Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 5

HISTORIA YA KANISA LA WAADVENTISTA WASABATO KATIKA KIJIJI CHA RUMASHI

NURU YACHOMOZA GIZANI

MARCH 13, 2024


THE COMFOR INTERNATIONAL MINISTRY
P O BOX 3 KAKONKO
HISTORIA YA KIJIJI CHA RUMASHI

Kijiji cha Rumashi ni miongoni mwa vijiji vilivyoanzishwa wakati wa siasa ya ujamaa na kujitegemea
iloiyoanzishwa na mwalimu J K Nyerere aliyekuwa Rais wa kwaza wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania
kuanzia mwaka 1961 baada ya uhuru hadi mwaka 1985 .mwalimu aliweza kuanzisha vijij vya ujamaa ili
iwe rahis kwa raia wake kuweza kupata hudumu muhimu za kijamii kama vile maji afya na elimu kijiji hiki
kinaweza kuwa kimeanzishwa kati ya mwaka 1972-1973 .

Rumashi nio miongoni mwa vijiji vinavyopatikana katika kata ya Nyabibuye wilaya ya Kakonko mkoani
kigoma .jografia ya eneo hili la kijiji cha rumashi ni ya kuvutia kwa wakazi wa eneo huska na wageni
wanaotoka katika maeneo mengine.kijiji hiki kipo jirani na mkoa wa Kagera kipo kilometa Zaidi ya 50
toka makao makuu ya wila ya kakonko pia kipo jirani na Nchi ya Burundi hivyo kina mwingiliano
mkubwa na watu wa nchi jirani ya Burundi hasa katika shuguli za kiuchumi hasa kilimo ambapo wakazi
wa eneo hili huajiri wafanyakazi /vibarua kutoka katika nchi jirani ya Burundi jambo linaloimarisha
mahusiano baina ya hizi pande mbili.

Katika suala la kijamii ,kuna shughuli ambazo wakazi wa kijiji cha Rumashi hunufaika kwa pamoja na
watu wa nchi hii jirani ya Burundi shughuli hizo ni kama kuoa na kuolewa ,shughuli za kidini hizi zote
zinaimarisha uhusiano baina ya watu hawa.

Kijiji hiki kimebarikiwa kwa kuwa na hali ya hewa nzuri na ardhi nzuri ambayo inayostawisha mazao ya
chakula kama vile mahindi mihogo,maharage, na mpunga katika eneo la mto Mwiruzi

MAISHA YA KILA SIKU YA WAKAZI WA KIJIJI CHA RUMASHI

DINI

Wanakijiji wa kijiji cha rumashi wamekuw na kuendelea katika shughuli za za kijamii hasa upande wa
Dini.Ukristo ndio Dini kuuu inayotawala katka kijiji cha rumashi ikiuwa na wafuasi wengi waliogawanyika
katika madhehebu Zaidi ya saba. Inafuatiwa na Dini ya uislamu ambayo ni ya pili kwa ukubwa baada ya
Ukristo katika kijiji hiki. Dini nyingine ni Dini za jadi ambazo nazo pia zina wafuasi wake katika jamii
inayopatikana katika kijiji hiki cha Rumashi .madhehebu maaarufu katika Dini ya UKristo katika kijiji cha
Rumashi ni pamoja na ,

Kanisa katoliki la Roma –Roman catholic church

Kanisa huru la kipentekoste la Tanzania –Free Pentecostal church of Tanzania

Kanisa la waadventista wasabato-The Seventh –Day Adventist Church

Tanzania Assemblies of God (TAG )

Evangelist Assemblies of God Tanzania (EAGT)

Kanisa la Kiinjili

Kanisa la kianglikana-The Anglican Church

Maranatha Reconciliation church

SHUGHULI ZA KIELIMU

Kijiji hiki cha Rumashi kimejaliwa kuwa na shule mbili za Umma ambazo zinaendeshwa na serikali na hizo
hutoa ELIMU ya msingi kwa watoto wa kijiji hiki .Shule ya Msingi Rumashi ambayo ni shule kongwe
hapo kijijini ilianzishwa mwaka 1973 lakini baada ya miaka kadhaa idadi ya watu iliongezeka na hivyo
serikali iliona kuwa kunahitajika ujenzi wa shule nyingine ili kukidhi haja ya ukuaji mkubwa wa idadi ya
watu hivyo serikali ikaweka mpango wa ujenzi wa shule ya msingi nyingine hapo kijijini mnamo mwaka
2005 shule ya msingi kalinzi ilitengwa rasmi na mpaka mwaka 2011 tayari wanafunzi wa shule ya msingi
kalinzi kuanzia darasa la tatu hadi darasa la saba walihamia kwenye majengo mapya ya shule hiyo.
Serikali iliendele ana ujenzi wa majengo mengine ya shule hiyo na mpaka kufikia mwaka 2022 tayari
wanafunzi wote wa darasa la kwanza na pili walikuwa tayari nao wameshahamia kwenye vyumba vya
madarasa vya shule hiyo mpya.hivyo mwitikio wa wazazi na walezi katika suala la Elimu uiisukuma
serikali kuona umuhimu wa kuboresha miundombinu ya shule hizo zote mbili.

SHIGHULI ZA KIAFYA
Hapa kijijini serikali imejityahidi kujenga zahanati moja ambayo inawahudumia wakazi wa kijiji hiki.
Lakini pia kijiji hiki kimebahatika kuwa na kliniki ya Baba Mama na Mtoto kwa ajili ya AFYA ya mama na
mtoto.pia zahanati hii inawahudumia wakazi wa kijiji hiki katika magonjwa kama vile Malaria,vipimo vya
Virusi vya Ukimwi ,pamoja na magonjwa ya zinaa kama vile Kaswende na Kisonono.

SHUGHULI ZA KILIMO

Wanakijiji wa eneo hili hujishughulisha katika kilimo cha mazao ya chakula na ya Biashara kama vile
mahindi, maharage,mihogo

Katika shughuli za kibiashara –wanakijiji hujishughulisha katika biashara ya ndani na nje

NURU ILIYOCHOZA GIZANI

Katika nyakati zote Mungu huteua mtu au watu kwa ajili ya kutekeleza mapenzi yake ili wawe nuru kwa
wengine.kuingia kwa ukweli wa neno la Mungu katika kijiji cha Rumashi ulikuwa ni mpango wa Mungu
kuwa kupitia kwa mtu mmoja hatimae giza la kiroho lingeangazwa kwa nuru kuu ya Kanisa la
Waadventista Wasabato.

NAMNA UJUMBE ULIVYOINGIA KIJIJINI

Bw.Gabriel Kaloza ambaye ni mshiriki wa kanisa la Waadventista Wasabato Rumashi ndiye mwasisi au
mwanzilishi wa kanisa la waadventista wasabato hapa kijijini ambaye alibatizwa mnamo mwaka
1982.mzee huyu alizaliwa kati ya miaka ya 1944 -45 kutoka kwa Bw. Na Bi. Sarah Kaloza.akiwa na umri
wa miaka 35 mzee huyu Gabriel kaloza alibarikiwa kupata mtoto wa kwanza kwa jina la Ayubu Gabriel
Kaloza kutoka kwa mke wake Bi Consolata Kaloza.akiwa kama muumini wa dhehebu la Roman Catholic
na msomaji mzuri wa masomo ya ya injili mwaka 1979 aliaanza kuhoji viongozi wake wa kidini juu ya
somo la injili ya Mtakatifu Luka sura 23;50-56 pamoja na Luka 24;1 ili kupata majibu sahihi lakini
alichukiwa na viongozi wake wa kidini kwa sababu ya maswali yake yaliyoonekana ya kizushi na
yasiyofaa ‘
Mnamo mwaka 1980 mzee huyu akiwa katika sherehe Fulani hapo kijijini walifika wageni waliokuwa
wakitokea katika eneo linguine mbali na kijiji hiki cha Rumashi.walionekana wasiojua maana walikuwa
wasio watumiaji wa pombe.wakazi wa yale maeneo ambapo wageni walifika hawakuwakaribisha vizuri
na hivyo ilimtuma Bw.Gabriel kuwakaribisha kwake nyumbani,Hawa walikuwa ni wafanyabiashaara wa
nguo za mitumba kutokea kijiji kingine cha CHERABULO ambacho ni kitovu cha ujumbe wa kiadventista
katika wilya nzima ya Kakonko na kanda ya tarafa ya Nyaronga.Wageni hawa walijitambulisha kwake
kama waadventista wa siku ya sabato na walikuwa na picha za kufundishia ambazo walimwachia mzee
huyu kama zawadi.

Baada ya kuwakarimu Mzee Gabriel alipata nafasi ya kuwauliza baadhi ya maswali kuhusu sabato ya siku
ya saba walimjibu baadhi ya maswali na mengine walimwahidi kuwawangerudi na watu wengine ambao
wangekuja kusadia kujibu maswali hayo.

Jjioni siku ya maandalio (ijumaa)mzee huyu aliwauliza watu hawa namna wanavyofanya ibada ndipo
wakamweleza kuwa huwa wanafanyia ibada kwenye jingo maalum na kama halipo wanaazima chumba
cha darasa ili wafanye ibada. Ndipo mzee huyu aliamua kwenda kw amwlimu mkuu wa shule ya msingi
rumashi ambapo aliweza kuomba chumba ambacho wangeweza kufanyia ibada pamoja na wageni hao.
Mwalimu LUCAS NZOHUMPA alikubali ombi la mzee huyu na kuwapa chumba cha darasa ambacho
walifanyia ibada siku iliyofuata yaani Sabato walifanya ibada ya ufunguzi wa Sabato na kesho yake
waliendeleza vizuri na hivyo wakmwachia mzee yule utaratibu wa namna ya kuendesha ibada wa kanisa
la waadventista wasabato .kesho yake wageni hawa waliendele na safari yao.

Baada ya kuwa mzee huyu aamepata mwanga wa namna ibada inavyoendeshwa aliendelea kufanya hivo
yeye peke yake na lakini kutokana na kazi aliyokuwa akifanya ya kueneza injili baadhi ya watu walijiunga
ambao baadhi yao ni pamoja na Bw, STEPHANO NZOHUMPA, DAMIAN BHUHUNGU,NA MZEE NZANIYE
hawa walipelekwa kwenye makambi CHERABULO mwaka 1982 wakabatizwa wote pamoja na Mzee
Gabriel.

Uongozi wa kanisa la waadventista Wasabato Cherabulo uliamua kumtuma mmishonari kwa ajili ya
kufanya mahui biri ya hadahara mwaka huohuo wa 1982 lakini ,mahubiri haya hayakuzaa matunda
katika mwaka 1982 mzee Gabriel aliomba kiwanja kwa ajili ya kujenga kanisa kutoka kwa Serikla ya kijiji
cha Rumashi ambapo alijenga jingo dogo akiwa peke yake

Ujumbe ukaenea katika vitongoji vya kijiji cha Rumashi,Mzee Gabriel Kaloza, Mungu alimwongoza katika
kuhubiri watu wa vitongoji vya kijiji hiki na ilipofika mwaka 1986 kulifanyika ubatizo mwingine ambapo
watu kama Mzee GODFRED MDYAHERA,LAURENT NGAVUNE ,THEOPISTA SABUWANKA,THOMSON
SABUWANKA Walibatizwa mwaka huo wa 1986.

Kazi ya injili ikapamba moto na idadi ya waumini ikazidi kuongezeka na kukawa njozi ya ujenzi wa kanisa
jipya ambapo mwaka huohuo 1986 walianza msingi na baadae mwaka 1991 lilitengwa rasmi na kuwa
kanisa badala ya kundi likawa na uongozi unaojitegeme na mzee Gabriel Kaloza alicahguliwa kuwa mzee
wa kwanza wa kanisa la waadventista wasabato Rumashi.

You might also like