Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 4

MUHULA WA TATU 2021

SHUGHULI ZA KISWAHILI

GRADE YA NNE

VIWANGO VYA KUTATHMINI

KUZIDISHA KUFIKIA KUKARIBIA MBALI NA


MATARAJIO MATARAJIO MTARAJIO MATARAJIO
KUSOMA
UFAHAMU
SARUFI
KUANDIKA

SEHEMU YA KWANZA

KUSOMA (alama 10)

Soma kwa sauti kifungu ulichopewa.

Mtoto tiifu ni mwema. Si mjeuri. Si mtukuku. Ana heshima na adabu njema. Akiitwa huitika
vizuri na kwa heshima. Akitumwa hakatai. Akikanywa asifanye kosa hutii.

Mtoto tiifu huwapenda wazazi wake. Huwasaidia wazazi wake kwa kazi zote za nyumbani.
Hazururi ovyoovyo na kuenda na watoto wengine watukutu. Yeye akitaka kutoka nyumbani
kwenda mahali huomba ruhusa kwa wazazi. Nao wazazi wakikataa asiende, hakasiriki wala
hanuni na kuvimba mashavu kama paka.

Mtoto tiifu hupenda masomo shuleni, hachelewi kuingia darasani. Hufanya kazi zote za
shuleni na huwasikiliza walimu wake kwa makini. Pia, hagombani na watoto wengine shuleni.
Yeye ni mfano mwema shuleni na nyumbani. Je, wewe ni mtoto mtukutu au tiifu?

SEHEMU YA PILI
UFAHAMU (alama 10)

Soma ufahamu kisha uyajibu maswali

RAFIKI YANGU

Rafiki yangu anaitwa Fatuma. Yeye ni msichana mwenye rangi ya kahawia . Yuko katika
darasa la nne katika shule ya Msingi Tumaini. Anaishi katika mtaa wa Mali pamoja na wazazi
wake.

Fatuma ana umri wa miaka kumi. Ana bidii sana katika masomo yake na somo
analolipenda sana kuliko yote ni Kiswahili. Husema ya kwamba Kiswahili ni lugha ya taifa na
kimataifa na hivyo anataka Waafrika wajivunie lugha yao ya Kiswahili. Hapendi jinsi waafrika
weusi wanavyofurahia lugha ya Kiingereza na kubeza Kiswahili. Yeye anataka kuwa mtangazaji
na pia mwandishi wa vitabu vya Kiswahili.

Rafiki yangu ni mzuri sana kwa sababu ni mpole, mnyenyekevu na mcheshi. Anapenda
sana kufurahi kila wakati. Mimi nampenda kwa sababu hunihimiza kutia bidii katika masomo.
Pia hunisaidia masomo mengineyo kama vile Hesabu na Sayansi. Tukiwa na shida husaidiana na
ndio sababu tunapendana sana.

Maswali
1. Rafiki ya mwandishi anaitwa _____________

2. Rafiki wa mwandishi ni wa jinsia ipi? ____________

3. Taja sifa tatu za rafiki aliyetajwa ____________, ___________, _______________

4. Rafiki ako katika darasa la ___________________

5. Anaishi katika mtaa wa ____________

6. Rafiki yangu ana miaka _________________

7. Somo analolipenda ni lipi?

8. Yeye anataka kuwa nani maishani?

9. Waafrika wanafurahia lugha ya _____ na kubeza Kiswahili.

10. Rafiki yangu hunisaidia katika masomo kama ________________

SEHEMU YA TATU

SARUFI (alama 30)

1. Kanusha
(a) Mama ameenda sokoni.
___________________________________
(b) Mkulima alinunua mbegu nyingi
________________________________________
(c) Tunaenda shuleni
____________________________________________
(d) Mwalimu atawaadhibu wanafunzi watukutu.
__________________________________________________
(e) Kesho nitasafiri mjini.
___________________________________________________
2. Tambua aina ya neno lililopigiwa mstari katika sentensi zifuatazo.
(a) Mkeka umeliwa na panya.
(b) Kufuli mbaya imetupwa.
(c) Gari liliendeshwa polepole.
(d) Msichana mrembo amepotea.
(e) Wao ni warefu sana.
3. Jaza nafasi kwa msamiati sahihi
(a) Tunatumia _____ kuchanja kuni.
(b) Anayefanya kazi ya ukulima ni ___________
(c) Mimea ambayo haihitajiki shambani huitwa _______
(d) Mmea mchanga huitwa ___________
(e) Huwa tunapanda ________ ambayo huota mimea tofauti.
4. Andika kinyume cha neno lilopigiwa mstari
(a) Mzee yule amepatikana akiwa amechapwa.
(b) Shangazi alinitembelea jioni.
5. Jaza mwanya kwa kiulizi -pi
(a) Mvulana ______ alichelewa shuleni?
(b) Kiatu _______ kilichoshonwa na fundi?
(c) Matunda ________ yaliyooza?
(d) Mti _______ ulioanguka?
(e) Mikoba _______ iliyonunuliwa?
6. Andika kwa idadi
(a) Watoto 8 _____________________________
(b) Vijiko 13 _____________________________

SEHEMU YA NNE

KUANDIKA (alama 20)

Andika insha kuhusu, ‘FAMILIA YANGU’

___________________________________________________________________________
___________________________________________________________________________
___________________________________________________________________________
___________________________________________________________________________
___________________________________________________________________________

You might also like