Download as rtf, pdf, or txt
Download as rtf, pdf, or txt
You are on page 1of 21

SEHEMU YA KWANZA

FOREX NINI?

Forex inasimama badala ya neno FOREIGN EXCHANGE, Ambapo unakuwa unabadili sarafu moja toka
sarafu nyingine. Mfano kama ukitoka Tanzania unatumia TSH ukaenda Kenya ambapo wanatumia KSH
itakubidi ubadilishe sarafu yako ya kitanzania kwenda katika saafu ya kikenya. Kwa zoezi hilo unakuwa

umeshafanya FOREX.

Hapo kinachofanyika ni hiki, TSH/KSH kwamba unauza sarafu ya kitanzania kwa kununua sarafu ya

kikenya. Hili tutaliona katika platform hii. utakutana na vitu kama USD/CHF GBP/JPY EUR/USD

kwa wakati mmoja ambapo fedha hizo zinakuwa katika pair moja.

Fedha hizo zinakuwa katika pair ambayo tunaita CURRENCY PAIR ambayo inakuwa na fedha mbili za

nchi tofauti,mfano wa currency pair unaweza kuwa USD/TSH hii ni pair ya United State Dollar (Fedha ya

Marekani) na Tanzania shilling (Fedha ya Tanzania).

Kubadilisha hela huku mtandaoni ni biashara ambayo inazungusha hela nyingi kupita aina yoyote ya

biashara ulimwenguni kwa siku. Kwa siku biashara hii mzunguko wake wa hela ni zaidi ya $5 TRILLION.

Wakati stock exchange ya New York kwa siku ni $22.4billion, Tokyo ni $18.4 billion na London ni $7.2

billion kwa siku. Na hizo ni stock exchange kubwa duniani, hivo FOREX ONLINE ni kubwa kuliko hizi stock
exchange.

• Nani wahusika katika Forex? (key player in the forex market)

Soko la Forex awali lilikusudiwa kwa ajilli ya Mabank makubwa na taasisi kubwa za kibiashara,ila

kutokana na mabadiliko makubwa ya technologia haswa kwenye 'internet',wafanyabiashara wadogo pia

(retail traders) nasi tumepata uwezo wa kuingia sokoni kupitia kwa dalali ama broker.

Key player (wahusika wakubwa kwenye soko)


1. Bank kubwa duniani (super bank) , ambazo hizi hufanya biashara hii kwa kiasi kikubwa

sana na huchangia sana uelekeo wa soko hili, bank hizo ni kama Citi Bank, JPMorgan,

UBS, Deutsche Bank and HSBC

2. Kampuni kubwa za kibiashara duniani (Large commercial companies), kampuni hizi

hufanya biashara hii kwa ajili ya biashara Zao, mfano kampuni kama Toyota katika

kuagiza vifaa nchi nyingine hulazimika kubadilisha fedha yao kwenda kwenye fedha ya

nchi ambako vifaa hivyo vinaagizwa.

3. Serikali na Bank za nchi (government and central bank

Je, hii biashara ina muhimu wowote kwako? Jibu linategemea wewe unahitaji nini

1. Kama unataka soko ambalo halilali.

2. Kama unataka fursa ya kufanya biashara mda wowote katika siku.

3. Kama unataka kutengeneza kiasi kikubwa cha pesa.

Basi nadhani FOREX ni mahala sahihi kwa hayo yote

NB: Kama utaweza tengeneza kiasi kikubwa cha pesa ndani ya mda mfupi, pia unaweza kupoteza

kiwango cha fedha ndani ya mda mfupi huohuo

4. FOREX ni biashara kama biashara zingine kama vile biashara ya nguo,biashara ya duka,biashara ya

madini, biashara ya mazao na zinginezo unazozifahamu na kila biashara inamtindo wake wa kuifanya na

hapo ndipo biashara zinatofautiana na hili biashara uweze kuifanya na kukuletea faida lazima uhifahamu

biashara hiyo na ni jinsi gani unaweza kuifanya.

Watu gani wanaokuwepo/wanaoshiriki katika hii biashara?

1. Benki kuu (Central banks)

2. Serikali (Government)
3. Umoja wa wawekezaji(investment coorperation)

4. Wafanyabiashara wa duniani kote(businessies worldwide)

5 Wafanyabiashara wadogo(Retail trader)

Maeneo vitovu katika hii biashara duniani ni:

1. NEW YORK (United States Dollar USD)

2. LONDON (Euro EUR and Pound GBP)

3. FRANKFURT (France franc CHF)

4. TOKYO (Japanese YEN JPY)

5. SYDNEY(Austarlian dollar AUD)

VIPINDI VYA FOREX MARKET (SESSIONS)

1.SYDNEY SESSION

Hii ni session ambayo inaanza saa 6:00 usiku mara baada ya soko kufunguliwa na inaisha saa2

asubuhi,hapa unaweza ukafanya biashara sarafu zote lakini unashauriwa kufanya biashara zaidi sarafu

zenye NZD na AUD kwasababu zinakuwa na mzunguko mkubwa kwa wakati huo sokoni.

2.TOKYO/ASIAN SESSION

Hiki kipidi kinaanza saa 8 usiku masaa 2 mara baada ya Sydney session kuanza na inaenda mpaka saa

4 asubuhi, hapa unaweza kufanya biashara sarafu zote lakini unashauriwa zaidi kufanya biashara sarafu

zenye JPY kwasababu zinakuwa na mzunguko mkubwa kwa wakati huo sokoni.

3.LONDON SESSION

Hiki kipindi kinaanza saa 4 asubuhi saa 1 kabla ya kipindi cha Tokyo na kufungwa na kwenda mpaka saa
12 jioni, hapa unaweza kufanya biashara sarafu zote lakini unashauriwa kufanya biashara sarafu za

EUR,GBP,USD na JPY kwa sababu zinakuwa na mzunguko mkubwa kwa wakati huo sokoni.

4.NEW YORK SESSION.

Hii inaanza saa 9 mchana na kufanya muunganiko na kipindi cha London(London session) kwa mda wa

masaa 4,yenyewe inaenda mpaka saa 5 usiku ambapo kipind cha sydney kinaanza tena hapa unaweza

ukafanyia biashara sarafu zote lakini unashauriwa kuafanya biashara zaid sarafu za USD,CAD,EUR na

GBP kwasababu zinakuwa na mzunguko mkubwa kwa wakati huo sokoni.

NB:-Masaa yote hapo ni kutegemeana na masaa ya AFRIKA MASHARIKI.(EAT +3GMT

Soko la FOREX hufunguliwa jumapili saa 6 usiku na kufungwa Ijumaa saa 5:59 usiku hivo ndani ya huu

mda una uwezo wa kufanya biashara

FAIDA ZA FOREX

1. Una uwezo wa kufanaya biashara sehemu yeyote ulipo na kwa mda wowote ndani ya siku tano za

week ndani ya saa 24 (24/5)

2. Unaweza kutoa faida hela zako mda wowote ndani ya week au hata weekend kulingana tu na broker

unayemtumia

3. biashara hii ya forex imewekewa Sheria rahisi sana ukilinganisha na biashara zingine.

5. Uwiano mzuri kwa kiasi kidogo unaweza ingiza faida kubwa. (Leverage)

HASARA ZA FOREX

1. Upatikanaji wa HASARA kubwa na kwa muda mfupi.unapotegemea kupata faida basi pia utegemee

kupata hasara kubwa pia

2. Hii sio biashara ambayo kila mtu anaweza kuifanya.


SWALI:Je unafikiri forex ni biashara kama zilivyo biashara nyingine na kama hapana kwanini na kama

ndio kwann?

AINA ZA WAFANYABIASHARA KATIKA FOREX

Hii ni eneo muhimu sana kulijua na wewe kufanya maamuzi unataka uwe mfanyabiashara wa aina gani.

Hivyo kabla hujaanza ni bora kujitathmini wewe ni mfanyabiashara wa aina gani na utumie njia zipi

katika kufanya biashara yako.

Ni muhimu kujua wewe ni mfanyabiashara wa aina gani katika forex ,hiyo itakusaidia kuweza kupanga

muongozo wa kibishara(trading plan) yako ili uweze kufanya biashara hii kwa kwa mafanikio makubwa.

Forex inajumuisha wafanyabiashara wa aina zifuatazo:-

1. DAY TRADER

Huyu ni mfanyabiashara ambae huingia katika biashara katika siku husika na kutoka katika trade siku

hio hio. Uzuri wa kuwa day trader ni mda wa kutosha wa kufanya zako analysis. mara nyingi huwa na

mda maalum wa kuingia katika trades zake. Na mda ukifika wanasubiri fursa ijitengeneze na kuingia

katika biashara(traders) zao, Mara nyingi hutumia chart za dk 30, liasaa 1 hadi saa 4 katika kufanya

uchambuzi(analysis).

2. SCALPER

Huyu ni mfanyabiashara anaekuwa katika soko kwa mda mfupi sana. Mara nyingi anaingia na kutoka

katika trade na dakika kadhaa tu. Kivutia kikubwa kwa trader wa aina hii huona faida au hasara ndani ya

mda mfupi tu. Msingi mkubwa wa scalper ni kuwa na uwezo wa kufikiri haraka na kuweza kumantain

pressure. Kulingana na mda mfupi wa fursa scalper huamua aingie katika hio fursa au aache,huwa

anadumu sokoni kwa muda mfupi tu na hutumia chart ya dk 5,dk15 mpaka dk30 kufanya uchambuzi
(analysis).

3. SWING TRADER

Huyu ni trader ambaye anaingia na kukaa sokoni kwa muda mrefu kulingana na na target yake

,anaweza akakaa kwa masaa 5,week mpaka mwezi.tunaweza kusema ni mfanyabiashara wanaoweza

kukaa sokoni mda mrefu kuliko aina nyingine ya trader kulinga na mtiririko wa soko ukitokea wa

kupanda au wakushuka wanakuwa wanaenda nao.

FOREX TERMINOLOGIES

Kama nilivyotangulia kusema ya kwamba katika FOREX tunahusika na jozi za sarafu

mbalimabali(currency pair), Misamiati hii kama utaweza kuielewa vizuri basi nina hakika kutakuwa

hakuna shaka ya wewe kuwa katika soko.

1. BASE CURRENCY

Hiki ni kiini msingi katika kununua au kuuza katika forex. kama utabuy EUR/USD Hii ni kumaanisha

unanunua euro ya ulaya na wakati huohuo unauza dola ya kiamrekani

2. QUOTE CURRENCY

Hii ni ile sarafu ya pili katika pair ya sarafu husika unapofanya trade. Mfano EUR/USD, USD ndio

quote currency.

FOREX 1

3. LONG/BULLISH/BUY

Hii ni termonology ambayo unasikia watu wakiiongelea. kama imepatikana fursa (opportunity) ya

long/bullish hapa maana yake NUNUA. Bull ni aina za mnyama ambae anakula majani hivo candlestick

zake nyingi zinakuwa zikiwakilishwa na rangi ya kijani. Huyu mnyama akitaka kukudhuru huinamisha
kichwa chini na anakunyanyua kwa kukuchota kukupeleka juu. Hivyo katika Forex hapa inamaanisha

soko linatoka chini linapanda juu.

FOREX 2

4. SHORT/BEARISH

Kama imepatikana fursa (opportunity) ya short/bearish hapa maana yake UZA. Bear ni aina ya mnyama

ambae anakula nyama, hivo candlestick yake huwakilishwa na rangi nyekundu. Huyu mnyama

anavyokudhuru huruka juu kisha hukushusha chini. Hii katika forex inamaanisha soko linatoka juu

kushuka chini.

FOREX 3

5. PIP (PERCENTAGE IN POINT)

Hiki ni kiasi cha thamani kinachocheza kulingana na mzunguko wa sarafu husika katika biashara. Au

tunaweza kusema ni mzunguko mdogo wa bei ambao currency pair unaoufanya kwa kupanda au

kushuka.Mfano Thamani ya USDCAD imetembea kutoka 1.34286 hadi 1.34984 itakuwa imetembea kwa

66pips,Hii tunaipata kwa kuchukua 1.34286 – 1.34948 ambapo tutapata 0.00662 na katika

thamani ya pip tunaanza kuhesabu kuanzia desimali ya nne hivyo basi kwa hapo USDCAD itakuwa

imeshuka kwa 66pips,na hiyo 2 tunaita micropip.kwa hiyo ni sawa na useme imemove pips 66.2,

Lakin kwa pair za Japanese Yen kama vile USDJPY,GBPJPY kwa hizi thamani ya pip tunaanza kuhesabu

kuanzia desmali ya tatu.

6. LOT SIZE

Hii ni thamani inayotumiwa kujua faida na hasara.

Standard Lot size: 1.00 = $10 kwa pip moja

Min Lot size: 0.10= $1 kwa pip moja


Micro Lot size: 0.01= $1 cent kwa pip moja

FOREX 4

7. TAKE PROFIT (TP)(chukua faida)

Hili ni eneo ambalo utaamua kutoka nje ya soko baada ya faida. Eneo ambalo utaona faida uliyopata

inakutosha au ni eneo ambali price inaweza kugeuka na kukuingizia hasara.

Unapoingia kwenye soko analysis zako zinakuonesha sarafu itapanda/kushuka mpaka eneo Fulani baada

ya hapo itageuka trends Ila haujui itachukua mda gani mpaka kufika katika hio bei(price) unaweza

ukafunga mannualy au automatically lakini mda mwingine huwezi kukaa kwenye screen yako mda wote

kuisubiri hio point. Unachokifanya unaset bei ikifika katika hilo eneo trade yake ijifunge automatically na

kisha wewe ukirudi au ukimaliza mambo yako kama itakuwa ilifika katika hio point uje ukutane na profit

yako. Hapo ndo panaitwa TAKE PROFIT.

8. STOP LOSS (SL)(kata hasara)

Hili ni eneo ambalo utaamua kutoka nje kwa hasara ama kwa kuona uchambuzi(analysis) wako ulikuwa

na makosa au unaamini upande wa hasara uliopo utaongezeka zaidi hivyo badala ya kupata hasara

kubwa unaamua kuchukua hasara kidogo. Wanasema kama hutakubali hasara basi jiandae kupokea

mama wa hasara kwa lazima.

Kwenye market ukishafanya analysis unaona kuna fursa ya kupanda kwa sarafu hivo unaamua kuinunua

ikiwa chini ili ikifika juu uiuze na ile tofauti ya bei ulonunua na utakayokuja kuuza ndo inakuwa faida Na

wewe uliingia sokoni kwa hio sarafu labda, Sasa baada ya kufanya hio uchambuzi inatokea (habari)news

mfano ya kushuka kwa ajira mfano marekani So kwa namna yoyote sarafu baada ya kupanda

itashuka.Maana itakuwa hafifu(week).Sasa unakuta na wewe ulishaingia kwa hiyo unagundua itashuka

sana hivyo unaamua kutoka katika soko katika hasara ndogo ili usipate hasara zaidi kwani haujui hio

sarafu itashuka mpaka wapi. Hio ndo inaitwa STOP LOSS,unaweza kutoka mannualy au kwa set ijitoe

automatically kama utakuwa busy au mbali na kifaa chako.

FOREX 5
AINA ZA ORDER KATIKA SOKO LA FOREX

Kuna aina mbalimbali za order katika soko la Forex ila za muhimu kuzifahamu ni:-

1. Market order/Instant order

2. Pending order

MARKET ORDER

Hii ni order ambayo unaifungua hili uweze kununua (buy) au kuuza(Sell) kwa bei iliyopo sokoni wakati

huo.Mfano umeenda dukani ukakuta kiatu kinauzwa elfu sabini bila hata ya kutaka punguzo au kusubili

bei ishuke unaamua kununua apoapo bei kama ilivyo utakuwa umefungua instant order ya

kubuy.(INSTANT ORDER)

PENDING ORDER

Hii ni order ambayo unaiweka sokoni kabla bei yako ya kuuza au kununua bado haijafikiwa ,hivyo

unakuwa kama unatega ili price ikifikiwa hiyo bei uliyoiweka basi order ifunguke na uingie sokoni.(order

zinakuwa zinaingia automatically katika soko)

Mfano,kama nyumba inauzwa milion 19 lakini wewe hautaki kununua kwa bei hiyo hivyo unasubiri bei

ikishuka na kufika million 15 ndipo ununue hivyo basi million 15 ni pending order yako ya kununua

nyumba hiyo.Mfano mwingine ni kama una gari unataka kuuza lakini bei unayoweza kuuza wakati huo

ni million 2 ambapo kwako wewe unaona sio stahiki hivyo unasubiri thamani ya gari ipande na ikifika

million 8 ndipo uuze hivyo basi million 8 ndio pending order yako ya kuuza gari.

AINA ZA PENDING ORDER

1. Buy stop

2. Sell stop

3. Buy limit
4. Sell limit

BUY STOP

Ukifanya analysis katika soko utagundua kuna fursa fulani inatokea katika soko. Au imeonesha dalili za

kutokea. Lakini sio mda wote utakuwa katika kioo chako cha kompyuta. Hivo unaweka pending order ya

kununua kama price itafika eneo fulani. Hivo utaweza kuendelea na shughuli zako kisha price ikifika pale

itajinunua na kukuingiza kwenye market.

SELL STOP

Ukifanya analysis katika soko utagundua kuna fursa Fulani ya kurudi chini(kushuka chini) inatokea katika

soko. Au imeonesha dalili za kutokea. Lakini sio mda wote utakuwa katika kioo chako cha kompyuta.

Hivo unaweka pending order ya kuuza(sell stop) kama price itafika eneo fulani. Hivo utaweza kuendelea

na shughuli zako kisha price ikifika pale itajiuza na kukuingiza kwenye market

BUY LIMIT

Hii ni order ambayo utaweka sokoni baada ya kufanya analysis na kuona kwamba price inashuka lakini

ikifika price flani itaanza kupanda hivyo basi unaweka BUY LIMIT katika price hiyo na mara baada ya

price kufikiwa order yako itafunguka na utakuwa umeingia sokoni kwa order ya kununua (buy).

SELL LIMIT

Hii ni order ambayo utaweka sokoni baada ya kufanya analysis na kugundua kuwa price inapanda lakini

ikifika price flani itaanza kushuka hivyo basi unaweka SELL LIMIT katika price hiyo na mara baada ya

price kufikiwa order yako itafunguka na utakuwa umeingia sokoni kwa order ya kuuza (sell).

AINA ZA KUFANYA BIASHARA.


Katika forex kuna aina mbili za kufanya biashara, hapa nitazielezea mbili za msingi ambazo wewe

ungependa kuchagua ni ipi itakuwa nzuri kwako.

1. Technical analysis

2. Fundamental analysis

TECHNICAL ANALYSIS

Huu ni aina ya uchambuzi wa soko kwa kuangalia mwenendo wa bei kupitia charts ambapo tunaangalia

jinsi bei (price) ilivyotembea wakati uliopita na tabia ilizoonesha na tunahusianisha na wakati huo

inavyotembea ili tuweze kutabiri/kutambua wakati ujao itaelekea wapi.

FUNDAMENTAL ANALYSIS

Huu ni ufanyaji wa biashara kwa kuliangalia soko kulingana na shughuli za kiuchumi,kisiasa na kijamii

ambazo hupelekea kuleta madhara katika suala zima la demand and supply

SUPPORT NA RESSISTANCE

Haya ni maeneo muhimu sana ambayo mfanyabiashara yoyote wa forex anatakiwa lazima

kuyajua. Support na Resistance ni maeneo ambayo ,price ya sarafu husika huwa na tabia ya

kugeukia mara nyingi hapo na hivyo wauzaji na wanunuzi kutafuta fursa ya kuuza au kununua

katika maeneo hayo.

Support - hili ni eneo ambalo bei(price) ya sarafu imefika katika kiwango chake cha chini na

pia ni maeneo ambayo wanunuzi pia hujiandaa kwa ajili ya kupandisha bei ya sarafu husika
kwenda juu.,na ni maeneo ambayo price imegusa kuanzia mara 2 na kuendelea na kugeuzia

hapo.

esistance - hili ni eneo ambalo bei(price) ya sarafu imefika katika kiwango chake cha juu na

pia ni maeneo ambayo wauzaji(sellers) pia hujiandaa kwa ajili ya kushusha bei ya sarafu husika

kwenda chini.,na ni maeneo ambayo bei imegusa kuanzia mara 2 nakuendelea na kugeuzia

hapo.

Jinsi ya kuchora Support na Resistance:

1. kwanza ni lazima ugundue mikunjo ya juu na chini, mikunjo ya juu ni resistance na mikunjo ya

chini ni support

2. weka mstari kwenye hiyo mikunjo ya juu ambayo tutaita resistance na weka mstari kwenye

mikunjo ya chini ni support.

3. hakikisha mstari wa juu unagusa kwenye candlestick zaidi ya moja, yani kuanzia mbili na

kuendelea na hata mstari wa chini pia ni lazima uguse kwenye candlestick zaidi ya moja kuanzia

mbili na kuendelea.

4. kama mstari wa juu utagusa candle moja na wa chini pia basi hapo tutasema resistance na

support haziko valid.

6. Ukishachora hiyo mistari ya support na resistance na ukahakikisha iko valid basi hapo ndio setup

yako itakua imekamilika now unasubiri entry point ifike ili uingie sokoni.

7. Sasa basi katika support na resistance entry point zetu huwa tunasubiri price iende juu ikagonge

kwenye hiyo line ya resistance then igeuze ianze kurudi chini kwa kuuza na kwenye support pia

hivyo hivyo tu nasubiri price igonge line ya chini na ianze kurudi juu ndipo hapo tunakaa tayari

kwa kununua.

8. Kitu muhimu ambacho unatakiwa ufanye wakati unataka kuingia sokoni kwakutumia support na
resistance ni kwamba, wakati price ipo kwenye support ikagonga na kugeuza kurudi juu,

unahesabu candle ya kwanza na yapili baada ya tatu ikianza unaingia hapo ndio uhakika kwamba

kweli price inapanda juu, na hata kwenye resistance pia unatakiwa usubiri hivyo hivyo yani ya

kwanza na yapili ikianza ya tatu tu unaingia sokoni

9. ila kuna wakati mwingine huwa kunakuaga na candle kubwa sana ambayo inanguvu kwenye

upande wa support ikiisha hiyo candle basi hainaaja ya kusubiri hadi zifike tatu coz kama

ikitokea kwenye support inamaanisha kunastrong bullish movement so ni kubuy tu baada ya

hiyo candle kuisha hadi kwenye resistance na ikitokea kwenye resistance basi ni kusell hadi kwa

support.

10. Pia ukishaingia sokoni basi ni lazima ujihami maana forex sio science kuna wakati unaweza

ukabuy katika sehemu sahihi ila ghafla soko likageuka na kurudi nyuma na kuendelea na safari

yake ya awali, hii huwa inatokea sana na ndio maana huwa tunashauriwa kutumia stop los

ambayo hii itatufanya tuwe salama zaidi hata kama soko likirudi nyuma litaishia kwenye SL yetu

na kutuacha na ela zetu za mtaji bado zipo.

support na Resistance hutumika kwa mtindo huu,

• Nunua (buy) wakati bei(price) inapofika kwenye eneo support,

• Uza(Sell) wakati bei(price) inapofika kwenye eneo resistance,

• Nunua (buy) wakati bei(price) imetoboa resistance na kupitiliza kwenda juu zaidi,

• Uza(Sell) wakati bei(price) imetoboa support na kuzidi kushuka chini.tutaona hapo ni

namna gani ikitoboa utakaiwa kuingia sokoni

MUHIMU;

1. Kama utaona bei(price) imefika maeneo ya support na resistance kabla ya kufanya


uamamuzi kuingia sokoni kununua au kuuza sarafu husika hakikisha umepata 'signal'

au alama ya kukuonyesha kuwa sasa bei inageuza .kuelekea unapotaka kuingia.

2. Support iliyotobolewa na bei(price) kuzidi kushuka chini zaidi hii hugeuka na kuwa resistance

mpya.

3. Resistance iliyotobolewa na bei(price) kuzidi kupanda juu zaidi hii hugeuka na kuwa support

mpya. Unaweza kuangalia mchoro hapo juu na kuona jinsi ambavyo resistance na support

hugeuka pale bei (price) inapotoboa na kuweka level mpya

SEHEMU YA PILI

CANDLESTICK PATTERN.

Candlestick patern ni moja ya kitu muhimu kutumia unapofanya analysis yako(kati ya kuuza au kununua)

kwasababu kitakupelekea kufanya maamuzi sahihi na kuleta matokeo chanya. CANDLESTICK pattern ni

lugha ambayo hutumiwa na wafanyabiashra wa forex(forex traders)endapo utajua kuitumia

vizuri:relaxed: itakusaidia kujua kujua soko linakutaka ufanye nini.

Kwa sasa nitaelekeza jinsi ya kuzitambua candlestic pattern na ujumbe unaotoa jinsi kuzitumia katika

kufanya biashara.

ENGULFING CANDLESTICS

Hii ni candlestic pattern ambayo inajumuisha candlestick mbili candlestick ya kwanza huwa fupi na
candle ya pili huwa ndefu kuzidi candlestick ya kwanza.

FOREX 7

Kuna aina mbili za engulfing

• BULLISH ENGULFING (BULLISH MOVEMENT)


FOREX 8

Hii ni aina ya pattern ambayo hutokana na kuwa na candle moja dogo ya sellers (wauzaji)

ikafuatiwa na candle kubwa moja ya wanunuaji (buyers), candle kubwa ya buyers umbo lake

huanzia chini kidogo ya candle ndogo ya sellers na kufungia juu ya candle hiyo ya sellers.

Pattern hii hutokea baada ya sellers (wauzaji ) kuanza kupoteza nguvu ya kuendelea kuwepo

sokoni na hivyo buyers(wanunuaji) kuanza kuchukua nafasi.

FOREX 9

Jinsi gani unaweza ingia sokoni na candle hii.?

1. Tafuta pattern hii ikiwa kwenye movement ya chini amabapo ni eneo la support

2. subiri candle inayofuata kufunga juu ya candle kubwa ya buyers ili kuhakiki

uwepo wa buyers(wanunuaji) sokoni. uhakiki huu ukitimia unaweza kuweka order zako

za kununua.katika soko na ukawa salama

• BEARISH ENGULFING (BEARISH MOVEMENT)

FOREX 10

Hii ni aina ya pattern ambayo hutokana na kuwa na candle moja dogo ya buyers(wanunuaji)

ikafuatiwa na candle kubwa moja ya wauzaji(sellers), candle kubwa ya sellers umbo lake

huanzia juu kidogo ya candle ndogo ya buyers na kufungia chini ya candle hiyo ya

buyers.Pattern hii hutokea baada ya buyers(wanunuaji) kuanza kupoteza nguvu ya kuendelea

kuwepo sokoni na hivyo sellers(wauzaji) kuanza kuchukua nafasi

FOREX 11

Jinsi gani unaweza ingia sokoni na candle hii.

1. Tafuta pattern hii ikiwa kwenye movement ya juu amabapo ni eneo la resistance

2. Subiri candle inayofuata kufunga chini ya candle kubwa ya sellers ili kuhakiki uwepo wa

sellers sokoni. uhakiki huu ukitimia unaweza kuweka order zako za kuuza sarafu
husika.katika soko na kuwa salama

DOJI CANDESTICK

Hii hutokea pale ambapo bei ya kuuza na kufungua imekuwa ni moja

INA ZA DOJI CANDLESTICK

• DRAGONFLY DOJI (BULLISH MOVEMENT)

Candle hii huonekana kama herufi ya T, hapa ni kuwa bei ya sarafu ya kufungua na kufunga ni

sawa,haina ule mwili kamili kama candlestick ya kawaida bali una mkia mrefu wa chini.

Maana halisi ya hili umbo ni nini?

wakati soko linapofunguliwa wauzaji(sellers) huvuta chini zaidi bei ya sarafu husika lakin baada

ya muda wanunuaji(buyers) huongeza nguvu zaidi kuipandisha bei ya sarafu hiyo juu,na

mwisho wanunuaji(buyers) hufanikiwa kuirudisha bei mahali ilipofungulia.

Jinsi gani unaweza ingia sokoni na candle hii.?

kwanza ili uweze kuingia sokoni kwa kutumia candle hii, hakikisha haya yafuatayo

1. Imetokea wakati bei ya sarafu husika iko uelekeo wa chini. (downtrend

movement(in support areas)), hivyo hutuashiria kuwa uelekeo wa soko unabadilika

kuanza kuelekea juu (bullish movement)

2. Subiri candle inayofuata baada ya dragonfly ifunge juu ya hii dragonfly ili kuhakiki

uwepo wa uelekeo mpya wa juu, ukishahakiki hivi unaweza kununua sarafu husika..

3. Jinsi mkia unavyokuwa mrefu zaidi,ndio uhakika zaidi wa wanunuaji kutawala

soko.

• GRAVESTONE DOJI (BEARISH MOVEMENT)


Candle hii huonekana kama herufi ya T iliyogeuzwa kichwa chini, hapa ni kuwa bei ya sarafu ya

kufungua na kufunga ni sawa,haina ule mwili kamili kama candlestick ya kawaida bali una mkia

mrefu wa juu.

Maana halisi ya hili umbo ni nini?

wakati soko linapofunguliwa wanunuaji(buyers) huvuta juu zaidi bei ya sarafu husika lakin

baada ya muda wauzaji (sellers) huongeza nguvu zaidi kuishusha bei ya sarafu hiyo chini,na

mwisho wauzaji(sellers) hufanikiwa kuirudisha bei mahali ilipofungulia.

Jinsi gani unaweza ingia sokoni na candle hii.?

kwanza ili uweze kuingia sokoni kwa kutumia candle hii, hakikisha haya yafuatayo

1. Imetokea wakati bei ya sarafu husika iko uelekeo wa juu. (uptrend movement (in

resistance area)), hivyo hutuashiria kuwa uelekeo wa soko unabadilika kuanza kuelekea

chini (bearish movement)

2. Subiri candle inayofuata baada ya gravestone doji ifunge chini ya hii gravestone

doji ili kuhakiki uwepo wa uelekeo mpya wa chini, ukishahakiki hivi unaweza kuuuza

sarafu husika..

3. Jinsi mkia unavyokuwa mrefu zaidi,ndio uhakika zaidi wa wauzaji kutawala soko

SHOOTING STAR (BEARISH MOVEMENT)

candle hii huonekana kama nyundo inayoning'inia hewani na mkia mrefu, hutokea wakati bei ya

sarafu husika iko kwenye uelekeo wa juu zaidi.candle hiz huwa zinajitengeneza upande wa

resistance kuashiria kuuza(sell)


Maana halisi ya umbo hili ni nini.?

Kama ilivyo kwa Gravestone Doji candle hii pia wakati soko linapofunguliwa wanunuaji(buyers)

hupandisha bei ya sarafu juu zaidi,lakini wauzaji(sellers) hupigania kurudisha bei chini,hivyo

kupelekea kutengenezwa kwa umbo la mraba. Jinsi mkia wa juu unavyokuwa mrefu zaidi basi

ndivyo inavyotoa uhakika wa sellers kuchukua nafasi zaidi.

Jinsi gani unaweza ingia sokoni na candle hii.?

1. imetokea wakati bei ya sarafu husika iko kwenye uelekeo wa juu (resistance )

2. subiri candle inayofuata ifunge chini ya hii shooting star ili kuwe na uhakika zaidi

wa sellers(wauzaji) sokoni, ikitokea hivi basi unaweza kutafuta nafasi ya kuingia sokoni

kuuza.

HAMMER (BULLISH MOVEMENT)

Candle hii huonekana kama pipi ya kijiti ya mraba au nyundo, huwa na umbo dogo sana ambalo

husababishwa na bei ya kufungia kuwa juu kidogo au chini kidogo ya bei ya kufungulia.

Maana halisi ya umbo hili ni nini.?

Kama ilivyo kwa Dragonfly doji candle hii pia wakati soko linapofunguliwa wauzaji(sellers)

huvuta bei ya sarafu chini zaidi,lakini wanunuaji(buyers) hupigania kurudisha bei juu,hivyo

hufanikiwa kuirudisha juu kidogo au chini kidogo ya bei ya kufungulia.

Jinsi gani unaweza ingia sokoni na candle hii.?

1. Imetokea wakati bei ya sarafu husika iko uelekeo wa chini. (downtrend

movement(in support), hivyo hutuashiria kuwa uelekeo wa soko unabadilika kuanza

kuelekea juu (bullish movement)

2. Subiri candle inayofuata baada ya hammer ifunge juu ya hammer ili kuhakiki

uwepo wa uelekeo mpya wa juu, ukishahakiki hivi unaweza kununua sarafu husika..

3. Jinsi mkia unavyokuwa mrefu zaidi,ndio uhakika zaidi wa wanunuaji kutawala


soko.

HARAMI.

Hii ni candlestic pattern ambayo inajumuisha candlestick mbili candlestick ya kwanza huwa kubwa

aundefu na candle ya pili huwa ndogo kuliko ile candlestick ya kwanza.

Jinsi gani unaweza ingia sokoni na candle hii.?

1. Tafuta pattern hii ikiwa kwenye movement ya chini amabapo ni

eneo la support

2. subiri candle inayofuata kufunga juu ya candle ndogo ya buyers ili

kuhakiki uwepo wa buyers(wanunuaji) sokoni. uhakiki huu ukitimia

unaweza kuweka order zako za kununua.katika soko na ukawa

salama

3. Tafuta pattern hii ikiwa kwenye movement ya juu amabapo ni

eneo la resistance

4. subiri candle inayofuata kufunga chini ya candle ndogo ya sellers

ili kuhakiki uwepo wa sellers sokoni. uhakiki huu ukitimia unaweza

kuweka order zako za kuuza sarafu husika.katika soko na kuwa

salama

6.HANGING MAN

huonekana kama pipi ya kijiti ya mraba au nyundo, huwa na umbo dogo sana ambalo

husababishwa na bei ya kufungia kuwa juu kidogo au chini kidogo ya bei ya kufungulia.

Maana halisi ya umbo hili ni nini.?

Candle hii ni wakati soko linapofunguliwa wanunuji(buyers) huvuta bei ya sarafu juu zaidi,lakini

wauzaji(selers) hupigania kurudisha bei chini,hivyo hufanikiwa kuirudisha chini kidogo au juu

kidogo ya bei ya kufungulia.

Jinsi gani unaweza ingia sokoni na candle hii.?


- wakati bei ya sarafu husika iko uelekeo wa juu. (uptrend movement(in ressistance),

hivyo hutuashiria kuwa uelekeo wa soko unabadilika kuanza kuelekea chini (bearish

movement)

- Subiri candle inayofuata baada ya hanging man ifunge chini yake ili kuhakiki uwepo wa

uelekeo mpya wa chini, ukishahakiki hivi unaweza kuuza sarafu husika..

- Jinsi mkia unavyokuwa mrefu zaidi,ndio uhakika zaidi wa wauzaji kutawala soko.

INVERTED HAMMER.

candle hii huonekana kama nyundo inayoning'inia hewani na mkia mrefu, hutokea wakati bei ya sarafu
husika iko kwenye uelekeo wa chini zaidi.candle hizi huwa zinajitengeneza upande wa support kuashiria
kununua(kubuy)

Maana halisi ya umbo hili ni nini.?

candle hii pia wakati soko linapofunguliwa wauuzaji(sellers) hushusha bei ya sarafu chini

zaidi,lakini wanunuaji(buyers) hupigania kurudisha bei juu,hivyo kupelekea kutengenezwa kwa

umbo la mraba. Jinsi mkia wa juu unavyokuwa mrefu zaidi basi ndivyo inavyotoa uhakika wa

wanunuaji(buyers) kuchukua nafasi zaidi.

Jinsi gani unaweza ingia sokoni na candle hii.?

- imetokea wakati bei ya sarafu husika iko kwenye uelekeo wa chini (support )

- subiri candle inayofuata ifunge juu ya hii inverted hammer ili kuwe na uhakika zaidi wa

wanunuzi (buyers) sokoni, ikitokea hivi basi unaweza kutafuta nafasi ya kuingia sokoni

kununua.

SPINNING TOP

Hii ni candlestick moja yenye umbo dogo na mkia mrefu juu na chini. Ikitokea katika ya eneo la

RESISTANCE na SUPPORT huashiria kubadilika kwa trends,

You might also like