Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 17

TAASISI YA ELIMU YA WATU WAZIMA

DAR ES SALAAM
KOZI: SHAHADA YA ELIMU YA WATU WAZIMA NA MAFUNZO

ENDELEVU

MWAKA WA MASOMO: 2013/2014 MWAKA WA PILI

MODULI: KUCHAMBUA NADHARIA ZA UHAKIKI

MSIMBO WA MODULI: KIU 07431

MWEZESHAJI: MWALIMU KILEO

AINA YA KAZI: KAZI YA KIKUNDI NAMBA TATU

WASHIRIKI KATIKA KAZI:-

1. SADI ISSA
2. TESHA ANTUSA
3. MLINGWA AGNESS
4. MASIMBA SHABANI R.A.
5. HABIBU ABASSI
6. MSHANA EMELINE
7. KISHIMBWE HALIMA
8. GODFREY RENATUSI
9. HAMISI SHABANI

SWALI:

Uhakika wa Fani katika Kitabu CHA KILIO CHA HAKI.


UTANGULIZI

“KILIO CHA HAKI” ni Tamthilia iliyoandikwa na Alamin Mazrui (1981). Tamthilia hii
inaelezea mapambano baina ya wafanyakazi na udhalimu wa makaburu. Tamthilia hii ina sawiri
mapambano ya nchi nyingi za kiafrika kutaka kujikomba kutoka kwa watawala wa kikoloni.

Katika tamthilia hii mwandishi amemchora mwanamke jasiri aliyejikomboa kimawazo na ndiye
aliyekua kiongozi wa mapambano na anadhihirisha udhalimu wa jamii yake unaowapata
wafanyakazi kwa Mwanamke huyu.Alifaulu katika kuwazindua wafanyakazi wenzake ili
wapambane na udhalimu na watetee haki zao. Mapambano haya yanaleta mwamko wa kisiasa
ambao ndio mwanzo wa matayarisho ya vita vilivyoikomboa nchi nzima kutoka na ukoloni.

UHAKIKI WA TAMTHILIA KILIO CHA HAKI

FANI

Kutokana na Gerald Njagi Matti. (2001).Introduction to the study of literature.

“Fani ni ufundi wa mwanafasihi anaoutumia katika uandishi wa kazi yake, ili aweze kufikisha
ujumbe wake kwa wasomaji wake. Katika uchambuzi wa tamlithiliya hii vipengele vilivyo
chambuliwa ni muundo, mtindo, lugha, wahusika, mandhari, maleba, vifaa, matumizi ya
jukwaa, jina la kitabu, kufaulu na kutofaulu kwa mwandishi.

MUUNDO

Muundo uliotumika ni wa rejea kwani kuna mwingiliano wa matukio na mchanganyiko


wamatukio,matini au mchanganyiko msimbo (code mixing).

Msanii AlaminMazrui aliandika tamthiliya hii katika maonyesho kumi, kama ifuatavyo:-
Onyesho la kwanza ukurasa wa kwanza hadi kumi na nne.

Mussa na Dewe wanasoma taarifa toka gazetini zinazo eleza kuwa Kamishina Hunderson
amemkamata Lanina wa Muyaka kwa tuhuma za mauaji ya watu watatu kwenye shamba la
Bwana Delamon.

Onyesho la pili ukurasa wa kumi na tano hadi ishirini.

Lamina kwa mara ya pili tena anahojiwa na makechero kwenye kituo cha polisi kuhusina na
mauaji ya watu watatu kwenye shamba la Bwana Delamon.

Onyesho la tatu ukurasa wa ishirini na moja hadi ishirini na nane.

Lanina anawajibu makachero kuwa Delamon na wenzake hawakuja kutunufaisha bali kuja
kunyonya nchi yetu ukurasa wa 24.

Onyesho la Nne (uk 29-36)

Lanina alirudi nyumbani lakini alikutana na lawama za mume wake Bwana Mwengo kwa
kumuachia familia kwa muda mrefu. Hata hivyo walisamehana na kutaka waendelee
kushirikiana.

Onyesho la Tano (uk 37-42)

Lanina anakutana na wazazi wake kijijini,baba yake anamlaani na hata kuwapiga yeye na mama
yake kwa sababu Lanina hafuati mila na desturi za kwao na mama yake ndiye aliyepewa
kumfunza.

Onyesho la Sita (uk 43-48)

Hapa wasaliti Matovu, Tereki naPelekha wanajifariji na kuwaona akina Musa na Dewe na
Lanina kuwa ni wajinga, kwa kukataa msamaha wa Bw. Delamon.

Onyesho la Saba (uk 49-55)

Wasaliti hawa wana washawishi Lanina arudi kazini kwa vile wameruhusiwa kuendesha
shughuli za siasa na mshahara unapanda juu kidogo. Lanina anakataa na kuwafukuza nyumbani
kwake.
Onyesho la Nane (uk 56-65)

Lanina yupo kwenye kioski cha mzee Ingeli. Musa, Dewe na Lanina wanakutana kupeana taarifa
kuwa eti Delamoni ameruhusu kuanzisha chama na kumruhusu kurudi kazini.

Onyesho la Tisa (uk 66-72)

Katika ofisi ya Bwana Delamoni wamesikia Sauti za wafanyakazi za waliokuwawanaimba


nyimbo za siasa.

Onyesho la Kumi (uk 73-77)

Hapa Lanina akiwa gerezani anakutana na Askari Malaya aliyekuwa anamtongoza Lanina, lakini
Lanina anamkatalia na kumpiga teke sehemu zake za siri, pia Lanina anaitwa na jaji na
kumsikiliza maelezo yake, uk 77.

MTINDO

Katika tamthilia hii mwandishi ametumia mtindo wa mwingiliano matini ambapo ameonyesha
mambo mabalimbali yaliyounda kazi hii ya fasihi. Mfanonidialojia, hapa mwandishi aneonyesha
mazungumzo mbalimbali ya wahusika wakijibizana.

Matumizi ya gazeti, pia mwandishi ametumia gazeti lengo lake ni kusambaza habari kwa watu,
hata wale waliogerezani, pia kuonyesha kuwa baadhi ya wahusika ni wasomi, na matumizi ya
gazeti yameonyeshwa katika uk 1 na 2.

LANINA KUPELEKWA MAHAKAMANI

Lanina wa Muyuka, mwanamke aliyekuwa mfanya kazi katika shamba maarufu la Bwana
Delamon, ametiwa tena kizuizini.

Pia alitumia lugh ya ushairi. Pia mwandishi ametuamia lugha ya ushairi katika uk 62.

 Ari yetu ndio mwokozi wetu


 Ari yetu lazima tuisujudie,
 Ari hii ya mwaka tuliyoivumbika,
 Iliyojaa joto lisiloburudika
 Ije ituongoze mpaka mwisho kufika,
 Na kutuzimia kiza cha mwaka

Pia matumizi ya simu.Pia yamejitokeza katika tamthiliya hii ya Kilio cha Haki, pale ambapo
Shindo alipompigia simu kamishna Hunderson. Lengo ni kuonesha uhalisia wa kimazungumzo.

Shindo:- “Eee….halo ka….ka…..kamishina Henderson yup…….yupo? wap…. “uk 67.

Uchanganyaji msimbo (code mixing); pia mwandishi wa KILIO CHA HAKI ametumia lugha ya
kuchanganya, kama vile Kingereza na Kiswahili, lengo lilikuwa kuonyesha katika matini
palikuwepo na watu tofauti kama vile wazungu na waswahili. Mfano katika uk 10.

Delamon:- (kwa hasira)

Coming Sir! Coming Sir!

Kwanini hamtafuti maboi wenye akili zaidi,

Foolish baboons!

Kimbo: Yes…Sa……

Delamon: nenda kamwite……..aaa…….aaa……

Matumizi ya lugha ya matusi, wa mfano Lanina aliyekuwa akitukanwa na baba yake

MATUMIZI YA LUGHA

Lugha ni ufundi anaotumia mwandishi katika kuandika kazi yake. Ni sifa za kipekee mfano.
Misemo, methali tamathali za semi kama takriri na tashibiha.

NAHAU/MISEMO
Kutokana na Gerald Njagi Matti. (2001). Anasema Nahau ni misemo iliyojegwa kwa kutumia
maneno ya kawaida lakini huwa imesitiri maana tofauti iliyobeba maneno katika hali ya
kawaida.

Katika tamthiliya hii mwandishi ameipamba kazi yake kwa kutumia misemo na nahau kama
ifuavyo:-“Mhitaji ni mtumwa” uk 24. Msemo huu ulijitokeza pale ambapo kachero wa pili
alipomwambia Lanina anyenyekee kwa sababu inaonyesha kuwa unapokuwa na shida lazima
unyenyekee.

Msemo mwingine ulijitokeza pale mama yake Lanina alipokuwa anamwambia mwanawe.
“Mkosa chema haachi kuguna” uk 37. Pia aliendelea kusena “Jicho la hasidi lisimkumbe” uk 37
hapa mama Lanina alikuwa anamwombea mwanawe dua.

“Huyu ni punda tu asiyekuwa na fadhila!” uk 38 msemo huu ulitumiwa na Baba yake Lanina
akimtaka asimsalimie na wala asimwite Baba kwani si Baba yake kutokana na tabia yake.

METHALI

Ni misemo inayotumiwa kuelezea kitu kwa njia ya picha, na kwa ufupi ili itoe maadili au
maonyofulani, methali huwa na sehemu mbili saehemu ya kwana husemwa na mshauri na ya pili
hukamilishwa na mshauriwa. Humfanya msikilizajiawe katika hali ya kufikiri, kuchambua na
kupatanisha ukweli, na hali ili ajue maana ya ndani iliyokusudiwa.

Katika tamthiliya hii ya “KILIO CHA HAKI” mwandishi ameipamba na kuipendezeasha kazi
yake kwa kutumia methali mbalimbali. Mfano katika ukurasa wa 27” ametumia methali “Hasira
hasara” mwandishi ametumia methali hii pale Matovu na Tereki walipokuwa wakimshauri
Lanina akubali kurejea kazini. Hivyo methali hii katika jamii yetu, inatufundisha kuwa tufikiri
kuona ndipo tujue maamuzi.

Methali nyingine ni “Dalili ya mvua ni mawingu” uk 36 pale baba Lanina alipokuwa anaongea
na mama yake Lamina kuhusu mabadiliko ya Lanina na minong’ono ambayo inasemwa kijijini
kuhusu Lanina.

Pia mwandishi ametumia tamathali za semi mbalimbali. Tamathali za semi ni maneno au


sentensi ambazo hutumiwa na wasanii wa fasihi ili kutia nguvu katika maana, mtindo na hata
sauti katika maandishi ama usemi, Tamathali hutumiwa kuipamba na kuongezea utamu katika
lugha ya fasihi. Kuna aina nyingi za tamathali za usemi baadhi yake ambazo zimejitokeza katika
tamthilia ya KILIO CHA HAKI ni:-

TASHIBIHI

Kutokana na Gerald Njagi Matti. (2001). Anasema tashibiha hutumika kulinganisha kitu kimoja
au zaidi kwa kutumia viunganishi kwa mfano. (Kama, mithili ya).

Mfano:- Nyinyi ni kama punda msiyojua fadhila. UK 22 alisema kachero wa kwanza kwa
Lanina pale walipomtia kizuizini.

 Anajikunyata kama anayesikia baridi uk 28 hii ni sauti ya msimuliaji ilisikika kutoka nje
 Nchi zetu ni kama jaa la bidhaa zinazowazidia uk 24, aliongea Lanina akiwambia
kachero wa kwanza na wa pili.
 Kimya kama hayawani uk 76, Lanina alikuwa akijisemea mwenyewe. Hii ina maana
kuwa kunyamaza kama kayawani ni kama kuwa mwendawazimu au mtu
aliyechanganyikiwa na mambo.

TAKRIRI

Ni kujirudia kwa maneno au sauti. Katika tamthilia hii takriri zilizotumika ni kama ifuatayo

 “Ndiyo ndiyo uk 16. Hii ina maana kuwa mwandishi alikuwa anakubaliana na jambo hilo
lakini kwa mashaka.
 ………….. na …………… nauk 16 na uk 17
 Kufikiria! Kufikiria! Uk 19
 Halafu! Halafu uk 29
 La! La! La! Uk 22
 Lamina! Lamina! Uk 29
 Tafadhari Tafadhari uk 42
 Twende! Twende! Nikakupeleke kwa shangazi yako akakufundishe kumtii bwana wako uk.
42.
Alisema baba Lanina akimueleza mkewe.
 Haya sema ulilonalo! Sema basi, sema na mimi nisikilize sema! Uk 30
 Mwengo aliongea akimwambia mkwewe Lanina.
 “Yawache yachache Dewe yawache yachache”
yawache yachache”
Alizungumza musa uk 4
 Lamina! Lamina!
Wakili alimuita Lanina uk 76

MDOKEZO

Ni kauli ambazo hazimalizii jambo au ni tamathali ambazo hudokeza kitu Fulani na kukiacha
bila kukimalizia au kukikamilisha kwa maana kwamba kinaweza kukamilishwa na mtu
mwingine kisanaa.

Mfano

 Usijali tutapata tu karibu………….. uk 1. Hapa mwandishi anajaribu kuonyesha matumaini


kuwa Dewe na mwenzake Mussa wangeruhusiwa kurudi nyumbani kwao.
(Alisema Dewe)
 “………… maharamia hawa wasio heshimu sharia……..”
Alisema Dewe uk 4
 “Nenda kamwite ……aaa…aaa…. Uk 10
Alisema Delamon.
 “Sasa tunaweza kuzungumza kama” uk 11 (alisema Delamon)
 “Afrika…. Tamaa ya mtu mweusi” Uk 5
Alisema Dewe
 Sisi wenyewe lakini…………
(Aliongea Delamon) uk 9
 Maneno usemayo ni mazuri bwana Delamon na tunayaelewa vyema.
Lakini…..lakini…...tukiwa tunataka……..
 Naam…..Basi labda mnayaweza (alisema Delamon)UK 12
 Ninyi ndio washenzi mnao…..mnao….Uk 12 (alisema Zari)
 Aaaa….rafiki zangu…..kusena kweli...kwa hakika….sifahamu kwa nini(Delamon Uk 13)

SITIARI

Sitiari hulinganisha vitu au watu bila kutumia viunganishi. Hulinganisha vitu kama vinafanana
kabisa.

Katika riwaya hii mwandishi ameweza kuipamba kazi yake kwa kutumia sitiari mbalimbali.

Mfano:“Mimi ndiye simba” Uk 32 hapa baba yake lanina alikuwa na maana ya kuwa yeye ndiye
mkuu wa familia akiomgea kitu hakuna wa kumpinga.

Mfano “Huyu ni punda tu asiyejua fadhila Uk 38 hapa tumemuona baba Lanina alikuwa
akimwambia mwanawe Lanina. Akimaanisha mwanawe hana shukrani maana shukrani ya punda
ni mateke.

Mfano “Siasa ni mchezo mchafu”Uk 76.Hapa mwandishi amelinganisha siasa na mchezo


mchafu, kama vile kufungwa gerezani na kuaibishwa mbele za watu.

TASHIHISI

Ni kuvipa vitu uwezo wa kufanya jambo anbalo halina uwezo au sifa ya kufanya jambo tofauti
na uwezo wa kibinadamu.

Mfano: mzee alisema:

 “Kwa nini ewe bara la Afrika


 Ewe nchi uliyepambwa kwa weusi
 Ewe roho wa kizazi chetu
 Tukutilieje mbolea siku baada ya siku
 Kwa kutaraji utatuzalia
RIDAA.

Kutokana na Gerald Njagi Matti. (2001). Anasema ridaa ni misemo ambayo kuonyeshwa
kushangazwa kwa jambo fulani. Misemo hii huambatana na matumizi ya alama za mshangao
katika kukubali jambo, kuchukia au kuonyesha heshima maalumu.

Mfano:

 Na malalamiko yatapungua!” Uk 15 alisema shindo


 “Tafadhali usinifanyie uhuni huo!” alisema Lanina Uk 25
 “Mimi si Malaya” alisema Lanina Uk 25
 “Aaa! Ni hilo tu Lanina” Uk 25 (alisema kachero)
 “Lanina! Tereki!” (alisema kachero) Uk 26
 “Ewe twende tukalale mama eh!” alisema Lanina Uk 30

WAHUSIKA

Kutokana na Gerald Njagi Matti. (2001). Anasema mwandishi Alamin Mazrui wa tamthilia ya
KILIO CHA HAKI amewatumia wahusika kwa kuwagawa katika makundi mbalimbali ambayo
ni wahusika wakuu, wahusika wasaidizi na wahusika mviringo.

MHUSIKA MKUU

Mhusika nkuu katika tamthilia yaKILIO CHA HAKIni Lanina. Alamini Mazrui alimtumia
Lanina kwa kutumia nadharia ya ufeministi. Lanina amekuwa mwanamke aliyepigania haki na
ukombozi wa mwanamke pamoja na kutetea maslahi ya wafanyakazi wenzake. Hivyo alisimama
kidete bila kukata tamaa katika kupigania haki pamoja na kuwa alipata mateso na manyanyaso
mbalimbali hadi kufikia hatua ya kuwekwa kizuizini.

Mfano
Katika ukurasa wa 14 anasema

“Lakini sisi tunajaribu kutetea haki zetu……”

Askari anampiga kofi na kusema wacha upuuzi wako huo. Haki! Haki unapigania kitu hata hujui
ukipewa utafanyia nini?

Pia Lanina ni mama wa watoto wawili yaani Dida na Badi.

Hii inadhihirika pale ambapo Lanina alipokuwa akimpapasa mwanawe Dida

“Pole Dida mwanangu.

Nimesharudi sasa hivi.uk 30

Wasifu mwingine wa Lanina ni mke wa Mwengo. Hii inadhihirika pale ampapo Mwengo
alipokuwa akiongea na Lanina.

Mimi ni mume wako ala!Umesahau? Kwa nini hunijibu? Kwa nini umenipuuza namna hii?

DELAMON

Huyu ni mhusika mkuu pia kwani ameonekana tangu mwanzo wa matukio katika tamthiliya hii
hadi mwisho. Hapa mwandishi ametumia nadharia ya ubada (ukoloni) akiwakilisha jinsi
wakoloni walivyo wagandamiza wafanyakazi wa kiafrika kiuchimi.

Hii imejitokeza katika ukurasa wa 13 pale ambapo Lanina anamjibu Delamon kwa hasira “…..
nyingi hamkuja hapa kwa manufaa/faida yetu…… mmekuja kwa maslahi yenu
wenyewe………… uk 13.

Pia Delamon ni mmiliki wa shamba kwa maana nyingine ni mnyonyaji,

Hii inajidhihirisha katika onyesho la 6

“Katika shamba la Delamon wakati wa mapunziko. Tereki, matuvu, Dewe, Mussa na mfanyakazi
mwingine wanatokeza wamevaa nguo za kazi. Uk 43.

WAHUSIKA WASAIDIZI
Mwandishi amewagawa wahusika wasidizi katika makundi mawili, ambayo ni wale wenye
msimamo wa nadharia ya Ki-Marx na wale wasaliti. Nadharia hii ya kimary huonyesha wahusika
wa kimaendeleo, pia huonyesha matumaini ya juu ya kizazi cha binadamu (tabaka fulani lina
kandamizwa lakini linaonyesha matumaini)

Wahusika aliowatumia kwa nadharia ya Ki-Marx ni Mussa na Dewe ambao walishirikiana na


Lanina katika harakati za kuwakomboa wafanyakazi ili kupata maslai yao ya kazi. (katika
ukurasa wa 2).

“Mussa (kwa hasira) “wasikilize wapumbavu hawa! Ati Lanina amechochea mgomo

Lanina hata hakuwepo siku ya mgomo.

Lanina, Dewe na Mussa walikuwa watu wenye msimamo, hawakukata tamaana waliendelea na
mapambo hadi mwisho katika uk 62 pale Lanina alivyokuwa anaonge na Mussa na Dewe.

“Ndugu zangu, ari yetu ndiyo mwokozi wetu, ari yetu lazima tuisujudie

Isitoshe walipenda maendeleo kwa sababu walikuwa wanapinga kunyanyaswa na kuonana na


makaburu uk 14.

“Lakini sis tunajaribu kutetea haki zetu tu kama….”

Mhusika mwingine ni baba Lanina, amechorwa na mwandishi kama mfuasi wa mfumo dume na
kuona kuwa mwanamke hawezi kutetea haki wala kufanya mapinduzi, ukurasa wa 38.

Baba akionyesha yenye ndiye msemaji wa mwisho.

“Mimi ndiye simba wa nyumba hii ningurumapo sitaki kuzisikia sauti zenu za kijinga hapa
(Akimgeukia Lanina)

Na wewe binti ya shetani?

Mimi si wale wanaume wengine unaochezeachezea. Mimi si kina Mwengo mimi ni dume kweli
kweli umesikia hivyo!

 Mtu katili
 Hafai kuigwa katika jamii
JUKWAA

Onyesho la Kwanza (uk 1-14)

Mussa na Dewe wanasoma taarifa tokea gazetini zinaeleza kuwa kamishina Hunderson
amemkamata Lanina wa Muyake kwa tuhuma ya mauaji ya watu watatu wenye shamba la bwana
Delamon.

Onyesho la Pili (uk 15-20)

Lanina anawajibu makachero kuwa Delamon na wenzake hawakuja kutunufaisha bali kunyonya
nchi zetu.

Onyesho la Nne (uk 29-36)

Lanina karudi nyumbani lakini amekutana na lawama za mume wake Bwana Mwengo kwa
kumuachia familia kwa muda mrefu. Hata hivyo walisamehana na kutaka waendelee
kushirikiana.

Onyesho la Tano (uk 37-42)

Lanina anakutana na wazazi wake kijijini, baba yake anamlaani na hata kupigwa yeye na mama
yake kwa sababu Lanina hafuati mila na desturi za kwao na mama yake ndiye aliyepewa
kumfunza.
Onyesho la Sita (uk 43-48)

Hapa wasaliti Matovu, Tereki naPelekha wanajifariji na kuwaona akina Mussa na Dewe na
Lanina kuwa ni wajinga, kwa kukataa ofay a Bw. Delamon.

Onyesho la Saba (uk 49-55)

Wasaliti hawa wana wanamshawishi Lanina arudi kazini kwa vile wamemhusiwa kuendesha
shughuli za siasa na mshahara unapanda juu kidogo. Lanina anakataa na kuwa fukuza nyumbani
kwake.

Onyesho la Nane (uk 56-65)

Lanina yupo kwenye kioski cha mzee Engeli. Mussa, Dewe na Lanina wanakutana kupeana
taarifa kuwa eti Delamon ameruhusu kuendesha shughuli za kisiasa na kuendeleza mapambano
ya kudai haki zao kazini.

Onyesho la Tisa (uk 66-72)

Katika ofisi ya Bwana Delamon wamesikia Sauti za wafanyakazi walipoamua kuimba nyimbo za
kimapinduzi.

Onyesho la Kumi (uk 73-77)

Hapa Lanina akiawa gerezani anakutana na Askari malaya,ambaye alimtongoza Lanina lakini
Lanina anamkatalia na kumpiga teke sehemu zake za siri, pia Lanina anaitwa na jaji ili kutoa
utetezi wake katika(uk 77).

MANDHARI

Kutokana na Gerald Njagi Matti. (2001). Anasema mandhari ni sehemu au mahali ambapo kazi
ya fasihi hutendeka. Katika tamthiliya ya KILIO CHA HAKI mwandishi ametumia mandhari
tofauti tofauti kama vile shambani (kwa bwana Delamon) uk 43 mahamamani, kijijini (kwa baba
na mama wa Lanina) mtunzi ametumia mandhari hayo ili kuonyesha matendo mbalimbali
ambayo yalitumika kuibua dhamira mbalimbali.

MALEBA NA VIFAA

Kutokana na Gerald Njagi Matti. (2001). Anasemamaleba ni mavazi anayotumia msanii katika
Sanaa yake. Kalika kumpamba mhusika. Mavazi yaliyotumika katika tamthiliya hii ni pamoja
na:-

Matambara uk 5 na uk 77. Matambara ni nguo zilizochanika zinazoonyesha suala la umaskini,


hapa alivaa mzee ambaye hali yake ya maisha ilikuwa duni.

Khanga uk 39, mama alipojifuta machozi kwa kutumia khanga. Khanga katika tamthiliya hii ya
kilio chetu inawakilisha utamaduni wamavazi ya mwanamke wa Kitanzania.

VIFAA

Vifaa ni zana zinazotumiwa na wahusika wa kazi ya fasihi ili kuweka uhalisia.

Mfano wa kiko kilichotumiwa na bwana Delamon inaashiria tabia za wakoloni kuvuta kwa
kutumia kiko, (ukurasa wa 10).

Sigara ni kifaa kilichotumiwa na Lanina kuonyesha tabia ya mwanamke huyu jasiri kuwa ni
mvutaji sigara. Pingu nabundiki ni silahazilizotumiwa na wakoloni ili kuwatisha na
kuwagandamiza waafrika ili wawanyonye kwa urahisi (ukurasa wa 14).

TASWIRA NA ISHARA

I. ISHARA

Kutokana na Gerald Njagi Matti. (2001). AnasemaTaswira na Isharani maelezo yanayoeleza


jambo kwa njia ya kufichika ili msomaji afikiri na kugundua mwenyewe.

Kutikisa kichwa, katika ishara hii tunaona Lanina akimkatalia Mwengo juu ya mawazo yake
potofu juu ya mkewake Lanina hii inapatikana uk 34. Pia mama yake Lanina alitikisa kichwa
kuonyesha kukubaliana na mumewe. Ishara hizi zinaonyesha matumizi mbalimbali ya viungo
vya mwili vya wahusika wake.

II. TASWIRA

Paneli la Kiswahili (2009-2014) wanasema taswira ni matumizi ya lugha inayotumia maneno


yanayojenga picha au fumbo fulani kwa msomaji.

KILIO CHA HAKI, inaonyesha mifadhaiko na manung’uniko yawafanyakazi wakidai haki zao
kama vile, mshara ndogo, mazingira mabovu ya kazi, na vifaa duni vya utendaji kazi.

Makaburu; hii ni taswira iliyotumika kuonyesha wanyonyaji ambao walikuwa wakiwanyonya na


kuwanyanyasa wafanyakazi wao kwa kuwalipa ujira mdogo na hata kufanya kazi kwa muda
mrefu.

Lanina; alikuwa akiwakilisha kundi la wapenda maendeleo, pia anawakilisha wanawake


wanaojitambua na wanaoelewa matatizo yanayowakumba wananchi wa maeneo wanayoishi.

Shamba la bwana Delamon. Hii ni taswira inayowakilisha mandhari yaliyokuwa yakitumika


kunyonya na kudhurumu haki ya wanyonge mfano; Lanina na wenzake.

Wanfanyakazi hii ni taswira iliyokuwa ikiwakilisha umma ulio kuwa ukionewa na kunyanyaswa
na bwana Delamon.

Picha ya jalada la KILIO CHA HAKIni ishara ya mwanamke anayedondosha machozi kwa kulia
kutokana na dhuluma na unyanyasaji anaofanyiwa na jamii yake.

KUFAULU KWA MWANDISHI WA RIWAYA YA KILIO CHA HAKI

Mwandishi ametumia lugha rahisi inayoeleweka yenye lugha ya kishairi, nyimbo na matumizi
mazuri ya wahusika waliobeba dhamira mbalimbali, hivyo kufanya kazi imvutie msomaji na
kuchangamsha hadhira. Kuna mfano wa shairi (uk 62).

 Ari yetu ndio mwokozi wetu


 Ari yetu lazima tuisujudie,
 Ari hii ya mwaka tuliyoivumbika,
 Iliyojaa joto lisiloburudika
 Ije ituongoze mpaka mwisho kufika,
 Na kutuzimia kiza cha mwaka

JINA LA KITABU

Jina la kitabu linasadifu yaliyomo. KILIO CHA HAKI, kitaswira linaangalia matatizo na
manung’uniko yaliyokuwa yakiwakumba wafanyakazi katika shamba la bwana Delamon.

Matatizo hayo ni kama vile, ujira mdogo, kufanya kazi kwa muda mrefu, mazingira mabovu ya
kazi pamoja na vifaa hafifu vya utendaji kazi, pia ukosefu wa demokrasia.

Matatizo na manung’uniko hayo ni vilio vya haki ambayo viliwapelekea wawe na vilio kutafuta
ufumbuzi wa matatizo hayo au waweze kujikomboa kutoka kwenye mikono ya makaburu.

“uk 9. Wafanyakazi walivyokuwa wakitoa sauti”. “Nirudishe jasho langu, nirudishe damu yangu,
nirudishe haki yangu, nirudishe utu wangu” (uk 36-42 na uk 8).

REJEA

Gereld Njagi Matti. (2001).Introduction to the Study of Literature.

Senkoro. (1982). Kitabu cha Fasihi.

Roninson Kruso. (1790). Vita na Amani.

You might also like