Kufa Kuzikana

You might also like

Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 21

MWALIMU FAGILI FARAJA MONDE 0780947386/0785090252/0756040644

RIYAYA YA KUFA KUZIKANA

NA

KEN WALIBORA

2003

NAIROBI –KENYA

Sura ya kwanza (1-6)

Riwaya inaanza mzungumzaji akiwa basini kwenye vilima vya Tungule


ambapo mamake alifia katika ajali ya barabarani. Alikuwa anaelekea
katika mjiwa Tandika mji mkuu wa kiwachema, kwa ajili ya
kuzawadiwa na waziri kwa kuwa miongoni mwa wanafunzi watatu
bora katika mtihani wa taifa wa shule za msingi.

Msemaji analinganisha kifo hicho na kifo kingine cha mwamu Alex


ambaye alikuwa mwalimu wa Hisabati shuleni kwake na mtetezi wa
wakanju na mpinga ukabila.

Pia nayuelezea kuhusu mbunge Johstone mabende ambaye alikuwa


mkorosho aliyekuwa anachukia wakanju na kuchochea chuki
miaongoni mwa wakoroso alipohutubia watu katika mkutano wa
hadharani katika kituo cha biashara cha Baraki kwa kusema kuwa
“Hatutaki madoadoa hapa. Wakanju sharti wahame warudi kwao
Kanju”.

Mwalimu Alex alimjibu kwamaba, “Mhesimiwa unaanza kuzungumza


kama mtu aliyefunguka skrubu za akili. Wakanju ni ndugu zetu
ata watu wa fikira kama zako ndio maharabu wa nchi” maneno
hayo yalimletea mwalimu Alex kuchukiwa na wakorosho wengi.

Baada ya muda mfupi, mwalimu Alex alirukwa akili kiasi cha kuanza
kuzungumza na vichaka na kutembea uchi njia. Twaelezwa pia kifo
cha mwalimu Alex huko kichakani karibu na mto Kibisi.
Alipigunduliwa na wanawake waliokuwa wamekuja kuchota maji.
Maiti ya mwalimu Alex ilikuwa imekatwakatwa na kutupwa huko.
Maiti hii ilichukuliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi

Siku moja baada ya kifo hicho, msemaji alikuta kijikaratasi kimetupa


kiamboni mwao chenye maneno “ Wakanjuu mumechokoza nyuki
kwa kumuua mukoroso. Ama muondoke au mufe muzingani.”

1|P a ge
MWALIMU FAGILI FARAJA MONDE 0780947386/0785090252/0756040644

Maneno haya yalimwogofya babake msemaj ambye ni mkanjuu. Lakini


alipomwuuliza rafiki na jirani wake mzee Zabloni ambaye alikuwa
mkorosho alimjibu kuwa ilikuwa kawaida ya wakorosho
kuwatishatisha wakanjuu.

Sura inaisha bado msemaji akiendelea na safari yake ya kueleke mjini


Tandika.Uk6

Sura ya pili (7-17)

Msemaji alifika jijini tandika aliko elekea alitaraji kupokelewa na rafiki


wake Tim ambaye alikuwa rafiki wa kufa kuzikana kutokana na kiasi
cha urafiki wao. Urafiki ulianza kutokana na hali hiz;

 Tim alimlinda Tom huko shuleni Baraki zidi ya wachokozi.


 Timu alikuwa anaenda nyumbani kwa Tom kujifunza kucheza
jita na nyimbo kipawa alichokuwa nacho babake rafiki yake Tom
 Tim hawezi kusahau siku alipoumwa na nyoka wakicheza na
nyumbani kwa Tom babake Tom akampa dawa.

Akida alitwelezeakuwa alipata fursa ya kuonana na rafiki yake Tim


alichukuliwa na mjombake kufanya kazi mjini baada ya kuanguka
mitihani ya kitaifa ya msingi.

Akida alienda mjini kwanza ili kuzawadiwa akama serikali


ilivyopanga, pili aliaagizwa na babake kwenda kwa kampuni ya
mawakili ya Gembo amwuulize Gembo kuhusu madai ya malipo ya
bima ya hayati mamake.Uk11. Vilevile alimwagiza aende kwa
kampuni ya wachapishaji ya HATUBAGUI publishers aulizie mhariri
wa Kiswahili au meneja wa uchapishaji kuhusu miswada wake wa
mashairi yaani walikawia kuuchapisha. Uk11

Akida alipokelewa na Tim kwenye kituo cha mabasi wakaelekea


mkahawani kwa chakula. Tim hakuishiwa na maswali ya kumwuliza
akida kuhusu kijiji cha baraki, wazazi wake, dadake na yote Akida
alimjibu Uk13.

Akida alionyesha ushamba alipoita sausage chuchu za ngombe, pia


anashanga kunywa soda baridi yaani ilikuwa mara yake ya kwanza
kula na kunywa vitu vya aina hiyo.

Kijana mmoja kwa jiana David alikuja mkahawani na alipomwona Tim


alikitoka mkahawani kwa kuwa Tim alikuwa na deni la Tim.

2|P a ge
MWALIMU FAGILI FARAJA MONDE 0780947386/0785090252/0756040644

Vilevile Timu alimpongeza kwa kushinda na kupita vizuri mitihani ya


kitaifa. Uk15

Tim alimwahidi Akida kuwa atamtembeza jiji zima kwa siku atakazo
maliza hapo mjini. Akida naye alimwambia kuwa muda huo
ungetosha kufuatia malipo ya bima ya mamake na suala la
kuchapisha vitabu vya babake.

Timu na Akida walishika njia ya kuelekea nyumbani kwa Akida,


wakati huo taa za umeme zilikuwa zimwangaza jiji zima. Walipitia
kichochor Fulani wakakuta watu walioshikwa na askari polisi ili
watoe hongo.

Walipokuwa wamesimama barabarani waliona wanawake ambao


walikuwa nusu uchi Timu akasema ni vivutio vya mji. Hayo yote
yalimshangaza akili Uk17.

Walipata gari kwelekea Shauri Moyo alikoishi Timu. Gari lilikuwa na


breki zinazo kwaluza na vyuma na lilijaa pomoni.

Sura ya tatu (18 -30)

Tunaelezwa kwa Tim alikuwa anafanya kazi ya ukarani kwenye


kiwanda cha kusindika mafuta, vile vile tunapewa taswira ya mahali
alipoishi Tim.

Asubuhi ya siku iliyofuata Akida alirauka kwamuka kwani alikuwa na


hamu ya kuliona jiji. Ilibidi Timu aende kazini aombe ruhusa ili aweze
kumtembeza vizuri Akida jijini Tandika. Uk 18-19

Nyumbani kwa Tim kulikuwa mengi ya kumfunza Akida kama namna


ya kutumia choo cha flashi, kufungua tapu ya bafuni, kuweka swichi
ya umeme na televisheni ilipowekwa ilipowekwa mazungumzo
yalikatiaka hadi ilipozimwa. Televishen ilipozimwa mazungumzo
yaliendelea na Akida alimwelezea yote ya kijijini yaani walioolewa,
waliokufa(mw. Alex)n.k

Akida hakukawia kumwuliza kuhusu picha ya kipusa iliyokuwa


ukutani. Alielezwa na Tim kuwa alikuwa mke mtarajiwa msichana wa
kabila la wasangura kwa jina Pamela.

Walishika gari asubuhi kwelekea eneo la viwanda ili Tim aombe


ruhusa. Siku hiyo Akida alitembezwa kila pembe ya jiji la tandika.

3|P a ge
MWALIMU FAGILI FARAJA MONDE 0780947386/0785090252/0756040644

Aidha Akida alionyeshwa ofisi ya waziri wa elimu, ofisi ya wakili


Gembo na ofisi ya wachapishaji waliokuwa na mswada wababake.

Safari yao iliishia mtaa wa mlimani kwa bwana Samsoni Tungu


mjombake Tim. Hapo Akida alipata tatizo la miguu inayonuka kwa
sababu ya viatu vya palstiki alivyotembeza jijini kwa siku nzima.

Mjombake Tim alikuja akawakaribisha kwa furaha tele. Shida ilitokea


Tm alipomtambulisha Akida kama rafiki yake, mjomba alipouliza
kabila lake, aliambiwa kuwa ni mkanjuu. Alikasirika na kusema
wakanjuu ni watu wajinga sana, wakanjuu wanapenda matanga.
Maneno haya yalimkashirisha Akida mpaka walipoondoka Uk.26

Baada ya hapo walielekea mkahawa kula chajio na kuelekea


nyumbani shauri moyo. Mpango wao wa asubuhi ulikuwa Tim aende
kazini na Akida angejipeleka kwa ofisi alizotaka kutembelea.

Tim alikumbukia kuweka Televisheni ilikuangalia na kusikiliza


taarifa. TV ilipowekwa walikuta taarifa huku waziri wa usalama nchini
kiwachema akiwapiga marafuku wachapishaji habari za wongo
kuhusu vita vya kikabila. Walipoweka Redio, ilidhihirisha ukweli
kuwa kulikuwa wachapishaji wa habari walikuwa hawaruhusiwi huko
Korosho isipokuwa mashirika ya kutoa msaada kwa waathiriwa wa
vita hivyo pekee ndio waliruhusiwa.uk30

Sura ya nne (30-34)

Asubuhi Timu alirauka kwenda kazini na Akida aliamka mapema


kwenda kununua gazeti la siku hiyo jijini. Timu alikuwa
amemwelekeza kunakouzwa gazeti yaani kwenye makutano ya
barabara ya Lumumba na wanambisi. Alikuwa amefika na kushika
gazeti hivi, polisi wakazingira sehemu hiyo na kuchukua magazeti
yote yaliyokuwa yanauzwa katika sehemu hiyo. Uk31

Akida alitafuta njia ya kumrudisha nyumbani kwa Tim lakini


alichanganywa na majumba ya mjini ambaya si rahisi kuyatofautisha.
Alienda kama kipofu hadi barabara moja iliyokuwa sambamba na
mtaro wa majitaka wenye ustani kando walimokuwa wamepumzikia
malofa, walalahoi na wapendanao. Mtaroni wasichana wadogowadogo
walikuwa wanakoga bila aibu.

Akida kwa uchovu alitoa viatu ambavyo vilikuwa vimemwachia


sagamba na sugu kwenye vyanda vya miguu. Akida alichukuliwa na

4|P a ge
MWALIMU FAGILI FARAJA MONDE 0780947386/0785090252/0756040644

usingizi na viatu vyake vilibwa na watu waliokuwa karibu naye(Ninja


na mwenzake). Akida alitembea kwa miguu bila kujua alikoenda
akakutana na msichana mrembo aliye mwelekeza njia ya kumrudisha
Shauri moyo kwa Tim.

Sura ya tano (35 - 46)

Akida aliporudi kwa Tim alimkuta mwenye shaka kwa kuwa


alimsubiria asubuhi kabla ya kwenda kazini hakumwona, aliporudi
kutoka kazini alikuwa hajarudi. Akida alimwelezea kuwa alipotelea
mjini, na kaibiwa viatu vyake. Tim alimchekelea tu baadal ay
kumfokea.uk 35

Jioni hiyo, Tim alitembelewa na mpenzi wake Pamela. Ilikuwa jioni ya


furaha na kuonyeshana mahaba. Baadaye Tim na pamala walicheza
na kuimba nyimbo za kimapenzi. Akida alilazimishwa ajiunge nao
katika kuimba na kuchza Jitaa. Uk 37-38

Akida aliwaimbia wimbo wa kimapenzi ambao alipenda kuimba


babake. Wimbo huo iliwaibua hisia za kimapenzi akawaliza machozi.
Pamale alimpenda sana Akida na akaahidi kuwa ndiye angeimba kwa
sherehe yao. Wakati wa saa mbili usiku walimsindikiza akarudi kwa
sangazi yake mtaa wa mama Nasambu.

Asubuhi akida alienda kwa Afisi ya bwana Gembo kudai malipo ya


bima ya marehemu mamake, alimkuta sekritari mwenye dharau na
mtovu wa nidhamu. Huko afisini akida alikutana na mzee yusufu
matuko.huyu alikuwa amekosa dole gumba katika ajali. Alikuwa
ametembelea afisi hii kwa miaka kumi ila kusaidiwa. Vile vile kuna
watu wengine ambao walikuja hapo afisini siku hiyo. Wengine
waliambiwa pricess ndefu, wengine faili zimepotea, wengine rudi siku
nyingine. Waathiriwa wengine walibaki afisini na kugoma kwamba
hawatoki mpaka wamwone Gembo mwenyewe.uk45

Sura ya sita (47 - 57) kuzawadiwa kwa Akida na kupatikana kwa


miswada ya mahairi ya babake.

Ni siku ya kuzawadiwa ya watahini bora watatu nchini kiwachema


akiwemo Akida. Sherehe ilikuwa ya saa tano asubuhi, Akida
alisindikizwa na Pamela na Timu alijiunga nao baadaye wakati
wengine walikuja na wazazi wao(Donald Kitenge aliyekuwa wapili na
Regina Kato aliyekuwa wa kwanza).tuliambiwa kuwa babake Donald

5|P a ge
MWALIMU FAGILI FARAJA MONDE 0780947386/0785090252/0756040644

Kitenge alikuwa mfanyikazi katika ngazi ya juu katika Baraza la


mitihani ya taifa(BMT) na Regina Kato alikuwa mpwa wa waziri wa
elimu Bwana Kato. Uk51

Baada ya sherehe za kuzawadiwa, Akida na wenzake walipitia kwenye


afisi za Hatubagui Publishers. Walipofika waliambiwa kuwa miswada
ya sululu ilichapishwa miezi sita nyuma na ilitumwa kwa posta.
Meneja alisema kuwa huenda wafanyikazi wa posta walinyakuwa
kifurusi hicho kama ilivyokuwa kawaida yao kudokoa za watu. Akida
alipewa nakala sita na meneja ampelekee babake uk52.

Walishika njia ya kurudi shauri moyo walipofika kwa kituo cha


magari walikutana na ummati wa watu waliokuwa wamebeba jitu la
miraba mine lililorejelewa kama MTOTO. Uk 54- 55. Mwanamke
mmoja alitembea akikusanya pesa za kumpeleka hospitalini huyo
mgonjwa wao. Mwanamume(mtoto) huyo alikuwa ametahiriwa baada
ya kuripotiwa mkewe kuwa hajatahiriwa, na kulingana na utamaduni
wa wachungwachungwa ilikuwa lazima kwa kila mwanaume.

Walipanda gari la kuwarudisha shauri moyo amabalo lilikuwa limejaa,


Tim alimpa abiria mwanamke zawadi ya Akida ampakatie. Walipofika
stendi wanaposhukia, Tim alishuka akasahau zadi ya akida na
mwanamke Yule. Walisubiria gari hilo papo hapo lakini liliporudi na
kukagua ndani zawadi hawakuiona.

Sura ya saba (58 -66) mwembe shomari kwa Tim

Asubuhi Akida alikuwa chumbani kwa Timu akiwazia yaliyokuwepo


siku iliyopita, Tim alimwambia kuhusu simu aliyopokea kutoka kwa
Tom kuwa Baraki vita vilikuwa vimechakaa watu wakiuana tuputupu.
Waliweka televishen lakini haikuwa na habari yoyote kuhusu vita vya
Baraki. Asubuhi walitega Redio ya BBC Kiswahili na ilitoa habari
kuwa “ mamia ya watu wakimbilia Usalama, watu takribani themanini
wameuawa na mia tatu wamejeruhiwa vibaya. Uk61

Inasemekana kuwa vita hivyo vyasababishwa na chuki kati ya


wakorosho na wakanju pamoja watu wenye ushawishi mkubwa
kisiasa. Akida alisoma kwenye gazeti lililoletwa na Tim akakuta habari
ya kukamatwa kwa mhariri mkuu wa gazeti la kiwachema leo na sauti
ya kiwachema kwa kuchapisha habari za kupotosha na kuvuruga
amani nchini.

6|P a ge
MWALIMU FAGILI FARAJA MONDE 0780947386/0785090252/0756040644

Pia gazeti lilikuwa na habari za kifo cha Yusufu Matuko aliye jitupa
kutoka gorofala 22 ya Tembo house baada ya wakili Gembo Tony
kukataa kuonana naye uk.62.

Asubuhi hiyo Timu alikuwa ameenda kazini, Akida alisikia mtu


anagonga mlango akamkuta ni Tamari dadake Tim kavimba miguu
hawezi hata kupanda vipandio vya kuingia chumbani mwa Tim. Akida
alisaidia kumbeba akamwingiza hadi kitandani na akampikia maji
akamkanda miguu na kumpa chai. Baada ya kufanya hayo yote,
Tamari alimpa kumfokea na kumtusi. Uk63

“Nyie wakanju ni wajinga


Nyie ni wauaji….
Nenda huko bwege wewe…
Unafanya nini katika nyumba ya kakangu?”
Akida alitoka nje ilikuzuia hasira zake, akamwona Tim anarudi
kutoka Kazini wakati wa saa tatu asubuhi. Tim alikuwa amefukuzwa
kazini na mjombake kwa sababu alienda kwa sherehe ya Akida rafiki
yake mkanju. Mjomba alisingizia kuwa wakanju wanaua wakorosho
kwa hivyo Tim alikuwa anasaliti kabila lake kwa kumleta mkanju
nyumbani kwake

Tim alipoingia ndani, Akida aliponyoka na kwelekea mjini asipopajua


akajikuta karibu na kituo cha redio sauti ya Kiwachema. Uk66

Sura ya nane (67 - 71) Kwa Timu na Baadaye mjini kwa Nyumba
za maiti

Akida alirudi kutoka mjini, alipofika Tamari na matusi yake alianzia


alipoishia. Mara hii Akida alipozwapozwa na Pam ambaye alikuwa
amemtembelea Tim mpenzi wake.

Pam alimwambia Akida kuwa Tamari aliponea chupuchupu kubakwa


akakimbia, alikuwa amelala msituni siku kadha. Amewaona watu
wakiuawa akiwemo babake Zablon ambaye alimwona anakatwakatwa
kwa panga na wakanju anaowajua miongoni mwao alikuwa mzee
sululu babake Akida.

Tim alikuwa ameenda kukagua maiti ya babake katika nyumba za


maiti mjini Tandika kwa kuwa walisema zile za Korosho na Nduchi
zilijaa pomoni.uk68

7|P a ge
MWALIMU FAGILI FARAJA MONDE 0780947386/0785090252/0756040644

Tim aliporejea alisema hakumwona babake miongoni mwa maiti


waliokuwepo bali alimwona mzee sululu. Walifuatana na Akida
wakarudi huko na walipofika walikuta maiti ile ilikuwa ya mtu
mwingine si Mzee Sululu.

Sura Tisa (72 - 79) Hospitalini Rufaa

Akida na Tim walifika hospitalini Rufaa. Kwenye hospitali hii huduma


zao zilikuwa mbovu. Wagonjwa hawasaidiwi, ukosefu wa madaktari,
kuta zilizokosa rangi paa zinazovuja na nyufa kila mahali.

Walienda hadi kwenye lango la wodi za wagonjwa wanaume, bawabu


aliwafokea na kuwafukuza kuwa muda wa kuona wagonjwa ulikuwa
umepita. Akida alimpa noti ya shilingi ishirini akawaruhusu kuingia
uk 73

Waogonjwa walikuwa wengi ndani lakini Akida alimtambuwa mgonjwa


mmoja ambaye alikuwa mzee Uledi. Huyu alikuwa amevunjika mguu
alipokuw anakimbia jeshi la wakorosho. Kabla ya kukimbia alikuwa
na Sululu ambaye hangemsaidia. Alimwacha kwake hajui kilichojili
kwa Sululu na familia yam zee huyu. Akida na Tim walipiga sachi
katika wodi zingine lakini hawakuona wazazi wao wakaondoka.

Sura ya Kumi (80 - 91)

Tim alishauri wapitie kwa Tom ktika mtaa wa mlimani ili aweze
kuwasaidia kuwapeleka kwa hospitali za Nduki na Korosho kwa gari
lake. Walipofika, walipokelewa na Janelle mke mzungu kutoka
Canada. Tom naye alirudi nyumbani kutoka kazini baada ya kupata
habari za kifo cha babake. Walikubaliana kuondoka pamoja siku
iliyofuata asubuhi waende hospitalini Nduchi mwali wa Mangala
ulipokuwa.uk87

Walipofika hospitalini, mtumishi wa hospitali hiyo aliwaomba pesa ili


awasaidie. Tim alimpa pesa akawasaidia kuwatafutia maiti Mangala
wakauona lakini Akida na Tim hawakuwaona wazazi wao. Tom
alijitolea kuwapeleka Tim naAkida hospitali la Korosho ili waweze
kuwasaka wazazi wao. Tom alikodisha polisi wawili wakaenda nao.
Walifika wakakagua maiti wote waliokuweko lakini wazazi wao
hawakuwemo. Walirudi Korosho Tom akakodisha gari la kupeleka
maiti ya babake katika mchware za Tandika.

8|P a ge
MWALIMU FAGILI FARAJA MONDE 0780947386/0785090252/0756040644

Siku iliyofuata Tom alitoa kiasi cha pesa kwa idara ya polisi ili wampe
ulinzi watakapokwenda kumzika babakekijijini.Tom alishauriwa na
Tim kumzika babake katika makaburi ya umma akakataa kwa
kusema kuwa lazima afuate mila na destuli za kwao yani mtu
huzikwa kwao.

Sura ya kumi na moja (92 - 104)

Safari ya kwenda kijijini Baraki kumzika Mzee mangala ilianza na basi


dogo la aina ya Mitsubishi lilibeba maiti na kusafiri wakati wa usiku.
To aliambatana na marafiki zake wa kazini, Akida na askari polisi
wane. Njiani hawakusumbuliwa na askari wa barabarani baada
kuwaona wenzao ndani ya gari.

Njiani mazingira yalikuwa yamebadilika kabisa. Palipokuwa na


vijiduka palikuwa na vifusi na rundo la majivu, vinga vya moto na
viwingu mosi. Nyumba nyingi zilikuwa zinateketea kwa moto.
Waliwaona mbwa ambao waliburuta mafuvu ya vichwa vya watu
waliouawa. Uk 94 – 96

Walipofika, nyumba yam zee Mangala nay a Tom zote hazikuwepo.


Walichimba kaburi karibu na lile la mkewe chini ya mwembe
wakamzika kama alivyo amru kabla ya kufa.

Tom alitoa hotuba (maneno ya mwisho) kama alivyoshauriwa na


marafiki zake na kwa ufupi alisema kosa la babake lilikuwa kuzaa
mkanju kikabila na mwenye ngozi nyeusi. Tom aliahidi kwenda kukaa
ngambo milele.

Kabla hawajaondoka Akida alipewa askari waende kwao akaone


kinachoendelea kuhusu babake. Njiani walikuta maiti za watu nyingi.
Alipofika mazingira ya kwao yalikuwa kama ndoto inayopita akilini
mwake. Nyumba zote ziliteketezwa kwa moto, baba hakumwona
ispokuwa vipande vy jitaa lake.

Walirudi walipozika, wakakuta gari lishawashwa moto tayari


kuondoka nusra liwaache. Gari lilisimama wakajitupa ndani. Tom na
marafiki zake wengine hawakuwemo garini Akida alipoulizia alipo
Tom, alielekezwa chini ya mwembewalipomzika babake.

Genge la washamburiaji likiongozwa na mkuu wa polisi mmoja lilikuja


wakawauliza vitambulisho na wakanju wote wakauawa na wengine
wakambiwa kuondoka himahima. Akida aliposikia hayo alimhurumia

9|P a ge
MWALIMU FAGILI FARAJA MONDE 0780947386/0785090252/0756040644

sana Tom rafikiye na hali hiyo ilimletea kushuka gari akarudi


alikolala Tom

Sura ya kumi na mbili (105 - 109)

Akida alimkuta Tom chini ya mwembe akiwa amechomwa mshale


kifuani. Alijaribu kumwita na kumpa msaada wa kwanza wa
kwamnza. Wakati huo Akida alisikia mchakato nyuma yake
akamnyamazisha Tom akakimbia na kujificha ndani ya shimo la taka
lililokuwa karibu na ua. Wavamizi walimkuta amelala hapo Tom
wakadhani ameachwa. Walitaka kumchoma mshale mwingine na
kumkatakata lakini mmoja wao alishauri wasiuwe maiti. Miongoni
mwao Akida alipochungulia vizuri alimwona mzee Zablon babake
rafikiye Tim.

Wavamizi walipoondoka, Akida alimficha akasubiria usiku alimbeba


akatumia torori hadi njia kuu alipopata gari la kutoa msaada la
Action Men ambalo hupeleka chakula cha msaada katika kambi ya
wakimbizi ya Mukutu mjini Tandika likawachukuwa. Njiani
waliwaona mbwa wakicheza na sehemu za mwiili ya binadamu

Sura ya kumi na tatu (110- 113)

Akida katika mtaa wa Falkland anaelekea kwa rafikiye Tim. Ni mahali


papya alipokodisha chumba Tim baada ya kufukuzwa kazini na
mjombake. Falkland ni mtaa mchafu sana uliojaa makabwela na
maskini hohehahe. Akida aliambatana na kijana mwingie
alimwelekeza hadi kwenye vyumba Tim anakolala.

Timu alikuwa ameishiwa baada ya kufukuzwa na mjombake kazini,


aliuza vitu vyote vya thamani alivyokuwa navyo na nakala za diwani
Kero za Mkiwa ili aweze kulipa madeni. Tim alielezea kuwa alitaka
kumpeleka David kotini kwa ajili ya kukata kumlipa pesa
alizomkopesha Tim miaka miwili nyuma.

Akida alimweleza Tim kuwa alimwona babake Baraki katika genge la


wavamizi wauaji. Pia alimjulisha kuwa Tom kapigwa mshale kifuani
amemwacha hospitalini Rufaa mjini.

Akida baada ya kuona maisha aliyoishi Tim alipendekeza aende aishi


katika kambi za wakimbizi ili asimzidishie mzigo Tim, lakini tim
alimkataza. Akida alitoa sbsbu nyingine ya Tamari, lakini alijulishwa
kuwa Pam na Tim walikuwa wameongea naye ju ya kukomesha

10 | P a g e
MWALIMU FAGILI FARAJA MONDE 0780947386/0785090252/0756040644

mizozano ya nawe. Kweli Tamari alipoamka alimkuta Akida na


hakuwa na shida yeyote naye kama ilivyokuwa mwanzoni.
Walikunywa chai bila vitafunio wala sukari.

Tim alienda kutafuta kibarua akamwacha Akida apumzike. Akida


alibaki na Tamari. Tamarai alimwomba akida msamaha kwa uhasama
wote aliomfanyia tangu shuleni.akida alikilalia kitanda chaTamari,
alipochukuliwana usingizi aliota Tamariakimwimbia wimbo,
wakionyeshana hisia za mapenzi.

Sura ya kumi na Nne (119-127)

Tunaonyeshwa maisha ya Tim,Akida na Tamari yaliyokuwa ya


kupambana na kuajibika kama ilivyosemekana kuwa maisha ya watu
wa Falkland ilikuwa ya “kufanya lolote ili kupata chochote.”

Tim na timu yake waliamua kufanya lolote la halali ili kukimu maisha
yao. Pia Tim na timu yake walifuata sana mkondo wa dini na kila
juma pili walienda kanisani kuhudhuria mahubiri ya Kasisi John.
Mahubiri ya kasisi ya tilia mkazo kupinga ukabila, uasherati na
ubaguzi.

Kama ilivyokuwa kawaida yao Tim na Akida kumtembelea rafiki yao


Tom hospitalini. Siku moja walienda huko hawakumkuta huko.
Walipouliza waliambiwa na mgonjwa kwenye kitanda jirani kuwa
kachukuliwa na mwanamke mzungu kwa matibabu Canada.
Walipokuwa wanarudi kwa Tim walipitia mtaa wa Mlimani kwa Tom
wakakuta mwenyeji mwingine mhindi. Hali hii ilionyesha wazi kuwa
To kauza nyumba yake kabla ya kwenda ngambo. Uk124

Kwa sababu ya umasikini Tim alifikiria kumpeleka David aliyemdai


shilingi ishirini zake mahakamani lakini alikatazwa na Pam.

Akida naye alielezea kuwa nafasi yakeya kusoma katika shule za


sekondari ilikuwa imeuzwa kwa mtoto wa tajiri mmoja alipoenda
kumwuuliza waziri, akawa anafukuzwa na sekritari.

Sura ya Kumi na tano (128-133) Falkland kwa Tim

Tim alikuwa na kibarua cha kukesha wakati wa usiku kiwandani,


Akida alipokuwa amelala asikia mguso wa Tamari. Baada ya kuwazia
mengi kuhusu nini kingejiri aliamua kumkataza malengo yake kwa
kuutupa mkono wa Tamari mbali. Kitendo hicho kilimkasirisha

11 | P a g e
MWALIMU FAGILI FARAJA MONDE 0780947386/0785090252/0756040644

Tamari na kesho yake Tim aliporudi alimsingizia Akida kwamba


kataka kumbaka usiku. Akida alimkasirikia sana Tamari akaamua
kutoka kwa Tim na kwenda zake.

Alipita katika vichochoro vya Falkland, akajikuta karibu na klabu


moja inayouza pombe ya busaa. Akida alifikiria kujitoa uhai ili
asikabiliane na hali za kumkasirisha kama hiyo. Aliamua aingie klabu
hiyo akapitishe muda na mawazo na waliokuwemo. Hapo ndipo
alipomsikia mlevi mmoja aliyejisifia kuua wanju wengi vitani. Maneno
hayo yalimkasirisha zaidi Akida baada ya muda mtu huyoaliyejisifia
alienda msalani Akida alimfuata nyuma akamsubiria nje ya choo
alipotoka alimtwanga kibao kipajani akazirahi. Akida aliogopa sana
akakimbilia kichochoroni kilichokuwa karibu akidhani amemua.

Sura ya kumi na Sita (134-143) Mjini Tandika

Akida alidhani amemua mzee zablon baba wa rafikiye Tim. Alitembea


mjini akajikuta kwa kituo cha mabasi yanayoenda Sangura. Kwa njia
ya kukimbia mkono wa polisi kwa kile alichokitenda aliamua atokoke
mjini Tandika akapanda basi lililoelekea mjini sangura.

Basi lilianza safari na Akida alitaka likimbie mwendo wa kasi ili


asisikwe na polisi. Njiani walikuta kisa cha wanafunzi wa chuo cha
Tandika waliogoma kwa sababu ya polisi kumwua mwenzao bila
sababu wakaweka mawe barabarani na kuvunjavunja vioo vya
nyumba jirani na chuo.

Basi liliendelea hadi wakati wa machweo lilipofika kituo cha biashara


cha Binge AKida alishuka ingawa hakujibu sehemu hiyo.

Sura ya kumi na saba (144- 151) Kituo cha Binge

Asubuhi mapema maduka yalikuwa hayajafunguliwa lakini watu


walikuwa wamepiga foleni washindania bidhaa ambazoni haba sana.
Akida aliingia mkahawa mmoja na kunywa chai.

Alipozungumza na muhudumu kuhusu wapi angeweza kupata kazi ya


shamba, mhudumu alimwambia kwa mzee Kijoka na kwa mzee
Muyaka. Akida alisita kwenda kwa Muyaka kwa kuwa walimwambia
alikuwa mkali vile alikuwa mwana jeshi aliyepigana katika vita vya pili
vya dunia.

12 | P a g e
MWALIMU FAGILI FARAJA MONDE 0780947386/0785090252/0756040644

Akida alielekezwa na muudumu wa hoteli njia ya kumfikisha kwa


mzee Muyaka. Alipofika kwa Muyaka walikubaliana kumlipa shilingi
mia tatu kila mwezi na kutambulishwa kawa Bi.Tina mkewe Muyaka.
Alipoulizwa kabila lake na Bi. Tina, alimdanga kuwa ni wa kabila la
wachungwachungwa.

Jioni Akida aliona haya alipomwona msichana alimfumania kule


mkahawani akikojoa asubuhi. Msichana huyu alikuwa bintiye
Muyaka aitwaye Cynthia.

Sura ya kumi na nane (152-159) Kwa mzee Muyaka

Akida alifanya kila aina ya kazi hadi Bi.Tina kamwambia “Lo!


Unabidii kama ya mchwa Madodo.” Tulielezwa juu ya Jerumani
mtoto wa kiume wa mzee Muyaka aliyerukwa akili kwa
kuwachungulia wanawake wakikeketwa. Jina lake Johnson lakini
kapewa Jina la Jerumani kwa sababu ya kuzungumza Kijerumani.
Alikuwa amesomea Ujerumani uhandisi katika chuo kikuu cha koln
akifadhiliwa na serikali ya Ujerumani. Alifukuzwa kabla hajamaliza
chuo kwa kuwapiga kwa mtalimbo skin heads waliomshambulia
mwanamke mweusi. Uk 155.

Kazi kuu ya Jerumani ilikuwa kuchota maji kwa kutumia mkokoteni


na kuwauzia watu wa Binge. Alipenda sana kushangilia mpirakiasi
cha kwamba timu yake ikifunga alikimbia uchi kwa kufaraha.

Jerumani na Akida hawakuishi kuchokozana lakini kila mtu alielewa


shida za mwenzake. Jerumani alimletea akida Jarida akikusudia
kumjulisha zaidi kuhusu taarifa ya vita vya ukabila nchini
kiwachema.

Sura ya kumi na Tisa (160-168) kwa Mzee Muyaka

Akida alisoma jarida alilopewa na Jerumani ambalo lilikuwa na ukweli


kuhusus vita vya korosho. Jarida lilionyesha kuwa mbunge Johnstone
Mabende na wakuu wa dini walikuwa na mkono mkubwa katika
kuchochea vita hivyo. Jarida hili lilichapiswa kisirisiri na kusambazwa
nchi kiwachema.
Jerumain alimaliza siku nyingi bila kuonekana. Bi-Tina kamtuma
Akida akamjulie hali. Akida mnyonge kavalia kaptura kwasababu ‘
mwuaji kapewa kazi ya kulinda uhai wa akimrejelea Johnstone
mabende aluyepewa uwawa wa usalama wa ndani uk 162 – 163

13 | P a g e
MWALIMU FAGILI FARAJA MONDE 0780947386/0785090252/0756040644

Tim alipolezwa hali ya mwanawezi ahamua ambetee nyumban


akae naye amuguze mpaka apate nafu. Ilichukuwa muda wawiki mbili
kupona. Alimwambia Akida kuwa angetoroka kwao asirudi tena kwa
sababu baba alikuwa hampiendi. Asubuhi moja akida hakumikula
kitandanda kwa kuwa walilala pamo. Walimusajalia kila mahali bila
kumwona. kupotea kwa Jerumani kuhamba tana na kupotea kwa
bunduki ya mzee muyaka.
Habari ya kupotea kwa bunduki ya mzee muyaka kisambaa
kote. Na askari polisi walinyosikia hivyo walikuja kwake wakamhoji
baada ya mahojiano walienda naye. Ngulu za mama cinthia kuwaomba
polisi wamwache bamkubwa ziligonga mwamba.
Bi – Tina ahuza fahari moja akawaliouga polisi mzee muyaka
akaacheluwa.

Sura ya Ishirini (169 – 173)


Jeruma alikuwa anesahalika kwa mezi mingi.
Akida anatuweheza kuwa hakuweza kumchezea cinthia kama
aliuyoonywa na mwajiri wake. mwanzoni. Lakini alikuja kunasa rafikiye
suzana aliyependa sana kumtembelea cynthia. Baada ya masomo
suzana kaobe wa na Joseph juran wa muyaka.
Msimu wa tohara ulijiri na bibi ye cynthia alikuya kwa muyaka kwa
ajili luyiya kutaka atahirirwe cynthia, jarubo ambalo mamake alipinga.
wakati wa usiku Bi.Tina ahfanya njama na Akida akamtorosha hadi
jijmin.
Baraki kwa kambi la waliogopa kusu cha ngarike wakati huo kuna
msichana aliyekufa kwa kuishiwa damu. Wengive walipehe kwa
hospitalim.
Akida pia alutueleza kuhusu habari iliyotolewa na redio ya mzee
muyaka kuwa waziri Johnstone mabende kawewa na mtu
asiyejulikana.

Sura ya Ishirini na moja. (174 – 181)


Shuguhiza Matayarisho ya sherehe ya pesi ya Nana ndiyo ilitawala kila
mtu nyumba kwa muyaka isipokuwa muyaka mwenyewe. Bi – Tina
alikuwa na kundi la wanawake tayari kwa sherehe nyumbani akivemo
mkwe. Akida alimenyana na shuguli la kuchumba mashimo ya kuweka
migomba ili kuogezea heba sherehe, baadaye alishngulika na
kumchinja mbuzi mzee muyaka alionekana hajali chochote ila kainama
tu anatia nakshi bakora yake.

14 | P a g e
MWALIMU FAGILI FARAJA MONDE 0780947386/0785090252/0756040644

Baadaye mzee muyaka kaletewa barua na mtoto wa jirani


akapokea na kutoipa muda. Baada ya shughuli za matayarisho kuisha
mzee muyaka kaagiza aletewe miwani yake ili asome barua hiyo na kwa
bahati mbaya haikupatikana.
Bi-Tina alitembea kijiji kiziuma akumtafuta atakaye wasomea barua
akamkosa mwishome alimlieta susana acliyeishia darasa la cha sita na
huyu hakuweza kuisoma kwa kusingia kuwa ukuwa na mwandiko wa
kukoroga.
Mwishowe Akida aliyitolea kuwasaidia kuisoma ingawa wao
hawakuamini anawe kusoma. Ahsoma bila kusila. Na barua yenyeule
ilitoka kwa nana ikiwaarifu kutotayarisha chochote kwa kuwa shevehe
ilikuwa imesimamishwa uk179.
Walipomaliza kusoma barua liyo, kila mtu aliduwa.
Akida alilipwa pesa zake na mzee muyaka kama walinyokubaliana
kuwa baada ya sherehe angeenda zake. Akida aliondoka ukisi kwelekea
kituo cha diashara cha binge kungoja basi.

Sura ya ishirini na mbili (182 – 193)


Akida kapanda basi na kuelekea mjin tandika. Alipofika, kil akitu
kimebadilika na kudidimika, njia zina mashimo, taa zaturafiki
hazifanyi, ombaomba uregi barabarani, mamalaya wanapigania
wanaume, wapiga kibari wamezidi mwenyewe kaibiwa pesa alizokuwa
nazo. Anafikiri njia nyingi za kujitoa uhai lakini zote hakuweze kana.
Akida alijipeleka kwa kituo cha polisi akajistaki kwa kumwua
mtu. katika koseli alimkuta kasisi John miongoni mwa watulumiwa. Na
wakosaji wa kila aina walikuwa huko.
Wafungwa walihetwa mahakani kustakuwa mara ya kwanza
kasisi John kasomewa mashtaka ya kutumia wasuhana nane ktk mtaa
wa maria nasambu kabla hawajafikisha miaka kumi na minne.
Akida naye alisomowa mastaka yake uk 191 lakini ushaludi ulionyesha
kuwa mzee zado na kafaa kwa kujitia kitanzi. Halafu alifugulia mastala
myungi ya Tito tembo ambaye alipigwa kubao kupan na mtu
asujiejulikan. Akida alikubali makosa yake lakin hakufungwa
kasamehew.

Alipotoka njee ya mahakama alisiikia mtu akitaja jina lake, mtu huyo
hakuwa mwingine bali Tim rafikiye 193.
Sura ya Ishirini na tatu (194 – 207)

15 | P a g e
MWALIMU FAGILI FARAJA MONDE 0780947386/0785090252/0756040644

Tim na Akida waliandamana hadi falkland ahtoshi tim katika chumba


kile. Tamari alikuwa amerenda shulen na chumbani kwa Tim kulikuwa
na maendeleo kuliko wakati ule. Tim alikuwa amepata kazi kule
Amken.
Akida ahmwuliza habari zababake mzee suhulu lankum Tim
hakumjibu chochole Bali alimwelezea kuhusu babake mzee zaplon
mapishi aliye kijitia kitanzi chumbani alimoishi kwa mjombake Tim
huko mtaa wa mlima 197. pia lunaambiwa kuhusu kifo nya mamake
na wadogo zake Tim ambao wahagamia vitam pia.
Akida alipewa baria aliyoandiika mzee zablion kabla ya kiyilia 198
Tim anaeleza kuwa alifukuswa kamsan na kasisi jolua kwa kumstaki
David aliyemko pa pesa zake. pia alielezea kuwa kasisi John
alumchongea/kumsemea vibaya kwa pam mpenzi wake akambetea
kumwacha uk 199.
Muda huo tamari alitoka shuleni akawakuta watu kiamboni
waneshrika bunduki, panga na mashoka. Tim alienda akazugumzao
wakamwambia walimfafuta mkanju alugeachihiwa siku hiyo
makakamani. Kusikia hayo Akida alitaka dunia immeze ila tamari
alimpa nguo zake (gani) akavaa na viatu ili asitambulike na njia hiyo
ilifaulu kwa kuwa wasakaji walipoingia hakuweza kumtambua
walidhani ni msichana dadake Tim 204 – 205.
Wasaji walipotka, waliamua Akida atolewe kwa Tim kwa usalama wa
kula mtu hapo kwa Tim na mtaa mzima wa falkdad alipehekwa kwa
mtaa wa mama nasambu kwa shangazi yake pam 206 – 207.

Sura ya ishirini na nne (208 – 213)


Wakati wa saa nne usika walifika kwa shangazi yake Pamela,
walifunguliwa lakini Tim hakungiza alibaki njee ya lango. Pamela
alishanganga kumwona nsuhana alijekuwa na santi ya kuume
akijitambulisha kama amta. Waheheka baadaye Tamari akanuelezea
yoke yaluyotokea 209.
Baada ya kupata kinywaji tamari alisindikizwa hadi langoni na pani
lakini Tim hakuongean naye. Shangaza yake pana alikuwa na zamu ya
usiku siku hiyo.
Pam na Akida walizungunza mengi kuhusu mapenzi yake na Tim
pan alyanbu kuelezea kuwa Tim kamtupilia mbali kama jongoo la mti
na Akida alimwambia kuwa Tim naye anasema vilevile. Pan pia alisema
kuwa shangazi yake alikataa ndoa yake na Tim kwa kusema kuwa
nimkoroso, wakoroso washamba, yeye ni fukara UK 212.

16 | P a g e
MWALIMU FAGILI FARAJA MONDE 0780947386/0785090252/0756040644

Sura ya ishirini na fano (214 – 222)


Asubuhi shagani yake pam alirudi kutoka kazini alipomkuta Akida
alimfukuza moja kwa moja. Pan alimwomba toili mlinzi wa mlango
aende naye kwake. Toli alikubali kisha wakaondoka pamoja na Akida
hadi mtaa wa tiwani. Nchumba cha mlinzi kilikuwa kimoja na paa la
bati ulikuwa na mafundu. Ndain walikilibishwa na kunguni, wende nk.
Toili alienda kwa kibarua cha kutwa cha kupakia mchanga ili apate cha
kilisha fanuha yake kubwa (wake wawili na watoto II)
Tim, pam, na Taman walimtambetea Akida kwa Toili na habari
nzuri waliyo mletea ni ya kuwa. Tom alikuwa amautafuta tangu
alipoondo jiji Tandika. Tim alipomwambia hali anaipitia Akida wakati
huo aliahidi kutumia pesa za tiketi ili aende canada kwa ajili ya
usalama wake.UK. 217 – 219.
Akida alipokuwa anasikiliza pedio sauti ya kiwachem utangaza
kumawa kwa Tume la haki ili kafufua waliouawa vitamin pia ilitangaza
kuhusus uchuguli wa kufo cha Johnstone mabende waziri wa usalama
wa Ndain kuwa kauwa na Johnson muyaka kwa bundu ki aliyoba
kutoka kwa babake. mwuaji huyo alikuwa anasakwa UK.121.
Rwaya maisha Akida akisindiikizwa hadi uwanya wa ndege na kuenda
Ontario canadas kwa kutumia ndege ya British airways UK.222.

TAMATHALI ZA SEMI KATIKA RIWAYA YA KUFA KUZIKANA

Mwandishi wa riwaya hii ametumia mbinu chungu nzima


kuwashilisha ujumbe wake kama zilivyoorodheshwa hapo chini.

1. Tashibihi
 Najihisi kama zumbukuku
 Najihisi kama samaki kwenye nchi kavu
 Vimepigwa pasi vikapigika kama sare ya askari polisi –Tim12
 Mwanafalsa amwagaye semi za hekima kama mhenga.17
 Walinyakuwarundo la mageti kwa kasi kama umeme.
 Nilikuwa kama nzi aliyenaswa kwenye utata wa utanda bui.
 Mwaka wa sita napuhekwa huku na huku kama mpira
uwanjani.
 Kainama kama kondoo 51 .
 Wakanju ni kama lila nafila hawa tangamani.
 Kingeleraza kinamtoka kama bomba la mafi 71.

17 | P a g e
MWALIMU FAGILI FARAJA MONDE 0780947386/0785090252/0756040644

 Zime bambuka rangi na kuacha mapakupaku mithiliya ngozi


ya chui 72.
 Aliyekataa katakata 74.
 Kasimama kama nguzo ya umeme 89.
 Mvua iliendelea kuaguka mithili ya mvua ya siku za nuhu 104.

2. Nahau
 Ghafla bini vuu 14.
 Tulipo piga hamadi 20.
 Miguu yangu ikafa ganzi 22.
 Nita shida huko ili nisimwage unga 27.
 Nili keti sako kwa bako
 Alitupokea kwa mawili matatu.
 Tulisalimu amri 89
 Alikua ameteremusha zipu 110.
 Maji yamezidi unga
 Wakanju walikula kalenda bure 138
 Funga breki 144.
3. Methali
 Mtoto wa panya hakosi mkia 12.
 Kipya kinyemi kingawa kidonda 13.
 Kusikia si kuona, tuone ndipo tuambe 14.
 Kukopa harusi kulipa matanga 14.
 Chako hakinuki ngawa kimeoza 24.
 Pavumapo palilie sikazi kudamirika 29.
 Hayawi hayawi huwa 30.
 Kupotea njia ndiko kujua 32.
 Mwenye macho haambiwi tazama
 Chakala simba halilali nguruwe 33.
 Mshoni hachagui nguo.
 Penye nia pana njia 53.
 Mtengo bila chambo haunasi 73.
 Dau la mnyonge haliendi joshi 124.
 Hasira ni hasara 182.
 Yaliopita si ndwele tugange yajayo 196.
 Dawa ya moto ni moto
4. Utohozi
Lori 10, friji 14, breki 17, choo cha flashi 18, shesi ya mkate 19,
swichi 19, fremu 19, magari leni tatu 22, soksi 23 kochi (kiti) 23

18 | P a g e
MWALIMU FAGILI FARAJA MONDE 0780947386/0785090252/0756040644

glasi 25 propaganda tupu 29, jaketi 31 kamera sampuli, flashi


48. Kondakta 57 sachi 70 aproni 81 plastiki soseji 97, klabu
132, paspoti 217, tiketi 2017.
5. Kuchanganya ndimi
 Chips,  Mortuary 27  Hot dogs 97
sausage 12  Process 45  Boss 103
 Red plum 19  TV crew  Honey 86
 Anyway 2  Shut up 61  Kashopping
 War and  Please Akida center 94
peace 23 take it easy
 Come in 23 70
 Seriously 26  Sweetie 132
6. Chuku
 Lakini masomo alikuwa mbumbumbu hawezi kuunga moja na
moja akapata mbili.
 Akipita mawimbi hujitenga (mjombake Tim)
 Ukimwona unashikwa na homa au kigugumizi (Pamela)
7. Tanakali sauti
 Kuenda kujiputeka pwata 28.
 Mara waa picha, ikajitoeza.
 Tapu !tapu ! migongo ya tapureta 41.
 Lilioninyororo nyororo.
 Moyo wanidunda dududu 63.
 Kuchechea checheche
 Kupapapatika papatupapatu
 Tak ! tik ! tak ! tik ! ya saa 69
 Nilisismama bwe-bwe 81.
 Nililia wee ! 89.
 Nikajipweteke pwata 89
 Nilikimbia chapuchapu.
8. Misemo
 Ngamia wa jageani akipatamaji hunjwa kupudukia 20
 Sahani zikiwa kwenye tuyahaziachi kugongana 30
 Bibilia yasema aduimpende
 Vita havina macho 123
 Umechechewa chehewa ukakuta mwana si wako.
 Kufanya kosa si kosa, kosa ni kumidia
 Changu kilichopika mboga kalihakiachi kuwa na ukah 142
9. Nidaa

19 | P a g e
MWALIMU FAGILI FARAJA MONDE 0780947386/0785090252/0756040644

 Eeh ! kuona mungu 102.


 Hahaula ! ladha nzuri ajabu !13
 Ahaa mbona nasahau 15.
 Oooh ! 16 lo !
 Lo ! Tim kachunuka 25
 Aah ! ngoja nikwambie, lahaula 152
 Lo ! nasi hatukuyatazama magazati leo ! 28.
 Al ! pam ! 35, ooh masinkini pole Akida 35
 Alaah !35, Lo ! masalale, 137
10. Nyimbo
 Akida kwa Tim na Pam 38.
 Wimbo wa mzee uredi hosipitalini.
 Tamari kwa Akida mapenzi

11. Barua
 Barua ya Nana kwa 38.

12. Shairi
 Mzee sululu kwa Akida juu ya hasira 42
 Sululu Akida (hasira) 64
13. Jarida
Jerumani. Akida 160

14. Ndoto
Akida-Tamari
15. Uzungumzaji nafsi
16. Hadithi ndani ya hadithi
17. Mbinu rejeshi

SEHEMU MBALI MBALI RIWAYANI

Mumbaimbai – shule alikosomea Taari mjini.

Baraki – Kijiji walikozaliwa A kida,Tim, Tamali

Tandika – mjiji mkuu wa kiwachema

Shauri moyo – Alikoishu Tim mara ya kwanza.

20 | P a g e
MWALIMU FAGILI FARAJA MONDE 0780947386/0785090252/0756040644

Mtaa wa mama nasamba. Alikoishi shangazi yake pam

Mtaa wa mlimani

Mtaa wa

Falkbandi – Mtaa wa kimaskin alikoishi timu

Binge – kitana cha biashara huko sangura

Sangura – kwa mzee muyaka na kwao pam

Nduchi – Hospitali ya kijijini.

Rufaa – Hospitali ya mjini Tandika.

21 | P a g e

You might also like