Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 2

Senior six

HAYAWI HAYAWI HUWA (Nothing is Impossible)

Kuna mengi ambayo, ninapoyafikiria, hata machozi ya furaha yananidondoka machoni. Kama watu
wengine, ikiwa wapo, nilijiunga na chuo kikuu cha Kyambogo mwaka wa elfu mbii kumi na moja. Safari
hii haikuwa rahisi kwangu kwasababu, kuna changamoto mbalimbali ambazo nilizipitia kama
mwanafunzi. Kwa mfano, ada za chuo kikuu ilikuwa changamoto kubwa, kiasi kwamba, muhula
ungekaribia mwisho bila kumalizia malipo yote, huwezi kupewa cheti cha kukuruhusu kufanya mitihani.
Chakula changu siku hizo, kilikuwa cha kubahatisha; ugali na maharagwe ndicho kilichokuwa chakula
rahisi ingawa nacho kilipatikana kwa nadra. Vile vile, madeni yalikuwa mengi kiasi kwamba ningemaliza
muhula bila kulipa kodi ya chumba nilimokilalia. Lakini, Mungu aliye mbinguni huwezi kuwasahau waja
wake, la murua, ni kumwamini kila kukicha. Baada ya miaka mitatu, nami niliibuka miongoni mwa
watahiniwa wazuri ambao walitunukiwa vilivyo na shahada ya kwanza katika elimu.

Ndoto nyingine ilinijia akilini usiku mmoja. Kwa nini nisiendelee na masomo ili nibobee Zaidi. Nikaanza
ukrasa mwingine mpya, nilijiungWaswali husema, ‘’mvumilivu hula mbivu’’, nao wahenga husema,
“achanikaye kwa mpini hafi na njaa’’. Nilijitahidi, nikaanza safari ya mashariki mwa nchi, nikafundishwa
na Maprofesa. Baada ya mikaka miwili, nilivuna mavuno ya shahada ya Uzamili. Hapa ndipo nilipo.
Mungu amenifungulia milango. kilichoonekana kama ni kitendawili, kimeteguliwa. Ndugu zangu
wapendwa, ninayo mengi yakuwasimulia, bali, kuwatakia faraja katika safari yenu ya kiakademia.
Kwangu yamekuwa, na yatazidi kutokea. Nawe, usikate tamaa, Mola atakuwezesha. Wasalaam!

Written by (Yameandikwa na): Bw. Bwambale Onismuss : bonismuss@gmail.com


Senior four

MPENZI WANGU (My love)

Wangu wa ubani! Sikiliza! Tazama! Kuna jambo la kukuambia, nalo latoka moyoni. Aah! Moyo wangu
waniuliza, maswali magumu tena mazito. Mengine siyawezi kuyajibu, bila msaada wako. Tega masikio
yote uweze kuyafahamu niyayokuambia.. Jambo la kwanza upasalo kujua ni kwamba; mara nyingi
ninapokuwa kitandani katika usingizi, kuna ndoto ninazoota, na, katika ndoto hizi, kuna mengi
yanayotendeka; tukiwa pamoja chini ya kivuli, ukiniambia maneno matamu, ukiniimbia nyimbo nzuri
kwa sauti yako nyororo. Siku nyingine, tulikuwa pamoja ufukweni mwa bahari ya Hindi, upepo mzuri
ukivuma kutoka baharini. Hivi juzi, kuna jambo uliloniambia. Ulisema kwamba, ‘’wewe ni mja mzito’’.
Swala hili lilinishtua. Nikatoka usingizini. Nikaamuka na kukaa kitandani. Kitandani nikatoka na
kurandaranda chumbani. Nilikosa la kufanya ila tu wasiwasi. Leo nimekuja kwako, uniambie ukweli wa
ndoto hizi ili niweze kutulia moyoni. Je, majonzi haya ni ya ukweli? Naomba jibu kutoka kwako.
Nakupenda sana. Wewe ni tamanio langu. Nakushukuru sana. Kabla sijasahau, nambari yangu ya simu ni
+256703-323-270. Kwa hivyo, waweza kunipigia simu au kunitumia ujumbe wakati wowote name
nitakuwa tayari kukujibu.

Written by (Yameandikwa na): Bw. Bwambale Onismuss : bonismuss@gmail.com

You might also like