Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 2

Uainishaji wa Ngeli za Kiswahili Kisemantiki

Uainishaji wa nomino huzingatia maana za nomino. Kigezo cha kisemantiki huziainisha nomino katika
ngeli kutegemea uhusiano wa kimaana uliopo kati ya nomino za ngeli moja. Kwa mfano majina kama vile
ya watu na wanyama huwekwa katika ngeli moja ya viumbe vyenye uhai.
Pia kuna ngeli zinazoonyesha ukubwa, udogo, udhalilishaji na kadhalika.
Ngeli huorodheshwa kisemantiki ifuatavyo:

Ngeli za 1 na 2
Ngeli hizi hujumuisha majina ya viumbe kama vile watu, wadudu, wanyama,na ndege. Nomino
zinazopatikana katika ngeli hizi mbili ni kama; mtoto -watoto, mtu-watu,mdudu-wadudu.Nomino nyingi za
viumbe vyenye uhai hupatikana katika ngeli hizi.
Kwa hivyo nomino nyingine zote zenye sifa hii ya uhai huchukua upatanisho wa kisarufi katika ngeli za l
na 2.

Mifano ifuatayo:
Umoja Wingi
Mtoto mwèrevu ametuzwa. -Watoto werevu wumetuzwa
Kiwete mwerevu ametuzwa. -Viwete werevu wametuzw
Mjusi mweusi ameuawa na paka. -Mijusi weusi wameuawa na paka
Nyuki ntdogo amemdunga mtoto. -Nyuki wadogo wamewadunga watoto

Ngèli za 3 na 4
Hizi ni ngeli za vitu.
Zinahusisha vitu visivyo na uhai; viumbe kama vile miungu na watu walio na uwezo mkuu; baadhi ya
viungo vya mwili; mimea; vitu yya asili; baadhi ya wanyama; majina yaliyoundwa kutokana na vitenzi,
pamoja na baadhi ya maneno ya kukopwa kutoka lugha za kigeni.
Mfano: mgongo, mti, miungu, mto, mgongo…nk.

Ngeli 5 na 6
Sifa kuu ya ngeli hizi kisemantiki ni kuwa huashiria sifa za ukubwa wa nomino zinazohusika; pia
huonyesha udhalilishaji. Ngeli hizi pia huhusi ya sehemu za mwili; baadhi ya maneno ya kigeni; baadhi ya
majina pamoja na majina yanayoonyesha nyadhifa wanazoshikilia watu.
Mfano, Tunda, goti, bega, jitu, jito….n.k.

Ngeli 7 na 8
Ngeli hizi huhusisha baadhi ya vitu au vifaa visivyokuwa na uhai nomino zinazotokana ną vitenzi vyenye
kuundwa kutokana :kinachotekelezwa na nomino hiyo k.m. funika-kifuniko-vifuniko ya lugha k.m.
Kiswahili,Kichaga; Kiluhya n.k.; pia huonyesha udh udogo.

Ngeli 9 na 10

Ngeli hizi huwakilisha nomino za vifaa vya kawaida k.v. shati, kalenda n.k. Ngeli hizi aghalabu
huwakilisha nomino za majina yaliyoazimwa (yaliyotoholewa) kutoka lugha za kigeni; huhusisha pia
majina ya vifaa vya Kazi kama vile nvundo, ngazi, ndoo……

Ngeli ya 11
Nomino zinazopatikana katika ngeli hii ni pamoja na zile zinazowakilisha majina ya vitu vyenye umbo refu
na jembamba kama vile unywele, ufito, ulimi, ujia n.k. Baadhi ya majina katika ngeli hii hupata wingi
wake katika ngeli ya 10 na nengine katika ngeli ya 14.

232
Ngeli ya 14
Hii huwakilisha vitu vya kidhahania vinavyofikirika tu kama.vile uzimja,itukufu, uchangamfu,uzuri,
pamoja na baadhi ya majina ya nchi kama yile Ulaya, Uchina, Uhabeshi, Ureno, Urusi, na umoja wa
sehemu ya vítu vidogo kama vile unywele,ushanga na ufito.

Ngeli 15
Ngeli hii huwakilisha nomino zinazoundwa kutokana na vitenzi kuonyesha natúkio ya watu au wanyama.
Kwa mfano:
Kucheza kwake kulitupendeza.
Kucheka kwake kunachekesha.
Hudhihirika kama nomino ikitumika kama kiima katika sentensi.

Ngeli 16,17 na 18
Huonyesha hali mbalimbali za mahali:
pa-mahali kamili.
ma- undani wa mahali.
ku- mahali kusiko dhahiri.

232

You might also like