Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 2

NAME: MUGO DUNCAN WAWERU REG NO: BEDA/2020/67026

BLA 2215 KISWAHILI MORPHOLOGY AND SYNTAX

Instructions

1. Eleza historia fupi ya sarufi mapokeo (alama 10)


 Historia Yake Mtazamo wa awali zaidi ambao ulishughulikia lugha ulikuwa wa kifalsafa. Sarufi
mapokeo iliasisiwa na wanafalsafa wa ulaya hasa Ugiriki. Hawa walishughulikia lugha tangu
karne ya kumi na tatu. Wakati huu, lugha iliangaliwa kama kipengele kimoja cha uchunguzi wa
taaluma nyingine (za falsafa) kama historia, fasihi, dini, mantiki na baalagha. Kule Ugiriki,
kipengele cha lugha kilishughulikiwa katika taaluma ya falsafa. Wachunguzi hodari wa falsafa ya
kigiriki walikuwa Aristole na Plato.
 Sarufi ya awali zaidi ilitungwa na Myunani aliyeitwa Dionysus Thrax na iliitwa Techne
Grammatike (The Art of Grammar). Baadaye warumi walitumia mfumo wa kisarufi wa Wayunani
katika lugha ya Kilatini bila mabadiliko mengi.
 Kati ya karne ya 12 hadi ya 14 kikundi cha wasomi kilichoitwa Modistae kilitoa kazi mbalimbali
zilizojikita katika sarufi ya makisio. Mtazamo wao wa kisarufi ulikuwa
 ukiitwa grammatica speculativa. Waliamini kwamba kuna sarufi bia moja inayohimiliwa na
uhalisia na urazini wa binadamu. Kufikia karne 17, maoni tofauti ya kisarufi yaliendelezwa.
Kufikia mwaka wa 1700, sarufi za lugha 61 zilikuwa zimeandikwa zikiwemo zile za Kiingereza,
Kifaransa, Kiarabu na Kiitaliano.
 Sarufi nyingi za mwanzo ziliandikiwa kwa makusudi ya kufundishia. Pia walitaka kuzisanifisha
kupitia maandishi.
 Katika kipindi hiki cha maendeleo ya sarufi, wataalamu waligawanyika kimaoni wengine
wakipendekeza sarufi fafanuzi au elezi na wengine sarufi elekezi.

2. Jadili misingi ya nadharia ya Sarufi Mapokeo (alama 2o)

 Mkabala wa Sarufi Mapokeo una misingi yake katika sifa maalum ambazo zinaibainisha sarufi hii.
Nadharia ya sarufi mapokeo basi inajikita katika misingi ifuatayo:
i) Lugha iliyochukuliwa kuwa msingi wa sarufi ilikuwa Kilatini. Hii ni kwa sababu mambo mengi ya
kitaalamu wakati huo yalichunguzwa na kuandikwa kwa Kilatini. Lugha ya Kilatini ilikuwa
mojawapo ya lugha awali sana kuwa na maandishi. Lugha zote zilichunguzwa kwa misingi ya
Kilatini. Lugha zote ulimwenguni zilichukuliwa kuwa na sarufi moja. Kwa muda mrefu lugha ya
Kilatini ilichukuliwa kama kielelezo cha matumizi ya kiwango cha juu kabisa cha lugha. Kwa hivyo
wanamapokeo, walichunguza na kuishilia na kanuni na sheria zilizoeleza matumizi yake. Kanuni
hizi zilichukuliwa kama kigezo cha kuchambulia lugha nyingine za ulimwengu – hata Kiingereza.
Kmf. Kilatini kina sifa ya kunyambulika kwa maneno. Kwa kutumia kigezo hiki wanamapokeo
walikiona Kiingereza kuwa na chembe za sarufi kwani hakina sifa hii sana kikilinganishwa na
Kilatini ilhali Kichina ambacho hakina tabia hii kilisemekana kuwa hakina sarufi.
ii) Sarufi mapokeo ilipendekeza kanuni za lugha Sarufi mapokeo ilieleza kwa jinsi ambavyo mtu
anatakiwa kuongea na kuandika. Kulikuwa na kanuni ambazo zilipasa kufuatwa katika kutumia
lugha kwa njia sahihi. Wanamapokeo walitoa sheria zilizoelekeza namna ya kutumia lugha.
Udhaifu wa kufanya hivi ni kwamba sarufi haipaswi kuwa ya kulazimishwa inapaswa kuwa ya
kueleza. Walisahau kwamba sarufi yapaswa kuangalia lugha kama ilivyo na kuieleza sio
kulazimisha sheria. Wazungumzaji hawatungiwi kanuni za jinsi ya kuongea lugha yao. Kila
mzungumzaji wa lugha fulani anazifahamu sheria za lugha yake bila sheria hizo kutolewa wala
kuandikwa. Sheria za lugha ni za kiasilia. Kwa kutumia umilisi wake, mzungumzaji asilia
anafahamu sheria zinazoongoza kwa mfano; wingi/uchache, ukubwa nk.
iii) Kazi za kisanaa zilihusishwa na falsafa. Kazi mbalimbali za wasomi mashuhuri wakati huo
zilichukuliwa kuwa ndizo zilizotumia lugha kwa njia sahihi zaidi. Matumizi ya lugha nje ya
ilivyotumika katika kazi hizi yalichukuliwa kuwa ni makosa. Hivyo mtazamo wa lugha ukawa
kuwa mabadiliko ya lugha yalikuwa ya kuharibu na kuwa hatua ya awali ya lugha fulani ilikuwa
bora na sahihi zaidi kuliko hatua ya baadaye. Udhaifu wa mawazo haya ni kwamba walichukulia
kwamba lugha haikui. Kutokana na maoni haya vitabu vya sarufi vilivyoonyesha kanuni za
utumiaji sahili wa lugha vilitungwa.
iv) Walionelea lugha kuwa ni ya kionomatopea Wanamapokeo walionelea kwamba kulikuwa na
uhusiano wa moja kwa moja kati ya neno na kile kinachorejelewa na neno hilo. Maneno kama
kengele, tingatinga na pikipiki – yanatokana na sauti inayotolewa na vyombo hivi. Katika lugha
nyingi za ulimwengu sio maneno yote ambayo yanaweza kuhusishwa moja kwa moja na
vyombo/vifaa vinavyozungumziwa. Maneno mengi hayachukui utaratibu huu. Katika Kiswahili
kwa mfano, maneno kama meza, kiti, ua na mengine mengi hayana uhusiano na vifaa hivi.
v) Walijishughulisha na kueleza kategoria za sarufi kmf. nomino na vitenzi. Wanamapokeo
walihakiki sentensi kwa kutambua vipashio vyake mbalimbali. Waliangalia jinsi vipengele hivi
vilivyotumiwa – vizuri au kimakosa katika sentensi, pia walijaribu kuvieleza vijisehemu hivi na
kuvitolea maana. Walipanga vipashio vya lugha katika makundi pia.
vi) Walionelea kwamba lugha ya maandishi ilikuwa bora kuliko lugha ya mazungumzo. Kwa
wanamapokeo, lugha ilikuwa ile iliyoandikwa. Maoni haya yalishikiliwa sana na Wagiriki. Maoni
yao yanafungamana na neno la Kigiriki grammar yaani sarufi linalotokana na neno la
Kigiriki grammatike linalotumiwa kwa maana ya 'kuandikwa'. Kutokana na neno hili basi
wanamapokeo wakachukulia kwamba lugha yoyote ambayo haikuwa imeandikwa au kuandikiwa
sarufi haikuwa lugha kamwe. Lugha ya Kilatini ndiyo iliyokuwa imeandikwa wakati huo. Sarufi za
lugha zote za ulimwengu ziliegemezwa kwa lugha ya Kilatini ambayo ilikuwa lugha ya wasomi
wakati huu na tena iliyoandikwa. Udhaifu wa mawazo haya ni kwamba lugha ya kuongea ndiyo
kongwe zaidi kuliko lugha ya kuandikwa, kabla maandishi yavumbuliwe, watu walikuwa
wakitumia lugha kwa kuwasiliana. Maandishi ni mbinu ya kuhifadhi lugha. Lugha si maandishi
wala maandishi si lugha. Kuna lugha nyingi za ulimwengu ambazo hazijaandikwa kmf. Kidorobo
na Kiogiek. Je hizi si lugha? Lugha ya kuongea ndiyo yenye msamiati kamili. Maandishi
yanawakilisha lugha ya kuongea. Isitoshe sio rahisi kuandika maneno yote ya lugha au sentensi
zake kwani mzungumzaji asilia wa lugha fulani ana uwezo wa kuzua maneno na sentensi
kochokocho.

You might also like