Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 3

UHAKIKI WA FASIHI

(LITERALLY ANALYSIS)
YALIYOMO
Dhana ya Uhakiki
Maudhui
Vipengele Vya Maudhui
Dhamira
Ujumbe
Migogoro
Falsafa
Msimamo
Msimamo wa Kimapinduzi
Msimamo wa Kibwanyenye
Mtazamo
Mtazamo wa Kiyakinifu
Mtazamo wa Kidhanifu
Itikadi
Fani
Muundo na Mtindo
Muundo
Wahusika
Dhana ya Mhusika
Aina za Wahusika
Muktadha
Mazingira
Msuko wa Matukio
Muundo wa Ushairi wa Kiswahili
Vijenzi Vya Shairi la Kiswahili
Mtindo
Lugha au Matumizi ya Lugha
Tamathali za Usemi
Mbinu Nyingine za Kisanaa.
UTANGULIZI.
Kazi hii inazungumza uhakiki wa fasihi. Baadhi ya wasomaji wa kazi hii wanaweza
kujiuliza uhakiki ni nini?
Kazi hii inaeleza maana ya uhakiki, na pande mbili muhimu za kazi ya kifasihi
ambazo ni fani na maudhui. Maelezo yote yataegemea kwenye mawazo ya
wataalamu mbalimbali
ambao waliwahi kuandika au kuzungumza juu ya mambo haya. Pia, kazi hii itaweka
wazi uhusiano uliopo kati ya uhakiki, fani na maudhui. Ni muhimu sana kuzungumza
vipengele vya fani na maudhui katika kazi hii kwa sababu mhakiki hawezi kuhakiki
vizuri kazi yoyote ya
kifasihi bila kuwa na uelewa pia na utambuzi wa vipengele vya fani na maudhui kwa
maneno mengine uhakiki umefungamana na vipengele vya fani na maudhui. Hivyo
basi, vipengele vyake kadha vitajadiliwa katika kazi hii. Kabla hatujaingia ndani ya
mjadala hebu tuanze na maana ya uhakiki.

Dhana ya Uhakiki
Kwa mujibu wa Wamitila (2002), uhakiki ni uchunguzi wa kazi ya kifasihi kwa
makini na kwa utaalamu. Uchunguzi wa aina hii huchunguza uchanganuzi, fasiri,
uelezaji, ufafanuzi, tathimini na utoaji wa kauli ya kijumla. Maelezo ya Wamitila
yanatutibithishia kuwa uhakiki na usomaji wa kawaida ni tofauti kabisa kwa kuwa
uhakiki hauishii kwa kusoma tu bali hupitia kusoma, na kutafakari kuhusu kazi hiyo
na kutathimini. Uhakiki huhitaji umakini na uelewa na wa kiwango cha juu
ukilinganisha na msomaji wa kawaida.

Mlaga (2017) Uhakiki ni uchambuzi na ufafanuzi wa vipengele vya fani na maudhui


ya kazi ya fasihi. Uchambuzi unahusisha ubainishaji wa vipengele vyote viwe ni vya
fani au maudhui, Kama vinavyojitokeza katika kazi husika. Mlaga anasema kwamba
Maelezo kuhusu vipengele vya fani na maudhui yanaweza kuwa yameegemezwa
katika uziefu binafsi wa mtu, nadharia fulani inayoongo za katika uchunguzi wa
jambo, na hata vionjo vya mtu binafsi vya kiujumi. (Ntarangwi, 2004), Uhakiki ni
kitendo cha kutathimini, kueleza, kuainisha na kutoa maoni juu ya kazi fulani ya
fasihi kwa kuongozwa na kaida maalumu. (Peck & Coyle), Uhakiki ni utathmini,
ufasili na uainishi wa kazi za fasihi, lakini haumaanishi kutafuta makosa ya kazi hiyo.

Kwa hiyo, Uhakiki ni kitendo cha kuchambua, kutathmini na kuainisha kazi ya fasihi
ili kuona ubora na udhaifu wa kazi hiyo kwa kutumia vigezo husika vya fani na
maudhui kwa kuegemea kwenye uzoefu binafsi wa mtu, nadharia fulani, au vionjo
vya mtu binafsi vya kiujumi.

Fani na Maudhui

Uhakiki wa fasihi anafuata misingi ya kuchunguza ‘jinsi’ ya yanayozungumziwa


katika fasihi na hayo ‘yanayozungumziwa’ hayo ndiyo yanayorejelewa na dhana za
fani na maudhui Wamitila (..kmhjm;2008). Kimsingi, dhana hizi mbili hazipaswi
kutenganishwa kwa kuwa kinachowasilishwa hakiwezi kuangaliwa bila ya
kuchunguza jinsi kinavyowasilishwa. Maudhui au yaliyomo katika kazi ya kifasihi
hayawezi kumfikia msomaji bila ya kuwepo na nyenzo za kuyapitisha au Uhakiki wa
fasihi kuyawasilisha. Uhusiano uliopo basi kati ya fani na maudhui ni wa
kutegemeana, bila fani maudhui hayapo; na maudhui nayo yawezi kuwasilishwa bila
ya kuwepo kwa fani. Hata hivyo, pana umuhimu wa kutenganisha dhana hizi mbili
ili kuweza kuzizungumzia kwa undani. Kwa hivyo, katika kazi hii vipengele
mbalimbali vya fani na maudhui vitachunguzwa kwa undani. Mchoro huu unaonesha
vipengele vya fani na maudhui na uhusiano uliopo kati ya fani na maudhui kama
vitakavyoelezwa badaye.

You might also like