Roughly Nakala

You might also like

Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 7

Mwaka 1961 Rais Kenedy wa marekani bila kiwashirikisha NASA alizungunza mbele ya KADAMNASI kuwa

miaka kumi kutoka mwaka huo wa 1961 marekani itapelekea nakumrejesha binadamu mwezini mwa
mafanikio.

Kiongozi wa NASA alivo ona hiyo habari alishtuka na alituma ujumbe ikulu ya white house na kumjulisha
raisi kuwa hiyo kitu aiwezekani.. Ikulu ya white house ilirejesha majibu mafupi sana kuwa hakuna
kisichowezekana. (nothing is impossible).

Anyway… Hivi.. Ushaga wahi kutana na wale watu wanaoshindaga kila kitu, unajua kwa upande
mwingine hawo watu ni failures.

Ni failures kwasababu katika mapambano yao wamechagua game rahisi (comfortability). Mara nyingi
ukichagua game rahisi ushindi ni lazima tofauti na wale walio chagua game ngumu.

Mtaalam mmoja anasema, Watu wengi walishaga kufa wakiwa na miaka 25 ila wanakuja kuzikwa
wakiwa na miaka 80.

Kinachosababish hayo yote ni kitu kinacho itwa comfortability, ni adui mkubwa sana wa kusonga mbele,
comfortability imesababisha watu wengi sana kufa na kuzikwa na uwezo wao mkubwa. (huenda
wangejaribu kufanya kitu wange leta mageuzi duniani)

Nmejaribu kufwatilia baadhi ya maeneo mengi Tanzania kila Kijana (sio wote) anatafuta kazi
(serikalini)!.. Ukifwatilia anachokitaka hasa ni ile comfortability ya ajira ya kusubiria mshahara na posho
za kazini na kuiba iba viela vya serikali (kwa kuandaa ripoti za uongo)

Sikatai na nakubali kweli kuwa asili ya binadamu ni kutotaka shida, akili ya binadamu inachotaka ni
comfortability! Na ukitaka ku enfluence jambo lako kwa watu basi tengeneza kitu kinaichoitwa
comfortability ambayo inaweza kutengenezwa kwa kusababisha kitu kinachoitwa Fair of Missing Out
(FoMO) na ukitaka kuwamaliza kabisa ongezea na kitu kinaitwa Possibility of Gain (PoG) ndio
makampuni ya betting wamwezaa hii sana na ndio maana vijana kwa wazee wengi wana amua ku beti
tu. 😂
Na kwa uwoga walio nao, wako tayari kufanya yote (kuacha kujaribu kitu kipya) ili walinde kile kidogo
walichonacho maana wanahisi kitawaponyoka.

Vile vile watu wengi wanafanya kazi wasio ipenda kwasababu tu wanaogopa kuacha wakihofia wakiacha
watalipaje bills na kodi za kuendesha maisha.

Lakini ukweli ni kwamba acha kidogo mungu akupe kikubwa, ukiendelea kushkilia icho kidogo muda wa
kufikiria na kutafuta kikubwa hautokuwa nao.

Kuogopa ku-take risk ndio tatizo, usichokijua ni kwamba, maisha yote ya binadamu yametawaliwa na
risk tupu…

Kwanzia mimba yako ilivotungwa tumboni mwa mama yako ni risk.. Kitendo cha kuzaliwa tu na kupita
kwenye uchi wa mama yako au kwa hata kama umetoka kwa upasuaji ni risk nyingine kubwa tu…

Kuzaliwa Afrika Mashariki haswa Tanzania na kushinda majanga yote ya asili kama maleria na maradhi
ya utotoni na mengine nayo ni risk kubwa tu..

Kwa kifupi ni kwamba risk ni sehemu ya ubinaadamu na alituumba ametukadiria na inatupaswa upitie
changamoto kama sehemu ya kutukomaza, mwili na akili ya binadamu haijaummbwa kuishi kwenye
comfortability.

Kwa mujibu wa historia ya manabii kadhaa wa mashariki ya kati wakiwemo akina Mussa, Issa (Yesu) na
Muhammadi…. Ukiacha mambo mambo mengine yenye manufaa kwa hawa manabii.. Nmegundua wote
wana sifa moja kuu yenye mafunzo makubwa mno kwa kila mwenye mazingatio… mwanzoni
hawakueleweka kwa ndugu zao au watu wao wa karibu…kitu kilicho walazimu kuhama na kwenda
kujipanga nje ya miji waliozaliwa.

Na mara baada ya kuhama na kwenda nje ya miji waliozaliwa hakika waliofanikiwa na walijipanga vema
zaidi ikiwemo kupata nafasi ya kusikiliza na kuweka zaidi pamoja na kupata wafuasi wa kweli.
Nini maana yake.? Maana yake ni kwamba nyumbani sio sehemu ya kuanza, kwani utankuta a na
vikwazo lukuki. Na utalazimika kukata tamaa tu.

Na maadui wa kwanza wanaotoka nyumbani kwako.. Huwa nasema adui wa kwanza na anaesababisha
ubakie maskini ni baba na mama yako (tulia ntakupa sababu kuu tatu).

Sababu Ya Kwanza… Wazazi wako hawapendi kuona unateseka, hivyo watafanya kila wawezalo ili
usipate shida, ikiwemo kukutaftia na kukuangaikia usiku na mchana bila kuchoka.. (Hapo ndipo shida
inaanza)

Akili ya binadamu haijaumbwa kutaftiwa wala kuhangaikiwa! Imeumbwa kujihangaisha na ikijiangaisha


ndipo I aongeze ka na kutanuka zaidi. Kitendo cha wazazi wako kukuangaikia na kukutaftia ndio mwanzo
wa wewe kuendelea kuishi kwenye comfortability na mwisho wa comfortablility huwa ni umaskini.

Sababu Ya pili… Wazazi wako hawawezi kuvumilia kuona ukiwa mjasiriamali unaeza kupambania kitu
kutoka mavumbini (from the bottom) wataishia kukutaftia au kukusisitiza utafte au kuomba kazi
serikalini au katika mashirika mengine. Ujasiriamali ni mgumu, inahitaji commitment ya hali ya juu..
Watakuzuia kujipambania na watakuina mwana mpotevu.

Sababu ya tatu.. Wazazi wetu bado wana imani za Kizamani ambazo haziwezi kukusaidia wewe kijana wa
kisasa na wa karne hii.. (elewa hii kijana wangu)

Iko hivi… Wazazi wako wamezaliwa miaka ya 1960s au hata 1970s na katika kukua kwao wamelelewa na
kuona watu wakifanikiwa kupitia kilimo na ufugaji.. (sio mbaya) lakini pia wao wamekuwa wakiamini na
kuona watu waliosoma angalau hadi hata astashahada wamekuwa na ajira na wana mshahara na
wanaendesha maisha yao.. (kwao wanaona ndio mafanikio) Okay.. Shida inakuja sasa hivi mambo
yashabadilika na wao bado wana imani hiyo.. Mishahara haipandi, sarafu inashuka kila leo mafuta
yanaoanda mara 10 ndani ya mwaka mmoja wakati mshahara hata mara moja haujapanda na ikipamda
nyomgeza ni shilingi elfu 12 😂
Mlezi wangu mmoja alifwata siku moja na kuniambia ninapopata pesa ninunue Ngombe na mbuzi na
akanisisitiza kuwa baada ya muda nitakua tajiri.. Wakati huo huo sehemu kubwa ya maeneo inakuwa na
kugeuka miji na serikali nayo imeanza kumwaga watu wake kukagua maporini yote na kuyalinda na
kuzuia shughuli zote za kibinadamu na na waona wafugaji na mifugo yao wanavo angaika usiku na
mchana kutafuta malisho. Pesa ya kununulia mifugo si bora nkanunua Bitcoin au Solana nka hold kwa
miaka kadhaa😂(kijana wa kisasa)

Skia.. Amna wazo linalokuja likiwa imekamilika, wazo linajitengeneza vema kadri utakavokuwa unaanza
na kuendelea, kunachotakiwa ni wewe kuanza. Anza kidogo kwa ulichinacho na ujiseti mbele kwa mbele.

Kwa wasio jua makampuni yote maarufu na yenye mafanikio kama Apple, Sumsung, Amazon, Tesla,
Google na mengineyo hapo awali yalikuwa na bidhaa na huduma tofauti kabisa na wanayo fanya kwa
sasahivi.

Kijana… Kuwa tofauti na wengine.. Acha kupoteza muda kuangalia kutafta kazi… maisha ni kama bufee….
Raha ya bufee ni wewe kujipakulia… Nyanyuka na uchukue sahani na uanze kujipakulia mwenyewe
chakula unachopenda na unachotaka, ukingojea mtu akukuchukulie ujue hatakuletea wala kukukadiria
unachopenda na kukiotaka kwa wakati huo.

Binafsi toka day one.. Katika maisha yangu hakuna kitu kiliniboa mno kama ajira, maisha ni mfupi sana
kuanza maswala ya kuwajibika kwa mtu au taasisi na kupelekeshwa…

Ajira ilisababisha nikae mbali na familia yangu kwa miaka kadhaa, ilifanya nisishuhudie tukio muhimu la
kuzaliwa kwa mtoto wangu wa pili, Sio hayo tu, ajira ilisababisha binti yangu wa kwanza awe
anaombewa kukaa kwa watu (majirani) pale mke wangu anapo lazimika kwenda hosipitalini (kwani
mtoto wa pili alikua na changamoto ya kiafya yanayo lazimasha afanywiwe checkups za mara kwa mara
ikiwemo kulazwa hospital ya rufaa.

Ajira Ilisababisha ipite miezi 4 bila kumuona mtoto wangu wa pili toka azaliwe, ilisababisha nikashindwa
kusimamia matibabu ya mwanangu na ikapelekea kifo chake akiwa bado mdogo kabisa wa miezi minne.
(Huenda ningekuwepo ningetoa wazo na kupendeeza vitu flani vyenye tija)
Ajira ilisababisha nipe kiapo… NaNa kujisema yafwatayo.. fanye nifanyalo! Ajira kwangu ni kitu cha
kupambania Nikiacha mapema zaidi iwezakanavyo, na kosa muda wa kuwa karibu na watoto wangu
pamoja na mke wangu

Njia pekee ya mimi kweza kufrahia na kuwa karibu nao ni kujifunza na kuwa trader! Kupitia trading
nitakuwa huru kufanya kazi zangu nyumbani muda ninao utakaa na kuwa mbele ya wanangu na mke
wangu.

Pia ntapata kipato rasmi na nitakua huru kuishi mji wowote ninao upenda, pia nitakua na wasaa wa
kusafiri mimi pamoja na familia yangu wakati wowote ninaotaka bila usumbufu na bila kupangiwa wala
kusumbuliwa na mtu yeyote.

Nmegundua trading ndio kazi pekee yenye kunifaa, na napaswa kujifunza usiku na mchana na ndani ya
miezi 6 niwe nimefanikiwa kuingiza faida inayotosha kuendesha familia na kulipa bills zote.

Safari ya trading ilianza rasmi mwezi wa November 2021. Lakini rasmi na kuanza kuwa seriaz ilikua ni
November 2023, Ambapo nilimtumia muda wa kama mwezi mmoja kusoma vitabu na kuangalia video za
trading mitandaoni (YouTube na instagram)

Baadaye nikafungua akounti kwa broker xm global limited (kwa sababu ana kubali mobile payment kama
Airtel Money na Tigopesa)

Kitu Kilichokuwa kina nipa tabu ni kuunga MT5 na acount ya broker lakini kupitia YouTube niloweza na
ikawa ni rahisi tu.

Ilianza kutumia demo na baada ya 2iki moja tu ni kaamua ku deposit dola 19.88 baada ya kuona
umeingia na kupokelewa fasta tu Nika ongeza dola 59.88 ndipo nikaanza ku trade..

Sio Muda ni kapoteza pesa yote, (ndani ya sku tatu tu) nkaona niongezee tena dola 59.88 ambapo
nilijitahidi (kuotea) nikapamdisha hadi dola 134 na nkajiona trader sasa(😂😂) nakumbuka nlitoa dolla 14
mbele ya washkaji uku nikiwatambia kuwa mi ni nafanyaga ishu za mtandaoni na zinaniingizia pesa.
Kesho yake nilivo amka Nika ingia ku trade kichwa kichwa.. Mbona ndani ya dakika 180 tu nishapoteza
izo dola 120 zilizobakia. 😂

Nkasema hata hapana.. Ngoja niwekee na nyingine ili nifukuzane na soko nirejeshe faida.. Kilichotokea
sasa.. Nakumbuka ilikua ni GOLD (XAUUSD) Ilipofika sa 10. Jioni ambapo soko la New York hufunguliwa..
Candle moja tu ilipanda na kushuka ndani ya sekunde moja ikanitoa nje na nikaunguza tena akount.
(nlikua siwekagi stop loss wala take profit nategemea nirukie kukata ikifika nibakotaka ifike😂)

Aijatosha… akili ikaniambia hapana.. Jaribu tena.. Nikaongeza dola 19… Na badae tena….

Okay.. Usichokijua ni kwamba, kila unapo amua kujiingiza na kufanya trading ni wazi kwamba umeamua
ku take risk, point ni kwamba, unatakiwa kuwa na management nzuri dhidi ya riks.

Skia… Wanasiasa na mabosi zako a Watakufanyia uwe tajiri, zaidi sana watakutumia kuingiza pesa na
kisha watakulipa sehemu ya faida kidogo tu ili usife 😂

Aijalishi unafanya kazi serikali au taasisi binafsi.. Kamwe utaishia kupata pesa kidogo ya kulipa bills na
kuendesha familia yako ya mke na watoto (awazidi wanne) kisha baadae unazeeka na ukisha kuwa
umefikia Miaka 60 awatakuhitaji tena.

Acha kuangaika na maneno pamoja na ahadi za wanasiasa na viongozi wa makampuni.. Izo ni speeches
na stori zao zimejaa unafkiri mno.. Aina utekelezaji zaidi ya ahadi za kumpa moyo mpuuzi ili aendelee
kujiona anako elekea ni kuzuri.

Kwa mujibu wa wanahistoria! Dola ya kirumi ilianguka mnamo mwaka 476 BC.,Lakini warumi wenyewe
ikiwa Chukua karne nyingi hadi kuja kuamini na kukubali rasmi kuwa walisha angushwa na sio wata wala
tena.

Nini maana yake?.. Maana yake ni kuwa ifike mahali ukubali na ujue kuwa umeshindwa au hujui. Hii
itakusaidia kuangalia namna ya kuanza upya na kujipambania tena…
Lengo la maisha haya ni uhuru (freedom), wala sio pesa na utajiri… Sema ni ile basi tu ujaelewa
dhumunila maisha.

Hakuna raha ya maisha zaidi ya kuamua kufanya au kutofanya utakacho wakati utakao na kwa watu
utakao.

Imagine. Uweza kuamua kusafiri nchi upendavyo ukiwa na uwapendao kwa wakati upendao.

You might also like