Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 4

HOTUBA YA MHESHIMIWA KHALIFA SAID KHALIFA, RAIS WA SERIKALI YA WANAFUNZI

CBESO WAKATI WA KUAGANA NA BUNGE NA KULIVUNJA BUNGE UKUMBI WA BUNGE,


CBE TAREHE 15 APRIL, 2024

YALIYOMO

HOTUBA HII IMEGAWANYIKA KATIKA VIPENGELE VIFUATAVYO:


.SHUKRANI
.UTANGULIZI
.UTEKELEZAJI WA MALENGO YA SERIKALI KWA MWAKA 2023/2024
.HITIMISHO

SHUKRANI
Assalam aleikum,bwana vesu asifiwe, nawasalimu kwa jina la iamhuri va muungano wa
tanzania

Nakushukuru sana Mheshimiwa Spika kwa kunipatia nafasi hii ya kulihutubia Bunge lako tukufu
ili niweze kutimiza wajibu wangu huo wa msingi Kikatiba. Lakini, shukrani zangu kubwa ni kwa
uongozi wako mahiri na shupavu. Umeliongoza Bunge vizuri. Najua haikuwa kazi rahisi. Penye
wengi pana mengi. Lakini kwa uhodari mkubwa umeweza kulifikisha jahazi bandarini salama
salmini. Hakika wewe ni nahodha makini na jemedari hodari, uliyethibitisha uhodari na umakini
wako katika uwanja wa medani

Shukran zangu za Awali; napenda kutumia nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa
rehema kwa kutujaalia uhai, afya njema na kutufikisha hapa siku ya leo kuweza kutimiza
majukumu ya Serikali

Pili, nichukue nafasi hit kumshukuru Mkuu wa Chuo Chetu Cha elimu ya biashara CBE Ndugu
Prof. edda tandi Iwoga, pamoja na Menejimenti yote kwa ushauri na msaada wake katika kipindi
chetu chote cha kutimiza majukumu yetu amekuwa msaada mkubwa kwetu.

Tatu, Tunawashukuru washauri wa Wanafunzi Bwn.faustine china na bwn. Marco kwa kuwa
walezi bora kwetu na kwa ustawi wa Wanafunzi wote kiujumla, tumeshirikiana nao vyema katika
kipindi chetu chote cha kutimiza majukumu vetu wamekuwa msaada mkubwa kwetu.
Kipekee,Nilivesimama hapa ni Rais wa Serikali ya Wanafunzi-(CBESO), kwa mwaka wa
masomo 2023/2024. Nikiongoza shughuli zote za serikali ipasavye ndani ya chuo chetu
haikuwa rahisi ila subra,weledi, ufanisi uthubutu na unyenyekuvu nilikuwa nao mpaka hivi sasa
tunaelekea kutamatisha safari ya uongozi

Kipekee kabisa, nipende kumshukuru Makamu wa Rais-CBESO, Waziri Mkuu katib


mkuu,Baraza la Mawaziri, Mhe Spika, Mh Naibu Spika, Mh Katibu wa Bunge, Waheshimiwa
Wabunge wote na Kamati ya Maadili-(judicial) Serikali ya Wanafunzi CBESO 2023/2024, kwa
ushirikiano waliotuonesha kuanzia mwanzo wa Vongozi wet hadi lea tunaelekea kumaliza
Uongozi wetu.
Mwisho kwa umuhimu: tunawashukuru ndugu Wanafunzi wenzetu wote kwa umoja na upendo

ushirikiano na uvumilivu wenu dhidi yetu katika kipindi chote tulichopo madarakani hadi sasa
tunaelekea kufikia tamati ya uongozi wetu.

UTANGULIZI
Ndugu Wabunge, Serikali ya Wanafunzi-CBESO 2023/2024 iliingia madarakani mnamo mwezi
Mei 2023 baada ya zoezi zima la Uchaguzi la kuwachagua Viongozi katika nafasi mbalimbali.

Mheshimiwa Spika;
Tarehe 12 Mei 2023 nilipozindua Bunge nilielezea mtazamo wangu kuhusu serikali yetu na
kutaja majukumu ya msingi na vipaumbele vya Serikali yangu. Nilisema tutatekeleza wajibu
wetu na vipaumbele hivyo kwa ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya hakika kazi iliendelea
Serikali ilikuwa na nia njema na thabiti kwa ajili ya kuwatumikia wanafunzi wote bila kujali itikadi,
rangi na Imani zao, hivyo kazi moja tu ilikuwa ni kuwarahisishia Wanafunzi huduma wawapo
hapa Chuoni na hata nje ya Chuo.
Mara baada ya utangulizi huo napenda kuchukua nafasi hii kuelezea sehemu ya Mipango ya
Serikali yetu kwa muda wote wa Uongozi wa Serikali ya Wanafunzi kwa mwaka wa Masomo
2023/2024.
Ndugu viongozi Serikali ilikuwa na malengo mengi katika kutekeleza sera zangu katika
kuwatumikia Wanafunzi katika nyanja mbalimbali hapa Chuoni kwetu.

MALENGO NA MAFANIKIO YA SERIKALI KWA MWAKA 2023/2024

WIZARA YA MAZINGIRA,MALAZI NA CHAKULA


.Kushauri utawala katika kuboresha miundombinu ya Kitaaluma kwa kukarabati baadhi va
miundombinu inayotuzunguka kama vile Madarasa/kuweka microphones na spikers lwa ajili va
sauti kwenve venue kubwa katika jenga la NEW BUILDINGS ] na hosteli za ndani ya chuo,
mfumo wa utoaji maji taka nk.

.Tuliomba menejimenti kufanya fermigation tarehe 23/5/2023 hosteli zetu za ndani kuua
vijududu kama kunguni na wengine na kumarisha usafi kwa wanafunzi wanufaika wa hosteli
.Pia tumefanikiwa kushauri mmiliki wa enea la canteen kununua runinga/TV] va inchi 54 pamoja
na king amuzi chake ili kuwezesha wanafunzi kuburudika na saka la mpira wakiwa eneo la chuo
.Tumefanikiwa kushauri menejimenti kununa pampu mbili mpya za kupandishia maji katika
hosteli za ndani va chuo ambapo baada ya kununuliwa zimeweza kupunguza chanagamoto ya
upatikanaji wa maji
WIZARA YA MICHEZO
Kuhahakisha upatikanaji wa vifaa vya michezo mbalimbali kama iezi, na mipira ambapo
nilishirikiana na NMB tukapatiwa jezi za basketball, football, volleyball na mipira pia kwa
kushirikiana na MHE. Mbunge wetu wa jimbo la ilala ndg.MUSSA AZAN ZUNGU tulipata jezi
pea mbili kwa kila mchezo na mipira
Kuanzisha mchakamchaka kila mwisho wa wiki kuimarisha afya ambapa sasa Kuboresha
mashindano mbalimbali va micheza ya ndani na nie ya Chuo, kwa lengo la
kufufua, kuinua na kuimarisha vipaji, matalani MASHINDANO YA SHIMVUTA
ambapo kwa mwaka 2023/2024 sisi tumefika hatua ya nafasi ya robo fainali Mpira wa Kikapu
kwa wanawake, robo fainali volleyball wanaume,nusu fainali volleyball wanawake na mshindi
wa tatu katika mpira wa miguu. Hongera kwa timu zetu na hongera kwetu sote, kwa kuwapa
moyo na kushirikiana nao bega kwa bega.

WIZARA YA MAMBO YA KIJAMII NA BURUDANI


.Aidha tumeweza kuendesha sherehe na matamasha mbalimbali; ya kumaliza muhula
2022/2023 ilivofanyika Tarehe 16/17/2023 katika Ukumbi wa VELVET Sinza

.Pia Sherehe ya kuwakaribisha Wanaoanza Masomo 2023/24 Tarehe 24/11/2023Katika Ukumbi


wa Gwambina lounge tulipata bahati na heshima kubwa ya kupata wasanii wakubwa ambao ni
RJ THE DJ, CHINO KID,MKATABA MC ,waliweza kutumbuiza,

.pia ndani ya serikali hii tulifanya CBE-GOT TALENT ambape lengo ni kuibua vipaji ndani ya
chuo na kutambua vipaji na kukuza thamani kwao.

.wizara inatarajia kufanya tukio la CHARITY tarehe 27/4 mwaka huu katika kituo cha watoto
yatima SIFA ORPHANAGE CENTER kilichopo bagamoyo
WIZARA YA ELIMU
.Pia kushauri Menejimenti katika kuwapatia vibali Wanafunzi kufanya majaribio kwa wale wote
ambao hawakuwa wamekamilisha ada kwa wakati ingawa si sheria.

. Wizara ilifanya ziara ya kunadi na kuzielezea kanuni mpya za mitihani

.Wizara imefanikiwa kuwaombea wanafunzi wa diploma kuendelea na chuo kwa kufanya


mitihani ya marudio kutokana na kuathirika na kanuni mpya za mitihani

.Wizara imeandaa semina itakayofanyika kesho kutwa tarehe 17/4/2024 ikihusiana na "LIFE
AFTER COLLEGE" itakayokuwa na mada mbalimbali

.wizara imeandaa tukio la "CARIER DAY" litakalo fanyika ijumaa hii tarehe 19/4/2024 ambapo
wizara itatambua vipaji na fursa mbali mbali za wanafunzi wetu wa CBE

WIZARA YA AFYA NA BIMA


.Wizara imesimamia upatikanaji kwa watumiaji wanafunzi wa bima wa hiari kutokana na bima
kutojumuishwa katika mfumo wa ada

. Wizara imesimamia upatikanaji wa maji na usafi katika maeneo ya maliwatoni

.Wizara kushirikiana na waziri mkuu imesimamia zoezi la uandikishaji wa namba za


vitambulisho vya Utaifa almaarufu kama NIDA ambapo zoezi hili lilifanyika chuo kwa wiki mbili
eneo la library mpya

. Kubwa kuliko wizara ikishirikiana na waziri mkuu imeshimamia upatikana wa vyandarua 200
wakazi wa hosteli ambavyo viligawiwa bure kabisa

. Wizara imefanikiwa kufanya tukio la "AFYA WEEK" tarehe 1 hadi tarehe 5/12/2023 ndani ya
chuo chetu kwa wiki nzima ambapo hospitali mbalimbali zilishiriki kupima afya za wanafunzi na
kutoa ushauri wa kitabibu

You might also like