Zaburi 1

You might also like

Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 3

Zaburi 1

Heri mtu yule asiyekwenda


Katika shauri la wasio haki;
Wala hakusimama katika njia ya wenye dhambi;
Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.

Bali sheria ya BWANA ndiyo impendezayo,


Na sheria yake huitafakari mchana na usiku.

Naye atakuwa kama mti uliopandwa


Kandokando ya vijito vya maji,
Uzaao matunda yake kwa majira yake,
Wala jani lake halinyauki;
Na kila alitendalo litafanikiwa.

Sivyo walivyo wasio haki;


Hao ni kama makapi yapeperushwayo na upepo.

Kwa hiyo wasio haki hawatasimama hukumuni,


Wala wakosaji katika kusanyiko la wenye haki.

Kwa kuwa BWANA anaijua njia ya wenye haki,


Bali njia ya wasio haki itapotea.
Zaburi 23

BWANA ndiye mchungaji wangu,


Sitapungukiwa na kitu.

Katika malisho ya majani mabichi hunilaza,


Kando ya maji ya utulivu huniongoza.

Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongoza


Katika njia za haki kwa ajili ya jina lake.

Naam, nijapopita kati ya bonde la kivuli cha mauti,


Sitaogopa mabaya;
Kwa maana Wewe upo pamoja nami,
Gongo lako na fimbo yako vyanifariji.

Waandaa meza mbele yangu,


Machoni pa watesi wangu.
Umenipaka mafuta kichwani pangu,
Na kikombe changu kinafurika.

Hakika wema na fadhili zitanifuata


Siku zote za maisha yangu;
Nami nitakaa nyumbani mwa BWANA milele.
IMANI YA MITUME

Namwamini Mungu Baba Mwenyezi, Muumba mbingu na nchi na Yesu Kristo


mwana wake pekee, Bwana yetu aliyechukuliwa mimba kwa uwezo wa Roho
Mtakatifu akazaliwa na bikira Mariamu, akateswa zamani za Pontia pilato,
akasulubiwa, akafa, akazikwa, akashuka mahali pa wafu, siku ya tatu akafufuka,
akapaa mbinguni, ameketi mkono wa kiume wa Mungu Baba Mwenyezi. kutoka
huko atakuja kuwahukumu walio hai na watu wafu,

Namwamini Roho Mtakatifu. kanisa takatifu ushiriki wa watakatifu, ondoleo la


dhambi kiyama ya mwili na uzima wa milele. AMINA

You might also like