Kanuni Za Kikundi Kikundi PFG

You might also like

Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 2

KANUNI ZA KIKUNDI KIKUNDI

KIKUNDI CHA PARTNERS FAMILY GROUP

1.0 UTARATIBU NA MICHANGO YA KUJIUNGA NA KIKUNDI

1.1 Kiingilio cha Kujiunga na Kikundi

a) Kikundi Cha PARTNERS FAMILY GROUP ni kikundi wazi kwa mtu anayefanya kazi halali hapa Dar
es salaam. Mwanakikundi anatakiwa kuwa Mwenye umri usiopungua miaka 18, anayejitegemea
au anayeanza kujitegemea, mwenye uwezo wa kulipa kiingilio, ada na michango mengine kwa
mujibu wa kanuni za kikundi.
b) Kujiunga na kikundi hiki ni lazima mwombaji ajaze fomu ya kujiunga na alipe kiingilio ambacho
HAKIRUDISHWI wakati wa kuacha/kuachishwa uanakikundi
c) Mwanakikundi yeyote mpya wa PARTNERS FAMILY GROUP anapaswa ndani ya miaka miwili ya
mwanzo wa kikundi hiki, kukopa kiasi chochote kwa madhumini ya kukuza kipato cha kikundi hiki
ili kufikia malengo ya kufungua miradi ya Pamoja ya kikundi hiki.
d) mwanakikundi mpya anapaswa kufanya malipo yote kwa muweka hazina na atatakiwa kutoa
risitikwa kila malipo atakayopokea.
e) Kiambatisho kwenye fomu ya kujiunga na kikundi kitakuwa ni copy ya kitambulisho chochote iwe
cha Taifa (NIDA)/Hati ya Kusafiria , cha mpiga kura ama leseni ya udereva.

1.2 Ada baada ya kujiunga

a) Mwanakikundi atakuwa na wajibu wa kulipa ada ya shilingi 50,000/- (EShilingi za kitanzania elfu
hamsini tu) kama kiingilio kwa wanaoanza.
b) Baada ya kujiunga basi kama mwanakikundi kila mmoja anapaswa kulipa ada ya kila mwezi kiasi
chaTsh 200,000 (Shilingi ya kitanzania laki mbili tu).

1.3 Kujitoa

a) Mwanakikundi akitaka kujitoa anatakiwa kutoa taarifa mwezi mmoja kabla kwa
Kwa njia maandishi ili aandaliwe stahiki zake.
b) Mwanakikundi anapaswa kulipa madeni yake yote anayodaiwa na kikundi kabla ya kujitoa,kama
atashindwa kulipa atakatwa kwenye marejeshoya ada alizolipa kama stahiki ya kujitoa kwa hiari.

2.0 MICHANGO YA KUSAIDIANA KATIKA SHINDA NA RAHA.


a) Kila mwanakikundi anatakiwa kutoa mchango wa Tsh.5000/= kwa ajili ya pole kwa mfiwa.
b) Mchango huu utatolewa iwapo mwanachama ataondokewa na
i. Baba
ii. mama,
iii. mme
iv. mke
v. mtoto.

c) Iwapo mwanakikundi amefariki kila mwanachama atatakiwa kutoa mchango wa Tsh.10,000/=.

d) Mwanakikundi akifariki stahili zake zote atapewa mrithi aliyeainishwa kwenye fomu ya kujiunga na
uanachama.

c) Mchango wa rambirambi utatolewa ndani ya siku saba (7) tangu taarifa ilipotolewa.

You might also like