Kiswahili Uace PP2

You might also like

Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 3

P320/2

FASIHI YA
KISWAHILI
Paper 2
3 Hours
WAKISO MUSLIM DECONDARY SCHOOL
Uganda Advanced Certificate of Education
FASIHI YA KISWAHILI (TAMTHILIA)
Karatasi ya pili
3 HOURS

MAAGIZO;
Jibu maswali Matatu tu. Chagua swali moja kutoka sehemu ya A, B, CH.
Sehemu B ni ya lazima kwa wanafunzi.
Usijibu swali zaidi ya moja kutoka kitabu Kimoja wala maswali mawili kutoka kitabu
kimoja.

Fungua

1|Page
SEHEMU A
MFALME EDIPODE NA SOFOKILE
1. Imani ya miungu na utabiri ndiyo maudhui ya pekee aliyoyashughulikia Sofokile katika
tamthilia ya Mfalme Edipode. Jadili. (alama 33)
2. Fafanua sifa za wahusika wafuatao katika tamthilia ya Mfalme Edipode. (alama 33)
i. Edipode
ii. Jokasta
iii. Laio
iv. Apollo

SEHEMU B
KILIO CHA HAKI NA ALAMIN MAZRUI
3. “Kilio ni maudhui ya pekee katika tamthilia ya kilio cha haki.” Jadili (alama 33)
4. Fafanua sifa za wahusika wafuatao katika tamthilia ya kilio cha haki (alama 33)
i. Bwana Delamon
ii. Tereki
iii. Lamina
iv. Mwengo

SEHEMU CH
MIZIGO: JOHN RUGANDA

5. Soma dondoo lifuatalo kisha ujibu maswali yaliyo hapo chini; (alama 34)

TINKA: Hamwoni ni lazima tuondoke? Sikiliza, hata Mimi sipendi kuondoka hapa ila inanilazimu.
Tafadhali nipeni amani, msinitese. Watu hawaishi pahali pamoja milele.Mtapokuwa watu
wazima mtakuja kuelewa halikuwa kosa langu. Mungu ni shahidi wangu .Nilijaribu
kuvumilia tabu za aina nyingi . Nyinyi hamwezi kuelewa tabu hizo.Nilijaribu kutimiza
wajibu kadiri nilivyoweza.
KAIJA: Lakini , mama , tumepazoea pahali hapa.
TINKA: Ninafahamu. Ninafahamu sana. Si makosa yangu. Wakija kufahamu haya ,hakuna
atakayenilaumu.
KAIJA: Kulitokea nini, mama?

Fungua
2|Page
TINKA: Nanyi mtakapokua mkumbuke kuwa nilisema ninayajutia .Nisingeweza kuvumilia zaidi.
(Tinka analia kwa sauti ya chini)
KAIJA: Mama, kulitokea nini?
NYAKAKE: Ni nini, mama?
TINKA: Msiniulize maswali. Mtanitia kichaa.
KAIJA: Usiwe na shaka mama, tueleze tu.
TINKA: Mungu wangu ! Nimekosa nini? Nimekosa nini?
KAIJA: Tuamini,mama.Hivi , huwezi kutuamini?
NYAKAKE: Kulitokea nini?
TINKA: Watakuwa wema kwenu , wanangu wapendwa. Watawatunza vizuri huko katika makao ya
watoto mayatima.
KAIJA NA NYAKAKE: Makao ya watoto mayatima!
TINKA: Ikiwezekana nitakuwa nikija kuwatembelea.
NYAKAKE: Maskini baba .Baba yuko wapi? Baba, baba.
TINKAV: Ameenda kwenye mazishi…ameenda, ameenda na hatutamwona tena. Ametutupa mkono.

Maswali;

a) Eleza mafunzo unayoyapata kutoka dondoo hili. (alama 10)


b) Taja na uelezee maudhui yanayotiliwa nguvu na dondoo hilo. (alama 06)
c) Ni mbinu gani za lugha zinazopatikana katika dondoo hilo? (alama 03)
d) Eleza chanzo na matokeo ya mgogoro baina ya Tinka na Wamala. (alama 05)
e) Eleza sifa za wahusika wanaopatikana katika dondoo hili. (alama 10)

MWISHO

3|Page

You might also like