Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 6

A THREAD BY FORTUNATUS BUYOBE

JUSTINE KASUSURA SAGA

Mnamo tarehe 02 August 2001, Dada aitwaye DOREEN alimpigia simu ndugu
JUSTINE KASUSURA ambaye alikuwa ni Dereva wa gari ya kampuni ya ulinzi
ya KNIGHT SUPPORT akimwelekeza afike ofisini kwani kuna maagizo
anatakiwa apewe.

Alipofika alikabidhiwa gari PICKUP DOUBLE CABIN na akaambiwa


ataambatana na SAID MUSSA kwenda airport(JNIA) kupokea mzigo.
Waliambiwa mzigo ni mali ya CITIBANK hivyo wataupokea na kuupeleka kwa
mhusika. Walikabidhiwa nyaraka zote muhimu za kuwasaidia kuutoa mzigo
huo.

Kilichoendelea kilikuwa kama mtihani wa "FILL IN THE BLANKS", Tunachojua


ni kuwa Ijumaa ya tarehe 03 August 2001,tulimuona RPC wa Dar enzi
hizo(SACP ALFRED TIBAIGANA) akitangaza kwenye TV kuhusu unyang'anyi
kwa kutumia siraha wa mamilioni ya fedha za kigeni uwanja wa ndege JNIA

Kamanda alitangaza kumshikilia SAID MUSSA, na kutangaza msako mkali wa


mtu aliyemtaja kwa jina la JUSTINE KASUSURA mikoani na
mipakani.Alitangaza dau la mil 10 kwa atakayesaidia kukamatwa kwake.Habari
hii ilizua mijadala maofisini,vijiwe vya kahawa,saluni na hata mahospitalini.
Ilikuwa ni rahisi kusikia mgonjwa kasahau kunywa dawa, au mama kaunguza
mboga,kisa tu alikuwa anasikiliza "ubuyu" wa KASUSURA ambaye tukio hili
"lilimuinua mawinguni". Hawakuacha kujitokeza waliojifanya kujua hili na lile
na kuongeza chumvi juu ya mkasa huu.

Wakati huo askari makini,aliyehudumu katika Benki kuu idara ya


"INTELLIGENCE AND FRAUD UNIT" alikuwa amehamishiwa jiji la MBEYA
kama RPC. Si mwingine bali ni SACP SAID MWEMA(ambaye baadaye alipanda
vyeo na kuwa INSPEKTA JENERALI WA POLISI TANZANIA).

Msako wa KASUSURA ulichukua muda mrefu bila kupatikana na minong'ono


isiyo rasmi ikawa inadokeza kuwa alishakamatwa mara kadhaa na kuachiwa
kwani KASUSURA "HAKUPENDA UDHIA KWENYE RUPIA". (Haya yalikuja
kuonekana uthabiti wake baada ya kukamatwa kwake)
Huko mkoani mbeya,Jumatatu tarehe 24,DEC 2001 majira ya saa 3 usiku,akiwa
nyumbani kwake, Inspekta wa polisi RICHARD THADEI alipokea simu kutoka
kutoka kwa "msamalia" aliyedai kumuona KASUSURA maeneo ya SOWETO
mkoani humo. Askari huyu akamjulisha RPC MWEMA na mtego ukawekwa.

Inasemekana ugomvi wa wanawake wawili kumgombea KASUSURA ndio hasa


ulifanya umakini juu yake uongezeke na hata kumbaini.jamaa alikuwa anavaa
kofia kubwa ya pama na alijiandikisha kwa jina la JOHN LAIZER
mfanyabiashara toka sumbawanga katika guest house aliyofikia.

Polisi mbeya walimfatilia na kubaini jamaa yupo anakata kilaji hoteli ya MOON
DUST na kafikia nyumba ya wageni ya THREE IN ONE Chumba namba
101K,wakaona ni vizuri kuingia chumbani kwake na kumsubiri akirudi kulala
wamkamate. Aliwekewa ulinzi wa siri kote alikokuwa.

KASUSURA akiwa hajui lolote alitoka bar na kwenda kulala ambapo alikamatwa
kiulaini sana "KUMYATIA KIZIWI" ilikuwa sio rahisi kuamini mtu
aliyetangazwa kuwa ni jambazi sugu angedakwa kiulaini bila purukushani
yoyote. Walipomsachi walimkuta na TSHS 256,000 tu.

Habari za kukamatwa KASUSURA(ikiwa takribani miezi mitano tangu kusakwa


kwake), zikasambaa kama moto nyikani. Hakuna aliyetaka habari hiyo impite.
Akasafirishwa mpaka Dar alikotuhumiwa kutenda uhalifu huo.

Jumatatu ya tarehe 7 jan 2002 KASUSURA,alipandishwa kizimbani mahakama


ya Kisutu akiwa ameunganishwa na wengine Sita ambao ni WICKLIFF URASSA,
LEONARD URASSA, LUCY URASSA(Alikuwa Mwanafunzi wa IFM) PROFILY
KWEKA, WÌLLIAM MBETWA na LIBENT LIKUNDWA.

Mwendesha mashtaka kamishna msaidizi wa polisi RAINHARD


LISAPITA,aliwasimea mashtaka matano ya Kula njama,Unyang'anyi wa kutumia
silaha na Wizi. Pia washtakiwa wawili walishitakiwa kwa kupokea mali ya wizi.
KASUSURA alikuwa akitetewa na wakili Msomi MAJURA MAGAFU.

Shaidi wa upande wa mashtaka SAID MUSSA alidai siku ya tukio,mtuhumiwa


akiendesha gari Toyota hilux Double cabin waliongozana kwenda kupokea
mzigo mali ta CITIBANK uwanja wa ndege JNIA. MUSSA aliendelea kueleza
kuwa alikutana na maafisa wa DAHACO akakabidhiwa mzigo.

Alisema mzigo huo ulikuwa ni fedha za kigeni USD 2 MILLION uliokuwa na


uzito wa kilo 20 na akaupakia nyuma ya gari na kufunga. Alirudi mbele kwenye
gari na KASUSURA akawasha gari wakatoka maeneo ya airport.
Mussa akadai,walipofika barabarani ya Nyerere mtuhumiwa alipaki gari lao
nyuma ya Toyota landcruiser iliyokuwa imeegeshwa na akamtolea bastora na
kumwambia "UHUSIANO WETU UNAISHIA HAPA" kishha akamwamuru
afungue alipoweka mzigo na akampokonya simu.

MUSSA akadai KASUSURA alipomuona kazubaa akachukua funguo na kwenda


kufungua nyuma. Wakashuka watu kwenye Landcruiser na kupakia ule mzigo
kisha wakamwamuru atimke. Akadai alikimbilia kituo cha polisi STAKISHARI
kutoa taarifa ambapo alishikiliwa kusaidia polisi.

Siku mbili tu baada ya kesi hii kusomwa, Tarehe 9 jan 2002 aliibuka IGP
OMARI MAHITA na kudai wanawashikilia askari wake nane wakiwemo watatu
waandamizi kwa kusaidia kumtorosha mtuhumiwa kila alipokamatwa(mara
tatu Dar na mara nyingine mikoa ya Arusha na Tanga)

Aliwataja Askari hao kuwa ni SSP BONAVENTURE MSHONGI(RCO-Tanga),


ASP BEATRICE MAONA na ASP DEUSDEDIT KAJUNA(Ofisi ya RCO-DSM),Sgt
EMANUEL na PC ROGATHE(Tanga) pia makonstebo JEREMIAH,ISAAC na
DAVID

Baada ya kauli hiyo Mkurugenzi tarehe 15 jan 2002 wa makosa ya jinai ADAD
RAJAB alitoa taarifa ya kuwaachisha kazi askari watano wa chini na
kuwafungulia mashtaka wote nane mahakamani.

Polisi hao walipandishwa makahamani tarehe 16 Jan 2002 kwa makosa ya


kumtorosha mtuhumiwa baada ya kumkamata,kesi yao iliendelea pamoja na ya
KASUSURA ambaye mkewe alifariki tarehe 22 Feb 2002. Aliomba dhamana
aende kuzika lakini mahakama ilimkatalia kwa hofu ya kutorokwa.

Kupitia ushahidi,Mahakama ilimwona KASUSURA ana kesi ya kujibu ambapo


katika utetezi wake alidai ni kweli alikuwa akiendesha gari iliyotajwa na
alipotoka nje ya Airport bosi wake alimwamuru ashuke garini na akakabidhiwa
gari nyingine na akapangiwa majukumu tofauti.

Pia alikana kumiliki bastora siku ya tukio kama ushahidi ulivyowasilishwa. Hata
hivyo Mh. Hakimu SILVANGILWA MWANGESI alimkuta na hatia na tarehe 30
March 2007 alimhukumu jela miaka 30 kwa unyang'anyi na miaka 5 kwa wizi
CONSECATIVELY (hivyo jumla miaka 35)pamoja na viboko 12.

Washtakiwa wenzake SITA hawakukutwa na kosa la kujibu hivyo waliachiwa


huru. Pia hata wale polisi NANE ushahidi haukutosha nao waliachiwa. Mmoja
wao SSP BONAVENTURE(RCO Tanga) alipanda cheo kuwa ACP na alikuwa
RPC wa Pwani,Simiyu n.k

Baada ya Hukumu KASUSURA alikuwa kivutio pale alipomshukuru Hakimu


kwa kumwambia "ASANTE SANA MHESHIMIWA" na wakati anapanda
karandinga alisikika akisema "NIMEONEWA,MIMI NI DEREVA
TU,NILIKABIDHIWAJE BASTORA WAKATI SIO JUKUMU LANGU?"

Wakili wa wa Mshtakiwa MAJURA MAGAFU alikata rufaa nahakama kuu


akiwasilisha hoja sita. Na hukumu yake ilitolewa tarehe 23 June 2010 na Mh. Jaji
THOMAS MIHAYO(kama sijakosea sasa ana mavyeo kibao kwenye bodi mbali
mbali na Tume ya uchaguzi)

Katika hukumu Jaji alisema Wangeweza kuitupilia mbali rufaa hiyo tangu
mwanzoni kwani ilikuwa nje ya muda,hata hivyo waliisikiliza ili kurekebisha
adhabu kwani wanahisi hakimu alipotoka alipohukumu CONSECATIVELY
badala ya CONCURRENTLY yaani sio kifungo kwa KUFUATANA bali PAMOJA.

Hivyo mahakama ikampunguzia kifungo KASUSURA na kuwa Miaka 30 badala


ya miaka 35. Kwa ufupi rufaa yake iligonga mwamba lakini alipata auheni ya
miaka ya kutumikia kifungoni. Hata hivyo KASUSURA hakukata tamaa na
alikata rufaa tena Mahakama ya Rufaa.

Safari hii hakuweka wakili bali alisimama mwenyewe kujitetea na akawasilisha


hoja TISA kupinga hukumu yake mbele ya majaji watatu SEMISTOCLES
KAIJAGE,MBAROUK MBAROUK na SAIDA MJASIRI ambao walimsikiliza
tarehe 11 April 2016

Kati ya hoja TISA za KASUSURA ni hoja TATU ziliwashawishi majaji hawa nazo
ni;
1. Kiapo chake cha kukiri kosa na Onyo kilichotolewa mahamani
kilipandikana nje ya muda wa kisheria ya mwenendo wa makosa ya jinai.
Alikamatwa Dec 24 akachukuliwa maelezo 26 Dec 2001
2. Muda waliodai ametenda kosa hilo,Mabadiliko ya Sheria ya KANUNI ZA
ADHABU inayoelekeza kifungo cha MIAKA 30 kwa anayekutwa na hatia
ARMED ROBBERY yaikuwa hayajaanza kutumika. Je, NI KWA NINI
HAKIMU ALIMUHUKUMU KWA SHERIA AMBAYO HAIKUWEPO?
3. KASUSURA alidai hadi wakati anahukumiwa,Upande wa Mashtaka
haukuwahi kumleta shahidi yoyote ambaye ni mmiliki wa mzigo unaodai
kuibiwa(CITIBANK) Pia kiasi kinachodaiwa kuibiwa hakikufanana kati ya
HATI YA MASHTAKA na kiasi walichotaja MASHAIDI. CITIBANK tu
ndio wangetoa utata.
Baada ya hoja hizi majaji waliwabana vilivyo mawakili wa serikali
TUMAINI KWEKA na CECILIA MKONONGO ambao walikosa kabisa
hoja kinzani. Majaji wakapanga siku ya hukumu iwe tarehe 09 May 2016

Siku ya hukumu kwa masikitiko makubwa hukumu ilianza kwa kusema


kuwa "THIS CASE WAS BADLY INVESTIGATED AND HENCE POORLY
PROSECUTED"

Kisha majai WAKATUPILIA MBALI kielelezo cha upande wa


mashtaka(MAELEZO YA KASUSURA YA KUKIRI KOSA NA ONYO)
kwani kilipatikana nje ya muda wa kisheria wa MASAA MANNE kama
inavyotakiwa na Haya ya 50 na 51 ya SHERIA YA MWENENDO WA
MAKOSA YA JINAI YA MWAKA 1985

Pia hakukuwa na kumbukumbu yoyote inayoonyesha kama kuna


mahakama iliwaongezea muda upande wa jamuhuri kama inavyotamka
Aya ya 51(1)(a) hivyo mahakama ilikosea kuhukumu kwa kielelezo
kilichopatikana "in CONTRAVENTION of requirements of the Law"

Jaji akasema Prosecutors walishindwa kudhibitisha kesi pasipokuwa na


shaka kwani kwa sababu wanazozijua wao walishindwa kumwita shaidi
kutoka CITIBANK ambaye ndiye angethibitisha kiasi kilichoibiwa na
kama kweli zilikuwa pesa zao. KIUFUPI KASUSURA AKATEMA
NDOANO AKAACHIWA HURU

Alipata uhuru baada ya kutumikia jela miaka TISA na ukijumlisha miaka


SITA ya rumande jumla ni 15. Inasemekana KASUSURA yupo zake
BIHARAMURO akiwa kaukata balaa. Yaani mida hii anakula tu firigisi za
kuku wa kienyeji. Swali ni JE, PESA ZILIENDA WAPI?

Ikumbukwe dola Mil 2 kwa currency ya mwaka 2001 ni kama bil 2 na


millioni 600. Kwa mwaka huu ni zaidi ya Bil 4 na ushee. Je nani alikuwa
mnufaika halisi wa pesa hizi ikiwa KASUSURA alikutwa na laki mbili na
nusu tu? Kwa nini CITIBANK hawakuitwa mahakamani? Walisahaulika
makusudi?

Na Swali la kujiuliza, Wale washtakiwa SITA "SILAYOS" na wengine


waliingizajwe kwenye kesi? Mtaani kuna vijimaneno vinasema Mmoja
kati ya wale polisi walioshitakiwa alifanya RENOVATION ya nguvu
kwenye nyumba yake kipidi kile KASUSURA anasakwa. Je lilikuwa ni zao
la pesa hizi?

You might also like