Download as docx, pdf, or txt
Download as docx, pdf, or txt
You are on page 1of 10

MTIHANI JUMUISHI WA DARUBINI

Cheti cha Kuhitimu Kisomo cha Sekondari

KIDATO CHA TATU ~ 2024
102/2 Kiswahili ~ Lugha ~Karatasi ya 2
APRILI – MEI ~ 2024 ~ Muda: Saa 2½
Jina: ________________________________________Nambari: ________________

Sahihi ya Mtahiniwa: _________Tarehe: __________________Saa: ___________

Maagizo
(a) Andika jina lako na nambari yako ya mtihani katika nafasi ulizoachiwa hapo juu.
(b) Tia sahihi yako kisha uandike tarehe ya mtihani katika nafasi ulizoachiwa hapo juu
(c) Jibu maswali yote.
(d) Majibu yako yaandikwe katika nafasi ulizoachiwa katika kijitabu hiki cha maswali.
(e) Majibu yote ni lazima yaandikwe kwa lugha ya Kiswahili.
(f) Usitoe ukurasa wowote kutoka kwenye kijitabu hiki.
(g) Karatasi hii ina kurasa 8 zilizopigwa chapa.
(h) Watahiniwa ni lazima wahakikishe kuwa kurasa zote zimepigwa chapa sawasawa na
kuwa maswali yote yamo.

Swali Upeo Alama

Ufahamu 15

Kwa matumizi ya mtahini pekee Ufupisho 15

Matumizi ya lugha 40

Isimujamii 10

Jumla 80

D003 F3 P2

1
1. UFAHAMU: (alama15)
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata
Tumeshuhudia baadhi ya ndugu wa familia moja wakiishi bila maelewano na wakati
mwingine kukata kabisa kabisa mawasiliano. Hivi leo kuna familia ambazo haziwezi kuketi
pamoja na kumaliza matatizo yao, na badala yake huchukua njia za vita ugomvi na hata
pengine mauaji kama suluhisho la migogoro yao.

Kawaida maisha sio mstari mnyoofu. Kuna milima, mabonde, kona na hata mashimo.
Ndiposa migogoro ni sehemu ya maisha yetu! Mara nyingi haiepukiki, isipokuwa kuipitia
na kupata suluhisho. Ipo migogoro baina ya ndugu ambayo huleta kutoelewana,
kukosesha amani na hata pengine kupoteza kabisa mahusiano. Ni wazi kuwa mahali
popote wanapoishi watu au kufanya kazi pamoja,hapakosekani migogoro kwani hata
vikombe vinapokuwa kabatini, havikosi kugongana.

Ukweli ni kwamba sote tunazaliwa na tabia tofauti, uwezo tofauti wa kuvumilia na hata
kuamua kutenda. Katika mazingira yoyote ya kutoelewana, kiasi kikubwa cha busara,
upendo, amani na imani huhitajika ili kuiondoa migogoro hiyo. Isipotafutiwa suluhisho
ama utatuzi wake ukatendeka kwa jazba na chuki, migogoro ya ndugu katika familia
hukua na kuzaa madhara makubwa.

Kuanzia utotoni au hadi uzimani, kunaweza kuwa na sababu nyingi ambazo huweza
kupelekea kuleta tofauti baina ya ndugu. Kwa ujumla, ndugu ni watu unaowaamini,
ambao hawatakupa kisogo. Walakini, hii sio wakati wote. Kwa bahati mbaya ukweli
umetuonyesha kuwa kuna uhusiano wa kindugu ambao huisha vibaya. Sababu kubwa
zikiwa ni mazingira ambayo ndugu wameishi ambayo wakati mwingine kuna upendeleo wa
mzazi kwa mtoto au watoto fulani na kuwafanya wengine wahisi wivu, kutopendwa na
kutengwa.

Zipo sababu za kiuchumi ambapo ndugu wengine katika familia wanafanikiwa zaidi kuliko
wengine na kuwa na maisha bora zaidi kuliko wengine. Hali hii pia inaweza kuleta
mfarakano kwa wale ambao hali zao ni tofauti na wengine, hasa iwapo hakukuwa na
mazingira ya utangamano katika familia tangu awali.
Ndugu wa familia moja huzaliwa wakiwa na tabia tofauti. Kila mshiriki wa familia ana
haiba na mtazamo wake tofauti katika masuala mbalimbali. Wengine hukasirika mara
kwa mara, wengine ni wakimya sana, wapo walio wakorofi na wengine wanaopenda amani,
hivyo jambo hili ni muhimu mno kulielewa mara inapotokea migogoro ili kutamua namna
ya kupata suluhisho.

Jambo la kusikitisha zaidi ni kwamba migogoro hii wakati mwingine hupelekea kuvuruga
mwelekeo wa maisha ya watoto hasa wakati wa ukuaji,kwani kulingana na tofauti zao,
wapo wale wanaoamua kuondoka nyumbani wakiwa bado na umri mdogo na kuhamia
mitaani.

Pamoja na migogoro kuwepo katika familia zetu ni vyema wazazi ama walezi waelewe
tofauti za kifamilia zinavyoweza kuchangia mfarakano baina ya ndugu wa familia moja.

2
Kwamba mzazi ama mlezi anapompendelea mtoto mmoja na kutokuwa karibu na
mwingine, anatengeneza mazingira ya tofauti baina ya watoto wake. Ni vyema kuweka
uwiano sawa baina ya watoto na familia ili kuweza kupunguza tofauti zinazoweza
kujitokeza.
Maswali
(a) Onyesha athari tatu za migogoro miongoni mwa ndugu katika familia. (alama3)
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………
(b) Eleza mambo matano yanayochangia kuwepo kwa watoto wanaorandaranda mitaani
kwa kurejelea kifungu (alama5)
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………
(c) Malezi yanachangia migororo baina ya ndugu. Thibitisha kwa kurejelea kifungu(alama1)
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………
(d) Taja na ueleze mbinu nne za kimtindo zilizotumika katika kifungu. (alama4)
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………
(e) Andika visawe vya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika kifungu. (alama2)
(i) Haiepukiki
……………………………………………………………………………………………………………..
(ii) Haiba
…………………………………………………………………………………………………………….

2. UFUPISHO (alama15)

3
Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali
Mifuko ni muhimu sana katika maisha ya binadamu ya kila siku. Baadhi ya mifuko
huundwa kwa namna ambayo inadumu na inaweza kutumiwa mara kadha wa kadha. Hii
huweza kuhifadhiwa na kutumiwa kwa kipindi kirefu. Asilimia kubwa ya mifuko ya aina
hii hutengenezwa kutokana na nguo au ngozi. Hata hivyo, ipo mifuko mingine ambayo si
ya uashi, haidumu. Hii ni mifuko myepesi, rahisi kubebeka na inayopatikana kwa wingi
sana. Hii ni mifuko ya plastiki.

Mifuko ya plastiki hupatikana katika maeneo mengi sana. Mifuko hii sio ghali
inapolinganishwa na ile ya nguo au ya ngozi. Hii ni ya gharama ya chni na hupendwa
kutokana na wepesi wake. Hata hivyo, mifuko hii inaweza kuwa chanzo cha matatizo
mengi. Matatizo haya hutokana na linalopasa kufanywa kuhusu mifuko hii baada ya
kutumiwa kwake. Mifuko ya nguo ambayo inatupwa kwenye jalala huishia kuoza na kuwa
sehemu ya uchafu wa jalala hilo. Kwa upande wake, mifuko huo. Hata inapofukiwa arthini
haiwezi kuoza hata kama kufukiwa huko ni kwa miaka mingi. Aidha hata pale
inapochomwa, haiwezi kuteketea hadi kuwa jivu kama ilivyomifuko ya karatasi.

Upo umuhimu mkubwa wa kuwepo kwa sera madhaubuti za kupambana na tatizo la

mifuko hii. lazima zitungwe sheria ambazo zinakabiliana na uchafuzi wa mazingira kwa
njia hii. kwa njia hii hatari zianzowakabili watu na wanyama zitapunguzwa kwa kiasi
kikubwa. Kwa hakika njia mojawapo ambayo ingeweza kutumiwa ni kuharamisha
matumizi ya mifuko hii katika upakiaji. Sheria zinaweza kupitishwa ambazo zinahimiza
matumizi ya mifuko mbadala kama ile ya karatasi kubebea vitu vidogo Fauka ya hayo,
pana haja ya kuwazia kuwepo kwa njia nzuri kuteketezea mifuko hiyo. Inawezekana
kuhimiza watumiaji kuirejesha mifuko hiyo mahali Fulani kwa ajili ya uteketezaji huo.
Hata hivyo, hali hii huenda ikawa ngumu kwa kuwa inahitaji nidhamu ya hali ya juu sana
kwa upand ewa watumiaji.
Maswali
(a) Fupisha ujumbe wa aya tatu za mwanzo kwa maneno 105 – 110 (alama10,1 utiririko)
Nakala chafu
………………………………………………………………………………………………………………………

……………………………………..
………………………………………………………………………………………….

4
………………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………..
Nakala safi

………………………………………………………………………….…
(b) Eleza mawazo makuu yanayojitokeza kaitka aya ya mwisho (maneno 50 – 55)
(alama5,1 utiririko)
Nakala chafu
………………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………………
……………………………………..………………………………………………………………………………

5
………………………………………………………………………………………………………………………
……………………………………..………………………………………………………………………………

3. MATUMIZI YA LUGHA (alama40)

(a) Dondoa sauti mwambatano zilizo kwenye maneno haya na utambue mahali sauti hiyo
hutamkwa (alama2)
(i) Afya
…………………………………………………………………………………………………………….
(ii) Anza
……………………………………………………………………………………………………………..
(b) Tumia vihusishi vifuatavyo kutunga sentensi (alama2)
(i) Kihusishi cha ‘a’ uganifu
………………………………………………………………………………………………………………
(ii) Kihusishi ‘na’ cha mtenda
……………………………………………………………………………………………………………..
(c) Bainisha matumizi ya kiambishi ‘ku’ katika sentensi ifuatayo (alama1)
Bonareri hakupata zawadi jana.
………………………………………………………………………………………………………………….
(d) Tunga sentensi yenye wakati uliopita hali ya kuendelea (alama2)
………………………………………………………………………………………………………………….
(e) Pigia mstari silabi inayotiwa shadda katika maneno yafuatayo (alama2)
(i) Walimwengu
(ii) Samehewa
(f) Tunga sentensi moja kubainisha maana mbili za neno chungu (alama2)
…………………………………………………………………………………………………………………
…...........................................................................................................................
(g) Taja aina za vitenzi vilivyopigiwa mstari katika sentensi ifuatayo (alama2)
Mama amewahi kupika jikoni.
…………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………….
(h) Onyesha muundo wa silabi ya kwanza katika maneno yafuatayo (alama2)
(i) Mke
………………………………………………………………………………………………………………

6
(ii) Ng’ombe
……………………………………………………………………………………………………………….
(i) Andika sentensi zifuatazo upya kulingana na maagizo bila kupoteza maana
(i) Mizizi ya mibaruti hii iliwaponya watu ambao walikuwa na shida kama hii yenu.
(Kanusha kwa umoja) (alama2)
………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………
(ii) Mama aliwahimiza warudi siku hiyo, la sivyo wangekosa tuzo
(Andika katika usemi halisi) (alama2)
………………………………………………………………………………………………………………
(iii) Sisi tunajua sheria japo tu wafisadi
(Anza kwa: Japo……….) (alama2)
……………………………………………………………………………………………………………
(iv) Fundi aliharibu taa.
(Geuza katika kauli ya kutendea) (alama2)
……………………………………………………………………………………………………………..
(j) Weka nomino zifuatazo katika ngeli mwafaka (alama2)
(i) Mtumba
……………………………………………………………………………………………………………….
(ii) Mapenzi
……………………………………………………………………………………………………………….
(k) Ainisha shamirisho katika senmtensi ifuatayo (alama3)
Mangwasha amemjengea mama yake mdogo nyumba kubwa kwa nyasi
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………….
(l) Tunga sentensi kubainisha aina ifuatayo ya sentensi (alama1)
Sentensi hisishi
………………………………………………………………………………………………………………….
(m) Andika maneno yenye miundo ifuatayo (alama2)
(i) Nafsi ya pili wingi, wakati uliopita, kirejeshi wingi, kauli ya kutendwa, kiishio
……………………………………………………………………………………………………………..

7
(ii) Ngeli (A – WA) umoja mzizi
……………………………………………………………………………………………………………..
(n) Tunga maana ya sentensi ifuatayo (alama2)
Ningalikuwa na pesa ningalinunua kitabu hiki.
………………………………………………………………………………………………………………….
...............................................................................................................................
(o) Tunga sentensi kudhihirisha matumizi ya vielezi vifuatavyo (alama2)
(i) Kielezi cha namna kiigizi
…………………………………………………………………….…………………………………………
(ii) Kielezi cha namna kikariri
……………………………………………………………………………………………………………….
(p) Andika sentensi mbili tofauti ukitumia vitenzi hivi vya silabi moja (alama2)
(i) Pa
……………………………………………………………………………………………………………
(ii) La
…………………………………………………………………………………………………………..
(q) Andikas sentensi yenye muundo ufuatao (alama2)
K (TS+T)
…………………………………………………………………………………………………………………

4. ISIMUJAMII (alama10)
Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali
A: Wewe njoo hapa haraka! (kwa sauti kubwa) Fanya upesi!
B: (Anakimbia mbio) Naja Sir.
A: (Anamtazama) Unajifanya mwerevu?
B: Hapana Sir… eeeeee …. Sir …. afande
A: Jina? Haraka
B: Sagilu Lesulia
A: (Akiandika) Kitambulisho haraka haraka
B: Sina hapa afande
A: Oooh,, huna kitambulisho? Utafanyiwa booking namna gani?
B: Naomba….
A: Tunawajua wazururaji kama nyinyi. Naomba! Naomba! Unaomba nini? Mndai kwamba
kuna curfew. Mnajiponza wenyewe na kuwahasiri wenzenu. Baadaye “Serikali saidia” Ingia
ndani usiniaharibie muda wewe. Ndani! Leo utakuwa mgeni wetu.

8
(Anamsukuma ndani.)
(a) Bainisha sajili ya makala haya (alama2)
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………
…………………………………………………………………………………………………………………
(b) Eleza sifa nane za sajili hii kwa kurejelea makala haya (alama8)

…………………………………………………………………………………………………………….……

Huu ndio ukurasa wa mwisho uliopigwa chapa

9
KWA MAJIBU:

MTIHANI JUMUISHI WA DARUBINI SERIES 003 ~ 2024

KSH. 60
MPESA NO: 0713452040

WHATSAPP/CALL:

0724289534 au 0713452040

10

You might also like