwa upande mmoja, malezi, haki na maslahi ya watoto
katika ndoa kwa upande mwingine. Kwa mujibu wa sheria ya ndoa,
ndoa ni muungano wa hiari kati ya mwanamume na mwanamke
unaokusudiwa kudumu kwa maisha yao yote. Sheria hii imeainisha
aina mbili za ndoa ambazo ni: Ndoa ya mke mmoja na Ndoa ya wake
wengi.

Ndio maana unapofunga ndoa unaulizwa, unataka kufunga ndoa ya


wake wangapi? Wakati mwingine kutokana na mazoea tunaamini
kwamba mpaka unakuja kanisani unajua ndoa yako ni ya mke mmoja
ndio maana huulizwi swali hilo badala yake linachukuliwa moja kwa

43
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

moja kwamba kuja kwako kanisani ni uthibitisho kwamba ndoa yako


ni ya mke mmoja. Siku moja litakapotolewa tangazo la ndoa
nakuomba utumie nafasi kidogo kulichunguza utagundua hiki
ninachokuambia.

5.1 Namna za kufunga ndoa kwa mujibu wa sheria za nchi


Sheria ya ndoa ya Tanzania ya mwaka 1971 inatambua namna tatu
za ufungaji wa ndoa ambazo ni:

1.Kidini:
Hii ni ndoa inayofungwa baina ya wanandoa wakristo, waislamu au
dini nyingine kwa taratibu za dini na madhehebu yao. Hii ina maana
kwamba ili ndoa ya aina hii itambuliwe ni lazima ifungwe kwa
majibu wa kanuni na taratibu za dhehebu husika. Mfungijishaji wa
ndoa hiyo lazima awe mwenye mamlaka ya kufungisha ndoa
anayetambulika kwa majibu wa sheria. Ndio maana wachungaji
wetu wanapofungisha ndoa wanasema kwa mamlaka niliyopewa na
Mungu na kwa mamlaka niliyopewa na Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ninakuuganisha wewe na wewe kuwa mke na mume tangu
sasa.

2.Kimila
Ndoa hii ni ile inayofungwa kwa kufuata mila na tamaduni za jamii
husika. Ifahamike wazi kuwa msichana kuishi kinyumba na mvulana
sio ndoa ya kimila. Ili ndoa itambulike kama ndoa ya kimila kuna
utaratibu ambao ni lazima ufuatwe. Kwenye kila jamii kuna wazee
waliotambuliwa na kupewa mamlaka ya kufungisha ndoa hizo.
Sheria inasema ili ndoa hiyo iweze kutambuliwa kwamba ilifungwa
kimila yule mfungisha ndoa hutakiwa kutoa taarifa juu ya kusudio la
44
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

kufunga ndoa hiyo kwa afisa tarafa ambapo atamwalika afisa tarafa
ili kuwepo siku ya tukio. Ndoa ya namna hii pia inaweza
kuandikishwa na kupewa cheti.

3.Kiserikali:
Ndoa hii hufungwa mbele ya afisa wa serikali mwenye mamlaka ya
kufungisha ndoa kwa kufuata taratibu zilizoainishwa na sheria ya
ndoa. Siyo kila afisa wa serikali anaweza au ana mamlaka ya
kufungisha ndoa ya aina hii, usije ukaamka asubuhi na kwenda ofisi
ya kata kwamba unakwenda kufunga ndoa. Ofisi yenye mamlaka ya
kufungisha ndoa za namna hii ni ofisi ya mkuu wa wilaya. Ndoa zote
hizi kisheria zinatakiwa kutangazwa kwa kipindi kisichopungua siku
21 ili kutoa nafasi kwa pingamizi kama lipo.

5.2 Dhana ya ndoa


Kisheria mwanamke na mwanamume walioishi pamoja kama mke na
mume kwa kipindi kisichopungua miaka miwili japokuwa
wanawezakuwa hawakufunga ndoa kwa namna yoyote kati ya
nilizozieleza hapo juu huchukuliwa kama mke na mume. Mara
nyingi hali hii hutokea pale ambapo mwanamke na mwanaume
wakiwa na akili timamu wanaamua kuishi pamoja kama mke na
mume chini ya dari moja wakipika na kupakua bila kufuata utaratibu
wowote kati ya uliotajwa hapo juu. Kwa kanisa letu la FPCT kufanya
hivyo ni dhambi ambayo inakufanya uwe nje (kutengwa) na ushirika
(Meza ya Bwana) ambapo kwa imani yetu ushirika ndilo tukio
linaloonyesha uhai wa mshirika na ushirika kati yake na Mungu.
Naomba ifahamike wazi kwamba dhambi inayopelekea mtu

45
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

kutengwa na ushirika wa kanisa siyo kuoa bali ni uzinzi na


uasherati.

Kwenye maisha ya kawaida watu wanaoishi kwa mfumo wa dhana


ya ndoa ni wengi ikilinganishwa na wale wanaoamua kufuata
utaratibu kabla ya kuishi pamoja. Na katika siku za hivi karibuni
kumekuwa na ongezeko la ukengeufu wa mioyo ya wanaume
kuitumia hii kama fimbo ya kuwaadhibia wanawake. Kwasababu
dhana hii inasimamam pale ambapo mmoja kati yao hakuwa na ndoa
iliyokuwa inaendelea alipoiingia katika mahusiano hayo. Kwahiyo ili
kuwa katika njia salama hasa kwa watoto wanaopatikana kwenye
ndoa ya namna hii inashauriwa kuhakikisha kwamba muungano huo
umerasimishwa kwa kufuata mojawapo ya taratibu zilizoelezwa hapo
juu licha ya kuwa mmekwishaanza kuishi pamoja.

5.3 Ndoa batili


Hii ni ile ndoa ambayo ni ubatili mtupu toka mwanzo na ubatili huo
unasababishwa na sababu ya wanandoa kuwa ndugu; mwanandoa
mmoja kuwa hana uwezo wa kuoa au kuolewa kwa kuwa na ndoa
nyingine inayoendelea au kwa kigezo cha kutotimiza umri,
mahakama au baraza limeamua ndoa isifungwe; mwanandoa
mmojawapo au wote hawakuwa huru au na hiari; wanandoa wote
hawapo siku ya tukio la ufungishaji wa ndoa na kama kuna
makubaliano ya ndoa kuwa ya muda maalumu. Ni vitu gani
vinavyofanya ndoa kuwa batili?

1. Maradhi ya zinaa

46
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

Kama wakati wa kufunga ndoa mmoja wa wafunga ndoa alikuwa na


maradhi ya zinaa na yule asiye na ugonjwa kama wakati wa kufunga
ndoa alikuwa hajui lolote anaweza kulalamika mahakamani na
ndoa ikavunjwa.

2. Kukataa kwa makusudi kutimiza ndoa


Kama baada ya kufunga ndoa mmoja wa wafunga ndoa atakataa
kuitimiliza ndoa anayekataliwa ana haki ya kuiomba mahakama
kuvunja ndoa hiyo.Maingiliano yanayotambulika kisheria ni yale
yanayofanyika siku ya ndoa na kuendelea na siyo kabla ya ndoa.
Kukataa kuitimiliza ndoa kunakuwa sababu ya kubatilisha ndoa
ikiwa mwenye kukataa hana sababu yoyote ya msingi na mwenye
kukataliwa ametumia kila mbinu kumshawishi aliyekataa lakini
ikashindikana kufanya tendo la ndoa.

3. Mimba ya mwanamume mwingine


Kama wakati wa kufunga ndoa mke atathibitika ana mimba aliyopata
kwa mwanamume mwingine, mume anaweza kuiomba mahakama
ivunje ndoa hiyo.Kama itathibitika kuwa mume alijua hivyo hali
wakati wa kufunga ndoa, lalamiko lake halitasikilizwa.

4. Wazimu au kifafa cha kipindi


Mmoja wa wafunga ndoa kama ana wazimu au kifafa cha kurudia
rudia na mwenzake alikuwa hajui hilo wakati wa kufunga ndoa,
atakuwa na haki ya kuiomba mahakama kuivunja ndoa hiyo.
Ieleweke kuwa ugonjwa ni lazima uwe unarudia rudia na siyo mtu
awe aliugua na kupona.

47
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

5. Kushindwa kutimiza ndoa


Kama mmoja wa wafunga ndoa atashindwa kuitimiliza ndoa basi
ndoa hiyo inaweza kubatilishwa. Kwa mwanamme kama anashindwa
kuitimiliza ndoa kwa sababu ya kukosa nguvu za kiume basi ana haki
ya kuiomba mahakama kuibatilisha ndoa. Ili kukosa nguvu za kiume
kuwe sababu ya kubatilisha ndoa ni lazima ithibitike kuwa hali hiyo
ilitokea kabla au wakati wa kufunga ndoa na siyo baada ya kufunga
ndoa wakati kitendo cha kuitimiliza ndoa kilishafanyika. Ili ndoa
iweze kubatilika ni lazima kukosa nguvu huko kuthibitishwe na
daktari kuwa hakuponi au kunapona lakini mwanamume hataki
matibabu.

Mwanamke anaweza kuwa na maumbile ambayo yanaweza kufanya


ndoa ishindwe kutimilizika.Ikithibitika hali hiyo lakini mwanamke
hataki tiba mwanamume anaweza kuomba mahakamani ndoa
kubatilishwa. Ili mahakama iweze kusikiliza shauri la kuomba
kubatilisha ndoa ni lazima shauri hilo lipelekwe haraka. Kama shauri
litakwenda mahakamani baada ya mwaka mmoja tangu tarehe ya
ndoa Mahakama haitalipokea. Pia ni lazima ithibitike kuwa
mlalamikaji alikuwa hajui kasoro hiyo wakati wa kufunga ndoa na
baada ya kuigundua hajawahi kuingiliana na mwenzie mwenye
kasoro hiyo.

Ndoa batili huvunjwa na mahakama pekee baada ya kupokea


malalamiko toka kwa mmoja wa wanandoa.Kama hakutakuwa na
malalamiko yatakayopelekwa mahakamani na anayedhurika na
kasoro hizo, ndoa hiyo itadumu ama labda mmoja afariki au kama
kuna talaka itatolewa na mahakama.

48
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

5.4 Ndoa batilifu


Hii ni ndoa ambayo kwa namna yeyote ile ilikuwa halali lakini ina
matatizo yanayoweza kumpelekea mwanadoa mmojawapo kuomba
ndoa ivunjwe. Sababu zinazoweza kuifanya ndoa iwe batilifu ni
pamoja na mwanandoa mmoja kutokuwa na uwezo wa kufanya tendo
la ndoa; mwanadoa mmoja ana kichaa au kifafa na mwanandoa
mmoja ana ugonjwa wa maambukizi; mwanandoa alipata mimba
kutoka kwa mtu mwingine tofauti na mwanamume aliyemuoa; tendo
la ndoa halifanyiki kwa kuwa mwanandoa mmojawapo amekataa
kufanya kwa makusudi; au mwanamke hajafikisha miaka 18
mahakama inaona kuna sababu nzuri na za kujitoshereza kuiweka
ndoa pembeni. Ikumbukwe kuwa ndoa batilifu kwa namna yeyote
ile ni ndoa halali mpaka mahakama itoe tamko la kuivunja.
Watoto wanaozaliwa ndani ya ndoa batilifu ni halali.

5.5 Sifa za wanandoa:-


1.Umri:
Umri wa chini wa kufunga ndoa kwa mujibu wa sheria zetu ni miaka
18 na iwapo itabidi kuoana kabla ya umri huo kwa msichana basi
itabidi apate idhini ya wazazi kama ametimiza miaka 15 na iwapo
ana miaka 14 itabidi apate idhini ya mahakama.Hata hivyo sheria
inaelekeza kama kutakuwa na ulazima wa kumwoa binti mwenye
miaka 14 basi mwanamume huyo aliyemwoa msichana huyo
hataruhusiwa kumwingilia kimwili mpaka hapo atakapotimiza miaka
18.Hata hivyo kuna wakati vipengele hivi vya sheria hutumika
vibaya na wazazi wakidhani ni katika kila hatua hutakiwa kutoa
idhini. Kutokana na kutungwa kwa sheria ya makosa ya kujamiiana
ya mwaka 1995 ndoa yoyote inayofungwa na wanandoa wenye umri

49
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

wa miaka chini ya 18 inakuwa batili na mwanaume huyo


atahesabiwa kuwa anabaka.

2.Hiari:
Lazima kila mmoja awe ameridhia kwa hiari yake bila hila kutumika
kupata hiari, kulaghaiwa au kulazimishwa na mtu yoyote. Hii ina
maana kwamba wanaofunga ndoa lazima wawe wamekubaliana wao
wenyewe, baada ya makubaliano ya watu hawa wanapokusudia
kufunga ndoa ndipo taratibu zingine zinazokubalika kwenye jamii na
kanisani zinafuata.

3.Jinsi:
Watu hao wanaokusudia kufunga ndoa lazima wawe watu wawili
wenye jinsi tofauti, mmoja awe mwenye jinsi ya kiume na mwingine
awe mwenye jinsi ya kike.Hii ina maana kwamba kwa sheria zetu
ndoa za watu wenye jinsi moja ni kosa na hazikubaliki

4.Wasiwe maharimu:
Maharimu ni watu wenye undugu wa karibu wa damu ambao
hawaruhusiwi kuoana. Kwa hiyo muungano huo usiwe wa watu
wenye undugu wa karibu ambao sheria imekataza watu wa uhusiano
huo kuoana. Watu wenye uhusiano wa kindugu waliokatazwa kuoana
wameelezwa katika kifungu cha 14. Kifungu hiki kinakataza mtu
kuolewa/kumuoa dada, kaka, baba, mama, babu, bibi, shangazi,
mjomba au mtoto aliyemuasili. Hao wanaokusudia kufunga ndoa
wanatakiwa wasiwe na undugu wa damu, kwa mujibu wa sheria zetu
watu wenye undugu wa damu hawaruhusiwi kuoana.

50
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

5.Pingamizi:
Kwa mujibu wa kifungu cha 18 sheria inatamka kwamba kabla ya
ndoa kufungwa ni lazima tangazo litolewe juu ya kusudio la kufunga
ndoa. Kifungu cha 26 kinatamka kwamba tangazo hilo liwe la siku
21 kabla ya ndoa kufungwa. Hata hivyo, kifungu cha 23 kinaruhusu
msajili wa ndoa kufungisha ndoa bila tangazo la siku 21 kama kuna
sababu za msingi. Lengo la tangazo ni kutoa nafasi kwa mtu mwenye
sababu ya kuzuia ndoa hiyo isifungwe kuweka pingamizi dhidi ya
ndoa hiyo kama inavyotakiwa katika kifungu cha 20(1). Kama
pingamizi limewekwa, basi mfungishaji ndoa hawezi kuifungisha
ndoa hiyo hadi pingamizi hilo litakapoondolewa.

Kifungu cha 20(2) kinampa nafasi mwanamke aliyeolewa katika


ndoa ya wake wengi kupinga mume wake kufunga ndoa na
mwanamke mwingine endapo huyo mke ana taarifa kwamba
mwanamke anayetaka kuolewa na mume wake ana maradhi ya
kuambukiza. Hata hivyo kwa kuwa UKIMWI ni ugonjwa ambao
umeingia karibuni haijajulikana kama pingamizi laweza kuwa
mwanamke anayetaka kuolewa ana virusi vya UKIMWI.

6.Mfungishaji kutokuwa na mamlaka


Kama wanaofunga ndoa wanajua wazi kuwa anayewafungisha ndoa
hana mamlaka hayo na kwa makusudi wakakubali awafungishe ndoa
basi ndoa hiyo itakuwa ni batili. Mfungishaji ndoa ili kuwa na
mamlaka anapaswa kusajiliwa na Msajili Mkuu wa Ndoa na kupewa
leseni ya kufungisha ndoa.

51
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

7.Kusiwe na ndoa nyingine inayoendelea:


Kama mmoja wa hao wanaotaka kufunga ndoa ana ndoa
inayoendelea na inatambulika kisheria haruhusiwi kufunga ndoa
nyingine.

8. Kutokuwepo kwa wafunga ndoa


Kama ndoa imefungwa bila ya wafunga ndoa kuwepo basi ndoa hiyo
haitambukuliki kisheria

9. Kudumu:
Wanakusudia kufunga ndoa wanathibitisha kwamba Muungano wao
unakusudiwa kudumu kwa muda wote yaani milele, hapatakuwa na
kuachana na kwamba kifo tu ndicho kitakachowatenganisha.

10. Mashahidi wa ndoa


Ili ndoa itambulike kisheria kwamba ni halali ni lazima ishuhudiwe
na mashahidi wasiopungua wawili ambao umri wao usipungue miaka
18 na wafahamu kinachosemwa na kutendeka wakati wa kufunga
ndoa. Wanaotaka kufunga ndoa wana wajibu wa kutoa taarifa ya nia
ya kufunga ndoa kwa mfungishaji ndoa siku 21 kabla ya siku ya
kufunga ndoa. Taarifa hiyo ionyeshe mambo yafuatayo:-
1. Majina kamili na umri wa wanaotaka kuoana.
2. Uthibitisho kwamba hakuna pingamizi dhidi ya ndoa
wanayotarajia kufunga.
3. Majina kamili ya wazazi wao na sehemu wanakoishi.
4. Hadhi ya wafunga ndoa.Yaani ifahamike kwamba mwanamke
hajaolewa, ametalakiwa au ni mjane,vivyo hivyo kwa mwanaume
pia.
52
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

5. Kama ndoa ni ya wake wengi au inatazamiwa kuwa ya wake


wengi. Pia katika fungu hili kama mtu anataka ndoa iwe ya mke
mmoja anapaswa kueleza. Baada ya taarifa yenye maelezo haya
kufikishwa kwa mfungishaji ndoa yeye anawajibika kutangaza nia
ya kufunga ndoa.
6. Matangazo haya hutolewa mahali ndoa inapotarajiwa kufungwa.
Kama ni ndoa ya Kiserikali tangazo litabandikwa nje ya ofisi ya
msajili wa ndoa ambaye ni Mkuu wa wilaya na kama ni ya kidini
tangazo litabandikwa kwenye nyumba ya ibada.

53
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

SURA YA SITA

MAANA NA MAKUSUDI YA NDOA YA


KIKRISTO
6.1 Ndoa ya kikiristo ni nini?
Ni muungano wa hiari kati ya mwanamume na mwanamke
uliowekwa wakfu na Mungu unaowaunganisha watu kiroho na
kimwili.Wanandoa wanatakiwa kujua kuwa Mungu ndiye
mwanzilishi wa ndoa na kwamba ndoa ya kikristo ni kielelezo cha
uhusiano kati ya Mungu na Kanisa Mwanzo 2:21-24. Wakati Mungu
anapanga alikusudia mahusiano ya ndoa yawe ya
kudumu maisha yote, kwahiyo mtazamo wa Mungu juu ya ndoa
hakuna kitu kinachoitwa kuachana au kutengana. Kujaribu
kukifikiria katika ndoa ya kikristo ni kufanya dhambi kabisa.

Kuna wakati wayahudi walimuuliza Bwana Yesu, swali lililolenga


kujua nini zilikuwa fikra zake kuhusu wayahudi kutoa talaka?
Ukifikiri kwa undani unaweza kugundua kwamba walitaka kujua
kama Yesu alifikiri ndoa iliyofutwa kutokana na talaka inakuwa
imefutwa mbele ya Mungu. Bwana Yesu aliwarejesha wauliza swali
kwenye ndoa ya kwanza kabisa ambayo iko katika kitabu cha
mwanzo sura ya pili na kuwakumbusha kuwa aliowaunganisha
Mungu mwanadamu asiwatenganishe Mathayo 19:6. Hapa Yesu
anaweka wazi kuwa Mungu anaichukulia ndoa kuwa ni kitu
kilichoshikamanishwa ambacho kujaribu kukitenganisha ni kufanya
uharibifu mkubwa kuwahi kutokea ndio maana alisisitiza kuwa kila
anayemwacha mkewe na kuoa mwingine, azini; naye amwoaye yule
aliyeachwa azini” Mathayo 19:9.

54
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

Ni mhimu kujua kuwa ndoa ndilo jambo linaloshikilia mambo mengi


katika jamii. Ni msingi wa jamii ya wanadamu na kwamba ukiharibu
ndoa unaharibu kanisa na jamii kwa ujumla. Vivyo hivyo kila mara
mwanamume akumbuke kwamba mwanamke alitoka ndani yake na
kwamba wanapooana humaanisha kuambatanishwa, kujaribu
kutenganisha ni kuleta madhara kwa walioambatana na jamii
nzima.Katika mpango wa Mungu ndoa ni msingi wa maisha ya jamii
yenye maadili mema ambayo husababisha uwepo wa jamii imara
yenye kupendana. Kupendana ni ile hali ya “kumkubali mtu
mwingine vile alivyo kwa dhati ya moyo wako na kukusudia
kumtendea iliyo haki mbele za Mungu na wanadamu.

Hii ina maana kwamba ndoa ya Kikristo inajengwa kwenye msingi


wa kupendana, kupendana huku sio kule kunakojengwa kwenye
vitu, mali au hali, ndio maana msisitizo unawekwa kwenye
kumwomba Mungu kabla ya kufanya maamuzi ya kufunga ndoa.
Maana ndoa ikifungwa unashikamanishwa na uliyempenda. Mungu
alipoanzisha ndoa alikusudia mwanamume kuwa na mke mmoja na
vivyo hivyo mwanamke kuwa na mume mmoja na hawa wawili
waishi hivyo maisha yao yote isipokuwa mmoja anapofariki. Ndio
maana Mungu huwachukia wale wanaoachana Malaki 2:16

6.2 Mambo muhimu juu ya ndoa ya Kikristo


1. Kuwaacha baba na mama
Kuwaacha ninakozungumza hapa sio kutoka na kwenda kuishi
sehemu tofauti, (ingawa kuishi sehemu nyingine ni bora zaidi) ila ni
kuwaacha wazazi kifikra na kujua kwamba mmekuwa taasisi kamili,
isiyoingiliwa, isiyoamriwa na yenye mamlaka kamili. Mnapoingia
kwenye ndoa mnaanza kufanya maamuzi, utendaji na utashi kwa
faida yenu na siyo faida wala utashi wa wazazi au ndugu wengine.
Mwanzo 2:24 na Zaburi 45:10 na 16. Baba, mama na ndugu
55
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

wengine kwenye familia wanakuwa wanufaika wa pili wa maamuzi


yenu, wanufaika wa kwanza ni ninyi pamoja na wale watakaotoka
viunoni mwenu.

2. Kuwa mwili mmoja


Mwanamume na mwanamke katika ndoa ya kikristo
wanaunganishwa pamoja kwa kila mmoja kukubali kwa hiari
kwamba atachukua na kutimiza wajibu wake kwa manufaa ya
mwenzake na kuahidi kumpenda zaidi ya yeyote. Ili kulitimiza hitaji
hili kila mmoja aache 50% ya yale anayoyapenda na 50% ya yale
asiyoyapenda ili kwamba muunganiko huu ubaki na 100%, kwa
sababu hatuna muunganiko wenye asilimia zaidi ya 100. Lakini
kama kila mmoja atataka kuingia na 100% ya vile anavyovipenda na
100% ya vile asivyovipenda, ndoa inakuwa mashakani maana ndoa
ni kusikilizana na kuachiana.

Asilimia zinazodondoshwa au kubakizwa huziamui wewe, mazingira


na utashi wa yule unayeungamanishwa naye ndivyo huamua. Uamuzi
huu hupatikana kupitia majadiliano, kila mmoja awe wazi
kumwambia mwenzake anapenda nini na hapendi nini, kile ambacho
mwenzako hakipendi lakini wewe unakipenda kichwa kuuma ili
uweze kukaa kwenye muunganiko huo kwa amani huna budi
kukiacha. Muda mzuri wa kuzungumza kipi kidondoke na kipi cha
kuingia nacho kwenye muunganiko ni kabla ya kuingia kwenye ndoa
na siyo baada ya kuingia. Mnapofikiria kuwa wachumba ndicho
kipindi sahihi cha kuelezana kipi unakipenda na kipi hukipendi.

Tunapata changamoto kwenye ndoa nyingi, wanapochumbiana


baadhi ya mambo huwa siri na wanajitahidi sana kuyaficha ili
yasijulikane maana yakijulikana ataachwa, wanasahu kwamba ni
56
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

bora kuachwa wakati wa uchumba kuliko magomvi yasiyoisha


kwenye ndoa. Kwenye biblia hakuna mahali palipoandikwa kwamba
Bwana anachukia wachumba kutengua uchumba bali anakuchukia
kuachana kwa walio na ndoa. Kwa hiyo ni muhimu sana kuziba ufa
kuliko kujenga ukuta maana gharama za kujenga ukuta ni kubwa
kuliko za kuzipa ufa.

Hao wawili wanakuwa siyo wawili tena bali mwili mmoja


unaotokana na kuunganishwa katika tendo la ndoa na upendo wa
kujitoa kwa moyo wa dhati. Ukiona wanandoa wamefikia hatua ya
kuweka masharti au ratiba kwenye tendo la ndoa kama umeme wa
mgao ujue ushirika huo uko mashakani. Au ukianza kusikia msemo
kama, “nipo hapa kwa ajili ya kulea wanangu”, jua hapo hapana
mwili mmoja kama ilivyokusudiwa, hawa watu walikwisha
kutengana siku nyingi ingawa kwa macho tunawaona wako pamoja.

Kimsingi tendo la ndoa ndicho kitu kinachowashikirikisha,


kuwakutanisha na kuwafanya wanandoa kuwa mwili mmoja, tendo
hili linatakiwa kufanyika kwa ustadi, heshima na mahali pasafi, ndio
maana maandiko yanasema ndoa na iheshimiwe na watu wote na
malazi yawe safi. Ni muhimu kujiandaa kwa ajili ya tendo hili, watu
wasirukiane na kukurupuka kama waoga nje, waanadane kwa umoja
na upendo ili iwawezeshe kufika kileleni pamoja. Kila mmoja
azungumze na mwenzake kwa lugha ya staha namna ambavyo
anapenda kufanyiwa ili ajisikie raha. Huu ndio wakati wa kuufurahia
uumbaji wa Mungu. Takwimu zinaonesha kwamba katika siku za
hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la kupungua kwa uwezo wa
wanaume kushiriki tendo la ndoa “upungufu wa nguvu za kiume”
na inathibitika wazi kwamba karibu 80% ya matatizo haya
yanatokana na sababu za kisaikolojia. Maneno anayoambiwa
mwanaume, msongo wa mawazo unaotokana na maisha magumu na
57
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

kukosekana kwa upendo (ukubalifu kutoka kwa mke) ndicho chanzo


kikuu cha matatizo.

Mara kadhaa kinamama bila kujua hasara zake hupenda


kuwalinganisha au kuwafananisha waume zao na watu wengine,
unaweza kusikia wakisema hivi na wewe wakiitwa wanaume
unaweza kusogea? Sijui wewe ni mwanaume wa namna gani? Najuta
kuolewa na wewe! Mbona baba fulani yeye anafanya hivi? Mbona
mama fulani mume wake kamfanyia hivi? Haya maneno ni madogo
sana, lakini kisaikolojia yana madhara makubwa katika ubongo wa
mwanaume kwa sababu yanazalisha maswali yasiyokuwa na majibu.
Na kwa kadiri kwanini zinavyoongezeka ndivyo uwezo wake wa
kushiriki tendo la ndoa unavyoshuka. Ni muhimu kinamama
kuchunga ndimi zenu, kamwe usithubutu kumlinganisha na au
kumfananisha mumeo na wengine.

Biblia inasema ndoa iheshimiwe na watu wote na malazi yawe safi.


Sababu nyingine inayoshusha au kupandisha morali kwenye tendo la
ndoa ni hali ya usafi aliyonayo mwanamke pamoja na mazingira ya
hapo tendo linapofanyikia. Mwanamume hawezi kufanya tendo la
ndoa kwa kiwango cha juu ukiwa mchafu, kitanda kichafu na kila
kitu kiko hovyo. Inabidi kila mahali kuwe safi, hata mpira huchezwa
vizuri kwenye kiwanja chenye nyasi fupi. Ndio maana kuna utaratibu
wa kufyeka nyasi na kumwagilia maji kwenye viwanja vya kuchezea
mpira kabla ya mechi.

Utakuwa umewahi kusikia kwamba wachezaji wa timu fulani


walishindwa kucheza vizuri kwa kuwa kiwanja kilikuwa kibovu.
Mama ukitaka mechi nzuri hakikisha kila eneo la kiwanja liko safi
kwa ajili ya mechi na siyo kutaka wachezaji wacheze mpira mzuri
kwenye kiwanja chenye nyasi nyingi kama unaanzisha pori tengefu.
58
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

Haya ni baadhi ya mambo ambayo yanaweza kusaidia kulifanya


tendo ndoa liwe imara wakati wote;
1. Uwe mbunifu kwa kuangalia ni sehemu ipi ukimshika mwenzako
anasisimka zaidi.
2. Mweleze mwenzako sehemu ambayo unapenda awe anaichezea
ili akupe hisia zaidi
3. Jiamini katika kutafuta mitindo mipya ya namna ya kufanya
tendo la ndoa ambayo itakuwa na faida kwa ndoa yenu. Usikubali
kutumia mtindo wa aina moja wakati wa tendo la ndoa, jitahidi
kufanya kitu kipya ili ndoa yako kuwa mpya kila wakati
4. Kila mmoja awe wazi kwa mwenzake na kutoa ushirikiano
inapohitajika ili kulifanya tendo hilo kuwa zuri.
5. Yajue yanayomkosesha raha ya kufurahia tendo la ndoa na
yanayomletea hisia haraka za kufanya mapenzi, kila mtu ana
maeneo yake muhimu ya kusisimka akiguswa

HATUA SITA ZA UKUAJI WA NDOA

Ndoa yenye mafanikio inahitaji wanandoa kuonyesha hali ya


kupendana mara nyingi zaidi kila wakati kwa kiwango kile kile na
mtu yule yule. Ndoa ni mchakato unaoibuka ukiwa na mabadiliko ya
kupanda na kushuka. Baadhi ya wanandoa hawatambui kuwa kuna
hatua zinazotabirika ambazo zinatokea katika maisha ya ndoa. Ndoa
mpaka kufikia hatua ya kukomaa inapita hatua kadhaa za ukuaji kwa
kuwa haiwezi kuwa katika hatua ile ile kutoka ilipofungwa mpaka

59
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

mnapokuwa wazee. Kuzielewa hatua hizi kunapunguza migogoro


katika ndoa maana jambo linapotokea unakuwa unajua fika kwamba
hiki ni kipindi fulani, kwahiyo katika kipindi hiki ninatakiwa kuwa
namna hii, kwa kuwa na uelewa huo kunakuwezesha kupita salama
kipindi cha nyakati ngumu. Hatua hizo ambazo ndoa hupitia ni kama
ifuatavyo:-

Hatua ya Kuvutia

Kila mtu anapenda hatua hii kwa sababu imejaa nguvu, shauku na
mapenzi. Uko katika mapenzi na uko wazi kuwa unataka kutumia
maisha yako yote na mwenzi wako. Unafikiria juu ya mwenzi wako
siku nzima na unajiona kama wewe ni mmoja! "Katika kipindi hiki
kila kitu kinakuwa sawa, maisha yanaonekana kama ni nusu ya
ufalme wa Mungu. Katika kipindi hiki majina yote mazuri
yanatafutwa na kuwa radhi kuhakikisha kwamba hakuna
anayekwazwa na matendo ya mwingine. Wakati mwenzi wako
anakushirikisha jambo la kufurahisha, linganisha shauku yako na
yake, usiwe mtoa hoja au maoni ya kuua shauku yake.

Awamu ya Kuamka

Hatua ya pili inajumuisha kuishi siku kwa siku na jinsi kila mwenzi
anavyochukua majukumu yake wakati wanaishi pamoja. Katika
hatua hii, unaanza kumjua mwenzi wako vizuri zaidi lakini maswali
yake yanaanza kukukasirisha. Unaanza kugundua kuwa yeye sio
mkamilifu na labda unajaribu kufikiri namna ya kubadilisha tabia
zake ili awe kamili kama wewe kwa kuwa unafikri wewe ni bora
kuliko yeye. Wakati ukifikiri hivyo yeye pia kwa upande wake
anawaza hivyo. Mwishowe huzuni inaweza kukua na kusababisha
kudorora kwa uhusiano huo kwasababu matarajio yako yameanza
kwisha. Katika hatua hii kukatishwa na kukatisha tamaa kunaanza
60
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

kwa uvumilivu mdogo wa kuvunjika kwa tofauti za kila mmoja. Hii


ni hatua ambayo wenzi wachanga wanaanza kutafuta msaada kwa
ndoa zao. Ninafurahi kukushirikisha kwamba nimegundua mwelekeo
mzuri unaibuka katika jamii yetu; mwamko wa umma umewahimiza
wenzi kutafuta msaada katika tiba na kuanza kuvuna faida za tiba ya
ndoa kwa uhusiano wao. Wanandoa ambao hawana mkakati wa
kujiweka hodari na wa karibu huwa wanapotea kabisa na kujikuta
ndoa zao zikiwa katika wakati mgumu zaidi.

Changamoto kubwa inayozikumba ndoa nyingi ni pale zinapoingia


kwenye hatua hii kila mmoja anataka kuiamini akili yake mwenyewe
huku akitupa lawama kwa mwezi wake jambo ambalo ni hatari sana
kwa ustawi wa ndoa. Unapoingia kwenye hatua hii kamwe usiiamini
akili yako tu, omba msaada wa ushauri kwa watu wengine
waliokutangulia kuingia kwenye ndoa huku ukimtwika Mungu
fadhaa zako maana yeye aliahidi kwamba hatatuacha kamwe. Watu
ambao unaweza kuomba msaada kwao ni wasimamizi wa ndoa yenu
(best man) na hapa ndipo penye umhimu wa kutafuta watu wakini
ambao watakusaidia kipindi kama hiki. Usiwe na msimamizi ambaye
yeye mwenyewe mambo yake hayaendi sawa kipindi hiki anaweza
asiwe wa msaada sana wakati wewe unamhitaji. Watu hao
wakishindwa unaweza kuwashirikisha wazazi wa pande zote pamoja
na wazazi wa kiroho (wachungaji)

Hatua ya Machafuko

Katika hatua hii, ndoa imeshaanza kuelekea mrama yaani kiwango


cha kufadhaika kiko kwenye chati. Ikiwa hauna ujuzi wa
mawasiliano kukusaidia katika hatua ya pili basi hatua ya tatu
itakuwa mbaya sana kwako. Ili kukutengeneza uelewa wa kutosha
nimezungumizia suala la mawasiliano katika sura itakayofuata.

61
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

Katika kipindi hiki wanandoa huelekea kukwama katika mzunguko


wenye uchungu kwa kuendekeza kubishana na kujiona bora kuliko
mwenzi wako. Huu ni wakati ambao wanandoa hufikia hatua ya
kutaka kujitenga au talaka. Ni kawaida kwa wanandoa kuanza
kujihusisha na shughuli ambazo zinahatarisha ndoa yao kama vile
unyanyasaji (kipigo na ugomvi wa mara kwa mara), kujiingiza
kwenye unywaji wa pombe, kuwa na mahusiano nje ya ndoa halali
ambayo kila mmoja anaitambua. Badala ya kuzingatia jinsi ya
kuboresha uhusiano wao ili kuendelea kuwa pamoja kwa kufikiri ni
ubaya gani uliojipenyeza kwenye ndoa yao. Badala ya kujaribu
kuungana tena, wenzi hao hutafuta kutoroka. Kutaka kujitenga au
kukimbia sio suluhisho katika kipindi hiki, watu wote waliofanikiwa
kudumu katika ndoa kipindi hiki kilipofika walijitahidi kadri
wawezavyo kusuluhisha na kumaliza tofauti zao.

Hatua hii inaweza kuepukwa kama wenzi wote wataamua


kujielekeza kuwa waangalifu na wanaojielimisha juu ya jinsi ya
kufanikiwa katika ndoa. Kwa bahati mbaya wengi hukwama katika
hatua hii kwa kuwa badala ya kurudi pamoja kila mmoja anajiona
bora zaidi. Utakumbuka Adam alijibu si ni huyu mwanamke
uliyenipatia? Ikiwa uko katika hatua hii pata msaada unaouhitaji
kutoka kwa watu mhimu ambao unadhani watakuwa na kitu chanya
cha kukusaidia, usithubutu kueleza hali hiyo kwa kila mtu maana
wengine sio wema muda wote walitamani ndoa yako ifikie hatua hii
ili wafurahi, na hapa ndipo msemo wa usimwamini kila rafiki
unapoleta maana. Hatua hii ni ya kukatisha tamaa sana kwenye ndoa;
hata hivyo usijikatie tamaa bado hali hiyo inaweza kuzuilika na ndoa
yako inaweza kudumu. Baba aliniambia siku ya harusi yangu,
usiende mahali ambapo hautakuwa na mke wako, alinisisitiza
kwamba kila mara nihakikishe nipo na mke wangu inapowezekana,
nisijaribu kwenda kwenye sherehe au burudani huku nikiwa sijui

62
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

mke aliko.Maana yake ni kwamba kila unapokwenda hakikisha


unakwenda naye, haimaanishi kuwa naye kimwili lakini ni hali ya
kuwa naye kiakili itakusaidia kukukinga na majaribu madogo
madogo.

Hatua ya Ushirika

Hapa ndipo mambo huanza kujulikana. Wanandoa wameunganishwa


zaidi. Wamejifunza mawasiliano na ustadi wa kutatua shida ambazo
zinahitajika ili kudumisha urafiki wao. Wana tabia ya heshima kwa
kila mmoja. Upendo wao umepita kutokana na uvumilivu wa tofauti
za kila mmoja hadi kukubaliwa kwa kila mmoja. Wanathamini
nguvu na tofauti za kila mmoja. Changamoto kubwa kwenye baadhi
ya ndoa watoto huwa ndio kipaumbele katika familia nyingi lakini
wenzi ambao hufikia hatua hii wameifanya ndoa yao kuwa
kipaumbele."Ujuzi muhimu zaidi wa ndoa ni kumsikiliza mwenzi
wako kwa njia ambayo hawezi kuwa na shaka kuwa unawapenda.
Hakikisha unatoa nafasi ya kumsikiliza mwenzako anasema na
anataka nini.

Hatua ya Urafiki

Mapenzi upya na uchezaji vinaonekana katika hatua hii ambayo


hujulikana kama "kiota tupu". Maana yake ni kwamba mnakuwa
mmeshajuana kwa kiasi cha kutosha sana, mnajuana nje ndani na
uvumilivu uko wa hali ya juu, hakuna kilichofichika kwa kila
mmoja, kila mtu anajisikia huru kuwa na mwenzake. Wanandoa
wana wakati zaidi pamoja wakati watoto wao wanapofikia miaka ya
ujana. Wanandoa katika hatua hii wana uelewa mkubwa wa kutimiza
mahitaji ya kila mmoja na kuthaminiana zaidi. Wanandoa hawa

63
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

wameendeleza urafiki wenye nguvu na wanafurahia wakati wao


pamoja. Mojawapo ya mambo mazuri ambayo unaweza kumwambia
mwenzi wako. Ikiwa ningeyafanya tena, nitakuchagua. Kitendo cha
wanandoa kuwa marafiki kinawaunganisha na kuwafanya kuwa
imara sana.

Utaratibu wa Utimilifu

Wanandoa wanapoifikia hatua hii wanakuwa thabiti na salama katika


hatua hii. Wanafurahia kushirikiana katika maisha ambayo
wameyajenga pamoja, imani kwa kila mmoja inakuwa juu sana,
wanaaminiana sana kiasi kwamba wanarudi kama ndio kwanza
wanachumbiana.Hapa mapenzi yanakuwa motomoto kila mmoja
anatamani kumwona mwenzake kila mara. Ndoa inakuwa ya
heshima na huweka mfano kwa wengine kiasi kwamba wanatamani
kuwaiga na kuishi maisha kama hayo. Kama kuna ndoa ambayo
unaiona katika hali kama hiyo leo jua wamekuwa irama katika hatua
zilizotangulia. Ni mhimu sana kuzijua hatua hizi na kujidhatiti ili
kukabiliana nazo.

64
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

SURA YA SABA
KUSUDI LA MUNGU JUU YA NDOA
7.1 Mwanzo wa Ndoa
Mungu ndiye mwanzilishi wa Ndoa, yeye ndiye aliyeumba
wanandoa wa kwanza Adamu na Eva kama mume na mke. Maandiko
yanasema katika Mathayo 19:4 “yeye aliyewaumba hapo mwanzo
aliwaumba mtu mume na mke” Mwanzo 2:18 “Bwana Mungu
akasema, si vema mtu huyu aishi peke yake, nitamfanyia msaidizi wa
kufanana naye” Mwanzo 2:22 Mungu alipomaliza kumuumba
mwanamke,alimchukua na kumleta kwa Adamu. Mwanzo 2:24 hapa
kuna maswali kadhaa ya kujiuliza ni kwanini Mungu alipomaliza
kumuumba mwanamke alimleta kwa Adamu? Je hapakuwepo mahali
pengine ambapo ungepswa kumweka? Majibu yake ni rahisi sana,
asingemweka eneo lingine kwa kuwa aliumbwa kwa ajili ya Adamu,
huyu mwanamume adamu ndiye aliyehitaji msaidizi kwahiyo ilikuwa
65
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

ni lazima msaidizi anapopatikana akabidhiwe. “Kwahiyo kule


kukabidhiwa na Mungu kunamfanya mwanamume amwache baba na
mama yake ili ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa
mwili mmoja”

7.2 Ndoa kama Taasisi


Ndoa ni taasisi, kwa kuwa ina kusudi la kuwepo kwake, ina mpango
wa kutimiza na ina watu kama rasilimali. Mungu aliifanya ndoa
kuwa taasisi ya kwanza kabla ya taasisi zingine; kabla ya kuwepo
kwa serikali, vyama, shule, kanisa au kampuni yoyote taasisi ya ndoa
ilikuwepo. Ndoa ni taasisi kwa kuwa ina kusudi la kuwepo,
ina mpango wa kutimiza, ina kanuni za kuiendesha, ina watu kama
rasilimali, ina ngazi za kimamlaka na ina mgawanyo wa majukumu.

Kwahiyo ili ndoa iweze kusimama imara na kutoa matokeo tarajiwa


ni lazima kila mwanandoa alijue kusudi lengwa, ikitokea kwenye
ndoa kila mmoja akawa na kusudi lake basi huo ndio unaokuwa
mwanzo wa ndoa hiyo kupalanganyika. Kadharika wanandoa waujue
vema mpango wa ndoa na kanuni zake, kichwa kwenye ndoa kibaki
kuwa kichwa na msaidizi abaki na kukubali kwamba yupo kwa ajili
ya mumewe. Ngazi za kiutawala pamoja na mgawanyo wa
majukumu ukisimamiwa vema ndoa itazaa matunda tarajiwa.
Matatizo katika ndoa huanza kujitokeza pale ambapo wanandoa kwa
makusudi au vyovyote vile wanapoamua kupindua misingi ya ndoa
na kushindwa kusimama kwenye nafasi zao.

7.3 Ndoa kama msingi wa familia na Kanisa


Wakati familia ni msingi wa jamii yoyote ndoa nayo ni msingi wa
familia. Hii ina maana kwamba, ndoa ndio msingi wa jamii kwa
kuwa ndoa inajenga familia na familia inajenga jamii; kwahiyo, ndoa
ni msingi wa jamii yote ya wanadamu. Ndoa ni msingi wa Kanisa pia
66
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

kwa kuwa familia ndiyo inayojenga Kanisa na familia inajengwa


kutokana na misingi ya ndoa.

7.4 Kwanini ni mhimu kuwa na ndoa


a) Ni agizo na Mapenzi ya Mungu
Sababu kubwa ya kwanini watu waingie kwenye ndoa, ni kwasababu
ndoa ni mpango wa Mungu maana Bwana mwenyewe alisema ‘si
vema mtu aishi peke yake’ Mwanzo 2:18. Kwa hiyo ukisoma mstari
huu utagundua kwamba Mungu ndiye mwanzilishi wa taasisi ya ndoa
kwa kuwa alikuwa na kusudi ambalo alikusudia kwamba lije
likamilishwe kupitia ndoa.

b) Kutimiza haja ya kuwa na mwenza


Kila mwanadamu ameumbwa na haja ya kuhitaji na kuhitajiana.
Hakuna aliyeumbwa mkamilifu kiasi cha kutohitaji msaada au
uwepo wa watu wengine. Kila mtu ana tundu la kuhitaji uwepo wa
binadamu mwingine karibu yake. Ndoa ilitengenezwa na Mungu kwa
ajili ya kutimiza hitaji hilo. ‘Ni heri wawili kuliko mmoja, kwa
sababu wakiwa wawili, mmoja akianguka, mwingine atamwinua’
Mhubiri 4:9

c) Kutoa upendo kwa mwenzi


Kila mtu ameambwa na tundu la kutaka kupendwa na kutoa upendo.
Ndoa inampa mtu fursa ya kuonyesha upendo wa Mungu kwa mtu
aliyemchagua. Sababu kubwa ya kuingia kwenye ndoa si kupendwa
bali kwenda kutoa upendo. Kinyume na hapo, ndoa hiyo itakuwa na
matatizo ya ubinafsi. Wapenzi na tupendane kwa kuwa pendo latoka
kwa Mungu. Kila apendaye amezaliwa na Mungu naye anamjua
Mungu. Yeye asiye penda, hakumjua Mungu, maana Mungu ni
upendo 1Yohana 4:7-9
67
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

d) Kumtumikia Mungu kwa pamoja


Mungu alipomleta binadamu wa kwanza duniani alikuwa na
makusudi ya kujenga ufalme wake duniani. Adam na Eva ni
watumishi wa kwanza katika kulitimiza kusudi hilo. Ndoa inatoa
fursa kwa watu wawili waliopendana kumtumikia Mungu kwa
pamoja ili kuujenda ufalame wake duniani, yaani ibada, injili,
utawala na mafanikio. ‘Kwa kuwa katika mwili mmoja tuna viungo
vingi, wala viungo vyote havitendi kazi moja; vilevile na sisi tulio
wengi, tu mwili mmoja katika Kristo na viungo kila mmoja kwa
mwenzake’ Warumi 12:4-5

d) Kuendeleza uzazi ya uumbaji (Kupata watoto)


Mungu katika kuujenga ufalme wake alihitaji watu kwa ajili ya
kulitumikia kusudi hilo. Hivyo ndoa ni mpango maalumu wa Mungu
wa kuongeza uzazi kwa kuzaliana. Pia ndoa inatoa fursa ya watoto
waliozaliwa katika ndoa hiyo kulelewa na kuandaliwa kitabia na
kiroho kwa ajili ya kulitumikia kusudi la Mungu. ‘Mungu
akawaumba mwanamume na mwanamke, akawaambia zaeni na
kuongezeka na kuitawala nchi’ Mwanzo 1:28-29

e) Kusaidiana kupata mahitaji ya msingi

Uzazi unapoongezeka na mahitaji ya msingi ya kifamilia


yanaongezeka. Hivyo kwa njia ya watu wawili kufungamana katika
agano la ndoa, inawapa fursa ya kufanya kazi na kupata kipato
kitakachosaidia kutimiza mahitaji mbalimbali ya kifamilia. ‘Ni
afadhali wawili kuliko mmoja, kwasababu wana malipo mazuri kwa
kazi yao’ Mhubiri 4:9

68
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

f) Kuimarishana kiroho

Ndoa imeanzishwa na Mungu kama taasisi ya kiroho yenye kukua


kulitimiza kusudi la Mungu. Kupitia ndoa watu wawili walio karibu
sana, wanapata nafasi ya kuinuana na kusaidiana kiroho kama Kristo
alivyo na wajibu wa kulileta Kanisa lisilo na mawaa mbele za Mungu
Baba, vivyo hivyo, mume ana wajibu wa kuifikisha familia yake
mbele za Mungu, ikiwa haina mawaa. Huu ni wajibu mzito sana
ambao mara zote mwanamume anatakiwa kuujua kwani kutenda
kinyume na hivyo iwe kwa kujua au kutokujua ni dhambi !

7.5 Sababu zisizo sahihi;


i. Kukimbia matatizo ya kifamilia

Kuna baadhi ya watu huamua kuingia kwenye ndoa ili kukimbia


namna wanavyodhibitiwa na wazazi, magomvi ndani ya kifamilia au
majukumu makubwa waliyonayo katika familia.Katika kutafuta
namna ya kujikwamua wanaamua kuingia kwenye ndoa ili kuanzisha
serikali yake binafsi ambayo itamfanya ajiengue kutoka katika
familia yake yenye matatizo fulani. Huu sio msukumo sahihi hata
kidogo wa kukusukuma kuingia kwenye ndoa. Kwasababu matatizo
hayakimbiwi isipokuwa yanatatuliwa, huko kwenye ndoa
unakokimbilia sio mbinguni hata huyo unayemkimbilia sio malaika
ni binadamu unaweza kukuta ana matatizo au maudhi makubwa zaidi
kuliko hata haya uliyoyakimbia.

ii. Kutafuta kuthaminika

Wengine kwa kukosa upendo, kusikilizwa na kuthaminiwa kwenye


ngazi ya familia, hujikuta wametumbukia katika ndoa kwasababu tu
alikutana na mtu ambaye alimwonyesha heshima na kumthamini,

69
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

jambo ambalo lilijaza haraka lile tundu moyoni mwake lililokuwa


linataka kuthaminika mbele za watu. Na baada ya hapo akaona
maisha ndio yale kwa kuwa anapata kile ambacho hakuwa akikipata.
Pamoja na hayo huu pia sio msukumo sahihi wa kukufanya uingie
kwenye ndoa. Ndoa ni zaidi ya hicho unachokiona kwa macho ya
nje,ndio maana unatakiwa kutafakari na kumshirikisha Mungu;
vinginevyo unaweza kukuta umeingia mahali ambako sipo
ulipokusudiwa.

iii. Kuponya majeraha

Wengine katika maisha wamewahi kuumizwa na wazazi, ndugu,


jamaa, marafiki na au waliingia kwenye uchumba, mwisho wa siku
waliokuwa wamewaamini na kufungua mioyo kwa ajili yao
wakawatenda vibaya hali iliyosababisha wabaki na majeraha ndani,
kwa hiyo ili kuponya kidonda cha moyoni wanaamua kutumbukia
haraka katika ndoa. Hiyo ni hatari sana kwani unaweza kujikuta
unabandikwa kidonda kingine kikubwa na kitakachoathiri maendeleo
yako.

iv. Kubaki mwenyewe

Wengine wamejikuta marafiki zao wote wameshaingia kwenye ndoa


na yeye bado hajakutana na mtu sahihi wa kufunga naye ndoa; kwa
hofu ya kuonekana amebaki mwenyewe katika jamii ya marafiki
zake anaamua kuvamia haraka taasisi hii ya ndoa, bila kuzingatia
vigezo muhimu, eti tu kwasababu aonekane ana ndoa. Usithubutu
kuingia kwenye ndoa kwa kufuata mkumbo huu, ni mhimu sana
kujitafakarisha kabla ya kujiingiza kwenye ndoa, usisahau kwamba
ndoa ipo kwa kusudi maalum.

70
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

v. Kujitegemea

Wengine wamezaliwa katika familia ambayo mtoto amekuwa


tegemezi sana kwa wazazi na walezi au wasaidizi wake kwa muda
mrefu. Ghafla umri unamsukuma kutoka kwa wazazi lakini anajikuta
hawezi kujitegemea katika mambo mengi, hivyo anaamua
kutumbukia kwenye ndoa ili apate mtu wa kuendelea kumtegemea
katika mambo fulani fulani.

vi. Kuogopa kuumiza

Wengine wamekuwa katika mahusiano ya uchumba kwa muda mrefu


kiasi kwamba mmoja anaogoa kuumiza moyo na hisia za mwenzie
kwa kumkatalia ombi la kufunga ndoa. Mtu wa namna hii anajikuta
ameingia katika ndoa si kwa kupenda bali kwa hofu tu. Hii pia ni
hatari sana, endapo mtu huyu atagundua upendo wake uko kwa mtu
mwingine wakati tayari wameshafunga pingu za ndao. Ndio maana si
ajabu hata kidogo kukuta mtu ni mke au mume wa mtu lakini hana
mapenzi naye isipokuwa mtu mwingine mpaka unafika wakati
anasema hata sijui ilikuwaje kukuoa/kuolewa na wewe.

vii. Hamu ya tendo la ndoa

Wengine wanaingia kwenye ndoa kwasababu ya kutimiza haja za


miili yao kupitia tendo la ndoa. Tendo la ndoa ni haja au ‘apetite’
kama njaa, kiu na usingizi. Haja hiyo ikitimizwa nafsi ya mtu
hushiba na kuridhika, lakini hiyo haimaanishi kutakuwa na upendo
katika yao. Ndoa ni upendo na sio tendo la ndoa. Tendo hili
likifanyika kutokana na upendo, huwa na maana zaidi kuliko
kutimiza haja ‘apetite’ ya mwili. Kama mtu aliingia kwenye ndoa
kwasababu ya kukidhi hitaji la tendo la ndoa maana yake ni huyo
aliyenaye ataonekana wa maana wakati wa tendo hilo lakini tendo
71
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

likikamilika umaana wake utakuwa umekwisha mpaka wakati


mwingine uhitaji ukitokea.
viii. Sababu ya ujauzito

Wengine kabla ya kuingia kwenye ndoa wanakuwa


wameshajihusisha na tendo la ndoa bila idhini matokeo yake
wanajikuta ni wajawazito hivyo wanalazimika kuingia kwenye ndoa
kama njia ya kuondoa aibu inayowakabili. Kutumia ujauzito kama
kigezo cha kutaka kuolewa sio njia sahihi kwasababu kuna
uwezekano mkubwa ujauzito huo umetokana na tamaa na sio
upendo, hivyo msingi wa ndoa hii utakuwa ni tamaa na sio upendo.
Usijitahidi kupambana kuficha matokeo ya dhambi kupitia ndoa,
kama ni aibu na iwe, maana aibu kubwa ilikuwa ile uliyoruhusu
kuzini na hiyo ndio dhambi. Isaya 55:8 “Maana mawazo yangu si
mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema Bwana”.
Najua umeusoma au kusikia na hata kuufundisha sana mstari huu.
Lakini leo katika kona hii ya ndoa nataka nikushirikishe tafsiri ya
mstari huu kwa kadiri ya neema ambayo Bwana amenijalia kwenye
hili eneo.

Ukisoma vizuri mstari huu utagundua ni kana kwamba kulikuwa na


ushindani au kutofautiana kimawazo kati ya Mungu na watu
wanaosemwa hapa. Yeremia 29:11 pia inasema “Maana nayajua
mawazo ninayowawazia ninyi asema Bwana”. Sasa ukiunganisha
maneno haya utagundua kwamba kuna mawazo na njia za
kiutekelezaji ambazo Mungu alikuwa nazo juu yao wakati nao
walikuwa na mawazo na njia za utekelezaji walizokuwa wakiziwaza
ambazo hazikuwa sawasawa na zile za Mungu ndiyo maana akasema
mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu. Kwa
lugha rahisi Mungu alikuwa akisema geukeni/acheni hayo

72
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

mawazo na njia zenu tekelezeni mawazo na njia zangu ndipo


mtafanikiwa.
Mungu alisema maneno hayo baada ya kuona matokeo ya mawazo
na njia zao ni mabaya, kwa kuwa yalikuwa nje ya kusudi lake.
Ukitaka kuthibitisha kauli hii soma mstari wa 7 katika Isaya 55
Biblia inasema, “Mtu mbaya na aache njia yake, na mtu asiye haki
aache mawazo yake; na amrudie Bwana naye atamrehemu, na
arejee kwa Mungu wetu naye atamsamehe kabisa”. Anaposema
mtu mbaya anamaanisha mtu ambaye anataka kutekeleza mawazo na
njia ambazo zipo kinyume na mawazo na njia za Mungu. Katika
maamuzi ya kupata/kutafuta mwenzi wa maisha najua kabisa kuna
vitu ambavyo ungependa awe navyo. Kuna namna fulani
ungetamani awe kiumbile, kiumri, kikabila, kielimu, utajiri, n.k
kwa kifupi tuseme haya ni mawazo yako juu ya mwenzi wako wa
maisha.

Ni kweli haya ni mawazo yako lakini usifikiri Mungu hana mawazo


ya nani anafaa kuwa mwenzi wako wa maisha. Ukweli wenyewe ni
kwamba Mungu wetu anayo mawazo mazuri juu ya nani anafaa
kuwa mke au mume wako.Hii ni kwasababu yeye ndiye aliyekuumba
na ndani yako ameweka kusudi ambalo anataka litekelezwe kwa njia
au mikakati yake. Kwa hiyo ili kusudi lake kwako liweze kutimia
anahakikisha unaoa au unaolewa na mtu aliyemkusudia ili
kurahisisha utekelezaji wa mawazo yake.Jifunze kuruhusu mawazo
ya Mungu na njia zake zitekelezwe katika maisha yako ili kusudi
lake lifikiwe. Kumbuka Mithali 16:1 inasema, “maandalio ya moyo
ni ya mwanadamu, bali jawabu la ulimi hutoka kwa Bwana”.
Unaweza kupanga au kuamua aina ya mke au mume unayemtaka na
ukaweka vigezo katika fikra zako na kwa kweli hilo sio dhambi
lakini Kibiblia/ Ki-Mungu si lazima iwe kama ulivyopanga
73
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

kwasababu mwenye kutoa jawabu la ulimi juu ya maandalio ya


moyo wako ni Mungu. Kazi ya Roho mtakatifu ni kukushauri na
kukuongoza na si kukulazimisha katika yaliyo mapenzi ya Bwana.
Hivyo hata katika suala la mwenzi wako yeye atafanya wajibu wake
ikiwa utamruhusu. Maamuzi yanabakia kwako kutekeleza mawazo
na njia zake kwako na kama ukikataa uwe na hakika
umekaribisha mabaya na kutotendewa haki katika ndoa yako.

Mpendwa wangu yaangalie maamuzi unayotaka kuyafanya,


hakikisha yamepata kibali cha Bwana ukikumbuka haya ni maamuzi
makubwa na yana gharama sana. Neno la Mungu lina maelekezo
yote kama kilivyo kitabu cha maelekezo (manual book), kwenye
hicho kitabu (Manual book) anasema,‘Tukitii, tutakula mema ya
nchi, tukikataa, tutaangamizwa kwa mauti’ Isaya 1:19

74
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

SURA YA NANE

MAMBO YANAYOMHUSU
MWANAMUME
8.1 Mwanamume ni nani hasa?
Mwanamume ni mtu yeyote mwenye jinsi ya Me wakati Baba ni sifa
na cheo cha ziada anachokipata huyo mwenye jinsi ya Me
kikiwakilisha uwajibikaji. Jinsi hii ya Me mwanamume anayo
kutokana na maumbile yake kibayolojia ambayo alijikuta yuko nayo.
Laiti kama kungekuwa na vikao kwa ajili ya kupitisha au
kumwondolea mtu hadhi ya kuwa na jinsi ya Me basi kuna watu nina
uhakika wasingalikubaliwa au wangenyang’anywa hadhi hiyo.

Kimsingi kuna utofauti kati ya kuwa mwanamume na kuwa baba,


maana kuwa baba ina sifa ya ziada inayomaanisha kuwajibika,
majukumu na kujituma. Siyo kweli kwamba kila mwanamume
anafaa kuwa baba; kama uko kwenye ndoa kwa namna unayoijua
wewe ukawa huwajibi kwa ajili ya familia yako na wala hujitumi
basi wewe bado ni mwanamume na sio baba. Sifa zinazomtofautisha
mwanamume na baba ni pamoja na hizi zifuatazo:-

1. Mbeba maono
Baba ndiye mwenye maelekezo ya namna ya kuishi maisha bora
hapa duniani kwa wote watokao ndani yake, yeye anawajibika
kuwaelekeza na kuwaongoza kwa kutangulia mbele kama mfano wa
kuigwa. Mwanzo 2:15-16. Hii iko namna hiyo kwa kuwa baba ndiye
mbeba kusudi la Mungu kwa familia, yeye ndiye mwenye patano na
Mungu juu ya namna atakavyomwakilisha kwenye ngazi ya familia.
Kwahiyo kama wewe una familia na huna maono ya wapi
unakoipeleka wewe ni mwanamume siyo baba; ni kwa bahati mbaya
75
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

sana ulishaanza kuishi na mtoto wa watu na mmeshaongeza


watanzania wengine nyuma yenu ingawa hujui unawapeleka wapi.

Kila kitu cha muhimu na lazima anachotakiwa kuwa nacho kiongozi


anatakiwa kuwa nacho baba kama kichwa cha familia Efeso 5:23
hivyo mambo yanapoharibika anatakiwa kuulizwa na kuwajibika
maana ni kiongozi wa familia. Lakini sasa mambo ni tofauti, baadhi
ya kinababa wamekimbia wajibu wao na wameukabidhi kwa watu
wengine, na wao wameungana na watu wengine kulalamika badala
ya kuchukua hatua.Mwanamke aliyefunzwa vizuri anajua kuheshimu
kwamba baba ni kiongozi wa familia ndio maana hata mkiamka
asubuhi anakuorodheshea mahitaji ya familia hata kama kabla ya
kulala ulieleza kwamba huna fedha;kwahiyo “Kama kwenye nyumba
yako huletewi orodha ya mahitaji basi kuna mahali mambo
yamekwenda kombo ama wewe au mkeo mmoja hajui namna ya
kutimiza wajibu wake”

2. Mfundishaji na mlea watoto


Baba ndiye mwenye wajibu wa kuwalea na kuwafundisha watoto.
Ndiye mwenye wajibu wa kuwarithisha maono kwa kuwa yeye ndiye
mwenye hayo maono wengine wamekuja kusaidia kuyatimiza.
Mithali 22:6 na Waefeso 6:4. Baba ndiye, anayetakiwa
kuwaadibisha watoto, ndiye anayewajibika kuweka mipaka ya kila
kitu ndani ya familia, ndiye anayetakiwa kuwaeleza zuri na baya
1Korintho 15:33. Mtoto mdogo anatakiwa kuzoezwa kuelezwa kwa
nini jambo hili ni jema na hili siyo jema. Epuka kueleza mambo kwa
bei ya jumla jumla, mtoto atashindwa kuelewa. Msaidie mtoto
kuelewa mambo unayomkataza kwa kutumia bei ya rejareja.

76
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

Kinababa wanasingizia kwamba unawafanya watoto kuwa wabaya


zaidi na kwamba mila zinatukataza Kumbukumbu 6:6-9. Amri hizi
ninazokupa leo zitakuwa katika moyo wako. Wafundishe watoto
wako kwa bidii. Nena kuhusu amri hizi uketipo nyumbani na wakati
utembeapo njiani, ulalapo na uamkapo. Zifunge kama alama juu ya
mkono wako, zifunge juu ya paji la uso wako. Ziandike kwenye
miimo ya milango ya nyumba yako na juu ya malango yako.

Weka mipaka juu ya nini kifanyike na kwa muda gani kifanyike


na makusudi yake nini Mwanzo 9:6, Mhubiri 3:1. Baba anatakiwa
kuweka mipaka ya kila jambo kwenye familia na kuhakikisha
kwamba kila mmoja anajua kwa nini jambo fulani liko jinsi lilivyo.
Lazima ratiba ya kila kitu ifahamike ili kuepuka kuchanganya
mambo kama ni muda wa ibada ijulikane na wote washiriki siyo
wengine wanafanya ibada huku wengine wanafanya mambo
mengine.Ratiba iliyowekwa isimamiwe na wazazi wote sio
kurushiana mizigo,wakati fulani unawasikia kina mama
wakiwaambia watoto wao baba yako akija utaona.

Waweke wazi juu ya hali yako kimapato. Wafahamishe watoto


wako kwamba kila jambo lina wakati wake chini ya jua na kwamba
kwa kila jambo Mungu ana makusudi yake.1Samweli 2:6, Hosea
6:1-3. Baadhi ya kinababa hushindwa kukaa na watoto wao na
kuwaelezea hali zao, wanashindwa kuwaeleza kinagaubaga juu ya
uwezo wa Mungu. Kwa kushindwa kutimiza wajibu wetu wa
kuwafundisha juu ya ukuu wa Mungu. Mtoto hajui lolote juu ya
miujiza ambayo Mungu anatutendea kila inapoitwa leo, leo watoto
wengi hawawezi kutaja majina ya vitabu vya biblia lakini anayajua
majina ya wachezaji wa mpira wa miguu huko Ulaya, anaweza
kupanga kikosi cha kwanza mpaka na wachezaji wa akiba.

77
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

Wasiliana na watoto wako ili kujua shida zao. Kuwasiliana ni


kupashana habari kati ya pande mbili tofauti juu ya jambo fulani au
kupashana habari ya nini kinaendelea. Kinababa wengi wanashindwa
kufanya mawasiliano mazuri na watoto wao na hivyo wanawaacha
wajiendeshe wenyewe matokeo yake inapelekea kila mtu katika
familia kuwa na mambo yake. Kinababa wameshindwa kutimiza
wajibu wao hasa kwa kushindwa kuwasiliana na watoto wao lakini
wanakuwa wepesi kulaumu kwamba watoto wa siku hizi
wameshindikana si kushindikana ila ni kushindwa kutimiza wajibu
wako kama baba.

3. Mfanyakazi kwa bidii


Mwanaume alikusudiwa na Mungu afanye kazi ya kuendeleza,
kutunza, kuzalisha, kupendezesha na kukuza watu na vitu kwa
utukufu wa Mungu Mwanzo 2:15. Kwahiyo ili uweze kutimiza
wajibu huu na kulinda heshima yako kama kichwa na baba ndani ya
nyumba lazima utafute fedha, lazima uwe na kazi ya kukuingizia
kipato na sio kushinda kijiweni. Hakuna namna ambavyo unaweza
kuipendezesha familia yako na wote walioko nyumbani mwako
kama hufanya kazi. Tunategemea ukiwa baba wote waishio kwako
wajisikie fahari kuwa na baba kama wewe sio kujawa na lawama za
kwa nini walizaliwa na baba kama wewe maana watoto mambo
mengi mazuri wanayasikia kwa jirani.

Mtu mmoja aliwahi kusema “Mke wako anaendelea kuishi kwako sio
kwa kuwa wewe ni mzuri isipokuwa ni kwa kuwa unaweza kutimiza
mahitaji yake ya msingi, siku utakaposhindwa kuyatimiza basi
unaweza kuumwa hata na mbwa wako mwenyewe”; akasema pia,
“kama unataka heshima toka kwa mke wako, watoto wako na jamii
kwa ujumla fanya mambo matatu, la kwanza fanya kazi, la pili fanya
kazi na la tatu fanya kazi maana kazi ni msingi wa maendeleo na
78
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

kipimo cha utu”.Kama unafanya kazi maana yake unapata kipato na


kama una kipato kizuri cha kutosheleza mahitaji muhimu ya familia
yako huhitaji kutumia nguvu ili watoto wako wajue kwamba wewe
ndiwe baba yao, hapana matendo yako na huduma nzuri kwao
vitakutambulisha.

4. Mtunza familia
Kama baba kwenye familia Mungu alikusudia wewe ndiwe uwe na
wajibu wa kwanza katika kuitunza familia hiyo; siyo Mungu tu na
hata sisi wengine ambao tunakutazama mategemeo yetu ni kwamba
wewe ndiwe mwenye wajibu wa kuilisha na kuihudumia
familia.Tunaposema familia yako tunazungumza mke na watoto
wengine ni ziada baada ya hawa kuridhika. Kumbuka maandiko
yanasema “utamwacha baba na mama” sasa kuna akina baba
wanajitahidi sana kuwaridhisha marafiki zao, wanakula hoteli huku
wakiwaacha wale walio wa msingi kwao wakihangaika. Hiyo siyo
sawa hata kidogo, 1Timotheo 5:8,“Lakini mtu yeyote asiyewatunza
walio wake yaani wale wa nyumbani mwake hasa, ameikana imani,
tena ni mbaya kuliko asiyeamini”.

Ni muhimu kufahamu kwamba unapoamua kuoa unakuwa


umeanzisha familia. Huwezi kuoa halafu maamuzi ya namna ya
kuishi na familia yako yakafanywa na mama au baba yako huku
ukimwacha yule uliyemwoa kama mfanyakazi wa ndani.Pia
hatutegemei uanzishe familia ambayo unakusudia kuitunza kwa
kutumia mazoea au historia ya namna wazazi wako walivyoishi huko
nyuma. Mwanaume funguka na elewa mazingira yako na hawa
watanzania wa leo ni tofauti na hata matunzo yao yanapaswa kuwa
tofauti. Ukiwa Baba wa familia lazima ujue kwamba suala la kula

79
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

kwa familia yako ni jukumu lako na siyo la mtu mwingine, wengine


kwenye familia wapo kuchangia juhudi zako.

Kwa wazazi mnaosoma kitabu hiki na kwa bahati nzuri watoto wenu
wameoa au kuolewa ninawasihini sana kwa neema za Kristo Yesu
rizikeni na kile mnachopata kutoka kwa watoto wenu msitake wala
kulazimisha kupata sawa na wenzi wa watoto wenu. Kumbukeni
watoto wenu baada ya kuoa au kuolewa wanaanzisha nyumba na
kwa kawaida nyumba haijengwi ndani ya nyumba nyingine,
kumsomesha mtoto kusitumike kama kigezo cha kumtaka
akuhudumie kuliko yule anayewajibika kwake.

Jambo la msingi la kuzingatia wakati wa kuihudumia familia ni


utofauti wa mahitaji ya watoto na ya mke wako.Vivyo hivyo mahitaji
ya watoto wa kike na wale wa kiume kama umejaliwa kuwa nao ni
tofauti pia kulingana na maumbile yao. Mahitaji haya yanajumuisha
chakula, malazi na mavazi. Mfano kama unaihudumia familia nguo
za ndani ni muhimu kujua kwamba mke wako pamoja na watoto wa
kike wanahitaji nguo zaidi kuliko watoto wa kiume, pia kama mke
wako akiwa mjamzito au ananyonyesha anahitaji chakula na
matunzo zaidi kuliko kipindi kingine chochote ambacho hanyonyeshi
na wala sio mjamzito. Na hata kwa upande wa usafi; kwa mfano
wanaume hatuhitaji maji kila mara tunapokwenda kujisidia haja
ndogo, lakini wanawake wanahitaji maji kila mara anapokwenda
kujisaidia ili waendelee kuwa wasafi, kwahiyo usifanye mazoea
kutaka kuitunza familia kwa bei ya jumla jumla.

5. Mlinzi wa familia
Kulinda ni kukinga au kuzuia madhara, hasara au uharibifu visitokee
mahali fulani au visimpate mtu au kitu fulani. Mlinzi ni mtu
anayechunga na kulinda mali isiibiwe, ikiwa hivyo ndivyo maana
80
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

yake ni kwamba baba amepewa wajibu wa kuwalinda mke na watoto


wake dhidi ya madhara yoyote. Anawajibika katika kila hali kuilinda
familia yake dhidi ya uharibifu na uvamizi wa nguvu za giza katika
ulimwengu wa roho pia. Akifanya hivyo hawi wa kwanza hivi
ndivyo walivyofanya kinababa wa zamani ambao kwetu ni mashujaa
wa imani Ayubu 1:5. Ni muhimu kuwaombea wanafamilia kwa
ujumla maana mambo yanayowatafuta ni mengi, wanakutana na
mitihani mingi ambayo kibinadamu kuishinda bila nguvu za Mungu
haiwezekani. Mungu anathibitisha kwamba kama ukiwalinda kwa
neno lake yeye anatimiza Mithali 6:20-23

Katika siku za hivi karibuni mambo yameanza kuwa tofauti,


limeibuka kundi la kinababa ambao hawajali na hawajishughulishi na
watoto wao kabisa.Unakuta baba hana muda wa kujua kama watoto
wamekula au hawajala, wamekwenda shule au hawajaenda n.k.
Majukumu haya yote na mengine mengi yameachwa mikononi mwa
kinamama.Mama ndiye aliyebebeshwa mzigo huu wa kuhakikisha
kila kitu kwenye familia kinakwenda, kinababa wako bize
kukimbizana na kitu kiitwacho maisha na wengine hata
hawakimbizani na chochote wako tu vijiweni kubishania mambo
yasiyo na tija kitu ambacho hupelekea malezi ya watoto
kumwelemea mama.

Kupitia kitabu hiki mtu wa Mungu nataka kukuhakikishia kwamba


kama wewe ni baba na umeshindwa kutimiza wajibu wako wa
kuwalinda watoto wako na mkeo kiasi kwamba umefikia wakati
wameanza kugundua au kuhisi kwamba hawako salama basi tegemea
kwamba kuna watu muda si mrefu wataanza kulifanya jukumu hilo
kwa niaba yako. Namna ya kupima kama umeshapata msaidizi wa
kukusaidia kulinda familia yako bila wewe kujua ni kuangalia
thamani yako kwa wale uliotakiwa kuwalinda kabla na
81
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

sasa.Mwanamume mwenzangu tafadhali sana hata kama una mambo


mengi kiasi gani hakikisha una muda wa kuwasiliana na watoto
pamoja na mke wako vinginevyo unaweza kudhani kila kitu kiko
sawa kumbe nchi ilishatekwa siku nyingi.

6. Tegemeo la familia
Tegemeo maana yake ni “tarajio la kupata kitu au hitaji kutoka kwa
mtu”. Kwahiyo wanafamilia wote wanategemea kupata mahitaji yao
kutoka kwa baba, baba amepewa wajibu na Mungu kuwa tegemeo la
wote walio chini ya uaangalizi wake ili awawezeshe kustahilimili
changamoto za kimaisha, awape mahitaji yao, awakuze ili wafikie
hatua ya kujitegemea na kuendesha maisha yao. Kwa hiyo kila alipo
baba lazima ajue kwamba waliopo nyumbani mwake wanamwona
kama tegemeo. Na unapokuwa tegemeo lazima ujitahidi kujua wale
wanaokutegemea wanakuonaje. Waefeso 6:4. Ili uonekane wewe ni
tegemeo lazima wale wanaokutegemea wafikie hatua ya kujipiga
kifuani kwamba tunaye baba, huyu ndiye hufanya hiki na kile,
ukiona kwenye familia yako mambo ni tofauti na hivyo anza
kujifanyia tathimini.

7. Mtetezi wa familia
Baba anawajibika kuitetea familia yake kwa nguvu na uwezo wake
wote.Hii ina maana kwamba kila mara unapoona mmoja wa
wanafamilia wako anapata shida unawajibika kusimama naye mpaka
mwisho kuhakikisha kwamba haki yake inapatikana.Huu siyo
mlango wa kufanya upendeleo bali ni wajibu wa kuhakikisha
kwamba walio chini ya dari yako hawakumbwi na madhara wala
uonezi. Bila shaka umewahi kusikia watoto wakitambiana mitaani
kwamba “usicheze na baba yangu, yeye ni kiboko” Maana yake ni
82
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

kwamba katika akili ya mtoto anajua duniani hakuna mwenye


uwezo, nguvu wala akili kuliko baba yake, anaamini hivyo mpaka
kesho.Na wewe hakikisha unakilinda kile anachokiamini na
kukifanya kwa vitendo. Lakini katika siku za hivi karibuni mambo
yameanza kubadilika na kuwa kinyume chake badala ya kinababa
kuwa watetezi wamekuwa watesaji, wanyanyasaji n.k; wanawapiga
watoto bila sababu, wanawatesa na kuwapiga wake zao, na wengine
wamekwenda mbali zaidi mpaka wamediriki kuwatoa kafara watoto
wao kwamba wanataka mali Mithali 28:16a.

8. Kuhani
Katika agano la kale Kuhani alihusishwa na usimamizi wa utoaji
dhabihu na sadaka katika madhabahu ya Mungu pamoja na
kusimamia ibada ya kumwambudu Mungu.Majukumu haya ya
kikuhani anayo baba kwenye familia maana ni kiongozi
anayemwakilisha Mungu katika mambo yote yahusuyo maisha ya
kiroho ya familia yake.Anawajibika kuijulisha na kuifundisha familia
yake juu ya mapenzi na rehema za Mungu zilivyo kuu kwao kama
familia,masuala ya utumishi ikiwa ni pamoja na kumtolea
Mungu.Mara zote baba usisahau kuomba rehema na neema juu ya
familia yako maana yumkini wamemtenda Mungu dhambi bila wewe
kujua Kumbukumbu 31:12-13. Kwahiyo kama watoto kwenye
familia hawamjui Mungu anayewajibika katika kuwafanya wamjue
ni baba, Kumbukumbu 6:6-9.

9. Mwalimu
Mwalimu ni mtu mwenye ujuzi wa kufundisha jambo, ni mtu
anayemwelekeza mtu mwingine ujuzi, ufahamu au uelewa. Baba
kama mwalimu kwa familia yake anao wajibu wa kuwafundisha
wanafamilia wake kila lililo jema. Kumbuka yeye ndiye mbeba
maono, ndiye aliyepewa kusudi na Mungu hivyo anao wajibu wa
83
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

kuanza kumfundisha msaidizi aliyeumbwa kwa ajili yake, lazima


aseme naye, amwonyeshe mipaka ya kila jambo na sio kukaa kimya
maana huyo msaidizi hataota. Watoto wasipojulishwa na
kufundishwa maneno ya Mungu hawatajua mambo ambayo Mungu
ameyatenda kwao. Lakini pia si rahisi kwao kumjua Mungu
wanayepaswa kumwabudu, inaweza kupelekea kizazi kijacho
kumwasi Mungu na kushikamana na miungu ya dunia. Waamuzi
2:10-12. Kwahiyo, ukiona maadili katika familia yamemomonyoka,
hakuna imani thabiti kwa Mungu aliye hai au watu wanaiabudu
miungu na kujishughulisha na mambo ya kishirikina hayo ni
matokeo ya udhaifu wa mwalimu wa familia. Hosea 4:9, familia
haiwezi kuwa tofauti na alivyo baba, hali ya baba ndio hali ya
wanafamilia. Naijua misemo ya mwalimu hazai mwalimu au
mchungaji hazai mchungaji, hayo ni maneno ya walioshindwa, lakini
siku zote watoto hujifunza kwa baba.

Kwa kawaida masikio ya watoto wadogo huwa ni macho badala ya


masikio ya kawaida hii ni kwasababu wao hujifunza, hushika na
kutendea kazi zaidi kile wanachokiona kuliko kile wanachokisikia.
Huwezi kuwaambia watoto kutenda mema ambayo mwenyewe
huyatendi ukategemea watayatenda; ukiwa nao au wakiwa mbele
yako wataonyesha wanakuelewa lakini ukiwapa mgongo wanafanya
kile ambacho hata wewe unakifanya. Kwanini, kwasababu watataka
kujaribu kwa nini unawakataza kitu ambacho hata wewe unakifanya;
nia yako ni nini? Kitendo cha akinababa kushindwa kutimiza wajibu
wao katika kuwafundisha watoto wao basi wale walioachiwa
majukumu ya kulea na kufundisha huwafundisha vile watakavyo na
matokeo ya walichofundishwa kikitoka usishangae bali kubaliana na
hali hiyo.

84
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

10. Mfalme/mtawala
Mfalme/mtawala ni nani?
Huyu ni mtu ambaye anasimamia ufalme au utawala.Kuna
uwezekano wa mtawala kuwa mzuri au mbaya, kuwa mtawala mzuri
mzuri au mbaya haiondoi sifa ya kuwa mfalme/mtawala.

Utawala ni nini?
Ni mchakato unaohusisha taratibu za usimamizi na uendeshaji wa
shughuli za kiserikali au taasisi. Mchakato huo hujumuisha namna
maamuzi yanavyofanywa, ushiriki katika kufanya maamuzi,
utekelezaji, usimamizi, ufuatiliaji na ufanyaji wa tathmini. Mtawala
mzuri ni yule anayetawala kwa kuonyesha mifano yaani kwa
kutangulia mbele kwanza na kuwataka wengine kumfuata na
anapoagiza jambo lifanyike afuatilie kuona limetekelezwa kama
alivyoagiza na kama ni tofauti basi atake kujua visababishi; kama
limetekelezwa vizuri, mtekelezaji apongezwe kwa kufanya kazi
kama alivyoelekezwa.

Mtawala mbaya ni yule anayeamua kila jambo mwenyewe bila


kuwashirikisha wengine kwenye utawala wake, yuko radhi
kuwatwika mizigo wenzake ambayo hata yeye hawezi kuibeba.
Maana yake ni kwamba anawaelekeza wengine kutenda mema
ambayo yako mbali naye. Pia hataki kujua wengine wanawaza nini
kuhusu jambo analopendekeza, anaiamini akili yake kuliko ya mtu
mwingine na huwaona walio chini yake wasioweza kitu chochote.
Mtawala wa namna hii anapotoa maelekezo ya kitu gani kifanyike
hupotea, hataki kujua kama utekelezaji umefanyika au haujafanyika.

Baba kama mtawala lazima ujifunze kusikiliza na kufanya uchunguzi


juu ya kile ulichoambiwa au juu ya maamuzi unayotaka kuyafanya ili
kuepuka kufanya maamuzi ya kukurupuka. Hakikisha unalijua jambo
85
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

hilo kwa undani, pata ushauri kwa watu wako wa karibu ili kwamba
usifanya maamuzi ya kukuumiza na kukufanya ujute baadaye.Baba
kama mtawala akianza tabia ya kusikiliza maneno ya uongo kutoka
kwa watu wasiokuwa na nia njema na familia anaweza kusababisha
madhara makubwa kwenye familia Mithali 29:12. Baba awe mfano
wa kuigwa katika mwenendo na usemi, asiwe mtu wa nia mbili, awe
mwenye kuisimamia nyumba yake vema,ajuaye kutiisha watoto
wake katika maadili yampendezayo Mungu na hata wanadamu pia.

SURA YA TISA
MAMBO YANAYOMHUSU
MWANAMKE
Kuna mambo muhimu yanayomhusu mwanamke ambayo
mwanamume anatakiwa kuyajua kabla hata hajafikiria kumtafuta
kama msaidizi au mwenza wa maisha, miongoni mwa mambo hayo
ni pamoja na mwanamke ni nani? Ni upi mwenendo na msingi wa
kutenda au kutotenda kwake? Kwa nini aliumbwa? Na aliumbwa
kwa kusudi gani? Utakumbuka Mungu anasema “si vema mtu huyu
aishi peke yake” Kwahiyo ina maana ili majukumu aliyopewa
mwanamume yatimizwe vizuri ni lazima mwanamke awepo. Hivyo
basi kila kitu alichonacho mwanamke alipewa ili kumsaidia
mwanaume kutimiza wajibu wake ndio maana kuna msemo kwamba
“kwa kila maendeleo ya mwanamume nyuma yake yupo mwanamke”
86
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

Ni muhimu mwanamke kuwa mwangalifu na mshauri mzuri kwa


mume wake ili aweze kumwakilisha Mungu vema katika majukumu
mbalimbali aliyopewa. Mwanamke akiwa mwongo, mchonganishi na
msengenyaji atakuwa anaibomoa nyumba yake kwa mikono yake
mwenyewe. Kwasababu mwanamume anamtegemea kama mshauri
wake, hivyo akimshauri ushauri wa hovyo atamkosesha na
kuikosesha familia.Mwanamke aliumbwa kuwa mlinzi wa
mwanamume ili asifanye makosa yatakayoleta madhara makubwa
kwa familia.Mungu ameweka wazi juu ya wajibu huo katika
Yeremia 31:22.

9.1 Sifa zinazomtofautisha mwanamke na mama

Mwanamke ni mtu yeyote mwenye jinsi ya KE, mama pia anakuwa


mwenye jinsi ya KE lakini ana sifa za ziada zinazomtofautisha na
mwanamke. Pia ipo tofauti kati ya kuwa mwanamke na kuwa mama,
mama ni daraja la juu lenye maana ya kujali, kulea, kuthamini,
kuheshimu na kupenda. Mama ni azaaye, ni mzazi wa kike ambaye
wajibu wake muhimu ni kuzaa. Katika mila na desturi binti
anapoolewa ndugu zake humtakia baraka za uzazi kama jambo la
pekee sana kwake Mwanzo 24:60. Wanapomtakia baraka za uzazi
haimaanishi zingine hawazijui au hazina maana, wanajua lakini zote
huwa hazitimilizwi kama uzazi haupo.Mwanamke aliumbwa maalum
kwa ajili ya kupokea mbegu za uzazi kutoka kwa mwanamume ili
kuzitunza katika tumbo la uzazi, azikuze na kisha azae mtoto.

Kuzaa ni jambo linalompa heshima na thamani mama kwani ndilo


linalomtofautisha na wanawake wengine. Ikitokea mwanamke
aliyeolewa akitazamia kuzaa akakosa mtoto huwa anasumbuka sana
moyoni kuliko mwanamume. Wataalam katika masuala ya saikolojia
87
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

ya wanawake wanasema “tumbo la uzazi la mama lina uhusiano na


tabia yake ya kike”.

1. Msaidizi wa mwanamume
Ndani ya mama Mungu ameweka nguvu na uwezo wa kumsaidia
baba kutimiza majukumu yake kuelekea kulitimiliza kusudi na
majukumu ndani ya familia kama ulivyo mpango wa Mungu. Uwezo
huu aliopewa mama ni muhimu ukitumika vizuri kwa makusudi
yaliyokusudiwa na siyo kule kutaka kuwa sawa na baba.Wakati
mama akijua na kujali kuwa yeye ni msaidizi mwanamke atataka
kuwa sawa na mwanamume, hakubali hata kidogo kuitwa msaidizi
wa mwanamume, kwake hilo analiona kama ni kushuka thamani, na
mara zote anapigania haki sawa kati yake na mwanamume.
Miongoni mwa usaidizi wa mama kwa baba ni pamoja na:-

2. Kushawishi
Inaaminika kwamba theluthi moja ya siku za maisha ya mwanadamu
yeyote aliyezaliwa duniani huitumia akiwa mikononi mwa mama,
mama ndiye humfundisha mtoto mambo mengi ya awali kuliko mtu
mwingine yeyote, Ezekiel 16:44 hapa ndipo penye umakini sana.
Kama mama akishindwa kushika nafasi yake kubaki na nafasi kama
mwanamke basi tegemea watoto wako kuwa katika mazingira
ambayo si yale uliyoyatazamia. Maandiko yanathibitisha kwamba
mwanamke/mama ana maneno yenye nguvu kubwa ya ushawishi,
yaani ni kwamba mwanamke/mama akiamua kukukamata kwa
maneno yake hakuna anayeweza kufurukuta, lazima unasalimu amri
Mithali 7:21,“Mategemeo yangu ni kwamba uwezo huu mama
atautumia kuwafundisha watoto wake na sio kinyume chake”.

3. Mzalishaji wa mali
88
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

Mungu kwa kufahamu kwamba mwanamke ameumbwa kwa ajili ya


mwanamume aliweka uwezo mkubwa wa akili ya uzalishaji mali
ndani yake ili kwamba uwezo huo utumike kumshauri mwanamume
namna ya kutafuta mali kwa ajili ya kuitunza familia Mithali 31:10-
13.Uwezo huu alionao mama unakusudiwa kutumika kumsaidia baba
ambaye ni kichwa cha familia ili kutimiza majukumu na wajibu
wake kwa familia na sio kukinzana kwani kufanya hivyo si mpango
wala kusudi la Mungu. Mama na baba katika mkitadha huu
wanatazamiwa kusikilizana kwa ajili ya mstakabali mzuri wa familia
na hasa wale waliowaleta duniani.

4. Mvumilivu
Kwa namna mwanamke alivyoumbwa ni mwenye uwezo mkubwa
wa kuvumilia hali na changamoto mbalimbali anazopitia. Mama ana
uwezo mkubwa wa kuchukuliana na hali yoyote hata watu wale
ambao kwa macho ya kawaida unaona kwamba hawakustahili na
haiwezekani kuwavumilia lakini anavumilia kwa kuamini kwamba
ipo siku watabadilika. Mfano mzuri wa uvumilivu ni pilikapilika za
ujauzito pamoja na kujifungua. Manesi na madaktari wanajua hili,
mama anapojifungua anaapa viapo vyote vya kutorudia lakini baada
ya miezi au miaka kadhaa unamkuta na mimba nyingine. Mambo
haya na mengine mengi yanaonesha uwezo mkubwa wa uvumilivu
alionao mwanamke. Uwezo huu wa uvumilivu kama ukithaminiwa,
kutunzwa na kulindwa unaweza kumsaidia mwamume katika
kutimiza wajibu wake.

5. Mtunza uhai
Kwa kawaida mama ni mwangalifu sana linapokuja suala la kutunza
uhai wa mtoto. Mama anayenyonyesha kwa mfano akisikia mtoto
analia akiwa ndani anaweza kujua kilio hiki mtoto kakojoa, ana njaa
89
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

au kuna jambo la hatari limempata. Kwa kawaida mama yuko radhi


kufa ili mtoto wake apone. Mara nyingi mama akiwa amebeba mtoto
hata akianguka hujitahidi sana mtoto awe salama. Mama aliyezaa
anamwangalia na kumtunza mtoto kwa uangalifu sana, muda wote
mawazo yake humfikiria mtoto kuliko kitu kingine chochote. Mara
kadhaa mtoto anapougua si ajabu pia kumkuta mama naye akiwa
kama mgonjwa. Na hata akiwa na usingizi wa namna gani ni
agharabu sana kusikia mama alimlalia mtoto.Na kwasababu ya kujali
uhai wa mtoto, uzoefu unaonyesha kwamba mama anapokuwa
amejifungua sehemu ya upendo wake ambao angempenda mumewe
huupunguza na kuuelekeza kwa mtoto wake.

6. Kunyonyesha
Afya na kukua kwa mtoto hutegemea maziwa ya mama. Maziwa ya
mama ndicho chakula pekee, bora na kamili kwa ajili ya makuzi ya
mtoto. Wataalam wanasema mama anatakiwa kumnyonyesha mtoto
wake ndani ya lisaa limoja baada ya kujifungua na aendelee
kumnyonyesha maziwa bila kumpa kitu kingine chochote ndani ya
miezi sita ya mwanzo.Maziwa ya mama ndiyo yanayosaidia
kutengeneza ubongo wa mtoto,kinyume chake kama mtoto
hatanyonyeshwa ipasavyo ubongo wake hautakuwa kwa kiwango
kinachotakiwa na madhara yake ni kwamba ubongo wake hautakua
katika kiwango kilichotazamiwa.

Katika kipindi hiki ni wajibu wa baba kumsaidia na kuhakikisha


kwamba mama anapata mahitaji yote ya msingi na mhimu, katika
kipindi hiki cha siku 1000 yaani kuanzia mimba inapotungwa mpaka
mtoto anapotimiza miaka miwili baba ajitahidi kuhakikisha mama
anapata matunzo na mahitaji mhimu kwa ajili ya afya yake na mtoto.
Kama mama atakosa matunzo muhimu katika kipindi hiki ni rahisi
90
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

sana afya yake kudhoofu na kama afya ya mama itadhoofu kuna


uwezekano mkubwa wa kuathiri afya ya mtoto.

Jambo moja ambalo wanaume wengi hawalitilii mkazo ni kipindi


mama ananyonyesha au akiwa mjamzito, si rahisi kufahamu kwamba
mama anakuwa na mtu mwingine ndani yake ambaye mahitaji yake
ya msingi anayapata kupitia kwa mama, matokeo yake ni kwamba
kama mama hatapata matunzo ya kutosha mtoto atadhoofu, kwa
kuwa mwili wa mama hautaweza kumhudumia mtoto mpaka
wenyewe uwe umetosheka.Kwahiyo katika kipindi hiki tunategemea
baba atumie cheo cha mtawala ili kuhakikisha kwamba watawaliwa
wanapata kila kitu kizuri wanachokihitaji kwa ajili ya ustawi na
uimara wa afya zao.

7. Mbembelezaji na mfariji
Mama kwenye familia tunategemea akitaka jambo kutoka kwa baba
atumie uwezo wake wa kubembeleza kwa kuwa ndani yake Mungu
ameumba uwezo huo Isaya 66:12-13 lakini akina mama wengi
wameshindwa kufanya hivyo badala yake wanatumia nguvu na
ubabe ambao kimsingi Mungu hajawapatia. Hatutegemei mama awe
mkali kama moto wa kiangazi ndani ya nyumba,mama anategemewa
kuwa mfariji ili kwamba baba anaporudi akiwa amevurugwa apate
faraja kutoka kwake.Ukweli ni kwamba wanawake wengi
wamewapoteza na kuwafukuzia mbali kinababa kwasababu ya ukali.
Hii ni kwasababu hakuna mwanamume ambaye yuko tayari
kudhalauliwa. Na akikuponyoka kutokana na ukali wako kumrudisha
utahitaji nguvu ya ziada. Lakini jiulize, kwanini utumie nguvu kubwa
wakati uwezo wa kumweka chini ya himaya yako kwa
kumbembeleza na kumfariji unao?

91
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

8. Mpole
Upole katika biblia lina uhusiano wa karibu na unyenyekevu pamoja
na uvumilivu. Hii ni tabia yenye nguvu sana ambayo iko kinyume na
ubinafsi na kiburi, upole humsaidia mtu kuvumila lawama hata kama
hakuzistahili huku akisamehe na kuachilia. Mama anayejitambua na
ambaye anaijua nafasi yake kama mama hii ndiyo silaha na nguo za
kuijenga ndoa yake.Mke ananyenyekea kwa mumewe kwa kuwa
anajua kuwa mume ni kichwa cha familia, anatii kama kumtii Kristo
lakini mwanamke wakati wote anataka haki sawa, ulinganifu,
kulingana na kuwa sawa jambo ambalo kwenye ndoa linaifanya
isambalatike. Mwanamume ukitaka kupima urefu na upana wake
mguse kwenye hili eneo la kutaka kuwa sawa naye, hapo utaona na
kugundua rangi zote alizonazo, usijaribu wala kuruhusu kujaribiwa
katika eneo hili kwa kutaka kuwa sawa na mumeo.Wataalamu
wanasema sura nzuri ya mwanamke inampa 75% za kuolewa lakini
upole na unyenyenyekevu zinampa 100% za kudumu kwenye ndoa.

9. Mwalimu
Maana na fasili ya mwalimu tumekwisha kuieleza katika kipengele
kilichotangulia hapo juu, hivyo mama anatakiwa kuwa na sifa za
mwalimu ambazo ni pamoja na zifuatazo:-
a. Mzazi/mlezi
b. Hakimu/mwamuzi
c. Daktari
d. Mshauri

Mama kwenye nyumba (ndoa) anatakiwa kuwa na sifa hizi, sio kila
mara mama atakuwa hakimu, na sio mara zote atakuwa daktari.
Anatakiwa kuuvaa uhusika kulingana na mazingira. Lazima ajue
mazingira aliyomo na kujua aina gani ya sifa ifanye kazi katika
92
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

mazingira hayo.Mfano baba katoka huko atokako kavurugwa,


kachoka tabia (sifa) inayotakiwa kutumika itakuwa ulezi na sio
ualimu.Maana ukianza ualimu utataka kumsahihisha kwenye maeneo
ambayo unaona na kudhani hakufanya vizuri,ukithubu utaambulia
kipigo.Na huu ndiyo umekuwa ugomvi mkubwa sana kwenye ndoa
nyingi. Ni muhimu kuyajua mazingira uliyomo na namna ya kucheza
na sifa hizo za mwalimu ili kuepusha kuchanganya mafaili.

10. Malikia
Malikia ni nani?
Ni mke wa mfalme, anastahili heshima kwa kiwango sawa na cha
mfalme. Anatumikiwa na wakati mwingine huwaamrisha walio chini
yake ili kutekeleza matakwa yake au yale ya mfalme. Mama kwenye
nyumba ipo siku na wakati anavaa hiki cheo, muda huo kutenda
kwake lazima kufanane na malkia.Sio anakuwa malkia halafu
anatenda kama muuza matembele, haiwezekani.Maana yake ni
kwamba kwenye nyumba unakaa na kutumikiwa,unaagiza
unachotaka kifanyike kisha unafuatilia kuona kama kimefanyika
kama ulivyoagiza.Bahati mbaya sana hiki ndicho cheo pekee
mwanamke anakitamani na kukipenda kuliko vyeo vingine. Anataka
kuamrisha kila mtu ndani ya nyumba mpaka na mfalme; hii ni ajabu!

Kumbuka malkia ni mke wa mfalme na siyo mfalme, hivyo hawezi


kumwamrisha mfalme,lakini anaweza kumwomba mfalme kwa
kumbembeleza ili atendewe jambo fulani analotaka kutendewa,
jitafakarishe na ukumbuke malkia Esta alivyofanya.

93
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

SURA YA KUMI
TOFAUTI ZA KIMAUMBILE KATI YA
MWANAMUME NA MWANAMKE
Kimaumbile mwanamume na mwanamke wametofautiana sana.
Utofauti huo wa kimaumbile unahusu pia utofauti katika mahitaji
yao, jambo ambalo linaonekana kuwa la muhimu kwa mwanamume
linaweza lisiwe na umuhimu ule ule kwa mwanamke. Ni muhimu
kwa mwanamume na mwanamke pia kujifunza na kuzijua tofauti hizi
za kimaumbile zilizopo kati yao. Kuzijua kunakusaidia kuishi kwa
amani maana jambo likifanyika utakuwa unajua huyu ndivyo
alivyoumbwa na Mungu hakuna namna ninavyoweza kumbadirisha
ila naweza kumwombea.

Kuzijua tofauti hizi kutamfanya mwanamume na mwanamke


kujitambua wao ni nani pamoja na kujua namna ya kutendea kazi
wajibu wao kila mmoja kwa nafasi yake.Utofauti wetu wa
kimaumbile ndio unaochochea uhitaji tulionao na makusudi ya
kuumbwa kwetu. Ni muhimu kuzifahamu tofati hizi ili ituwezeshe
kujua jinsi ya kuishi na kumhudumia mwenzi inavyostahili,
miongoni mwa tofauti zilizopo kati ya mwanamume na mwanamke
ni kama inavyooneshwa kwenye jedwali hapa chini.

Totauti Mwanamume Mwanamke

94
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

Mpangilio Ubongo wa Ubongo wa mwanamke


wa ubongo mwanamume umeumbwa bila kuwa na
umeumbwa ukiwa na vyumba vidogovidogo
vyumba vidogovidogo kama ulivyo ubongo wa
ambapo kila chumba mwanamume, isipokuwa
kidogo kimoja katika ubongo wake
hushughulika na jambo mambo yote
moja maalum. yameshikamanishwa
pamoja ndiyo maana
anaweza kufanya mambo
mengi kwa wakati mmoja
bila kuathirika.
Akiwa anafanya jambo Yeye hujisikia vizuri
moja likamshika anapofanya kazi zaidi ya
mawazo vizuri ukijaribu moja kwa wakati
kumpa taarifa nyingine mmoja.Sote ni mashahidi
wakati huo hataweza wazuri wa hili, siyo rahisi
kuielewa kwa haraka. kumkuta mama nyumbani
Mwanamke ni muhimu akifanya jambo moja na
kulijua hili, kwa sababu kulimaliza kisha anaanza
inakuwezesha kugundua lingine, mara nyingi
mwenzangu hapa kuna unamkuta anafagia,
kila dalili kwamba wakati huo huo anapika
hayuko sawa na ni kama na kufua pia. Hii kwa
kuna kitu kimeshika mwanamume
ubongo wake usijaribu haiwezekani hata kama
kupeleka hoja yoyote inamgharimu kifo.

95
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

Akipewa mambo ya Anaweza kuratibu mambo


kuratibu hutaka lifanyike mengi kwa wakati
moja kwanza likiisha mmoja. Hahitaji jambo
ndipo jingine lianze na kufanyika kwanza kabla
akichoka au jingine halijaanza,
kukasirishwa na jambo ameumbwa kwa uwezo
anahitaji sehemu ya kwamba anaweza kufanya
kuwa peke yake ili yote kwa mara moja.
kutulia na kutuliza Uwezo huu wanaume
kichwa bila bughudha. lazima kuukubali na
Kwahiyo mama wakati kuuthamini maana Mungu
kama huu hakikisha baba alishawapatia hawa mama
wa watu hapati zetu, kuubeza ni
usumbufu wala kujisumbua.
bughudha kutoka kwako Akiwa amechoka au
au kwa watoto maana amekasirishwa na jambo
kufanya hivyo anaweza kuwaza na
kutamwongezea kusema maneno mengi
matatizo na pengine kwa wakati mmoja. Kwa
madhara zaidi yanaweza kuwa ni hivyo basi, baba
kutokea. Mama wewe jitahidi uwe mbali kidogo
ndiyo tulizo lake, ili aseme kila anachotaka
ulipewa wajibu na kusema ili roho yake
Mungu kumlinda hebu ifurahi maana kusema
hakikisha unamlinda huko ndiko
katika kipindi hiki. kunakomwezesha kutoa
sumu mwilini, usijaribu
kumnyamanzisha maana
hutaweza.

96
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

Hitaji la Hitaji la msingi kwa Na hata kwa mwanamke


msingi mwanamume lina hitaji la misingi lina
vipengele vitatu vipengele vitatu ambavyo
ambavyo ni:- ni:-
a.Heshima, a. Kupendwa, kama
mwanamume kila alipo ilivyo kwa mwanamume,
siyo tu kwamba anahitaji mwanamke pia siyo tu
bali anadai kuheshimiwa kwamba anahitaji bali
kwa gharama yoyote ile, anadai kupendwa kwa
hii inamfanya ajisikie na gharama yoyote ile,
kuuona uthamani wa kwake kupendwa ndilo
kuwa mwanamume na jambo muhimu sana
kiongozi kwenye kuliko mengine
familia. Anataka watu anayoweza kutendewa.
wote ndani ya nyumba Mwanamke akioneshwa
wajue na waliishi hilo. upendo wa ndani hisia
Anataka kila wakati zake zinakuwa
waheshimu na kuthamini zimegusika lakini akikosa
uwepo wake hata kama upendo kila kitu
hatimizi wajibu wake kinavurugika Kolosai
kama baba, ameumbwa 3:19. Kwahiyo baba
hivyo hakuna namna kwenye nyumba
tunavyoweza anawajibika kuhakikisha
kumbadirisha kwahiyo upendo wake kwa mkewe
mwenye wajibu wa unaonekana na siyo
kuwajulisha na kufikirika. Hakikisha kila
kuhakikisha kwamba mara unaonekana na
baba huyu ndani ya kuonyesha kwamba
nyumba anapewa unampenda mkeo kwa
heshima anayoistahiri ni maneno na vitendo, yaani
mama kwenye hiyo yale usemayo yathibitike
nyumba Kolosai 3:18 kwa vitendo. Kutompenda
97
mkeo ni sawa na
kutojipenda pia Waefeso
5:28
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

b. Hamu ya b.Kuzungumzishwa, kwa


kujamiiana, Kwa kawaida mwanamke kwa
namna Mungu namna alivyoumbwa na
alivyomuumba Mungu hapendi
mwanamume alimwekea kuambiwa au kutumwa
hamu ya kutaka kwa kuagizwa,
kujamiiana wakati kuamrishwa,
wowote na hili kushurutishwa au
limethibitishwa na kulazimishwa bila
wataalam kwamba hamu upendo. Akifanyiwa
ya mwanamume hivyo anapoteza
kujamiiana iko juu sana mwelekeo na uwezo wake
ikilinganishwa na wa kuwaza na kutenda
mwanamke. Anaweza kazi unapungua. Anahitaji
kujamiiana wakati kuzungumzishwa,
wowote na mahali kusikilizwa na kupeana
popote bila kujali, habari. Mwanamume ni
akishachemka hajiulizi lazima utenge muda wa
mara mbili kama sehemu kuzungumza na mke
inafaa au haifai na hili wako hata kama una
ndilo jambo lililoshika shughuli nyingi kiasi gani
sehemu kubwa ya hisia maana kutofanya hivyo
zake. Kisaikolojia kunafanya uwezo wa
mwanamume anaweza akinamama wengi
kumaliza au kuhisi hamu kwenye ndoa kupungua
ya kujamiiana kwa na kwa kuwa wanataka
kumtazama mwanamke kutimiza majukumu kwa
hata kama hajakutana kutumia uwezo wao hitaji
naye 2Samwel 11:2-4 hili la kuzungumzishwa
na Mathayo 5:27-28. huamua kulitafuta mahali
pengine wanapoona
panafaa.
98
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

c. Mwenzi wa c. Huba na mapenzi


kushirikiana katika motomoto, yapo mambo
burudani, kila ambayo mwanamke
mwanadamu ameumbwa akitendewa na
na hobi zake. Wapo mwanaume hujihisi
wanaopenda michezo kupendwa, mambo hayo
wengine, siasa. Hobi ni sio makubwa sana ni ya
mambo ambayo kawaida sana, miongoni
humfurahisha na mwa mambo hayo ni
kumburudisha mtu kama kuletewa zawadi
ambayo yanaweza hata kama zawadi hiyo ni
kumfanya atumie muda ndogo au kutembea
mwingi kuyazungumza pamoja njiani.
au kuyatenda. Mwanamke anapenda
Mwanamume anapenda unapotembea naye uwe
kuwa na mwanamke unamtambulisha kwa
ambaye ana hobi kama watu kwamba huyu ndiye
zake, hivyo mwanamke mke wangu. Lakini ni
tumia akili yako kujua ajabu sana kwamba wapo
hobi za mume wako ni baadhi ya wanaume tangu
zipi uweze kushirikiana wawepo hawajawahi
naye katika hiyo. Sio kutembea na wake zao
lazima kwenda naye barabarani yaani hata
kwenye vibanda vya wake zao wakitaka
kutazama mpira kama kuwasubiri wao wanatoka
ndiyo hobi yake lakini mbio kama wakimbiza
ukaonesha kusikitika mwenge, huu ndio wakati
pale anapokuambia team wako wa kubadilika.
yake imefungwa, hata
siku moja usijalibu
kutaka kumkebehi pale
anapokuambia team
99
yangu leo imefungwa.
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

Tofauti ya 1. Mwanamume husema 1.Kwa kawaida


kusema na kile anachowaza moyoni mwanamke husema
kusikia mwake, kwahiyo anavyohisi (feelings),
ukisikia mwanaume kwahiyo akisema neno
kasema kitu ujue hicho fahamu kwamba linatoka
ndicho kilichoko kwenye hisia zake. Kama
mawazoni mwake. akikuambia sijisikii
vizuri, usihoji maana yake
anahitaji huduma ili
kurekebisha hilo.

100
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

2. Mwanamume ana 2. Mwanamke anao


uwezo wa kuzungumza uwezo wa kuzungmza
maneno kama 13,000 maneno kama 25,000 kwa
kwa siku, anavutwa na siku, ndio maana
kushikwa haraka anapenda
kusikiliza maneno au kuzungumzishwa ili
mambo yenye mantiki au kwamba maneno hayo
hoja zenye ushawishi. yaishe. Hata kama baba
Kwake jambo ambalo hushindi nyumba
halina mantiki hulipuuza usisahau 25% ya maneno
haraka ndio maana hayo anatakiwa
hapendi kusikiliza jambo kukuambia wewe
moja mumewe. Wakati
linalorudiwarudiwa. unapozungumza naye au
Kwahiyo ukitaka unapomwambia jambo
kumkamata mwanaume anakusikiliza na wakati
zungumza jambo mara huo huo anatafuta kujua
moja, na hakikisha hasa ni nini nia yako ya
kwamba lina mpangilio moyoni, anajitahidi
wa kimantiki. Hivi kutaka kujua kilichopo
hujawahi kumpelekea nyuma ya neno hilo
hoja mume wako ulilomwambia. Kwa
akabaki anakushangaa kawaida mwanamke
kwanini umekwenda na anavutwa haraka
hoja hiyo kwake? kusikiliza maneno
Wakati yeye yanayogusa hisia, hachoki
akikushangaa wewe kuyasikiliza hata kama
unaona kwamba hicho yanarudiwarudiwa. Kwa
kilikuwa kitu mhimu mfano anapoambiwa na
sana kufanyika; ni mwanaume nakupenda,
mhimu sana kuzifahamu hachoki hata kama
hizi tofauti kwa maslahi linarudiwa rudiwa mara
101
mapana ya ndoa zetu. kwa mara.
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

Tofauti Kwa kawaida Anapokuwa na jambo


katika mwanamume jambo ambalo halijapatiwa
kutatua likimchosha na kila ufumbuzi unaomridhisha
matatizo akijaribu kulifikiria moyoni mwake hata kama
haoni namna ya kulipatia litaonekana limekwisha
majibu huamua kuliacha kwa kutumia utaratibu
na kuanza jingine. mliojiwekea lakini kwake
Hufanya maamuzi linakuwa halijaisha.
haraka na kuanza jambo Mawazo yake huendelea
jingine hata kama kuzunguka, kufikiri na
analoliacha halijapata kurudia rudia juu ya
ufumbuzi alioukusudia. jambo hilo mpaka
Kwa kifupi wanaume ufumbuzi wa kumlidhisha
hawana uvumilivu au utakapopatikana.
kuvuta sibira kwamba Wanawake katika maisha
hili linaweza kukamilika wana uvumilivu sana,
au kuzaa matunda anataka kuona jambo
baadaye. likifanyika kwa
kushughulikia chanzo na
sio tatizo.

102
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

Haiba na Kwa mwanamume Mambo yanayojenga


kujikubali mambo yanayojenga haiba au mwonekano
haiba na kujikubali ni wake wa nje na kujikubali
tofauti na yale ni tofauti na yale
yanayojenga haiba ya yanayojenga haiba ya
mwanamke. Cheo, kazi mwanaume. Kwa
au shughuli mwanamke watoto,
inayomwingizia kipato mavazi na vitu vya
na kumwezesha nyumbani kwa ujumla ni
kuendesha maisha vizuri vitu mhimu sana kwake.
ndio mambo Vitu hivi humpa furaha,
yanayompatia heshima ujasiri, kujikubali na
na kujikubali. kujiamini. Mambo haya
Anapokuwa hana kazi ndiyo yanayojenga
maalum inayomwingizia thamani yake kama
kipato humfanya ajisikie mwanamke, ndio maana
kunyanyasika sana na ugomvi mwingi kwenye
hukosa ujasiri. Ndio ndoa huanzana na mavazi.
maana ni nadra sana Ni aghalabu sana kusikia
kuona mwanamume mwanamke na
akiridhika kuhudumiwa mwanamume
na mke hata kama wanagombana kwa kuwa
mwanamke huyu mwanamume huyu hataki
anampa heshima zote kujenga, ila utasikia huu
bado mawazoni kwake ni mwaka wa pili sijaona
anaona kama kuna kitu nguo yake bila kujali
kinapungua. anazo nyingi mpaka
zinauliana.

103
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

Mchakato Mwanaume anawaza Mwanamke anahisi


wa kuwaza kwanza kisha anahisi kwanza kisha anawaza
baadaye. Mawazo yake vile alivyojisikia. Anao
hujengwa kwenye hoja uwezo wa kutunza
zenye ushawishi na kumbukumbu za matukio
mantiki, kwa kawaida na mambo madogo
anazungumza kile madogo kwa kiwango
anachowaza. Anaweza kikubwa kuliko
kukumbuka matukio mwanamume. Hawa ndio
mengi lakini mambo au wanajua tarehe za
maelezo madogomadogo kuzaliwa mtoto na kila
anayasahau kwa urahisi. kilichotokea siku hiyo
Ukitaka kupima hili Luka 2:16-19
muulize akueleze watoto
wake walizaliwa lini na
kipi kilitokea siku hiyo,
hana majibu

SURA YA KUMI NA MOJA


NAFASI YA MWANAMKE KATIKA
NDOA KIBIBLIA
Ukitazama makanisani, katika jamii na hata maofisini suala la
migogoro ya ndoa limekuwa jambo la kawaida. Siku hizi hata wale
walioapa kwamba hawataachana mpaka kifo nao huachana au
kupeana talaka limekuwa jambo la kawaida sana. Wakati umefika
ambapo kila aliye wa Bwana ijulikane! Je tumesahau kwamba sisi si
wa ulimwengu huu, na shetani amewapofusha wanandoa kwa kuwa
104
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

hawazijui nafasi ambazo Mungu amewapa ili waweze kulitimiza


kusudi jema. Ukisoma Biblia utagundua katika ndoa mwanamke
amepewa nafasi na mwanaume pia ili kuhakikisha ndoa inatimiza
kusudi lake. Kibiblia mwanamke amepewa nafasi nyingi zaidi ya
mwanamume nafasi hizo ni kama ifuatavyo:

Mwanamke kama mjenzi kwa mumewe, mwanamke kama msaidizi,


mwanamke kama Mleta kibari kwa mumewe, mwanamke kama
mshauri wa mumewe na mwanamke kama mlinzi kwa mumewe.
Hebu tusome Mithali 14:1,”Kila mwanamke aliye na
"hekima" huijenga nyumba yake; Bali aliye "mpumbavu" huibomoa
kwa mikono yake mwenyewe",Neno nyumba katika mstari huu
linamaanisha ndoa.Mwanamke amepewa nafasi katika ulimwengu
wa roho kujenga nyumba kwa mikono yake. Ikiwa kinamama
wataamua kukaa katika nafasi zao, ukweli ni kwamba ndoa zitapona
na kanisa litaimarika.

"Mpumbavu" ni mtu yule anayejua anachopaswa kufanya lakini


hakifanyi. Sikia mama neno hili ambalo Roho anakukumbusha,
simama katika nafasi yako katika ndoa, nafasi mojawapo ni kuijenga
nyumba yako, kumbuka kuwa kama kuna suala la kujenga, uwe na
uhakika, si suala la siku moja, bali ni suala la kila mara panapotokea
ufa. Huwezi kujenga nyumba ambayo imekamilika, bali unajenga
nyumba ambayo haijakamilika. Hivyo hekima yako inahitajika pale
ndoa yako inapokuwa katika changamoto ili ujenge mahali penye
nyufa. Mambo yafuatayo yatakusaidia kuijenga nyumba yako:-

11.1 Utiifu kwa mumeo


Maandiko yanasisitiza wanawake kuwatii waume zao Waefeso 5:22-
24, 1Petro 3:1.Mitume waliandika maandiko haya ili kuwaonya
wanawake kutokana na mienendo yao mbele za waume zao kitabia
105
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

na hasa katika suala zima la utiifu.Bahati mbaya baadhi ya


wanawake sio watiifu kwa waume zao na tena wengine wana dharau
kubwa sana.Ni mhimu kufahamu kuwa mke si mke bila mume, na
mume si mume bila mke.Hata siku moja ndoa yako haiwezi
kujengwa kwa kiburi na dharau.Najua unaweza kusema tabia zake
zinanifanya nimdharau na kumsema vibaya.Suala siyo tabia zake,
bali ni wewe kutumia hekima katika kukabiliana na tabia zisifofaa
alizonazo mumeo kwa kuwa kumdharau ni kuendelea kubomoa na si
kujenga, ni kuendelea kuleta tatizo na siyo kutatua tatizo.Sikia ewe
mwanamke, maandiko yanatuambia katika Waefeso 5:22, "Enyi
wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu".

Ili mwanamke aweze kujenga nyumba yake hana budi kumtii


mumewe, tena amtii kama vile anavyomtii Bwana wetu Yesu Kristo.
Hili si jambo dogo, ni jukumu kubwa lakini lenye baraka na ushindi
kwenye ndoa.Naam haijalishi mume wako yukoje usionyeshe
dharau, mtii tu maana ndiye mume wako huba mbadalaambaye
unatakiwa kumtii kama kumtii Kristo.

Mtume Petro anawaonya wanawake akisema ‘kadhalika ninyi wake,


watiini waume zenu; kusudi, ikiwa wako wasioliamini neno,
wavutwe kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile neno’ 1Petro 3:1.
Sijui kama msomaji wangu unaona uzito uliopo kwenye mstari huu.
Kwa lugha nyepesi utiifu wa mke kwa Mume unawafanya wengine
kumwamini Yesu tunayemtumaini. Naam kukosa utiifu kwa mumeo
kunawazuia wengine kumwamini Yesu, je unajua gharama ya
kuwazuia wengine kumjua Kristo kwasababu ya kukosa utiifu kwa
mumeo (asomaye na afahamu siri hizi).

Fahamu kwamba dhaharau ni sumu kwenye ndoa yako mama, jizuie


kabisa.Naam utiifu ndio jawabu la kila kitu kwa mwanamume,
106
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

nataka kukuhakikishia kwamba wanaume wanachokitafuta kwa wake


zao ni utii na siyo elimu zao, uchumi wao wala madaraka.Naam
kumdharau mumeo ni kubomoa nyumba yako, ni kumruhusu Shetani
kuharibu ndoa yako, ni kumuingizia mume wako fikra za wanawake
wengine tofauti na wewe.Unadhani ni kwa nini siku hizi kina mama
wengi hawataki kuwatii waume zao? Wanategemea kweli ndoa zikae
salama wakati mioyo yao imejaa dharau, kiburi na visasi
visivyoisha? Ndivyo neno la Bwana linavyotufundisha?Sikia
mwanamke jambo hili, haijalishi mumeo anakufanyia vituko gani,
ikiwa kweli Bwana Yesu ni tegemeo lako, hutajaa dharau na kiburi
kwa mumeo.Wewe unachopaswa kufanya ni kuonyesha kuwa
unamtii tena kama kumtii Bwana wetu Yesu.

Umeona mwanamke anapokuwa mtiifu kwa mumewe kinachotokea?


Maandiko yanasema,"mwenendo wa mke ukiwa vizuri; unaweza
kumvuta hata mume asiyeamini. Mume wako akigundua unamtii
toka moyoni pasipo unafiki nakueleza utashangaa kitakachotokea.
"Utii wako ni mbinu mojawapo ya kuijenga ndoa yako. Usikubali
Ibilisi akudanganye na hila zake,wewe mtii mumeo."Usipomtii
mumeo" unatenda dhambi. kwa nini kwasababu "dhambi ni uasi"
1Yohana 3:4, kwa lugha nyingine unaasi maagizo ya Mungu ya
kumtii mumeo.Maandiko hayasemi umtii mume anayemwamini
Bwana Yesu, bali hata kama hamchi Mungu wewe "mtii tu". Mungu
akutie nguvu na hekima uweze kujenga ndoa yako.

11.2 Kutunza siri za ndoa


Katika kuijenga ndoa ni lazima ujifunze kutunza, kuhifadhi na
kuficha mapungufu ya wenza wetu;naam hiyo ndiyo hekima. Baadhi
ya akina mama bila kujali wanaongea na nani, wamekuwa wakieleza
mambo ya ndoa na siri za waume bila hata kufikiri athari yake.
Kufanya hivyo ni kubomoa sio kujenga.Unawajibika kumtunzia siri
107
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

licha ya mapungufu aliyonayo na uzidi kumwomba Mungu kwamba


aiponye ndoa yako. Na hata kama ni muhimu kueleza kwa lengo la
kujenga ni muhimu kuwe na mipaka ya nani unazungumza naye na
nini unamweleza maana si kila kitu wanapaswa kukijua. Katika
kulisistiza jambo hili Paulo anaagiza kupitia kwa Tito kwamba
awatumie wazee wa kike wenye mwenendo wa utakatifu ‘Ili
wawatie wanawake vijana akili, wawapende waume zao na
kuwapenda watoto wao, na kuwa wenye kiasi, kuwa safi,
kufanya kazi nyumbani mwao, kuwa wema, kuwatii waume zao
ili neno la Mungu lisitukanwe’ Tito 2:3-4.

Miongoni mwa vitu ambavyo Ibilisi anatumia ni "kina mama kumpa


nafasi katika kutoa siri za ndani wakidhani watasifiwa au kusaidiwa.
Sikia mama na uelewe, haijalishi mumeo ana mapungufu kiasi gani,
usitoe nje, tunza kwani huo ni udhaifu wa mumeo. Usitumie udhaifu
wake kumpiga nyundo kichwani, utumie kumjenga na kumuombea.
Sijasema kuwa usitafute msaada kwa wapendwa, hapana, ila Roho
akuongoze kwa mtu ambaye ana hekima ya Mungu, si kila mtu
unamueleza mambo ya ndoa yako, linda kinywa chako uwe na siri.
Narudia tena, tunza siri za mume wako hata kama anakutesa.

Ukisoma Tito2:3-5, neno la Mungu linasema ili wawatie wanawake


vijana akili, wawapende waume zao na kuwapenda watoto wao, na
kuwa wenye kiasi, kuwa safi, kufanya kazi nyumbani mwao, kuwa
wema, kuwatii waume zao ili neno la Mungu lisitukanwe" Nataka
uone hili neno, "kuwa wenye kiasi" "self-control".Sikia mwanamke,
jitahidi usiseme mambo ya ndoa yako, maandiko yanasema, uwe na
kiasi katika yale utendayo yakiwemo ya mumeo;unafikiri
unapopeleka siri za mume wako nje unamsaidia? la hasha! Humsaidii
bali unatoa nafasi kwa shetani ili aweze kuwavuruga. Mpende
mumeo na muombee.
108
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

11.3 Matumizi ya kinywa chako


Mara kadhaa nimewasikia wanawake walioolewa wakisema maneno
yasiyofaa kwa waume zao. Nimesikiia wanawake wakiwaita waume
zao wajinga,wapumbavu na mengine ambayo nisingependa
kuyaandika hapa.Ninachotaka ukijue ni hiki, imeandikwa Mtu
atashiba kwa matunda ya kinywa chake. Tambua kwamba mume
wako ana nafasi yake kama mwanandoa kwako, na nafasi mojawapo
ni kuwa kichwa chako.Na ni ukweli usiopingika kwamba maneno
yanaumba kwahiyo ni kana kwamba kila baya unalotamka kwake
unaliumba kwenye kichwa chako mwenyewe na hivyo tarajia
mabaya na uharibifu kwenye ndoa yako.

Fahamu pia kwamba katika ulimwengu wa roho kuna pepo ambao


kazi yao ni kufuatilia maneno/mawazo mabaya ambayo mtu
anayanena ili kuyaumba yatimie. Mfano ukiwa na wazo kwamba
Mume wangu si mzuri uwe na uhakika kuna pepo watakuja juu yako
na kuhakikisha siku zote wanakufanya umuone mume wako mbaya.
Je hujasoma katika Zaburi 36:4 inasema ‘Huwaza maovu
kitandani pake, hujiweka katika njia mbaya; ubaya hauchukii”.
Naam tafsiri yake ni kwamba hali ya sasa ya mtu huyo ni matokeo ya
mawazo yake,naam mwanandoa huyu amewaza na kunena mabaya
juu ya mume wake na kwasababu hiyo ameiingiza ndoa yake kwenye
mabaya.Ni lazima ujifunze kunena mananeo yenye kuijenga ndoa
yako na si kubomoa, ndivyo na nafsi yako, fikra zako zitakapokiri
hivyo,naam ndivyo na BWANA Mungu naye atahakikisha hayo
yanakujia.

Miongoni mwa viungo ambavyo Ibilisi anavitumia kuangamiza


watoto wa Nuru ni pamoja na 'vinywa vyao' au maneno ya vinywa
vyao yasiyo na uzima ndani yao wanayoyatamka bila kujua madhara
109
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

yake. Mithali 18:7-8. Kinywa cha mpumbavu ni uharibifu wake


mwenyewe na midomo yake ni mtego wa nafsi yake. Maandiko
yanasema,maneno yanayotoka kinywani mwa mpumbavu huharibu
nafsi yake na maneno hayo ni mtego wa nafsi yake.Jizuie usimnenee
mumeo maneno mabaya, kwani yeye ni kichwa chako "Zaburi 36:4.
Mpumbavu anaponena bila utaratibu hujiweka katika njia ya
uangamivu na mtu wa namna hii hachukii ubaya. Mungu amekupa
nafasi uitumie kujenga na si kubomoa. Haijalishi mume wako
yukoje, wewe mnenee mema kila wakati Mithali 12:14a "Mtu
atashiba mema kwa matunda ya kinywa chake.

Siku zote mtu hujazwa yale asemayo kutoka kinywani mwake.


Ukisoma Mithali 12:22 midomo ya uongo ni chukizo kwa BWANA
na kuna kunena bila kufikiri.Acha umbeya wewe si wa ulimwengu
huu maana ya kale yamepita sasa yamekuwa mapya. Mithali
13:3, Yeye alindaye kinywa chake huilinda nafsi yake;bali afunuaye
midomo yake atapata uharibifu. Linda kinywa chako mama ili
uilinde nafsi yako na uepuke uharibifu.Ombea kinywa chako na
kikabidhi kwa Bwana ili kitumike kama silaha ya haki.

11.4 MSAMAHA
Ndoa nyingi zina shida kwasababu ya wanandoa kushindwa
kusameheana. Ni kweli kwenye ndoa kuna mambo mengi ambayo
katika hali ya kibinadamu yanaweza kukufanya ushindwe kusamehe,
nami kama Mwalimu sinabudi kukufundisha kile ambacho neno la
Mungu limeelekeza kwamba tafuteni kwa bidii kuwa na amani na
watu wote, Waebrania 12:14.Watu wote ukianza na mumeo,
hatutegemei uwe na mahusiano mazuri na watu wa nje, wakati mume
wako hutaki kumsamehe, utakuwa unajidanganya nafsi yako. Hivyo
bila kujali mumeo/mkeo amefanya kosa gani ni lazima ujifunze
kusamehe na kusahau. Hii ni kwasababu kutokusamehe ni kumpa
110
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

Ibilisi nafasi ya kuendelea kuwavuruga.Si hivyo bali usitegemee


maombi yenu yatakuwa yanasikilizwa wakati kati yenu kuna
vinyongo vitokanavyo na kutokusamehe. Kushindwa kwako
kusamehe kunaharibu mahusiano na Mungu Mathayo 6:14 na kwa
mwanamume kwa kushindwa kwake kukaa kwa akili na wewe kama
mke, maandiko yanasema maombi yake hayatasikilizwa.

Maandiko yanatuasa tuwasamehe waliotukosea kabla hatujaomba


lolote Marko 11:25,26. "Nanyi kila msimamapo kusali, sameheni,
mkiwa na neno na mtu ili baba yenu aliye mbinguni awasamehe
ninyi makosa yenu. Lakini kama ninyi msiposamehe, wala baba yenu
aliye mbinguni hatawasamehe ninyi.’’ Mimi naamini kuwa, mtu
akiweza kuwa na roho ya kusamehe anashinda vikwazo vingi na
atakuwa na afya nafsini mwake siku zote. Ukisoma hayo maneno
utaelewa jambo hili. Ukitaka maombi yako yasikilizwe na Mungu
lazima uwasamehe waliokukosea. Lakini pia usipowasamehe
unatenda dhambi kwa Mungu.

Ukiichunguza hii mistari vizuri haisemi tunatakiwa kuwasamehe


wale wanaojitokeza kutuomba msamaha, inatuhimiza kusamehe bila
kuombwa msamaha.Tatizo linalozikumba ndoa nyingi ni pale
anayetakiwa kusamehe anasema; nimemsamehe mpaka nimechoka.
Unakumbuka wanafunzi wa Yesu waliuliza "Mtu anikose mara ngapi
nami nimsamehe? Hata mara saba? Yesu aliwajibu sikuambii hata
mara saba bali saba mara sabini,wanafunzi wakamjibu,Bwana
tuongezee imani.Hapa Yesu alikuwa anawafundisha wanafunzi wake
kwamba wasamehe hata bila kuombwa msamaha.Haijalishi
unakosewa mara ngapi kwa siku wewe samehe.

Jambo baya zaidi ambalo linalokuwa kwa kasi ni kitendo cha


mwanamke kugundua kwamba mume wake anamkosea naye
111
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

pasipokujua au kwa makusudi analipa kisasi kwa kufanya kama


anavyofanya mumewe. Usilipe kisasi mwanamke, kisasi ni cha
Bwana, mume wako akikosea wewe mbebe kwenye maombi. Najua
utanimbia, "nimeomba mpaka nimechoka, ni sawa kwa jinsi ya
kibinadamu; lakini kwa jinsi ya Rohoni, hutakiwi kuchoka Yakobo
5:10-18, na Mathayo 5:14.
11.5Kujali mahitaji ya mwenzako (tendo la ndoa)
Paulo Mtume aliwaandikia hivi wanandoa wa Korinto ‘Lakini kwa
sababu ya tamaa zenu kila mwanaume na awe na mke wake
mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe.
Mume na ampe mkewe haki yake, na vivyo hivyo mke na ampe
mumewe haki yake. Mke hana amri juu ya mwili wake, bali
mumewe; vivyo hivyo mume hana amri juu ya mwili wake, bali
mkewe. 1Wakorinto 7:1-5. Kimsingi andiko hili linalenga
wanandoa wote wawili. Biblia iko wazi kwamba kwa sababu ya
zinaa (tendo la ndoa) kila mume awe na mke wake mwenyewe.

Moja ya sababu muhimu za wewe kuolewa ni ili kumtosheleza


mumeo kwa habari ya tendo la ndoa kama ilivyo na kwako pia. Kwa
wanandoa wengi haja ya tendo la ndoa inatofautina, hata hivyo mara
nyingi uhitaji wa tendo la ndoa kwa Mwanamume uko juu kuliko
mwanamke.Pamoja na hayo kila mmoja anamuhitaji mwenzake ili
kutoshelezwa katika hitaji hili muhimu. Baadhi ya wanawake kwa
kujua ukweli huu na tofauti hii ya uhitaji wa tendo la ndoa, kwa
kutokufikiri athari zake kwa wenzi wao, kwao binafsi na hatima
(‘future’) yao huwanyima waume zao haki ya tendo la ndoa hasa
pale wanapokuwa wametofautiana juu ya jambo fulani. Mbaya zaidi
wapo akina mama ambao wakikasirika huwanyima waume zao haki
hii ya msingi kwa muda mrefu na wanaishi nyumba moja na wengine
wanalala kitanda kimoja.

112
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

Mume wako akijua kwamba unatumia ugomvi/tofauti zenu au hata


kwa makusudi kumnyima haki yake ya tendo la ndoa, na jambo hilo
likawa endelevu uwe na uhakika taratibu unaanza kuharibu ndoa
yako.Maana,Shetani hutumia nafasi ambazo wana wa Mungu
wanampa na ndiyo maana wana Mungu wanasisitizwa kutokumpa
shetani nafasi. Ndani ya mume wako yataingia mawazo mabaya
Ezekieli 38:10 na kumweleza‘mbona kuna wanawake wengi, ni
suala la kwenda kumaliza haja yako kwa mwanamke yoyote
mwingine’.Wazo jingine pia litamwambia kwa nini huyu mwanamke
akutese kiasi hiki, kwa nini usiwe na nyumba ndogo.

Naam, hata kama hatafanya hayo, uwe na uhakika kwamba tayari


kwenye ufahamu wake umeshapanda mbegu mbaya na
itaendelea kukua endapo utaendelea na tabia yako ya kumnyima
haki yake. Usishangae siku moja kukuta ametoka nje ya ndoa,
usikimbilie kumlaumu Shetani, maana wewe ndiye uliyefungua
mlango na kumkaribisha.Nakumbuka mwamume mmoja alisema hizi
ndoa za Kikristo zinatutesa sana wanaume na zinawafanya hawa
wanawake wajisahau sana kwa kuwa wanajua Biblia imetuzia kuoa
mke zaidi ya mmoja.Naam ilibidi nitumie muda mwingi kurejesha
ufahamu wa huyu ndugu kwenye msingi wa ki-Mungu kwa kuwa
nilijua tayari kuna wazo lilishaingia moyoni mwake na nilijua wapi
linampeleka.

Nimeandika jambo hili kwa kirefu kwasababu mara nyingi sehemu


kubwa ya kesi za wanandoa inapofika kwenye suala la unyumba,
wanawake ndio wanaowanyima waume zao. Nakiri hata wanaume
wapo lakini ni mara chache sio kama ilivyo kwa wanawake.
Mwanamke sikia,kitendo cha Mungu kukupa huyo mume ni heshima
ya pekee sana kwamba ni wa kwako pekee yako.Ukitaka kujua
gharama yake waulize wanawake ambao wameolewa na mume
113
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

mmoja namna inavyowagharimu kihisia, kifikra na kimaisha. Ni


lazima ujifunze kujali na kutimiza mahitaji ya mwenzi wako
vinginevyo unafungua mlango kwenye ufahamu wa mumeo na
kumwambia angalia kule nje kuna wanawake wengine.

Ukweli ni kwamba kuna sababu mbalimbali ambazo hupelekea


wanawake kwenye ndoa kufanya hivyo,ila ushauri wangu ni
kwamba, uamuzi wa namna hii (kumnyima tendo la ndoa mumeo) ni
wa kuharibu na si kujenga.Hivyo haijalishi huyo baba kakukosea nini
(labda ziwe sababu za kiafya), suala la tendo la ndoa kwake ni
muhimu sana na ni haki yake, kutokumpa haki yake ni kumkaribisha
Shetani mzimamzima kwenye ndoa yako.Ni vizuri mkahakikisha
kwamba tofauti zenu zote mnazimaliza kabla hamjaingia kulala,
itawasaidia sana ili kwamba mkishafika kulala iwe ndio paradiso
yenu kwa muda huo.Kitendo cha kuingia kitandani kulala kabla ya
kumaliza tofauti zenu kinazuia uwezo wa tendo la ndoa kufanyika
kwa ustadi.

114
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

SURA YA KUMI NA MBILI


MAMBO YA KUFANYA ILI
KUMSAMEHE MWENZI WAKO

Nimesulibiwa pamoja na Kristo, wala si mimi tena ninayeishi bali


Kristo ndiye aishiye ndani yangu. Uhai nilio nao sasa katika mwili,
ninaishi kwa imani ya Mwana wa Mungu, aliyenipenda na kujitoa
kwa ajili yangu Wagalatia 2:20. Hii ina maana kwamba ukifanyiwa
mabaya hufanyiwi wewe bali Kristo aliye ndani yako. Mume wako
akikutukana au mkeo akikudharau linda kinywa chako huku ukijua
kuwa hufanyiwi wewe bali Yesu aliye ndani yako. Katika kila jambo
utakalofanyiwa usirudishe kwa kuwa anayefanyiwa ni aliye ndani
yako. Kwa kufanya hivyo unatoa nafasi kwake kupigana badala yako
maana yeye alikwisha kuahidi kwamba akugusaye anaigusa mboni
yake.Changamoto kubwa iliyotufikisha hapa tulipo ni ile hali ya
kutaka kujitetea ili tusionekane tuliopitwa na wakati na ambao
hatujui kujitetea.

Mpende mwenzako na mwombee.Mmesikia kwamba imenenwa,


umpende jirani yako na umchukie adui yako;Lakini mimi
nawaambia,wapendeni adui zenu na waombeeni wanaowaudhi
Mathayo5:43-44. Kuna wanandoa waliopendana kama kumbikumbi
hapo awali lakini sasa wameudhiana kiasi cha kuonana kama
maadui, pamoja na hayo jilazimishe kumwombea mwenzako kila
anapokuudhi hata kama kibinadamu inaonekana kuwa ngumu.Tena
mpende hata akikufanyia ubaya,kitendo hiki cha kumpenda na
kumuombea wakati mawazoni alitazamia utalipa kisasi
kinatengeneza hatia ndani,likumbuke jambo hili kila wakati maana ni
muhimu.
115
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

Watu wengi pamoja na kwamba wanajaa kwenye nyumba za ibada


linapokuja suala la kusamehe wanatenda kinyume na maagizo ya
Yesu, yeye alisema "wapendeni adui zenu".Kwa nini unamchukia
mume au mke wako? Chuki imeharibu ndoa nyingi,lakini katika
1Wakorinto 13:4-8 inaeleza wazi juu ya tabia za upendo wa watu
wa nuruni kuwa ni uvumilivu, ustahimilivu, uaminifu,upendo
wakati wowote,hufadhili, hautakabari, hauhesabu mabaya,
hauoni uchungu n.k.

Samehe na kusahau.Ukisoma Luka 17:4-5 maandiko yanatuambia,


“hata saba mara sabini”, maana yake hata usipoombwa msamaha
wewe samehe. Kusamehe ni uamuzi wa mara moja lakini kusahau ni
vita vya imani. Ngoja nikuulize swali, Je siku ulipookoka ulikuwa na
uhakika gani kuwa umesamehewa dhambi zako na wala Mungu
hazikumbuki tena? Hivi ni kweli Mungu anaweza kukuambia ufanye
kitu ambacho anajua huwezi kufanya? Kwahiyo anapokuagiza
kusahau anajua unaweza kusahau, kumbuka ukimsamehe mume au
mke wako, usikumbuke makosa yake na wala usiyaweke moyoni.
Msamehe bila unafiki ndani yake, tunayaweza mambo yote katika
yeye atutiaye nguvu, Wafilipi 4:13. Soma pia Yakobo 4:7, Waefeso
4:27 na Wafilipi 4:8 na usisahau unasamehe kwa faida yako
mwenyewe na hata usiposamehe ni kwa hasara yako pia.

Peleka hasira kwenye maombi, "Muwe na hasira lakini msitende


dhambi jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka;wala
msimpe Ibilisi nafasi Waefeso 4:26-27.Huu mstari watu
wameutumia isivyo; kutokana na maneno hayo wamefanya vitendo
vingi viovu kwa mawazo,maneno na matendo, Biblia haiwezi
kujipinga yenyewe.Lakini, soma mistari ifuatayo: "Uchungu wote na
gadhabu na hasira na kelele na matukano yaondoke kwenu maana
116
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

hasira ya mwanadamu haitendi haki ya Mungu"Yakobo 1:20. Basi


matendo ya mwili ni dhahiri nayo ni haya Uasherati, uchafu, ufisadi,
kuabudu sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka,
uzushi, husuda, ulevi, ulafi na mambo mengine yanayofanana na
hayo.Nawaonya, kama nilivyokwisha kuwaonya kabla kwamba watu
watendao mambo kama hayo, hawataurithi ufalme wa Mungu
Wagalatia 5:19-21.

"Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, usiue; na mtu akiua


itampasa hukumu; bali mimi nawaambieni, kila amwoneaye ndugu
yake hasira itampasa hukumu.Yesu anasema ukimuonea ndugu
yako hasira unastahili hukumu.Maandiko yanasema,ikitokea
ukakasirika kwasababu ya maudhi, jitahidi usitende dhambi.Kwa
kuwa tupo chini ya jua na tumeuvaa mwili hatuwezi kukwepa
kukasirika, lakini "tukikasirika tusitende dhambi".Hivyo kuwa na
hasira ni dhambi,ndiyo maana Yesu anasema,ukimwonea hasira
mwenzako unastahili hukumu,yaani umefananishwa na muuaji,
mwasherati na mwabudu sanamu.

Ikiwa umekasirika nakushauri tubu,mwambie Mungu jinsi


unavyojisikia bila kuficha na mwombe kile ambacho ungependa
akufanyie, utajikuta unaumimina moyo wako kwake naye ataichukua
hasira yako na uchungu uliokuwa nao. Kosa la wengi wakiudhiwa
wanapeleka uchungu na hasira kwa aliyewaudhi kwa lengo la kulipa
kisasi, sivyo biblia inavyoagiza, wewe upeleke uchungu na hasira
zake kwa Yesu kwa njia ya maombi.

12.1 Mambo ya kuimarisha ndoa yako


Mwanzo 1:27 na 2:7 inatuambia kuwa mtu ni roho aliye na nafsi
anayeishi katika mwili, biblia pia inasema “tunaishi kwa imani”
117
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

Warumi 1:17.Kila eneo la maisha yetu tunatakiwa tuliishi kwa


imani.Tunaposhindwa kufikia kiwango fulani cha maisha au
tunaposhindwa kufanya kile ambacho maandiko yametuambia
tunaweza kutakuwa na imani fulani ambayo imepungua au kupotea.

Imani chanzo chake ni kusikia na kusikia huja kwa neno la Kristo


Warumi 10:17. Maisha ya ndoa hatuyaishi kwa tabia, uzoefu, elimu,
ujuzi, maarifa wala kuvumilia matatizo kwasababu kila binadamu
anacho kiwango cha mwisho cha uvumilivu na hicho kinapofikiwa
huwa hasikilizi wala kuambiwa lolote. Tunadumu kwenye ndoa kwa
kuwa tunaishi kwa neno; na neno hilo ndilo linalotuwezesha
kuyatenda yote kwa kadri ya linavyotuelekeza.Na kwa mwongozo
wa neno hilo tunafanikiwa kushinda kutofikia kiwango cha mwisho
cha uvumilivu.Kwahiyo kama tukifanya na kuishi vile neno la
Mungu linasema,maisha yetu ya ndoa yatakuwa sawasawa na
mapenzi ya Mungu.

Kila tatizo linalotokea kwenye ndoa lazima lina chanzo chake na


chanzo hicho kinaweza kuwa katika roho, nafsi au mwili, hakuna
tatizo la ndoa linaloweza kutokea nje ya hayo maeneo matatu. Na ili
kulitatua lazima ushughulikie zaidi chanzo cha tatizo husika.
Ukisoma Waefeso 5:22-33,utaona ndoa inahusisha roho, mwili na
nafsi.Ukiona mpaka ndoa imekufa maana yake Roho Mtakatifu
alikwishaondoka siku nyingi kwenye ndoa hiyo, na utajua Roho
Mtakatifu hayupo kwenye hiyo ndoa pale tunda lililo katika
Wagalatia 5:22-23 linapokuwa halipo.Kwasababu mume na mke
wanaoana katika roho, katika mwili, na katika nafsi ili ndoa iende
vizuri lazima kuwe na makubaliano katika maeneo yate.

12.2Maadui 10 wa ndoa yako


118
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

Adui wa kwanza wa ndoa yako ni mwili. Ndoa ni kusudi la Mungu


na mwili upo ili kupingana na kila kitu cha Mungu Wagalatia 5:17.
Ndio maana ili ndoa iende vizuri lazima mwanaume na mwanamke
wawe mwili mmoja.Sasa ili hili liwezekane Mungu anasema“Mke
hana amri juu ya mwili wake bali mumewe; vivyo hivyo mume hana
amri juu ya mwili wake, bali mkewe” 1Wakorintho 7:4,Yakobo 4:1
inasema vita vyatoka katika miili yetu, vita dhidi ya kusudi lolote la
Mungu huanzia kwenye mwili. Kwahiyo kila siku jifunze jinsi ya
kuuombea mwili wa mwenzi wako ili uweze kukubali kuishi maisha
ya ndoa sawasawa na neno la Mungu. Paulo anasema tuitoe miili
yetu ili iwe dhabihu iliyo hai takatifu ya kumpendeza Mungu
Warumi 12:1.

Kuna wakati wanawake wanatumia miili yao kutaka kuwakomesha


wanaume, mwanamke anakosana na mumewe anafikiri njia rahisi ya
kumrekebisha au kumrudisha kwenye mstari ni kumnyima tendo la
ndoa akiamini kwamba kufanya hivyo kutamfanya ajirudi.Wakati
akipanga hivyo mwanaume naye anaingiwa na tamaa ya mwili na
kufikiri nikiwa rijali kwa nini nisumbuke, naye anajiingiza kwenye
kukidhi haja ya mwili. Wengi waliofikiri namna hii wamejikuta ndoa
zao zikisambaratika kirahisi na shetani aliwajaribu kupitia miili yao
ili kusudi lile Mungu alilowakusudia wasilifikie.Wanandoa
wenzangu ninawashauri sana kwamba kila mara kabla ya kufikia
maamuzi fulani fikilia mwisho mwema ambao Mungu aliwakusudia.
Na pia kumbuka kwamba mwili huo unaotembea nao umewekezwa
na mwenza wako.

Nafsi:
Kwenye nafsi ndipo kuna nia, hisia na maamuzi juu ya maisha,
kufikiria kwetu juu ya maisha kunatokea kwenye nafsi; kwahiyo basi
ikitokea Shetani akakamata nafsi mojawapo kati ya mume au mke;
119
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

anakuwa amefanikiwa kuivunja ndoa kirahisi.Moja ya mamlaka


tuliyonayo ndani ya Kristo ni mamlaka juu ya mawazo na fikra
2Wakorintho 10:5. Kwa kutumia mamlaka hii,unaweza kubadilisha
mawazo na fikra ya mwenzi wako kama havimtii Kristo.

Unapoona mwenzako ana tabia fulani ambayo haimpendezi Kristo,


chimbuko lake ni ulimwengu wa roho kwani tulivyo nje ni matokeo
ya yule mtu wa ndani. Tabia ni matokeo ya nafsi ya mtu kuvurugwa
eneo fulani. Hivyo ni muhimu kujenga nafsi zetu ili maamuzi
tunayofanya yawe maamuzi ya kumpendeza Mungu. Kumbuka nafsi
inalishwa na kuona, kusikia, kunusa kuonja na kugusa kama ulivyo
mwili, hakikisha nafsi yako inashibishwa kwa neno la Mungu ili kile
kitakachotoka kiwe kwa ajili ya kuujenga ufalme wa Mungu.

Changamoto kubwa kwenye ndoa za leo ni pamoja na ile hali ya


kuwaziana mabaya siku zote kunakotokana na kutoaminiana
ambavyo msingi wake umejengwa kwenye nafsi.Ashukuliwe Mungu
kwa kuwa alilijua hilo na kupitia maandiko matakatifu zikabainishwa
njia kadhaa zinazohusu jinsi ya kuijenga nafsi ili iwe imara,
mojawapo ni kunena kwa lugha 1Wakorintho 14:4.Lakini pia
maandiko yanasema adui anaweza kufuatilia miguu ili kuingia katika
nafsi yako Zaburi 56:6. Hivyo inatakiwa kuiombea miguu ya mume
au mke kwa jinsi ya rohoni ili adui asifanikiwe kukamata nafsi
yake.Hakikisha muda wote unafanya hivyo kwanini, kwasababu
kumwombea yeye ni kujiombea, maana katika hali ya kiroho miili
yenu mmebadirishana,wewe umebeba mwili wake na yeye amebeba
mwili wako,kwahiyo kumuombea ni kujiombea wewe.

Kutotambua nafasi yako katika ndoa:


Mume na mke wamepewa nafasi mbili tofauti kwenye ndoa ambapo
kila mmoja anawajibika kusimama kwenye nafasi yake bila
120
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

kuteteleka wala kuingilia kwa namna yoyote ile nafasi ya mwenzake.


Paulo anatuambia mume na ampende mke wake kama Kristo
alivyolipenda kanisa.Kama Kristo alivyo kichwa cha kanisa
Wakolosai 1:18 ndivyo Paulo anailinganisha ndoa kama Kristo na
kanisa, maana yake mwanaume ndiye kichwa.

Baada ya mwanadamu wa kwanza kuasi, moja ya adhabu ambayo


Mungu aliyoitoa kwa mwanamke ni kutawaliwa na mwanamume
Mwanzo 3:16.Kwahiyo mwanamume ndiye anayemtawala
mwanamke kwenye ndoa hata hivyo hilo halina maana kwamba
mwanamume amtese na ajione ni bora kuliko mwanamke.Ndio
maana katika kuweka uwiano sawa wa kuhakikisha mwanamume
havuki mipaka katika kumtawala mke wake Yesu alimpa amri ya
kumpenda.Hata hivyo mojawapo ya matatizo makubwa katika ndoa
za siku hizi ni ubabe uliopitiliza kutoka kwa akina baba katika
kuwatesa wake zao kinyume na lilivyo agizo la kuwapenda pamoja
na ile hali ya mwanamke kutaka kuwa mtawala mwenye ulinganifu
kwenye ndoa.Ukweli ni kwamba kwenye ndoa ukijaribu kuingiza
harakati (activism) unakuwa umeshindwa kabla ya kuanza.

Mwanamke ni msaidizi kwa mume wake.Wanandoa wanapotambua


nafasi zao na kushirikiana katika kila jambo watafanikiwa zaidi.
Ingawa mtu mmoja anaweza kushindwa, watu wawili wanaweza
kujikinga. Kamba ya nyuzi tatu haikatiki kwa urahisi. Mhubiri 4:12.
Ni mhimu sana wanaume wakajua kuwa mke ana nafasi ya kuwa
msaidizi.Sio mtawaliwa kwasababu kuwa msaidizi ni tofauti na
kutawaliwa.Nafasi ya msaidizi mwanamke alipewa ili kutimiza
kusudi la Mungu.Yohana 14:26 inatuambia Roho Mtakatifu ni
msaidizi na bila Roho Mtakatifu hatuwezi kufanya kusudi la Mungu.
Vivyo hivyo, pasipo mwanamke mwanamume peke yake hawezi
kufanya kila kitu kwa kiwango ambacho Mungu amemkusudia.
121
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

Tamaa:
Tamaa ni moja ya vitu vinavyoleta shida katika ndoa.Asili ya
mwanamke ni kutamani Mwanzo 3:6, tamaa hii ipo katika vitu.
Hivyo Mungu alipokuwa anatoa adhabu kwa mwanamke,
alimwambia na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala.
Mwanamume mara nyingi tamaa yake inakuwa kwa wanawake siyo
kwenye vitu. Hii ni kutokana na asili ya mwili wa mwanamume
ambao uwezo wake wa kuzaa haufungwi katika majira na nyakati
kama ilivyo kwa wanawake.Kwa lugha nyingine mwanamume
anaweza kuzalisha saa yeyote lakini mwanamke inategemeana na
majira.Na kwa kuwa Mungu alitwambia zaeni mkaongeze Mwanzo
1:28, dhambi ilivuruga na kuliweka hilo kwenye tendo la ndoa. Ndio
maana Yesu alisema “Kila amtazamaye mwanamke kwa kumtamani,
amekwisha kuzini naye moyoni mwake” Mathayo 5:28

Kwa nini haisemi “amtazamaye mwanamume”, ni kwasababu tamaa


ya mwanamke Mungu aliiweka kwenye vitu. Hivyo ni muhimu kwa
wanandoa kuombeana ili kwamba kila mmoja tamaa yake isiwake,
fikiria kama mke tamaa yake ya vitu ikiwaka na wewe ukawa huna
uwezo wa kuvipata na mwisho akaamua kwamba vitu hivyo anawaza
kuvipata kwa kuwatumia wanaume wengine nini kitatokea? Wakati
huo huo ni mhimu kwa mwanamke kumuombea mume wake ili
asiwake tamaa kwa wanawake wengine maana sasa ndoa hiyo badala
ya kuwa ndoa utakuwa uwanja wa mapambano.

Wapendwa wanandoa wenzangu tusisahau kwamba chanzo cha


dhambi yoyote ile ni tamaa na maandiko yanasema wazi kwamba
kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na
kudanganywa na ile tamaa ikichukua mimba huzaa dhambi na
dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti Yakobo 1:15. Kwa lugha
122
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

nyingine inaanza tamaa, inafuata kitendo (dhambi) na matokeo yake


mauti (ndoa kufa). Kwahiyo kitu cha msingi sana kwenye ndoa ni
kusimama na kuombeana ili kwamba mmoja wenu asivutwe na
kudanganywa na tamaa, maana mkilegea katika eneo hilo mtavutwa
na ndoa inaweza kuwa hatarini.

Kutotambua uzuri wa mke wako:


Moja ya sababu iliyosababisha umwoe huyo uliyenaye ni kwa kuwa
ulimpenda na kumwona ni mzuri kuliko wengine ambao hukuwaoa.
Kitabu cha wimbo ulio bora kinatupa picha jinsi mwanamume
anavyotakiwa kuuona,kuutambua na kuuthamini uzuri wa mke wake
na kumtukuza Mungu kwa uumbaji wake.Mwanamume Sulemani ni
moja ya kielelezo cha namna ambavyo wanaume wanatakiwa kuwa,
alikuwa akijaribu kuyaelezea maumbile ya mke wake na jinsi
anavyofaidi kuwa naye;hivi ndivyo mwanamume anatakiwa
kumuona mke wake.

Hili ni eneo la muhimu kwani Shetani akiweza kubadilisha jinsi


mume anavyomtazama mkewe,mwanamume ataanza kuona
wanawake wengine ndio wazuri.Hii ni tamaa ambayo inatoka
kwenye mwili. Kwa kuwa mwili unapinga mapenzi ya Mungu
Wagalatia 5:16 inatuambia uasherati ni moja ya matendo ya mwili,
tamaa ya mwili ndiyo itamfanya mtu ajaribiwe.Hivyo mwanamke
anatakiwa atumie nafasi yake aliyopewa na Mungu juu ya mwili wa
mume wake 1Wakorintho 7:4, nakuuombea sana ili tamaa
isimshinde mume.

Kutoondoka kwenu:
Kwasababu hiyo mtu atamwacha baba na mama yake naye
ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja
Waefeso 5:31.Huu msitari ukiusoma haraka unaweza kudhani
123
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

unaongelea kuwaacha baba na mama kwa jinsi ya mwili.Maandiko


yanasema mtu atamwacha, kumbuka mtu ni roho.Anachoongelea
Paulo ni kwamba mtu anapoingia kwenye ndoa lazima aondoke
kwao kwa jinsi ya rohoni na kuwaacha wazazi wake.Paulo haongelei
kuwatenga wa nyumbani na kuwasahau.

Kitu ambacho Paulo anaongelea ni lazima mahusiano ya mtu na


wazazi wake yabadilike.Siyo mtu unakuwa kwenye ndoa halafu kila
kinachotokea kwenye ndoa unakwenda kuwaambia wazazi;
ukishaingia kwenye ndoa,kuna nafasi ambayo wazazi wako
wanaipoteza katika ulimwengu wa roho na mke wako ndio anakuwa
wa kwanza.Nafasi ya mke ukimpa mama yako ndoa haiwezi kwenda
vizuri, Mwanamke naye anatakiwa kuondoka kwao kwa jinsi ya
rohoni ili mume wake amtamani.“Sikia, binti, utazame, utege sikio
lako,uwasahau watu wako na wa nyumba ya baba yako.Naye mfalme
atautamani uzuri wako,maana ndiye bwana wako nawe umsujudie
Zaburi 45:10-11.

Njia mojawapo ambayo Shetani anaitumia kuvuruga ndoa za watu ni


kukurudisha kwenu kwa jinsi ya rohoni. Kwahiyo unakuwa kwenye
ndoa lakini unapofika wakati wa masuala na mashauri au mambo ya
msingi unaenda kwa wazazi wako au ndugu zako badala ya kwenda
kwa mke au mume kwanza. Mwanamume kumbuka na hili likukae
akilini kila mara kwamba wazazi wako siyo wasaidizi kwako ila
mkeo.Na kwa mwanamke usisahau hata siku moja baba yako sio
kichwa chako,kichwa chako ni mumeo; huyu ndiye wa kushauriana
na kupanga naye maana hakuna namna ambavyo unaweza kufanya
maamuzi bila kukishirikisha kichwa;ndio maana katika mazingira ya
kawaida ukionekana unafanya mambo yasiyofaa kwenye jamii watu
wanasema yule ndugu kichwa chake sio kizima, na kwa hali iyohiyo
kwenye ndoa.Sisemi usiombe ushauri kwa ndugu zako lakini mambo
124
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

ya ndoa inatakiwa yamalizwe na wanandoa kwa msaada wa Roho


Mtakatifu.

Mlango mwingine ambao Shetani anautumia kuvuruga ndoa za watu


ni mama mkwe na mawifi. Umewahi kujiuliza kwa nini mama mkwe
huwa ni moja ya chanzo cha migogoro katika ndoa za watoto wao.
Na pia mawifi wakati mwingine ndio huwa wanamchukia mke wa
kaka yao,kumbuka Shetani akitaka kuharibu kusudi la Mungu
anatafuta penye mlango ili apite na imeshaonekana mlango ambao
mara zote unakutwa wazi ni huu wa mawifi na mama mkwe.
Wanawake wanajua na wanapoolewa huanza kujizatiti mapema
namna watakavyopambana na mawifi wakiolewa.Mwenye jukumu la
kumkinga mke na kadhia hii ni wewe mwanaume,weka mipaka ya
wazi kati ya mkeo na dada zako au ndugu wengine, waeleze wazi
kuwa huyo ndiye msaidizi ambaye Mungu kakupatia, anayemdharau,
kumbeza na vinginevyo anakubeza wewe kwa kuwa huyo ni nyama
katika nyama zako.Ukishindwa kusimama katika nafasi yako kama
mwanamume usishangae mkeo akakosa heshima aliyoistahili na
kubaki kama jamvi la wageni.

Kutoilinda imani:
Hiki ndicho kipengele cha muhimu kuliko vyote kwani maandiko
yanasema tunaishi kwa imani.Hivyo hata katika ndoa tunatakiwa
tuishi kwa imani. Kwa kuwa maisha yetu yanategemea imani yetu
kwa Kristo, vita kubwa iliyopo kati yetu sisi na shetani ni kile
kilichopo ndani yetu ambacho ni imani, siyo ndoa. Ndoa ni mlango
ambao Shetani anautumia kukutenga na imani kwa Yesu. Unapoona
ndoa imevunjika au ina misukosuko ujue kwamba kuna kiwango
fulani cha imani ambacho kimepungua au hakipo kabisa. Maandiko
yanatueleza kwamba pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu,
matatizo mengi kwenye ndoa ni matokeo ya kile kilichokosekana
125
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

ndani. Kitu kikubwa cha kukipigania ni imani, siyo ndoa.Paulo


anasema nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani
nimeilinda 2 Timoteo 4:7.

Yesu akirudi ataangalia kama umeilinda imani siyo ndoa kwani


ukiilinda imani na neno la Kristo likawa ndani yako kwa wingi,
utaishi vizuri katika ndoa.Imani inapopungua miongoni mwa
wanandoa ndipo kutoaminiana kunaanza,kutoaminiana kukianza
kunazaa kutosikilizana,kutosikilizana kunaleta mjukuu mmoja
aitwaye upendo kupungua na kwa kuwa upendo amepungua njia za
ziada zisizo za Ki-Mungu za kuhuisha huyo upendo zinaanza
kutafutwa.Yesu alimwambia Petro“lakini nimekuombea wewe ili
imani yako isitindike; nawe waimarishe ndugu zako” Luka 22:32.
Kwa hiyo imani inaweza kutindika (ku-fail) na katika ndoa imani
inapotindika ndipo matatizo huonekana kwa jinsi ya mwili. Hivyo
cha muhimu ni kuwa na neno la kutosha ili imani yako katika Kristo
isitindike.Nami pia kupitia kitabu hiki ninawaombea wanandoa wote
kwamba imani yenu juu ya Mungu aliyepelekea ninyi kuungana na
kuwa mwili mmoja isitindike ili kwamba ndoa yenu ilitimize kusudi
la kuwepo kwake.

Kutokuwa na Maombi:
Maombi ni muhimu sana katika ndoa, ni muhimu kwa kuwa suala la
ndoa pia ni la kiimani, changamoto kubwa ambayo inazikabiri ndoa
nyingi kwa sasa ni wanandoa kuanza maombi wakishapatwa na
matatizo ila wanapokuwa kwenye raha wakiitana majina yote mazuri
huoni wala kusikia maombi; kumbe kwa kufanya hivyo inakuwa ni
sawa na kulala wakati milango ikiwa wazi. Ni mhimu kuomba kwa
sababu maombi ndio nguzo inayozuia matatizo yasitokee.Usisubiri
umepigwa na adui ndipo uingie kwenye maombi.
126
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

Ukiuliza wanandoa wengi kwa mara ya mwisho ni lini walifunga na


kuomba kwa ajili ya ndoa yao unaweza kushangaa sana, hii ni kwa
sababu ufahamu wa watu wengi umefungwa kwamba kuomba ni pale
ndoa zinapokuwa haziendi vizuri.Sasa kwanini usiwe unafunga na
kuiombea ndoa kila mara ili Shetani asipate mlango wa kuingia
balada ya kusubiri? Wanawake ni watu muhimu sana kwenye eneo
hili la kuomba na kuomboleza kwasababu wamepewa karama ya
kuomba.Mungu anasema juu ya kutafuta wanawake waombolezaji na
sauti za maombolezo katika Sayuni Yeremia 9:17-19.

Hivyo akina mama watumie karama hiyo na kubeba ndoa zao katika
maombi kwani bila maombi ndoa haitaenda.Tusisubiri kufanya
maombi wakati tukiwa na matatizo, ukweli wenyewe ni kwamba
ukiwa na matatizo huwezi kuomba badala yake utalalamika kwa nini;
kwasababu kila utakapokuwa unajitahidi kusema unaomba utaiona
sura ya yule aliyesababisha tatizo husika na kama kulitokea maneno
basi sauti ile itakuwa ikijirudiarudia masikioni.Ni vema wanandoa
wakawa na utaratibu wa kufanya maombi ya shukrani katika yale
mengi ambayo Bwana amewatendea bila kusahau ulinzi kwenye
ndoa na familia kwa ujumla wake na kila mwanandoa ahakikishe
analo neno la Mungu kwa wingi ndani yake.

Kutovunja ndoa za kiroho kama zipo:


Ndoa inaweza kuvamiwa katika ulimwengu wa roho kutokana na
mume au mke kuwa na ndoa (maagano) zingine kwa jinsi ya rohoni.
Kumbe katika ulimwengu wa roho kuna ndoa zingine. Kuwa katika
ndoa zingine katika ulimwengu wa roho maana yake ni nini? Ni ile
hali ya kujikuta ukiwa unazini na wanawake au wanaume usiowajua
ndotoni au unashangaa hamu ya kushiriki tendo la ndoa na mkeo au
127
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

mumeo linaondoka kabisa.Wanaume wakati mwingine wakitaka


kushikiriki tendo la ndoa na wake zao nguvu za kiume zinakuwa
hamna lakini kwa wanawake wengine wanakuwa hawana
shida.Msipokuwa makini mnaweza kujikuta mnagombana sana ndani
ya nyumba bila sababu na adui amekaa pembeni akiwashangaa;
kinachotakiwa ni kuomba na kutumia damu ya Yesu kuvunja ndoa
hizo katika ulimwengu wa roho.

12.3Mambo ya kukumbuka
Wazia nyumba ambayo imeachwa bila kutunzwa kwa muda mrefu
kidogo hali iliyopelekea rangi yake kuanza kubanduka banduka, paa
yake imeharibika na nyasi zilizoota hazijakatwa, kwa kuitazama
nyumba hiyo imepigwa na dhoruba kwa miaka mingi nayo
imechakaa. Je kuchakaa huko kumeifanya ibomolewe? Si lazima,
ikiwa msingi wake ni imara na muundo wake ni thabiti, nyumba hiyo
inaweza kurekebishwa.Je hali ya nyumba hiyo inakukumbusha ndoa
yako?Kwa miaka mingi, huenda dhoruba za mfano zimeiathiri ndoa
yako, inawezekana mmoja wenu au nyote wawili mmeiachilia ndoa
yenu kwa kiasi fulani. Hata kama hali katika ndoa yako iko
hivyo,usiende haraka kwamba inapaswa kuvunjwa.Ndoa yako
inaweza kurekebishwa.Mengi yanawategemea wewe na mwenzi
wako mnavyotimiza wajibu wenu katika ndoa.Kufanya hivyo
kunaweza kuimarisha ndoa yenu wakati wa majaribu.

Wajibu
Wajibu katika ndoa humaanisha kulazimika kutimiza au kujiwekea
masharti ya jambo fulani.Ni ile hali ya kusurutishwa kutimiza jambo
fulani kwa mwenzako hata kama kunaonekana ugumu fulani katika
128
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

kulitimiza.Wajibu hauombewi samahani,huwezi kusimama na


kujitetea kwamba sikutimiza wajibu wangu kwasababu sikuwa
nikijua kwamba nawajibika kutimiza wajibu huo.Wakati mwingine
neno hili wajibu hutumika kuhusu mikataba na makubaliano ya
kibiashara.Kwa mfano, mjenzi anaweza kuhisi analazimika kutimiza
matakwa ya mkataba wa kujenga nyumba ambao alitia sahihi. Hata
hivyo, anahisi ni sharti atimize ahadi yake. Ingawa ndoa sio mkataba
lakini ndani yake kuna masharti fulani.

Mathayo 19:4-6 akawajibu, “Je hamkusoma kwamba hapo mwanzo


Mungu aliwaumba mtu mume na mtu mke. Naye akasema,
Kwasababu hii mtu atamwacha baba yake na mama yake naye
ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili
mmoja?’Hivyo si wawili tena, bali ni mwili mmoja.Kwahiyo kile
alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.Yote
yaliyotajwa katika mistari hii ndio wajibu ambao kila mwanandoa
anao kwa mwenzake, kutenda au kuwaza kutenda tofauti na hivyo ni
kutenda dhambi.

Ushirikiano
Siyo kwamba wanandoa hawatofautiana mawazo na mtazamo,
hapana hata vyombo vikiwa pamoja kwenye kabati vinagongana
itakuwa binadamu.Wanapogombana/kutofautiana wanapaswa
kujitahidi kutatua tatizo hilo, si kwasababu ya nadhiri walizofanya
bali kwasababu wanapendana.Yesu alisema hivi kuhusu mume na
mke wao si wawili tena, bali mwili mmoja.Inamaanisha nini kuwa
mwili mmoja na mwenzako? Paulo aliandika kwamba wanaume
wanapaswa kuwawapenda wake zao kama miili yao wenyewe
Waefeso 5:28, 29.Hivyo basi, kuwa mwili mmoja humaanisha
kuhangaikia hali njema ya mwenzako kama unavyohangaikia hali
yako mwenyewe.Wanandoa wanatakiwa kubadili mtazamo wao,
129
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

badala ya kufikiria mambo kama waseja (wasiooa),wayafikirie kama


waliooana.

Je wewe na mwenzi wako mnapojitazama kama watu waliofunga


ndoa au kama wasiooana? Inawezekana mkawa mmeishi pamoja
kwa miaka mingi na bado msiwe “mwili mmoja.”Je jambo hilo
linaweza kutokea? Fikiria kuna watu wapo kwenye ndoa lakini
mke/mume anafanya mambo yake ambayo hata mwenzake hajui na
asingependa ajue, watu wa namna hii ungewaweka kwenye kundi
gani? Ndoa humaanisha kushirikiana maishani na kwa kadri
mnavyoshirikiana ndivyo ndoa yenu inavyositawi. Je wanandoa
wanaweza kuishi pamoja bila furaha wala kushirikishana kwa sababu
ya watoto? Na je kuna wanaoweza kuendelea kuvumilia kwa sababu
wanaona talaka ni jambo lisilofaa kimadili? Wewe ukijipima uko
kwenye kundi gani? Ungependa kuendelea kuwa kwenye hali hiyo
au unatamani kuhama kutoka kwenye kundi hilo ulilomo?

Kutokuwa na Ubinafsi
Lakini yakupasa ufahamu jambo hili, kwamba siku za mwisho
kutakuwa na nyakati za hatari. Kwa maana watu watakuwa wenye
kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye
kiburi, wenye kumkufuru Mungu, wasiotii wazazi wao, wasio na
shukrani, wasio watakatifu, wasio na upendo,wasiopenda
kupatanishwa, wasingiziaji, wasiozuia tamaa zao, wakatili,
wasiopenda mema, wasaliti, wakaidi, waliojaa majivuno, wapendao
anasa zaidi kuliko kumpenda Mungu.Inaonekana watu wengi
kwenye ndoa hujifikiria wenyewe zaidi kuliko kuwafikiria wenzi
wao.Katika ndoa nyingi, kujitoa kumfanyia mwenzako jambo fulani
bila kuwa na hakika kwamba atakufanyia vivyo hivyo,huonekana
kama ni udhaifu.Hata hivyo ukweli umejidhihirisha kuwa ndoa
nyingi zilizofanikiwa ni zile ambazo wanandoa wote wameonyesha
130
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

roho ya kujidhabihu. Hakuna namna ndoa inaweza kufanikiwa na


kuwa mfano wa kuigwa kama kila mmoja anavutia kwake, nataka hii
ikutafakarishe juu ya kanuni ya kuachia asilimia niliyoitaja katika
sehemu zilizotangulia. Unawezaje kufanya hivyo sasa? Badala ya
kufikiria swali la ninafaidikaje, jiulize ninafanya nini ili kuimarisha
ndoa yangu?’
Kila mmoja wenu asiangalie mambo yake mwenyewe tu, bali
ajishughulishe kwa faida ya wengine Wafilipi 2:4 unapotafakari
kanuni hiyo ya Biblia jipe nafasi ya kuchanganua matendo yako ya
juma. Ni mara ngapi ulimtendea mke/mume wako kwa fadhili kwa
sababu tu ulitaka kumnufaisha? Mke/mume wako alipotaka
kuzungumza; Je ulijipa nafasi kumsikiliza ingawa moyo wako
haukuwa radhi naye? Ni mambo mangapi uliyoyatenda ambayo
yalimpendeza mwenzako zaidi ya vile yalivyokupendeza wewe?
Unapochanganua maswali hayo,usiwe na wasiwasi kwamba matendo
yako mema yatapuuzwa au yakose kuthawabishwa. Kitabu kimoja
cha kitaalamu kinasema,“Katika mahusiano mengi, mtu
anapomtendea mwenzake mema, yeye hutendewa vivyo hivyo, kwa
hiyo fanya yote uwezayo kumtia moyo mwenzi wako atende mema
kwa kutenda mema wewe mwenyewe.” Matendo ya kujidhabihu
huimarisha ndoa kwa sababu yanaonyesha kwamba unaithamini na
unataka idumu.

Katika kitabu cha Mithali 14:1 inasema ‘Kila mwanamke aliye na


hekima huijenga nyumba yake: Bali aliye mpumbavu huibomoa
kwa mikono yake mwenyewe’. Tafsiri ya neno nyumba ni familia,
naam na familia inajumuisha baba, mama na watoto endapo
mmejaliwa. Hata hivyo katika hali ya kawaida watoto watalelewa
katika msingi mzuri endapo ndoa imetengamaa. Ifahamike kwamba
neno nyumba limetumika ili kutupatia urahisi wa kuelewa namna
nyumba za kawaida zinavyojengwa ili tuchunguze dhana hiyo
131
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

kiroho.Kwa lugha rahisi ndoa yako ni nyumba, hivyo ubora, uzuri na


mvuto wa ndoa yako unategemea namna unavyoijenga kwa hekima.

Ni vizuri ukafahamu kwamba suala la ujenzi/maboresho ya ndoa


yako ni jukumu la kila siku ya kuishi kwa ndoa yenu mpaka kifo
kiwatenganishe.Kila mmoja katika ndoa ni lazima ahakikishe
anasimama kwenye nafasi yake na kufanya yale yampasayo ili
kuifanya ndoa kuwa bora zaidi. Endapo hakutakuwa na jitihada za
wanandoa kutaka kuimarisha ndoa yao, Shetani atatumia fursa hiyo
kuivuruga. Kujenga ninakokuzungumza hapa ni kule kuhakikisha
ndani ya ndoa kuna mahusiano na mawasiliano mazuri baina
yenu ambayo yatafanikisha kutekelezwa kwa kusudi la Mungu.

132
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

SURA YA KUMI NA TATU


MAWASILIANO KAMA MSINGI MKUU
KATIKA NDOA
Kabla ya dhambi familia ilikuwa mahali bora pa kuishi. Watu
walielewana na kupendana kila mmoja akitumikia furaha ya
mwenzake.Dhambi ikaleta tatizo kubwa katika mawasiliano na
mahusiano ya mume na mke. Adamu akasema, huyo mwanamke
uliyenipa awe pamoja nami ndiye aliyenipa matunda ya mti huo,
nikala" Mwanzo 3:12. Hali ya kulaumiana iliharibu uhusiano kati ya
mume na mke na kati yao na Mungu wa mbinguni. Hali hiyo
ilivuruga uhusiano baina yao, mazingira yao na viumbe
vilivyowazunguka.

Michongoma na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga za kondeni


Mwanzo 3:18. Hali hiyo iliendelea kuiathiri familia kwa vizazi
vyote vilivyofuata.Mtoto wa kwanza wa Adamu aitwaye Kaini
alimuua mdogo wake Habili baada ya kutofautiana katika maswala
ya ibada nyumbani kwao. Mwanzo 4:8 Kaini akamwambia Habili
nduguye,Twende uwandani ikawa walipokuwapo uwandani,Kaini
akamwinukia Habili nduguye, akamwua.Hata mahusiano ya wazazi
na watoto yaliendelea kuzorota.

Mawasiliano ni mchakato wa kuwasilisha taarifa kwa njia ya


ubadilishanaji wa mawazo, hisia, malengo, tabia, matarajio,
mitazamo kupitia mazungumzo, ishara na maandishi.Ni
ubadilishanaji wa taarifa unaoleta maana baina ya pande mbili au
zaidi ambazo zinaweza kuwa viumbe hai au kinyume chake.
133
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

Tunapowasiliana, tunazungumza, kusikiliza na kuzingatia.Kwa


kawaida mawasiliano lazima yawe na mtumaji (chanzo) na
mpokeaji.Mawasiliano hufanyika kwa uingiliano wa wote wawili,
ambapo mtumaji huingiza ujumbe kwa njia ya kituo
kinachoshirikisha mpokeaji.

Kuna sehemu kuu tatu katika mawasiliano ya ana kwa ana miongoni
mwa binadamu sehemu hizo ni pamoja na: - miondoko ya mwili, toni
ya sauti na maneno. Kulingana na utafiti imethibitika kwamba 55%
ya athari hulingana na miondoko ya mwili. Kwa mfano: jinsi mtu
alivyokaa, ishara za uso, mikono na macho, 38% hulingana na toni
ya sauti, na 7% hulingana na maudhui (ujumbe au maneno)
yaliyotumika katika mawasiliano. Kwahiyo mwanandoa
unapowasiliana hakikisha unazingatia asilimia hizi, upo uwezekano
mkubwa wa kuwa unaeleza kitu fulani lakini msikilizaji akikutazama
anapata ujumbe tofauti na ule unaousema.

Mawasiliano katika Ndoa ni kama barabara ya njia mbili


inayoruhusu magari kuingia na kutoka; yaani wanandoa wawili
ambao mmoja akiongea mwingine anasikiliza na mwisho wanapata
jibu la kudumu la tatizo lililokuwepo.Mawasiliano mabovu
husababisha kutokuelewana katika ndoa na mahusiano ya aina
yoyote.Ni kitu cha kawaida kuona mabishano ambayo yanaanza
asubuhi jua linaochomoza na kuendelea hadi jua linapozama jioni
bila ufumbuzi. Mabishano kama hayo yasiyo na ufumbuzi ni kama
bomu linalosubiri muda ili lilipuke.Kila mara kunapotokea
kutokuelewana kutokana na aina fulani ya mawasiliano iliyotumika
wewe ambaye hujaelewa jitahidi kumwomba mtoa ajumbe aeleze
kwa kina alikuwa anakusudia nini kupitia ujumbe wake.

134
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

Kuna wakati baadhi ya wanandoa hudhani kwamba kuliacha tatizo


bila kulizungumzia ni kutatua, hiyo si kweli na hali kama hiyo haileti
afya ya ndoa bali ugonjwa na matokeo yake ndoto ambazo mtu
alikuwa nazo kuhusu ndoa huyeyuka kama barafu iliyokutana na jua
la mchana. Kanuni muhimu katika kuhakikisha ndoa inakuwa imara
ni pamoja na kila mwanandoa kujitoa kwa kuhakikisha kila siku
anawekeza kwenye mawasiliano ili ndoa kustawi.Mawasilinao katika
ndoa au mahusiano yoyote ni kama gundi inayounganisha ndoa. Na
ikitokea hiyo gundi ikaacha kufanya kazi basi mahusiano au ndoa
huanza kukatika vipande vipande; ndoa bila kuwasiliano lazima
itakufa. Katika jamii nyingi za kiafrika watu hawapo wazi kueleza
kile wanachohitaji kutoka kwa mwenza wao; hakikisa unasema kile
unachotaka bila kuzunguka.

Kama hujaridhika na mitindo ya tendo la ndoa ya mke wako sema ili


ajue unataka kitu kipya, kama hujaridhika na chakula anachopika
sema ili msaidiane na kuona inakuwaje, watoto, huduma kanisani
maana wengine ni kanisani tu na mambo ya nyumba hana mpango,
ndugu, kama hujaridhika na jinsi anavyotumia pesa sema ili ajue.
Kubaki kimya na kudhani atajua mwenyewe hata kama utahuzunika
hatakuelewa eleza wazi ili kujenga ndoa yako.Kama unahitaji kitu
fulani kutoka kwa mwenzako sema nahitaji kitu fulani na kama kuna
kitu fulani anafanya wewe unaona kinakuletea shida mwambie kwa
upole na moyo wa upendo na pia mwambie kwanini unaona
kinakuumiza kubaki kimya ni kama bomu ambalo linasubili muda na
muda ukifika litalipuka. Kama unahitaji muda wa kujibakia
mwenyewe tu kufikiria mambo fulani fulani sema ili mwenzako ajue
ila si kuwa mkali na kufukuza watu bila kusema kulikoni; kuna
wakati binadamu huhitaji awe yeye mwenyewe na Mungu wake,
muhimu mawasiliano.Huishi na malaika kwamba atajua kila kitu
ambacho wewe unapenda au hupendi
135
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

13.1 Ndoa ni kujengana kila leo


Kama mwenzako anakasirika kutokana na kile ulichomwambia
kwamba hakikuwa sawa au vinginevyo inawezekana hajakulewa
vizuri jaribu kurudia kuelezea hadi aelewe kwa upendo na
hekima,usichoke kufanya hivyo. Jinsi tunavyowasiliana
tunatofautiana ki-jinsi na kimalezi ni muhimu kuwa makini kusoma
lugha ya mawasiliano ya mwenzi wako. Wanaume mawasiliano yetu
ni ya moja kwa moja na wanawake mawasilino yao yanabebwa na
hisia na wao ndo wanaoumizwa sana kwahiyo usiwe mwepesi
kuamini kwamba anafanya jambo usilolipenda kwa kuwa
amekudharau, usitumie hisia kuamua mambo sema naye.

Si busara kuongea na mwenzi wako kwa hasira kwani hasira wakati


mwingine husababisha kulia machozi, kupiga au kupigana, Kutupa
vitu hata kama ni vya thamani kama simu za mikononi, vyombo n.k
na wengine hubaki mabubu na kushindwa kuongea. Ndoa zote imara
zina kitu kimoja kinachofanana nacho ni mawasiliano mazuri. Wote
tunakubaliana kwamba ndoa nyingi zenye matatizo chanzo kikubwa
cha matatizo hayo ni mawasiliano mabaya. Mawasiliano ni pamoja
na kuwepo kwa wakati wa maongezi, kumsikiliza mwenzi wako
anapoongea, na kusema kila unachohitaji kwa mwenzako.

Msingi wa wawasiliano katika mahusiano ya ndoa ni katika mambo


makuu matatu ambayo ni:-
A. Uwepo katika maongezi kwa mwenzi wako, upatikanaji wako
pale mwenzi wako anapotaka kuongea kitu.Wote mnahitajika
kuwepo katika maongezi tena kwa kuhusika vizuri kwa lile
linalozungumzwa.Wewe unayetaka kuongea hakikisha mwenzi

136
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

wako yupo tayari kukusikiliza siyo kulazimisha akusikilize


wakati unajua anafanya kitu kingine au unamwona kabisa ana
haraka, usitake kitu hicho kijadiliwe muda huo; ukilazimisha
kijadiliwe au kijibiwe muda huo unaweza kuzua ugomvi wa bila
sababu au ukapewa majibu ambayo kimsingi hayakustahiri
muhimu tafuta muda muafaka.

B. Msikilize kwa makini mwenzako na kama huna muda wa


kusikiliza mwambie ni wakati gani utakuwa tayari kusikiliza
kwa makini kuliko kusikiliza huku unafanya kitu kingine.
Kitendo cha yeye kuwasiliana na wewe huku ukiwa unafanya
kitu kingine kinaashiria dharau na kutojali.Kwa upande wa akina
mama wanapenda wanapozungumza uwe unaangaliana naye,kila
anaposema uwe unaitikia, hali hiyo inamwongezea kujiamini na
kuona kwamba mwenzangu anajali na kufuatilia kile
ninachokiongea,hii ni mhimu sana kwa mwanaume kuichukua
maana itawasaidia.

C. Husika katika mazungumzo au maongezi, hakikisha mwenzako


anapata hisia kwamba unasikiliza, unajali na unachangia kile
anachoongea na ongea kwa upendo, ukaribu kwani anayeongea
naye ni mtu muhimu sana kwako.Usijaribu kuonesha kwamba
mwenzako anaongea kitu kilichopitwa na wakati, unaposoma
eneo hili mwanandoa mwenzangu jaribu kulihusianisha na
tofauti za mwanaume na mwanamke kimaumbile.Nina uhakika
kama ukiyaelewa vuzuri maeneo haya ndoa yako haitabaki kama
ilivyokuwa. Shida kubwa iliyopo kwenye ndoa nyingi ni ugumu
wa mawasiliano uliopo baina ya wanandoa pamoja na tabia ya
wanaume kushindwa kujali hisia za wenzao wakati
wanapoongea.

137
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

Kuwa wazi kueleza hisia zako na mawazo yako kuhusiana na lile


mnaloongea.Lenga katika kutatua tatizo siyo kushinda mjadala au
mabishano.Hakikisha unamsikiliza mwenzako vizuri na unaelewa
ana maanisha kitu gani kwani wanaume wengi hata kabla mke
hajamaliza kuongea tayari tunadakia“nilikuwa najua unataka kusema
hivyo”Heshimu mawazo ya mwenzi wako hata kama huwezi kupata
jibu sasa kwa tatizo alilokwambia; kuliko kutoa majibu ambayo
huishia kumkatisha tamaa. Tumia muda mwingi kufanya maongezi
kujadili mambo unayodhani ni ya msingi kuliko kutumia muda
mwingi kuongea kile ambacho si muhimu na kuacha kile ambacho ni
muhimu.Kuwa mwepesi kusamehe na mwepesi kusahau pia, ili ndoa
yako iwe imara, idumu na iwe mfano kwa wengine epuka kitu
kinaitwa "Nimekusamehe ila sitasahau."

13.2 Ongea kile unachomaanisha;


Wengi hupenda kulalamika badala ya kuongea kile anataka.Usiende
kulala kabla ya kutatua tatizo, Usilale na gubu au donge moyoni
hakikisha umeliyeyusha kabla hujalala.Usiongee na mume wako
kijeuri au kihuni au bila heshimu au kibabe hasa wanaume;
usimlaumu mwenzako mbele za watu. Unapotoa maamuzi yoyote
usitoe kwa hasira.Usianze mjadala kwa kukumbushia mambo
yaliyopita zamani hasa wanawake.Usidhani mwenzako anakuumiza
kwasababu hakubaliani na wewe inawezekana yupo sahihi hivyo
mpe muda.

Familia ilianza na mtu mmoja.“Adamu akawapa majina kila mnyama


wa kufugwa, na ndege wa angani, na kila mnyama wa mwituni;
lakini hakuonekana wa kumsaidia Adamu aliyefanana naye"
Mwanzo 2:20. Hali hiyo ya familia kuwa na mtu mmoja
haikumvutia Mungu na hivyo akaitafutia majibu.“Bwana Mungu

138
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa


kufanana naye.” Mwanzo 2:18 hali hiyo ya upungufu katika familia
ya Adamu haikuwa ya kushitukiza kwa Mungu, bali aliijua tangu
awali kuwa Adamu angehitaji mwenzi wa maisha.Umuhimu wa
familia kuwa na zaidi ya mtu mmoja imefafanuliwa. Mhubiri 4:9-10
“Afadhali kuwa wawili kuliko mmoja; Maana wapata ijara njema
kwa kazi yao. Kwa maana wakianguka, mmoja wao atamwinua
mwenzake; lakini ole wake aliye peke yake aangukapo, wala hana
mwingine wa kumwinua!”

Lakini dhambi imetengeneza mazingira ambayo wakati fulani


linaweza kukujia wazo kuwa pengine ni vema mtu kukaa peke yake
bila kuoa au kuolewa, wewe sio wa kwanza kuwaza namna hiyo;
hebu soma hii Mathayo 19:10-12 “Wanafunzi wake wakamwambia,
Mambo ya mtu na mkewe yakiwa hivyo, haifai kuoa. Lakini yeye
akawaambia, Si wote wawezao kulipokea neno hili, ila wale
waliojaliwa. Maana wako matowashi waliozaliwa hali hiyo toka
matumboni mwa mama zao; tena wako matowashi waliofanywa na
watu kuwa matowashi; tena wako matowashi waliojifanya kuwa
matowashi kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Awezaye kulipokea
neno hili na alipokee.”

Jambo moja unalolisikia mara nyingi ni wazazi kuwalalamikia


watoto wao na watoto kuwalalamikia wazazi wao kuwa hawawapi
muda wao. Kuna msemo kwa wazazi kuwa watoto wanapokuwa
watoto wanatukanyaga miguuni lakini wakiwa wakubwa
wanatukanyaga mioyoni. Lakini watoto nao wanalalamika kuwa
wazazi hupenda kujigamba kuwa walipokuwa watoto hawakuwa
wajinga wala hawakufanya yale maovu watoto wanayotenda jambo
ambalo watoto wamekuwa wakitilia mashaka. Watoto wanadai
wanajua kinachoendelea kwa wazazi wao kuliko wazazi wanavyojua
139
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

kinachoendelea kwaao. Watoto wanasema ni rahisi kupata ushauri


kutoka kwa wale wa rika lao (maana wanapatikana) kuliko kupata
ushauri kutoka kwa wazazi wao kwa kuwa ama hawapatikani au
hawana ushirikiano (ni wakali). Njia ya kulisuluhisha hilo ni kwa
wazazi kutowachokoza watoto na watoto kutokosa kuwatii wazazi
wao. Wakolosai 3:21“Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto
wenu, wasije wakakata tamaa.”Wakolosai 3:20“Ninyi watoto,
watiini wazazi wenu katika mambo yote; maana jambo hili lapendeza
katika Bwana.”

Nyumbani panatakiwa kuwa mahali pa kuvutia kwa kila mmoja


huweza kutekeleza jukumu lake na lile la mwanafamilia mwingine
bila kushurutishwa wala manung’uniko.Baba anaweza kubeba mtoto
mgongoni mama anapokuwa hayupo nyumbani na mama kujaribu
kubadilisha balbu baba anapokuwa nyumbani. Nyumbani ndio
mahali ambapo havikomi vitu vya kuwafanya mcheke na kufurahi.
Nyumbani ndio mahali ambapo watu husahihishana kwa upendo.
Waefeso 4:31 “Uchungu wote na ghadhabu na hasira na kelele na
matukano yaondoke kwenu, pamoja na kila namna ya ubaya.”
Wakolosai 3:8-9 “Lakini sasa yawekeni mbali nanyi haya yote,
hasira, na ghadhabu, na uovu, na matukano, na matusi vinywani
mwenu. Msiambiane uongo, kwa kuwa mmevua kabisa utu wa kale,
pamoja na matendo yake.”

Kutoambiana uongo inamaanisha kwamba ulichosema na kusikia


ndicho kilichomaanishwa. Wataalam wa mawasiliano wanatuambia
kuwa kuna ngazi tano za mawasiliano ambazo ni mawasiliano ya
mtu mmoja, mawasiliano ya watu wawili, mwasiliano ya kikundi,
mawasiliano ya halaiki, na mawasiliano ya umma. Kwahiyo katika
kuboresha mahusiano nyumbani mawasiliano ni kitu kisichoepukika
na kinachofanyika wakati wote (hata unapokuwa umelala),
140
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

kwasababu unawasiliana hata pale unapokuwa hujakusudia


kuwasiliana. Ili ujumbe uwe na ufanisi ni lazima uwe wazi (usio na
uwezekano wa kuleta tafsiri isiyokusudiwa), sahihi (si habari
zisizothibitishwa), unaohitajika na mpokeaji, na unaofaa kwa wakati
husika.

Mawasiliano binafsi
Haya ni mawasiliano yanayofanyika kwenye akili yako mwenyewe
bila kushirikisha upande wa pili. Mara nyingi mawasiliano haya
hufanyika kimya kimya ingawa wakati fulani yanaweza hufanyika
kwa sauti. Hapa ndipo penye kituo cha hisia zetu, imani zetu,
misimamo yetu na maamuzi yetu, hii ni dhamiri inayotushuhudia
kwa ndani, mtu wa nje yako hawezi kuisikia ingawa kwako muda
wote unakusurutisha. Luka 15:18 “Nitaondoka, nitakwenda kwa
baba yangu na kumwambia, Baba, nimekosa juu ya mbingu na mbele
yako.” Mawasiliano haya Mungu huyatumia anapotaka kukuelekeza
kitu cha kufanya, lakini pia hata shetani huyatumia kukushawishi
kufanya yaliyo kinyume na mapenzi ya Mungu.

Mawasiliano ya wawili
Haya ni mawasiliano baina ya watu wawili. Katika mawasiliano haya
kuna uwezekano wa maana iliyokusudiwa kupotoshwa. Mwanzo
3:10 Akasema, Nalisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa
mimi ni uchi; nikajificha. Kwahiyo unapowasiliana na mwenzako
kila mara hakikisha unathibitisha kile alichokisikia kama kinaendana
na kile ulichokisema au kukimaanisha. Hii ni kwa sababu kila mmoja
kati yenu ana namna ya kusikia na kutathimini vitu anavyovisikia,
jitahidini kuzizuia hisia zenu kwenye eneo hili la mawasiliano.

141
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

Kusema siyo jambo la kukimbilia kulifanya kwani linahitaji ustadi na


weledi. Ubora wa kilichosema hupimwa kwa matokeo yake. Hivyo
kilichosemwa kitakuwa na umuhimu pale kitapoweza kufikisha
ujumbe uliokusudiwa. Basi kila mtu na awe mwepesi wa kusikia,
bali si mwepesi wa kusema; wala kukasirika.” Yakobo 1:19 Yesu
anasema “Mtu akiwa na masikio ya kusikia, na asikie.” Marko 4:23.
Yesu hapa anamaanisha si kila mwenye masikio anaweza kusikia
kwa kuwa kusikia huja pale masikio yanapopewa uwezo wa kusikia
kile kisichosikiwa na masikio mengine. Kile kilichobebwa na ujumbe
na ambacho hakionekani wazi wazi kwa msikilizaji wa juu juu.

Mara zote mwanandoa mwenzako anapozungumza na kuwasilisha


ujumbe jitahidi kusikia na kusikiliza ili ikuwezeshe kuendana naye
vinginevyo utajikuta unaambulia maneno kama unajua wewe
hunisikilizi na kwa kuwa hunisikilizi inadhihirisha wazi kwamba
hunijali na hata hunipendi au mbona wengine unawasikiliza kwanini
kwamgu ni tofauti? Maneno haya sio maneno mazuri hata kidogo
kusikika kwenye ndoa zetu.

Kusikia na kusikiliza:
Kusikiliza ni kujaribu kuzielewa hisia za mwingine. Ni kukubali kile
kinachosemwa bila kuhukumu mantiki yake ama namna
kinavyosemwa. Kukubali haimaanishi kukubaliana moja kwa moja
na msimamo wa msemaji bali ni kutambua na kuelewa kuwa
kilichosemwa ndicho msemaji anachokihisi na anachomaanisha.
Kusikiliza pia humaanisha uwezo wa kurudia kilichosemwa katika
jitihada za kujiridhisha kama ulichoelewa ndicho kilichokusudiwa na
kilichokuwa kwenye hisia za mzungumzaji. Ni lazima ujiridhishe
kama kile unachokusudia kukiweka kwenye kumbukumbu zako ni
kile kilichomaanishwa na mzungumzaji au ni tafsiri yako tu isiyo
sahihi.
142
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

Kama nilivyotangulia kusema kwenye ukurasa uliotangulia hapo juu


ni kwamba, ujumbe unaotumwa na mwanadamu kwenda popote
unabebwa na vitu vitatu ambavyo ni sauti, mkao wa sauti na lugha ya
mwili. Inaonekana kwamba asilimia 7 ya ujumbe inabebwa na sauti,
asilimia 38 inabebwa na mkao wa sauti, wakati asilimia 55 inabebwa
na lugha ya mwili. Tunatakiwa tusikilize kile kilichoko nyuma ya
maneno ambacho ndicho hubeba ujumbe wenyewe yaani mkao wa
sauti na lugha ya mwili. Kusikia ni tofauti na kusikiliza. Kusikia ni
kutambua kinachoendelea kwenye akili ya mzungumzaji na utayari
wa kukipokea kwa utekelezaji wakati kusikiliza ni vile akili yangu
inavyokipokea inachosikia na inavyoathirika nacho. Kwenye kusikia
tunatafsiri na kujaribu kuelewa kile tulichosikia.

Wakati fulani kukaa kimya ni njia bora zaidi ya kuonesha unasikia.


Mithali 17:27-28 “Azuiaye maneno yake ni mwenye maarifa; Na
mwenye roho ya utulivu ana busara. Hata mpumbavu akinyamaza,
huhesabiwa hekima;Akifumba midomo yake, huhesabiwa ufahamu.”
Mithali 21:23 “Mtu azuiaye kinywa chake na ulimi wake, atajilinda
nafsi yake na taabu.” Mithali 26:20 Moto hufa kwa kukosa kuni; Na
bila mchongezi fitina hukoma. Kwahiyo sio kila unachokisia
unakijibu, vingine kwa ajili ya manufaa ya ndoa yenu unaamua
kuvipuuza kwa kukaa kimya, kumbuka kwamba mwanamke
akikasirika au kuchoshwa na jambo anaongea sana wakati
mwanaume akiwa katika hali hiyo anataka sehemu ya utulivu, kama
busara haitatumika na mwanaume ukataka kujibu kila kinachosemwa
na mkeo hata mwezi hautaisha huo muungano utakuwa
umesambaratika.

Usitarajie ukamilifu kwenye familia yako,

143
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

Hapo ndani ya nyumba yenu hayupo mkamilifu, wala wanaoishi


humo sio malaika.Kama hivyo ndivyo hakuna namna ambavyo
unategemea ndani ya nyumba kuwe na mazuri tu, hata wewe
mwenyewe sio mkamilifu. Kwahiyo kama unataka kubadilisha hali
hiyo anzia kwako mwenyewe. Mhubiri 7:20 “Bila shaka hakuna
mwanadamu mwenye haki hapa duniani, ambaye afanya mema,
asifanye dhambi.”1Yohana 1:8“Tukisema hatuna dhambi,
twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo mwetu.” Zaburi14:3
“Wote wamepotoka, wameoza wote pamoja, Hakuna atendaye
mema, La Hata mmoja.” Warumi 7:18 “Kwa maana najua ya kuwa
ndani yangu, ndani ya mwili wangu, halikai neno jema; kwa kuwa
kutaka nataka, bali kutenda lililo jema sipati.”

Maana yake ni kwamba katika maisha ya ndoa ni mhimu kujua


kwamba kila mmoja anayo mapungufu yake na kwamba anaweza
kumkosea mwenzake na kuna wakati mnajikuta mmekoseana kila
mmoja kwa mwenzake, je hali hiyo inaachwa hivyo? Hapana lazima
kuwe na mawasiliano juu ya namna ya kurekebisha hicho
kilichotokea.Na kuna wakati unaweza kudhani umefanya vizuri
kumbe kwa upande wa mwenzako unajikuta kalipokea tofauti na vile
ulivyomanisha au kusudia, kwahiyo ni mhimu kufanya mawasiliano
ili kila upande upate taarifa za upande wa pili.

Shughulikieni tofauti zenu mapema


Wakolosai 3:19 “Ninyi waume, wapendeni wake zenu msiwe na
uchungu nao.” Waefeso 4:26 “Mwe na hasira ila msitende dhambi;
jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka.” Katika misitari hii
utagundua kwamba mwanaume umepewa mzigo mzito wa
utekelezaji, umeambiwa kumpenda mkeo na usiwe na uchungu naye,
upendo unaosemwa hapa ni ule wa bila sababu, yaani akifanya vizuri
unampenda, akiteleza bado unampenda sio kuonesha mapenzi katika
144
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

nyakati za furaha tu na wakati wa misukosuko unaonekana kama


asiyehusika; hapo utakuwa hujatimiza wajibu wako sawasawa na
kumbuka kwamba unaruhusiwa kuwa na hasira lakini usitende
dhambi, kila mmoja akajitafakarishe hili litawezekanaje?

Msikumbushane dhambi mlizosameheana


Isaya 43:25 “Mimi, naam, mimi, ndimi niyafutaye makosa yako kwa
ajili yangu mwenyewe, wala sitazikumbuka dhambi zako.” Luka
23:34 “Yesu akasema, Baba, uwasamehe, kwa kuwa hawajui
watendalo. Wanandoa wengi wako kwenye ndoa kwa kutegesheana
makosa, unaongea na mtu ana orodha ya makosa kayatunza kama
anavyotunza nguo zake, mwenzetu haisaidii hata kidogo isipokuwa
inakumaliza mwenyewe bila kujijua.Iko namna hii inapotokea
mkakaa chini kwa lengo la kumaliza tofauti zilizopo ndani ya ndoa
yenu ambazo pengine zimetokana na kupishana kwenye kupashana
habari kwa namna yoyote ile usianze na kumbukumbu ya yale
ambayo yamekuwa yakitokea nyuma,usije na orodha ya unakumbuka
wakati fulani ulifanya hivi nikasamehe,juzi kati ukanikosea tena
nikakusamehe na nyingine nyingi. Kufanya hivyo ni kutonesha
kidonda cha mwenzako. Lakini ubinadamu wetu ndio unaosababisha
tuwakosee wenzetu,hivi kwa namna tunavyomkosea Mungu
angetuhesabia nani angesimama?

Msilipize kisasi
Kulipa kisasi kwenye ndoa ni jambo baya sana, ni nani hasa
unayemlipa kisasi? Kumbuka kwamba mke hana amri juu ya mwili
wake na kadharika wewe pia na katika ulimwengu wa roho miili
yenu mmebadirishana, ikiwa hivyo ndivyo maana yake ni kwamba
kisasi unacholipa unajilipa mwenyewe, maanandiko yanaonyesha
wazi kwamba kulipa kiasi ni dhambi Warumi 12:19-21 wapendwa,
145
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

msilipize kisasi,bali ipisheni ghadhabu ya Mungu, maana


imeandikwa: “Kisasi ni juu yangu, mimi nitalipa, asema Bwana.”
Badala yake: “adui yako akiwa na njaa, mpe chakula, akiwa na kiu,
mnyweshe.Maana ukifanya hivyo,utampalia makaa ya moto
yanayowaka kichwani pake. Usishindwe na ubaya, bali uushindeni
ubaya kwa wema.

Shetani amefanikiwa kutuondoa kwenye kusudi la Mungu kupitia


visasi ndani ya ndoa, eneo kubwa ambalo linaongoza kwa visasi ni
kutoka nje ya ndoa (kuwa na mahusiano ya kindoa na asiyekuwa
mke au mume wako).Kufanya hivi kwa walokole ni dhambi maana
unakuwa unazini.Kinachotokea kwenye ndoa ni mmoja kupata tetesi
za mwenzake kutokuwa mwaminifu badala ya kukaa chini na
kuzungumza naye huku akimtwika Mungu fadhaa zake ambaye
kimsingi ndiye aliyewaunganisha naye anaamua kulipa kisasi kwa
kuitii sauti ya shetani inayomwambia kwani wewe umekosa nini
mpaka anakufanyia hivi? Kwani wewe ukifanya itakuwaje? Angejua
ni vibaya kufanya hivyo kwanini yeye alifanya au anataka kujiona
yeye ndio bora? Hayo yanapojaa masikioni anashindwa kugundua
kwamba ni sauti ya adui ambayo inamshawishi ili kusudi aharibikiwe
kwa kuwa kinyume na mpango wa Mungu kwake, anaamua kuitii na
kujikuta akilipa kisasi.Mungu atupatie neema yake katika eneo hili ili
tushinde.

Mungu anawapenda wenye dhambi.


Yesu alipokuwa akila chakula nyumbani kwa Lawi, watoza ushuru
wengi pamoja na wenye dhambi walikuwa wakila pamoja naye na
wanafunzi wake, kwa maana kulikuwa na watu wengi waliokuwa
wakimfuata.Baadhi ya walimu wa sheria na mafarisayo walimwona
akila pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi,wakawauliza
wanafunzi wake,mbona Yesu anakula pamoja na watoza ushuru na
146
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

wenye dhambi? Yesu aliposikia haya akawaambia, walio wazima


hawahitaji tabibu, bali walio wagonjwa. Sikuja kuwaita wenye haki,
bali wenye dhambi Marko 2:15-17, maana yake ni kwamba ili
tuweze kudumu kwenye ndoa lazima tujue tunaishi na watu ambao
sio wakamilifu, ni wadhambi ambao tunatakiwa kuwapenda kila
mara na kwa nguvu zetu zote.

Warumi 5:8 “Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe


kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa
tungali wenye dhambi.” 1Yohana 3:1 “Tazameni, ni pendo la namna
gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu na ndivyo
tulivyo.Kwasababu hii ulimwengu haututambui,kwa kuwa
haukumtambua yeye.Warumi 8:32-33 Yeye asiyemwachilia Mwana
wake mwenyewe, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje
kutukirimia mambo yote pamoja naye?Ni nani atakayewashitaki
wateule wa Mungu? Mungu ndiye mwenye kuwahesabia haki.”
Yote katika yote mistari hii inatuhimiza kupendana bila kujali
chochote hata Yesu alitupenda tulipokuwa hatuna thamani, usisahau
kwenye maagizo ya ndoa yupo mmoja aliyeagizwa kupenda kuliko
mwingine; huyo mistari hii inamhusu zaidi.

13.3 Madhara ya mawasiliano hafifu kwenye ndoa


Mawasiliano kwenye ndoa ni jambo la umuhimu sana, ni kama
chumvi kwenye chakula.Baada ya kuchunguza nimekuta ndoa nyingi
hazina furaha zimejaa migogoro ya mara kwa mara kwa kwasababu
ya kukosa mawasiliano mazuri, sijui kama wanandoa wanafanya kwa
bahati mbaya au nikutokujua umuhimu wa jambo hili katika maisha
yao ya ndoa. Kila mmoja anawaza kivyake anaishi kivyake anapanga
mipango kivyake na kutenda yale anayoyaona yanamfaa kwa ajili
yake mwenyewe. Sasa ndoa ambayo inaishi kwa mtindo huu ambapo
hakuna mawasiliano baina ya mume na mke sidhani kama ndoa hiyo
147
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

itakuwa na furaha, bali ni ndoa itakayoongoza kwa matatizo na


migogoro.

Kukosa mawasiliano katika ndoa ni sawa na gari zuri lakini likakosa


injini sidhani kama gari hio pamoja na uzuri wake litatembea.
Vivyohivyo ndoa ikikosa mawasiliano hufa na kupoteza mwelekeo
wake. Ili kujenga na kuimarisha ndoa ni lazima wanandoa wenyewe
waamue kujenga mnara wa mawasiliano mazuri baina yao, wakae
pamoja kila siku waongee na kushauriana juu ya maisha yao
wenyewe na kuhusu malengo ya watoto na mipango ya baadaye.
Wakiwa faragha wanandoa wanashauriwa kuwa wanazungumza na
kuambiana juu ya hisia zao pamoja na kuwekana wazi kwa baadhi ya
mambo ambayo unatamani mwenzio ajipambe nayo. Huu ndio
wakati wa kuchagua nini unapenda kifanywe na mwenzako ili
ufurahi zaidi. Angalizo mazungumzo haya yasitumike kama mtego
wa kumnasa mwenzako hasa atakapokuambia jambo jipya ukadhani
kalifahamu kwa kuwa alikwenda kujifunza nje.

Mawasiliano ni muhimu sana, usikubali hata kidogo kutofautiana na


kugombana kwenu kuwanyamazishe kuongea na kunahisiana. Pia
kuna baadhi ya mambo yanayochangia sana ndoa kukosa maelewano
kwasababu ya kutokuwa na mawasiliano mazuri baina ya wanandoa
hao.Kwanza kabisa ni hili jambo la mwanamume kuwa mkali
anapokuwa nyumbani kwake.Yaani unapokuwa na familia yako
wewe ni kufoka tu na kutoa amri za ajabuajabu unapoongea wewe
hutaki mtu yeyote akushauri wala apinge hili linapelekea hata mkeo
anaanza kuogopa kuongea na wewe akidhani kuna mahali anaweza
kusema tofauti na fikra zako mkaishia kugombana; kadhalika watoto
pia hawako huru kutaka kukaa na wewe. Mwanaume mwenzangu
husi sio uanaume unaotakiwa bali ni udikiteta ndani ya nyumba na

148
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

ninakuhakikishia hujengi ila unabomoa, hakuna kujenga kwa namna


hiyo kwamba akili yako ndiyo pekee inaweza na kujua kila kitu.

Jambo lingine linalokata mawasiliano baina ya wanandoa ni kazi,


wewe na kazi na kazi na wewe tu yaani unatumia muda mwingi sana
katika kufanya kazi hata ukiwa nyumbani unapafanya ni sehemu ya
kazi pia. Kufanya kazi sio jambo baya lakini hakikisha kazi hiyo
isiwe chanzo cha kukatika kwa mawasiliano. Mfano mvua ni nzuri
na kila mmoja anaihitaji kwasababu tofauti tofauti lakini inapozidi
inaharibu barabara na kusababisha mawasiliano ya pande mbili
kukatika. Je hawa waliokatikiwa mawasiliano huendelea kuisifia
mvua au huilaani? Ndivyo ilivyo kwenye kazi yako siku ikikata
mawasiliano kwenye ndoa yako. Inafika wakati ukirudi umechoka
hauna muda wa kukaa na mkeo pamoja na watoto wako hata kwa
robo saa. Wewe ukitoka familia imelala ukirudi familia imelala.
Jambo hili ni baya sana kwenye ndoa tena ni baya sana maana
utakuwa haujui hata maendeleo ya watoto wako wala afya zao.
Jibane japo kwa uchache robo saa tu ya kukaa na familia yako
mcheke na kufurahi kwa pamoja au ukiona haiwezekani basi jitahid
mda wa chakula kula pamoja na familia yako tena ikiwezekana
kwenye sahani moja.

SMATPHONE hili ni jinamizi lililotenganisha ndoa nyingi sana


katika zama hizi. Kwani wanandoa wengi si wa kike au wa kiume
hutumia muda mwingi kwenye simu janja wakiwa wanaperuzi
kwenye mitandao ya kijamii tena mbaya zaidi unaweza kuwakuta
wanandoa wapo chumbani wenyewe wawili tu lakini kila mtu yupo
bize na vidole vyake kwenye simu badala ya kutumia muda huo
kubadirishana mawazo, jambo hili ni baya sana tena ni baya mmno.
Kwanza hupunguza mapenzi kati ya mke na mume na ni rahisi
kupata vishawishi vya mtu kwenda kinyume na ndoa yake.
149
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

Tuelewane, sikatazi wanandoa kuingia kwenye mitandao ya kijamii


ninatoa ushauri kuwa kufanye kwa kiasi na kwa muda maalumu na
pindi unapokuwa na mwenzako basi zima data na uhamishie hisia
zako mikono yako na vidole vyako katika mwili wa mwezio peruzi
katika mwili wa mwenzio utakavyo huku mkiongea juu ya
mustakabali wa maisha yenu na watoto wenu.

Hebu mfanye mwenzako aelewe kuwa unamjali na kumpenda


jitahidi muongee muda wote nafasi inapopatikana acha kutumia simu
au kuangalia TV ukiwa na mwenzako chumbani.Na kukitokea
hitilafu au malumbano ndani ya ndoa yako basi jifunze kuufunga
mdomo wako na kama ukiufungua basi lainisha maneno na useme
kwa lengo la kuijenga ndoa yako na kumjenga mwenzako. Siri ya
kudumisha ndoa yenye furaha ni pamoja na kuoa au kuolewa na mtu
ambaye ni rafiki yako. Kwa maana nyingine urafiki mwema
hupelekea kuwa na ndoa yenye furaha baadaye. Msitegemee kuwa
tendo la ndoa pekee ndilo lijenge ndoa yenu hapo mtakuwa
mnajidanganya, fikiria kama ikitokea kwa bahati mbaya mmoja
wenu akafanyiwa upasuaji utakao pelekea kutofanya tendo la ndoa je
mtaendelea kuifurahia ndoa yenu au ndio mtaishia hapo?

Hakikisha hukati mawasiliano na mke au mume wako, likitokea


jambo linalowakwaza, kaeni ninyi wawili mlimalize. Hakikisheni
mnadumisha upendo wenu wa kwanza mlio anza nao. Kumbuka
ndoa ni kitu kigumu kinahitaji kila mmoja kujitoa kikamilifu kwa
mwenzake pamoja na kumuona mwenzake ni wa muhimu sana
kwake.

150
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

SURA YA KUMI NA NNE


NDOA YENYE FURAHA
Ndoa ambayo itadumu kuwa na furaha katika muda wote ni ile
ambayo wanandoa wataelewana na kudumisha mawasiliano kama
mwanzo yaani kama walivyokuwa wakiwasiliana kabla ya kuona.
Jaribu kupiga picha kipindi cha uchumba wenu, hivi ulikuwa
unajisikiaje unapohitaji kuwasialiana na mchumba wako harafu
kukawa na kikwazo katikati, ulipata usingizi au ulisumbuka?
Inakuwaje wakati ule ulisumbuka lakini sasa hivi huoni shida hata
mwezi unakatika bila kuwasilina na mke au mume wako?
Unakumbuka namna mlivyokuwa mkiongea kwa furaha na kufikia
hatua ya kugonganisha mikono? Hali hiyo iko wapi sasa? Nani
kaichukua na kwa nini? Yafuatayo ni mambo ambayo kama
yakifuatwa na wanandoa kikamilifu yaweza kuwafanya kuishi kwa
furaha katika maisha yao ya ndoa.

1. Usikate mawasiliano
Kumbuka siku unakutana na mchumba wako kwa mara ya kwanza
mlielewana kwa njia ya mawasiliano, hivyo bila mawasiliano mazuri
kati ya mke na mume fahamu ndoa yenu iko kwenye matatizo.
Kuongea pamoja, kuelezana pamoja kile ambacho kila mmoja
anakihitaji katika maisha yenu ya ndoa huleta maelewano mema kati
yenu. Ni kweli kwamba kadri mnavyozidi kuishi pamoja
mawasiliano yaweza kupungua kwasababu ya kuzoeana sana lakini

151
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

kamwe msiruhusu kabisa mawasiliano kukatika. Mawasiliano mema


kati yenu ni muhimu katika kuelewa hitaji la mwenzako na huleta
furaha katika mahusiano yenu.

Mawasiliano ni muhimu, tumia maneno mengi zaidi kuwasiliana na


Yule uliyemchagua kuishi naye japo vitendo ni muhimu zaidi kama
kumshika mkono, kumkumbatia, kumvalisha, kuvaa nguo wewe
mwenyewe nguo nzuri, jipulizie pafumu ile ambayo mke au mume
wako anaipenda, mpe zawadi japo ni ndogo na za kawaida, vitu hivi
huboresha sana mawasiliano ya wana ndoa.

2. Sikilizaneni
Masikilizano mema ni muhimu kwa afya ya ndoa yenu. Kuwa tayari
muda wote kumsikiliza mwenzako. Baada ya ratiba ngumu za siku
kuwa na hamu ya kumsikiliza mwenzako kwa kumuuliza maswali
mbalimbali, lakini kumbuka wakati mwingine hata mke au mume
wako naye anahitaji kukuuliza au kukusikiliza, hivyo epuka kutoa
hitimisho wewe tu! Fungua masikio yako na usikilize kile
anachosema mwenzako. Usitake kuwa mzungumzaji wa mwanzo
mwisho kama mhubiri kanisani, humo ndani ni kuzungumza sio
kuhubiri, hakuna hotuba kuna mazungumzo maana yake unasema
ulichonacho na kutoa nafasi kwa mwenzako naye kusema alicho
nacho huku ukisikiliza.

3. Ucheshi na ukweli
Moja ya kitu muhimu sana katika kuwa na ndoa bora ni ucheshi kwa
wana ndoa. Ni vigumu sana kubaki na hali ya kufurahi na kucheka
pamoja lakini mnaweza kufanikiwa katika hili kwa kutembelea wote
katika maeneo mapya kwa pamoja mkiwa wenyewe tu wewe na
mume ama mke wako. Kuwa muwazi na mkweli ni msingi muhimu
sana kwa wanandoa, hakikisha unakuwa mkweli kwa mke au mume
152
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

wako hiyo itawafanya muaminiane wote na ndoa yenu itakuwa ni ya


furaha siku zote.

4. Onyesha upendo
Hakikisha unatumia muda mwingi kuongea na yule umpendaye.
Unaweza kuwa mbali na mume au mke wako lakini unaweza
kumudu kuongea na umpendaye hata kwa njia ya simu, ili mradi tu
kuonyesha kuwa unampenda na kumjali. Onyesha unampenda sana
mke au mume wako daima. Kila siku hakikisha unadhihirisha
upendo wako kwake usichoke.Mbusu mke au mume wako,
mkumbatie kila mara kama ishara ya upendo. Kama mtapendana kwa
dhati basi bila shaka mtaheshimiana, na kila mmoja atamthamini
mwenzake. kila siku tafakari kwa nini ulimpenda yeye tu na wala si
mwingine, hii itakufanya umpende zaidi.Usijali wengine watasema
nini juu yako, shida kubwa inayotukabili ni kule kushindwa
kuonyesha upendo kwa wake au waume zetu kwa kuogopa macho ya
watu;wanaume wanaogopa kuambiwa wameshikwa na wake zao,
sielewi hivi kushikwa na mke wako ni kosa? Sasa kama hujashikwa
na mke wako ambaye ni nyama katika nyama zako unataka kushikwa
na nani zaidi?

5. Furahi pamoja na mke au mume wako


Kudumisha upendo kwa wanandoa ni rahisi tu, furahia kuwa pamoja
na umpendaye, ongeeni pamoja, fanyeni mambo mbalimbali ya
kifamilia pamoja na kwa upendo.Wakati watu wawili wanapoishi
pamoja, ni lazima watatofautiana kwa baadhi ya mambo kwasababu
binadamu wote tunatofautiana namna tunavyo fikiri na kutoa
maamuzi.Wakati hali ya kutoelewana inapotokea kwa wana ndoa,
tumieni hekima kumaliza tofauti hizo ili kuacha upendo wenu uzidi
kuwa imara na wala si dhaifu.
153
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

6. Kuvumiliana.
Wanandoa wanaofanikiwa katika maisha yao ni wale wanaopokea na
kutoa msamaha. Ni wale wanaosamehe na kusahau makosa ya
wengine.Hivyo kusameheana ni jambo la muhimu sana katika
mahusiano.Wanandoa wanaofanikiwa kuishi muda mrefu wakiwa na
furaha daima ni wale wanaovumilia hali zote za maisha. Mfano
wakati wa magonjwa, wakati wa utajiri, wakati wa umaskini, wakati
wa afya njema. Kama wanandoa wataweza kuvumiliana katika hali
zote basi wataishi kwa furaha.

MAMBO 9 YATAKAYOMFANYA Mke WAKO KUFUNGUKA

Mfanye ajisikie Maalum. Hili ni hitaji la ulimwengu kwa


wanawake wote. Mfanye mke wako ahisi kuwa maalum. Hakikisha
anahisi kama yeye anatosha na unamtamani yeye tu. Mtende kama
mwanamke. Fanya vitu kama vidogo vidogo ambavyo kwa macho ya
kawaida vinaonekana kama havina maana kama kmfungulia mlango
wa gari kama mmebarikiwa kuwa nalo, zungumza naye kwa upole na
kutumia wakati pamoja naye. Ikiwa anafanya kazi kwenye kampuni
yako au unayoiongoza, majibu yako kwa wanawake wengine yawe
kama mke wako yuko pembeni yako.Usiwajibu wanawake wengine
hovyo kwa kuwa si mkeo, akisikia hivyo hujihisi vibaya kwani akili
yake humtuma kwamba hivyo unavyowaona wanawake wengine
ndivyo unavyomwona yeye hata kama husemi. Heshimu ndoa yako
utabarikiwa sana kama utamfanya mke wako ajue kuwa yeye ni
maalum na mhimu kwako.

Kuwa tayari kujitoa dhabihu kwake. Mwanamke anakuwa


mwenye furaha ikiwa anao uhakika kwamba yuko salama na
kwamba mume wake yuko tayari kufa kwa ajili yake. Iko namna hii
154
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

mara zote wanawake wanaamini mwanaume anatangulia kufa na


kwahiyo anatamani kupata uhakika kwamba hata kama ukifa bado
ataendelea kuwa na thamani ile ile ya wakati wa uhai wako? Ikiwa
utamuuliza mwanamume kama atakuwa tayari kuandamana mbele ya
mshambuliaji ikiwa bunduki inaelekezwa kwa mkewe; wanaume
wengi hujibu bila kusita; NDIYO. Hii ni kweli hata ikiwa wako
kwenye hatihati ya talaka. Lakini huyu mtu huyo hatakwenda pwani
naye kwa sababu anachukia pwani.Kama bado hujawa katika
kiwango cha kujitoa kufa kwa ajili ya mke wau mume wako bado
kuna kitu kinapungua kwenye ndoa yao. Kumbuka mke huja kwako
kwa maana ya kufa na kuzikana.

Weka mahitaji yake mbele. Wanaume wengine kimsingi wana


makosa kwa sababu ni wabinafsi. Wanaume hawa hawajui maana ya
kuwa na ndoa na hata hawaoni thamani ya mke. Mwanaume wa
namna hii huwaona ndugu zake na marafiki kuwa bora kuliko
mkewe, wengine huwathamini sna wazazi na watoto kuliko mke.
Haimaanishi wazazi na watoto wasipendwe hapana hao wanapashwa
kuwa namba mbili baada ya huyu ambaye ulipewa na Mungu.
Kumbuka wazazi wako hukuwachagua ili wawe wazazi ila mkeo
ulimchagua mwenyewe hwa hiari bila kushurutishwa na mtu,
kumweka nyuma ni kujishusha mwenyewe. Ikiwa unataka mke wako
akupende, akupe umakini na juhudi anayostahili basi mweke mbele
na mpe thamani anayoistahiri."Mbingu haitakuwa mbingu kwangu
ikiwa sikutana na mke wangu huko." ~ Andrew Jackson

Sikiza hisia zake. Najua hii ni rahisi kusema kuliko kufanya.


Ninachukulia kusikiliza kuwa aina ya sanaa ambayo ukiijua utaunda
kuthamini na heshima ambayo watu wengi hawatapata. Wanaume
kwa ujumla ni wasikilizaji duni kwa sababu tunachukua vitu vile
155
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

vile. Lazima ujiepushe na lugha kama vile "kila wakati" na


"washirika" wakati mke wako anapoongea. Tafuta ujumbe wa kina
kutokana na hisia zake. Shida wanaume tunataka kutazama mambo
kwa namna tunavyoona sisi wakati ukweli na uhalisia tumeumbwa
tofauti. Hapa kwenye kujali hisi ndipo penye chanzo kikubwa cha
migogoro mingi kwa kuwa maongezi mengi ya wake zetu hutokana
na namna wanavyohisi. Kwahiyo hukasirika sana pale wanapoona
kwamba hatujali kile wanachokiongea badala yake mawazo na akili
zetu ziko juu ya kitu kingine tofauti na kile kinachoonekana kuwa
kinachoendelea. Angalia taarifa zake za kihemko kama hitaji lake la
kuelewa na kuungwa mkono na kutofautisha juu yako.

5) Toa Haki Yako ya Kukasirika Na Yeye. Jitoe mwenyewe kuwa


utaacha kukasirika na mke wako na uangalie jinsi faida zinaanza
kutuliza. Mke wako anajua kuwa yeye si kamili na atakushukuru
sana ikiwa hautakasirika naye. Wanawake wengi hawapendi watu
kuwa na hasira nao. Fanya hali yako kuwa shwari na iliyowezeshwa
iwezekanavyo badala ya kutisha au kutenda hasira. Atakuona kama
Bingwa wake!

6) Angalia Nyuma yake. Usiruhusu familia yako izungumze vibaya


juu ya mke wako. Sio kwa uso wake au nyuma yake. Wakati uko nje
kwa umma; kumfanya ajisikie salama kwa kuwa macho kwa
mazingira yako na mwamko wa hali. Wewe ni mrefu vipi kama
mwanaume? Mke wako ni mrefu kiasi gani? Ikiwa wewe ni urefu wa
futi sita na ana urefu wa futi tano; ana uzoefu tofauti sana kuliko
wewe wakati mbele ya wengine. Mfanye ajue anaweza kukutegemea
ili umlinde.

156
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

7) Fanya kazi na Mbwe zake, sio dhidi yao. Waume wengi


hukasirishwa na mkewe kwa sababu hawatafsiri hisia zake kwa
usahihi. Waume wanaposikiliza, wanatafsiri kuwa wanafanya kazi ya
lousy na hawathaminiwi kwa bidii yao. Wanaume, msichukue
mambo kibinafsi. Wakati mwingine mke huwa mnyonge kwa sababu
amechoka au hajisikii vizuri. Inaweza kuwa na uhusiano wowote na
mume. Weka akili hii wakati ujao inaonekana kuwa mke wako ana
amnesia juu ya ndoa yako ni kubwa au ikiwa unajiona amesahau
kuwa wewe ni mume mkubwa.

"Hakuna kitu bora au cha kupendeza zaidi kuliko wakati watu wawili
ambao wanaona uso kwa nyumba kama mtu na mke, wakichanganya
maadui zao na kufurahisha marafiki zao." ~ Homer

8) Usiongee Ugly kwake. Haijalishi unasikitishwa sana au mke wako


anaweza kuwa mgumu sana; usimwite majina yake. Hata ikiwa
atajibu kwa kejeli au kwa maana ya maneno; usimrudishie maneno
yake. Najua hii haionekani kuwa sawa. Zaidi ya kile ninachosema
hapa sio sawa. Hii sio juu ya usawa. Hii ni kuhusu kuwa mtu wa
heshima na heshima. Kuwa mtu ambaye anaweza kudumisha
msimamo huu wa kuwa mtu mzuri hata wakati mambo ni magumu.

9) Mfanye Umuhimu Wake. Ikiwa mke wako anakuuliza msaada


fulani na kitu; acha kile unachofanya na umsaidie. Usifanye mazoea
ya kumuacha kila wakati na kumwambia utafika baadaye. Hii sio
tabia ya "Ndio mpendwa" bali ni mashindano ya vitendo.

"Mke na afanye mume afurahi kurudi nyumbani, na amfanyishe


huruma kumuona aondoka." ~ Martin Luther

JINSI YA KUWA Mke Mkuu

157
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

Jinsi ya Kuwa Mke Mkubwa ~ Siri 7 Ambazo Atakuwa Na Mume


Wako Kubusu Ardhi Unayotembea

"Nyuma ya Kila Mwanadamu Aliyefanikiwa Ni Mwanamke


Mkubwa!" ~ Mwandishi Haijulikani

1) Mjengee kama Mlinzi wako. Je! Unaamini mumeo? Je!


Unamfanya ahisi nguvu kwa maneno unayosema au unamshusha na
kumfanya ahisi dhaifu? Je! Unafuata uongozi wake au unavunja
mjeledi na unatarajia kufuata kila amri yako? Wanaume daima
wanajua ikiwa mwanamke wao anamwamini au la. Mwezesha mume
wako na uangalie wasiwasi wako mwenyewe unapungua. Shika
mkono wake wakati uko nje kwa umma. Mwambie kwamba
hukufanya uhisi salama.

2) Kuwa wazimu katika Kupenda Naye. Onyesha upande wako wa


kucheza, mzuri. Kuwa mjinga. Kuwa rafiki yake. Mpe tabasamu lako
bora; kama ile ungepeana na askari wa trafiki ikiwa unakaribia
kupata tikiti la kasi. Msamehe makosa ya zamani zake na uwe hatari
tena. Usitembee njia ya wafu walio amini ambao wanaamini kuwa
harusi ya jua inapaswa kuisha. Jicho la nyanya ni wazo na linaweza
kudumishwa na kukuzwa na tabia ya kupendeza ya upendo.

"Katika suluhisho zote za nyumbani, mke mzuri ni bora." ~ Kin


Hubbard

158
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

3) Kuthamini; Sio muhimu. Kumbuka kumshukuru mumeo kwa vitu


anavyofanya. Watu wote wanapenda kuthaminiwa na waume
wanakuwa waume wakuu wakati juhudi zao zinakubaliwa. Ni kosa la
kawaida kuwa mpata makosa lakini hii huvunja roho ya mtu kwa
wakati. Usichukue nafasi. Ni rahisi kupuuza nzuri anakufanyia.
Wake wengi huzuni kwa vitu ambavyo hafanyi wakati kwa kweli
yeye hufanya sana. Ikiwa mumeo ni mtoaji mzuri; basi ikubali. Ikiwa
yeye ni zaidi ya mtoaji mzuri; kumaanisha yeye ni mtu wa kufikiria,
wa kufurahisha, na wa kimapenzi; basi kweli kumwaga juu ya
shukrani. Kwa muda mrefu kama mumeo anafanya angalau katika
aina ya 80% ya matarajio yako, tafadhali acha ruhusa ya kawaida ya
20%.

4) Mwonyeshe Heshima na Mbali ya hatua. Wake wengi hutenda


haki hadharani lakini wapewe nyumbani nyuma ya milango
iliyofungwa na Bwana awasaidie. Kuwa mwepesi wa hasira. Acha
mumeo azungumze bila usumbufu, kukosoa au kurekebisha. Waume
mara nyingi hupata rep mbaya kama wasikilizaji lakini wake
wanaweza kuwa mbaya tu.

"Mimi na mke wangu Mariamu tumeoana kwa miaka arobaini na


saba na sio mara moja tukawa na hoja kubwa ya kutosha kuzingatia
talaka; mauaji, ndio, lakini talaka, kamwe. " ~ Jack Benny

5) Kuwa Shabiki wake Mkubwa. Ikiwa unataka kuleta sifa bora


katika mumeo, mpe moyo. Kila mtu anahitaji kutiwa moyo.
Usiruhusu mumeo aende bila kipimo cha kila siku cha maneno
mazuri kutoka kwako. Watu hustawi kwa kutia moyo. Ikiwa mumeo
hatapata kutoka kwako, atatafuta masaa mengi kazini au kwa kupiga
risasi kulungu. Atapata sifa kwa njia moja au nyingine. Usifanye
mumeo aifute kupitia vyanzo vya nje kwa sababu hakuipata kutoka
kwako.
159
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

"Ndoa nyingi itakuwa bora ikiwa mume na mke wataelewa wazi


kuwa wako katika upande mmoja." ~ Zig Ziglar

6) Msalimie Kwa Ushawishi. Ninawaambia wanaume wasaliti wake


zao kwanza na wafanye hivyo kwa shauku. Wake, unaweza
kuchukua ndoa yako kwa kiwango kikubwa cha kutimiza ikiwa
utakutana naye na roho ile ile ya furaha. Wacha uso wako uangaze
kwa njia ambayo unaonyesha kwamba unafurahi kumwona. Fanya
hii tabia ya kufanya hata ikiwa una siku mbaya. Kamwe usiruhusu
hali kuamuru jinsi unavyompenda mwenzi wako. Bila shauku, ndoa
yako itasimamiwa kwa kiwango cha utapeli.

7) Pendezwa na Masilahi yake. Sitasahau siku niliyorudi nyumbani


kubadili mtindo wangu wa Taekwondo na mke wangu alikuwa
amevaa sare mpya na akasema "Nadhani ningependa kwenda nawe
usiku wa leo." Alikaa nayo kwa miaka na kuwa bingwa wa serikali
mara tatu miaka mbili mfululizo alipopata ukanda wake mweusi.
Tulikuwa na mafunzo mazuri ya wakati na kwenda kwenye
mashindano pamoja. Mume wako anavutiwa na nini? Sio lazima
upate ukanda wako mweusi lakini angalau unaweza kujifunza lugha
ya mambo ambayo mume wako anapendezwa nayo; chochote
kinachotokea kuwa.

"Heri mtu anayepata rafiki wa kweli, na anafurahi zaidi ambaye


hupata rafiki huyo wa kweli katika mke wake." ~ Franz Schubert

160
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

KUHUSU MWANDISHI
MWANDISHI
Edward B. Saimon ni mtoto wa kwanza kuzaliwa katika
familia yenye watoto sita ambayo ni ya bwana na bibi
Bihaga Saimon Masela. Huyu ni mwalimu wa malezi ya watoto na
vijana, amekuwa akifundisha semina mbalimbali kwenye jamii na
kanisani.

Kitaaluma ni msomi ambaye amesoma shada ya kwanza ya ustawi


wa jamii na utawala kutoka chuo kikuu cha Makerere nchini Uganda
na shahada ya uzamili katika sheria (LLM) kutoka chuo kikuu cha
Atlantic International cha Marekani. Ndugu Edward ni mkurugenzi
mtendaji wa taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Umoja wa
wawezeshaji KIOO iliyopo Kigoma, pia ni mkurugenzi mtendaji wa
kituo cha elimu na mafunzo ya ufundi kilichopo Ilagala. Ni mratibu
wa mashirika yanayojishughulisha na lishe nchini kwa kanda ya
161
Mambo ya kuzingatia ili kuwa na ndoa yenye furaha……….. Edward B. Saimon

Magharibi. Pia ni mjumbe wa bodi mbalimbali zikiwemo za shule,


Maji na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali. Amekuwa akishiriki
katika mambo mbalimbali ndani ya jamii ambayo yamempa uzoefu
na uelewa juu ya jamii na changamoto zilziopo kwenye jamii.

Kwa upande wa familia yeye ni baba wa watoto watatu ambao


wameelezwa vizuri kwenye eneo la shukrani. Ninajivuna kuwa hivi
nilivyo na ninamshukuru Mungu kwa karama na kipaji hiki.

162

You might also like