Professional Documents
Culture Documents
TCRA Communications Statistics For Q3 2023-2024 KSW - 1715007469
TCRA Communications Statistics For Q3 2023-2024 KSW - 1715007469
Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania
Takwimu za
Mawasiliano
Robo mwaka inayoishia Machi 2024
www.tcra.go.tz
ISO 9001: 2015 CERTIFIED
1
ISO 9001: 2015 CERTIFIED
Takwimu zimeandaliwa kulingana na viwango vya Umoja wa Mawasiliano Duniani (ITU) vya
kukusanya na kuandaa takwimu za huduma za mawasiliano/TEHAMA.
2
ISO 9001: 2015 CERTIFIED
Yaliyomo
1 Takwimu za Huduma za Mawasiliano ya Simu 1
1.1 Takwimu za usajili wa laini za Simu 5
1.2 Takwimu za bei za huduma za mawasiliano ya simu 6
1.3 Takwimu za dakika za huduma ya sauti 9
1.4 Takwimu za SMS 13
1.5 Idadi ya mitambo ya kurushia mawimbi ya simu (BTS) ki-mkoa 16
2 Takwimu za Pesa Mtandao 18
2.1 Usajili wa pesa mtandao 18
2.2 Idadi ya usajili na miamala ya pesa mtandao 19
3 Takwimu za Huduma ya Intaneti 20
3.1 Usajili wa huduma ya Intaneti 20
3.2 Matumizi ya mwezi ya huduma ya Intaneti 21
3.3 Uwezo wa kuunganisha huduma ya Intaneti (Internet link capacity) 21
3.4 Usimikaji na ubora wa kasi ya huduma ya Intaneti 22
3.5 Takwimu za Vikoa 23
4 Takwimu za Huduma za Utangazaji 24
4.1 Ving’amuzi vinavyotumika 24
4.2 Mabadilliko ya idadi ya ving’amuzi kwa robo mwaka 24
4.3 Idadi ya ving’amuzi vilivyotumika kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita 26
4.4 Usajili wa televisheni kwa njia ya waya (Cable TV) 26
4.5 Idadi ya televisheni ka njia ya waya kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita 28
4.6 Ueneaji wa huduma za utangazaji 28
5 Takwimu za Huduma za Posta na Usafirishaji (Courier) 29
5.1 Usajili kwa vipokezi vya posta 29
5.2 Wateja wa huduma ya usafirishaji 29
5.3 Vitu vilivyotumwa ndani ya nchi 30
5.4 Vitu vilivyotumwa nje ya nchi 31
5.5 Vitu vilivyopokelewa kutoka ndani ya nchi 32
5.6 Idadi ya vitu vilivyopokelewa kutoka nje ya nchi 32
5.7 Idadi ya vitu vilivyotumwa ndani na nje ya nchi kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita 33
5.8 Idadi ya vitu vilivyotumwa nje ya nchi na kupokelewa kutoka nje ya nchi 33
6 Takwimu za Ubora wa Huduma na Majaribio ya Ulaghai/uhalifu Mtandaoni 34
6.1 Ubora wa huduma (QoS) 34
6.2 Majaribio ya ulaghai/uhalifu mtandaoni 35
7 Idadi ya Leseni na Vyeti 44
7.1 Leseni 44
8 Hitimisho 46
i
ISO 9001: 2015 CERTIFIED
1. Takwimu za Huduma za
Mawasiliano ya Simu
Takwimu za huduma za mawasiliano ya simu kuhusu usajili, bei, dakika za simu, ujumbe mfupi (SMS) na
vifaa vya mawasiliano zimeainishwa kwa mwezi, robo mwaka na mwaka.
Jumla ya idadi ya laini zilizosajiliwa imeongezeka kutoka milioni 70.3 katika robo ya mwaka iliyoishia Disemba
2023 hadi milioni 72.5 kwa robo inayoishia Machi 2024. Hilo ni ongezeko la asilimia 3.1 kama inavyoonekana
hapo chini.
Disemba 2023 Machi 2024
Jedwali 1.1.1 Idadi ya laini za simu za mkononi na mezani za P2P zilizosajiliwa kwa kila
mtoa huduma
Airtel Halotel Tigo TTCL Vodacom Jumla
Takwimu katika Jedwali 1.1.1 zinaonesha ongezeko la wastani la kila mwezi la 1.7% la usajili wa laini za simu
za mkononi na mezani ndani ya robo ya mwaka iliyoishia Machi 2024.
1.1.2 Usajili wa laini za simu kwa ajili ya P2P na M2M kwa kila mtoa huduma
Jedwali 1.1.2 linaonesha laini zilizosajiliwa kwa mawasiliano ya P2P na M2M kwa robo ya mwaka iliyoishia
Machi 2024.
Jedwali 1.1.2 Idadi ya laini za P2P na M2M zilizosajiliwa
1
ISO 9001: 2015 CERTIFIED
Jedwali 1.1.2 linaonesha kuwa laini zilizosajiliwa kufikia mwishoni mwa Machi 2024 zilikuwa takriban laini za
simu laki tisa kwa ajili ya mawasiliano ya M2M nchini ambayo ni sawa na 1.3%, wakati usajili wa laini za P2P
ukiwa 98.7% ya usajili wote.
Hata hivyo, kwa usajili wa M2M, Vodacom ana 56.2% ya laini zote zilizosajiliwa kama inavyoonekana kwenye
Chati 1.1.3b. Airtel inashika nafasi ya pili kwa 34.5%, ikifuatiwa na Halotel kwa 6.0%.
26.4% Airtel
30.5% Airtel
Halotel
34.5% Halotel
Tigo Tigo
TTCL
56.2% TTCL
Vodacom
12.8% Vodacom
6.0%
2.3%
28.0%
2.7%
0.7%
1.1.5 Mabadiliko ya usajili ya kila robo mwaka kwa kila mtoa huduma
Kulikuwa na ongezeko la usajili wa laini za P2P katika robo ya mwaka inayoishia Machi 2024 la takriban
milioni 2.2 ikilinganishwa na ongezeko la milioni 3.2 iliyorekodiwa katika robo ya mwaka iliyoishia Disemba
2023. Chati 1.1.5a inaonesha mabadiliko hayo.
2
ISO 9001: 2015 CERTIFIED
Mabadiliko
Chati 1.1.5a Mabadiliko ya usajili
ya usajili wawa
lainiP2P yakatika
za P2P roborobo
ya ya
tatu
tatu2024 kwa kwa kila
ya 2023/2024
mtoa huduma
kila mtoa huduma.
-1,134
2.2
Airtel
Halotel 768,823
Milioni
Tigo 577,251 Ongezeko la usajili
wa laini za P2P
TTCL 25,803
Vodacom 834,476
Chati 1.1.5b Mabadiliko ya usajili wa laini za M2M katika robo ya tatu ya 2023/2024 kwa
Mabadiliko ya usajili wa M2M ya robo ya tatu 2024 kwa
kila mtoa huduma
kila mtoa huduma.
Airtel 8,586
Halotel 55,350
Tigo -112
103,970
TTCL 488 Ongezeko la usajili
wa laini za M2M
834,476
Vodacom 39,658
Mikoa yenye laini chache zilizosajiliwa katika robo ya tatu ya 2024 ni Kaskazini Unguja yenye laini 66,277,
Kusini Unguja yenye laini 99,736, na Kusini Pemba yenye laini 111,871.
3
ISO 9001: 2015 CERTIFIED
ChatiUsajili wawalaini
1.1.6 Usajili zasimu
laini za simu za mkononi
za mkononi na mezanina mezani
ki-mkoa kwa mkoa
Mwanza 4,803,249
Arusha 4,364,431
Mbeya 4,171,381
Dodoma 3,869,789
Morogoro 3,644,014
Tabora 3,506,194
Kilimanjaro 2,797,087
Tanga 2,675,465
Geita 2,417,513
Pwani 2,381,767
13.3
Mtwara 2,014,202
Mara 1,806,790
Kagera 1,784,059
Iringa 1,692,084
Singida 1,686,139
Simiyu 1,666,313
Kigoma 1,446,809
Songwe 1,406,743
Njombe 1,275,338
Lindi 1,259,976
Rukwa 1,190,756
Katavi 749,433
7 4
ISO 9001: 2015 CERTIFIED
Ramani 1.1.6 Mgawanyo wa laini za simu za mkononi na mezani ki-mkoa hadi Machi 2024
1.1.6 Telecom subscriptions shares by region as of March 2024
Mwanza
6.63%
Mara
Kagera
Shinyanga 2.49%
2.46%
2.71%
Arusha
Simiyu 6.02%
Geita
2.30%
3.33%
Kilimanjaro
3.86%
Kigoma Manyara
2.00% 2.50%
Tanga Kaskazini Pemba 0.15%
Tabora
3.69% Kusini Pemba 0.15%
4.84%
Singida
Kaskazini Unguja 0.09%
2.33% Dodoma
Kusini Unguja 0.14%
Katavi 5.34% Mjini Magharibi 0.63%
1.03%
Dar es salaam 18.41%
Morogoro
Pwani
Iringa 5.03%
3.29%
Rukwa 2.33%
Mbeya
1.64%
5.75%
Ufunguo Songwe
0-5 Njombe Lindi
1.76% 1.74%
6-10
1.94%
11-15
Ruvuma
Mtwara
16-20 2.64%
2.78%
Mgawanyo wa laini za simu za mkononi na mezani kwa kila mkoa umeoneshwa kwenye Ramani 1.1.6.
Mgawanyo huo unaonesha kuwa Dar es Salaam inaongoza kwa kuwa na 18.4% ya laini ikifuatiwa na Mwanza
yenye 6.6%, Arusha yenye 6.0% na Mbeya yenye 5.8% ya laini zilizosajiliwa.
Mikoa yenye asilimia ndogo za laini kwa Tanzania Bara ni Katavi (1.03%), Rukwa (1.64%) na Lindi (1.74%), na
kwa Zanzibar ni Kaskazini Unguja (0.09%), Kusini Unguja (0.14%) na Kusini Pemba (0.15 %).
1.1.7 Usajili wa laini za simu katika kipindi cha miaka mitano iliyopita
Mwenendo wa usajili wa laini za simu za mawasiliano ya P2P kwa miaka mitano iliyopita hadi 2023
umeoneshwa katika Jedwali 1.1.7.
5
ISO 9001: 2015 CERTIFIED
Takwimu katika Jedwali 1.1.7 zinaonesha ongezeko la laini za simu kwa wastani wa 10% kwa mwaka na
ongezeko la wastani wa kiwango cha kupenya (penetration) cha 9% kwa mwaka. Kiwango cha kupenya kwa
huduma za mawasiliano ya simu hadi Disemba 2023 kilifikia 111%, ikimaanisha kuwa wakazi 10 walitumia
laini 11 kwa huduma za mawasiliano ya simu.
Kama inavyooneshwa katika muhtasari hapo juu, wakati bei za kupiga simu ndani ya mtandao, nje ya
mtandao, SMS kitaifa (local SMS) na data hazikubadilika, bei za kupiga simu za kimataifa zilipungua kwa 3%
na bei za SMS kimataifa ziliziongezeka kwa 15%.
Jedwali 1.2.1 linaonesha kuwa watoa huduma wote hutoza TZS 30 kwa dakika moja ndani na nje ya mtandao,
isipokuwa Halotel inayotoza TZS 10 kwa dakika moja ndani ya mtandao na TZS 20 nje ya mtandao. Wastani
wa bei ya huduma ya sauti ndani ya mtandao katika robo ya mwaka inayoishia Machi 2024 ilibaki sawa na
robo ya mwaka inayoishia Disemba 2023.
9 6
ISO 9001: 2015 CERTIFIED
Jedwali 1.2.1 pia, linaonesha kuwa bei ya huduma ya sauti kimataifa zilitofautiana baina ya watoa huduma.
Wastani wa bei ya huduma ya sauti kwa dakika moja kwa Afrika Mashariki na nchi nyingine ni TZS 727.80 na
1,899.00, mtawalia.
Wastani wa bei za SMS kitaifa (TZS 7.80) na data (TZS 9.35) kwa Machi 2024 zilibakia kama zilivyokuwa
kwenye robo ya mwaka iliyoishia Disemba 2023. Hata hivyo, wastani wa bei ya SMS za kimataifa kwa Sekta
imebadilika hadi TZS 189.60 kutoka TZS 164.40 iliyorekodiwa katika robo ya mwaka iliyoishia Disemba 2023.
Kielelezo hapo juu kinaonesha kuwa bei za huduma za mawasiliano ya simu katika vifurushi zimebadilika
katika robo mwaka inayoishia Machi 2024 ikilinganishwa na robo mwaka inayoishia Disemba 2023. Bei za
huduma ya sauti ndani na nje ya mtandao, na SMS zilipungua kwa viwango tofauti, huku bei ya data katika
kifurushi iliongezeka kwa 2.8%.
Jedwali 1.2.3 linaonesha kuwa wastani wa bei za huduma za mawasiliano ya simu katika kifurushi ziko chini
kuliko bei za huduma za mawasiliano ya simu bila kifurushi.
7
ISO 9001: 2015 CERTIFIED
Wastani wa bei za huduma ya sauti ndani na nje ya mtandano kwa Sekta imepungua hadi TZS 4.50 na TZS
6.07 kwa dakika, mtawalia, katika robo mwaka inayoishia Machi 2024, kutoka TZS 4.89 na TZS 6.26 katika
robo mwaka inayopita. Aidha, bei ya SMS katika kifurushi ilipungua kwa 0.6% na data iliongezeka kwa 2.8%.
Jedwali 1.2.4 linaonesha kuwa wastani wa bei za huduma ya mawasiliano ya simu bila kifurushi ni karibu
mara tano zaidi ya wastani wa bei katika kifurushi. Hiyo ndiyo sababu ya watumiaji wengi (99.9%) kupendelea
kujiunga na huduma za vifurushi.
1.2.5 Wastani wa bei za huduma za mawasiliano ya simu bila kifurushi kwa Sekta
katika kipindi cha miaka mitano iliyopita
Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, mwenendo wa wastani wa bei za huduma za sauti na SMS bila
kifurushi kwa Sekta, kitaifa na kimataifa umeoneshwa kwenye Jedwali 1.2.5a, 1.2.5b na 1.2.5c.
Jedwali 1.2.5a Mwenendo wa wastani wa bei za huduma za sauti kwa miaka mitano
iliyopita
Jedwali la 1.2.5a linaonesha kuwa wastani wa bei za huduma za sauti kwa dakika ndani na nje ya mtandao
zilipungua kati ya mwaka 2019 hadi Disemba 2023. Aidha, gharama hizo zililingana kuanzia mwaka 2020
hadi Disemba 2022. Ulinganifu huo ulisababishwa na kushuka kwa gharama za muingiliano wa mawasiliano
ya simu za sauti (interconnection charges) baina ya watoa huduma katika kipindi hicho.
Jedwali 1.2.5b Mwenendo wa wastani wa bei za huduma za sauti kimataifa kwa miaka
mitano iliyopita
Jedwali 1.2.5b linaonesha kuwa kuna mienendo tofauti ya wastani wa bei za huduma za sauti kimataifa
kutokana na viwango vya tozo za huduma za mawasiliano vinavyowekwa na watoa huduma wa kimataifa.
11 8
ISO 9001: 2015 CERTIFIED
Jedwali 1.2.5c Mwenendo wa wastani wa bei za kutuma SMS kitaifa na kimataifa katika
kipindi cha miaka mitano iliyopita
Pia, katika kipindi cha miaka minne iliyopita mwenendo wa wastani wa bei za huduma za mawasiliano
katika vifurushi umeoneshwa kwenye Jedwali 1.2.5d.
Robo mwaka inayoishia Disemba 2023 Robo mwaka inayoishia Machi 2024 Badiliko
Jedwali 1.3.1 linaonesha kuwa Januari 2024 ulikuwa mwezi wenye idadi ya dakika nyingi zaidi ikilinganishwa
na miezi mingine ya robo mwaka huo.
9
ISO 9001: 2015 CERTIFIED
Jedwali 1.3.1 linaonesha takriban dakika bilioni 35 zilitumika katika robo mwaka iliyoishia Machi 2024
ikilinganishwa na dakika bilioni 39 katika robo mwaka iliyoishia Disemba 2023. Hata hivyo, idadi ya dakika
ndani ya mtandao ilikuwa kubwa zaidi ikilinganishwa na nje ya mtandao kitaifa katika robo mwaka inayoishia
Machi 2024.
Mgawanyo wa dakika ndani na nje ya mtandao nchini zinaoneshwa kwenye Chati 1.3.1.1a.
53% 47%
Ndani
Nje ya ya mtandao Ndani Nje
mtandao ya mtandao
ya mtandao
Chati 1.3.1.1a inaonesha kuwa dakika nyingi za sauti nchini zilitumika kwenye simu za ndani ya mtandao
(53%) kuliko simu za nje ya mtandao (47%). Takwimu zinaonesha kuwa watu walipendelea kupiga simu
ndani ya mtandao mmoja.
Mgawanyo wa dakika ndani na nje ya mtandao nchini kwa kila mtoa huduma umeoneshwa kwenye Chati
1.3.1.1b na 1.3.1.1c. Airtel imeongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya dakika za ndani na nje ya mtandao nchini.
Chati 1.3.1.1b Mgawanyo wa dakika ndani Chati 1.3.1.1c Mgawanyo wa dakika nje ya
ya mtandao kwa kila mtoa huduma mtandao kwa kila mtoa huduma
32.05% 25.93%
30.43%
23.51%
TTCL
0.20%
0.71%
6.17%
15.54%
27.39%
38.07%
13 10
ISO 9001: 2015 CERTIFIED
Jedwali 1.3.1.2 Idadi ya dakika ndani ya nchi kwa miaka mitano iliyopita
Jedwali 1.3.1.2 linaonesha kuwa idadi ya dakika ndani ya mtandao ni kubwa ikilinganishwa na idadi ya
dakika nje ya mtandao nchini. Hata hivyo, tofauti ya dakika hizo imeendelea kupungua kutokana na watoa
huduma kutumia karibu viwango sawa vya bei za kupiga simu.
Kielelezo kinaonesha ongezeko la idadi ya dakika kwenda na kutoka nje ya nchi katika robo mwaka inayoishia
Machi 2024. Idadi ya dakika kwenda nje ya nchi iliongezeka kwa 108.9%. Kwa upande mwingine, kulikuwa na
ongezeko la 111.7% kwa idadi ya dakika kutoka nje ya nchi. Vilevile, takwimu zinaonesha kulikuwa na idadi
kubwa ya dakika kwenda nje ya nchi ikilinganishwa na zilizotoka nje ya nchi.
Jumla ya dakika kwenda na kutoka Afrika Mashariki na nchi nyingine za kimataifa kwa robo mwaka
inayoishia Machi 2024 imeoneshwa katika Jedwali 1.3.2.
11
ISO 9001: 2015 CERTIFIED
Jedwali 1.3.2 linaonesha kulikuwa na dakika nyingi zaidi kwenda na kutoka EA na RoW katika mwezi Machi
2024 ikilinganishwa na miezi mingine ya robo inayoishia Machi 2024.
27%
73%
Kwenda EA
Kutoka EA Kutoka
Kwenda EA EA
Chati 1.3.2.1 inaonesha kuwa dakika kwenda EA ni mara 2.7 ya dakika kutoka EA.
28.5%
71.5%
Kwenda RoW
Kwenda RoW KutokaKutoka
RoW RoW
1.3.2.3 Idadi ya dakika kwenda na kutoka EA na RoW kwa miaka mitano iliyopita
Mwenendo wa idadi ya dakika kwenda na kutoka EA na RoW umeoneshwa katika Jedwali 1.3.2.3.
Jedwali 1.3.2.3 Idadi ya dakika kwenda na kutoka EA na RoW kwa miaka mitano iliyopita
12
ISO 9001: 2015 CERTIFIED
Kama inavyooneshwa katika Jedwali 1.3.2.3, idadi kubwa ya dakika zinakuja kutoka EA na RoW kuliko kwenda
katika maeneo hayo isipokuwa mwaka 2023. Aidha, dakika za kwenda na kutoka EA na RoW zimekuwa
zikipungua, isipokuwa mwaka 2023.
Kielelezo kinaonesha kupungua kwa idadi ya SMS katika robo inayoishia Machi 2024 kwa 0.2% kwa SMS
zinazotumwa ndani ya mtandao na 1.4% kwa SMS zinazotumwa kutoka mtandao mmoja kwenda mitandao
mingine. Kwa ujumla, idadi ya SMS ilipungua kwa 1%.
Idadi ya SMS kwa robo mwaka inayoishia Machi 2024 imeainishwa kwenye Jedwali 1.4.1.
Jedwali 1.4.1 linaonesha mabadiliko ya idadi ya SMS ndani na nje ya mtandao katika kipindi husika. Mwezi
Machi 2024 ulikuwa na idadi kubwa ya SMS ikilinganishwa na Januari na Februari ya mwaka huo.
Kwa kipindi chote, mgawanyo wa SMS nje ya mtandao ulikuwa mkubwa (59%) kuliko ndani ya mtandao
(41%). Hii inaonesha kuwa katika kipindi hicho, SMS nyingi zilitumwa kwenda nje ya mtandao. Mgawanyo
wa SMS ndani na nje ya mtandao imeoneshwa kwenye Chati 1.4.1.
Asilimia ya meseji za ndani na nje ya mtandao
Chati 1.4.1 Mgawanyo wa SMS ndani na nje ya mtandao
41% 59%
13
ISO 9001: 2015 CERTIFIED
Jedwali 1.4.2 Idadi ya SMS za ndani ya nchi kwa miaka mitano iliyopita
Jedwali 1.4.3 linaonesha idadi kubwa ya SMS ilipokelewa kutoka RoW kuliko zilizotumwa RoW. Aidha, idadi
kubwa ya SMS ilipokelewa kutoka EA na RoW kwa mwezi Machi 2024 kuliko miezi mingine katika kipindi
husika. Uwiano wa SMS zilizotumwa na kupokelewa umeoneshwa kwenye Chati 1.4.3a na 1.4.3b.
98.1% 99.9%
14
ISO 9001: 2015 CERTIFIED
1.4.4 Idadi ya SMS kwenda na kutoka EA na RoW kwa miaka mitano iliyopita
Idadi ya SMS kwenda na kutoka EA na RoW kwa miaka mitano iliyopita imeoneshwa katika Jedwali 1.4.4.
Jedwali 1.4.4 Idadi ya SMS kwenda na kutoka EA na RoW kwa miaka mitano iliyopita
Kufikia Machi 2024, asilimia ya simu janja (smartphones) kwa idadi ya watu imeongezeka hadi 32.59%
kutoka 32.13% iliyorekodiwa mwishoni mwa Disemba 2023. Aidha, asilimia ya simu za rununu (feature
phones) kwa idadi ya watu imepungua kutoka 85.62% mwishoni mwa Disemba 2023 hadi 85.56% Machi
2024. Asilimia za vifaa vingine kwa idadi ya watu zimeoneshwa kwenye Jedwali 1.5.
15
ISO 9001: 2015 CERTIFIED
1.6 Idadi ya mitambo ya kurushia mawimbi ya simu (Base Transceiver Stations - BTS)
ki-mkoa
Jedwali 1.6 linaonesha idadi ya BTS katika mikoa mbalimbali ya Tanzania, likionesha kiwango cha usimikaji
wa mitambo ya 2G, 3G, 4G na 5G hadi Machi 2024.
2G 3G 4G 5G
Tanzania Bara
Zanzibar
Kaskazini Pemba 62 61 56 0
Kaskazini Unguja 79 81 78 2
Kusini Pemba 57 57 55 1
Kusini Unguja 114 114 113 2
Mjini Magharibi 175 202 196 37
16
ISO 9001: 2015 CERTIFIED
Jedwali 1.6 linaonesha kuenea kwa kiasi kikubwa kwa teknolojia ya 2G na 3G, ikiwa na BTS 13,205 na 12,026,
mtawalia. Japokuwa teknolojia ya 4G haijaenea kama 2G na 3G, idadi ya BTS za 4G zimefika 11,225. Aidha,
BTS za 5G zimefika 638. BTS hizo zimeenea zaidi katika maeneo ya mijini kama vile Dar es Salaam na Mjini
Magharibi. Hata hivyo, Dar es Salaam inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya BTS za teknolojia zote (2G, 3G,
4G na 5G), na kuifanya kuwa kitovu cha mawasiliano nchini.
17
ISO 9001: 2015 CERTIFIED
40 Sh Sh
0.2%
20
Milioni Milioni
52.9 53.0
0
Disemba 2023Sales ($) Machi 2024
Jedwali 2.1 linaonesha kuwa akaunti za pesa mtandao ziliongezeka kwa wastani wa asilimia 0.02 kwa mwezi
katika robo mwaka iliyoishia Machi 2024. Mgawanyo wa akaunti za pesa mtandao umeoneshwa kwenye
Chati 2.1.
Mgawanyo wa asilimia za usajili wa Pesa Mtandao
Chati 2.1 Mgawanyo wa akaunti za pesa mtandao
3%
8%
M-Pesa
89%
Zaidi ya
ya usajili wa Pesa
Tigo Pesa Mtandao umetawaliwa
20% 38% na M-Pesa, Tigo Pesa
Sh Airtel Money na Airtel money
Halo Pesa
T-Pesa
31%
18
ISO 9001: 2015 CERTIFIED
Chati 2.1 inaonesha kuwa soko la pesa mtandao lina ushindani, na M-Pesa iliongoza kwa kuwa na 38% ya
usajili.
Kama inavyooneshwa katika Jedwali 2.2a, idadi ya miamala ya pesa mtandao kwa robo inayoishia Machi
2024 imekuwa ikiongezeka kwa wastani wa 1.58% kwa mwezi. Pia, miamala ya pesa mtandao ilipungua
kutoka 549,529,470 katika robo inayoishia Disemba 2023 hadi 473,163,645 kwa robo inayoishia Machi 2024.
Table 2.2b Idadi ya usajili na miamala ya pesa mitandao kwa miaka mitano iliyopita
Miamala ya pesa mtandao kwa miaka mitano iliyopita, kama inavyooneshwa kwenye Jedwali 2.2b,
iliongezeka kutoka bilioni 3 mwaka 2019 hadi bilioni 5.3, sawa na 19% ya ukuaji kwa kila mwaka. Katika
kipindi hicho, wastani wa miamala kwa kila mteja ulipungua kutoka miamala 117 mwaka 2019 hadi 100
mwaka 2023.
19
ISO 9001: 2015 CERTIFIED
3. Takwimu za huduma ya
Intaneti
3.1 Laini za Intaneti
Idadi ya laini za Intaneti inatokana na laini ambazo zimetumia huduma ya Intaneti angalau mara moja
katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita, bila kujali teknolojia iliyotumika (FTTX, 2G - GPRS na EDGE, 3G, 4G,
au 5G).
Idadi ya laini za Intaneti iliongezeka kutoka milioni 35.9 kwa robo mwaka iliyoishia Disemba 2023 hadi
milioni 36.8 kwa robo mwaka iliyoishia Machi 2024 kama inavyooneshwa hapo chini.
Jedwali 3.1b Idadi ya laini za Intaneti kwa teknolojia katika robo mwaka inayoishia Machi
2024
Teknolojia Usajili
2G 12,256,233
Jumla 36,771,612
Jedwali 3.1b linaonesha kuwa Intaneti ya simu ndiyo njia maarufu zaidi ya kupata Intaneti, ikiwa na laini
24,431,561. Teknolojia ya 2G bado ina matumizi makubwa, ikiwa na laini 12,256,233. Teknolojia za Faiba
Nyumbani (Fiber to the Home - FTTH) na Faiba Ofisini (Fiber to the Office - FTTO) zina idadi ndogo ya laini
49,163 na 5,126, mtawalia.
Idadi ya laini za Intaneti kwa miaka mitano iliyopita imeoneshwa kwenye Chati 3.1.
20
ISO 9001: 2015 CERTIFIED
Chati 3.1 Idadi ya laini zinazotumia huduma ya Intaneti kwa miaka mitano iliyopita
9.8%
Wastani wa kiwango
cha ukuaji katika usajili
wa huduma ya intaneti
kwa kipindi cha miaka
mitano iliyopita.
Chati 3.1 inaonesha wastani wa ongezeko la kila mwaka la 9.8% la idadi ya laini zinazotumia huduma ya
Intaneti kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita. Laini zinazotumia Intaneti ziliongezeka kutoka milioni 25.8
mwaka 2019 hadi milioni 35.9 mwaka 2023.
299 335
Petabytes
Disemba 2023
Petabytes
Machi 2024
12%
Jedwali 3.2 Kiasi cha data kilichotumika katika robo mwaka iliyoishia Machi 2024
Jedwali 3.2 linaonesha kuwa kila mteja alitumia wastani wa MB 3,714 kwa mwezi Machi, ambayo ni ya juu
kuliko Januari na Februari 2024.
21
ISO 9001: 2015 CERTIFIED
3G 86% 88%
Asilimia ya watu
waliofikiwa na Intaneti ya 4G 79% 80%
kasi (3G, 4G au zaidi)
5G - 13%
3G 70% 72%
Asilimia ya eneo
lilofikiwa na Intaneti ya kasi 4G 63% 64%
(3G, 4G au zaidi)
5G - 1%
Jedwali 3.4, linaonesha kupanuka kwa wigo wa 3G, 4G na 5G kufikia 88%, 80% na 13% ya watu nchini,
mtawalia. Pia, asilimia ya eneo lilofikiwa na Intaneti ya kasi 3G, 4G na 5G ni 72%, 64% na 1%, mtawalia.
22
ISO 9001: 2015 CERTIFIED
ne.tz 34 35
me.tz 10 8
info.tz 4 3
hotel.tz 3 3
Mobi.tz 5 5
tv.tz 4 5
mil.tz 4 3
23
ISO 9001: 2015 CERTIFIED
4. Takwimu za Huduma za
Utangazaji
Sehemu hii inawasilisha takwimu za usajili wa huduma za televisheni kwa njia ya mitambo iliyosimikwa
ardhini (DTT), satilaiti (DTH) na kwa njia ya waya (Cable TV) pamoja na asilimia ya watu waliofikiwa na
huduma za utangazaji.
Vilevile, idadi ya visimbuzi vinavyotumika kwa Multichoice (DStv), Star Media na Zuku imepungua. Hakukuwa
na badiliko kwa visimbuzi vya Agape na BTL kwa kipindi husika. Mabadiliko hayo yameoneshwa katika
Chati 4.2.
27 24
ISO 9001: 2015 CERTIFIED
Azam 142,284
BTL 0
CONTINENTAL 58
MULTICHOICE -6,882
90,194
Idadi ya visimbuzi
vilivyoongezeka kwa
robo mwaka
Star Media -38,204 iliyoishia Machi
2024
ZUKU -7, 062
JUMLA
TOTAL 90, 194
Mara
78,669
Kagera Shinyanga
83,476 Arusha 67,359
Simiyu
Geita 13,830 296,075 Kilimanjaro
153,787
42,069
Kigoma
49,909 Manyara
Tabora 25,470
Kaskazini Pemba 2,902
63,284 Tanga
Kusini Pemba 3,102
108,782
Singida
Dodoma Kaskazini Unguja 315
46,362
Katavi Kusini Unguja 1,653
169,543
19,246 Morogoro Mjini Magharibi 110,063
150,111 Dar es Salaam1,429,580
Iringa
Pwani
Mbeya 75,428
Rukwa 61,627
233,311
20,293
Songwe
Njombe Lindi
25,084
Ufunguo 1,514
27,167
0-100,000
Ruvuma
100,001 - 1,000,000 59,115 Mtwara
38,493
1,000,001 - 10,000,000
25
ISO 9001: 2015 CERTIFIED
1,880,636
1,781,340
1,702,877
1,667,465
1,613,031
1,577,315
1,472,317
1,432,398
1,341,686
1,092,891
DTT DTH
Kuna ongezeko la visimbuzi kwa njia ya antena na dishi kama ilivyooneshwa kwenye Chati 4.3, ambapo
mwaka 2023 kulikuwa na idadi kubwa ya visimbuzi vilivyotumika.
Idadi ya usajili wa televisheni kwa njia ya waya ki-mkoa katika kipindi husika umeoneshwa kwenye Chati
4.4.
29 26
ISO 9001: 2015 CERTIFIED
Shinyanga 3,450
Mwanza 1,875
Tabora 1,290
Dodoma 940
Geita 923
Singida 680
50%
Nusu ya idadi ya usajili
wa televisheni kwa njia
Mara 670 ya waya unapatikana
Shinyanga, Mwanza,
Songwe 598 Tabora na Dar es
Salaam
Arusha 590
Kagera 585
Simiyu 507
Manyara 407
Rukwa 353
Njombe 281
Mbeya 275
Ruvuma 268
Tanga 240
Kigoma 200
Iringa 196
Katavi 185
27
ISO 9001: 2015 CERTIFIED
4.5 Idadi ya televisheni kwa njia ya waya kwa miaka mitano iliyopita
Idadi ya televisheni kwa njia ya waya iliongezeka kati ya 2020 na 2022. Aidha, idadi hiyo ilipungua mwaka
2023 kama inavyooneshwa kwenye Jedwali 4.5. Kupungua kwa usajili wa televisheni kwa njia ya waya kwa
mwaka 2023 kumechangiwa na kuongezeka kwa usambaaji wa televisheni kwa njia ya antena na dishi.
Jedwali 4.5 Idadi ya televisheni kwa njia ya waya kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita
2019 2020 2021 2022 2023
Jedwali 4.6 Ueneaji wa huduma za utangazaji kwa kipindi cha Machi 2024
Kiashiria Machi 2024
31 28
ISO 9001: 2015 CERTIFIED
5. Takwimu za Huduma
za Posta na Usafirishaji
(Courier)
Sehemu hii inawasilisha takwimu za wateja wa posta na huduma za usafirishaji, bidhaa za Posta zilizotumwa
na kupokelewa, kama vile barua, vifurushi na vipeto, kwenda na kutoka ndani ya nchi, Afrika Mashariki (EA)
na mataifa mengine (RoW).
Jedwali 5.2 linaonesha idadi ya Kampuni/Taasisi zinazotumia huduma ya usafirishaji kwa mwezi Januari na
Februari 2024 ilikua kubwa kuliko wateja binafsi.
Idadi ya bidhaa za Posta zilizotumwa katika kipindi husika imeoneshwa kwenye Jedwali 5.3. Takwimu
zinaonesha barua zilitumwa zaidi katika kipindi cha robo mwaka iliyoishia Machi 2024, ikifuatiwa na nyaraka
(documents). Mizigo (cargo) imetumwa kwa idadi ndogo zaidi katika kipindi husika.
29
ISO 9001: 2015 CERTIFIED
Jedwali 5.3 Idadi ya bidhaa za Posta zilizotumwa ndani ya nchi kwa robo mwaka iliyoishia
Machi 2024
Mwezi Barua Vifurushi Vipeto Nyaraka Mizigo Jumla
Mgawanyo wa idadi ya bidhaa za Posta zilizotumwa na TPC na watoa huduma wengine wa huduma za
usafirishaji ndani ya nchi umeoneshwa katika Chati 5.3. TPC ana idadi kubwa zaidi (94.3%) ya bidhaa za
Posta zilizotumwa ndani ya nchi.
Chati 5.3 Mgawanyo wa asilimia za vitu vilivyotumwa ndani ya nchi
Chati 5.3 Mgawanyo wa idadi ya bidhaa za Posta zilizotumwa ndani ya nchi
5.7%
94.3%
Kielelezo hapo juu kinaonesha kuwa idadi ya bidhaa za Posta zilizotumwa nje ya nchi kupitia TPC ilipungua
kwa kiasi kikubwa (69%) ikilinganishwa na bidhaa za Posta zilizotumwa kupitia watoa huduma wengine wa
usafirishaji.
Jedwali 5.4 linaonesha idadi ya bidhaa za Posta zilizotumwa nje ya nchi. Takwimu zinaonesha kuwa barua
zimetumwa zaidi nje ya nchi katika robo ya mwaka iliyoishia Machi 2024, ikifuatiwa na nyaraka na vifurushi.
33 30
ISO 9001: 2015 CERTIFIED
Jedwali 5.5 Idadi ya bidhaa za Posta zilizopokelewa ndani ya nchi kwa robo ya mwaka
iliyoishia Machi 2024
Idadi ya bidhaa za Posta zilizopokelewa kutoka nje ya nchi imeoneshwa kwenye Jedwali 5.6. Barua kutoka
nje ya nchi zimepokelewa zaidi katika robo ya mwaka iliyoishia Machi 2024, wakati mizigo kutoka nje ya nchi
ilipokelewa kwa kiwango kidogo zaidi katika kipindi husika.
Jedwali 5.6 Idadi ya bidhaa za Posta zilizopokelewa kutoka nje ya nchi kwa robo ya mwaka
iliyoishia Machi 2024
31
ISO 9001: 2015 CERTIFIED
Mgawanyo wa idadi ya bidhaa za Posta zilizotumwa na zilizopokelewa umeoneshwa katika Chati 5.6. Chati
inaonesha kuwa Tanzania inatuma bidhaa za Posta chache zaidi nje ya nchi (31%) kuliko inavyopokea kutoka
nje ya nchi (69%).
Mgawanyo wa bidhaa za Posta zilizotumwa nje ya nchi na
Chati 5.6 Mgawanyo wakupokelewa
bidhaa za Posta zilizotumwa
kutoka nje yanje ya nchi na kupokelewa kutoka nje
nchi
ya nchi
31%
69%
5.7 Idadi ya bidhaa za Posta zilizotumwa ndani na nje ya nchi kwa miaka mitano
iliyopita
Idadi ya bidhaa za Posta zilizotumwa kwa miaka mitano iliyopita imeoneshwa kwenye Chati 5.7.
Idadiyaya
Chati 5.7 Idadi bidhaa
bidhaa za zilizotumwa
za Posta Posta zilizototumwa
ndani na nje ya ndani na
nchi kwa nje mitano
miaka
iliyopita nchi kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita
9,280,229
00000
00000
4,024,371
2,873,312 2,745,674
2,371,970
00000 2,123,212
0
2019 2020 2021 2022 2023
Bidhaa za Posta zilizotumwa ndani ya nchi Bidhaa za Posta zilizotumwa nje ya nchi
Chati 5.7 inaonesha kuwa bidhaa za Posta nyingi zaidi zilitumwa ndani ya nchi kuliko nje ya nchi. Aidha, idadi
ya bidhaa za Posta zilizotumwa kwa ujumla imekuwa ikishuka.
35 32
ISO 9001: 2015 CERTIFIED
5.8 Idadi ya bidhaa za Posta zilizotumwa nje ya nchi na kupokelewa kutoka nje ya
nchi kwa miaka mitano iliyopita
Idadi ya bidhaa za Posta zilizotumwa nje ya nchi imepungua kutoka bidhaa za Posta 2,873,312 kwa 2019
na kufikia bidhaa za Posta 493,053 kwa 2023 kama inavyooneshwa kwenye Chati 5.8. Vilevile idadi ya
bidhaa za Posta zilizopokelewa kutoka nje ya nchi ilipungua.
Bidhaa za Posta zilizotumwa nje ya nchi na vilizopokelewa
kutoka
Chati 5.8 Idadi ya nje yazanchi
bidhaa Postakwa kipindi
zilizotumwa njecha miaka
ya nchi mitano iliyopita
na zilizopokelewa kutoka nje ya
nchi kwa miaka mitano iliyopita
7,999,942
00000
00000
00000
2,873,312
00000
1,116,069 937,124 979,625
564,528 493,053
326,826 219,453 164,312
0
2019 2020 2021 2022 2023
Bidhaa za Posta zilizotumwa nje ya nchi Bidhaa za Posta zilizopokelewa kutoka nje ya nchi
33
ISO 9001: 2015 CERTIFIED
6. Takwimu za Ubora wa
Huduma na Majaribio ya
Ulaghai/uhalifu Mtandaoni
6.1 Ubora wa huduma (QoS)
Ufuatao ni muhtasari wa matokeo ya ubora wa huduma (Quality of Service - QoS) wa mitandao ya simu
nchini, kuanzia Januari hadi Machi 2024. Vipimo vilifanyika kwa kuzingatia vigezo vya QoS na mbinu za
vipimo vilivyoainishwa katika Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (Ubora wa Huduma), 2018.
Airtel walifikia lengo katika maeneo yote kumi na tatu ya huduma yaliyopimwa. Halotel na Tigo walifikia
lengo katika maeneo kumi na mbili kati ya maeneo kumi na tatu ya huduma yaliyopimwa. Vodacom walifikia
lengo katika maeneo kumi na moja kati ya kumi na tatu yaliyopimwa na TTCL walifikia lengo katika maeneo
Upatikanaji wa mtandao (lengo > 99%)
tisa, kama inavyooneshwa kwenye Chati 6.1.1.
100
80
60
40
20
0
Airtel Halotel Tigo TTCL Vodacom
ARUSHA DODOMA IRINGA LINDI MARA MTWARA MWANZA NJOMBE PEMBA RUVUMA SIMIYU TANGA UNGUJA
Airtel na Vodacom walifikia lengo katika maeneo yote kumi na tatu. Halotel walifikia lengo katika maeneo
kumi na mbili, Tigo walifikia lengo katika maeneo kumi na TTCL alifikia lengo katika maeneo mawili kama
inavyooneshwa kwenye Chati 6.1.2.
37 34
ISO 9001: 2015 CERTIFIED
Simu zilizoshindwa kuunganishwa (lengo < 2%)
25
20
15
10
0
Airtel Halotel Tigo TTCL Vodacom
ARUSHA DODOMA IRINGA LINDI MARA MTWARA MWANZA NJOMBE PEMBA RUVUMA SIMIYU TANGA UNGUJA
Airtel, Vodacom, Halotel na Tigo walifikia lengo katika maeneo yote kumi na tatu ya huduma zilizopimwa,
Simu zilizokatika
wakati TTCL walifikia lengo katika maeneo kumi na moja,(lengo < 2%)
kama inavyooneshwa kwenye Chati 6.1.3.
2.5
1.5
0.5
0
Airtel Halotel Tigo TTCL Vodacom
ARUSHA DODOMA IRINGA LINDI MARA MTWARA MWANZA NJOMBE PEMBA RUVUMA SIMIYU TANGA UNGUJA
35
ISO 9001: 2015 CERTIFIED
Airtel walifikia lengo katika maeneo nane kati ya tisa, Tigo walifikia lengo katika maeneo matano kati ya
sita, Halotel walifikia lengo katika maeneo kumi na moja kati ya kumi na tatu, Vodacom walifikia lengo
maeneo nane kati ya kumi na moja, na TTCL walifikia lengo maeneo nane kati ya kumi na mawili ya kama
Upatikanaji
inavyooneshwa Chati 6.1.4. wa huduma ya 2G (lengo > -85dBm)
2G
-20
-40
-60
-80
ARUSHA DODOMA IRINGA LINDI MARA MTWARA MWANZA NJOMBE PEMBA RUVUMA SIMIYU TANGA UNGUJA
Halotel, Tigo na Vodacom walifikia lengo katika maeneo yote kumi na matatu ya huduma yaliyopimwa. Airtel
walifikia lengo katika maeneo kumi na moja, wakati TTCL walifikia lengo katika maeneo nane ya huduma,
Upatikanaji wa huduma ya 3G (lengo > -85dBm)
kama inavyooneshwa kwenye Chati 6.1.5.
3G
-20
-40
-60
-80
ARUSHA DODOMA IRINGA LINDI MARA MTWARA MWANZA NJOMBE PEMBA RUVUMA SIMIYU TANGA UNGUJA
39 36
ISO 9001: 2015 CERTIFIED
Tigo walifikia lengo katika maeneo yote kumi na tatu ya huduma yaliyopimwa. Airtel walifikia lengo katika
maeneo kumi na mbili. TTCL na Vodacom walifikia lengo katika maeneo kumi na Halotel walifikia lengo
Upatikanaji
katika maeneo tisa ya wa inavyooneshwa
huduma, kama huduma ya 4G (lengoChati
kwenye > -95dBm)
6.1.6.
4G
-20
-40
-60
-80
-100
ARUSHA DODOMA IRINGA LINDI MARA MTWARA MWANZA NJOMBE PEMBA RUVUMA SIMIYU TANGA UNGUJA
Airtel na Vodacom walifikisha lengo katika maeneo yote kumi na tatu ya huduma yaliyopimwa. Tigo
walifikisha lengo katika maeneo kumi na moja, Halotel walifikisha katika maeneo kumi na mbili, na TTCL
Simu zilizofanikiwa (lengo > 95%)
walifikisha lengo katika maeneo manne, kama inavyooneshwa kwenye Chati 6.1.7.
100
80
60
40
20
0
Airtel Halotel Tigo TTCL Vodacom
ARUSHA DODOMA IRINGA LINDI MARA MTWARA MWANZA NJOMBE PEMBA RUVUMA SIMIYU TANGA UNGUJA
37
ISO 9001: 2015 CERTIFIED
Airtel, Halotel na Vodacom walifikia lengo katika maeneo yote kumi na tatu ya huduma zilizopimwa, Tigo
walifikia lengo katika maeneoSimu
kumi kuhamishika
na mbili, TTCL walifikia
(lengolengo katika maeneo kumi, kama inavyooneshwa
> 98%)
kwenye Chati 6.1.8.
100
80
60
40
20
0
Airtel Halotel Tigo TTCL Vodacom
ARUSHA DODOMA IRINGA LINDI MARA MTWARA MWANZA NJOMBE PEMBA RUVUMA SIMIYU TANGA UNGUJA
Watoa huduma wote walifikisha lengo katika maeneo yote yaliyopimwa kama inavyooneshwa kwenye Chati
Ubora wa sauti (lengo > 3.5)
6.1.9
0
Airtel Halotel Tigo TTCL Vodacom
ARUSHA DODOMA IRINGA LINDI MARA MTWARA MWANZA NJOMBE PEMBA RUVUMA SIMIYU TANGA UNGUJA
41 38
ISO 9001: 2015 CERTIFIED
Vodacom, Tigo, na Halotel walifikia lengo katika maeneo yote kumi na tatu ya huduma zilizopimwa, na Airtel
Kasi ya kupakua data (lengo > 4,000 Kbps)
na TTCL walifikia lengo katika maeneo kumi na mbili, kama inavyooneshwa kwenye Chati 6.1.10.
35000
30000
25000
20000
15000
10000
5000
0
Airtel Halotel Tigo TTCL Vodacom
ARUSHA DODOMA IRINGA LINDI MARA MTWARA MWANZA NJOMBE PEMBA RUVUMA SIMIYU TANGA UNGUJA
Airtel, Halotel, Tigo na Vodacom walifikia lengo katika maeneo yote kumi na tatu ya huduma zilizopimwa,
TTCL walifikia lengo katika maeneo tisa ya huduma, kama inavyooneshwa kwenye Chati 6.1.11.
Muda wa kupata huduma ya data (lengo < 400ms)
600
500
400
300
200
100
0
Airtel Halotel Tigo TTCL Vodacom
ARUSHA DODOMA IRINGA LINDI MARA MTWARA MWANZA NJOMBE PEMBA RUVUMA SIMIYU TANGA UNGUJA
39
ISO 9001: 2015 CERTIFIED
Halotel na Airtel walifikia lengo katika maeneo yote kumi na tatu yaliyopimwa. Tigo alifikia lengo katika
maeneo kumi na mbili, Vodacom alifikia lengo katika maeneo matano, na TTCL alifikia lengo katika eneo
Simu kushindwa kusoma mtandao (lengo < 2%)
moja kama inavyooneshwa kwenye Chati 6.1.12.
60
50
40
30
20
10
0
Airtel Halotel Tigo TTCL Vodacom
ARUSHA DODOMA IRINGA LINDI MARA MTWARA MWANZA NJOMBE PEMBA RUVUMA SIMIYU TANGA UNGUJA
Watoa huduma wote walifikia lengo katika maeneo yote kumi na tatu yaliyopimwa, kama inavyooneshwa
kwenye Chati 6.1.13.
Muda wa simu kusoma mtandao (lengo < sekunde 5)
0
Airtel Halotel Tigo TTCL Vodacom
ARUSHA DODOMA IRINGA LINDI MARA MTWARA MWANZA NJOMBE PEMBA RUVUMA SIMIYU TANGA UNGUJA
43 40
ISO 9001: 2015 CERTIFIED
0
Airtel Halotel Tigo TTCL Vodacom
ARUSHA DODOMA IRINGA LINDI MARA MTWARA MWANZA NJOMBE PEMBA RUVUMA SIMIYU TANGA UNGUJA
Matokeo ya upimaji wa ubora wa huduma za simu na Intaneti kwa kipindi cha Januari hadi Machi 2024
yanaonesha kuwa Airtel ilikuwa na 97.2%, Halotel 94.9%, Tigo 94.8%, Vodacom 91.5%, na TTCL 70.1%, kama
ilivyooneshwa kwenye Jedwali 6.1.
Jedwali 6.1 Matokeo ya ubora wa huduma za simu na Intaneti kwa robo mwaka zinazoishia
Disemba 2023 na Machi 2024
Kwa kulinganisha vipindi hivyo, Jedwali 6.1 linaonesha kuwa watoa huduma watatu wameboresha huduma
zao katika robo mwaka inayoishia Machi 2024 huku ubora wa huduma ukishuka kwa watoa huduma wawili.
Aidha, wastani wa ubora wa huduma za simu na Intaneti kwenye sekta umepanda kwa asilimia moja (1%).
41
ISO 9001: 2015 CERTIFIED
Takwimu zinaonesha kuwa majaribio ya ulaghai yamepungua kwa watoa huduma wote kwa angalau 15%
isipokuwa Vodacom ambaye yameongezeka kwa 30% kutoka majaribio 2,876 katika robo mwaka inayoishia
Disemba hadi majaribio 3,735 katika robo inayoishia Machi 2024.
Chati 6.2a inaonesha majaribio ya ulaghai ki-mkoa. Mikoa ya Rukwa na Morogoro ndiyo inayoongoza, ikiwa
na zaidi ya theluthi moja ya majaribio yote ya ulaghai nchini. Mbeya, Dar es Salaam na Tabora zinafuata kwa
majaribio ya ulaghai kwa zaidi ya 1% hadi 10%.
Mikoa mingine ya Kaskazini Pemba, Kusini Unguja na Kusini Pemba ina idadi ndogo ya majaribio. Kila mkoa
ulirekodi 0.01%.
Chati 6.2a Majaribio ya ulaghai/uhalifu wa kimtandao ki-mkoa
Chati 6.2a Idadi majaribio ya ulaghai ki-mkoa kwa robo mwaka inayoishia Machi 2024
Rukwa 6,861
Morogoro 6,126
Mbeya 1,625
Dar es salaam 757
Tabora 462
Mwanza 186
Arusha 144
Songwe 143
Katavi 116
Kilimanjaro 99 Rukwa na Morogoro ni
Dodoma 93 mikoa inayoongoza kwa
kuwa na zaidi ya robo
Kagera 84 tatu ya majaribio hayo.
Pwani 65
Iringa 59
Tanga 56
Ruvuma 51
Shinyanga 51
Singida 38
Kigoma 33
Mjini Magharibi 33 0.01% Mikoa mingine kama
Kaskazini Pemba, Kusini
Geita 31 Unguja na Kusini Pemba ina
Mara 26 idadi ndogo ya majaribio ya
udanganyifu.
Njombe 23
Simiyu 23
Manyara 21
Lindi 19
Mtwara 12
Kaskazini Unguja 3
Kaskazini Pemba 2
Kusini Unguja 2
Kusini Pemba 1
Mgawanyo wa asilimia ya majaribio ya ulaghai mtandaoni kwa kila mtoa huduma iliyooneshwa katika Chati
6.2b.
Chati 6.2b Mgawanyo wa asilimia ya majaribio ya ulaghai mtandaoni kwa kila mtoa huduma
43
ISO 9001: 2015 CERTIFIED
Amateur Stations 18 18
Ship Stations 45 47
HF Radio Stations 22 21
Utangazaji
Community Radios 11 17
Community Televisions - -
Weblogs (Blogs) 60 67
Online Radios 6 7
Cable Televisions 56 60
47 44
ISO 9001: 2015 CERTIFIED
Intercity Transporters 50 65
Intracity Courier 14 15
Public Postal 1 1
Domestic Courier 45 46
7.2 Vyeti
Idadi
45
ISO 9001: 2015 CERTIFIED
8. Hitimisho
Hali ya mawasiliano katika robo inayoishia Machi 2024 imeonesha maendeleo makubwa kwa kuongezeka
kwa utumiaji wa huduma za mawasiliano, ikichochewa na ushindani endelevu wa bei za huduma. Moja
ya mafanikio hayo ni kuenea kwa mtandao wa simu za mkononi katika teknolojia mbalimbali, ambapo
mtandao wa 3G umeenea kwa 88% ya watu, na hivyo kuongeza upatikanaji wa huduma ya Intaneti.
Aidha, kuenea kwa mtandao wa 4G kwa 80% ya watu kumeongeza kasi na upatikanaji wa uhakika wa
huduma ya Intaneti. Wakati uo huo, 5G imeenea kwa 13% ya watu huku ikileta zama mpya ya mtandao
wa kasi ya juu ambayo ni muhimu kwa mahitaji ya Intaneti ya kasi. Mafanikio hayo yameambatana na
uboreshaji wa huduma za mawasiliano, udhibiti wa majaribio ya ulaghai na uimarishaji wa miundombinu
ili kufikia Uchumi wa kidijiti.
Kadhalika, Sekta ya utangazaji ilipata mwelekeo mzuri wa ongezeko la 2.5% la visimbuzi ikilinganishwa
na robo mwaka iliyopita. Ukuaji huo umechangiwa na kuongezeka kwa ubora wa huduma kwa wateja wa
huduma ya utangazaji. Maboresho hayo ya pamoja katika sekta ya mawasiliano ni muhimu katika kukuza
jamii iliyounganishwa na iliyowezeshwa kidijitali.
49 46
ISO 9001: 2015 CERTIFIED
Mawasiliano Towers,
20 Sam Nujoma Road,
14414 Dar es Salaam, Tanzania.
Email: dg@tcra.go.tz
@tcra_tanzania
50