Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 4

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAISI (TAMISEMI)

MKOA WA MTWARA

HALMASHAURI YA MANISPAA YA MTWARA MIKINDANI

KITANGULIZI CHA MTIHANI WA DHIHAKA KIDATO CHA NNE

015 ELIMU YA DINI YA KIISLAMU

Muda:Masaa:3 Aprili, 2024


Maelekezo
1. Mtihani huu una sehemu A,B na C
2. Jibu maswali yote kutoka sehemu A na B , na maswali mawili kutoka sehemu C
3. Majibu yote yaandikwe katika kijitabu chako cha kujibia
4. Andika namba yako ya Mtihani katika kila ukurasa wa kijitabu chako cha kujibia
5. Simu za Mkononi haziruhusiwi katika chumba cha Mtihani

1
SEHEMU A (Alama 15)
Jibu maswali Yote katika sehemu hii
1. Chagua herufi ya jibu sahihi katika vipengele (i) hadi (x)
i. Ipi sifa ya Mtu alie Elimika kwa mtazamo wa uislamu?
A. Alama za ufaulu katika vyeti
B. Uwezo wa kutambua mazingira
C. Uwezo wa kuchambua na kueleza
D. Ufanisi na ubora wa kividendo
E. Aina ya ajira unayoweza kupata
ii. Ifuatazo ni mifano ya Fiqh Ibadat isipokuwa:
A. Sala
B. Miirath
C. Zakat
D. Funga
E. hijjah
iii. Mfumo wa Maisha ya kujitenga na Raha za Maisha ya Dunia ili kupata wasaa wa kumtumikia
Mungu.
A. Umajusi
B. Uislamu
C. Utawa
D. Ukristo
E. Uyahudi
iv. Shahada mbili husisitiza jambo gani katika maisha ya Muislamu?
A. Kufanya kazi ya kuwatamkisha wengine
B. Kuanza jambo na jina la Allah (s.w) na Mtume (s.a.w)
C. Wajibu wa kumtii Allah (s.w) na Mtume (s.a.w)
D. Kutambua uwepo wa miungu wengi hapa Duniani
E. Hakuna nabii mwingine isipokuwa Muhammad (s.a.w)
v. Jambo lipi ni lazima kutekelezwa katika mchakato wa kumuosha maiti?
A. Kumfunika shuka maiti gubigubi
B. Kuanza na kumuweka maiti udhu
C. Kutumia maji ya kisima au mto
D. Kutumia kitanda kilichotobolewa
E. Kujizuia kuongea wakati wa kuosha
vi. Sababu ipi ilipelekea maquraysh kupinga kwa nguvu kubwa ujumbe wa Mtume Muhammad (s.a.w)?
A. Kuharibika kwa maslahi yao ya kimali
B. Kuharibiwa kwa makanisa yao
C. Mustakbali wa miungu yao ya sanamu
D. Kupoteza ushawishi wa kuhudumia Qa’aba
E. Kufukuzwa katika mji mtakatifu wa Makkah
vii. Nabii yupi kati ya wafuatao alipewa ndugu yake kuwa Mtume msaidizi?
A. Is-haq(a.s)
B. Musa(a.s)
C. Yusuf (a.s)
D. II-yaas(a.s)
E. Idrisa (a.s)
viii. Aina ya Hadith ambayo huanza kwa kusema; Allah kasema
A. Hadith qudussiyy
B. Hadith nabawiyy
C. Hadith Hassan

2
D. Hadith mutawati
E. Hadith Dhaibu
ix. Zifuatazo ni sababu za Qur’an kushushwa kidogo kidogo Isipokuwa
A. Kuuthibitisha moyo wa Mtume(s.a.w)
B. Kuwapa nafasi wengine kuleta mfano wake
C. Kufanya wepesi wa kufikia ujumbe wake
D. Waumini kupata wepesi wa kuihifadhi
E. Kufanya wepesi katika utekelezaji
x. Allah amesema: Haitokei msiba katika ardhi wala katika nafsi zenu ila umekwisha andikwa katika
kitabu kabla hatujaumba.Kwa yakini hilo ni sahali kwa Allah.’’ Aya hiyo inaeleza kuhusu itikadi gani
ya Uislamu?
A. Upweke wa Allah (s.w)
B. Vitabu vya Allah (s.w)
C. Qadar ya Allah (s.w)
D. Mitume ya Allah (s.w)
E. Malaika wa Allah (s.w)

2. Oanisha nyakati za sala kulingana na mwenendo wa jua katika ORODHA A na majina ya sala
zinazotekelezwa katika nyakati hizo katika ORODHA B kisha andika herufi ya jibu sahihi kwa kila
kipengele katika karatasi ya kujibia
ORODHA A ORODHA B
i. Kuanzia urefu wa kivuli unapokuwa sawa na kitu halisi A. Maghrib
hadi kivuli kinapokuwa mara dufu ya urefu wa kitu B. Istisqaa
halisi C. Alfajir
ii. Kuanzia mawingu yanapobadilika na kuwa ya njano D. Dhuha
hadi usiku wa manane E. Al-asr
iii. Baada ya jua kugeuka upande wa magharibi hadi pale F. Qusuf
urefu wa kivuli unapokuwa sawa na kitu halisi G. Al-Ishaa
iv. Kuanzia pale ambapo alama ya mstari mweupe H. Dhuhur
inajitokeza upande wa mashariki hadi mwangaza
unapodhihiri
v. Kuanzia jua linapozama hadi pale mawingu mekundu
yanayobadilika na kuwa ya njano.
vi. Baada ya kuchomoza kwa jua kiasi cha mita tatu hadi
kabla ya jua kufika kati kati.

SEHEMU B (Alama 54)


Jibu maswali yote kutoka sehemu hii kwa kutoa maelezo mafupi
3. Ainisha kazi sita za Malaika zinazohusiana na Maisha ya Mwanadamu
4. Eleza haki mbili kwa kila viungo vyako vifuatavyo
(a) Macho
(b) Mdomo na ulimi
(c) Masikio
5. Kwa kurejea kazi za msikiti wa Mtume Muhammahad (s.a.w) wa madina, ainisha kazi sita ambazo
misikiti yetu hivi leo inawajibika kuzifanya.
6. Bwana Msomi analalamikiwa na mkewe kuwa hamtekelezei haki zake za ndoa. Mkumbushe Bwana
Msomi wajibu wake kwa mkewe kwa hoja sita.
7. Ainisha njia sita za uchumi zilizo haramishwa kwa mujibu wa sharia ya kiislamu.
8. Ainisha mambo sita aliyoyafanya Umar bin Abdul Aziz yaliyopelekea kuitwa Khalifa wa tano.

3
SEHEMU C (alama 30)
Jibu maswali mawili
9. Mnamo 29 Shaaban Qaanan ibn ‘Ammi alihesabu mali yake kwa ajili ya zakat na akajikuta ana aina
mbalimbali za mali:-
(a) Duka lenye bidhaa zenye thamani ya Tsh million 100.
(b) Mpunga tani 4 kutoka katika shamba lake la umwagiliaji.
(c) Ng’ombe wa maziwa 40.
Kokotoa zakat yake.
10. Eleza tofauti nne zilizopo baina ya Sura za Makkah na zile za Madinah.
11. Eleza vigezo sita utakavyotumia kuthibitisha usahihi wa Matini ya Hadithi

You might also like