Download as pdf or txt
Download as pdf or txt
You are on page 1of 60

BIASHARA

MTANDAONI
Muongozo Utakaokusaidia Kujitengenezea Kipato
Kupitia Mtandao.

ISAACK NSUMBA
1
UTANGULIZI

Kwa ujibu wa waziri wa mawasiliano, habari na


teknolojia muheshimiwa Dkt. Faustine
Engelbelt Ndugulile katika kikao cha bunge
amethibitisha juu ya ongezeko la watumiaji wa
huduma za intaneti nchini Tanzania.

Idadi hiyo imeongezeka kutoka 26,832,089


Julai mwaka 2020 mpaka kufika 29,017,817
April 2021 sawa na ongezeko la asilimia 8.3.

Kwa taarifa hiyo imethibitisha kwamba, jumla


ya watumiaji wa intaneti nchini Tanzania ni
asilimia 49% ya jumla ya idadi ya watanzania
wote.

Hii ndio sababu haswa inayochangia kupanda


kwa bei za vifurushi vya data (mb/data
bundles) lakini pia ndio husababisha biashara
ya smartphone kupanuka zaidi pamoja na
makampuni yanayotoa “public internet” (wi-fi)
kupata soko zaidi.

2
Kwa upande mwingine, ongezeko la watumiaji
wa mtandao limeleta mabadiliko makubwa
sana kuanzia ngazi ya mtu binafsi mpaka ngazi
ya kitaifa, kwani hivi sasa kuna vikao na
mikutano mikubwa inafanyika kupitia
mtandao.

Nimeshuhudia wachungaji wengi sana


wakiendesha ibada zao kupitia mtandao, ibada
hizo zimefanikiwa na wachungaji hao
wamefanikiwa kutengeneza waumini wengi wa
mtandaoni ambao wameshiriki katika ukuzaji
na uendelezaji wa huduma za kiroho.

Unaposoma kitabu hiki, nataka ufahamu kuwa


sehemu ya kwanza ya wewe kuanzia kufanya
chochote unachotaka kufanya ni katika
mitandao ya kijamii, ukiitumia vizuri na kwa
muongozo wa maarifa utakayoyapata humu
utapata matokeo makubwa kama waliyopata
wengine.

3
SURA YA KWANZA

Hatua 3 Za Kutengeneza Kipato


Kupitia Mtandao
Watu wengi kwa kukosa taarifa, ufahamu,
muongozo na maarifa sahihi wameshindwa
kutengeneza kipato kupitia mtandao kwa
sababu ya kutokujua kuwa kuna hatua muhimu
za kufuata ili mtu aweze kufika hatua ya
kujitengenezea kipato kupitia mtandao.

Hatua ya KWANZA;
Tafuta Watu, Wafuasi, Views Au Hadhira
(Connect More)
Unachotakiwa kufahamu ni kwamba, msingi wa
mafanikio ya biashara yoyote ile ni watu,
hakuna biashara yoyote ambayo inaweza
kufanikiwa bila watu kuhusika, ndio maana
ukiwafuatilia kwa makini watu wengi
waliofanikiwa utagundua kuwa wanafahamiana
na watu wengi sana.

4
Muhamasishaji wa kimataifa, mfanyabiashara
na mwandishi wa vitabu Bwana Porter Gale
katika kitabu chake cha “Your Network is your
Networth” (unlock the hidden power of
connection for wealth, success, and happiness
in the digital world) anafundisha jambo moja
muhimu kwamba, kiini cha mafanikio yoyote ni
watu.

Hii ni kusema kwamba, mtu yeyote


anaedharau na kupuuzia nafasi ya watu katika
maisha yake amejiweka mbali na njia muhimu
ya mafanikio.

Hakuna mafanikio yasiyotokana na watu na


wala hakuna hatua ambayo mwanadamu
anaweza kufika kiasi cha kutowahitaji watu na
ndio maana watu waliofanikiwa wameweka
kipaumbele zaidi katika kujenga, kuboresha na
kuimarisha mahusiano yao na watu wengine.
SHUHUDA WANGU
Miaka kadhaa iliyopita nilikuwa nina hasira
zilizopitiliza kiasi kwamba sikutaka kabisa

5
kuwa na mazoea na watu kwa kuhofia
kuumizwa.

Kadri nilivyokuwa nikijifunza kanuni za


mafanikio nikagundua kuwa ili niweze
kufanikiwa nahitaji watu, kwahiyo, ilinibidi
nianze kushughulika na tatizo langu la hasira
kwa sababu nilijua kuwa kadri
nitakavyofahamiana na watu wengi ndivyo
makwazo nayo yanakuwa mengi.

Sio hivyo tu, niligundua kuwa wafanyabiashara


wakubwa, watu maarufu wote wana uwezo
mkubwa wa kudhibiti hasira zao, na hapa
ndipo nilipopata msukumo zaidi wa kujua
namna gani ya kuhimili hisia zangu kwa sababu
nitakutana na watu wengi ambao kila mmoja
ana tabia zake.

Kwa sababu ya nia ya dhati niliyokuwa nayo,


Ilinichukua muda mchache sana kujifunza hadi
nikafanikiwa, na baada ya kufanikiwa

6
nikaandika kitabu kitakachowasaidia watu
wengine kukabiliana na hasira kinachoitwa
“HISIA KIINI CHA MAFANIKIO” (kimeandikwa
kwa Kiswahili, unaweza kukitafuta ukakisoma)

Hatua ya kwanza na ya muhimu ya


kutengeneza kipato kupitia mtandao ni wewe
kufahamiana na watu wengi watakaokuwa
wanafuatilia kile unafanya, nitakufundisha
katika sura ya pili namna ya kukuza hadhira
yako ya mtandaoni.

Hatua ya PILI; Kujua Wanachokihitaji


(Identify what they need)
Baada ya kupata watu wanaoweza kuwa
wanakufuatilia kupitia whatsapp, facebook,
instagram, twitter, linkeldin na tiktok
unatakiwa kufahamu uhitaji wa watu hao.

Ufahamu huo utakusaidia wewe kujua ni kitu


gani ambacho hawa watu wanakihitaji na
wewe utakuwa tayari kuwapatia.

7
Kumbuka, haufanikiwi kutengeneza kipato kwa
kuwapatia watu kitu ulichonacho ila
unafanikiwa kutengeneza kipato kwa
kuwapatia kile ambacho wao wanakihitaji.

Hii ni kusema kwamba, kitu chochote bila


kujali kina thamani kiasi gani, ikiwa hakiko
katika mahitaji ya watu ni vigumu sana watu
kukupatia fedha kupitia hicho.

Kwa upande mwingine ni kwamba, kitu


chochote kisicho na thamani mbele yako ila
kinahitajika na watu kinaweza kukutengenezea
fedha nyingi sana.

Jiulize, watu wanaokufuatilia kupitia status


zako za whatsapp, facebook, instagram au
katika mtandao wowowte ule uneotumia
wanahitaji nini, ukishajua uhitaji mkubwa
walionao itakusaidia kujua ni kitu gani ufanye
ili wao wawe tayari kukulipa.

8
Hatua ya TATU;
Uza Thamani (Sell Value)
Tafsiri iliyo rahisi kuhusu fedha ni ile
inayosema “MONEY is a transaction of VALUE”
(fedha ni mbadilishano wa thamani)

Kwa mujibu wa hii tafsiri ni kwamba, ni


vigumu sana kupata fedha ikiwa hakuna
thamani unayotoa kiasi cha kuwashawishi watu
watoe fedha zao kukupa wewe, lakini pia kama
hautakuwa na thamani yoyote unaweza
kutumia nguvu nyingi sana kuvutia fedha
katika maisha yako na unaweza usifanikiwe, au
ukafanikiwa kwa kiwango kidogo tofauti na
nguvu ulizowekeza.

Ukweli ni kwamba, fedha ina tabia ya kuvutika


kwa watu wenye thamani, kwahiyo ili uweze
kuivutia fedha katika maisha yako unatakiwa
kutengeneza thamani fulani itakayowafanya
watu waone ujnastahili kupata fedha kutoka
kwao.

9
Ili uweze kujifunza zaidi kuhusu fedha nashauri
usome eBook changu kinachoitwa “MONEY
PASSCODE” (Siri zitakazokusaidia kupata
mafanikio ya kifedha) unaweza kuipata kwa
kutumia mawasiliano yaliyo mwanzoni au
mwishoni mwa kitabu hiki.

10
SURA YA PILI

Mbinu zitakazokusaidia Kukuza


Hadhira Yako Ya Mtandaoni
(How to Grow Your Online
Audience)
Katika sura ya kwanza tumeona kuwa msingi
wa mafanikio yoyote ni watu, kwahiyo ili
uweze kupata kipato kikubwa kupitia mtandao
lazima uwe na idadi kubwa ya watu
wanaokufahamu na kukufuatilia.

Zipo mbinu nyingi ambazo zinaweza kumsaidia


mtu kuongeza idadi ya wateja wa mtandaoni,
katika sura hii nitakufundisha mbinu tano
ambazo nimezitumia na kuthibitisha kuwa
zinafanya kazi.

11
Mbinu ya kwanza, Ladder Technique (Mbinu
Ngazi)
Hii mbinu inakutaka ufahamiane na mtu
mmoja ambae kupitia huyo utafahamiana na
watu kadhaa wanaomzunguka, wakati fulani
hii mbinu inaitwa “mbinu buibui” ambapo
ukimpata mtu mmoja unahakikisha unawapata
na wengine walio katika mzunguko “cycle”
yake.

Ili kukuthibitishia kuwa hii mbinu inafanya


kazi, jiulize wewe umenifahamu mimi kupitia
rafiki yako ambae yeye nae alinifahamu
kupitia rafiki au ndugu yake.

Hii ndio mbinu ya kwanza kuitumia na


imenisaidia sana, wakati naanza kufundisha
kupitia mtandao nilikuwa nawatumia wale
ambao tayari ninafahamiana nao na
wanafuatilia madarasa yangu kuwapata ndugu,
jamaa na marafiki zao.

12
Kitu pekee kilichonisaidia kuwashawishi wao
kuniletea watu wengine ni kufanya mambo
kwa ubora, nilikuwa nikiwafundisha masomo
ambayo yaliwasaidia sana kutatua changamoto
zao pamoja na kujibu maswali yao kwa ubora
uliowaridhisha.

Kuna msemo unasema “wachekeshe walio


karibu, walio mbali watasogea” maana yake ni
kwamba, ukiwatumia vyema wale uliokwisha
kufahamiana nao itakuwa rahisi kuwapata
wengine ambao wewe hauwafahamu ila
wanafahamiana na wale unaofahamiana nao
wewe.

Mbinu ya pili, Reach Out Techinique (Mbinu


ya Kuwafikia)

Hii mbinu inakutaka uwe na utaratibu wa


kuwafikia watu kadhaa na kuwaomba wawe
sehemu ya miasha yako, njia rahisi ya
kufanikiwa katika hili ni kuonesha kuwa

13
unawakubali sana na utajisikia vizuri ikiwa
utapata nafasi ya kuwa na mawasiliano nao.
Bila shaka umewahi kukutana na maneno
katika uwanja wako wa meseji “Inbox”
yanayosema “samahani kwa kuja inbox kwako
bila taarifa, naitwa…..naomba usave namba
yangu ili tuwe marafiki”

Hiii ni moja ya mbinu unayoweza kuitumia


kukuza idadi ya watu unaofahamiana nao
kupitia mtandao.

Kama ni whatsapp watasave namba yako na


hiyo itakusaidia wewe kuongeza idadi ya watu
ambao wanakufahamu.

Mimi mpaka sasa nina utaratibu wa kutafuta


watu ambao nawaita “Potential People” (watu
ambao mimi na wao tutafaidiana) kwa huduma
ambazo mimi natoa na zile wanazotoa wao.

14
Ili uweze kufanikiwa katika hili na upate
msukumo wa kulifanya ni lazima ujue kuhusu
kanuni ya mlimbikizo inayokutaka
kutokudharau uchache.

Nilipokuwa naanza nilijipa kazi ya kufahamiana


na mtu mmoja kila siku ambapo kwa wiki ni
watu 7, kwa mwezi ni watu 30 na kwa mwaka
ni watu 360.

Hautakiwi kudharau nafasi ya mtu mmoja,


ukipata nafasi ya kufahamiana na mtu mmoja
hakikisha unaitumia vyema, hii ndio tafsiri ya
msemo unaosema “haba na haba hujaza
kibaba”

Kila unaemuona ana watu wengi leo, kuna siku


alikuwa hana watu na alianza kuwapata
kidogokidogo mpaka wakafika idadi kubwa
unayoiona leo.

15
Mbinu ya tatu, Exchanging Techinique (Mbinu
Ya Kubadilishana Watu)
Hii ni pale ambapo utaandika meseji ambayo
ina namba yako ya whatsapp na kasha kuwapa
watu watume katika magroup yao pamoja na
kupost katika status zao.

Ili mbinu hii iweze kufanya kazi, ni lazima


wewe nae uwe na utaratibu wa kupost taarifa
za wenzako.

Hapa ni kama mnabadilishana watu, yaani


watu wako wanakwenda kwa mtu mwingine na
watu wa mtu mwingine wanakuja kwako, kadri
utakavokuwa na juhudi za kutuma link za
wenzako ndivyo unaongeza uwezekano wa
wenzako kutuma link yako.

Changamoto kubwa ya hii mbinu ni pale


ambapo utaitumia kwa mtu anaefanya kitu
sawasawa na kile unachofanya wewe.

16
Ili uweze kupata matokeo kwa kutumia mbinu
hii unatakiwa kuwapa watu ambao wana watu
wengi zaidi yako.

Mbinu ya nne, Bait Technique (Mbinu Ya


Kutumia Chambo)
Hii mbinu unatakiwa kuitumia kunasa watu ili
waje kukufuatilia.

Namjua mtu mmoja anaitwa “Raphael, Mr


Think in USD” nilimfahamu baada ya kukuta
post yake inasema “namna ya kunasa
warembo” post ilikuwa imesukwa vyema kiasi
kwamba nilipomaliza kusoma nilimtafuta ili
nijifunze zaidi.

Cha ajabu, baada ya kusave namba yake na


kumfuatilia kwa siku kadhaa nikagundua kuwa
hafundishi kuhusu mapenzi, ila anafundisha
kuhusu digital marketing, forex pamoja na
cryptocurrency”

17
Nikajua kuwa, mbinu aliyotumia kuninasa mimi
na wengine wengi ni mbinu ya chambo ambapo
anatafuta kitu kinachoweza kuwavutia wengi
kuja wakishakuja anawapa kitu ambacho yeye
ni mtaalamu katika hicho.

Wakati fulani nilikuwa nataka kuwafundisha


watu kuhusu fedha, biashara na uwekezaji,
nikajua kwamba kama nitaanza kuwafundisha
moja kwa moja kuhusu fedha sio wengi
watakaokuja katika madarasa hayo, ikanibidi
niyatumie mapenzi kama chambo na ilinisaidia
kupata watu wengi sana na baada ya kuwapata
ndipo nikaanza kuwafundisha kuhusu fedha.

Kwa mujibu wa mwandishi Dale Carnegie


katika kitabu chake cha HOW TO WIN FRIEND
AND INFLUENCE PEOPLE anasema “for you to
capture them, show things they are interested
with” (ili uweze kuwapata, waoneshe mambo
ambayo wao wanayapenda au kuyakubali).

18
Ili uweze kuitumia mbinu hii unatakiwa
kufanya mambo makubwa matatu, jambo la
kwanza ni kuwa na ujuzi wa kusuka matangazo
“copywriting” kama alionao Raphael (Mr Think
in USD) jambo la pili ni kujua kitu gani
ambacho ukikiandika kinaweza kuwavuta watu
kwa haraka (content selection) na kitu cha
tatu ni kujiunga katika magroup mengi kadri
uwezavyo ambapo lengo lako litakuwa kuvua
watu na kuwaleta inbox kwako ili wawe
sehemu ya network yako.

Mbinu ya tano, Sponsorship Technique (Mbinu


Ya Udhamini)
Hii mbinu inatumika pale ambapo inakulazimu
kulipia ili kutangaza huduma unayotoa.
Kuna namna za aina mbili za kudhamini
matangazao yako, ya kwanza ni kwa kuwapa
watu wenye followers/views wengi zaidi yako
wapost taarifa zako ili watu wao wakutafute,
ya pili ni kwa kutumia “Ads manager” ambayo
inapatikana instagram pamoja na facebook.

19
Ili uweze kutumia Ads manager unatakiwa
kuwa na ufahamu, mimi nilisomea kozi
mtandaoni kutoka taasisi moja inaitwa
“Mwalimu Hemedi Centre” na alinifundisha
zote mbili (Facebook na Instagram) kwa ada
ndogo kabisa.

20
SURA YA TATU

Njia 10 Unazoweza Kuzitumia


Kutengeneza Kipato Mtandaoni
Kuna njia nyingi ambazo watu mbalimbali
huzitumia kutengeneza kipato kupitia
mtandao, katika sura hii nitakufundisha njia
kadhaa ambzao ni rahisi kiasi kwamba hata
wewe unaweza kuzitumia kujitengenezea
kipato.

Njia ya KWANZA; Kufundisha

Moja kati ya bidhaa inayohitajika zaidi katika


kizazi cha sasa ni taarifa sahihi, hii ni kwa
sababu kumekuwa na taarifa nyingi kuhusu
mambo mbalimbali, wewe unaweza ukaamua
kuwa na taarifa sahihi zinazoweza kuwasaidia
watu.

Taarifa hizo unaweza kuzipata kupitia kusoma


vitabu, kusoma Makala mbalimbali au kupitia

21
taaluma yako na ukazitoa kupitia madarasa ya
mtandaoni (Online Class)

Lakini pia, taarifa hizo unaweza kuzipata


kupitia uzoefu katika ujuzi fulani ulionao na
ukashea ujuzi huo na watu wengine kwa
malipo ya kiasi fulani cha fedha.

Mfano, Mimi ni mtaalamu katika eneo la


mahusiano, uchumba, Ndoa, malezi Uchumi
pamoja na Uongozi.

Hayo nimeyajua kupitia uzoefu pamoja na


kusoma vitabu vingi na Makala mbalimbali kwa
miaka mingi.

Naweza nikaamua leo kwamba, kila mmoja


anaetaka kujifunza kupitia madarasa yangu ya
mtandaoni alipie kiasi fulani cha gharama za
uendeshaji.

Wakati naanzisha LOVE ACADEMY ONLINE


CLASSES (madarasa ya mahusiano kupitia

22
mtandao) nilikuwa nina watu wachache sana
na niliweza kuwatumia hao kuonesha uwezo
wangu mkubwa nilionao na walikuwa tayari
kunilipa.

Hata wewe unaweza kutafuta kitu ambacho


watu wanakihitaji na ukawapa ufahamu,
maarifa na taarifa sahihi kuhusu kitu hicho kwa
kiasi fulani cha fedha kwa kila atakaetaka
kujifunza.

Namjua mtu mmoja anaitwa JOEL KADAGA


yeye amebobea kwenye Graphics Designing
kiasi kwamba anawafundisha watu wengine ili
wao nao waweze kuwa wabobevu.

Namjua mtu mmoja anaitwa SirJeff Denis,


huyu ni mbobevu wa Forex trading kiasi
kwamba anatoa elimu na ufahamu kupitia
mtandao na anaingiza fedha nyingi kupitia
hicho anachofanya.

23
Uzuri ni kwamba, ujuzi ulionao, taaluma
uliyosomea, kipaji ulichonacho, uzoefu wa
maisha ulionao, huduma uliyonayo ni biadhaa
yenye thamani unayoweza kuitumia kuingiza
fedha ikiwa utajua namna sahihi ya kuifanya
ikuletee fedha na endapo utakutana na watu
wanaohitaji.

Kumbuka, ili watu waweze kukulipa kupitia


elimu unayotoa mtandaoni ni lazima ufike
hatua ambayo watakufahamu kama mtaalamu
unaeaminika na wengi, hawawezi kukulipa
endapo hawakuamini, na hawawezi kukuamini
kama haujajiweka kama mtaalamu
(Expert/competent person)

Njia ya PILI; Huduma.

Nilikutana na mtu mmoja ni mwanafunzi wa


chuo Fulani hapa Tanzania, yeye anatoa
huduma za kuandika barua, CV, cover letter
pamoja na research na anapata wateja wengi
kwa kufanya hivyo.

24
Nilikutana na Dada anaitwa Aneth, wakati huo
alikuwa mwanachuo ambae kazi yake kubwa ni
kuwasaidia watu kuongeza views kupitia status
za whatsapp, huduma yake kwa mtu mmoja
inaanzia shilingi 1,500 mpaka shilingi 5,000 na
anapata wateja wengi wanaohitaji huduma
hiyo.

Mfumo wa masoko wa sasa (digital marketing)


umerahisiaha sana kukutana na watumiaji wa
huduma uliyonayo bila kuonana nao uso kwa
uso, unachotakiwa ni kuwa na huduma fulani
ambayo inahitajika na watu na kujua namna
gani unaweza kuwashawishi watu wakulipe
kwa huduma unayowapa.

Namfahamu rafiki yangu mmoja, yeye anatoa


huduma ya kuzitangaza akaunti za mitandao ya
kijamii (Digital platforms Branding) na
anawatangazia watu maarufu na wanamlipa
fedha nyingi kupitia kazi yake hiyo.

25
Jiulize, una huduma gani ambayo watu
wanaihitaji kiasi kwamba unaweza kuiingiza
sokoni na wakawa tayari kutoa fedha mfukoni
kwao kukupatia wewe?

Njia ya TATU; Kuuza huduma kupitia ujuzi.

Ujuzi wowote ulionao ni bidhaa yenye uwezo


wa kukupatia fedha, unachotakiwa kufanya ni
kujitangaza kama mtu mwenye aina fulani ya
ujuzi na uliyebobea katika ujuzi huo
(Competent-Skilled Person)

Kuna mtu mmoja ana ujuzi wa kuchora,


unaweza kumtumia picha yako na akaichora
kwa penseli na kisha kukutumia popote ulipo
ikiwa na ubora wa hali ya juu.

Kuna mtu ana ujuzi wa kufanya Graphics


Designing na huduma zake anazitoa kupitia
mtandao, hana ofisi isipokuwa ana ujuzi,
smartphone pamoja na computer anayofanyia
kazi za namna hiyo.

26
Kama una ujuzi wa namna hii unayo nafasi
kubwa sana ya kutengeneza kipato kupitia
mtandao, endapo utajua namna gani ya kukuza
jina na kuonesha uwezo wako katika kufanya
graphics.

Ninachoweza kukushauri kama una ujuzi au


huduma yoyote uliyonayo jifunze kuwafanyia
kazi watu wanaojulikana kwa malipo kidogo au
bila malipo kabisa huku ukiwaomba watutaje
katika platforms zao.

Kwanza, inaweza kukujengea uaminifu wa


watu wengine kwa kuona unafanya kazi na
watu wanaojulikana, lakini pia inaweza
kukuongezea wateja na hata kuiongeza
thamani yako sokoni.

Jiulize, ni aina gani ya ujuzi ulionao unaoweza


kuutumia kuhudumia watu kupitia mtandaoni,
kama hauna ujuzi wowote nakushauri
ujibidiishe kutafuta.

27
Njia ya NNE; Kuandika maudhui (Content
Creating)

Mwaka 2020 nilipewa kazi na kampuni fulani


ambayo ilinitaka niwe naandika maudhui kila
siku asubuhi na kisha nawatumia wao wapost
katika kurasa zao.

Nilifanya hivyo ambapo wao walikuwa


wananichagulia mada ya kuzungumzia kwa siku
na kisha mimi naandika maudhui kuhusiana na
mada hiyo.

Mwaka 2021 nilikutana na mtu anaitwa


Abdulatif Mohammed Kyota (DR TYPH) ambaye
alikuwa akitafuta mtu anaeweza kumpa kazi
ya kumuandikia maudhui yahusuyo mahusiano
kupitia ukurasa wake wa facebook.

Watu maarufu wengi huwa wana watu ambao


kazi yao kubwa ni kusimamia uendeshaji wa
mitandao yao ya kijamii (Media Managers) ili

28
iendeleze shughuli hizo hata pale ambapo
wenyewe wanakuwa bize.

Hii ni moja kati ya njia unzoweza kuzitumia


kutengeneza fedha kupitia mtandao.

Lakini pia unaweza kutengeneza blog (uwanja


ambao utakuwa unapost maudhui yako huko)
na kasha ukalipwa baada ya blog yako kukua
na kufuatiliwa na watu wengi.

MillardAyo alianza kazi kama Blogger ambae


kazi yake ilikuwa kuripoti matukio mbalimbali,
na kwa sababu alikuwa na juhudi, ujuzi wa
mtandao na bidii katika kutafuta taarifa mpya
na nyeti ilikuwa rahisi kwake kulipwa na hivi
sasa amekua na analipwa fedha nyingi zaidi ya
mwanzo.

29
Njia ya TANO; Ununuzi Na Uuzaji Wa Sarafu
(Forex & Crypto Currency)

Hii njia itakusaidia endapo utakuwa na


ufahamu wa kutosha kuhusu soko la dunia
kupitia mtandao, ufahamu huo utakusaidia
kujua kupanda na kushuka kwa thamani ya
sarafu ili uweze kujua ni muda gani sahihi wa
kununua na ni muda gani sahihi wa kuuza ili
upate faida.

Kumbuka, njia hii itafanya kazi na kukuletea


matokeo ikiwa utanunua sarafu kwa bei ndogo
na kuiuza kwa bei kubwa, kwahiyo ili uweze
kutumia njia hii kukuingizia kipato unalazimika
kuwa ni mtu unaetafuta taarifa za soko mara
kwa mara na kuwa makini (attentive)

Mimi sijawahi kuitumia hii njia, ila


ninawafahamu watu kadhaa ambao wao
wamefanya, na wengine wanafanya mpaka
sasa na inawasaidia kuingiza kipato.

30
Njia ya SITA; Youtube

Njia hii inakutaka uwe ni mtu unaepakia video


kupitia youtube ambazo watu watakuwa na
kazi ya kwenda kuziangalia.

Utakapofika hatua fulani ya idadi ya watu


wanaofuatilia chanel yako utaanza kulipwa, na
kadri ambavyo wanaokufuatilia wanaongezeka
ndivyo ambayo uwezekano wa kupata fedha
zaidi huwa mkubwa.

Njia hii unaweza kuitumia kwa kipaji chako,


taaluma yako au kwa kutumia maarifa
uliyonayo.

Kuna mtoto anaitwa Mai Zumo, ana kipaji cha


kuchekesha ambapo huwa anatengeneza
videos na kuzipakia katika channel yake ya
youtube.

31
Kuna mtu anaitwa Ezden Jumanne, yeye ni
mkufunzi wa masuala ya maisha ambaye huwa
anapakia zinazolenga kuelimisha jamii.

Kuna waimbaji wengi ambao nyimbo zao


wanaziweka youtube na kadri ambavyo
wanafuatiliwa ndivyo wanaingiza fedha zaidi.

Uzuri kuhusu hii njia ni kwamba utaendelea


kunufaika na malipo ya video zako muda wote
ikiwa tu itaendelea kutazamwa mara kwa
mara.

Hii ndio sababu kwanini waandishi wa habari


wengi wanapotaka kuweka video wanatafuta
kichwa ambacho kinaweza kuvutia watu wengi
zaidi kwenda kuitazama.

Lakini pia, hii ndio sababu kwanini watu


wengine hutunga hata taarifa za uzushi na
kuzitengenezea video na kisha video hiyo
kuwekwa youtube ikatazamwe zaidi.

32
Hata wewe unaweza kuitumia hii kama njia ya
kukuingizai kipato ikiwa utajua ni kitu gani
unachoweza kukitengenezea video na
ukazipakia huko.

Njia ya saba; Kuandika electronic Books


(eBooks)

Electronics books ni vitabu vilivyo katika


mfumo wa kielektroniki au vilivyo katika
nakala tepe (softcopy) ambavyo mtu ataweza
kuvisoma kupitia simu yake au kompyuta.

Watu wengi hawana elimu ya kutosha kuhusu


hili na ndio maana inakuwa vigumu wao kujua
kuwa kuna uwezekano wa mtu kuandika kitabu
na akakiuza kupitia mtandao.

Kwa Tanzania hapa kuna application kadhaa


zinazohusika na uuaji wa vitabu kupitia
mtandao kama kipajiApp.

33
Unaweza kuandika juu ya chochote kile
unachotaka watu wajue, au ukatafuta
chochote ambacho watu wanahitaji kujua na
ukawaandikia kitabu ambacho utakiuza kupitia
mtandao.

Kumbuka, nimesema ujuzi, maarifa au uzoefu


wowote ulionao kuhusu maisha ni bidhaa
ambayo unaweza kuiingiza sokoni na
ikakuletea fedha endapo itakutana na
wanaoihitaji.

Namjua dada mmoja ambaye kwa muda sasa


amekuwa mbobevu katika upishi wa cake kiasi
kwamba akaandika kitabu kinaitwa SIRI ADIMU
ZA UPISHI WA KEKI, huyu anachofanya ni
kugeuza uzoefu na ujuzi alionao kuwa biadhaa.

Kuna kozi nyingi zinatolewa mtandaoni


zinazohusu uandishi, mimi nimesoma kozi 6
zinazohusiana na uandishi kwa mwaka 2019
mpaka 2022, hata wewe ukiamua unaweza

34
kujifunza kozi hizo ukiwa sehemu yoyote
Tanzania na endapo una smartphone pamoja
na data.

Njia ya NANE; Affiliate marketing

Huu ni mfumo wa masoko na mauzo ambao


lengo ni kukuza uuzaji wa bidhaa au huduma
za kampuni fulani.

Ukitaka kuingiza kipato kwa kutumia hii njia


kazi yako kubwa inakuwa ni kutafuta wateja
wa bidhaa huduma fulani ambapo wale wateja
wakinunua wewe utapata gawio (commission)
la asilimia fulani ya faida iliyopatikana.

Joel Nanauka ana duka la vitabu ambapo alitoa


nafasi ya watu fulani kutangaza vitabu
vinavyopatikana dukani kwake na wakifanikiwa
kuuza yule aliyetangaza anapewa gawio.

Hii njia ni rahisi na ni nzuri endapo utakuwa na


uwezo mkubwa wa kuashwishi watu kiasi cha

35
wao kufika hatua ya kuwa tayari kulipia
huduma au bidhaa fulani unayotangaza ili
wewe upate kiasi fulani baada ya mauzo.

Hapa unakuwa kama wakala wa mtandaoni


(online agent) na utalzimika kuwa na watu
wengi wanaokufuatilia ili uweze kupeleka
wateja wengi zaidi.

Kumbuka, njia hii haukupatii fedha kwa wewe


kutangaza, ila itakupatia fedha endapo
utafanikiwa kuwafanya watu wanunue.

Jukumu lako kubwa linakuwa ni kuhakikisha


wewe umekuwa sehemu ya mauzo ya bidhaa
au huduma fulani katika kampuni au taasisi
utakayokuwa unafanya nayo kazi.

Unahitaji ujuzi wa kutangaza (marketting)


pamoja na ujuzi wa kuuza (sales skills) ili
uweze kufanikiwa endapo utachagua kuitumia
njia hii.

36
Njia ya TISA; Kufanya matangazo

Umewahi kuona msanii asiyemiliki duka la


nguo akifanya matangazo ya nguo kupitia
kurasa zake?

Hii ni njia nyingine inayoweza kukusaidia hata


wewe kufanya matangazo ya bidhaa
mbalimbali za watu wengine, hii itakusaidia
sana ikiwa utakuwa na utaratibu wa kuongeza
idadi ya watu wanaokufuatilia kila siku katika
majukwaa yako ya mtandao (Online platforms)

Ili uweze kutumia njia hii unatakiwa kuwa na


ujuzi wa kushawishi (persuasion skills) juu ya
ubora wa bidhaa au huduma unayoitangaza.

Hii ni kwa sababu, idadi kubwa ya watu


wanaokufuatilia wanakuwa na Imani nawewe
kwa sehemu fulani, hivyo ukionesha kuamini
kile unachotangaza inawafanya wao nao
kujenga Imani juu ya hicho.

37
Njia ya KUMI; kuuza bidhaa

Katika njia hii unaweza ukaamua kununua


bidhaa kwa bei ya jumla na kuziuza kwa bei ya
rejareja, kazi yako kubwa inakuwa ni kuzipost
bidhaa hizo.

Uzuri ni kwamba, njia hii anaweza kuitumia


mtu yeyote, hata kama hauna duka unaweza
kuitumia.

Mfano, ukawa kaenda duka la wauzaji wa simu


na ukawaomba uwe unafanya kazi ya
kutangaza simu zao ili uweze kuwaletea
wateja.

Wao watakupa bei ya kila simu, kazi yako


wewe itakuwa ni kuongeza kiasi cha fedha
kidogo ambacho kwako kitakuwa kama faida ili
ukitoa fedha ya muuzaji wewe ubaki na iliyo
yako.

38
Ili uweze kupata wateja kirahisi kuna mambo
unatakiwa uwaoneshe kuwa hawatahusika
nayo.

Mfano hela ya kutolea pamoja na gharama za


kutuma kama unaweza usiziweke ila zinakuwa
ndani ya gharama ya simu.

Mfano, simu umenunua 220,000 unamwambia


mteja kuwa hii simu inauzwa 285,000 na
hautalipia usafiri wala gharama ya kutolea.

Mteja akikutumia wewe 285,000 unatoa


220,000 ya muuzaji, unatoa 15,000 ya usafiri
(kama yuko nje ya mkoa uliopo wewe) na
unabaki na 50,000

Faida ya kufanya hivi ni kusababisha athari ya


kisaikolojia (psychological effect) kwa mteja
kwa kumuonesha kuwa umemsaidia
kumuondolea gharama za usafirishaji ambazo
alitakiwa zilipie yeye, asijue kama ndani ya

39
bei ya simu amelipia na usafiri pamoja na hela
ya kutolea.

Mambo hayo kumi uliyojifunza katika sura hii


yote yanafanya kazi, unaweza kutumia njia
zaidi ya mbili kulingana na uwezo ulionao.

Katika sura inayofuata nitakufundisha mambo


yanayoweza kukusaidia kuuza kupitia
mtandao, hakikisha unasoma kitabu hiki mpaka
mwisho.

40
SURA YA NNE

Mambo Yanayoweza
Kukusaidia Kuuza Kupitia
Mtandao
Unaweza ukawa na bidhaa au huduma nzuri
sana, pamoja na bidhaa uliyonayo unahitaji
kufahamu mambo kadhaa ili ufahamu huo
ukusaidie kuuza bidhaa au huduma zako
mtandaoni.
1. Matangazo
Unatakiwa kuwa na utaratibu wa kuitangaza
(to brand) bidhaa au huduma unayotoa kupitia
kurasa zako.

Kama wewe unauza vitenge, ni matarajio


yangu nikitembelea katika kurasa zako na
majukwaa yako nikute mambo yanayohusiana
na kile unachouza.

41
Hii inawafanya watu wakujue wewe pamoja na
bidhaa uliyonayo, lakini pia unalipa jina lako
nafasi kubwa ya kuibuka katika akili zao pale
watakapokuwa wanahitaji huduma au bidhaa
ulizonazo.

Kumbuka, usipotangaza basi unatakiwa kujua


kuwa kuna watu wanatangaza bidhaa zao na
hivyo watu wanaofuatilia majukwaa yako
wakizihitaji watakwenda kununua kwa wale
wanaotangaza huduma zilezile ambao wewe
pia unazo.

Kuna mambo kadhaa unayotakiwa kuyaepuka


katika utangazaji wa bidhaa au huduma zako,
jambo la kwanza epuka kuitangaza kwa namna
moja kila siku, jambo la pili, epuka kudhani
kuwa watu wanaijua bidhaa yako au huduma
unayotoa, ukiwa na mawazo ya namna hiyo
hautatangaza kwa kudhani kuwa watu
wanazijua huduma zako. Kosa la mwisho
unalotakiwa kuliepuka ni kupost taarifa zako

42
binafsi na mambo mengine kuliko vile
unavyopost kuhusu bidhaa au huduma yako.

Kuna mtu anauza dawa za kupunguza uzito, ila


kila ninapotembelea status zake nakuta
amepost picha za marafiki zake anaowatakia
heri ya siku zao za kuzaliwa, kwa maneno
mengine ni kwamba, anatumia muda wake
mwingi kupost mambo mengine mengi zaidi ya
vile anavyopost kuhusu bidhaa ana huduma
zake; wewe usiwe kama huyo.
2. Mahusiano mazuri na wateja
Kwa mujibu wa kampuni ya Sales Management
Association imethibitika kwamba, msingi wa
biashara yotote kufanikiwa kimauzo ni
mahusiano mazuri kati ya mteja na mwenye
biashara au muuzaji.

Hii ni kwa sababu, mtu hujisikia vizuri sana


kuona kuwa uwepo wake unathaminiwa na
kutambulika, ukiweza kujenga hali ya
kumfanya mtu ajione mwenye thamani,
mwenye kuheshimika na kutambulika mbele

43
zako, ni rahisi sana wewe kuipata fedha iliyo
mfukoni kwake.

Hii ni kwa mujibu wa kanuni inayoitwa “law of


Reciprocity” inayosema kuwa “ukimfanyia mtu
kitu kitakachomfanya afurahi, unakuwa
umempiga deni la yeye kukufanya ufurahi pia
kwa kukufanyia kitu”

Kwahiyo, ukiwafanya watu wengine


waufurahie uwepo wao katika maisha yako,
wao watakufurahisha kwa kununua bidhaa zako
au huduma unazotoa.

Hii ndio sababu kubwa kwanini makampuni


makubwa yanatunza taarifa za wateja wao ili
ziwawezeshe kudumisha mahusiano ya
kibiashara kati ya kampuni na wateja.
3. Ubora
Moja ya hitaji la kila mwanadamu ni kupata
kilicho bora kwa bei nafuu, unapokuwa na
bidhaa au huduma zenye ubora unajiweka
katika nafasi kubwa na inakuongezea

44
uwezekano wa kupata wateja mara mbili zaidi
ya yule mwenye bidhaa zenye ubora mdogo.

Hakikisha bidhaa unaouza au huduma unazotoa


zina ubora unaoweza kumshawishi mteja
kulipa fedha yake lakini pia hakikisha bei yako
iko ndani ya uwezo wa wale unaowalenga
kuwauzia bidhaa hiyo.
Unaweza ukawa na bidhaa nzuri sana, lakini
changamoto ikawa kwenye bei ya bidhaa yako.

Ndio maana, unashauriwa kuwa na taarifa za


wateja wako “customer profile” zinazoonesha
umri wao pamoja na kipato walichonacho, hii
itakusaidia kujua wanao uwezo wa kulipia kiasi
gani kwaajili ya bidhaa yako.

Kisaikolojia, kila mteja huwa ana hofu ya


kupoteza fedha yake kwa kulipia huduma
ambayo haina ubora unaoridhisha, ili uweze
kumuondolea hofu ya namna hiyo mteja wako
ni kuhakikisha bidhaa azako zina ubora wa hali

45
ya juu na bei ambayo mteja anaweza kuimudu
(affordable price)
4. Ujuzi
Mfanyabiashara, muhamasiahaji na mwandishi
wa vitabu Bwana Sabri Suby katika kitabu
chake kinachoitwa “SELL LIKE A CRAZY”
(namna ya kuuza zaidi) amebainisha kuwa mtu
mwenye ujuzi wa kuuza ana uwezo mkubwa
sana wa kupata wateja wengi hata kama
bidhaa yake ina ubora mdogo na ina bei kubwa
kuliko mtu ambae bidhaa yake ina ubora
mkubwa na bei ndogo asiye na ujuzi (rudia
tena kuisoma hii sentensi kabla hujaendelea
mbele)

Unahitaji ujuzi utakaokusaidia kuuza bidhaa


zako, ujuzi huo unatakiwa uambatane na
ufahamu kuhusu saikolojia ya mteja ili uweze
kuenenda kulingana na mahitaji husika ambayo
mteja anayo.

Mteja anamuheshimu na kumthamini sana


muuzaji anaeelewa hitaji kubwa la mteja
wake, ujuzi wa kuuza utakusaidia kuyajua

46
mahitaji makubwa ya kihisia ambayo kila
mteja anakuwa nayo anapohitaji bidhaa fulani.

Kumbuka kuuza ni Sanaa na Sanaa ni ufundi,


hauwezi kuwa fundi kama hauna ujuzi.

Uzuri ni kwamba, ujuzi wa namna ya kufanya


mauzo unaweza kuusoma kupitia mitandao,
unaweza kusoma kwa kozi za kulipia au
kusoma vitabu na Makala kadhaa na kisha
kutendea kazi kile ambacho umejifunza ili
kupima kipi kinafanya kazi na kipi hakifanyi
kazi.

47
SURA YA TANO

Mambo Yanayoweza Kukuzuia


Usiuze Bidhaa Au Huduma Zako
Mtandaoni
Suala la kufanikiwa kufanya mauzo kwa mtu
ambae haujawahi kuonana nae ila umekutana
nae kupitia mtandao sio jepesi kama ambavyo
wengi wanavyodhani, ila ukweli ni kwamba ni
jambo linalowezekana!

Katika sura hii nitakufundisha mambo ambayo


yanaweza yakasimama kama kikwazo cha
wewe kuuza bidhaa au huduma zako kupitia
mtandao, uzuri ni kwamba kama ukifanikiwa
kuyashughulikia mambo haya ipasavyo suala la
kupata wateja na kufanikiwa kuuza bidhaaaa
au huduma zako halitakuwa na ugumu
wowote.

48
1. Kushindwa kuaminika
Wanasaikoilojia wamebainisha kwamba
binadamu anakabiliwa na aina 70 za hofu,
moja ya aina za hofu zinayomkabili binadamu
ni hofu ya kupoteza.

Aina hii ya hofu kila mmoja anayo hasa


anapokutana na mtu ambae hamfahamu,
mtandaoni ni vigumu sana mtu kununua bidhaa
au huduma yako ikiwa haujafanikiwa kumfanya
akuamini.

Jukumu lako kubwa halitakiwi katika kupata


fedha kutoka kwa wateja, ila jukumu lako
linatakiwa liwe ni kuhakikisha umefanikiwa
kujenga Imani ndani yao.

Ukifanikiwa kujenga Imani yao juu yako ni


rahisi sana kufanikiwa kuuza bidhaa zako.

49
Njia rahisi ya kufanikiwa katika hili ni
kuwaonyesha mrejesho wa watu unliowahi
kuwahudumia na wakaridhika na bidhaa yako.

Hii itakusaidia sana kuweka mizizi katika


mioyo yao na kuwafanya wajue kuwa wewe ni
mtu muaminifu na kama wakitoa fedha zo
kukupa zitakuwa katika mikono salama.
2. Bei
Moja kati ya kundi nililokutana nalo mtandaoni
ambalo lina changamoto ya mauzo ni kundi la
wauzaji wa tiba lishe au virutubisho.

Wengi wao wanatoa bidhaa ambazo gharama


yake ni kubwa sana kuliko uwezo wa mtu
kumudu.

Unakuta watu wanaomfuatilia wengi ni vijana


ambao wapo katika mapambano ya kujikomboa
kiuchumi na wana changamoto ya kiafya ila
bidhaa ya kuondoa tatizo lao inauzwa 200,000
hii bei kwa sehemu kubwa inaweza ikawa
kikwazo cha mtu kufanikisha mauzo.

50
Hii inapelekea watu hawa kuzitangaza bidhaa
zao kwa muda mrefu bila kupata matokeo kwa
sababu bei sio rafiki kwa wateja.

Kutokufanikiwa kuuza haina maana kwamba


watu hawana shida, ila ni kwa sababu uwezo
wa wao kulipia bidhaa hiyo hawana au ni
mdogo kulinganisha na bei husika.
3. Stagnated Audience
Kuna wakati ambapo kitu kinachokuzuia usiuze
mtandaoni ni kuwa na idadi ya watu
wanaokufuatilia isiyoongezeka au iliyodumaa.

Kama ambavyo tumejifunza katika sura ya


kwanza kuwa msingi wa mafanikio ya biashara
yoyote ile ni watu, hakuna biashara inayoweza
kufanikiwa bila watu.

Na hii ni kwa sababu hauanzishi biashara


kwaajili yako, ila kwaajili ya watu, ili uweze
kuuza unahitaji watu utakaowauzia.

51
Ikiwa tayari umekwishawauzia watu ulionao
hivi sasa, basi unahitaji watu wapya ili
uwauzie huduma au bidhaa ya zamani na
unahitaji huduma au bidhaa mpya ili uwauzie
watu wa zamani pamoja na watu wapya (rudia
kuisoma tena hii sentensi)

Kumbuka, kadri unavyoongeza idadi ya watu


wanaokufuatilia ndivyo unavyopanua wigo
wako wa kufanya mauzo, hakikisha unatumia
mbinu nilizokufundisha katika sura ya pili ili
kukuza wigo wako wa watu.

4. Lack of skills
Kuna watu ambao wana bidhaa au huduma
nzuri, bei waliyoweka ni nzuri pia ila
kinachokwamisha wasiuze ni ujuzi wa kuuza
(sales skills)

Kuuza ni Sanaa na Sanaa ni ufundi na hauwezi


kuwa fundi kama hauna ujuzi.

52
Bila kujali unauza nini unahitaji ujuzi
utakaokusaidia kutoa fedha kutoka katika
mfuko wa mteja na kuifanya ije mfukoni
kwako.

Hii ndio sababu kwanini makampuni kadhaa


yameajiri maafisa masoko na mauzo (sales and
marketing officers) ambao kazi yao kubwa ni
kuhakikisha bidhaa za kampuni zinawafikia
wateja na wanafanikisha kuziuza.

Kama hautakuwa na ujuzi, hata kama bidhaa


zako zina ubora na una bei ndogo bado
utakutana na changamoto, hii ni kwa sababu
suala la kuuza halitokei hivihivi, ila
linafanikishwa kwa kuwa na ujuzi wa mauzo.

53
HITIMISHO

Nimewahi kusikiliza speech ya profesa Patrice


Lumumba iliyokuwa inaitwa “Wisdom Of Life”
(Hekima za maisha) na katika speech yake hiyo
alinukuliwa akisema kwamba “A good dancer
must know how to dance according to the
tune” yaani mcheza muziki mzuri ni muhimu
kujua namna ya kuucheza muziki huo
kulingana na mdundo”

Miaka ya nyuma kidogo mitandao ya kijamii


ilionekana kama sehemu ya kupotezea muda,
ilionekana kama sehemu ya watu kupost picha
zao, kwa wakati tulionao mitandao ya kijamii
ni sehemu ya wewe kupeleka bidhaa au
huduma yoyote uliyonayo.

Badala ya kuitazama kama sehemu ya


kupotezea muda wewe unatakiwa kuitazama
kama sehemu iliyobeba fursa nyingi kwaajili
yako.

54
Unapowaona wachungaji wanaitumia mitandao
ya kijamii kuendesha ibada na kutoa huduma
za kiroho basi unatakiwa kufahamu kwamba
mambo yamebadilika sana na wameona fursa
iliyojificha katika mitandao hiyo.

Kabla hujakiingiza kitabu hiki katika orodha ya


vitabu vyangu ulivyosoma, hakikisha unaandika
ni huduma au bidhaa gani utakayoanza kuitoa
kupitia mitandao na kuwafikia watu wengi.

Ni matumaini yangu kwamba, kitabu hiki


kitakusaidia sana kubadilisha mfumo wa
maisha yako ikiwa kile ulichojifunza humu
ndani utakifanyia kazi kwa muda mrefu,
hongera!

55
VITABU VINGINE
Nimekuandikia vitabu vingine
vitakavyokusaidia kuongeza
maarifa zaidi pamoja na
kukuimarisha wewe binafsi na
kuimarisha mahusiano yako
1. SANAA YA KUTOA NA KUPOKEA
KATIKA MAHUSIANO
2. SANAA YA MAWASILIANO KATIKA
MAHUSIANO
3. SANAA YA UTONGOZAJI
4. THE GOLDEN WOMAN
5. MANIFEST YOUR MANHOOD
(DHIHIRISHA UANAUME WAKO)
6. HISIA KIINI CHA MAFANIKIO
(EMOTIONAL MUSLES)
7. MWANAMKE MASHINE
8. BORESHA MAHUSIANO YAKO

56
9. MUACHE AENDE
10. MUONGOZO WA USOMAJI WA VITABU
11. HUYU NDIYE (MUONGOZO
UTAKAOKUSAIDIA KUMTAMBUA MWENZI
SAHIHI)
12. SHULE YA BIASHARA
13. MONEY PASSCODE (SIRI
ZITAKAZOKUSAIDIA KUPATA MAFANIKIO YA
KIFEDAH)
14. MAISHA NI KUSUDI (KWANINI
ULIZALIWA NA KWANINI BADO UNAISHI?)

NB: Vitabu vyote vimeandikwa kwa lugha ya


Kiswahili na vipo katika mfumo wa pdf,
unaweza kuvipata kupitia whatsapp au
email, Ili kuvipata tumia mawasiliano
0654722733.

57
TEMBELEA MITANDAO YA
KIJAMII YA ISAACK NSUMBA ILI
KUJIFUNZA ZAIDI

YouTube: Isaack Nsumba


(Utapata VIDEO nyingi za
kukufundisha mambo mbalimbali)
Instagram: Isaack Nsumba
(Utapata mafunzo kila siku
yatakayokusaidia)
Facebook: Isaack Nsumba
(Utapata mafunzo kila siku na pia
shuhuda mbalimbali.)

58
59

You might also like