Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 19

L IM A WAM

KU IT
M I

MODULI NAMBA 2

Uandaaji sahihi wa
kitalu cha miche
Shukurani
KIJITABU HIKI KIMEANDALIWA KWA AJILI YA KUFIKISHA MAUDHUI YA
TAALUMA YA NAMNA YA KUANZISHA NA KUENDELEZA BUSTANI YA MITI
KWA MKULIMA MDOGO NA MKUBWA PIA.

KIMEANDALIWA KWA MICHORO ZAIDI ILI KUMRAHISISHIA MSOMAJI


KUJARIBU KILA KITU KWA USAHIHI ZAIDI. MARA BAADA YA KUKAMILIKA,
KIMEPITISHWA KWA WADAU MBALIMBALI NA WATAALAMU WA MISITU
ILI KUTOA UZOEFU NA UTAALAMU WAO ILI KUBORESHA UTOAJI WA
MAFUNZO SAHIHI YA UANZISHWAJI NA UENDELEZAJI WA BUSTANI YA
MITI HAPA TANZANIA.

NAPENDA KUTOA SHUKURANI ZA PEKEE KWA TAASISI YA UENDELEZAJI


WA MISITU TANZANIA HUSUSANI KITENGO CHA huduma kwa wakulima
wa miti KWA KUWEZESHA KAZI HII KUKAMILIKA.

PIA NAPENDA KUTOA SHUKURANI ZA PEKEE KWA WAFADHILI WA TAASISI


HII AMBAO NI GATSBY NA dfid KWA KUWEZESHA KUFADHILI UANDAAJI
WA KIJITABU HIKI.

MWISHO, NAPENDA KUTOA SHUKURANI ZA PEKEE KWA BWANA JOSEPH


MAKANZA KWA KUCHORA MICHORO na kusanifu KIJARIDA HIKI NA
PIA SHUKURANI ZA PEKEE KWA BWANA HAMISI MALINGA NA GEORG
STRUNDEN KWA USHAURI WA KITAALAMU KUHUSIANA NA MICHORO NA
MAUDHUI yA KITABU HIKI.

Utangulizi

Watafiti na wataalam wa misitu wanaamini kuwa watanzania wengi


wamehamasika na wanapenda kilimo cha miti ya mbao.

Moduli hii inatoa maelekezo ya namna ya kuzalisha miche bora


itokanayo na kupanda mbegu bora, inatoa mafunzo ya namna
ya upandaji mzuri wa mbegu na uanzishaji mzuri wa mashamba
ya miti.

Inatoa mwongozo kwa wenye bustani za miti ili nao watoe


mafunzo ya namna ya upandaji mzuri kwa wanunuzi wa miche.

Hatua zilizoelezewa humu zinahusisha uandaaji kwa mbegu za


Milingoti na Paina pia.

Moduli hii itatueleza kisa cha MACHOKODO aliyenufaika kwa


Kilimo cha Miti baada ya kujifunza na kutumia utaalam alioupata
kutokana na mafunzo kujitengenezea faida na kubadili Maisha
yake.

1
1. MAANDALIZI YA KUWATIKA MBEGU

Unapotaka kuwatika HAKIKISHA UNATUMIA MBEGU


MBEGU Chagua eneo BORA KWA KUWA ZITAKUPA
ambalo linafaa kwa UKUAJI WA HARAKA NA
kutengeneza tuta la KUKUPA KIPATO KWA MUDA
kusia mbegu ambalo MFUPI. BUSTANI NZURI BILA
lina mteremko, jua MBEGU BORA HAINA FAIDA
kidogo NA ULINZI KABISA.
KUHAKIKISHA MICHE
AIHARIBIWI

Pima eneo ambalo ni Pima kama futi 4 kwa futi 10


msitatili KWa futikamba. au zaidi kulingana na miche
unayotaka kuzalisha.

2
Lima kwa kuinua tuta
lenye urefu tajwa
AU PIGILIA MABANZI
NA JAZA UDONGO.
Sawazisha kwa kutumia
jEMBE AU mpini wa
jembe au ubao ili
kupata tuta lililo na
sura ya kitanda.

Weka sawa udongo kwa


kutumia rake na kupigapiga
udongo ili ulainike. Pia
toa mawe, magugu na vijiti
kwenye hilo tuta lenye
sura ya kitanda

JUU YAKE WEKA KAMA INCHI


2”-3” ZA MCHANGA WA
KAWAIDA...
MCHANGA JUU YA TUTA LA
KUOTESHEA HUSAIDIA
KATIKA UOTAJI WA MBEGU NA
HURAHISISHA UNG’OAJI WA
MICHE WAKATI WA KUHAMISHA
MICHE KWENDA KWENYE
VIRIBA

3
EPUKA MAKOSA/ZINGATIA

UsiwekE Mbolea ya samadi


kwenye tuta la kuoteshea
mbegu....Samadi huwa na
vimelea wengi ambao huweza
kuathiri uotaji wa mbegu.
Samadi husababisha kuwepo
na wadudu kama minyoo,
funza na wadudu wengi
ambao hukata mizizi ya miche
na wadudu wengine hula
mbegu kabla ya kuota na
kusababisha hasara kubwa
sana

Weka mchanga juu ya tuta ili


kurahisisha Uotaji wa miche...

MCHANGA HUSAIDIA MBEGU


KUOTA HARAKA, PIA HUSAIDIA
UNAPOHAMISHIA KWENYE VIRIBA
MCHANGA HUACHIA MICHE BILA
KUNG’ANG’ANIA

INCHI 2-3 zA
mchanga
udongo

4
2. KUSIA MBEGU KWENYE TUTA
Mbegu za milingoti
(Eucalyptus) ni ndogo
ndogo sana, changanya
mbegu na mchanga Kipimo
1 cha MLINGOTI na vipimo 3
vya mchanga kisha sambaza
juu ya tuta

mbegu mchanga

Kwa mbegu za Paina chora vistari kwenye tuta na


kuzimwaga bila kuchanganya na mchanga funika na
mchanga kidogo.

Funika kwa nyasi KAVU kwa Mwagilia maji taratibu


muda wa wiki moja (2) hadi bila kusababisha udongo
tatu (3).... NYASI HUONGEZA kutepeta kwa maji.
JOTO KWA UDONGO NA
KUSISIMUA UOTAJI WA HARAKA
NA NYASI ZIONDOLEWE BAADA
YA KUONA MAJANI MAWILI
YAKIWA YAMEANZA KUTOKA KWA
MBEGU ( KUOTA)

5
Mwagilia mara
mbili kwa siku
vizuri, asubuhi
na jioni.
ASUBUHI JIONI

kumwagilia maji mpaka


udongo unatepeta
KUNAWEZA kusababisha
ugonjwa wa ukungu
(Fangasi), wadudu
waharibifu kama
minyoo, funza na
panzi....

Ukiona dalili zozote


za magonjwa ya miche
bustanini pata ushauri
wa Mtaalamu wa Misitu
ili akueleze ni dawa
gani waweza kutumia

EPUKA MAKOSA/ZINGATIA

baada ya wiki usifanye hivi namna hivi


3 Funika kwa
nyasi kwa paa
la mwinamo...

KAMA ENEO LA
BUSTANI LINA
JUA KALI SANA
FUNIKA MICHE
KWA NYASI

6
3. KUCHANGANYA UDONGO WA KUJAZA KWENYE VIRIBA

Kwa Milingoti Weka:-

udongo udongo wa
mchanga.
wa msituni mfinyanzi.
kipimo 1
vipimo 3 vipimo 3

Udongo
wa kujaza
kwenye viriba.

Kipimo: lori, tOLORI, beseni, DEBE

Kwa Paina Weka :-

udongo udongo wa
wa msituni mfinyanzi. mchanga.
VIPIMO 3 VIPIMO 3 KIPIMO 1

Udongo
KIPIMO 1 wa kujaza
UDONGO TOKA
MSITU WA PAINA
kwenye viriba.
(MYCORRHIZA)

Kipimo: lori, tOLORI, beseni, DEBE

7
EPUKA MAKOSA/ZINGATIA DOKEZO KUHUSU VIRIBA

Chekecha udongo KILO MOJA YA PLASTIC NI


ili kuondoa mizizi na SAWA NA VIRIBA TUPU 600 VYA
takataka nyingine halafu INCHI 3 KWA 4. MCHANGANYO
changanya vizuri kabla ya WA UDONGO TOLOLI MOJA NI
kujaza kwenye viriba SAWA NA VIRIBA 470

Sasa unaweza kujaza Udongo


kujaza kwenye viriba...

KABLA YA KUANZA KUJAZA UDONGO


KWENYE VIRIBA, NYUNYIZA MAJI
UDONGO, UCHANGANYE UDONGO
VIZURI, INGIZA VIDOLE VIWILI
NDANI YA KIRIBA, JAZA UDONGO,
SHINDILIA VIZURI KISHA PANGA
KWENYE MISTARI. UKUBWA WA VIRIBA
NI INCHI 3-4 KIPENYO NA UREFU NI
INCHI 3

8
4. KUHAMISHIA MICHE KWENYE VIRIBA

Ili kuhamisha miche


Anzia kwenye kona YA
TUTA KWA KUnyanyua
udongo kwa kijiti,
kisha ingiza mkono
chini na inua mche au
miche kadhaa mkononi.

...hamisha mche
kutoka katika tuta
la kusia mbegu
kwenda kwenye
viriba...

IWEKE MICHE HIYO KWENYE


CHOMBO KAMA BAKULI
IKIWA NA MAJI NA ANZA
KUPANDIKIZA MICHE MMOJA
KWA KILA KIRIBA

9
Wakati wa Kuhamisha miche shika kwenye vijani viwili
(coteledons) na usishike kwenye SHINA AU mizizi. Kwa
kushika kwenye mizizi kunaweza kusababisha kufa kwa mche
kwani... vidole huwa na chumvichumvi na mafuta ambavyo
huDHURU mche.

Panga viriba vilivyo na miche


kwenye mstari eneo ambalo
ni safi kama uwanja.

MWAGILIA MICHE HIYO MARA IKIWA UMECHELEWA


MBILI KWA SIKU. MWAGILIA KUOTESHA MICHE
KILA SIKU ASUBUHI NA UNAWEZA KUONGEZA
MAPEMA NA JIONI... UKUAJI HARAKA
TUMIA CHOMBO CHENYE BUSTANINI KWA KUPIGA
MATUNDU MADOGO MBOLEA YA NPK YA
KUEPUSHA KUDHURU MAJIMAJI INAYOITWA
MICHE BUSTA PAMOJA NA
KUPIGA DAWA YA KUUA
WADUDU WAHARIBIFU WA
MICHE

10
EPUKA MAKOSA/ZINGATIA

Epuka MIZIZI ILIYOJIKUNJA KAMA


HERUFI (J)...TOBOA SHIMO LA KUTOSHA
KWA KIJITI NA SI KWA KIDOLE, chomeka
mchE halafu vuta juu kidogo ili mzizi
usipinde

...EPUKA
KUMWAGILIWA
MAJI MENGI SANA
MPAKA MICHE
INAZAMISHWA
KWENYE MAJI

11
5.KUPUNGUZA/KUKATA MIZIZI
Kata mizizi kila unapoona
inaanza kuingia ardhini KWA
KUtumia kisu kikali au waya....
Au hamisha miche kila
baada ya wiki mbili

ng’oa
mizizi mizizi
magugu
haijakatwa imekatwa
kwenye
viriba

6. KUIKOMAZA MICHE

Hiki ni kitendo cha kuikomaza miche kwa


kupunguza kiwango cha umwagiliaji
maji ili ianze kuzoea hali ya shambani
itakakopandwa

12
BAADA YA MIEZI SITA MICHE YAKO
ITAKUWA TAYARI KWA KUPANDWA
SHAMBANI AU KUUZA KWA MTEJA

...urefu unaofaa kwa SABABU YA KUIKOMAZA


kupandwa milingoti ni MICHE NI KWA AJILI YA
Sentimeta 20-25 na Mipaina KUIANDAA MICHE KWA
ni sentimeta 10-15 MAZINGIRA MAGUMU YA
SHAMBANI NA PIA HII
HUFANYIKA KWA MICHE
ILIYOBAKI MPANDO WA
MWAKA HUO NA KUSUBIRI
HADI MPANDO WA MWAKA
MWINGINE...

ZINGATIA ENEO
KAMA NINATAKA
LA BUSTANI LIWE
KUANZISHA
NA CHOO, STOO,
KITALU CHA
OFISI, MAJI YA
KIBIASHARA
KUNYWA. PIA TUNZA
MAMBO GANI YA
KUMBUKUMBU ZOTE
KUZINGATIA?
ZA UZALISHAJI NA
MAUZO.

13
7. GHARAMA ZA KUKUZA NA KUUZA MICHE

dr ULALO WA FAIDA NA HASARA CR

MTAJI/ MAPATO MATUMIZI/ GHARAMA

Mtaji wa fedha (Saccos) 5,000 Kununua reki 700

Nyongeza ya mtaji 100,000 Kulipa vibarua 40,000

Kununua viriba 14,000

Kununua mbegu 50,000

Mauzo ya miche 200,000 Kununua jembe 2,000

Mauzo ya miche 50,000 Vibao vya kwenye matuta 500

Mauzo ya miche 20,000 Kutengeneza bango 1,000

Kununua makeni 3,000

Kununua madawa 3,000

Tofauti ( faida) 254,500

JUMLA 375,000 JUMLA 375,000

*angalizo: tarakimu zilizoandikwa hapa ni mfano tu.

Ukiona matumizi ni makubwa kuliko MAPATO Ujue umefanya


biashara kwa HASARA

Ukiona Mtaji au mapato ni Makubwa kuliko matumizi ujue


kuwa umefanya biashara kwa FAIDA. Jumlishia pembeni
kwanza kisha jumla iliyo kubwa kati ya kulia na kushoto
ndiyo iandikwe kwenye jumla kuu. Kisha kama kushoto
ndio kudogo andika TOFAUTI HASARA au kama kulia ndio
kudogo Zaidi hivyo juu ya jumla kuu andika TOFAUTI FAIDA

kisha andika hiyo tofauti ili UWEKE UWIANO/ BALANSI.

14
Vigezo vya mahali sahihi pa kuweka
bustani
1. Mahali panapofikika vizuri kwa gari
2. Mahali ambapo nguvukazi inaweza patikana
kiurahisi
3. Mahali ambapo pana maji ya uhakika
4. Mahali ambapo hapana mteremko mkali
5. Mahali ambapo rasilimali muhimu kama udongo
vinapatikana mapema.
6. maji kwa ajili ya umwagiliaji

Vitu vya muhimu kuwepo katika


bustani ya kibiashara
1. Pawepo choo kwa ajili ya wafanyakazi na wageni
2. Pawepo ofisi na stoo kwa ajili ya nyaraka na
vifaa vya bustani
3. Weka wigo kwa ajili ya kulinda miche yako
4. Maji safi kwa ajili ya kunywa wafanyakazi na
wageni bustanini
5. Bango kwa ajili ya kutangaza biashara yako
(Biashara matangazo)

Mbegu bora maana yake nini?


Ni mbegu zilizotokea kutoka kwenye miti
iliyopandwa maalumu kwa ajili ya kuzalisha mbegu
na kwamba Chavusha ( Poleni) hutoka katika
uzao ambao ni bora na hufanywa kwa mikono ya
wataalamu au wadudu toka katika miti ( Baba) yenye
uzao mzuri.

15
Jedwali la Kalenda ya shughuli za bustani za miti

SHUGHULI MUDA WA MWAKA


1. Kuchagua eneo la kuweka bustani Mei
2. Kuagiza/ kununua mbegu za Mipaina Mei na Juni
3. Kuandaa bustani ya mipaina Juni
4. Kukusanya udongo kwa ajili ya bustani Juni
5. Kutengeneza tuta la kusia mbegu Juni
6. Kuchanganya udongo kwa ajili ya
kuweka kwenye viriba Juni/ Julai
7. Kujaza udongo kwenye viriba Julai
8. Kuhamisha miche kwenye viriba Julai
9. Umwagiliaji wa miche iliyoko
kwenye viriba Julai- Desemba
10. Kuandaa bustani ya Milingoti Septemba
11. Kutengeneza tuta la kusia
mbegu za Milingoti Septemba
12. Kuchanganya udongo kwa Septemba/
ajili ya Milingoti Oktoba
13. Kuhamisha miche kwenye viriba Oktoba
14. Umwagiliaji wa miche iliyoko Oktoba/
kwenye viriba Novemba
15. Kung’oa magugu kwenye miche
ya Milingoti na Mipaina Novemba
16. Kukata Mizizi kwenye Mipaina
na Milingoti Novemba
17. Kukomaza miche Mipaina na Novemba/
Milingoti Desemba
18. Kupanda mashambani/ kuuza Desemba-
Mipaina na Milingoti Februari

16
FORE S TRY DE VE LOPM E N T TRUS T
U E N D E L E Z A J I M I S I T U TA N Z A N I A
2 0 B A L O Z I ROA D, G A N G I L O N G A , I R I N G A , P O B OX 2
t: +255 262700550 | I N F O @ F O R E S T RY- T R U S T. O R G

You might also like