Professional Documents
Culture Documents
Jifunze Forex Kwa Lugha Ya Kiswahili Toleo La Pili
Jifunze Forex Kwa Lugha Ya Kiswahili Toleo La Pili
Jifunze Forex Kwa Lugha Ya Kiswahili Toleo La Pili
UTANGULIZI
FOREX NINI?
Forex inasimama badala ya neno FOREIGN EXCHANGE, Ambapo unakuwa unabadili
sarafu moja toka sarafu nyingine. Mfano kama ukitoka Tanzania unatumia TSH
ukaenda Kenya ambapo wanatumia KSH itakubidi ubadilishe sarafu yako ya
kitanzania kwenda katika saafu ya kikenya. Kwa zoezi hilo unakuwa umeshafanya
FOREX.
Hapo kinachofanyika ni hiki, TSH/KSH kwamba unauza sarafu ya kitanzania kwa
kununua sarafu ya kikenya. Hili tutaliona katika platform hii. utakutana na vitu kama
USD/CHF GBP/JPY EUR/USD
kwa wakati mmoja ambapo fedha hizo zinakuwa katika pair moja.
Fedha hizo zinakuwa katika pair ambayo tunaita CURRENCY PAIR ambayo inakuwa
na fedha mbili za nchi tofauti,mfano wa currency pair unaweza kuwa USD/TSH hii ni
pair ya United State Dollar (Fedha ya Marekani) na Tanzania shilling (Fedha ya
Tanzania).
Kubadilisha hela huku mtandaoni ni biashara ambayo inazungusha hela nyingi kupita
aina yoyote ya biashara ulimwenguni kwa siku. Kwa siku biashara hii mzunguko wake
wa hela ni zaidi ya $5 TRILLION. Wakati stock exchange ya New
4. Speculators
Je, hii biashara ina muhimu wowote kwako? Jibu linategemea wewe
unahitaji nini
1. Kama unataka soko ambalo halilali.
2. Kama unataka fursa ya kufanya biashara mda wowote katika siku.
3. Kama unataka kutengeneza kiasi kikubwa cha pesa. Basi nadhani FOREX ni mahala
sahihi kwa hayo yote
NB: Kama utaweza tengeneza kiasi kikubwa cha pesa ndani ya mda mfupi, pia
unaweza kupoteza kiwango cha fedha ndani ya mda mfupi huohuo
4. FOREX ni biashara kama biashara zingine kama vile biashara ya nguo,biashara ya
duka,biashara ya madini, biashara ya mazao na zinginezo unazozifahamu na kila
biashara inamtindo wake wa kuifanya na hapo ndipo biashara zinatofautiana na hili
biashara uweze kuifanya na kukuletea faida lazima uhifahamu biashara hiyo na ni
jinsi gani unaweza kuifanya.
Watu gani wanaokuwepo/wanaoshiriki katika hii biashara?
1. Benki kuu (Central banks)
2. Serikali (Government)
3. Umoja wa wawekezaji(investment coorperation)
4. Wafanyabiashara wa duniani kote(businessies worldwide)
5 Wafanyabiashara wadogo(Retail trader)
Maeneo vitovu katika hii biashara duniani ni:
1. NEW YORK (United States Dollar USD)
2. LONDON (Euro EUR and Pound GBP)
3. FRANKFURT (France franc CHF)
4. TOKYO (Japanese YEN JPY)
5. SYDNEY(Austarlian dollar AUD)
VIPINDI VYA FOREX MARKET (SESSIONS)
1.SYDNEY SESSION
Hii ni session ambayo inaanza saa 6:00 usiku mara baada ya soko kufunguliwa na
inaisha saa2 asubuhi,hapa unaweza ukafanya biashara sarafu zote lakini unashauriwa
kufanya biashara zaidi sarafu zenye NZD na AUD kwasababu zinakuwa na mzunguko
mkubwa kwa wakati huo sokoni.
2.TOKYO/ASIAN SESSION
Hiki kipidi kinaanza saa 8 usiku masaa 2 mara baada ya Sydney session kuanza na
inaenda mpaka saa 4 asubuhi, hapa unaweza kufanya biashara sarafu zote lakini
unashauriwa zaidi kufanya biashara sarafu zenye JPY kwasababu zinakuwa na
mzunguko mkubwa kwa wakati huo sokoni.
3.LONDON SESSION
Hiki kipindi kinaanza saa 4 asubuhi saa 1 kabla ya kipindi cha Tokyo na kufungwa
na kwenda mpaka saa 12 jioni, hapa unaweza kufanya biashara sarafu zote lakini
unashauriwa kufanya biashara sarafu za EUR,GBP,USD na JPY kwa sababu zinakuwa
na mzunguko mkubwa kwa wakati huo sokoni.
4.NEW YORK SESSION.
Hii inaanza saa 9 mchana na kufanya muunganiko na kipindi cha London(London
session) kwa mda wa masaa 4,yenyewe inaenda mpaka saa 5 usiku ambapo kipind
cha sydney kinaanza tena hapa unaweza ukafanyia biashara sarafu zote lakini
unashauriwa kuafanya biashara zaid sarafu za USD,CAD,EUR na GBP kwasababu
zinakuwa na mzunguko mkubwa kwa wakati huo sokoni.
Soko la FOREX hufunguliwa jumapili saa 6 usiku na kufungwa Ijumaa saa 5:59 usiku
hivo ndani ya huu mda una uwezo wa kufanya biashara
FAIDA ZA FOREX
1. Una uwezo wa kufanaya biashara sehemu yeyote ulipo na kwa mda wowote ndani
ya siku tano za week ndani ya saa 24 (24/5)
2. Unaweza kutoa faida hela zako mda wowote ndani ya week au hata weekend
kulingana tu na broker unayemtumia
3. biashara hii ya forex imewekewa Sheria rahisi sana ukilinganisha na biashara
zingine.
5. Uwiano mzuri kwa kiasi kidogo unaweza ingiza faida kubwa. (Leverage)
HASARA ZA FOREX
1. Upatikanaji wa HASARA kubwa na kwa muda mfupi.unapotegemea kupata faida
basi pia utegemee kupata hasara kubwa pia
2. Hii sio biashara ambayo kila mtu anaweza kuifanya.
SWALI:Je unafikiri forex ni biashara kama zilivyo biashara nyingine na kama hapana
kwanini na kama ndio kwann?
AINA ZA WAFANYABIASHARA KATIKA FOREX
Hii ni eneo muhimu sana kulijua na wewe kufanya maamuzi unataka uwe
mfanyabiashara wa aina gani. Hivyo kabla hujaanza ni bora kujitathmini wewe ni
mfanyabiashara wa aina gani na utumie njia zipi katika kufanya biashara yako.
Ni muhimu kujua wewe ni mfanyabiashara wa aina gani katika forex ,hiyo itakusaidia
kuweza kupanga muongozo wa kibishara(trading plan) yako ili uweze kufanya
biashara hii kwa kwa mafanikio makubwa.
Forex inajumuisha wafanyabiashara wa aina zifuatazo:-
1. DAY TRADER
Huyu ni mfanyabiashara ambae huingia katika biashara katika siku husika na kutoka
katika trade siku hio hio. Uzuri wa kuwa day trader ni mda wa kutosha wa kufanya
zako analysis. mara nyingi huwa na mda maalum wa kuingia katika trades zake. Na
mda ukifika wanasubiri fursa ijitengeneze na kuingia katika biashara(traders) zao,
Mara nyingi hutumia chart za dk 30, liasaa 1 hadi saa 4 katika kufanya
uchambuzi(analysis).
2. SCALPER
Huyu ni mfanyabiashara anaekuwa katika soko kwa mda mfupi sana. Mara nyingi
anaingia na kutoka katika trade na dakika kadhaa tu. Kivutia kikubwa kwa trader wa
aina hii huona faida au hasara ndani ya mda mfupi tu. Msingi mkubwa wa scalper ni
kuwa na uwezo wa kufikiri haraka na kuweza kumantain pressure. Kulingana na mda
mfupi wa fursa scalper huamua aingie katika hio fursa au aache,huwa anadumu
sokoni kwa muda mfupi tu na hutumia chart ya dk 5,dk15 mpaka dk30 kufanya
uchambuzi (analysis).
3. SWING TRADER
Huyu ni trader ambaye anaingia na kukaa sokoni kwa muda mrefu kulingana na na
target yake ,anaweza akakaa kwa masaa 5,week mpaka mwezi.tunaweza kusema ni
mfanyabiashara wanaoweza kukaa sokoni mda mrefu kuliko aina nyingine ya trader
kulinga na mtiririko wa soko ukitokea wa kupanda au wakushuka wanakuwa
wanaenda nao.
FOREX TERMINOLOGIES
Kama nilivyotangulia kusema ya kwamba katika FOREX tunahusika na jozi za sarafu
mbalimabali(currency pair), Misamiati hii kama utaweza kuielewa vizuri basi nina
hakika kutakuwa hakuna shaka ya wewe kuwa katika soko.
1. BASE CURRENCY
Hiki ni kiini msingi katika kununua au kuuza katika forex. kama utabuy EUR/USD Hii
ni kumaanisha unanunua euro ya ulaya na wakati huohuo unauza dola ya kiamrekani
2. QUOTE CURRENCY
Hii ni ile sarafu ya pili katika pair ya sarafu husika unapofanya trade. Mfano
EUR/USD, USD ndio quote currency.
3. LONG/BULLISH/BUY
Hii ni termonology ambayo unasikia watu wakiiongelea. kama imepatikana fursa
(opportunity) ya long/bullish hapa maana yake NUNUA. Bull ni aina za mnyama
ambae anakula majani hivo candlestick zake nyingi zinakuwa zikiwakilishwa na rangi
ya kijani. Huyu mnyama akitaka kukudhuru huinamisha kichwa chini na
anakunyanyua kwa kukuchota kukupeleka juu. Hivyo katika Forex hapa inamaanisha
soko linatoka chini linapanda juu.
4. SHORT/BEARISH
Kama imepatikana fursa (opportunity) ya short/bearish hapa maana yake UZA. Bear
ni aina ya mnyama ambae anakula nyama, hivo candlestick yake huwakilishwa na
rangi nyekundu. Huyu mnyama anavyokudhuru huruka juu kisha hukushusha chini.
Hii katika forex inamaanisha soko linatoka juu kushuka chini.
5. PIP (PERCENTAGE IN POINT)
Hiki ni kiasi cha thamani kinachocheza kulingana na mzunguko wa sarafu husika
katika biashara. Au tunaweza kusema ni mzunguko mdogo wa bei ambao currency
pair unaoufanya kwa kupanda au kushuka.Mfano Thamani ya USDCAD imetembea
kutoka 1.34286 hadi 1.34984 itakuwa imetembea kwa 66pips,Hii tunaipata kwa
kuchukua 1.34286 – 1.34948 ambapo tutapata 0.00662 na katika FOREX thamani ya
pip tunaanza kuhesabu kuanzia desimali ya nne hivyo basi kwa hapo USDCAD
itakuwa imeshuka kwa 66pips,na hiyo 2 tunaita micropip.kwa hiyo ni sawa na useme
imemove pips 66.2,
Lakin kwa pair za Japanese Yen kama vile USDJPY,GBPJPY kwa hizi thamani ya pip
tunaanza kuhesabu kuanzia desmali ya tatu.
6. LOT SIZE
Hii ni thamani inayotumiwa kujua faida na hasara.
Standard Lot size: 1.00 = $10 kwa pip moja
Min Lot size: 0.10= $1 kwa pip moja
Micro Lot size: 0.01= 10 cent kwa pip moja
6.HANGING MAN
huonekana kama pipi ya kijiti ya mraba au nyundo, huwa na umbo dogo sana ambalo
husababishwa na bei ya kufungia kuwa juu kidogo au chini kidogo ya bei ya
kufungulia.
Maana halisi ya umbo hili ni nini.?
Candle hii ni wakati soko linapofunguliwa wanunuji(buyers) huvuta bei ya sarafu juu
zaidi,lakini wauzaji(selers) hupigania kurudisha bei chini,hivyo hufanikiwa kuirudisha
chini kidogo au juu kidogo ya bei ya kufungulia.
Jinsi gani unaweza ingia sokoni na candle hii.?
1. wakati bei ya sarafu husika iko uelekeo wa juu. (uptrend movement(in
ressistance), hivyo hutuashiria kuwa uelekeo wa soko unabadilika kuanza kuelekea
chini (bearish movement)
2. Subiri candle inayofuata baada ya hanging man ifunge chini yake ili kuhakiki
uwepo wa uelekeo mpya wa chini, ukishahakiki hivi unaweza kuuza sarafu husika..
3. Jinsi mkia unavyokuwa mrefu zaidi,ndio uhakika zaidi wa wauzaji kutawala soko.
7. INVERTED HAMMER.
candle hii huonekana kama nyundo inayoning'inia hewani na mkia mrefu, hutokea
wakati bei ya sarafu husika iko kwenye uelekeo wa chini zaidi.candle hizi huwa
zinajitengeneza upande wa support kuashiria kununua(kubuy)
Maana halisi ya umbo hili ni nini.?
candle hii pia wakati soko linapofunguliwa wauuzaji(sellers) hushusha bei ya sarafu
chini zaidi,lakini wanunuaji(buyers) hupigania kurudisha bei juu,hivyo kupelekea
kutengenezwa kwa umbo la mraba. Jinsi mkia wa juu unavyokuwa mrefu zaidi basi
ndivyo inavyotoa uhakika wa wanunuaji(buyers) kuchukua nafasi zaidi.
Jinsi gani unaweza ingia sokoni na candle hii.?
1. imetokea wakati bei ya sarafu husika iko kwenye uelekeo wa chini (support )
2. subiri candle inayofuata ifunge juu ya hii inverted hammer ili kuwe na uhakika
zaidi wa wanunuzi (buyers) sokoni, ikitokea hivi basi unaweza kutafuta nafasi
ya kuingia sokoni kununua.
8. SPINNING TOP
Hii ni candlestick moja yenye umbo dogo na mkia mrefu juu na chini. Ikitokea katika
ya eneo la RESISTANCE na SUPPORT huashiria kubadilika kwa trends,
9. RAILWAY TRACK
Hii ni candlestick pattern ambayo huwa na candlestick mbili zinazofuatana zenye
urefu na umbo sawa.hivi pia zinapoonekana eneo la support and resistance uashiria
kujeuka kwa soko
AINA ZA RAILWAY TRACK
• BULLISH RAILWAY TRACK:Katika hii candlestick ya kwanza inakuwa ni
bearish na ya pili ni bullish lakini zenye urefu na umbo sawa.Hii huashiria soko
litageuka kuelekea juu kwenda kununua(buy) endapo ikitokea kwenye
support.
10. PIERCING
Hii ni candlestik pattern ambayo huashiria kugeuka kwa soko kuelekea juu kwenda
kununua (buy) endapo ikitokea kwenye support.Kwenye Piercing candlestick ya
kwanza inakuwa ni bearish ikiwa na kiashiria kuwa soko lilikuwa linashuka chini na
candlestick ya pili huwa ni bullish na inafunga katikati ya candlestick ya
kwanza(middle at the past candle) kuonesha soko limefika katika eneo la kugeuka.
11. DARK CLOUD COVER
Hii ni candlestick pattern ambayo huashiria kugeuka kwa soko kuelekea chini kwenda
kuuza (sell) endapo ikitokea kwenye resistance,Kwenye Dark cloud cover candlestick
ya kwanza inakuwa ni bullish kuonesha soko lilikuwa linapanda juu na candlestick ya
pili huwa ni bearish na inafunga katikati ya candlestick ya kwanza kuhashiria kugeuka
kwa soko.kuelekea upande wa kuuza(kusell)
Channels
hii nayo inafanana saana na trendlines na hata katika mazingira yake ni vile tu kama
trendline ila tofauti yake na trendiline yenyewe ina mistari miwili kwa pamoja juu na
chini yaani mfano wa reli hivi kwa hiyo mstari wa juu utakua resistance na wachini ni
support kwa maneno mepesi kabisa.au unawezea kusema ni njia ambayo bei
huifuata na hujenga kingo ambapo bei inakuwa inatembea ndani yake ila baada ya
mda inavunja kingo mojawapo kutegemea ilikuwa ni ya kupanda(uptrend) au
kushuka(downtrend).
AINA ZA CHANNEL
• Downtrend channel(chaneli ya kushuka)
• Uptrend channel(chaneli ya kupanda)
• Sideway channel(chaneli msambamba)
Baada ya kuiona app hio click INSTALL na itakuwa kwa simu yako sasa kwa matumizi
Unapokuwa umeingia katika application kwa mara ya kwanza screen itakuonesha
namna ya kusajili akaunti mpya na kulog kama acc utakuwa nayo teyari(log in
existing account)
kwa kuwa utakuwa ulshafungua account kwa broker utaminya ''log in to an existing
account'' mbele yake litakutaka uchague broker utachagua broker unayemtumia na
account uliyojisajili mfano TEMPLER,OCTAFOREX,TICKMILL etc .baada ya hapo
utajaza username na password yako sasa kama hapa chini
QUOTES
Hii ni sehemu ambayo huonesha viwango dhahiri katika muda sahihi vya sarafu
mbalimbali. Quotes ya kawaida huonesha aina ya pair na bei ya kuuza na kununa.
kama utataka kuongeza pair zaid utagusa alama ya kujumlisha inayooneka kwa juu
ili kuongeza pair ambayo haipo katika list na unahitaji iwepo.
Sehemu inayofuata inaonesha chart kam ilivyoandikwa
Haya katika chart tunaona kuna alama tano juu tuue zinawakilisha nini zote
ehemu ya kwanza katika chart inaonesha kimsalaba ambapo hiutwa CROSSHAIR
Sehemu ya pili ni kama herufi F iliyolala. Hapo ndipo huweza kuset indicators yoyote
pamoja na kuchora mistari ya resistance na support na mingineyo.
Sehemu ya tatu $ hapa hutoa nafasi ya kuchange chati kutoka chati ya sarafu moja
kucheki chati ya sarafu nyingine.
Sehemu ya nne ni sehemu ya kubadilisha timeframe za chati husika. Ina alama ya
saa
Na ile sehemu iliopo mwishoni kabisa pale ni sehemu ya kuwekea oda sokoni, kati
buy au sell/sell stop au buy stop/ sell limit au buy limit.
sehemu ya pili katika chart
sehemu ya tatu katika chart
Sehemu ya nne katika chart
Sehemu ya tano na ya mwisho katika chart
Haya tuende na kipengele kinafuta baada ya chart ambacho kinaonesha trades zako
nacho kwanye metratrade 4
Taarifa za akaunti
- PROFIT- faida/hasara iliopatikana baada ya kuclose trade
-BALANCE- kiasi kilichopo katika akaunti yako.
- EQUITY- Kiasi kilichopo katika akaunti yako + matokeo ya trade ulisofungua
zaweza kuwa hasara/faida
- MARGIN LEVEL (%)- Equity/margin * 100
- MARGIN- Kiasi kinachohitajika ili kuendesha position zilizofunguliwa.
- FREE MARGIN- Equity-Margin
Vipengele vilivyowekwa kwa mfumo wa number
1.Aina ya sarafu uliyotrade
2. Aina ya oda uliofanya katika hio sarafu sell/buy
Sio kila mvunjikoa wa nje(breakout) katika eneo la consolidation ni LAST KISS lakini
kila LAST KISS unayoiona ni BREAKOUTS katika soko.
MUHIMU: pindi uonapo LAST KISS ingia katika trade katika candlestick ya pili kutoa
ya kwanza iliyorudi kwnye box baada ya breakout kulingana na uelekeo.
bearish kangaro
bullish kangaroo
wick au mkia wa candlestick hii lazima uwe mrefu
Angalia mfano hii kulikuwa na strong trend kisha Kangaroo tail ilivyopinga strong hio
kuigeuza na kutengeneza bearisha kangaro .
Pia wakati mweingine Kangaroo tail zinazojitengeneza katikati ya Trend na zilizo
kinyume na hio trend. Huwa ni uongo zinadanganya ili ufanye maaumizi(fake
formation)
mifano mingine fanya mazoezi utaiona zaid kwenye chart hapo ni baadhi ya mifano
tyu nimetoa
BIG SHADOW
Kama umekuwa mfuatiliaji wa chart utakuwa ushawahi kuona kuna CANDLESTICK ni
ndefu sana na hakuna NEWS au Factor yeyote kubwa. Hii pia lazima itokee katika
eneo la RESISTANCE na SUPPORT. Na inasimama au ni kiashiria kama REVERSAL.
Baadhi ya watu wanaweza kuifananisha hii na ENGULFING, Lakini nataka kukwambia
hii ni zaidi ya ENGULFING.
inapojitengeza katika resistance kama hapa juu tunaita bearish big shadow ikiashiria
kusell
na inapokuwa katika support tunaiita bullish big shadow ikamaanisha kubuy au
kununua
UNAPOAMUA KUFANYA MAAMUZI UNAPOONA BIG SHADOW ZINGATIA HAYA
1. Huu ni muundo wa CANDLESTICK mbili kwa . Candlestick ya pili katika kuundwa
huku ndio tunayoiita BIG SHADOW CANDLESTICK.
2. BIG SHADOW CANDLESTICK lazima iwe kubwa kwa urefu wa juu na chini kuliko
candlestick iliopita nyuma yake.
3. BIG SHADOW lazima itokee kwenye maeneo ya SUPPORT na RESISTANCE.ndo
maeneo ya kufanya maamuzi
4. BIG SHADOW hutokea kwa kwenda juu na chini kulikokithiri zaidi.
5. Kwa BULISH BIG SHADOW, Stop loss huwekwa pips chache chini ya ile BULLISH
BIG-SHADOW CANDLESTICK
6. Kwa BEARISH BIG-SHADOW, Stop loss huwekwa pips chache juu ya ile BEARISH
BIG-SHADOW CANDLLESTIICK
WAMMIES AND MOOLAHS.
Hii ni pale price inapogusa mara mbili kwa kufuatana katika eneo la SUPPORT au
RESISTANCE, ambayo huwa inafuatana.
Wammies and moolahs hutokeaa katika timeframe yoyote, kwa soko la aina yoyote,
Wammies and Moolahs ni kitu cha toleo la kipekee la DOUBLE-TOP and DOUBLE-
BOTTOM. Ukizifuatilia kwa makini aina hii aina ya muundo, unaeza ukawa unatrade
njia hii tu na ikakupa matokeo chanya kwa asilimia nyingi.
Wammies and Moolahs pia ina kaa uzuri katika muundo wa PATTERN zinazoashiria
REVERSAL ya soko.
Traders ambao huingia na kutoka katika trade katika maeneo ambayo wanachukulia
hii kama njia hii ni ya msingi na ya manufaa kwao.kataka ktafuta fursa za kuingia
katika soko
WAMMIES ni pale price inagusa eneo la SUPPORT katika chart yako sokon .
MOOLARS ni pale bei inapogusa katika eneo la RESISTANCE katika chart
yako
SIFA ZA WAMMIES
1. Soko linagusa eneo la Support mara mbili.
2. Kugusa kwa mara ya pili huwa juu zaidi ya mara ya kwanza.
3. Kunakuwa na candlestick zisizopungua sita katikati ya hio miguso miwili.
4. Soko hutengeneza bullish candlestick katika mguso wa pili
5. Stop loss inawekwa pips chache chini ya ile candle iliogusa mara ya kwanza.
SIFA ZA MOOLAH.
1. Soko linagusa eneo la Resistance mara mbili.
2. kugua kwa pili huwa chini ya ule mguso wa kwanza kutokea.
3. Kunakuwa na candlestick zisizopungua sita katikati ya miguso hio miwili
4. Soko hutengeneza bearish candlestick baada ya mguso wa pili.
5. Trader huingia kwa SELL STOP pips chache kutoka katika ile Bearish candlestick.
6.Stop loss inawekwa pips chache juu kidogo ya ile candle iliogusa mara ya kwanza.
BIG BELT
Soko la Forex hukumbwa na nyakati za ajabu wakati mwingine ambzao hata unaweza
usielewe zimetokea vip. Tunaamini kuwa candle inapojifunga ndipo candle nyingine
inatakiwa kufunguka lakini unakuta candle imefunga sehemu nyingine na inayofuata
inafunguka sehemu tofauti. Kwa mtu aliyekuwa nje ya soko hii inakuwa fursa nzuri
sana kwake.
TRENDY KANGAROO.
Hii inakuwa tofauti kidogo sana na Kangaroo Tail. Hii hutokea ambapo soko lipo
katika trend Fulani kisha unakuta soko limetulia linacheza ndani ya eneo Fulani na
candles hazitoki katika hilo eneo kwa mda flani.
na baadae inakuja kutokea cndle ya kangaro tailkufanya maamuzi either ni kusell au
kubuy
EXITING TRADE.
MAMBO YA KUJUA WAKATI UNAINGIA KATIKA SOKO LA FOREX
1.Kutambua fursa ya kufanya trade na hapa unachagua kiasi cha hela unachotaka
kukitoa kwa ajili ya kuingia katika trade hio, Ndipo unaangalia matumizi ya lot size,
idadi ya position na Risk management.
2,Unatengeneza mpango wa kufanya hio trade, kwa kufuata sheria za njia
unayotumia katika kufanya trade.ka ma wewe mwenyewe ulivyojipangia
3.Kuingia katika soko, Ingia katika soko katika kwa bei ambayo unajua ni thamani
yenye kuleta manufaa katika fursa iliyopatikana. ukiona umechelewa kuingia achana
na hiyo fursa na utafute fursa nyinginee
4.Kutoka nje ya soko, Hapa ndipo utahesabu kama umetengeneza faida kiasi gani au
umepata hasara hasara.
5.Kujifunza kutokana na trade unazaokuwa unaingia , Kutambua mapungufu
uliyoyafanya kuanzia hatua ya kwanza mpaka ya tano.
6.kuwa na malengo na kufanya forex na target yako maalam unayojua ikifika
unaweza toka katika market nk.
7.unapoaana kuna kitu kimetokea katika trade yako tofauti na ulivyotarajiamfano
news(habari) na ukaona trend imeahribiwa jifunze kutoka katika hiyo trade
# copide notes
Kwahiyo ili soko litembee kwenda juu au kurudi chini ni lazima kuwe na kuzidiana
kwa nguvu kati ya demand na supply na endapo wakitoshana nguvu basi soko huwa
linakua linafanya haki, yani watakao nunua watanunua sawa na watakao uza.
Kwahiyo kutokana na sababu hii ya kinachopelekea soko litembee juu chini au chini
juu, ndio sababu ya kwanza inayopelekea supply na demand kukataa ile dhana ya
kwamba eti uimara wa zone unapimwa na idadi ya miguso mingi ya candlestick.
Kwa sababu endapo ukanda utaguswa na candle Mara nyingi hii inamaanisha supply
na demand nguvu zao hazina utofauti sana au ndio zinaelekea kwenye uwiano sawa,
ila endapo itaguswa na candle moja au mbili then reaction ya kwenda juu au chini
ikawa imetokea basi hapo tunasema demand na supply hawako katika usawa na hapo
lazima kutakua na pips nyingi sana.
Kwamfano chukua kitenesi kidundishe kwenye sakafu then kiangalie vile kitakwenda
juu na kurudi kugonga sakafu then kitakwenda baadae
kitapungua kasi na baadae zaidi kitaishiwa nguvu na kitaanza kuroll na hatimae
kitatulia sehemu moja.basi hata
kwenye zone candlestick zitakwenda zitagusa na kugusa tena na tena na baadae
zitatulia hapo kwa muda mwingi bila kushuka sana wala kwenda upande wa pili, so
kadri zone inavyoguswa Mara nyingi ndio udhaifu wake unaongezeka.kwenye mpira
ukiruhusu timu pinzani iwe inakuja kwenye himaya yako Mara kwa Mara lazima
utafanya makosa tu na utaachia na utafungwa goal so miguso ikitokea mingi itafikia
mahali usawa utaonekana na usawa ukitokea basi ukatili utafuata(initiative), hii ndio
tofauti ya hao jamaa na ndio maana kuna watu wanasemaga support na resistance
haina jipya nlimskiaga mtu aliwahi sema hivi pia na marumbano yalikua mengi mno
ingawa sijajua kama na yeye alitumia point hii au alikua na maana nyingine,
anyway tutaendelea na somo baadae now chukua hiko aye.