Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 38

KUHESHIMU HITILAFU ZA

WANACHUONI

NA

JITIHADA ZAO

ABDULQADIR MUHAMMAD AL-AHDAL

30/04/2023 Ce - 10/Shawwal/1445 Ah

Dar Es Salaam – Tanzania

YALIYOMO
1. Shukrani
2. Neno la wafasiri
3. Dibaji
4. Kujipamba na adabu za kuhitilafiana na kuvumiliana katika
jitihada za wanachuoni
5. Mazingatio katika maneno ya wanachuoni wakubwa.
6. Haifai 'kumkhalifu' imamu kwenye swala katika masuala ya
jitihada baina ya wanachuoni
7. Haifai kulazimishana misimamo katika mambo ya jitihada
8. Mambo wanayohitilafiana wanachuoni
 Kusoma bismillah katika swala
 Kusoma kunuti katika swala ya alfajiri
 Kumfuata imamu katika kunuti
 Kutikisa kidole katika Tahiyyatu
 Kunyanyua mikono wakati wa kusoma dua.
 Kusoma dua baada ya swala za faradhi
 Hukumu ya kupangusa uso kwa mikono baada ya dua
9. Hitimisho
10. Rejea

1
SHUKRANI
Bismillah Rahmaan Rahiim

Kwanza kabisa namshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma


mwenye kurehemu. Mjuzi wa mambo yote ya siri na ya dhahiri.
Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kuandika risala fupi
kuhusu adabu za hitilafu na kutafsiriwa risala hii na wanafunzi wangu
wapendwa niliowapa jukumu la kufanya kazi hiyo kutafsiri kuandika na
kuhariri. Namuomba Allah mtukufu aijalie kazi yangu hii iwe ni kwa ajili
ya kutaraji malipo kwake na iwe ni sadaka yenye kuendelea kwa wazazi
wangu.
Aidha nitumie fursa hii kuwashukuru kwa dhati kabisa na kipekee
wanafunzi wangu walio fanya kazi ya kufasiri kuandika na kuhariri
kitabu hiki ambao ni
*Wachapaji*
1) Amry Ally Shambula
2) Ibrahiim Juma Isingo
*Wafasiri*
1. Abdillah Masawe.
2. Bashiri Shabani Dule
*Wahakiki*
1. Shaaban Ibrahim
2. Wenge Mohamadi Wenge
3. Maulid Hussen Maulid
Nakiri kwamba wamefanya kazi yao hii kwa moyo wa kujituma na
umakini, namuomba Allah mtukufu aifanye kazi yao hii iwe ni kwa ajili
ya kutaka radhi zake na awalipe malipo yasiyo kifani.

Bila kumsahau kwa juhudi za kipekee ndugu Hamisi Kibali ambaye


amekuwa na mchango wake muhimu wa uhariri katika kazi hii,
wakiwemo na wengine wengi walioshiriki kwa namna moja au nyingine
kufanikisha kazi hii, Allah awalipe kheri na baraka tele.

Pia namshukuru kila msomaji wa kitabu hiki naye namuombea kwa


Allah amhifadhi na kila shari na ampe kila la kheri.

Wabillah taufiiq

Sheikh Abdulqadir Muhammad Ibn Ahmed Al -Ahdal .


Dar Es Salaam Tanzania Tarehe 02/ 04/ Jumaadal Aakhiri 1445 Hijiria - 17 /10/2023

2
NENO LA WAFASIRI
Bismillah Rahman Rahiim
Sifa zote njema anastahiki Allah mtukufu mwingi wa rehema na
tunamtakia Rehma na Amani Mtume wetu Muhammadi

Kitabu hiki cha kiswahili ni zao maswali mbalimbali ambayo Sheikh


wetu Abdulqadir Al-ahdal huwa anayajibu kwa lugha ya kiarabu, na
kutupa jukumu na idhini ya kukitafsiri kwa lugha ya kiswahili na
kukiita “KUHESHIMU HITILAFU ZA WANACHUONI NA JITIHADA ZAO” .

Tukiri kuwa jukumu tulilopewa na Sheikh wetu mpendwa halikuwa ni


jepesi kwasababu ni kazi inayohitaji umakini wa hali ya juu ili
kufanikisha hilo, lakini tulilipokea sote kwa pamoja na kuitekeleza kama
ilivyoelekezwa na Sheikh wetu.

Ifahamike kuwa, kupewa jukumu hili sisi baadhi ya wanafunzi wa


Sheikh kinyume na wengine hii ni kutokana na fadhila za Allah
anamfadhilisha amtakaye ila haimaanishi kuwa sisi ni bora zaidi kuliko
wenzetu wengine.

Hivyo tumejitahidi kadiri ya uwezo wetu katika kufanikisha kazi yetu hii,
huku tukiamini kuwa kitabu pekee kisichokuwa na makosa ni kitabu
cha Allah mtukufu.

Hivyo basi mapungufu yoyote yatakayoonekana kwenye kitabu hiki


ifahamike kwamba haikuwa dhamira yetu kuandika makosa tutafutiwe
udhuru, na pale ambapo tumepatia tuombeeni dua ili tuzidi kupatia
zaidi, nasi tunataraji kwa Allah mtukufu kuwa atatusamehe makosa
yetu na kutulipa tulipopatia. Ni sisi wanyonge wanaotaraji huruma za
Allah
*Wachapaji*
 Amry Ally Shambula
 Ibrahiim Juma Isingo

*Wafasiri*
 Abdillah Masawe.
 Bashiri Shabani Dule

*Wahakiki*
 Shaaban Ibrahim
 Wenge Mohamadi Wenge
 Maulid Hussen Maulid

3
DIBAJI
KATIKA majukwaa mbalimbali ambayo Shekhe Abdulqadir Muhammad
Al-Ahdal ameendesha mihadhara na kutoa fat-wa; misikitini au kwenye
vyombo vya habari, amekuwa akiulizwa maswali mbalimbali
yanayotokana na Waislamu kuhitilafiana katika mambo kadha wa
kadha.

Kitabu hiki kinalenga kuyaweka pamoja majibu ya maswali hayo,


hususani yanayohusu swala, kwa lugha ya Kiswahili ili iwe rejea
rahisi kwa waumini wa dini yetu tukufu ya Kiislam.

Mfano wa maswali hayo ni:-


1) Ni upi usahihi, kusoma bismillah kwa sauti au kuisoma kwa siri
katika swala?
2) Je, inajuzu kusoma kunuti katika Swala ya Alfajiri?
3) Je, yafaa kumfuata imamu katika kunuti ya alfajiri kama wewe
huamini katika kunuti hiyo?
4) Sheria inasemaje kuhusu kutikisa kidole katika Tahiyyatu?
5) Vipi kuhusu kusoma dua katika hotuba (khutba) ya Ijumaa na
kuinua mikono?
6) Na je, ni sahihi kusoma dua baada ya swala?

Ingawa hoja zinazohusu masuala haya zinatokana na jitihada za


wanachuoni lakini wakati mwingine zimekuwa zikisababisha malumbano
makali hadi umma kugawanyika, jambo ambalo ni hatari kwa
mustakabali wa dini na halikubaliki.

Ni kwa mantiki hiyo, kitabu hiki kinaanza kwa kueleza adabu za


kuhitilafiana na kuvumiliana katika masuala yanayohusu jitihada za
wanachuoni kwa kuangalia kauli zao.

Kitabu hiki pia kinaeleza namna ambavyo mashekhe wamekemea tabia


ya kulazimisha mtu kufuata jambo ambalo linatokana na jitihada za
wanachuoni bali kwa kubainishiana hoja na kumwacha kila mmoja
kufuata hoja anayoona kwake ina mashiko.
***

4
KUJIPAMBA NA ADABU ZA KUHITILAFIANA NA KUVUMILIANA
KATIKA JITIHADA ZA WANACHUONI

Ni jukumu adhimu la kila mlinganiaji wa dini hii tukufu ya kiislamu


kujua daraja zinazosababisha kutofautiana (hitilafu) pamoja na
kujipamba na adabu za kutofatiana. Ikitokea haja ya kumkosoa mtu
basi ni vyema ichungwe misingi ya sheria.

Kutokujua hiyo misingi na kisha kuiheshimu na kuichunga, imekuwa


sababu ya kuzuka kwa migogoro katika jamii ya kiislamu.

Kimsingi, waislamu wamegawanyika katika makundi mawili kuhusiana


na suala zima la kuhitilafiana katika masuala ya jitihada.

Kundi la kwanza:
Kuna wale ambao hawakubali hitilafu yoyote ile hata ambayo
inakubalika kisheria, isipokuwa kauli na msimamo wao tu ndiyo
wanaoukubali. Msimamo huo huwa chanzo cha mijadala yenye kuleta
migogoro katika jamii ya kiisilamu.

Kundi la pili:
Hili lipo kinyume na kundi la kwanza kutokana na kukubali kila aina za
hitilafu hata kama inakwenda kinyume na misingi ya kisheria ambayo ni
Qur-an na Sunnah pamoja na makubaliano ya wanachuoni.

Kundi hili linakubaliana hata na makundi yaliyopotea kama vile Shia na


Ahmadiya (Kadiani). Jambo la kushangaza ni kuwa wanakwenda tofauti
na ndugu zao wa Ahlusunnah waljamaa katika mambo ambayo
yanawakusanya pamoja.

Kundi hili hutegemea kanuni isemayo; "Tunaungana katika yale


tuliyokubaliana, na tupeane udhuru kwa mambo tuliyohitilafiana".

Lengo lao kubwa ni kuukusanya ummah wa kiisilamu uwe kitu kimoja


hata kama wanaokusanywa wako kinyume na misingi ya dini.

5
Makundi yote haya mawili yakipimwa katika misingi ya dini utagundua
kuwa kuna sehemu wanapatia na kuna sehemu wanakosea.
Kwa nini tunasema hivyo?

Kwa upande wa kundi la kwanza ambao msimamo wao ni kwamba


hakuna kuvumiliana katika suala la kuhitilafiana, wahusika watakuwa
sahihi endapo wanakusudia hitilafu inayopingana na misingi ya kisheria
waziwazi.

Lakini pia wawe wanakusudia hitilafu ambayo inafaa kisheria kwa


maana ya wanachuoni kuhitilafiana kama ilivyo madhhebu manne ya
Ahlusunnah waljamaa walivyohitilafiana mpaka kukapatikana
madhhebu hayo; Hanafiyah, Maalikiyah, Shaafiiyah na Hambaliyah.

Kinyume cha hapo, kundi hili litakuwa limekosea.

Ama kundi la pili lenye msimamo uliojengeka juu ya kanuni ya


"tunaungana katika yale tuliyokubaliana na tupeane udhuru katika yale
tuliyohitilafiana" ikiwa wanakusudia hitilafu za kifiqihi za madhehebu
manne basi itakuwa ni sawa kwa sababu tofauti hizi hazipingani na
misingi ya sheria ya dini.

Lakini kama wanakusudia kuvumiliana (kupeana udhuru) katika tofauti


ambazo zinakwenda kinyume na misingi ya dini, basi hili ni kosa.

Mfano wa kosa ni kama vile kuwavumilia Mashia katika maneno yao


mazito dhidi ya maswahaba (allah awaridhie) na hata wake wa Mtume
Muhammad (Swalla Allahu alayhi Wasallam). Au kuvumiliana na
Makadiani ambao wao wanaitikadi kuwa Utume unaendelea, hali ya
kuwa itikadi hii ni batili na haikubaliki kisheria.

ً ً
‫منصوصا ّبينا لم‬
ُ ‫ أو عىل لسان نبيه ملسو هيلع هللا ىلص‬،‫ "كل ما أقام هللا تعاىل به الحجة ف كتابه‬: ‫قال الشافع رحمه هللا‬
‫ي‬ ‫ي‬
1
".....‫يحل اإلختالف فيه لمن علمه‬

Amesema lmamu Shafii (Allah amarehemu): "Kitu chochote ambacho


Allah ameweka wazi kwa viumbe wake na kikaeleweka kwao basi

.263/2 ‫ أعالم الموقعٌن‬، 565/1 ‫نتهى من كتاب الرسالة‬1

6
hawana namna ila kufuata tu, na hawaruhusiwi kwenda kinyume
nacho."2
Imamu anaendelea kusema kwamba ikitokea wamepinga, basi upingaji
huo ndio ambao Allah anaulaumu kwao.

Na ikitokea mtu anauliza kwamba ipo wapi hiyo lawama ya Allah, basi
atajibiwa kwamba Allah amesema:

٤ :‫ﭧﭐﭨﭐﱡﭐ ﲠ ﲡ ﲢ ﲣ ﲤ ﲥ ﲦ ﲧ ﲨ ﲩ ﲪ ﲫ ﱠ ابلينة‬

"Na hawakuhitilafiana wale waliopewa kitabu ila baada ya


kuwajia hiyo bayana (uongofu)."

Basi yule ambaye atakwenda kinyume na aya ambayo haibebi maana


zaidi ya moja wala hadithi sahihi, basi haiwi halali kwake kukhalifu. 3



MAZINGATIO KATIKA MANENO YA WANACHUONI WAKUBWA

Imamu Abuu-Hanifa (Allah amrehemu) ambaye alifariki dunia mwaka


150 hijiria amesema:

"Yeyote atakayekuja na kauli ambayo ni nzuri (bora) kuliko kauli


yetu, basi yeye atakuwa yupo sawa zaidi."4

Na amesema tena: "Yule ambaye maneno yetu yanamkera, basi


hakika ya sisi hatukerekwi naye, bali nyoyo zetu zimekunjuka
kwake (hatuna chuki naye)."5

2
Tazama "arisala" (1/560), Aalamul-muwaqiyna (2/263)
3
Rejea iliyopita.
4
Taarekh Baghdadi (13/352)
5
Taarekh Baghdadi (13/352)

7
Amesema mwanachuoni Yunus Aswadafiy, akimzungumzia Imamu
Shafii ambaye alifariki dunia mwaka 204 hijiria (Allah awarehemu):
"Sijapatapo kumuona mtu mwenye akili kuliko lmamu Shafii. Nilijadiliana
naye siku moja katika mambo ya dini na hatukuafikiana kisha
tukaachana halafu tukakutana siku nyingine, basi lmamu Shafii
aliponiona akanishika mkono kisha akasema:

„Ewe Abuu Mussa kwani haiwezekani tukabaki kuwa ndugu hata


kama hatujakubaliana katika masuala?’"

lmamu Dhahabi akisisitiza maneno hayo na kumsifu Imamu Shafiy,


amesema: "Jambo hili linaonesha ukomavu wa akili yake na uelewa wake
katika sheria, kwani wanachuoni wa rika moja huwa hawaachi
kuhitilafiana."6



HAIFAI KUMKHALIFU IMAMU KWENYE SWALA KATIKA MASUALA


YA JITIHADA ZA WANACHUONI

Amesema Imamu Nawawiy (Allah amrehemu):

"Haimpasi mufti wala kadhi kumkemea kila aliye kinyume na yeye


maadamu hajakwenda kinyume na Kitabu (Qur-ani) na Sunnah
pamoja na makubaliano (ijimai) ya wanachuoni na qiyasi (kigezo)
kilicho wazi kabisa."

Amesema tena Imamu Nawawi:

"Wanachuoni wanamkemea yule ambaye anapinga jambo ambalo


wanachuoni wamekubaliana. Ama kwa yale waliyohitilafiana
hairuhusiwi kumkemea, kwani kila mwanachuoni ambaye amefika
daraja za kujitahidi hata kama atakuwa amekosea usahihi wa suala
husika lakini kisheria amepatia”.

6
Siyaru a’laami nnubalaa (10/16-17)

8
Amesema mwanachuoni Ibun Qudamah (Allah amrehemu): "Haimpasi
yeyote kumkemea mtu yeyote ambaye anafanyia kazi kauli ya
madhehebu yake.

‫ ينبغي للمأموم أن يتبع إمامه فيما يسوغ‬:

Amesema Sheikh Al-islaam lbun Taymiyah (Allah amrehemu): "Yampasa


maamuma kumfuata imamu kwa mambo ambayo kila mtu
anaruhusiwa kuwa na mtazamo wake, ikiwa imamu atakunuti basi ni
wajibu kwako uitikie “aamiyn” hata kama wewe hukubali kunuti, na
akiacha kukunuti basi na wewe acha kukunuti hata kama wewe
unaikubali kunuti", kwani Mtume (Swallallahu Alayhi Wasallam)
anasema: "hakika amewekwa imamu ili afuatwe."

Mtume Muhammad (Swallallahu Alayhi Wasallam) pia amesema:


"Msihitilafiane na maimamu wenu.”

Kumbuka pale lbun Masoud (Allah amridhie) alipompinga Othman bin


Afan kwa kuswali rakaa nne katika maeneo ya Mina, wakati Mtume
(Swallallahu Alayhi Wasallam) alikuwa akiswali rakaa mbili za safari
katika eneo hilo, lakini pamoja na kumpinga aliswali nyuma yake rakaa
nne, na alipoulizwa juu ya jambo hilo akajibu kwa kusema:
"Kutofautiana ni shari."11

11
Rejea kitabu Majumua Fatawa, Juzuu 23, uk 115 - 116.

9
Na akasema tena: "Mtu yeyote ambaye amefikia daraja ya jitihada
inayoruhusiwa kisheria basi haifai kumlaumu na kumwona kuwa
amepata dhambi, kwani hakika ya Allah amemsamehe alipokosea
kwenye hiyo jitihada yake, bali inapasa kuwa naye pamoja na kumpenda
kwa kuwa ana imani na uchamungu, na ni mwenye kusimamia yale
ambayo Allah amewajibisha katika haki za huyo mwenye kujitahidi.
Miongoni mwa hizo haki ni kumpongeza na kumwombea dua pamoja na
haki nyingine…. "12
Na amesema tena: "Ikiwa kauli inakwenda kinyume na Sunnah
(mwenendo na mafundisho ya Mtume yaliyo wazi) na makubaliano ya
wema waliotangulia, basi ni lazima akemewe huyo mtu, ikiwa si hivyo
atakemewa kwa kubainishiwa udhaifu wa hoja zake.

"Na ikiwa katika masuala ambayo hayakutajwa na Sunnah (mwenendo


na mafundisho ya Mtume yaliyo wazi) wala makubaliano ya wanachuoni,
na jambo hilo wanachuoni wamehitilafiana, basi hapingwi yule ambaye
atalifanya kwa jitihada yake au amechukua kutoka kwa mwanachuoni
mwingine.

Amesema lbun Taymiyah: "Masuala ya jitihada ambayo mtu


atayafanyia kazi kwa kauli ya baadhi ya wanachuoni, hapingwi mtu
huyo na wala hatengwi."14

Amesema Sheikh Ibun Uthaymin (Allah amrehemu): "Ama kwa watu wa


kawaida (.... ‫ )العوام‬wanalazimika kisheria kufuata yale wanayoelekezwa
na wanachuoni wao, ili wasije wakatoka katika njia sahihi, kwa sababu
kama tungesema kila muumini wa kawaida awe kila kauli atakayoisikia
aichukue, basi hilo lingepelekea umma kutokuwa pamoja. Kwa sababu
hiyo amesema Sheikh wetu Abdurrahmaan Assaadiy (Allah amrehemu)
„Waumini wa kawaida yawapasa kufuata rai za wanachuoni wa miji
yao."15
12
Rejea kitabu Majumua Fatawa, juzuu ya 27, uk 233.

14
Rejea kitabu Majumua Fatawa juzuu 20 uk 207.
15
Rejea kitabu Likaati Babu Maftuuh, juzuu ya 3, uk 79.

10


HAIFAI KULAZIMISHANA MISIMAMO KATIKA MAMBO YA JITIHADA

Sheikh al-Islaam ibun Taymiyah (Allah amrehemu) wakati anaongelea


masuala ya Fiqhi ambayo wamehitilafiana wanachuoni ndani yake,
alisema: "Hakika msingi wa masuala haya ndani yake kuna hitilafu
mashuhuri baina ya wanachuoni, na masuala ya jitihada haifai watu
kukemeana isipokuwa kwa kubainisha hoja… Siyo kwa kupinga tu
bila hoja. Usitumie kumuiga mwanachuoni mwingine kuwa ndiyo
hoja kuu ya kumkemea ndugu yako katika mambo ya jitihada, kwani
kitendo hicho ni kitendo cha watu wajinga wanaofuata matamanio
ya nafsi zao."17



MAMBO AMBAYO WANACHUONI WAMEHITILAFIANA

Mambo yenye kuhitilafiana ni mambo ambayo wanachuoni


wametofautiana mitazamo kutokana na uelewa wa dalili na hoja
mbalimbali za kisheria zilivyokuja kuzungumzia mambo hayo.

Mfano wa mambo hayo ambayo yamekuwa yakisababisha maswali kwa


waumini, ni haya yafuatayo:-

1. Hukumu ya kusoma bismillah katika swala.


(i) Hoja za wanaodhihirisha bismillah.

17
Rejea kitabu Majumua Fatawa, Juzuu ya 35, uk 212.

11
(ii) Hoja za wanaosoma bismillah kwa siri.

2. Kusoma kunuti katika swala ya alfajiri.


(i) Hoja za wanaokubali kunuti ya alfajiri.
(ii) Hoja za wanaopinga kunuti ya alfajiri.
(iii) Kumfuata imamu katika kunuti ya alfajiri.
(iv) Wosia wa wanachuoni kwa maimamu wa swala.

3. Kutikisa kidole katika tahiyatu.


4. Khatibu kunyanyua mikono wakati anaomba dua kwenye khutba.
5. Kusoma dua baada ya swala na kunyanyua mikono wakati wa dua.

Tutaelezea mambo haya kwa mchanganuo mfupi namna wanachuoni


walivyotofautiana na hoja zinazotegemewa na kila upande.



1. KUSOMA BISMILLAH KATIKA SWALA

SWALI
Kuna maimamu ambao wanaposwalisha hudhihirisha Bismillah
na wengine hawadhihirishi, Ni upi usahihi wa hilo?

MAJIBU:
Wanachuoni wamehitilafiana juu ya kusoma bismillah kwa sauti au kwa
siri katika swala. Na jambo hili halitakiwi kuleta mfarakano katika
umma, kwani kila mmoja ana mashiko (ushahidi) wake.

Ushahidi wa kuisoma Bismillah kwa siri katika swala.


Mosi: Swahaba Anas (Allah amridhie) amesema: "Nimeswali nyuma ya
Mtume (Swallallahu Alayhi Wasallam), Abuubakar, Omar na Othmaan,
walikuwa wakianza kusoma Alhamdulillah katika swala bila ya
kudhihirisha Bismillah."18

Pili: katika Sahihi Muslim amesema Anas: "Sijasikia mmoja wao


anasoma bismillah kwa sauti katika swala."19

18
Rejea Sahihi Bukhari, hadithi namba 89.
)399( ‫) و مسلم‬343( ‫رواه البخاري عنه‬19

12
Ushahidi wa wanaodhihirisha bismillah katika swala:
Mosi: Katika Sahihi Bukhari, kwenye kitabu kinachozungumzia fadhila
za Qur-an, pia amesimulia Anas (Radhi za Allah ziwe juu yake) kwamba
aliulizwa juu ya kisomo cha Mtume (Swallallahu Alayhi Wasallam)
akasema: "Kisomo chake alikuwa anavuta, kisha akasoma Bismillah
Rahmaan Rahiim, yaani alikuwa akivuta neno bismillah na neno
rahmaan na neno Rahiim."20

Pili: Kutoka kwa Abuu Nuaimu (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema:
“Nimeswali nyuma ya Abuu Hurayrah ambapo alianza kusoma Bismillah
Rahmaan Rahiim kisha akasoma Suuratul Faatiha mpaka akafika
“Waladhwaalliin” na akasema “aamiin”, na pindi alipotoa salamu
akasema; Naapa kwa yule ambaye nafsi yangu ipo mikononi mwake,
hakika yangu mimi nimeswali swala kama alivyoswali Mtume
(Swallallahu Alayhi Wasallam)."21

Tatu: Anas amesema: "Muawiyah (Radhi za Allah ziwe juu yake) alipofika
mji wa Madina aliwaswalisha watu na akaacha kusoma bismillah kwa
sauti, wakampinga wale waliohudhuria swala hiyo katika Muhajirina, na
aliposwali mara nyingine akasoma bismillah kwa sauti."22

Nne: Amesema lbn Kathir katika tafsir yake: "Kwa sababu wanazuoni
wamekubaliana juu ya swala ya mwenye kudhihirisha bismillah na
mwenye kuisoma kwa siri, tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa hili."23

Hii inamaanisha kuswihi kwa swala ya mwenye kusoma bismillah kwa


siri na kwa anayesoma kwa sauti.

20

21
Hadithi hii ameipokea Annasai kwa namba (905), Ibun Khuzaymah namba (499), Alhaakim katika kitabu Mustadrak,
juzuu ya (1/uk 232), Sunanulbayhaqiy, juzuu ya (2/ uk 46), Imamu Shafii katika Al-Ummu, juzuu ya (1/uk 232), Naswbu
Raya, juzuu ya (1/uk 353), Tafsir Ibun Kathiri, juzuu ya (1/ uk 66) na Daarulqutniy kama hadithi namba 14. Daarulqutniy
amesema hadithi hii ni sahihi na wapokezi wake wote ni wakweli.
22
Rejea tafsir lbun Kathir, Juzuu ya 1, uk 66, Chapa ya Daarulhadithi, Cairo.
23

13
Tano: Amesema lbn Qayyim: "Mtume (Swallallahu Alayhi Wasallam)
alikuwa anadhihirisha bismillah mara chache, na mara nyingi alikuwa
akiisoma kwa siri kuliko alivyokuwa akiidhihirisha."24
Sita: Imamu wetu Shafi (Allah amrehemu) anaona kudhihirisha
bismillah katika swala ni lazima, ingawa alikuwa anaswali nyuma ya
mtu ambaye hadhihirishi bismillah.

Amenukuu hilo Sheikh al-Islaam lbun Taymiyah kutoka kwa lmamu


Shafii kwamba alikuwa akiswali nyuma ya wafuasi wa madhehebu ya
imamu Maliki ambao wao hawasomi kabisa bismillah, hali ya kuwa
madhehebu yake (Shafii) kudhihirisha Bismillah ni wajibu.26



24
Rejea Zaadulmaad, Juzuu ya 1, uk 206. Chapa ya

26
Rejea Majumua Alfatawa, Juzuu 23, uk 379.

14
2. KUSOMA KUNUTI KATIKA SWALA YA ALFAJIRI

SWALI:
Ni upi usahii, kukunuti kwenye kila swala ya Alfajiri au
kutokunuti kama wanavyofanya maimamu wengine?

MAJIBU:
Maana ya kunuti:
Neno kunuti lina maana nyingi takriban kumi kama alivyosema Ibun
Hajar katika kitabu chake cha Fat'hu l-baari, juzuu wa 2: uk 491.

Baadhi ya maana hizo ni ibada, utii, kunyamaza, dua, unyenyekevu,


kukiri kuwa wewe ni mja wa Allah, kisimamo, kurefusha kisimamo
kwenye swala na kudumu na utii juu ya Allah.

Wamehitilafiana wanazuoni tangu zamani juu ya kudumu na dua ya


kunuti katika swala ya alfajiri kwa kauli tatu:

Kauli ya kwanza:
Hairuhusiwi kukunuti katika kila swala ya alfajiri isipokuwa kwenye
majanga, tena katika swala zote tano.

Hii ni kauli ya imamu Thauriyyu, imamu Abuu Hanifa na imamu


Ahmadi. Na imenukuliwa kauli hiyo pia kutoka kwa maswahaba kama
Abdullah Ibun Omar, Abdullah ibun Abasi, Abdullah ibun Masoud na
Abuu Maaliki Saad ibun Twaariqi Al-Ashjaiy.

Aliulizwa swahaba Abuu Maaliki Saadi ibn Twaariki Al-ashjaiy (allah


amridhie): "Hakika wewe uliswali nyuma ya Mtume (Swallallahu Alayhi
Wasallam), ukaswali nyuma ya Abuubakar, pia Omar, Othmaan na Ally
(allah awaridhie). Je, walikuwa wanakunuti katika swala ya alfajiri?
Akajibu kwamba jambo hilo ni uzushi.

Na katika mapokezi mengine akasema: Ewe mwanangu jambo hilo ni


bida'a.27

27
Amepokea lmamu Tirmidhiyyu hadithi namba 402.

15
Pili: Amepokea Ibn Abii Shayba na wengineo kutoka kwa Abii Makhlad,
akisema: "Nimeswali pamoja na Ibn Omar (allah amridhie) hakukunuti
katika swala ya alfajiri na akasema sijamuona yeyote katika maswahaba
zetu akifanya jambo hilo"28

Tatu: Imekuja katika sahihi mbili (Bukhari na Muslim) na vitabu vingine


kutoka kwa Anas (Radhi za allah ziwe juu yake) akisema: "Hakika ya
Mtume alikunuti mwezi mzima akiwaombea dua mbaya makabila mawili
katika waarabu, Ri‟li na Dhakuwan, waliomuasi Mtume (Swallallahu
Alayhi Wasallam) kwa kawaua maswahaba sabini wa Mtume
(Swallallahu Alayhi Wasallam). Akasoma kunuti katika swala zote tano
na wakawa wanaitikia „Amiin‟ wale walioko nyuma ya Mtume
(Swallallahu Alayhi Wasallam), kisha akaacha kukunuti."29

Ufafanuzi unatolewa kwamba Mtume (Swallallahu Alayhi Wasallam)


aliacha kukunuti kipindi ambacho hakukuwa na majanga, na kama
angelihusisha jambo hilo la kunuti katika swala ya alfajiri, basi
lingelinukuliwa kwetu kwa hadithi nyingi, wala lisingelikuwa ni lenye
kujificha kwa makhalifa waongofu.

Nne: Kutoka kwa Ummu Salama (Radhi za Allah ziwe juu yake)
amenukuu kutoka kwa Mtume (Swallallahu Alayhi Wasallam): "Hakika
yake amekataza kukunuti katika swala ya Alfajiri." 30

Tano: Kutoka kwa Ibun Abasi (Radhi za Allah ziwe juu yake) amesema:
"Kukunuti asubuhi ni bida'a (uzushi katika dini)."31

Kauli ya pili:
Msimamo wa pili unasema dua ya kunuti ni jambo lililopo kisheria
katika swala ya alfajiri. Hii ni kauli ya imamu Maaliki na Imamu Shafii.

Mosi: Wanategemea aya Allah anasema:


٨٣٨ :‫ﭧﭐﭨﭐﱡﭐ ﱁ ﱂ ﱃ ﱄ ﱅ ﱆ ﱇ ﱈ ﱉ ﱠ ابلقرة‬

28
Al-majmui ya nnawawiy (3/466) ‫المجموع للنووى‬
29
766 ‫ومسلم‬4904 ‫البخاري‬
30
Al-majmui ya nnawawiy (3/466) ‫المجموع للنووى‬
31
Rejea iliyopita ( ‫)المصدر السابق‬

16
“Zilindeni swala, na hasa swala ya kati na kati na simameni kwa ajili
ya Allah nanyi ni wenye kukunuti (kunyenyekea).”32

Wanasema swala ya kati na kati ni swala ya alfajiri na kunuti yake.

Pili: Ni hadithi ya Anasi ibun Maaliki (Radhi za Allah ziwe juu yake)
ambaye amesema: "Hakuacha Mtume (Swallallahu Alayhi Wasallam)
kukunuti katika swala ya alfajiri mpaka alipoondoka duniani." 33

Tatu: Amesema imamu Annawawiyyu:"Madhehebu yetu ni Sunnah


kukunuti katika swala ya alfajiri, iwe kuna majanga au hakuna majanga
na wamelizungumzia jambo hili wengi katika wema waliotangulia na
waliokuja baada yao au wengi katika wao, nao ni Abuubakar Swiddiq,
Omar ibn Khatwaab, Othman ibn Affan, Ally Ibun Abiy Twalib, Ibn Abas
na Al-Barraa ibn Aazib (allah awaridhie…..

Amepokea Al-bayhaqiyyu kwa mapokezi yaliyo sahihi na vilevile kauli


hiyo imesemwa na mataabii na kundi kubwa la waliokuja baada ya
hao.34

Nne: Pi amesema imamu Annawawiyyu: Ally (Allah amridhie) amekunuti


katika swala ya alfajiri na jambo hili limethibiti kwa Ally (Allah amridhie)
kwa kauli sahihi na mashuhuri."35

Tano: Aliulizwa Abuu Othman juu ya kunuti katika swala ya alfajiri


kuwa ni baada ya rukuu?. Akajibu ndiyo. Akaulizwa ni kutoka kwa
nani? Akasema "kutoka kwa Abuubakar, Omar, na Othman (Allah
awaridhie). Ameipokea Al-bayhaqiyyu katika hadithi hasan (sahihi).36

Kauli ya tatu:

32
Suratul-Baqarah (2/238)
33
Hadithi hii ameipokea Imamu al-Bayhaqiyyu kwa namba 3105, Daar-kutuniyyu kwa namba 1694, Imamu Ahmad kwa
namba 12657, Ibun Abii Shayba kwa namba 312, Abdulrazzaki kwa namba 4964, Bazaar kwa namba 556 na Atwahawi
1:143 na Al-Hakim 2:201. Na ameisahihisha Imamu Maaliki na Imamu Shafii, Daar-kutuniyyu, Al-Haakim, Bayhaqiyyu na
Nawawiyyu na Al-balkhiyyu…. Tazama kitabu Al-majmuua ya Imamu Annawawiyyu 3:465-467.
34
Rejea Al-Majmuu ya lmamu Annawawiyyu 3:465-467.
35
Rejea Al-majmuua 3:465-467
36
Rejea al-Majmuua ya Imamu Annawawiyyu 3 :465-467.

17
Kunuti ni jambo ambalo limefutwa na halipo kisheria katika hali zote,
iwe katika majanga au laa. Na hii ni kauli ya baadhi ya watu wa
madhehebu ya Hanafi na baadhi ya watu wa lraq.

Ushahidi wao ni hadithi ya Mtume (Swallallahu Alayhi Wasallam) iliyopo


katika bukhari na muslimu pale alipokunuti kwa muda wa mwezi
mzima akiwaombea dua mbaya makabila mawili ya waarabu kisha
akaacha, kwa maana kwamba aliacha moja kwa moja. (ndivyo
wanavyoamini).

Amesema Sheikh Wetu, Abdulqadir Mohammed Al-ahdal (Allah


amuhifadhi): "Masuala haya ni masuala ambayo wanachuoni
wamehitilafiana kama tulivyokwishaona, na kila upande una mashiko".

Amesema imamu Ahmadi:

"Walikuwa waisilamu wanaswali nyuma ya wanaokunuti na nyuma ya


wasiokunuti."37



3. KUMFUATA IMAMU KATIKA KUNUTI KWENYE SWALA YA


ALFAJIRI

SWALI:
Kama mimi nimekinaishwa na msimamo wa kwamba Mtume (Swallallahu
alayhi wasallam) hakukunuti, ninaweza kumfuata imamu anayekunuti
katika swala?

MAJIBU:

Sheikh al-Islaam Ibn Taymiyyah (Mwenyezi Mungu amrehemu) amesema


kwamba iwapo imamu atafanya kitendo kilicho kinyume na mtazamo wa
maamuma ndani ya swala katika yaliyo na mitazamo miwili tofauti.
Mfano: kusoma kunuti katika swala ya alfajiri, kuswali witri yenye rakaa
tatu mfululizo na atahiyyatu moja, ibada hizi zina mitazamo mingine pia

37
Faslul-khitwab (7/456), ‫فصل الخطاب في الزهذ والرقائق واآلداب‬.

18
katika utekelezwaji wake. Hivyo maamuma anatakiwa kumfuata imamu
kwa utaratibu atakaoufanya hata kama yeye haoni hivyo. 38

Sheikh Ibn Baz (Allah amrehemu), amesema: “Imamu anaposoma kunuti


katika swala ya alfajiri hakuna tatizo kwa maamuma kumfuata imamu
wake, ingawa kilicho bora ni kutokusoma kunuti katika swala ya alfajiri.
Lakini iwapo maamuma ataswalishwa na imamu anayesoma kunuti
alfajiri haina tatizo kwake kuitikia dua ya kunuti na kunyanyua
mikono.”39

Aliulizwa mwanachuoni Ibn Uthaymiyn (Allah amrehemu) kuwa: “Imamu


wetu ana kawaida ya kusoma kunuti katika swala ya alfajiri. Je,
tumfuate katika swala na tuitikie dua yake?

Akajibu kwa kusema: “Yeyote atakayeswalishwa na imamu anayesoma


kunuti katika swala ya alfajiri anatakiwa kumfuata imamu wake katika
kunuti na aitikie dua, kwani Imamu Ahmad (Allah amrehemu) ametoa
ushahidi wa jambo hilo pia".40

Mwanachuoni mbobezi wa hadith, Muhammad Nasir din al-Albani (Allah


amrehemu) aliulizwa: Kuna baadhi ya watu wanasoma kunuti katika
swala ya alfajiri, je, tunapaswa kuswali nyuma yao? Tukunuti pamoja
nao au tuache?

Akajibu: “Haifai kwa muislamu kumkhalifu imamu wake ndani ya swala,


hata kama anaona imamu wake yuko kinyume na sunnah au
amekhalifu rai yake, kwa sababu Mtume (Swallallahu Alayhi Wasallam)
anasema: “Hakika amefanywa imamu kuwa ni wa kufuatwa katika
swala”. Akisema “Allah Akbar” nanyi fanyeni hivyo, akiswali amesimama
nanyi simameni, akiswali kwa kukaa nanyi kaeni nyote”.

Kisha shekhe akaendelea kusema : Imamu anaswali kwa kukaa kwa


kuwa ana udhuru wa kisheria bila shaka, lakini maamuma hana
udhuru, kwani anaweza kuswali kwa kusimama. Hivi unadhani kwa nini
Mtume (sallallah alayhi wasallam) amemuamrisha maamuma naye
aswali kwa kukaa hata kama hana udhuru?

38
Al-ikhtiyaaraatul-Fiq-hiya (uk:68).
39 Maj-muu fataawa wamaqaalaatu mutanawia, juzuu (14/177).
40
Majmoo' Fataawa wa Rasa'il al-'Uthaymeen (14/144).

19
Jibu ni ili pasitokee tofauti baina yake na imamu ndani ya swala. Kwa
kuthibitisha hilo huu hapa ushahidi mwingine wa Hadithi: “Hakika
amefanywa imamu kuwa ni wa kufuatwa katika swala, basi msipingane
naye.”

Hivyo imamu akinyanyuka kutoka kwenye rukuu na akanyanyua


mikono yake kwenye kunuti wewe usimkhalifu, Kwa nini umkhalifu
wakati yeye ana mashiko yake?

Akauliza tena muulizaji: Nikimfuata katika kusoma kunuti na kunyanyua


mikono sio uzushi?

Akajibu kwamba : Imamu wako haoni kuwa kitendo hicho ni uzushi, na


kama anaona kuwa jambo hilo ni uzushi basi usimfuate kwa sababu
ameenda kinyume na misingi ya dini.

Muulizaji akahoji tena: Vipi, nikimbainishia huyo imamu kabla ya swala


kwamba kitendo hicho ni uzushi ?

Shekhe akajibu kwamba : Kwani wewe nani?! Je, wewe ushakuwa


Sheikh Al-Islam kwamba ukimwambia utakuwa umeshamfikishia hoja
na atakinai?!.41



4. IMAMU AEPUKE KUWAGAWA WATU

SWALI:

Kama imamu haoni kufaa kwa kusoma kunuti katika swala ya alfajiri,
lakini anaswalisha watu wanaoona kufaa kwa kunuti. Ni lipi jambo
sahihi analotakiwa kufanya?

JIBU:
Endapo imamu akiwaswalisha watu wanaoona kusoma kunuti ya alfajiri
inafaa, basi asome kunuti ili kuepuka kuwagawanya.

Sheikh Al-Islam Ibn Taymiyyah (Allah amrehemu), amesema: Inatakiwa


kwa maamuma amfuate imamu wake katika yale yanayoruhusiwa

41
Kaseti No. (262) yenye kichwa cha habari. “Fataawa kwa njia ya simu”

20
kutokana na jitihada za wanachuoni. Hivyo imamu akikunuti naye
maamuma aitikie "Aamiyn" na ikiwa imamu hakukunuti maamuma
naye hatokunuti.

Hii ni kwa sababu ya kauli ya Mtume (Swallallahu alayhi wasallam):


“Hakika amefanywa imamu kuwa ni wa kufuatwa (katika swala)".
Halikadhalika Mtume amesema: "Msitofautiane juu ya maimamu wenu".

Naye Abdullah bin Masoud (Allah amridhie) alikerwa na kitendo cha


Uthman bin Affan (Allah amridhie) kuswali rakaa nne katika viwanja wa
Mina badala ya rakaa mbili za safari kama alivofanya Mtume (swallah
alayhi wasallam) hata hivyo Abdullah bin Masoud aliswali nyuma ya
Uthmani. Alipoulizwa juu ya hilo, akajibu : "Kuhitalifiana ni shari".42



KUHITILAFIANA KATIKA MAMBO KAMA HAYA SIO ADHABU, BALI


HUWA NI REHEMA.

Sheikh al-Islam ibn Taymiyyah (Allah amrehemu) amesema:

Mijadala katika hukumu za kisheria (Fiq-hi) huwenda ikawa ni


rehma itakapokuwa haikusababisha shari kutokana na kutokuwa
wazi hukumu yake. Kutokana na hili ametunga mtu kitabu akakiita
kitabu cha ihtilafu,lmamu Ahmad akamwambia kiite "kitabu
jumuishi"43

Al-Qurtubi (Allah amrehemu), amesema:

“Maswahaba walitofautiana kuhusu hukumu za matukio mbalimbali,


lakini pamoja na hayo walikuwa ni wamoja.”44

42
Mjmuu fatawa (23/115-116).
43
Majmuu fatawa (14/159)
44
Ahkamul-qurani (4/194)

21
Amesema shekh wetu Abdulqadir (Allah amhifadhi) : Kwa masikitiko
makubwa, mwenye kuutazama umma wa kiislamu leo hii, atakuta kuna
misingi mingi imekengeukwa isipokuwa wale ambao wamerehemewa na
Mola. Utakuta sababu za nusra zimeachwa, na kuchukua sababu za
migawanyiko na mifarakano.

Kwa sababu hiyo makundi potofu na maadui wa uislamu wametumia


fursa hii ya mifarakano kuzidi kuwagawa zaidi waislamu. Kutotunza
manhaji (njia) ya wema waliotangulia, ni kwenda kinyume na njia yao
iliyonyooka, lakini kwa bahati mbaya sana wengi hawajui.

Umefika wakati wa kuzinduka na kurekebisha makosa ya fikra na


misimamo, kwani kuiga wanachuoni wakubwa ni jambo linalokubalika
kisheria, na jitihada ni mlango uliokuwa wazi kwa aliyefikia daraja ya
jitihada katika wanachuoni.

Anasema sheikh al-islamu kuwa:

Jitihada kwa wanachuoni ni jambo linalo kubalika kiujumla, na


kuwaiga wanachuoni pia ni jambo linalokubalika
kiujumla.Wanachuoni hawalazimishi kila mmoja kuwa ni
mwenyekujitahidi (mtafiti), na pia hawamzuii yeyote kuiga
mwanachuoni yeyote.45

Ninamwomba Mwenyezi Mungu, Mola wa Arshi tukufu, aziunganishe


nyoyo zetu, na atuondolee chuki vifuani mwetu na vifundo, na atujaalie
nguvu na mshikamano dhidi ya maadui zetu.



45
Majmuu fatawa (20/24)

22
5. KUTIKISA KIDOLE KATIKA TAHIYATU

SWALI:
Kuna hili la kutikisa kidole kwenye swala na wengine hawatikisi. Ni
yapi mafundisho sahihi kuhusu hili?

JIBU: wanachuoni wamehitilafiana katika hili kwa kauli mbili. Kuna


wanaoona inafaa kutikisa kidole, na wengine wanaona haifai kutikisa
kidole:

ّ … ( ‫حديث وائل بن ُحجر رض هللا عنه عندما يصف صالة النب ملسو هيلع هللا ىلص قال‬
‫ فرأيته‬، ‫ثم قبض ثنتي من إصبعه‬ ‫ي‬ ‫ي‬
46
" ‫يحركها يدعوا بها‬

Ama ushahidi wa wanoona inafaa kutikisa ni hadithi ya waaili bin hujri (


allah amridhie) alipokuwa akielezea swala ya mtume (salallah alayhi
wasallam) akasema :" … Kisha akakunja vidole viwilli katika kidole
chake na nikamuona akitikisa wakati anaomba dua"

Ama wengine ni wale wasemao kuwa inafaa kutikisa kidole kwenye


atahiyatu, lakini kauli hii haina nguvu.

47 ّ
"‫يشي بإصبعه إذا دعا وال يحركه‬
‫النب ملسو هيلع هللا ىلص كان ر‬
‫ "أنه ذكر أن ي‬: ‫رض هللا عنه‬
‫الزبي ي‬
‫حديث عبدهللا بن ر‬

Ushahidi wa kundi hili hadithi ya abdallah bin zubeir (allah amridhie ) :


amesema kuwa mtume ( sallah alayhi wasallam) alikuwa akiashiria
kidole chake anapoomba dua, lakini akitikisi" Abuu duad.

Na mimi (Nawawi) nasema: "Hata kama tukitumia kauli yenye nguvu ya


kutokutikisa kidole, lakini ikatokea mswaliji akatikisa, swala yake
haitobatilika."48



46
363 ‫ وصححه االلبانً فً اإلرواء الغلٌل‬، ٨٨9 ً‫أخرجه النسائ‬
47
‫ ذكرالبٌهقً بإسنا ٍد صحٌح عن ابن زبٌر ورواه ابو داؤود بسن ٍد صحٌح‬:545/3 ‫قال الحافظ النووي رحمه هللا فً المجموع‬
48
Rejea kitabu Raudwatu Atwaalibiin juzuu ya 1 uk 443-1444

23
6. KUNYANYUA MIKONO WAKATI WA KUSOMA DUA KATIKA
KHUTBA

SWALI:

Wakati wa hotuba (khutba) ya Ijumaa kwenye kipengele cha dua,


watoa hotuba wengi (makhatibu) hawanyanyui mikono juu kama
wanavyofanya kwenye dua nyingine. Hili si kosa?

MAJIBU:
Wanachuoni wamehitilafiana juu ya jambo hili katika kauli mbili tofauti.

Kauli ya kwanza:
Inasema haifai kwa khatibu kunyanyua mikono wakati wa kusoma dua.

Ushahidi wa kundi hili ni kama ifuatavyo:


Mosi, amesema Imamu Nawawiy katika kitabu chake, Sherhe ya Sahihi
Muslim: "Na (khatibu) asinyanyue mikono katika khutba na hiyo ndiyo
kauli ya lmamu Maliki pamoja na wanachuoni wa kishafii na wengine
katika wanachuoni."

Pili: Amrah lbun Ruaybata alimwona Bishri Ibun Mar-waan akiwa


mimbarini huku amenyanyua mikono yake miwili wakati wa dua.
Akasema: “Mwenyezi Mungu atie ubaya katika mikono hii miwili. Hakika
nimemwona Mtume (Swallallahu Alayhi Wasallam) anaomba dua wakati
anakhutubu na alikuwa hanyanyui mikono isipokuwa kidole chake cha
shahada."49

Tatu: Hili jambo la kunyanyua mikono ni katika sababu za kujibiwa dua


isipokuwa katika maeneo ambayo Mtume (Swallallahu Alayhi Wasallam)
hakunyanyua mikono basi nasi hatunyanyui katika maeneo hayo.

Mfano ni katika khutba ya Ijumaa, Mtume (Swallallahu Alayhi


Wasallam) hakunyanyua mikono yake, isipokuwa tu pale alipokuwa
akiomba mvua (katika khutba) ndipo alinyanyua mikono yake.

49
Angalia hii katika Sahihi Muslim, hadithi namba 874.

24
Na vilevile Mtume (salallah alyhu wasallam) alikuwa hanyanyui mikono
akiomba dua kati ya sijida mbili na kwenye tahiyyatu (tashahudi) ya
mwisho kabla ya salamu.

Ni kwa msingi huo, wenye msimamo huu wanahitimisha kwa kusema


hawanyanyui mikono yao juu katika maeneo ambayo Mtume wa Allah
(Swallallahu Alayhi Wasallam) hakunyanyua mikono yake, kwa sababu
kitendo chake cha kunyanyua mikono ni HOJA na kuacha kwake pia ni
HOJA.

Na hivihivi pia baada ya kutoa salamu katika swala tano alikuwa akivuta
nyiradi zilizothibiti kisheria na alikuwa hanyanyui mikono.

Ama kuhusu maeneo ambayo Mtume (Swallallahu Alayhi Wasallam)


alinyanyua mikono yake basi ni sunna kwa mujibu wa kundi hili
kunyanyua mikono miwili, kwa sababu jambo hili ni katika sababu za
kujibiwa dua.

Kundi hili pia linasema: Katika Maeneo ambayo muisilamu anamwomba


Mola wake na haikupokewa kutoka kwa Mtume (Swallallahu Alayhi
Wasallam) kama alinyanyua mikono yake ama la, basi katika maeneo
hayo sisi tutanyanyua mikono kutokana na hadithi zilizofahamisha
kuwa kunyanyua mikono ni katika sababu za kujibiwa dua.50

Nne: Amepokea Imamu Bukhari kutoka kwa Anasi (radhi za Allah ziwe
juu yake)” akisema: “Siku moja Mtume (Swallallahu Alayhi Wasallam)
aliingia nyumbani kwa Ummu Suleym, akamletea Mtume (Swallallahu
Alayhi Wasallam) tende na samli, kisha Mtume (Swallallahu Alayhi
Wasallam) akasema: "Rejesheni samli katika chombo chake na tende
katika mfuko wake, kwani mimi nimefunga” kisha akasimama akaelekea
kwenye upande wa nyumba, akaswali swala isiyo kuwa ya faradhi, kisha
akamwombea dua Ummu Suleym na watu wa nyumbani kwake.

Hapa haijaeleza kuwa alinyanyua ama hakunyayua.

50
Rejea kitabu Majumua Fatawa ya shekh Ibun Baazi Juzuu ya 6 UK 158.

25
Kauli ya pili:
Hii inasema inafaa kwa khatibu kunyanyua mikono yake anapoomba
dua.

Kwa mujibu wa kundi hili, amesimulia Qadhil iyaadhi kutoka kwa


baadhi ya salafi (wema waliotangulia) na baadhi ya wafuasi wa Imamu
Maliki kuwa, “Inafaa kwa khatibu kunyanyua mikono yake wakati
anapoomba dua, kwa sababu Mtume (Swallallahu Alayhi Wasallam)
alinyanyua mikono yake ndani ya khutba ya Ijumaa alipokuwa akiomba
dua ya mvua"

Faida kuhusu hukumu ya kunyanyua mikono nje ya swala


Amesema Sheikh lbun Baazi (Allah amrehemu):"Kunyanyua mikono
wakati wa dua ni miongoni mwa sababu za kujibiwa dua mahala popote.

Kwani amesema Mtume (Swallallahu Alayhi Wasallam): “Hakika ya


Mwenyezi Mungu ni mwenye haya na Mstiri, anamuonea haya mja wake
ambaye amenyanyua mikono yake kumuomba yeye na akairudisha sifuri
(patupu).

Pia amesema Mtume (Swallallahu Alayhi Wasallam) katika ile hadithi ya


mtu anayenyanyua mikono kumuomba Allah hali ya kuwa kinywaji
chake ni cha haramu, chakula chake ni cha haramu, mavazi yake ni ya
haramu na amelelewa kwa haramu, vipi Allah atamjibu mtu huyu dua
yake?.

Na katika sababu za kutojibiwa dua ni kunywa vya haramu, kula vya


haramu, na kulelewa katika mazingira ya haramu.
Mwisho Mtume (Swallallahu Alayhi Wasallam) amesema kuhusu huyu
mtu ambaye kinywaji chake ni cha haramu chakula chake ni cha
haramu na amelelewa kwa haramu vipi mtu huyu atajibiwa dua yake?

Hii inaonesha kuwa kunyanyua mikono miwili wakati wa kuomba dua ni


katika sababu za kujibiwa dua, hata ukiwa kwenye ndege au kwenye
treni au kwenye gari au kwenye chombo cha kwenda mwezini au katika
hali yoyote ile, mtu atakapoomba atanyanyua mikono yake.

26
Hili jambo la kunyanyua mikono ni katika sababu za kujibiwa dua
isipokuwa katika maeneo ambayo Mtume (Swallallahu Alayhi Wasallam)
hakunyanyua mikono basi nasi hatunyanyui katika maeneo hayo.

Mfano katika khutba ya ijumaa hakunyanyua mikono yake, isipokuwa


alipokuwa akiomba mvua (katika khutba) alinyanyua mikono yake.

Na vile vile kati ya sijida mbili na tahiyyatu ya mwisho kabla ya salamu


hakunyanyua mikono yake. Hatutanyanyua mikono yetu katika maeneo
ambayo hakunyanyua Mtume (Swallallahu Alayhi Wasallam) mikono
yake, kwasababu kitendo chake cha kunyanyua mikono ni HOJA na
kuacha kwake pia ni HOJA.

Na hivi hivi baada ya kutoa salamu katika swala tano alikuwa akivuta
nyiradi zilizothibiti kisheria na alikuwa hanyanyui mikono, basi
hatutanyanyua mikono yetu katika maeneo hayo kwa kumuiga Mtume
(Swallallahu Alayhi Wasallam). Ama kuhusu maeneo ambayo Mtume
(Swallallahu Alayhi Wasallam) amenyanyua mikono yake basi ni sunnah
kunyanyua mikono miwili katika maeneo hayo, kwa sababu jambo hili ni
katika sababu za kujibiwa dua.

Na vile vile katika maeneo ambayo muisilamu anamuomba Mola wake


na haikupokewa kutoka kwa Mtume (Swallallahu Alayhi Wasallam)
kwamba alinyanyua katika maeneo hayo au aliacha kunyanyua, sisi
tutanyanyua katika maeneo hayo kutokana na hadithi ambazo
zilizofahamisha kuwa kunyanyua mikono ni katika sababu za kujibiwa
dua.51



51
Rejea kitabu Majumua Fatawa Juzuu ya 6 UK 158.

27
7. KUSOMA DUA BAADA YA SWALA ZA FARADHI:

SWALI:
Sheria ya dini inasemaje kuhusu kusoma/kuomba dua baada ya
swala ya faradhi?

MAJIBU:
Wanachuoni wamehitilafiana pia kuhusu kusoma dua baada ya swala ya
faradhi kwa mtu mmoja mmoja au kwa pamoja katika kauli mbili.

Kauli ya kwanza: Wanachuoni wa kauli hii wanasema jambo hilo ni


bida'a, yani uzushi katika dini na hivyo halifai.

HOJA ZAO:
Mosi: Hoja ya kwanza wanasema: “Mtume (Swallallahu Alayhi Wasallam)
hakufanya wala maswahaba zake hawakufanya hilo na kama jambo hilo
lingekuwa ni kheri basi wangetutangulia kulifanya.

Wanazidi kusema kwamba lau kama angefanya Bwana Mtume


(Swallallahu Alayhi Wasallam) basi lisingefichikana kwetu kwani
tungepokea hadithi nyingi juu ya hilo kutoka kwa maswahaba
mbalimbali.

Pili: Wamesema sehemu sahihi ya kuomba dua ni ndani ya swala kabla


ya salamu baada ya tahiyyatu ya mwisho kama alivyoamrisha bwana
Mtume (Swallallahu Alayhi Wasallam) pale aliposema: "Pindi mmoja
wenu anaposoma tahiyyatu ya mwisho basi ajikinge kwa Allah kutokana
na mambo manne ambayo ni:
(i) Adhabu ya moto wa jahannam
(ii) Adhabu ya kaburi
(iii) Fitna za uhai na umauti
(iv) Fitna za masihi dajali.

Katika riwaya nyingine bwana Mtume (Swallallahu Alayhi Wasallam)


amesema kwamba "Baada ya mtu kusoma attahiyyatu kabla ya salamu
basi na achague miongoni mwa dua ambayo atapendezwa nayo"52

(52)
Hadithi hii ni sahihi kaipokea Imamu Tirmidhiy kwa Namba 289.

28
Tatu: Watu wa kundi hili wanasema kila baada ya swala kumalizika
huwa hakuna dua bali ni dhikri maalumu (nyiradi).

Ushahidi wa hayo wanasema ni pale Allah anaposema:

٣٠١ :‫ﲍﱠ النساء‬


‫ﲎ‬ ‫ﭧﭐﭨﭐﱡﭐﲅﲆﲇﲈﲉﲊﲋﲌ‬

"Mkishamaliza kuswali basi mkumbukeni (mtajeni) Mwenyezi/Mungu


hali ya kuwa mmesimama na mkiwa mmekaa na mkiwa mmelala.”2

Pia wanasisitiza kwamba muumini anapokuwa ndani ya swala huwa


anaongea na Mola wake na ndiyo sehemu ambayo inapendeza zaidi
kuomba dua. Kwamba hakuna sababu ya kutoka nje ya maongezi na
muumba wako halafu ndipo uanze tena kumwomba!

Nne: Ni hadithi ya Mtume (Swallallahu Alayhi Wasallam) pale


alipoulizwa: "Ni dua gani yenye kujibiwa haraka? Akasema ni dua yenye
kuombwa usiku wa manane na dua inayoombwa nyuma ya kila baada
ya swala tano za faradhi.”53

Maana ya neno “nyuma” ya swala tano kusudio lake wanasema ni ndani


ya swala kabla ya kutoa salamu.

Amesema Allah Mtukufu wakati anasimulia kisa cha nabii yusuf (alayhi
salaam) :
٨٥ :‫ﱼ ﱠ يوسف‬
‫ﱽ‬ ‫ﭧﭐﭨﭐﱡﭐ ﱳ ﱴ ﱵ ﱶ ﱷ ﱸ ﱹ ﱺ ﱻ‬
"Na wote wawili wakakimbilia mlangoni na mwanamke akairarua
kanzu yake Yusuf kwa nyuma.”54

Hii ina maanisha nabii Yusuf ( Amani zimfikie ) alikuwa ameivaa kanzu
yake na ndiyo maana ikaweza kuraruliwa (kuchanwa) kwa nyuma.

Na kauli hii ni ya baadhi ya wafuasi wa madhehebu ya imamu Ahmed


ibun Hambali. Miongoni mwao ni Shekhe Al-Islam Ibun Taymiyah na
katika wanachuoni wa zama hizi ni pamoja na:

(53)
Ameipokea lmamu Tirmidhiy kwa namba 3499 na lmamu Annasai kwa namba 9936. Na ameisahihisha Sheikh al-Albaan
katika Sahihi Tirmidhiy kwa namba 3499.
(54)
Suuratu Yusuf (12:25)

29
1. Sheikh lbun Baaz.
2. Sheikh lbun Uthaymin.
3. Sheikh Al-Albaaniy (Allah awarehemu).
4. Vile vile ndiyo kauli ya Sheikh Fauzan (Allah amhifadhi).

Kauli ya pili:
Wanachuoni wa kauli hii ya pili wao wanaona dua husomwa ndani ya
swala na hata baada ya kutoa salamu, yaani baada ya kumalizika kwa
swala.

HOJA ZAO:
Mosi: Ni hadithi ya Mtume (Swallallahu Alayhi Wasallam) isemayo:
Mnamsabihi (Sub-haana Allah) na mnamshukuru (Alhamdulillah) na
mnatukuza (Allahu Akbar) nyuma ya kila swala mara thelathini na
tatu.55

Hadithi hii inamaanisha kuwa hizi nyiradi pamoja na dua husomwa


nyuma ya kila swala wakimaanisha baada ya kumalizika kwa swala.

Na amesema Mtume (Swallallahu Alayhi Wasallam) “Yeyote atakayesoma


Ayatul- kursiy nyuma ya kila swala ya faradhi, hakuna kitu
kinachomzuia kuingia peponi isipokuwa ni umauti.56
Swali la kujiuliza hapa ni, je, ayatul-kursiy na hizi nyiradi huwa
tunazisoma kabla ya kumalizika kwa swala au baada ya kumalizika kwa
swala?. Bila shaka jibu lake huwa tunasoma baada ya kumalizika kwa
swala kama alivyotuelekeza bwana Mtume Muhammad (Swalla Allahu
alayhi Wasallam).

Pili: Wanasema amesema Allah Mtukufu katika suuratul Asharhi 94:7:

٧ :‫ﭧﭐﭨﭐﱡﭐﱓﱔﱕﱖﱠ الرشح‬

"Na ukipata faragha basi fanya juhudi".

Imethibiti kutoka kwa lbun Abbasi pale alipotafsiri aya hii akasema:
"Ukipata faragha (muda) katika swala zako fanya juhudi maana yake ni

(55)
Hadithi ameipokea lmamu Muslim katika sahihi yake kwa namba 595
56
Hadithi hii ameipokea lmamu Annasai katika Sunanulkubraa kwa nambari 9848

30
kuzidisha dua na kumwomba Mola wako shida zako (iwe ndani ya swala
au nje).57

Tatu: Ama hoja yenu ya aya ya suratu annisai (103) kuwa hakuna dua
baada ya swala ila kuna dhikri (nyiradi) tu siyo sahihi, kwasababu aya
hii allah alikuwa anawazungumzia watu walioko vitani, Amesema sheikh
Assaadiy katika tafsiri ya aya hii: "Mtakapomaliza swala zenu (swala ya
khofu/vita) na swala nyingine basi mtajeni Allah katika kila hali zenu.

Na imewekwa haswa dhikri baada ya swala ya hofu kwa kuwa ina


sababu nyingi, miongoni mwazo ni kuwa hofu husababisha kudhoofika
kwa moyo, na pindi moyo ukidhoofika basi na mwili nao hudhoofika juu
ya kupambana na adui.

Lakini dhikri ya kumtaja Allah na kuvumilia wakati wa vita huleta


ushindi dhidi ya adui.

Amesema Allah katika Suuratul Anfal (8:45)


٤٥ :‫ﭧﭐﭨﭐﱡﭐ ﲷ ﲸ ﲹ ﲺ ﲻ ﲼ ﲽ ﲾ ﲿ ﳀ ﳁ ﳂ ﳃ ﱠ األنفال‬

"Enyi mlioamini mkikutana na jeshi basi kuweni imara na


mkumbukeni (mtajeni) Mwenyezi Mungu sana ili mpate kufanikiwa.”

Nne: Wanasema: Muumini ameamrishwa afanye dua akiwa ndani ya


swala na nje ya swala kwani dua ni ibada kama alivyosema Mtume
Muhammad (Swalla Allahu alayhi wasallam): " “Dua ni
lbada"58
Na Allah amesema katika suuratul ghaafir
٦٦ :‫ﭐﭧﭐﭨﭐﱡﭐ ﱍ ﱎ ﱏ ﱐ ﱑﱒ ﱠ اغفر‬

"Na amesema Mola wenu niombeni nitawajibu."

Na dua ni jambo la mustahabu (linapendeza) kwa imamu na maamuma


na kwa jamaa na hata kwa mmoja mmoja baada ya kumalizika kwa
57
Angalia Tafsiri ya lbun Kathir na tafsiri ya Qurtubi.
58
Hadithi hii imepokelewa na lmamu Bukhari katika kitabu chake cha al-Adabu lmufrad kwa nambari 714.

31
swala, na kumalizika kwa dhikri/nyiradi za baada ya swala, kuomba
hali ya kuwa umenyanyua mikono yako juu, kwa sababu kunyanyua
mikono ndiyo asili na ni katika sababu za kukubaliwa kwa hiyo dua.

Amesema Mtume (Swallallahu Alayhi Wasallam) "Hakika ya Allah ni


mwenye haya na anamwonea haya mja wake ambaye amenyanyua
mikono kwa kumwomba halafu airudishe patupu.59

Tano: Wanasema dua baada ya kumalizika swala inafaa kutokana na


hadithi ya Mtume (Swallallahu Alayhi Wasallam) pale alipomuusia
swahaba wake Muadhi (Radhi za Allah ziwe juu yake) kwa kumwambia
mara tatu: "Wallah mimi nakupenda ewe Muadhi usiache kusema kila
nyuma (baada ya kila swala):

“Ewe Mola wangu nisaidie ili nikutaje wewe, na nikushukuru wewe,


na nizifanye ibada zangu vizuri kwa ajili yako."60



INAFAA KUPANGUSA USO BAADA YA KUOMBA DUA?

Wanachuoni wametofautiana katika rai zao juu ya jambo hili. Na sababu


ya kutofautiana ni hadithi ifuatayo:

Amesema Bwana Mtume Muhammad (Swallallahu Alayhi Wasallam);


"Utakapomwomba Allah, basi omba kwa matumbo ya vitanga vya
mikono yako na wala usiombe kwa migongo ya vitanga vya mikono
yako, na utakapomaliza dua, basi pangusa uso wako kwa vitanga
hivyo."Hadithi hii ameipokea Abuu Daud na lbun Maajah.

Amesema Sheikh Al-islaam lbun Taymiyah (Allah amrehemu) "Kuhusu


Mtume (Swallallahu Alayhi Wasallam) kunyanyua mikono yake
katika dua, zimepokelewa hadithi nyingi zilizo sahihi katika jambo

59
Hadithi hii ameipokea lmamu Tirmidhiy na ameisahihisha Sheikh al-Albaani katika Sahihi Tirmidhiy kwa Nambari 3556.
60
Hadithi hii ameipokea Abuu Dauud na ameisahihisha Sheikh al-Albaani katika sahihi ya Abi Dauud kwa nambari 1522.

32
hilo. Ama kuhusu kupangusa uso hakuna isipokuwa hadithi moja au
mbili (zisizo sahihi) ambazo huwezi kusimamishia hoja, na Allah
ndiyo Mjuzi zaidi."

Angalia hii katika Fatawa Alkubraa, Juzuu ya 2, Ukurasa 219.

KAULI ZA WANACHUONI KUHUSU JAMBO HILI

1. Madhehebu ya Hanafi

Kupangusa uso baada ya dua kwao ni Sunnah kwa kauli iliyo sahihi.
Angalia kwenye kitabu cha Sherhe Al-haswkafiy, juzuu ya 1, ukurasa
507.

2. Madhehebu ya Maliki

Wao wanaona kuwa hupendeza kupangusa uso kwa mikono baada ya


dua kama alivyokuwa akifanya Bwana Mtume Muhammad (Swallallahu
Alayhi Wasallam). Angalia kitabu Alfawakihuddawany, juzuu ya 5,
ukurasa 335.

3. Madhehebu ya Shafii:

Wafuasi wa lmamu Shafii kupitia kwa lbun Hajar Al-haythami (Allah


amrehemu) katika Fatawa zake Amesema: "Kwenye hili sijaona kabisa
hadithi sahihi wala dhaifu baada ya kufanya juhudi za utafiti na
upekuzi, kwa hiyo haifai kulifanya."

Na katika kitabu Mughni Al-muhtaji, juzuu ya 4, ukurasa 370


pamesemwa haya: "Ama kupangusa uso baada ya dua nje ya swala,
amesema mwanazuoni lbun Abdissalam (Allah amrehemu) kuwa
jambo hili halifanywi ila kwa mtu mjinga."

33
4. Madhehebu ya Hambali

Katika kitabu cha Al-mughni, juzuu ya 1, ukurasa 449 tunasoma: "Sisi


tuna kauli ya Mtume (Swallallahu Alayhi Wasallam) ambayo
inaonesha kuwa alikuwa akinyanyua mikono yake wakati wa
kuomba dua na akimaliza anapangusa uso wake kwa mikono yake
(yaani ndani ya swala na nje ya swala).

Naye lmamu Al-Swanaani (Allah amrehemu) amesema: "Kuwekwa


sheria ya kupangusa uso kwa mikono miwili baada ya kumaliza dua,
pamesemwa hekima yake ni kwa kuwa Allah hairudishi mikono ya
mwenye kuomba dua patupu, basi ni kwamba mikono hiyo imepokea
baraka kutoka kwa Allah. Hivyo ikanasibu kuwa baraka hiyo ipakwe
usoni ambapo ni sehemu tukufu na yenye heshima katika mwili wa
mtu, na pia ina haki ya kuheshimika."

Angalia kitabu Subulu salaam, juzuu ya 4, ukurasa 427.

Amesema Sheikh lbun Uthaymin (Allah amrehemu): "Basi kwa mwenye


kuona hadithi hiyo ni sahihi itakuwa jambo hilo (kupangusa uso kwa
mikono) kwake ni Sunnah, na mwenye kuona kuwa hadithi hiyo
kwake ni dhaifu, basi itakuwa jambo hilo (kupangusa uso kwa
mikono) kwake ni bida'a (uzushi)."

Kwa hivyo basi katika jambo hili kumekuwa na kauli tatu baina ya
Wanazuoni (Allah awarehemu).

1. Kauli ya kwanza wao wanaona kuwa jambo hili ni Sunnah kwa kuwa
hadithi hiyo wanaiona kuwa ni sahihi.

2. Kauli ya pili wao wanaona kuwa jambo hili ni bida'a (uzushi)


kwakuwa hadithi hiyo wanaiona ni dhaifu.

3. Kauli ya tatu wao wanaona wala siyo bida'a (uzushi) bali ni Mubah
(inapendeza). Ukifanya hatuwezi kusema kuwa umefanya bida'a (uzushi)
na ukiacha inapendeza zaidi, lakini mwenye kupangusa hatutamlaumu
kwa kuwa anategemea hadithi iliyotajwa na ameiona kuwa kwake ni

34
sahihi. Na jambo hili ni katika mambo ambayo wanazuoni
wamehitilafiana.

Angalia kitabu Al-mumtii, juzuu ya 4, ukurasa 41.

Na amesema Sheikh Fauzaan (Allah amuhifadhi) "Mwenye kupangusa


uso wake hatumlaumu kwani Jambo hili lina mlango mpana."

Angalia katika Alfatawa, juzuu ya 26, ukurasa 148.



35
HITIMISHO
Amesema mwanachuoni, sheikh Ibn Uthaymin kwamba "Baada ya
kubainisha kuwa dua baada ya swala za faradhi ni bida'a (uzushi) na
wala haifai, akauliza muulizaji: “Itakapokuwa mwenye kufanya hivi ni
mtu mzima (imamu) je, nimchukie? Akajibu Sheikh lbun Uthaymin
kwamba msemeshe kwa hekima na wala usimchukie kwa kuwa si
haramu, bali kinyume chake (kuacha) ni bora zaidi.

Katika kumalizia: Hakika mfano wa masuala kama haya haifai


yasababishe kuleta mpasuko baina ya waislamu na kunyanyua sauti za
hasira na kuvimbisha mishipa ya shingo hadi kufikia kuhamana baina
ya ahlusunnah waljamaa, kwani ni masuala yenye „hitilafu‟ na hivyo
kinachofaa ni kuvumiliana.

Anasema Sheikh al-Islaam lbun Taymiyah: "Na kwa hili wanasema


wanachuoni wenye kusifika katika kuamrisha mema na kukataza
mabaya katika watu wa Shafii na wengineo; Hakika ya mfano wa
masuala haya yenye jitihada ndani yake, huwa hayapingwi kwa mkono
na hatakiwi yeyote kulazimisha watu wafuate msimamo wake katika
masuala yenye hitilafu, badala yake huzungumzwa kwa hoja za kielimu.

Kwa msingi huo atakayebainikiwa na usahihi wa moja ya hoja kati ya


kauli mbili atafuata hiyo, na atakayefuata kauli ya pili hatakiwi
kuchukiwa.”61

Na akasema tena Shekhe:

Maana yake: "Kama ingelikuwa kila walilohitilafiana waisilamu wawili


(Ahlusunna wal-jamaa) likasababisha kuhamana, basi pasingelibaki
baina ya waisilamu udugu wa kiimani na mshikamano ." 62


61 kitabu Majumua cha lbun Taymiyah, Juzuu ya 30, uk 80.


62
/Majumui fatawa ya ibn Taymiya 24/ 173.

36
REJEA

 Qur-ani tukufu.
 Hadithi za mtume Muhammad (Swallallahu alayhi
wasallam)
 Tafsir Ibun Kathir (Ibun Kathir)
 Tafsiri al-Qurtubiy (Imamu Qurtubiy)
 Fat-hul baary (Ibun Hajar al-As-Qalaniy)
 Al-ummu cha (lmamu Shafii).
 Taarikhu Baghdadi (Al-Khatwib Baghadad).
 Siyar A’alam Annubalaa (Imamu Dhahaby).
 Majumua Fatawa (Ibun Taymiyah).
 Al-Adabu Sharia (Ibun Taymiyah).
 Liqaati Babu Maftuuh (Ibun Uthaymin).
 Zaadulmaad (Ibun Qayim).
 Al-majmuua (Imamu Annawawiyyu) .
 Raudwatu Atwaalibiin (imamu Nnawawiy)



37

You might also like