Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 209

ISHI NDOTO YAKO

Siku 30 za Kuanza Kuishi Maisha Unayoyatamani

Joel Arthur Nanauka


© Julai 2021 Joel Arthur Nanauka

Kitabu hiki kimeandikwa na Joel Nanauka, Kikiwa ni


kitabu cha 7 katika mfululizo wa Success Diaries.

Haki zote zimehifadhiwa. Huruhusiwi kunakili,


kudurufu au kutumia sehemu ya kitabu hiki bila idhini
ya mwandishi. Kufanya hivyo itakuwa ni ukiukwaji wa
haki za mwandishi, na ukiukwaji wa taratibu hii
unaweza kupelekea mashitaka toka kwa waandaaji wa
kazi hii.

Joel Arthur Nanauka


Dar - Es - Salaam, Tanzania. Afrika Mashariki
Simu: +255 756 094 875 / +255 745 252 670
Barua pepe: jnanauka@gmail.com
Tovuti: www.joelnanauka.com

Kimesanifiwa na: Andrew Rwela


Simu +255 743 200 738
Email: rwelaandrew@gmail.com
UTANGULIZI

Unajua una uwezo mkubwa ndani yako? Usikubali


kuishi maisha ya wastani.

“Sehemu tajiri kabisa duniani sio kwenye


machimbo ya dhahabu America ya kusini au
kwenye visima vya mafuta vya Iraq na Iran. Sio
kwenye machimbo ya almasi ya Afrika ya kusini
wala kwenye akaunti za benki kubwa duniani.

Sehemu tajiri kabisa katika dunia haiko mbali na


wewe, ni kwenye makaburi. Huko yamelala
makampuni ambayo hayakuanzishwa, ubunifu
ambao haukutolewa, vitabu vizuri kabisa ambavyo
havikuandikwa, michoro ambayo haikuchorwa.

Kwenye makaburi kuna HAZINA kubwa na UWEZO


mkubwa ambao umeondoka duniani bila ya
kutumika kabisa” Dr. Myles Munroe Haya ni moja ya
maneno mazito sana yaliyowahi kunitafakarisha

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 01


sana kwenye maisha yangu. Niliugundua kuwa
nisipokuwa makini na kuweka nguvu katika
malengo ya maisha yangu nami nitaenda kufukia
utajiri wangu makaburini, na mimi siko tayari kabisa
kufanya hivyo; wewe je?

Ndani yako kuna uwezo na hazina kubwa sana


ambayo ukianza kuitumia kwa kiwango cha juu
itakusaidia sana kutoka hapo ulipo na kwenda
kiwango cha juu sana cha maisha yako.

Kikwazo cha kwanza ni kuamini kuwa kuna kitu


kikubwa na cha tofauti ndani yako, ni kuamini kuwa
pamoja na changamoto ambazo unazipitia leo bado
unaweza kufikia kiwango cha juu cha mafanikio
kwenye maisha yako.

Kama umekuwa unajiuliza kila siku,” nitaanzaje?”


Kama umekuwa unajiuliza kila siku “mbona niko
kwenye wakati mgumu ndoto yangu itatimia kweli?”

Kama umekuwa kila siku unajiona hauwezi na


umefika mwisho na hakuna matumaini tena. Kama

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 02


uko kwenye giza nene na haujui uanzie wapi; kama
umejikuta umekwama kwenye kazi ama mahusiano
ambayo yamekuwa ni mwiba kwako; kama
umekuwa kila usiku unatoa machozi kwa magumu
unayopitia na unajiuliza,” lini mambo haya
yataisha?” … basi kitabu hiki ni kwa ajili yako.

Sina shaka kuwa siku hizi 30 zitafungua ukurasa


mpya wa maisha yako na nakushauri kwa kila siku
utakayosoma jaribu kuchukua hatua bila
kuchelewa. ANZA KUISHI NDOTO YAKO. Kumbuka
Ndoto Yako Inawezekana.

See You At The Top

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 03


SIKU YA 01

Jifunze Kwa Colonel Sanders.


Usiruhusu Changamoto Zizuie Ndoto Yako

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 04


Akiwa na miaka 5 alifiwa na baba yake, Akiwa na
miaka 16 aliamua kuacha shule, Akiwa na miaka 17
tayari alikua kapoteza ajira 4, Akiwa na miaka 18
aliamua kuoa, Akiwa na miaka kati ya 18-22, alikua
msimamizi wa njia za reli lakini hakufanya vizuri na
akafukuzwa.

Baadaye alijiunga na jeshi lakini alifukuzwa pia,


Akatuma maombi shule ya sheria ila hakupata
nafasi, Akawa wakala wa kutoa bima lakini
alishindwa pia.

Hatimaye akapata ajira kama mpishi na mwosha


vyombo wa mgahawa mdogo nchini Marekani.
Alijaribu kupigania kumpata mtoto wake ambaye
alikuwa ameondoka na mama yake ila akashindwa,
na kuamua kumshawishi mkewe kurejea nyumbani.

Akiwa na miaka 65 alistaafu ajira yake ya kupika na


kuosha vyombo katika mgahawa na baada ya
kustaafu alipata mafao yake kutoka serikalini kiasi
cha dola za kimarekani 105, takribani shilingi za
kitanzania 231,000/= kwa sasa.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 05


Baada ya kuona maisha yamekuwa magumu sana
alifanya jaribio la kujiua, akiamini hakuna thamani
ya kuishi tena, na kwamba ameshashindwa kabisa.
Kwa bahati nzuri jaribio lake la kujiua halikufanikiwa
na akapona.

Baada ya muda akaamua kukaa chini ya mti na


kuandika mambo ambayo alitamani hadi wakati huo
awe amefanikiwa kuyafanya, ila aliona ayaandike
yale aliyoyakamilisha tayari, akagundua kuna
mambo mengi hakuyafanya bado.

Baadaye alijiuliza swali: “Hivi kuna jambo gani


ambalo naliweza kulifanya vizuri kuliko jambo lolote
lile katika maisha yangu?” Akagundua lipo jambo
moja ambalo anaweza kulifanya vizuri zaidi kuliko
mtu yeyote yule anayemfahamu, na ilikua ni namna
ya kupika.

Akaamua kuchukua dola za kimarekani 87 sawa na


shilingi za kitanzania 191,400/= kutoka kwenye
hundi yake ya pensheni na kununua kuku.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 06


Akawakaanga kwa kuwachanganya na viungo
mbalimbali na akapata mchanganyiko wa aina yake
unaovutia.

Akaamua kupita nyumba kwa nyumba na kuwauza


kwa majirani zake katika mji wa Kentucky
alipokuwa anaishi. Kuku wake wakapendwa sana,
na akaamua kuanzisha mgahawa wake uitwao
Kentucky Fried Chicken (KFC) (Kuku wa
kukaangwa wa Kentucky) uliokua ukitengeneza
mchanganyiko wa kuku alioubuni.

Hatimaye biashara yake ikakua na akafungua


migahawa mingi ya KFC nchini Marekani.
Mchanganyiko ule ukazidi kupendwa na kutanua
wigo wa biashara yake.

Huyu si mwingine ni Colonel Harland Sanders


mwanzilishi wa migahawa ya KFC duniani. Licha ya
kustaafu akiwa "fukara wa kutupwa" katika umri wa
miaka 65, lakini hadi wakati anafariki mwaka 1980
akiwa na umri wa miaka 90 alikua katika orodha ya
mabilionea wakubwa nchini Marekani.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 07


Kwa sasa migahawa ya KFC imeenea kote duniani
katika nchi takribani 123, ikiwemo Tanzania, na ni
migahawa ya pili mikubwa uliyoenea zaidi duniani
baada ya migahawa ya McDonald's.

Mwaka 2013 migahawa ya KFC ilifanya mauzo ya


dola bilioni 23 sawa na shilingi za kitanzania trilioni
50. Maana yake ni kwamba mauzo ya KFC kwa
mwaka mmoja ni karibia mara mbili ya bajeti ya
Tanzania ya mwaka 2016/2017

Kumbuka muasisi alikua FUKARA hadi uzee wake


(miaka 65) na akadhani ameshindwa maisha na
kujaribu kujiua. Lakini baada ya kutafakari akaona
bado ana nafasi ya kujaribu tena. Akajaribu japo
katika umri wa uzee, na hatimaye Mungu
akamfanikisha. Akawa BILIONEA MKUBWA sana
nchini Marekani.

Je wewe umekata tamaa ya maisha? Ulitamani


kusoma lakini ukashindwa kwa kukosa ada?
Umesoma lakini umekosa ajira? Miaka inapita na
unaona wenzio wanaajiriwa wewe uko tu

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 08


nyumbani? Je Umejaribu biashara lakini kila wakati
unapata tu hasara? Unahisi kukata tamaa? Unahisi
Mungu amekuacha?

Hapana, usikate tamaa, Mungu hajakuacha.


Jipange tena na uanze upya. Haujakawia bado....
Kitu kikubwa ni "mtazamo wako" (attitude).

Haijalishi mambo ni magumu kiasi gani. Una kila kitu


cha kukufanya ufanikiwe. Amua kubadili mtazamo
wako leo ili ubadili historia ya maisha yako kwani
inawezekana, anza sasa.

WAZO lolote ulilonalo, NDOTO yoyote uliyonayo


unaweza kuanza kuiishi kwa mafanikio kama
utaamua kuwa inawezekana. Usikubali hali
uliyoipitia huko nyuma iwe kizuizi cha mafanikio
yako ya kesho. ISHI NDOTO YAKO Kumbuka Ndoto
Yako Inawezekana.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 09


SIKU YA 02

Anza Kufanyia Kazi


Ndoto Yako Leo, Usichelewe!.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 10


Elisha Gray alikuwa mtu wa kwanza kupata wazo la
kusafirisha sauti kwenye waya (teknolojia ya simu)
hata hivyo alizembea kuchukua hatua kwenda
kusajili wazo lake, kila siku alikuwa anaghairisha.

Baada ya Muda Alexander Graham Bell, naye


akapata wazo hilo hilo na akaamua kuchukua hatua
kwenda kulisajili.

Mnamo tarehe 14 February 1876 Alexander alienda


ofisi ya usajili wazo/ hakimiliki (patent) akasajili.
Baada ya kughairisha kwa miaka mingi Elisha naye
alienda ofisi ya usajili wazo siku hiyohiyo.

Ila alipofika akaambiwa kuna mtu anaitwa


Alexander amekuja na kusajili wazo hilo saa moja
iliyopita, hivyo hautaweza kuruhusiwa kulifanyia
kazi. Akasema "mimi nilikuwa nalo tangu mwaka
jana…” Wakamjibu “Jambo la muhimu sio kuwa na
wazo bali jambo kubwa ni kuchukua HATUA".

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 11


Hadi leo dunia inamtambua Alexander Bell kama
ndiye mgunduzi wa simu kwa sababu alichukua
HATUA.

Ukiwa na wazo bila kuchukua hatua utashangaa


wenzako wanasonga mbele na wewe uko palepale.
Wakati mwingine utashangaa unazungumzia wazo
anakuja mwingine analifanyia kazi na anafanikiwa.

Mawazo huwa hayakusubiri, yakiona unachelewa


kuyatekeleza yanaenda kwa mtu mwingine.

Je, leo una wazo lolote ambalo umekuwa


unalighairisha mara kwa mara? Chukua hatua leo na
lifanyie kazi ili usije ukajutia wakati wengine
watakapolifanyia kazi na kufanikiwa.

Kama bado unasumbuliwa na tabia ya kughairisha


mambo katika maisha yako, nakushauri utafute
kitabu changu cha ISHINDE TABIA YA
KUGHAIRISHA MAMBO na ukisome na kitakusaidia
sana kuanza kufanyia kazi wazo lako leo.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 12


Je, leo unapanga kuchukua hatua gani kuanza
kufanyia kazi wazo lako?

Kumbuka Ndoto Yako Inawezekana.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 13


SIKU YA 03

Jambo Muhimu Kufanya Kama


Ulijaribu Ndoto Yako Na Ikafeli

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 14


Sir Edmund Hillary alijaribu kwa mara ya kwanza
kuupanda mlima Everest (mita 8,848), ambao ndio
mlima mrefu zaidi duniani bila mafanikio.

Katika safari hiyo ya kwanza sio tu alishindwa


kufika kileleni bali pia mwenzao mmoja alifariki
njiani. Pamoja na kuwa walishindwa, waliandaliwa
sherehe ya mapokezi baada ya kurudi jijini London.
Kwenye jukwaa walilopokelewa kulikuwa na picha
kubwa ya mlima Everest.

Sir Edmund alipopewa nafasi ya kuongea, akageuka


nyuma akanyoosha kidole kwenye ile picha ya
mlima akasema kwa sauti kubwa.

“Mount Everest, you have defeated us, but I will


return and defeat you, because you can't get any
bigger but I can”.

Akiwa na maana kuwa "Mlima Everest


umetushinda, ila nitarudi na kukushinda, kwani
wewe hauwezi kukua zaidi ya ulivyo sasa, ila mimi
nitaendelea kukua".

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 15


Na kweli alirudi na kuwa mtu wa kwanza kufanikiwa
kuupanda mlima Everest hadi juu.

Sijui changamoto gani unayokutana nayo kwa sasa,


ila ninachojua ni kuwa UNAWEZA KUAMUA KUWA
MKUBWA KULIKO CHANGAMOTO YAKO.
USIKUBALI CHANGAMOTO YOYOTE IKUANGUSHE
LEO.

"GET BIGGER THAN YOUR CHALLENGE”

Kuanzia leo anza kupanga mbinu za kukusaidia


kukua ili urudi kuushinda mlima wako kwani una
nafasi ya kukua kuushinda mlima wako. Kama
ulishindwa kufanya huko nyuma, leo unaweza
kuamua kuwa mkubwa kuliko changamoto yako na
ukaanza kufanya.

Kumbuka Ndoto Yako Inawezekana.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 16


SIKU YA 04

Acha Mbegu Yako Ikue,


Usiifukue Hadi Ndoto Yako Itimie

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 17


Kwenye kufukuzia ndoto yako kuna kitu kinaitwa
"invisible effect span" huu ni ule muda ambao
utakuwa hauwezi kuona kwa waziwazi matokeo ya
kile unachofanya ingawa haimaanishi kuwa hakuna
kitu kinaendelea.

Ni kama vile kuna wakati ambao ukipanda mbegu


yako ardhini itabidi uisubiri kwa muda fulani kabla
haijachipua, ingawa kusubiri kwako kunamaanisha
kuendelea kumwagilia na kuitunza.

Ukweli ni kuwa hata kama kwa nje hauoni


kinachoendelea chini ya udongo, ila mbegu huwa
inaendelea kukua na kutoona inavyokuwa
haimaanishi kuwa haikui. Ukiwa na haraka ya
kutaka kuona inavyokuwa na ukaifukua mbegu
yako, itabidi uanze upya kwa kupanda nyingine
tena.

Kama una uhakika na unachokifanya na unapitia


kipindi kama hiki cha "invisible effect span" usijione
wewe wa ajabu kwani kila mtu huwa anapitia wakati
huu.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 18


Tatizo la watu wengi hawako tayari kuvumilia hata
kidogo, wakifanya kitu kisipoleta matokeo tu kwa
siku moja wanaacha wanaanza kingine.

Hii unakuwa kama kila siku unapanda na unafukua


mbegu yako, matokeo yake kila mtu anakuona
unakuwa bize kupanda ila haupati mavuno.

Je, wewe ni mfukua mbegu maarufu?

ACHA TABIA YA KUFUKUA MBEGU KILA SIKU! Je,


kuna kitu gani ambacho unatakiwa kukizingatia na
kukifanya bila kuachia njiani?

Leo dhamiria kuwa utaendelea kufanya kilicho


sahihi kuelekea kutimiza ndoto yako bila kukata
tama.

Kumbuka Ndoto Yako Inawezekana.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 19


SIKU YA 05

Jibu La Changamoto Zinazoikabili


Ndoto Yako Liko Njiani

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 20


Mwaka 2012 niliandika kitabu changu cha kwanza
ambacho kinaitwa YOU CAN RISE AGAIN
(UNAWEZA KUINUKA TENA). Kitabu hiki kilikuwa ni
matokeo ya kukutana na watu wengi sana ambao
walikuwa wamekata tamaa ya maisha.

Kati ya watu ambao siwezi kuwasahau maishani


mwangu ni dada mmoja ambaye alikuwa
amekusudia kujiua kwa sababu kila dalili iliyokuwa
inamzunguka ilionyesha kuwa hawezi kufanikiwa
tena.

Aliposoma kitabu hicho alinipigia simu na kuniambia


stori yake na kisha akasema "Nimeamua kuamini
ulichoandika na nitajaribu tena". Leo hii ni
mfanyabiashara mkubwa anayemiliki kampuni ya
ukopeshaji fedha.

Nilichogundua ni kuwa, hakuna tatizo lisilo na


suluhisho, hakuna hali isiyo na majibu. Hatua ya
kwanza katika kuinuka tena ni kuhakikisha kuwa
HAUPOTEZI TUMAINI lako. Inawezekana kila dalili
inaonyesha kuwa umekwisha, hautaendelea tena,

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 21


hautafanikiwa tena, AMUA kuamini kuwa bado kuna
tumaini la wewe kushinda changamoto
inayokukabili na unaweza kuinuka tena.

Nani angeamini kuwa, Nelson Mandela anaweza


kuwa Rais wa Afrika ya Kusini baada ya kukaa
gerezani kwa miaka 27?

Nani angeamini Colonel Sanders angeweza


kuanzisha KFC akiwa na miaka 65 baada ya
kustaafu? Nani angeamini Oprah Winfrey angeweza
kuwa bilionea pamoja na kubakwa mara nyingi na
kupata ujauzito akiwa na miaka 14?

Nani angeamini Glenn Cunighum angeweza


kutembea tena na kushinda dhahabu katika maisha
yake, baada ya miguu yake kuungua moto na
kusababisha atumie "wheelchair" (kiti
wanachotembelea walemavu wa miguu) kwa miaka
mingi?

Na wewe pia unaweza kuinuka tena. Anza siku


yako leo kwa matumaini na fungua ukurasa mpya

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 22


wa kuamini ndoto yako tena. YOU CAN RISE AGAIN
(Unaweza kuinuka tena). Bila kujali umeshindwa
kuishi ndoto yako huko nyuma, leo una nafasi
nyingine.

Leo bila kujali unapitia changamoto kubwa kiasi


gani, bila kujali kuna watu wangapi ambao
wanakuamini ama la, jiambie wewe mwenyewe
“Changamoto hii nitaishinda na nitatimiza ndoto
yangu”.

Kumbuka Ndoto Yako Inawezekana.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 23


SIKU YA 06

Njia Nzuri Zaidi Ya Kutumia Fedha


Zako Ili Ndoto Yako Itimie

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 24


Northcoste Parkinson's alitunga kanuni maarufu
inayoitwa -"Parkison's law ". “Kanuni hii inasema
kuwa siku zote matumizi ya mtu huwa
yanaongezeka kadiri kipato chake
kinavyoongezeka”.

Ili upate mafanikio ya kifedha kwa kuwa na pesa za


ziada mara kipato chako kinapoongezeka
unatakiwa kufanya mambo mawili: -

Moja ni kuhakikisha kuwa kipato chako


kinaongezeka kwa kasi kuliko matumizi yako
yanavyoongezeka. Hii ina maana kuwa, kwa asilimia
ongezeko la kipato chako liwe juu kuliko matumizi
yako. Kama kipato chako kimeongezeka kwa 10%,
basi matumizi yako yaongezeke chini ya 10%.

Mbili ni kuamua kuwa hautaongeza matumizi yako


hadi kipato chako kitakapofikia asilimia fulani na
ongezeko hilo litakuwa la chini pia. Hii maana yake
ni kuwa unajilazimisha kuendelea kuishi maisha
ambayo umekuwa unaishi kwa muda zaidi hata
baada ya kipato chako kuongezeka.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 25


Kumbuka nia kubwa hapa ni kuweza kupata pesa
ya ziada ambayo unaweza kuitumia kuwekeza, ama
kufanya jambo fulani la kimaendeleo. Kuna watu
wengi sana kipato chao cha sasa ni mara mbili ya
kipato chao cha miaka mitano iliyopita, lakini
hawawezi kubakiwa na kitu kila mwisho wa mwezi.

Tatizo ni kuwa kipato chao kiliongezeka lakini pia


hapohapo waliongeza matumizi yao kwa kiwango
cha juu.

Kumbuka inapofika suala la fedha, jambo kubwa sio


UNAPATA KIASI GANI Bali UNABAKIZA kiasi gani
baada ya matumizi yako yote. Ukiona hakuna
unachobakiza ina maana hapo umeshaingia kwenye
mzunguko wa umaskini.

Leo fanya mahesabu na uangalie namna ya kuvunja


kanuni ya Parkison. Ili uanze kuishi ndoto yako
unahitaji kuwa na nidhamu ya pesa na uyadhibiti
matumizi yako kuanzia leo.

Kumbuka Ndoto Yako Inawezekana.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 26


SIKU YA 07

Hatua 3 Kuu Za Kufuata Ili


Uweze Kuanza Kazi Ambayo
Ni Ndoto Yako

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 27


Wakati mwingine unaweza kujikuta unafanya kazi
ambayo sio ndoto yako, pengine ulijikuta kwenye
kazi hiyo kwa sababu haukupata ambayo ulikuwa
unaitafuta ama uliingia kwa nia ya kuijishikiza ili
baada ya muda uondoke lakini ukajikuta
umeshindwa kutoka hapo.

Kama kwa sasa unafanya kitu ambacho haukipendi


na unatamani kukibadilisha, hatua hizi zitakusaidia
sana.

i. Tambua sababu inayokusukuma kubadilisha


kazi.
Kabla haujaanza kuchukua hatua ya kutafuta kazi
mpya, jiulize na upate jibu la swali hili "Ni nini
kinakusukuma kutafuta kazi mpya?"

Kuna watu wanasukumwa na kutaka kuongeza


kipato zaidi, wengine wanataka cheo kikubwa zaidi,
wengine wanataka kubadilisha wanachofanya,
wengine wamegombana na bosi wa sasa, wengine
wanaona wamekaa muda mrefu sehemu moja, na
wengine wamegundua wanachofanya sio kitu

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 28


wanachokipenda kwa dhati kukifanya n.k.
Kila sababu huwa ina mchakato wake wa kupitia
hadi kupata kazi mpya. Hivyo lazima ujue wewe
unasukumwa na nini?

Kama mwaka huu unataka kubadilisha kazi. Basi


fuatilia kwa umakini hatua hizi na utajifunza mbinu
za kukusaidia kupata kazi mpya.

Je, umeshajua sababu yako ya kutaka kubadilisha


kazi ni ipi?

ii. Chambua sifa zinazohitajika katika kazi mpya


unayotaka na jipange.
Kwa kila kazi nyingine unayoitaka kuna sifa muhimu
zinazohitajika. Sifa hizi zinaweza kuwa ni kiwango
cha elimu, uzoefu, umri n.k.

Kabla haujaanza kutuma maombi (ku-apply) ya kazi


yoyote jaribu kuchunguza na ujue kwa undani kazi
unayoitafuta wanataka sifa gani hasa. Namna nzuri
ni kupitia matangazo ya kazi ambayo huwa
yanatokewa kwa nafasi unayoitafuta, yasome na

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 29


uyachambue. Ukishamaliza, fanya "personal
competence analysis" (Jichunguze sifa ulizonazo
kulinganisha na zinazohitajika).

Kwa zile unazokosa angalia jinsi utakavyozijenga


kwa muda ulionao. Tengeneza mpango wako
ambao unaweza kuwa wa muda mrefu ama wa
muda mfupi.

Nilipotaka kupata kazi umoja wa mataifa (UN)


ilinilazimu nisome kozi mbili za ziada na moja
ilinigharimu mwaka mzima kuimaliza, ila ilinisaidia
kupata kazi ninayoitaka. Kwako inawezekana
ikahitajika muda mfupi zaidi ama mrefu zaidi.

Nawe jiulize, unajipangaje kwa mwaka huu kujenga


uwezo usiokuwa nao wa kazi mpya unayoitafuta?
Mara nyingi kazi mpya tunazozitafuta zinahitaji pia
tuwe na ujuzi mpya.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 30


iii. Amua kuhusu makampuni/ mashirika
unayotaka.
Moja ya mbinu nzuri sana ya kutafuta kazi ni
kufanya "focused job searching" - Hii inamaanisha
sio tu unajaribu kuapply kila kazi iliyo mbele yako
bali unachagua mashirika maalumu/ kampuni
ambazo unazilenga.

Unaweza kuweka lengo lako katika NGO's pengine


za kilimo, mashirika ya kimataifa, serikalini, benki
n.k Kadiri ambavyo unalenga katika aina fulani ya
taasisi ndivyo inavyokuwa rahisi kutafuta taarifa,
kujenga uwezo na mtandao unaotakiwa.

Kupata kazi unayotaka ni kama vile kutafuta


mchumba, unakuwa na vigezo vyako na
unahakikisha unalenga wa aina hiyo.

Ukiwa mtu ambaye kila anayepita unamfukuzia


utashangaa unazeeka mambo hayajaeleweka au
utashangaa unampata ambaye haendani kabisa na
wewe kwa sababu mwishoni utalazimika kufanya
maamuzi kwa presha ya muda.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 31


Nakutakia mafanikio unapoanza safari yako ya
kuelekea kupata kazi unayoipenda.

Kumbuka Ndoto Yako Inawezekana.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 32


SIKU YA 08

Jinsi Ya Kung’aa Haraka


Kwenye Ndoto Yako

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 33


Unapokuwa unaishi katika ndoto yako unatakiwa
ujue kuwa kuna watu wengi sana ambao nao
watakuwa wanafaya kilekile ambacho wewe
unakifanya. Hata hivyo kuna mambo ambayo
ukiamua kuyafanya yatakusaidia sana kufanikiwa
kwa haraka na kujitofautisha mapema sana na
wengine wote ambao wako kwenye field yako.

Ukifuata hatua hizi nne ambazo watu wengi


zimewasadia utafanikiwa kung’arisha ndoto yako
kwa haraka sana.

i. Gundua "Core Genius" yako


Core Genius ni ENEO fulani au AINA FULANI ya
kufanya kitu unachofanya ambapo hupata matokeo
makubwa sana. Kila unachofanya kuna watu
walishafanya ama kuna watu wanafanya tayari. Ili
uweze kufanikiwa kwa haraka tafuta kwa bidii
kugundua nguvu yako ya tofauti katika kile
ufanyacho.

Nguvu yako inaweza kuwa katika ubunifu wa


mambo yako, namna ya uandishi, staili ya uongeaji

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 34


au mkazo wa sauti n.k. Usijaribu hata siku moja
kutoka kwenye "Core Genius" yako kwani
utajipoteza kwenye game, hata kama hujaona faida
yake kwa sasa. Jaribu kutafakari na upate jibu la
swali hili, Je, unaijua Core Genius yako?

ii. Wekeza katika "skills" muhimu zote


Kwenye kila ulichoamua kufanya kuna ujuzi (skills)
muhimu ambazo zinahitajika. Pata muda uzitafute,
uzijue na uanze kutumia muda wako kuwekeza
katika kupata ujuzi wote muhimu katika eneo lako.
Jitahidi kila siku upate maarifa mapya ya
kukuongezea ujuzi katika eneo lako.

Kitaalamu unatakiwa uwe na kati ya ujuzi (skills)


tano hadi saba ili upate matokeo makubwa na ya
haraka. Je, ni ujuzi gani unaohitajika uwe nao ili
ufanikiwe katika eneo lako? Jaribu kutafakari na
kupata majibu ya swali hili leo.

Ukigundua kuwa kuna ujuzi wa muhimu ambao


hauna, tafuta namna ya kuwa na mpango wa
kuupata na kuuendeleza.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 35


iii. Anza na fursa iliyopo
Mwaka 2000 nilianza kupata wazo la kuandika na
watu waweze kusoma. Akili yangu ya kwanza ikawa
kuomba nafasi kwenye jarida la shule nipewe
ukurasa nianze kuandika.

Kwa sababu hakuna aliyewahi kuona kazi yangu,


sikupewa nafasi. Nilichoamua ni kuanza kuandika
kwenye karatasi nyeupe zenye ukubwa wa A4 na
kila jumatatu nikaanza kuzigawa darasani.
Nakumbuka mada yangu ya kwanza ilikuwa "Who is
to be blamed?" (“Nani wa kulaumiwa?”), ambayo
ililenga kuwafanya watu wawajibike na maisha yao.

Haikuchukua muda watu wakaanza kuzipenda kazi


zangu. Kazi zangu zikawa maarufu na mhusika wa
jarida la shule akanipa nafasi ya kuwa naandika kila
Jumatatu na na kuweka ubaoni ambapo kila
mwanafunzi aliweza kuona.

Hivyo ndivyo safari yangu ilivyoanza. Usiwe kila


siku unasema kuna fursa kubwa unaisubiri.
Usisubiri nafasi kubwa, anza na kinachowezekana.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 36


Je, leo unaweza kuanza kufanya nini?

iv. Jifunze kwa waliotangulia, tafuta mwalimu wako.


Pamoja na kuwa Christiano Ronaldo na Lionel Messi
wamefanikiwa kupata tuzo nyingi sana katika eneo
la uchezaji wa mpira, lakini bado wako chini ya
uangalizi wa walimu wao (makocha).

Unaweza kuwa na kipaji kizuri au uwezo wa


kipekee lakini kama hautakuwa tayari kujifunza kwa
waliotangulia ama kuwa chini ya uangalizi wa
mtu/watu wa kukusaidia hautafika mbali sana.

Nilipotaka kufanya kazi Umoja wa Mataifa nilitafuta


watu wawili wa kunilea katika eneo hilo na
walinisaidia ndoto yangu ikafanikiwa na muda wote
niliofanya ulikuwa ni wa mafanikio. Nilipotaka
kuanza kujiajiri katika kile ninachofanya sasa
niliwatafuta watu waliotangulia na kufanikiwa katika
eneo hili nilipata mwongozo wao na nikaendelea
kujifunza.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 37


Hata sasa najifunza kwa wengi ndani na nje ya nchi.
Hii ni muhimu kwani siku utakayodhani kuwa
umefika, ujue ndio mwanzo wa anguko lako.

Katika mkakati wako wa mwaka huu usisahau


kuweka mkakati wa kujifunza kwa wengine na
kupata mtu wa karibu wa kukusaidia. Kabla
haujaendelea kusoma, andika sasa majina ya watu
ambao utaanza kujifunza kwao.

Unaweza kujifunza kwa kukutana nao, kusoma


vitabu vyao au wanachoandika kwenye mitandao
ya kijami ama kujifunza kupitia video zao.

v. Uwe na "Focus"
Kwa mujibu wa mwalimu wa mafanikio Tony Robins,
watu wengi wanafeli sio kwa sababu hawana
uwezo mkubwa, bali ni kwa sababu hawajengi
uwezo wa hali ya juu na ulio bora katika kitu kimoja
(mastery). Akili yao inatapatapa.

Katika ulimwengu wa sasa mwanadamu wa


kawaida kila siku anapokea taarifa toka vyanzo

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 38


mbalimbali kwa ukubwa wa sawa na 34GB kila siku
(Ukiweka taarifa za ukubwa huu kila siku kwenye
kompyuta ya kawaida inajaa baada ya wiki).

Kwa siku mtu wa kawaida kwa ulimwengu wa sasa


kupitia mitandao ya kijamii, TV, Email, Billboard n.k,
huwa anasoma na kusikia takribani maneno
105,000 (Hii ni kwa mujibu wa utafiti wa chuo kikuu
cha California - San Diego).

Hata hivyo ubongo wako hauna uwezo wa kutumia


taarifa zote hizo. Hivyo sehemu ya kwanza ya kuwa
na focus ili UISHI NDOTO YAKO ni kuhakikisha
unadhibiti taarifa zinazoingia kwenye ufahamu
wako kupitia masikio au macho.

Je, huwa unatumia njia gani kudhibiti kutokusoma/


kusikiliza kila taarifa, bali zile tu zinazokufaa?

Kumbuka Ndoto Yako Inawezekana.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 39


SIKU YA 09

Mjue Aina Ya Bosi Uliyenaye,


Ili Asiwe Kikwazo Katika
Kutimiza Ndoto Zako

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 40


Mtu ambaye anakusimamia utendaji wako wa kazi
huwa anaweza kuwa sababu ya wewe kufanikiwa
zaidi ama kuwa ni kikwazo katika safari ya kuelekea
kutimiza ndoto ulizonazo.

Kuna aina nne za mabosi ambao wamekwamisha


wengi na wewe ni muhimu ujifunze namna ya
kuwakabili wasije wakakwamisha ndoto zako.

Aina ya kwanza ya bosi: Bosi Anayetaka


kusimamia kila kitu (Micromanager).

Unaweza kupata kazi nzuri unayoipenda ila ukipata


bosi wa hivi unatakiwa kujua namna ya kudeal naye
kwani anaweza kukusababishia “stress” (msongo
wa mawazo) za hali ya juu.

Bosi wa namna hii anapenda kusimamia kila kitu


bila kujali ni kidogo kiasi gani. Hata ikitokea
anakuagiza kununua chakula atakupa maelekezo
kama vile ndio mara yako ya kwanza kununua.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 41


Akikupa kazi huwa hakupi nafasi ya kutumia
ubunifu, kila saa yuko shingoni kwako kukufuatilia
unavyotekeleza kazi zako.

Mara nyingi ukifanya kazi na mtu wa namna hii


unaweza kujiona kama vile huwezi kazi kwa sababu
mabosi wa hivi wengi huwa wanaona wao ndio
wanajua zaidi ya kila mtu.

Madhara yao makubwa ni kuwa wanapenda


kukosoa sana kwa sababu wao hudhani wao ni
bora kuliko mtu yoyote na wanaamini njia zao za
kufanya kitu ndio sahihi. Huwa hawakupi nafasi ya
kutumia ubunifu hata kidogo.

Ukiwa naye wa namna hii inabidi kazi zako uzifanye


kwa kasi sana kabla ya muda uliotarajiwa ili uepuke
kuulizwa ulizwa kila wakati na jitahidi kabla ya
muda unaotakiwa uwe umemaliza. Lakini pia uwe
mtu ambaye unampa mrejesho (feedback) mara
kwa mara katika kazi anazokutuma.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 42


Hicho cha kwanza kitamfanya akuamini zaidi kadri
siku zinavyoenda na hii ya pili itakusaidia kumfanya
asikuulize-ulize sana.

Hata hivyo tatizo likizidi pengine utahitaji kuongea


naye kumueleza jinsi ufuatiliaji wake wa karibu
unavyoathiri ufanisi na mkubaliane namna bora ya
kufanya kazi.

Aina ya pili ya bosi: Bosi ambaye hapatikani

Kuna wakati unaweza kufanya kazi na bosi ambaye


kumpata ofisini ni shida sana. Hii inaweza
kusababisha kazi zako zote zinazohitaji uhusika
wake kukwama, ama kuchelewa sana.

Bosi wa namna hii inawezekana asiwe anapatikana


kwa sababu shughuli nyingi za kiofisi zinafanyika
nje hivyo anakuwa na safari nyingi sana ama
unakuta anatumia kazi kujishikiza tu ila ana
MICHONGO yake binafsi mingi isiyohusiana na ofisi.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 43


Usipokuwa mwangalifu unaweza ukajikuta una vitu
vingi vilivyokwama kwa sababu kumpata ni shida.
Mabosi wa hivi mara nyingi hata kuwapata kwenye
simu ni shida na siku wakikaa ofisini hadi unajiuliza
"hivi kuna nini leo?"

Kwa sababu ya kutopatikana kwao kirahisi, mara


nyingi ni ngumu kuwazoea na huwezi kujua kama
wamefurahi ama wamekasirika.

Ukiwa na bosi wa namna hii ni vizuri kuhakikisha


kuwa unazungumza naye na kukubaliana njia nzuri
ya kufanya kazi, kuwasiliana n.k. Usipofanya hivyo
kazi zikichelewa utalaumiwa wewe na atakuambia
"MBONA HUKUNIAMBIA hili wakati ni KITU CHA
HARAKA"?

Aina ya tatu ya bosi: Bosi asiye na uwezo


(Incompetent Boss).

Huyu ni yule ambaye kila ukimuona kwenye hiyo


nafasi unajiuliza maswali mengi sana kuwa
amefikaje hapo?

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 44


Mabosi wa namna hii huwa wanakuwa na
mbwembe na maneno mengi sana ila kazi hawa
hawajui. Kwa sababu ya ukweli huu, huwa
wanakuwa wakali sana kwa mambo ambayo hata ni
madogo.

Unachotakiwa kujua ni kuwa mbwembwe na


maneno mengi na kutumia mabavu pasipokuwa na
hoja, ndio mbinu yao ya kujilinda na kuficha udhaifu
wao. Hawa ndio wale ambao ukitofautiana nao
kidogo tu utasikia "Mimi ndio bosi nimeshasema
tumefunga mjadala"

Mabosi wa namna hii, wanategemea zaidi


MAMLAKA yao kuliko USHAWISHI WAO.
Hawashindani kwa HOJA bali wanashindana kwa
MABAVU.

Ukishawagundua cheza nao kwa step kwakuwa


huwa wanapenda sana kuthibitisha mamlaka yao
kwa kufukuza watu kazi au kutoa maonyo kwa
barua.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 45


Ili ufanikiwe katika kuishi ndoto yako ni lazima uwe
makini namna unavyohusiana na mabosi walio juu
yako.

Aina Ya Nne Ya Bosi: Bosi anayekuchukua bila


sababu za msingi (Bigot Boss)

Hii ni aina ile ya mabosi ambao unakuta wameanza


kukuchukua bila wewe kujua sababu
zinazowafanya wakuchukie. Mara nyingine mabosi
hawa wanaweza hata kukukuchukia kwa sababu
zilizo nje ya kazi.

Kuna wakati anaweza kujitahidi sana kufanya kazi


kwa bidii lakini unashangaa kadiri unavyofanya kwa
bidii ndivyo anavyozidi kukuchukua. Kuna wakati
chuki za bosi wa namna hii zinaweza kutoka hata
na jinsi unavyovyaa vizuri ama jinsi unavyopendwa
kwenye mazingira ya ofisini kwako.

Wakati mwingine inawezekana ikawa ni kwa


sababu kuna mtu alishawahi kugombana naye huko
nyuma ambaye umefanana naye sana ama

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 46


mmefanana jina na kila anapokuona anamkumbuka
na chuki zinakujia wewe. Hawa ni aina ile ya mabosi
ambao ni ngumu sana kuwaridhisha na
kuwafurahisha, mara zote huwa wanaona udhaifu
na mambo ya kulaumu tu kutoka kwako na ni
ngumu sana kwao kuona kitu kizuri cha kukusifia.

Kwa bosi wa namna hii maana yake ni kuwa tatizo


haliko kwako bali liko kwake. Kitu unachoweza
kukifanya ni kutumia “Cognitive Dissonance”: Hapa
unachofanya ni kutafuta kitu ambacho anakipenda
sana na huwa anafurahia kukiongelea.

Kwa mfano ukigundua anaipenda timu fulani ya


mpira wa miguu na kila inapocheza huwa
anashabikia kwa bidii basi tafuta mada itakayogusa
timu yake na atakapoanza kuwa na furaha
kuizungumzia hapo ndipo unaweza na wewe
kuchomekea mambo yako.

Kiufupi ni kuwa ili uendane na bosi wa namna hii ni


lazima utafute kuzungumza naye mambo ambayo
anayafurahia sana kila wakati ili kupunguza “gap” la

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 47


kukuchukia. Hata hivyo kama utaona chuki zake
zinaathiri sana utendaji kazi wako ni vyema kufuata
taratibu za kazi ili kutatua ambayo inaweza hata
kuhusisha kuhamishwa kitengo ama kbadilishiwa
majukumu ambayo hayatahitaji uwe unaripoti
kwake moja kwa moja.

Aina Ya Tano: Bosi mjuaji wa kila kitu na mtumia


mabavu (Despot Boss).

Umeshawahi kukutana na bosi ambaye yeye anajua


kila kitu na hataki ushauri kutoka kwa mtu yoyote
Yule? Yaani yeye anachosema anataka ndiyo uwe
uamuzi wa mwisho kabisa, hana muda kabisa wa
kupata maoni ya wengine wanavyofikiria.

Mabosi wa namna hii hata pale anapokuja


kukuomba ushauri ukweli ni kuwa anakuwa
ameshaamua kitu cha kufanya tayari.

Mabosi hawa wanapenda kulazimisha mambo


yafanyike kama wanavyotaka wao namara nyingi
hupenda kutumia mamlaka kupitisha hoja zao. Mara

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 48


nyingi utawasikia wanasema “Mimi ndio bosi,
nimeshasema”. Aina hii ya bosi wanapenda sana
ugomvi hata kwa kitu kidogo, ukikosea kufanya jinsi
wanavyotaka hawatachukua muda kukuuliza kwa
nini umefanya ulichofanya bali wataona kuwa
umewadharau, wenyewe huwa wanajiona ni
“Smart” kuliko mtu yoyote Yule pale ofisini.

Ukijaribu kuwapa mawazo mbadala kila wakati


ataanza kukuchukia. Unapotaka kuwashauri mabosi
hawa usijaribu kuwapa ushauri wa moja kwa moja
bali jaribu kama kuwauliza swali ili baadaye
ionekane imetoka kwao.

Kwa mfano badala ya kusema “Bosi mi nafikiria


tukifanya njia hii tutapata matokeo makubwa sana”
sema “Bosi unashauri nini kuhusu kutumia njia hii?”.

Kumbuka mwisho wa siku mabosi wa namna hii


huwa wanapenda sana kuchukua sifa hata kama
wewe ndio umetoa wazo watasema kuwa wazo ni
lao na ukijari bu tu kuonyesha wazo lako ni bora
kuliko wao, watakuchukia siku zote.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 49


Tunasema mabosi wa namna hii “Cheza nao kwa
step”.

Kumbuka Ndoto Yako Inawezekana.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 50


SIKU YA 10

Sababu 6 Zinazowakwamisha
Watu Wengi Wasifikie Kilele
Cha Ndoto Zao

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 51


i. Malengo lukuki bila vipaumbele.

Kuna watu mwaka huu wamerudia kosa lilelile


ambalo wanalifanya miaka yote. Kuwa na malengo
mengi yaliyorundikana bila kuwa na vipaumbele
vinavyotakiwa.

Huwezi kufanya vitu vyote ndani ya miezi 12.


Chagua mambo machache ambayo utayapa
rasilimali zote zinazohitajika (muda, nguvu, pesa
n.k). Hii ndio maana ni muhimu kujua malengo yako
ya muda mrefu, ya kati na ya muda mfupi.

Ili ndoto yako kubwa uliyonayo iweze kukamilika, ni


lazima uweke mpango wa kutimiza vipengele
vidogovidogo vya ndoto yako hadi pale
utakapofanikiwa.

ii. Kutofanya kitu kinachochangia kwenye ndoto


yako kila siku

Watu wengi sana huwa wanaandika ndoto yao


kisha wanaanza kukimbizana nayo. Henry Ford

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 52


alisema kuwa "ukitaka kumla tembo hadi kummaliza
basi mkate vipandevipande kwanza"

Mafanikio ya ndoto yako ya mwaka, yapo katika


uwezo wako wa kutekeleza kila siku kitu
kinachochangia kwenye ndoto hiyo. Unatakiwa uwe
na uwezo wa kugawa mambo utakayofanya toka
kwa mwaka, kuja mwezi, wiki hadi siku. Je, leo
unafanya nini kinachochangia mafanikio ya ndoto
yako ya mwaka?

iii. Kushindwa kujenga tabia zinazotakiwa

Unapotaka kufanikiwa katika ndoto ambayo


haujawahi kufanikiwa katika maisha yako
inamaanisha pia ujenge tabia ambazo haujawahi
kuwa nazo katika maisha yako.

Kosa lingine wanalolifanya watu ni kuwa na ndoto


kubwa mpya bila kujiwekea mkakati wa kujenga
tabia mpya pia. Inaweza kuwa ni tabia ya kuweka
akiba, kujisomea, mazoezi, kuamka mapema n.k.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 53


Swali: Hebu jiulize kwa mwaka huu umefanikiwa
kujenga tabia gani mpya ya kukusaidia kutimiza
ndoto yako ambayo mwaka uliopita haukuwa nayo?
Ukisoma kitabu changu kingine cha TABIA 12
ZINAZOLETA MAFANIKIO utajifunza tabia
unazotakiwa kuzijenga ili ufanikiwe kwa haraka
ndani ya muda mfupi.

iv. Kushindwa kujenga uwezo unaotakiwa.

Kwa kila ndoto mpya unayotaka kuitimiza kwenye


maisha yako kuna aina mpya ya uwezo au maarifa
ambayo unayahitaji.

Watu wengi sana huwa wanaongeza kiwango cha


ndoto bila kuwa na mikakati ya kujiongezea uwezo.
Unaweza kuongeza uwezo kwa kujifunza kupitia
wengine, kusoma vitabu, kuhudhuria semina au
kwenda kwenye mfumo rasmi wa shule.

Je, kwa ndoto ndoto uliyonayo kwa sasa unahitaji


uwezo gani ili uweze kuitimiza?

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 54


v. Kutokuwa na mfumo wa kuwajibika.

Moja ya sababu kubwa inayowafanya watu


wanaofanikiwa kwenye ajira washindwe kufanikiwa
wanapojiajiri ni kwa sababu wanapokuwa
wameajiriwa huwa wanakuwa na mfumo mzuri wa
kuwawajibisha tofauti na wanapojiajiri.

Ni watu wachache sana ambao wana nidhamu yao


binafsi (self-discipline) kwa sababu hiyo wanahitaji
MTU mwingine wa kuwasaidia kuwajibika kwenye
malengo yao. Huyu anaweza kuwa mwenzi, rafiki
ama “mentor” wako.

Ni hatari kutokuwa na MTU ambaye anakusaidia


kuwajibika katika utaratibu rasmi. Mwaka huu
tafuta MTU wa namna hii na utaona tofauti kubwa.
Hii ndio maana hata wachezaji bora duniani bado
wanakuwa chini ya kocha anayewawajibisha na
kuwasimamia ili wafanikiwe zaidi.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 55


vi. Tabia ya Kughairisha Mambo

Hebu jaribu kujiuliza wakati mwaka huu unaanza


ulisema utafanya nini? Kama uliandika mahali hebu
jaribu kupitia upya orodha yako na uangalie ni
mambo mangapi kati ya yale uliyaandika umefanya?

Moja ya sababu kubwa inayowafanya watu


wasipige hatua muhimu kwenye maisha yao ni
kuwa "Mr & Mrs Tommorow". Wao kila siku
wanakuambia nitafanya kesho, matokeo yao miaka
inaenda hakuna walichofanya.

Kuna kitu chochote ambacho ukikumbuka leo


unajilaumu na unatamani ungekuwa umefanya
mapema. Usipokuwa mwangalifu unachogharisha
leo utajilaumu kesho pia.

Bado mwaka huu utakuwa Mr / Mrs Tommorow?


Jitahidi kuzikabili sababu hizi ili zisichangie
kukwamisha mafanikio ya ndoto yako.

Kumbuka Ndoto Yako Inawezekana.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 56


SIKU YA 11

Taa Hizi Mbili Nyekundu Zikiwaka


Ujue Ndoto Yako Iko Hatarini

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 57


Kila dereva mzuri anayeendesha gari, mara tu
atakapoona kuna taa kwenye "dashboard" yake
inawaka kuashiria kitu hakiko sawa, atashughulikia
haraka la sivyo atajikuta gari linaharibika ama
anapata ajali.

Wewe ni dereva wa maisha yako na kuna taa


nyekundu mbili ambazo kila wakati lazima
uziangalie kwenye "dashboard" ya maisha yako.

Moja ni pale unapoona kama vile umepoteza


mwelekeo na unaenda usikokujua. Hii haimaanishi
kuwa hauna kazi au biashara, inawezekana unayo
ila ukiangalia unaona kabisa hakuna mahali
inakupeleka.

Hii inawezekana pia unalipwa mshahara lakini wote


unaishia kwenye kukusaidia kupata mahitaji
muhimu tu na hakuna cha ziada unachoweza
kufanya zaidi (Survival Income).

Au inawezekana unafanya kwa muda mrefu ila


hakuna mabadiliko yoyote ambayo unayaona.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 58


Taa ya pili ni pale unapoona bidii yako haiendani na
matokeo yako. Inawezekana wewe si mvivu ila
ukweli ni kuwa matunda ya maisha yako hayafanani
kabisa na nguvu unazotumia.

Wakati mwingine ili uvuke kiwango kingine lazima


ufanye mambo kwa namna ya tofauti ama uanze
kuambatana na watu tofauti.

Je, gari yako iko salama? Kuna taa yoyote kati ya


hizi inakuwakia?

Ukiona una dalili hizi, usiendelee kukimbiza gari,


pata muda wa kutafuta ushauri na kurekebisha ili
uende salama. Inawezekana kuna maamuzi ya
haraka utahitaji kuyafanya ili kujinusuru.

Kumbuka kadri unavyochelewa kufanya maamuzi


ndivyo hali inavyozidi kuwa mbaya na gharama ya
maamuzi itakuwa kubwa zaidi.

Kumbuka Ndoto Yako Inawezekana.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 59


SIKU YA 12

Ilipojificha Siri Ya Mafanikio Yako

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 60


Siku ya kwanza nilipomuona Nick Vujicic nilijifunza
kuwa kinachofanya watu wasifanikiwe, si kwa
sababu hawana vile ambavyo wengine wanavyo ila
ni kwa sababu hawajaweza kutumia vile
walivyonavyo kwa kiwango cha juu.

Akiwa hana mikono wala miguu, Nick anaishi


maisha ya furaha na mafanikio kuliko watu wengi
walioko duniani ambao wamekamilika kuwa na
viungo vyote walivyonavyo.

Katika udhaifu wake huo, Nick ananishangaza sana


kwani anatembea dunia nzima kuwatia watu moyo
ili kufikia ndoto zao. Kiuhalisia ilikuwa anatakiwa
yeye ndiye atiwe moyo na afarijiwe kutokana na
hali yake lakini hali iko tofauti.

Ukweli ni kuwa kinachowafanya wengi washindwe


katika maisha ni ule mtazamo na tafsiri waliyonayo
kutokana na changamoto zinazowakabili.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 61


Kuna mambo 3 ya kuzingatia kutokana na maisha
ya Nick: -

i. Kuwa na furaha maishani ni uamuzi wako.

Bila kujali hali na matatizo unayopitia, suala la


kuamua kuwa na furaha ni uamuzi wako
mwenyewe. Wanasaikolojia wanahusisha sana hali
yako ya furaha na kiwango cha mafanikio yako.
Kiufupi ni kuwa, furaha hufanya akili yako iongeze
ubunifu, unaongeza ufanisi wa kufanya mambo na
huvutia watu wengi na fursa nyingi upande wako.

Kama Nick anaweza kuwa mwenye furaha katika


hali yake, je wewe unashindajwe kuwa na furaha.
Usiisubiri furaha ije, jiambie nafsini mwako “bila
kujali kinachoendelea katika maisha yangu leo
nachagua kufurahi”

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 62


ii. Ukiamini na kuamua kufanya jambo unaweza.

Kwa hali halisi ya Nick, sikuwahi kufikiri kuwa


anaweza kutumia kompyuta ama kuandika, ila
nilishangazwa sana nilipoona video yake anaweza
yote hayo lakini pia anaweza hata kuogelea (ajabu).
Kitu cha kutambua ni kuwa, ukiamua na kuamini
unaweza kufanya kitu fulani, inawezekana.

Unataka kuwa mfanyabiashara, inawezekana.


Unalenga kufanya kazi katika kampuni kubwa ya
kimataifa, inawezekana. Unalenga kujenga nyumba
au kununua gari mwaka huu, Inawezekana. Unataka
kufaulu vizuri masomo yako, inawezekana. Bila
kujali madhaifu yako, imani yako ya kuwa
inawezekana inatosha kukufanya uvuke vikwazo
vyote.

iii. Mafanikio yanatokana na unavyojiona

Sehemu nyingi anazoenda Nick, huwa


wanamuhurumia na wengine hata kulia kutokana na
hali yake. Najiuliza, kuna watu wangapi kwa sababu

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 63


hawana kiungo kimoja tu wamekata tamaa na
wengine wanakaa barabarani tu kuomba msaada,
hawaamini kama kuna maisha tena ya mafanikio.

Najiuliza wangapi wameachwa kwenye ndoa zao na


wamekata tamaa ya kuinuka tena, najiuliza ni
wangapi wameumizwa na waliowapenda na
kuwaamini na hawaoni tumaini tena.

Najiuliza ni wangapi wametafuta kazi kwa muda


mrefu na wamekata tamaa tayari, hivi ni wangapi
wanasoma kitabu hiki leo na wamejaribu kila
biashara na kila wazo limefeli na wanaona
haiwezekani tena, hivi ni wangapi wanafikiria kuwa
kwa sababu waliwahi kufeli mitihani huko nyuma
basi hawataweza kufaulu tena?

Nick anatufundisha kuwa, mafanikio yetu


yanatokana na tunavyojiona na tunavyotafsiri yale
yanayotokea maishani mwetu. Usikate tamaa kwa
sababu ya kile usichonacho, tumia kidogo
ulichonacho na utashangazwa na matokeo yake.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 64


Je, na wewe umepitia hali kama ya Nick? Jifunze
kutoka kwake. Ama kuna mtu unayemfahamu
anapitia hali kama ya Nick na anashindwa kuishi
ndoto yake? Mpe mbinu hii toka kwa Nick ajifunze.

Kumbuka Ndoto Yako Inawezekana.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 65


SIKU YA 13

Usiruhusu Maisha Yako Ya Leo


Yakuamulie Maisha Yako Ya Kesho

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 66


Miaka kadhaa iliyopita kuna rafiki yangu mmoja
alinitembelea nilipokuwa nakaa maeneo ya
Kinondoni jijini Dar es Salaam. Alipoingia ndani
akakaa kimya kwa muda kidogo kisha akaniuliza
"Ina maana siku zote huwa unatoka humu?"
nikamwambia ndio, akasema "Ile furaha unaitoa
wapi?"

Nikamwambia kwa sababu "NIMEIONA KESHO


YANGU INANG'ARA KULIKO LEO YANGU".
Kilichomshangaza ni kuwa alikuta godoro liko chini
na hakuna samani yoyote ile (Hakukuwa na kiti,
meza, kabati au kochi).

Kulikuwa kuna ndoo chache na hakuna hata TV, ila


alikuta kuna vitabu vya kutosha na akashangaa kwa
sababu hakuna siku aliniona nikiwa mnyonge ama
niliyekosa furaha, kila siku nilikuwa namtia moyo
kuhusu ndoto yake na pale alipoonyesha kukata
tamaa.

Kabla hajaondoka akaniambia "Joel, ukweli ni kuwa


mimi ndio nilikuwa natakiwa nikutie wewe moyo

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 67


kutokana na hali yako na sio wewe kila siku unanitia
moyo na kuwatia moyo wengine"
Maisha ni namna unavyoyatazama, ukiona
unakokwenda hata kama haujafika utaishi kwa
furaha na hali ya ushindi mkubwa akilini mwako.

Usikubali hali ngumu ya leo ikusababishe upoteze


ndoto yako ya kesho. Leo siishi kama nilivyokuwa
naishi wakati ule. Bila kujali leo uko katika mazingira
magumu kiasi gani, kataa kuamini kuwa
hautafanikiwa. Kesho yako ni nzuri kuliko leo kama
hautakata tamaa.

Hata kama ulipo leo sipo unapotaka kuwepo,


USIKUBALI KUPOTEZA TUMAINI, HALI YAKO
INAWEZA KUBADILIKA.

Kumbuka Ndoto Yako Inawezekana.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 68


SIKU YA 14

Jikubali Thamani Yako


Ni Kubwa Mno

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 69


Thamani yako unaipima kutokea wapi?
Uwezo wako wa kufanya mambo makubwa kwenye
maisha unatokana na jinsi unavyojithamini na
kujikubali (self-esteem). Hii inamaanisha kiwango
ambacho unajiona UNAWEZA na UNASTAHILI kuwa
vile unavyotaka, ndio kitajulisha UTAFANIKIWA kwa
KIWANGO GANI.

Changamoto ya watu wengi sio kwamba hawana


uwezo mkubwa sana ndani yao, bali uwezo wao
UMESHINDWA kudhihirika ama UMEKUFA kabisa
kwa sababu wamedhani Kuwa thamani yao
inatokana na wanachosema WATU ama VITU
walivyonavyo sasa.

Kuna watu wamepoteza kabisa thamani yao kwa


sababu ya mtu waliyempenda aliwanenea maneno
ya kuwaonyesha HAWANA thamani. Kuna watu
wamepoteza thamani yao kwa sababu ya kosa
moja walilowahi kulifanya huko nyuma na
likawaletea aibu au kufeli na hadi leo
hawajajisamehe.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 70


Kuna watu ambao thamani yao wanaipima kwa
elimu yao na kuna wale ambao thamani yao
wameamua kuipima kwa kiwango cha pesa
walizonazo.

Hatua ya kwanza ya kutimiza ndotoyako ni


KUJIKUBALI kwanza kwa 100% bila kujali nani
hakukubali au hali yako ya sasa.

Wewe ni wa thamani sana bila kujali bosi wako,


mpenzi wako, rafiki yako ama adui yako anasema
nini kuhusu wewe. Usijithaminishe kwa mavazi,
pesa au maneno ya watu.

THAMANI yako ni kubwa kwa sababu UNA KITU


KIKUBWA SANA NDANI yako na KESHO YAKO
INANG'ARA sana.

Jithamini na jiambie "Bila Kujali nilivyo ama


wanachosema wengine, mimi ni wa Thamani sana"
Una UWEZO mkubwa sana ndani yako umejificha,
ila usipokuwa makini unaweza kujikuta unashindwa
kuutumia hadi unaoondoka duniani. Nakukumbusha

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 71


tena kuwa, wewe ni wa thamani sana.

Kumbuka Ndoto Yako Inawezekana.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 72


SIKU YA 15

Jinsi Ya Kuifanya Kila Wiki Kuwa Ya


Mafanikio Ili Utimize Ndoto Yako

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 73


Taasisi iliyoko nchini Uingereza inayoitwa MIND
inayojishughulisha na afya ya akili iliwahi kufanya
utafiti kwa wafanyakazi 700 ambao ulitoa matokeo
yenye mambo mengi ya kujifunza.

Katika utafiti huu, ilionekana kuwa watu wengi


huiona siku ya Jumatatu ni kama mateso makubwa
kwao. Ilionekana kuwa mmoja kati ya watu watano
huwa wanasingizia kuugua siku za Jumatatu ili
wasiende ofisini, lakini moja ya tatu huwa
wanachelewa kwenda ofisini wakisingizia matatizo
ya usafiri ama matatizo ya kifamilia ambayo
hayapo.

Utafiti ulidhihirisha kuwa 25% ya watu wanaichukia


Jumatatu kwa sababu wanachukia kazi
wanayofanya na hawatamani kuendelea nazo. Kwa
sababu hiyo kuna watu wengi sana siku ya
Jumatatu ni siku ambayo wanapoteza muda kazini
bila kuwa na ufanisi.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 74


Kuna mambo kadhaa unatakiwa kuzingatia: -

i. Hata kama kazi uliyonayo hauipendi, ili mradi


umekubali kuifanya, jitahidi kufanya kwa ubora wa
hali ya juu. Hakuna faida ya kuboronga, wakati
mwingine unavyofanya kazi ya sasa inaweza
kuamua kama utapata unayotaka ama la.

ii. Kama kila ikifika Jumatatu unaanza kusikia hasira


na huzuni ya kwenda ofisini kwako, ina maana
unachofanya sio sahihi kwako, jitahidi kufanya
maamuzi ya kubadilisha, hakuna manufaa yoyote
ya kuendelea kufanya kitu ambacho haukipendi
kwenye maisha yako yote yaliyobakia.

iii. Kila wiki kabla haijaanza jifanyie tathmini kuhusu


maisha yako na ujiulize kama mwelekeo wa maisha
yako uko sahihi. Panga ratiba yako, mambo
unayotaka kuyafanikisha na jiulize, wiki hii nataka
kufanikiwa katika jambo gani kubwa?

Ukigundua umekosea njia using'ang'anie kuonyesha


kwamba uko sahihi, fanya maamuzi ya

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 75


kurekebisha kwa haraka.

Kumbuka Ndoto Yako Inawezekana.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 76


SIKU YA 16

Jinsi Ya Kitumia Accumulative


Advantage Ili Kutimiza Ndoto Zako

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 77


Wataalamu wa mambo ya ekolojia walifanya utafiti
kugundua aina ya miti iliyoko kwenye msitu
mkubwa duniani wa Amazon. Walipochunguza
waligundua kuwa kuna miti (species) takribani
16,000 ya aina tofauti tofauti.

Hata hivyo waligundua kuwa kuna aina 227 kati ya


hizo ndio ambazo zimechukua nafasi kubwa ya
msitu wote, takribani nusu ya miti yote iliyoko
msitu. Kwa maneno mengine asilimia 1.4 ya aina
yote ya miti ndio imejaza msitu kwa 50%. Swali
likawa ni nini kimeifanya miti hii kuwa na uwezo wa
kukua kwa wingi kuliko miti mingine.

Walipochunguza wakagundua kuwa aina hizi za miti


zilizojaza misitu kwa wingi huwa zinapoanza kukua
zinakuwa kwa kasi kuliko miti mingine. Hii hufanya
miti hii ipate jua zaidi na kunyonya virutubisho na
maji ardhini kuliko ile mingine.

Baada ya muda huwa inakuwa na nguvu na


inafanya ile mingine iwe dhaifu na ishindwe kufanya
kazi vizuri. Hii ndio inaitwa kanuni ya “accumulative

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 78


advantage” ambayo kwenye maisha ya wanadamu
pia inafanya kazi. Ilikufanikiwa zaidi ni lazima uwe
unafanya kitu cha ziada kuliko wengine. Ni lazima
uwe unaweka bidii kuliko mtu wa wastani, uwekeze
ubunifu kuliko ilivyozoeleka, ujitoe zaidi wakati
wengine wanasema wamechoka n.k.

Kitaalamu wanasema ukiweza Kila siku kufanya


kwa 1% zaidi ya mtu wa kawaida, baada ya muda
mfupi utakuwa umekuwa mbali sana. Kuanzia leo
anza kutumia kanuni ya “accumulative advantage?”
kama mbinu ya kutimiza ndoto yako.

Kumbuka Ndoto Yako Inawezekana.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 79


SIKU YA 17

Wajue Wezi 5 Wa Muda


Wanaokwamisha Ndoto
Za Watu Wengi

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 80


Moja ya rasilimali muhimu sana unayohiitaji ili
uweze kufanikiwa ni muda, ukweli ni kuwa uwezo
wako wa kutumia muda vizuri unaweza kukupa
fursa ya kufanikiwa kwa haraka kuliko watu
wengine wengi ambao wanatumia muda wao
vibaya.

Kila siku, hata hivi leo utakutana na wezi wa muda


wako ambao unatakiwa kuwakabili ili wasikwamishe
safari kuelekea katika kufanikisha ndoto yako.

MWIZI WA 01: Disorganised life (Maisha yasiyo na


mpangilio)
Kuna watu kila siku akiamka asubuhi anatumia
dakika 20 kutafuta nguo ya kuvaa, kuna mwingine
leo amehangaika kutafuta ufunguo wa gari kwa
sababu jana alisahau aliuweka wapi, au haujawahi
kusikia mtu anatumia dakika 15 kutafuta soksi ya
pili kwa sababu zote alizonazo ni za mguu mmoja?

Kuna mwingine ofisini kwako kila siku kuna kitu


amesahau alipoweka, kila wakati utasikia anasema
"yaani niliweka hapa nakumbuka kabisa, sijui nani

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 81


amechukua" Watu wa namna hii tunasema
wanasumbuliwa na "Clutter Syndrome" dalili za
ugonjwa wa kutopanga mambo yao vizuri. Kama
kila siku unatumia dakika 30 kutafuta vitu ambavyo
hujui umeviweka wapi, kwa mwaka utatumia dakika
10,800 ambazo ni sawa na kupoteza wastani wa
siku 8 kila mwaka.

Kuanzia leo panga vitu vyako vizuri usiku kabla


haujaenda kulala. Amua na andaa nguo utakayovaa,
panga dawati lako la kazi vizuri ama eneo lako la
biashara na panga ratiba yako ya siku vizuri.
Hakikisha kuwa vitu ambavyo unavitumia kila siku
na mara kwa mara unaviweka sehemu maalumu kila
wakati.

Je, na wewe unasumbuliwa na ugonjwa wa "Clutter


Syndrome" unaokuibia muda wako kila siku?
CHUKUA HATUA LEO.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 82


MWIZI 02: Maelekezo yasiyokamilika (Incomplete
Instructions).

Moja ya uwezo ambao watu wengi wamepoteza


kwa sasa ni uwezo wa kusikiliza kwa makini
(attentive listening). Watu wengi siki hizi
hawasikilizi ili KUELEWA ila wanasikiliza ili KUJIBU,
matokeo yake wanakosa kupata taarifa muhimu
wanazopewa.

UNAPOPEWA maelekezo au UNAPOTOA


maelekezo kwa mtu mwingine hakikisha
yamekamilika kwa 100% kwani usipofanya hivyo
utafanya tofauti na itakulazimu kutumia muda
mwingine KUREKEBISHA ulichofanya.

Ukipewa maelekezo na bosi wako hakikisha


umeelewa vizuri, USIKURUPUKE kufanya halafu
unakuja kuambiwa urudie kazi ama unaonekana
umefanya tofauti.

Unapopokea maelekezo, hakikisha unaandika au


unaweza kurudia kuyasema kwa aliyekupa ili kuona

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 83


kama umeelewa alivyotaka, ama uulize swali
usipoelewa. Usiwe wale watu ambao ni waoga
kupata ufafanuzi matokeo yake wanafanya ndivyo
sivyo kila wakati na wanalazimika kurudia kazi.

Kama wewe unampa maelekezo mwingine,


hakikisha unatoa maelekezo yaliyojitosheleza. Kila
unapotoa maelekezo nusunusu yatakurudia na
utajikuta hiyo kazi inakuchukulia muda wako zaidi.
Ukialikwa mahali, pata maelekezo
yanayojitosheleza ya agenda, muda, mahali husika
n.k.

Kuna mtu alishawahi kualikwa kwenye mkutano Dar


es Salaam akaenda eneo la posta, kumbe mkutano
ulikuwa mbezi, kisa ni kwamba hoteli zilikuwa
sehemu mbili zinazofanana majina yeye akadhania
itakuwa ni ile anayoifahamu, ilibidi atumie pikipiki ili
kuwahi, jambo hili linaondoa utulivu wa akili,
kupoteza muda na hata kupoteza ufanisi.

Siku zote kabla haujaanza kazi yoyote ile


HAKIKISHA UMEELEWA VIZURI, hii itakuokolea

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 84


muda wako mwingi wa kuambiwa "sikumaanisha
hivyo". Kama unatoa maelekezo usidhani mtu
ataelewa unavyotaka, bali HAKIKISHA AMEELEWA
wewe unavyotaka.

MWIZI WA 03: Watu wanaokupumzikia

Kuna watu ambao kama mko nao ofisi moja


wakishafanya kazi zao wakimaliza muda
wanapotaka kupumzika na kukusanya nguvu
wanachofanya ni kuanza kutembea kwenye meza
za wengine na kupiga stori.

Usipokuwa makini kila wakati watakuwa


wanakutumia wewe kupumzika na wanakufanya
uache kazi zako na kuwasikiliza. Hawa huwa
wanaitwa kwa lugha ya kilatini, OFFICUS
INTERRUPTUS.

Watu hawa pia hupatikana maeneo ya biashara,


kwenye vyombo vya usafiri na hata mashuleni.
Utashangaa tu wanakuja na kukuanzishia stori
hazina kichwa wala miguu.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 85


Ukiwagundua unatakiwa usiwape hata dakika moja
kwani ukiwazoesha siku ya kwanza watakuwa kila
siku wanafanya hivyo.

Wakati mwingine watu hawa wanaweza kuwa mbali


na wewe ila wakipata ofa ya muda wa maongezi,
utakuta wanakupigia simu na wala hawana agenda
ya maana, wanaanza kukuuliza "mambo vipi", "ishu
zinaendaje", "mechi ulicheki jana", "kuna jamaa
tulimaliza naye unakumbuka?”

Kiufupi mazungumzo yao huwa hayana hata


muunganiko. Unakuta ndani ya dakika 10 kuna
mambo kama 10 tofauti ameongea. Watu hawa
ukiwaruhusu kwa siku wanaweza kukupotezea kati
ya masaa 2 hadi 3, ambayo ungeyatumia kwa
mambo mengine na kupiga hatua.

Siku hizi hata kwenye makundi (groups) za


WhatsApp hawa utawakuta. Akifanya kazi muda
wake wa kupumzika anakuja anaanza kutuma
meseji na kuanzisha mada mbalimbali na anataka
kila mtu achangie.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 86


Yeye ni muda wake wa kupumzika, kama wewe ni
muda wako wa kazi, USIKUBALI AKUPUMZIKIE. Leo
ukimgundua mtu huyu, mwambie haraka
USINIPUMZIKIE.

MWIZI wa 04: Vikao visivyo na ufanisi (Ineffective


Meetings)

Taasisi ya utafiti ya Gallop ya nchini marekani


iliwahi kufanya utafiti na kugundua kuwa kadiri
unavyopanda juu kimajukumu unaweza kujikuta
unatumia takribani 80% ya muda wako kwenye
vikao.

Changamoto kubwa huwa ni kuwa na vikao visivyo


na ufanisi na vinavyokuchukulia muda zaidi ya ule
unaotakiwa. Bila kujali vikao hivi unavifanya kwa
kukutana uso kwa uso, kwa njia ya simu ama
Skype, ni lazima uhakikishe unatumia muda mfupi
uwezavyo.

Moja ni hakikisha kila kikao kinawekewa ajenda


hata kama unakutana na mtu mmoja, ajenda

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 87


ziwekwe wazi kabla ya kukutana.

Mbili ni muhimu kukubaliana muda mtakaotumia


kwa ajili ya kikao chenu na ikiwezekana kama kuna
ajenda nyingi, kuwe na muda maalumu wa
kujadiliana kila ajenda husika.

Tatu ni kudhibiti watu wanaopenda kutoka nje ya


mada. Kuna watu huwa wanasababisha vikao kuwa
virefu kwa sababu kila baada ya muda mchache
huwa wanaingiza mada tofauti na kuanza kujadili na
kuacha mada kuu iliyowakutanisha.

Mwingine katikati ya mada anashika simu halafu


anaanza kujichekesha, au anashtuka mkimuuliza tu
kuna nini, anaanza kuwaonyesha picha au meseji
isiyohusiana kabisa na mnachojadili. Usiruhusu
kujadili mada isiyo husika hadi mmemaliza mada
iliyowakutanisha.

Nne: Kudhibiti “Attention Seekers” Hawa ni wale


ambao wanapenda kuchangia kila kipengele hata
wasivyovijua vizuri ili mradi tu waonekane. Matokeo

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 88


yake huwa wanarudiarudia yale ambayo wengine
wameongea. Kumbuka MAFANIKIO YA KAZI/
BIASHARA SIO VIKAO VINGI bali VIKAO VYENYE
UFANISI.

MWIZI wa 05: Kujihusisha na kila kitu

Kuna mambo mengi sana ambayo yanaendelea


katika mazingira yanayotuzunguka na kama
unataka kuwa na ufanisi huwezi kuhusika katika kila
jambo. Kuna watu huwa wanashindwa kabisa
kujizuia na wanataka kuhusika kwenye kila kitu.
Kuna sababu tatu kubwa zinazowapelekea kuwa
hivyo.

Moja ni kuwa Mr/Mrs Yes, yaani unakuta mtu


anakubali vitu ambavyo anajua kabisa hana muda
wa kufanya, ama moyoni anajua HATAKI kufanya.
Jifunze kusema HAPANA, sio udhaifu bali ni njia ya
kuokoa muda wako. Kuna watu wanaona kama
kusema hapana ni dhambi, ukiwa hivyo utapoteza
muda mwingi sana.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 89


Pili ni kutaka kuwa kila mahali, hali ambayo
hujulikana kama “Omnipresent Syndrome”. Kuna
watu hawataki kupitwa, wanataka kila stori
washiriki, kila harusi wawepo, kila mtoko wako
mbele, kila mechi waangalie, kila meseji kwenye
group wasome na wachangie n.k.

Jifunze kuchagua vitu vya kushiriki kulingana na


ratiba yako, usijilizamishe kushiriki kwenye kila kitu.

Tatu ni kutaka kujionyesha wanaweza kila jambo


Omnipotent Syndrome. Kuna watu
kinachowapotezea muda ni kutaka kujionyesha
wanaweza kila kitu, matokeo yake wanataka
wafanye kila kitu hata vile wanavyoweza kugawa
kwa wengine hawawezi kabisa kugawa kwa
wengine (delegation) au hata wakigawa unakuta
bado wanafuatilia kila sekunde inakuwa kama wao
ndio wanafanya tu.

Kumbuka Ndoto Yako Inawezekana.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 90


SIKU YA 18

Usiruhusu Maisha Yako Ya Leo


Yakuamulie Maisha Yako Ya Kesho

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 91


Kuna watu wengi sana wana uwezo mkubwa lakini
wameruhusu uwezo wao kufa na imewasababisha
kushindwa kabisa kufikia kilele cha ndoto
walizonazo. Leo jifunze vitu hivi vinavyoua ndoto za
watu wengi ili uwezo wako usije kufa kama wa watu
wengine.

Jambo la 01: Kuwa sehemu isiyoruhusu uwezo


wako kutumika.

Umeshasikia mchezaji anaamua kuhama timu


kubwa sana ambako hapewi nafasi ya kucheza
ingawa analipwa mshahara mkubwa na anahamia
timu ndogo ambayo ana uhakika wa nafasi ya
kucheza?

Kama una uwezo mkubwa sana ndani yako lakini


mahali ulipo uwezo huo hauna nafasi ya kutumika
basi uwe na uhakika kuwa utaendelea kushuka
chini kila siku. Kuna watu wengi sana walikubali
kupata mshahara mkubwa kwa kuruhusu uwezo
wao kutotumika, na matokeo yake baada ya muda
wanajikuta hawana thamani kwa sababu umuhimu

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 92


wao hauonekani tena. Kuna watu wengi sana
wanafanya kazi katika makampuni makubwa yenye
majina maarufu ila hawana nafasi kabisa ya
kuonyesha uwezo wao. Siku zote usifurahie cheo
ambacho kinakunyima fursa ya kufanya kwa
kiwango cha juu.

Mahali popote ulipo, tafuta fursa kwa nguvu zote za


kufanya kitu kitakachokuza UWEZO wako. Ukiona
uwezekano wa kupata fursa haupo kabisa, jitahidi
kutafuta MAHALI ambako uwezo wako utatumika.
Kumbuka kuwa kadiri uwezo wako unavyotumika
ndivyo unavyozidi kuwa bora na kadiri ambavyo
hutumii ndivyo unavyozidi kushuka chini.

Usifurahie kuitwa jina kubwa au cheo kikubwa bila


kupewa fursa kubwa ya kufanya. Hii ndio maana
hata kama umejiajiri ama haujapata kazi bado, kila
siku jitahidi kutafuta fursa ya kufanya kitu ili kukuza
uwezo wako.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 93


Usikubali siku ipite bila uwezo wako (kipawa,
taaluma, uzoefu n.k) kutumika.

Jambo la 02: Kufanya mambo kwa kufuata


viwango vinavyokuzunguka.

Nimeshawahi kumuuliza mtu kwa nini anachelewa


ofisini kwake na jibu alilonipa ni kuwa "zamani
nilikuwa nawahi, ila nikagundua kuwa kila mtu
anachelewa hivyo na mimi nikaanza kuchelewa".
Huu ni mfano mmoja tu, ila kuna watu wengi sana
wanajikuta viwango vyao vinaongozwa na watu
wanaokuzunguka badala ya kuongozwa na
VIWANGO VINAVYOTAKIWA ama WANAVYOWEZA
KUFANYA.

Kumbuka, ili uonekane wa tofauti katika kile


unachokifanya ni lazima ufanye kwa kiwango cha
tofauti. Usikubali kushusha viwango vya kile
unachofanya kwa sababu kila mtu anafanya
kiwango cha chini.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 94


Dunia ya leo imejaa watu waliokata tamaa, hivyo
hufanya mambo kwa uvivu na kwa viwango vya
chini kwa sababu hawana matumaini ya kufanikiwa
tena. Wewe ukifanya kwa viwango vya juu
wasivyovizoea unaonekana "mjuaji",
"kimbelembele" na "mnoko" ila hiyo ndio njia pekee
ya kujitofautisha kwa haraka.

Uwezo wako huwa unatanuka kulingana na


kiwango cha majukumu unachojipa (Potential
Elasticity). Kadiri unavyofanya kwa kiwango cha
chini kama wengine ndivyo UWEZO wako
unavyozidi KUSHUKA CHINI kama wengine.

Leo jiulize, Ni jambo gani unaweza kufanya kwa


kiwango cha tofauti na kile ulichozoea au watu
walichozea kukuona nacho? USIKUBALI UUE
UWEZO WAKO KWA KUFUATA VIWANGO VYA
WENGINE.

Jambo la 03: Kutotumia uwezo wako uliojificha.


Kila mtu ana uwezo fulani uliojificha ndani yake
(Hidden Potential) ambao kama akiugundua na

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 95


kuanza kuutumia utamletea matokeo makubwa
sana. Kuna watu wengi sana ambao wameshawahi
kununua television mpya na katika vitu
walivyopewa ni pamoja na remote control (rimoti).
Jambo kubwa ambalo unaweza kujiuliza ni kuwa
katika vitufe vyote vya rimoti, wewe huwa unatumia
vingapi?

Mara nyingi wengi hutumia kitufe cha kubadilisha


chaneli, kuongeza sauti, na pengine ku-pause
kidogo. Lakini umeshawahi kujiuliza vile vitufe
vingine vingi vilivyobakia vinafanya kazi gani?
Umeshawahi kujaribu kuvitumia?

Unachotakiwa kujua ni kwamba ulipokuwa


unauziwa televisheni yako, bei uliyouziwa ilijumlisha
pia gharama za kila kitufe katika remote control
yako. Kwa wewe kutokutumia hakuondoi uwezo wa
vitufe hivyo.

Watu wengi sana wanaishi kama remote, wana


uwezo mkubwa sana ndani yao ila hautumiki
kabisa. Ili uwezo wako utumike ni lazima uamue

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 96


kufanya vitu vipya ambavyo haujawahi kuvifanya,
ufanye mambo kwa kiwango ambacho haujawahi
kufanya hapo kabla.

Kuna watu wamekariri maisha yao na hakuna kitu


kipya wamejaribu kufanya tangu mwaka umeanza,
katika wanachokifanya hawajawahi kufanya
kiwango cha juu zaidi ya walivyozoea.

Kama wewe unafanya kitu kilekile kwa namna ileile


miaka nenda rudi basi uwe na uhakika uwezo wako
hautapanuka zaidi ya ule ulionao sasa hivi.

Kuna vitu vikubwa sana una uwezo wa kuvifanya ila


hautavijua hadi uanze kuvifanya. Kuanzia leo, ANZA
KUBONYEZA VITUFE AMBAVYO HUJAWAHI
KUVITUMIA.

Jambo la 04: Kutowekeza katika kupata maarifa


mara kwa mara

Siku moja nilikuwa nasoma makala moja iliyokuwa


inazungumzia maisha ya Lionel Messi, tangu

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 97


alipowasili katika timu ya Barcelona. Moja ya kitu
kilichonishangaza ni pale waliposema kuwa akiwa
Barcelona, kila baada ya mazoezi alikuwa anabakia
na Ronaldinho na anamfundisha kupiga free kick
wakati kila mtu akiwa ameondoka.

Kuna siku kadhaa ambako alikuwa anapiga free


kick mia moja. Hii ilimsaidia sana kwani alipoanza
kupewa nafasi ya kupiga free kick kwenye mechi za
kimashindano alianza kufunga kirahisi sana.

Swali kwako, Ni lini mara ya mwisho ulisoma kitabu


ama makala ama kuhudhuria semina ya kukusaidia
kujenga uwezo maalumu kwenye eneo lako la
kitaaluma? Huwa kila siku unatumia asilimia ngapi
ya muda wako kujijenga kimaarifa ili uwe bora
kuliko jana?

Siku zote kumbuka kuwa thamani yako


inayoonekana inatokana na uwekezaji wako
usioonekana (Your value in public is the result of
your personal investment in your ability).
Siri mojawapo kubwa ya kukuza uwezo wako ni kila

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 98


siku kuongeza maarifa na ujuzi katika eneo
maalumu uliloamua kuwa bora. Kwa mujibu wa
mtaalamu wa masuala ya kujiendeleza, Brian Tracy,
anasema kuwa maarifa unayoyajua sasa yatakuwa
yamepitwa na wakati baada ya miaka 2.5 hadi 3.

Hebu jiulize, unatumia asilimia ngapi ya kipato


chako cha mwezi kuwekeza katika maarifa ya
kukusaidia kukuza uwezo wako kwa kununua
vitabu, kuhudhuria mafunzo n.k.

Unatumia asilimia ngapi ya muda wako kupata


maarifa ya kukutofautisha? Kama matumizi yako
yamejikita kununua nguo, simu, viatu na chakula tu
bila kuwekeza katika maarifa ujue kuna siku
thamani yako itakuwa ndogo sana na watu
hawatakuwa tayari kukulipa tena.

Jambo la 05: Kutapanya nguvu zako


Siku moja mmoja wa matajiri makubwa duniani
Warren Buffet na aliyekuwa Rais wa marekani,
George Bush Sr, walikuwa kwenye mgahawa
wakihojiwa.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 99


Mwandishi akawauliza swali. Kuna sifa gani moja
wanayodhani imewafikisha hapo walipo? Cha ajabu
ni kuwa wote waligeuka na kwa wakati mmoja
wakasema "Focus".

Kwa tafsiri ya Steve Jobs, Focus maana yake ni


kusema Hapana kwa kila kitu kisichochangia katika
malengo yako ili utumie muda, fedha na nguvu zako
katika kile ulichochagua.

Kuna watu wengi wana vipaji na uwezo mkubwa


sana ila tatizo ni kuwa wanajaribu kufanya kila kitu
na wanataka kufanana na kila mtu.

Ili uwezo wako uwe wa kipekee unatakiwa uchague


eneo mojawapo katika maeneo mengi unayoweza
na amua kujikita hapo kwa nguvu zote. Mafanikio
ya kweli ni matokeo ya watu kuamini kuwa wewe ni
NGULI (guru) katika eneo fulani la ujuzi.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 100


Usiwe na mchecheto wa kutaka kufanana na kila
mtu, unataka kulima kila zao, unataka kuuza kila
bidhaa. Chagua eneo lako na jikite hapo.
Ukishajenga misuli baadaye unaweza kutanuka
kirahisi. Kuna watu tangu mwaka uanze
wameshafanya mambo kumi na hakuna hata moja
limefanikiwa kwa sababu ya kukosa focus, wako
busy ila hawana matokeo.

John Maxwell kwenye kitabu chake cha "TALENT IS


NEVER ENOUGH" anasema mtu mwenye KIPAJI
kikubwa na akili nyingi asiye na focus, atashindwa
katika mafanikio na mtu mwenye akili za wastani na
kipaji cha kawaida lakini mwenye focus.

Jitathminini kwa kina na ujue, KWENYE MAISHA


YAKO UMEAMUA KU-FOCUS KWENYE JAMBO
GANI?

Kumbuka Ndoto Yako Inawezekana.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 101


SIKU YA 19

Itafute “Ndiyo” Ya Ndoto Yako


Kwenye Kila “Hapana”
Unayokutana Nayo

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 102


Mwaka 1991 Mark Victor Hansen na Jack Canfield
walianza kuuza kitabu chao cha “The Chicken Soup
for the soul”. Ili kufanikisha mauzo yao waliamua
kumtafuta wakala mzoefu wa kuwasaidia kuuza
kitabu chao kipya, wakala huyo alikuwa anaitwa Mr.
Jeff Herman.

Baada ya makubaliano waliamua kwenda hadi New


York na kukutana na makampuni makubwa ili
kuweza kuuza kitabu chao. Walifanikiwa kukutana
na makampuni 20 na yote yaliwakatalia. Baada ya
hapo walijaribu kutuma maombi kwa njia ya barua
kwa makampuni 30 na yote yaliwakatalia pia.

Baada ya kujaribu kwa muda mrefu na kuona kama


haiwezekani, wakala wao alikata tamaa na kuamua
kuachana nao. Mark na Jack walikuwa na
matumaini na kazi hiyo na hawakuwa tayari kuiacha
ndoto yao njiani.

Waliamua kutengeneza fomu maalumu ili kila wakati


wanapokuwa kwenye semina zao na mikutano
waandikishe watu ambao watakuwa tayari kununua

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 103


kitabu chao kama kitachapishwa na wakajikuta
wamepata watu 20,000 walio tayari. Katika juhudi
za kutaka kuendeleza kuuza zaidi waliamua kutoa
stori zao 30 bure kwa majarida mbalimbali ili
kuanza kuuza jina la kitabu chao. Jack anaeleza
kuwa hadi kitabu chao kimekubaliwa basi
walikataliwa jumla ya mara 130. Kwa sasa kitabu
hichohicho kilichokataliwa mara zote hizo kimeuza
zaidi ya nakala milioni 8.

Kama kuna kitu ambacho ni lazima ukijue katika


kutimiza malengo yako na kuifuatilia ndoto yako ni
kuwa kuna nyakati ambazo utajikuta ni wewe peke
yako ndiye ambaye unaiamini ndoto yako kuliko
mtu mwingine yoyote yule.

Najaribu kujiuliza, hivi yule wakala kwa sasa yuko


wapi na anawaza nini baada ya akina Jack kuwa na
mafanikio makubwa sana na sasa ni matajiri sana.
Ndivyo inavyokuwa, kuna watu wengi sana ambao
leo wanaweza kuona kama vile ndoto yako haiwezi
kufanikiwa lakini kuna siku watajilaumu kwanini
walikuacha njiani.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 104


Ili ufanikiwe kufikia katika kilele cha ndoto yako ni
lazima uzingatie mambo yafuatayo:

Jambo la kwanza ni kuwa ni lazima ufikie sehemu


ambayo umeamua kuamini kwa 100% kuwa hakuna
hali yoyote, au kukosa imani kwa mtu yoyote juu ya
kile unachokiamini kukukatishe tamaa ya kuendelea
kufuatilia kuitimizia ndoto yako.

Ni lazima ujue kuwa mara nyingi unaweza kupitia


hali na nyakati fulani katika maisha yako ambazo
zitakuwa zinakatisha sana tamaa, na katika nyakati
hizi utaona kama vile ile nguvu ya kuamini katika
ndoto yako kunafifia, hii ni dalili kuwa uko karibu
sana na kufanikiwa usikubali kuachia njiani.

Lakini katika nyakati hizi ni wazi kuwa utapitia


wakati wa kubaki peke yako. Inawezekana kuna
watu walikuwa karibu sana na wewe wakati
unaanza kuiishi ndoto yako ama kutekeleza
mipango yako lakini baada ya muda wakakuacha
njiani; inawezekana ulipoanza kutekeleza wazo
fulani kuna watu walisema watakuwa pamoja na

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 105


wewe na watakusapoti na walishaanza, lakini
baada ya kuona muda mrefu unapita na hakuna
mabadiliko walikata tamaa na kukuacha peke yako;
tambua kuwa hili ni jambo la kawaida kwa kila
anayetaka kuiishi ndoto yake na hautakiwi
kukatishwa tamaa hata kidogo.

Jambo la pili ni lazima ujue kuwa kila unapokataliwa


mara moja, jua unakaribia kukubaliwa hatua
inayofuata (Every NO takes you closer to YES).
Kwa kila hapana unayokutana nayo inakusogeza
karibu zaidi na ndiyo iliyo mbele yako.

Ni lazima ujue kuwa utakutana mara nyingi na


kuambiwa haiwezekani, hatuko tayari, muda bado,
hili wazo halitafanikiwa n.k. Unachotakiwa kujua ni
kuwa kwa kila hatua moja ya kufeli inakusogeza
hatua moja mbele ya kufaulu kama ukiamua na
kutokukata tamaa.

Siku moja nilikuwa nasoma kitabu nikakutana na


kanuni inaitwa- “SWSWSWSW” (Some will, Some
Won’t, So What, someone is Waiting) ikimaanisha

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 106


baadhi watakubali, baadhi watakataa, ila sitajali,
kwani kuna mtu anasubiri akubali. Kama kweli
unataka kufanikiwa katika ndoto yako ni lazima
uamini katika hili na uamini kuwa kila unaposhindwa
ama kukataliwa katika hatua moja basi kuna mtu
mahali fulani anayesubiri kukubali ili kukuwezesha
kufanikiwa.

Sina uhakika umeshajaribu mara ngapi na


umeshakataliwa mara ngapi, sina uhakika kama leo
utajaribu na utakutana na vikwazo vingapi. Kitu
ambacho nina uhakika nacho ni kuwa kama
ukifanya shauri la uhakika kuwa hautakuwa tayari
kuishia njiani bila kujali wangapi wamekuacha peke
yako, ama mara ngapi utakataliwa na kukatishwa
tamaa basi ni lazima utafanikiwa.

Kumbuka Ndoto Yako Inawezekana.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 107


SIKU YA 20

Watu Unaoambatana Nao Leo


Wanajulisha Mafanikio
Yako Ya Kesho

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 108


Jeff Nelson katika kitabu chake cha “The Slight
Edge” anasema kuwa maisha yetu kifedha, kiwango
cha furaha, idadi ya fursa tunazopata n.k. ni
wastani wa maisha ya watu 6 wanaotuzunguka kila
wakati, yani watu wa karibu yetu.

Hii inamaanisha hatima yetu inategemea sana


tunaambatana na watu wa namna gani (Our
destination is determined by our association).
Maana yake ni kuwa mafanikio yetu katika maeneo
mbalimbali yanachangiwa na watu tulioamua
kuwaweka karibu katika maisha yetu ya kila siku.

Ili kuweza kufanikiwa ni lazima kujua njia mojawapo


ya kubadilisha hali yako ya sasa ni lazima pia
ubadilishe vipaumbele vyako na unaoambatana
nao: kwa kukaa nao, kusoma vitabu vyao au
unaowaangalia kwenye TV, movie au kwenye
mitandao ya kijamii.

Kumbuka wanaokuzunguka ndio wanaojulisha


wewe utakuwa unapata taarifa gani, aidha za
kukusaidia au siku nzima mnaongelea watu

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 109


wengine na mambo yasiyochangia katika kuelekea
ndoto yako. Kumbuka kabla hujabadili nafasi ama
mwelekeo wako wako, unatakiwa kwanza kubadili
watu unaoambatana nao (Before you change your
position, you will first need to change your
association).

Maisha ya watu waliofanikiwa huwa yanaongozwa


na vipaumbele vifuatavyo inapofika suala la watu
wa kuambatana nao: -

Wanakaa mbali na watu wenye mitazamo hasi


(negative people) kila wakati. Kuna watu ambao
huwa hawawezi kuona kitu chema katika maisha ya
mtu mwingine, kila wakati wanaona mabaya. Ni
watu ambao hawawezi kukutia moyo katika uwezo
ulio nao, ila wako pale kukukatisha tamaa.

Kila unapokuja na wazo jipya watakuambia hilo


haliwezekani, ama siku ukishindwa ni kama vile
walikuwa wanasubiri, watakuwa wa kwanza
kukuambia “nilijua tu utafeli, utashindwa”.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 110


Watu wa namna hii ni hatari sana kwani huvunja ile
hali ya kujiamini kwako na hukufanya uone kuwa
hautaweza tena kufanikiwa katika maisha yako.
Hebu kagua maisha yako leo, Je kuna watu ambao
uko nao karibu wenye sifa hizo?

Kama wapo, waambie wabadilike lakini


ikishindikana punguza ukaribu nao kwani maneno
yao yanaweza kukufanya ushindwe kabisa kufikia
ndoto yako.

Waliofanikiwa Wanachagua kimkakati watu wa


kuwa na urafiki nao mitandaoni Miaka mitatu
iliyopita nilifanya utafiti mdogo kuona watanzania
wengi wamependa (like) kurasa (page) gani katika
mtandao wa facebook.

Nilishangazwa sana kuona kuwa watanzania wengi


walikuwa wamelike zaidi page za udaku, pombe na
vichekesho. wachache sana walikuwa wamelike
page zenye kutoa mafunzo ya kuwasaidia kujenga
uwezo wao ama kupata ushauri wa kimaisha.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 111


Ni hatari kukuta mtu anaamka asubuhi na kitu cha
kwanza kufanya ni kuanza kuangalia skendo mpya
za siku hiyo, burudani na hata mitandao ya utupu.
Katika dunia ya leo, mitandao imekuwa ni sehemu
ya “association” yetu.

Kuanzia leo kagua makundi ya WhatsApp


uliyojiunga, Jiulize, Hivi kila kundi nililopo lina
msaada kwangu au linanipotezea muda? Hivi
ninapoamka asubuhi natakiwa kuangalia kurasa
gani za facebook au kusoma vitu vya aina gani
kujijenga kwa ajili ya mafanikio ya siku hiyo?

Kama utagundua kuna kurasa, makundi ya


WhatsApp au kuna watu una urafiki nao katika
mitandao wasio na faida, usione haya. JIONDOE
MARA MOJA. Je, unataka kuifikia ndoto yako?

ZINGATIA UNAAMBATANA NA WATU WA NAMNA


GANI, aidha kwa kukutana nao uso kwa uso ama
kupitia mitandao.

Kumbuka Ndoto Yako Inawezekana.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 112


SIKU YA 21

Jinsi Ya Kubadilisha Kukataliwa


Kuwa Fursa Ya Kutimiza Ndoto Yako

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 113


Mara nyingi kwenye maisha unahitaji kuwa tayari
kuchukua hatua moja kubwa (leap step) ambayo
inaweza kuwa ndio chanzo cha mafanikio yako na
itakufungulia mwanzo mpya katika maisha yako
kuanzia hapo.

Mike Kelley alifanikiwa kusoma kwa muda wa


mwaka mmoja tu katika shahada yake ya kwanza
na baada ya hapo alishindwa kabisa kuendelea na
masomo yake chuoni. Kwa sababu ya kukosa elimu
ya kutosha Mike alijikuta anauza bidhaa za urembo
katika kisiwa cha Hawaii nje ya hoteli ya Maui,
Hawaii.

Kwa muda mrefu akiwa anaendelea na biashara


yake alijaribu sana kupata tenda kubwakubwa toka
kwa makampuni na mahoteli mbalimbali yaliyokuwa
maeneo ya karibu lakini hakufanikiwa kwa sababu
kulikuwa tayari kuna wafanyabiashara ambao
walikuwa wamebobea na walikuwa wanawauzia
mahoteli hayo makubwa kwa miaka mingi sana.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 114


Ili aendelee kufanya biashara yake vizuri Mike
alikuwa anapenda sana kusoma majarida ya
kumjenga kibiashara na kumsaidia kujua
kinachoendelea katika eneo lake la biashara.

Siku moja katika kusomasoma aligundua kuwa


hoteli kubwa ya Maui ilikuwa imepata meneja mpya.
Hapo akaona hiyo ndiyo fursa ya kupata mkataba.

Badala ya kumsubiri meneja mpya aje aripoti


hotelini Mike alijigharamia na akasafiri kwa ndege
hadi eneo linaloitwa Colorado na akaenda
kumtafuta huyo meneja huku akiwa na maelezo,
vipeperushi na baadhi ya bidhaa anazoziuza.

Alipofika na kufanikiwa kukutana naye alimpongeza


na kisha alimweleza kuhusu biashara yake na
kumwambia angefurahi kumuona atakapokuja
kuripoti katika kazi yake mpya.

Baada ya meneja kuripoti Hawaii ni kama vile


alimsahau kabisa Mike lakini siku moja Mike
alishangaa akipigiwa simu na akafanikiwa kupewa

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 115


mkataba ambao unamwingizia mamilioni ya pesa
kila mwaka. Kwa sasa Mike anamiliki kampuni
kubwa sana yenye wafanyakazi zaidi ya 175 na
anaingiza zaidi ya dola milioni 5 kwa mwaka.

Hii ni siri mojawapo ya mafanikio katika maisha yetu


ya kila siku kama tunataka kutimiza ndoto zetu, ni
lazima uamue kuchukua hatua ambayo siyo ya
kawaida. Mike alikuwa na hofu alipofikiria kuhusu
kukutana na meneja mpya, alijiona bado ni
mfanyabiashara mdogo, alihisi pengine
angemkatalia lakini aliamua tu kwenda.

Ili ufanikiwe ni lazima uchukue hatua hata pale


unaposikia hofu (Feel the fear and do it anyway).
Kuna mambo mengi tunayofikiri hayawezekani
kumbe yanawezekana sana kama tukiamua tu
kuchukua hatua fulani isiyo ya kawaida.

Ili uweze kufanikiwa ni lazima uamini kile Dr. Myles


Munroe alichoambiwa pale alipokuwa anahofu ya
kumtumia mtu kitabu chake ili amwandikie maneno
ya utangulizi (forewords) na akawaambiwa

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 116


“Never say no to yourself before you have tried it”
akimaanisha usijiambie haiwezekani kabla
haujajaribu. Hivi ni mara ngapi umetamani kuchukua
hatua fulani katika maisha yako au ulipata wazo
kumwambia mtu fulani kitu lakini hata kabla
haujajaribu ukajiambia “hawezi kukubali,
atanikatalia”.

Hivi kuna mambo mangapi ambayo leo ungekuwa


umeshafanikiwa kama ungeamua kuchukua hatua
bila kuogopa ama bila kufikiri kwamba
ungekataliwa? Hata leo kuna vitu vingapi ambavyo
unaogopa kuchukua hatua eti kwa hofu tu
utakataliwa.

Siku moja nilikutana na mtu analalamika


ameongezewa kazi nyingi ofisini na hajaongezwa
mshahara nilipomuuliza umeongea na bosi wako
kuomba nyongeza akasema “Hapana, kwa sababu
najua hatakubali”.

Nikamwambia nenda kajaribu ukiwa umeandika


ongezeko la kazi zako na uwe na hoja za nguvu.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 117


Cha ajabu alipoenda bosi wake alishangaa sana
kuona uzito wa kazi alizonazo kwa sasa tofauti na
fikra alizokuwa nazo, akakubali siku hiyo hiyo
akaandika barua ya nyongeza ya mshahara.

Kama unafanya biashara usiogope kumfuata mtu


eti kwa hofu hatanunua, kama unataka mkopo
usihofu kuomba eti kwa hofu ya kutokupewa,
usiwaze kukataliwa kabla haujajaribu.

Watu wanaofanikiwa kutimiza ndoto zao ni wale


ambao wanajaribu jambo lilelile ambalo huwa
wanahofia halitafanikiwa. Leo, hebu jaribu
kuorodhesha ni mambo gani ambayo unaona ni
mawazo ambayo yanaweza kubadilisha maisha
yako lakini kila ukitaka kuchukua hatua unapata
hofu kuwa hautafanikiwa.

Ukishafanikiwa tafadhali amua mara moja kuchukua


hatua kama Mike. Usichoke kuendelea kujaribu kila
wakati hata kama mara ya kwanza hautafanikiwa.
Ila naomba uniahidi kuwa siku ukifanikiwa
utaniambia na mimi pia nifurahi pamoja nawe.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 118


Kumbuka Ndoto Yako Inawezekana.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 119


SIKU YA 22

Mambo 2 Ya Kuzingatia Ili


Kuharakisha Mafanikio
Ya Ndoto Yako

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 120


Kuna mambo mawili ambayo kama ukiweza
kuyazingatia kuanzia leo basi yataharakisha sana
mafanikio ya ndoto ulizonazo kwenye maisha yako.
Moja ni lile ambalo tunajifunza kutokana na maisha
ya Anthony Burgess.

Alipofikisha miaka 40 Anthony Burgess aligundulika


kuwa ana mwaka mmoja tu wa kuishi baada ya
madaktari bingwa kugundua kuwa alikuwa na
uvimbe mkubwa sana katika ubongo (brain tumor)
ambao ulikuwa unazidi kukua kila siku.

Mara baada ya kupewa taarifa hii aligundua kuwa


hana muda mrefu wa kuishi na mawazo yakaanza
kumjia kwani kwa wakati huo alikuwa amefilisika
kabisa na hana chochote kile kifedha.

Alianza kuwaza jinsi mke wake Lynne


atakavyoteseka baada ya yeye kufariki. Kabla ya
kugundulika na tatizo hili Burgess hakuwahi kuwa
mwandishi mahiri wa vitabu vya hadithi (novel)
lakini siku zote alijua kuwa ana kipaji na uwezo huo
ndani yake.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 121


Baada ya kutafakari maisha ya mke wake
yatakuwaje aliamua kutumia muda wote uliobakia
wa mwaka mmoja kabla hajafariki kuandika vitabu
ili hata baada ya kufa basi mke wake aendelee
kufaidika na mauzo ya vitabu hivyo.

Akiwa katika hatua hii hakujuakama vitabu hivyo


vitafanikiwa kuuzwa kwa wingi lakini hakuwa na
chaguo la kufanya kitu kingine.

Burgess anasema “Ilikuwa ni mwezi wa kwanza


mwaka 1960, nilipoambiwa rasmi kuwa nina mwaka
mmoja tu wa kuishi”. Kwa namna isiyo ya kawaida
ndani ya mwaka huo mmoja alifanikiwa kuandika
vitabu vitano. Cha kushangaza kilichotokea ni kuwa
hakufariki kama madaktari walivyotabiri na baada
ya hapo alifanikiwa kuandika vitabu zaidi ya 70
kabla hajafariki.

Hili ni jambo la kawaida sana kwa wengi wetu,


huwa hatufanyi kitu hadi pale hali inapoonekana
haina namna au suluhisho lingine. Hii inamanisha
kama utalitambua hilo kila siku basi unaweza

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 122


kufanikiwa kufanya mambo makubwa kila siku.
Ubongo wako una nguvu ya kipekee ambayo
inaweza kuanza kufanya kazi mara tu
utakapotambua kuwa hauna muda wa kutosha.

Watu wanaofanikiwa ni wale ambao kila wakati


wanajua kuwa muda walionao kufanya mambo ni
mchache, kwa sababu hiyo huwa wanajikuta
wanaulazimisha ubongo wao kufanya mambo
mengi ndani ya muda mfupi.

Kama asingeambiwa kuwa ana mwaka mmoja wa


kuishi basi Burgess angekufa bila ya kuandika
vitabu vyake vyote sabini. Kuna wengi wataondoka
duniani bila kutoa vipaji na uwezo walionao ndani
yao, naamini wewe hautakuwa mmoja wa hao watu.

Ili leo ichangie katika mafanikio yako ni lazima uiishi


kama vile hauna muda wa kutosha, Acha kupoteza
muda kwenye mambo yasiyochangia mafanikio
yako, acha ku-chat mambo yanayopoteza muda
wako, acha kusoma vitu vinavyojaza ubongo wako
na mambo hasi (negative).

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 123


Ili ufanikiwe ni lazima HAMU yako ya mafanikio iwe
kubwa kuliko HOFU yako ya kushindwa. Siku moja
kijana mmoja alimfuata Socrates na akataka
amwambie siri ya mafanikio, basi Socrates
akamwambia wakutane kesho yake asubuhi mtoni.

Asubuhi ilipofika Socrates alimwambia yule kijana


waingie ndani ya mto kidogo na ghafla akamchukua
na kumtumbukiza kichwa chake ndani ya maji.
Akiwa anahangaika kupata hewa Socrates
aliendelea kumshikilia kitambo kidogo kisha
akamwachia.

Baada ya hapo walipotoka nje ya maji Socrates


akamuuliza yule kijana, “Wakati nimekuingiza ndani
ya maji, ulitamani nini zaidi?” yule kijana akasema,
“hewa”. Socrates akamwambia “kama ukitamani
mafanikio kama ulivyohangaika kutafuta hewa
wakati uko ndani ya maji basi utafanikiwa, hiyo ndio
siri ya mafanikio hakuna siri nyingine ya mafanikio”

Hili ndio jambo la pili unalolihitaji baada ya kuanza


kujua kuwa una muda mchache basi lazima uwe na

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 124


shauku ya kutimiza ndoto yako kama vile
unavyokuwa na shauku ya hewa unapokuwa ndani
ya maji. Watu wengi huwa wanasema wanataka
kufanikiwa lakini ndani kabisa ya mioyo yao shauku
yao ya mafanikio bado ni ndogo ukilinganisha na
hofu yao ya kufeli.

Utajua kama shauku yako ya mafanikio ni ndogo


kama ukifeli mara moja unakata tamaa; utajua kama
shauku yako ya mafanikio ni ndogo kama kila siku
unasema utaanza kufanya ila hadi leo haujaanza;
utajua kama shauku yako ya mafanikio ni ndogo
kama maneno ya watu yanakukatisha tamaa kuiishi
ndoto yako.

Utajua kama shauku yako ya mafanikio ni ndogo


kama unaweza kuangalia tamthilia kwa lisaa limoja
kila siku lakini huwezi kusoma kitabu kwa dakika
ishirini kila siku.

Utajua kama shauku yako ya mafanikio ni ndogo


kama unaweza kununua vocha kila wiki ila hauwezi
kununua kitabu, jarida, CD ama DVD ya mafunzo

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 125


fulani. Hali kadhalika utajua kama hauna shauku ya
mafanikio kama unajifunza mambo mengi kila siku
lakini hauyafanyii kazi.

Mafanikio katika maisha huwa yanaongozwa na


kanuni. Kama ukianza leo kuishi kwa kujua kuwa
muda wako sio wa kupoteza na pia kuishi kwa
shauku ya kiwango cha juu ya mafanikio yako basi
sina shaka utafanikiwa.

Kumbuka Ndoto Yako Inawezekana.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 126


SIKU YA 23

Aina Ya Watu Wanaotimiza


Ndoto Zao Kwa Haraka

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 127


Profesa Martin Seligman ni profesa wa saikolojia
katika chuo kikuu cha Pennsylvania na inaaminika
kuwa ndiye mtu ambaye amechukua muda mwingi
sana kujifunza juu ya kitu ambacho kinamsukuma
mtu kuwa mwenye mafanikio katika maisha yake.

Baada ya kufanya utafiti wa kisaikolojia kwa muda


mrefu sana, Profesa Martin alikuja na majibu
ambayo kila mtu anayetaka kufanikiwa ni lazima
ayajue kwa faida yake.

Hitimisho la utafiti wake wa miaka mingi ulieleza


kuwa kiwango cha mafanikio baina ya watu
hutokana na tofauti ya maamuzi ya aina mbili
ambayo watu huyafanya ndani ya akili yao mara
wanapokutana na changamoto fulani katika maisha
yao.

Moja ni kundi la watu linaloamini kuwa kila


wanaposhindwa basi huwa ni matokeo ya udhaifu
walionao na hawana nguvu/ uwezo wa kuukabili na
kuushinda. Kundi la pili ni lile la watu ambalo
huamini kuwa kushindwa kokote wanakokutana

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 128


nako ni udhaifu ambao wanaweza kuufanyia kazi na
wakarekebisha na kupata matokeo mazuri baada
ya hapo.

Ili uwe mtu ambaye unafanikiwa katika maisha yako


na katika kila mpango unaoweka na kuufuatilia ni
lazima uwe mtu ambaye kila wakati unajikagua ili
kuona kuwa uko katika kundi gani kati ya haya
mawili. Kwa maneno mengine kila kundi
utakalokuwepo kati ya haya mawili yana uwezo wa
kukufanya kuwa mtu wa mafanikio ama vinginevyo.

Kundi la kwanza wao huamini kuwa sababu kubwa


ya kushindwa kwao ni kwa sababu wao ni watu
ambao hawana uwezo na hakuna namna wanaweza
kufanikiwa katika maisha yao.

Hawa ndio wale watu ambao tangu mara ya


mwisho walipofeli basi hawajaweza kuinuka tena,
kwani tafsiri yao ya kushindwa ni kuwa wao
hawafai na hawana uwezo kabisa wa kufanikiwa
tena katika maisha yao.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 129


Ukitaka kujua kama na wewe unaangukia katika
kundi hili, jiangalie kila wakati unapokuwa
umeshindwa kutimiza lengo lako ama kufanikiwa
katika jambo fulani, nini huwa kinakutokea ama
huwa unachukua hatua gani.

Kama wewe ni mtu ambaye kila unaposhindwa basi


huwa unaanza kujiona kama mtu usiyefaa ama
usiye na uwezo kabisa, hii ni dalili kuwa unaangukia
katika kundi hili.

Hebu jiulize, tangu mara ya mwisho uliposhindwa


katika jambo fulani kwa nini haujarudi tena
kujaribu? Wengi watakuambia ni kwa sababu
wanajiandaa vizuri lakini ukweli ni kuwa ndani yao
kuna hali imeshaingia ya kujikatia tamaa na kujiona
hawawezi.

Hata wewe unaposoma leo inawezekana kuna


jambo unatamani kulifanya maishani mwako ila kila
unapokumbuka jinsi ulivyoshindwa mara ya
mwisho, kuna sauti inakuambia “Wewe hili
hautaweza, waachie wengine”.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 130


Kama kweli unataka kufanikiwa basi usikubali
kabisa wakati wowote kuingia katika mtego huu.

Kampuni ya Talent Smart ilifanya majaribio kwa


watu zaidi ya milioni moja waliofanikiwa na
wakagundua kuwa asilimia 90 ya wote ni watu
ambao wana uwezo mkubwa wa kutokukubali
kuamini kuwa kufeli kunatokana na wao
kutokuweza kabisa. Kwa sababu hii watu wa namna
hii huwa tayari kila wakati kujaribu tena na tena
hadi wanafanikiwa.

Hili ndio kundi la pili; ni aina ile ya watu ambao siku


zote wanaposhindwa basi huweza kujitofautisha
kati yao na kule kuishindwa kwao. Ili ufanikiwe ni
lazima ujue kuwa kuna tofauti kubwa sana kati yako
na kushindwa kwako.

Unaposhindwa haimaanishi wewe huwezi kufanya


chochote bali inamaanisha ukiweza kutafuta
maarifa zaidi na ukafanya tena unaweza
kufanikiwa. Hii ndio maana kuna watu ambao
wanafeli mitihani lakini wakirudia baada ya

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 131


kujiandaa basi huwa wanaweza kufaulu tena.
Wakati nasoma chuo kikuu katika shahada yangu
ya kwanza nilifundishwa na mwalimu ambaye kwa
wakati huo alikuwa ana Phd lakini alishawahi kupata
division zero (daraja sirufi) akiwa kidato cha sita.

Baada ya kufeli kwa kiwango hicho aliamua


kuchukua hatua na akajisomea na akarudia mitihani
mwaka uliofuata kisha akafaulu na kuendelea na
masomo hadi alipomaliza shahada ya kwanza,
akaenda kusoma nje ya nchi na leo ni mwalimu wa
chuo kikuu.

Hivi umeshawahi kujiuliza inawezekanaje mtu


yuleyule aliyeshindwa jambo jana, leo akaweza?
Kilichobadilika sio mwili wa nje bali mtazamo wa
ndani, maarifa na tafsiri ya mambo aliyoamua kuipa.

Ndivyo ilivyo kwa kila mtu kwa maneno mengine


hakuna mshindwaji wa kudumu (there is no
permanent failure) katika maisha, kila mtu ana
nafasi sawa kufanikiwa akiamua kubadili mtazamo
wake.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 132


Hata wewe hivyo ulivyo leo, unaweza kuamua juu
ya mtazamo wako kuhusu mambo uliyowahi
kushindwa huko nyuma ama yale ambayo
yatatokea mbele ya safari.

Jambo moja ambalo siku zote nimeliamua katika


maisha yangu ni kuwa haijalishi nimeshindwa mara
ngapi katika jambo fulani, ninaamini kuna njia ya
kufanikiwa katika hilo.

Utafiti wa profesa Martin unatuonyesha kuwa kila


mmoja wetu anao uwezo wa kuhama kutoka
upande mmoja kwenda mwingine. Kabla
haujalalamika kuhusu mtaji au fursa, anza kukagua
mtazamo wako juu ya yale yaliyotokea katika
maisha yako.

Mimi naamini kuwa unao uwezo wa kufanikiwa na


kupiga hatua kama utaamua kubadili mtazamo na
tafsiri yako juu ya yale uliyowahi kuyapitia ama
unayoyapitia.

Kumbuka Ndoto Yako Inawezekana.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 133


Hata wewe hivyo ulivyo leo, unaweza kuamua juu
ya mtazamo wako kuhusu mambo uliyowahi
kushindwa huko nyuma ama yale ambayo
yatatokea mbele ya safari.

Jambo moja ambalo siku zote nimeliamua katika


maisha yangu ni kuwa haijalishi nimeshindwa mara
ngapi katika jambo fulani, ninaamini kuna njia ya
kufanikiwa katika hilo.

Utafiti wa profesa Martin unatuonyesha kuwa kila


mmoja wetu anao uwezo wa kuhama kutoka
upande mmoja kwenda mwingine. Kabla
haujalalamika kuhusu mtaji au fursa, anza kukagua
mtazamo wako juu ya yale yaliyotokea katika
maisha yako.

Mimi naamini kuwa unao uwezo wa kufanikiwa na


kupiga hatua kama utaamua kubadili mtazamo na
tafsiri yako juu ya yale uliyowahi kuyapitia ama
unayoyapitia.

Kumbuka Ndoto Yako Inawezekana.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 134


SIKU YA 24

Historia Ya Maisha Magumu


Isikuzuie Kufanikisha Ndoto Yako

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 135


Wakati mwingine ukisoma historia za watu na
ukilinganisha maisha yao ya sasa unaweza kujikuta
mwili wako wote unasisimka kwa mshangao kwani
mara nyingine inaonekana kama vile ni habari
zinazoshangaza sana.

Mwaka 2014 nilisoma habari za kijana mmoja


ambaye baba yake alimtaliki mama yake ghafla
akiwa na watoto 4, wakati huo pia mama huyo
alikuwa hana kazi ya kumpatia kipato.

Familia yao ilikuwa inaishi katika mji wa Tocopilla


(tafsiri yake ni kona ya shetani) nchini Chile na
maisha yao yalikuwa ya kimaskini sana na hivyo
ilimlazimu kijana huyu aanze kuhangaika kutafuta
pesa akiwa na umri wa miaka 6.

Kutokana na hali ngumu ambayo walikuwa nayo


kifedha ilibidi kila wakati mama yake afanye kazi ya
kuosha samaki na kufanya usafi katika nyumba za
jirani ili aweze kupata pesa za kuisaidia familia
yake. Wakati kijana huyu akiwa bado mdogo ilibidi
ajiingize katika shughuli za kucheza sarakasi,

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 136


kupigana ngumi za mtaani na kuosha magari ili
aweze kupata pesa. Baadaye aliamua kujiunga
katika uchimbaji wa madini ambako alikuwa
analipwa kiasi cha takribani Tsh 90,000 kwa mwezi.

Hata hivyo kipaji chake cha kucheza mpira wa


miguu kilianza kugundulika alipoanza kucheza
kwenye viwanja vya matope na vumbi katika mji wa
Tocopilla na kuanza kuitwa jina la ‘El Nino Marvailla”
(mtoto wa maajabu).

Leo hii amepata mafanikio kwa kucheza kombe la


dunia la mwaka 2014 kupitia nchi yake ya Chile na
sasa baadaye kwenda kucheza ligi kuu ya
Uingereza ambako alipewa mshahara wa zaidi ya
kiasi cha paundi 130,000 kwa wiki (Tsh. Milioni
370).

Kijana ninayemzungumzia anaitwa Alexis Sanchez


ambaye mwaka juzi alitoa msaada wa mamilioni ya
pesa ili kukarabati viwanja 5 katika eneo alilozaliwa
na kukulia. Sina shaka kuwa kuna watu kama
Sanchez ambao wamepitia magumu mengi sana na

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 137


wameamua kuyatumia magumu hayo kuhalalisha
kufeli kwao; wakati mwenzao aliamua kuyashinda
na kutengeneza historia mpya.

Kuna watu wametokea familia za kimaskini sana,


wamesoma kwa shida sana na wengine hata
wazazi wao waliwakataa.

Jambo la kujifunza la kwanza kutoka kwa Sanchez


ni kuwa USIRUHUSU HISTORIA YAKO YA NYUMA
IHARIBU MAISHA MAZURI YALIYOKO MBELE
YAKO. Ili ujitoe katika umaskini ni lazima uwe tayari
kushindana na fikra inayokuambia kuwa udhaifu
wako wa jana utakuzuia mafanikio yako ya kesho.

Bila kujali aina ya maisha unayoishi sasa ni magumu


ama mabaya kiasi gani, ama unajiona uko mbali
kiasi gani na ndoto yako, bado unayo fursa ya
kubadilisha maisha yako.

Kupitia maisha ya Sanchez ni wazi kuwa kila mmoja


wetu anayo nafasi ya kipekee na nafasi sawa ya
mafanikio katika maisha. Bila kujali mtu leo

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 138


anaingiza kipato gani katika kazi aliyoajiriwa ama
biashara anayofanya; kama utaamua kufanya kwa
bidii na kuwa wa tofauti na wengine wote basi
unayo nafasi ya kubadilisha maisha yako kwa
kipindi kifupi.

Wakati Sanchez anacheza mtaani hakujua kuna


watu wanapita wakitafuta watoto wenye vipaji,
alikuwa anafanya bidii na kufanya kwa ubora wote
kama sehemu yake ya maisha ya kila siku.

Ukweli ni kuwa haujui ni lini fursa yako


itakayobadilisha maisha yako itakuja, inaweza kuwa
leo ndio siku ambayo utakutanishwa na mtu
atakayekuunganisha na fursa itakayotengeneza
historia mpya katika maisha yako.

Kila ambacho unakifanya kila siku bila kujali


unalipwa kwa kiasi gani ama nani anakuangalia,
fanya kama vile kuna mtu anakufanyia tathmini ili
akupandishe cheo ama akupe mtaji zaidi wa
biashara yako. Ukiwa na mtazamo wa namna hii
kwa kila siku utajikuta unakutana na fursa kubwa

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 139


kila siku katika maisha yako. Pamoja na yote haya,
tunajifunza kuwa wakati tunapokuwa hatuna kazi/
aina ya biashara inayofanana na ndoto zetu basi
kile tulichonacho kwa wakati huo mkononi mwetu
hata kama kinadharaulika na wengine kiasi gani
ama ni kidogo kiasi gani, tukifanye kwa bidii na
uaminifu huku tukiendelea kuamini na kuifutilia
ndoto yetu kubwa.

Kuna wakati utalazimika kuishi maisha ambayo


wengine watayadharau, kuna wakati utalazimika
kupanga nyumba katika mitaa ambayo inaonekana
ni ya watu wa chini ama kuvaa nguo za kawaida
sana.

Kuna wakati utalazimika kufanya mambo


yanayoonekana hayastahili kufanywa na mtu kama
wewe ama kuna wakati utalazimika kufanya mambo
ambayo wengine watatafsiri kwamba
unajipendekeza kwa bosi kwa sababu ya bidii na
uaminifu wako.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 140


Katika haya yote kumbuka; hapo ulipo ni kipindi cha
mpito bado haujafika kituo cha mwisho, endelea
kuiamini ndoto yako. Kama vile ambavyo Sanchez
ameweza kubadilisha maisha yake nawe pia
unaweza.

Ili ufike juu kabisa na kuyafanikisha malengo yako ni


lazima uamue kutokatishwa tamaa na magumu
unayoyapitia sasa na kila siku inapoanza ujiambie
“Hata changamoto hii nitaishinda na nitafanikisha
malengo yangu”.

Kumbuka Ndoto Yako Inawezekana.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 141


SIKU YA 25

Ufanye Nini Ndoto Yako


Inapojaribiwa Na Kukataliwa

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 142


Mwaka 2011 katika gazeti la Forbes lilimtaja Tyler
Perry kama mtu anayelipwa pesa nyingi zaidi katika
sekta ya usanii na uigizaji. Mwaka 2013 alitoa kiasi
cha shilingi dola milioni 1 ili kusaidia ujenzi wa kituo
cha vijana kwa Askofu T.D Jakes nchini marekani.

Huu ni uthibitisho tosha kuwa amefanikiwa sana


kifedha. Wakati kila mtu alimsifia na kutaka kuwa
kama yeye, Perry alizungumzia historia yake
iliyomtoa kila mtu machozi.

Katika utoto wake Tyler Perry alinyanyaswa sana


kijinsia na watu waliomlea, akiwa shule ya
sekondari alifukuzwa kwa matatizo ya ada na hii
ilimpelekea apoteze mwelekeo wa maisha yake
kabisa. Katika historia ya maisha yake Perry
ameshawahi kujaribu kujiua mara mbili na mara ya
mwisho alifanya hivyo alipokuwa akiwa na miaka
22.

Baada ya kunusurika kufa, Perry aliamua kuhamia


Atlanta ambako alianza kufanya kazi za hali ya chini
na kuanza shughuli za uigizaji. Ilipofika mwaka 1992

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 143


aliandika na kuanza kuiishi ndoto yake kwa
kutengeneza igizo la kwanza “I know I have been
changed” (Najua nimebadilishwa).

Ili kufanikisha uzinduzi wake alikuwa akiweka akiba


ya fedha kwa muda mrefu sana, cha ajabu siku ya
uzinduzi walikuja watu 30 tu na aliweza kufanya
show weekend moja tu na baada ya hapo show
haikupata wateja.

Hata hivyo Perry alikuja kufanikiwa tena baada ya


miaka sita (6) kwa kuwa aliendelea kujaribu kila
wakati. Maisha ya Perry yanatuambia kuwa kila
mmoja wetu anaweza kuwa anayo historia mbaya
na ya kukatisha tamaa katika maisha yake.

Historia ambayo tukiitafakari sio tu inatukatisha


tamaa bali pia inatufanya tuone uhalali wa
kushindwa kwetu na kutokuchukua hatua katika
maisha yetu. Hata hivyo pamoja na kunyanyaswa
kijinsia na kushindwa kuendelea na shule; Perry
hakukubali kukata tamaa kuiishi ndoto yake.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 144


Kilichonishangaza zaidi katika maisha ya Perry ni
kuwa baada ya kuwa ametunza pesa zake kwa
shida sana kwa miaka mingi, alikuja kufeli vibaya
sana alipojaribu tena kuiishi ndoto yake.

Hebu fikiria, mtu amefanya kazi ngumu za kuosha


vyombo, kufagia barabara n.k kisha anatunza pesa
kwa miaka kadhaa halafu siku anayowekeza pesa
yake ili aiishi ndoto yake ya miaka mingi anajikuta
amefeli vibaya sana katika maisha yake na
amepoteza kila kitu.

Hapa kuna funzo kubwa sana; katika maisha


tunaweza kuwa na fursa ambayo tumejiandaa na
tukawa na uhakika sana kwamba kwa wakati huo
tukifanya tutafanikiwa bila shaka, lakini mambo
yasiende tulivyofikiri.

Hivi haujawahi kuapply kazi na ukafanya interview


ukawa na asilimia 100 utapata? Au haujawahi
kuahidiwa pesa na mtu unayemwamini lakini
ikatokea hajakupatia? Au hujawahi kufuatilia dili
fulani la pesa

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 145


hadi linakukosesha usingizi kwani unakuwa
umeshaanza kupanga hadi na matumizi kabla pesa
haujapata halafu mwisho wa siku unakuja kuikosa
pesa yote?

Fikiria, yaani mtu ambaye leo anapata mabilioni kwa


kuigiza, kuna siku aliandaa show wakaja watu 30
tu?

Hii ndio kama vile unaamini unaweza kucheza mpira


ukienda kwenye majaribio unaambiwa umeshindwa,
unaamini wewe ni mwimbaji mzuri ukitoa albam
hata kopi mia moja hauuzi, unaamini wewe una
ndoto za biashara lakini ulipojaribu ulifeli ukapoteza
hadi mtaji, unaamini una ndoto ya kilimo lakini
kilimo chako cha kwanza ulipata hasara kubwa.
Kumbuka Ndoto uliyonayo lazima itajaribiwa.

Katika mazingira kama haya, umkumbuke mtu kama


Tyler Perry ambaye baada ya kupoteza kila
alichokuwa nacho na kuanza kuishi maisha yasiyo
na mwelekeo tena hakuiacha ndoto yake ife,
aliendelea kuifuatilia na leo hii amefanikiwa sana.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 146


biashara umefika na dalili zote zilionyesha hivyo.
Kufumba na kufumbua alitapeliwa pesa yote na
akaanza maisha mapya kwa kuomba kuhifadhiwa
katika nyumba ambayo hata madirisha
hayajawekwa, nyumba ilikuwa nje kabisa ya jiji la
Dar es Salaam na ofisi aliyokuwa anafanyia kazi
ilikuwa katikati ya mji, hii ilimlazimu kuwa anaamka
alfajiri sana ili aweze kuwahi ofisini.

Leo ninavyozungumza amefanikiwa sana na


anasafiri kwenda nje ya nchi kikazi mara kwa mara
na amepanda hadi kuwa mkurugenzi wa kampuni
kubwa sana hapa Tanzania, hii iliwezekana baada
ya kuamini tena kuwa anaweza kuinuka na kuiishi
ndoto yake upya.

Nawe pia usikubali kuanguka kwa mara moja


kukuzuie kutimiza ndoto yako ya muda mrefu.

Kumbuka Ndoto Yako Inawezekana.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 147


SIKU YA 26

Kanuni Ya Uakisi Wa Mambo


Itakavyoharakisha Mafanikio
Ya Ndoto Yako

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 148


Watu wengi sana wanatamani kuona mambo
yanabadilika katika maisha yao, wanatamani kupata
mabadiliko katika biashara zao, wanatamani kuona
mabadiliko katika mahusiano yao na katika kila hali
inayowazunguka lakini watu haohao huwa hawataki
kabisa wenyewe kubadilika.

Katika safari yako ya mafanikio ni lazima ujue kuwa


kila mabadiliko ambayo unayatamani katika maisha
yako, siku zote huwa yanaanza na wewe
mwenyewe kubadilika.

Kuna kanuni ya mafanikio ambayo inaitwa “Law of


Correspondence” ama kanuni ya uakisi wa mambo.
Kanuni hii inasema hali yoyote ile ambayo unaiona
nje yako basi ni matokeo ya vile ambavyo uko ndani
yako.

Hivyo basi ili uweze kubadilisha hali ya nje yako


ambayo haupendi kuendelea kuiona ni lazima ujue
namna ya kubadilisha hali ya ndani yako. Kwa
maneno mengine kuanza kuhangaika na kubadilisha
maisha yako kutokea nje yako ni upotezaji wa

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 149


muda, unachotakiwa kufanya ni kuanza kwanza
kubadilisha namna ulivyo ndani yako.

Kisaikolojia inaonyesha kuwa watu wanahusiana na


sisi kutokana hasa na jinsi ambavyo tunajiona ndani
yetu na sio haswa tunavyojiweka nje yetu. Kitu cha
ajabu kuhusu mioyo ya wanadamu ni kuwa
inawasiliana kimyakimya hata bila kutoa sauti
kabisa.

Hii ndio maana kama ukiwa mtu ambaye haujiamini


basi hakuna mtu ambaye atakuamini kabisa, pia
ukiwa mtu ambaye haujithamini basi utashangaa
hakuna mtu anayekuthamini pia katika maisha yako.

Watu ambao wamefanikiwa kutoka kiwango kimoja


kwenda kingine cha mafanikio yao siku zote
wamelazimika kufanya mabadiliko katika maeneo
ya ndani mawili ya maisha yao.

Na wewe kama utaamua kufanya mabadiliko ya


namna hii basi utajikuta ghafla maisha yako
yameanza kubadilika na utaanza kupata matokeo

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 150


mazuri ya kile ambacho unakifanya. Mabadiliko ya
kwanza unayoyahitaji katika maisha yako ni
kuhusiana na mambo ambayo unayaamini. Mfumo
wako wa mambo ambayo unayaamini unachangia
kwa kiasi kikubwa mambo ambayo utayapata katika
maisha yako.

Watu waliofanikiwa huwa wanaamini mambo


ambayo wengi wasiofanikiwa huwa hawayaamini.
Nitakupa mifano michache:

Kwa mfano watu ambao huwa wanafanikiwa


huamini kuwa pesa ziko nyingi sana duniani na
zinapita katika njia maalumu na inatakiwa wajue tu
namna ya kufanya mambo ambayo yatawasaidia
wao kuingia katika njia pesa inakopita ili waweze
kuzipata pia.

Kwa upande mwingine watu wasiofanikiwa huwa


wanaamini pesa ni chache sana duniani na ziko kwa
mikono ya watu wachache ambao wataendelea
kuzishika hata wao wakifanya chochote kile
hawataweza kuzipata.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 151


Jambo lingine wanaloamini ni kuwa katika dunia
kuna watu wana uwezo maalumu ambao
wamechaguliwa na kutengwa na Mungu ili
wafanikiwe na wao wako kwenye kundi lingine la
watu ambao hawajaumbwa ili kufanikiwa kabisa.

Kuamini katika mambo kama haya, hata kama


yanaonekana ni madogo sana lakini unatakiwa
kujua kuwa yana athari kubwa sana katika
kututofautisha kuhusiana na viwango vyetu vya
mafanikio.

Ni muhimu sana kila wakati kujichunguza kuhusiana


na mambo ambayo unayaamini na jinsi ambavyo
yanakuathiri katika kuelekea safari yako ya
mafanikio.

Aina ya mambo tunayoyaamini hutokana na familia


tulizokulia, mambo tuliyopitia katika maisha yetu na
hata watu ambao huwa wanatuzunguka kila siku.
Watu wengi ambao wamekulia katika mazingira ya
kimaskini hujikuta wanaamini kuwa wameumbwa
kuwa hivyohivyo maisha yao yote.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 152


Leo hebu jichunguze na angalia ni mambo gani
unayoyaamini ambayo yamekuwa kikwazo cha
mafanikio yako. Ukishayajua, amua mara moja
kuyakabili kwa kubadilisha fikra za maisha yako.

Mabadiliko ya pili ambayo unayahitaji ni mabadiliko


ya vipaumbele vya maisha yako. Vipaumbele ni
mambo ambayo kwako umeyaweka kuwa ni ya
muhimu kuliko mambo ya kawaida.

Ukichunguza maisha ya watu waliofanikiwa na watu


ambao hawajafanikiwa, tofauti ya kwanza utaiona
katika vipaumbele vyao tangu wanapoamka hadi
wanapokwenda kulala usiku.

Unachotakiwa kujua ni kuwa, mafanikio ni


mkusanyiko wa mambo ambayo unayafanya kila
siku. Hivyo kadiri unavyoweza kufanya mambo kwa
vipaumbele vilivyo vya umuhimu na vyenye
mchango mzuri kwa maisha yako, ndivyo kadiri
utakavyoharakisha mafanikio katika maisha yako.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 153


Eneo la kwanza la kipaumbele ni matumizi ya PESA
yako. Hebu jiulize, Hivi vipaumbele vya matumizi ya
pesa yangu ni katika mambo gani?

Vipaumbele vya matumizi ya pesa ya waliofanikiwa


huwa katika mambo ambayo yanawajenga kwa
muda mrefu ama uwekezaji katika ardhi, kusoma
vitabu, semina, familia n.k lakini ukichunguza
vipaumbele vya watu ambao hawafanikiwi, utaona
wanawekeza zaidi katika nguo, vinywaji, michezo
na burudani n.k

Kwa ufupi ni kuwa vipaumbele vya watu


waliofanikiwa ni katika mambo ambayo yana
manufaa ya muda mrefu na vipaumbele vya
matumizi ya watu wasiofanikiwa ni katika mambo
ambayo yana faida ya muda mfupi, mambo
yanayolenga kuleta raha na umaarufu.

Hii ni rahisi sana kujua kama wewe uko kundi gani.


Hebu chukua pato lako la mwezi uliopita na jiulize,
hivi pesa zangu nimewekeza zaidi katika mambo
gani?

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 154


Ukiangalia kwa makini utajua tu, hautahitaji mtu wa
kukuambia kama utafanikiwa ama hutofanikiwa.

Eneo lingine la kuangalia kipaumbele chako ni


namna ambavyo unautumia MUDA wako tangu
unapoamka hadi unapoenda kulala. Watu
wanaofanikiwa hujulikana zaidi kwa kuutumia muda
wao katika mambo ambayo yana mchango mkubwa
katika kutimiza malengo yao wakati watu
wasiofanikiwa hupenda kutumia muda wao katika
kujifurahisha zaidi.

Kwa mfano watu waliofanikiwa hutumia angalau


saa moja kujisomea kitu kipya kila siku ili kuongeza
maarifa, watu ambao hawafanikiwi hutumia angalau
masaa matatu kuangalia tamthilia, movie, muziki
ama mpira wa miguu.

Kiufupi ni kuwa ukiamua kuikagua ratiba yako tangu


unapoamka hadi unaenda kulala unaweza kujijua
mwenyewe kuwa upo kwenye njia ya mafanikio
ama unaelekea kufeli.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 155


Matumizi ya muda wako ni kiashiria cha muhimu
sana kuelekea katika kilele cha mafanikio yako na ni
lazima uutumie katika namna ambayo itachangia
mafanikio yako makubwa. Watu ambao hawajali
namna ya kutumia muda wao vizuri ni watu ambao
huwa hawafiki mbali sana.

Hii ndio maana kuna watu wana muda mwingi hadi


hawajui waufanyie nini na wakati huohuo kuna watu
wana mambo mengi hadi muda hauwatoshi. Ukiona
una muda mwingi hadi haujui uufanyie nini basi ujue
kuna tatizo kubwa katika vipaumbele vyako.

Leo jikague na uangalie namna bora ya kutumia


muda wako ili ukusaidie katika kufikia malengo
yako.

Kumbuka Ndoto Yako Inawezekana.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 156


SIKU YA 27

Nguvu Iliyojificha Ndani Yako


Inayoweza Kubadilisha
Maisha Yako Kwa Haraka

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 157


Leo ningependa ukumbuke msemo ambao Ken
Levine aliwahi kusema “We all make choices, but in
the end our choices make us.” Akimaanisha kuwa
wote tunaweza kufanya maamuzi lakini mwisho wa
siku maamuzi ndiyo huamua aina ya maisha
tunayokuwa nayo.

Huu ndio ukweli wa mambo katika maisha yetu,


kwa popote tulipo sasa na chochote tulichonacho
kwa sasa ukweli ni kwamba vimetokana na
maamuzi ambayo tuliyafanya huko nyuma kwenye
maisha yetu.

Hata hivyo watu wengi sana wamekwama kwenye


maisha yao kwa kushindwa kufanya maamuzi sahihi
na kwa wakati kuhusiana na maisha yao na yale
wanayoyataka kuyapata.

Ukweli ni kuwa kudumaa kwingi ambako watu


wamekutana nako kwenye maisha yao kunatokana
haswa na tabia ya kutopenda kufanya maamuzi
katika maisha yao. Hii ndio maana Mark Twain
alisema “miaka ishirini kuanzia leo utajutia zaidi

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 158


mambo ambayo hukufanya zaidi ya yale
uliyofanya”. Kama kweli unataka kufanikiwa katika
ndoto za maisha yako basi ni lazima ufanye
maamuzi thabiti katika maisha yako kuhusiana na
mambo muhimu.

Kabla hatujaangalia ni aina gani ya maamuzi


tunayotakiwa kuyafanya kama tunataka kufanikiwa
katika maisha yetu ni muhimu kujua kuwa bila kuwa
na mwelekeo thabiti (focus) wa kitu ambacho
unataka katika maisha yako basi itakuwa ngumu
sana kwako kuweza kufanya maamuzi sahihi.

Hivyo basi jambo la kwanza kabla haujaendelea


kujifunza aina na namna ya kufanya, ni lazima
ujiulize “Hivi mimi nataka kupata nini kwenye
maisha yangu”. Kadiri unavyokuwa “clear” kwenye
mwelekeo wa maisha yako ndivyo unavyopata
urahisi zaidi wa wewe kufanya maamuzi kila wakati
inapobidi.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 159


Ili ufanikiwe utahitajika kufanya aina mbili zifuatazo
za maamuzi katika maisha yako: -

Amua kuwajibika kuhusu maisha yako.


Mafanikio huanza na kutambua kuwa kila hali
uliyonayo ni wajibu wako kuibadilisha na sio mtu
mwingine yoyote yule. Ni lazima ufike sehemu
ambayo unaamini kwa dhati kuwa “Hatima ya
maisha yako iko mikononi mwako”.

Kila wakati unapoanza kulaumu mtu, serikali, bosi


wako, wazazi, marafiki, maadui ama bahati mbaya
ulizowahi kuzipata katika maisha yako hapohapo
unapoteza nguvu ya kubadilisha maisha yako.

Haijalishi nani alikufanyia nini kibaya, yaliyopita ni


historia na kuanzia hapo ulipo unao uwezo wa
kutengeneza historia mpya. Lazima ufanye
maamuzi hayo leo na uyafanye sasa hivi. Amua
kuwasamehe wote waliokukosea katika maisha
yao, amua kuwa unazo nguvu na uwezo wa
kufanya kitu kizuri kuanzia wakati

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 160


huu, amua kuwa unaweza kabisa kuanza upya.
Fanya maamuzi ya kuwajibika na maisha yako.

Jambo lingine katika kuwajibika na maisha yako ni


kutokubali kuwa mtu ambaye kila wakati unawaza
“Hivi watu watasemaje nikifanya hivi?”

Haujaumbwa kuwaridhisha watu umeumbwa


kutimiza kusudi la maisha yako. Usiendelee kuishi
maisha ya kuumia ili mradi tu kuna watu
unawafurahisha na unaogopa eti ukichukua uamuzi
fulani watasemaje.

Kuna watu leo wapo kwenye kazi wasizozipenda


kabisa ila wanaogopa kuacha na kutafuta kazi
nyingine kwa sababu tu wanahofia watu
watasemaje, kuna watu leo wako kwenye
mahusiano ambayo wanaumia kila siku na
wanakosa ujasiri wa kusema ama kuchukua hatua,
eti wanaogopa watu watasemaje?

Usikubali kuishi maisha yako yote kwa kuumia eti ili


mradi tu unawaridhisha watu wengine. Maisha yako

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 161


ni yako mwenyewe. Usiishi maisha ya kutafuta
“hadhi” ishi maisha ya kutimiza “NDOTO”. Don’t live
to GAIN a STATUS but live to FULFILL your DREAM.

Amua kufanikiwa katika malengo makubwa sana.


Napenda msemo ambao Les Brown aliwahi kusema

- “Shoot the Moon because even when you fail, you


will land on the stars” (Lenga Mwezi kwani hata
ukikosa kuupata utaangukia katika nyota).

Kama kweli unataka kupata mafanikio ni lazima uwe


na malengo makubwa sana katika maisha yako.
Malengo madogo hupelekea mafanikio
madogomadogo sana ambayo huwa hayawafikishi
watu mbali.

Kila wakati ninapofundisha kuhusu malengo huwa


nawaambia watu waweke kitu kinaitwa
“Breakthrough goal”. Lengo kubwa moja ambalo
ukifanikiwa kulipata basi litakupa hadhi mpya katika
maisha na utakuwa umefanikiwa kwa kiwango
kikubwa sana.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 162


Hili ni lengo ambalo siku likitokea basi kila mtu
atajua umefanikiwa ikiwemo na wewe mwenyewe
pia.

Hebu fikiria sasa unataka kufanikiwa katika ndoto


gani kubwa kwenye maisha yako? Kuna mwingine
atataka kushinda medali katika michezo ya olimpiki,
mwingine kujenga nyumba, mwingine itakuwa
kuandika kitabu na kuuza kopi elfu kumi, mwingine
kurekodi albam yake n.k.

Kila mmoja anayefanikiwa ni lazima huwa anaweka


lengo la namna hii. Ukifanikiwa katika malengo ya
namna hii yatakupa ujasiri wa kuweka malengo
mengine makubwa zaidi.

Najua unajiuliza mbona nikiweka malengo makubwa


nitafeli. Kumbuka kile alichosema Bill Cosby "In
order to succeed, your desire for success should
be greater than your fear of failure." Ili ufanikiwe ni
lazima shauku yako ya kufanikiwa iwe kubwa kuliko
hofu yako ya kushindwa.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 163


Usihangaike na hofu ya kushindwa, jenga hamu
yako kubwa ya kufaulu katika jambo unalotaka.
Uwe kama mtu ambaye hajui kuogelea aliyetupwa
kwenye maji.

Hivi kama ndio wewe haujui kuogelea ukitupwa


kwenye maji, utasema ngoja tu nife kwa sababu
sijui kuogelea? Bila shaka hapana. Utajitahidi kadiri
unavyoweza kujiokoa. Ndivyo ilivyo, unapojiwekea
ndoto kubwa unajikuta unafanya bidii kuyafikia kwa
kila namna.

Hivyo baada ya kuamua ndoto kubwa ulilonalo


katika maisha yako, hebu jiulize, “Hivi kuna vitu
gani/ mambo gani natakiwa kuyaacha ili kuweza
kutimiza lengo ninalotaka kulifikia?” Kama
ulivyotumia muda kuweka “breakthrough goal”.
Tumia muda pia kuandika mambo gani unatakiwa
kuyaacha ili kuweza kutimizandoto yako.

Ni vyema kujua kuwa maamuzi unayofanya kuhusu


maisha yako ndio kitu pekee kinachoweza
kubadilisha maisha yako. Kama unayachukia

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 164


maisha yako ya leo, jua kuwa yalitokana na
maamuzi yako ya jana, hivyo ili uweze kuishi
maisha ya tofauti kesho ni lazima ufanye maamuzi
ya tofauti leo.

Sina shaka kuwa utafanikiwa katika ndoto yako


kama utayafanyia kazi haya unayojifunza kwa
vitendo na bila kuchoka.

Kumbuka Ndoto Yako Inawezekana.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 165


SIKU YA 28

Hatua Muhimu Unazotakiwa


Kuzipitia Kabla Haujafanikisha
Ndoto Yako

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 166


Muda pekee ambao unaweza kuepuka vikwazo
katika maisha yako ni pale ambapo unakuwa
haufanyi kitu chochote kile cha maana.

Ukiona wakati wowote ule unakabiliwa na


changamoto na vikwazo, ni ishara tosha kuwa uko
katika kupiga hatua kuelekea mbele. Hakuna mtu
ambaye amewahi kufanikiwa bila kukabiliana na
vikwazo vya aina fulani akiwa njiani kuelekea
kuitimiza ndoto yake.

Na ili ujihakikishie kuwa utafika katika kilele cha


mafanikio ni lazima uhakikishe kuwa kila wakati uko
katika mwendo wa kusonga mbele bila kukata
tamaa.

Hii ndio maana Mwanaharakati wa haki za watu


weusi wa marekani, Martin Luther King Jr aliwahi
kusema kuwa “kama huwezi kuruka basi kimbia,
kama hauwezi kukimbia basi tembea, kama
hauwezi kutembea basi tambaa, ila kwa namna
yoyote ile fanya kila unachoweza kuelekea katika
kuitimiza ndoto yako”.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 167


Wakati nafanya utafiti wangu binafsi juu ya maisha
ya watu waliofanikiwa katika yale ambayo
wamekuwa wanayafanya, niligundua kuwa kuna
nyakati za aina tatu ambazo kila mmoja wao aliwahi
kuzipitia.

Na kwa sababu waliweza kuzishinda basi kila


mmoja wao aliibuka kuwa mshindi na kufika kileleni.
Moja ni hali ya kusikia maumivu makali ndani yao
wakiwa wameanza kufuatilia na kuishi lile jambo
ambalo wanalitamani katika maisha yao.

Jambo hili lilielezwa vizuri na kwa ufasaha zaidi na


mwanariadha maarufu wa nchini Czech, Emil
Zatopek (Alishinda medali tatu za dhahabu katika
mashindano ya olimpiki yaliyofanyika Helsinki,
Finland) ambaye alisema kuwa
kinachowatofautisha vijana na watu wazima ni
namna wanavyoweza kukabiliana na maumivu na
mateso wanayoyapata pale wanapokuwa
wameanza safari ya kuelekea katika mafanikio yao.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 168


Katika kuifuatilia ndoto yako na kutimiza malengo
yako, utakutana na nyakati za maumivu nyingi sana
ambazo kwa kweli zitakuwa zinakufanya ukose
nguvu ya kuamka tena na kuchukua hatua nyingine
mbele. Nikiwa shule ya msingi niliwahi wakati fulani
kushiriki mbio za mita 200.

Wakati bado sijashiriki nilikuwa naona kama ni kitu


kirahisi sana na naweza kukifanya bila tatizo lolote.
Hata hivyo nilipoanza kukimbia, nilianza kwa
mbwembwe na nikatoka spidi kali bila kujua kuwa
suala la mbio lina timing zake.

Nikiwa mita kama hamsini kumaliza nilishangaa


kuona kila mtu ananipita kama nimesimama vile, na
kila nikijaribu kuongeza kasi naona kama niko
palepale, huku misuli ikiuma na nikihisi kama harufu
ya damu kifuani.

Nyakati kama hizi huwa zinawatokea watu wengi


sana. Unaweza kukuta mtu ameanza kufanya
jambo kwa kasi kubwa sana, lakini ghafla
anakutana na changamoto zinazomfanya apunguze

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 169


kabisa kasi ya yale aliyokuwa anayafanya.
Unashangaa tu, huoni mtu tena akiendeleza kasi ya
kufuatilia ndoto yake. Watu waliofanikiwa huwa
wanakiona kipindi hiki kama ndicho muhimu cha
kuthibitisha kuwa ndoto yao ni ya uhalisia.

Usikubali maumivu yakufanye uache kufuatilia


ndoto yako. Kuna msemo wa kiingereza maarufu
unasema “Feel the pain, and do it any way”. Hisi
maumivu lakini endelea tu kufanya ulichokusudia.
Kumbuka siku zote kuwa maumivu ndio gharama
unayoilipa ili kufanikiwa katika yale unayoyatafuta
kwenye maisha yako.

Wakati wa pili ni ule ambao mtu anaona kama ni


bora akate tamaa kuliko kuendelea. Kama
umeshawahi kuangalia mchezo wa ngumi,
utagundua kuwa kuna wakati bondia anaweza
kupigwa ngumi akaanguka chini, na refa akianza
kumuhesabia ukimwangalia bondia machoni utaona
ni kama vile anajiuliza niendelee ama nisiendelee.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 170


Kila aliyefanikiwa, lazima amepitia katika hali hii,
ambapo huwa anafika kiwango anajiuliza swali la
kuendelea ama asiendelee.

Katika kufuatilia mafanikio yako na kutimiza


malengo ya maisha yako, ni lazima siku moja
utajikuta umepitia katika hali kama hii ambayo
itakufikisha katika tafakari ya kuendelea ama
kuishia njiani.

Watu waliofanikiwa, huuita wakati huu kama


“Destiny Deciding Moment” - wakati ambao
huamua hatima yako. Inawezekana na wewe uko
kwenye wakati huu leo, na umefika hatua unaona
kama vile hauna nguvu za kuendelea hatua moja
mbele. Ningependa nikukumbushe kuwa ukiweza
kuvumilia na kushinda wakati kama huu basi ujue
una uwezekano mkubwa sana wa kufanikiwa
kufikia kilele cha ndoto yako.

Jambo la muhimu la kukumbuka ni kuwa, kushinda


ni utamaduni ambao huwa unatengenezwa kama
ambavyo kushindwa kulivyo. Ukijizoeza kuwa mtu

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 171


ambaye kila changamoto kidogo basi unajikuta
umeshakata tamaa na unaacha kuendelea basi kila
wakati utakuwa mtu wa kuanza upya kwa kukimbia
changamoto.

Hebu jiwekee malengo leo ya kuwa utaendelea


“kukomaa” hadi mwisho ili upate matokeo
unayotaka. Kama njia moja haijafanya kazi basi
jaribu njia nyingine, hadi umepata unachotaka.
Usikubali kuishia njiani.

Wakati wa tatu ni ule ambao utapoteza marafiki


kwenye maisha yako, na wengi wao watakuwa ni
wale ambao ulikuwa unawachukulia kama watu
muhimu sana kwenye maisha yako. Kwenye safari
ya mafanikio ni lazima ujue kuwa kila hatua itakuwa
na mtandao mpya na itakuondolewa baadhi ya
watu katika mtandao wako.

Kuna watu ambao wakiendelea kuwa sehemu ya


maisha yako ya kila siku watakufanya uchelewe
kufika unakoenda.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 172


Watu wengi wana mawazo madogo sana katika
maisha yao na mara utakapoanza kuwaza mawazo
makubwa watashindwa kabisa kuendana na wewe
(They will fail to contain your big ideas).

Hili ni jambo la kawaida na kila ambaye


amefanikiwa katika maisha yake amelipitia.
Usishangae kuona aina fulani ya watu wameanza
kuwa mbali na wewe na kila ukitafuta sababu
huipati. Siku zote kumbuka kila kiwango kipya cha
maisha yako kitatengeneza watu wapya na
kitapunguza wale wa zamani.

Utaumia sana kuwapoteza baadhi ya marafiki, lakini


kama vile ambavyo kila mmoja wetu angependa
kuendelea kuishi na wazazi wake hata baada ya
kuingia kwenye ndoa na ili uwe mtu mzima mwenye
familia lazima uwaache wazazi wako. Kuwaacha
wazazi haimaanishi hauwapendi ila ni kuonyesha
kuwa uko kwenye hatua nyingine ya maisha yako.

Vivyo hivyo kuna watu utawaacha kwenye maisha


yako sio kwa sababu hauwapendi, bali kwa sababu

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 173


kiwango cha juu ulichoenda wao wameshindwa
kubadilisha kiwango chao pia.

Kumbuka Ndoto Yako Inawezekana.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 174


SIKU YA 29

Zingatia Kanuni Hizi 2 Za Pesa Ili


Ndoto Yako Isiishie Njiani

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 175


Kati ya maeneo muhimu sana katika maisha yako
ambayo unatakiwa kuyawekea uzito na kipaumbele
katika safari yako ya kimafanikio, ni eneo la kifedha.
Watu wengi wana nia na mipango mizuri ambayo
imekwama na kushindwa kutekelezeka kwa sababu
tu hawana pesa za kutosha kufanya wanachotaka.

Hata hivyo kwa upande mwingine kuna watu


ambao kwa nje ukiwaangalia utaona wana kipato
kikubwa, wana kazi nzuri, wana mshahara mzuri.
Lakini ukweli ni kuwa hali yao ya kifedha ni ya
kukimbizana kutoka mshahara hadi mshahara.

Kwa maneno mengine, ikitokea bahati mbaya


wakapoteza kazi yao wanayofanya kwa miezi
mitatu tu, hawataweza kuishi kwa amani kwani
hawana akiba wala vitega uchumi vya kuwapatia
kipato cha ziada.

Mafanikio ya kifedha ni matokeo ya kufanya


maamuzi thabiti lakini pia ni matokeo ya kuamua
kuishi maisha ya nidhamu ya pesa ambayo watu
wengi wameshindwa. Hivi umewahi kujiuliuza kwa

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 176


nini hali yako ya kifedha, iko hivyo kwa sasa? Na je
una mpango wowote wa kubadilisha hali yako ya
sasa, ama wewe ni aina ile ya watu ambao
hutegemea bahati itatokea na kisha watafanikiwa?

Kuna watu ambao walishawahi kupata pesa nyingi


sana lakini leo ni maskini, kuna wengine
walishawahi kufanikiwa sana kibiashara lakini leo
wamefilisika. Mafanikio ya kifedha yana kanuni
ambazo ni lazima uzizingatie ili uweze kukua na
kufanikiwa. Leo ningependa tuzingatie kanuni nne
ambazo unatakiwa kuzizingatia katika kujenga
uwezo wako wa kufanikiwa kifedha.

Kanuni ya kwanza ni kuwa na bajeti. Kanuni hii


inalenga kukufanya ujiulize swali la msingi
linalosema “Pesa yangu huwa inakwenda wapi?”
Watu wengi sana wanapata pesa ila hawawezi
kabisa kueleza huwa zinatumika kwa matumizi gani.

Hii ndio maana ukianza kutafakari pesa ambazo


zimepita mkononi mwako tangu mwaka huu uanze
na ukiangalia mambo uliyofanya utashangaa sana.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 177


Kama wewe ni mfanyakazi uliyeajiriwa hebu jiulize,
tangu umeanza ajira jumla umepokea mshahara wa
shilingi ngapi? Ukishapata jibu lake, hebu angalia
mambo uliyofanya hadi sasa kwa kulinganisha na
pesa zilizopita mkononi mwako.

Mafanikio ya kifedha sio matokeo ya kiwango cha


pesa unayopata, bali ni matokeo ya kiwango cha
pesa unachoweza kukibakiza mkononi mwako na
jinsi utakavyoweza kukizalisha katika maisha yako.

Kila mwezi hakikisha una bajeti ya matumizi yako


ambayo unakusudia kuyatumia katika maeneo
mbalimbali. Kwa kufanya hivyo utajijengea nidhamu
ya kutotumia pesa kwa mambo ambayo sio ya
muhimu.

Uzuri ni kwamba hauhitaji kuwa mtaalamu ili


kutengeneza bajeti, unachotakiwa kufanya ni
kuorodhesha mahitaji yako na kuweka kiwango cha
pesa unazotarajia kutumia.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 178


Kisha unaweka vipaumbele katika maeneo ambayo
unaona ni muhimu zaidi kwanza kabla ya mengine
katika kutumia pesa yako.

Ukianza kuwa makini na kufuatilia pesa zako


zinaenda wapi, utagundua kuwa kuna pesa nyingi
sana ambazo unazipoteza bila wewe mwenyewe
kujua kwa kununua ama kutumia katika vitu visivyo
vya lazima.

Kujiwekea bajeti ni pamoja na kuweka kiwango


kidogo cha pesa ambacho utakuwa unakiweka
kama akiba katika maisha yako kila wakati
unapopata pesa.

Watu wengi ukiwaambia waweke akiba huwa


wanakimbilia kusema kuwa hawana kipato cha
kutosha, lakini watu wanaofanikiwa kifedha huwa
wanaanza kuweka akiba kwa kiwango kidogo kisha
wanaendelea kuongeza kadiri kipato chao
kinavyokuwa.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 179


Akiba hii ndio baadaye huitumia kuwekeza ama
kununua vitu vitakavyowaingizia pesa zaidi katika
maisha yao.

Leo, ningependa upate muda na kisha uandike


kipato chako na matumizi yako ya mwezi kwa
ufasaha. Hii itakupa picha kwa mwezi unatumia
kiasi gani na utafanyia kitu gani.

Swali la muhimu hapa ni kuwa, “pesa yangu huwa


inakwenda wapi”? Huwezi kufanikiwa kifedha kama
haujui kabisa pesa yako hutumika kwa mambo gani.

Kanuni ya pili ni ile ambayo ilitungwa na mwandishi


nguli wa Uingereza, Bwana Cyril Northcote
Parkinson ambayo ilipewa jina lake na kuitwa
“Kanuni ya Parkinson”. Kanuni hii husema kuwa
“katika hali ya kawaida mwanadamu anapoona
kipato chake kimeongezeka basi na yeye huongeza
matumizi ili yafikie kumaliza ongezeko la kipato
kipya alichokipata.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 180


Kwa sababu hiyo, hata kama mtu ataongezewa
kipato mara kumi, utashangaa bado anaishi kwa
shida kama vile kipato hakijaongezeka. Ili ufanikiwe
kifedha ni lazima ufanye juhudi za makusudi
kuikiuka kanuni hii.

Unatakiwa ufanye maamuzi katika maisha yako


kuwa hautabadilisha kwa haraka aina ya maisha
unayoyaishi ili ongezeko la kipato ulilolipata liwe na
faida kwako.

Watu wengi wakiongeza kipato/mshahara/faida,


basi haraka sana anabadilisha nguo anazovaa,
anabadilisha gari, hata nyumba ghafla anaenda
kuchukua ya bei ghali sana, ili mradi tu anataka
kuwathibitishia watu kuwa kipato chake
kimeongezeka.

Kama kweli unataka kufanikiwa kifedha ni lazima


uhakikishe kuwa mabadiliko ya maisha yako
hayaendi kwa kasi zaidi ya kipato chako. Hii ni
kusema kuwa kwa kila ongezeko ambalo unalipata
kifedha hakikisha kuwa haubadilishi staili yako ya

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 181


maisha itakayosababisha utumie chote
kilichoongezeka badala yake tumia kile
kinachoongezeka kuwekeza zaidi.

Watu ambao kanuni hii imewaathiri katika maisha


yao ndio wale ambao kila wakati wanalazimika
kuishi juu zaidi ya kipato chao. Ni rahisi sana kujua
kama unaishi juu ya kipato chako kwa kuangalia
aina ya madeni na mikopo uliyonayo.

Kama wewe una madeni na mikopo ambayo yote


imelenga kutatua shida za kila siku au kwa ajili ya
fasheni basi ujue kuna tatizo katika mfumo wako
wa matumizi.

Hapa nazungumzia kama wewe huwa kila wakati


unakopa kwa ajili ya kununua nguo, kulipa kodi ya
nyumba, kununua gari ya kutembelea, kununua
simu ya kisasa, viatu n.k basi ujue kuna tatizo katika
mfumo wako wa kifedha na unahitaji kubalika
haraka kabla umaskini wa kipato haujakuvamia.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 182


Leo ningependa ufanye tathmini ya mikopo na
madeni uliyonayo yametokana na mambo gani.
Kama ukigundua madeni na mikopo yako mingi ni
ya aina ya kuleta umaskini kama nilivyoeleza hapo
juu basi mara moja amua kubadilisha mwelekeo.

Kwanza amua kutojiingiza tena katika matumizi ya


namna hii na pili weka mkakati kabambe wa kuanza
kuyalipa bila kuchelewa. Ushauri wangu kwako ni
kuwa siku zote, tumia mkopo kwa ajili ya shughuli
ya kibisahara, uwekezaji ama kuzalisha zaidi na sio
kununua vitu visivyozalisha.

Usikubali kuishi kwa furaha iliyo "FEKI", Hakuna


faida yoyote katika maisha kama kwa nje kila mtu
anaona uko sawa lakini wewe ndani yako unajua
mambo hayako sawa na huyafurahii maisha kama
wengi wanavyokufikiria.

Kanuni ya "Locus of Control" inasema kadiri


ambavyo unaona kuna jambo liko juu ya uwezo
wako na hauwezi kulitatua ndivyo ambavyo utazidi
kujiona hauna thamani na utaendelea kukata tamaa.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 183


Usikubali kuendelea kutatizwa na jambo ambalo
ukweli unaweza kupata msaada. Kuna mambo
mengi unayofikiria hayana majibu lakini ukweli ni
kuwa yana majibu yake kama ukiamua kutafuta
msaada.

Usihitimishe kuwa hapo ulipofika ndio mwisho,


bado kuna njia, bado kuna matumaini, bado kuna
majibu mahali.

Kumbuka Ndoto Yako Inawezekana.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 184


SIKU YA 30

Majaribu 3 Ya Kuyashinda Ili


Ndoto Yako Ifanikiwe

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 185


Kila lengo ulilonalo maishani mwako lazima litapitia
wakati wa changamoto na kujaribiwa ambako
kutasababisha uanze kuona kama vile kile ambacho
unakiamini ama unataka kukifanya hakitaweza
kufanikiwa tena.

Kila mtu ambaye unamuona amefanikiwa sana


katika maisha yake na pengine unatamani kuwa
kama yeye, ukijaribu kuzungumza naye atakuambia
mambo ambayo ameyapitia na kuyashinda katika
maisha yake kabla hajafikia hapo alipo leo.

Kwa maneno mengine kama kweli unatamani kuwa


kama mtu fulani, ni muhimu sana pia kutafuta kujua
changamoto ambazo wamezipitia na kujua namna
walivyozitatua.

Kwa lugha nyepesi ningesema namna nzuri ya


kutamani kufanikiwa kama wengine ni kuanza na
kutamani kujua changamoto walizozipitia na namna
walivyozitatua.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 186


Pia unatakiwa kukumbuka, mara nyingi watu huwa
hawapendi kuonyesha wakati wanapopitia
changamoto ila wanapenda kuonyesha mafanikio
hadharani.

Na kwa sababu hii, watu wengi sana wamejikuta


kuwa hawajui kabisa changamoto ambazo wengine
wamezipitia na kudhani kuwa yale ambayo wengine
wamefanikiwa ni mambo yaliyopatikana bila kuwa
na changamoto zozote.

Katika kufuatilia safari za mafanikio za watu wengi,


nimegundua kuwa kuna majaribu matatu ambayo
lazima yataijaribu ndoto yako. Na kila ambaye leo
unamuona amefanikiwa ni lazima atakuwa amewahi
kupitia katika hali hizi na akafanikiwa kuzishinda
pia.

La kwanza ni jaribu la muda (Test of time): Hii


inamaanisha kuwa ndoto yako inaweza isitokee
kwa kasi ya haraka kama vile ambavyo ulikuwa
umepanga na umefikiria. Watu wengi wanapoanza
kufanyia kazi wazo fulani huwa wanakuwa na

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 187


matumaini ya kufanikiwa kwa haraka sana kwa
sababu kuna watu walisikia walifanya na
wakafanikiwa, kitu ambacho watu wengi waliofikia
hatua za juu huwa hawaweki wazi kwa urahisi ni ile
miaka waliyowekeza na nguvu walizotumia kwa
muda mrefu.

Kuna watu ambao nimeshakutana nao ambao


walianza biashara kwa matumaini makubwa lakini
baada ya muda wanagundua kuwa kile
walichokuwa wanakitarajia hakiji haraka kama
walivyokuwa wanafikiria.

Changamoto ya muda inamaanisha unatakiwa uwe


tayari kusubiri hadi pale kitu unachotaka
kitakapotokea. Kuna mambo kwenye maisha ni
kama ujauzito, bila kujali unaharaka kiasi gani ya
kupata mtoto ni lazima usubiri kwa miezi tisa kabla
hajampata.

Ili ufanikiwe ni lazima ufanye maamuzi thabiti kuwa


bila kujali unachokitaka kinachukua muda mrefu
kiasi gani, bado utaendelea kukifuatilia na kukifanya

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 188


kwa bidii kwa sababu ni jambo linalogusa moyo
wako sana. Uwezo wako katika kufuatilia jambo
ambalo unaliamini sana katika maisha yako bila
kukata tamaa pale linapochukua muda mrefu zaidi
na ulivyotarajia ni sifa mojawapo muhimu sana ya
watu ambao wanafanikiwa.

Hebu jaribu kufikiria mtu kama Nelson Mandela


ambaye alikuwa tayari kusubiria ndoto yake kwa
miaka 27 na baada ya hapo ikaja kutokea. Usiwe
mwepesi wa kukata tamaa, pale ambapo jambo
limechelewa kidogo kuliko ulivyotarajia.

Kumbuka kuwa katika maisha kuna mambo


yatachukua muda mfupi na kuna mambo mengine
yatachukua muda mrefu sana hadi yamekamilika.

La pili ni jaribu la kuachwa peke yako (Isolation):


Huu ni ule wakati ambao ghafla unajikuta umebaki
peke yako na wale wote ambao ulikuwa
unawahesabu kuwa ni watu wako wa karibu zaidi
hakuna mahali pa kuwaona kabisa.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 189


Yoyote aliyewahi kufikia kiwango cha juu cha
mafanikio lazima atakusimulia wakati ambao
alikuwa hakuna mtu wa karibu wa kumsaidia
kumvusha.

Huu ndio ule wakati ambao unampigia rafiki yako


wa karibu simu na hapokei, unamtafuta kwenye
WhatsApp na unaona kabisa ikiionyesha kuwa
amesoma lakini hakujibu kabisa.

Huu ndio ule wakati ambao kuna watu ambao


uliwasaidia na unategemea wangekuwa msada
kwako lakini cha kushangaza hawakusaidii kabisa.
Ili ufikie kilele cha mafanikio yako lazima utambue
kuwa, wakati huu utafika na ni lazima uwe tayari
kuukabili.

Kuna mtu utakuta wakati fulani ulikuwa na marafiki


wengi sana lakini ghafla mambo yalipoenda kombo
umebakia peke yako. Hiki ndicho kipindi unajikuta
unajifungia ndani peke yako, umekuwa mpweke na
unaanza kama kuona dunia haikutaki kabisa.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 190


Ili ufikie kilele cha ndoto yako ni lazima ujifunze
kuukabili wakati huu na kuushinda kabisa. Kama leo
uko kwenye kipindi hiki basi kumbuka kuwa ni
sehemu muhimu ya kuipitia kabla haujafanikiwa
katika maisha yako.

La tatu ni kuishiwa nguvu za kuendelea (Moment of


Fatigue): Kuna wakati unaweza kujikuta ile hamasa
yote ambayo ulikuwa nayo mwanzoni katika
kufuatilia ndoto yako imepotea ghafla. Unajikuta
hupendi tena hata kuongelea kile ambacho ulikuwa
unakifanya mbele ya wengine.

Kati ya siku unapoanza kuamini na kufuatilia


malengo yako hadi siku utakayofanikiwa, utakutana
na kipindi ambacho nguvu zitakuwa zimekuishia na
utakuwa hautamani kabisa kuendelea mbele.

Hapa nazungumzia kile kipindi ambacho ukiamka


asubuhi wazo linakujia la kukuambia ni bora
uachane na hiki kitu. Huu ndio ule wakati kila mtu
anakuambia, usiendelee kupoteza muda tafuta kitu
kingine ufanye.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 191


Katika kitabu changu cha TIMIZA MALENGO YAKO,
nimeeleza namna watu waliofanikiwa jinsi
walivyoweza kupitia hali kama hii na wakafanikiwa
katika sura inayoeleza sifa na tabia za watu
wanaofanikiwa, kama unapitia hali hii nakushauri
ukitafute na ukisome.

Ni lazima siku zote ukumbuke kuwa mafanikio yako


sio matokeo ya msukumo wa mambo yanayotokea
nje yako bali ni yale mambo yanayotokea ndani
yako. Nguvu ya kuendelea mbele lazima ianzie
ndani yako.

Kuna wakati hautajisikia kabisa kuendelea kusogea


hatua moja, lakini kama kweli unataka kufanikiwa ni
lazima ujifunze kufanya si kwa sababu unajisikia
kufanya bali kwa sababu unajua umuhimu wake.

Nakumbuka siku moja nilisoma habari ya


mfanyabiashara mmoja wa marekani Thom
Packets, ambaye alikuwa amefanikiwa sana. Hata
hivyo siku moja kuna mtu alikutwa amekufa ofisini
kwake na hii ilimuingiza matatizoni hadi akafilisika.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 192


Siku moja akiwa amekunywa vidonge 35 ili ajiue
akaota ndoto na sauti ikamwambia “Bado kuna
matumaini, usikate tamaa”. Alipoamka na kujikuta
yuko hai bado, akaamua kutokata tamaa tena
katika maisha yake.

Na alianza kuishi kwa kuifuatilia ndoto yake na


mwishowe aliweza kufanikiwa tena.
Bila kujali kuwa leo unapitia jaribu gani kati ya haya
matatu, kitu kikubwa cha kukumbuka ni kuwa ili
kufanikiwa ni lazima uyashinde na uvuke upande
wa pili.

Kumbuka Ndoto Yako Inawezekana.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 193


HITIMISHO

Mtu wa kwanza mwenye wajibu wa kuhakikisha


kuwa ndoto yako inatimia ni wewe mwenyewe. Kwa
sababu yoyote ile usikubali kuingia kwenye kundi la
watu ambao watashindwa kutimiza ndoto za
maisha yao.

Kitabu hiki kimekupa mbinu mbalimbali unazoweza


kuzitumia ili kukamilisha ndoto ambayo unayo
kwenye maisha yako, hata hivyo mbinu hizi
haziwezi kuleta matokeo bila kuanza kuzifanyia
kazi. Ili ufanikiwe kwa haraka kufika unakoenda,
kuna mambo yafuatayo unatakiwa kuanza
kuyafanyia kazi:

• Kuweka mpango thabiti wa hatua ambazo


utazichukua mara baada ya kumaliza kitabu hiki
• Kuamua kwa ufasaha ndoto ambazo umezifuatilia
na umekusudia kuzitimiza mwaka huu
• Tafuta mtu wako wa karibu unayemwamini na
uongee naye makusudio yako ya kuhakikisha

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 194


unaanza kuishi ndoto yako na umuelezee hatua
ulizokusudia kuchukua.

Nakutakia mafanikio unapoelekea kutimiza ndoto


yako.

Kumbuka Ndoto Yako Inawezekana.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 195


KUHUSU MWANDISHI

Joel Arthur Nanauka,


Joel Amepata elimu yake rasmi kwenye chuo kikuu
cha Dar es Salaam katika masomo ya Biashara na
Uongozi, Commerce and Management) na pia
katika Diplomasia ya Uchumi (Economic
Diplomacy)
Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 196
Kutoka katika chuo cha Diplomasia (Centre for
Foreign Relations - CFR).

Joel amejikita kuwasaidia watu kuwa na matokeo


makubwa katika wanachokifanya (peak
performance trainings) na kushinda vikwazo
ambavyo vimeathiri watu wengi.

Anatoa mafunzo kwa makampuni mbalimbali na


watu binafsi wanaotaka kutimiza malengo yao ya
kibiashara na kitaaluma kupitia program maalumu
ya malezi (Mentoring and Coaching).

Amewahi kuwa mshauri wa kibiashara kwa


wajasiriamali wanawake kupitia program ya Graca
Machel Trust (GMT), Mshauri na mlezi wa Africa
Entrepreneurship Award (Tuzo za wajasiriamali
vijana Africa), Mshauri na mkufunzi wa kibiashara
na kiuongozi kwa vyombo vya habari Tanzania bara
na visiwani kupitia Tanzania Media Foundation.

Pia amewahi kufanya kazi kama mwajiriwa wa

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 197


Umoja wa Mataifa kupitia shirika la UNESCO
linalojishughulisha na elimu, sayansi, teknolojia na
utamaduni.

Alitambuliwa na kampuni ya Avance Media yenye


makao yake makuu nchini Ghana kama kijana
mwenye ushawishi zaidi nchini Tanzania katika
eneo la kutoa Elimu ya Maisha na Uandishi
(Personal Development and Academia) kwa mwaka
2019/2020.

Amewahi pia kutambuliwa kama kiongozi bora


kijana wa dunia katika kongamano la kimataifa
nchini Taiwani - China mwaka 2012 na pia amewahi
kuwa mwanafunzi bora wa kitaifa kidato cha nne na
mwanafunzi bora katika masomo ya Diplomasia ya
Uchumi.

Mwaka 2020 pia Joel Nanauka ametambuliwa na


kampuni ya Avance Media yenye makao yake
makuu nchini Ghana kuwa miongoni mwa vijana 100
wenye ushawishi mkubwa barani Afrika katika

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 198


eneo la kutoa elimu ya maisha na uwandishi yaani
(Personal Development and Academia) akiwa
ameandika jumla ya vitabu 22 vilivyoweza
kubadilisha maisha ya watu katika nchi mbalimbali
Duniani.

Joel, ni mkurugenzi wa taasisi ya Africa Success


Academy inayojishughulisha na kutoa mafunzo kwa
taasisi mbalimbali, wajasiriamali, wanawake na
vijana walioko vyuoni na mashuleni ili kuwajengea
uwezo.

Joel amemuoa Rachel na wamebarikiwa watoto


wawili, Joyous na Joyceline.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 199


Vitabu Vingine Nilivyokuandikia
HARDCOPY (Nakala ngumu)

1. Timiza Malengo Yako (Mbinu 60 walizotumia


watu maarufu kufanikiwa)

2. Ishi Ndoto Yako (Siku 30 za kuishi maisha


unayotamani)

3. Tabia 12 Zinazoleta Mafanikio.

4. Ishinde Tabia Ya Kughairisha Mambo.

5. Ongeza Kipato Chako (Maarifa juu ya fedha,


Biashara na uwekezaji)

6. Nguvu Ya Mwanamke.

7. Mbinu Za Kufanikisha Ndoto Katikati Ya


Changamoto.

8. How To Pass Your Exams With Ease.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 200


9. Uzalendo Na Ujenzi Wa Taifa.

10. Ufanisi Kazini

11. Boresha Mahusiano Yako.

12. Money Formula

13. Core Genius

Kupata vitabu hivi nilivyokuandikia wasiliana na


namba zifuatazo:

0683 052 686

0745 252 670

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 201


eBooks / SOFTCOPY (Nakala laini).

1. Money Formula (Elimu ya fedha isiyofundishwa


shuleni)

2. Hatua Sita Za Kujiajri

3. Muongozo Wa Mafanikio

4. Core Genius (Jinsi ya kugundua uwezo wako wa


kipekee)

5. Jinsi Ya Kufanikiwa Katikati Ya Nyakati Ngumu.

6. Saikolojia Ya Mteja

7. Mbinu Za Kujenga Ujasiri Na Kujiamini.

8. Surviving The Crisis.

9. Namna Ya Kuondokana Na Madeni

10. Uzalendo Na Ujenzi Wa Nchi.

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 202


11. Mbinu Za Kuongeza Kipato.

12. Strategy 2021, Siri Za Kupata Matokeo


Makubwa Ndani Ya Mwaka Mmoja.

13. Nifanye Biashara gani?

14. Maono

15. Marafiki

Kupata eBooks hizi nilizokuandikia wasiliana na


namba ifuatayo:

Whatsapp +255 745 252 670

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 203


Kozi Nilizokuandalia, Unaweza Kuzisoma Online.

1. Mbinu Za Kuuza Zaidi.

2. Jinsi Ya Kujenga Kipato Cha Uhakika Kwa


Kujiajiri.

3. Jinsi Ya Kuondona Na Madeni.

Kupata kozi hizi wasiliana nasi

Whatsapp 255 762 312 117

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 204


Tembelea Mitandao Yangu Ya Kijamii

YouTube: Joel Nanaka


(Utapata VIDEO nyingi zenye Kukusaidia kufikia
malengo yako)

Instagram: @JoelNanauka_
(Utapata mafunzo kila siku yatakayokusaidia kupiga
hatua maishani)

Facebook: JNanauka
(Utapata mafunzo kila siku na pia shuhuda
mbalimbali za watu waliojifunza kupitia mimi)

Ishi Ndoto Yako | Joel Nanauka | 205

You might also like