Swabru Jamila

You might also like

Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 9

Muislamu anahitaji subira katika kila jambo zuri au baya na katika kila hali; kwenye furaha na huzuni,

siha na maradhi, utajiri na umasikini, neema na dhiki, utiifu na maasi. Anasema Allaah (Subhaanahu wa
Ta'aalaa):

‫َو َنْبُلوُك م ِبالَّش ِّر َو اْلَخ ْيِر ِفْتَنًةۖ َوِإَلْيَنا ُتْر َج ُعوَن‬

Na Tutakujaribuni kwa mitihani ya shari na kheri. Na Kwetu mtarejeshwa. [Al-Anbiyaa: 35]

Dunia ni nyumba ya mtihani ambako mja atakuwa akigeuzwa kukabili hali zote za kheri na shari na
hatima yake ni kuelekea kwenye makazi ya malipo kama Anavosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

١﴿‫﴾َتَباَرَك اَّلِذ ي ِبَيِدِه اْلُم ْلُك َو ُهَو َع َلٰى ُك ِّل َش ْي ٍء َقِد يٌر‬

Amebarikika Ambaye Mkononi Mwake umo ufalme Naye juu ya kila kitu ni Muweza

٢﴿ ۚ ‫﴾اَّلِذ ي َخ َلَق اْلَم ْو َت َو اْلَح َياَة ِلَيْبُلَو ُك ْم َأُّيُك ْم َأْح َس ُن َع َم اًل‬

Ambaye Ameumba mauti na uhai ili Akujaribuni ni nani kati yenu mwenye ‘amali nzuri zaidi. [Al-Mulk: 1–
2]
Kwa hiyo Muislamu hana chaguo ila asubiri katika mitihani ili apate fadhila tele Alizoahidi Allaah
(Subhaanahu wa Ta'aalaa) na Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) au sivyo atakuwa
miongoni mwa waliokhasirika kama Alivyohukumu Mwenyewe Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) katika
Suwratul’Aswr. Pia, Muumini atambue kwamba hakuna mtihani ila Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)
Humteremshia mja Wake rahmah na kwa kumpa faraja Naye Haendi kinyume na ahadi Zake. Anasema:

٥﴿ ‫﴾َفِإَّن َم َع اْلُعْس ِر ُيْسًرا‬

Basi hakika pamoja na kila gumu kuna wepesi.

٦﴿ ‫﴾ِإَّن َم َع اْلُعْس ِر ُيْسًرا‬

Hakika pamoja na kila ugumu kuna wepesi. [Al-Inshiraah: 5–6]

Tumenukuu visa kadhaa vilothibiti ili viwe ni mafunzo kwetu na viweze kumthibitisha Muislamu
anaposibiwa na mitihani. Juu ya hivyo, tuna mifano bora kabisa vya Rusuli wa Allaah (Subhaanahu wa
Ta'aalaa) waliokumbana na kila aina ya mitihani, Na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Akawasifu kwa
subira zao:
٨٥﴿ ‫﴾َوِإْس َم اِع يَل َوِإْد ِريَس َو َذ ا اْلِكْفِل ۖ ُك ٌّل ِّم َن الَّصاِبِريَن‬

Na Ismaa’iyl na Idriys na Dhal-Kifli, wote ni miongoni mwa wenye kusubiri. [Al-Anbiyaa: 85]

Akamsifu Nabiy Ayyuwb:

٤٤﴿ ‫﴾ِإَّنا َو َج ْد َناُه َص اِبًراۚ ِّنْع َم اْلَع ْبُدۖ ِإَّنُه َأَّواٌب‬

Hakika sisi Tulimkuta mwenye subira mno, uzuri ulioje wa mja, hakika yeye ni mwingi wa kurudiarudia
kutubia. [Swaad: 44]

Na Anasema (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

٣٥﴿‫ِ﴾َفاْص ِبْر َك َم ا َص َبَر ُأوُلو اْلَع ْز ِم ِم َن الُّر ُسل‬

Basi subiri (ee Muhammad ‫ )صلى هللا عليه وآله وسلم‬kama walivyosubiri wenye azimio madhubuti miongoni
mwa Rusuli [Al-Ahqaaf: 35].
01-Swabrun Jamiyl: Maana Na Aina Za Subira

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

٢٨﴿‫ۖ ﴾َو اْص ِبْر َنْفَسَك َم َع اَّلِذ يَن َيْدُع وَن َر َّبُهم ِباْلَغَداِة َو اْلَعِش ِّي ُيِريُد وَن َو ْج َهُه‬

Na isubirishe nafsi yako pamoja na wale wanaomuomba Rabb wao asubuhi kabla jua kucha na jioni,
wanataka Wajihi Wake. [Al Kahf: 28]

1.Subira Katika Utiifu

Kunahitajika subira katika utiifu kwani baadhi ya ‘ibaadah zina tabu na mashaka na nyinginezo zinahitaji
imani na azimio la nguvu hata nafsi iridhike. Mfano mtu anapoamka usiku akiwa hakushiba usingizi lakini
pamoja na hayo anajitahidi kuamka kwa ajili ya Qiyaamul-layl (kisimamo cha usiku kuswali) au kuamka
mapema kwenda Msikitini na pengine hali ya hewa ni baridi kali, au Swawm masiku marefu ya joto kali,
au kuitolea mali yake aipendayo Zakaah na Swadaqah, au kuvumilia misukusuko inayopatikana katika
kutekeleza ‘ibaada ya Hajj n.k. Yote hayo ni ‘ibaadah na anaifanya kwa ustahmilivu. Mifano yake ni kauli
za Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

٤٥﴿ ‫﴾َو اْسَتِع يُنوا ِبالَّصْبِر َو الَّص اَل ِةۚ َوِإَّنَها َلَك ِبيَر ٌة ِإاَّل َع َلى اْلَخ اِش ِع يَن‬

Na tafuteni msaada kupitia subira na Swalaah; na hakika hilo ni kubwa isipokuwa kwa wanyenyekevu.
[Al-Baqarah: 45]

١٣٢﴿‫ۖ ﴾َو ْأُم ْر َأْهَلَك ِبالَّص اَل ِة َو اْص َطِبْر َع َلْيَها‬


Na amrisha ahli zako Swalaah, na dumisha kusubiri kwayo. [Twaahaa: 132]

١٦﴿ ‫﴾َتَتَج اَفٰى ُج ُنوُبُهْم َع ِن اْلَم َض اِج ِع َيْدُع وَن َر َّبُهْم َخ ْو ًفا َو َطَم ًعا َوِمَّم ا َر َز ْقَناُهْم ُينِفُقوَن‬

Mbavu zao zinatengana na vitanda, wanamuomba Rabb wao kwa khofu na matumaini, na katika yale
Tuliyowaruzuku wanatoa. [As-Sajdah: 16]

Subira Katika Maasi

Mja anahitaji subira katika maasi kwani binaadamu hukabiliwa na yaliyo haramu na machafu; mfano
kula ribaa na mali za mayatima, kuchukua haki za watu ikiwa ni mali au heshima ya mtu, kuzuia ulimi
usitaje ya upuuzi au ghibyah (kumteta, kumsengenya mtu), an-Namiymah (kufitinisha) na kila aina ya
maneno maovu. Hayo ni baadhi ya mambo ambayo nafsi hutamani kujiridhisha isikie raha na kutimiza
matamanio yake, na shaytwaan humtia wasiwasi na kuiamrisha hiyo nafsi itende maovu hayo kama
Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa

Hakika nafsi ni yenye kuamrisha sana maovu. [Yuwsuf: 53]

Hapo ndipo mja anapohitajika kufanya jihaad ya nafsi ajizuie na afanye subira na kutokuiendekeza nafsi
yake.

‫ ((َأَال ُأْخ ِبُر ُك ْم باْلمُؤ ِم ن؟ َم ْن َأِم َنُه الَّناُس َع َلى‬:‫َع ْن َفَض اَلَة ْبِن ُع َبْيٍد (رضي هللا عنه) َأَّن َر ُسوَل ِهَّللا َص َّلى ُهَّللا َع َلْيِه َو َس َّلَم َقاَل ِفي َح َّج ِة اْلَو َداِع‬
)) ‫َأْم َو اِلِهْم َو َأْنُفِس ِهْم َو اْلُم ْس ِلم َم ْن َسِلَم الَّناُس ِم ْن ِلَس اِنِه َو َيِدِه َو اْلُمَج اِهُد َم ْن َجاَهَد َنْفَس ُه ِفي َطاَع ِة ِهَّللا َو اْلُمَهاِج ُر َم ْن َهَج َر اْلَخ َطاَيا َو الَّذ ُنوَب‬
‫أحمد والحاكم قال األلباني "إسناد صحيح" سلسلة األحاديث الصحيحة‬
Kutoka kwa Fadhwaalah bin ‘Ubayd ((Je, nikujulisheni kuhusu Muumini? Ni yule anayeaminiwa na watu
juu ya mali zao na nafsi zao. Na Muislamu ni yule anayeweka amani kwa watu kwa ulimi wake na mkono
wake. Na mpiganaji jihaad ni yule anayefanya jihaad ya nafsi yake katika kumtii Allaah, na mhamaji
hijrah ni yule anayehama makosa na madhambi)) [Ahmad na Al-Haakim. Kasema Imaam Al-Albaaniy
katika Silsilatul-Ahaadiyth Asw-Swahiyhah: “Hii isnaad ni Swahiyh”]

3- Subira katika Qadhwaa (Yaliyopangwa) na Qadar (Yaliyokadiriwa) ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

Majaaliwa yanaweza kuwa katika yale ya kheri au ni katika mitihani inayomsibu mtu. Anasema Allaah
(Subhaanahu wa Ta'aalaa):

Basi mwana Aadam pale Rabb wake Anapomtia mtihanini, Akamtakaramu na Akamneemesha, husema:
“Rabb wangu Amenitakarimu.”

Ama Anapomtia mtihanini, Akamdhikishia riziki yake, husema: “Rabb wangu Amenidunisha.” [Al-Fajr:
15–16]

Aina hii ya Subira inahusiana pia na aina za misiba inayomsibu mtu ikiwa ni kifo cha mpenzi wake, mali,
maradhi, shida, huzuni, dhiki, maafa n.k

Na bila shaka Tutakujaribuni kwa kitu katika khofu na njaa na upungufu wa mali na nafsi na mazao. Na
wabashirie wenye kusubiri.

Wale ambao unapowafika msiba husema: “Hakika sisi ni wa Allaah na hakika sisi Kwake ni wenye
kurejea.”

Hao zitakuwa juu yao Barakah kutoka kwa Rabb wao na rahmah, na hao ndio wenye kuongoka. [Al-
Baqarah: 155–157]

Subira Kutokana Na Maudhi ya watu:


Miongoni mwayo, inayohitajia subira ya hali ya juu ni dhulma na maudhi ya watu. Na ndio maana Allaah
(Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ametaja kuwa subira ya aina hii inahitajika azimio la nguvu kuvumilia na
kutokulipizia na kusamehe watu wanaosababisha hayo:

Na atakayevuta subira na akasamehe, hakika hilo bila shaka ni katika mambo ya kuazimiwa. [Ash-
Shuwraa: 41–43]

Na mkilipiza, basi lipizeni kulingana na vile mlivyoadhibiwa. Na mkisubiri, basi bila shaka hivyo ni bora
kwa wenye kusubiri.

Na subiri (ee Muhammad ‫)صلى هللا عليه وآله وسلم‬, na haiwi subira yako isipokuwa kupitia kwa Allaah. Na
wala usiwahuzunukie, na wala usiwe katika dhiki kutokana na njama wanazozifanya.

Hakika Allaah Yu Pamoja na wenye taqwa, na wale ambao wao ni wenye kufanya ihsaan. [An-Nahl: 126–
128]

Aina hii ya subira inawahusu pia walinganiaji Dini yetu ya Kiislamu, pale mtu anapoamrisha mema na
kukataza maovu kama Luqmaan alipomuusia mwanawe:

Ee mwanangu! Simamisha Swalaah, na amrisha mema na kataza ya munkari, na subiri juu ya yale
yatakayokusibu. Hakika hayo ni katika mambo ya kuazimiwa. [Luqmaan: 17].

Na hii ni sifa miongoni mwa sifa za Manabii kwani walivumilia walipokadhibishwa na kuudhiwa na
kaumu zao kwa kila aina ya maudhi hadi ikawa ni huzuni kubwa kwao. Nabiy Nuwh ('Alayhis-Salaam)
alifanyiwa istihzaai na watu wake. Nabiy Luutw ('Alayhis-Salaam) alipata maudhi ya kashfa kutoka kwa
watu wake. Nabiy Ibraahiym ('Alayhis-Salaam) aliingizwa kwenye moto na watu wake na akatengwa
mbali. Nabiy Yuwsuf ('Alayhis-Salaam) alitaka kuuliwa na nduguze, akaingizwa kisimani, kisha akauzwa
kwa bei ndogo mno, kisha akazuliwa kashfa ya mke wa Waziri, akaingizwa jela miaka kadhaa. Nabiy
Swaalih ('Alayhis-Salaam) alikadhibishwa na watu wake kuhusiana na miujiza ya ngamia. Nabiy Muwsa
('Alayhis-Salaam) alipata maudhi kuanzia kwa Fir’awn hadi watu wake. Nabiy ‘Iysaa ('Alayhis-Salaam)
alipata maudhi na kutaka kuuliwa na watu wake. Na maudhi mengi mbali mbali yalimfikia Nabiy
Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipoudhiwa na watu wake Maquraysh wa
Makkah hadi kifua chake kikawa na dhiki mno na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Akampooza kwa
kumwambia:
Na kwa yakini Tunajua kwamba kifua chako kinadhikika kwa yale wanayoyasema. [Al-Hijr: 97]

Manabii wote hao walivumilia, wakasubiri na wakaweka dhanna nzuri kwa Rabb wao na kuamini
waliyoahidiwa na wakaendelea na ulinganiaji wao wa Dini, na wakapata radhi za Allaah (Subhaanahu wa
Ta'aalaa) na wakawa ni wenye kushinda na kufaulu duniani na Aakhirah.

02-Fadhila Za Subra Katika Qur-aan

Subira imetajwa katika Qur-aan mara nyingi mno kama walivyonukuu ‘Ulamaa. Wengine wamesema
kwamba imetajwa zaidi ya mara themanini kwa kusifiwa wale wenye kuvumilia mitihani inayowasibu.
Ama kwa ujumla, subira imetajwa katika Qur-aan zaidi ya mara mia.

1.Wenye kusubiri hupata mapenzi ya Allaah:

Na Allaah Anapenda wanaosubiri. [Aal-‘Imraan: 146]

2. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Yu pamoja nao daima:

3.Hakika Allaah Yu Pamoja na wanaosubiri. [Al-Anfaal: 46]

Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ameahidi kuwalipa malipo mazuri kabisa kwa sababu ya kusubiri kwao
katika utiifu.
Na kwa yakini Tutawalipa wale waliosubiri ujira wao kwa mazuri zaidi ya yale waliyokuwa wakitenda.
[An-Nahl: 96]

Wenye kusubiri wameahidiwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) malipo mema yasiyohesabika.

Hakika wanaosubiri watalipwa kikamilifu ujira wao bila ya hesabu. [Az-Zumar: 10]

You might also like