Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 1

MKATABA WA UPANGAJI NYUMBA

Mkataba huu leo tarehe ………………………………………… kati ya mwenye nyumba


ndugu………………………………………………… wa SLP Dar es Salaam na mpangaji
ndugu………………………………………………… kwa vile mwenye nyumba anamiliki nyumba mtaa
wa ……………………………………., Dar es Salaam na amempangisha nyumba na atapanga kwa
masharti yafuatayo:-

HIVYO MKATABA HUU UNASHUHUDIA YAFUATAYO;

1. Mpangaji amekubali kupanga nyumba kwaajili ya makazi kwa hiari yake mwenyewe, amekubali
kulipa kodi kwa kipindi cha mwezi kwanzia tarehe 01/05/2024 mpaka 31/05/2024
2. Kodi yake ni 200,000/= kwa mwezi mmoja na analipa ya mwezi mmoja kama
alivyokubaliana na mwenye nyumba
3. Mpangaji atatumia nyumba hiyo kwa makazi yake halali, na mpangaji anaweza kuendelea na
mkataba kwa makubaliano ya pande zote mbili.
4. Mpangaji atatimiza masharti yote ya mkataba huu aliyopanga ya nyumba hio bila kubugudhiwa
na mwenye nyumba.

MPANGAJI ANAWAJIBIKA KUFANYA YAFUATAYO;

I. Kulipa kodi kama alivyokubaliana na mwenye nyumba katika mkataba huu.


II. Mpangaji aruhusiwi kumpangisha mtu mwingine, sehemu aliyoipanga bila kupata idhini ya
maandishi kutoka kwa mwenye nyumba.
III. Mpangaji atalipia gharama za umeme na maji atakavyotumia.
IV. Kama mpangaji akimaliza muda wa kupangisha atakabidhi chumba/nyumba bila kuvunja au
kuharibu sehemu yeyote ya nyumba na kuacha vyote ulivyovikuta ndani ya nyumba hiyo. Na pia
hairuhusiwi kutoboa ukuta isipokuwa kwenye maeneo ya kuwekea mapazia.
V. Kama hautoendelea kupanga kwa kipindi kingine unatakiwa kutoa taarifa miezi mitatu (3) kabla
ya mkataba kuisha muda wake.
VI. KODI HAITORUDISHWA BAADA YA MAKUBALIANO NA MWENYE NYUMBA.
VII. Mpangaji haruhusiwi kumpangisha mpangaji mwingine ndani ya chumba chake. Endapo
akimpangisha mtu mwingine mkataba utaanza upya.

Kwa kuthibitisha makubaliano hayo wahusika mtathibitisha kwa kuweka sign mkataba huu kama
ifuatavyo;

JINA LA MWENYE NYUMBA SAHIHI

……………………………………………. ………………………

JINA LA MPANGAJI SAHIHI

……………………………………………. ………………………

SHAHIDI WA MWENYE NYUMBA SAHIHI

……………………………………………. ………………………

SHAHIDI WA MPANGAJI SAHIHI

……………………………………………. ………………………

You might also like