Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 6

JE, MTU ANA UWEZO WA KUTENDA

KINYUME NA MAAGIZO YA MUNGU?


“Nao husema, Bwana haoni; Mungu wa Yakobo hafikiri”
Zaburi 94:7

Na,
Ev. Malugu John
0763577531/0658626432
• Je, Bwana ameshindwa kukomesha uovu juu ya ulimwengu huu
uliochanganyikiwa?
• Sauti nyingi za kudhihaki zinasikika kila kona, maelfu ya watu
wanajifurahisha katika dhambi? Wengine wakitenda dhambi za siri
kwamba BWANA hawaoni. Je, Mungu anawaangaliaje hawa?
• Kwanini BWANA yupo kimya? Angalia mfano huu
❑Yona 1-2 1Basi neno la Bwana lilimjia Yona, mwana wa Amitai,
kusema, 2 Ondoka, uende Ninawi, mji ule mkubwa, ukapige kelele juu
yake; kwa maana uovu wao umepanda juu mbele zangu.
• Kwanini MUNGU anamuagiza kwanza Yona Kwenda kutangaza injili
kabla mji haujaangamizwa?
• Mungu ni mwingi wa Rehema, anachukia mtu kufa katika dhambi
❑ Ezekieli 33:11 “Waambie,Kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, sikufurahii
kufa kwake mtu mwovu; bali aghairi mtu mwovu, na kuiacha njia yake mbaya,
akaishi. Ghairini, ghairini, mkaache njia zenu mbaya; mbona mnataka kufa, Enyi
nyumba ya Israeli?”
• Mtume Petro anasemaje kuhusu uvumilivu wa Bwana?
❑ 2 Petro 3:9 “Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani
kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote
wafikilie toba.”
❑ 2 Petro 3:15 “Nanyi uhesabuni uvumilivu wa Bwana wetu kuwa ni wokovu, kama
vile na ndugu yetu mpenzi Paulo alivyowaandikia kwa hekima aliyopewa;”
➢Mungu anakuvumilia ili utubu lakini wengine wanautumia uvumilivu huu
kujifurahisha na Mungu anazidi kuwaita na kuwavumilia ili watubu
• Mtume Paulo naye aliandika?
❑ Warumi 2:4 “Auwaudharau wingi wa wema wake na ustahimili wake na uvumilivu wake,
usijue ya kuwa wema wa Mungu wakuvuta upate kutubu”
• Wako wengine wamekaa kwenye mafundisho yasiyo sahihi yaani
mafundisho ya wanadamu na wamefikiwa na ukweli lakini bado
wanajifurahisha katika mafundisho yao kwa kuwa BWANA yupo kimya?
Tazama Yohana anavyoandika?Y
❑Ufunuo 2: 20 Lakini nina neno juu yako(Thiatira), ya kwamba wamridhia yule mwanamke
Yezebeli, yeye ajiitaye nabii na kuwafundisha watumishi wangu na kuwapoteza, ili wazini
na kula vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu.21 Nami nimempa muda ili atubu, wala
hataki kuutubia uzinzi wake.22 Tazama, nitamtupa juu ya kitanda, na hao wazinio pamoja
naye, wapate dhiki kubwa wasipotubia matendo yake; 23 nami nitawaua watoto wake
kwa mauti. Na makanisa yote watajua ya kuwa mimi ndiye achunguzaye viuno na mioyo.
Nami nitampa kila mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yake.
• Ikiwa mtu hatazingatia, Mungu anatangaza kumlipa sawasawa na
matendo yake.
❑ Ufunuo 22:12 “Tazama,naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu
kama kazi yake ilivyo.”
• Mpendwa Yesu Kristo anakuita, amekuvumilia wewe tu utubu maana
anakuona jinsi ulivyo lakini bado unajifurahisha katika dhambi na
wengine wanajidanganya kwa kutenda dhambi za siri. Yeremia
anasema;
❑ Yeremia 23:24 “Je,
mtu ye yote aweza kujificha mahali pa siri, nisimwone? Asema
Bwana. Je! Mbingu na nchi hazikujawa nami? Asema Bwana.”
• Huwezi kujificha zaidi ya kujidanganya mwenyewe tu.
• Amua kuungama na kuacha kabisa dhambi naye BWANA
atakurehemu;
❑ Isaya 55:6 ”Mtafuteni
Bwana, maadamu anapatikana, Mwiteni, maadamu yu karibu;
7 Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na
amrudie Bwana, Naye atamrehemu; Na arejee kwa Mungu wetu, Naye
atamsamehe kabisa.
• Inakupasa utafakari njia zako na umrudie BWANA naye atakurehemu na
utakapokaidi na kuona ni vyema kujifurahisha katika dhambi, BWANA
anatangaza kukuangamiza kabisa kwa maana umechagua mwenyewe.

MUNGU AKUBARIKI

You might also like