Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 81

H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

PY
Chapa ya Kwanza 2020

© Hakimiliki, Mwl. Francis M. Langula


+255754711247/+255717123348
CO
francis.langula@gmail.com
Dar es Salaam

Usanifu wa Jalada & Kurasa


DL Bookstore
+255787163013
dlbookstore@zoho.com
EE

Arusha

ISBN 978 9987 7892 28 3

HAKI ZOTE ZIMEHIFADHIWA


FR

Haki zote zimehifadhiwa. Hairuhusiwi kunakili, kurudufisha, au


kukitoa kielektroniki au kutumia sehemu ya kitabu hiki bila idhini ya
mwandishi au mchapishaji. Kufanya hivyo ni uvunjifu wa sheria ya
haki miliki.

ii
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

PY
CO
HEKIMA YA NENO LA MUNGU KUWASAIDIA MABINTI
KUJITUNZA
Wimbo Ulio Bora 2:7 “Nawasihi enyi binti za Yerusalemu, kwa paa
na kwa ayala wa porini, msiyachochee mapenzi wala kuyaamsha
hata yatakapoona vyema yenyewe…”
EE
FR

iii
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

VITABU VINGINE NILIVYOANDIKA

1. MUNGU ANAKUTAKA KWENYE CHUMBA CHA MAOMBI

PY
2. ULINZI MKAMILIFU WA MUNGU KWA WATU WAKE
3. MALAIKA NA UTENDAJI WAO KATIKA MAISHA YA MWAMINI
4. KIUMBE KIPYA CO
5. SASA NINAANZA KUISHI (NAMNA YA KUTAMBUA KUSUDI)
6. KUWA MWANAFUNZI
7. HEKIMA YA KUMSAIDIA MSICHANA KUOLEWA
8. HEKIMA ITAKAYOMSAIDIA BINTI KUJITUNZA
EE
FR

iv
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

YALIYOMO

UTANGULIZI…...............................................................................vii

PY
SEHEMU YA KWANZA….................................................................1
TAFSIRI YA ANDIKO LA MSINGI…….......................................1
SEHEMU YA PILI……...................................................................…5
CO
KUHUSU MWANDISHI WA WIMBO ULIO BORA…............….5
SEHEMU YA TATU….................................................................…..9
SIFA ZA PAA NA AYALA, HEKIMA NA MAONYO
AMBAYO BINTI ANAWEZA KUYAPATA KUPITIA
WANYAMA HAWA…………......................................................9
EE

SEHEMU YA NNE……..............................................................….19
ADUI MKUU WA PAA NA AYALA NA
SIFA ZAKE AKIMUWAKILISHA KIJANA WA KIUME…….......19
FR

SEHEMU YA TANO…….................................................................27
UPANDE WA PILI WA AYALA NA PAA….............................…27
SEHEMU YA SITA…………........................................................…33
BINTI/MSICHANA KUUWEZA MWILI WAKE…...................…33

v
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

SEHEMU YA SABA….....................................................................35
MAENEO YA BINTI KUJILINDA ILI ASIYACHOCHEE
WALA KUYAAMSHA MAPENZI…..........................................35
SALA YA WOKOVU………….....................................................….69
HITIMISHO……..............................................................................71

PY
CO
EE
FR

vi
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

UTANGULIZI

N inaamini Neno la Mungu lina kila kitu tunachohitaji, tukiamua

PY
kulifuata litatupa majibu ya kila eneo la Maisha ambalo tuna
maswali; hata kuhusiana na mabinti kujitunza wasinaswe na adui
kwenye maswala ya mapenzi na hisia za mapenzi kabla ya wakati
wake, ni wazi kwamba Neno la Mungu linatupatia majibu na
muongozo wa namna ya kujilinda na kujitunza.
CO
Andiko hilo nililonukuu ni wazi kabisa kwamba Neno la Mungu
linampatia hekima binti ambayo akiweza kuifumbua itamsaidia
kujilinda na kujitunza mbali na zinaa na mapenzi na kuzilinda pia
hisia zake katika kipindi hiki cha dunia iliyoharibika.
Katika kitabu hiki, nitaeleza kwa undani sana kutokea kwenye
andiko hilo la Wimbo Ulio Bora 2:7 na kwa ufunuo wa Roho
Mtakatifu tutafunua siri nyingi na kuyafumbua mafumbo mengi
EE

ambayo yatampatia binti Hekima ya Neno la Mungu itakayomsaida


msichana kujitunza.
Ili msomaji aweze kufuatana nami vema katika kuelewa andiko hili,
ninapenda kulifafanua kwanza ili wakati wote atakapokuwa
anasoma kitabu hiki aweze kulielewa kwa ufasaha andiko hili la
FR

msingi kwa ujumla wake.


Andiko hili la Wimbo Ulio Bora 2:7; Kwa tafsiri nyepesi ni sawa na
kusema “Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, Kwa [Kutumia
HEKIMA ya] paa na kwa [HEKIMA ya] ayala wa porini,
[JILINDENI] Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, Hata

vii
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

yatakapoona vema yenyewe.” Ni sawa kabisa na kusema


“Ninakusihi, wewe binti unayesoma hiki kitabu, kwa kutumia
HEKIMA ya Paa na kwa HEKIMA ya Ayala wa porini
utakayojifunza katika kitabu hiki, JILINDE, usiyachochee
mapenzi, wala kuyaamsha, hata yatakapoona vema yenyewe.”

PY
CO
EE
FR

viii
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

PY
SEHEMU YA KWANZA
TAFSIRI YA ANDIKO LA MSINGI
CO
MAANA YA KUSIHI

K wanza kabisa nataka nianze kutafsiri sehemu ya kwanza


kabisa ya andiko letu la msingi ambayo inasema “Nawasihi
enyi binti za Yerusalem”.
EE

Mwandishi Anaposema binti za Yerusalem, alikuwa anawaandikia


au anawasihi mabinti wa eneo Fulani lililokuwa linaitwa au
linaloitwa Yerusalemu; kwa sasa au kwa funidsho la kitabu hiki
Yerusalemu inaweza kuwakilishwa na eneo lolote ambalo wewe
FR

binti unayesoma kitabu hiki upo. Kwa hiyo yaweza kuwa,


ninawasihi enyi binti za Tanzania, Kenya, Uganda au binti za Dar
es salaam, Dodoma au mkoa wowote au binti za kanisa fulani au
eneo lolote unaloweza kutaja.
Lakini pia Neno hilo “Nawasihi” kwenye andiko letu la msingi,
Ukifuatilia tafsiri zingine linaongelea mambo yafuatayo:­

viii
1
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

Maana ya kwanza ni kwamba; ninakuamrisha ewe binti wa


Yerusalemu Kujifanyia kiapo wewe mwenyewe kwamba
hutayaamsha mapenzi, au kwa lugha nyingine ni sawa na kusema
“Ninakuamrisha wewe binti wa Yerusalemu, ujiapize kutoyaamsha
mapenzi” yaani binti ajiapize kwa kusema kwamba, “mimi fulani,
kwa PAA na kwa AYALA sitayaamsha mapenzi wala
kuyachochea mpaka yatakapoona vyema yenyewe”

PY
Maana ya Pili, anaposema “Nawasihi” ni sawa na kusema
“NINAWAONYA mabinti, kwa PAA na kwa AYALA, msiyaamshe
mapenzi wala kuyachochea mpaka yatakapoona vyema
yenyewe”
Maana ya tatu, neno hilo hilo, linamaana ya binti kujipa wajibu
CO
mwenyewe (Kujiwajibisha) kwamba, kwa PAA na kwa AYALA
hutayaamsha mapenzi mpaka yatakapoona vyema yenyewe; binti
kujiwajibisha kutoyaamsha mapenzi.
Sasa, hayo maneno “kwa PAA na kwa AYALA” yasikusumbue,
nitayaelezea kwa undani sana katika kitabu hiki kwa kadiri
tunavyoendelea kujifunza; kwa sasa, jambo pekee la kufahamu ni
EE

kwamba, Paa na Ayala ni aina za wanyama .


Maana ya nne ya kusihi ni ile ya Kiswahili ambayo naamini
tunaielewa sote. Ukiona mtu anatumia neno hili “ninakusihi” kwa
kumaanisha, ujue ana maana kwamba, angekuwa anaweza hilo
jambo ambalo anakusihi ulifanye angekufanyia yeye kwa niaba
FR

yako. Kwa hiyo, kwa tafsiri ya andiko hilo maana yake ni kwamba,
anaposema ninakusihi anamaanisha “Ningekuwa naweza, mimi
ndio ningekusaidia kutoyaamsha mapenzi kwa niaba yako au
kwenye mwili wako” lakini sasa kwa sababu huo si mwili wangu ni
wako, siwezi kufanya chochote kwa niaba yako, kwa hiyo kwa
kutambua umuhimu wa kutoyaamsha mapenzi, ninakuomba

2
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

(ninakusihi) kwa moyo wangu, chonde chonde, ewe binti wa


Yerusalem, usiyaamshe mapenzi wala kuyachochea mpaka
yatakapoona vema yenyewe.
MAANA YA PAA NA AYALA
Hawa ni aina ya wanyama ambao ni jamii ya mbuzi au swala,
Wanyama hawa ni wanyamapori. Wanyama hawa, Paa na Ayala,

PY
kwa sababu ya asili yao, ni kitoweo pendwa [ni chakula kinono] kwa
Wanyama pori wa jamii ya paka kama vile Chui, Simba na
Wanyama wengine wakali. Kwa lugha ya sasa tunaweza kusema,
Paa na Ayala ni kama PILAU kwa Wanyama pori jamii ya paka.
Kwa sababu, paa na ayala ni chakula pendwa cha Wanyama jamii
CO
ya Paka, hivyo husababisha Paa na Ayala wanakuwa hatarini
kupata mashambulizi kutoka kwa Wanyama hao wa jamii hiyo ya
paka.
Naamini mpaka sasa umeanza kuelewa kwanini Mwandishi wa
Wimbo uliobora, ambaye ni Suleimani, alianza kwa kusema “Kwa
Paa na kwa Ayala Usiyaamshe mapenzi”. Kwa sababu, kwa
asili, simba au chui, wakipata Wanyama wengine kama nyumbu
EE

katika mawindo, ni sawa na mtu kula chakula asichokipenda, lakini


wakipata Paa na ayala wanakuwa ni sawa wamepata chakula
wanachokipenda na kukifurahia.
Ninaamini, kuna hekima na hatari nyingi sana ziko kwa hawa
FR

Wanyama, Paa na Ayala, ambazo zinamkabili binti wa sasa, ndio


maana Neno la Mungu likasema “Kwa Paa na kwa Ayala,
msiyaamshe mapenzi wala kuyachochea”.
Kuna vitu ambavyo anavyo binti, hawa Wanyama pia wanavyo ndio
maana wametajwa na kuhusishwa na binti na mapenzi.

23
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

PY
CO
EE
FR

4
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

PY
SEHEMU YA PILI
KUHUSU MWANDISHI WA WIMBO ULIO BORA
CO
S uleimani ndio mwandishi wa kitabu cha Wimbo Ulio Bora, na ni
mmoja wa wenye hekima wakubwa kati ya wenye hekima
waliowahi kuishi duniani, na kimsingi ndiye alikuwa mwenye
hekima kuliko dunia nzima katika kipindi chake na hata baada yake
EE

sawa na maandiko yasemavyo katika 1 Wafalme 4:30­31a


“hekima ya Sulemani ikapita hekima ya wana wote wa
mashariki, na hekima zote za Misri. Kwa kuwa alikuwa na
hekima kuliko watu wote;”
1 Wafalme 4:29­33 Neno la Mungu linasema, Suleimani alinena
FR

mifano yenye mafunzo elfu tatu, alitunga nyingo elfu moja na tano.
Suleimani alikuwa anajua habari za kila mti na matumizi yake, kwa
lugha ya sasa tunaweza kusema alikuwa anajua biolojia yote
yakuhusiana na miti, alikuwa anajua habari za Wanyama na ndege,
wadudu, na samaki wengi, kama si wote, pamoja na tabia zao.

5
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

Alikuwa anaweza kuhusisha tabia za wanyama na watu aina Fulani


na tabia zao.
1 Wafalme 4:32­34 [32]Naye akanena mifano elfu tatu, na
nyimbo zake zilikuwa elfu moja na tano. [33] Akanena habari za
miti tangu mwerezi ulioko Lebanoni hata hisopo umeao
ukutani; pia akanena habari za wanyama, na za ndege, na
vitambaavyo, na samaki. [34] Wakaja wa mataifa yote ili

PY
waisikie hekima ya Sulemani, toka wafalme wote wa
ulimwengu, waliokuwa wamepata habari za hekima yake.
Kwa hekima Mungu aliyompatia, Suleimani akagundua, kuna
Wanyama wanaitwa Ayala na Paa, ambao sifa zao na tabia zao au
mazingira yao, yanafanana sana na mabinti ndio maana akasema
CO
“Enyi mabinti wa Yerusalemu, kwa Paa na kwa Ayala,
msiyaamshe mapenzi”.
Maana yake ni kwamba, kuna mafumbo yako kwa hawa Wanyama,
ambayo binti akiweza kuyafumbua, yatampatia hekima au siri
zitakazomsaidia asiyaamshe wala kuyachochea mapenzi.
Kwa sababu ya Hekima ya Suleimani, Ndio maana ukifuatilia
EE

maandiko utagundua mahali pengi sana, anatufundisha kujifunza


kwa Wanyama na wadudu mbalimbali. Kuna mahali katika bibila
kitabu cha mithali anasema “tujifunze kuweka akiba kwa
Chungu” lakini pia kuna pengine amezungumzia Wanyama kama
mbwa, nyoka, Kunguru, Tai,
FR

Mithali 6:6­8 [6]Ewe mvivu, mwendee chungu, Zitafakari njia


zake ukapate hekima.[7]Kwa maana yeye hana akida, Wala
msimamizi, wala mkuu,[8]Lakini hujiwekea akiba ya chakula
wakati wa jua; Hukusanya chakula chake wakati wa mavuno.

6
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

Mithali 26:11 Kama vile mbwa arudiavyo matapiko yake;


Kadhalika mpumbavu afanya upumbavu tena.
Mithali 23:31­32 [31]Usiitazame mvinyo iwapo ni nyekundu;
Iitiapo bilauri rangi yake, ishukapo taratibu;[32]Mwisho wake
huuma kama nyoka; Huchoma kama fira.
Mithali 30:17 Jicho la mtu amdhihakiye babaye, Na kudharau

PY
kumtii mamaye; Kunguru wa bondeni wataling’oa na vifaranga
vya tai watalila.
Neno la Mungu linasema kwamba, watu walikuwa wakitoka mahali
mbalimbali duniani kwenda kwa Suleimani kujifunza habari
mbalimbali. Ninaamini watu walikuwa wakienda kwakwe kujifunza
CO
habari za Wanyama, wadudu, miti, na viumbe mbali mbali, na
hawakwenda mikono mitupu, walimpelekea mali.
Moja ya Hekima za Suleimani ni wakati amefanya maamuzi ya
kutambua mtoto anayegombaniwa ni wa nani kati ya wale
wanawake wawili makahaba inayopatikana katika kitabu cha 1
Wafalme 3:16­28
EE

Sasa, Huyu Sulemani mwenye hekima hii ndio anawaambia


mabinti, “enyi mabinti wa Yerusalemu, kwa Paa na kwa Ayala,
msiyachochee mapenzi wala kuyaamsha, mpaka yatakapoona
vyema yenyewe”.
Kauli hiyo “mabinti wa Yerusalemu”, kama nilivyosema, ni kauli
FR

wakilishi, ikiwakilisha kila binti anayempenda Mungu. Ni sawa


kabisa na kusema, enyi mabinti wa Kanisani, au enyi mabinti wa
Tanzania, au wa Kenya au wa nchi yeyote ambao mnampenda
Mungu, kwa Paa na kwa Ayala, Msiyaamshe wala kuyachochea
mapenzi mpaka yatakapoona vyema yenyewe.

7
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

PY
CO
EE
FR

8
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

PY
SEHEMU YA TATU
SIFA ZA PAA NA AYALA, HEKIMA NA MAONYO
AMBAYO BINTI ANAWEZA KUYAPATA KUPITIA
CO
WANYAMA HAWA

N ataka nieleze kidogo kuhusu Paa na Ayala, lakini wakati


naeleza Paa na Ayala, lengo langu sio Paa na Ayala bali ni
EE

wewe binti unayesoma kitabu hiki. Kwa hiyo, wakati naeleza


kuhusu Paa na Ayala, wewe binti anza kujiweka mahali pa hao
Wanyama. Ninapowaelezea Wanyama hawa, ukiwa unajiweka
wewe binti, utaanza kujua namna ya kujilinda ili usiyaamshe hayo
mapenzi. Utaanza kuona au kupata hekima ya kujilinda kama binti.
FR

SIFA ZA PAA NA AYALA


Sifa ya kwanza: Paa na ayala ni Wanyama ambao wako makini
“sensitive” sana wanapokuwa katikati ya Wanyama wengine.
Kwa hiyo, binti anayezunguziwa hapa ni binti ambaye yuko makini

9
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

sana. Paa na ayala ni kati ya Wanyama ambao wako makini sana,


muda wote wako makini, yaani wako “alert” wakijua kwamba
chochote kinaweza kutokea, muda wowote wanaweza kuvamiwa
na Wanyama wakali ambao wanawaona Paa na Ayala ni kama
pilau (chakula pendwa kitamu).
Hivi, wewe binti unayesoma kitabu hiki, unajua, kuna vijana wa
kiume wakikuangalia wanakuona kama chakula pendwa kwao,

PY
yaani pilau; kama vile tu Chui na Simba wanavyowaona Paa na
Ayala?
Wewe binti unaweza ukawa unajiona kawaida, na wakati mwingine
hata mzazi anamuona binti yake kama bado mtoto, lakini wapo
vijana wakiume wakikuangalia, wanaona na kulitamani hilo umbo
CO
lako na hayo maziwa yako madogo yaliyosimama, wanaona ni
kama nyama tamu.
Yaani wewe binti unapita tu huna hata wazo lolote baya labda
unaenda shuleni, lakini kuna wakaka au vijana wanakuona pilau na
wanatamani wakutafune saa yeyote wakipata fursa.
Paa na Ayala, sifa yao ya kwanza, wako makini (sensitive and alert)
EE

muda wote wanapokuwa katikati ya Wanyama wengine. Kwa hiyo,


hata wewe binti, masaa yote unatakiwa uwe makini unapokuwa
katikati ya VIJANA WA KIUME wengine na hata katikati ya
MABINTI WENZIO, ukijua kwamba CHOCHOTE KINAWEZA
KUTOKEA.
FR

Sifa ya pili: Paa na Ayala ni Wanyama wenye macho makubwa,


na hii ni sifa yao muhimu nyingine.
Macho ya Paa na Ayala ni makubwa yenye uwezo wa kuona nyuzi
180, yaani wanaweza kuona nusu duara. Yaani akiwa ameangalia
mbele anaweza kuona tangu upande wa kulia mpaka wa kushoto,

10
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

ni nyuma tu hawawezi kuona. Macho ya mwanadamu hayawezi


kuona nyuzi 180’, yanaona zaidi ya nyuzi 90 lakini hayafikii kuona
nyuzi 180, lakini Paa na Ayala wanaweza kuona nyuzi 180 ambapo
ukubwa wa macho yao ndio unawapa uwezo huo mkubwa wa
kuona. Kwa hiyo kwa sababu ya huo ukubwa na uwezo wa macho
yao ambayo Mungu amewapatia, inawasaidia muda wote kuwa
waangalifu.

PY
Hii pia ni sifa ya mabinti, binti unatakiwa uwe na uwezo wa kuona
zaidi ya vijana wa kiumbe, uone “nyuzi 180”. Binti unatakiwa
kuona kuanzia mbali kabisa, hata kijana wa kiume akija na nia
mbaya unaweza kuiona nia yake mbaya kuanzia mbali kabisa. Binti
unapaswa uweze kuona (kugundua) kila aina ya mbinu anayotumia
CO
kijana wa kiume kwa lengo la kukuharibu; kijana anayeanzia kona
(angle) ya mbali na kuja kwako kwa vizawadi zawadi unamuona,
unaletewa kizawadi lakini wewe umeshaona nyuma ya zawadi
anataka kuyaamsha mapenzi na kukuvua nguo. Sio binti unapokea
tu zawadi na wakati zawadi zingine ni mbinu za kukuharibia
usichana wako na maisha yako kwa ujumla.
Unajua binti, ukikutana na kijana ambaye ni mjanja na anakutaka
EE

kimapenzi, hataanza kwa kukuambia ninakutaka, ataanzia kona ya


mbali kabisa, yaweza kuwa kona ya vizawadi, kona ya kukuita
majina mazuri mazuri, yaweza kuwa kona ya kukuambia maneno
matamu matamu, kona ya kukusifia kwamba wewe ni mzuri sana,
kona ya kukuambia wewe una akili sana, au unajitambua sana
FR

kuliko mabinti wengine, au unaonekana una hatma (future) nzuri


nk, haya yote kijana anaweza kuwa akikuambia ili umuone kama
anakutakia mem asana na kumbe ni mtego ili kumfanya binti awe
mwepesi kumkubali pindi atakapo mletea hoja yake yenye mtego
nyuma yake, kwa hiyo ni lazima binti uwe na macho ya kumuona
kuanzia mbali.

11
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

Sifa ya tatu: Paa na Ayala wamejifunza namna fulani isiyo ya


kawaida ya kukimbia ambayo wanaitumia kuwashinda adui
zao, Wanyama wakali.
Kama umewahi kufuatilia Wanyama jamii ya Paa na Ayala, huwa
wanakimbia kwa kurukaruka huku wakihama kutoka upande mmoja
kwenda mwingine (jumping and zigzag running or stotting ,
hawakimbii moja kwa moja (straight). Wanapokimbia kwa kwa

PY
kurukaruka, wanatuma ujumbe aina mbili, wa kwanza ni kwa
Wanyama wenzao paa na ayala, wakiwaambia kwamba kuna
hatari, lakini ujumbe wa pili walikuwa wanaituma kwa adui (chui na
simba) wakiwaambia kwamba tumeshawaona na hamtuwezi
tunaweza kabisa kuwashinda.
CO
Hivi unajua, mabinti wana uwezo mkubwa sana wa kuwashinda
vijana wa kiume, na hii ni kwasababu ya asili ya binti ukilinganisha
au kufananisha na kijana wa kiume. Kiasili, binti ana uwezo
mkubwa sana kwa kuizuia tamaa ya mwili wake kuliko kijana wa
kiume. Binti anaweza akamuona kijana wa kiume uchi bila nguo na
wala mwili wake usishtuke wala kusisimka, sana sana atashangaa
kwanini huyu kijana wa kiume anakaa uchi. Lakini, kijana wa kiume
EE

hawezi kumuona msichana bila nguo na kupuuza kirahisi bila mwili


wake au hisia zake kushtuka hata kama ni kidogo. Mwanaume
yeyote akimwona mwanamke au binti bila nguo anapata shida na
asipokuwa na maarifa ya kutosha na maamuzi thabiti basi atajikuta
akiendelea kutaka kumuangalia na kupata madhara ya kihisia na
FR

hata kufikia kushawishika kufanya maamuzi mabaya jambo ambalo


ni tofauti kabisa kwa wanawake.
Hivi umewahi kujiuliza kwa nini wanaovaa nguo nusu uchi ni
wadada na sio wanaume? Sababu kubwa ni kwamba, wanawake
hawavutiwi na maungo ya mwanaume anapokaa bila nguo, yaani
mwanaume akivua nguo, sana sana utaona binti anaondoka lakini

12
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

sivyo kwa mwanaume. Tamaa ya mwanaume inaamshwa kwa


macho (kuona) lakini tamaa ya msichana (mwanamke) haiamshwi
kwa kuona.
Ninachotaka ukione hapa ni kwamba, binti anao uwezo mkubwa
sana wa kumzuia mwanaume asiguse mwili wake au kujizuia kwa
mwanaume. Hii ni kwa sababu tamaa ya binti haianzii kwenye
macho inaanza badae ikiwa huyu binti ataruhusu kijana wa kiume

PY
amfanyie vitu vya kuonyesha kumjali.
Kwa sababu ya changamoto ya macho kwa vijana wa kiume, ndio
maana Neno la Mungu linasema katika kitabu cha Ayubu
“Nilifanya agano na macho yangu; sitamuangalia msichana
kwa kumtamani” Ayubu 31:1
CO
Neno halisemi sitamuangalia mwanaume kwa kumtamani bali
linasema mwanamke, kwa sababu shida ya macho sana ni kwa
wanaume na sio wanawake; kwa hiyo kijana wa kiume anapaswa
kufanya agano na macho yake yasimkoseshe katika kumtazama
mwanamke.
Tamaa ya msichana haiko machoni iko moyoni, nikimaanisha iko
EE

kwenye hisia zake. Msichana anatamani baada ya kugundua kijana


wa kiume anamjali sana, anamuwaza sana. Ndio maana shida
huwa inatokea baada ya msichana kuanza kuona kijana wa kiume
anamuwaza sana, anamtafuta sana, anamfuatilia sana, anamjali
sana. Kwa nini nasema hivi, ujumbe wangu kwako binti ni kwamba,
FR

UNAPASWA KUANZA MAPEMA SANA KUMDHIBITIL huyu kijana


anayeonyesha kukujali sana, kwa sababu ukichelewa na ikafika
mahali pa kuamsha hisia zako za mapenzi itaanza kukuletea shida
kubwa sana.

13
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

Pamoja na kwamba tamaa ya mwanaume iko karibu sana, yaani


iko kwenye macho lakini, tamaa ya mwanaume ni rahisi kutulia pia,
yaani ni rahisi kuinuka na ni rahisi kutulia ikiwa macho yake
hayaoni na akijizuia fikira zake zisitengeneza na kutunza picha ya
alichokiona, lakini kwa upande wa pili, pamoja na kwamba tamaa
ya (au hisia za) binti iko mbali lakini ikiamshwa ni ngumu sana
kutulia. Ninaamini hii ndio sababu andiko letu la msingi

PY
LINAMUONYA BINTI KUYAAMSHA MAPENZI, sababu akiyaamsha
yatamtesa.
Kwa hiyo, hawa Paa na Ayala, walikuwa wamepewa uwezo na
Mungu wa kuwashinda maadui zao wakuu ambao ni chui na simba
na Wanyama wengine. Ukiona Paa au Ayala amekamatwa, ujue
CO
kuna makosa ya kiufundi ameyafanya sio kwamba hana uwezo
ndani wa kushinda. Na ndivyo ilivyo kwa binti, ukiona binti
amekamatwa na kijana wa kiume na kuangushwa, ujue kuna
makosa amefanya, na ndio hasa sababu ya kitabu hiki kuwa
mikononi mwako, ili ujifunze na usifanye makosa ambayo mabinti
wengi wameyafanya na yakawagharimu Maisha yao. (Nimeainisha
baadhi ya makosa hayo kwenye sura ya sita ya kitabu hiki)
EE

Usiwe mmoja wa mabinti ambao wanafundishwa na hawapokei


mafundisho na mwisho wake wanaishia kujuta kwamba ningejua
ningesikiliza na kufanyia kazi yale niliyoyasoma na kufundishwa.
Pokea mafundisho haya na yaruhusu yageuze maisha yako jumla.
Mabinti wengi wanaanguka kwa sababu ya kutofuatilia vitu
FR

ambavyo wanafundishwa.
Kwa hiyo, Paa na Ayala, walikuwa wanakimbia kwa kurukaruka
kwa sababu ya hizo jumbe mbili nilizosema yaani moja kuwapa
taarifa wenzao na mbili kuwaonyesha adui zao kwamba
hawawawezi. Hii inatufundisha kwamba, ni vizuri sana binti ukiona
mahali kuna shida, hakikisha unawasaidia na mabinti wengine;

14
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

kumbuka kwamba usalama wako ni pamoja na usalama wa mabinti


wengine; kama unaona jambo linamtatiza binti mwenzio lakini
wewe umelimudu, basi mwambie, akikataa ni yeye amekataa lakini
wewe umefanya sehemu yako. Binti usifurahie kwamba wewe uko
safi wakati mabinti wenzio wamekwama, hakikisha unamfundisha
na binti mwingine kila ambacho wewe umekishinda au umejifunza
kuhusu kujitunza; unapaswa kufahamu kwamba, mabinti wengine

PY
wanakosea sio kwa kupenda ni kwa sababu kwa kutokujua,
hawajafundishwa wala kuelekezwa njia sahihi, kwa hiyo wewe
ambaye umefundishwa kawafundishe mabinti wengine pia, au
unaweza ukawapatia na wao kitabu hiki wajifunze. Jifunze kuwa
binti unayesambaza habari njema kwa mabinti wenzio.
CO
HEKIMA NA MAONYO KUTOKA KWA PAA NA AYALA
NI HEKIMA AU SIFA GANI TUNAWEZA KUZIPATA KUTOKA
KWA PAA NA AYALA AMBAZO ZITAMSAIDIA BINTI WA SASA?
1. Umakini
Muda wote binti unapokuwa katikati ya vijana wa kiume na hata
mabinti wenzio, unapaswa kuwa makini kwamba chochote
EE

kinaweza kutokea, kwa hiyo kijana yeyote wa kiume akikufuata


unapaswa kuwa makini. Yaani hata kama anakuja kwa lengo
linaloonekana ni jema. Hata kama ni mwanafunzi mwenzio anakuja
kwa ajili ya majadiliano ya shule (discussion) au mwanamaombi
mwenzako anakuja kwa ajili ya kuomba au kutafakari neno la
FR

Mungu, wewe binti unakuwa tu makini. Unakuwa na masikio na


macho ya umakini ili iwe rahisi kugundua na kushughulika na
jambo lolote lisilo sahihi linaloweza kuibuka baada au wakati wa
discussion. Mtoto wa kike anatakiwa kuwa makini.

15
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

2. Uwezo wa kukimbia
Paa na Ayala wana uwezo mkubwa sana wa kukimbia. Ni
Wanyama wa pili kwa kasi (speed) ukilinganisha Wanyama pori
wote. Baadhi ya Paa na Ayala wanaweza kukimbia mpaka kasi ya
kilometa 97 kwa Saa (97Km/Hr) ambayo ni kasi kubwa sana na ni
kasi ya magari. Kila binti anao uwezo ndani yake wakuikimbia au
kuiepuka hatari ya mapenzi, ndio maana Neno la Mungu

PY
likafananisha mabinti na Wanyama hawa; ukiona binti amekamatika
kwenye maswala ya mapenzi ujue kuna mahali alifanya uzembe
lakini si kwamba hakuwa na uwezo ndani yake wa kuyashinda
maswala ya (hisia za) mapenzi.
3. Wepesi katika kubadili uelekeo
CO
Paa na Ayala wana wepesi katika kubadili uelekeo, yaani anaweza
akawa anakimbia uelekeo fulani halafu ghafla akageuka na
kukimbia uelekeo mwingine kabisa, na mbinu hii huwapa tabu sana
maadui zao (simba, chui nk).
Wewe binti unayesoma kitabu hiki, kama ulikuwa umekimbia
uelekeo Fulani na unaona kabisa kuna hatari imekukaribia au
EE

inakukamata, leo fanya maamuzi ya kubadili uelekeo, leo ndio siku


ya kubadili uelekeo, geuza uelekeo mpaka aliyekuwa anakufukuzia
ashangae ni nini kimekutokea mpaka umebadilika kwa kiwango
hicho? Maarifa haya yakupe ujasiri wa kubadili uelekeo mpaka
wanaokufukuzia wakushangae.
FR

Wewe binti, usiwe mzito katika kufanya maamuzi. Unaona kabisa


huyu kijana wa kiume hauna hatima (future) naye zaidi ya
kukuharibia maisha yako, unaona kabisa kwa kweli haya
mahusiano yanaenda kukunyonga usichana wako halafu
unashindwa kufanya maamuzi eti kwa kuogopa utaumia moyo

16
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

ukiamua kumuacha. Hiyo sio asili yako, hiyo sio sifa ya binti, sifa ya
binti ni uwezo wa kufanya maamuzi anapogundua ueleko alio nao
ni hatari kwa maisha yake.
4. Urembo (beauty)
Paa na Ayala ni Wanyama wenye sifa ya urembo au ni Wanyama
warembo au kwa lugha nyingine watamu kwa Wanyama ambao ni

PY
maadui zao. Na hii ndio sababu ya kuwindwa na Wanyama wengi.
Ni Wanyama ambao hata kwa muonekano ni warembo.
Na hii ni mojawapo ya sifa za mabinti (wasichana wadogo). Mabinti
wote huwa ni warembo tu, msichana akiwa mdogo anakuwaga tu
mzuri (mrembo). Tatizo ni kwamba kuna mabinti wao hawajioni
CO
kuwa ni warembo, japo ukweli ni kwamba ni warembo, na hii ndio
sababu siku akiambia na kijana wa kiume kwamba ni mrembo,
jambo hilo haliondoki ndani yake na linaweza kuwa mtego wa
kujirahisi. Lakini, kama wewe binti umejitambua ni mrembo, ikitokea
kijana anakuambia mrembo haiwezi kuwa sababu ya kujirahisi, kwa
sababu anakuwa ameongea kitu ambacho wewe mwenyewe
unajitambua.
EE

Kwanza kabisa, wewe binti unatakiwa wewe mwenyewe kujiona


mrembo sababu ndivyo ulivyo. Urembo wako binti hauko kwa
kuambiwa na kijana wa kiume, wewe tayari ni mrembo hata kabla
hakuna mtu amekuambia; kuambiwa mrembo haipaswi kuwa
taarifa mpya kwako wewe binti. Anayekuambia wewe ni mbaya,
FR

mwambie hujaniangalia vizuri, kuna kitu ambacho hujakigundua


kwangu.
Lugha hii ya urembo, tukiisema ki­wanyama maana yake walikuwa
ni Wanyama wanono au watamu ndio maana wanawindwa na
Wanyama wengi. Na hivi ndivyo iliyo hata kwa mabinti, kwa sababu

17
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

ya urembo wao unaosababishwa na wao kuwa mabinti wadogo,


wanawindwa na wanaume wengi. Dunia ya sasa ilivyo ni kwamba,
mabinti sio tu wanawindwa na vijana wa kiume bali wanawindwa
mpaka na watu wazima ambao wengine wana umri hata sawa na
wazazi wa hao mabinti.
Dunia ya sasa utashangaa hata wanaume watu wazima na wenye
nafasi kubwa katika jamii na taasisi kubwa na wao wanawawinda

PY
mabinti, unakuta mkurugenzi yuko busy kutafuta vibinti vya miaka
kumi na au ishirini ya mwanzo ili alale navyo. Hawa ni wakurugenzi
wasio na akili timamu, walioharibikiwa akili zao. Wengine
wanatafuta kulala na mabinti ambao ni sawa kabisa na watoto wao
kiumri. Hii ni kwa sababu, roho ya uzinzi inaharibu akili ndio maana
CO
unakuta mkurugenzi anayetegemewa kufanya maamuzi ya
kampuni kubwa anakuwa busy na vibinti vya umri mdogo ambavyo
ni sawa na watoto wake.
5. Uwezo wa kufanya kile wanachokitaka kitokee
Paa na Ayala wakiamua wanaweza kufanya kile wanachokitaka
kitokee (to maneuver). Uwezo huu wa ku­maneuver akiwa
EE

anakimbia ndio ulikuwa unampa ugumu mkubwa sana adui yake


anapomfukuzia. Muwindaji alikuwa akipata ugumu sana kupata
hawa Wanyama, na ukiona amempata Paa na Ayala, ujue kuna
kosa Fulani Paa amefanya, yaweza kuwa ni ka­Paa/Ayala kadogo
hakajitambui au kuna makosa ya kiufundi yamefanyika.
FR

18
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

PY
SEHEMU YA NNE
ADUI MKUU WA PAA NA AYALA NA SIFA ZAKE
AKIMUWAKILISHA KIJANA WA KIUME
CO
A dui mkuu wa Paa na Ayala ni chui kisha ndipo huja maadui
wengine kama simba, mbwa pori, mamba nk. Nataka nieleze
kidogo kuhusu huyu mnyama anaitwa chui kwa sababu ndiye adui
EE

mkuu wa paa na ayala; wakati ninamuelezea chui, wewe binti


unayesoma kitabu hiki, weka picha ya kijana au vijana wa kiume.
Kwa hiyo kama kuna kijana yuko karibu na wewe binti na sio kaka
yako wa damu, wakati naelezea kuhusu chui, vuta picha ya huyo
kijana.
FR

Pamoja na kwamba Paa na Ayala wana uwezo wa kukimbia sana,


lakini kasi ya Chui ni Zaidi. Paa na Ayala ni wa pili kwa kasi (speed)
ya kukimbia, anayeongoza kwa kasi kwa Wanyama ni Chui. Chui
anakimbia kwa kasi ya kati ya kilometer 109 mpaka 120 kwa saa
(109­120Km/hr). Ukijaribu kulinganisha kasi ya Chui na Paa na
ayala utagundua, Paa na Ayala hawamuwezi kabisa Chui kwa kasi.

19
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

Chui ni wa kwanza kwa kasi, kisha wanafuatia Paa na Ayala, halafu


ndipo wanakuja Simba na Wanyama wengine.
Lakini kwa upande wa pili, udhaifu mkubwa wa Chui ni kwamba
hawezi kukimbia kwa kasi hiyo kwa muda mrefu kama Ayala na
Paa. Pamoja na kwamba Chui ana kasi kubwa lakini akikimbia
muda mfupi anachoka na anahitaji dakika 15 au Zaidi za
kupumzika, tofauti na Ayala na Paa ambao pamoja na kwamba

PY
hawamfikii Chui kwa kasi lakini wanaweza kukimbia kwa muda
mrefu bila kuchoka.
Hizi sifa pia wanazo vijana wa kiume wenye nia mbaya na binti,
wengi wana kasi katika kufukuzia mabinti ili wapate wanachokitaka;
namna nzuri ya kushughulika nao ni kutowaruhusu kabisa kupata
CO
wanachokitaka, wakifukuzia kwa muda bila matokeo watachoka na
kuhamia kwa binti mwingine.
Sifa (au nguvu) nyingine waliyonayo Chui ni mkazo katika ufuatiliaji
(focus). Kama umewahi kufuatilia namna ambavyo Chui
wanafuatilia Wanyama jamii ya swala, utagundua Chui huwa ana
mkazo kwa mnyama mmoja kati ya wengi. Chui akiona kundi la
EE

Swala au Paa na Ayala, anachofanya anaangalia mmoja tu


anayemtaka, akishamuona mmoja anayemtaka ataanza
kumkimbiza na wakati anamkimbiza kunaweza kuwa na kundi
kubwa karibu naye kuliko yule anayemkimbiza lakini Chui habadili
mkazo wake kwa yule anayemtaka, atamfukuka huyo huyo mmoja
mpaka ampate. Na hii ni sifa ya vijana wa kiume pia, wakianza
FR

kumfukuzia binti, anaweza akang’ang’ana na binti mmoja kiwango


ambacho binti akadhani yeye ni mzuri kuliko mabinti wote ndio
maana anafuatiliwa sana, kumbe sivyo ni kwamba binti anategewa.
Na mara nyingi hawa vijana akishampata tu binti akalala naye
nakumuharibia maisha basi ataachana naye na kuanza kufukuzia
mwingine.

20
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

Sifa nyingine ya Chui ni ushirikiano. Na hii sifa wanayo vijana wa


kiume pia.Vijana wa kiume huwa wana tabia ya kuambiana
kuhusiana na binti wakati wanamfukuzia. Binti akimkataa kijana
mara nyingi kijana huwa anawaambia vijana wenzie na wakati
mwingine wanapatana na mwingine akajaribu na ikitokea kijana
amempata binti basi ataanza pia kuwaambia vijana kwamba
nimeshampata yule; na hapo ndipo binti unashangaa unapita

PY
mahali, kila mtu anajua habari zako wewe na kijana fulani kwa
sababu umeshatangazwa kwa vijana wengine.
Unajua, kwenye maswala ya uzinzi kwenye jamii zetu, ni kama vile
aibu kubwa iko kwa binti kuliko kwa kijana wa kiume, japo dhana
hiyo sio sahihi kwa sababu kiroho tatizo liko kwa wote
CO
wanaojihusisha na uzinzi; lakini ni kama vile jamii zetu zimelipokea
jambo hilo kwa namna hiyo kwamba aibu kubwa ni kwa binti na sio
kwa kijana wa kiume; ndio maana msichana hawezi kutembea na
kijana wa kiume halafu ukamsikia anajisifia kwa tendo hilo lakini
kwa vijana wa kiume ni kawaida kabisa kwa wao kujisifia kwamba
ametembea na binti fulani na fulani. Ni vizuri wewe binti utambue
hili kwamba vijana wa kiume huwa wanaambiana kuhusu mabinti
ambao wanafanya nao ngono na pia wanashirikia katika
EE

kumfukuzia binti.
Sifa ya nyingine ya chui ni wepesi (swiftness) ambayo naweza
kuifananisha na sifa ya vijana wa kiume walivyo wepesi kugundua
uhitaji wa binti na kuutumia huo ili kumpata binti. Kwa mfano vijana
FR

wa kiume wengi ni wepesi kugundua kama binti ana shida ya


mahitaji fulani kama vile pesa. Na kijana akishagundua binti huyu
shida yake ni pesa basi kila akikutana na huyo binti atampatia
pesa. Wakati mwingine kijana wa kiume anagundua wewe binti
humtaki lakini hela zake unazitaka, kwa hiyo kila akija atakupatia
pesa. Au mwingine amegundua changamoto ya binti ni kwamba

21
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

anakaa mbali na anatembea mwendo mrefu, kwa hiyo kijana wa


bodaboda anaichukua hiyo kama fursa ya kumpata binti kirahisi.
Anambeba kwa bodaboda na anakataa asimlipe hela kwa kigezo
kwamba ameamua kumsaidia lakini ukweli ni kwamba anataka
atumie fursa kumpata.
Binti anaambiwa na kijana wa bodaboda, leo usilipe na kila ukihitaji
usafiri nitafute nitakusaida bure kabisa, na binti bila kufikiria

PY
anafikiri amepewa ofa, asiwaze kwamba yule bodaboda ni mfanya
biashara, haiwezekani atoe hizo ofa wakati yeye mwenyewe jioni
atatakiwa apeleke hesabu kwa boss wake. Kwa kijana ambaye
amekusudia kumuharibia binti maisha, anaweza akakubali
kumpakia bure au kumsaidia binti kwa muda mrefu hata miezi
CO
kadhaa, akiwa na lengo kwamba binti amuamini na amfungulie
moyo wake; lengo lake ni kwamba ukikaa mwenyewe ndani
chumbani, umuwaze yeye kwamba ni mtu mzuri sana, mwenye
huruma sana na umfungulie moyo wako, yaani aingie ndani ya
moyo wako. Na anajua akishaingia ndani ya moyo wako, atakuwa
rahisi sana kuupata mwili wako. Wewe binti, kama kuna kijana
yeyote ndani ya moyo wako umeanza kumuona ni mtu mzuri sana
na umeanza kumuhurumia na umemfungulia moyo, ujue unajiweka
EE

hatarini kwa kijana huyo siku akiamua kutaka mwili wako.


Sifa nyingine ya chui ni kujiamini. Na hii pia wanayo vijana wa
kiume, kuna vijana wanajiamini sana kwa mabinti. Binti anajaribu
kila mbinu ya kumfukuza, kumtishia kwamba atamsema kwa
FR

mwalimu, wazazi n.k. na hata wakati mwingine kumtukana lakini


kijana anarudi tena na tena. Kujiamini huku kwa vijana wa kiume
mara nyingi kunamfanya binti aone kuwa kijana ana nia thabiti ya
kuwa nae katika mahusiano ya kweli na pengine ana nia njema ya
kumchumbia na kumuoa hapo baadae, lakini ukweli ni kwamba,
vijana wengi wa kiume huwa wanajiamini ili kuwadanganya na

22
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

kutimiza malengo yao ya kuwapata mabinti na kuwaharibia maisha


yao hasa baada ya kufanikiwa kufanya nao mapenzi.
Sifa nyingine ya chui, ni kuwa wana uwezo wa kuongeza kasi yao
kwa haraka (acceleration). Pia wana uwezo wa kuvizia na kurukia
vitu kwa haraka. Na Ndivyo walivyo vijana wa kiume wengi,
wanaweza wakawa wanamfuatilia binti kimya kimya kwa kuvizia.
Binti unashangaa huwa unapita mahali kumbe kuna kijana au

PY
vijana wanakufuatilia na kukuvizia, unakuta kijana anakufuata
wewe humfahamu kabisa lakini yeye anakufahamu kila kitu,
kuanzia jina, umri, nyumbani kwenu, shule yako, njia unayopita kila
siku, marafiki zako n.k. mpaka unashangaa. Lengo lake ni
kuonekana yeye si mgeni (stranger) kwako na iwe rahisi kupata
CO
nafasi kwako. Hii ni sifa mojawapo wanayoitumia vijana wa kiume
wawindaji wa mabinti.
Mbinu kubwa ya paa na ayala ambayo inamsaidia kujilinda na chui,
japo chui amemzidi kwa kasi, ni uwezo wake wa kukimbia
akirukaruka na kupiga kona kona (Stotting and Zigzag running) na
hii ndio inampatia wepesi kukabiliana na Chui na Wanyama wa
aina hiyo pamoja na kwamba wamemzidi kasi. Kumbuka kwamba,
EE

kama nilivyosema kabla, anapokimbia kwa kurukaruka na


kuhamahama, anakuwa anatoa taarifa kwa wenzie kwamba kuna
adui lakini pia anamjulisha Chui au adui yake kwamba huniwezi.
Binti unayesoma kitabu hiki, unajua moja ya dawa ya kushughulika
na kijana ambaye umegundua ana nia mbaya na wewe ni kuanza
FR

kuwaambia na wenzio habari zake, waambie kwamba kijana fulani


si mtu mzuri, ana nia mbaya na mabinti. Unavyoendelea kumtunzia
siri za tabia yake mbaya utakuwa unaendelea kumfuga na kumpa
nguvu; unapomuweka wazi (expose) kwa wenzio na hata kwa watu
wazima (wazazi, walezi, walimu nk), hii itakulinda na wewe pia.
Unapowaambia wenzio, kwa namna nyingine ni kufikisha taarifa

23
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

kwake kwamba umegundua nia yake mbaya na hauko tayari


kuendelea kuivumilia. Maandiko yanathibitisha kwamba, paa ana
uwezo kabisa wa kujiponya na mkono wa mwindaji; Katika Mithali
6:5 “Ujiponye kama paa na mkono wa mwindaji, Na kama
ndege katika mkono wa mtega mitego.”
Andiko hili linathibitisha uwezo wa paa kujiponya, kwa hiyo ikitokea
paa amekamatwa na mwindaji ujue kuna shida mahali, kuna mahali

PY
alijisahau. Binti anayenaswa na kijana wa kiume katika mapenzi ni
wazi kwamba kuna mahali amekosea, lakini ukweli ni kwamba kila
binti anao uwezo wote wa kujiponya na uwindaji wa vijana wa
kiume.
Mara nyingi, kama si mara zote, paa na ayala huwa wanakamatwa
CO
wakati wanaposimama kuangalia kama Chui bado anawafuatilia.
Wakati Paa na Ayala wanakimbia kwa ile aina yao ya ukimbiaji,
wakiwa wanamkimbia Chui, kuna muda Paa au Ayala anasimama
kuangalia kama Chui bado anamkimbiza; muda huo amesimama
ndio mara nyingi hujikuta amekamatwa, lakini sio kwamba hawana
uwezo wa kuwashinda maadui zao, wanao uwezo wote. Paa na
Ayala wakiwa makini wakaendelea na aina yao ya ukimbiaji wao,
EE

hata kama wanaangalia basi waangalie huku wanakimbia, sio rahisi


wakamatwe na maadui zao.
Mabinti wengi pia huwa wanajikuta wamenaswa na mtego pale
wanaposimama kuangalia na kusahau mbinu zao. Mabinti wengi
hunaswa wanaposimama kuangalia kama kijana anampenda kweli,
FR

anajaribisha kumkubalia ajenda yake labda ya kwenda naye


kwenye matembezi (outing), au labda ya kukaa naye karibu
akiamini maneno ya kijana kwamba anataka urafiki tu wa kawaida,
na bila kufahamu hujikuta amenaswa kwenye mtego. Mabinti wengi
wananaswa wanapolegeza misimamo yao kwenye namna
wanavyohusiana na vijana wa kiume. Mwingine alikuwa na

24
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

msimamo wa kutomtembelea kijana wa kiume, lakini baada ya


kuwa kijana ‘amemkimbiza’ muda mrefu anaamua kulegeza
msimamo na kukubali kuanza kumtembelea kijana wa kiume
nyumbani kwake na mwisho wa siku hujikuta mtegoni.Mabinti
wengi hawajui hata namna ya kutofautisha upendo na tamaa, na
mambo mengi wanayohisi ni upendo unakuta yanasukumwa tu na
tamaa na sio upendo wa kweli. Ninaamini Asilimia 99 ya vitu

PY
ambavyo mabinti wengi wadogo wanavitafsiri kama upendo toka
kwa kijana wa kiumbe, ni tamaa.
Kile kinachotafsiriwa kuwa ni upendo kwa mahusiano ya binti na
kijana wa kiume mara nyingi kama si zote ni tamaa, kama wewe
binti haujafikia umri wa kuolewa na hauko tayari kuolewa
CO
mahusiano yeyote ya kimapenzi mtakayokuwa nayo na kijana wa
kiume hayana upendo ndani yake bali yamejaa tamaa mbaya
yenye uharibifu. Upendo wa kweli huzaa uwajibikaji, yeyote
anayesema anakupenda na hayuko tayari kuwajibika kwa maisha
yako huyo mtu hakupendi anakutamani. Binti ni vizuri utambue hili
na usijiingize kabisa kwenye mahusiano ya mapenzi kama hujafikia
umri na wakati wa kuolewa. Kwa hiyo, kama hakuna ndoa ujue
hakuna upendo.
EE

Unajua Upendo ni zao la Mungu. Ndio maana maandiko yanasema


Mungu ni Upendo. Kwa hiyo upendo wa kweli hauwazi uzinzi,
haumsukumi mtu kufanya uzinzi. Hisia Nyingi tunazoita upendo ni
tamaa tu zinatesa mabinti na vijana.
FR

KWA NINI PAA, AYALA NA CHUI?


Tunachopaswa kufahamu ni kwamba, kila mnyama ambaye Neno
la Mungu limemtaja, huwa kuna funzo kubwa nyuma yake. Biblia
huwa haitaji tu Wanyama bila sababu, liko funzo kubwa kutokana
na huyo mnyama na mara nyingi ni funzo toka kwa tabia za

25
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

mnyama husika. Kwa hiyo lengo sio mnyama kimsingi, bali ni funzo
au ile hekima kutoka kwa tabia za huyo mnyama.
Mimi kuandika haya yote kuhusu Paa na Ayala na Chui, usije
ukadhani ninataka sana ujue habari za Wanyama, kitabu hiki sio
shule ya Wanyama, bali lengo lake ni wewe BINTI UPATE HEKIMA
(FUNZO) INAYOTOKA HAPO KWA HAO WANYAMA. Kama wewe
binti unayesoma hiki kitabu utaelewa tabia za paa na ayala na

PY
miondoko yao halafu usipate funzo na kujua cha kufanya kwenye
Maisha yako ya ubinti basi hiki kitabu kimeshindwa kukusaidia na
hakitakuwa na maana kwako. Sasa, baada ya maelezo hayo
niliyoweka hapo juu, nataka nikukumbushe tena lile andiko letu
ambalo pia nimelifafanua kwenye utangulizi na kutokana na
CO
maelezo tuliyojifunza . Nitalinukuu tena andiko letu la msingi nikiwa
nimeweka maelezo ndani yake ili uelewe vizuri zaidi
Wimbo uliobora 2:7 “Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, Kwa
[Kutumia HEKIMA ya] paa na kwa [HEKIMA ya] ayala wa porini,
[JILINDENI] Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, Hata
yatakapoona vema yenyewe.”
EE

Andiko hilo ni sawa kabisa na kusema “Ninakusihi, wewe binti


unayesoma hiki kitabu, kwa kutumia HEKIMA ya Paa na kwa
HEKIMA ya Ayala wa porini uliyojifunza katika kitabu hiki,
JILINDE, usiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, hata
yatakapoona vema yenyewe.”
FR

26
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

PY
SEHEMU YA TANO
UPANDE WA PILI WA AYALA NA PAA
CO
M ithali 5:19a “Ni ayala apendaye na paa apendezaye...”.
Andiko hili litatusaida kuelewa kwanini Mfalme Suleimani
aliwataja wote Ayala na Paa kwenye andiko letu la msingi la
Wimbo Ulio Bora 2:7. Tukiunganisha andiko letu la msingi na
EE

sehemu hii ya kwanza ya andiko hili la Mithali 5:19 tunaweza kuwa


sahihi kabisa tukiliandika hivi andiko la Wimbo uliobora 2:7
“Nawasihi enyi binti za Yerusalemu, kwa PAA [APENDEZAYE]
na kwa AYALA wa porini [APENDAYE], msiyachochee mapenzi
wala kuyaamsha hata yatakapoona vyema yenyewe”
FR

PAA ANAWAKILISHA UREMBO WA NJE WA BINTI(MSICHANA)


Mithali 5:19a “Ni ayala apendaye na paa apendezaye...”
1. “Paa Apendezaye”. Paa anawakilisha urembo wa nje, kwa
sababu kinachopendeza ni kizuri. Kwa hiyo anaposema ‘Paa
apendezaye’ anazungumzia urembo au uzuri wa nje wa msichana.

27
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

Kwa hiyo, wewe binti unayesoma hiki kitabu, kwa uzuri wako wa
nje na kwa urembo wako, usiyachochee mapenzi wala kuyaamsha.
Unajua, kuna mabinti/wasichana ambao kinachowaharibu au
kilichowaharibu ni kwamba walijiona wazuri sana; alianza
kuharibikiwa pale alipojigundua yeye ni mzuri kuliko wadada
wengine, labda kwa rangi yake, au sura yake au umbo lake, na
wakati mwingine alipokuwa akisifiwa sana na kila mtu kwamba

PY
yeye ni mzuri.
Wapo wasichana wa aina hiyo, kwamba wanajiona wazuri sana na
uzuri wao ndio unawapoteza. Ndio maana Neno la Mungu
linasisitiza, kwa paa akimaanisha kwa urembo wako, kwa uzuri
wako, kwa heshima yako, kwa mvuto ulio nao, kwa muonekano
CO
wako mzuri, kwa umbo (shape) lako, usiyachochee mapenzi.
AYALA ANAWAKILISHA HISIA ZA NDANI YA BINTI(MSICHANA)
Mithali 5:19a “Ni ayala apendaye na paa apendezaye...”
2. “Ayala Apendaye”. Ayala anawakilisha hisia za ndani. Ayala
anawakilisha hisia za ndani kwa sababu kupendeza au urembo
(ambao unawakilishwa na paa) ni kitu cha nje lakini kupenda ni kitu
EE

cha ndani. Hivi vitu viwili, kupendeza na kupenda, vinafanya kazi


kwa pamoja; yaani Urembo wa nje na hali ya hisia za ndani.
Andiko lingine linaloweza kutupa mwanga mwingine wa Ayala ni
Zaburi 42:1a “Kama Ayala aioneavyo shauku mito ya maji…”
FR

Andiko hili linaonyesha wazi, Ayala anawakilisha kiu au shauku ya


ndani, au shauku ya nafsi au kwa lugha nyingine hisia za ndani.
Binti asipokuwa makini na urembo wake wa nje na hisia au kiu
zake za ndani, anaweza akajikuta vimemuamshia mapenzi kabla
ya wakati wake.

28
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

Ninaliweka tena hapa andiko letu la msingi kwa mtazamo mpya


kutokana na tafsiri nilizotoa hapo juu.
Wimbo uliobora 2:7 “Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, Kwa Paa
(kwa Muonekano wa nje ­ [yaani urembo, heshima, mapambo, sura
na mvuto wako]) na kwa ayala wa porini (kwa hisia zako za ndani –
[Yaani kwa Kiu yako ya mapenzi, hisia za mapenzi au za
kupenda]), Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, hata

PY
yatakapoona vema yenyewe.”
Unajua, kuna namna kila binti, na sio tu kila binti, kila binadamu
ndani yake ana hisia za kupenda au za mapenzi, na hisia hizo sio
dhambi. Kuna wadada wakisikia hali fulani ya hisia za mwili
wanafikiri tayari wameshamkosea Mungu na Shetani anatumia
CO
fursa hiyo kumkatisha tamaa. Ni vizuri kufahamu kwamba, binti
yeyote akiwa ameshavunja ungo (amepevuka), kuna kipindi katika
mzunguko wake wa mwezi hisia zake zinabadilika na kuwa juu
tofauti na siku zingine. Hata vijana wa kiume pia vipindi vya hisia
zao vinapishana, kuna wakati hisia zao za mwili zinakuwa juu
kuliko wakati mwingine. Yai la mwanamke linapojitengeneza ndani
ya binti, kuna wakati linafikia linakuwa tayari kukutana na mbegu ili
EE

kutengeneza mtoto, na wakati huo ndipo kuna namna hisia za binti


zinabadilika na kuwa juu, na hilo yai lisipokutana na mbegu ndipo
hufika kipindi hupasuka na ndipo binti anaingia kwenye siku zake;
sasa haya ni maumbile ya kawaida na hakuna tatizo lolote kwenye
hisia hizo.
FR

Ndio maana Neno la Mungu linasisitiza, kwa Paa na kwa Ayala,


akimaanisha kwa urembo wako wa nje lakini pia hata unapokuwa
na hali fulani ya hisia za ndani za mapenzi, bado usiyaamshe
mapenzi.

29
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

Tatizo sio urembo wala tatizo sio hizo hisia za ndani, tatizo ni je
unaitikiaje hizo hisia zinapokuja? Hizo hisia sio dhambi, siku
ukiolewa utaelewa kwamba hisia sio dhambi. Ukiolewa halafu
ukajikuta huna kabisa hisia ndio utaelewa hiki ninachokuambia.
Hizo hisia ni Mungu ameziweka lakini ziamshwe kwa wakati wake.
Hizi sifa za nje na ndani za Paa na Ayala ni tatizo kubwa kwa
wasichana wasipojua kuzimudu. Wewe binti unayesoma hiki kitabu,

PY
ninakusihi, urembo wako usikufanye uyaamshe mapenzi, na hata
hizo hisia, hata zikija kwa nguvu kiasi gani, usiziruhusu
zikayaamsha mapenzi. Siku zote itikia kinyume na hisia na sio kwa
uelekeo wa hisia zako, usizitimizie hisia zako matakwa yake.
Usiziendekeze hisia zako, unao uwezo wote wa kuzimudu bila
kukukosesha.
CO
HAYAJAZIMIKA WALA HAYAJAFA, UKIYACHOCHEA YATAWAKA,
UKIYAAMSHA YATAAMKA.
Turudi tena kwenye andiko letu la msingi, kuna jambo lingine
tunatakiwa tuliangalie hapo:­
Wimbo Ulio Bora 2:7 “Nawasihi enyi binti za Yerusalemu, kwa
EE

PAA na kwa AYALA wa porini, msiyachochee mapenzi wala


kuyaamsha hata yatakapoona vyema yenyewe.”
Neno la Mungu linasema “msiyachochee mapenzi wala
kuyaamsha”; kama umewahi kupikia kuni ni rahisi kuelewa neno
lililotumika hapo “msiyachochee”. Kuni zinazochochewa ni zile
FR

ambazo zina moto au zinawaka, kuchochea mara nyingi huwa ni


kuchukua kuni zingine na kuziongezea. Huwezi kuchochea kuni
zisizowaka. Maana yake ni kwamba, mapenzi kama moto mdogo
mdogo yamo ndani ya kila binti kama nilivyoeleza juu, au kwa lugha
rahisi ni kwamba hisia za mapenzi zimo kwa binti ndio maana binti
anaambiwa asiyachochee au asizichochee hizo hisia. Kila

30
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

binadamu ndani yake anazo hisia fulani za mapenzi hasa


anapokuwa amepevuka; tofauti zetu ni kwamba wenginze
wanazichochea wengine hawazichochei.
Lakini pia Neno linasema “Wala kuyaamsha”, Neno halisemi
“wala kuyafufua”; maana yake ni kwamba hayo mapenzi
hayajafa, kwa sababu wanaoamshwa hawajafa bali wamelala; kwa
hiyo, mapenzi ndani ya binti yamelala hayajafa. Kila binti anazo

PY
hisia za mapenzi ndani yake, isipokuwa tunatofautiana ulalaji wa
hizo hisia au tunavyoziamsha hizo hisia. Kuna mabinti wengine,
kutokana na vitu anavyojihusisha navyo kusoma, kutazama,
kusikiliza, vinasababisha hisia zao zinakuwa zimelala usinginzi wa
mang’amung’amu (usinginzi nusu) au wengine hazijalala kabisa
CO
ziko macho sababu wameziamsha. Kwa hiyo, binti yangu,
usiyachochee wala kuyaamsha mapenzi mpaka yatakapoona
vyema yenyewe; yaani mpaka umri utakaofikiwa rasmi kiafya, na
kupata kibali kutoka kwa Mungu na wazazi, na kumpta mwenza, na
kufunga naye ndoa, ndipo utakaoanza kufanya mapenzi na
mwenza wako.
Bahati mbaya ni kwamba, mapenzi yakiamka, kuyalaza ni kazi
EE

nyingine ngumu. Ndio maana mabinti wengi wakishajiingiza


kwenye maswala ya mahusiano ya mapenzi, wanakuwa
hawamuelewi mtu yeyote anayejaribu kuwarekebisha. Ndio maana
unaweza ukakuta binti, wakati mapenzi yamelala, yaani
hajajihusisha na maswala ya mapenzi, anakuwa msikivu sana kwa
FR

wazazi, mama na baba au walezi; wakimuambia usiende huku


haendi, usiwe karibu na kijana fulani anatii lakini mara tu baada ya
kuruhusu kuamshwa mapenzi na kuingia kwenye mahusiano ya
kimapenzi, akili zote zinaruka na anaanza kutokuwa msikivu kwa
wazazi, walezi, walimu nk.

31
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

Unashangaa binti baada ya kuwa amejiingiza kwa maswala ya


mapenzi, anahisi kama wote wamepitwa na wakati utadhani yeye
ndio mwanzilishi wa mapenzi, kumbe yalikuwepo tangu Adamu na
Eva.
Ndio maana Neno la Mungu katika Mithali 6:32 linasema, “mtu
aziniye na mwanamke hana akili kabisa; afanya jambo
litakalomwangamiza nafsi yake.”

PY
Hosea 4:11 “Uzinzi na divai na divai mpya huondoa fahamu za
wanadamu.”
CO
EE
FR

32
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

PY
SEHEMU YA SITA
BINTI/MSICHANA KUUWEZA MWILI WAKE
CO
U jumbe ambao nimekuwa nikijaribu kuuleta kwako binti ambaye
unasoma kitabu hiki ni kwamba, unapaswa kuuweza mwili
wako pamoja na mazingira yako, ili kwa namna yeyote ile,
usiamshe hisia za mapenzi na mwisho wake ukajikuta umepata
EE

madhara ya kiroho na ya kimwili au kijamii au kimaisha kwa ujumla.


Sasa, katika sehemu hii, nataka tuangalie kwa undani Zaidi namna
ambavyo Neno la Mungu linatusisitiza kuuweza mwili.
1 Wathesalonike 4:3­5 [3]Maana haya ndiyo mapenzi ya
Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati; [4]kila
FR

mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na


heshima; [5]si katika hali ya tamaa mbaya, kama mataifa
wasiomjua Mungu.
Anaposema uasherati kwenye andiko hilo, ni wazi anazungumza
na vijana na mabinti ambao hawajaoa na kuolewa, kwa sababu

33
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

angekuwa anaongelea wanandoa angesema uzinzi. Lakini pia


andiko hilo linaongelea kwamba, uko ujuzi wa kuuweza mwili ndio
maana nasema “kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili”. Kama
nilivyoeleza huko juu, tatizo sio hisia ambazo ziko kwa mabinti,
tatizo kubwa ni kutokujua namna ya kuziweza au kuzimudu hizo
hisia. Kwa hiyo, binti yangu, unapaswa kujua kuuweza mwili wako
na hisia zako. Na ukweli ni kwamba kila binti anauweza mwili wake,

PY
nikimaanisha kwamba anao uwezo ndai yake wa kuuweza mwili
wake. Mungu hawezi kukupa mwili unaokushinda binti yangu,
Mungu amekupa huo mwili unao uwezo wa kuumudu na hisia zake.
Hujapewa miili miwili wala hisia za watu wawili, umepewa hisia
zako peke yako, labda kama kuna pepo au nguvu za giza ndani; na
kama lipo pepo linaondoka sasa unaposoma kitabu hiki kwa jina la
Yesu.
CO
Kila binti, anapaswa kuweza au kujua kujizuia tamaa za mwili wake
zisimkoseshe, asiziamshe na zikamkosesha. Unajua njaa pia ni
tamaa kama zingine, ni tamaa ya chakula; kuna watu sababu ya
njaa anaiba au hataki kufunga, sasa hapo shida sio njaa lakini mtu
ameshindwa kuimudu njaa au wengine ni kuiendekeza njaa kama
Esau alivyoiendekeza njaa akauza uzaliwa wake wa kwanza. Na
EE

ndivyo ilivyo kwa tamaa zingine, kwa hiyo, wewe binti, usikubali
mwili ukuendeshe. Bodaboda inaendeshwa na dereva aliyeipanda,
haimuendeshi aliyeipanda. Ukikubali bodaboda ikuendeshe
itakupeleka mtaroni na hata kukuua, na tatizo halitakuwa bodaboda
bali ni aliyeipanda, lakini ukiiendesha bodaboda inaweza
FR

kukusaidia na kukupeleka mahali ambapo usingeweza kufika


kirahisi.

34
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

PY
SEHEMU YA SABA
MAENEO YA BINTI KUJILINDA ILI
ASIYACHOCHEE WALA KUYAAMSHA MAPENZI
CO
N inajua kwamba kitabu hiki kinaweza kusomwa na mabinti
ambao wamefikia umri wa kuolewa lakini sehemu kubwa ya
kilichofundishwa kinawalengwa sana mabinti ambao hawajafikia
EE

kabisa umri wa kuolewa japo hata binti aliyefikia umri wa kuolewa


ana mambo mengi anaweza kujifunza na yakamsiaida kujitunza.
Yafuatayo ni maeneo matano muhimu sana ya kujilinda na
kujitunza ili binti usiyachochee wala kuyaamsha mapenzi kabla ya
wakati wake:­
FR

1. Jiepushe na aina yeyote ya mahusiano ya kimapenzi (au


kama wapenzi, wachumba, uboyfriend nk, hata kama hamfanyi
chochote) kama unajua bado hujafikia wakati wa kuolewa.
Ninaposema mahusiano ya kimapenzi ninamaanisha mahusiano

35
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

yeyote kama wapenzi hata kama mnasema hamna chochote


mnafanya na mnasema kwamba mnajitunza msifanye zinaa; kwa
usalama wako binti jiepushe na mahusiano ya aina hiyo pia.
Jiepushe na mahusiano yeyote ya urafiki ambao una lengo la kuja
kuoana au kuwa wachumba kama unajua wakati wako wakuolewa
haujafika.
Unakuta binti bado anasoma shule ya msingi (Primary) au

PY
sekondari (O­Level au hata A­Level) halafu anasema nina
mchumba wangu. Kuna mabinti wengine, wanajiita wameokoka na
wanakuwa na “boyfriends”, na hii boyfriend hawamaanishi rafiki wa
kawaida wa kiume bali ni mpenzi wake. Kama wewe binti una
“boyfriend” na unasema umeokoka, nina mashaka makubwa na
CO
wokovu wako. Ninajua tamaduni hizi za kizungu zimeingia na huku
kwetu na hata mpaka makanisani, lakini ukweli unabaki pale pale,
mahusiano yeyote ya kimapenzi nje na kabla ya ndoa ni dhambi na
hayakubaliki.
Wewe binti unayesoma kitabu hiki, kama ulikuwa na mahusiano ya
kimapenzi au boyfriend, huu ndio wakati muafaka wa kuvunja
mahusiano hayo ambayo yamekuwa kinyume na mpenzi ya
EE

Mungu. Ukweli ni kwamba, maamuzi ya kuvunja mahusiano au


kuachana yanaweza yasiwe rahisi lakini ni muhimu sana kwa
usalama wako na ubinti wako. Unajua, mnapokuwa na mahusiano
na kijana wa kiume, mahusiano hayo sio kwamba ni ya mwilini
pekee bali unapaswa kufahamu kwamba na nafsi zenu zinahusika
FR

pia. Sasa, namna mnavyohusiana au mnavyoendesha mahusiano


yenu ndio itaamua na nafsi zenu zinaungana (soul tie) kwa kiwango
gani. Kwa kadiri unavyoendelea kumruhusu kijana/mvulana na
kumpa uhuru kwenye mwili wako, ndio kwa kadiri hiyo hiyo na
muunganiko wa nafsi (soul tie) zenu unakuwa mkubwa na inakuwa
ngumu zaidi kuachana, hii inapelekea mabinti wengine kusema

36
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

ninampenda sana huyu kijana siwezi kabisa kumuacha wakati


mwingine hata ambapo binti amegundua kabisa kwamba huyu
kijana sio mtu sahihi na sipaswi kuhusiana naye. Ukweli ni
kwamba, tatizo sio kwamba binti anampenda sana kijana bali ni
kwamba nafsi (hisia) zimeungana kwa kiwango kikubwa kiasi
ambacho saa yakutengana hisia au nafsi inasikia maumifu sababu
ya mazoea. Ukweli ni kwamba, hayo maumivu hayasababishwi na

PY
upendo bali yanasababishwa na muunganiko wa hisia/nafsi pamoja
na mazoea mabaya mliyokuwa nayo. Kwa hiyo, kama mmeungana
sana nafsi zenu, majeraha na maumivu yatakuwa makali zaidi na
kinachomtesa binti sio upendo bali ni maumivu ya nafsi au hisia.
Maumivu saa ya kuachana ni suala la kawaida, lakini ukweli
mwingine ni kwamba, maumivu hayo hayawezi kukuua… kuna
CO
mabinti wengine kwa sababu ya hali ya muunganiko wa nafsi
wanasema “mimi siwezi kuishi bila kijana fulani nahisi
nitakufa”; huwezi kufa kwa sababu mtu huyo sio Mungu wala sio
pumzi unayopumua; ni kweli itauma lakini itapona na haitakuua.
Yale maumivu ni kwasababu ya hisia kuungana na sio uhalisia
unaoweza kumuua mtu.
Lakini pia, kumbuka unaposoma kitabu hiki iko neema kubwa ya
EE

Mungu kukusaidia kukutenganisha na kila mtu asiye sahihi,


naamini kama wewe ni muhanga wa ninachokisema hapa, basi
neema ya Mungu na mafuta ya Roho Mtakatifu yatakusidia
kuachana na kila mtu asiye sahihi na kuuponya moyo wako kwa
wepesi na kwa haraka bila maumivu makali, lakini usisahau
FR

kwamba, Mungu anakutarajia ufanye maaumuzi hayo sahihi


haraka.
Ili uelewe vizuri ninachokisema hapa kwamba kinachomtesa binti
wakati wa kuachana ni mazoea, mfano mzuri ni sawa na mtu
aliyejizoeza kula aina fulani ya chakula (labda maziwa) kila

37
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

inapofika saa 4 asubuhi, mtu huyu akifanya hivi kwa muda mrefu,
itafika mahali ikifika saa 4 akakosa kikombe cha maziwa atahisi
kama ndio anakufa kwa hali ya mwili wake kuhitaji maziwa. Sasa
kiuhalisia ni kwamba, pamoja na hali anayojisikia wakati wa
kunywa maziwa ukifika, bado hali ile haiwezi kumuua. Ndivyo ilivyo,
unapokuwa unawasiliana sana na kijana wa kiume hasa
mawasiliano ya kimapenzi na kujaliwa sana, nafsi yako inakuwa

PY
inalishwa, na baada ya muda inakuwa imezoea kulishwa maneno
matamu matamu toka kwa huyo kijana na hata kuulizwa kama
umekula au umelalaje/umeamkaje/unaendeleaje/umevaaje nk;
sasa ikifika muda ambao nafsi imezoea kujaliwa kwa maneno au
matendo fulani halafu haipati hicho chakula toka kwa kijana huyo,
nafsi itakuwa na uhitaji mkuwa na hata kusikia kama vile huwezi
CO
kuishi bila maneno na mazoea mliyokuwa nayo, na hapo ndipo
sasa binti huanza kuhisi kwamba bila huyo kijana hawezi kuishi,
lakini ukweli ni kwamba baada ya muda na kwa neema ya Mungu
juu yako unayesoma kitabu hiki, ukifanya maamuzi ya kumaanisha
na kung’ang’ania, hiyo hali itaisha na utafunguliwa kabisa toka
katika kifungo hicho cha nafsi.
Kama binti hujaingia kwenye hiki ninachokieleza, basi jilinde
EE

usinaswe kabisa; lakini kama wewe tayari umenaswa na


mahusiano haya ya kabla ya wakati, fanya maamuzi magumu na
ya kumaanisha kuachana na mahusiano hayo, kisha jipe muda wa
kupona na kukata huo muunganiko, kama inawezekana tafuta
mtumishi wa Mungu mwenye mafuta ya Roho Mtakatifu mwambie
FR

akuwekee mikono kukata huo muunganiko (connection), lakini pia


unaweza ukamshirikisha mzazi au mlezi wako; ninakuhakikishia
utaona Mungu akikuvusha hapo.
Ujumbe wa kwanza ambao ninataka kufikisha kwako binti, ili
kujilinda usiyachochee mapenzi ni huu, jiepushe na aina yeyote ya

38
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

mahusiano ya kimapenzi (ikiwemo uchumba na kuwa na boyfriend)


kama bado hujafikia wakati au umri wa kuolewa. Jambo hili
linawezekana kabisa ikiwa binti amefanya maamuzi. Inawezekana
kabisa binti akaishi bila kuwa katika mahusiano ya kimapenzi
mpaka itakapofikia wakati wake wa kuolewa akawa na mchumba
wa kuelekea ndoa. Na hakuna uchumba kama hakuna lengo na
uhakika wa ndoa mbele. Unakuta mabinti wako shule na

PY
wanasema nina mchumba, uchumba sio jambo dogo uchumba ni
commitment inayohusiasha mapatano au agano mpaka kwa
wazazi, kama wakati huo bado usijihusishe kabisa na mahusiano
ya kimapenzi. Uchumba ni agano la kuelekea ndoa, mfano mzuri ni
wakati Yusufu amemchumbia Mariam, malaika anamwambia
Yusufu, usimuache mkeo kwa sababu mimba aliyonayo ni kwa
CO
uwezo wa Roho Mtakatifu (Mathayo 1:20). Kwa hiyo, kama bado
hujafikia umri wa kuolewa, na kijana bado hayuko tayari kubeba
wajibu wa ndoa, yaani hajaja kwenu kujitambulisha na kulipa
maharI, haruhusiwi kuitwa mchumba.
Swali la msingi la kujiuliza wewe binti, je wakati wako wa kuolewa
umefika? Kama jibu ni bado, basi huruhusiwi kuwa katika
mahusiano, na kama uko kwenye mahusiano ya kimapenzi yavunje
EE

sasa, kwa sababu lazima utaishia kuyaamsha mapenzi kabla ya


wakati wake na yatakusumbua na kukupeleka pabaya na hata
kukuharibia Maisha na hatma yako.
2. Jilinde namna unavyohusiana au kuishi na watu wa jinsia
FR

tofauti (wavulana)
Hili ni eneo la pili muhimu sana kwa wewe binti kujilinda, yaani
namna unavyohusiana na kuishi na vijana wa kiume (wavulana).
Ninaposema “jilinde unavyohusiana”, simaanishi kuwa na
mahusiano ya kimapenzi, hapana, ninaongelea mnavyojikuta

39
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

mkiwa pamoja kwa sababu mbalimbali za kimaisha labda shuleni,


au kanisani au kwenye shughuli fulani ya kijamii. Hatuwezi kuzuia
binti kujichanganya au kuwa pamoja (to interact) na kijana wa
kiumbe lakini ni muhimu sana kujilinda wewe binti kila wakati
unapokuwa pamoja nao.
Ni vizuri kutambua kwamba, asilimia kubwa ya vijana wa kiume,
kama sio wote, huwa wana ajenda ya (jambo lao la) siri

PY
wanapohusiana au kuwa karibu na msichana; mara nyingi mabinti
wengi wanapokuwa karibu na kijana wa kiume huwa hawana nia
mbaya japo wapo kadhaa wenye nia mbaya; lakini vijana wengi wa
kiume huwa wana ajenda zao za siri (wana nia mbaya)
wanapohusiana au kujichanganyana mabinti, isipokuwa wengi
CO
huwa hawadhihirishi nia zao haraka kwa sababu wanakuwa
wanamsoma binti kwamba atamuelewaje akiidhihirisha nia yake
mapema, lakini ikitokea amepata mwanya basi atautumia ipasavyo.
Lakini, kwa upande mwingine, inawezekana kijana wa kiume hana
ajenga yeyote ya siri (hana nia mbaya), lakini vijana wengi wa
kiume huwa, bila kutaka, wanajikuta wanaingia kwenye mtego
katika kuhusiana na mabinti. Hii inatokana na nilichokieleza katika
EE

sura zilizopita za kitabu hiki kwamba tamaa ya mwanaume au


kijana wa kiume iko kwenye macho au inaamshwa na macho Zaidi.
Kwa hiyo, ni vizuri sana wewe binti uwe makini sana namna
unavyohusiana na mvulana. Kwa sababu anaweza akawa, wakati
mnajichanganya au kuwa pamoja naye, hana nia mbaya kabisa,
FR

lakini kwa sababu ya tamaa kuanzia kwenye kutazama, na hana


msimamo mzuri kwenye wokovu, akajikuta anaanza kutoka kwenye
mstari na kukutaka kimapenzi.
Ninaposema jilinde ninamaanisha, Namna mnavyohusiana au
kujichanganya na kijana wa kiume, isichochee wala kuyaamsha
mapenzi. Unajua, moja ya sehemu nyeti (sensitive) sana katika

40
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

mahusiano kuliko maeneo yote katika jamii, kanisa n.k ni


mahusiano kati ya msichana na mvulana. Mahusiano haya kati ya
binti na kijana wa kiume, yanaumiza kichwa wazazi, kanisa, jamii
na hata taifa kwa sababu yasipochukuliwa kwa umakini yanaweza
kusababisha madhara makubwa sana, ikiwemo madhara ya
kisaikolojia, kiafya, kimahusiano, msongo wa mawazo na wakati
mwingine hata kusababisha kifo.

PY
Ndio maana Suleimani anasema katika kitabu cha Mithali 30:19
“Kuna mambo matatu yaliyo ya ajabu kwangu, Naam, kuna
manne nisiyoyafahamu. Mwendo wa tai katika hewa; Na
mwendo wa nyoka juu ya mwamba; Mwendo wa merikebu
katikati ya bahari; Na mwendo wa mtu [mvulana] pamoja na
CO
msichana.” Moja ya miendo asiyoielewa Suleimani ni mwendo wa
msichana na mvulana, kwa hiyo usishangae sana wazazi wako
wasipokuelewa; wanapotaka maelezo mengi wanapokuona
unahusiana na kijana wa kiume wewe binti. Ndio maana hata
wazazi hawaelewi mwendo wenu, ndio maana hata kanisa wakati
mwingine haliwaelewi miendo yenu.
Kama mwendo wa kijana pamoja na msichana haueleweki hata
EE

kwa wenye hekima, maana yake ni kwamba, kila binti anatakiwa


kuwa makini na mwendo huo, binti asipokuwa makini, mwendo huu
wa binti na kijana wa kiume, unaweza kuyaamsha mapenzi na
yatamletea shida. Wewe mtoto wa kike unataka nini kuwa karibu
sana mtoto wa kiume? Unatafuta nini kwa vijana wa kiume?
FR

Neno la Mungu limeweka misingi namna sahihi ya kuhusiana ili


mapenzi yasiamshwe kwa msichana.
1 Timotheo 5:2 “wanawake wazee kama mama; wanawake
vijana kama ndugu wa kike; katika usafi wote.”

41
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

Katika mstari huu, Paulo anamwambia Timotheo ambaye ni kijana


wa kiume, ya kwamba ahusiane na mabinti kama ndugu wa kike
katika usafi wote.
Waefeso. 5:3 “Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala
uchafu wo wote wa kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu;”
Msingi Wa Neno La Mungu Wa Uhusiano Kati Ya Kijana Wakiume

PY
Na Msichana Ni, Katika Usafi Wote (yaani usafi wa Mwili,
Mwenendo, Roho)
Mambo saba (7) muhimu ya kuzingatia kwa msichana
anapokuwa karibu na kijana wa kiume ili asiyaamshe mapenzi,
na iwe katika usafi wote:
CO
Sasa hii hailazimishi kijana wa kiume na binti kuwa karibu, lakini
ikitokea kumekua na ulazima wa kuwa karibu basi haya mambo
saba yazingatiwe ili ukaribu huo uwe katika usafi wote na
usioyaamsha mapenzi.
I) Kumcha Mungu ndio kuwe kinga kuu ya uhusiano wenu
EE

2 Wakorintho 7:1 “Basi, wapenzi wangu, kwa kuwa tuna ahadi


hizo, na tujitakase nafsi zetu na uchafu wote wa mwili na roho,
huku tukitimiza utakatifu katika kumcha Mungu.”
2 Wakorintho 4:1­2 “Kwa sababu hiyo, kwa kuwa tuna huduma
hii, kwa jinsi tulivyopata rehema, hatulegei; lakini tumekataa
FR

mambo ya aibu yaliyositirika, wala hatuenendi kwa hila, wala


kulichanganya neno la Mungu na uongo; bali kwa
kuidhihirisha iliyo kweli twajionyesha kuwa na haki, dhamiri za
watu zikitushuhudia mbele za Mungu.”

42
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

Kumcha Mungu ni nini linapokuja suala la mahusiano kati ya binti


na kijana wa kiume?;
(a)Ni kukataa mambo ya aibu yaliyositirika (ya siri).
Kumcha Mungu kwa binti kunapimwa kwa mambo yake ya
sirini. Tukitaka kujua unamcha Mungu wewe binti, tutaangalia
mambo yako ya siri. Maisha ya mwanadamu, ukiwemo na

PY
wewe binti unayesoma kitabu hiki, yako kwenye maeneo
matatu, moja maisha ya wazi (public life) ambayo mara nyingi
ni maishaambayo huonyesha kila mtu ni safi na hakuna
anayeonyesha uovu wake katika Maisha ya wazi; mbili ni
Maisha ya binafsi (private life), haya ni wakati watu huwa
wawili peke yao, mfano mzuri ni wanandoa, Maisha yao binafsi
CO
ni wakati wako wawili na sio wanapokuwa mbele za watu; tatu
ni Maisha ya sirini, Maisha haya ya sirini ni yale unajua wewe
na Mungu wako, hakuna mtu mwingine anajua. Mungu huwa
anaangalia Maisha ya sirini kuja Maisha ya wazi. Ucha Mungu
wa kweli huwa unaanzia kwenye Maisha ya mtu ya sirini. Je,
wewe binti unaishije Maisha ya sirini na huyo kijana wa kiume?
Mungu huwa anaangalia kwanza Maisha yenu ya sirini ndipo
EE

kisha Maisha ya nje.


(b) Ni kutoenenda kwa hila (tricky) ni kutoendana na hila
Kumcha Mungu ni kutoenenda kwa hila au ujanja ujanja. Kama
uhusiano wenu unamcha Mungu, huo uhusiano hautakuwa na
FR

mambo ya ujanja ujanja. Ukigundua huyo mkaka ana mitego


mitego fulani, maana yake ni kwamba huyo mtu hana ucha
Mungu ndani yake, jiepushe naye. Hila ni mtego, yaani
anasema jambo hili lakini nyuma yake anamaanisha jambo
lingine baya, anakufanyia jambo fulani kama zuri lakini lengo
lake ni kukupata na akufanyie kitu ambacho si kizuri. Mfano

43
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

mkaka anakupa zawadi nzuri lakini lengo lake ni kuuteka moyo


wako na hisia zako ili akupate kirahisi.
(c) Ni Kutolichanganya Neno la Mungu na uongo
Kumcha Mungu ni kutolichanganya Neno la Mungu. Kwa hiyo
ukigundua namna ambavyo mnahusiana inachanganya au
inalichanganya Neno, yaani ni kinyume na Neno; mnajiita

PY
mmeokoka lakini namna mnavyohusiana inachanganya maana
yake uhusiano wenu hauna ucha Mungu ndani.
Mnavyohusiana inaharibu ushuhuda wa Neno la Mungu.
(d) Ni dhamiri za watu kuwashuhudia usafi
CO
Ukiona dhamiri za watu zinapata shida na namna
mnavyohusiana, ujue huo uhusiano unavuka mpaka wa ucha
Mungu, hata kama hakuna kitu chochote kibaya kinaendelea
kati yenu.
(e) Maana nyingine ya kumcha Mungu
Lakini pia, jambo lingine, kumcha Mungu ni kutambua uwepo
EE

wa Mungu kwa kila mnalolifanya. Kila mnachofanya mnafanya


mkitambua uwepo wa Mungu, ninaposema kutambua uwepo
wa Mungu ninamaanisha, kumfanya Mungu na Neno lake
kuwa ndio kipimo cha kile mnachokifanya.
Mahusiano yakivuka kipimo cha ucha Mungu, kitakachofuata ni
FR

kuyaamsha mapenzi.
II) Mahusiano yenu lazima yawe na malengo, mahusiano
yasiyo na malengo ni rahisi sana kufanya kisichotakiwa.
Jambo la pili muhimu wewe binti unapohusiana na kijana wa kiume
(kama kweli ni lazima muhusiane au mjichanganye) ili msiyaamshe

44
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

mapenzi, mahusiano yenu lazima yawe na lengo au malengo.


Kama kukitokea ukaribu wowote kati yako wewe binti na kijana wa
kiume, basi huo ukaribu lazima uwe na lengo; na lengo likiisha,
hakuna haja ya ukaribu au uhusiano wa karibu kuendelea.
Mfano, wewe binti mmekutana na kijana kwa lengo la mazoezi
labda ya kwaya au kusifu na kuabudu; basi, msitoke nje ya lengo,
hayo mazoezi ya kwaya au kusifu na kuabudu yakiisha, msianze

PY
kubadili lengo, msiende nje ya lengo mtajikuta mmeenda mahali pa
kuyaamsha mapenzi kabla ya wakati wake; lengo lililowakutanisha
Ppamoja likiisha kila mmoja aende kwao.
Kuna mabinti walianza vizuri tu, wakakutana na vijana kwa lengo
zuri (labda la mazoezi ya kusifu na kuabudu; au kujifunza jambo
CO
fulani), lakini zoezi au funzo lilipoisha wakaanza kutoka kwenye
lengo, wakaanza kusindikizana, badae kuanza kuwasiliana usiku
sana na mwisho wakayaamsha mapenzi na kujikuta wamemkosea
Mungu; mwanzo lilikuwa lengo zuri la kumtukuza Mungu, lakini
hawakulizingatia na kutoka nje ta lengo. Binti yangu, kama hakuna
lengo, hakuna haja ya kuwa na ukaribu na kijana wa kiume, salamu
tu zinatosha. Sio sifa mzuri kwa binti kuwa na ukaribu na Watoto
EE

wa kiume, inakuchafua na wakati mwingine inakushusha binti


thamani yako mbele ya jamii.
Ndio maana Neno la Mungu linasema katika 2 Wakorintho 6:14
“Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo
sawasawa;” Kufungiwa nira kwa jinsi isivyo sawasawa ni
FR

kuhusiana nje ya lengo sahihi. Hata kwa vijana wa kiume, wewe


binti, usifungiwe nao nira (usihusiane nao) nje ya lengo sahihi.
Likiisha lengo la kuhusiana msiendelee kuhusiana.

45
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

III) Weka wazi mipaka ya mahusiano yenu.


Kama ni lazima wewe binti kuhusiana na kijana wa kiume, basi
hakikisha unakuwa na mipaka na unaweka mipaka hiyo wazi ya
hayo mahusiano yenu; hii itasaida sana msiamshe mapenzi katika
kuhusiana. Unajua, usalama wa nyumba au eneo umefungwa
kwenye mipaka ya hiyo nyumba au eneo. Ukiona mtu haeleweki
halafu anaingia kwenye mipaka yako maana yake usalama wako

PY
uko kwenye hatari. Jambo hili liko hivyo hata kwenye mahusiano;
msichana yeyote lazima awe na mipaka na aweke mipaka wazi ya
mahusiano yake. Mabinti wengi huwa wanaanguka katika dhambi
ya uzinzi bila wao kupanga ni kwa sababu ya kutokuwa waangalifu
na mipaka ya mahusiano yao.
CO
Unajua, hata kwenye nyumba, kuna wakati unaweza ukaibiwa kwa
sababu tu ya uzembe, labda umesahau kufunga geti na mwizi
anapita anaona geti liko wazi, huo ni uzembe wa kutotunza mipaka.
Wewe binti, lazima uweke mipaka vizuri katika mahusiano yako.
Weka mipaka mizuri ya mawasiliano ya simu na ujumbe (meseji).
Binti makini, hawezi kumruhusu kijana amtumie ujumbe ya aina
yeyote, yaani iwe ujumbe wa mapenzi, matusi na yeyote yeye
EE

anaikubali tu.
Binti makini, ataweka mipaka ya aina za meseji ambazo
anamruhusu kijana wa kiume amtumie; akiona ujumbe mbaya toka
kwa kijana wa kiume, haichekei bali anamuonya kwa ukali na
akiendelea kuvuka mpaka wa meseji basi anamfungia (block).
FR

Kuna vijana wa kiume, kwa lengo na kumjaribu binti kama kweli


ameweka mpaka wa mawasiliano, wanajifanya wamekosea na
kutuma ujumbe mbaya kwa binti. Ni vizuri wewe binti ufahamu, vitu
vingi ambavyo vijana wa kiume hufanya kwa wadada sio bahati
mbaya ni makusudi kabisa kwa lengo la kutaka kujua kama
umejiewekea mipaka na hiyo mipaka ni imara kwa kiwango gani.

46
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

Mfano, unaweza kukuta kijana wa kiume anamshika binti ziwa au


makalio halafu anajifanya kusema “samahani bahati mbaya”,
mara nyingi kama sio zote huyo kijana anakuwa amekusudia na sio
bahati mbaya; na wengi wakigundua hauna shida sana na mpaka
huo wa kushikwa, ataendelea kuuvuka mpaka na kujaribu mpaka
mwingine na mwisho kusababisha madhara. Au, kwa mfano,
unakuta kijana wa kiume anakutumia wewe binti picha chafu za

PY
uchi au za ngono halafu akituma tu anakutumia ujumbe kukuambia
“samahani nilikosea” na binti anaamini kwamba kweli alikosea.
Ikitokea amekutumia picha za aina hiyo usiwe mpole, mkaripie na
ikiwezekana mfungie (block) kabisa. Jiulize kwa nini hajakosea na
kumtumia mama yake mzazi picha ya aina hiyo na akutumie wewe
kama sio ukosefu wa nidhamu huo na kujaribu kuvuka mpaka
CO
wako? Au kwa nini asikosee na kutuma kwa mchungaji wake?
Mara nyingi kijana anachofanya huwa ni kuujaribu mpaka wako
kama kweli upo; akiona unacheka cheka na hauwi mkali kulinda
mpaka huo, atajua huo mpaka haupo, kesho yake au siku nyingine
hatakutumia picha ya utupu bali atakutumia video za ngono;
ukiendelea kutulia atagundua na huo mpaka pia ulishavunjika,
ataenda zaidi na Zaidi.
EE

Ni muhumu sana wewe binti kufahamu kwamba, vijana wa kiume ni


wajanja sana na wana mbinu nyingi na wana akili katika kumlaghai
binti sawa kabisa na mbinu za Chui katika kuwinda Paa na Ayala
kama tulivyojifunza. Neno la Mungu linatambua kwamba wanaume
wana akili ndio maana linasema katika 1 Petro 3:7 “Ninyi waume,
FR

kaeni na wake zenu kwa akili” na hakuna mahali linasema


ninawapa hiyo akili kwa sababu wanaume tayari wanayo hiyo akili
ya kuishi nao, na wengine huitumia vibaya.
Kwa hiyo, wewe binti, hakikisha unaweka mipaka wazi ya
mawasiliano na simu; ukitumiwa ujumbe mbovu usiichekee,

47
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

akirudia ujumbe mbaya ya pili mfungie (block), kwa sababu


anataka akuharibie Mmaisha yako. Ukweli ni kwamba, uovu na
anguko la binti huwa linaanzia mbali kabisa, huwa linaanza kwenye
mipaka midogo midogo kupuuzwa na kuvunjwa.
Hivi unajua, ukitaka kuvamia nyumba yenye uzio au ukuta na geti,
lazima utaanzia mpaka wa mbali ambao ni ukuta wenye geti,
ukivuka ukuta, labda utakutana na geti lingine labda la chuma,

PY
ukivuka utakutana na mlango wa sebuleni wa mbao, ukivuka
utakutana labda na mlango mwingine wa koridoni, ukivuka
utakutana na mlango mwingine wa chumbani. Huwa hawavamii
kuanzia mlango wa chumbani bali huazia kwenye mipaka ya mbali
kabisa ya nje ya geti au ukuta wa nje.
CO
Hata kijana kwa binti pia ni hivyo hivyo, huwa anaanzia mipaka ya
mbali kabisa, ya kujifanya amekosea ujumbe (meseji), mipaka ya
muda wa kuwasiliana.
Msichana yeyote makini lazima awe na mipaka ya muda wa
kuwasiliana; haijakaa sawa kabisa wewe binti unaruhusu muda
wowote kuongea na simu na vijana wa kiume, hata kama
EE

hamuongei jambo lolote baya lakini ni heshima kwa binti kuwa na


mipaka ya kuwasiliana na vijana wa kiume, na hiyo ndio sifa ya
msichana anayejitunza.
Sifa ya msichana ni “ugumu wa kuingilika”; hakuna mwanaume
anataka kuoa “pazia”; pazia maana yake kila mtu anaweza
FR

kumpata muda wowote anaotaka. Kila mwanaume anataka aoe


“milango migumu kama ya chuma”; yaani binti asiyeingilika kwa
urahisi. Japo kila mwanaume anapenda aoe binti mgumu kuingilika,
lakini wakati anamfukuzia binti, haonyeshi kama kweli ugumu wa
kuingilika ni sifa ambayo wanaume waoaji wanaihitaji. Mwanaume
akiwa anakutaka kimapenzi atataka uwe kama “pazia” lakini ikifika

48
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

saa ya kuoa hawezi kuchagua “pazia” kuoa bali atatafuta “mlango


mgumu”.
Sifa ya msichana ni ugumu wa kuingilika, na heshima ya msichana
iko hapo. Ni sawa kabisa na sifa ya ikulu. Kwa mfano, kila mtu
akitaka kwenda ikulu anaweza kwenda muda wowote anaotaka bila
kikwazo wala kizuizi chochote, hiyo haitakuwa ikulu tena bali
itakuwa ni sawa na choo. Sifa ya ikulu ni vikwazo vya kuingilika;

PY
Ugumu wa kuingilika na ndio thamani ya ikulu.
Narudia tena, sifa ya msichana ni ugumu wa kuingilika, ni ugumu
wa mipaka yake kuingilika, ni kukaza mipaka yake, yaani wewe
binti, unaukaza mpaka wako wa mawasiliano mpaka vijana wa
kiume wanasema “dah, huyu binti ndio binti sahihi wa kuoa
CO
ikifika wakati sahihi wa kuoa”; kwa sababu atagundua unaweza
kujitunza hata baada ya ndoa. Ukweli ni kwamba, hakuna
mwanaume anayependa ku­share mke, kwa hiyo ni imani ya kila
mwanaume kwamba, binti asiyeingilika kirahisi ndiye binti anayefaa
kwa ndoa wakati ukifika. Ugumu wa mipaka na wa kuingilika ndio
humuhakikishia mwanaume muoaji kwamba hatakuja ku­share na
wanaume mwingine pindi atakapomuoa huyo binti.
EE

Msichana yeyote anayejitambua, lazima awe na mipaka binafsi,


kwamba “jambo hili hapana, na sijiruhusu kufanya” nk.
Ninaposema mipaka siongelei dhambi tu, mipaka mingine ni
muhimu kwa binti hata kama sio dhambi. Kwa hiyo, hapa siongelei
dhambi tu bali ninaongelea mipaka ya mbali kabisa.
FR

Ikitokea wewe binti, mmeonana na kijana wa kiume, lazima kuwe


na mipaka ya maeneo ya kuonana ikiwa ni lazima kuonana (kama
hakuna ulazima, hamuhitaji hata kuonana wawili); sio wewe binti
unakubali kuonana na kijana wa kiume porini; unakubali kuwa na
appointment na kijana wa kiume “maporini usiku”; mwisho wa siku

49
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

utajikuta mmeyaamsha mapenzi. Nimesema “porini” nikimaanisha


mahali popote ambapo ni pa maficho na usiri (private places);
yaweza kuwa chumbani au mazingira ambayo yataficha chochote
mtakacho kifanya au kutaka kukifanya. Wewe binti, usikubali wala
usithubutu kumtembelea kijana wa kiume chumbani kwake hata
kama huyo kijana ameokoka au unamuamini kwa kiwango kikubwa
au hata kama anaumwa (wewe sio daktari wala mchungaji),

PY
kufanya hivyo ni kuvuka mipaka ambayo inaweza kukupelekea
kuamsha mapenzi na kupata madhara makubwa usiyoyatarajia.
Kosa kubwa alilofanya Tamari, ni kumtemebelea Amnoni chumbani
kwake kwa sababu Amnoni alikuwa mgojwa.
2 Samweli 13:10 – 11 “Amnoni akamwambia Tamari, kilete
CO
chakula chumbani, nipate kula mkononi mwako. Basi Tamari
akaitwaa mikate aliyoifanyiza, akamletea Amnoni nduguye mle
chumbani. Naye alipokwisha kuileta karibu naye, ili ale,
Amnoni akamkamata , akamwambia, njoo ulale nami, ndugu
yangu”
Binti, lazima uweke mipaka ya kueleweka kwa sababu, kama
nilivyosema, huwa hakuna mwizi anaingia chumbani bila kuingia au
EE

kupitia kwenye geti kubwa, ukiona mwizi yuko chumbani kwako bila
wewe kujua, kuna mawili, moja kuna milango ameshafungua
iliyomruhusu kuingia chumbani kwako, kama milango yote
imefungwa basi ujue huyo sio mwizi bali ni mchawi.
Hakuna binti anayeweza kuvuliwa nguo na kijana wa kiume kama
FR

huyo binti hakuruhusu mipaka ya mbali kwanza ivunjwe. Ukiona


kijana amemvua nguo binti, ujue kuna mipaka mingi ilivunjwa kabla
ya kuvuliwa nguo. Mpaka wa mwisho kabisa wa binti ni nguo zake,
na huu mpaka hauwezi kufikiwa kama mipaka mingine ya mbali
ilitunzwa vizuri. Hakuna binti mwenye ujasiri wa kuruhusu nguo
zake zivuliwe na kijana wa kiume kama hajamruhusu huyo kijana

50
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

kuvunja mipaka mingine ya mbali. Kimsingi, ukiona binti anavuliwa


nguo ujue moyo wa huyo binti ulishabaki wazi kwa huyo kijana siku
nyingi; au kwa lugha nyingine, huyo binti hakuulinda moyo wake na
akamruhusu kijana kuingia ndani ya moyo wake kiwango ambacho
akavuka mipaka yote mpaka akafikia mpaka wa mwisho ambao ni
nguo. Kijana yeyote wa kiume ambaye utampa nafasi kubwa
kwenye moyo, ni rahisi kukufanyia chochote kwenye mwili wako.

PY
Nitaeleza kwa undani kuhusu KULINDA MOYO badae kwenye
kitabu hiki.
Binti, linda mipaka ya namna mnavyoongea na kijana wa kiume,
linda mipaka ya kugusana; wewe binti usikubali kuguswa kila
mahali na kijana wa kiume. Kuna maeneo ambayo kijana wa kiume
CO
haruhusiwi kabisa kukugusa hata kama ameona kitu cha kukufuta
au kukusaidia. Sio wewe binti, kijana anakuambia nimeona uchafu
kwenye ziwa lako au makalio na wewe unakubali tu akufute uchafu
hapo tena unasema akufute vizuri. Usikubali mvulana akuguse
eneo lolote ambalo ni eneo lako binafsi, wazungu wanaita “private
parts”. Haya maeneo yanaitwa “private” kwa sababu wewe pekee
ndio unaruhusiwa kujigusa na sio mtu mwingine hata kama anataka
ashike kwa jina la unabii au kukuombea. Haruhusiwi mtu kukushika
EE

private parts hata kama anasema anataka kukuwekea mikono ili


kukuombea.
Wewe binti, unapaswa kuainisha au kuzitambua sehemu zako za
ndani (define your private parts) ambazo hautamruhusu mtu yeyote
FR

kuzigusa. Ziko sehemu za binafsi au za ndani (sehemu nyeti) za


binti (private parts) zinajulikana wazi kama vile maziwa, makalio,
sehemu za siri, mapaja, kiuno nk, lakini wewe binti unaweza
ukaongezea zingine ambazo na ukaamua kwa gharama yeyote
haruhusiwi mtu kuzigusa. Hata kama sio sehemu nyeti au za siri
kama nilivyoonesha hapo, lakini haifai kuguswa tu hata mikono au

51
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

mabega na kijana wa kiume bila sababu za msingi. Lakini pia,


kwenye eneo hili kuna mtego ninatakiwa kuutegua; binti makini
hataishia kwenye hizo sehemu za ndani/binafsi (private parts)
nilizotaja pekee, binti makini ataenda zaidi na kuziainisha sehemu
ambazo haruhusu mtu wa jinsia tofauti kumgusa. Lakini, sio tu
kuainisha sehemu za mwili wake, bali atakuwa makini aina ya
mguso wowote ambao atagundua una hila ndani yake.

PY
Binti unayesoma kitabu hiki, usikubali mguso wowote wa hila toka
kwa kijana wa kiume hata kama ni wa kukushika tu mkono; nasema
hivi kwa sababu, kuna vijana wa kiume atakushika mkono tu na
hajagusa pengine lakini ushikaji wake mkono una hila ndani yake;
kuna vijana wengine hata hakushiki popote lakini unagundua
CO
namna anavyokuangalia tu kuna hila ndani yake; yaani namna
anavyokuangalia na kufanya ishara fulani analeta ujumbe fulani wa
uzinzi na uovu; maana yake ni kwamba binti usikubali hata hizo
ishara na miguso ya aina hiyo.
Bibila inasema yapo macho yajaayo uzinzi ­ 2 Petro 2:14 “wenye
macho yajaayo uzinzi…”
EE

Siku zote usisahau kwamba, kwa kadiri mipaka uliyojiwekea


inavyovunjika ndio kwa kadiri hiyo hiyo hatari ya kuyaamsha
mapenzi inasogea. Msichana makini lazima awe na vitu ambavyo
anajizuia kufanya na vitu ambavyo anajiruhusu kufanya; wazungu
wanasema “to do and not to do list”.
FR

Kama wewe binti unayesoma kitabu hiki hukuwa na vitu


unavyojizuia kufanya yaani “not to do list”; ninakushauri uandae
orodha ya vitu hivyo sasa. Orodha hii inaenda ndani zaidi ya
dhambi na vitu ambavyo unazuiliwa na mchungaji wako au
kanisani. Orodha hii inakuwekea mipaka mingi zaidi ya dhambi ili
kukulinda usiyaamshe mapenzi na kuanguka.

52
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

Kama umenielewa vizuri katika point hii, ninatarajia wewe binti


unayesoma kitabu hiki, utaandaa orodha hiyo na kuanza kuiishi.
Unaweza ukaamua kumshirikisha mama yako au mlezi wako au
mama mtu mzima akusaidie kuandika orodha hiyo ya vitu
usivyojiruhusu kufanya; wamama mara nyingi huona mbali zaidi
kwa hiyo ukimshirikisha kuandaa orodha hii atakusaidia wakati
mwingine kuona vitu ambavyo wewe sio rahisi uvione, kwa sababu

PY
mama huyo pia aliwahi kuwa msichana na amekutana na
changamoto za usichana wakati mwingine kubwa kuliko hata wewe
na akazivuka; kuna akili ambayo binti anaweza kuipata kwa
mwanamke mtu mzima, mama mtu mzima ana jicho la pili, ni rahisi
kuiona hatari ambayo binti haioni; lakini, sio tu mama, unaweza
ukamshirikisha na baba yako pia kama mna mahusiano mazuri au
CO
hata mchungaji wako pia.
Ongea nao wakushauri ni vitu gani ambavyo ni hatari kwako
vinavyoweza kuhatarisha ubinti wako, na wakikushauri, viweke
kwenye orodha yako binafsi ya vitu ambavyo unajizuia kufanya. Na
uwe mwaminifu kuifuata orodha hiyo bila hata kufuatiliwa na mtu,
wewe tayari ni binti mkubwa, jifunze kufanya mambo bila
kulazimishwa na kufuatiliwa, Watoto ndio wanahitaji kufuatiliwa;
EE

uwe mwaminifu kuilinda orodha yako bila kulazimishwa wala


kufuatiliwa. Ukiandaa hiyo orodha, iweke mahali ambapo utakuwa
unaiona mara kwa mara, iombee hiyo orodha yako na umuombe
Mungu akusaidie.
FR

Orodha hiyo itakusaidia sana, siku ukitaka kuivunja, dhamiri yako


ya ndani itakukumbusha na kupiga kelele na kukulinda; moja ya
kitu orodha hii itafanya ni kuifanya dhamiri yako kuwa makini
(active) sana kwenye orodha hiyo ikitokea unavuka mpaka.
Ikitokea umevunja moja ya kitu katika orodha yako, usikifute hicho
kitu kwenye orodha bali nenda mbele za Mungu mwambie

53
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

nimekosea naomba unisamehe na amua tena kuendelea kuilinda


orodha yako, lakini pia unaweza ukamshirikisha
mama/baba/mchungaji (kutokana na ukaribu mlio nayo na wepesi
wa moyo wako) kile umevunja kwenye orodha na mkapatana tena
kwamba hutaivunja.
Mfano Wa Orodha ya mambo ambayo binti anapaswa kujizuia
kufanya (Not To Do List):­

PY
• Sitafanya mapenzi na mwanaume yeyote kabla ya ndoa (I
will not have sex with any man before marriage)
• Sitafanya busuna mwanaume kabla ya ndoa (I will not kiss
or deep­kiss with any man before marriage)
CO
• Sitamtembelea kijana wa kiume chumbani kwake peke
yangu wala sitamruhusu kijana wa kiume kunitembelea
chumbani kwangu (I will not go to any man's house/room nor
will I allow him come to mine)
• Sitaenda sehemu yeyote ambayo si rafiki kwangu (sehemu
hatarishi) na kijana wa kiume au mwanaume mchana wala
EE

usiku (I will not go anyplace not friendly to me with no man


during the day nor at night)
— Ikitokea ni lazima nitoke na kijana wa kiume, haitakuwa
usiku na itakuwa ni sehemu ya wazi na salama (If I have to go
out with a man, it shouldn't be at night and should be
FR

open/safe place)
• Sitaangalia picha, video na tamthilia za ngono wala
sitamruhusu mtu yeyote kunitumia picha za aina hiyo (I will not
watch ponography or movies of such nature)

54
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

• Sitajiridhisha kwa kujichua (I will not do masturbation)


• Sitatumia kilevi cha aina yeyote wala sitavuta sigara/bangi
maisha yangu yote (I will not drink nor smoke)
• Sitamfungulia moyo wangu kijana au mwanaume yeyote
kabla ya wakati wangu wa kuolewa kufika (I will not open my
heart before time to any man, when time comes I will open to

PY
only seriously committed one for marriage and the one am
ready to commit myself for marriage)
— The commitment should be formal not verbal only.
• Sitamruhusu kijana au mwanaume yeyote kuwa na
CO
mazungumzo machafu naye (I will not entertain any man or
having nasty talks with them)
• Sitamruhusu kijana au mwanaume yeyote kugusa sehemu
zangu za siri (I will not allow any man to touch my private parts
nor will I touch any man's private parts)
— Mguso (kumbatio – hugs, kushika mikono – holding hands
EE

etc) wowote na kijana wa kiume wenye hila ndani yake


sitauruhusu (Only safe hugs or holding hands is allowed)
• Sitamtumia ujumbe wala kuongea na kijana wa kiume
baada ya saa 2 usiku labda kama ni muhimu sana na lazima (I
will not talk or text any man from 08 PM at night, unless it is
FR

very urgent and necessary)


• Sitaruhusu kuzungukwa au kuwa na marafiki waovu (I will
not surround myself with bad company/ friends)

55
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

— Hii inahusisha kujiondoa au kutojiunga kwenye makundi ya


WhatsApp na mitandao ya kijamii pia (This inclues bad
WhatsApp (Social media) Groups)
• Sitatembelea, kama si lazima, mahali popote ambapo si
pazuri kiroho kama, mfano Bar, club nk (I will not,
unnecessarily, visit places that are not spiritual friendly)

PY
• Sitaongea lugha chafu au mazungumzo mabaya ambayo
yanaweza kuniamsha hisia zangu (I will not allow myself to use
bad languages; I am committed to change the way I speak)
• Mimi sio msichana rahisi rahisi na sitajirahisi kwa kijana
yeyote wa kiume wala mwanaume yeyote (I will not see myself
CO
cheap nor acting as one)
• Sitavaa kwa namna ambayo inaonyesha maungo yangu na
kujiaibisha – nitavaa kwa heshima (I will not wear clothes that
show parts of my body ­ I shall dress responsibly)
• Sitamtumia ujumbe au kumpigia simu kijana yeyote wa
kiume bila sababu hata kama tunafahamiana kanisani, shuleni
EE

au chuoni.
• Nitajiepusha na mizaha na kutaniana kuliko pitiliza na vijana
wa kiume
• Nitaridhika na hali ya maisha niliyonayo na sitakuwa na
FR

tamaa na vitu nisivyokuwa na uwezo navyo.


Mimi ni binti wa thamani wa Mungu mkuu sana, kwa hiyo nitaishi
Maisha ambayo yanaionyesha thamani yangu ya kiroho (I am a
precious prophetess of the most­high God, so I will live to portray
my inward/spiritual Identity)

56
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

Mwili wangu ni Hekalu takatifu la Roho Mtakatifu, na nimedhamiria


kuutoa mwili wangu kwa Mungu na kwa ajili ya Mungu pekee (My
body is the holy temple of the Holy Spirit and I have dedicated it
(my body) to Him and only Him).
Mungu nisaide.
IV) Usianzishe mahusiano yeyote kama hauna uhakika

PY
yatakuwa katika usafi wote na utakatifu.
Unapoanzisha mahusiano yasiyo na usafi utajikuta unatengeneza
mazingira ya kuyaamsha mapenzi. Hakikisha unalinda usafi na
utakatifu wako kwa gharama yeyote; lakini pia hakikisha haujengi
ukaribu na watu wasio safi. Ukigundua kijana yeyote (na hata binti
CO
mwenzio) hana usafi (kwa maana ya usafi wa kiroho na kitabia) au
Ukigundua mtu yeyote ambaye una ukaribu naye kwamba sio mtu
safi, achana naye mara moja wala usijaribu kumbadilisha.
Hakikisha mtu ambaye unahusiana naye ni mtu safi kwa maeneo
yote, ni msafi katika lugha (maongezi) yake, ni msafi katika meseji
zake anazokutumia, ushuhuda wake kwa ujumla ni safi. Ukigundua
kijana ana maongezi mabaya, achana naye, usiendelee kusikiliza
EE

maneno yake kwa sababu maneno ni roho na yanaweza kabisa


kukuathiri ukiendelea kuyasikiliza; kimsingi unapoendelea
kumsikiliza mtu unapokea roho yake au kwa lugha nyingine
atakuvuvia kile alicho nacho; kama kijana ni mchafu kitabia, hata
kama akikuambia maneno mazuri achana naye usimsikilize, kwa
FR

sababu kilicho nyuma ya maneno yake ni maisha yake machafu na


yanaweza kukuchafua na wewe pia. Roho ya Samsoni
ilidhoofishwa na maneno ya Delila mpaka akajikuta amkosea
Mungu.

57
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

Hata kama kijana ana vipawa (kuimba, kucheza, kupiga mziki,


kuhubiri, kuchekesha nk), ukimgundia sio msafi wa kitabia na
kiroho, achana naye, usiweke ukaribu naye kabisa; mwache aende
na vipawa vyake.
1 Tim 5:2 “wanawake wazee kama mama; wanawake vijana
kama ndugu wa kike; katika usafi wote.”

PY
Waefeso 5:3 “Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala
uchafu wo wote wa kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu;”
V) Usijiamini kupita kiasi, usimuamini kijana wa kiume.
Jambo jingine la kuzingatia ili binti usiyaamshe mapenzi ni
CO
usijiamini kupita kiasi, lakini pia kwa upande wa pili usimuamini
kijana wa kiume.
Wale Wanyama ambao tumesoma habari zao, yaani Paa na Ayala,
moja ya sifa zao ni kwamba, akiwa pamoja na wanyama wengine
muda wote yuko makini kuangalia nini kitamtokea ili ajilinde. Na hivi
ndivyo binti makini anatakiwa kuwa. Wewe binti, hutakiwi
kumuamini kijana wa kiume, ni lazima uwe makini unapoishi naye
EE

au anapojaribu kuwa karibu na wewe; lakini pia usijiamini kupita


kiasi.
Neno la Mungu linasema, “msiyaamshe mapenzi” ni kwa sababu
yamelala hayajafa, kwa hiyo ukijiamini kupita kiasi unaweza
ukajikuta umefanya vitu ambavyo vinayaamsha mapenzi na
FR

kujisababishia madhara. Kwa hiyo, usijiamini kupita kiasi lakini pia


usimuamini kijana wa kiume, maadamu si kaka yako wa damu hata
kama mnaitana kaka na dada.

58
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

VI) Mahusiano yenu yasiwe ya siri ­ Msiwe na vitu mnafanya


kwa siri, hata kama vitu hivyo sio vibaya.
Wewe binti, epuka mahusiano ya siri na kijana/vijana wa kiume.
Usiwe na vitu vya siri kati yako wewe binti na kijana wa kiume; hii ni
ikiwa ni lazima kuwa na ukaribu (uhusiano) na kijana wa kiume,
lakini kama si lazima ni vizuri zaidi kutokuwa na ukaribu kabisa na
kijana wa kiume (salamu tu inatosha); lakini ikiwa ni lazima basi

PY
hakikisha huo uhusiano au ukaribu usiwe wa siri. Mnapokuwa na
vitu vya siri ndipo unakuta vinaanza kupenya vitu viovu kati yenu
ambavyo vitayaamsha mapenzi.
VII) Kiwango sahihi cha mahusiano kati yako wewe binti na
kijana au vijana wa kiume kiwe ni cha kaka na dada tu.
CO
Ninachomaanisha ni kwamba, ikiwa ni lazima kuhusiana, basi
hakikisha kwamba mnahusiana kwa kiwango cha kaka na dada na
si vinginevyo. nasisitiza, husianeni kwa kiwango cha kaka na dada.
Ninaposema kiwango cha kaka na dada ninamaanisha kuwa,
muheshimiane kana kwamba mmezaliwa tumbo moja, yaani
unapokutana na kijana wa kiume kwa maongezi au mambo
EE

mengine, hebu weka picha ya kaka yako; fikiri vile


unavyomheshimu na ambavyo kamwe hapawezi kuwa na hisia
zozote za mapenzi.
1 Timotheo 5:2 “wanawake wazee kama mama; wanawake
vijana kama ndugu wa kike; katika usafi wote.”
FR

Paulo anamwambia kijana Timotheo, kwamba unapohusiana na


mabinti, muhusiane kama ndugu wa kike au dada. Vivyo hivyo
wewe binti unayesoma kitabu hiki, unapohusiana na kijana wa
kiume, uhusiane naye kama ndugu wa kiume, yaani kaka.

59
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

Ninaposema kiwango cha mahusiano cha kaka na dada simaanishi


tu zile kaka na dada za kuitana lakini mnayofanya yanakinzana na
mnavyoitana. Kwa sababu kuna watu wanaitana kaka na dada,
lakini namna wanavyohusiana sio kama kaka na dada.
Ninamaanisha kwamba, zaidi ya kuitana kaka na dada, lakini pia
kila mnachokifanya kiwe kwenye kiwango cha (standard ya) kaka
na dada. Ili unielewe vizuri ngoja niseme kwa mifano; kwa mfano,

PY
binti unamuandikia ujumbe huyo kijana unamuita kaka, na ikatokea
huo ujumbe umekosea umeenda kwa kaka yako wa tumbo moja,
basi huo ujumbe usiwe na ukakasi wowote kwa kaka yako.
Binti Jiulize: "Kama unamuandikia huyo kijana unayemuita kaka
ujumbe, na ukakosea ukaenda kwa kaka yako wa damu, je
CO
utakuwa na amani? au Je hiyo meseji unayomuandikia huyo kijana
unaweza ukaituma kwa kaka yako wa damu na kaka yako asikuone
una matatizo yeyote? Kama huwezi basi ujue hiyo meseji imevuka
mpaka wa kaka na dada tunaouongelea".
Wewe binti uliyeshika kitabu hiki, je hayo maongezi unayoongea na
huyo kijana unayemuita kaka, unaweza ukaongea maongezi hayo
na kaka yako wa damu na kaka yako asikuone kwamba una
EE

matatizo? Kama huwezi basi hayo maongezi yamevuka mpaka au


kiwango cha (standard ya) kaka na dada. Je hiyo sauti
unayomuongelesha huyo kijana unayemuita kaka, unaweza
ukamuongelesha kaka yako wa damu kwa sauti hiyo? Je hiyo
mikao unayomkalia kijana wa kiume je unaweza kumkalia hivyo
FR

kaka yako wa damu? Je hayo mnayofanya na huyo kijana wa


kiume mkiwa wawili unaweza kufanya na kaka yako wa damu? Je
story mnazopiga na huyo kijana mnaweza kupiga na kaka yako wa
damu? Hizo picha unazomtumia huyo kijana au mnazotumiana,
unaweza kuzituma kwa kaka yako wa damu? Haya ni maswali
muhimu sana ya kujiuliza ili kuhakikisha unahusiana kwa kiwango

60
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

cha kaka na dada sawa sawa na maandiko yanavyokutaka na sio


vinginevyo. Kama mahusiano ya binti na kijana yakivuka mpaka
huu, ni rahisi sana mahusiano hayo kuyaamsha mapenzi na
wakajikuta wameanguka katika dhambi ya uasherati na hata kupata
madhara makubwa kama ujauzito, magonjwa ya zinaa n.k. Kwa
hiyo, kama ni lazima kuhusiana, basi isizidi kwenye mpaka huu wa
kaka na dada.

PY
3) Linda moyo wako usinaswe (linda hisia zako za mapenzi)
Close your heart to all men except your daddy and blood brothers.
Eneo la tatu la muhimu sana kwa binti kujilinda na kujitunza ili
usiyachochee wala kuyaamsha mapenzi kabla ya wakati wake ni
eneo la moyo wako.
CO
Namna mojawapo ya kujilinda usiyaamshe mapenzi wewe binti, ni
kuulinda moyo wako usinaswe na hisia za mapenzi. Mabinti wengi
wanajikuta wameingia kwenye maswala ya mapenzi sio kwamba
mwanzo walitaka, lakini kuna vitu ambavyo waliviruhusu wakajikuta
moyo umenaswa.
EE

JILINDE ZAIDI MOYO WAKO NA KIJANA WA AINA HII


Kuna namna ambapo inaweza kutokea, na ni kawaida, kwa
msichana au mtoto wa kiume kujikuta amevutiwa na mtu wa jinsia
tofauti. Yaani binti, bila kupenda wala kupanga anajikuta anavutiwa
na kijana wa kiume, yaani ndani yako binti unajikuta umemkubali
FR

kuliko wengine, ukimuona kati ya wengi unamuona kama wa tofauti


na wengine (“crush”), kuna namna ni kama moyo wako
umegongana naye, ni kama unaona ana tofauti na wengine,
unamuona spesho. Sasa kama kuna eneo la kuulinda zaidi moyo
wako wewe binti ni kwa kijana wa aina hiyo, pamoja na kwamba
unapaswa kuulinda moyo wako kwa vijana wa kiume wote, lakini

61
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

kwa kijana ambaye moyo wako unamuona wa tofauti huyo ni wa


kujilinda naye zaidi.
Na wakati mwingine Shetani ni mjanja sana, anasababisha kijana
wa aina hiyo, ndio anaanza kusogea karibu na wewe utadhani
amejua nini kinaendelea moyoni mwako; wakati mwingine wewe
binti usipokuwa makini, huyo mkaka anaweza akagundua kwamba
moyo wako ume “crush” naye kwa sababu inawezekana mkiwa

PY
naye karibu na moyo wako umevutwa naye, binti unaweza kujikuta
unamuangalia au kuzungumza naye tofauti na wengine kiasi
akagundua kwamba kuna kitu.
Kwa nini nasema unapaswa kujilinda sana moyo wako, kwa
sababu tamaa ya msichana iko ndani yake na haiko kwenye macho
CO
tu kama mwanaume, shida kubwa ya msichana sio kumuona
mwanaume bila nguo, shida kubwa ya binti ni pale kijana
akishaingia ndani ya moyo wake. Na unajua binti, kijana wa kiume
akishaingia sana ndani ya moyo, haitakuwa ngumu kukuvua nguo
zako. Ukishamfungulia kijana wa kiume moyo wako kama
nilivyosema kabla, akaingia ndani yako mzima mzima,
umejitengenezea tatizo kubwa ambalo linaweza kukutesa.
EE

Binti, unajuaje umemfungulia kijana wa kiume moyo na ameanza


kuingia au ameshaingia ndani ya moyo wako?
Wakati hayupo unamuwaza yeye tena wakati mwingine
unashindwa kabisa kujizuia kumuwaza. Uko chumbani au ndani
FR

peke yako, lakini masaa yote usiku unamuwaza mkaka fulani ndani
yako, ukisikia simu inaita au meseji unawaza labda atakuwa yeye
anapiga au unatamani angekuwa ni yeye anapiga, ujue kuna
namna umeruhusu moyo wako kuingiliwa.

62
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

Lakini pia akisogea karibu unasikia furaha, na unatamani awe


karibu muda wote, akienda mbali unapata shida na kummiss sana,
ukiona haya uwe mwangalifu kwa sababu anaweza akawa
ameshaingia au ameanza kuingia kwenye hisia za mapenzi.
Binti yangu, jilinde moyo wako usije kuruhusu vitu ambavyo
vinamfungulia kijana wa kiume moyo.

PY
Unamfunguliaje kijana wa kiume moyo wako?
Neno la Mungu linasema katika Mithali 18:16 “Zawadi ya mtu
humpatia nafasi;”
Unajua, kuna mabinti wamewafungulia mioyo vijana wa kiume bila
CO
wao (mabinti) kupenda au bila hata kujua kama wanafungua mioyo
yao; kwa kuwaruhusu wakaka kuwapa vitu na wakavikubali na
kuvipokea. Hivi wewe binti unajua, ukipokea kitu changu kwa
shukrani ya kweli toka ndani ya moyo wako; maana yake ni
kwamba umeufungua moyo wako kwangu? Ninachomaanisha ni
kwamba, ili shukrani ya kweli itoke kwenye moyo wa mtu ni lazima
kiwepo kitu ambacho yule mtu atakipokea kwenye moyo wake
ndipo moyo ufunguke kutoa shukrani za kweli.
EE

Kwa hiyo, binti, kama unapokea vitu kutoka kwa kijana wa kiume,
vile vitu vitaufanya moyo wake ufunguke kwake katika kupokea na
kumshukuru na kwa namna hiyo bila wewe kujua unajikuta
unaanza kumfungulia moyo. Kwa hiyo, jilinde sana na vitu
FR

anavyokupa kijana wakiume, lakini pia jilinde na maneno matamu


matamu anayokuambia.
Ninaposema jilinde ninamaanisha, usiendelee kupokea zawadi
zake wala usiendelee kuyaendekeza maneno yake ‘matamu
matamu’ kukuelekea wewe. Maneno yote matamu
anayokuongelesha, usiyachukue na kuyaweka ndani ya moyo

63
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

wako. Kijana wa kiume akikuambia wewe ni mzuri, usilichukulie


kwa uzito, usilichukue hilo neno na kuanza kulitafakari.
Ni kweli kuambiwa mzuri, hasa kutoka kwenye jinsia tofauti, ni
jambo ambalo mtu yeyote hulifurahia. Kiasili, kuna tofauti, wewe
binti kuambiwa mzuri na mabinti wenzio na kuambiwa mzuri na
kijana wa kiume, kwa asili moyo wako utafurahia zaidi kuambiwa
mzuri na kijana wa kiume, lakini ninakushauri na kukuonya binti

PY
yangu, usilichukue neno hilo na kuliingiza ndani ya moyo wako;
lichukue kama neno la kawaida tu. Lakini pia kijana wa kiume,
akikuambia ninakupenda, kuna tofauti kubwa sana na mdada
mwenzio akikuambia ninakupenda au akikuita majina mengine
mazuri mazuri kama baby, sweetie, honey, mpenzi nk; haya yote
CO
yakitoka kwa kijana wa kiume kukuelekea, usipokuwa makini
yanaweza kabisa kuufungua moyo wako kwa kijana huyo wa
kiume.
Binti yangu, tangu sasa, usiruhusu hayo kutoka kwa kijana wa
kiume kukuelekea, na kama ikitokea amekuambia, basi tangu sasa
anza kuchukulia kiwepesi wepesi kila kitu kizuri anachokuambia
kijana wa kiume, na usikiendekeze au ‘kukishikilia’moyoni mwako.
EE

Binti, ninakushauri kwa usalama wako, acha kabisa kupokea


zawadi za vijana wa kiume acha kuendelea kuyachukulia kwa uzito
maneno wanayokuambia. Lakini pia, uwe makini na muda
unaopokea simu kutoka kwa kijana wa kiume. Unajua kuna mida ya
hatari, kuna namna ambavyo kuna utofauti wa wewe binti kuongea
FR

na simu na kijana wa kiume saa saba mchana na kuongea naye


saa nane usiku.
Ukweli ni kwamba, uongeaji wa saa nane usiku lazima utakuwa
tofauti sana na uongeaji wa saa saba mchana hasa ikiwa vijana wa
jinsia tofauti wanaongea. Wewe binti ni shahidi, kijana akikupigia

64
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

simu mchana, kuna sauti (tone) unajikuta umeiweka, lakini akipiga


saa nane usiku, utajikuta kuna sauti tofauti inajiweka yenyewe.
Hata kama amepiga anataka maombi, usimuendekeze, sababu
wewe sio mchungaji. Kuna vijana wengine wana mbinu nyingi,
baada ya kugundua kuwa wewe ni mpenda maombi na unampenda
Mungu, anakuja na mbinu ya kutaka maombi. Anakupigia saa tisa
usiku na kujifanya anaumwa sana na anataka maombi, na wewe

PY
bila kujua mtego wake, na sauti (tone) yako ya usingizi unaanza
kumuonea huruma za kisichana na kumuombea na baada ya hapo
mnalala. Siku ya pili, anakupigia tena saa tisa usiku, kwa gia ya
kukupa ushuhuda wa maombi yako ya jana usiku, anakuambia
yaani ulivyoomba jana umekata tu simu nikapona kabisa. Siku ya
CO
tatu anapiga tena saa nane usiku, mara hii anakuambia
nimekukumbuka na nimekumbuka ile sauti ya maombi,
anakuambia, “unajua Mungu alijibu yale maombi sio tu kwa sababu
ya Imani bali na ile sauti pia yaani, unaombaje kwa sauti tamu
hivyo halafu maombi yasijibiwe”, unafurahi siku inapita. Siku
inayofuata anaacha, hakupigii kwa sababu anajua tayari
ameshapanda kitu ndani ya moyo wako, na moyo wako ni kama
umezoea kuyapokea maneno yake; unajikuta wewe mwenyewe
EE

unamtafuta usiku kumjulia hali na kwa namna hiyo tayari umempa


nafasi ameingia kwenye moyo wako.
Mfano huu nimeutoa, sio lazima uwe umemtokea binti, lakini
ninataka nikufungue namna unavyofikiria kuhusiana na mahusiano
FR

na wasiliano na kijana wa kiume, na hii ikusaidie kuwa mwangalifu


na kuulinda moyo wako usije ukanaswa. Mwanaume pekee salama
ambaye anaruhusiwa kuingia kwenye moyo wako ni baba yako na
kaka yako wa damu, na baada ya hapo ni mume wako akishakuoa;
wengine wote kama ulikuwa umewafungulia moyo wako, anza
kuwatimua moyoni mwako kwa sababu watakuletea shida.

65
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

4) Jilinde na marafiki (hata wa kike) unaojihusisha nao


Jambo jingine muhimu ambalo litakusaidia wewe binti usiyaamshe
mapenzi kabla ya wakati wake ni kujilinda na marafiki. Hapa
kwenye marafiki, naongelea marafiki wote wa kike na wa kiume.
Binti unaweza ukawa uko vizuri na unajiheshimu, lakini kama una
marafiki ambao sio wazuri, hao marafiki wanaweza kabisa
kukusababisha ukayaamsha mapenzi kabla ya wakati wake.

PY
Usijiambatanishe na rafiki yeyote asiye mcha Mungu, hata kama ni
wa kike. Ukijiunganisha na watu wasio wazuri, wenye tabia mbaya,
utajikuta na wewe tabia yako njema inaharibiwa. 1 Wakorintho
15:33 “Mazungumzo mabaya huaribu tabia njema”
5) Linda vitu unavyojilisha (kusikiliza, kutazama, kuongea nk)
CO
Kama binti unataka usiyaamshe mapenzi, linda sana vitu
unavyosikiliza, kutazama na kuongea. Kumbuka kwamba, kila
unaposikiliza unakula, unapotazama unakula, na mnachoongea
mnajilisha; na ukila tutaona matokeo. Hata kama hujui chakula
kinafanyaje kazi, ukila vizuri ni lazima tunaona matokeo. Kwa
mfano tukichukua mtu ambaye ni mwembaba kabisa, na tukaanza
EE

kumlisha vizuri alfajiri uji wa maziwa, saa nne asubui chai ya


maziwa, mkate wa siagi, na mayai ya kukaanga na saugage, halafu
saa saba mchana chipsi mayai na kuku wa kukaanga, saa kumi
jioni uji wa ulezi wenye maziwa, saa mbili usiku wali nyama na
mharage halafu saa nne usiku kipande cha keki na juice;
tukaendelea na ratiba hii ya chakula kwa muda wa miezi mitatu,
FR

baada ya miezi mitatu lazima atanenepa hata kama hana elimu


yeyote ya ufanyaji kazi wa vyakula; ni lazima tutaona matokeo ya
kile chakula tulichomlisha.
Ndivyo ilivyo hata kwako binti, kila unachosikiliza unailisha nafsi
yako, na ulichokula kinajua kazi yake hata kama wewe hujui

66
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

kinafanyaje kazi katika nafsi yako. Kila unachosikiliza,


unachotazama, unachosoma, mnachozungumza, kinajua kazi yake
ndani ya nafsi yako, huhitaji kujua kinaenda kufanya nini, wewe
subiri baada ya muda utashangaa unaanza kuona matokeo kwenye
tabia zako na maisha yako kwa ujumla. Tabia zako nyingi kama si
zote na hisia zako za sasa ni matokeo ya vitu ambavyo umekuwa
unajilisha kwa njia ya kutazama, kusikiliza na kuzungumza.

PY
Umewahi kujiuliza kwa nini sasa hivi duniani watu wengi, hasa
vijana wanaitikia sana hisia za mapenzi? Sababu kubwa ni kwamba
wanajilisha zaidi maswala ya mapenzi. Ukifuatilia utagundua,
asilimia 90 au zaidi ya miziki ya dunia inazungumzia mapenzi, lakini
pia tamthilia na filamu karibu zote huzungumzia mapenzi. Shetani
ameshajua namna ya kukamata watu kwa njia hii ya ‘kuwalisha’
CO
aina fulani ya ‘chakula’.
Ni vizuri wewe binti ukafahamu kwamba, hisia na utashi (maamuzi)
yako huitikia kile ambacho unalisha fikra au nia yako ya ndani; nia
au fikra zako zikijaa mapenzi, hisia zako zitakuwa zinaitikia zaidi
maswala ya mapenzi kuliko kitu kingine na utajikuta maamuzi yako
kwenye hisia na masuala ya mapenzi yanaathirika sana.
EE

Kwa sababu vijana wengi wamejaza maswala ya mapenzi kwenye


nafsi zao kupitia vitu wanavyosikiliza na kutazama ndio maana
vijana wengi huitikia sana masuala ya mapenzi, inafika mahali binti
akimuona kijana wa kiume anawaza mapenzi tu, au pia kijana wa
kiume akimuona binti anawaza mapenzi tu, kwa sababu ndani yao
FR

wamejaza zaidi fikra na hisia za mapenzi. Kwa hiyo ni muhimu


sana kwako wewe binti ambaye kitabu hiki kiko mikononi mwako,
ujilinde na vitu unavyojilisha (kusikiliza, kutazama, kusoma,
kuongea nk) nafsi yako ili usiyaamshe mapenzi kabla ya wakati
wake sawa sawa na andiko letu la msingi la Wimbo ulio bora 2:7

67
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

PY
CO
EE
FR

68
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

SALA YA WOKOVU

K ama wewe binti umesoma na kuelewa yote niliyoandika katika

PY
kitabu hiki; na unaona kabisa haujaenenda sawasawa katika
njia ya wokovu kwa habari ya kujitunza, basi ninakusihi ukiri sala hii
kwa imani na Yesu atakusaidia kuanza upya na kuenenda katika
njia inayokupasa ili uishi maisha safi katika ubinti wako na hatimaye
uwe mama bora hapo baadae. Mungu akubariki unapofanya hivyo
sasa.
CO
“Bwana Yesu, niko mbele zako, nimetambua ya kwamba mimi
ni mwenye dhambi na ninastahili hukumu, lakini pia
ninatambua ya kwamba wewe Yesu ulisulibiwa msalabani na
ukafa ili kulipa hukumu yangu, na siku ya tatu ukafufuka
kukamilisha wokovu kwa kila anayekuamini. Na mimi leo,
ninaamini ndani ya moyo wangu na ninakiri kwa kinywa
changu ya kwamba wewe Yesu ndio njia ya kweli na uzima ya
EE

kwenda mbinguni. Ninaomba unisamehe dhambi zangu zote,


na uniokoe leo. Ufute jina langu kwenye kitabu cha hukumu na
uliandike kwenye kitabu cha uzima. Unijaze na Roho wako
Mtakatifu aniwezeshe kudumu katika wokovu. Nimeomba haya
na kuamini, KATIKA JINA LA YESU, AMEN.”
FR

69
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

PY
CO
EE
FR

70
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

HITIMISHO

B inti yangu, baada ya kupata maarifa haya na kwa Neema ya

PY
Mungu, ishi kwa ujasiri ukijua unao uwezo wa kushinda dhambi
na kuvuka salama katika kipindi hiki cha ujana.
Neno la Mungu linasema katika 1 Yohana 2:14b “Niwaandikia
ninyi vijana kwa sababu mna nguvu na na Neno la Mungu
linakaa ndani yenu, nanyi mmemshinda yule mwovu.”
CO
Kwa hiyo, hakikisha unatenga muda wa kutosha kusoma Neno la
Mungu, kutafakari na kuomba, majibu ya maswali yote utayapata
humo.
Ni vizuri pia kuwa na mtu unayemwamini, aliyeokoka kwa ajili ya
kukuongoza na kukusaidia kuvuka salama. Anaweza kuwa mzazi,
mlezi au hata mchungaji. Hakuna jambo ambalo halina majibu au
EE

suluhisho. Hata kama unadhani ulishaharibu maisha yako na huoni


namna ya kurekebisha, tafuta msaada kwa watu niliowataja hapo
juu au unaweza kuwasiliana nami kwa namba za simu nilizoweka
hapa chini.
Mungu akubariki sana
FR

71
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

Vitabu vingine vilivyoandikwa na Mwl. Francis M. Langula


• KUWA MWANAFUNZI
• SASA NINAANZA KUISHI (NAMNA YA KUTAMBUA

PY
KUSUDI)
• HEKIMA ITAYOMSAIDIA MSICHANA KUOLEWA
• KIUMBE KIPYA
Fuata link hizo hapo chini kama unapenda kujifunza zaidi bure kwa
CO
njia ya Audio & Text na Mwl. Francis M. Langula
• TELEGRAM
— Mafundisho ya wote (Audio):
https://t.me/Neno_na_Pst_Francis
— Mafundisho maalumu ya vijana (Audio):
EE

https://t.me/RYG4Christ
• WhatsApp : +255754711247
• Youtube: Pastor Francis M. Langula
• Facebook
FR

— https://www.facebook.com/francis.langula
— https://www.facebook.com/UponyajiWaKiMunguKwaWote
• Instagram: @francis.langula

72
H E K I M A YA K U M S A I D I A B I N T I K U J I T U N Z A

PY
CO
EE

Bonyeza hapa kutoa ushuhuda


wako
FR

73

You might also like