Professional Documents
Culture Documents
Fonolojia Na Fonetiki Za Kiswahili
Fonolojia Na Fonetiki Za Kiswahili
Fonolojia ni nini?
Ni tawi mojawapo katika taaluma ya isimu linalojumuisha vipengele vya matamshi,
mkazo,kiimbo, lafudhi, toni, mfuatano wa sauti katika kuunda silabi, mfuatano wa sauti
katika kuunda mofimu, mfuatano wa mofimu katika kuunda maneno na tahajia / otografia
zake.
Fonolojia ni tawi la taaluma ya isimu linaloshughulikia uchunguzi, uchambuzi, na
uanishaji wa sauti pambanuzi katika lugha mahususi. Tawi hili hujishughulisha na
sauti ambazo hutumika kutofautisha maana za maneno katika lugha maalum /
mahususi. Fonolojia hujihusisha na sheria / kanuni zinazoandamana na utoaji wa sauti
pamoja na utumiaji wa sauti hizo pambanuzi.
Fonolojia imejikita katika lugha maalum ikichunguza namna binadamu
anavyotamka sauti na kuziunganisha ili kuleta maana katika lugha maalum inayohusika.
JINSI YA
MATAM MAHALI PA KUTAMKIA / MATAMSHI
SHI
Mido Mido- Meno,Uf Kipind Kaak Kaak Kaak Kida Mido- Mido- kishi Korom
m oMenomo izi- uka gumua gumua laini ka kaakaam kaakaam mo oe
Meno,Ba a -ufizi a aa Tong o gumu o laini
ada ufizi e-aak
aaK
laini
Nazali ɲ
m ɱ n ɳ
ŋ N
Vipasuo ɢ ʔ
p b t d ʈ ɖ k g q
c ɟ
Vikwamiz β θ ðs ẕ Ʒ j ʍ ʕ
i ɸ f v z s ʃ ç x ɤ χ ᴚ ħ h ɦ
Vizuio- ɥ
Kwamizi υ ɹ ɻ j ɰ
w
Vitambaz
a-
Kwamizi
ɺ ʙ
Vitambaz ɭ ʎ
a l
Vimadend
e
r ʀ
Vipigo ɾ ɽ ʀ
Ijektivu ῤ ť ḱ
Implosivu ɖ ɠ
ɓ
Vidoko- ͽ ʇ c
Kati
Kitambaz ʖ
a-Kidoko
Mifano na: 1
Sauti [b] [a] [r] [g]
[+kons ] [+sil ] [+ghun ] [+ghun ]
[+ghun ] [+ghun ] [+kont ] [+kor ]
[+mid ] [+chin ] [+mad ] [+kons ]
[-kont ] [+son ] [+ant ] [- kont ]
Alasauti za lugha ni viungo mbalimbali maalum vya mwili wa binadamu. Viungo hivi
ni muhimu sana katika sayansi ya lugha hususani katika tawi la fonetiki na fonolojia.
Viungo hivi hutumika kuunda au kuzalisha sauti mbalimbali ambazo hushughulikiwa
katika tawi hili la fonetiki katika isimu ya lugha. Massamba na wenzake (2004)
Alasauti hizi ni mapafu ambayo hufanya kazi ya kuvuta hewa ndani na kutoa nje ya
kifua cha binadamu kupitia katika chemba ya kinywa au chemba ya pua. Umio ,koromeo
ni aina nyingine ya alasauti ambayo huwa na namna fulani ya kambakamba ya nyama
laini zinazoitwa nyuzisauti. Nyuzisauti zina uwazi katikati unaoruhusu hewa kutoka nje
ya kifua cha binadamu na kuingia ndani ya mapafu ya binadamu. Nyuzisauti zinapokuwa
zimeachana hewa hupita kwa urahisi kwenda nje na hivyo kusababisha sauti
zinazotamkwa kutokuwa na mtimbwiliko mfano sauti [t],[p] nakadhalika. Lakini
zinapokuwa zimekaribiana au zimegusana hewa kutoka mapafuni hulazimika
kuzisukuma ili kuziachanisha na kusababisha sauti zinazotamkwa kuwa na mtimbwiliko
mfano sauti [r], [b] nakadhalika.
Alasauti nyingine ni kinywa ambacho kinajumuisha ulimi, kaakaa gumu, kaakaa
laini, ufizi, na meno. Ulimi una sehemu kuu tatu; sehemu ya mbele ambayo inajumuisha
incha ya ulimi ambayo hukutana na alasauti ama viungo vingine kama meno, ufizi,kaakaa
gumu,kaakaa laini ili kutamka sauti [t], [d], [θ], [i] na kadhalika. Kiwiliwili au bapa la