Kiswahili Uace PP3

You might also like

Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 3

P320/3

FASIHI YA
KISWAHILI
Paper 3
3 Hours

WAKISO MUSLIM DECONDARY SCHOOL


Uganda Advanced Certificate of Education

FASIHI YA KISWAHILI (RIWAYA)

Karatasi ya Tatu

3 HOURS

MAAGIZO;
• Jibu maswali Matatu tu. Chagua swali moja kutoka sehemu ya A, B, CH.
• Sehemu B ni ya lazima kwa wanafunzi.
• Usijibu swali zaidi ya moja kutoka kitabu Kimoja wala maswali mawili kutoka kitabu
kimoja.

1|Page
SEHEMU A:
UTENGANO: Said A Mohamed
1. Bwana Maksuudi mwenyewe ndiye chanzo cha utengano katika jamii yake. Jadili
(Alama 33)
2. (a) Mwanamke ameathirika vipi kutokana na migogoro ya kifamilia? Eleza ukirejelea
mifano mwafaka katika riwaya ya Utengano. (Alama 18)
(b) Eleza njia mbalimbali wanazotumia wanawake katika kupigania haki zao katika
riwaya ya Utengano (Alama 15)
SEHEMU B
BARAKA ZA MAMA: VICENT T MUHEREZA
5. Soma dondoo hili na kisha ujibu maswali yatakayofuata hapo chini yake;
Nilimkodolea macho hadi alipotokomelea upande wa VIP alikoingia chini ya ulinzi mkali wa
askari waliomzunguka kila pembe kiasi mwenyewe hangepata nafasi hata ya kuyatemea mate.
“Sasa Ni Waziri Wa Biashara!” nilishangaa. Nilijiliwaza kwa kujiambia kuwa subira huvuta
heri. Jambo lililonipendeza katika kazi yangu lilikuwa kutazama ndege zilizotua huku nyingine
zikipaa mithili ya panzi katika mwezi wa mshenene kama ulivyorejelewa na maheremu
mamangu katika enzi za uhai wake. Ndege zile zilinipa mawazo kwamba ni wengi wazitumiao
tofauti na fikira za kitoto tulizokuwa nazo tukiwa kijijini kwamba kila ndege ionekanayo angani
huwaimembeba rais. Niliukumbuka wimbo wetu katika enzi zetu za utoto tuliouimba huku
tukipungia mkono ndege tulizoamini zilimbeba rais wetu.
Bye bye Museveni
Bye bye Museveni
Bye bye Museveni
Nilitabasamu mwenyewe nilipokumbuka wimbo huo. Tofauti na kazi nilizofanya awali, ile kazi
ya kituo cha ndege ilinilipa vizuri kiasi kwamba katika miezi mitano ya kwanza niliweza
kujinunulia shamba la kahawa pamoja na kuijenga nyumba ya kifahari kijijini Rutooma baada ya
miaka mingi ya uchochole. Matunda ya kazi niliyoifanya yalianza kujionyesha wazi.
Nisingethubutu kuikwepa kazi hata iwe ni siku moja kwa vile ingemaanisha hasara ya elfu mia
moja siku hiyo tu. Ningerauka asubuhi na mapema iwezekanavyo, nipige mguu hadi kazini
umbali wa kilomita moja hivi kati ya eneo la Minister’s village nilikoishi, na kituo cha ndege
nilikofanya kazi. Katika chumba kikubwa nilimoishi peke yangu, ningejionea fahari mwenye

2|Page
kupiga hatua kubwa kimaisha. Hatua ambazo ningeweza kulinganisha na kunusurika kifo. Kwa
kiwango hicho, kijijini nilianza kutambulika. Waliokuwa hawanifahamu kwa sura, walilijua jina
langu. Nadhani waliulizana,”Humjui Yule mwanawe marehemu Mariamu? Yule mwenye
nyumba nzuri ya kisasa?”
Maswali
a) Weka dondoo hili katika muktadha wake (alama 08)

b) Mwandishi alitumia tamathali au mbinu gani katika dondoo hili? (alama 08)

c) Dondoo hili linatilia nguvu maudhui gani? Fafanua (alama 08)

d) Unapata taswira gani kutokana na wimbo wa mwandishi wa ‘Bye bye Museveni’ kama
ulivyotumika katika dondoo hili? (alama 04)
e) Ni mafunzo yapi upatayo kutokana na dondoo hili? (alama 06

SEHEMU CH:
UHASAMA KILIMANI: George Black Masereka
11. (a) Jadili sababu zilizosababisha wanajamii wa ufalme wa Bunyangabo kuupinga uongozi
wa mfame kamanzi na maliwali wake. (Alama 15)
(b) Jadili njia tofauti anazotumia mhusika Mbaka Lututu kuondoa uongozi mbaya katika Riwaya
ya Uhasama kilimani. (Alama 18)
12. (a) Eleza mivutano inayowakabili wanajamii wa riwaya ya Uhasama Kilimani. (alama 18)
(b) Tambua wasifu wa Mhusika Mbaka Lututu katika riwaya hii. ( Alama 15)
MWISHO

3|Page

You might also like